Tufaa Jekundu Sehemu ya Pili
NEW AUDIO

Ep 02: Tufaa Jekundu

Tufaa Jekundu Sehemu ya Pili
Tufaa Jekundu Sehemu ya Pili

UFAA JEKUNDU

SEHEMU – 2

“Hapana, hakutenzwa, muuaji hakuwa na haja ya penzi la nguvu wala ugomvi bali alikuwa na kiu ya kuua tu,” yule daktari

akajibu kwa ufasaha. Kila mara alitamani aseme jambo ambalo lilimtatanisha hata yeye kama daktari lakini alijikuta

akikinzana na nafsi yake…

SASA ENDELEA

“Samahani afande, mkuu wako naweza kumpata?” Akauliza yule daktari.

“Yeye ndo kanituma kwa maana kesi hii iko mikononi mwangu, kama una la kumwambia basi mimi ni mtu muafaka,” Chubi

akazungumza huku akiiweka kalamu yake vyema mfukoni mwake.

“Sikiliza kwa makini, kuna kitu ambacho sijakielewa nimekikuta kwenye ule mwili,” akaeleza na kuuona wazi umakini wa

macho na masikio ya Chubi. Yule daktari akatoka kijifuko cha plastiki na kukitua mezani kwa mtindo wa kukirusha.

“Nini hiko daktari?” Akauliza. Daktari Zaytuni akajiegemeza kwenye meza na kumtazama Chubi kwa karibu zaidi.

“Kwenye kinywa cha marehemu nimetoa kitu hiki ambacho kilikuwa ndani yake,” akaelezea huku akimwonesha kile kimfuko

pale juu ya meza. Chubi akakivuta na kukifungua taratibu akatoa macho baada ya kuona risasi ndogo ya shaba iliyoandikwa

‘TSA 1’ kwa kukwanguliwa na kitu chenye mcha kali na kufanya weusi. Akaigeuza geuza na kuirudisha bahashani huku

akihakikisha haachi alama yoyote ya vidole katika risasi hiyo. TSA1, akawaza akiwa kimya huku akimwangalia yule daktari.

“Umesema umeikuta wapi?” Akauliza tena.

“Kinywani mwa marehemu, kiliwekwa upande wa kushoto na kufunikwa na ulimiî akaeleza daktari. Chubi alibaki kimya huku

mambo mengi yakipita kichwani mwake kama mkanda wa filamu. Kwa nini’ Akajiuliza.

“Asante daktari, nitakuja pindi nikiwa na shida,” Chubi akamwambia yule daktari na kuondoka zake.

***

“Ndiyo Chubi, nipe ripoti kijana wangu, najua kwa vyovyote vile utakuwa umefika hatua nzuri,” Mkuu wake wa kazi alijiweka

vizuri kitini akimtizama kijana huyo alipokuwa akiiweka ile bahasha mezani.

“Mkuu mambo yote yameenda vizuri, lakini kuna hili moja ambalo linenitatiza, labda wewe unaweza kujua maana yake,” Chubi

alimsogezea ile bahasha. Mkuu wake akaifungua na kuiona ile risasi, naye akaipindua pindua, akatikisa kichwa kama

mtu ambaye hajaelewa chochote, risasi, akawaza.

“Risasi!” Akasema kwa sauti huku akiinua uso kumtaza Chubi.

“Ina maana marehemu alipigwa risasi?” Akauliza.

“Hapana, daktari anasema risasi hii ameikuta kinywani mwa marehemu,” Chubi akaeleza.

“Lo, huu ni utata!î Mkuu akapatwa na wasiwasi sana. Akaitazamatena kwa makini.

“Inawezekana alipigwa risasi ya kisogo na risasi hii ilikwama kinywani, yes! inawezekana, au unasemaje?” akamalizia

kusema.

“T-S-A 1, mh! Ni aina gani ya bunduki?” Akauliza. Chubi akamkazia macho mkuu wake wa kazi hasimwelewe anachosema.

“Mkuu, risasi hii imekutwa kinywani mwa marehemu,” Chubi akasema kwa msisitizo.

“Na marehemu ana jeraha kubwa kisogoni. Huwezi kufikiri kuwa alipigwa risasi kisogoni ikakwama kinywani?” Mkuu

wake akaongeza sentensi na kuuliza swali ambalo lilimchanganya Chubi. Inawezekana, Chubi akawaza huku akitikisa kichwa juu

chini.

“Chubi, nataka ufanye juu chini tumpate huyo mchumba wake hata kama walikwishaachana au walitaka kufunga ndoa hivi

karibuni. Namwitaji hapa haraka, kwa sababu inawezekana kafanya haya kutokana na ugomvi wao,” akaamuru. Chubi akasimama

kiukakamavu.

“Mkuu tuliweke hivi kwa sasa, kama Kayinda asiporudi pale hotelini ndipo tumtafute ila kwa sasa tumtafute huyu,” akasema

na kutoka mle ofisini akimwacha Mkuu wake akijibu kwa kichwa huku bado anaitazama ile risasi.

DUMBWINI – saa 8 mchana.

Chubi aliegesha gari yake pembezoni mwa mgahawa uliokuwa tupu, hakukuwa na mteja ndani yake isipokuwa mwanadada

muuzaji tu, aliyekuwa kavaa gauni refu lililoficha mpaka ukucha wa kidole chake cha mguu, huku mikono yake ikiachwa

viganja tu na uso wake ukiwa wazi, lakini nywele hata moja haikuwa nje ya vazi hilo, weupe wa uso wake ulionesha wazi

kuwa alikuwa Mwarabu wa asili. “Karibu sana, jisikie nyumbani ati,” mwanadada yule akamkaribisha Chubi.

“Asante nimekaribia, naweza pata soda baridi?”

“Bila shaka,” yule dada akajibu na kumpatia kinywaji. Alipokuwa pale mezani akimfungulia kinywaji na kummiminia kwenye

bilauri, Chubi alimshika kiganja chake cha mkono na kumtazama usoni. Wakagongana macho, macho makali ya Chubi yalimfanya

binti yule kugeukia kando.

“Niachie mkono tafadhali, sio vyema mbele ya mume wangu,” Yule mwanadada akamwambia Chubi huku akiangalia upande

wa pili.

“Namtafuta Shamsi Haroub, unamjua?” Akauliza.

“Ndiyo, lakini sijamwona kama siku mbili hivi, na hapa ndipo hasa maskani kwake,” yule mwanadada akajibu.

“Nina shida naye sana, unamjua mchumba wake Batuli?” Akauliza.

“Batuli, ndiyo namjua, mara kadhaa amekuja naye hapa kula urojo, lakini wiki moja hii aliniambia kuwa wamekorofishana

na kufuta mipango yote ya ndoa yao,” akaeleza yule mwanadada. Chubi akatulia kimya akimtazama yule dada huku mkono wake

ukiwa bado kiganjani kwake.

“Una namba yake?” Akauliza.

“Ndiyo”.

“Nipatie,” akaomba. Dakika moja baadae Chubi alikuwa kaweka simu sikioni akisikiliza sauti ya upande wa pili.

“…hello, ee Shamsi (…) samahani aisee nipo hapa Dumbwini CafÈ naweza onana na wewe nina shida sana,” ukimya

ukatawala.

“Tuonane hapo Ngome Kongwe kwani nitakuwa maeneo hayo baada ya saa moja tokea sasa,” Shamsi akajibu, na makubaliano

yakapitishwa jinsi ya kuonana. Chubi alimaliza kinywaji chake na kumuaga yule dada huku akimshukuru, alipotoka nje

akawasiliana na mkuu wake wa kazi na kumpa ujumbe huo kisha akaomba gari na askari wawili kusaidia kumkamata mtuhumiwa huyo

waliyempa namba mbili, namba moja akiwa Swebe Kayinda.

NGOME KONGWE

CHUBI aliwasili dakika kadhaa kabla ya Shamsi na kuketi eneo waliloelekezana. Akiwa na gazeti lake mkononi akifuatilia

habari mbalimbali za kitaifa, simu yake iliita, alipoitazama ilikuwa namba ya Shamsi akaipokea na kumwelekeza.

Shamsi alifika mahala pale na kuketi mkabala na Chubi pasi na wasiwasi wowote.

“Ndiyo kaka nimeitika wito wako,” Shamsi akaanzisha mazungumzo. Baada ya kujuliana hali na mazungumzo ya hapa na

pale Chubi akaenda kwenye lile lililomfanya amtafute.

“Shamshi, unamjua Batuli?”

“Ndiyo namjua,” akajibu huku akijiweka vyema kitini kwa kuwa alihisi jambo jipya linakuja kwani mwanamke huyo waliachana

wiki kadhaa nyuma.

“Batuli una uhusiano wowote na yeye?” Chubi akauliza.

“Ndiyo, alikuwa mpenzi wangu, tulipanga kuoana lakini amenisaliti, nimeachana naye, kama wamtaka we endelea naye,” Shamsi

akaongea huku akionekana wazi kuwa na hasira na jambo hilo.

“Hapana sio hivyo, Batuli hatunaye tena,” Kauli hiyo toka kwa Chubi ilimpa shoku Shamsi akabaki kakodoa macho huku mwili

ukimtetemeka kwa mbali.

“Wasemaje bro¥ ?” Akauliza tena kutaka uhakika zaidi. Akajibiwa vilevile. Shamsi akainama chini mikono kichwani akaingia

kwenye huzuni nzito. Sekunde kadhaa za ukimya zikajidai kati ya wawili hao.

“Amekufaje?” Shamsi akauliza huku akimwangalia Chubi usoni kwa macho makavu lakini yalojawa weweseko.

“Ameuawa na maiti yake imepatikana leo asubuhi mahala pake pa kazi,” Chubi akaeleza kwa upole. Shamsi akabaki kimya

akiwaza hili na lile huku uso wake ukitazama juu kidogo, akatikisa kichwa kushoto kulia, akauma meno na kupiga ngumi

mezani.

“Nilimwambia Batuli, nilimwambia mimi … nilimwambia ‘ushibokee wanaume wenye pesa, wengine wapo kwenye biashara zao’,

hakunisikia, masikini Batuli,” Shamsi alisikitika sana na kuanza kulia.

“Sasa tunataka tumpate muuaji, na wewe unaweza kusaidia sana katika hilo. Tutaondoka sote mpaka kituo cha polisi kwa

mahojiano zaidi,” Chubi akamweleza. Kutokana na utayari na utii wa Shamsi, Chubi hakuona haja ya kumchukua kwa nguvu,

aliondoka naye kirafiki na kumkabidhi kwa vijana wa polisi ambao walifika naye kituoni Bububu.

MAHALI FULANI TANZANIA

Moshi wa sigara uliongíarishwa kwa mwanga hafifu wa taa ya halogen ulipishana katika anga la chumba fulani kidogo lakini

chenye nakshi matata sana. Kilijitosheleza kwa kukutana watu wachache tu na bila shaka kilikua maalumu kwa kazi hiyo. Kama

hakujenga mmiliki mwenyewe basi mjenzi aliweza kuyatafsiri vyema mawazo ya mtu aliyesanifu kijichumba hicho.

“Ah! Ah! Ah! Koh! Koh! Koh! Na safari hii wataisoma namba,” sauti nzito yenye mkwaruzo ilisikika ikisema maneno hayo

kutoka ndani ya chumba kidogo mara tu baada ya kukohoa kma iliyopaliwa na kitu.

“Kwa nini unasema hivyo?”Sauti nyororo ya Nyotanjema ilisikika ikiuliza.

“Tunamwita taratibu kisha tutamtia mkononi na baade kummaliza. Agizo tulilopewa ni ‘shoot on the spot’ hakuna kingine,”

ile sauti ya kukwaruza ikaendelea kusema huku chumba chote kikiwa kimejaa moshi wa sigara uliokuwa ukipishana kutoka huku

kwenda kule. Nyotanjema, mwanamke mrembo kuliko unavyofikiria alikuwa ndani ya chumba kidogo akitazamana na mtu huyo

asiyemjua wala hakuwahi kumwona sura kwa kuwa kila walipokutana walivaa vinyago na kuficha nyuso zao.

Itaendelea….

Tufaa Jekundu Sehemu ya Tatu

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment