LIFESTYLE

Namna Sahihi ya Kuongea na Mpenzi Wako

Namna Sahihi ya Kuongea na Mpenzi Wako
Namna Sahihi ya Kuongea na Mpenzi Wako
Unapo-chat Na Girlfriend Wako Kwa Staili Hii:

Wewe: Oya!
Yeye: Nambie!
Wewe: Mzima!
Yeye: Mi Mzima Ww Je?
Wewe: Niko Poa
Yeye: Ok

Isikupite Hii: Makosa 7 Usimfanyie Mwanamke Wako

Kuna Jamaa Mwingine Yuko Online Ana-chat na Msichana Huyo Huyo Kwa Staili Hii:

Jamaa: Mambo Vipi Mrembo?
Msichana: Poa Mzima Wewe?
Jamaa: Mi Niko Poa Kabisa Halafu Ninapopata Bahati Ya Ku-chat Na Wewe Hata Kama Nilikuwa Najisia Hovyo Afya Yangu Huimarika Ghafla.
Msichana: Mh! Kivipi Yani?
Jamaa: Uzuri Wako Tu Kwangu Ni Dawa Tosha.
Sio Siri Mungu Kakupendelea Sana Rafiki Yangu.
Msichana: Dah! Yaani Rafiki Yangu Huishi Kunifurahisha Asubuhi Yote Hii Ushaanza Kunipamba.
Ujue Maneno Yako Yatanifanya Niringe Wakati Sistahili.
Jamaa: Hapana Unastahili Kabisa Kuringa Wangu!
Kweli Wewe Ni Mzuri Wala Sio Uongo Ila Sema Tu Wewe Hujioni.
Msichana: Mh! Sawa Bana Asante.
Jamaa: Ila Wangu Ujue Nini? Uongo Mbaya Mi Nakupenda
Sipati Picha Ni Furaha Kiasi Gani Nitakuwa Nayo Pale Utakaponifanya Mwenye Bahati Ukaamua Kunipa Nafasi Ya Kuwa Na Wewe.
Msichana: Hapana Wangu Mi Tayari Nipo Kwenye Mahusiano Ila Ukweli Ni Kwamba Huwa Najisikia Furaha Sana Pale Ninapo-chat Na Wewe.
Jamaa: Unastahili Kuwa Na Furaha Malaika Wangu!
Kwasasa Wacha Nikutakie Siku Njema.
Nataka Nifanye Kazi Moja Hivi Ntakustua Baadae.
Msichana: Asante Sweetie! Ntakumiss Muda Ambao Hautakuwepo Hewani
So Usikawie Kurudi Online Sawa Eh?

Soma: Siri kuu 6 za kumpata mpenzi bora

Unaweza kusema “huyu mwanamke ni cheap analainishwa kwa maneno tu”!
Lakini ukweli ni kwamba wanawake kwa ujumla wapo hivyo. Siku zote wanapenda kusikia maneno matamu kutoka kwa wapenzi wao:

Wakati mwingine unaweza kujikuta una pesa na ni mtaalamu wa kuhonga lakini bado mpenzi wako akachukuliwa na jamaa asiyekuwa na pesa kisa maneno laini laini.
Hivyo basi epuka kuzungumza/ku-chat na mpenzi wako kana kwamba una-chat na mshkaji wako wa kijiweni.

Huyo ni mwanamke unapaswa kumbembeleza la sivyo atachukuliwa na wanaojua kunyenyekea.
Mwisho naomba nikwambie moja katika ya mistake kubwa ambazo hupaswi kufanya ktk mahusiano nikuacha mwanya mshkaji mwingine akachukua nafasi ya kumfurahisha mpenzi wako.
Nadhani imeeleweka.

Siku Njema Wapendwa Wangu

Leave a Comment