STORY

‘Shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 3

‘Shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 3

‘Shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 3

Simulizi : ‘shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10

Sehemu Ya Tatu (3)

Mashine ya kuprint noti na Kuuza mnara wa Eiffel.

Moja ya matukio ya kukumbukwa zaidi yaliyofanywa na Lustig ilikuwa ni kuwauzia watu Mashine ya kuprint noti za dola ya Marekani.

Waliouziwa hawakuwa wajinga kiasi kama unavyoweza kuhisi bali Lustig alikuwa anatumia akili ya ziada ambayo mtu aliyekuwa anatapeliwa abadani asingeweza kutia shaka kwa muda huo.

Kama tunavyofahamu kuwa kuna meli za starehe ambazo watu hupanda pale wanapokuwa mapumziko kwa ajili ya kuvinjari tu (Cruise Ships). Lustig alipendelea zaidi meli za starehe zilizokuwa zinasafiri kutoka New York mpaka Jijini Paris ufaransa. Abiria wa meli hizi walikuwa ni watu wenye kujiweza kwa kipato na hii ilimvutia zaidi Lustig.

Lustig alikuwa akishakupanda katika meli, alitumia masaa kadhaa kufanya upembuzi wa abiria gani amtapeli. Akishakupata mtu wa kumtapeli kwa kutumia uwezo wake wa hali ya juu wa kujieleza na kumteka mtu kwa maongezi alikuwa anamuita Chemba na kumuonyesha kiboksi kidogo cha saizi ya kati ambacho kwa ndani kinakuwa na mfumo complex na kina vitufe vya kubonyeza kwa juu. Kiboksi hiki alikitengeneza kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba kinadanganya macho na mtu kuamini kuwa kuna sayansi ya hali ya juu imetumika kukitengeneza.

RELATED: AAAH! SHEMEJI

Kisha Lustig alikuwa anampa mtu maelezo kuhusu kiboksi hicho kuwa kina mfumo maalumu pamoja ya madini ya ‘Radium’ ambapo kina uwezo wa kucopy noti za dola 100 za marekani kwa usahihi wa 100%.

Ili kuthibitisha hilo Lustig aliweka vipande kadhaa vya karatasi zenye rangi nyeusi ndani ya kiboksi hicho na kusubiri kwa muda kadhaa ambapo kiboksi hicho kinaprint fedha halali kabisa noti ya dola 100 ya marekani.

Kisha Lustig anamueleza zaidi kuwa kiboksi hicho kina uwezo wa kuprint noti moja ya dola 100 kwa kila masaa 6. Kutokana na mtu kuhisi kuwa atapata faida kubwa akiwa na kiboksi hicho chenye uwezo wa kumpatia dola 100 kwa kila masaa 6 pasipo kuvuja jasho hivyo walikuwa wakinunua kwa moyo mkunjufu kabisa na Lustig aliwauzia kiboksi hiki kwa dola elfu thelathini za marekani kwa kiboksi kimoja

Kumbuka hapa wako ndani ya meli inayosafiri kuelekea Paris, Ufaransa kwahiyo huyu mtu akishanunua kiboksi baada ya masaa sita kiboksi kile kitaprint noti ya dola 100, baada ya masaa sita mengine kitaprint noti nyingine ya dola mia.. Lakini baada ya hapo kitaanza kuprint karatasi za kawaida nyeusi na hapa ndipo mtu hushituka kuwa amekwisha tapeliwa lakini kwa muda huu meli inakuwa imeshafika Paris na Lustig ameshashuka kwenye Meli na kutokomea.

Eiffel Tower: mnara uliouzwa mara mbili na Lustig kwa wafanyabiashara mashuhuri jijini Paris.

Kuna siku Lustig alikuwa Paris, akiwa ameshashuka kwenye meli baada ya kumuuzia mtu mashine ya kuprint hela. Katika mizunguko yake akakutana na habari kwenye gazeti ambayo ilimsisimua. Habari hii ilikuwa inahusu taarifa ya serikali ikizungumzia kuhusu ni jinsi gani ilivyokuwa inaingia gharama kubwa kutunza mnara wa Eiffel.

Makala hii lengo lake hasa ilikuwa ni serikali wanajitetea baada ya raia kulalamika kuwa serikali hawako makini kuutunza mnara huo kwani umekuwa mkuu kuu na haupendezi tena. Katika makala hiyo serikali ilijitetea kuwa hata kuupaka rangi mnara huo ni gharama kubwa mno kwahiyo wananchi wawe wapole tu.

‘Shetani’ Mtanashati Na Amri Kuu 10 | Ep 3

Leave a Comment