Mzoa Takatakata Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA : HAFIDHI J IKRAM
*********************************************************************************
Chombezo : Mzoa Takataka
Sehemu Ya Tatu (3)
โSalumu usilie swala la kunisaidia mie ushachelewa nakufaa!!!
baada Mwanaidi kutamka vile akaanza kutapa tapa mwisho akatulia kimyaa
nikabaki kumtikisa huku nikimwita
kwa nguvu โMwanaidiiiiiiiiiiiโฆ.
mama yake huku nae akiwa analia akaja mbio akiwa na majilani vilio vikaongezeka basi tukaenda kumzika kipenzi changu aliye niingiza kwenye ulimwengu wa
mapenzi
yani kama bikra tulitoana wote tukamuombea alazwe mahala pema peponi katika makaburi ya keko mwanga
ndio tulipo mlaza baada kutimia kama wiki moja hivi kidume nipo mzigoni na Benz langu jipya nazoa takataka
nikiwa sina hili wala lile gafla bin vuu nikajikuta nalowana mwili mzima baada gari moja hivi kupita kwa kasi eneo lile kulikuwa na dimbwi la maji machafu ya
vua yaliyo chanyika na yachooni dereva hakuwa muungwana hata kidogo nilizani atasimamisha gari kuniomba samahani lakini hakufanya hivyo
baazi ya watu wakakilaani kitendo
kile nikatoka
na mkokoteni
wangu kwa ajili ya kusonga
mbele zaidi siku hiyo nilipiga
kazi yani najaza rumbesa nikienda
dampo nazimwaga kisha nakuja kujaza tena ilikuwa siku ya neema kwa sababu wazoa takataka manispaa ya temeke wameweka mgomo kisa mshahara mdogo
mie nalipwa na yule nitakaye beba takataka zake iwe mia tano au zaidi basi nashukuru tu nikajisemea waweke mgomo daima kwa hali hii sitokufa njaa kamwe
nikiwa bado katika kuchakalika si nikamuona yule boya
aliye kuwa anatembea na marehemu
Mwanaidi akiwa kaongozana na kisichana flani hivi kikiwa ndani ya sale za shule kwa jinsi walivyo shikana bila shaka ni wapenzi nikasikitika sana ila nikaitaji
kwenda kumuokoa
yule binti ila nikajiuliza inawezekana washafanya ngono si zaidi ya mara moja hata nikienda kumtonya nitakuwa nishachelewa
basi nikapiga moyo konde itakavyo kuwa wacha iwe โoyaa mangi babu,
โyeah niambie mzoa takataka,
โnaomba uniangalizie mkokoteni wangu huu kuna sehemu naenda mara moja, โpoa hamna shida,
basi nikatoka zangu kuwafatilia nyuma nyuma mpaka nikawaona kwenye kichochoro kimoja wapo hivi wamesimama yule binti akatoa kanga kwenye begi lake
na kujitanda yani aonekane kama mmama flani hivi ila nikawafata pale pale yule jamaa baada kuniona akastuka ila alijikaza tu nikamuuliza โhivi wewe ni zaidi
ya gaidi ehee!!! mpaka sasa ushauwa wangapi umeambukiza wangapi yani
mpaka kabinti haka kadogo unataka
kwenda kukauwa duhuu”โฆโฆ
โwee boya tu sema shida yako usepe kama takataka hapa hakuna, ndivyo alivyo nijibu yule jamaa si akanyanyua mkono wake kunipiga kofi kwa kitendo cha
haraka nikamdaka na kuubamiza ule mkono ukutani akapiga yowe la uchungu tu nikamgeukia yule binti na kumwambia โmapenziโฆ.naโฆ.shule haviendaniiii
ukiwa shuleni!! tulia darasaniโฆembu msikilize mwalimu anafundisha nini kuwa makini ukitoka shuleni usipite vichochoroni nenda moja kwa moja mpaka
nyumbaniii
wakati namwambia hivyo binti yule mchozi ukamtoka baada kugundua kumbe basha wake ni muasilika kwa sauti ya kilio akaniambia โsijui nikushukuru vipi
kaka yangu kwa kuniokoa na janga hili maana ndio nilikuwa naenda nae guest
ndio maana nilipo mwambia anunue condom alikataa kwa kisingizio utamu wa pipi ule bila ganda,
nikamwambia binti
โsiku zote tamaa ni hatal!!! kwa kupenda vitu vizuliii ndio maana mnafer
sikutaka kuongea sana nikaseba kuwai Benz langu mie kama msaada
nishatoa,!
Binafsi nilijisikia faraja sana kwa kuweza kumuokoa yule binti katika mdomo wa mamba. Nikarudi moja kwa moja nilipoupaki mkokoteni wangu.
โoyaa mangi mi ndio nawasha mchuma huu!!! ni maneno niliyo mwambia mangi baada kufika pale
dukani kwake, nae akanijibu kwa kusema
โsawa kaka hamna shida!”
basi nikau sukumiza mkokoteni wangu mpaka ninapo ishi
lakini hofu ikanishika ghafla baada kumuona mzee mmoja hivi akifoka kwa maneno ya ajabu ajabu.
โhabari za kusema kesho au mwakani sitaki ninacho taka ni pesa yangu tu pumbavu zenu hii nyumba sio ya baba zenu!!! hakuna cha bure hapa”โฆ.
Nikawa natetemeka huku nikijiuliza iwapo mkataba wa Madebe ukiwa umeisha itakuwaje na ndani
nina shillingi elfu kumi na tano tu!
basi nikampita bila kumpa salamu maana nilimuhofia nikiwa najiandaa kufungua mlango ghafla nikaguswa begani kwa kupigwa pigwa.
โwee kijana!!!
alikuwa yule mzee huku macho yakiwa mekundu akanikazia na kuniulia โhivi ulivyo pita pale uliona gogo au?”
nikashindwa cha kumjibu akaniuliza tena kwa sauti ya ukali zaidi
โnakuuliza wewe ulivyo pita pale uliniona gogo au jiwe!!!
huku nikibabaika nikamjibu.
โnisamehe mzee wangu unajuwa tena muda mwingine kazi zetu hizi zinatupa mawazo chungu nzima”
Akaniambia
โhaya tuyaache hayo hiki chumba mpaka sasa kina miezi sita hakijalipiwa kodi kwa hiyo ninacho taka ni pesa yangu lasivyo uhame!!!
nikamjibu โkwa leo mzee wangu sina kitu nivumilie mpaka wiki ijayo nitakupatia pesa yako,
Akawaka kwa hasira
โwee!!! kijana yani nimetoka kijijini huko kibada kuja hapa kufata pesa yangu alafu nirudi mikono mitupu hapa nilipo sina hata sentano ya nauli. Nitarudi kwa
miguu au utanipakiza kwenye mkokoteni wako?”
nikamjibu โkuhusu nauli nitakupa baba!
โhaya nipe hiyo nauli ukumbuke na ya soda njiani maana kibada nimbali basi nikaingia chumbani na kutoka na ile pesa shillingโฆelfu kumi na tano
nikampa ila nikashangaa alivyo zipokea haraka na kuondoka zake ila sikutaka kujali sana zaidi ya kuingia zangu ndani nifanye mambo mengine
zikiwa zimepita siku kama mbili hivi
siku hiyo nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe nikastushwa na sauti ya makelele โyeyooo!!!
kucheki ni Madebe akiwa na mabegi yani kwa jinsi alivyo kuwa kama vile katoka America basi nikaenda mbio kumpokea tuka kumbatiana kwa furaha nikabeba
mabegi na
kuingia nayo ndani โvipi kaka mbona ulinikimbia?”
โhapana ndugu sijakukimbia ila kuna zali lilitokea ghafla. Yani hata muda wa kuja kukutonya haukuwepo basi nikakwea pipa na kwenda kwa madibaa!!!
โkwa madiba, ndio wapi kaka?”
โkumbe kwa madiba hupajui ndugu?”
โndio sipajui ila nasikia sikia tu vijana wakipataja,
โni South africa hiyo!
โahaa kumbe South,
nafikaga ndotoni tu, โha!ha!ha! unafikaga ndotoni tena ila usijali utafika live yani itakuwa sio ndoto tena vipi yule binti wa siku ilee ulitusua au akazingua?”
โmimi tena nilitusua mpaka mtoto akazimika mwenyewe kila day anakuja ning’ate kitumbua, โha!ha!ha! wee noma kwa hiyo siku ile sikupata dhambi?”
โdhambi za nini tena
Madebe?”
โsi nilivyo enda kumkamata kinguvu yule demu nikamtishia kukikata kitumbua chake nikinyofoe chote iwapo tu atakataa kulala na wewe,
โduhuu kumbe ulimtisha hivyo ila usikonde kaka wewe mwenyewe utamuona akija hapa na kutupikia msosi, basi
Madebe akacheeka na kusema
โbasi kama hivyo itabidi hili ghetto nikuachie wewe afu mimi nichukuwe chumba cha pale karibu na chooni,
โehee ume nikumbusha kitu kaka!!!
โkitu gani hiko tena?”
โjuzi kati kuna mzee flani kaja hapa akaanza kufoka mbaya akitaka pesa ya kodi bila shaka atakuwa baba mwenye nyumba tu!
Madebe akaniuliza โyukoje huyo mzee?”
nikamuelezea jinsi alivyo akasema
โahaa yule boya sio nyoko zake yani kitendo cha kumwambia niko South tu kaja hapa kudai kodi ya nyumba sio
vipi wewe hajakusumbua?”
โwee asinisumbue tena mchezo kaniwakia mbaya kama sina pesa nihame kwakuwa ndani nilikuwa nina pesa kidogo nikamtoa ndio akasepa,
โduhuu ulimpa pesa shilling ngapi?”
โnilimpa elfu kumi na tano tu baada kusema vile
Madebe akacheka sana na kusema
โkudadeki yule mzee mwanga sana ila
Salumu kaka nisamehe mie kwa kutokwambia mapema hata ningetokea kufa ghafla sijui ingekuwaje
binafsi hii nyumba ni yangu na washkaji wote kitaa wana fahamu hilo ila some time sipendi kujionyesha tu
kuhusu nilipo zipata pesa mpaka nikanunua nyumba hii ni hizi hizi kazi zetu namiliki hadi daladala kama tatu hivi maduka ya nguo ninayo mawili huko k/koo.
Kusema kweli napiga pesa sana”โฆ..
โlakini kaka kwa nini usingeniajili niwe hata konda kwenye daladala hata moja kuliko kuwa mzoa takataka?”
โsikia nikwambie kitu Salumu sio kama nakuacha uwe mzoa takataka ukajuwa mi napenda uwe hivyo hapana ndugu nakuandalia mazingira kwanza yani siku ya
siku ukija kutoka basi utoke kweli,!
basi nikaweza kulizishwa na maelezo yake
Madebe huku akisema โyule mzee hiyo pesa atainya tu kumbe ni Ankor wake
nakumbuka zikapita siku kama nne hivi siku hiyo nikiwa natoka zangu dukani kwa Rahma kupiga story mbili tatu nakaribia nyumbani nikaweza kuona kama
chumba ninacho kaa mimi kuna watu wanabishana hivi. Basi sikuwa na wasiwasi nikajuwa labda washikaji tu wamekuja kama kawaida yao
kupiga story mbili tatu lakini nafsi ikaniambia Salumu
kuna hatari ipo karibu yako maana mapigo yangu ya moyo yakaanza kwenda mbio baada kusikia sauti nzito ya mwanadada ikitokea chumbani mule. Kwa kusema
โsikia
Madebe usijifanye mjanja hata kidogo mie jana tu nimepiga simu South kuulizia huo mzigo nikajibiwa ya kwamba mzigo wote umekabidhiwa wewe!!!
nikamsikia
Madebe akimjibu yule Dada โmzigo mimi sijauchukuwa ila Jacko anaongopa tu”โฆ.
โwewe Madebe acha mambo ya kifara hapa usitufanye sisi watoto wadogo ukazani ukitupa pipi tutalainika
ukweli wote ninao kwenye simu yangu wakati unakabidhiwa mzigo kuna video walishuti jamaa amenitumia. Sasa embu cheki hii huyu si wewe ukiwapa tano
jamaa,
sasa chaguwa moja tu kati ya mambo mawili je umlete yule kijana unayeishi nae tumbebeshe mzigo tumboni au ufe!!!
baada kusema vile nikasikia sauti za wale watu wakijiandaa kutoka mule ndani nikatoka mbio na kwenda kujificha nyuma ya choo ila nikaweza kuwaona ni
mipandikizi ya mibaba yani kama wale wacheza miereka kina John Cena au Batister hata yule mwana Dada nae zinga la jitu basi wakaingia kwenye magari
waliyokuja nayo na kuondoka zao.
Nikabaki kujiuliza ni mzigo gani huo”โฆ. alio uchukuwa
Madebe mpaka anadaiwa vile na kijana yupi anaye itajika kubebeshwa huo mzigo tumboni. Bila shaka ni mimi tu je ni mzigo gani, nijuwavyo mimi mzigo unao
bebwa tumboni ni mimba tu tena kwa Wanawake basi sasa mimi nibebeshwe mzigo why?”
nilijiuliza maswali mengi pasipo kupata jibu. Basi nikajinyanyua na kwenda chumbani nilipo ingia
Madebe sikumkuta nikajiuliza labda katoka kwenda chooni au dukani tu nikawa nina hofu balaa hata hamu ya kula sikuwa nayo mawazo yakanisonga
usingizi nao ukanichukuwa nikaja kustuka usiku wa manane kucheki pembeni ya kitanda hakuna mtu โhivi
Madebe atakuwa kaenda wapi?” usiku huo kitanda nilikiona kama kina miba basi nikaichukuwa cm yangu na kumpigia Rahma
ikawa inaita tu bila kupokelewa nikamcheki
Madebe yeye hapatikani dahaa,
hofu juu ya hofu ikanitanda zaidi nisijuwe nini kitatokea juu yangu
Usiku ulikuwa mrefu sana kwangu mie nikatamani kukuche haraka niweze kujuwa mustakabari mzima wa maisha yangu. Nikaitizama saa ndio kwanza saa tisa
kasorobo kidume nilikuwa natetemeka kama vile kifaranga cha kuku kilicho nyeshewa vua,
Taratibu nikajinyanyua na kutoka zangu nnje, Kitendo cha kutoka tu nikashitukia kama vishindo vya watu wakija eneo lile, Sikuweza kujuwa wala kufahamu ni
watu gani hao ila nikajihami mapema kwa kukimbia na kwenda kujificha sehemu ambayo nilihisi kabisa hawatoweza kuniona. Iwapo wamekuja kwa rengo la
kunifata Mimi, au Madebe nikiwa nimejificha nikaweza kushuhudia kikundi cha watu kama sita hivi wakiwa wameficha sura zao kwa vitambaa usoni mkononi
kila mmoja akiwa na dhana yani,
Nyundo panga chupa nikajikuta natumbua macho tu ghafla nikashitukia nakabwa kwa nyuma huku nikizibwa mdomo nisiweze kupiga kelele nikajikaza kujitoa
wapi nikaisikia sauti ikinisihi nitulie โSalumu kaka ni miee tulia basi, Kumbe alikuwa Madebe akaniachia na kunipa.
โpole sana kaka!”
nikamjibu
โusijali nishapoa,
Akaniambia
โsasa hapa naitaji tucheze mchezo wa kicommando!”
Nikauliza
kwa sauti ya chini
โtuucheze vipi huo mchezo?”
โsi umewaona wale maboya wamekuja kwenye kumi na nane zangu, sasa ninacho kihitaji ni kuwafunza adabu maana nishaandaa kikosi cha Maafande watafika
hapa muda si mrefu!”
Nikamuuliza kwa shahuku kubwa ni kweli au?”
โndio ni kweli ndugu naitaji niwachomeshe tu kisha nitubu dhambi zangu nianze kuswali swala tano zote yani niwe mtu safi kabisa!”
baada Madebe kusema vile akaniambia twenzetu,’ tukawa tukinyata kuwanyatia wale vijana wawili waliobaki nnje wengine wameingia chumbani kupiga search
baada kuwafikia tu wote kwa pamoja kila mmoja akamrukia wa kwake na kwenda nae mpaka chini nilijitahidi kwa nguvu zote kumkaba yule jamaa huku
nikivutia hisia jinsi ninavyo sukuma, Mkokoteni wangu pindi ninapo pandishaga kirima jamaa akafurukuta mwisho akawa kimyaa tulicho kifanya baada ya hapo
ni kuvaa magwanda yao na vile vitambaa tukakaa nnje
Tukiwa na sura za ukauzu balaa. Ghafla mlango ukafunguliwa na kutoka wale jamaa wengine na kusema, โOyaa hawa watoto wa Malaya hawapo humu ndani
sijui wameenda wapi kama vipi tutawatimbia kesho!” baada kusema vile wakatupita ikiwa ishara ya kwamba twenzetuni hawakujuwa kama wanafanya kosa
kubwa sana kitendo cha kutupa migongo tu kila mmoja akaandaa Rungu lake kwa nguvu ya ajabu tukaenda kukita kwenye vichwa vyao, Kila mmoja akayumba
na kwenda chini haraka haraka tukavua yale magwanda punde tu maafande hao.
โkazi nzuri vijana tena ongera sana kwa kuweza kutusaidia kazi ya kuwakamata hawa Nguchiro, ilikuwa kauli ya pongezi kutoka kwa Afande Mark basi, kwanza
wakawapima pumzi isije ikawa tumeuwa nikashusha pumzi baada kuonekana kumbe wazima ila wamezimia tu,
Kesho yake Asubuhi nikiwa dukani kwa mpenzi wangu Rahma kuna jamaa mmoja hivi akaja na kuanza kumsumbua sumbua Rahma kwa kumtongoza wakati
kidume ninae miliki mzigo niko hapohapo.
โsikia binti mi binafsi nimetokea kukupenda nipo tayari kukupa chochote ukitakacho katika maisha yako!”
Rahma akamjibu
โsikia kaka naomba unikome kama ulivyo likoma ziwa la Mama yako kama pesa ninazo mpaka nashindwa kujuwa wapi pa kuziweka!”
โNenda zako huko Malaya mkubwa tu wewe unazani nani asiyekufahamu ulikuwa unajiuza kule Temeke mwisho,’ siku zote mwanaume akitongoza na
kukataliwa utamkuta lazima aponde nikashikwa na hasira kwa kitendo cha mpenzi wangu kuitwa Malaya hata kama ni kweli,
Nikaenda kumkunja yule jamaa nikamtandika kichwa kilicho mfanya abimbilike kwenye ngazi maana tulikuwa juu kidogo nikamshukia chini na kuanza
kumshambulia kwa mateke nikaja kushikwa na Madebe na kunisihi niache binafsi nikabaki kushangaa kwa jinsi Madebe alivyo vaa yani katinga kanzu kubwa
nyeupe na barakashia nzuri mkononi kashika tasbihi na Msahafu, akaniambia
โSalumu kaka huu sio muda wa kufanya matendo ya ajabu ajabu kama haya siku zote Allah (s.w.t) anasema katika Qur’an ya kwamba Na penye chukizo pasi
jiepushe,
Ikiwa na maana kufanya hivyo itakuwa ni bora zaidi kwako kuliko ukaingia kwenye maasi wakati Madebe ananihusia hivyo kumbe yule jamaa akaingia ndani ya
gari yake na kutoka na bastora bila kuuliza akafyatua risasi iliyokuwa ikiitaji kunipata mimi, Madebe akaja kukinga ikampata moja kwa moja kwenye tumbo.
Yule jamaa akawasha gari na kukimbia eneo lile nikabaki kuita โKakaa!”
Kakaa!!! kwa sauti ya chini iliyo ambatana na maumivu Madebe akasema โSalumu mdogo wangu huna haja ya kulia binafsi nakufa kifo cha kishujaa sana angali
nishatubu mazambi yangu Salumu naomba upiganie kuhusu ile Nyumba maana hati niliandika jina lako nilitambua sitoweza kuishi muda mrefu nitakufa tu,
Usijaribu kutaka kulipa kisasi”โฆ.
ghafla Madebe akatoa macho na kutulia kimya sikuweza kuamini kama nampoteza kamanda wangu,
Mkombozi wangu wa maisha yangu nililia sana na kuita โKaka!!!kaka!!!
hakuweza kuamka tena police walifika na kufanya uchunguzi wakaondoka na mwili wa marehemu mkononi mwangu nikabaki na Tasbihi pamoja na Msahafu tu
nikajiapia kama sheria itashindwa kumnasa yule jamaa na kumchukulia hatua nitamnasa mimi nikajivika roho ya kishetani nikakodi boda boda kwenda kituo cha
police niweze kujuwa kinacho endelea taarifa za kifo cha Madebe zilisambaa kama umeme uliokatika ghafra Temeke nzima walistushwa kwa kifo cha mmbabe
huyo sio Temeke tu Tandika Buguruni hadi Mbagara na vitongoji vyake. Watu wakazidi kujazana kuja nyumbani kwenye msiba ule hapo nikaweza kuwaona
ndugu zake feki wakilia kwa uchungu machozi ya kinafiki tu,
Hatimae tukaenda kumzika Madebe kwa heshima zote za dini yetu ya Kiislamu kwenye makaburi ya mtoni mtongani, tokea Madebe azikwe ni siku ya nne sasa
eti ndugu wanajadili mari za marehemu.
โwewe tena usiongee kabisa wakati marehemu yupo hai si ulimfukuza nyumbani kwako kama mmbwa afu leo hii unaitaji ugaiwe gari upati kitu hapa!”
โnani amekwambia sipati nisipopata patachimbika tu!
โkwanza tambueni ya kwamba sisi tunajadili mari tu ila tukae tukitambua ya kwamba marehemu enzi za uhai wake kuna kijana alikuwa anaishi nae kama ndugu
yake ambaye ni yule pale!”
โbwana ee huyo Kijana sisi atatusaidia nini kama aliye mfadhili kuishi keshaondoka kama vipi amfate kaburini”
sio siri maneno aliyokuwa akiyatamka Dada yule yakazidi kuuchoma moyo wangu ila nikapiga moyo konde tu nisije kutenda kitu cha ajabu, wakaulizana โsasa
naona tunapanga tu kugawana mali je Hati miriki nani anazo?” kila mmoja akanigeukia mimi yule Dada mwenye maneno ya Nyodo akaniuliza โwewe mbwa
tunaomba utupatie Hati miriki zote!”
Nikainuka pale nilipokuwa nimekaa nikiitaji kwenda kumfumua zinga la teke yule Dada nikakumbuka aya aliyo nisomea Marehemu kabla hajafa nikashusha
hasira na kuwaambia hivi โbinafsi hakuna hata mmoja wenu ninae mtambua hapa sasa basi Hati zote ziko katika mikono yangu na mimi ndio mrithi halali wa
mali hizi.
Nyie toeni mimacho tu binafsi alicho kizungumza huyu Mama ni ukweli mtupu ya kwamba lazima mnishilikishe mimi!”
Yule Dada akasema
โnadhani wewe kijana unijui sio sasa nakupa masaa 24 tu uwe tayali ushatoa Hati zote vinginevyo utakufa siku si zako!”
kwa nnje nikamuona yule Bibi muokota machupa ya maji akiniita nikatoka kwenda kumfata,
โShikamoo Bibi!”
โmarhabaa Baba yangu kwanza pole sana kwa kufiwa na ndugu yako!”
Hasante Bibi nishapoa ukizingatia wote njia yetu ni moja tu mbele yake nyuma yetu!”
โNi kweli kijana ila jiandae na vita vilivyoko mbele yako ni vizito sana, โBibi unasema!?
โni ukweli mtupu ninao kwambia yule binti mwenye kidomo domo ni Mchawi mwanga mkubwa tu usipokuwa makini atakupoteza ila kwakuwa mi nipo
nitakusaidia usijali!” baada Bibi yule kusema maneno yale akaondoka zake huku akiokota makopo tu nikarudi na kukuta mzozo tu,
Zile vurugu hazikuweza kunitisha kwa chochote kile. Nikabaki kuwatizama tu jinsi wanavyo tukanana.
Kisa mali za marehemu dahaa,
โNdio nishasema vyovyote itakavyo kuwa na iwe tu zile gari tatu ni za kwangu mimi!”
โwee tena ishia hapohapo yani uchukuwe gari zote tatu peke yako alafu sie wengine tugawane nini?”
โhilo mtajuwa nyie wenyewe nikiwa kama mtoto wa kiume na Kaka wa marehemu nastahiri kuchukuwa kila kitu!”
โendelea kujidanganya hivyo hivyo eti mtoto wakiume kama kidume kweli uliye kamilika utachukua ila nikiwa kama Mwanamke ninaye jielewa tena
nasimamisha kama unavyo simamisha wewe Yale magari tunagawana!”
Wakazidi kuzozana tu mpaka kufikia hatua ya kurushiana makonde dahaa aibu hii jamani ndio kwaanza. Marehemu kazikwa siku si nyingi kidonda kwenye moyo
wangu kikiwa bado kibichi nawaona ndugu zake sijui feki au original wana dundana.
Nilicho kifanya ni kuingia chumbani na kuchukua panga nikatoka nalo kwa kasi ya ajabu na kupangusa ukutani huku nikipandisha sauti
โkila mmoja atoke apotee ndani ya nyumba hii.
Wakataharuki na kuanza kukimbizana yule aliyekuwa anataka magari matatu akawa mbishi kutoka akasema โwee boya acha kunitishia panga Niko hapa kudai
haki yangu siogopi kitu!”
Ahaa kumbe aogopi ehee kwa kasi ya ajabu nikamtandika panga la mgongo ila nilitumia ubapa akapiga yowe la. Uchungu.
โjamani nakufaa akatoka mbio mpaka nnje nikawa namkimbiza wale ndugu wengine wakajuwa kumbe jamaa hatanii kila mmoja akatokomea zake na kuahidi
kunionyesha si najifanya mjanja nitaona tu.
Baada kupita siku kama tatu hivi tokea tukio la kuwatimua wale ndugu nikaanza kuotaota ndoto za ajabu usiku some time nakula mavi au nyama mbichi za
binaadamu nikiamka Asubuhi nakuwa nimechoka vibaya mno naweza nikawa nimelala upande huu wa kitanda nikija kushituka Niko chini ya kitanda au
uvunguni kabisa.
Nikaitaji kumtafuta Bibi baada kufahamu vita ndio vimeanza hivyo.
Hakika nilianza kuwa mnyonge sana, furaha sikuwa nayo
kabisa, Rahma akajitahidi kuniuliza nini tatizo sikuwa na jibu la kumpa.
โSalumu kipenzi changu mbona umeanza kukonda ghafla,
Au ndio kumuwaza ndugu yako
Madebe?”
Nilimtizama Rahma huku nikiwa nimeshika tama”โฆโฆ
akaniuliza tena,
โSasa baby ukikaa kimya utakuwa unitendei haki niambie nini tatizo
Ehee!”
akakishika kichwa changu kwa mikono yake miwili, mikono
rainii kisha akakiegemeza kichwa changu kifuani kwake.
Utasema mtoto ambaye anataka kunyonya”โฆโฆ
Nikajikunyata maana Rahma
ndio mwenye kunipa faraja kwa matatizo haya yanayo nisibu,
Washikaji nao hawakuacha
kunipa moyo na kuahidi watakuwa bega kwa bega pamoja nami katika vita hivi,
Siku hiyo nikiwa nafua nguo zangu nikiwa sina hili wala lile nikahisi kama mlango wa chumbani umefunguliwa na mtu kuingia ndani nikaacha kufua na kuingia
ndani kwa kunyata ajabu sikuweza kuona mtu. Nikasonya na kutoka zangu nnje ajabu nikamkuta Bibi kakaa kwenye kisturi nilipo muona nikafurahi sana.
Shikamoo Bibi!”
โmarhabaa mjukuu wangu kijana wangu mwenzako wiki hii yote nilikuwa naumwa kutwa kucha nipo ndani nikashindwa hata kujinyanyua niweze kutoka nnje!”
โDahaa pole sana Bibi yangu unaumwa nini?”
โMaralia ndio inayo nisumbua unionapo sijala chochote tokea juzi naishia kunywa maji tu!”
โDuhuu pole sana lakini hospital si umeenda au umemeza dawa tu?”
โmmh! uwezo tu wakununua chakula sina nitawezaje kwenda hospital au kununua dawa nilikata mualuvera nikaukamua nikanywa!”
Binafsi ni kweli Bibi hakuwa katika hali nzuri kihafya nikaingia ndani na kuandaa chai baada kuandaa kila kitu nikamkaribisha aweze kunywa chai akaingia ila
nikamsikia kama ameguna hivi kisha akasonya.
Nikataka kumuuliza ila nikanyamaza nisije kuzua mambo yasio nihusu.
Nikaenda nnje kuendelea kufua dakika kama tano hivi nikasikia ananiita.
“Wee Salumu”
Nikaenda kumsikiliza anasemaje baada kufika akaniambia kitu ambacho kilinistua sana
ITAENDELEA
Mzoa Takatakata Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;
