Pasipoti ya Gaidi The Return of Kamanda Amata Sehemu ya Nne
IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE
Simulizi : Pasipoti ya Gaidi ‘The Return of Kamanda Amata’
Sehemu Ya Nne (4)
Kamanda Amata alikuwa wa kwanza kuiacha casino hiyo na kutoka nje, moja kwa moja aliiendea gari aliokuja nayo Cjoba na kuingia siti ya mbele akaketi huku Chiba akiwa nyuma ya usukani. Kimya hakuna aliyeongea, wote macho yao yalikuwa yakiangalia kule kwenye lango la casino hiyo. Briston akatokezea na kuteremka ngazi taratibu akaelekea kwenye maegesho na kuingia ndani ya gari yake kisha akaiwasha tayari kuondoka.
“Sasa?” Chiba akauliza.
“Tunamfuatilia mguu kwa mguu, yaani usiku huu mpaka tujue nini anafanya na ikiwezekana nitakwenda kuikagua nyumba yake…”
“Nyumba yake? Vipi kama mkewe na watoto wapo huko?” Chiba akamkatisha na kumuuliza.
“Usijali, kila kitu kitajulikana papo hapo,” akiwa katika kusema hayo, ile gari ya Briston ikapita mbele yao na kupunguza mwendo, kioo cha upande ule waliokuwa akina Amata kikateremka taratibu kisha Briston akawaoneshea dole la kati na kile kioo kikapanda taratibu huku ile gari ikiselelereka barabarani kulifuata lango la kutokea. Chiba akaweka mkono katika katika funguo ya gari tayari kuwasha, Amata akamzuia huku akimwonesha ishara ya kidole kuangalia kule katika lango la kutoke casino. Chiba akainua macho na kumwona mrembo aliyesimama huku akichezea simu yake.
“Kaka tupo kazini kaka, achana na hayo, kila siku bibi yako anakuonya…”
“Aaaa bibi yako keshazeeka, ye mwenyewe enzi zake alikuwa hivihivi. Kazi na dawa; huyu lazima nimkamate leo hii, cheki mtoto Yule,” Amata akaongea.
“Kwa hiyo tunamfuata Briston au?” Chiba akauliza.
“Ameshatujua, tukisubutu tu tumeisha, Yule hafai kabisa. Sasa ipo hivi, kanifanyie utambuzi wa hizo picha za hao jamaa wawili, mi niache na huyu mrembo,” alimaliza kusema hayo akiwa tayari nje ya gari hiyo. Chiba akawasha na kuondoka eneo lile.
Briston usiku ule moja kwa moja alielekea hoteli ya New Africa ambako daima hukutana na kijana wake Kubra Khaleb. Wawili hao walikutana kwa dharula haikuwa imepangwa kuwa hivyo.
“Vipi comrade?” Kubra akauliza.
“Mpango umestukiwa?” Briston akajibu huku akilisaidia feni kumpepea.
“Unasema! Mpango upi?”
“Mcehzo wote wa Ikulu umegundulika…”
“Nani kagundua wakati kazi ile tumeifanya kwa umakini wa hali ya juu?” Kubra aliwasiwasika kwa hilo.
“Sikiliza Kubra! Tulifanya kwa weledi wetu wote, lakini kuna watu wana vichwa vya ajabu, huyu jamaa tusipomdhibiti sasa tumeumia na anatufuatilia nyayo kwa nyayo,” Briston akaeleza.
“Unafikiri atajua yote?”
“Kubrah! Kama kagundua kuwa silaha za waasi zilikuwa zinatoka Ujerumani na mpaka digala mwenye kamjua na kapambana naye, unafikiri hatojua kuwa mipango hii yote ina lengo moja? Sasa keshajua kilichotokea ndani ya Ikulu, keshanijua mimi, bila shaka keshakujua wewe. Na leo nimekutana na Kepteni Banzilahagi pamoja Kimosa Kabalege Yule afisa wa ubalozi katika idara ya usalama, sasa hapa sijui kama kawaona au vipi, maana baada tu ya kuondoka wale jamaa na ye akaja mezani kwangu…”
“Ha! Yaani kaja mpaka mezani kwako umemwachia? Huku na silaha?” Kubrah akang’aka kuuliza.
“Kubrah, nilikuwa nahitaji kujua nini anakijua juu ya hili, nimeona anajua lakini hasa ni swala la uvamizi zaidi ya hapo hakuna anachokijua,” akaeleza.
“Good! Sasa inabidi tumdhibiti usiku huu,” Kubrah akaeleza mpango.
“Ni sawa, kazi nimempa Lulu, nina uhakika atalifanikisha, akimpata atatupigia ili tukamalizie kazi,” akamwambia Kubrah.
“Oooh una jina zuri sana Lulu, yaani kitu chenye thamani sana ambacho kwanza hakipatikani kirahisi,” Amata alimwambia mrembo huyo wakati akiwa naye ndani ya gari.
“Mmmmmh maneno yenu tu hayo,” Lulu akajibu.
“Napenda nikapitishe usiku huu na wewe,”
“Waoh! Is it possible?” Lulu akatia shaka.
“Hauamini?”
“Siwezi kuamini moja kwa moja kwa sababu, umekaa pale ndani hata kumpapasa mwanamke yoyote hujajaribu…” Lulu akaeleza.
“Uliniona?”
“Aaaa sana, sisi huwa tuna macho mia…”
“Nyinyi na nani?” Amata akamkatisha.
“Ah we! Tuko wengi tunafanya shughuli zetu hapa,” Lulu akaeleza huku macho yake akiyapeleka nje.
“Nimekuchagua wewe, mrembo, unapenda tukamalizie usiku huu wapi? Nyumbani kwangu?” Amata akauliza huku mkono wake tayari ukipapasa paja la mrembo huyo, taratibu kutoka kwenye goti kuelakea pajani.
“Nyumbani kwako namwogopa mkeo,”
“Sina mke!”
“Basi mpenzio,”
“Ah… hapana sina mpenzi, nimekuchagua wewe leo…”
“Napenda New Africa,” Lulu akachagua. Amata akaondoa mkono wake pajani mwa Lulu, akakamata gia ya gari huku mkono wa kulia ukitekenya ufunguo na gari hiyo ikawaka, akaweka gia namba moja na kuondoka taratibu.
Iliwachukua takribani dakika kumi na sita tu kuwasili New Afrika, Kamanda Amata akangiza gari maegeshoni na kushuka na membo huyo akiwa mkono wake wa kuume kauzungusha kiunoni mwa mrembo huyo huku mabusu ya hapa na pale yakiendelea.
“603,” mwanadada wa mapokezi alimtajia namba ya chumba huku akimkabidhi kadi maalumu ya kufungulia mlango wa chumba hicho.
“Nahitaji whisky tafadhali…”
“Mmmmh na Amarula!” Lulu akaongeza huku wakiondoka pale mapokezi na kumwacha Yule mwanadada akishughulikia hilo.
Ndani ya chumba hicho Amata alimbwaga Lulu kitandani na kuanza kumpiga mabusu mazito ya kinywani huku Lulu naye akionesha ufundi wa hali ya juu katika kuumung’unya ulimi wa Amata. Kengele iliyogongwa mlangoni iliwaachanisha wawili hao na Amata akauendea mlango na kupokea vinywaji walivyoagiza. Lulu aliinuka na kpekua pochi lake, akatoa simu ndogo na kubofya haoa na pale na wakati huo Amata alikuwa amekwisha fika.
“Achana na simu dear!” akamwambia.
“Aaaa ndiyo nilikuwa nazima ili tule raha kwa raha, naomba nimalizie process basi,” Lulu akaongea kwa sauti ya kubana pua, Amata akamruhusu naye akabofya ‘send’ kisha akazima simu na kuitupa pembeni.
Madam S alibaki akizunguka zunguka huku na huko, kichwa chake kilionekana kuchanganyikiwa wazi kabisa.
“Chiba simaini unachoniambia kabisa, una uhakika na hilo jambo?” akauliza.
“Bila shaka Madam, Amata aliniita kufika pale Las Vegas name nikafanya hivyo, na akanipa hizo ishara nikakamata picha za hao watu, nimezicheki hapa kwenye mtandao wetu na majibu ndiyo hayo,” Chiba akaeleza.
“Banzilahagi, Kepteni wa Jeshi la Wananchi tena ana kitengo nyeti sana jeshini, kama atakuwa ndani ya mpango huu tumekwisha na katika hili lazima tuchukue hatua ya haraka sasa hivi, huyo Kimosa Kabalege naye pia!” Madam akazungumza huku akivuta kiti na kuketi, “Kamanda yuko wapi?” akauliza.
“Aaaaa nimemwacha viungani ana misheni nyingine,” Chiba akajibu huku akibana kicheko kilichojionesha wazi mashavuni mwake.
“Unacheka nini? Au unamfichia siri? Sema tu kama yuko na mwanamke, maana Yule sijui ana ugonjwa yaani sielewi…”
“Aaaa hayo umesema wewe Madam mi husiniweke hatiani,” Chiba akamaliza kusema huku akiifunga kompyuta yake.
Madam S akainua simu yake ya mkononi na kubofya namba Fulani kisha akaweka sikioni mwake kwa sekunde kadhaa, “Hapatikani…” akashusha simu hiyo na kupiga namba nyingine, akaweka tena sikioni.
“Gina! Hello!” Madam alipoita jina hilo Chiba akafumba kinywa chake kwa hofu, anaharibu lo! Akawaza.
“Uko wapi? (…) ok, sasa nataka uhakikishe unamchunga mtu anayeitwa Banzilahagi Yule kepteni wa jeshi, anaishi Makongo plot namba 703, nipe kila dondoo za nyendo zake,(…) ok vyema, fanya hivyo,” akamaliza na kukata ile simu. Chiba akashusha pumzi huku mikono sasa ikiwa kiunoni. Kisha akabofya namba ingine na kuweka sikioni.
“Scoba! Unasomeka wapi? (…) ok! Nimekupata, sasa ipo hivi, nataka uweke jicho katika nyumba ya Afisa Baalozi Kimosa Kabalege na unipe dondoo zote za nyendo zake usiku huu na mpaka nitakapokupa amri nyingine,(…) ok, ok!” akakta simu na kuketi.
“Naona mbananisho umeanza,” Chiba akamwambia Madam huku akiitazama saa yake.
“Inabidi tufanye kazi kwa mtindo huo kwa kuwa mpaka sasa hawa tunawashuku,” akajibu Madam S.
Lulu alimwonesha manjonjo ya kutosha Amata kitandani hapo, ilikuwa shughuli nzito ukizingatia walikuwa tayari wametanguliza kinywaji. Lakini ghafla, Amata alichomoka kutoka kitandani na kumwacha mwanamke Yule palepale, akaketi kiatandani.
“Vipi jamani, unanikatisha utamu!” Lulun akalalamika. Amata akamwoneshea kiganja chake cha mkono kumuashiria anyamaze. Akaingiza mkono wake chini yam to na kutoa bastola, akavuta slider yake na kuiachia, risasi moja ikakaa sawa, kwa haraka akavaa bukta na kusimama pembezoni mwa kabati.
“Kuna nini?” Lulu akauliza.
“Shhhhhhh!!!!” akamwaonesha kwa kukiweka kidole juu ya midomo yake. Kisha akanyata na kuliendea dirisha na kujibana sawia pembeni yake. Dirisha lile likavutwa polepole kufunguliwa na mkono wenye bastola ukajitokeza kule pale kitandani, Amata akaiweka bastola yake pembeni na kwa kasi ya ajabu akakukamata mkono wa Yule mtu na kuukunja.
“Aaaaaiiggghhh!” ule mkono ukateguka mifupa, akamvuta ndani kwa nguvu na yule jamaa akaingia na kioo cha dirisha, alipoingiza shingo akampa pigo moja kali la karate na yule jamaa akatua ndani kama mzigo na bastola ikimtoka mkononi na kuselereka mbali. Lulu akakurupuka kitandani na kupiga sarakasi moja maridadi akainyakua ile bastola. Amata hakutegemea kile kitendo alipogeuka tu, risasi moja ilipita karibu kabisa na uso wake na kufumua kioo cha dirisha. Akjitupa kwa nyuma na kukoswa na risasi nyingine kutoka kwa Lulu, Amata akainyakuwa bastola yake lakini kabla hajaishika vizuri, Lulu aliilenga kwa risasi na kuiondoa mahala pale, Amata akaikosa. Shabaha ya Lulu ilimshangaza Amata, akaona akizubaa na kudharau kwa kuwa mwanamke anaweza kuaibika. Aliinua taa ya mezani na kumrushia kwa nguvu, ikampiga usoni, Lulu akapoteza mwelekeo, wakati akijiandaa kufyatua risasi yake akajikuta bakikutana na miguu mizito ya Amata iliyotu tumboni mwake na kumfanya ajibamize vibaya ukutani. Amata akajiinua lakini kabla hajawa wima, aliliona teke kali la mwanmke huyo likija usono mwake, akaepa na mguu ule ukapita wakati huo nay eye akauzungusha wa kwake na kuupiga kwa chini wa Yule mwanamke uliobaki wima sakafuni, akamchpota ngwala maridadi na kubwaga vibaya.
“Mhhhh! Aaagh! Mpenzi unaniua?” Lulu akalalama huku akijaribu kujiinua. Amata akamwahi na kumkamata night dress yake akampiga kichwa kimoja maridadi na Lulu akalegea na kusihiwa nguvu, Amata akamsukuma na kupigiza ukutani, akaanguka kando akiwa hana fahamu na damu zikitiririka katika tundu za pua yake…
“Mhhhh! Aaagh! Mpenzi unaniua?” Lulu akalalama huku akijaribu kujiinua. Amata akamwahi na kumkamata night dress yake akampiga kichwa kimoja maridadi na Lulu akalegea na kusihiwa nguvu, Amata akamsukuma na kupigiza ukutani, akaanguka kando akiwa hana fahamu na damu zikitiririka katika tundu za pua yake. Amata akamwacha pale chini na kuiendea suruali yake, akaivaa haraka na fulana yake ikafuta juu yake, bastola yake akaibana sawia kiunoni mwamke kisha akamwendea Yule jamaa aliyemwacha pale usawa wa dirisha baada ya kipigo kile akampekua na kumkuta na simu tu mfukoni mwake, akaichukua na kubofya kidubwasha cha kupigia kisha akaitoa loki yake na kupekuwa kwenye boksi la ujumbe mfupi.
‘…hakikisheni huyo Malkia anahifadhiwa vyema, safari inakaribia alfajiri ya kesho…’
Baada ya ujumbe ule ukafuatiwa na mwingine ukisema…
‘…wapo chumba namba 603, muue mwanaume, mwanamke tuachie…’
Amata akatabasamu kwa ujumbe ule na alipouchunguza akagundua kuwa ulitumwa na mtu mmoja kwa tofauti ya muda wa saa moja, akaujibu ule wa pili kwa kutumia simu ileile, akajua wazi wakiupokea ujumbe huo lazima hao walioutuma wachanganyikiwe.
‘…nimekufa mimi…’
Kisha akautuma na kuitia ile simu mfukoni, akaunyakua mkoba wa Yule mwanamwali na kumwaga kila kilichopo, akakuta mashine ndogo ya kurekodi sauti, akaichukua zaidi ya hapo hakukuwa na kingine cha maana za ya kijitabu kidogo cha anwani za watu akakichukua na kutoka ndani ya chumba kile haraka, badala ya kutumia lifti kuteremka mara hii akatumia ngazi za kawaida tena isitoshe ngazi za dharula kwani alihofu kukutana na watu asiowatarajia, moja kwa moja akaiendea gari yake lakini kabla hajaifikia, alipojitokeza tu upande wa pili wa hoteli ile kutokea nyuma, alimwona kijana mmoja akiwa usawa wa tairi la mbele akifanya jambo Fulani kwenye gari hiyo.
Amata akajificha na kuangalia kila kitu kwani alihofia hicho anachofanya kijana huyo. Baada kama ya dakika mbili hivi Yule kijana akatoka na kuliacha gari la Amata kisha akaingia kwenye gari kama ya tano hivi katika maegesho yale. Amata akafikiri moj na mbili, akapita kwa haraka nyuma ya gari zile, na kuiacha ile ya kwake, akiwa anakimbia huku kainama aliliifikia ile gari Toyota Mark II na kuchukua fungua yake yenye uwezo wa kufungua kila kitasa cha gari, akafungua buti na kujitia ndani kisha akafunga na kuacha nafasi ndogo ya kupata hewa, akatulia kimya.
Ndani ya gari hiyo kulikuwapo vijana watatu, nao walikuwa kimya muda wote hakuna aliyeongea ila tu mitikisiko ya gari kila walipojigeuza. Baadae akasikia mmoja akijikohoza na kufuataiwa na kauli.
“Asee huyu jamaa vipi hadi sasa!” mmoja akasema.
“Dakika kumi sasa, sio kawaida maana tunachelewa,” mwingine akajibu kisha ukimya ukatawala tena.
“Mpe taarifa Master juu ya hali hiii kisha yeye atatuambia la kufanya,” mtu wa tatu akatoa wazo na mara hiyo Amata akasikia mlio wa batani za simu akazisikiliza kwa makini sana ili aweze kugundua ni namba gani iliyopigwa, akatikisa kichwa baada ya kuona kasahau baadhi ya milio, hii anaweza Chiba, akajisemea moyoni. Lakini aktega sikio kusikiliza nini kitaongelewa.
“Ee Master, jamaa hajarudi hadi sasa tuchukue hatua gani?” akauliza. Kisha ukimya ukafuata, Kamanda Amata akajua kwa vyovyote mtu wa upande wa pili atakua akiongea.
“Sawa! Master,” kisha ukafuatwa mlio wa simu kukatwa. Amata akainua simu yake taratibu na kutuma ujumbe mfupi kwa kampani yake kuwajulisha kinachoendelea.
“Huyu jamaa naye mbona haji? Au bado anakula raha, mh! Leo Lulu anal oleo,” mmoja wao katika gari ile akawaambia wenzake mara Amata akasikia mlio wa simu inayoita.
“Yes! Ndio… he! Ok sawa!” Yule jamaa akaongea hayo katika simu kisha ile gari ikawashwa na kuondolewa mahala pale. Amata akaangalia kwenye uwazi mdogo wa buti hilo akaoana kuwa bado hawajaiacha hoteli ile na baadae wakaingia barabara ya Maktaba.
Briston alitikisa kichwa akamwangalia Kubrah.
“Ametuweza mshenzi huyu!” Bristona akasema.
“Na mimi nimemuweza, subiri usikie,” Kubrah akajibu na kumfanya Briston kumtazama, “Mbona unaniangalia?” akamuuliza.
“Umesema umemuweza?”
“Ndiyo, we sikiliza tu ndani ya saa moja lijalo, nimemuwekea motto katika gari yake akiingia tu puuuuuu!” Kubrah akasema kisha wote wakaangua kicheko lakini Briston akanyamaza ghafla.
“Vipi?” Kubrah akauliza.
“Nasikitika kwa kifo cha huyu jamaa na Lulu, inabidi tuwe tayari, kesho asubuhi tukimuondoa Malkia na sisi tuondoke kisha plan B ichukue nafasi kwa kuwa kule Mpumbutu jamaa wameshaharibu na Mkuu wa wakuu amekasirika sana, anataka kuongea na huyu Rais wa hapa, sikia tutakuwa na kikao kizito pale Cape Town juu ya hili haraka iwezekanavyo,” Briston akamwambia Kubrah.
“Tuondoke, tushughulike na huyu kimburu,” Kubrah akasema.
“Hayuko peke yake, wako kama wane hivi, wote lazima washughulikiwe,” Briston akiajbu huku akifungua mlango kutoka. Nje ya hoteli hiyo kila mmoja alichukua gari yake na kuondoka. Lakini Kubrah aliitazama sana gari ya Amata na akaiona ikiwa palepale, ina maana huyu mshenzi bado yupo humu ndani? Akajiuliza. Na taratibu akaondosha gari yake pale hotelini huku akimwagiza mmoja wa vijana wake kuiangalia ile gari mpaka itakapoondoka.
Ile gari aliyopanda Amata iliingia ndani ya majengo yasiyokwisha ambayo bado yalikuwa yakiendelea na ujenzi, ikaingia na kufika mahali ndani ya kitu kama chumba hivi. Ikasimama na milango ikafunguliwa huku wale jamaa wakiteremka hai hai.
“Vipi huko?” mtu mmoja aliyeonekan kama mlinzi aliuliza.
“Jamaa kauawa bwana na tunayemsaka inaonekana katoroka eneo lile,” akajibu mmoja wa walioshuka kwenye ile gari.
“Kwa hiyo tunafanyaje?”
“Mpango ni uleule, kesho asubuhi, tunaondoka na Malkia na kuelekea kisiwani kwani mpango mwingine unatakiwa kuchukua nafasi, weka kila kitu sawa kama mpango ulivyo,” akatoa maagizo ambayo Amata alikuwa akiyasikia vyema. Kwa kutumia simu yake akatuma ujumbe mfupi kumpa Madam S juu ya hayo anayoyasikia. Kisha akatulia palepale kusubiri watu hao watoke eneo hilo ili naye aweze kujitokeza na kufanya yake.
IKULU
USIKU UOHUO
SIMU YA RAIS iliita kwa fujo, mheshimiwa bado alikuwa hajalala na wala hakuwa hata na lepe la usingizi, alipoitazama akajua ni ile simu nyeti ambayo huweza kukaa zaidi ya siku tatu bila kuita isipokuwa kwa jmabo muhimi na la kiusalama tu, akaitazama na kuona kwenye kioo TSA, akaiweka sikioni mara moja.
“Taarifa kutoka TSA juu ya usalama wa taifa usiku huu, naomba kikao cha dharula kama inawezekana,” upande wa pili ukasubiri jibu. Bila kusita Mheshimiwa Rais akakubali kikao hicho usiku huo akakata simu na kutoa taarifa kwa wanausalama wachache juu ya ujio wa Selina ndani ya jingo hilo jeupe.
Saa tisa usiku, mwanamama huyo aliwasili Ikulu na kupokelewa na mtu alioyeandaliwa na moja kwa moja alifikishwa kwenye ofisi ya Rais kwa mazungumzo.
“Kwanza samahani kukukatisha usingizi,” akaanza kwa kusema hivyo.
“Hapana Sellina, siwezi kupata usingizi kwa hali hii ambayo inanikabili, na najua ni wewe tu kwa sasa unaeweza kunipa jibu ambalo litanifariji, nipe maendeleo ya kazi niliyowapa,” Rais akamwambia kisha akatulia kitini.
“TSA tupo kwenye uchunguzi wa hali ya juu sana katika swala la uvamizi wa Ikulu uliofanyika hapa na tumeshagundua mambo mengi sana kuliko unavyotarajia kusikia…”
“Enhe…”
“Kwanza kabisa, mkuu umezungukwa na maadfua kila kona ndani ya idara zako na nchi yako kwa ujumla. Uvamizi wa Ikulu ulipangwa na watu walio chini yako kwenye idara nyeti za uslama…” akamweleza kila kitu lakini hakutaja wahusika wa tukio hilo. Mheshimiwa Rais alikuwa katika hali ya hasira na uchungu alipokuwa akipokea taarifa hiyo fupi lakini iliyojaa utaalam wa kikachero wa hali ya juu, moyoni mwake alimshukuru aliyekuwa na wazo la kuanzisha idara hii ambayo sasa anaielewa umuhimu wake.
“Sasa kuna watu ambao wapo chini ya jicho letu na tunahitaji kuwakamata mara moja ikiwezekana kwa amri yako usiku huu, hawa watatueleza vyema juu ya mpango mzima tangu mwanzo na nani anahusika,” Madam Sellina akaeleza na Rais akalipokea kwa kutikisa kichwa akiashiria kuwa amekubaliana naye. Lakini mpaka hapo hakuwa anajua ni nani na nani.
“Nani na nani?” akauliza.
“Wa kwanza ni Kepteni Benzilahagi…”
“Kepteni? Wa jeshi au wa meli?” akauliza kwa hamaki.
“Bora angekuwa wa meli, ni wa jeshi tena JW, tunamshuku kutokana na nyendo zake siku hizi, baadae nitakujulisha nyendo hizo lakini sio leo kwa sababu za kiusalama. Mbaya zaidi mtu huyu yupo kwenye kitengo nyeti sana ndani ya jeshi letu, nikiwa na maana kuwa anajua kila kitu, kila siri, kila mpango wa jeshi letu. Ni msaliti…”
“Akamatwe na ahojiwe mara moja!” Rais akatoa amri na kupiga ngumi juu ya meza baada ya kutajiwa kitengo cha mtu huyo.
“Na wa pili nani? Nataka kumjua!” akang’aka mheshimiwa.
“Wa pili ni afisa ubalozi wa Nduruta anaitwa Kimosa Kabalege, sasa kwa huyu tulisita kwa sababu za kidiplomasia,” Madam S akaeleza.
“Kamata, weka ndani ahojiwe. Sellina unataka kunambia hii ni njama kutoka Nduruta?” akauliza Mheshimiwa Rais huku akionekana wazi kuhamanika kwa mpango huo.
“Ndiyo Mheshimiwa, kumbuka umeamuru vikosi vyako vya JW kuvaa kofia ya UN na kwenda kuendesha operesheni dhidi ya waasi wa X65, waasi hawa kwa uchunguzi wetu ni watu wa Rais Sebutunva wa Nduruta na washirika wake ambao siku hizi umeona wakikutenga katika mambo mengi ya ki-kanda. Tumegundua kwamba wafadhili wakubwa wa waasi hawa ni vyama vyenye mlengo wa kushoto huko Ughaibuni, kwa biashara ya mabadilishano wa vitu wao hupeleka Almasi na kupewa silaha nzito na za kisasa. Hivyo basi kama kisasi kutoka kwa jirani yao Sebutunva ndiye aliyefanya mipango yote ya kutekwa kwa First Lady akishirikiana na watu ambao ni mapandikizi ambao kila siku unakula na kunywa nao…”
“Stop!!! Ishia hapohapo Sellina. Sasa nimeielewa TSA na kazi yake, mmefanya kazi kubwa sana na je habari zozote juu ya mke wangu?” akauliza kwa shauku.
“Ninavyoongea na wewe hapa tupo kazini, na kwa kuwa tulikwambia ni saa sabini na mbili tutakuwa na jibu, nakuhakikishia tuko mbioni kumpata First Lady katika saa zizi hizi,” Madam S alimhakikishia Sellina hayo asemayo. Baada ya dakika chache zilizofuata waliagana huku.
Oda ya kukamatwa Kepteni Benzilahagi ilifika makao makuu ya jeshi, Upanga. Usiku huohuo polisi wa jeshi, sita walikuwa ndani ya Nissan Patrol ya kijani wakielekea nyumbani kwa Kepteni huyo, walitumwa kazi moja tu, kumkamata Benzilahagi na kumpeleka walikoamriwa.
Scoba alisthuliwa na simu iliyokuwa ikifanya fujo mfukoni mwake alipoikwapua alikutana na TSA 2.
“Sema namba 2,” akaitikia.
“Kuna jamaa wanakuja hapo, waache wafanye kazi, kutoka ulipo hakikisha tu operesheni imekwenda sawa wala usitie nguvu yoyote,” Chiba akamaliza.
“Copy!”
Alipoishusha simu hiyo aliona taa za gari zilizowashwa full zikicheza na kuyumbayumba akajua moja kwa moja kuwa hiyo gari iko kasi sana kupita maelezo.
Kepteni Benzilahagi aliiweka vizuri bastola yake ikiwa full, akaipachika kiunoni mwake na kuvaa fulana yake pull neck pamija na jinzi yake nyeusi. Akaketi kitako akinywa pombe kali makusudi kusubiri kile anachokitarajia. Muungurumo wa gari ulimuondoa pale kitini, akasimama na kujiweka vizuri kitini huku simu yake iliyokuwa sikioni. Kengele ya mlango ikafuatia, akasimama na kuelekea mlangoni hapo, macho kwa macho akakutana na MP waliovalia kijeshi wakiwa kamili na barua yao mkononi ya kumkamata.
“Mmetumwa kunikamata mimi?” akawauliza huku akiwarudishia ile karatasi.
“Ndiyo, tunavyoongea hivi sasa unatakiwa kuondoka nasi,” wakamwambia.
“Kwa kosa gani hasa?”
“Kosa utalijua hukohuko ukifika,” wakamueleza.
“Sawa hakuna tabu, nipeni dakika moja tu nimuage mama watoto kisha nakuja,” akawaambia, nao wakamruhusu na kumsubiri palepale. Benzilahagi akatembea kwa mikogo huku akipiga mluzi kuelekea chumbani.
“Suzi! Suuuuzi! Mi naondoka Suzi naenda kazini…” akaongea huku akiingia chumbani na kuufunga mlango nyuma yake. Pumbavu sana, subirini hapohapo narudi, akasema kwa sauti ya kujisikia mwenyewe moyoni. Akavuta kabati kubwa na kulisukuma pembeni kisha akatoa funguo zake na na kufungua mlango uliokuwa nyuma ya kabati hilo, alipoingia ndani ya kijichumba hicho, akarudisha lile kabati palepale na kuufunga mlango kisha akateremka ngazi zinazokwenda chini kisha akapita kwenye kitu kama andaki na kutokea nje ya ukuta kulikokuwa na kitu kama chemba ya maji taka. Alipomaliza kuurudishia ule mfuniko wa chuma, akajipukuta vumbi na kutokomea katika majumba ya jirani.
“Asee huyu jamaa anaaga kwa maneno au kapanda kitandani kabisa?” MP mmoja akauliza.
“Ah kweli hebu tumfatilie hukohuko dakika kumi sasa,” mwingine aliyekuwa kiongozi wao akawaambia kisha akawaongoza kuingia ndani ya jumba lile, walipoufikia lango wa chumbani, wakagonga, kimya, hakuna jibu wakagonga tena na tena, kimya kilekile kikaendelea. Alipousukuma, ukafunguka, wakaingia chumbani, wakatanabahi hakuna mtu, kitanda tupu.
“Unataka kusema kaondoka hapa hapa?” mmoja akauliza huku akitupa godoro upande wa pili, hakuna mtu. Mwingine alikuwa akipekuwa makabati bila mafanikio.
“Jamaa katoroka, lakini kapitia wapi? Mbona hakuna mlango humu? Atakuwepo tu mumu humu. Dakika ishiririni ziliwachukua kupekua chumba hicho lakini hawakuona mtu wala nyau.
“Ni aibu, tumewezwa!” Yule kiongozi wao akaongea huku mikono ikiwa kichwani na wakati huo akitoka nje ya chumba kile, “Hebu zunguka nyumba muifanyie ukaguzi huko nje,” akaamuru na vijana wake wakafanya hivyo.
Chiba akiwa ndani ya gari yake ametulia tuli, aliona kitu kama kivuli kikipita nyuma ya ga ri hiyo, alipogeuka akamwona mtu, mwanaume anayeishia kizani. Machale yakamcheza, akainuka na kuufungua mlango taratibu kisha akafuata njia ile ambayo yule kijana aliingia. Kona ya kwanza nay a pili akasikia mlio wa injini ya gari iliyokuwa ikiwashwa na gari ile ikaondoka zake. Chiba akajikuta anashindwa la kufanya kwa wakati ule, akarudi haraka kwenye gari yake na alipoiwasha na kuigeuza akasimamishwa na wale MP.
“Teremka chini ukiwa mikono kichwani,” akaamuriwa. Chiba akateremka na kusimama akiwa mikono kichwani. Wakampekua harakaharaka na kumwacha pembeni.
“Unafanya nini hapa usiku huu?” mmoja akauliza.
“Kuna mtu namsubiri,” akajibu.
“Haujaona mtu kapita hapa sasa hivi?”
“Nimemwona, alitokea upande huu!” akajibu.
“Kaenda wapi?”
“Kapita hapa hivi kaingia upande wa pili,” akawaelekeza na wale MP wakalekea upande ule, alipohakikisha wamepotelea kizani akawash agri na kuondoka kwa kasi kuelekea upande ule ambao Benzilahagi amekwenda na gari, akajaribu kuifuata bila mafanikio, Kepteni Benzilahagi alikuwa ametoweka.
Ukimya ukatawala, Amata akasukuma juu mfuniko wa buti lile, kwa uwazi mdogo akatazama nje hakuona kitu zaidi ya giza. Wameondoka, akawaza na kufungua lile buti kisha akatoka na kulifunga taratibu, akanyata na kujibanza kando ya pipa moja lililojaa zege ndani yake. Hakukuonekana kitu kingine zaidi ya giza lile na miale hafifu ya taa za nje iliyokuwa ikipenya kati ya uwazi na uwazi. Ijapokuwa kulikuwa na giza lakini Amata aliweza kuona kwa taabu mlango wa bati uliokuwa umerudishiwa tu, akavuta hatua mbili tatu na kuufikia alipotaka tu kuugusa akasikia michakacho ya hatua za binadamu kutoka upande wa pili wa mlango ule ambao ulikuwa haujafunga kabisa na kuruhusu nafasi kama ya milimita tano hivi kuwa wazi, akarudi na kujificha nyuma yake, akasubiri.
“Tizo!” sauti ikaita kutoka ndani.
“Sema we!” Tizo akaitikia. Amata akatikisa kichwa baada ya kujua kuwa jina la huyo kijana ni Tizo.
“Usichelewe kaka, digala anatia timu sasa hivi ili tucheki mpango wa kesho,” ile sautin ikatoa maagizo.
“Poa poa,” akajibu huku akiufungua ule mlango, akatoka na kuurudisha tena nyuma yake kisha akavuta hatua kuelekea kwenye lango kubwa la chumba kile.
Kutoka alipojificha Kamanda Amata akapiga mruzi wa taratibu uliomfanya Tizo asimame pale alipo, kabla hajajua nini kinaendelea, alijikuta akipata pigo zito lililotua katikati ya paji lake la uso, kisha Amata akamdaka kabla hajafika chini. Tizo alikuwa hana fahamu, Amata akamburuza taratibu na kumpakia kwenye ile gari, ndani ya buti na kumfungia. Kisha moja kwa moja akauendea ule mlango na kuufuangua, kelele za ule mlango zilimfanya Amata kuganda kama kapigwa shoti ya umeme. Sekunde kadhaa mbele, akateremka ngazi zilizokuwa zikielekea chini ya jingo hilo na huko akakutana na mlango mwingine mzuri tena isitoshe ni wa kisasa. Akautazama kwa jicho lake la kikachero, kwa maana mlango huu haukuwa na kitasa.
Chini yake kulikuwa na zuria zito, akalikanyaga na ule mlango ukafunguka, Amata alipitisha jicho harakaharaka na kuona ndani kile chumba kuna nini. Watu wawili walikuwa wamekati katik sebule safi, mmoja mwafrika na mwingine alikuwa na asili ya kichina si kichina, kifilipino si kilipino, alikuwepokuwepo tu. Akiwa katika kutafakari, akaona mtu wa tatu akiongezeka akiwa na vinywaji mkononi. TSA 1 akaitazama saa yake, saa zinayoyoma, karibu alfajiri itanikuta, akawaza kisha akapenyeza mkono katika mlango huo na kuupeleka upande wa kushoto kuitafuta swichi ya taa hiyo maana alijuwa kuwa kaatika sheria za mafundi umeme za kimataifa swichi ya taa huwekwa upande tofauti na ule ambao mlango hufungukia. Akaipata na kuibofya.
“Ta!” mlio huo wa swichi ukafuatiwa na giza nene.
“Aaaaa shittt! Tanesco! Hili shirika bora wabinafsishe tu, namna hii!” mmoj wa wale jama akapiga makelele. Amata kama umeme akajirusha ndani na bastola mkononi, akajibiringisha na kutua kwenye kona aliyoitaka. Risasi ya kwanza haikufanya kosa, ikavunja bega la mmoja wao, ile ya pili ikafumua kichwa cha mwingine. Taa zikawaka, Amata akageuza macho mlangoni na kuona domo la bastola likimtazama, akajikunja na kuruka back akiziacha risasi za bastola hiyo zichimbe ukuta wakati yeye keishatua upande mwingine.
“Ah! Ah! Ah! Umejiingiza kwenye domo la mamba siyo?” Yule kijana aliyeonekana kujazia mwili wake akamwambia Amata, “Nilijua hutoweza kupafahamu hapa kumbe wewe mtundu sana kama nilivyopewa taarifa, sasa leo utaishia humu humu,” akaongeza huku bastola yake bado ikiwa mkononi.
“Nini kimekuleta kama si kifo chako?” akauliza.
“Nimemfuata First Lady,” Amata akajibu akiwa bado nyuma ya meza alikojificha baada ya ile sarakasi maridadi.
“First Lady! Unajua sisi tulivyomchukua tulikuwa wangapi? Na unajua mbinu tuliyoitumia? Halafu wewe uje peke yako ukiamini kumpata. Kwa taarifa yako na alfajiri hii anaondoka anapelekwa hukooooo akale honeymoon!” Yule jamaa mawnye asili isiyo rasmi akasema. Amata kwa jicho lake la kikachero aligundua kuwa huyo jamaa aliyesimama kama mita tano hivi mbele yake alikuwa hatazami upande ule isipokuwa mwingine, akageuza jicho kwa chati na kumuona Yule aliympiga risasi ya bega akiwa anachomoa bastola yake taratibu, akasubiri mkono wake ukae sawa kiunoni na lilipotimia hilo, alijirusha na kumtandika teke la usoni, mguno wa uchungu ukasikika, kwa kasi ya ajabu Amata akaiweka sawa bastola yake na kuifumua taa, giza likarudi tena na milio ya risasi ikasikika huku na huko.
“Umeniua bro!” sauti ilisikika kutoka pale chini, Amata akajua tayari washauana wenyewe kwa wenyewe.
“Nikikutia mkononi wewe nyau utajua kilichomtoa kanga manyoya,” Yule jamaa akaunguruma kwa hasira.
“Huwezi, na sasa nataka unieleze ni wapi alipo First Lady!”
“Ha! Ha! Ha! Ha! Kweli huna akili nah ii ndiyo kwa heri yako,” baada ya ile sauti kumaliza maneno yale, Yule jamaa akaanza kupiga risasi ovyo ndani ya ile sebule huku akipiga na kelele za kutisha. Amata alijikunyata kimya kwenye moja ya kuta ambapo palikuwa na kabati kubwa la vitabu, risasi nyingine zilichimba kuta, nyingine zikapita karibu na kabati hilo, Amata alikuwa akiomba dua tu zisifike pale alipo. Risasi zile zilipotulia, harufu ya baruti ilitawala.
“Aaaaaaaa hauna ujanja ushakufa wewe!” ile sauti ya Yule jamaa ikaendelea kutamba huku Amata akiskia hatua nzito zikivutwa kwa upole, akaendelea kutulia kuona kama mtu huyo atafika eneo lile. Punde tu mwanga wa kurunzi ukapiga pale alipo Amata, akaendelea kujibanza kiasi kwamba Yule jamaa hakuweza kumuona. Akasimama, akachukua simu yake na kuiweka sikioni.
“Windo letu limejileta lenyewe, liko huku fikeni haraka tumalize kazi…” Yule jamaa aliongea kwa simu na mtu wa upande wa pili, kabla hajaishusha ile simu, Amata akajitokeza na bastola mkoni lakini kabla hajafyatua guu la Yule bwana likatua juu ya mkono wa Amata na kumpoka ile bastola, konde zito likatua shavuni, Amata akaenda chini.
“Aaaaahhhh utanitambua leo,” lile jamaa lilikoroma huku likimfuata Amata na mikono yake likikunja ngumi. Likamdaka shingo, likamwinua.
“Aaaaaaiiihhhhh!” Amata alijaribu kupiga kelele na kujitikisa, wapi, alijikuta pumzi ikizidi kumwishia. Akajitahidi na kuinua mikono yake akaukamata uso wa Yule jamaa, vidole gumba vya kamanda vikatua machoni pa Yule bwana, akaanza kukandamiza. Jasho lilikuwa likimtoka Amata kwa mkabo ule lakini na yeye hakumwachia alikandamiza macho kwa nguvu na alikuwa akiongeza mkandamizo mpaka Yule bwana akaona isiwe tabu akamwacha na Kamanda akabwagika chini. Wakati jamaa anajipapasa macho yake kama yapo au la, alijikuta akipokea makonde mazito mazito ya siyo na hesabu ya liyompeleka chini.
“Na sasa utanieleza vyema yuko wapi First Lady?” Amata akang’aka huku mishipa ya hasira ikimdinda kwenye paji la uso. Akamtandika teke moja lililotua shavuni na jamaa akajibwaga upande wa pili, akajaribu kujiinua na kutambaa kwa magoti huku Amata akimfuata kwa pembeni taratibu.
“Niambie First Lady yuko wapi?” Amata akazidi kuuliza. Mara ghafla, Yule jamaa akaidaka miguu ya kamanda na kumnyayua hewani, Amata aliruka sarakasi na miguu yake ikapiga kwenye paa la juu, akahisi maumivu kwenye moja ya kisigino chake, lakini alivumilia. Yule jamaa aliokota kiti cha mbao na kumtandika mgongoni Amata akapepesuka, huku kile kiti kikitawanyika vipande vipande.
Saa ya Chiba ikapiga ukulele, akaiinua na kuangalia kwenye kioo, kijitaa chekundu kilikuwa kikiwaka, haraka akaivuta kompyuta yake ndogo na kuifungua. Kamanda Amata, akawaza, punde tu ile saa ikamfinya, akaibofya kwa juu na kuruhusu ujumbe ule uingie, kijimkanda chembamba kikajitokeza.
“Rescue First Lady…TSA 1”
Chiba aliuelewa ujumbe ule, haraka akampigia Scoba na Gina wote walikuwa tayari katika kona tofauti za jiji, akawataka kuelekea Masaki haraka, nao ila kupinga waliitii amri ya TSA2 na kuelekea pande hizo.
Chiba aliingia garii na kuondoka kwa kasi kuelekea eneo la tukio. Usiku huo hakukuwa na gari yoyote barabarani hivyo ilikuwa ni kupiga mwendo kadiri ya injini yako itakavyo.
***
Briston Kalangila aliicha barabara ya Oysterbay na kuikamata ile inayoelekea Sea Cliff, mwendo wa gari yake ulikuwa wa kasi kiasi kwamba kila lilipokata kona tairi zilipiga kelele. Huku akiwa kauma meno moyoni mwake kulikuwa na jambo moja. Huyu jamaa anastahili akatwe vipande vipande, aliwaza huku akiendelea kuliweka guu lake zito kwenye pedeli ya mafuta na kuifanya gari hiyo kukimbia isivyo kawaida.
Akili ya kikachero ya Briston alaifanya kazi, alipofika katika yale majengo, akapitiliza kwa kasi ileile na kwenda kusimama mbele kisha akateremka na kuziweka tayari bastola zake.
Kazi moja tu, kwanza jamaa wameshaharibu mpango, iliyobaki ni kutoroka nchi, akajiongelea moyoni mwake huku akipachika sawia zile bastola na kuyafuata yale majengo kwa mlango wa nyuma ambao ni wachache waliujua.
Scoba alikuwa wa kwanza kuwasili eneo lile akitokea upande wa Coco beach, mkononi akiwa na kitu kama simu alichokivaa kilikuwa kikimwonesha wapi mahala alipokuwa akitakiwa kufika, akaiinua na kuisogeza karibu na kinywa.
“Nimetua salama uwanjani!” akasema na kushusha mkono huku nusu akikimbia na nusu akitembea.
“Copy, nipo jirani,” Chiba akajibu na wote wakasikia kupitia vidubwasha vyao vidogo vilivyopachikwa sikioni.
Dakika chache jumba lile lilizingirwa na watu watatu; Chiba, Scoba na Gina aliyeingia na kuegesha gari yake nyuma ya jingo lingine kabisa. Yeye ndiye aliyemwona Briston tangu aliposhuka kwenye gari yake na kuingia kupitia mlango mdogo wa nyuma ya majengo yale. Akatikisa kichwa kwa kuwa sasa alihakiki juu uhusika wa mtu huyo, anafata nini huku? Akajiuliza na kuinua mkono wake wenye saa akaizungusha pete ile ya pembeni mwa saa yake kisha akabonyeza kitufe cha pembeni na kuisogeza kinywani.
“Briston Kalangila ameingia kwa mlango wa nyuma!” akapeleka ujumbe wa maneno ulioweza kuwafikia wote kwa wakati mmoja. Aliposhusha mkono wake na kuichomoa bastola tayari kwa lolote akauendea ule mlango aliyoingilia Briston, akasimama pindi tu alipoufikia, akatulia tuli! Akisikiliza nini kinaendelea ndani, kimya. Alipouweka mkono wake juu ya komeo ili kuufungua akasikia muungurumo wa gari nyingine, ilikuwa Land Cruiser ikasimama jirani kabisa na ile gari ya Kalangila, akashuka kijana mmoja mfupi aliyekomaa na kushupaa misuli. Gina akamkumbuka mtu huyo, alimwona kule New Afrika alipokuwa na Scoba, hakuwa mwingine, ni Kubrah Khaleb. Naye akauelekea ule mlango, Gina akajibanza nyumba ya pipa kubwa la takataka, akamtazama Yule kijana akiingia katika ule mlango kisha akaufunga nyuma yake.
Gina akatuma taarifa nyingine kwa mtindo uleule na wote wakapata ujumbe huo. Kisha akachukua simu yake na kuingiza namba za siri akampa taarifa Madam S ya kuwa wapi wapo kwa wakati huo, alipoizima na kuipachika mahala pake, akauendea ule mlango na na kuusukuma taratibu nao ukasukumika, akajitoma ndani na kujificha nyuma ya simtank kubwa la maji.
“He! He! He! We unafanya nini hapa! Na imeingilia wapi, le utachezea Masai,” sauti ya kimasai ilisikika nyuma ya Gina, hakutoa nafasi ya kusikiliza sentensi ya pili wala inayofuati, aligeuka na pigo moja la maana liliotua shingoni mwa Yule Masai na kumpelaka chini, kimya. Utaamka baadae! Akajisemea moyoni kisha akavuta hatua nyingine chache na kujificha kwenye kibaraza kilichokuwa na mlango wa kuingilia ndani. Kutoka ndani alisikia vipigo vya kimya kimya na miguno vikiendelea.
Kutoka pale chini Amata alinyakua mguu wa kiti na kuurusha kwenda kwa Yule jamaa, akaudaka na kuuvunja kwa goei lake kisha akavitupa vile vipande huku na kule, akavua shati lake na kulitupa kando hukun akiuma meno kwa hasira. Aliiruka meza na kwa minajiri ya kutua pale alipo Amata, kosa! Amata akajizungusha na nyayo la guu lake likatua kwenye korodani, Yule jamaa alitoa yowe la uchungu, Amata akainuka na kuruka tik tak na miguu yake yote miwili ikapiga usoni na kumwinua wima kisha akajibwaga juu ya meza. Kwa haraka Yule jamaa akainuka na kukutana na Amata uso kwa uso, kwa mikono yake miwili akampiga Amata huku na huku kwenye masikio kisha konde moja zito likatua kwenye chembe, Amata akarudi nyuma na kugumia maumivu. Yule bwege akachomoa kisu kikali kutoka kwenye travota yake na kumjia Amata kwa kasi.
“Aaaaaaaaggggghhhhhh! Im killliiinngggg yyyooooouuu!” pigo moja kisu kile lililikosa sikio la Amata, akaepa, pigo la pili likachana fulana aliyovaa kwa ubavuni na kuipapasa ngozi ya eneo hilo, damu zikaanza kuvuja. Pigo la tatu likatua kwenye nyama ya mkono kati ya kiganja na kiwiko. Akaitunisha misuli ya mkono, kile kisu kikatua na kuchoma sentimeta kama mbili ndani ya nyama ya mkono huo, Yule jamaa akakichomoa na kukiinua juu. Akakishusha kwa lengo la kupiga pembeni mwa shingo. Alipokishusha kwa nguvu, Amata aksogea kando na kupeleka pigo moja kali la karate likatua mbavuni na kuvunja ubavu mmoja.
Mapigo ya kifo, akawaza akilini mwake huku akipeleka pigo la kung fu lililotanguliza vidole viwili vilivyoachama, pigo lila likatua tena mbavuni na vidole vile vikakamata mbavu, kwa hasira aliyokuwa nayo, Amata aligeuka mnyama, alivuta na kufyatua mbavu nyingine, akachomo mkono na kumtandika pigo kali la paji la uso, lililomzungusha Yule jamaa kisha bila kuchelewa Amata alaongeza pigo la mwisho lililotua katikati ya uti wa mgongo na kukamata vertebra, akafuta juu na kuzifyatua kisha kwa teke lake moja akamtandika mgongoni na kumwabwaga upande wa pili akiwa hana uhai, macho yamemtoka.
“Wasalimie kuzimu!” akamwambia huku akisimama wima baada ya pigo lile la nguvu. Taa za akiba zikawaka ndani ya chumba kile. Mbele ya Amata kulikulikuwako watu watatu; Briston, Khubrah na mtu mwingine.
“Nilisikia habari zako kumbe unaweza ee?” Briston alimwambia Amata aliyekuwa kasimama imara tayari kwa lolote.
“Naweza sana kuliko unavyofikiria, siamini kabisa kama wewe, Bristona Kalangila, namba 301 TNS unaweza kusaliti kazi yako. Lakini sio kosa lako, wewe ni pandikizi na dawa ya pandikizi kama wewe ni kung’olewa ili maoteo yasipate nafasi,” Amata alinguruma huku akisimama kawaida.
Briston aliusukuma mwili wa Yule jamaa, akaitazama na ile mingine miwili, kisha akamwangalia Amata.
“TSA 1 !” akatamka kwa sauti ndogo.
“Niite Kamanda Amata, unstoppable! Kama ulikuwa hunijui ndio mimi,” Amata akainua kidole chake cha shahada na kumnyoshea mtu huyo mwenye tambo kubwa.
“Umetudhalilisha, umeidhalilisha idara, nakwambia leo hii utaeleza kila siri iliyo moyoni mwako…”
“Keleleeee!!!!” Briston akapiga ukulele na kufyatua risasi iliyopita milimita kadhaa kwa Amata.
“Wewe unaweza kuniambia mimi maneno kama hayo, wewe ni motto mdogo sana kwangu, na leo nitakuchinja kama kuku. Mlete huyo!” Briston akaongea kwa hasira na mara kijana mmoja akatokea akiwa kamkamata nywele mke wa Rais na kusukuma kwa nguvu sakafuni.
“Sasa atakatwa kichwa mbele ya macho yako!” Briston akamwambia Amata.
“Kamwe hilo haliwezi kutokea, huyo atakayemkata kichwa atakata roho sekunde tano kabla hajatekeleza hilo,” Amata akajibu na kusimama huku kajishika kiuno na damu bado zikimvuja polepole kwenye jeraha lake la mkono. Yule kijana aliyemsukuma First Lady sakafuni akauvuta upanga mkali mwembamba mkononi mwake na taratibu akamwendea Yule mwanamke na kuuinua juu.
“Na upanga huu ndiyo utakaokukata na wewe!” Briston akamwambia Amata.
“Mchinje basi, mbona unaniangalia mimi?” Amata akamwambia Yule kijana, na alipoona anaanza kushusha ule mkono, Amata akapiga kisigino cha kiatu chake chini, kisu kidogo, chembamba kikafyatuka mbele ya kiatu hicho na kikadidimia kwenye koromeo la Yule jamaa mwenye upanga. Akauacha upanga na kujichika koo huku akianguka chini na kukoroma vibaya. Kamanda Amata aliruka kutoka pale alipo na risasi za Briston zakachimba tiles za sakafu.
Mara hiyo mlango ulifunguliwa kwa pigo moja la nguvu, Gina akabingirika ndani na miguu yake ikatua kifuani mwa Khaleb, kijana huyo akayumba lakini akasimama imara na kuikunja mikono yake kwa namna ya ajabu, pigo alililolipiga likapanguliwa na Gina kwa ustadi lakini mwanmke huyu alihisi maumivu kwenye mifupa yake kutokana na jinsi Khaleb alivyokomaa mwili. Pigo la pili lilimsukuma Gina na kujibamiza kwenye kabati.
“Freeeza!” Scoba na Chiba wakaingia kwa mara moja ndani ya chumba hicho na mtupiano wa risasi haukuwa wa kawaida…
Khaleb akaona wazi kuwa hapo mambo yameishaharibika, alitazama huku na huko na kufungua mlango wa kuingia ndani zaidi lakini kabla hajapotelea, Gina alikuwa tayari wima, aliruka sarakasi moja maridadi na kutua mgongoni mwa kijana huyo, akaenda chini na kuporomoka ngazini. Khaleb akainuka kwa haraka na kurudi juu, katikati ya ngazi hizo akakutana na Gina aliyefura kwa hasira. Gina akaruka hewani na kumchapa teke maridadi lililompotezea mwelekeo kijana huyo lakini haraka alijiweka sawa na kumdhibiti Gina kwa mapigo ya kimbunga, mwanamke huyo akajikuta anashindwa kuhimili kasi hiyo huku akivuta hatua kurudi alikotoka, Khaleb alimchapa teke moja matata la kifua lililomsukuma mpaka sebuleni ambako sasa mapigano ya risasi yalikuwa yametulia.
Khaleb alipojitokeza tu akakutana uso kwa uso na Amata, pigo la kwanza lilitua mbavuni, Khaleb alipotaka kujishika kwa maumivu Amata akaruka teke kali na kumtwanga sikioni, majanga. Kijana huyo alipeleka mapigo kama kumi na tano ya karate kwa Amata lakini yote yalipanguliwa kwa ustadi, akajikuta anaishiwa.
Khaleb akatumia hila, akajikunja na kujiweka tayari kwa mapigano, akamtisha Amata kama anampelekea pigo na Amata alipoepa, mwenzake akaruka sarakasi na kujipiga kwenye kioo kikubwa cha dirisha, kikapasuka naye akatoka nje, akainuka haraka na kukimbia. Chiba na Scoba bastola mkononi wakapita palepale dirishani na kuanza kumtoa mbio huku wakirusha risasi lakini Khaleb alikuwa mwepesi zaidi yao, alikwea ukuta kwa jinsi ya ajabu na kujitupa nje.
Taa za gari za polisi zilipendezesha anga la nje ya majengo hayo, vijana walioongozwa na Inspekta Simbeye waliwasili dakika chache baada ya Madam S na Hosea Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa (TNS) kuwasili.
Ndani ya sebule hiyo walikuta hali mbaya ya vifo na mapigano. Madam S alielewa kuwa ni dakika chache tu zilizopita mirindimo ya risasi ilisitishwa kutokana na harufu kali ya baruti. Bwana Hosea alipoingia tu alikutana macho kwa macho na Briston Kalangila, mtu wake katika idara namba 301 aliyemoa jukumu la kuongoza wana intelijensia ndani ya jengo la tukufu la Ikulu. Akatikisa kichwa na kumtazama kwa makini.
“Huyu ni nani Briston?” akamtupia swali huku mkono wake ukimwoneshea mke wa Rais ambaye alikuwa ameketi na kuuegemea ukuta.
“First Lady! Nimemkuta humu ndani,” akajibu huku akisimama.
“Amekujaje?” swali la pili.
“Ametekwa, na mimi kama mdau wa usama nilikuwa katika kumwokoa kutokana na kazi na cheo change nilipaswa kufanya hivyo nikiwa undercover,” Briston akaeleza, “Na hawa vijana nahisi majambazi ndiyo waliyokuwa wakinizuia mimi kufanya kazi yangu kama mwanausalama,” akaongeza.
“Acha uongo Briston!” Madam S aling’aka, “Hivi unatufaya sisi hatuna akili siyo? Nani asiyejua uliyoyafanya? Na utaenda kueleza yote leo, tuliku suspect tangu siku za mwanzo, tutakuhiji zaidi na tutaujua ukweli,” Madam akang’aka.
“Umeniuzi, umenisaliti, mchukueni!” Hosea akamwambia Madam S. inspekta Simbeye aliingia ndani ya sebule hiyo, na mara moja wakamtia pingu Briston na kutoka nae. Polisi wengine wakachukua miili ya marehemu na kuibeba machelani kuiondoa eneo lile.
“Pole sana mama!” Madam S alimpa pole First Lady huku akimwinua kutoka pale alipoketi, “Amata, pekua nyumba hii mwanzo mwisho. Simbeye majengo haya yaw echini ya ulinzi wa polisi mpaka amri nyingine itakapotolewa, ujenzi usimamishwe kwanza ili uchunguzi uchukue nafasi yake,” akamaliza na kuvua koti lake kubwa alilovaa na kumvika First Lady kwa kuwa nje kulikuwa na manyunyu mazito ya mvua.
8
NDURUTA
TAARIFA HIYO ya kusambaratika kwa mpango mahsusi uliopangwa na Mkuu wa Wakuu, Rais wa Nduruta Mheshimiwa Sebutunva ilifika makao makuu ya nchi hiyo, na ilipokelewa na mwenye Rais. Alikuwa ameketi, akasimama, akajishika kiuno kisha akaeti tena na kuiinamia meza safi iliyotangenezwa kwa fomika. Kichwa kilimzunguka akiwa hajui lipi la kufanya, hasira ya wazi ilionekana kumtawala. Akamwita mpambe wake.
“Tafadhali, toa taarifa kuwa siwezi kuonana na mtu yeyote kwa leo, najisikia vibaya,” kisha akasimama na kutoka mle ofisini huku akimwacha Yule mpame akitoa saluti ya utii.
Kiongozi huyo alitoka kwenye jumba lile ambalo ni mkaoa makuu ya nchi na kuelekea katika nyumba yake binafsi iliyojengwa katika milima ya Haropolo nje ya mji mkuu wa Nduruta. Katika nyumba hii alitumia sana kupumzika wakati ambapo hakuwa na kazi ofisini hasa siku za mwisho za juma.
“Mpango umesambaratika…” sauti ilisikika katika simu aliyokuwa ameiweka sikioni, sauti hiyo ya mmoja wa watu wake, Kepteni Benzilahagi.
“Taarifa hiyo imenichukiza sana kwa sababu imeharibu mipango yetu yote, anyway najua mimi nini nitafanya, nashukuru kwa maelezo na taarifa zote za hao jamaa nimewajua wanavyoketi na wanavyosimama, na sasa najua nitashughulika nao vipi. Nenda mapumzikoni nitakapokuhitaji nitakwambia, code yako ya simu ya siri iwe ileile tafadhali,” akamjibu kisha akakata simu.
Rais Sebutunva akatulia kimya kisha akatikisa kichwa kana kwamba kuna kijimdudu kimeingia sikioni lakini sivyo. Nitamwadhibu, haniwezi hasilani! Akapitisha uamuzi na kisha akvuta simu nyingine na kuongea na washirika wake, nao waliipokea habari hiyo kwa masikitiko na kukubaliana kila mmoja katika nchi yake atafute jinsi ya kumbana Rais wa Tanzania ili kumkomesha.
Kama kuna kilichomuumiza kichwa zaidi ni kutojulikana wapi yupo Briston Kalangila, pandikizi lake alilolipenyeza katika idara hiyo miaka kadhaa nyuma a ndiyo aliyempangia mpango mzima wa kumteka First Lady. Baada ya taarifa kutoka kwa Benzilahagi kuwa amekoswakoswa kukamatwa na Yule afisa ubalozi naye aliyeporochoka sekunde za mwisho, Sebutunva aliambiwa wazi na kijana huyo kuwa Bristoni kalangila hakuwa naye isipokuwa alikuwa na wale magaidi wa kukodi waliokuwa wakimshikilia Fisrt Lady na ndiyo waliyoukamilisha mpango huo. Jitihada za kumtafuta Briston ziligonga mwamba katika simu zake zote. Sebutunva akaishiwa nguvu, kama watakuwa wamemkamata, nimekwisha maana anaweza kutoa siri zote, akawaza kwa msikitiko. Wacha niliache ila kesho lazima niandae hotuba ya nguvu kwa watu wangu na najua tu hata wao wataisikia, akawaza na kujifariji kwa hilo.
SIKU ILIYOFUATA
SHEREHE ZA UHURU WA NCHI YA NDURUTA
KITUO CHA TAIFA cha Televisheni ya Nduruta kilikuwa kikirusha matangazo ya moja kwa moja kutoka mji mkuu ya nchi hiyo. Siku hiyo kulikuwa na seherehe kubwa ya kitaifa iliyowakutanisha wananchi wengi wan chi hiyo katika uwanja mkubwa wa mpira na mwisho wa sherehe hizo Rais wan chi hiyo alilihutubia Taifa, hotuba iliyoshangiliwa kwa nderemo na vifijo na wananchi wa Nduruta.
Katika hotuba hiyo ilionesha wazi Rais huyo kuwa na hasira hasa kutokana na mashambulizi ya waasi kule Mpumbutu, alilisema wazi jeshi la UN lililoshirikiana na majeshi ya Tanzania kuwasmbaratisha waasi hao kwani limekiuka mkataba wa kimataifa wa kulinda amani katika eneo hilo. Alilishambulia jeshi hilo kuwa badala ya kulinda amani ya eneo hilo wao wameua waasi.
Huku akishangiliwa na wananchi wake alisisitiza kuwa nchi yake haiwezi kukaa kimya na lazima jumuia ya Kimataifa ilizungumzie suala hilo na si kulifumbia macho. Baada ya hotuba hiyo kali na ya kibabe kulifuatiwa na michezo ya kivita kutoka katika jeshi hilo la Nduruta huku likionesha zana zake za kivita za kisasa kabisa ambazo ilisemekana kuwa hakuna nchi iliyowazunguka ambayo inamilika zana kama hizo za karne hii.
Baada ya maonesho hayo kulifuatiwa seherehe katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo huku Sebutunva akikutana na wageni wake katika hafla iliyoandaliwa ndani ya jingo la Ikulu. Kati ya wageni wengi walialikwa Rais wa Tanzania hakualikwa katika sherehe hizo na kila mmoja katika ugeni huo alikuwa akijiuliza mwenyewe pasi kuwa na jibu. Ikabidi wamezee tu, wapo waliojua mgogoro huo wa chini kwa chini na wapo ambao hawakujua lolote.
DAR ES SALAAM
SIKU YIYO HIYO
Rais Robert Sekawa wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na sura yenye tabasamu, alizima luninga yake ya ofisini na kuitupi rimoti kwenye meza ndogo iliypo jirani yake, akavuta faili lake la khaki akapekua hapa na pale kisha akalifunga na juu yake kulionekana herufi moja kubwa na tarakimu mbili nyeusi ‘X65’. Mmeisoma namba, akajisemea. Ndani ya Ikulu hiyo wafanyakazi hasa wa idara ya usalama walikuwa hai hai kuweka sawa hili na lile baada ya kutembelewa ghafla na Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo Bwana Hosea.
Nusu saa baadae, msafara wa Rais uliondoka mpaka Hospitali ya Muhimbili kwenye wodi ya watu wazito, huko alikuwa amelazwa First Lady akipatiwa tiba hii na ile baada ya kuokolewa kutoka mikononi mwa wale magaidi watekaji. Hali yake ilikuwa sawa, alikuwa amekwisharuhusiwa. Boadyguard wake alikuwa makini pale pembeni tu mwa kitanda. Baada ya itifaki za hapa na pale waliondoka na kurudi nyumbani ambapo daima huwepo kwa mapumziko.
OFISI NDOGO
“Pole sana Amata kwa majeraha, naona safari hii ngoma ilikuwa nzito mpaka umekubali kisu kitue mwilini mwako!” Madam S akampa pole Amata aliyekuwa na bendeji mkononi mwake na plasta kadhaa ubavuni mwake lakini shati alilovaa lilizuia zisionekane.
“Asante sana, ilibidi niruhusu kisu hiki kitue mkononi ili nipate wasaa wa kumwadhibu mshenzi Yule kwa uzuri na mbinu yangu ilifaa,” akajibu.
“Kazi haijaisha vijana, tumempata First Lady, lakini tumetorokwa na watu watatu, Benzilahagi Kepteni wa Jeshi, Yule afisa wa Ubalozi, Banginyana mwenyewe na huyu sijui tumwite gaidi au kaburu huyu nani huyu Khaleb. Kama tunataka mti usimee tena lazima tuondoshe na mizizi yake,” Madam aliongea, “Nini mmepata kule jana? Chiba !” akaongeza.
“Madam ile si nyumba wala sio jingo ile ni kambi ya jeshi, tumekuta silaha za kivita, mabomu ya aian aina, na vitu vingine visivyofaa, isitoshe tumekuta waraka mzito sana ambao ulitutisha na laity tusingewahi kulichunguza swala hili basi miezi michache ijayo tungongea mengine,” Chiba akaeleza huku akitoa bahasha moja kubwa na kumkabidhi Madam S.
“Enhe!” Madama akabetua kichwa chake.
“Na pia tumeikuta hii pasipoti,” akamkabidhi. Madam S akaipokea na kuifungua akasoma maelezo yaliyomo ndani na kuitazama picha ya huyo mwenye pasipoti.
“Kubrah Khaleb,” akatamka jina aliloliona hapo.
“Katika maelezo niliyoyaangalia katika mtandao wa wahalifu duniani…”
“Kama kawaida yako,” Madam akamkatisha.
“Kama kawaida; huyu jamaa ni gaidi anayetafutwa huko India, inasemekana ndiye aliyesababisha ile ajali ya treni pale New Delhi, ametoroka na hajulikani alipo,” akaeleza.
“Kwa hiyo hii ndiyo pasipoti ya Gaidi?” akauliza Madam, wote wakacheka.
“Ndiyo, pasipoti ya gaidi,” Chiba akajibu. Kisha akeleza na mengine mengi ambayoo yaliwekwa kwa picha na maandishi.
“Sawa, sasa uchunguzi wetu wa pili utaanzia katika kile tulicho nacho, ambacho mtuhumiwa mmoja na pasipoti ya gaidi, baada ya hapo tutaona hatua nyingine lakini jueni kwamba kazi haijaisha. Amata upone haraka, Dr. Jasimin yuko njiani ataingia usiku wa leo kwa ajili ya majeraha yako tu kisha ataondoka tena kwani kazi yake hajamaliza bado,” akamaliza na kuwaanglia vijana wake, “Gina, hakikisha mzigo unafika hapa mara moja kwa siri, Scoba kamata usukani kama kawaida na Chiba weka ulinzi, Amata twende ground zero,” wote wakanyanyuka na kila mmoja alijuwa wajibu wake kwa wakati huo.
KITUO KIKUU CHA POLISI
CHUMBA KILIKUWA NA GIZA ukimya mzito ulitawala, kelele za watu waliokuwa vyumba vingine ama wakilia kwa vipigo au wakipiga makelele tu ya hasira ndizo zilisikika. Lango la chuma la chumba hicho lilifunguliwa askari mmoja akaingia akiwa kavikwa soksi usoni mwake lakini huku mwilini alionekana na sare ya kipolisi ya kawaida. Hatua zake zilikuwa nzito si hivyo unavyofikiria wewe bali kwa kuwa Briston alikuwa amechoka sana akaona hatua hizo zikiwa nzito na Yule kijana akamfikia. Katika mkono wake alikuwa na guo kubwa jeusi zito, akamvika Briston kichwani na kulifunga kwa shingoni.
“Mmmmmh mhhhh!” Briston aliunguruma lakini hakuweza kuongea lolote kwa nukta hiyo. Akamwondoa kwenye kile kiti akiwa na pingu zilizofungwa kwa nyuma na mnyoror uliofungwa miguuni kwake na kumpa nafasi ya kutembea japo kwa mwendo wa hatua ndogondogo tu. Akatolewa ndani kupitishwa njia ya ndani kwa ndani huku kelele za wahalifu wengine zikisikika maana walimwona akipitishwa.
Katika moja ya chumba kidogo gari moja Land Cruiser ilikuwa imeegeshwa huku ikiwa inanguruma. Mlango ukafunguliwa, Briston akaingizwa ndani yake na kuketi katika kiti cha peke yake, nyuma yake kuliketi watu wawili na mbele waliketi wawili pia. Ile gari ikatoka taratibu pale ndani. Kutokana na vyoo vyake vyeusi, vinene, visivyoingia risasi, iliondoka na mtu myeyote asiweze kuona ndani yake kuna nini au kuna nani…
SHAMBA
SAFE HOUSE
DAKIKA TISINI BAADAE ile gari iliegeshwa katika jengo maalumu huko Gezaulole, jingo kuukuu la kihistoria lililotelekezwa miaka mingi. Ndani ya jingo hili kulikuwa na ofisi mbalimbali ambazo TSA walikuwa wakizitumia. Kwa ujumla lilikuwa jingo la siri sana, hakuna mkazi aliyekuwa akilisogelea kwa kuogopa kile kinachodhaniwa mashetani au wanyonya damu. Muda wote lango lake lilionekana limefungwa ni mara chache tu lilionekana kufuguliwa na hata hivyo hawakuwahi kumwona aliyelifungua isipokuwa lenyewe peke yake lilikuwa likijifungua na kujifunga.
Hakuna aliyezungumza, mara tu gari ilipoegeshwa Briston aliteremshwa akiwa katika hali ileile ya kufunikwa uso wake, pingu na minyororo mikononi na miguuni, alikokotwa namna hiyo mpaka kwenye chumba maalumu kilicho ndani kwa ndani, akaklishwa kweye kiti cha chuma, miguu yake ikabanwa katika miguu ya kiti kile kwa kufungwa kwa vifaa maalumu.
Chiba aliwasha mitambo yake katika chumba maalumu tayari kwa kurekodi kile atakachokizungumza mtu huyo. Ndani ya chumba kile kulikuwa na watu wawili, Kamanda Amata na Scoba. Gina na Chiba walikuwa katika chumba kile chenye mitambo hiyo ya kurekodia. Briston alikuwa ameketi kitini na lile guo jeusi lililofunika kichwa chote.
Ndani ya chumba kingine cha siri ambacho kilitumika kuegesha gari hizo maalumu za TSA ilisimama Land Rover ambayo ilikuwa na madirisha mawili tu upande wa dereva lakini sehemu ya nyuma ilifungwa kabisa. Madam S akateremka kutoka upande wa dereva upande wa pembeni wa gari hiyo kukafunguka mlango na Hosea, Mkurugenzi wa idara ya Usalama wa Taifa na wasaidizi wake wawili wakateremka na kushangaa eneo hilo waliloingizwa.
“Huku tafadhali!” Madam akawaelekeza na jamaa hao wakamfuata mpaka kwenye chumba maalumu kilichofunguliwa kwa ajili yao. Wakaingia ndani ya chumba hicho na kumkuta Kamanda Amata pamoja na Scoba lakini hawakuweza kuwatambua kwa kuwa walikuwa wamevaa sox na kuficha nyuso zao.
“Mtu wenu huyu hapa tunahitaji kujua nini na uhusika wake katika sakata zima la uvamizi wa Ikulu,” Madam S akamweleza Hosea. Kimya cha sekunde kadhaa klikapita, Mkurugenzi huyo akawapa ishara vijana wake kuwa wafanye kazi yao, hawa walikuwa na taaluma ya utesaji tu na siyo kitu kingine. Taa kali ikawashwa kummulika Bristona usoni na mmoja wale jamaa akamwondoa lile guo usoni mwake, mwanga mkali wa ile taa ukampiga usoni, akatikisa kichwa na kushindwa kuwatazama vizuri watu waliopo katika chumba hicho.
“Briston Kalangila, umesaliti ofisi na kazi yako, ukajiingiza kwenye hujuma dhidi ya taifa lililokulea?” Hosea akauliza.
“Hapana!” akajibu kwa sauti ya kukwaruza.
“Katika lile jingo kule Masaki ambako kikosi maalum kilikuwa katika uokozi wa First Lady, ulikuwa unafanya nini?” Hosea akauliza tena.
“Nilikuwa katika majukumu ya kikazi mkuu!” akajibu.
“Inasemekana bastola yako imeua watu wawili ambao ni wafanyakazi wa idara ya usalama katika jingo la Ikulu…” Hosea akachimba swali.
“Si kweli, mapigano yalikuwa makali sana na tulizidiwa na watu wale kwa kila hali,” akajibu kwa kujiamini. Hosea akawapa ishara wale vijana wake kwamba wamtie disprin kidogo. Wale vijana ambao muda wote hawakuonesha hata tabasamu, mmoja wao akafungua mkoba wake na kutoa taulo huku mwingine akiomba kusogezewa maji yaliyokuwa katika dumu kubwa la lita kumi na mbili. Biston akafunikwa taulo usoni na miisho yake ikakutanishwa nyuma ya kichwa chake, alijaribu kugugumia lakini watu wale wawili hawakuonesha kuwa na huruma hata kidogo. Kile kiti kikabinuliwa kwa nyuma na kumfanya Briston atazame juu, kichwa chake nacho kikainuliwa na kisha Yule mwingine akafungua lile dumu na kumimina yale maji usoni mwa Briston kwa sekunde thelathini.
Briston alijaribu kujirusharusha pale kitini lakini hakufaulu lolote, alitikisa kichwa lakini kilibanwa sawasawa, alishindwa kupumua na kujikuta maji yale yakiingia puani na kumpa mateso makali. Baada ya kuonesha ishara, wale mabwana wakaistisha zoezi lile na kumuweka Bristoni sawa kama alivyokuwa mwanzo, wakamwondoa lile taulo. Briston akapiga kelele, akatikisa kichwa, akapiga chafya, alikuwa akihiema kwa nguvu na pumzi zake zilikuwa zikikoroma. Teso hilo lilikuwa ni teso bay asana ambalo hata Madam S hakutegemea kuliona katika kazi yake lakini hakusema lolote kwa kuwa kazi ni kazi.
Baada ya chafya zile na akili kumkaa vizuri, zoezi lile lilirudiwa tena kama mara tatu hivi, Briston alijikuta katika hali mbaya, alipiga chafya na kuvujwas maji kwenye pua zake, alikohoa na kutapika maji.
“Aaaaaaa! Akkkhhhaaaaaa! Yes, Yes,” Briston alijikuta akiropoka huku bado akitapika . Hosea akatembea tembea huku na huko, akasimama na kumtazama Briston huku akimkinga kwa lile taa kali.
“Ulikutana na Benzilahagi Yule Kepteni wa jeshi pamoja na afisa balozi kutoka ubalozi wa Nduruta katika Casino ya Las Vegas Upanga, Briston unajua wazi kuwa jeshi la Tanzania lilikuwa huko Ngoko kupambana na waasi, na inasemekana hao waasi waliokuwa chini ya Banginyana Kanali mtoro wa Nduruta. Unajua nini juu ya hilo?” Hosea akuliza. Briston akabaki kimya.
“Again!” akasema. Na wale vijana wakarudia lile zoezi mara nyingine, Briston aligugumia na akaachwa huru kwa mara nyingine.
“Mkuu, mkuu, mkuu unaniua mkuu, koh! Koh! Koh!” aliongea na kukohoa kwa nguvu huku akitema maji, Briston sasa alikuwa katika hali mbaya zaidi.
“Aaaaaakkkhhhh! Khaaa! Khaaa!” Akahema kwa nguvu na kwa taabu, “ Yes, tupo, tupo wengi,” akajibu kwa taabu.
“Wengine wapo wapi? Na ni akina nani?” Hosea akauliza.
“Wapo, wengine we-ngi wa-po nda-ni ya wa-ki-mbi-zi, khaaaaak! khaa!” akakoroma na kutema maji ya kutosha, “…na na ha-ta aaaa ha! ha! ha!…”
“Unacheka? Unafikiri tupo kwenye kicheko hapa! Malizia kauli yako…” Hosea aling’aka.
“Aha! Aha! Aha! … hii vita ni ku-bwa sa-na, haiishi leo wa-la ke-sho…”
“Na mapandikizi yake yako wapi? Kabla hatujakuongezea dozi nyingine…”
“Aaaa Mkuu.. ma-mapandikizi, aaaaha! Aha! Aha!… hata ha-pa wapo, na wata-kuteke-te-zeni…”
“What!” Hosea akashangaa, na jambo lisilotegemewa likatokea. Wale jamaa waliokuwa wakimtesa Briston, walimwacha na na kuchomoa bastola zilizokuwa viunoni mwao. Kamanda Amata aliruka kutoka aliposimama na kumpiga dabo kiki Madam S, akaanguka upande wa pili na risasi za yule jamaa zikamkosa na kuchimba ukuta.
Yule mwingine risasi zake zilikata vile vifungo vya chuma na Briston akawa huru, akanyanyuka na kukibetua kile kiti kwa miguu yake kisha akakipiga kikiwa hewani na moja kwa moja kikatua kwenye kioo ambacho kilitenganisha kile chumba na kile cha mawasiliano walichokuwa Chiba na Gina lakini kioo kile hakikuonesha hata dalili ya ufa au kuathirika.
Scoba alijitoa pale alipo, akabingirika chini na guu lake likatua tumboni mwa mmoja wa wale vijana, akayumba na kufyatua risasi ovyo. Kutoka pale chini Briston akajinyanyua haraka na kukutana uso kwa uso na Hosea.
Kamanda Amata akaona hapo mambo yameharibika, kwa sekunde kama tano hivi ndani ya chumba hico ilikuwa hekaheka. Wakati Hosea anajaribu kujiweka sawa, risasi ya mmoja wa wale jamaa ikatua begani mwa Hosea, nay a pili ikatua pembani kidogo mwa bega hilohilo lakini sasa ni kifuani, Hosea akapaishwa na kujibamiza ukutani, isha akajibwaga chini. Mlango ukafunguliwa wale jamaa wakamkamata Briston kumtoa nje. Amata aliinuka na kujitoa mhanga, kama kuna kitu ambacho walijilaumu ni kuaminiana kiasi kwamba waliingia ndani ya chumba hicho bila silaha. Risasi zilikuwa zikirindima bado huku wale jamaa wakitoka ndani ya chumba kile wakiwa na mtu wao.
Chiba alishangazwa na hali ile, akampiga Gina begani na Gina akavuta droo na kutoa bastola, moja akaipachika kiunoni na nyingine akaikamatia mkononi, Chiba akafanya vivyo hivyo, wakauendea mlango, Chiba akaufungua na kutulia kando, Gina akapita na kujibana kwenye mlango mwingine, Chiba naye akafuatia na kisha wakaingia milango tofauti wanayoijua wao na kuuweka kwenye shabaha mlango mkuu.
Katika chumba kile cha mateso, Hosea alikuwa chini akigalagala na damu zikimvuja, baada ya wale jamaa kutoka na Briston ndani ya chumba kile, Amata alimuwahi Hosea na kuchomoa bastola zake alizokuwa amezibana ndani ya koti, akaziweka sawa, na kujitokeza kwenye ule mkango huku akiwaona wale jamaa wakipotelea katika mlango mwingine. Kwa shabaha hadimu alifyatua risasi na kuliwahi bega la Yule jamaa.
Maumivu makali yakapenya bega la Yule mjinga, akamwacha Briston na kupiga kelele za maumivu.
“Jikaze! Twende!” mwenzake alipiga kelele huku akirusha risasi zilizowazuia Gina na Scoba kujitokeza. Kamanda Amata alivuta hatua kwa kukimbia kule aliko Yule jamaa, alipomkaribia akaruka hewani na kutanguliza miguu yake, hiyo ilimfanya Yule bwege kushinwa kufanya lolote, wakati akijitafakari, miguu izito ya Amata ikatua kifuani mwake na kumpeleka chini, na wakati huohuo risasi zilimiminwa pale walipo lakini ziliwakosa.
“Wasiende popote hao, Kamanda!” Madam S alipiga kelele. Kamanda Amata alitua chini na Yule jamaa, akakamata kichwa chake na kukipiga chini, Yule jamaa akapoteza fahamu. Amata akanyanyuka haraka na kupita mlango mwingine ambao alijua kwa vyovyote vile angekutana nao. Kwa upande wa ndani Gina na Chiba walikuwa na kazi ngumu ya kupambana na wawili hao.
Briston na kijana wake walikuwa mahiri wa kukwepa mashambulizi na kutupa risasi zilizoharibu samani nyingi za nyumba ile. Walikuwa wamekaribia kabisa pale ile Land Rover iliposimama ambapo ni ndani kwa ndani ya jumba lile.
“Kamata usukani kijana niwafundishe adabu hawa manyang’au,” Briston alimwambia Yule kijana huku akikamata vyema Shot Gun kutoka kwa yule kijana wake, akawa anafayatua kumlenga Gina na Chiba ambao walidhibitiwa na risasi hizo ambazo ziliwafanya washindwe kujitokeza.
“Nani aliyekwambia mtu akiingia humu huwa anatoka hai?” Sauti hiyo ya Amata ilimfanya Briston kushtuka, alipogeuka alikutana na yule jamaa aliyevaa sox usoni. Kamanda Amata akavua ile soksi usoni na kuacha sura yake wazi, Briston alibaki kaduwaa.
“Unashangaa ulifikiri nani, ni mimi unstoppable!”….
Amata alimwambia. Kutoka ndani ya ile gari, Yule kijana ambaye alikuwa tayari kwenye usukani, aljitoa kimasomaso na silaha yake mkononi, akampiga kikumbo Briston na kurusha risasi upande wa Amata lakini akiwa bado hewani, bastola ya Chiba ilifanya kazi nzuri sana pale tu alipojitokeza na Yule bwege akabwagwa chini mzima mzima akiwa na hali mbaya. Wakati huo Kamanda Amata alikuwa tayari ameshahama eneo lile na kujitupa kando. Akanyanyuka haraka na kumwahi Bristo ambaye naye alikuwa chini akitambaa kuifuata ile bunduki yake ambayo sasa ilikuwa kama mita moja hivi, si mbali sana, lakini kabla hajafika alijikuta akipigwa teke moja kali la mbavu, likamgeuza uelekeo, akajibiringisha na kuinuka, kabla hajakaa sawa alimwona Amata akija kasi, akajihami na kukinga mikono.
Amata alipoona hilo akageuza mbinu, aliruka na mguu wake ukakanyaga kwenye ukuta kisha akaruka sarakasi ya kujibatua nyuma na kumshindilia mateke mawili maridadi kabisa kifuani. Briston aliyumba naye akaachia pigo moja zito lakini lilipita hewani kwani Amata alikuwa tayari katua upande mwingine. Alipogeuka amtazame kijana huyo akakutana na mapigo ya karate ambayo yote aliyapangu kisha akapiga pigo moja matata lililomfikia Amata usoni na kumrudisha nyuma. Damu zikamtoka kwenye tundu moja la pua, akafuta na kuitazama, ikamtia hasira. Kamanda akizungusha mikono yake kwa kasi ya ajabu na kuona jinsi mboni za macho ya Briston zilivyokuwa zikihangaika kuitazama hiyo mikono, akamwendea na badala ya kumpiga kwa mikono, akamchota ngwala moja maridadi, akaenda naye kimo cha ndama, kisha akaijigeuza hewani, wakati Briston anafika chini yeye akashuka nusu sekunde baadae na kumtandika kwa kisigino katikati ya kifua. Mwanaume Yule akajiviringa chini na kuinuka wima huku akitema damu.
Pigo limemwingia, Amata akawaza na kutikisa kichwa. Briston akamvamia Amata kwa konde zito la kilo nyingi, Amata akageuka mzima mzima na lile konde likapita juu ya bega huku Bristona akiwa nyuma yake, akaudaka mkono wa jabali hilo na kuukunja kwa nguvu.
“Aaaaaaaiiihggghh!” Briston akatoa yowe la maumivu. Amata akavunja mifupa ya ule mkono kissha akamgeukia na kumpa vichwa vitatu vya maana, makonde na mateke mazito mazito. Briston akajibamiza ukutani na alipojitoa kurudi, TSA 1 aliruka hewani na kumtadika mateke mawili ya upande mmoja wa kichwa na kumpeleka chini hoi. Briston hakuwa na nguvu tena ya kunyanyuka mahala pale, Chiba na Gina walisogea taratibu, Yule kijana mwingine alikuwa tayari hana uhai.
Kwa taabu asana aliinua uso wake na kumtazama Amata, kisha akarejesha kichwa chake sakafuni.
HOSPITALI YA MUHIMBILI
ULINZI MKALI wa polisi uliimarishwa kwa tika hospitali hiyo ya Taifa, vijana wa FFU ndani ya mavazi yao ya kikazi walizingira hospitali hiyo kila kona kuhakikisha kuwa mtuhumiwa au watuhumiwa aliopo humo wasifanikiwe kutoroka.
Katika moja ya vitanda vya chuma, Briston alilazwa huku pingu moja ikiwa mkononi mwake na ule mwingine ukiwa na ogo, kijana wake aliyenusurika lakini akiwa kavunjwa bega alilazwa katika wodi nyingine naye akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Katika moja ya vyumba vya watu maalumu VIPs, Hosea alikuwa amelazwa huko na hali yake ilikuwa tete kwani alikuwa akipumulia mashine huku madaktari wakiwa makini kumwangalia. Madam S alisimama pembeni mwa kitanda hicho akimtazama mkurugenzi huyo akiwa hoi pale kitandani.
“Hali yake inaendeleaje?” akamwuliza muuguzi aliyekua jirani na hapo.
“Siyo mbaya, anaendelea vyema usihofu,” Yule muuguzi akajibu. Madam S alitoka ndani ya wodi hiyo na kusimama nje kabisa akiangalia nyendo za watu waendao na warudio. Dakika kama mbili hivi, BMW nyeusi ilisimama kando yake, akateremka ngazi na kuingia kisha ile gari ikaondoka.
Kituo kilichofuata ilikuwa ni Ikulu, Madam S aliikuwa na kikao maalum na Mkuu wa Nchi siku hiyo, akainua mkono wake na kutazama saa iliyotulia vema. Saa nane mchana, ilimwonesha, akateremka na kuzipanda ngazi, moja kwa moja akaongozwa mpka katika ofisi maalumu ambayo dakika chache tu Rais Robert Sekawa aliungana naye.
“Pole kwa majukumu Selina!” akampa mkono na kisha kuketi, akaamuru walinzi wake waondoke na kuwaacha wao wawili tu, “Ndiyo, sikuamini kabisa kama Briston anaweza kuwa msaliti…”
“Usiseme msaliti, sema pandikizi na sio yeye tu wako wengi sana , yeye mwenyewe amekiri jana kuwa wapo wengine tena kwenye idara nyeti na muhimu za serikali,” Madam akamkatisha, kisha akatulia kidogo. Akaingiza mkono katika mkoba wake na kutoa mashine ndogo ya kunasa sauti akawasha na kuiweka katikati yao, waksikiliza mahojiano yote mpaka pale palipoanza mapigano. Rais Robert alibaki kinywa wazi, kaduwaa kwa yale aliyoyasikia.
“Ok, sawa najua hatua za kuchukua lakini kwanza inabidi kufanya uchunguzi mkubwa wa kiitelijensia katika idara zote kuona kama kuna yeyote aliyechanganyika uraia basi tumuwekee kiulizo…”
“Zaidi, Briston anawajua nahisi hata kwa majina na wapi walipo maana kasema wapo kwenye idara nyeti za serikali na pia miongoni mwa wakimbizi waliopo huko mipakani na wengine ndani yetu ambao tumewapa na uraia kabisa,” madam akamkatisha tena na kumdadavulia juu ya hilo.
“Hali yake ikoje?” akauliza Rais.
“Nani?”
“Briston,”
“Sio mbaya, hakupata kipigo cha kufa ila cha kulegeza mwili,” Madam akaeleza.
“Sawa, Briston atakaa gerezani kwa amri yangu, na hatoruhusiwa kuliona jua, nitaongea na Kamishna wa Magereza juu ya hili, ili tumbane polepole na atueleze,” Rais alisisitiza.
Mazungumzo yao yalichukua takribani saa mbili na kuweka mambo mengi sawa.
SIKU ILIYOFUATA
GEREZA LA UKONGA
MSAFARA WA GARI za polisi na ile Defender ya Magereza ambayo ndani yake Briston na kijana wake waliwekwa ulikuwa ukiegeswa katika lango la mahabusu lililopo upande wa kusini wa gereza hilo. Briston akateremshwa akiwa kafungwa minyororo miguuni na pingu katika mikono yake. Akaamuriwa kuchuchumaa chini, kisha akafuatia kuteremshwa Yule kijana wake na baada ya hapo wakaingizwa ndani ya mahabusu hiyo.
Saa mbili baadae walitenganishwa na kila mtu kuwekwa katika chumba chake, ndani ya chumba hicho kulikuwa na kitanda kidogo kilichojengewa ukutani na godoro jembamba na blanketi, hakikuwa na taa.
“Haya ndiyo makazi yako kwa sasa!” Yule askari maegereza akamwambia na alipotoka katika eneo lile mlangoni akasimama Chiba na Amata. Wakatazamana kwa sekunde kadhaa.
“Briston Kalangila, TNS 301, mbio za sakafuni huishia ukingoni. Haya ni makao yako mpaka utakapoamua kuiambia serikali ukweli na mpango mzima kwa jinsi ulivyo, kinyume na hapo utazeeka na kufia humua ndani kifo ambacho hutokisahau katika siku zako zote utakazokuwa kaburini, nitakuja kukuona tena,” Amata akamaliza. Alipotoka pale mlangoni Yule Askari Magereza akalifunga lile lango lililotanguliwa na lango linguine la chuma.
“Kunnnnhhhh!” mzizimo wa lango lile ulipenya katika masikio ya Briston, giza likakijaza chumba chote hapakuwa hata na tone la mwanga, akapapasa na kukifikia kile kitanda, akiwa ndani ya nguo maalum za kifungwa, akajilaza juu yake.
? MWISHO ?
Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;