STORY

‘shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 1

'Shetani' Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 2
‘shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 1

IMEANDIKWA NA : THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi : ‘shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10
Sehemu Ya Kwanza (1)

Ni kisa kinachomuhusu moja ya ‘wapigaji’ (tapeli) mashuhuri zaidi na aliyekuwa na mbinu mwanana kiasi cha kwamba namuweka katika kundi la “Wapigaji Daraja la Kwanza”. Huyu alikuwa ni mahiri kiasi kwamba alifanikiwa kuuza mara mbili mnara maarufu wa Eiffel ulipo jijini Paris kwa wafanya biashara wakubwa maarufu. Umahiri wake katika ‘upigaji’ uliwahi kutishia hata ‘afya’ wa mfumo wa kibenki na uchumi wa marekani.

Jina lake halisi imekuwa ni gumu kujulikana kwani kipindi cha uhai wake aliwahi kutumia zaidi ya majina 47 tofauti.. Pia alikuwa na hati za kusafiria za zaidi ya nchi 17 tofauti.
Maisha yake yaligubikwa na mlolongo wa uongo kiasi kwamba ni ngumu hata kujua asili yake na familia yake aliyotokea.
Lakini jina rasmi lililokubalika kumuita ili angalau kujua ni nani anayeongelewa lilikuwa ni Victor Lustig.

Victor Lustig

RELATED: ‘Shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 2

Leave a Comment