NJIA 8 za KUMWACHA mpenzi wako kwa AMANI.
LIFESTYLE

Njia 8 za kumwacha mpenzi wako kwa amani.

NJIA 8 za KUMWACHA mpenzi wako kwa AMANI.
NJIA 8 za KUMWACHA mpenzi wako kwa AMANI.

iko njia mbili tu ambazo uhusiano baina ya wapenzi wawili utaandika historia. Ama uhusiano utadumu hadi kifo kiwatenganishe ama utavunjika. Hata hivyo uzoefu unaonyesha kuwa kwa walio wengi hawajaweza kuwa kwenye uhusiano wa kudumu, wanakuwa wamepitia katika mahusiano mengine na hivyo kupitia awamu Fulani Fulani za kuvunja mahusiano.Na kuna namna mbili ambazo uhusiano utavunjika. Ama kwa amani ama kwa ugomvi.

Isikupite Hii: Jifunze faida za kummsis mpenzi wako kwenye mahusiano.

Kumaliza mahusiano si kitu rahisi sana hata kama ni hakika umemchoka mwenzi wako na hata kama uhusiano wenu si mzuri kiasi kwamba uko tayari kuwa huru. Kwa hiyo basi, kuvunja mahusiano ya kimapenzi ni jambo ambalo haliwezi kuepukika. Hata hivyo kumaliza mahusiano kwa amani ni vizuri na inapendeza kuliko kuumaliza kwa ugomvi na jazba. Kumbuka “The Golden Rule”: Kwamba ungekuwa ni wewe ungependa uachwe vipi? Kama upo katika mahusiano yasiyo na tija na unafikiri kwamba imefika wakati unahitaji uhusiano wenu uvunjike, basi dondoo zifuatazo zitakusaidia kumaliza mahusiano na mpenzi wako kwa amani. Kitu kimoja kikubwa cha kuzingatia ni kuweka Jazba pembeni:


1. Kuwa Na Uhakika Na Unachotaka Kufanya

Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti aka “Maamuzi magumu”. Kama una hisia naye pia itamfanya achanganyikiwe na ajisikie kuwa bado anayo nafasi ya kuwa na wewe ama anaweza akaamua na yeye kukukomoa na kukuacha kabisa wakati kumbe bado una hisia za mapenzi na yeye . Hata hivyo kama una uhakika kwamba ni kweli hauutaki uhusiano uliopo basi kuwa tayari kukata kabisa mahusiano yenu la sivyo kuwa tayari kukiona cha moto . . . maana utakuwa unachezea hisia zako

2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano

Uhusiano unapovunjika mara nyingi ndugu, jamaa na marafiki wanapenda kujua sababu. Unapojua sababu zinazopelekea wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale unapoulizwa. Pia itakusaidia kumaliza mahusiano katika namna njema. Hata kama mwenzi wako hataamini au ataamini juu ya kuvunjika kwa uhusiano wenu, kuwa honest au mkweli ni muhimu. Mweleze unahitaji kusonga mbele na maisha yako bila yeye na mjibu maswali yote kwa uaminifu. (Fikiria huko nyuma kama uliwahi kuachwa bila sababu ulivyojisikia)

BOFYA HAPA KUENDELEA Njia 8 za kumwacha mpenzi wako kwa amani.

Leave a Comment