SIMULIZI

Ep 1: Top Secret Namba 12333 Kutoka Whitehouse

SIMULIZI Top Secret Namba 12333 Kutoka Whitehouse Ep 1
SIMULIZI Top Secret Namba 12333 Kutoka Whitehouse Ep 1

IMEANDIKWA NA : THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi : Top Secret: Nyaraka Namba 12333 Kutoka Whitehouse
Sehemu Ya Kwanza (1)

“Deception is a state of mind and mind of the State.”

James Angleton

CIA Chief of Counterintelligence (1954 – 1975)

Alhamisi March 13, 1953 Washington D.C

“Put that away.” Hiyo ndiyo ilikuwa sentesi ya kwanza Rais Dwight Eisenhower kuitamka mara baada ya kuingia ndani ya Oval Office katika makazi yake ya White house.

Alitamka maneno hayo mara baada ya kumuona moja ya wageni wake waliokuja ofisini kwake anatoa makaratasi kutoka kwenye briefcase.

Huu ulikuwa mtindo wa Rais Eisenhower pale anapotaka kuongea na mtu mambo ya siri nzito na akiwa hana mpango wa kuwashirikisha Baraza la Mawaziri au Baraza la Ulinzi.

Kikao hiki kilikuwa ni kikao cha siri kubwa na kilihusisha washiriki watatu tu. Rais Dwight Eisenhower na wageni wawili ambao walikuwa ni ndugu. Mtu na kaka yake.
Mmoja aliitwa John Foster Dulles ambaye alikuwa ni Waziri wa mambo ya nje wa Marekani na Wapili aliitwa Allen Dulles ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Shirika ka kijasusi la Marekani, CIA.

Eisenhower alikuwa na utaratibu wa kutotaka kuwepo na aina yoyote ya nyaraka inaweza kuihusisha ofisi ya Rais pale ambapo akitaka kuamuru ifanyike jambo amblo alihisi linaweza lisiungwe mkono na jamii ya kimataifa. Na hii ndio ilikuwa sababu ya kumuamuru Allen Dulles arudishe makaratasi yake kwenye briefcase.

Wiki tatu zilizopita kilifanyika kikao kama hiki kati ya watatu hawa na katika kikao hicho walizungumza juu ya changamoto kubwa iliyokuwa mbele yao.
Changamoto yenyewe ilikuwa ni Mohammad Mosaddegh, Waziri Mkuu wa Iran.

Miaka miwili iliyopita serikali ya uingereza walituma ombi Marekani kuwaomba wawasaidie kuandaa mpango kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Mosaddegh mara baada ya kufanikiwa kushinda uchaguzi wa mwaka 1951. Kipindi hicho Rais wa Marekani alikuwa na Harry Truman na akakataa kuihusisha marekani katika suala hilo.

Baada ya Rais Truman kuondoka madarakani na Dwight Eisenhower kuchukua madaraka, Serikali ya Uingereza chini ya waziri mkuu Winston Churchhill wakajaribu tena kushawishi serikali mpya ya Marekani kuwaunga mkono kumuondoa madarakani Waziri Mkuu Mosaddegh.

Wasiwasi mkubwa wa Uingereza dhidi ya Mosaddegh ulikiwa ni mwenendo wa wake dhidi ya kampuni za kimagharibi na hasa hasa namna ambavyo aliiandama kamupuni ya AIOC (Anglo-Persian Oil Company (kwasasa kampuni hii ni sehemu ya kampuni ya BP)).

Kampuni hii ambayo ilikuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya serikali ya Uingereza na serikali ya Iran. Lakini kwa mujibu wa mkataba mapato yote yalikuwa yanaenda kwa serikali ya uingereza na serikali ya Iran ingeanza kupewa mapato mara tu kampuni ikianza “kujiendesha kwa faida” ambapo serikali ya Iran itapatiwa 16% ya mapato.

Lakini kwa miaka yote Waingereza walihakikisha rekodi za kampuni zinaonyesha kuwa kampuni inaendeshwa kwa hasara ili wasiwe wanalipa 16% kwa serikali ya Iran.

Baada ya Waziri Mkuu Mohammad Mosaddegh kushinda uchaguzi mkuu wa kwanza wa kidemokrasia nchini humo mwaka 1953 akatoa pendekezo kuwa vitabu vya uhasibu vya kampuni ya AIOC vifanyiwe ukaguzi kujiridhisha kama kweli kampuni inaendeshwa kwa harasa. Waingereza wakakataa.

Mosaddegh akatoa ofa nyingine kuwa mkataba uandikwe upya na uwape serikali zote mbili umiliki wa 50/50 wa kampuni ya AIOC. Waingereza wakakataa pia.

Ikumbukwe kuwa kutokana na mkataba huo visima vyote vya mafuta ndani ya nchi ya Iran vilikuwa chini ya kampuni ya AIOC.

Katika kipindi hiki Iran ilikuwa ni moja ya nchi masikini zaidi duniani.
Hii ilimaanisha kuwa wananchi wa Iran walikuwa wanaishi kwenye moja ya nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta lakini wenyewe wapo kwenye lindi la umasikini.

Ndipo hapa ambapo baada ya juhudi zake zote za kwanza kuleta uwiano juu ya unufaikaji wa mapato ya kampuni ya AIOC kushindikana, Waziri Mkuu Mosaddegh akapeleka muswada bungeni wa kuitaifisha kampuni ya AIOC.

Hapa ndipo akaamsha hasira za Uingereza na wakaweka nia kwamba ni lazima Mosaddegh aondoke madarakani. Kikwazo kikubwa kilikuwa ni kwamba Mossadegh alikuwa amechaguliwa kidemokrasia kwa kupigiwa kura na alikuwa anakubalika mno na wananchi wa Iran.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndipo hapa wakaona umuhimu wa kuwaomba ‘kaka zao’ wamarekani wawasaidie kutimiza amza yao.
Kipindi Marekani ilikuwa iko kwenye vita nchini Korea na Uingereza ilikuwa inawaunga mkono katika vita hiyo kwa kuchangia wanajeshi. Hivyo Uingereza waliamni ombi lao hili kwa Marekani litapata kibali safari hii.

Turejee kwenye kikao Whitehouse..

Wiki tatu nyuma katika kikao chao cha kwanza Rais Eisenhower alikuwa amewapa ‘homework’ wakaandae mkakati ambao watakuja kuuwasilisha leo hii.

Ndipo hapa ambapo Mkurugenzi wa CIA Allan Dulles akaanza kumpa mkakati alioufikiria.

Kwanza akaanza kumpa tahadhari kadhaa za kuzingatia kuhusu mpangi ambao watauweka.

  • mpango huo ni vyema usijadiliwe kwenye Baraza la Mawaziri au Baraza la Usalama wa Taifa, kwasababu lazima utazua mtafaruku mkubwa kwasababu ni dhahiri baadhi ya watu wataupinga.
  • pia kama ni watu wachache wataufahamu hii ina maana uwezekano wa siri kuvuja utakuwa ni mdogo.
  • Pia Allan Dulles akashauri ni lazima oparesheni hii itekelezwa pasipo watu kujua kuna uhusika wa marekani ili kufanya wananchi wa marekani kukubaliana na serikali mpya itakayo wekwa kama ikitokea oparwsheni ikafanikiwa.

Kwa kuzingatia hayo basi, Allan Dulles akamshauri Rais Eisenhower atumie mamlaka yake aliyopewa na sheria ya usalama wa taifa ya mwaka 1947 (U.S. National Security Act, 1947), kuidhinisha operation ya usiri mkubwa zaidi (Covert operation) kumpindua Rais Mohammad Mosaddegh.

Sheria hii inampa mamlaka Rais wa Marekani kuamuru kufanyika kwa “covert operation” pasipo kumuweka Rais kutambuliwa uhusika wake kwenye hilo ikitokea siri ya operation hiyo imevuja.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa maneno mengine Sheria hii inampa uwezo Rais kukana kuhusika kuamuru oparesheni kufanyika au kufahamu chochote juu ya kufanyika kw oparesheni hiyo ikitokea siri imevuja kuhusu oparesheni hiyo. Hii ndio inajulikana kama ‘Plausible Denialbility’.

Kwahiyo; kwa kuzingatia vigezo vyote hivi ambavyo Allan Dulles mkurugenzi wa CIA aliviainisha, akawaeleza Rais Eisenhower na kaka yake John Dulles waziri wa mambo ya nje kuwa ni idara moja tu katika vyombo vyote vya ulinzi na usalama ndani ya Marwkeani yenye weledi, uwezo, watu, ufanisi na ruhusa ya kisheria kutekeleza mkakati wa dizaini hii.

Idara hiyo ni kitengo maalumu ndani ya CIA kinachojulikana kama SAD (Special activities Divisio).

ITAENDELEA

Leave a Comment