Mwanamke Mwenye Juba Jeusi Sehemu ya Tano
KIJASUSI

Ep 05: Mwanamke Mwenye Juba Jeusi

SIMULIZI Mwanamke Mwenye Juba Jeusi
Mwanamke Mwenye Juba Jeusi Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE

*********************************************************************************

Simulizi : Mwanamke Mwenye Juba Jeusi

Sehemu ya Tano (5)

New Africa Hotel

Kamanda Amata alipaki gari yake aina ya Freelander katika maegesho ya New Africa Hotel, akiwa ndani ya suti yake nyeusi, iliyopambwa kwa shati jeupe kwa ndani na tai ndogo ya shingoni, ilipita kama dakika moja hivi akiwa bado kushuka, akiangalia huku na kule, alipoona hali ni ya kuridhisha aliufungua mlango wa gari hiyo na kuteremka kwa upole. Kajoto ka jiji la Dar es salaam kalikuwa kakifika eneo hilo kwa kusindikizwa na upepo wa baharini, Amata alijiweka tai yake vizuri na alipokwishafunga vizuri mlango wa gari yake aliijongea ngazi ndefu ya kupanda eneo la juu la hotel hiyo ambalo lilikuwa na casino kubwa ya kisasa.

Kamanda Amata daima alipenda kuja katika casino hii kila mwisho wa wiki kwa ajili ya kujifurahisha kwa michezo mbalimbali iliyosheheni humo ndani, kupata vinywaji na kutengeneza marafiki wapya.

Akiwa ndiyo kwanza anataka kuanza kupanda ngazi zile, alisikia mlio mzito wa gari nyuma yake, Amata alisimama na kugeuka upande wa maegesho, aliiona gari moja ndogo ya rangi ya machungwa ikirudi kinyumenyume na kuegeshwa, mlango ulifunguliwa na binti mmoja mweupe, mrefu, aliyevaa gauni refu jekundu lenye mpasuo upande wa kulia uliopasuliwa mpaka juu ya goti kama sentimeta ishirini hivi. Baada ya kufunga mlango na kuupachika mkoba wake begani, alivuta hatua za wastani kuielekea ngazi ile. Kamanda Amata alimeza mate na kujikohoza kidogo kisha akageuka upande ule aliokuwa akielekea na kuendelea kupanda ngazi kana kwamba hakuna alichokiona. Moja kwa moja aliingia ndani ya ukumbi ule mkubwa uliosheheni watu wa rangi mbalimbali, wake kwa waume waliovalia nadhifu, kila mmoja akiwa katika harakati zake, Amata aliiendea kaunta kubwa iliyopo hapo na kuketi katika moja ya viti vilivyozunguka.

“Nipe Vodka, changanya na barafu tafadhali” alimueleza kijana aliyekuwa akitoa huduma ya vinywaji nyuma ya kaunta hiyo. Sekunde chache tu, bilauri yenye kiuno kirefu ilikuwa mbele yake, Amata aliinyanyua na kupiga funda moja kisha akaishusha na kung’aza macho huku na kule akiangalia nyendo za watu mle ndani, jicho la Amata likatua mgongoni mwa mwanadada aliekuwa ameketi na kumuelekezea mgongo akiwa katika meza ya mchezo aina ya Pai Gow Poker, alipotazama vizuri aliona katika viti vile kimoja kilibaki wazi bila ya kukaliwa na mtu, aliinua bilauri yake na kupiga funda lingine, alipoishusha ilikuwa kama ilivyotoka dukani, haikuwa na kitu. Amata alivutiwa na binti huyu kwa kuuona tu mgongo wake, akaiendea meza ile na kujikuta kaketi kwenye kile kiti kilichomruhusu kutazamana na binti yule uso kwa uso.

“Unaingia kwenye mchezo?” aliulizwa swali na mmoja aliyeonekana ndiye akichezesha mchezo ule.

“Yap, bila shaka,” alimjibu huku akijiweka vyema kitini. Wakati mchezo ukiendelea katika meza ile iliyowakutanisha watu kama watano hivi wenye pesa zao. Mwanaume mmoja alitokea upande wa nyuma wa yule mwanadada aliikaribi meza ile, Amata alimtazama yule bwana aliyekuwa na tambo kubwa, alifika nyuma ya yule mwanadada na kumsika mabegani kisha wakanyonyana ndimi zao na yule mwanaume alimnong’oneza maneno Fulani na kuondoka akimuacha yule mwanadada palepale. baada ya michezo mitatu hivi Amata alishinda ule wa mwisho na baada ya kuchukua kitita chake aliwakaribisha wale wenzake kinywaji, alinyanyuka na kutoka eneo lile, kabla hajaiacha meza ile alisita kidogo na kugeuka pembeni.

“Utapenda kupata kinywaji na mimi?” alimuuliza yule mwanadada

“Yes, nahitaji tafadhali” alijibiwa. Amata aliushika mkono wa yule mwanadada na kuongozana naye mpaka katika ile kaunta.

“Kama mwanzo tafadhali” Amata alimwambia yule kjana muuzaji ambaye alimkumbuka na kumpatia kinywaji, “Unatumia nini mrembo?” Amata alimuuliza yule mwanadada baada ya kuisogeza kwake ile bilauri ambaye kabla ya kujibu alitoa kicheko cha mahaba kilichomfanya Amata apagawe na kumtumbulia macho.

“Nipatie Grappa tafadhali na vipande vya barafu” alimueleza yule kijana ambaye alitekeleza ombi lile haraka.

“Si vibaya tukifahamiana” Amata alianza uchokozi

“Aaaaa! Ha! Ha! Ha!” yule mwanadada alicheka tena kwa cheko lake lilelile, kisha akaendelea, “Naitwa Shainista.”

“Shainista, mmmh! Jina zuri kweli nafikiri ni mara ya pili kulisikia katika maisha yangu. Mimi naitwa Am…” kabla hajamalizia yule mwanadada akaunganisha “…Kamanda Amata bila shaka.” Amata alishtuka kwa kukuta jina lake tayari linafahamika na Shainista.

“Umejuaje jina langu?” akauliza

“Mtu kama wewe nani asiyejua jina lako? Ukizingatia nilikuwa natafuta sana bahati hii ya kukutana nawe Amata, Kamanda Amata” Shainista aliongea huku akiyarembua macho yake yaliyomfanya aonekane kama amekula kungu manga, “Ni bahati sana leo kukutana nawe.”

“Shinista” Amata aliita na kumvuta karibu yake, “We ni mrembo sana, unavutia…” kabla hajamaliza ngonjera alizotaka kuanzisha alikatishwa “…shhhhhh!!!!, maneno mengi ya nini? Nipo kwa ajili yako, huu usiku wetu leo, usiku wa mashujaa” Shainista aliongea huku hali yake ikimuhamasisha Amata kimapenzi. Amata alibaki hana la kuongea, kila akimwangalia Shainista, alihisi moyo wake ukimuenda mbio.

“Na nini hutokea mashujaa wanapokutana?” aliuliza Amata

“Aaaaaa! Mmmmm! Ni kupeana burudani mpaka jogoo anawika” Shainista alijibu huku akipandisha gauni lake jekundu juu kidogo na kuruhusu paja lake jeupe kuonekana nje. Kisha wakiwa wameshikana mikono walitoka katika casino hiyo na kuteremka chini. Shainista alimvuta Amata kuelekea katika gari yake na wa lipoifikia Shainista aliiegemea na kumtazama Amata kwa macho yenye kuongea lugha tamu ya mapenzi, ulikuwa wakati mgumu sana kwa Amata, akajikuta midomo yake ikikutana na ile ya Shainista nan kubadilishana mate kwa takribani dakika mbili.

“Mmmm Amata twende!” Shainista alisema hayo huku akifungua mlango wa gari yake.

Amata alimtoa garini na kuufunga ule mlango, akamvuta na kuielekea gari yake.

“Tutatumia hii,” alimueleza huku akiufungua mlango na kumvutia ndani Shainista ambaye hakuwa na ubishi katika hilo. Land Rover Freelander ailiondoka kutoka katika maegesho ya New Africa Hotel na kuelekea baharini kisha kukunja kushoto kufuata barabara ya Kivukoni.


George McField, aliendesha taratibu gari yake katika barabara ya baharini ipitayo kandokando ya hospitali ya Ocean Road, huku akihakikisha haipotezi gari ya Amata iliyokuwa mbele yake kama mita mia moja hamsini hivi, akilini mwake akitaka kuhakikisha kuwa usiku huo ni usiku wa mwisho wa Amata. Aliendelea kupiga mruzi huku akiifuata ile gari, aliiona ikiiacha Ocean Road na kukunja kulia kuelekea Upanga Sea View, baada ya mwendo wa kama nusu kilomita ile gari iliingia kwenye nyumba moja kubwa nzuri na geti kujifunga nyuma yake. George McField aliipita kidogo nyumba ile na kwenda kuiegesha gari yake kwa mbele kidogo, kisha akatulia ndani bila kushuka ili kuwapa muda wa kula maisha kabla hajaendea kuichomoa roho ya mmoja wao, aliichukua simu yake na kutuma ujumbe Fulani ksha akatulia garini.

Dakika kadhaa gari moja aina ya Subaru ilifika pale na vijana watatu wakatelemka na kuielekea gari ya McField.

“Tunamchukua hai, ila tunamzimisha kwa muda, na lengo kubwa ni atueleze wapi alipo Chakwima ili nae tummalize” McField aliwaeleza wale vijana.

“Sawa!!” waliitikia na kurudi kwenye gari yao wakisubiri taarifa ingine.

Jumba lile lilikuwa kubwa la kuvutia, lenye mataa ya kila aina ya urembo ndani yake, Amata alikokotana na Shainista na wote wawili wakajitupa katika zuria laini lenye manyonya manyoya, Amata akiwa chini na Shainista juu yake, ndimi za wawili hawa zilikuwa zikibadilishana uzoefu, Amata alilivuta juu gauni la Shainista na kuruhusu eneo la mapaja mpaka makalio kuwa wazi, alipapasapapasa na kuminyaminya makalio laini ya mwanadada huyu, amabaye alishindwa kuvumilia hali hiyo na kuanza kutoa sauti za mahaba zilizokuwa zikimhamasisha Kamanda kuendelea na makeke yake, wakapinduana na sasa Shainista akawa chini na Amata juu, shati la Amata lilitupwa pembeni na kuruhusu kifua chake kipana kutazamana na chuchu chongofu za Shainista, upembuzi wa mavazi uliendelea kila mmoja kwa mwenzake, Amata alipoifikia kufuli ya Shainista na kutaka kuitoa alishikwa mkono

“Subiri kamanda, mbona una haraka?” Shainista alimweleza Amata na kumsukumia chini kisha yeye akajiinua kutoka pale na kuelekea katika mlango Fulani na kuingia, baada ya dakika chache alitoka akiwa kajifuga nguo maalumu ya kulalia, yenye wepesi ambao uliruhusu macho makali ya mwanaume kupenya na kutalii kona za mwili ule, kwa ishara ya kidole alimwita Amata naye akanyanyuka kumfuata.

Amata alitupwa kitandani akiwa kama alivyozaliwa na Shainista akaja juu yake akiwa hivyo hivyo, taa hafifu iliyofunikwa na kitunga maalum aliuficha mwanga na kupenyeza mionzi kadhaa. Baada ya shughuli pevu iliyofanyika juu ya kitanda kile kikubwa na kumuacha kila mmoja hoi kwa jinsi yake, Shainista alichukua glass mbili zilizokuwa tayari na kinywaji ndani yake, akampatia moja Amata na yeye akabaki na nyingine.

“Cheers kwa afya!” Shainista aligonga glass yake kwa Amata na kuinywa mfululizo, Amata aliisogeza glass ile mdomoni na mara akasita kufanya hivyo, akamtazama Shainista usoni. Akatulia kimya kwa sekunde kadhaa huku glass ile ikiwa bado mkononi.

“Vipi Kamanda? Kunywa, tuendelee raundi ya pili” Shainista alisisitiza. Amata alinyanyuka na kuelekea bafuni ambako aliufungua mlango na kutazama ndani yake hakuona kitu, alipita kwenye dirisha moja baada ya jingine, kengele za hatari zililia kichwani mwake, alihisi hapo kuna jambo au hatari inayomnyemelea, alipoona usalama upo alirudi kitandani na kuichukua tene ile glass kisha akainywa robo tatu na kumpa Shainista amalizie kunywa, Shainista alikataa, Amata akamlazimisha lakini Shainista alikataa katakata kuinywa, Amata akaanza kuona kizunguzungu, alimuona Shainista mara mnene, mara mwembaba aliona chumba kile kinazungukazunguka, akajaribu kunyanyua mkono wake lakini aliona mzito.

“Umenipa dawa za kulevya Shainista, nitakuua kwa mkono wangu” alizungumza maneno hayo kwa tabu, akiwa ndani ya boxer tu alitumia fahamu yake ya mwisho iliyobaki na kuutafuta mlango huku alihisi moyo wake ukienda mbiyo kupita kawaida, kwa kupepesuka alitokea sebuleni na luupata mlango wa nje na kuifuata gari yake, alitembea kwa kuyumbayumba lakini kabla hajaifikia gari yake, kitu kizito kilimpiga kisogoni na kumpeleka chini, bila ubishi alianguka kwenye kokoto na kupoteza fahamu.


Ndege iliyomchukua Punde Kishime ilitua katika uwanja wa kimataifa Dar es salaam, na alipokamilisha mambo yote kule ndani alijitokeza nje na kulakiwa na wafuasi wa chama chake na kundi la waandishi wa habari lililokuja kumlaki na kumhoji juu ya hiki na kile. Hasa juu ya tukio la mlipuko uliotokea katika moja ya mikutano yake, hali haikuwa shwari kwani waandishi walikuwa wakisukumana huku na kule kupata habari hiyo lakini Punde Kishime aliongea kwa kifupi na kuwaambia kuwa swala lote hilo linashughulikiwa na polisi, hivyo kwa majibu wanayotaka basi waende polisi kuuliza. Baada ya muda mfupi alitoka na wafuasi wake wachache na kuingia kwenye gari iliyokuwa hapo tayari kuelekea town.

Jua lilikuwa likififia pande za maghalibi tayari kulipisha giza la usiku lililokuwa likija polepole, Land Cruiser prado ilikuwa ilikuwa ikisogea taratibu katika mitaa ya Msasani, mheshimiwa Punde Kishime alikuwa akirejea nyumbani kwake kwa mapumziko baada ya mikikimikiki ya hapa na pale, kwenye gari alikuwa yeye na dereva wake tu, kichwani akitawaliwa na mawazo mengi, alipanga na kupangua, mara alicheka mwenyewe na wakati mwingine alijikuta akipata hasira ghafla. Akiwa mbele ya geti lake, dereva wake akijiandaa kupiga honi ili waingie ndani, ndipo walipoiona gari nyingine akitokea ghafla kwa nyuma yao na kusimama upande wa kushoto wao sambamba na mlango alioketi Kishime, ghafla watu wawili walishuka kwenye gari ile kwa kasi ya ajabu, mmoja kwa kutumia kitako cha bunduki alipiga kioo na kukisambaratisha kisha akaichomoa lock ya mlango huo na kuufungua, wale wengine walimtoa nje Kishime na kumuingiza kwenye gari yao kisha wakaondoka kwa kasi, yule dereva alijikuta hana la kufanya maana kitendo kile kilichukua kama sekunde kumi na tano tu. Aliteremka chini huku akipiga kelele za mwizi lakini haikusaidia hata watu walipokuja hakukuwa na gari tena eneo lile isipokuwa lile tu la Kishime. Mtaa mzima ulibaki na gumzo juu ya tukio lile, habari zilivuma kama upepo na muda si muda defender ya polisi iliingia eneo la tukio, walijaribu kuongea na wananchi ili kujua kilichojiri, kisha wakaingia kuonana na mke wa Punde Kishime na kufanya itifaki zao za mahojiano na mwisho waliahidi kulifanyia kazi.

Madam S aliteremsha mkono wenye simu chini kutoka sikioni, uso wake ulionekana kusawajika kwa mawazo lukuki, aliitupa mezani ile simu na badala yake aliinua bilauri iliyojaa kilevi na kubugia chote, aliiangalia tena simu yake haikuwa na dalili za kuita wala ujumbe mfupi, akainyanyua tena na kubofya vitufe Fulani Fulani na kuiweka tena sikioni lakini jibu lilikuwa ni lile lile ‘namaba unayopiga haipatikani’.

Madam S alichanganyikiwa baada ya kumtafuta kamanda Amata bila mafanikio, hakujua nini kimempata Amata, hata alipojaribu kuwasiliana na watu wanaofanya kazi na Amata kwa ukaribu akiwamo Chiba bado hakukuwa na jibu sahihi.

Madam S alijikuta usingizi wote ukimkatika na kuanza kufanya kila awezalo kumpata Amata. Alibadili nguo na kuvaa kikazi zaidi, bastola yake ya Colt 45 ikiwa mahali pake na vifaa vingine, akachukua gari yake Nissan March kobe na kuingia barabarani, yeye na Amata walishawekeana mikakati kuwa mmoja wapo asipopatikana kwa simu basi lazima atakuwa hatarini. Breki ya kwanza ilikuwa mbele ya nyumba moja ndogo ya kisasa maeneo ya Kinondoni Makaburini nyumbani kwa Gina. Gina alishangaa kukutana na mwanamama huyo mtu mzima usiku huo mnene.

“Usiogope msichana, unanifahamu mimi?” madam S aliuliza

Gina alimtazama kwa tuo lakini hakuonesha dalili ya kumfahamu mama huyo

“Hapana, wewe ni nani?” aliuliza

“Unamjua Amata? yule jamaa anayefanya kazi za clearing and forwarding, ofisi yake ipo mtaa wa Samora”

“Ndiyo.” Alijibu huku akitingisha kichwa juu chini

“Ok! Mimi ni mama yake, namtafuta simpati kwenye simu, nimeambiwa kuwa wewe ni mchumba wake”

“Ha!” Gina alishangaa kwa kauli hiyo, “Amata mi siyo mchumba wangu ni boss wangu”

“Vizuri, sasa mimi nina shida naye, mimi ni mama yake mzazi, kama una namba yake ambayo mnaitumia kwa siri naomba umpigie”

“Mama, unanishtua kuniambia Amata humpati”

“Lakini wewe unajua nyendo zake weekend?”

“Aaa, kila weekend hupenda kutembelea New Africa Cassino, sasa sijui kama na leo alikwenda huko”

Baada ya majibu hayo Madam S alimuaga Gina na kuelekea New Africa.

Bado ukumbi huo ulijaa watu waliokuwa wakinywa pombe aina aina, wakicheza kamali na michezo mingine mingi, kwa mwendo wa taratibu Madam S alipita katikati ya watu hawa na kuielekea kaunta huku macho yake madogo yakiwa makini kuangalia nyuso za watu waliomo humo, kwa harakaharaka na akili ya kiintelijensia alielewa nani muovu na nani mwema. Alivuta kiti akaketi juu yake pale kaunta na kuagiza toti moja ya John Walker, taratibu akawa akinywa huku akipepesa macho yake makali. Baada ya dakika chache alitoka ukumbini mle na kuteremka ngazi zile za nje kisha akasimama kwenye bustani akagundua kuwa eneo lile lote lina kamera za usalama, akajivuta na kuingia mlango mkubwa wa hoteli hiyo ya kimataifa, moja kwa moja akaipita kaunta ambapo kulikuwa na watu bado akaingia milango ya nyuma, kila mlango ulikuwa umeandikwa juu yake hivyo haikuwa shida kutambua kule anakokwenda, mlango wa kwanza, wa pili na watatu ndiyo haswa alioutaka, ulikuwa na maadishi SECURITY, alikishika kitasa na kukinyonga taratibu kuelekea chini, mlango haukufunguka, akajua bila shaka utakuwa umefungwa, akatoa funguo yake maalum kwa milango mibishi kama hiyo, jino moja, mlango ukakubali, madam S akaingia ndani ya ofisi hiyo pana iliyojazwa na vijiluninga vingi kuzunguka pande tofauti, kila kijiluninga kilikuwa kikionesha matukio mbalimbali yanayoendelea katika honteli hiyo. Madam S akasogelea moja ya runinga iliyokuwa ikionesha maegesho ya magari, akakiendea chombo maalum kinachohifadhi kumbukumbu hiyo na kukirudisha katika kumbukumbu ya nyuma huku akiangalia picha zinazopishana, mara ghafla akakisimamisha na kukirudisha taratibu, hakuamini anachokiona, kamanda Amata akiwa katika kunyonyana ndimi na mwanadada Shainista, kisha alona mpaka walivyoingia kwenye ile gari na kuondoka, lakini gari ya Shainista ilibaki palepale. ‘Nimeiona hii gari kwenye maegesho’ aliwaza, harakaharaka akakiruhusu kile chombo kiendelee na kazi yake kisha yeye akatoka kwa staili ileile na kurudi nje, ile gari ya Shainista bado ilikuwa palepale imeegeshwa, aliiendea na kuizunguka kisha kwa kutumia simun yake ya kisasa akaipiga picha kwenye namba zake za usajili T 0B7 AXQ, kisha akaziingiza katika mtandao wa mamlaka ya mapato Tanzania ili itambulike, kwa nywila zake za kijasusi ule mtandao ulitii, dakika chache baadae ujumbe ulirudi, ‘Shainista Presdor’ pia ukaleta na mwaka wake wa kuzaliwa na data zote muhimu, kilichomvutia zaidi ni picha ya mrembo yule iliyotokea juu ya kioo cha simu ile, madam S alitikisa kichwa ‘huu ndiyo ulemavu wa kamanda Amata, warembo’. Madam S aliwasailiana na rafiki yake anayefanya kazi mitandao ya simu na kumpa kazi ya kumpatia namba za simu za huyo Shainista, dakika chache tu akatumiwa sms akapewa na namba ya simu anayotumia, kazi imekwisha!


Msitu wa Kazimzumbwi, msitu wa hifadhi ya serikali pande za kisarawe, Punde Kishime alishushwa kwenye gari na kuingizwa katikati ya msitu huo. Alikarishwa chini ya mti mmoja wapo na mbele yake vijana watatu walikuwa wamesimama wakimwangalia.

“Punde Kishime, kwa heshima yako uliyokuwa nayo ndani ya serikali ya chama chenye dola tusingekufanyia haya yote, lakini sasa hatuna budi, hatutaki kukuzuru lakini tunahitaji utupe majibu juu ya maswali yafuatayo” Chiba alianza hotuba yake huku akichuchumaa chini kumkabili Kishime.

“Tunajua kuwa wewe hukutekwa kama kutekwa bali ulipelekwa ughaibuni kwa kazi maalumu ambayo hata wewe ulikuwa huijui hapo kwanza, jibu ndiyo au hapana” Chiba aliendelea.

“Kwanza ninyi ni nani? Mnajua huu ni uhalifu?” Kishime aliuliza, kofi kali lilimtua shavuni, Kishime akajikuna kidogo kidogo.

“Nimekwambia jibu ndiyo au hapana”

Kishime alipandwa na hasira akataka kunyanyuka, kichwa kimoja kikatua juu ya paji lake la uso, akaanguka chali, Kishime hakuwa na kauli nyingine.

“Ninyi mnajua kabisa kuwa nilitekwa, na niliporudi niliandikisha maelezo yote polisi, kwa nini msiulize kule” Kishime aliwajibu.

Baada ya mahijiano ambayo yalionekana wazi hayana tija kwani Kishime alikuwa mbishi kueleza ukweli ikabidi staili ya kisovieti itumike.

“Kishime, unataka kuwasaliti Watanzania, kumwaga damu yao isiyo na hatia, kupora mali zao kwa uroho wa madaraka, sasa utawaeleza Watanzania ukweli wa hayo yote”. Mwisho wa kauli hiyo mateso yasiyo nahuruma yakaanza, alishikwa alifungwa kamba mikononi na miguuni kisha wale jamaa wakaanza kunyofoa kucha za vidole vya mikono, Kishime uvumilivu ulimshinda, maumivu makali yakautawala mwili wake, aliomba msamaha lakini haikuwa suluhisho. Kutokana na mates ohayo Punde Kishime alieleza kila kitu mwanzo mpaka mwisho kila alipobisha au kujaribu kukataa alipata kibano kilichomfanya akubali, na hiyo ilichangiwa na tape recorder ya Chiba ambayo alirekodi mazungumzo ya simu kati ya Kishime na mtu mwingine, pia kikao chao walichokifanya huko Dodoma Hotel, baada ya kujisikia sauti yake Kishime alikuwa hana la kusema akajua sasa amekwisha.

“Ndiyo siasa zenu hizo za siku hizi siyo?” Chiba alimuuliza Kishime ambaye kwa wakati huo alikuwa akilia kwa vikwifukwifu na damu zikimtoka katika vidole kadhaa alivyonyofolewa kucha na jamaa wale.

“Sasa sikiliza, ole wako ukaseme kwenye mikutano yako juu ya hili, ndipo tutakapokupoteza kabisa, sisi tunakwenda ila wewe utarudi kwa mguu” wakamfungua kamba za miguu na kumuacha na zile za mikono kisha wakaondoka na ile gari yao na kumuacha msituni usiku wa manane.


Hali ilikuwa mbaya sana kwa kamanda Amata baada ya mateso makali aliyopewa, kutokana kwamba mara ya kwanza aliwatororka safari hii walimfunga kwa minyororo na kumpa kipigo kutoka hapo. Mc Field alifurahi sana kwa kuwa alijua wazi kuwa sasa kampata Amata na kwa kuwa yuko chini ya himaya yake atahakikisha anamuua kwa mkono wake huku akijivunia ushindi wa kumpata Chakwima kutokana na maelezo ya kamanda Amata.

George McField alimtazama Amata kwa dharau pale alipokuwa ananing’inia katika minyororo

“Ha ha ha ha huna ujanja kidume, Tanzania Secret Agency namba 1, leo utakuwa namba ziro” McField aliongea kwa dharau akimtazama Amata ambaye hata macho yake yote yalijaa damu iliyoganda, akiwa nusu mfu hakuwa na lolote lam kujitetea.

“Na kesho ndiyo kilele cha maandalizi yetu, wakati wewe umeshakufa wenzio tutakuwa na kikao cha kuitathmin nchi yetu, ninavyoongea wadau wameshafika na kila mmoja anatembelea eneo ambalo atalimiliki mwakani baada ya uchaguzi mkuu ambao iwe isiwe lazima nchi hii tuichukue kama zingine za Afrika, tuiweze Libya tuishidwe Tanzania, ina nini” McField aliongea kwa nyodo huku wafuasi wake wakiwa pembeni wakimwangali na kumsikiliza. Kamanda Amata aliyasikia maneno hayo na kuyaweka akilini japo alikuwa na hali isiyotabirika, aliomba Mungu wake tu amnusuru katika janga hilo. Mara vilisikika viatu vya kike vikiingia upande ule mapaka eneo lile nyeti, Shainista alikuwa amewasili kwenye jumba lile, kasri la Dr Kazumari, Mc Field alimkumbatia na kumnyonya ndimi.

“Mtazame bwana wako wa jana usiku” McField alimueleza Shainista. Kwa cheko lake lile lile alicheka na kumtemea mate Amata.

“Go Fish!” Shainista alimwambia maneno hayo Amata, hasira kali zilitawala ubongo wa Amata alitamani kama amtafune na kummeza kiumbe huyo wa kike.

“Bye, ukiniitaji kwa lolote nitafute New World Cinema jioni ya leo” McField alimueleza Amata na kisha wakarudishia lile limlango kubwa la mabati na kuondoka zao wakimuacha Amata akipambana na Israeli mtoa roho.

New world Cinema – Mwenge

Noah nyeusi iliingia kwenye maegesho ya ukumbi huo wa kisasa wa maonesho ya cinema, lakini siku hiyo hakukuwa na cinema bali kulikuwa na kitu kingine tofauti kabisa. Kundi kubwa la sarakasi kutoka Afrika ya Kusini linalojulikana kwa jina la MAMA AFRICA lilikuwa nchini kwa mualiko wa kampuni kubwa ya kwanza ya simu za mkononi Tanzania. Watu walikuwa wengi kwelikweli kutoka pande mbalimbali za mkoa, wake kwa waume, wakubwa kwa watoto walizagaa katika uwanja huo huku wakiwa tayari kuingia ndani kushuhudia maajabu hayo ya sarakasi mahairi za kundi hilo.

George McField aliteremka na kuuendea mlango mkubwa kisha kuingia ndani ya ukumbi ule ambako tayari watu wengi walishachukua nafasi zao na vikundi kadhaa vilikuwa tayari vikitumbuiza kwa nyimbo mabalimbali. Viti vya juu kabisa vilivyotenganishwa kwa kioo kikubwa na imara na sehemu nyingine ya ukumbi huo vilivyojulikana kama VIP vilikuwa bado viko wazi kwa kuwa vilikodiwa na watu maalum kwa ajili ya kutazama onesho hilo. Watu kutoka The Sixs walikuwa tayari kuingia ukumbini hapo lakini wengi walikuwa hawafahamiani wala hawajawahi kuonana, ni tiketi tu walizotumiwa ziliwafikisha hapo na kujua kila kitu unachotakiwa kufanya kabla ya kuketi kitini kwako.

Wadada watatu warembo waliovalia sketi fupi za suti za kijivu walikuwa wakikaribisha wageni wale maalum kwa ukarimu wa hali ya juu, maandalizi yalikamilika.

BMW moja metallic ilisimama jirani kabisa ya mlango mkubwa, mtu mmoja alishuka aliyevalia shati jepesi la hariri jeupe na suruali ya kijivu, aliteremka na kuingia katika ukumbi huo moja kwa moja alipinda upande wa kushoto na kukutana na warembo wale waliopewa maelekezo maalum ya kuwatambua wageni wao, aliliendea kabati maalum lililopangwa miwani nyingi kwa mtindo wa kupendeza na kuchagua moja inayomfaa. Akiwa katika kuchagua, mwanadada mmoja kati ya wale alimuendea akiwa na mfuko maalumu ambao ndani yake kulikuwa na kasha maalum. Akamsabahi kwa kumpatia mkono kisha akamkabidhi ule mfuko na yule bwana akachukua miwani moja nakutokomea ndani, vivyo hivyo ikawa kwa mtu wa pili aliyekuja baada ya dakika tano tu tangu yule wa kwanza kuwasili.


Usiku uliotangulia

Madam S, alijaribu kupiga namba alizopewa na shoga yake lakini zote hazikupatikana, hasira zilimtawala hakujua afanye nini, alipanga na kupangua bado hakupata jibu makini la kutatua shida yake, alibaki kasimama karibu kabisa na kijimti kimoja kandokando ya maegesho ya magari, ndipo alipoiona Noah nyeusi ikisimama jirani kabisa na eneo hili kosha mlango wake wa kusukuma ukafunguliwa kutoka ndani na mwanadada mrembo akateremka. Madam S alikodoa macho yake kwa mrembo yule na kumfuatilia nyendo zake. Shainista alirudi New Africa casino, mara hii hakuingia ndani bali alisimama jirani kabisa na ile gari yake ya kisasa kana kwamba kuna mtu aliyekuwa akimsubiri.

Madam S alikuwa akimuangali huku akiitazama ile Noah iliyomleta ikiingia barabara ya maktaba kuelekea upande wa mahakama ya Kisutu, hakuona umuhimu wa gari ile akili yake yote ilikuwa kwa mwanadada huyu ambaye alimuona akinyonyana ndimi na kamanda Amata alipokuwa akiangali katika kile kijiruninga cha usalama. Mtu mmoja, pande la baba alishuka na kumuendea Shainista, alimkumbatia na kumnyonya ndimi kwa mahaba mazito.

“Mxiuuuuuii ! Malaya mkubwa!” sauti ya kunong’ona ilimtoka madam S. Wapenzi wale wa usiku waliingia ndani ya gari ya Shainista, na wakati huo madam S aliingia katika gari yake tayari kuwafuata ili ajue wapi atakapombana mwanamke yule mshumami, muda kidogo ile gari iliwashwa na kuondoka eneo lile. Madam S aliifuatilia kwa nyuma mta kwa mtaa, barabara kwa barabara. ‘Huyu mwanamke ndiyo wa kuniambia wapi alipo Kamanda,’ alijiwazia huku akiongoza mwendo na kuifuata kwa mbali gari ya Shainista, waliiacha barabara ya Ally Hassan Mwinyi na kuchukua ile ya Agha Khan kutokea Ocean road na kuifuata Sea View, madam S alipoona anaweza kushtukiwa kama anawafuata alizima taa za gari yake na kuiendesha bila taa akifuata barabara kwa hisi ya hali ya juu akiongozwa na taa za nyuma za ile gari anayoifuata.

Mbele ya jumba kubwa waliloingi Shainista na yule jamaa madam S akaegesha gari kwenye nyumba mbili nyuma na kuiendea nyumba hiyo kwa miguu, alilipita geti kubwa na kufuata mlango mdogo ulio pembeni tu mwa geti kuu, alijaribu kama anausukuma ukafunguka, akashangaa ina maana mlango huo ulikuwa wazi makusudi au lisahaulika kufunga, hakuna jibu. Alitulia sekunde kadhaa na kuingia mpaka kwenye kauwanja kapana hivi, alipotazama huku nahuko aliiona gari ya kamanda Amata, Land Rover Free Lander, madam S aliitazama ile gari na wazi akajua kuwa kamanda Amata lazima yumo ndani ya nyumba hii, aliichomoa bastola yake Colt 45 na kuifyatua kilinda usalama, imara mikononi mwake akaliendea ua kubwa lililo jirani kabisa na ngazi za kupandia kuingia kibarazani akatulia hapo kusubiri taa za ndani zizimwe, na haikuchukua muda ilikuwa hivyo isipokuwa chumbani ambako kulitoka mwanga wa bluu. Kwa mwendo wa hadhari kubwa aliuendea mlango mkubwa na kuutikisa kwa pozi, mlango ule uligoma kufunguka, akatoa funguo yake na kuufungua kama yeye ndiye aliyeuchonga, akaingia katika sebule kubwa yenye kila kitu ndani yake, alipoangalia huku na huku na kukuta kuwa hali ni shwari aliuendea mlango wa chumbani na kutulia akitega sikio kusikia kinachoendelea. Ukimya mkubwa ulitawala chumbani mle, madam S alishikwa na wasiwasi alitegemea kusikia kelele za watu walio katikati ya dimbwi la mahaba lakini haikuwa hivyo, wasiwasi ukaanza kumshika, akatazama nyuma hakuna mtu ni yeye tu, akanyonga kitasa na mlango ukafunguka, akaingia chumbani humo taratibu, kitanda kitupu, utata! Alishtushwa na maji ya chooni, akajibanza nyuma ya pazia kubwa na mara mlango wa chooni ukafunguliwa na Shainista akatoka na nguo ya kulalia tu, mlango wa choo ulibaki wazi madam S aliona mpaka ndani hakuna mtu akajitokeza kama mzuka mbele ya mwanadada yule.

“Malaya mkubwa wewe, haya niambie haraka, huyo uliyeingia naye hapa ndani ni mume wangu na ninawafuatilia kutoka mbali, yuko wapi kabla sijakuua,” madam S alitumia triki mbadala kumchanganya Shainista.

“Sasa mumeo si umsubiri nyumbani kwako, unakuja kutuharibia starehe zetu tu hapa,” Shainista aling’aka kwa sauti

“Funga domo lako wewe kabla sijakupoteza,”

“Tangu lini mumeo akakaa kwangu?”

“Wewe si umezoea kuiba waume za watu, leo usiku huu huyu wa pili bisha!”

Shainista alibaki kushangaa kinywa wazi.

“Kama kweli niliyekuja nae ni mumeo mfate kwenye nyumba yake ile kule ya upande wa pili.”

Madam S alitazama kwa chati kweli kulikuwa na nyumba nyingine ndani ya wigo mmoja na ilikuwa taa zake zinawaka kuwa ndani kuna dalili ya mtu.

“Na yule kijana, kamanda Amata, yuko wapi?” aliuliza huku domo la kiwambo cha bastola yake likiwa linamtazama Shainista, hakukuwa na chembe ya mzaha katika uso wa madam S muda huo.

“Sasa unamtaka mumeo au kamanda Amata, mbona hueleweki we bi kizee, sema shida yako haraka” Shainista aligeuka mbogo hali iliyomuuzi sana madam S, aliirudisha bastola yake kiunoni na kumuendea Shainista kumtia adabu lakini kabla hajamfikia alijikuta akipigwa na kitu kama gongo kichwani akapepesuka na kupoteza nuru ya macho akaanguka chini, kiza kinene kikafunika nuru hafifu aliyoweza kuiona, alijaribu kunyanyua mkono lakini wapi alikilaza kichwa chake na kutulia tuli.

“Watu wengine umri umeenda kufuata vya watu tu!” alisema Shainista huku yule bwana akiuvutia mwili wa madam S nje na kuufungia kwenye kichumba kidogo ndani ya jiko, waliwa na mpango baada ya kumaliza sherehe yao pale kitandani basi wakautupe baharini uokotwe huko. Walikumbatiana na kujitupa kitandani mahaba yakaanza.

Rejea New world Cinema

Mara hii ukumbi ulikuwa umejaa watu na onesho lilikuwa tayari kuanza. Katika sehemu ya VIP watu kama kumi walikuwa wameketi na viti vitatu vilibaki wazi, wote wakiwa ndani ya suti nadhifu nyeusi zilizoyaficha mashati meupe ya kisasa kabisa. Masikioni mwao walipachika vifaa maalumu vya kusikilizia ambavyo pia huweza kunasa sauti ya anayeongea, hakuna aliyekuwa akimtazama mwenzie usoni kila mmoja alikuwa anaangalia kinachoendelea jukwaani.

“Baada ya kikao tuonane,” Gonzalenz alimwambia McField

“Sawa Boss” aliitikia McField huku akijipanga kuwa kikao hiko kitapokaribia kumalizika apotee na asionekane tena maana alijua wazi kuwa baada ya klikao hicho maisha yake yatakuwa hatarini ikiwezekana kupotea kabisa nah ii imetokana na uzembe aliyoufanya na kuwaingiza mabosi wateja wake kwenye hatari ya kuharibu mambo yao. Ndani ya chumba kimoja kulikuwa na watu wawili, mmoja mzungu na mwingine mwafrika walionekana wakirekebisha kamtambo Fulani ka elektroniki huku McField akiwa jirani kabisa kuangalia kila kitu.

Sarakasi za MAMA AFRICA zilianza kwa mbwembwe sana pale jukwaani ilisikika watu wakishangilia na kupiga makofi muda wote.

VIP bado viti viwili vilibaki wazi na wajumbe wake wote ni wa kutoka Tanzania bado hawajaingia kikaoni.

“McField, bado watu wawili, jaribu kucheki kuna tatizo gani?” sauti ilimfikia McField kupitia kile kidubwasha cha sikioni yeye akiwa upande mwingine wa usalama, na wajumbe wengine wote walisikia kauli ile na kutazama kweli viti viwili havina watu.

Tax moja ilisimama mbele ya mlango mkubwa wa ukumbi huo, Punde Kishime aliteremka na kuelekea ndani akiwa na wapapmbe wake wawili ambao walitakiwa kubaki sehemu Fulani, kama kawaida alikwenda kuchagua miwani na yule mwanadada wa mapokezi alimuendea kumsalimia na kisha kumkabidhi box la zawadi ndani ya ule mfuko kama alivyowapatia wengine. Punde Kishime akaingia katika chumba Fulani chenye namba sawasawa na ile ya ule mfuko akauafungua na kutoa lile kasha kwa ndani na kulifungua, suti safi ilikuwa ndani yake, Punde Kishime alizivalia na kutoka kiujana zaidi, alichuku kidubwasha cha sikioni na kukipachika kisha akapanda ghorofa ya juu na kuchukua siti yake kuketi. Kwa kupitia vile vidubwasha vya sikioni walianza kubadilishana mawazo ya hapa na pale lakini haikuwa rahisi kwa mtu mwingine kuelewa kinachoendelea, kilikuwa ni kikao cha aina yake.


Lango la bati lilisukumwa na Dr Kazumari aliingi katika banda hilo, akiwa katika mavazi yake ya mtoko. Kamanda Amata ambaye fahamau zake zilikuwa zimerudi sawia alijifanya kuning’inia palepale alimuona Dr Kazumari tangu anaingia. Jicho la Dr Kazumari lilimtazama Amata pale katika minyororo na kumpuuza tu kisha moja kwa moja akaingia kwenye gari yake iliyokuwa humo ndani tayari kutoka, akaingia na kuketi nyuma ya usukani kisha akaliwasha, moshi ulikijaza kile chumba kisha akalitoa kwa mwendo kidogo, wakati gari ile ikitoka ulisikika mlio wa kitu kinachokatika, Kazumari alitoa shimgo nje kuangalia nyuma na aliona kamanda Amata anaanguka kutoka pale alipofungwa.

“Shiiiit!” akashuka garini na kwenda kutazama kulikoni…..

…..wengine wakaropoka kuwa ni mashindano ya magari ili mradi kila mtu alisema lake, walipokaribia eneo la Kunduchi kwenye machimbo ya kokoto gari ya Amata ailikuwa karibu kabisa na ile Lexus, aliitoa ile shot gun na kulenga gurudumu la nyuma, shabaha ya kwanza haikuwa sahihi, kwani dereva wa ile gari aliona hivyo akayumbisha kwa makusudi mazima na kumpoteza Amata maboya, lakini shabaha ya pili ilipiga side mirror na kumfanya yule derteva sasa kutokuona nyuma, shabaha ya tatu ililipata gurudumu lile sawia na kishindo kikubwa kikasikika, ile Lexus, ilipinduka na kubingirika kwenye korongo kubwa linalotumika kuchimba kokoto, lilipofika chini kabisa na kujikita udongoni, mlipuko mkubwa ulitokea na gari ile kuteketea kwa moto, hakuna hata aliyetoka, Amata aliteremka kule chini akiwa na ile shortgun mkononi, aliitazama ile gari ikiwa inateketea kabisa, aliweza kumuona mtua aliyekuwa ndani yake akiwa anaungua vibaya lakini kamanda Amata hakuwa na msaada mwingine, alipanda juu alikoiacha gari yake na kurudi mjini kwa kasi sana….


“Kila mtu na ashike njia yake haraka, hapa mambo yamekwishaharibika, tuonane Dhaka baada ya siku tatu” ilkikuwa sauti ya Gonzalenz akiwaambia wenzake wakati Kamanda Amata alipokuwa akishughulika na wale jamaa kule kwenye chumba cha mawasiliano. Amata aliposhuka chini kuja kumwangalia McField, alijichanganya mwenyewe, wahusika wa mikutano wote walikuwa wamerudi vyumbani kusubiri amri nyingine, Amata alipoondoka hapo kuifukuza ile gari ndipo wale wageni walipoondoka eneo lile bila bugudha yoyote na kila mmoja kurudi hotelini alikofikia, bwawa limeingia luba.

Hasira kali zilimtawala bwana Gonzalenz hakujua afanye nini maana kwa mara ya kwanza katika kazi zao wamekutana na vyombo hatari vya usalama na kuharibu mtandao wao ulioota mizizi katika sehemu nyingi duniani, moyoni mwake alimuwaza McField, aliamini wazi kuwa huyo ndiye alieharibu kila kitu katika mpango huo, alifikiri kumsaka na kumuua usiku wa siku hiyo huku akiwaza kuondoka na Punde Kishime usiku huo kuelekea Bangaladesh kwani alijuwa wazi kuwa akikamatwa na polisi lazima atatoa siri nyingi juu yao.

George McField alipodondoka pale mara moja alijiinua na kujificha kwenye chumba kilichotumika kukusanyia tiketi wakati wa onesho na alipomuona Amata ameondoka kuifukuzia ile gari, ndipo akatoka na kuchukua gari ingine kisha kuelekea kwanza kwa Shainista ili kumuona mateka wake, madam S ili ammalizie kabisa maana alimuacha na hali mbaya sana akiwa hana fahamu, na kwa kuwa alijua kuwa ameshalikoroga, alijipanga akimaliza kazi ya madam S ni kukimbilia kwa Dr Kazumari kubeba vitu vichache alivyohifadhi huko ili aondoke usiku huo, hakupenda kabisa kuonana na Gonzalenz maana alijua huo utakuwa ndiyo mwisho wake.

Punde Kishime alikuwa akitirirkwa na jasho jingi, hakujua la kufanya, tama ya cheo, utajiri na madaraka makubwa sasa vilikuwa vikimzomea, kila alikotaka kwenda moyo wake ulipinga alibaki akihangaika tu, alifika nyumbani kwake akiwa hajielewi, aliingia ndani na kupita kila chumba, alirudi chumbani kwake na kumkuta mkewe amelala kwa minajiri ya kujipumzisha jioni hiyo, alimtazama akatikisa kichwa, machozi yakaanza kumtoka, ama kweli, tamaa mbele mauti nyuma, alitamani ardhi ipasuke aingie, maana alishajua kuwa sasa mambo ni mabaya, atauweka wapi uso wake punde akitakiwa kusimama katika mahakama na kupambana na sheria wazi ambayo yeye mwenyewe anaijua, ziko wapi zile nyimbo za uzalendo alizokuwa akiimba pamoja na rafikiye Chiwawa Chakwima, akiapa kamwe hatoisaliti nchi na wananchi wenzake, lakini leo imekuwa hivyo, ama kweli zimwi likujualo halikuli likakwisha. Punde Kishime aliivuta droo ya kitanda chake na kuitoa bastola yake aipendayo na kuibusu, mara akasikia kelele za kugongwa mlango alisita kidogo, kisha akaliendea dirisha kubwa kuangalia ni nani anayegonga hodi muda huo.

Kamanda Amata alikua tayari mbele ya geti la Shainista pale Upanga sea view, alitazama vizuri akaikuta gari yake ipo kwenye maegesho kama alivyoiacha kaiendea na kufungua droo ya dashboard akatoa simu yake ya kisasa kabisa ambayo humsaidia kwa mambo mengi katika kazi yake na kuiwasha, moja kwa moja akiwa na ile shortgun mkononi aliiendea ngazi ya mlango mkubwa na kuugonga, malango ulifunguliwa, uso kwa uso na Shainista.

“Karibu dear, nilikumiss” Shainista alimkaribisha Amata huku akimlegezea macho ambayo mwanaume lijali lazima utulie na uatafakari mara mbili, akamsogelea kutaka kumkumbatia.

“Toka! Kaa mbali na mimi Malaya mkubwa wewe na leo ndiyo mwisho wa maisha yako” Amata aling’aka, usoni kulikuwa na mikunjomikunjo ya hasira na uchungu, alimtazama yule msichana mrembo aliyekuwa amesimama akionesha wazi akimuogopa Amata. Kamanda Amata aliinua simu yake iliyokuwa ikiwakawaka kitaa cha kijani kwenye kioo chake, akaiangalia na kumgeukia Shainista.

“Yuko wapi madam S? umemuweka wapi nambie?” aliongea kwa nguvu, sauti yake iliyopaa kwa nguvu ilimfikia madam S kule alikofungiwa na kushtuka kutoka kwenye usingizi mzito, alijinyanyua kwa shida na kujikung’uta vumbi, kisha akasimama wima na kuujaribu mlango ulikuwa umefungwa.

Shainista alijiuma kidole huku akimwangalia Amata, aliiachia nguo yake ndefu na kuruhusu sehemu sehemu kubwa ya mwili wake upande wa mbele kuonekana, chuchu zilizochongoka vema na kusimama saa sita, zilizojaa vyema zilitazamana na macho ya yenye uchu ya kamanda Amata,.

“Huwezi kunilaghai kwa kamwili kako hako,” Amata alimwambia Shainista akafyatua risasi moja iliyopiga kioo na kukitawanya vibaya.

“Mshenzi wewe! Unafikiri ndiyo ntakwambia huyo bibi yako alipo, kwanza unaharibu nyumba yangu, huna uwezo wa kulipa, mbwa wewe” Shainista alibwata kwa kelele zote ambazo zilimtia hasira Amata, kuitwa mbwa, mshenzi tena na mwamnamke kwake ilikuwa ni dharau kubwa sana. Aliinua shortgun yake na kuiamuru kuondoa uhai wa mrembo huyo, risasi ya kwanza ilipita kifuani na kumuacha Shainista akikodoa macho huku mkono wake ukiwa aumeziba tundu la risasi lililokuwa kifuani mwake.

“Amata mpenzi unaniua?” aliongea kwa sauti ya shida sana.

“Mbona bado hujafa, kwanza hun thamani katika taifa hili,” Amata alimwambia huku akiinua tena bunduki yake na kupiga risasi ya pili kichwani.

“Kawasalimie kuzimu, Malaya wewe” Kamanda Amata aliushuhudia mwili wa Shainista ukitua juu ya coffe table nzuri ya kioo na kuitawanya katikati vipande viwili, kwenye kioo kilicho mbele yake alimuona mtu mwenye mwili mkubwa akimnyatia kutoka nyuma, kwa kasi ya ajabu, Amata alipiga round kick na kutua juu ya shavu la jamaa yule ambaye hakuyumba wala kutetemeka, alitulia tuli na kurusha ngumi ambayo Amata aliikwepa kwa ustaci mkubwa ila ngumi ya pili ilimpata na kumpeleka chini juu ya mwilio wa Shainista, alijiviringa kwa haraka na kunyanyuka lakini alichelewa teke moja kali lilimrusha mapaka kwenye ndoo ya maua, Amata alitambaa kumkimbia yule jamaa, kisha akanyanyuka kwa haraka na kutumia ukuta kama support alijiukanyaga kwa mguu wake na kujirusha samasoti iliyomfanya atue nyuma ya yule jamaa, yule jamaa alipogeuka alikutana na karate za haraka zilizotua maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumpotezea stamina, kabla hajazinduka, Amata alipiga sweep kick na kumshuhudia jamaa mnene akianguka kama mzigo sakafuni, alipogeuka alikutana na domo la shortgun lililoutoa uhai wa Shainista.

“Bunduki hii hii iliyouondoa uhai wa Malaya wako sasa itakumaliza wewe” Amata alizungumza huku akimfuata taratibu jamaa yule mbaye alikuwa anasota akirudi nyuma. Ukuta ulikuwa kizuizi kwake, hakuweza kuendelea kurudi nyuma, alitulia akimtazama Amata aliyekuwa akimsogelea taratibu, simu ya Amata ikaita, akaitoa mfukoni na kuitazama ‘Chiba’, kosa. Yule jamaa pamoja na ukubwa wa mwili wake alijinyanyua kwa haraka na kupiga teke ile bunduki mikononi mwa Amata, na kumtoka, kisha akasimama wima kumkabili kamanda, kabla hajatulia sawasawa, Amata aliupiga kwa teke mguu wa yule jamaa ambao ulikuwa akiutegemea kutengeneza stamina, kisha kwa teke la kuzunguka alipiga shavuni na yule jamaa akageuzwa kwa nguvu ya teke lile na kuanguka kifudifudi, bila kujizuia alitua kwa tumbo kwenye meza iliyovunjika na kioo kinene kilichokuwa hapo kilimtoboa vibaya tumboni na kupoteza maisha. Kamanda Amata akarekebisha tai yake na kuiokota ile bunduki kisha kuanza kutafuta ni wapi madam S alipo!….

Gonzalenz, aliujua mchezo anaotaka kufanyiwa na McField, kutoka mafichoni aliko alimbana Punde Ksihime ili amuoneshe ni wapi Mc Field aliwekeza nguvu zake, yaani makazi na shughuli zake zingine. Kishime alimuelekeza njia mpaka Keko na kuifikia nyumba ya Dr Kazumari. Gonzalenz aliteremka akiwa ndani ya koti lake jeusi, na bastola yake ndefu iliyofungwa kiwambo cha sauti ilikuwa ndani ya koti hilo, moja kwa moja aliuendea mlango mkubwa, geti, na kuusukuma, haukuwa umefungwa ilionesha dalili zote kuwa kuna mtu kaingia muda si mrefu,

….haukuwa umefungwa ilionesha dalili zote kuwa kuna mtu kaingia muda si mrefu, nae akaingia bila hata kuuliza na alipofika nyuma ya nyumba hiyo alikuta kuna gari moja nyeusi aina ya Noah imeegeshwa tena ikiwa bado inaunguruma, mara kijana mmoja alitoka ndani ya lile banda alimofungiwa Amata akipiga kelele.

“Wamemfunga kamba!”

“Nani?” sauti ya mwingine iliuliza

“Dokta” alijibu yule wa kwanza, mara akamuona aliye mbele yake akisita na kujishika kifua, kwa mshangao na yeye aligeuka nyuma na kukutana na domo la bastola, Magnum 22, ikiwa mikononi mwa Gonzalenz. Sura isiyo na mzaha hata kidogo.

“McField yuko wapi?” Gonzalenz aliwauliza wale vijana. Kwa woga kijana mmoja akamuoneshea nyumba iliyo jirani hapo katika wigo mmoja tu ambayo ilitengenishwa na lile banda la kuhifadhia makolokolo mbalimbali. Akawapa ishara ya kuongoza huko ndani nao wakatii. Katika sebule ndogo iliyosheheni vitu mbalimbali vya kielektroniki, McField alikuwa akifungafunga baadhi ya vitu hivyo ili aweze kutoroka.

“Ha! ha! ha! ha! ha!” Gonzalenz alitoa cheko lake la dharau kwa McField, lililomfanya ageuke kutazama nyuma.

“Shiiit!” aling’aka McField na kusimama kidete akitazamana na ile bastola ya Gonzalenz.

“Utamtoroka kila mtu, lakini siyo mkono wa Gonzalenz,” alitamba jamaa huyo huku akiwa kamnyoshea Mc Field ile bastola, “Umetuangusha sana safari hii McField, tusingefika hapa lakini kwa sababu ya uzembe wako tumeharibu kila kitu, tulikwambia kazi yako ni kummaliza Chakwima na kuhakikisha kazi imekamilika, kwa nini hukutimiza hilo? Wewe unaijua vema kazi yetu na siri zote, na umefanya vizuri sehemu mbalimbali na hii ndiyo iliyonifanya nikupe kazi tena, sasa kwa nini safari hii umetuangusha? Najua ulilaghaiwa na yule Mmafia Max Petito, sasa kama tulivyommaliza yeye na wewe pia utamalizwa hivyo hivyo, unafikiri kuna siri duniani, nyendo zako zote kule Firenze tunazijua, mapatano yako na Petito tunayo,” Gonzalenz akatoa karatasi zilizokunjwa na kumrushia usoni McField, kisha akaendelea “Sasa leo roho yako naondoka nayo mimi, kama mkataba wetu unavyosema, si unakumbuka!” aliongeza. Wale vijana walikuwa wamesimama pembeni wakisikiliza kwa makini. McField alipotaka kufungua mdomo kujibu kitu Gonzalenz akawahi kumkatiza,

“Sikia we mbwa huwezi hata kidogo kujibizana na mimi…” huku akiondoa usalama wa bastola ile tayari kuutoa uhai, “Na sasa mwili wako utatupwa hapa na hakuna hata ndugu yako atakayelijua hili,” McField alikuwa akitazama vidole vya Gonzalez vinavyojiandaa kucheza na trigger ya bastola hiyo, McField aligeuka kwa kasi ya ajabu na kubonyeza kitufe Fulani kwa kutumia mguu wake kisha yeye akalala chini. Gonzalenz aliona kitu kama embe la chuma likianguka kutoka juu na kutua mbele kidogo ya miguu yake, mara moja alikitambua kitu hicho na kujirusha sarakasi moja kali sana kwa nyuma, (vijana huiita ‘back’) na kutua mlangoni, alipokuwa ametoka nje kiwiliwili kabla hajaishia mkono wake ulichomwana vitu vyenye ncha kali na kuufanya kiganja chake kushikiliwa na kitu hicho katika muimo wa mlango. McField alikuwa ametumia bomu la misumari ambalo halitumii mlipuko wa kawaida ila misumari mingi inayowekwa ndani yake, na linapolipuka basi madhara yake ni makubwa sana, mabomu ya aina hiyo hutumika sana na magaidi, liliwahi kutumika tarehe 6 March, 1970 huko Greenwich, na idadi kubwa ya mabomu hayo yalitumika mwaka 1999 wakati Neo-Nazi David Copeland alipotega vitu vya mtindo huko London, na June 9, 2004 huko Cologne, Ujerumani, bomu kama hilo lilitumiwa na magaidi wa ki-Nazi wa kundi la National Socialist Underground na sehemu nyingine nyingi. McField alikuwa na kifaa hiki hatari ndani ya nyumba yake ndogo, na kwa muda huo alilitumia kujiokoa, kutokana na mlipuko ule wale vijana walijeruhiwa sana hata kupoteza maisha kwani hawakukijua kitu kile hata jinsi ya kujiokoa. McField alitoka pale chini na kwa kitendo cha haraka akabonya kitufe kingine na kabati kubwa lililokuwa hapo likasogea pembeni lenyewe na kuruhusu kijimlango kidogo kufunguka, McField aliteremka ndani ya kamlango hako kwa kutumia ngazi zilizokuwamo ndani yake na kisha ule mlango ukajifunga na lile kabati kurudi mahali pake.

Gonzalenz alikuwa na maumivu makali kwa kuwa bila kujali aliunasua mkono wake kwa nguvu na kuruhusu damu nyingi kumtoka, alivua shati lake na kujifunga ule mkono kisha yeye akabaki na koti alilolivaa juu ya fulana yake ya ndani, alitaka kuiendea gari yake aliyoiacha kule nje lakini akagundua kuwa McField hakutoka, hivyo akarudi nyuma na kuingia ndani lakini hakukuta mtu zaidi ya ile miili ya wale vijana wawili, alijaribu kutazama hapa na pale huku bastola yake ikiwa katika mkono wa kulia, alifungua hapa na pale, alipekua huku na kule hakuna dalili ya mtu.

“Bastard! Siwezi kuzidiwa akili na mtoto mdogo niliemfundisha kazi mwenyewe” aliongea peke yake na kutoka nje ya jengo lile kuiendea gari yake, la haula hakuikuta ile gari. Akarudi ndani haraka na kuingia kwenye ile Noah na kuondoka eneo lile.

McField aliposhuka kupitia zile ngazi, zilimuongoza moja kwa moja na kutokea karibu na bonde la Keko ka kutumia ujia maalum uliotengenezwa kwa kazi hiyo ya kujiokoa, alijikung’uta nyuzi za buibui zilizomjaa mwilini na kujichanganya mtaani, bado akilini mwake alitaka kurudi kwa ajili ya baadha ya vitu muhimu kuvichukua na kisha kutafuta njia ya kutoroka nchini, huku akijua wazi kuwa sasa anasakwa kwa udi na uvumba, alijua kuwa ana maadui wawili wakubwa, Gonzalenz wa kiongozi mtendaji wa The Sixs na kamanda Amata wa TSA, kila alipomkumbuka kijana huyu kijasho cha kwapa kilimtoka. Kwa tahadhari kubwa alirudi katika nyumba ile ya Dr Kazumari na kuingia kwa kupitia mlango wa nyuma, mlango mdogo uliokuwa unaongoza katika vyoo vya jumuia, alipohakikisha usalama alijitoma ndani ya ile nyumba ndogo ambayo kwa muda mfupi tu uliopita alifyatua lile bomu la misumari, aliingia na kuurudisha mlango nyuma yake, kagiza kakatawala mle ndani alipotaka kuishika switch ya ukutani awashe taa alishangaa taa ikiwaka, akashtuka.

“Karibu nyumbani, nilikuwa nakusubiri kwa hamu sana!” sauti ya Amata ilipita masikioni mwa McField ambaye aliishiwa nguvu, alihisi kukutana na Mzuka asiyoutegemea kwa muda huo, alijilaumu kurudi lakini angefanya nini, ilimbidi, alimtazama Amata aliyekuwa ameketi katika kikochi kidogo huku akiwa na glass ya mvinyo mkononi mwake na katika mkono wake wa kulia akiwa amekamatia Remington 1100 Tactical Shotgun ya USA iliyotengenezwa mwaka 1963 na bwana Wayne Leek na swahiba wake R Kelley.

McField aliiona wazi hatari iliyomkabili, alichekecha akili huku akiendelea kumtazama Amata ambaye alimuona jinsi alivyotulia hata mboni za macho yake hazikutikisika.

“Ulifikiri utanikimbia mpaka lini? Sasa upo mikononi mwangu, na dunia itajua udhalimu wenu, hivi ninavyokwambia, Mahmoud Bashir tumeshamtia mkononi akijaribu kutoroka kuelekea Kilimanjaro ambako angechukua ndege, na sasa ninavyoongea na wewe Bw Washington atatiwa mkononi, vibaraka wengine sikutajii ila wote mpo wanted na wewe umeshakamatika” Amata aliongea kwa kujiamini

“Unafikiri mimi unaweza kunikamata kama kuku namna hiyo? Kama ulifikiri kuna urahisi basi ondoa hilo wazo na ninaapa mbele yako hutonipata kamwe, nimeiponyoka mikono ya FBI itakuwa wewe, nani wewe!” McField aliongea kwa kujiamini huku akivuta hatua ndogondogo,

“Tulia hapo hapo ulipo!” kamanda Amata alimtuliza huku akisimama na kuishika sawia ile bunduki yake mkononi mwake, McField alitulia kwani alijua janja yake imejulikana, Amata alizunguka na kusimama upande wa ile meza kubwa yenye vifaa vingi vya kielectroniki huku akimuweka McField upande wa mlango,

“Geuka nyuma bwege wewe!” Amata aliamuru tena, McField aligeuka na kuitumia nafasi hiyo, aliruka juu na kuitanua miguu yake, mguu wa kwanza uliipiga bunduki ile na kuitupia upande wa pili na mguu wa pili ulitua sawia katika shavu la Amata na kumpepesua, Amata alijishikilia kwenye meza huku akiwa kampa mgongo McField ambaye alikuwa ametua sakafuni sekunde chache zilizopita, McField alijivuta kumuendea Amata, haikuwa rahisi, kutoka alipojishikia pale mezani alijigeuza haraka na kumpiga konde zito McField ambaye alilipangua kwa ustadi lakini la pili lilimpata usoni, akiwa kachanganyikiwa kwa konde lile kabla hajajiweka sawa, karate mbili za nguvu zilitua shingoni mwake na kumzindua, hajakaa sawa mguu wa Amata ulitembea kwa ustadi na kutua sawia upande wa sikio na kumpeleka McField chini lakini kabla hajatua aliuona mguu wa pili wa Amata auliokuwa umedhamiria kummalizia akiwa chini, katika nguvu ileile ya kuanguka alijirusha na kuukanyaga ukuta kicha kurudi uoandea wa pili Amata Liona mtu akipita juu yake alipojipanga kumkabili alichelewa, mapigo mawili mazito yalitua katika uti wa mgongo, Amata alisukumwa mbele na alipojaribu kugeuka mguu mzito wa McField ulimsindikiza kumkanyaga mgongoni, kamanda Amata alijigonga vibaya ukutani na kuchanika katika paji la uso. Alipogeuka alikutana ngumi nzito lakini akaiwahi kuikwepa na kugeuka nayo kisha kuidaka kwa mbele na kuuvuta chini ule mkono, yowe la maumivu lilimtoka McField pale alipohisi mifupa yake ikivunjika, kwa kutumia kiwiko alimpiga mbavuni na kumsukumia nyuma, McField alitulia akizishangaa ngumi kama mvua zikitua usoni, ngumi zenye hasira zilizompeleka McField bila kipingamizi, alitambaa ili akaiokote ile Shotgun lakini alipotaka kuishika tu, Beretta 92, bastola ya kamanda Amata ilipiga kidole kimoja cha mkono wa McField na kusababisha McField kuiacha ile bunduki na kumgeukia Amata. Kamanda Amata aliiokota ile shotgun na kuirudisha bastola yake mahali pake ndani ya suti, kisha akachukua simu yake na kuongea maneno machache, sekunde chache polisi wenye silaha walivamia nyumba hiyo na kumtia pingu McField akiwa chini ya uangalizi makini wa kamanda Amata, wengine walienda kumchukua Dr Kazumari kama walivyoelekezwa na wote wawili waliwatia katika gari maalum tayari kuwaondoa eneo lile.

“Safi sana Kamanda,” ilikuwa ni sauti ya Inspekta Simbeye aliyefika hapo na vijana wake tayari kutoa msaada,

“Ndiyo kazi yetu, kulilinda taifa,” Amata alijibu huku akitoa kitambaa chake na kujifuta damu zilizokuwa zikitoka katika jeraha lake.

Uchunguzi wa awali ulifanyika katika nyumba ile na kugundulika mambo mengi ya siri, nyaraka za siri, pia katika chumba Fulani kulikutwa miili ya watu iliyokuwa imehifadhiwa katika majokofu maalum kwa kazi hiyo, hakuna aliyejua ni nini ilikuwa dhumuni la kuhifadhi miili ile, hiyo ilikuwa siri ya Dr Kazumari. Katika kijumba kile kulikutwa mtambo maalum unaoweza kupiga simu kwa kutumia namba yoyote ya nchi yoyote na kumpoteza mpigiwaji kujua simu inatoka mahali fulani kumbe si kweli, kwa amri ya Inspekta Simbeye nyumba ile iliwekwa chini ya uangalizi wa polisi hakuna aliyeruhusiwa kuingia, utepe wa njano uliosomeka ‘police line don’t cross’ ulizungushwa.

“Afande, hakikisha huyo mtu umemtunza vizuri, ni mtu hatari sana anaweza kutoroka hata ndege ikiwa hewani” kamanda Amata alimtahadharisha Inspekta Simbeye.

“Usiwe na shaka Kamnda!” alijibu.

“Ok, naomba vijana wawili wenye silaha tuelekee kwa Punde Kishime yeye ndiye main point ya tukio zima”

Kamanda Amata na vijana wawili wa polisi waliondoka na ile Ladrover 110 kuelekea Msasani kwa Punde Kishime…


Breki za ile landrover ziliisimamisha hiyo gari mbele ya nyumba kubwa ya kisasa eneo la Msasani, kamanda Amata alishuka akifuatiwa na wale vijana wawili wenye silaha,

“Wekeni ulinzi nje mimi naingia ndani,” aliwaamuru nao wakatii, wakajigawa mmoja akawa upande wa mbele na mwingine upande wa nyuma. Amata aliusogelea mlango na kugonga kengele, nyayo zilisikika zikija upande wa mlango na mara ukafunguliwa,

“Karibu” mtumishi wa ndani alimkaribisha Amata

“Asante baba yupo?” aliuliza

“Hapana ametoka kama nusu saa ilopita”

“Kaenda wapi?”

“Amenambia anaenda shamba,”

Kamanda Amata alizungusha akili yake akajua kuwa hapa anachezwa shere, alifikiria kidogo na kisha akamtazama yule msichana,

“Sikia, sisi ni polisi tunamtaka baba yako kwa ajili ya usalama, kuna majambazi wanataka kumvamia tumepewa taarifa,na wanamtafuta popote alipo, niambie yuko wapi?”

“Baba hayupo jamani kaenda shamba”

“Kaenda na nani?”

“Peke yake tu, mama na watoto hawapo tangu wiki moja ilopita” Amata alichukua simu yake na kupiga namba Fulani huku akisogea kwenye gari ile.

“Ndiyo hebu muulize kama anajua shambani kwa Mheshimiwa Kishime” Amata alikuwa akiongea na Chiba aliyekuwa mafichoni pamoja na bwana Chakwima baada ya muda Amata alionekana kupewa maelekezo Fulani.

“Ok, sasa vijana msitoke hapa mpaka mtakapopata amri nyingine, kama atarudi hakikisheni anakuwa chini ya ulinzi na mtoe taarifa ka Inspekta mi nakwenda huko shamba. Amata aliingia katika ile landrover na kuondoka kwa kasi kufuatia maelekezo aliyopewa.


DEFENDER ya polisi iliiacha nyumba ya Dr Kazumari, ndani yake ikiwa na polisi sita waliosheheni silaha na watu wawili Dr Kazumari pamoja na McField wakiwa njiani kuwapeleka kituo cha polisi cha kati. Waliiacha barabara ya Chang’ombe na kuchukua ile ya Nyerere kuelekea Nkurumah, king’ola cha gari hiyo kilizifanya garinyingine kutawanyika na kuiachia njia ili ipite kiurahisi.

McField akiwa ameketi kajiinamia akili yake ilikuwa inafanya kazi mara mia, kelele za honi ya treni zilimshtua na alipotazama aliona treni ile ikitokea stesheni kuelekea safari zake zingine, hakupoteza nafasi, kitendo bila kuchelewa, kutoka pale alipoketi aliichanu miguu yake miwili na kuwapiga mateke makali wale polisi walioketi mbele yake, akabla hawajatahamaki ngumi moja ilitua katika eneo nyeti la mmoja aliyening’inia mlangoni na kuachai mlango kisha kuanguka vibaya barabarani, wakati wengine wakishtushwa na kitendo hicho McField aliruka kwa kupitia mlango wa nyuma na kutua barabarani kwa ufundi wa hali ya juu, gari nyingi zilizokuwa zikija zilipoteza muelekeo ili zisiwagonge watu hao na matokeo yake ziligongana zenyewe kwa zenyewe. Milio ya risasi ilisikika, na kuwafanya watu kutafutana kwenye ile njia panda ya barabara ya Nyerere na Shaurimoyo, McField aliutumia mwanya huo na kupanda kwenye ukingo wa daraja bila kuchelewa alijirusha hewani na kwenda kutua katika behewa la mizigo lilifunikwa turubai juu yake, huku treni ile ikienda kasi, polisi walijaribu kulenga shabaha lakini walikosa, waliishuhudia treni ile ikipotea na McField juu yake. Taarifa za utoro huo zilifika vituo mbalimbali vya polisi na mara moja polisi wa Buguruni waliwahi akuizuia treni hiyo kabla haijavuka Buguruni, lakini tafuta tafuta na wewe hawakumuona McField, baada ya majadiliano marefu waliamua kuiruhusu iendelee na safari.

Inspekta Simbeye aliwalaumu sana vijana wake kwa uzembe lakini mwishoni alikiri kuwa yule jamaa ni hatari, alishindwa kujua atamuambia nini na vipi kamanda Amata aliyempata mtu huyo kwa shida sana, alijikuna kichwa na kuzunguka huku na kule bila kupata jibu.

Dr kazumari aliwekwa selo apumzike kabla ya kipindi cha mahojiano kufanyika kati yao.


KAMANDA Amata alisimamisha gari yake karibu na geti kubwa jeusi, ndani ya geti hilo kulikuwa na shamba kubwa sana mazao na mimea mbalimbali ilipandwa kiufundi sana, ilionekana wazi kuwa aliyefanya hiyo kazi ni mtaalamu wa hali ya juu. Amata alilisogelea geti na kugonga, mlinzi wa kimasai alikuja na kufungua kidirisha kidogo, akachungulia nje.

“Ikusaidie nini rafiki?” aliuliza

“Baba amekuja huku?” kamnda aliuliza

“Oh! Hapana leo haijaja kabisa, mara ya mwisho ilikuja hapa majusi”

Amata alichanganyikiwa, aliegemea gari na kufikiri machache, kisha akaingia garini na kuligeuza kwa fujo, simu sikioni akisubiri upande wa pili umjibu.

“Yes, Chiba, huyu jamaa inaonekana katutoroka na lazima ihakikishwe anatiwa mkononi leo hii, fanya unaloweza akamatike, jaribu kumtrace mpaka umpate kisha nipe uelekeo” baada ya kumaliza akakta simu na kuirusha kwenye kiti, aliiacha barabara ya shambani na kuingia kwenye lami kuelekea Kisarawe kisha kuchukua uelekeo wa Pugu na kurudi mjini.

Japokuwa kulikuwa na foleni na msongamano wa magari lakini Amata alitumia uzoefu wake wote kuweza kupita barabara hiyo ya Nyerere na kufanikiwa kufika katikati ya mji, jasho lilikuwa likimtoka kwa joto la Dar es salaam.

Mbele ya kituo cha polisi kati aliteremka na moja kwa moja aliuendea mlango wa Inspekta Simbeye na kuufungua, alimkuta Inspekta akiwa amekaa kitini huku akichezesha kalamu yake,

“Vipi Inspekta, mbona huko nje hali si tulivu sana?” aliuliza Amata

“Kamanda, nasikitika kukujulisha kuwa yule jamaa katutoroka, mchezo alioufanya sijawahi kuona binadamu kama yule, ile ni killing Machine,”

Amata alijishika kichwa, akashusha mikono kiunoni.

“Unasema?” aliuliza huku akizungukazunguka, “Shiit, McField katoroka, Kishime hajulikani alipo, kazi ishakuwa ngumu Inspekta”

“Vijana wapo wanamsaka kila kona” Simbeye alijitetea

“Yule jamaa hasakwi kwa mtindo huo baba angu” Amata alikuwa mpole ghafla na kuketi kitini.

“Ok sasa naomba taarifa zisambae kote haraka iwezekanavyo ili kazi ifanyike katika kila uchochoro wa nchi hii” Amata alitoa amri na kisha kunyanyuka kitini, alionekana wazi kuchanganyikiwa, akalegeza tai yake na kuruhusu hewa kidogo iingie mwilini, “Nahitaji kumuona Dr kazumari tafadhali” aliomba, na kisha wote wawili wateremka ghorofa ya chini ‘Shimoni’ na kukumkuta Kazumari akiwa hoi. Amata akamwangalia na kuwapa ishara vijana kumleta upande mwingine.

Akiwa ameketishwa kwenye kiti maalum cha chuma huku mikono yake yote ikiwa imefungwa kwa kamba, uchi wa mnyama, alikuwa ni yeye na askari polisi wawili vijana walioonekana kutokuwa na mchezo hata kidogo.

Dr kazumari, alitulia tuli bila kujua afanye nini kwa muda huo, Amata aliingia ndani ya chumba hicho, akatoa koti lake na kulitundika kwenye kitundikio maalum na kuketi kiti kilichotazamana na Dr Kazumari.

“Daktari, uliyepewa dhamana ya kutibu watu katika taifa la Tanzania na kokote ulimwenguni, leo hii unihujumu nchi yako mwenyewe kwa kuhifadhi na kusaidia kupanga njama chafu kama hizi, kweli, watanzania watafurahi kusikia habari hii na kushsudia unavyonyongwa endapo utapindisha au kunipa majibu ya uongo juu ya maswali yangu yafuatayo” ….

Amata alijiweka sawa na kutazamana na Dr Kazumari,

“Haya nieleze kwanza, hawa unaowasaidia katika kazi hii dhalimu ni akina nani na wanataka nini?” Amata aliuliza kisha akamtazama Dr Kazumari kusubiri jibu, ukimya wa sekunde kadhaa ukatawala, “Huna jibu? Dr, hatupendi kutumia njia ngumu kukulazimisha kuongea lakini kama unahitaji tutaanza muda si mrefu” aliongeza Amata huku akiitazama saa yake. Dr Kazumari bado alikuwa kimya hakujibu kitu, Amata alimtazama na kutikisa kichwa kwa masikitiko, teke moja kali lilitua shavuni mwa Dr Kazumari na kumpeleka chini pamoja na kiti chake, yowe la uchungu na msaada lilisikika la kini hakuna aliyejali, wale vijana wa polisi waliinua kile kiti na kukiweka sawa kisha wakarudi kusimama palepale mahala pao pa mwanzo na kumuacha Kamanda aendelee na kazi yake,

“Kazumari, tusipotezeane muda, jibu maswali yangu” Amata aling’aka akaichomoa bastola yake kiunoni na kufyatua risasi moja iliyochimba milimeta kadhaa kutoka katika mguu wa Kazumari,

“Aaaaaa nasema, nasema, msiniue jamani” Kazumari alilia huku akiwa tayari haja ndogo imeshamtoka.

“Haya sema haraka!” Amata aliichukua ile bastora na kumgusisha ule mdomo wake kwenye paja lake kutoka na joto kali la ule mdomo wa bastola ilikuwa ni vigumu kwa Kazumari kuvumilia.

“Nasema jamani, siwajui kwa jina lakini wapo hapa nchini kwa shughuli zao binafsi za uwekezaji” akatema bonge la damu pale chini.

“Endelea” Kamanda Amata akamuamuru,

“Mimi sihusiki na wao, mnanionea tu, ila wao wamenishawishi kuwasaidia katika maswala ya matibabu hivyo nikatumia nyumba yangu kama ofisi, na wananilipa pesa nyingi sana” Kazumari akaongea kwa kulia kama mtoto.

“Nieleze tangu ulivyokutana nao mpaka wao wakushawishi, inaonekana wewe unajua mengi, ukikaidi nakutoa uhai” Amata aliendelea kumhoji

“Aaaa jamani msiniumize, mimi hawa walinifuata kazini miezi kama miwili ilopita kuniomba msaada wa kitabibu” ….

Miezi miwili ilopita – Hospitali ya temeke

Dr. Kazumari akiwa katika ofisi yake, mara hodi ikagongwa mlangoni kwake naye bila kufikiri akamkaribisha mgeni wake.

Vijana wawili wenye matambo makubwa walioonekana wazi ni watu wa mazoezi ila mmoja wao alionekana ni mnene zaidi, walisimama mbele yake.

“Karibuni viti vijana,” aliwakaribisha

“Asante dokta” mmoja lijibu, “Najua utapata mshtuko kwa kupokea wageni usiowatarajia kama sisi, lakini siku zote tunaambiwa kuwa mgeni njoo mwenyeji apone” baada ya maneno hayo wote watatu waliangua kicheko, kisha yule mmoja akendelea,

“Dokta, sisi tuna shida kubwa tumekuja kwako utusaidie tutakulipa malipo mazuri sana endapo utatupa huo msaada”

“Msaada gani vijana mbona mnanitia hofu?”

“Aaaa usihofu dokta, kama tunaweza kuongea hapa au hata popote utakapo ilimradi tu ni sisi watatu tulijue hili swala” aliongeza yule jamaa, kisha wakakubaliana kutoka nje ya eneo lile, wakaelekea baa ya jirani iliyokuwa na watu wachache mchana huo na kujichagulia viti vilivyowatosha, kila mtu aliagiza kinywaji chake na mazungumzo yakaanza.

“Dokta mimi naitwa BIG” alijitambulisha yule jamaa mwenye mwili mkubwa, mimi si Mtanzania nisikufiche, mimi ni kutoka Afrika ya kusini ila najua vyema Kiswahili si ajabu kuliko wewe!” kisha wote wakacheka tena, na yule BIG kaendelea, “Huyu hapa ni swahiba wngu anaitwa Rodolph Mampasi, yeye ni Mkongo.”

“Nshukuru kuwfahamu, mimi ni Dr. Kazumari, daktari bingwa mpasuaji pia nafahamu sana mambo ya mifupa ‘orthopaedic’, sasa nambieni shida yenu.” Dr Kazumari alijieleza.

“Ok, dokta sisi shida yetu ni hii, tuna jamaa yetu mmoja ambaye katuelekeza kwako anaitwa Beka wa Beka.” BIG alipotaja jina hilo aliona wazi Dr kazumari akishtuka na kutumbua macho, BIG akaendelea; “Tunachotaka sisi ni kuingia mkataba na wewe kama unavyofanya na Beka, ila sisi tutakulipa pesa nyingi sana kwa sababu kazi yako ukiifanya vyema basi utakuwa ni mmoja wetu kimataifa, sijui inawezekana?”

“Kwa nini isiwezekane? Kinachotakiwa ni malipo tu lakini pia kufichiana siri maana hii ni kazi haramu ninyi wenyewe mnaju hilo” aliwajibu Kazumari.

“Tutakachokifanya sisi, tutakuletea hata watu wetu walio nje wanapopata matatizo haya au kukusafirisha wewe kwenda huko kufanya kazi hiyo, Dr tutakulipa kwa dola za Kimarekani” BIG aligongea msumari wa moto.

“Hamna shida, lakini mnajua hii kazi hatufanyii katika ofisi zetu, nina clinic yangu ya siri ninayofanyia, hivyo kama mna shida basi hapo ndipo pa kukutania” Dr Kazumari aliwaeleza.

Mazungumzo kati yao yalichukua takribani nusu saa wakabadilishana kadi za kibishara na kuwekeana mikakati na mipaka ya kazi ikiwa mojawapo ni kufichiana siri.

Jioni ya siku hiyo watu wale pamoja na Dr Kazumari walikutana katika clinic ile ya siri aliyokuwa akiitumia Dr kazumari kwa kazi zake, hakuna mtu aliyeijua lakini wengi waliamini tu kuwa ni nyumba yake ya kuishi, ilikuwa imesheheni vifaa tiba vya kutosha, BIG alifurahi sana kuona clinic hiyo iliyo chini ya ardhi na juu yake kufunikwa na nyumba ya kawaida sana isiyo na kuu lolote, mlango wa kuingilia huko chini ulikuwa katika banda kubwa la mabati ambalo alilitumia kama stoo na gereji ya gari zake. Nyuma kabisa ya nyumba hiyo na lile banda palikuwa na kajumba kengine ka wastani kenye chumba kimoja na sebule ambacho Dr Kazumari alikatumia kama ofisi yake endapo hataki kukutana na mtu, ndani yakajumba hako kulikuwa na mlango wa siri ambao unaweza kukutoa nje kwakupitia chini ya ardhi na kutokea kwenye bonde la Keko kupitia bomba la zamani la majitaka.

“Dr, hiki chumba unakitumia?” BIG aliuliza

“Nakitumia mara chache sana,”

“Sasa tukitaka utukodishe kwa ajili ya kazi zetu hasa za kielektroniki maana pamejificha sana” BIG alitoo ombi. Pesa ya Kimarekani iliahidiwa tena juu ya kijumba hicho. Mc Field alipofika nchini alitumia eneo hilo la maficho kama ofisi yake nyeti ya mawasiliano, aliweza kuwasiliana na mtu yeyote, nchi yoyote, kwa namba yoyote na mtandao wowote anaoutaka bila tatizo, na hapa ndipo walipotumia kupiga simu kwa Punde Kishime mara kadhaa kwa kutumia namba ya mtu mwingine hata jeshi la polisi walipofuatilia hawakuweza kupata uelekeo sahihi wa simu hiyo ilikotokea isipokuwa walijikuta katika nyumba ya mtu mwingine kabisa.

Rejea chumba cha mateso…

“Sawa, kwa maelezo yako yote nimeelewa kuwa wewe ulikuwa mshirika wao wa karibu sana,” Amata akakohoa kidogo, “Sasa, kwa taarifa yako, hawa rafiki zako walikuwa kwenye mpango wa kupindua nchi, unalijua hilo?” Dr Kazumari alisikiliza kwa makini, akatikisa kichwa kukataa.

“Dr, ulianza kuonesha ushirikiano vizuri sasa umeanza kuniudhi tena, narudia sitaki kutumia nguvu, nieleze ukweli, unalijua hilo au hulijui?” Amata aliuliza

“Kweli hilo silijui, silijui kabisa”

“Vijana hebu mpeni njia ya kujibu huyu jamaa,” Kamanda Amata aliwaamuru wale vijana kufanya kazi yao. Kipigo cha maana kilichukua nafasi, mateso makali ya kupigwa shoti ya umeme yaliendeshwa mwilini mwa Dr akzumati mpaka alipopiga kelele za kukiri,

“Aaaaaaaaaaa!!!!! Mnaniua, ntasema, ntasema kabisa!” alilia kwa uchungu akiwa chini yeye na kiti chake

“Muacheni,” aliwaambia wale vijana; “Haya sema”

“Ndiyo, ndiyo nafahamu, walinijulisha siku hizi” alijibu huku akilia

“Nani alikujulisha?”

“Nilipigiwa simu na mtu anayeitwa, anayeitwa, anayeitwa…”

“Anayeitwa nani?”

“Gonzalenz! Ambaye ndiye alikuwa ananiingizia pesa benki kwa kazi hii”

Amata aliduwaa ghafla aliposikia jina hilo, Gonzalenz, akamgeukia Dr. Kazumari na kumtupia swali.

“Umeshawahi kukutana nae?”

“Hapana, ilikuwa nikutane nae jana jioni pale New World Cinema” Amata alimkatisha kwa kusema; “Pole nah ii niliyovaa ndiyo suti yako?”

Baada ya mateso makali Dr. Kazumari alieleza kitu mpaka safari ya kumteka Punde Kishime ilivyofanyika, Kamanda Amata akiwa anasikiliza hayo yote huku saa yake ikirekodi kila linalosemwa, alihisi mfinyo wa saa yake akaiinua na kubofya kitufe Fulani, ujumbe wa siri ukaingia kwa mtindo wa fax,

‘Traced at Bongoyo Island’ ujumbe ule ulimkuna kiasi Fulani Amata, Chiba alikuwa amekwishacheza na mitambo yake na kupata uelekeo wa wapi Punde Kishime alkuwapo kwa kutumi mtambo wa GPS ambao unaweza kukuonesha mahali ulipo ikitegemeana ni kitu gani umetumia, Punde Kishime alielekezwa na Gonzalenz kutokutumia simu,na kila walipomtafuta kwa kutumia uelekeo wa simu yake ilionekana ipo nyumbani na ni kweli ilithibitika kuwa hapo, lakini kosa ailolifanya ni kufungua mtandao wake wa mawasiliano kwa kutumia kompyuta ndogo ya Gonzalenz lengo ikiwa ni kulipoteza faili Fulani lililopo katika hifadhi za nyaraka za ofisi kabla halijashtukiwa na watu wa usalama, alipoingiza tu nywila yake na kufungua tovuti ya wizara ndipo signal zilipofika kwa mtaalamu wa ICT wa TSA Chiba wa Chiba na palepale alitafuta uelekeo na kuweza kung’amua kuwa mtumiaji yupo katika kisiwa cha Bongoyo usiku huo, akatuma taarifa haraka kwa Kamanda Amata na kazi ya kumnasa ikaanza …


“Madam, uko sawa hakuna shida zaidi, nakuruhusu unaweza kwenda kuendelea na majukumu ya kitaifa” alizungumza daktari wa jeshi, Dr Jasmine mwenye nyota mbili begani au kijeshi huitwa Luteni.

“Asante dokta,” Madam S alishukuru na kuinuka kwenye kiti, moja kwa moja alielekea maliwato na kujiweka sawa, alipojiona yuko timamu, akainua saa yake na kuitupia jicho, ilikuwa tayari saa nne asubuhi, akabofya kitu Fulani kwenye saa yake kisha akatamka maneno Fulani kwenye kioo cha saa hiyo na kutulia.

“Hapa kuna mzigo wako” ilikuwa sauti ya Dr Jasmine, akampatia kikoba kidogo cha mkononi. Madam S alikipokea na kukifungua ndani, macho yake yaligongana na .357 Mgnum, bastola ya Mmarekani iliyotengenezwa 1934 ilikuwa imelala kwa utulivu ndani yake,

“Asante!” alishukuru madam S na kutoka nje ya chumba kile cha daktari. Alivuta hatua chache na saa yake ilirudisha majibu kwa mtindo wa fax, hizi ni saa maalum ambazo hutumiwa na watu wenye kazi maalum hasa za kiusalama. Alisogea kwenye maegesho na kushangaa kuikuta gari yake ikiwa pale salama salimini, na funguo zake zikiwa zinaning’inia kwenye usukani, akaketi na kuitekenya, gari ikawaka akaiingiza barabarani, taratibu alitoka katika barabara itokayo Lugalo jeshini na kukata kulia kuifuata ile ya Bagamoyo kuelekea Mwenge, pale alinyoosha kuelekea Morroco ambako moja kwa moja alifika katika kituo cha polisi cha wanamaji pale karibu na Feli Magogoni.

“Karibu mama” polisi mmoja aliyevalia sare zake nyeupe alimkaribisha.

“Asante, nataka kuelekea kisiwa cha Bongoyo, naomba msaada wenu” akatoa ombi huku akionesha kitambulisho chake, bila kusita yule askari akampeleka ndani na kujaza katika daftari Fulani kisha wakaingia kwenye boti iendayo kasi na kuelekea katikati ya bahari kuelekea kisiwa kile, Madam S akiwa ndani ya boya lake na miwani maalum kwa kazi za majini kama hizo alituilia tuli, akimwangalia kijana huyo alivyokuwa mahiri kukiongoza chombo hicho. Aliinua saa yake na kuielekeza kinywani kisha akaongea,

“Niko njiani Kamanda, uelekeo tafadhali,” kisha akaushusha na mara ile saa ikatoa mlio Fulani, akatazama kwenye kioo chake tena.

“Kusini maghalibi Madam tunakusubiri” Madam S aliufikisha ujumbe kwa muongoza chombo kisha akatulia na chombo kile kikafuata uelekeo kilioamuriwa.

“Karibu tena Madam,” sauti ya Amata ilimkaribisha kwenye boti nyingine maalum iliyokuwa ikimsubiri, na ndani yake kulikuwa na Kamanda Amata, pamoja na Chiba aliyekuwa akicheza na kompyuta yake ili kuhakikisha uwepo wa windo lao.

Kisiwa cha Bongoyo

Kisiwa cha Bongoyo, kisiwa kinachopendwa na watalii wa ndani na nje. Ni kati ya visiwa vine mashuhuri katika jiji la Dar es salam, kipo umbali wa kilomita 2 na nusu kutoka Msasani Peninsula ambapo unaweza kufik kwa boti kwa muda wa dakika 30 tu ukitokea pale Slip Way.

Punde Kishime na Gonzalenzi walijichanganya katika kisiwa hicho tangu jioni ya siku iliyopita walijificha katika vichaka vya humo ili wasionekane na asubuhi hiyo walikuwa miongoni mwa watalii wengi weusi kwa weupe. Wakiwa ndani ya kibanda kimoja cha msonge wakipata maji ya madafu ndipo Punde Kishime alipomueleza Gonzalenzi juu ya hilo faili la siri na kwa vile aliweza kuingia katika mtandao wa wizara kutokea popote aliitumia kompyuta ndogo ya Gonzalenzi na ndipo Chiba alipomnasa kiurahisi.

“Hey, kaa tayari tunaondoka sasa hivi” Gonzalenz alimwambia Kishime, naye akazima ile kompyuta na kumpatia mwenye yake akaitia kwenye kibegi chake kidogo. Gonzalenz alimgeukia Kishime na kumwambia, “Sikiliza Kishime, tunaondoka tunakwenda Bangladesh, lakini kumbuka mpango wetu haujafa, upo palepale, utakaa kule mafichoni, sisi tutafanya vingine na sasa tutatumia mtutu kuichukua nchi hii kama demokrasia imeshindikana na wewe ndiye Rais wetu utakayesimama kama mkataba wetu ulivyo.”

“Sasa hapa tunatokaje rafiki?” Kishime aliuliza

“Hapa, kuna usafiri unakuja hapa dakika tano zijazo.” Gonzalenz alimjibu kisha akamwitya wakaingia kwenye chumba fulani, Gonzalenz alitungua mavazi kadhaa ya kuogelea yanayotumiwa na wazamiaji akajivalisha na kumsaidia Kishime kuvaa, ilikuwa kazi sana kwa Kishime kwa kuwa tangu azaliwe hajawahi kuva vitu kama vile zaidi ya kuona kwenye kipindi cha life under water, akayavaa shingo upande yalipomkaa sawia na kutundika ile miwani ‘mask and snorkel’ shingoni mwake, mikononi wakakamata miguu ya kuwasaidia kuogelea ‘fins’ na kuingia katika boti kana kwamba wanenda kupiga mbizi kumbe safari iliwadia.


Kamanda Amata alishuka kwenye boti na kukiendea kibanda kimojawapo kilicho karibu akaagiza Sprite baridi, akiwa ameketi kwenye kiti kirefu akiangaza macho huku na kule akisaidiwa na miwani yake inayoweza kuvuta vitu vya mbali pindi ageuzapo shingo yake, alipepesa huku na kule hakuona mtu hata wa kumfananaisha.

“Vipi huko madam?” aliuliza kwa njia ya kinasa sauti chake kilichopachikwa sawia masikioni mwake,

“Bila bila,” alijibiwa. Bado msako uliendelea, ilikuwa ni vigumu sana kutokana na uwingi wa watu uliyoijaza pwani ile, hawa wakicheza mpira, wengine wakiogelea, wengine wakiendesha vipikipiki vya majini basi ilimradi ilkikuwa shangwe, Amata alipita kucheki kila chumba kuona nini kilichopo, moyo ulimshtuka katika chupa cha wapiga mbizi, saa ya mkononi ilikuwa juu ya meza ndogo, akaisogelea na kuitazama kwa utulivu kisha kwa kutumia kitambaa maalumu akaichukua na kuitia kwenye kijimfuko cha plastiki na kurudi kwenye boti,

“Oya hebu che finger prints hapo,” alimuamuru Chiba, kama kawaida alifanya mambo na dakika chache aliweza kupata alama hizo kwenye kioo cha ile saa na alipoingiza katika mtambo wake na kuziscan zikaonekana vyema kisha akafanya kuzimatch katika mtandao wao wa utambuzi, alama nyingi zilipita katika kioo cha kompyuta yake kwa kasi na baada ya sekunde chache zikasimama na kushoto kwake kukatokea picha ambayo bila kificho ilijulikana, chini kukajiandika maelekezo yote.

“Yupo,” Chiba alisema. Amata alifikiria kitu kisha akatikisa kichwa,

“Nipe vifaa vya kupigia mbizi, nina wasiwasi anaweza kuwa anatoroshewa huko, hawa jamaa wamejizatiti sana Chiba,” Amata alizungumza huku akifungua mfuni ko mkubwa ulio chini kidogo upande wa nyuma wa boti hiyo na kutoa vifaa vya kupigia mbizi na kuanza kuvalia, baada ya kuvaa ile diving suit alivaa dive boot, kisha akajipachika kila kinachobidi, dive computer, weight belt, akajitupia shingoni mask & snorkel, akahakikisha air tank yake iko sawa pressure gauge akaikagua na pipes zote kisha altenate air source akahakikisha iko makini akiwa katika kujiweka sawa akakatishwa na Chiba, “Kamanda, Kamanda!.”

“Niambie Chiba” Amata aliitikia na kugeukia kule kwa Chiba, Chiba akmuoneshea alama ya mkono kuonesha ndani ya maji, kisha akavua yale ma headphone yake na kumpa Amata naye akayavaa, kwa utulivu sana alianza kusikia mikoromo ya kitu kama mashine inayotembea yenye mvumo kama gari au boti uliotulia sawia, akavua na kumrudishia.

“Kuna chombo chini, kwa vyovyote hawa jamaa wanaondoka na hicho” Chiba akaeleza, kamanda Amata akainua saa yake na kumwita Madam S, sekunde chache akawa amefika na kupewa data zote.

“Ok, Kamanda, dive, Chiba sogeza chombo deep sea, nipe simu yako ya upepo!” Madam S aliketi kitini na kuvaa zile headphone zingine zilizounganishwa na simu ya upepo. Chiba aliiwasha boti na kuitoa pale ilipo kisha akaizungusha upande wa pili wa kisiwa akifuata zile signa zilikokuwa zikiongezeka, Amata alijivika kila kitu mwilini na kisu chake tayari alikibana sawia mguuni huku kimoja na huku cha pili mkononi akiwa na bunduki aina ya rifle maalum kwa kupigania ukiwa ndani ya maji iliyoseheni risasi na bastola zake zilizofungwa vizuri alizipachika kiunoni mwake zikiwa na seal isiyoruhusu maji kupita.

Wakiwa umbali kama wa kilomita nne kutoka kisiwa cha Bongoyo, mawimbi makali yalikuwa yakiwasumbua lakini Chiba alionekana kuimudu vema boti ile ya ya ukubwa wa wastani lakini iendayo kasi sana. Kwa mbali aliona kitu cheupe kimesimama alipotazama kwa darubini aligundua ni boti ndogo imesimama lakini haina watu ndani, Amata alitikisa kichwa na kujiandaa kwa kazi.

Madam S alikuwa bize kwenye mtambo wa mawasiliano akiwasiliana na jeshi la wanamaji lililoonesha ushirikiano mzuri sana na wakamuahidi kuianza hiyo kazi mara moja.

“All the best Kamanda!” Madam S alimtakia uzima na kumpigia saluti kisha Kamanda akajitupa ndani ya maji kinyumenyume. Madam S alitazama mtibuko wa maji na Kamanda jinsi akipotelea majini, kisha akajitupa kitini na kushusha pumzi ndefu.


“Tuondoke hakuna kuchelewa vijana” Gonzalenz aliwaamuru vijana wake na chombo kikaanza kugeuka taratibu, boti hiyo yenye uwezo wa kupita chini ya maji na juu kama zingine ilikuja kwa kazi ya uokoaji tu wa watu hao wawili, ilikuwa na uwezo wa kwenda kasi kuliko unavyofikiria.

Punde Kishime alisaidiwa kuvua yale maguo yake na kupewa suti nadhifu sana, na kuongozwa hadi deki ya chini kisha akakabidhiwa funguo ya chumba cha mapumziko hakuruhusiwa kutoka, alipofungua na kuingia ndani alikaribishwa na warembo wawili wa kiarabu, wenye nywele ndefu zinazoishia makalioni walimvuta Kishime na kumlaza taratibu katika kitanda mwororo.

Gonzalenz alienda moja kwa moja katika chumba cha nahodha na kuwakuta vijana mahiri wako pale kwa kazi yao, aliwapa salamu na kuwapongeza kwa kazi.

Nahodha wa chombo kile alionekana kutetemeka pale katika mashine yake, Gonzalenz akamtazama na kumtupia swali, “Vipi mbona hivyo?”

“Tumezingirwa kila upande,” nahodha akajibu.

“What?” Gonzalenz alienda kwenye screen ndogo ambayo inaweza kuona umbali wa kilomita mbili, akaweka mikono kichwani akaishiwa nguvu, hana la kufanya.

“Ok hatuna jinsi ni kujitahidi kujiokoa, tumia zana ulizonazo waweke watu kwenye hali ya kujihami ukipata upenyo fanya yako mi nalala” Gonzalenzi aliondoka na kushuka kwenye deki ya chini akaingia chumbani kwake na kujifungia, kisha akawasha screen yake inayoweza kumuonesha kila kinachoendelea katika kila kona ya boti hiyo ya kisasa na kutoa taarifa kwa security.


Kamanda Amata, aliogelea mpaka umbali Fulani chini ya bahari na kuikuta boti kubwa ya kisasa ikiwa imetulia majini, akajaribu kuizunguka na upannde mmoja akakuta kuna ngazi ndogo ya kupandia, akakwea hapo mpaka akaukuta mlango mdogo kama dirisha, akautazama lakini hakujua ni jinsi gain ataufungua, akatazama vizuri pembeni yake akaona kama kadi yenye namba kadhaa, mara moja akajua kuwa kimlango hicho hufunguliwa kwa namba maalum, kwake haikuwa tatizo, akiwa bado anaeleaelea pale akipishana na samaki, wakati akifikiria jinsi ya kuziotea zile namba akaona ule mlango ukifunguka wenyewe, akasita kuingia akajua wazi huu mtego, akakata shauri akaingia taratibu mpaka mwili wote ukawa nadani kasha kile kimlango kikajifunga, na mara maji yaliyojaa mle ndani yakaanza kutoka kwa kutumia mabomba maalumu yaliyokuwa yakiyasukuma nje, mara kukawa hakuna maji, Amata akavua ule mtungi wa gesi na kuuweka chini kasha akachomoa bastola zake zote mbili na kutembea ka mwendo wa polepole, kona moja akasimama na kutazama huku na kule, juu aligundua kuna camera inayogeuka kila anakoelekea, akajifanya hajaiona kisha akainua mkono wake na kuifyatua kwa risasi moja, kwisha kazi, hakuna mlio uliosikika kwani bastola zote alikuwa amezifunga kiwambo cha sauti. Amata aliendelea kunyata kuelekea upande wa pili wa chombo kile, mara akasikia watu wakiongea kama wanakuja upande wake, akajibanza kwenye upenyo mmoja na kusubiri, bastola akazirudisha mahala pake na kujiandaa kwa mpambano wa mikono, akapita wa kwanza, na alipopita wa pili tu akamdaka shingo na kumbakna kabali maridadi kasha kumvutia kwenye ule upenyo na kumvunja shingo bila kelele. Yule mwenzake alipojikuta anaongea peke yake, akasimama na kugeuka nyuma, peupe, akarudi taratibu akiwa pale kwenye ule upenyo Amata akampigia mruzi hafifu, alipogeuka akamsukumia mwili wa mwenzake kasha akachomoa bastola yake, wakati jamaa anaudaka ule mwili tayari risasi ilifumua kifua chake pembeni kidogo ya moyo, chali. Kamanda Amata akatoka pale kwenye ule upenyo na wakati huo tayari alikuwa amekwishaiona camera nyingine nayoa akaifumua kwa risasi moja kasha akaingia mlango ule waliotokea wale jamaa. Akaingia mpaka katikati na kukuta korido ndefu yenye vyumba kadhaa, mlango wa kwanza ulimvutia zaidi, alama ya kuonesha kuwa ni hatari kilichomo ndani akachukua funguo yake isiyoshindwa kitasa chochote, akaitazama na kucheka kidogo, akakumbuka siku alipokabidhiwa funguo hiyo na Madam S alipoambiwa, ‘Hii ni funguo inayofungua 98% ya vitasa vyote duniani’, alipoitumbukiza na kuizungusha tu mlango ukakubali, akaingia ndani, nyaya nyingi za umeme na maswitch makubwamakubwa yalijaa kila upande, hakuwa na haja ya kupoteza muda, alizima switch zote na kila kitu ndani ya boti ile kilizimika.

Chumba cha Nahodha

“Shiit !” nahodha alihamanika baada ya kuona kila kitu kimezimika, dashboard yote iko off, taa na kila kitu, hakuna mawasiliano wa la hakuna nini ndani ya chombo hicho, hatari, hakuna la kufanya, alivuta droo yake na kutoa bunduki yake kisha akaelekea kwenye control room, alipokatiza upenyo Fulani alistukia teke moja la mikono na bunduki ikamtoka, kabla hajaelewa kinachoendelea, ngumi moja maridadi iliyotua puani ikamtia kiwewe, akataka kurudi anakotoka, hakupiga hata hatua mbili ngwala moja kali iliyomfanya aanguke mzima mzima na kutanguliza uso chini, “Freeze!!!”, sauti zilitoke nyuma ya Kamanda Amata, bila kujalia akiwa kwenye mwendo wa kukimbia kumkimbilia yule nahodha aliruka sarakasi ya kitoto lakini kwa ufundi mkuba alipotua alikuwa kapiga goti moja chini na bastola zake mkononi tayrai zilishjafanya kazi, wale jamaa wawili wote wakaenda chini bila ubishi damu zikichafua eneo la tukio.

“Tulia hivyo hivyo!” alimuamuru yule nahodha, “Simama polepole, haya niongoze wapi yupo Gonzalenz?” Yule naohodha alikuwa akitembea akisitasita wakati Amata alikuwa hataki kupoteza muda, akasimama na kugeuka, ‘Twende!” alimuriwa tena lakini bado alikodoa macho Amata hakufanya masihara alifytaua risasi moja na kupiga kiganja cha mkono, yowe la uchungu likamtoka, kabla hajafanya lolote wengine wawili wakatpokea mbela yao, Kamanda Amata akaruka na kumsukuma kwa mguu wa nguvu uliomkanyaga, begani na kumsukuma mpaka kwa wale jamaa kisha muda huohuo bastola za kamanda zikacheua na kugawana watuhumiwa, wote chali. Kamanda Amata akachukua walkie talkie yake na kuwasiliana na nchi kavu kuomba msaada, Chiba alipokea mawasiliano na kutekeleza, dakika chache wanajeshi wa majini ‘Navy’ vijana wa Kigamboni wakaivamia boti hiyo na kuendesha shughuli nzito isiyo na huruma, ilikuwa ni vichapo kila kona, ulivunjwa kila mlango kuhakikisha hakuna anayebakia, Kamanda Amata alikuwa deki ya chini akibamiza kila mlango kumsaka ama Gonzalenz au Punde Kishime.

  • * *

Gonzalenz alikuwa chini kabisa kwenye chumba cha siri, akijaaribu mbinu za kutoroka kwa chombo kingine cha siri lakini haikuwezekana kwa sababu. Boti haikuwa na umeme kila kona,a alikuwa tayari amekwishajifungia ndani ya kimashine hicho amabacho kingetoka nje na kuilipua hiyo boti lakini ilishindikana alibaki hana ujanja jasho la kwapa likimtiririka. Punde Kishime alipoona hayo uzalendo ukamshinda hakujua afanye nini, alitoka nje ya chombo kile na kuanza kukimbia ovyo alipita mlango Fulani na kujifungia kwenye kichumba kidogo akitetemeka.

Gonzalenz alimuona Kamanda Amata akiwa amefika katika ile sehemu, hamna ujanja, akatoka nje ya kila chombo na moja kwa moja kumvamia Amata, kwa utulivu mkubwa kamanda alimpa makonde ya haja yaliyozibua mifereji yake ya damu na kumuacha hoi.

“Kill me please” aliomba auawe kilazima.

“kamwe siwezi kukuua, ulimwengu lazima ukufahamu kwa kazi za kishetani unazofanya kwa kuwalaghai viongozi na wanasiasa dhaifu ili kuzinunua nchi zao nawe na mashetani wenzzio kugawana kama mnavyogawana nyama ya kitoweo. Hamuoni aibu kmnyonya mtu aliyekwishanyonywa tangu enzi na enzi, hata lepe la damu hana. Lazima Afrika ikujue wewe kupe mkubwa unayesababisha machafuko huku na huko, ndugu wakiuana wenyewe kwa wenyewe, Afrika ikionekana bara la mapinduzi kila wakati kwa sababu yenu, kwa nini mnatuonea sisi watu weusi, hamtaki watoto wetu wasome kwa raha na kuishi maisha bora, isipokuwa wenu tu ndiyo wenye haki ya kuishi na kuwa na ndoto za kuitawala dunia, kwa niaba ya wote wewe lazima unyongwe huku ulimwengu ukishuhudia, dhalimu mkubwa wewe…” Amata alishikwa na hasira na kumpiga teke moja kali lililotia chini ya kidevu na kumtupia upande wa pili chali, akamnyanyua na kumsindikiza kwa makonde mazito mpaka kwenye korido ndefu na kumfikisha akiwa hoi hawezi hata kutembea, askari wawili wakaja na kumti pingu.

“Muhifadhini hakikisheni hafi, roho yake ikitoka muidake tafadhali.” Kamanda aliamuru kisha akaenda kataika control room na kurudisha umeme alioukata, chombo kile kikarudiwa na uhai upya. Kazi ya kumsaka Punde Kishime ikaanza humo ndani.

Akiwa kiwa kwenye kile chumba kidogo, Kishime alikuwa akitetemeka hajua la kufanya, suruali yake imekwishalowa mkojo mwingi tu wakati yeye mwenyewe hata hajui kama kajikojolea, alipotaka kufungua mlango kutoka akakutana uso kwa uso na Kamanda Amata.

“Mheshimiwa, mbio zako za sakafuni zimeishia ukingoni? Ulifikiri ni wapi utafika kwa kuwadhulumu wananchi haki yao ndani ya nchi yao, na wewe kuwa kibaraka wa weupe ukiwatumikia kama mtumwa, hivi hizi siasa zenu za siku hizi mnazitoa wapi, siasa za uchu wa pesa mpaka mnawasahau bibi na babu zenu waliowaleta duniani, pesa pesa pesa, ulitegemea uwe Rais wanchi hii kwa njia hii, njia ya kuingia mikataba ya kishetani, ya kuwataka watu waoane jinsia moja, au waoe mifugo yao na mifugo ioe mabwana zao, mnataka muhalalishe utoaji mamba na takataka zinngine huku damu za Watanzania zikiwa ni sadaka kwa mizimu yenu ambayo hata ilipo tu masikini hujui. Siasa gain hizi za kutufanya watumwa kwenye nchi yetu wenyewe? Sasa leo hii jopo la waandishi wa habari wanakusubiri huko nje wakutoa kwenye luninga ili wananchi wakushuhudie jinsi ulivyo mbwa mwitu ndani ya ngozi ya chui. Umethaminiwa ukapewa ukatibu wa wizara ukapata sifa kubwa nchini mwisho ukawaona waliokuweka hapo ni wajinga na wapumbavu ukaamua kuwageuka kwa mbinu za ajabu ajabu, basi kila mtu atashuhudia jaji atakapokuhukumu kifo na nafikiri wote watashangilia kwa hilo.” Kisha Kamanda Amata akamchukua na kutoka nae.


Nahodha wa jeshi la maji captain Majaliwa, alifanikiwa kukipandisha juu ya maji chombo kile cha ajabu na kila aliye jirani aliweza kukiona kwa ukaribu zaidi, boti za jeshi na polisi zikasogea jirani kabisa na kuwachukua wote walikuwa bado wakihema, raia wa nchi tofauti walikuwa wakifanya kazi humo ndani wanawake kwa wanaume.

Madam S alisimama juu ya boti akiwa na Chiba wakitazama jinsi mateka wale wakiingia kwenye boti kubwa ya kijeshi, lakini hamu yao ilikuwa kuwaona wale wanaowataka wao Gonzalenz na Kishime.

Baada ya mateka wote kutolewa pamoja na wale ambao ni majeruhi kutokana na mapigano yaliyozuka ndani ya boti ile, Gonzalenz alitolewa botini akiwa ameshikwa huku na huku, huku mikono yake ikiwa imefungwa pingu, shati lake lilikuwa halitamaniki kwa jinsi lilivyolowa kwa damu zilizokuwa zikimtoka, huyu alipelekwa kwenye boti maalumu kisha akafuatiwa na Punde Kishime aliyekuwa na pingu mikononi mwake akisindikizwa na kamanda Amata nyuma yake, aliongozwa kwenye boti maalum aliyopakiwa Kishime, akaingia humo. Chiba akaisogeza ile boti yake karibu kabisa na ile boti ya polisi iliyowapakia wawili wale, Madam S akakutana na Amata wakapeana mikono ya ushindi kisha wakaungana katika boti ile na bila kuchelewa boti ile iliondoshwa eneo lile na kuacha shughuli zingine zikiendelea kati boti ile ya wageni na zile za jeshi na polisi.


Ndani ya gereza la Ukonga Punde Kishime, Gonzalenz, BIG na wengine waliopatikana katika mkakati huo, nyuma wakiwa wamezungukwa na askari wenye bunduki, vichwa waliinamisha chini kwa aibu ya kukamatwa kwao.

Makabidhiano yalifanyika na na wale mateka wote waliwekwa kwenye chumba kimoja wakisubiri uamuzi wa serikali. Wandishi wa habari nao hawakuwa nyuma kupata habari na picha za kutumia katika vyombo vyao ili tu kuipamba habari ile. Ilikuwa siku isiyosahaulika kwa vyombo vya usalama siku hiyo, mafanikio waliyoyafikia yalikuwa makubwa, kuzima mbio za uchaguzi kwa mgombea wa chama cha upinzani aliyekuwa kibaraka wa mabwanyenye waliotunisha matumbo yao huku na huko yakisubiri kuambiwa ‘Tayari’.

HATIMA

Kamanda Amata aliketi kimya katika kiti cha nyuma cha V8 hiyo iliyowachukua kuwapeleka kwenye kikao kifupi katika jengo la wizara ya ulinzi. Akiwa mwenye mawazo, Amata hakuwa na raha kabisa.

“Vipi Kamanda mbona hauna furaha?” Madam S alisaili hali hiyo.

“Nasikitika sana kumkosa Mc Field, yaani naona kama hatujafanya kazi au kazi yote ni bure”

“Usiwaze sana Kamanda, kazi uliyoifanya inastahili pongezi mbele ya Watanzania wote waliokuwa wakifuatilia mkasa huu kwa nja mbalimbali, huyo hayawani tutampata tu, Kamanda tumeweka ulinzi mipakani, msako wa mtu kwa mtu unaendelea sehemu zote muhimu kama viwanja vya ndege, bandari na vituo vya mabasi, makachero wetu wanafanya msako kwenye kila hoteli na sehemu za wageni, hivyo tutulie tusubiri majibu,” wakati Madam S akimaliza kuongea hayo tayari gari ilikuwa ikiegeshwa katika maegesho ya wizara hiyo.


Mahakama kuu ya Tanzania ilitowa hukumu kwa watuhumiwa hao, kifungo cha maisha kwa Gonzalenz na BIG katika magereza ya Tanzania, Punde Kishime aliwekwa kizuizini huko kijijini kwao Kizogolota katika mkoa wa Geita, hakuruhusiwa kujihusisha na shughuli yoyote ya kisiasa, kusafiri popote nje ya wilaya aliyopo, isitoshe alinyang’anywa vibali vyote pamoja na hati za kusafiria.


Siku kadhaa zilipita, msako wa kumsaka Mc Field haukuzaa matunda, Kamanda Amata alikata tamaa ya kumpata mtu huyo. Maadam hakupata taarifa ya kuonekana kwake, basi aliamini kuwa jasusi huyo bado atakuwa humuhumu nchini na ipo siku watakutana na ndipo moto utawaka.

Alichukua rimoti yake na kuzima Tv iliyokuwa ikionesha kipindi cha muziki Kass Kass na kisha kuamua kwenda kujipumzisha.

MWISHO

DOWNLOAD: Kontawa Ft Maua Sama – Sikuachi

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment