Kuna mambo ya msingi ambayo mwanamke anahitaji kutoka kwa mwanamme ili kufurahi na kutulia katika mahusiano japokuwa sio rahisi kukwambia mojakwa moja.Na endapo utasoma na kufwata mafundisho haya lazima mwanamke wako hatokusahau hata kama mkiachana
MAMBO 6 YA KUMFANYIA MPENZI WAKO ASIKUSAHAU MILELE
Kuridhishwa Kwenye tendo la ndoa
Mwanamke anapenda aridhishwe Kwenye tendo la ndoa. Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako. Utundu na ufundi unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako. Mwanamme anatakiwa kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo.
Kuheshimiwa
Wanawake wanapenda kueshimiwa kwa maneno na matendo. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, Malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya. Wanawake hawapendi kukosewa heshima hasa mbele za watu, hata kama ni kwa mambo madogo madogo.
Kupewa nafasi na kipaumbele.
Wanawake wanapenda kuwa namba moja au kupendwa kuliko yeyote. Kumpenda mwanamke haikuishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Wanawake wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla na katika maisha yao.
Isikupite Hii: Njia 6 ya Kumzuzua Mwanamke Mpaka Akupende
Nafasi ya kuongea na kujieleza
Wanawake wanapenda wapewe nafasi ya kuongea na kujieleza vile watakavyo. Mpe uhuru mpenzi wako kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali pale anapoongea sana. Kwa kawaida wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, wakati wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine. Kwa hiyo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao.
Kusaidiwa katika shida na matatizo yao
Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo. Kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo. Kama mwanaume hatamfanyia mpenzi wake hili atakuwa amekosa sifa za kuteka penzi la mwanamke.
Kujaliwa Na Kubembelezwa
Wanawake hupenda kubembelezwa hasa pale wanapokuwa na huzuni. Wanawake wengi hupenda kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa. Wanawake hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.
Hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine. Ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa.
Isikupite Hii: Sababu 4 za wanaume kuumia zaidi kwenye mapenzi.