LYRICS

Hussein Machozi – Jela

Hussein Machozi – Jela Lyrics
Hussein Machozi – Jela Lyrics

Bora nirudi jela
Bora nirudi jela
Bora nirudi jela
Bora nirudi jela

Miaka kenda imepita tangu nifungwe jela
Kosa nilisingiziwa nimekula pesa ya umma
Niliacha familia mke wangu na mtoto mmoja
Leo Jumatano siamini umepita msamaha wa raisi
Katika ya watu ishirini walioachiwa nilikuwepo na mimi
Vitu vyangu nilikabidhiwa tayari nishakuwa raia
Huko nje sikujua mambo yalivyobadilika
Laiti ningelijua bora ningebaki jela ah

Jela jela aah (bora nirudi jela)
Aa haa nimeshindwa nimeshindwa mie (bora nirudi jela)
Kipande cha sabuni 950 (bora nirudi jela)
Nambie kilo ya unga itakuaje (bora nirudi jela)

Kila nilipopita watu walinishangaa
Kumbe mavazi nilovaa wakati wake ushapita
Safari yangu haijaisha nyumbani kwangu naelekea
Na hamu ya kumuona mke wangu na mwanangu Mwamvita
Nilitaka kuzimia mbele macho yangu nilichokiona
Pale nyumba yangu ilipokuwa limejengwa bonge la ghorofa
Nilijaribu kuuliza mmiliki ni kigogo mmoja
Kumbe sio eneo tu pekee anamiliki na yangu familia

Jela jela aah (bora nirudi jela)
Aa haa nimeshindwa nimeshindwa mie (bora nirudi jela)
Kipande cha sabuni 950 (bora nirudi jela)
Nambie kilo ya unga itakuaje (bora nirudi jela)

Wakati nikizubaa getini mwa lile ghorofa
Geti lilifunguliwa ilitoka Lexus mayai iih
Dereva alikuwa ni mwanamke
Mbona sura yake kama naijua vile
Oh my God Ni mama Mwamvita cheki alivyobadilika
Hanitambui tena aah inaumaa
Hanitambui tena aah bora nirudi jela

Jela jela aah (bora nirudi jela)
Mh mh nimeshindwa nimeshindwa mie (bora nirudi jela)
Kipande cha sabuni 950 (bora nirudi jela)
Mh mh nambie kilo ya unga itakuaje (bora nirudi jela)

Jela jela aah (bora nirudi jela)
Mh mh nimeshindwa nimeshindwa mie (bora nirudi jela)
Kipande cha sabuni 950 (bora nirudi jela)
Mh mh nambie kilo ya unga itakuaje (bora nirudi jela)

Hussein Machozi – Jela Mp3 Download

Also, check more tracks from Harmonize;

Leave a Comment