Vita ya Ukraine na Urusi
E NEWS

Vita ya Ukraine na Urusi

Vita ya Ukraine na Urusi
Vita ya Ukraine na Urusi

Urusi na Ukraine, ili kuelewa chanzo cha mgogoro wao vizuri ni muhimu kujua kidogo historia ya nyuma kuhusu uhusiano baina yao. Hapo kitambo zote zilikua zinaunda Umoja wa kisovieti (USSR), na muungano huo uliundwa rasmi mwaka 1922 na kuvunjika mwaka 1991. Umoja huo ulipovunjika Ukraine ilijipatia uhuru wake kwa mara ya pili tena mwaka huo huo 1991, Kwa maana hapo awali walipata uhuru wao mwaka 1917 lakini baadae ndio waliunganishwa kwenye umoja wa Kisovieti mwaka 1922 ambao kwa wananchi wengi wa Ukraine waliona hauna manufaa yoyote kwao. Tangu kuvunjika kwa muungano huo, Urusi na Ukraine zimekua na mvutano wa hapa na pale chanzo kikuu kikitajwa kua maslahi ya kiusalama zaidi, Na Urusi ndio amekua tishio zaidi sababu ndio taifa lenye nguvu zaidi kwa ukanda huo na Dunia kwa ujumla wanafahamika vizuri tu.

Chanzo Cha Ugomvi

Serikali ya Ukraine ilibainisha mpango wake wa kutaka kujiunga na NATO, Nia hiyo haikuwafurahisha Urusi ambao waliamua kujibu kwa kupeleka wanajeshi zaidi ya 100,000 kwenye mpaka wa Ukraine. Kwa mujibu wa picha zilizotolewa na Wizara ya ulinzi ya Urusi zilionesha vikosi vyake vikiendelea na mazoezi ya kijeshi kwenye eneo la mpaka huo. Note: NATO – Ni jeshi la pamoja linaloundwa na nchi 27 za ulaya, Marekani, Canada na Uturuki. Nchi zinazounda umoja huu kwa kiasi kikubwa zinafuata misingi ya Kibepari na nyingi pia zimekua na uadui na nchi ya Urusi katika masuala mbalimbali.

KWANINI UKRAINE WANATAKA KUJIUNGA NA NATO? Chanzo kikuu ni kujiimarisha kiusalama, Tangu Umoja wa Kisovieti ulivyovunjika, Hofu mara kadhaa imekua ikitokea kwamba Urusi anaweza kuivamia Ukraine, Lakini mara zote Urusi amekua akipinga mpango huo. Licha ya kupinga, Mwaka 2014 Urusi walifanikiwa kutwaa Rasi ya Crimea ya kusini mwa Ukraine, Na kuanza kuwaunga mkono waasi wanaoiunga mkono Urusi ambao waliteka sehemu kubwa za Mashariki mwa Ukraine.

Mwaka 2014 Urusi walifanikiwa kutwaa Rasi ya Crimea ya kusini mwa Ukraine, Na kuanza kuwaunga mkono waasi ambao pia wanaiunga mkono Urusi ambao waliteka sehemu kubwa za Mashariki mwa Ukraine. Urusi walitwaa Pwani hiyo hasa baada ya kutokea kwa Mapinduzi Ukraine mwaka huo huo 2014 ambayo yalimuondoa madarakani Rais wa wakati huo Viktor Yanukovych ambae anatajwa kwamba alikua ni kibaraka mkubwa wa Urusi. Na mpaka sasa sehemu kama Donetsk na Luhansk kutokea Ukraine ni maeneo ambayo yalijitangaza kuwa huru na hata vita iliyokua inaendelea Ukraine kabla ya hii inayotaka kutokea ilikua ni kutokea vikosi vya hizo sehemu ambazo zinataka kuendelea kujiongoza zenyewe. Na inasemekana Urusi amekua akitoa msaada wa kijeshi kwa waasi hao ili kuiondoa kabisa serikali ya Ukraine, Na ndio maana nao serikali ya Ukraine mpango wao wa kujiunga NATO ni kutaka kupata msaada ya usalama ambao unazidi kuwa hatarini sababu ya Urusi kufanya mbinu nyingi hatari za chinichini. Moja ya hatari nyingine inayoendelea pia ndani ya Ukraine, Ni mipasuko ambayo kuna watu wanatamani kuwepo chini ya Urusi na wengine wanataka kubaki kama walivyo. Kwenye mgogoro huo NATO haikuingilia moja kwa moja, Lakini jibu lao lilikua ni kupeleka wanajeshi wa ziada katika nchi za Ulaya Mashariki kwa mara ya kwanza, zikiwemo Estonia, Latvia, Lithuania, Poland na Romania. Sasa hali hiyo ndio inawafanya Urusi kila siku kupiga kelele kwamba vikosi hivyo viondolewe, Ina maana kama NATO wataendelea kupeleka vikosi zaidi Ukraine ni kuzidi kuongeza tishio zaidi kwa usalama wa Urusi.

HIVYO BASI, Chanzo cha mgogoro wa Urusi na Ukraine ni; Urusi hataki kuona Ukraine akijiunga na NATO kwa hofu ya usalama kwake wakati nao Ukraine wanataka kufanya hivyo kwa hofu ya usalama ndani yake yote ni kwa sababu ya matendo ambayo wanadai yanafanywa na Urusi ndani ya nchi hiyo. WW3 🤔 Kama vita itazuka inaweza kua Vita ya Tatu Ya Dunia, sababu itahusisha mataifa mengi kwa wakati mmoja na zaidi ni hofu ya matumizi ya silaha za Nyuklia ambazo zinaweza kuathiri karibia dunia nzima. Na ikumbukwe Urusi yeye anaungwa mkono na Korea Ya Kaskazini, Venezuela na China ambazo nazo ni nchi zenye nguvu nzuri tu kijeshi.

SOURCE: Je Wajua >>> https://www.instagram.com/je_wajua2018/

Taarifa ya Tarehe 26 febuari, 2020 Kutoka BBC

Uvamizi wa Ukraine: Vikosi vya Urusi vinazingatia miji muhimu
Haya ndiyo matukio ya hivi punde:

  • Mji mkuu Kyiv, ulishuhudia mashambulio ya makombora na makabiliano makali usiku kucha lakini wanajeshi wa Ukraine bado wanaudhibiti mji huo.
  • Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema vikosi vya Vladimir Putin vimesalia umbali wa zaidi ya kilomita 30 kutoka katikati ya jiji la Kyiv.
  • Vikosi vya Urusi huenda sasa vinajipanga upya baada ya jaribio la awali lililofeli la kujipenyeza katika wilaya kuu za serikali huko Kyiv, Jack Watling, mtaalam wa kijeshi kutoka tanki ya fikra ya Rusi, aliambia BBC.
  • Katika mji wa mashariki wa Kharkiv, ambao ni mji wa pili mkuu wa Ukraine, maafisa wanasema kuwa wanajeshi wamepambana na shambulio la Urusi. Wametoa tahadhari ya kurusha makombora, na kuwaonya raia kusalia majumbani mwao.
  • Pia kumekuwa na mapigano karibu na mji wa kusini wa Odesa, Rais Zelensky anasema.
  • Urusi inasema imeuteka mji wa kusini-mashariki wa Melitopol – lakini Uingereza imetilia shaka madai hayo.
  • Zelensky anasema miji ya magharibi na kati ikiwa ni pamoja na Lviv imekuwa ikilengwa na makombora
Uwezo wa kijeshi wa Ukraine na msaada wa NATO

Jeshi la Ukraine ni dogo zaidi kuliko lile la Urusi, lakini linapata usaidizi kutoka kwa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO.

Marekani haijatuma wanajeshi wowote nchini Ukraine lakini imetuma wanajeshi 3,000 zaidi nchini Poland na Romania ili kuimarisha vikosi vya NATO, na imewaweka wanajeshi wengine 8,500 katika hali ya tahadhari.

Marekani pia imetuma silaha zenye thamani ya dola milioni 200, ikiwa ni pamoja na kombora la kushambulia vifaru la Javelin na kombora la kudungua ndege la Stinger. Pia imeruhusu nchi wanachama wa NATO kukabidhi silaha zilizotengenezwa Marekani kwa Ukraine.

Uingereza imepeleka makombora 2,000 ya kushambulia vifaru ya masafa mafupi nchini Ukraine, imetuma wanajeshi 350 zaidi nchini Poland, na kuongeza mara mbili uwezo wake wa kijeshi kwa kutuma wanajeshi 900 zaidi nchini Estonia.

Uingereza imetuma ndege zaidi za kivita kusini mwa Ulaya na meli ya wanamaji pamoja na wanajeshi wengine wa NATO kupiga doria bahari ya Mediterania.

Pia imewatahadharisha wanajeshi wake 1,000 ili iwapo kutatokea shambulio, wasaidie wakati wa mzozo wa kibinadamu nchini Ukraine.

Denmark, Uhispania, Ufaransa na Uholanzi pia zimetuma wanajeshi na meli zao Ulaya Mashariki na mashariki mwa Mediterania.

Na kwa upande mwingine, Ufaransa pia inapanga kuliongoza jeshi la Nato nchini Romania na kutuma wanajeshi wake huko, lakini Nato inasema kuwa itachukua wiki kadhaa kukamilisha mpango wake wote.

SOURCE: BBC Swahili – Februari 26, 2022

SOUCRE: Bongo Fasta – Youtube Channel

Leave a Comment