STORY

‘Shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 2

'Shetani' Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 2

Simulizi : ‘shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10

Sehemu Ya Pili (2)

Genesis’

Victor Lustig inaaminika na wengi kuwa alizaliwa Austria-Hungary (Czech Republic ya sasa) na akiwa katika umri wa makumi alihamia nchini Marekani.

Akiwa bado kijana Lustig alijiingiza katika ‘mishe mishe’ za mitaani za halali na haramu. Rafiki zake wanasema kwamba mwanzoni kabisa Lustig alijifunza michezo ya karata na akawa mahiri kiasi kwamba unaweza kudhani hakuna duniani mtu mwingine mwenye uwezo wa kuchezea karata kumshinda Lustig.

Lustig alimudu kwa umahiri kila aina ya ‘card trick’ (palming, slipping cards, dealing from the bottom n.k.). Kitu pekee ambacho labda kilimshinda ilikuwa ni kuzifanya karata ziongee, na kwa kuwa hilo haliwezekani basi yafaa kusema Lustig alikuwa ni ‘master’ wa michezo ya karata.

Kipindi hiki ilikuwa inakaribia miaka ya 1950 na ndio vitaa kuu ya pili ilikuwa inaishia, na uchumi wa marekani ulikuwa unakua kwa kasi kubwa sana na watu wa kipato cha kati na cha juu walikuwa wanaongezeka kwa kasi sana. Lustig akaiona fursa ya ‘malisho’ mapya ya maisha yake ya uhalifu na akaamua kujiingiza rasmi katika ‘upigaji’.

Kama nilivyoeleza katika makala mbali mbali kuwa wahalifu wengi wa Daraja la kwanza huwa wanakuwa na falsafa wanayoiamini na kuwaongoza. Kwa mfano Pablo alijiongoza kwa Sera ya ‘Plata O Plomo’.

Lustig kwa upande wake pia alikuwa na falsafa aliyoiamini na kuifuata na kumfanya kuwa pengine ndiye ‘mpigaji’ mashuhuri zaidi katika historia ya ulimwengu..

Katika vitabu vya dini Mwenyezi Mungu aliwapa wanadamu amri kuu 10 za kuwaongoza kuishi maisha matakatifu, lakini yeye Lustig alijiwekea amri kuu 10 za kumuongoza kufanikisha Utapeli.

Amri hizo alizojiwekea zilikuwa ni hizi;

1. Kuwa msikilizaji makini (hii ndio sifa inayofanikisha utapeli, sio kuongea sana.

2. Usijionyeshe Umeboreka (never look bored)

3. Muache unayeongea naye aonyeshe mlengo wake wa kisiasa kisha kubaliana nae.

4. Muache unayeongea naye adhihirishe imani yake ya dini, kisha jifanye una imani sawa naye.

5. Gusia maongezi ya kimpenzi, lakini usiingie ndani sana isipokuwa tu pale unayeongea naye akionyesha kupendelea maongezi hayo.

6. Kamwe usigusie mazungumzo ya magonjwa au ugonjwa isipokuwa tu kama kuna ulazima wa kuzungumzia.

7. Kamwe usilazimishe kutaka kujua mambo binafsi ya unayeongea naye (kuwa mvumilivu kadiri unavyoongea naye ataropoka mwenyewe)

8. Usijisifu au kujikweza – acha umuhimu wako ujidhihirishe wenyewe.

9. Usiwe na muonekano rough (mchafu/hovyo hovyo)

10. Usilewe.

Hizi ndizo amri kuu 10 za Bw. Lustig alizozifuata na kumuongoza katika maisha yake na kumfanya kuwa ‘mpigaji’ mashuhuri zaidi katika historia..

ITAENDELEA

‘Shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 3

Leave a Comment