LIFESTYLE

Maswali 9 Ya Kuzingatia Kabla Kuingia Katika Mahusiano

Maswali 9 Ya Kuzingatia Kabla Kuingia Katika Mahusiano

Kuingia katika mahusiano mapya baada ya kutoka katika mahusiano yaliotangulia si jambo la rahisi. Wengi huchukua muda mwingi hadi wajipate wameingia katika mahusiano mapya.

Watu wengi ambao hujipata wametoka katika mahusiano kwa kawaida huwa wamepitia mengi. Labda mahusiano hayo ya awali yalikuwa ya vita, uongo, kudanganyana ama kucheat. Hivyo kuingia katika mahusiano mapya yanahitaji muda kwanza ili uweze kuuguza kidonda cha moyo ambacho utakuwa umepitia.

Maswali 9 Ya Kuzingatia Kabla Kuingia Katika Mahusiano
Je Ex wako ushamtoa akilini?

Hili ni swali muhimu la kujiuliza kabla kuingia katika mahusiano mapya. Hii ni muhimu kwa kuwa si jambo la busara kuingia katika mahusiano mapya ikiwa bado unamfikiria Ex wako.

Umeboeka?

Wengine huingia katika mahusiano kwa sababu wameboeka na maisha ya upweke. Aina hii ya watu hujikuta katika mahusiano mapya ili waweze kupata kuburudishwa. Hii haifai kwa sababu ni muhimu kwako wewe kujikubali kimaisha hivyo kuwa katika mahusiano hakufai kuwa kigezo cha kuyachangamsha maisha yako yanayoboa.

Je unajifanyia mambo wewe mwenyewe?

Swali hili wengi hulipuuza kwa kuwa hawaoni umuhimu wake. Lakini hili ni swali muhimu la kujiuliza. Mtu hafai kuingia katika mahusiano kama yeye wenyewe hajiangalii kimaisha.

Ni lini ulijipeleka out, kula chakula cha afya, kufanya mazoezi katika gym, kusoma kitabu au chochote kile ambacho kinakusisimua ndani yako? Kama hujafanya lolote katika haya basi hufai kuingia katika mahusiano mapya. Kama huwezi kujiangalia wewe mwenyewe je mwingine utaweza?

Isikupite Hii: Maswali 8 Mazuri ya Kumuliza Mpenzi Wako Wakati wa Kuchati.

Unajua ni kitu gani kilichovunja uhusiano wako wa awali?

Kabla hujaingia katika mahusiano mapya swali hili unafaa uwe umejiuliza mara kwa mara. Ni muhimu kujua kosa lililofanyika katika mahusiano yako ya awali ili uweze kurekebisha kosa kama hilo wakati ambapo utajikuta katika mahusiano mapya. Hilo ni muhimu sana kuzingatia.

Ulijifunza nini katika mahusiano yaliyotangulia?

Kila mahusiano ambayo mtu huingia kawaida hujifunza mambo mapya. Hivyo kabla kuingia katika mahusiano mapya unafaa ujue yale mafunzo ambayo umeyashuhudia katika mahusiano yako yaliyotangulia. Hii itaboresha mahusiano yako mapya

Je unajipenda binafsi.

Hili ni swali muhimu la kujiuliza. Na kama hujipendi wewe binafsi inamaanisha ya kuwa hauko tayari kuingia katika mahusiano mapya.

Isikupite Hii: Maneno 6 ya kumfurahisha mpenzi wako

Je unatafuta mtu akufurahishe?

Kama lengo lako kuu la kuingia katika mahusiano mapya ni kupata mtu akufurahishe basi hauko tayari kuingia katika mahusiano mapya. Mahusiano yana malengo zaidi ya kujifurahisha so kwako itakuwa una safari ndefu ya kutembea ili ujue umuhimu wa mahusiano.

Je kuna jambo ambalo lilikutokea bila kutarajia?

Wakati mwingine watu hujikuta wameingia katika mahusiano kwa kuwa kuna tukio limewakumba bila kutarajia. Labda ni kupata janga, kukosana na marafiki, kuachwa ama hata kufiwa na umpendaye.

Ukijipata katika hali hii halafu ghafla unataka kuingia katika mahusiano mapya si jambo la busara. Hii ni kwa sababu umechukua hatua ya kuingia katika mahusiano bila kuangalia madhara au umuhimu wake.

Je unajua kwa nini unataka kuingia katika mahusiano?

Swali hili ni muhimu kujiuliza kwa sababu wengi wanaweza kuingia katika mahusiano bila ya hata kujua madhumuni ya kuingia katika mahusiano hayo. So kama hujui dhamira ya kuingia katika mahusiano mapya basi pia si muhimu kuingia ndani yake kama kipofu.

Ngoma 10 Bora za Mwezi may, 2020.

Leave a Comment