LYRICS

Dizasta Vina – Karibu Duniani Lyrics

ALBUM MP3 DOWNLOAD Dizasta Vina - A Father Figure MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina – Karibu Duniani Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled Karibu Duniani, a number eleven song from his album titled A Father Figure Album.

SIMILAR: Dizasta Vina t Dash – Mwanasesere

Karibu Duniani Lyrics by Dizasta Vina

Yeah
Huh

Nimekuleta duniani bila idhini
Tega sikio kwa makini nikueleze
Kabla hujabwaga manyanga chini
Nataka uijue hii ngoma ndo’ uicheze

Nikutoe utumwani
Hata uchague dini yako mwenyewe
Mimi baba yako, kwahiyo naomba nielewe
Hauwezi kupata mwingine
Kamwe usiendeshwe na pembe zako
Maisha yako yako mikononi mwako mwenyewe

Naomba uijue hali yetu
Umezaliwa na kuwa hapo ni safari ndefu
So, kipindi usiote ndefu
Usivimbe, ufumbue macho
Kisha uyatazame ya walimwengu… tazame ya walimwengu

Heshimu hili jina la ukoo
Linda kama jinsi unavyoilinda hii roho
Palipo uzalendo kuna moyo
Na uzalendo unaanza na kuwa loyal

Tabia ya upole ni shida kuisanifu
Lakini amani na hekima ndo’ majibu
Hasira picha ya karibu inayokuziba usione mbali
Kiasi uone tija kuinasibu

Sitakuwepo kukupeleka kwenye toy store
Ucheze nazo michezo kwenye korido
Uwe mpuuzi ushindwe cheza na books
Iwe nuksi kiasi uone revolution is not possible

Siahidi kuwa baba mkamilifu
Napambana japo mi ganda la udhaifu
Amani gharama usijingize kwenye bifu
Kosea ujifunze ili usiigize utakatifu

Kuna dini kama mia, mwanangu
Sijui ipi ni njia, mwanangu
Uifate ipi sina jibu
Ningemfata mola nimuulize
Mbingu ingekuwa ikaribu

Karibu duniani
Karibu duniani
Ah, karibu duniani

Kua ujue tofauti ya halisi na batili
Kuhakiki na kubashiri
Umasikini na utajiri usafiri
Uone tofauti ya usafi na ukafiri
Kisha ujiulize kama utaasi au utasawiri

Tupa uongo mwanangu, chukua tija
Funga mdomo mwanangu, fungua kichwa
Punguza mwendo, wengi walijifia kwa haraka
Kwa sababu ya kukaidi sheria na mamlaka

Ikumbuke hii siku, umekua baba
Uliyasikia majukumu leo umeyajua sasa
Mwanaume ulifichwa msosi tambua kwamba
Hauwezi kuheshimu kazi kama hujajua shamba

Kabla hujanishusha mi’ hadhi kumbuka
Nimekufunza, nimekufuta kamasi
Nimekuvisha kufuli, nimeahirisha shughuli
Utanizidi kiburi ila hauwezi ukaivuka tamati, mwanangu

Hamna urafiki na simba na mwanangu
Hata akikufundisha kuwinda mwanangu
Kuna siku atawinda kisha windo litamshinda
Atakosa nyama na utahitaji kumlinda, mwanangu — usiue

Mbivu, mbichi, ngumu, rahisi na nyepesi
Piga kitabu au uingie kijiji cha mapenzi
Mwanangu, ufuska utaua hadhi yako
Nimekupa vyote ninavyovijua — kazi kwako

Ukweli kuhusu hivyo vyama vya siasa
Chumba kimoja, usijedanganywa na vitasa
Zote game kama drafti drafti
Usishangae kuziona kamati zenye kamati

Pesa sabuni, zitafute kila siku
Ukipata usikate watu, mwenye fedha ndo’ ana kisu
Usisadiki kila tabasamu
Kati yao kuna halisi, kuna haramu
Dadisi upate fahamu

Karibu duniani
Karibu duniani

Asili haijali usawa, tambua hilo
Dunia ngumu, kuzaliwa tu ni kuwa hero
Hakikisha kisomo hakichezi mbali
So chunga ngono, chunga mikono, serikali

Kisha uache kuvamia michakato
Kama ambavyo ulikoma ziwa la mama yako
Cha ndege kiota cha mtu sumu
Ukiishi nacho bila macho
Mwanangu, utazikwa siku si zako, heeh

Usiwe mnyang’anyi, tafuta fungu lako
Ukidhurumiwa ujifunze kutokana na uchungu wako
Maana utashushwa na utundu wako
Poteza mali lakini usipoteze utu wako

Pata shida umjue ndugu thabiti
Kumjua ndugu si rahisi
Usidanganywe na uchungu wa dhiki
Pesa ni nguvu lakini hekima ni nguvu zaidi, ah

Ungali na afya, jiongezee ujuzi
Bahati ya jirani nayo usitembelee uchi
Usiegemee kuti, kuwa na nidhamu
Afu fadhiri binadamu ila usitegemee mchuzi

Kua uone michongo inapofeli
Mchungu muhogo muwa mmoko uliozamisha meli
Propaganda na zogo na chokochoko
Na utapewa uongo ili ujifunze kuiheshimu kweli

We Mwafrika hauko simple, una nguvu
Ni vile uliibiwa history na mzungu
Unachonena kinywani ni tija
Kuna mstari mdogo kati ya amani na vita

Penda kuwa na lugha nadhifu
Maneno thabiti yanaunda uaminifu
Acha masihara, kaza mwendo ado ado
Fanya ndoto kuwa malengo na malengo kuwa mpango

Goddamn, I’m a father now
Yeah
I can’t believe that I’m a father, how?
Nimeacha kushangaa shangaa, so
Nafanya kazi ukue, so you make your father proud

Rafiki adhimu ni kazi
Mweshimu kama unavyoheshimu wazazi
Mweshimu jirani, mbwa na binti yake
Binti ni mlezi, ukimuharibu jua umeharibu kizazi, mwanangu

Usijechoka kungojea
Kamali ni mbaya, usije omba kubobea
Wajanja walipotea, ogopa pombe na madawa
Maana mwili mmoja hauna spare

Karibu duniani
Karibu duniani
Karibu duniani

Dizasta Vina – Karibu Duniani Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment