STORY

Adam na Hawa Ukweli Kuhusu Tunda

Adam na Hawa Ukweli Kuhusu Tunda, Usaliti na Siri Nyingine Nyingi
Adam na Hawa Ukweli Kuhusu Tunda, Usaliti na Siri Nyingine Nyingi

JE ADAMU NA HAWA WALIKULA TUNDA GANI BUSTANI YA EDENI?

Watu wengi hufikiri kwamba tunda ambalo Adamu na Hawa waliambiwa wasile katika bustani ya Edeni lilimaanisha uhusiano wa kingono. Lakini Biblia haifundishi hivyo.

Hebu fikiria hili: Hata kabla Hawa hajaumbwa, Mungu alimwamuru Adamu asile matunda ya “mti wa ujuzi wa mema na mabaya.” (Mwanzo 2:15-18) Amri hiyo haikumaanisha uhusiano wa kingono kwa sababu Adamu alikuwa peke yake. Zaidi ya hayo,

Mungu aliwapa Adamu na Hawa amri hii iliyo wazi: “Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia.” (Mwanzo 1:28).

RELATED: Kanumba Alivyojiunga Freemason

Je, Mungu mwenye upendo angewapa wenzi hao wa ndoa agizo la ‘kujaza dunia’ – jambo ambalo bila shaka, lingehusisha uhusiano wa kingono – kisha awahukumu kifo kwa kutii maagizo yake? – 1 Yohana 4:8.

Kwa kuongezea, Adamu hakuwepo Hawa ‘alipoanza kuchukua na kula kati ya matunda aliyokatazwa. Baadaye alimpa mume wake pia alipokuwa pamoja naye, naye akaanza kula.’ Mwanzo 3:6.

Mwishowe, Mungu hakuwahukumu Adamu na Hawa walipofanya ngono na kuzaa watoto. (Mwanzo 4:1,2) Kwa hiyo ni wazi kwamba tunda ambalo Adamu na Hawa walikula halikumaanisha tendo la kufanya ngono bali lilikuwa tunda halisi lililokuwa mtini.

DOWNLOAD MP3

Leave a Comment