Mwanamuziki (Dalida) aliekuwa anaua wapenzi wake
LIFESTYLE

Mwanamuziki (Dalida) aliekuwa anaua wapenzi wake

Mwanamuziki (Dalida) aliekuwa anaua wapenzi wake

Majina yake kamili ni Iolanda Cristina Gigliotti maarufu kama Dalida. Yeye alizaliwa Cairo Egypt mwaka 1933, baadaye mwaka 1956 akahamia Ufaransa kuendeleza carrier yake ya muziki na mitindo. Kabla ya kuhamia Ufaransa alikuwa amechukua taji la Miss Egypt mwaka 1954.

Desemba 1967 Dalida alipata ujauzito wa mwanafunzi wa Kiitaliano mwenye umri wa miaka 22, Lucio. Dalida alitoa mimba hiyo hali iliyomfanya kuwa tasa.

Septemba 1970 mume wake wa zamani (1956–1961) Lucien Morisse, ambaye walikuwa na uhusiano mzuri naye, alikufa kwa kujiua, alijipiga risasi kichwani.

Aprili 1975 mpenzi wake, mwimbaji Mike Brant alijirusha kutoka ghorofani huko Paris hadi kifo. Alikuwa na umri wa miaka 28. Dalida alikuwa amechangia mafanikio ya Mike kwa asilimia kubwa, Dalida ndiye alimtoa kimuziki Mike mwaka wa 1971 alipompandisha katika tamasha kubwa la Olympia.

SIMILAR: Mwanamke Mwenye Mvuto zaidi Anaishi Duniani Kwa Sasa

Julai 1983 mpenzi wake wa miaka 9 (1972-1981), Richard Chanfray, alikufa kwa kujiua mwenyewe kwa kuvuta gesi ya moshi ya gari lake aina ya Renault 5.

Swali alilokuwa anateswa nalo Dalida miaka yote ni kwamba kwanini kila mtu wake wa karibu hasa katika mapenzi anaishia kujiuwa mwenyewe? Jibu alilolipata ni kwamba labda yeye ndio sababu.

Usiku wa kuamkia tarehe 3 Mei 1987, Dalida alijiua kwa kuzidisha kipimo cha dawa zenye nguvu huku akiacha karatasi iliyokuwa na ujumbe wa kifaransa uliosomeka “La vie m’est insupportable. Pardonnez-moi.”

KIFARANSA: “La vie m’est insupportable. Pardonnez-moi.”
KIINGEREZA: “Life is unbearable for me. Forgive me.”
KISWAHILI: “Maisha hayawezi kuvumilika kwangu. Samahanini.”

Dalida alizikwa katika makaburi ya Montmartre huko Paris akiwa na umri wa miaka 54. Alikuwa anaimba muziki wake katika lugha 5 tofauti tofauti, Kifatansa, Kiarabu, Kiitaliano, Kijerumani na Kiingereza.

Similar Lifestyle Post;

Leave a Comment