Mauaji ya Kasisi Sehemu ya Pili
KIJASUSI

Ep 02: Mauaji ya Kasisi

SIMULIZI Mauaji ya Kasisi
Mauaji ya Kasisi Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE


Simulizi : Mauaji Ya Kasisi

Sehemu ya Pili (2)

“Mimi ni bwana Melchior Ndege, mtu wa huko Iriyamurahi”

“Hapa nimefikaje na ni wapi?”

“Tangu unafikishwa pale godown mimi nilikuona na sura yako si ngeni kwangu, nakufahamu sana, wewe ni Fr Gichuru wa kanisa kuu siyo?”

“Sawa kabisa! Zaidi ya hapo wewe ni Malaika kwangu, hakika Mungu amekutuma”

“Napenda tuzungumze kidogo” yule mzee alimwambia Fr Gichuru. Fr Gichuru alimwangalia kwa makini yule mzee aliyekaa mbele yake juu ya kiti kidogo cha miguu mitatu.

“Father, kwa nini hawa jamaa wamekuteka wewe? Maana kama hela huna!”

“Bwana Ndege, hii ni hadithi ndefu sana” Fr Gichuru akatulia kidogo kisha akaanza kumueleza kila kitu mzee yule, hakumficha hata jambo moja, kuanzia safari yake ya Roma mpaka aliporudi, mpaka alivyotekwa na jinsi ilivyokuwa. Mzee Melchior Ndege alitulia tuli kama maji ya mtungini, alimwangalia yule kasisi asiye na kosa kisha akakohoa kidogo.

“Father, mimi ndiyo niliyekuleta humu ndani, ndiye niliyekutoa kule, wala si mbali ni mtaa wa tatu tu hapo, nimekufuatilia kwa muda mrefu sana na hata mpango wa wewe kutekwa mi niliujua mapema.” Maelezo yale yalimshtua sana Fr Gichuru, alishindwa kuelewa inakuwaje mzee huyo kumfuatilia na kujua hata kutekwa kwake.

“Sijakuelewa bado bwana Melchior!” Fr Gichuru aliuliza kwa mshangao

“Na hiyo nayo ni hadithi ndefu father Gichuru, nitakwambia jiweke tayari” akachukua chupa yake ya maji na kupiga mafunda kadhaa kisha akaiweka chini na kuendelea, “Bill, ni mtu anayetafutwa sana kila kona ya dunia hii, ni jasusi la kutisha la kimataifa linalotumiwa na makundi mengi kuekeleza mauaji au wizi wa kimataifa, hapa ninavyokwambia tayari FBI wameshafika Kenya kwa ajili ya kumnasa mtu huyu, Bill hawezi kuja hapa kwa kuitaka hiyo monstrance tu kama alivyosema, ama kuna kitu kingine nyuma yake au hiyo monstrance ina jambo lingine ambalo ninyi hamlijui, mimi hapa usinione mzee, mi siyo mzee” yule mzee aliposema hayo aliingiza mkono wake ndani ya kofia aliyojifunika ambayo ilikuwa imeunganishwa na jacket lake na kwa kutumia nguvu alivua kitu kama gozi nene usoni mwake na kulitupa chini kisha akajifuta vizuri na kumtazama Fr Gichuru ambaye alikuwa amepigwa na butwaa akmtazama kijana huyo mtanashati kwa sura, kumbe alivaa sura bandia.

3

Siku chache zilizopita

Simu ya mezani kwa Melchior Ndege iliita, mara moja aliacha kazi aliyokuwa akiifanya na kuitazama simu hiyo alisita kidogo kuipokea, lakini kelele za simu ile zilimfanya aipokee

“Hello!” aliita

“…aa! Ok, sawa (…) sasa hivi nashughulikia”

Melchior aliinuka kwenye kiti chake na kuingia kwenye lift iliyompeleka juu kama ghorofa tano hivi katika jengo la KICC, aliuendea mlango Fulani na kuufungua kisha kuingia ndani

“Karibu sana Ndege, keti, maana kwa jinsi unavyohema itakuwa unahabari nzito” Gallus Shikuku alimkaribisha Ndege ofisini kwake.

“Nimepata simu kutoka ofisi ndogo ya uwanja wa ndege” Melchior alianza kuzungumza

“Mh niambie kijana!” alijiweka vizuri kitini na kuiegemea meza yake kubwa akimtazama Melchior Ndege.

“Mtu tunayentafuta kwa udi na uvumba ameingia nchini, Bill”

Gallus Shikuku hakuamini anachokisikia kwa kijana huyo alimkazia macho na kumuuliza tena swali lilelile, naye akapata jibu lilelile.

“Bill…” Gallus Shikuku alilirudia jina hilo, “Kaja kufanya nini tena? Kajileta mwenyewe” aliongea peke yake.

“Ok! Ndege nimeisikia hiyo habari, sasa vijana kazini, naomba umchunguze Bill anavyoketi na anvyosimama na wakati huo mimi nawasiliana na vyombo vyote vinavyomsaka ili tupate usaidizi maana huyu mtu ni wa hatari sana na tukienda vibaya anatumaliza.”

Melchior alitoka ofisini kwa boss wake bwana Gallus Shikuku na kurudi ofisini kwake kujipanga kwa kazi aliyopewa. Bwana Gallus Shikuku alijishika kichwa na kuzunguka kutoka huku na huku, aliiona sasa bahati imekuja kwao ya kumtia mkononi mkorofi huyu, Bill, aliyeshindikana, FBI wanamtafuta, Interpool wanamsaka kila kona ya dunia, lakini jinsi anavyowatoroka ni utata mtupu, wengine wakadiriki kusema ni mchawi lakini haikuwa hivyo.

Gallus Shikuku aliketi kitini na kuvuta laptop yake na kufungua sehemu ya kuandika ujumbe, baada ya kuhakikishiwa kuwa aliyeonekana ni Bill na watu wake walio uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kumtumia picha za haraka na yeye kuzifikisha katika kitengo maalumu cha utambuzi, picha hizo zilitoa jibu lilelile, Bill Van Getgand. Shikuku alitoa taarifa kwa vyombo husika vya usalama ambavyo tayari vilisambaza habari na picha ya jasusi huyo popote duniani atakapoonekana basi mara moja wataarifiwe ili atiwe nguvuni.

Melchior Ndege aliondoka na kuliacha jengo la KICC na kujichanganya mjini kadiri ya maelekezo aliyopewa na watu wanaomfuatilia Bill, ili kujua ni wapi amefikia. Haikuwa kazi kwani alimuaona mtu huyu mnene akiwa na ile fimbo yake ya kutembelea, mara hii Ndege alishtuka kidogo, hakuambiwa kuwa huyu jamaa anatembea kwa msaada wa fimbo, alichukua kamera yake kubwa aina ya Cannon Cibershot na kumpiga picha kadhaa akiwa pale nje ya Plazza Hotel akilipana na muendesha tax, mara moja zile picha aliziingiza katika computer yake ndogo na kuzituma kwa bosi wake na maelezo machache.

Bill Van Getgand alipanga chumba namba 207 katika hotel hiyo, akiwa kaja Nairobi kwa kazi moja tu ndogo ya kuhakikisha anaipata monstrance aliyotumwa na tajiri wake kutoka Ujerumani, Don Andreas, kwa pesa nyingi sana.

Melchior Ndege, aliweka vijana eneo lile kuhakikisha wanapata nyendo zote za Bill mchana huo ili wajue jinsi ya kumtega.


Melchior Ndege aliendelea kubaki pale nje ya hotel hiyo akifuatilia kujua ni wakati gani bwana Bill atatoka ili na yeye afanye kazi yake, alilolisubiri likatimia, muda kama wa saa nne usiku hivi Bill alitoka na kwenda kusikojulikana, alipopotelea na gari hilo alilolikodi, Melchior alitoka katika gari yake na kuchukua vifaa vyake vichache na kuelekea katika hoteli ile, moja kwa moja hakupitia katika ofisi ya mapokezi, aliingia katika lifti na kupanda mpaka ghorofa ya pili, alikitafuta chumba namba 7, haikuchukua muda alikipata, kwa kutumia funguo zake maalum alicheza na kitasa kile na mlango ule ukafunguka, akaingia na kuurudisha nyuma yake. Akatazama kile chumba kwa macho ya kiintelijensia kisha akakiendea kile kitanda kikubwa na kuivuta droo ya kitanda hicho kisha kwa upande wa chini akabandika kidubwasha maalum kisha akafanya hima kutoka katika chumba hicho. Alipofika chini, pale alipoegesha gari lake aliingia na kuketi ndani, kisha akawasha chombo Fulani kama simu na kuweka vidubwasha Fulani masikioni mwake alibonyabonya vitu Fulani na kutulia, haikuchukua muda Bill alirudi na mwanamke fulani wakikokotana na kuingia ndani ya hotel hiyo. Melchior aliwasha kile kidude chake na kujiwek tayari kisha akalaza kiti cha gari yake na kusubiri, mara baada ya sekunde kadhaa akaanza kusikia mazungumzo ya mahaba yaliyokuwa yakitoka katika chumba hicho, mara alisikia mikoromo ya raha za dunia, akabonyeza kitufe cha kurekodi kila kinachozungumzwa kisha yeye akajitupa katika usingizi akiwa ndani ya gari hiyo.

Katikati ya usiku melchior ndege alishtuka kwa simu iliyomuita ndani ya gari, aliitazama saa yake ilikuwa tayari imetimu saa tisa kasoro robo usiku, aliwasha mashine yake na kusikiliza machache yaliyoongelewa chumbani humo, Melchior alipata habari nyingi ambazo Bill alimshirikisha yule kahaba Rose na kumshawishi aweze kumfanyia kwa malipo ya pesa nyingi za kigeni. Mazungumzo yote melchior alikuwa ameyapata katika chombo chake kile. Alipogundua kuwa tayari ulikuwa ni usiku sana aliamua kuondoka eneo lile.

Asubuhi siku iliyofuata aliwasilisha ripoti kwa boss wake Bw Shikuku na kwa pamoja waliisikiliza kwa makini na kupanga mikakati ya kazi ikiwamo Melchior kusafiri katika ndege ambayo Fr Gichuru angeitumia kwenda Roma kwani huyo bwana Bill naye alipanga kusafiri kwa ndege hiyo ikiwa ni moja ya njama zake za kujiweka karibu na kasisi huyo.

Mpango ukasukwa na kila kitu kikawa sawa kabisa, Melchior Ndege akawa tayari kwa safari hiyo.

Akiwa ujerumani aliweza kumfuatilia vizuri sana mtu mnene Bill nyendo zake zote na kujua ni nini na ni nani aliyekuwa akionana nae mara kwa mara na kwa nia gani, alipolijua na kuhakikisha kuwa hapo cha kuhitaji, Melchior Ndege alichukua ndege na kuelekea Roma Italy ambako alijichanganya na watalii mbalimbali katika viwanja vya Vatican lakini yeye akiwa na lengo tofauti kabisa, alipopata nafasi ya kuingia ndani ya jengo hilo la kihistoria alijariu kutafuta kama anaweza kuona muhusika yoyote labda angemuuliza habari fulani fulani juu ya hiyo Monstrance ambapo sasa ndicho alichogundua kuwa Bill, mtu mnene ndicho hasa kilichomleta.

† † †

Yule mzee aliyekuwa sasa kijana alimtazama Fr Gichuru aliyekuwa amepigwa na butwaa kwa habari hiyo ambayo kwake ilikuwa kama riwaya nzuri masikioni mwake, alimtazama kijana huyu na kumuona hakika ni Malaika kwake.

“Na kuhusu kutekwa kwangu we ulijuaje?” Fr Gichuru alimtupia swali yule kijana.

“Ndiyo maana nakwambia ni stori ndefu sana, mimi nilijua kila kitu mpaka mpango wa wewe kuletwa hapa, anyway, hatuwezi kumaliza yote hapa maana muda nao unatuacha, mpango uliopo sasa kwanza, tunataka tumnase huyu mtu mnene kwani yeye ni jasusi linalotafutwa kila kona ya ulimwengu, kisha wewe tukuweke kwenye usalama, hivyo basi mimi na wewe tutatoka hapa na nitakupeleka sehemu ambayo utakaa huko mpaka amri nyingine itakapotolewa” Melchior Ndege alimaliza kuzungumza na kuinuka pale alipoketi kisha kujikung’uta vumbi katika zile nguo kuukuu.

“Sasa, unajua mimi ni Kasisi, hata kama nakwenda huko lazima viongozi wangu wajue na kuna zana ambazo ni muhimu kuondoka nazo kutokana na mfumo wa maisha yangu” Fr Gichuru alitoa ombi.

“Yeah, najua sana juu ya hilo, lakini kwa sasa kama wameshakuteka ujue hawatashindwa kukuua, kwa hiyo wewe twende na taarifa kwa viongozi wako sisi tutazipeleka kwa njia tunayoijua, maana kwa sasa hatuamini mtu” Melchior aliendelea. Japokuwa alijaribu kumbembeleza fr Gichuru lakini alikataa katakata, alipendekeza arudi kwanza parokiani kwake ndipo afanye taratibu kama hizo. Melchior Ndege hakuona haja ya kupoteza muda, alimchukua fr Gichuru na kupita nae katika vichocjoro kadhaa kisha wakafika nyuma ya jingo moja kubwa, kulikuwako hapo kituka kibanda lakini kilichofunikwa na manyasi marefu yaliyorundikwa baada ya kukatwa. Ndege akapekua pekua na ndani yake kulikuwa na pikipiki kubwa iliyofichwa hapo, akaitoa na kuwasha, muungurumo wake ulieleweka kabisa kuwa pikipiki hilo ni bidhaa ya Mjerumani BMW. Wote wawili wakakaa juu yake na Melchior Ndege akaliongoza kuelekea mjini. Moja kwa moja walifika mbele ya kanisa kuu la familia takatifu, Nirobi mjini na kumuacha hapo,

“Sasa, ukiwa tayari unifahamishe maana tunataka usalama wako fr,” Melchior Ndege alimuasa.

“Sawa Melchior, na Mungu akubariki sana katika hili,” alimalizia fr Gichuru na kuingia ndani ya wigo wa kanisa hilo, wakati Melchior Ndege akiondoka eneo lile na kurudi katika majukumu yake.

† † †

Kijua cha asubuhi kilianza kuchomoka katika maeneo ya viwanda ya Nairobi kandokando ya barabara ya Mombasa, walinzi waliopewa kazi ya kumchunga Fr Gichuru walikwenda kumtazama ili kuhakikisha kuwa yupo salama, walipofika hawakuamini wanachokiona, mlango ulikuwa wazi katika mtindo uleule kama Maria Magdalena alipofika katika kaburi la Yesu alfajiri. Wakatazamana, hawakuwa na lakufanya, wakatoa taarifa haraka kwa wakubwa waliomleta mateka huyo.

“Yaani aisee msilete ujinga, tunakuja sasa hivi” ilikuwa ni sauti ya Blach Cheetah kwenye simu hiyo, na mara simu ile ikakatwa.

Dakika kumi na tano, Black Cheetah, Mellina Wanjiku na Bwana Gichui walifika pale godown na kushuhudia hali hiyo, waliwaita walinzi wote pale laikini mmoja hakuonekana,

“Mwenzenu yuko wapi?” lilikuwa swali kutoka kwa Gichui kwenda kwa wale walinzi, hawakuwa na jibu, walibaki kutazamana tu, “Nawauliza ninyi, walinzi gain mpo hapa na mtu anatoroka? Ninyi mmekula njama,” aliongeza kisha akawasukumia wote kwenye kile kichumba na kuufunga mlango kwa nje.

Taarifa za kutoweka kwa fr Gichuru hazikumfurahisha Bill mtu mnene hata kidogo, alihisi kuwa hiyo ni njama na hasa kwa kuwa mlinzi mmoja hakuonekana kati ya hao.

Pamoja na adhabu walizowapa walinzi wale lakini hakuna kilichozaa matunda.

Bill aliwaita vijana wa kazi katika kivhumba kidogo ndani ya godown hilo na kuwapa kazi ya kumsaka popote alipo Fr Gichuru na atakapoonekana hakuna cha kusubiri ni kumuondoa uhai tu na mambo mengine yatafuatia.

“Sasa tukimuua ndiyo tutapata hiyo monstrance?” Mellina aliuliza.

Bill alibaki kimya kwa swali hilo kisha akamtazama Cheetah na Gichui, akimaanisha watoe wazo hapo cha kufanya.

“Sikia, yule Gichuru ameshajua mengi juu yetu, sasa tukimuacha atatoa siri polisi, halafu mission itashindikana. Hivyo tunamuua kisha tunavamia kanisa ki-ambush na kuchukua tunachokitaka” Black Cheetah aliwaeleza wanzake.

“Safi!” Bill mtu mnene alimpongeza.

Baada ya kikao hicho kifupi, walitawanyika na kuanza kazi ya kumsaka kasisi huyo.

Alfajiri ya siku iliyofuata

“Baba, mimi leo sijisikii vizuri, mwili wote unaniuma sana, naomba unisaidie kigangoni kwa misa mimi nitabaki hapa” fr Gichuru alimuomba paroko wake fr Joe Simith

“Kwa kweli fr inabidi ubaki, kwani hawa maharamia wanaweza kukukamata njiani, ubaki hapa mimi nitakwenda kigangoni”. Baada ya makubaliano hayo fr Joe alichukua gari ya mission na kuondoka zake na kumuacha Fr Gichuru akisubiri muda wa ibada saa kumi na mbili kamili asubuhi.

Fr Gichuru alivalia kanzu yake nyeusi na kofia ya kikasisi nyeusi yenye nyoya jeusi katikati, mkononi akiwa na rozali yake aliterenka ngazi taratibu ili apate muda wa kusali alfajiri hiyo kabla hajaingi katika misa. ‘Moyo wangu una huzuni kiasi cha kufa’ alijiwazia wakati amesimama kwenye ngazi za nyumba yao, kisha kwa hatua za taratibu aliteremka na kukanyaga uwanja wa kanisa hilo kongwe, ‘Baba ikiwezekana kikombe hiki kinipitie mbali,’ aliendelea kupata tafakari hii ya uchungu, hatua chache alisimama, ‘ Lakini si kwa mapenzi yangu bali yako yatimizwe.’

Subaru ya kijivu ilikuwa imesimama karibu kabisa na barabara ipitayo mbele ya kanisa hilo kubwa, hata fr Joe alipopita hapo aliiona lakini hakuitilia maanani. Nadni ya gari hiyo kulikuwa na watu watatu, awili wanaume na mmoja mwanamke. Black Cheetah aliitazama saa katika dashboard ya gari hiyo, ilikuwa tayari ni saa kumi na moja alfajiri akamwambia Gicui aliyekuwa nyuma ya usukani huo, “Twende sasa, mlinzi atafungua tu huu muda ni sawa,” kwa mwendo wa taratibu Gichui aliielekea geti kuu na alipofika getini kwa mbali aliona vivuli kama vya watu, akawasha taa katika mtindo wa full na kuwamulika, alikuwa ni sista na fr, akawasha tena taa mara kadhaa katika mtindo huo. Yule kasisi akalisogelea geti kutazama kulikoni, alifika getini na kusimama akilitazama gari hilo. Milango ikafunguliwa, Black Cheetah akatoka akiwa ndani ya koti lake jeusi na kulielekea geti, sasa uso kwa uso na fr Gichuru.

“Kwa kosa ulilolifanya la kututoroka, jua la leo si halali wewe kuliona” Black cheetah, alimueleza fr Gichuru huku akiondoa usalama wa bastola yake na kuruhusu risasi niingie katika chemba, fr Gichuru aliutazama mdomo wa bastola ile,

“Si kwa mapenzi yangu, bali yako yatimizwe” Fr Gichuru alisema mara hii kwa sauti iliyoweza kusikiwa na Black Cheetah pekee, mkono wa jambazi huyo ulikuwa ukitetemeka hata kutaka kupoteza nguvu.

“Black Cheetah, unachelewaaa!” ilikuwa sauti ya Mellina ikimstua Black Cheetah na bila ajizi vidole vyake vikapata nguvu na kufyatua trigger ya ile bastola, risasi mbili zilipenye katika kifua cha kasisi huyo na kumnyayua kabla ya kumbwaga chini chali na mifereji ya damu kuanza kuchuruzika kutoka mgongoni alaikolalia.

Kwa mwendo wa kasi ile Subaru iliondolewa mahali pale na kusababisha kelele za tairi pindi ilipoingia barabarani.

Fr Gichuru hakuwa na nafasi hata ya kuomba maji, “Yametimia, Baba mikononi mwako naiweka roho yangu” alitamka maneno hayo kwa shida huku damu nyingine zikitoka kinywani na kisha kichwa chake kikaelemea uapnde wa kushoto na kukata roho.

INSPEKTA Saitoti alikuwa akigongagonga kalamu yake mezani kwake huku akionekana wazi kuwa kichwa chake kilikuwa na mambo mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingine yalimchanganya kichwa., mara alivuta kabrasha hili mara lile lakini hakujua anachotaka kufanya kwa muda huo, akiwa katika hali hiyo aligutushwa na hodi iliyogongwa mlangoni mwake kisha mwanamama mmoja aliyevalia kiraia aliingia kwa ukakamavu na kubana miguu yote miwili kuonesha nidhamu ya kijeshi.

“Jambo afande?” Inspekta asitoti alisabahi

“Jambo!” alijibu yule mwanamke au kana anavyojullkana Sargeant Maria, “Afande natoa taarifa ya kuumia afande Otho’ katika mapano na moja kati ya majambazi tunayoyatafuta”

“Oh! Pole sana afande, nieleze kwa kina,” Inspekta Saitoti aliomba aelezwe huku akimpa ishara ya kuketi kitini sergeant Maria.

Alipokwishakueleza kinagaubaga kila kilichojiri, alitulia kitini kimya akisubiri amri ya boss wake itasema nini, mara Inspekta Saitoti alikohoa kuashiria kuuvunja ukimya ule.

“Ok! Sasa kutokana na hilo, naomba afande Otho nimuondoe kwenye operesheni hii na nikupe kijana mwingine machachri wa kukusaidia, koplo Kariithi, au we unasemaje?” alimuuliza huku akimkazia macho,

“Sina neno afande, kijana yupo kamili na anaweza kazi,” Maria alijibu kwa sauti ya ukakamavu hasa.

“Ok basi nitampa taarifa na mara moja ataungana na wewe katika hili, hakikisheni tunawatia mbaroni wauaji ili sheria ichukue mkondo wake,” sergeant Maria alisimama na kubana miguu yake sawia, “Sawa afande!” alijibu, akageuka na kutoka nje.

Inspekta Saitoti alibaki tena peke yake mle ofisini, sasa hakuwa anagongagonga ile peni tena pale mezani bali alikuwa akibofya namba za simu yake ya mezani na kuweka kile kisikilizio sikioni mwake kusubiri sauti ya upande wa pili iongee lolote.

Alipokwisha kuongea na mtu wa upande wa pili alitulia tena kitini na kufungua runinga yake ndogo iliyowekwa ofisini humo na kufuatilia habari za kimataifa. Mara mlango uligongwa na alipomkaribisha mgongaji, aliingia kijana wa makamo, mwenye kadiri ya miaka kama ishirini na minane hivi, mwenye siha nzuri ya kuvutia, aliyejengeka kimazoezi, alisimama mbele ya Inspekta kikakamavu, Inspekta Saitoti alimtazama kijana huyu, kisha akavuta motto wa meza na kutoa bahasha ya khaki akamkabidhi, na maneno machache yakafuatia ya kumpa majukumu ya afande Otho ambaye kwa kipindi hicho alikuwa hospitalini akiuguza jeraha lake. Kariithi alirudi nyuma hatua mbili na kupiga mguu chini kisha akageuka kikakamavu na kutoka nje ya ofisi ile.

˜˜˜

Sergeant Maria alikuwa akimuelekeza mambo Fulani Fulani koplo Kariithi juu ya wapi wameishia na nini cha kufanya juu ya sakata hilo la mauaji ya Kasisi.

“Ok, mi nafikiri sasa cha kufanya ni kufuatilia nyendo za hawa jamaa ili tuweze kuwatia mkononi” Kariithi alitoa ushauri.

“Ni sawa, lakini bado hatujajua adui yetu anapenda kuonekana wapi,” Maria alieleza dukuduku lake katika hilo.

“Nimekuelewa afande, hapa kuna sehemu kubwa nne za kufanya doria, Dagoreti Corner, Kawangware, Korogocho na Uthiru Kenoo, nafikiri tukifanya doria kali pande hizo tunaweza kama si kuwatia mkononi basi kupata japo harufu yao” koplo Kariithi alieleza kwa kujiamini na mkakati ukapangwa wa kufanya doria ya kimyakimya maeneo hayo yote.

Ulikuwa ni usiku wa balaa katika mitaa hiyo, hakuna aliyekamatwa kwa maana polisi hao waliwajua wanaowatafuta, hawakufanya kamatakamata kama za huku kwetu Bongo.

Uthiru Kenoo…

“Leo hii lazima tumalize kazi!” Cheetah aliwaambia wenzake huku aking’ata pande kubwa la mutura na kulishushia na tusker, akabeua na kuwatazama wenzake kwa zamu, “Maisha hayana guarantee, hasa haya yetu, Bill atatulipa pesa nyingi sana ukizingatia pesa tu aliyomlipa yule kahaba Rose ni ndefu itakuwaje kwetu sisi?”

Mellina alionekana kuwa mbali kabisa kimawazo, walipomgutusha wenzake alionekana kama mtu aliyetoka katika usingizi,

“We vipi? Mbona hauko nasi kabisa?” Wambugu alimuuliza

“Ah! Nafsi yangu inanisuta sana, hivi kwa nini tunafanya unyama huu kwa sababu ya pesa? Tumemuua kasisi wa watu bila kosa,” Mellina alionekana kusikitika sana.

“Aaa ha ha ha ha Mellina, wewe ni jambazi wa kike, muuaji ambaye hata Mungu hana muda wa kukusamehe, leo hii ujutie kifo cha mtu mmoja, mtu asiye na faida, hana watu wanaomtegemea wala nini, pesa pesa Mellina, hata Yuda Iskariote alimtoa Yesu auawe kwa vipande thelathini vya fedha, nini wewe!!!” Cheetah aliongea huku akiwa amesimama akigonga meza yake kwa ngumi, tayari pombe ilikuwa imekwishafanya kazi yake kichwani, alihema kwa nguvu na kuwatazama tena kwa zamu, “Ninawaamini sana vijana wangu, kwa kuwa Mellina ameonesha mashaka sasa nabadili program, leo hii tunaenda kuibeba hiyo Mostrance, lazima ipatikane, kwa udi na uvumba, kama jina la riwaya ya Innocent Ndayanse, leo hii ili kesho Bill atupe dolari zetu na kila mtu atawanyike kivyake, kama kukamatwa na akamatwe kivyake,” amakweli pombe mwana haramu, Cheetah alitoa bastola yake na kuifutafuta vumbi hakujali kama watu walikuwa wakimwangalia, Wambugu akainuka na kumnyang’anya ile bastola kisha kumvutia nje na kumuingiza kwenye gari, alishaona kuwa sasa Cheetah hakuwa yeye.

Mellina alikaa nyuma ya usukani na kutaka kuiondoa gari ile lakini alikuta mbele yake kuna watu wawili wamesimama wakimtazama, ‘Polisi’ alijiwazia huku akikanyaga clutch na kutumbukiza gia ya kwanza, alipoanza kukanyaga accelerator wale polisi wakatoa bastola zao tayri kwa mashambulizi,

“Shiiittt!” Mellina alikanyaga mafuta kwa nguvu na huku bado mguu haujatoka sawasawa katika clutch na kuuzungusha usukani, norinda iliyotokea hapo haikuwa ya kawaida, vumbi lilitimka usiku huo na watu walio jirani walisikika wakipiga mayoe ya woga, Cheetah na Wambugu tayri bastola mikononi wakishambulia upande ule walipo wale askari, lakini umahiri wa Mellina katika usukani uliwafanya wakose shabaha, ile Subaru iliizunguka na kuingia barabarni kisha Mellina akatumbukiza gia ya pili mara ya tatu na kuwaacha watu midomo wazi. Mwendo haukuwa wa kawaida kuelekea mjini huku baadhi ya gari ya polisi zikifuata nyuma kwa kupiga ving’ora ili kupisha njia kumbe kwa jinsi hiyo walimpa mwanya Mellina kuchanja mbuga, dakika kama tano kulikuwa na pengo kubwa kati ya polisi na Mellina.

“Weka gari pembeni,” aliamuru Cheetah kisha akafungua mlango na kuwaamuru wenzake kumfuata, wote walitoka na moja kwa moja wakaenda katika maegesho ya NAKUMATT supermarket maeneo ya Westland na kuingi kwenye Toyota Prado, kwa kutumia funguo za bandia waliiwasha ile prado na kuitoa pale maegeshoni na kuileta barabara kubwa, waliyaacha mafgari ya polisi yapite kisha wao wakaingia nyuma yao na kufuata taratibu.

“Sasa tunakwenda moja kwa moja kuchukua ile Mostrance sasa” Cheetah aliamuru na kila mmoja akajiweka sawa kwa hilo, bastola zilizoshindiliwa risasi za kutosha zilikuwa tayari mikononi na viunoni mwao.

˜˜˜

“Ah!” koplo Kariithi alitikisa kichwa kwa kuchelewa kufika eneo la tukio,

“Vipi koplo?” sergeant Maria alimuuliza huku akiweka vizuri jacket lake.

“Yaani ningewapata hawa leo, nakuhakikishia afande ungeijua shabaha yangu leo” Kariithi alimueleza huku akivuta hatua fupifupi kuwaelekea wale polisi wawili waliokuwa pale kwa doria ambao ndiyo waliwapigi redio ili wafike hapo.

“Siku yao ipo! Usiku huu halali mtu mpaka tuwatie mkononi kwa gharama yoyote ile” sergeant Maria alimueleza koplo Kariithi. Kishapo wote wakaingia garini na akabla hawajatoka eneo lile walipata taarifa kuwa gari aina ya Subaru forester iliyotumiwa na majambazi hao imeonekana maeneo ya Westaland imetelekezwa, nao wote wakaenda hapo kuiona, kama walivyoambiwa waliikuta pale imetulia.

“Koplo, tunapambana na watu makini, tujiweke vyema” Maria alimtahadaharisha Kariithi.

Wakiwa wanajiandaa kuondoka wakati huohuo polisi wakifanya mchakato wa kuiwekea mtego ile gari labda watarudi kuichukua, mara walikatishwa na kelele kutoka katika maegesho ya supermarket hiyo.

“Oooh my car my car” (Oooh gari yangu, gari yangu), Sergeant Maria alitega sikio na kushuka katika gari yao kisha akaelekea kule kwenye ile kelele, mama mmoja wa kizungu alikuwa akilia kwa uchungu kuwa gari yake imeibwa, sergeant Maria alimtuliza na kumuuliza maswali machache kisha akamchukua na kwenda nae kituo cha karibu kwa ajili ya kuanza uchunguzi, alipokwishamkabidhi kwa wahusika, akarudi garini na kumkuta Kariithi akiwa bize kusikiliza muziki uliokuwa ukipigwa ndani ya gari hiyo, aliingia na kujifungia mlango.

“Koplo, kwa vyovyote Cheetah na wenzake wameiba ile gari,”

“Nilikuwa nafikiri hivyo pia, afande huu lazima uwe usiku wa kazi” Kariithi alisisitiza.

“Endesha gari!” Maria aliagiza

“Twende wapi afande?”

“Twende tukabane karibu na kanisa kuu kwa muda kidogo tukisubiri taarifa nyingine, labda tutaokota kitu huko.” Kariithi akaitoa ile gari kujiunga na magari mengine kuelekea katikati ya mji. Ilikuwa imetimu saa nne usiku, bado foleni ilikuwa kubwa ya magari katika jiji la Nairobi.

˜˜˜

Ngumi ya hasira ilitua juu ya meza ya chuma katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya Nairobi, huku akiuma meno aliuangalia mwili wa Fr Gichuru uliolala kwenye kitanda hicho ukiwa ndani ya mfuko maalum wa plastiki.

“Bill, Bill, Billllllllll !!!!! lazima ulipe kifo hiki kwa gharama yoyote,” Melchior Ndege alijikuta akiongea peke yake mle ndani ya chumba kile kidogo cha kuhifadhia maiti.

Hali ya utulivu ilitawala nje ya eneo la jingo hilo kubwa, watu waliokaa kwa utulivu kwenye vibenchi vidogo vilivyowekwa maalumu kwa kazi hiyo. Melchior Ndege alitoka akiwa kama mtu asiyejielewa na moja kwa moja aliingia kwenye gari yake na kuliacha eneo hilo kurudi ofisini.

Aliketi na kutulia akiwa na mawazo mengi sana juu ya hili sakata, sasa aliona kuwa kazi inaanza rasmi, kumsaka Bill na genge lake, kujua ni nani yuko nyuma ya Bill katika hili.

Mlio wa simu ulimshtua Melchior mawazoni, akaitazama simu ile iliyokuwa ikipiga kelele bila kunyamaza, akainyanyua na kuiweka sikioni, hakuongea kitu bali alijaribu kusikiliza sauti ya upande wa pili, nako kulikuwa kimya, walitegeana…

….zaidi ya kusikia pumzi inayopanda na kushuka kutoka upande wa pili, melchior hakuna alichosikia kutoka kwa mpiga simu, akaitua taratibu na kuiweka mezani bila kuirudisha kwenye kitako chake na kuifanya iendelee kuwa hewani, zaidi ya hilo alibofya kitufe cha kuruhusu sauti isikike kwa nguvu ‘loud speaker’ kisha akajituliza kitini. Akishika hiki na kile juu ya meza yake mara mlango uligongwa na kufunguliwa na mgongaji aliyejitoma ndani bila kukaribishwa, hakuwa mwingine ni yule boss wake bwana Shikuku aliyeingia akiwa amefura kwa hasira ambayo ilimtisha hata Melchior, akajitupa kwenye kiti cha upande wa pili na kushusha pumzi ndefu,

“Mr Ndege, FBI wapo hapa” alimwambia Melchior ambaye alionekana kushtushwa kidogo kwa taarifa hiyo

“Oh shit, wataharibu mipango yetu” Ndege alimjibu huku akiiweka kalamu yake mezani na mkono kuuelekeza shavuni.

“Sio wataharibu, wameshaharibu,” bwana Shikuku alitamka hayo huku akitikisa kichwa, kisha akamuangalia melchior na kumwambia, “Wameshatuomba tujitoe kwenye huu mkakati ili wao wafanye kazi ya kumnasa bwana Bill, wameniuzi”

“What?!” bwana Ndege aliuliza kwa mshangao mkuu.

“Ndiyo hivyo,” Shikuku akajibu kwa mkato huku akiangalia pembeni.

“Bill hawezi kuondoka mikononi mwetu kijingajinga wakati tunajua wazi jinsi alivyoendesha mambo ya kijasusi katika Afrika Mashariki, na sasa yupo kwetu tena, kule Tanzania alitoroka hatukuweza kumtia mkononi kwa sababu hizi hizi, sasa na leo tena haiwezekani,” Melchior aliongea kwa uchungu, kisha akatulia na baadaye kumtazama boss wake, “Bill nitamtia mkononi kabla ya wao kufanikisha hilo” alimwambia boss wake huku akifungafunga vitabu vyake, akasita kidogo na kusema, “Lazima tujue nyuma ya mauaji ya kasisi kuna nini, mpaka Bill ahusike, tusipompata Bill hatutaweza kutatua juu ya kifo hiki cha utata, mimi nina mwanzo wa mkasa na Bill ana hatima ya mkasa, lazima nimpate mimi na siyo FBI”

˜˜˜

5

Dar es salaam – Tanzania

MVUA kubwa iliendelea kunyesha katikati ya jiji la Dar es salaam, maji yalizijaza barabar zote na kufanya ugumu wa watembea kwa miguu kuonekana dhahiri, akina mama viatu mkono wakizikunja nguo zao kwa juu huku mifuko ya plastiki ikiwa imefunika vichwa vyao ili kuokoa nywele za gharama zisiharibike, magari nayo yalipita shida kwa namna moja au nyingine, yakitumbukia kwenye mashimo ya liyojitengeneza kutokana na mvua hiyo, basi jiji lote lilikuwa vururuvururu. Kila mtu alionekana kuchukia hali ile ambayo serikali inaifumbia macho mara zote, shida kubwa ikawa kwa wale waishio mabondeni waliokuwa wakifukuzwa kila siku tangu enzi za mheshimiwa Makamba lakini waling’ang’ana utafikiri walizaliwa hapo, huyu akisonya, yule akimkashifu kiongozi Fulani wa chama na serikali.

“Bora tuwachague wapinzani mwaka ujao” mwingine alisikika akisema hayo huku akiwa juu ya moarobaini uliokuwa ndani ya maji nusu nzima. Ilhali anasahau kuwa mvua hizo ni mabadiliko ya tabia nchi ambayo mimi na wewe ndio visababishi.

“Ila mi Mabwepande ndio siendi” alijibiwa na yule aliyekuwa juu ya paa lanyumba iliyochoka ambayo kwayo uhai wake ulifika tamati, alisahau kabisa kuwa haikomoi serikali bali anawaumiza watoto wake ambao hakuhusika katika kuchagua eneo la kuishi.

Wakati upande mwingine watu wakiwa wamejazana katika daraja kubwa la Tabata Matumbi wakivumilia harufu kali ambayo ilisemekana ni ya mwili wa binadamu uliokwama katika maji yam to Msimbazi huku jeshi la polisi likisaidi kazi hiyo, wengine walikuwa wakichanganya vichwa, akili na mawazo yao vikiwa tofauti na matakwa ya mioyo yao.

Ndani ya jengo la JM MALL, ghorofa ya saba mlango namba 705 ni watu wawili tu mwanamke na mwanaume walikuwa wameketi wakitazamana mmoja akishindwa kuamua na mwingine akishindwa kushauri nini cha kuamua. Wakiwa bado katika kushangaana wawili hawa mara mlango ulifunguliwa na bibi mmoja wa makamo ambaye nywele zake zilishahitilafiana na weusi wake wa asili na kuubeba weupe ambao wengi hupenda kuuita mvi, aliingia moja kwa moja na kuketi kwenye kiti kikubwa ambacho kilikuwa pembeni kidogo ya meza ile safi iliyozungukwa na mapambo murua ambayo ukiketi basi yatakupa burudani ya macho na kuondosha ile ambayo muandishi wa kitabu cha SHIDA, Ndyanao Balisidya aliita ‘kiwi cha macho’.

“Karibu Madam S” Kamanda Amata alisimama na kupeana mkono na mwanamama huyu aliyebobea kwenye kazi za kikachero tangu usichana wake.

“Nimekaribia Kamanda” akajibu huku akijiweka vizuri pale kochini ambapo aliweza kuonana na mrembo aliyemkuta ofisini humo. Mara baada ya kujiweka sawa alimtzama Amata na kumpa bahasha moja ya khaki ambayo juu yake imeandikwa maandishi yanayoitambulisha kuwa ni mali ya serikali, akaitupia mezani na Kamanda Amata akaichukua na kuifungua, baada ya kuisoma akaitupia mezani,

“Nairobi tena! Kuna nini madam?” Kamanda Amata aliuliza

“Mauaji ya Kasisi, jasusi Bill Van Getgand yuko Nairobi, FBI na taasisi nyingine za kikachero zimetuma watu wao kumnasa, lakini sifikiri kama ni vyema wakamchukua ndani ya ardhi yetu wenyewe, huyu ameshatekeleza mambo Fulani ya kijasusi katika nchi yetu na zingine za Afrika Mashariki” madam S alikuwa akiongea bila mapumziko akionekana wazi amehamanika kwa hilo.

“Madam, mi niko safarini,” kamanda Amata alitoka katika meza yake na kuchukua vifaa vyake vichache vya kiofisi, akamwita Gina na kumpa maagizo Fulani Fulani ya kiofisi kisha akatoka na madam S, boss wake wa miaka mingi na kuondoka zake.

˜˜˜

BOEING 737 ilishuka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Ilikuwa alasiri tulivu uwanjani hapo palipoonekana kuwa na ulinzi mkali wa polisi na ule wa vyombo binafsi vya ulinzi.

Baada ya itifaki zote kukamilika, kamanda Amata alitoka nje na kukamata tax moja kabla ya kuamua wapi anataka kwenda mchana huo. Alijiweka katika saiti ya nyuma na kumwambia dereva ampeleke katika hoteli kubwa ya nyota tano katikati ya jiji hilo la Nairobi.

Kamanda Amata alifika katika Hotel Intercontinental, katika mtaa wa Posta na kuweka kambi yake hapo akiwa naa kazi moja tu aliyotumwa na serikali yake ama kumkamata Bill ili ajibu kwa yale aliyoyafanya siku za nyuma au uhai wake ubaki Afrika Mashariki na mwili wake urudi kwao, ilikuwa ni moja kati ya hayo lililotakiwa kutekelezwa. Amata alitupia begi lake kitandani na kuchukua kifaa chake maalum kilichoweza kung’amua kama humo ndani kuna aina yoyote ya mlipuko au chombo chochote kitakachoweza kuhatarisha maisha yake, aliporidhika na usalama wake, akalisogelea dirisha kubwa na kuvuta kidogo pazia lake na kutupa macho yake nje upande wa chini ambako pilikapilika za wakazi wa Nairobi waliokuwa wakirudi majumbani kutokea makazini zilikuwa kubwa, kana kwamba hakuridhika na kile alichokua akikitazama alivuta kibegi chake na kutoa kiona mbali na kukisogeza karibu na macho yake, naam kile alichokiangali kilikuwa kikionekana kwa uzuri wa hali ya juu, vijana waliokuwa wakijidunga madawa ya kulevya katika moja ya mitaa hiyo ulioonekana wazi kuwa haukuwa ukitumika na wapita njia, alitazama kwa makini vijana wale walivyojidunga mpaka kuanza kusinzia pale chini, Amata alitikisa kichwa kwa masikitiko, ‘Nguvu kazi ya taifa inatoweka’. Akiwa katika kutafakari hayo mara alisikia ving’ora vya polisi na kufuatiwa na gari mbili zilizopita kwa kasi kuelekea upande wa pili wa eneo hilo, ‘Shughuli za kiusalama hizo’, alijiwazia kwa mara nyingine na kutoka pale dirishani kisha kuketi katika kochi moja lililopo pale chumbani. ‘Bill Van Getgand, umekuja tena, sasa hakika hutoponyoka kwenye mikono hii,’ akaivuta laptop yake na kuanza kuperuzi habari mbalimbali za jasusi huyo, akirejea hasa yale matukio yaliyofanywa na mtu huyu pale Dar es salaam …

Miaka mitano iliyopita

Kilimanjaro Hotel

Kamanda Amata aliuangalia mwili usiokuwa na uhai uliokuwa ukielea katika bwawa la kuogelea la hoteli hiyo kubwa ya kimataifa iliyopo pembezozi mwa bahari ya Hindi. Watu kadhaa walizunguka eneo hilo wote wakiwa wametokwa na hamu ya kujiburudisha kwa maji hayo ambayo sasa yalikuwa mekundu kwa damu ya mtu huyo aliyeonekana kuwa na asili ya America. Akiwa amepiga goti moja pale katika ukingo wa bwawa hilo, kamanda Amata aliinua kichwa chake na kutazama uelekeo ambao labda muuaji alikuwapo, kwa maana mtu huyo aliuawa kwa risasi iliyotoka katika bunduki aina ya Sniper Rifle ya Kimarekani, naam macho yake yalitua mahali sawia, dirisha moja lililokuwa katikati kama ghorofa ya nane hivi katika jingo lililokuwa na benki ya Meridian Biao enzi hizo. Alipotuiliza macho yake alishuhudia pazia la dirisha hilo likifungwa ghafla kana kwamba aliyekuwa hapo dirishani alikuwa akimtazama Amata pia. Ili asimpoteze maboya mtu huyo Kamanda Amata kwa kutumia simu yake maalum iliyounganishwa na saa ya mkononi alipeleka ujumbe wa sauti kwa Madam S aliyekuwa upande wa pili wa jingo hilo, nae bila kusita alituma kikosi cha watu wanne kwenda kufanya uchunguzi katika ghorofa hiyo.

Hisia za Amata hazikuwa bure, jasusi Bill Van Getgand lilikamilisha kazi yake kupitia ofisi ya mtu Fulani ndani ya jingo hilo kwa kutumia bunduki ya Sniper Rifle, wakati vijana wale wakigawana majukumu mmoja apande kwa lift, mwingine kwa ngazi ya kawaida na wengine wabaki nje kutazama kinachoendelea, ndipo yule aliyepanda kwa ngazi alipopishana na Bill aliyekuwa akishuka huku akitanguliwa na mwanadada mmoja mwenye umbo dogo aliyekuwa amebeba koba kubwa la kuhifadhia guitar lakini akiwa kwenye hali ya kutojiamini, yule afisa usalama alitulia kidogo na kuwaangali huku akipishana nao na mara hiyo akatoa taarifa kwa walio nje kumwafuatilia watu hao bila kuwapoteza.

Kwa uchunguzi wa muda mfupi uliofanyika katika chumba kilekile ambacho Amata alikihisi tangu mwanzo liliokotwa ganda moja la risasi ambayo ni ile iliyotumika kumuua bwana yule.

Kamnda Amata alilitazama ganda lile na kutikisa kichwa kukubali hisia zake.

“Mnasema mmeweka watu wawafuatilie hao mnaowahisi?” aliwauliza wale vijana chipukizi katika kazi hiyo.

“Ndiyo na tunatumaini bado wanawafuatilia” alijibu mmoja wao. Kamanda Amata akainua simu yake ya upepo na kuwauliza vijana wale waliopewa kazi,

“Ndiyo, tupo hapa Red Carpet Upanga, wameingia ndani na bado hawajatoka, gari yao ipo hapa nje inawasubiri,” jibu lilimridhisha Amata, aliingia garini na mara moja kuelekea Upanga, akawakuta vijana wake wakiwa wametega pa si kuwaona watu hao, masaa mawili yalikuwa yamepita, Amata aliteremka na kuzunguka lile jingo la ghorofa mbili na alipofika nyuma yake alitikisa kichwa kwa kuugundua upumbavu wa vijana hao waliobaki ndani ya gari wakati nyuma ya jingo kuna ngazi zinazoweza kumtoa mtu yoyote aliye ndani ya jingo hilo, akarudi mpaka mbele na kuwapa taarifa hiyo ambayo iliwafanya wafadahaike sana kwa ujinga walioufanya.

Hakika Bill Van Getgand alikuwa ametokea upande wa pili pamoja na yule mwanadada na kuchukua tax iliyokuwa imeegeshwa huko nyuma na kuondoka zao mpaka uwanja wa ndege ambako walichukua ndege na kuelekea Nairobi.

Baada ya kumsukasuka yule dereva wa tax aliyewabeba Bill na yule mwanadada hakuna jibu la maana walilopata zaidi ya kubaki na lile koba la gitaa ambalo ndani yake kulikuwa na bunduki kubwa iliyotumika kwa mauaji yale lakini hakukuwa na guitar, baada ya uchunguzi wa hali ya juu kufanyika uliohusisha vyombo mbalimbali vya kiintelijensia ilionekana Bill amehusika na mauaji hayo na si sehemu moja tu basil maeneo mbalimbali duniani, nah ii iliifanya nchi yetu kuingia kwenye matatizo ya kimahusiano na nchi husika ya mrehemu yule kwani iligundulika alikuwa ni mtu muhimu serikalini ambaye alikuja kwa shughuli za kiserikali na kufikia hapo hoteli ya Kilimanjaro.

Rejea Nairobi Intercontinental Hotel…

Kamanda Amata aliishusha picha ndogo ya Bill aliyokuwa akitumbulia macho na kuirudisha kwenye kikoba maalum. Mara kengele ya mlango wa chumba chake ikagongwa, akanyanyuka taratibu na kuuendea mlango huo huku bastola yake ndogo ikiwa mkononi mwake, akiwa kaificha kwa nyuma alimruhusu mtu huyo kuufungua mlango. Mwanadada mwembamba, mrefu wa wastani aliupenyeza mwili wake ndani ya chumba cha Amata, Amata alimeza mate ya uchu hasa alipokutana macho na paja mwororo la mwanadada huyo ambalo lilibaki wazi baada ya sketi yake iliyofungwa kwa vifungo upande wa kulia kulipa nafasi paja hilo kuonekana, kiuno chake kidogo kilibeba kajiumbo ka wastani, si kanene sana, lakini kenye mvuto mahsusi kwa mwanaume yoyote rijali, mikono ya Amata ilipoteza nguvu na kuiruhusu ile bastola yake kurudi mfukoni bila kutarajia, macho yake yalikuwa yakitalii kifua cha mwanadada huyo ambapo blauzi aliyoivaa yenye vifungo vichache mbele iliruhusu nusu ya titi lake ambalo halikuhifadhiwa kwa sidiria kuonekana na kumfanya kamanda kuinuka kutoka pale alipoketi na kumjongelea mwanadada huyu, kabla hajamfikia …

Kabla hajamfikia, yule msichana aliweka magazeti aliyokuwa nayo mkononi juu ya meza ya kioo iliyokuwa hapo ndani.

“Wakati unasubiri kuonana na mwenyeji wako, usome magazeti haya!” sauti tamu ya yule dada iliyapenya masikio ya Kamanda Amata. Baada ya kuyaweka magazeti hayo pale mezani, aligeuka na kutoka nje huku macho ya Amata yakimsindikiza kwa kila hatua aliyoivuta, alitoka na kuurudishia mlango nyuma yake. Amata alibaki kapigwa na bumbuwazi, ‘Mwenyeji, mwenyeji wangu,’ alijiuliaza, kengele za hatari zikalia kichwani mwake, akainama kuchukua yale magazeti lakini kabla hajayachukua kutoka pale mezani, akasita, akatazama saa yake, muda ulikuwa umekwenda sana, akaachana nay ale magazeti na kujiandaa kwenda kuoga.

Dakika chache zilimpita akiwa maliwato na alipomaliza, aakaufungua mlango, akasimama ghafla, akatupa macho yake juu ya kitanda kikubwa kilichopo katika chumba hicho hakuamini anachokiona, akafikicha macho kana kwamba anachokiona ni kiini macho.

“Come to me boy..” sauti ya msichana yule aliyekuja na magazeti ilimfikia tena Amata masikioni, akamtazama kwa makini msichana huyu mrembo aliyejilaza kitandani na kujifunika shuka mpaka maeneo ya kifuani na kuishika kwa mkono mmoja huku mwingine ukifanya ishara ya kumuita Amata kitandani. Lilikuwa ni jicho baya na kali la Amata lililomfanya yule msichana kuurudisha mkono wake chini na kupatwa na sura ya woga. Amata akautazama mlango ambao yeye aliufunga lakini alishangaa huyu msichana kapita vipi mpaka kujitoma ndani ya chumba hicho, kisha akarudisha macho yake pale kitandani, “Toka!” alimuamuru yule msichana, lakini hakuonekana kuitii amri hiyo, “Mmmm boy, kwa nini unanifukuza wakati nimekuja kukuburudisha?” alianza kutumia silaha ya sauti yake kumlainisha Amata, “Tokaaaa!” Amata aling’aka kwa hasira huku akimfuata yule msichana pale kitandani, yule msichana akanyanyuka haraka na kukiacha kitanda kile, akasimama pembeni akiwa uchi wa mnyama, akachukua nguo zake na kuzivaa kisha akaufungua mlango na kutoka nje. Kamanda Amata akakiendea kioo cha ukutani na kujitazama kisha akaanza kuvaa suti yake nadhifu aliyoichagua kwa siku hiyo. Akiwa pale kiooni alihisi mlango ukifunguliwa kwa mara nyingine, kabla hajageuka aksikia sauti kutoka nyuma yake, “Tulia hivyohivyo, ukijifanya mjuzi, tunaondoka na pumzi yako,” Amata akaona sasa mambo si mambo, akaendelea kujiandaa huku mtutu wa bastola yenye kiwambo cha sauti ikimtazama.

“Ok, umependeza, sasa utaondoka na sisi, bwana Bill anataka kukukona usiku huu kwa maana hana uhakika kama jua la kesho utaliona,” yule jamaa alimwambia Amata huku akimruhusu kutangulia mlangoni ambapo palikuwa na watu wengine wawili, hamna ujanja. Kamanda Amata aliongoza taratibu nje ya chumba kile na kuifikia korido ndefu, mbele yake kulikuwa na mtu mmoja, nyuma yake kulikuwa na mwingine yule mwenye bastola ambayo sasa alikuwa ameifunika kwa koti lake la suti kiasi kwamba kwa mtu mwingine hasingeweza kujua kama mkoni hapo kuna mguu wa kuku. Waliingi ndani ya lifti kwa mtindo huo huo, hakuna aliyeongea kati yao, wakateremka mpaka chini na kuongoza kwenye gari moja la kifahari aina ya Cardilac, gari ya kifahari na gharama ya hali ya juu, Amata alitangulizwa kuingia ndani kiti cha nyuma kisha wawili kati ya wale watatu wakaingia mmoja huku na mwingine kule, yule mwenye bastola akiwa mmoja wao, mwingine wa tatu akaingia siti ya mbele.

“Karibu sana Amata,” ilikuwa sauti ile tamu ya mrembo aliyeongea huku akigeuka nyuma na kumtolea tabasamu pana Kamanda. Taratibu waliyaacha maegesho ya hotele ile na kutokomea mjini, barabara chache na foleni za hapa na pale katika jiji hilo la Nairobi ziliwafanya wachukue muda kidogo kufika wanapopakusudia, mwanadada yule aliyekuwa akiendesha gari hiyo kwa umahiri mkubwa alikatiza kwatika vichochoro mbalimbali na kutimiza kusudio lake.

Mguu wa kulia wa mwanadada yule ulihama kutoka katika pedeli ya mafuta na kukanyaga ile ya breki huku mikono yake ikiuzungusha usukani kwa kidole kimoja kuingia katika maegesho ya hoteli ya Safari Park.

Wote wakashuka na yule mwanadada alitangulia kuelekea ndani ya hotel ile akifuatiwa na wale wengine wakati Kamanda Amata alikuwa katikati ya wote, wakaingia na kupita mapokezi kisha kuingia upande mwingine na kuchukua lifti kushuka ghorofa moja chini, walipotoka walikaribishwa na maandishi makubwa ya kuwakawaka yaliyosomeka, Safari Park Casino, casino ya kisasa iliyojengwa chini ya ardhi katika hotel hiyo, mlangoni walisimama wazaume wawili waliovalia suti nyeusi na kuonekana wameshiba kimazoezi, walikuwa wamesimama mithili ya sanamu ya bismini.

“Clean!” mmoja wa wale waliomtangulia Amata alitamka neon hilo akimaanisha hakuna shida, mara mlango wa kioo ukafunguka na wote wakaingia ndani. Taa za rangi mbali mbali ziliujaza ukumbi huo ambao ulionekana kuwa na shughuli nyingi, wanaocheza kamali walikuwapo, wacheza uchi nao walilipamba jukwaa wakicheza miziki yao michafu, waliokuwa wakinyonyana ndimi hadharani nao hawakukosa, wale waliokana jinsia zo hawakuwa mbali, ilimradi tu dhambi zote zilihifadhiwa ndani ya casino hilo.

“Huku tafadhali,” Amata alielekezwa ngazi ndefu zilizokuwa zikipanda juu, akazifuata bila ubishi mpaka juu, pale wale wasindikizaji wakamuacha na kupokelewa na wengine kisha akaingizwa ndani ya chumba safi na nadhifu kilichoja samani za gharama ya hali ya juu, mbele yake kulikuwa na mtu mnene amaye alisimama na kuja kumlaki kwa bashasha, “Oooh Kamnda Amata, karibu sana, nisingefurahi kama nisingeonana nawe leo hii, karibu sana,” Bill alimkaribisha Amata na kumuongoza kitini, kisha akampatia glass yenye kinywaji na kuketi katika mtindo wa kutazamana.

˜˜˜

Akiwa kwa mwendo wa miguu huku akipiga mruzi usiku huo, Melchior Ndege alikuwa akipita mbele ya hotel hiyo ya Safari Park, mara akapitwa na gari moja ya kupendeza inayovutia macho, akasimama kuitazama gari ile, Cardillac ya bluu nyeusi, iliyokwenda na kuegeshwa kwa utulivu. Lakini alipata mshtuko baada ya kuwaona wale walioshuka kutoka garini, aliwatazama kwa makini na kuoamua kubadili uelekeo wa safari yake. Melchior aliyaamini macho yake yaliyomwambia kuwa umuonaye ndiye Kamanda Amata, ‘Shiiit, amefika lini?’ alijiuliza na kusukuti kwa sekunde chache kabla kuruhusu miguu yake kuamriwa na ubongo juu ya lile linalopaswa kutendwa kwa wakati huo. Alipotazama vizuri, kwa macho yake ya kipelelezi akajua wazi kuwa Kamanda alikuwa kwenye hatari, akavuka kijibarabara kidogo na kuelekea mlango mkubwa wa hotel ile kisha akaingia ndani, alipofika mapokezi hakutaka kupoteza muda kwani aliwaona wapi wameingilia, akafuata, wakati wao wakifunga mlango wa lifti kuteremka chini yeye akazifuata ngazi zinazoelekea hukohuko chini. Alizuiliwa mlangoni na kupekuliwa, “Haturuhusu kuingia na silaha, weak pale unapotoka utaichukua.” Melchior alisogea kwenye meza ndogo ambayo ilikaliwa na mwanadada mrembo akaichukua bastola ya Melchior na kumpatia kadi maalum ya kumbukumbu. Akaelekea kaunta na kuketi juu ya kiti kimoja kirefu mbele ya kaunta hiyo. Akiwa anakunywa kinywaji chake taratibu huku macho yake akiwa kayaongoa kule wlikopelekwa Kamanda Amata, ambapo palitenganishwa na ukumbi mkubwa kwa vioo maalum vinavyoruhusu mtu wa ndani kuweza kuona kinachoendelea ukumbini lakini yule wa ukumbini asiweze kujua nini kinaendendele ndani ya chumba kile. Melchior akatoa miwani yake maalumu na kuipachika usoni, miwani hii ilikuwa na madini ambayo yaliweza kupenya kwenye kioo cha aina yoyote pia yaliweza kukuruhusu kuona mtu kama amebeba silaha au vipi, maana iliruhusu kuona vitu vigumu tu vilivyo mwilini mwa mtu. Alimuona Kamnda Amata akiwa na Bill wakizungumza, lakini hakuweza kujua wanazungumza nini, aliwatazama walinzi wa mlango wakuingia kule juu aliwaona wakiwa na bastola mbili kila mmoja, kisha akawatazama wafanyakazi wa casino hiyo na kuona kila mmoja alivyoipachika silaha yake, kisha akayarudisha macho yake na kuyatuliza kule aliko Kamanda Amata na kuendelea kuona kinachojiri, huku akiendelea kunywa kinywaji chake. Mara alihisi, akipapaswa kwa nyuma maeneo ya kiunoni, akageuka na kukutana macho na mwanamke mshumami, aliyejiremba akarembeka, yule mwanamka aliyeonekana ana kila dalili ya ulevi machoni mwake alizunguka na kusimama mbela ya Melchior, akamrembulia macho, Melchior hakuonesha hata kumjali kwani yeye alitaka kujua tu nini kitatokea kule ndani, “Mwanamke unataka nini? Kama kinywaji chukua uende, mi sihitaji mwanamke saa hii,” Melchior alimwambia yule mwanamke, akamnunulia kinywaji kisha kwa akapewa shukrani ya sonyo kali na refu, “Go fish!” yule mwanamke alimwambia Melchior.

˜˜˜

“Bado mnanifuata Kamanda!” Bill alimwambia Amata huku akimimina kinywaji katika glass yake.

“Kwanza nashangaa kukuona huku, umekuja kufanya nini?” Amata alimuuliza Bill, cheko kali lilimtoka mpaka walinzi wake waligeuka kutazama ndani.

“Kamanda Amata, mimi si motto mdogo au punguani, najua ninachofanya na ninajua kila anayeingia katia wigo wangu popote pale katika pepo zote nne za dunia,” Bill aliongea kwa kujiamini, “Nina macho Kamanda, siyo haya mawili, mengi tu, na nilijuwa kuwa utakuja, maana una kiu na mimi, lakini ujue hata mimi nina kiu na wewe, umeshaniharibia mambo mengi sana,” akapiga fuinda moja kinywaji chote kikaishia tumboni mwake, akabeua kwa shibe ya kinywaji.

“Bill Van Getgand, unajua unachokizungumza? Nimekuja Nairobi, nashangaa naambiwa wewe unanihitaji, nisingeshindwa kuwararua hawa nyau wako hata kama wangekuwa hamsini, lakini kwa heshima yako nikawaacha na kuwatii kwa kuwa umeniita, na ungependa kuniona kabla ya jua la kesho kwa kuwa unajua kuwa jua la kesho sitaliona, ok, niambie ulichotaka kuniambia, unataka kunipa deal?” Kamanda Amata aliuliza.

“Oh, Kamanda, mi nipo hapa takribani wiki mbili sasa, nimekuja kibiashara, lakini nilijuwa safari yako ya kuja hapa Nairobi, nikajua wazi kuwa wewe ni mgeni wangu, ndo maana nikakukaribisha uje tustarehe, lakini nataka uniambie umekuja kufanya nini hapa Nairobi,” Bill alihoji kijanja.

“Bill, maswala yangu ya kikazi siwezi kukwambia wewe kuwa nimekuja kufanya nini, kama hilo ndilo uliloniitia basi hutopata jibu,”

“Hivi unajua kuwa upo mikononi mwangu?” Bill aliuliza

“Hata kama, lakini huwezi kunilazimisha nikwambie nimekuja kufanya nini,”

Bill akachomoa bastola yake na kumnyooshea Amata, “Utaniambia tu, maana hata nikikuua hapa hakuna atakayejua kama umekufa zaidi ya mimi na wewe mwenyewe,”

“Sitishiki na hiyo bastola ya Kirussi Bill,” Amata alijibu kijeuri, lakini kabla hajakaa vizuri, bastola ya Bill ikafyatuliwa, risasi ikapenye katikati ya paja na paja la Amata, ile sofa ikatimua vinyoya kidogo, Amata alitetemeak ka hofu, kijasho chembachemba kikamtiririka, akaona kuwa kumbe hapo hakuna usalama wala mzaha, hakuna urafiki kama upo basi ni wa mashaka.

“Usifikiri nakutania, nataka unieleze lile lililokuleta, na ukijifanya mjanja nakuua,” Bill aliongea huku akimlenga na ile bastola yake iliyoonekana wazi iko tayari muda wowote kufanya itakachoamuliwa, kabla hajajaibu, Bill alifyatua risasi kadhaa, moja katikati ya mapaja ya Amata, ya pili upande wake wa kushoto nay a tatau upande wa kulia, hali ile ilimfanya Amata aweweseke na kushindwa kujua atfanye nini, alibaki kutetemeka na kulowa jasho mwili mzima, akabana meno kwa hasira, “Nimekuja kukufuata wewe hayawani, na nakupa muda mchache tu utakuwa mikononi mwangu, Bill, ndipo dunia itakapojua kuwa roho moja dhalimu imeondoka duniani.”

“Aaaaaaa ha ha ha ha ha!” Cheko la Bill lilipasua anga la chumba kile, “Kamanda Amata, Tanzania Secret Agency, hapa mmefika, nitawaacha hapa na mi nitaondoka na kile kilichonileta. Kama hauamini hujiulizi nimejuaje kuwa huko hapa! Ujue kuwa muda wowote nitaitwaa roho yako kabla ya jua la asubuhi inayofuata.” Bill akamalaiza risala yake na kugugumia tena glass nyingine ya kinywaji kikali, “Nimefurahi kukuona!” alimalizia na kuichukua fimbo yake ya kutembelea kisha kuondoka eneo lile.

“Tutaonana tena soon,” Amata alijibu kijeuri na kunyanyuka kuelekea mlango, kabla hajatoka mlangoni alisimama na kugeuka nyuma akagongana macho na Bill, wakatazamana, “Siku yetu inakuja,” alimwambia na mara wale walinzi wakamvuta kumtoa katika mlango ule alioutumia kuingilia na kenye ngazi alikuwana na yule mwanadada aliyemjia chumbani akiwa ameweka pozi akitazama yanayoendelea ukumbini mle, wakatazamana kwa sekunde, “Unahitaji lifti yangu?” yule mwanadada alimuuliza Amata huku tayari akiongozana nae kumsindikiza, mara simu ya yule mwanadada ikaita, “Yes Boss…” aliitika, sauti ya upande wa pili ilisikika vizuri masikioni mwa Amata japo ilikuwa ndogo, “Nakupa usiku huu tu ukamstareheshe Kamanda, maana ana msongo wa mawazo, kisha urudi kabla jua alijachomoza,”

“Sawa boss, umesomeka,” alijibu kisha akamwangalia Amata, “Leo mimi na wewe mpaka kuchee, boss ameruhusu,” kisha akamshika mkono Amata na kujichnganya nae katikati ya watu ndani ya casino ile…

˜˜˜

Nyimbo za masifu ya jioni zilikuwa zikirindima katika masikio ya walio jirani na eneo hilo la kanisa la Holy Family, masista waliokuwa kanisani mida hiyo walikuwa wakimalizia sala zao za jioni kabla ya kwenda kulala, kusubiri siku inayofuatia, ikiwa ni siku chache tu tangua mazishi ya Fr Gichuru yamalizike, bado mioyo yao ilikuwa imejawa na huzuni ukizingatia kwao kasisi huyo alikuwa ni mtu wa pekee sana, mwenye karama ya uponyaji ya hali ya juu, mpole, mcheshi, mwenye upendo na mcha Mungu.

Ibada ilimalizika na watawa hao wa kike walianza kutoka kuelekea nyumbani kwao, nyumba iliyo umbali wa kama mita mia mbili kutoka kanisa hilo, taa za nje zenye mwanga wa njano zilipendezesha eneo hilo, maua na miti michache ilifanya kabaridi kawe kakali kiasi. Masista wote walimalizika isipokuwa sista Rose ambaye alikuwa akimalizia kupanga vitu vya ibada itakayofuatia, kisha afunge sakristia. Haikumchukua muda alimaliza na kujianda kutoka ndani ya jengo hilo ili akaungane na wenzake. Alipoukaribia mlango tu alijikuta akibanwa na mkono wenye nguvu, uliombana barabara katika shingo yake hata akajikuta anakosa pumzi na mwili wake kukosa nguvu, mkono ule ulilegezwa kidogo na kumruhusu sista Rose kuweza kufurukuta kidogo, akataka kupiga kelele lakini alibadili mawazo ghafla baada ya kukutana na bisu kubwa na kali lililoshikwa na mkono wa mwanamke, Mellina alimkazia macho mwanamke mwenzake kana kwamba anamwangalia kuku au sungura.

“Monstrance! Onesha haraka iliko,” ilikuwa sauti ya Mellina ikimtoka huku mkononi bado kalishikilia lile jisu lake tena akiwa kalinyooshea kwa sista Rose. Ilikuwa ni wakati mgumu sana kwa mtawa yule wa kike, hakuwa na ujanja, hatari zote zilimkabiri, “Tuoneshe ilipo monstrance, tunaitaka monstrance sasa hivi, ukileta ujuaji nakutumbua na hili bisu,” Mellina alimwambia Sista Rose huku akiwa bisu lake kaliegesha nchaye katika ziwa moja la mtawa yule aliyekuwa akitetemeka kwa hofu kuu huku akilisukuma kama anayetaka kutoboa.

“Utaonesha au tukumalize kama yule kasisi wenu? Maana na ye alikuwa mbishi kama wewe” Cheetah alimuuliza kutoka nyuma yake, ndipo yule sista akajua kuwa aliyemkaba alikuwa ni mwanaume. “Ni ni nitawaonesha!” alijibu yule sista. Kisha wote kwa pamoja wakaongozana kuelekea milango mingine iliyotengenezwa vizuri kabisa ndani ya vyumba hivo vya kanisa hilo kubwa. Baada ya kupita milango kadhaa mara waliteremka ngazi kuelekea chini na huko walikuta stoo kubwa lakininzuri yenye vitu vingi tena vya thamani kubwa, sista Rose akawaonesha kabati moja kubwa lililofungwa ukutani, Mellina akaliendea na kufungua milango yake, “Waoh!” alijisemea kwa sauti ambayo kila mmoja alisiikia. “Nini Mellina?” Cheetah aliuliza, alipokaza macho yake alishuhudia monstrance kubwa ya dhahabu safi ikiwa imetulia kabatini, akamuacha yule mtawa na kuliendea kabati akainyanyua ile monstrance kwa umakini wa hali ya juu na kuiweka mikononi mwake, kisha kwenye begi walilokuja nalo maalumu kwa kazi hiyo. Sista Rose alikuwa akitetemeka sana akiangalia walivyokuwa wanaichuku bila heshima yoyote kwa chombo hicho kitakatifu.

“Tafadhali muiache hiyo monstrance,” sista Rose aliwasihi Cheetah na Mellina.

“Acha ujinga wako,” alijibiwa na mellina huku akipata pigo moja la ubapa wa kile kisu kikubwa. Sista Rose akabaki kimya huku machozi yakimtoka baada ya pigo lile, walipohakikisha wameiweka sawa katika begi lile la ngozi, Cheetah akalibeba na kumtazama sista Rose, akacheka cheko la dharau, “Kazi yetu imekwisha, kwa heri msalimie paroko,” Cheetah alimwambia sista Rose huku akimpita na kuuelekea mlango waliouingilia. Pigo moja la judo lilitua mwilini mwa sista Rose, akapepesuka, kabla hajajitambua, mellina akampa pigo lingine lililompoteza akili na kumbwaga chini kama mzigo, kisha guu nene la Mellina lilikanyaga koromeo la sista yule kwa sekunde kadhaa likimkandamiza chini na kumfanya kurusharusha miguu na mikono huku na kule na kuzimika. Ilikuwa tabu kuujua mlango waliongilia, kila walipoufungua huu walijikuta eneo lingine kabisa, walipojaribu huu hali ilikuwa ileile, Cheetah alionekana kuchanganyikiwa maana alipoingia aliona milango michache lakini sasa anaona milango mingi kuliko ile ya kwanza, iliwachukua dakika nyingi kuutafuta mlango ule bila mafanikio.

˜˜˜

Melchior Ndege, aliendelea kupepesa macho yake maangavu ndani ya casino lile lililosheheni watu wa kila aina, muda ulivyozidi kwenda ndivyo watu walivyoongezeka ndani yake, alihakikisha hampotezi Amata machoni pake, na liona wazi jinsi alivyokuwa amegandwa na mwanadada yule. Melchior alijaribu kuvuta kumbukumbu ni wapi amekwisha wahi kumuona yule mwanadada lakini jibu hakulipata kirahisi japokuwa sura ilikuwa ikimjia.

Alimuona Kamanda Amata akiwa anakunywa kinyaji kikali huku mwanamke yule akiwa pembeni yake na akionekana kumhamasisha, mara amsike kiunoni mara ambusu mara ampapase hapa na pale, kisha aliwaona wakikokotana kutoka nje ya casino ile.

Melchior alishusha glass yake taratibu na kuiweka katia meza ya kaunta kisha akateremka kutoka katika kile kiti kirefu na kuuendea mlango wa casino kutoka nje, akachukua bastola zake pale mlangoni nakuiendea lift iliyompandisha hadi juu na kutoka mlango mkubwa wa hoteli. Katika maegesho ya magari alimuona Amata akiwa na yule mwanamke, sasa ilionekana wazi kuwa mapenzi yanachukua nafasi yake, akajifanya anapiga simu, ili kupoteza muda ajue kitachoendelea. Muda si mrefu, ikasimama gari pembeni yao, Jeep Cherokee ya kibuluu hivi, yule mwanamke akamvutia ndani Amata na gari ile ikatoweka. Melchior alitazama hapa na pale na kuona gari nyingi zilizokuwa zimeegeshwa na wamiliki wake walikuwa wakila starehe ndani ya hoteli ile, akaiendea moja wapo, Toyota Celica, akatoa funguo yake, wengi huiita Malaya, funguo inayoweza kufungua takribani lock zaidi elfu kumi za magari bila shida achana na switch zake. Alizungusha mara mbili tu mult lock zikaachia akaingia nyuma ya usukani na kulitekenya nalo likacheka, taratibu akaingia barabarani na kuifuata ile Jeep Cherokee, alikanyaga mafuta na kuhakikisha haiachi mbali gari ile, kati yake aliacha gari kama mbili hivi na kuendelea kuifuata, baada ya barabara tatu nne na vichochoro kadhaa ilianza kuuacha mji na kuchukua barabara ya kuelekea Thika, Melchior aliendelea kuwafuata na walipokaribia maeneo ya Kalimoni, akaona hapana, akaongeza mwendo na kuifikia ile Jeep, akaipita na kukaa mbele yao. Kila dereva wa ile jeep alipoijitahidi kuipita ile gari ya Ndege haikuwa rahisi, Melchior akaongeza kasi na kuiacha kama mita ishirini hivi kisha akafunga breki kali sana na ile jeep ilikuja na kuigonga ile Toyota kwa nyuma, kutoka katika ile jeep, mtu mmoja akateremka na kuifuata ile Toyota akaangalia ndani lakini hakuona dalili ya mtu, alitazama huku na kulea asione kitu, akarudi garini mwake na kuingia, alipofunga mlango tu alihisi kitu cha baridi kikigusa shingo yake, “Tulia hivyohivyo,” sauti ilimwambia, kisha Ndege akaunyoosha mkono wake na kuichomoa bastola ya yule dereva, wakati huo tayari kipigo cha haraka kilishampa usingizi wa muda yule mwanamke aliykuwa na Amata, “Toa gari barabarani, weak kando ile,” Melchior Ndege aliamuru na amri ikafuatwa, mbele kabla ya mahali alipoambiwa aiegeshe gari ile palikuwa na daraja kubwa sana la mpishano wa barabara, wao sasa walikuwa barabara ya juu, yule dereva akafanya hila kwa kugongesha ile gari katika ukingo wa daraja, ile gari ikayumba kidogo, Melchior, mle ndani ya gari akaangukia upande wa pili na kumpa nafasi yule dereva kufanya lolote, lakini kabla hajafanya hivyo, maana Melchior alimuona akichomoa bastola nyingine sehemu Fulani ya dashboard yake, kitendo bila kuchelewa, kwa kutumia miguu yake miwili alimbana kabali njema, gari iliyumba lakini Melchior hakujali, mara akasikia kishindo kikubwa, ile gari ilijipiga kwenye ukingo wa daraja, ikahamia upande wa pili ikakutana na Toyota prado na kujibamiza kisha akaangukia nje ya barabara. Kamanda Amata akiwa hajui lolote linaloendelea kutokana na usingizi mzito alioulala mara tu baada ya kuingia mle garini, alijigonga kichwa kwenye muhimo wa dirisha, akshtuka na kuanza kushangaashangaa, huku damu zikimtiririka kutoka kwenye jeraha dogo lililotokea katika kichwa chake baada ya kujigonga kule.

Melchior alitoka kwa shida kidogo katika gari ile baada ya kuvunja kioo cha mbele, kisha akamsaidia Kamanda Amata kutoka nje, bado Kamanda alikuwa hajarudiwa na akili sawasawa alikuwa kama zezeta hivi, Melchior akamshika mkono na kutembea nae kuelekea pale alipoiacha ile gari alioichukua kule hotelini, aliwakuta polisi wawili akiitazama ile gari huku wakiwa na wanaandikaandika vitu Fulani wakisaidiwa na taa za barabarani. Melchior aliufungua mlango wa mbele na kumtumbukiza Kamanda kiti cha kushoto kisha yeye akazunguka kiti cha kulia, “Halo, vipi, mbona unakuwa kama hauheshimu mamlaka?” mmoja wa wale askari akauliza, Melchior akawasha gari huku akimwangalia yule askari, “Nenda pale karibu na njia panda utakuta ajali ya gari aina ya Jeep Cherokee, hiyo ndiyo ukaipime, hii sio ajali,” kisha akaondoka kwa kasi mpaka kwenye mzunguko mkubwa na kuhama njia kuchukua njia inayorudi mjini, kwa mwendo uleule wa kasi ya ajabu.

AGA KHAN HOSPITALI

Parkland Avenue-Nairobi

Melchior ndege aliegesha gari katika lango la hospitali ile na daktari mmoja alikuwa pale tayari na kitannda cha magurudumu, akisaidiwa na manesi wawilli walimlaza kamnda Amata na kuingia naye ndani, moja kwa moja wakamuweka kitandani kwemye chumba cha peke yake, wodi maalumu, daktari alipomuangalia vizuri aliona wazi hali yake si nzuri, hivyo akaamuru awekewe drip ya glucose ili iweze kumrejeshea nguvu japo kidogo. Wale wauguzi wakafanya hivyo lakini pia walicheki mapigo ya moyo na kuweka kumbukumnbu zake kati faili maalumu lililokuwa pale, Kamanda Amata alilala kimya akiwa hajitambui tena, jeraha lake lilishonwa na kuwekwa katika hali ya usafi.

Melchior Ndege, alipekuwa kwenye mifuko ya Amata lakini hakuona chochote, akabaki kumtazama pale kitandani alipozungukwa na mitambo tiba ya kisasa ambayo ilikuwa inaangalia mwenendo wa mwili kwa ujumla kama mapigo ya moyo na mambo mengine. Melchior Ndege alitoka nje na kufunga mlango mkubwa kioo kisha kurudi ofisini kwa daktari.

“Rafiki yako inaonekana amepewa sumu kali sana ambayo imempotezea fahamu na kuathiri mfumo wa urendaji kazi wa mwili wake, itamchukua masaa mengi sana kuirudia hali yake ya kawaida,” Daktari alimweleza Melchior Ndege, haikuwa rahisi kulielewa swala hilo, lakini aligundua kuwa Bill alidhamiria kummaliza Amata. Akashusa pumzi ndefu na kumtazama daktari.

“Huyu ni mtu wetu, katoka Tanzania,” akamwambia kwa kifupi, daktari akatikisa kichwa kuashiria kuwa ameelewa, kisha Melchior akampa habari nzima jinsi alivyomuona kuanzia pale hotel ya Safari park mpaka kule kwenye ajali.

Hasira zilizidi kumtawala Melchior na moyoni akaapa lazima Bill alipe yote ayafanyayo, hapo akagundua kuwa Bill ni jasusi la kimataifa lenye mbinu za kuua bila kutumia silaha na kuwafanya watu kutojua ni nini chanzo cha kifo. Aliagana na daktari na kuomba kurudi baadaye kidogo lakini apewe taarifa ya kila kinachoendelea.

Safari yake na gari ile ya kukodi iliishia katika mtaa wa Riara, akashuka na kuilipa tax hiyo kisha akaliendea geti kubwa jeusi lilofungwa sawia, akabofya kengele, mara likafunguka naye akajitoma ndani, “Karibu sana kijana!” alikaribishwa na sauti ya boss wake bwana Shikuku, “Vipi mbona usiku sana ?” akaongeza swali, ndipo Melchior alipoinua mkono wake kuitazama ile saa yake iliyomuonesha kuwa ni saa nane kasoro robo usiku. Wakaingia sebuleni na kuzungumza machache, Melchior alimpa habari yote ya Kamanda Amata. Shikuku alisikitishwa sana na habari hiyo, kisha wote wawili usiku huo wakatoka na kuelekea kule hospitali kumuona Kamanda, walimkuta katika hali ileile isipokuwa sasa ilikuwa mbaya zaidi kwani mapigo ua moyo yalishuka sana, hata daktari alikuwa na wasi wasi juu ya hilo maana hayakuonekana kupata unafuu wowote.

“Shiiiittt!!!!” aliinua simu yake na kubofya namba Fulani kisha kusikiliza sauti ya upande wa pili, baada ya mazungumzo mafupi aliikata na kuiweka mezani, akajishika kichwa kwa masikitiko, mara simu yake ikapata uhai na kujitikisatikisa pale mezani, aliinyakuwa na kusikiliza, “Yeah… ndiyo… ee. Fanyeni haraka tafadhali,” akakata simu na kuitia mfukoni.

“Vipi, ni nani hao?” Ndge alimuuliza bosi wake.

“Nilikuwa nawapa taarifa juu ya mtu wao huko Tanzania, ili wajue ni nini watafanya, sasa wamesema wayanijibu haraka iwezekanavyo,” Shikuku alijibu.

“Hivi Bill amedhamiria haswa kufanya mauaji ya mtindo huu sivyo?” Ndege alimuuliza Shikuku.

“Yule ni shetani, sio binadamu, hivi umesema yuko wapi saa hii?” Shikuku aliuliza swali kwa Ndege.

“Niliwaacha, Safari Park casino, lakini sidhani kama bado wako hapo, ngoja tufatilie wale watu wa kwenye ile gari ili tujue kwa undani juu ya sakata hili na nini kipo nyuma yake, simpendi kabisa Bill, na aombe Kamnda Amata asiamke milele, lakini Shikuku nakuhakikishia, Kamnda akiamka atavunja mpaka miiko ya kazi yake ili amtafute huyu hayawani na kwanza atamuua kisha amuulize maswali anayoyataka,” melchior Ndege aliongea kwa hasira na kutoka nje ya chumba cha daktari.

Mkono wa bwana Shikuku ulimshika bega Melchior Ndege pale alipokuwa ameegemea ukuta akiwa amewaka hasira zilizojaa uchungu.

“Malchior, punguza jazba, pamoja na FBI kuwa hapa, isiturudishe nyuma, ingia kazini, mimi nakuamuru, kama kuna swali mi nitajibu; Kamanda atapona tu, najua walimuwahi katika namna ambayo hakuitegemea,” yalikuwa ni maneno ya Shikuku kwa Melchior, akageuka kumtazama mtu huyo mwenye mwili mkubwa, mkuu wa idara ya usalama wa Taifa hapo Kenya, Melchior alitabasamu kwa bashasha baada ya kuambiwa ‘Ingia kazini’, alitoka pale alipo na kuelekea tena chumba cha daktari kisha akaingia kumuona Kamanda, alimutoa alama ya saluti ya heshima, na kumuhakikishia Kamnda kuwa sasa analipiza kisasi kwa ajili yake, kishapo akatoka nje na kuagana na Shikuku.

˜˜˜

DAR ES SALAAM

Saa 9:15 Usiku

KELELE za simu ya mezani ya Madam S ilipiga kelele usiku huo, mlio wa dharula ulimshtua kutoka katika usingizi mzito, “Aaaa nini tena saa hizi?” aliongea kwa sauti ya hasira na kuinyakua ile simu masikioni mwake, “Hallo nini saa hii?” aliipokea na kutupa swali hilo; huku akisikiliza sauti ya upande wa pili, “Madam, kuna taarifa kutoka Nairobi kuhusu Kamanda Amata, hali yake ni mbaya sana yuko kufani,” sauti hiyo iliongea kwa upole, ilikuwa ni simu kutoka ofisi ya usalama wa Taifa ikimpa taarifa hiyo Madam, mkuu wa kitengo maalum chenye watu wachache makini wanaofanya kazi za umakini kwa umakini wa kimakini. Aliishika ile simu bila kuongea. “Unasemaje?” akauliza, akajibiwa tena jibu lilelile. Madam S alishikwa na kigugumizi, midomo ilimchezacheza, hakuamini anachoambiwa, ni jana tu mchana alipoagana na Kamanda wake pale JNIA na kumpa usia wa nguvu, Madam alibaki kimya na simu ikiwa hewani nab ado hajaishusha kutoka sikioni mwake, akashusha pumzi kisha akafungua kinywa chake, “OK, asante kwa taarifa, fanya kila kinachowezekana Kamanda afike hapa mara moja,” akakata simu na kurudisha mkono wake mahali pake, “Uuuuhhhhh!!!!” akashusha pumzi nzito kwa mara nyingine, akajilaza kitandani kwake huku mawazo lukuki yakiwa yamemtawala kichwani mwake. Akafikiri la kufanya na kumpigia daktari wao pale Muhimbili, ushauri aliopewa aliuona una maana sana, yule daktari alimshauri ikodiwe ndege ya haraka kutoka Nairobi imlete Dar, badala ya kukodi kutoka Dar. Utaratibu ukaandaliwa haraka kwa ushirikiano na Bwana Shikuku kule Kenya. Usingizi haukuja tena kwa Madam S, akaifungua kompyuta yake ya kazini ambayo imeunganishwa moja kwa moja katika kitanda chake, alipojaribu kuingiza password yake, ikagoma, haikufunguhka, akajaribu tena na tena, wapi. Alipoona imeshindikana, akampigia simu Chiba, mtaalamu wa ICT wa kitengo chao, naye akajaribu kuifungua lakini ikawa ngumu, akatumia mbinu zote kuitafuta maana alishajua kuwa wajanja wameiiba kimtandao, na kwa maana hiyo siri zote za usalama wa Tanzania ziko hatarini kuvuja, kijasho kilimtoka Chiba, usingizi ulikatika, akiwa mezani kwake alikuwa akishindana na mtandao kuloitatua tatizo hilo huku Madam S akimuahidi kufika hapo mapema ili kujua kulikoni. Majibu yalikuja na kugundua kuwa kompyuta ya Madam S imekuwa ‘Hiked’ sehemu Fulani huko Nairobi, mchezo ukaanza kunoga, sasa mapigano ya kimtandao, Chiba hakukubali, alifanya juu chini kuinusuru, ‘Kamanda Amata wanataka kumuua na mtandao wanataka kuukamata, shiit,” alijiwazia kisha akaiacha kompyuta yake na kuelekea kwenye kabati lake, akavaa nguo haraka haraka na kuibeba ile kompyuta kisha kuchukua gari yake haraka akawahi katika ofisi ya mawasiliano ya Usalamawa Taifa, pale kuna kompyuta kubwa zaidi inayoweza kujua vizuri sana, ni wapi na ni nani aliyefanya hivyo, haikuchukua muda aliinasa, na kuifunga kabisa kwa namba ambazo mwingine asingeweza kuzifungua. Akasimama na kumtazama kijana aliyekuwa akisaidiana naye kazi hiyo, Man’sai.

“Dah, hatujui ni kiasi gani wamepata siri zetu,” Chiba alimueleza Man’sai aliyekuwa kasimama karibu na meza kubwa yenye screen kubwa sana ya kompyuta inayoweza kuzileta kompyuta nyingi za ulimwenguni na kutafuta kila wanachokitaka.

“Sasa Bro, cha kufanya ni kiunguza kabisa hiyo kompyuta yao waliyotumia kutu ‘hike’,” Man’sai alisema.

“Tutafanyaje, maana inabidi tupate code namba ya BIOS,” Chiba alisema

“Ah no, siku hizi huwezi kuua kompyuta kwa kuiharibu BIOS maana technolojia imepanda kaka, Operating System za sasa zina uwezo wa kutest kila hardware na software zilizopo katika kompyuta bila kupitia kwenye BIOS, cha kufanya hapa tuondoe taarifa zetu kisha mi nitaweka kirusi kibaya sana kwa jina la faili moja, najua kwa vyovyote watafungua tena, maana kwa sasa wanaonekana wapo offline, kisha huyo kirusi atavuruga system yote ya kompyuta yao,” Man’sai alijibu kwa kujiamini, kijana mwenye elimu ya ICT kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam.

“Ok, fanya hivyo wakati mi nafanya mengine,” Chiba alimalizia. Kijana Man’sai alikaa makini kwenye laptop yake akitengeneza shetani hilo alilolipa jina TOP SECRET, kazi iliyochukuwa kama lisaa limoja hivi na kuifanikisha akiwa kachoka sana. Kisha akamwendea Chiba na kumwambia kazi tayari ili apate ruhusa ya kufanya mlipuko huo, akakubaliwa, kazi ndogo, akaingiza kile kirusi kwenye mfumo wa kompyuta ya Madam S na kukiacha hapo, wakati document zingine zote akiwa zimebanwa na Chiba kwa pin ngumu.

˜˜˜

REJEA NAIROBI… kanisa la familia Takatifu…

Ilikuwa ni kazi ngumu kwa Black Cheetah na Mellina kutoka ndani ya wigo wa kanisa maana tayari sergeant Maria na koplo Kariithi walikuwa pale na wengine wanne wenye silaha, walitanda kila upande kuhakikisha majambazi hao hawatoki bila kuacha roho zao.

Gichui, aliyekua akiendesha gari siku hiyo aliwapa taarifa kwa simu kuwa jamaa wamejipanga vipi huko nje, wakamuamuru, aanzishe show kwa kupiga risasi za hewani. Naye akafanya hivyo, mlio wa risasi zile ukawafanya wale askari kuchanganyikiwa kidogo, Black Cheetah alitoka katika mlango mkubwa akiwa na lile begi na kukimbilia upande wa pili wa ukuta huo ambako ndiko waliokoingilia, huku Mellina akitambaa mwendo wa nyoka kulifuata geti kubwa akiwa na bastola yake aina ya revolver mkononi mwake.

Gichui alipiga norinda na kutimua vumbi liliwachanganya Mellina na Kariithi ambao walikuwa tayari kujibu mashambulizi, Sargeant Mellina alijitupa chini na kubingirika kwa usatadi mpaka kwenye ukuta wa wigo wa kanisa hilo huku akishuhudia vijana wake wakijiweka tayari, “Freeze!!!!!!” sauti ya askari mmoja lisikika upande wa pili, Kariithi bado alikuwa akijaribu kuona afanye nini, akajitoa na kukimbilia upande wa sauti ile ilipotokea, akiwa anakata kona ya ule ukuta alisikia mlio wa risasi na kushuhudia mwili wa yule askari ukijibwaga chini kama kiroba, “Shiittt!” akng’aka kwa hasira, alimuona Cheetah, aliyeifanya kazi hiyo akiishia gizani, akajaribu kulenga na kufyatua risasi mbili lakini hakumpata, mara ile gari yao ilipita kwa kasi na kuelekea upande ule alipo Cheetah, haikuhitaji kusimama, kawani Cheeta alirusha begi ndani ya gari na kujirusha kupitia dirishani, lakini kabla hajamalizi miguu risasi moja ilipita katikati ya mguu wake na kufumua mifupa ya ugoko, Gichui aliizungusha gari kwa ustadi na kumfanya Cheetah kutumbukia ndani, “Aaaaaaaaiiiiggggghhhhhh!!!!” ulikuwa ukelele wa maumivu kutoka kwa Cheetah.

“Vipi brother?” Gichui aliuliza huku akiizungusha tena ile gari na kumgonga askari mwingine, sasa alikuwa akilielekea geti kuu la kanisa lile.

“They have shot me, bastards!” wamenipiga wanaharamu alimwambia Gichui, huku akiiweka tayari bastola yake. Sergeant Maria akiwa pale chini aliilenga sawia ile gari na kabla hajapiga risasi alihisi kama kitu kimenguka pale alipolala kwa nyuma yake alipogeuka aliona mwanamke kibonge akitua juu ardhi kavu na bastola mkononi, akiwa pale chini alijigeuza na kupiga mtama mmoja maridadi, Mellina alilipokea pigo hilo na kubwagwa chini, alijitahidi kujiinua kisarakasi lakini kabla hajawa wima mtama mwingine wa Mellina ulimrudisha chini na kumfanya hoi pale ardhini, sasa alishindwa kujiiunua. Bastola ya Mellina ilicheua na risasi ikapita mililmita chache kwenye uso wa Maria aliyekuwa pale chini, teke moja kali la afande Maria lilipeperusha bastola ile kutoka mikono ya Mellina ikapaa juu, kisha aliushusha mguu wake na kuutuza juu ya uso wa Mellina.

Koplo Kariithi alijitoa mhanga na kucukua ile SMG ya askari ambaye aliku marehemu, kuilenga gari ya Gichui, ‘nice shot’ risasi moja alipiga tairi ya nyuma na kuipotezea muelekeo ile gari, ikayumba na kuyumba lakini ikakaa tena barabarani, risasi ya pili kutoka kwa Kariithi ikakishusha kioo cha nyuma na bila kukosea ikafumua kisogo cha Gichui na ile gari ikayumba myumbo mkuu na kugonga mti. Wakati Kariithi akiifuta, ghafla nyuma yake kulitokea gari aina ya BMW kwa kasi ya ajabu ikafunga breki kali karibu kabisa na ule mti ilipogonga ile gari ya Gichui, kwa haraka watu wawili walishuka na kuifungua milango wakamtoa Cheetah na kulibeba begi kisha kurudi ndani, ile gari nayo ikazungushwa kwa mtindo wa U turn na risasi moja iliyotoka ndani ya gari ile ilimpata koplo kariithi mkononi, ukelele wa maumivu ulimchanganya sergeant Maria, akamsahau Mellina na kumkimbilia Kariithi, “Soldier!!!” Askari, sergeant Maria aliita kwa sauti na askari wote wakaja eneo hilo na kumbeba mwenzao wakimpakia kwenye gari, wengine wakabaki kufanya utaratibu wa kumuondoa Gichui ambaye alikuwa hana maisha tena na kichwa chake kikiwa kimevurugika kwa risasi ya Kariithi, moja kwa moja walimfikisha katika hospitali ya taifa ya Nairobi.

5

MADAM S alisimama kwenye mlango maalum wa kioo akimtazama Kamanda Amata aliyekuwa amelala kitandani akiwa ndani ya mitambotiba, sasa alikuwa ameamka baada ya kazi kubwa ya daktari wa muhimbili ya kumtoa sumu mwilini, alifumbua macho, aliweza kuongea japo kwa shida, alikutana macho na bosi wake, akamtazama, “Karibu Nairobi Madam,” Kamanda alimkaribisha madam S.

“Aliyekwambia hapa Nairobi ni nani?” Madam alimuuliza Kamanda.

“What?” akajiinua na kuketi, “Niko wapi?” akauliza.

“Upo Muhimbili, karibu sana Dar es salaam, Kamanda umefanya mambo ya kijinga sana Kamanda, siwezi kukuvumilia hata kidogo, tumekaa kikao na kuona kukutoa wewe katika cheo chako cha TSA 1 na kumpa mtu mwingine,” Madam S akameza mate, “Kila mara nakuonya na wanawake wako hutaki kunisikia, kwa nini? Sasa wlitaka kukuua, mshukuru bwana Shikuku na kijana wake Ndege, ulikuwa marehemu tayari, na sasa tungekuwa tunautafuta mwili wako. Kamanda huna maana tena kwetu na kwa serikali kwa ujumla, tunaandaa utaratibu wa kukustahafisha hasa kwa uzembe unaouonesha, unajua wewe ni kama roho ya serikali, wakikubana wewe watakuwa wamepata kila kitu, kila siri, na sumu waliyokupa si ajabu imekufanya utoe siri nyingi bila kujijua.” Madam akageuka na kuondoka zake na kufunga milango nyuma yake, Kamanda Amata akabaki kajiinamia kisha akajitupa kitandani kwa hasira, “Biiiiiillllllllllllllll !!!!!!!” alipiga ukelele wa nguvu kisha akapoteza fahamu…

Ilikuwa ni zamu ya madaktari na wauguzi kuhakikisha wanaokoa maisha ya Kamanda Amata katika dakika hizo, haikuwa rahisi maana ilionekana mapigo ya moyo yakishuka zaidi, walijaribu mbinu zote za kitaalamu lakini bado hali ilikuwa tete, baada ya kuhangaika kwa muda refu, kidogo hali yake ilianza kurudi na mapigo ya moyo yalirejea kwenye hali ya kawaida ingawaje bado alikuwa katika usingizi mzito uliogubikwa na taswira ya Bill kama mtu wa kutisha na hatari, aliyetaka kuyakatisha maisha ya Kamanda kwa mtindo ambao hakuutegemea, wauguzi na madaktari walishusha pumzi wakiwa wamekizunguka kitanda cha Amata, walifarijika zaidi walipomshuhudia akiwa amefumbua macho akiwaangalia mmoja baada ya mwingine, “Kuna nini?” aliuliza, “Mbona mmenizunguka hivyo?”

“Kamanda! Ulikuwa katika hali mbaya sana, kiasi kwamba bila jitihada za hawa wote tungekukosa,” Daktari alimueleza akiwa amemuinamia. Ilikuwa kama hali ya mshangao kwa Amata, alijitazama kama mtu aliyerukwa na akili, “Yuko wapi Bill?” aliuliza. “Bill?! Bill ni nani?” aliulizwa na daktari, Amata alizungusha shingo yake na kuona wauguzi tu na madaktari, akajilaza kitandani kwa mara nyingine. “Ok, tumuache apumzike sasa,” ilikuwa ni kauli ya daktari akiwaambia wale wauguzi pamoja na wasaidizi wake, wote wakakiacha kile chumba na kurudi katika idara zao. Akili ya Kamanda Amata haikutulia, muda wote ilimuwaza Bill, hasira zikaanza kuuteka moyo wake, maneno ya Madam S yakamvunja nguvu, ‘Bill anataka kunisababishia kushushwa cheo na kustahafishwa kabisa,’ alijiwazia; ‘Haiwezekani,’ alinyanyuka katika kile kitanda alichokilalia, akajichomoa drip iliyokuwa ikiendelea kuingia mwilini mwake, akatazama huku na kule hakuona nguo yake yoyote zaidi ya yale mavazi aliyovaa, mavazi ya hospitalini, hakujali, akauendea mlango na kutoka, huku na kule, hakuna mtu, akatoka mlango wa pili na mpaka ule wa nje, akiwa pale nje alikutana na watu mbalimbali hakujali wala kushangaa, alipita eneo la walinzi na kufikia maegesho ya tax, akajichagulia moja, “Wapi mzee?” dereva Tax alimuuliza, “Kinondoni, mkabala na Leaders Club,” akampa maelekezo, wakatokomea kutoka hapo.

“Una simu hapo?” Amata alimuuliza yule dereva tax.

“Ndiyo braza,” akajibiwa.

“Niazime nipige mahali, pia niambie ni shilingi ngapi,”

“Haina shida, hapa utanipa shilingi elfu thelethini,” lilikuwa ni jibu lingine la dereva tax.

Kamanda Amata alichukua simu na kubofya namba Fulani, kisha kuweka sikioni, “Baada tu ya kukata simu hii, naomba uingize shilingi elfu hamsini katika namba hii, (…) niangalizie kama kuna ndege inayoondoka mida hii kupitia Nairobi, iwe inaelekea hapo au inapita hapo, niandalie safari tafadhari, nina dharula, call aborted” Akakata simu na kumrudishia, dedreva tax, akamuamuru kusimama, akashuka na kuagana nae baada ya kumpa maelekezo kuwa hela yake itaingia kwa simu.

˜˜˜

“Pamoja na maumivu ulonayo, nitakupa malipo yako ya mwisho, umenifanyia kazi kubwa sana Cheetah,” Bill Van Getgand alikua akimuangalia Cheetah kwa jicho la uchungu sana hasa pale kijana huyo alipokuwa akiugulia kwa maumivu ya jeraha lake, hakuweza kwenda hospitali kwa kuhofia polisi, hivyo alijificha katika moja ya magheto yake katika mji mdogo wa Kinangop ya kaskazini. Bill akatoa bunda la noti na kumpatia, “Ugawane na Mellina, lakini usisahau kumnunulia sanda Gichui,” akanyanyuka na kulitwaa lile begi la ngozi na kumpa Wambugu kisha kwa kutumia ile fimbo yake akaujongelea mlango wa kutokea nje ya ghto hilo, akasimama na kugeuka nyuma, akawa akitazamana na Cheetah. “Asante braza, nitafanya hilo, wewe ni mwema sana, maana mwingine angeshapata mzigo wake na kutoroka hata asingekumbuka kazi kubwa aliyofanyiwa na swahiba zake,” Cheetah aliongea kwa tabu kidogo, akionekana wazi ni mwenye maumivu makali katika jeraha lake. “Nami na shukuru kwa kazi njema mliyonifanyia, nasikitika sana juu ya Gichui lakini naamini Mellina mtaonana usiku huu, lazima akufuate. Kwa kuwa mimi sijakudhulumu haki yako basi naomba na wewe usimdhulumu Mellina haki yake. Cheetah lazima ujue hata waovu wana aina ya wema uliobaki mioyoni mwao,” Bill akanyanyua ile fimbo yake ya kutembelea, akaongea huku akiwa ameiyooshea kwa Cheetah pale kitandani, akitoa maneno ya faraja na kumshukuru, mkono wake wa kulia ulioishika ile fimbo ukafyatua kibati Fulani karibu kabisa na kwa kushikia, ukakibonyeza tena ka namna nyingine, mara kitu kama msumari kikachomoka kwa kasi kutoka katika ncha ya fimbo ile na kuzama moyoni mwa Cheetah, macho yakamtoka Cheetah, akabaki akimtazama Bill, damu ilitiririka na kuichafua fulana yake, akalegea na kudondokea kifuani, “Asta la Vista baby,” Bill alitamka maneno hayo na kuchukua tena lile bunda la noti akaligawanya nusu, nusu akaiacha pale kitandani na nusu akatoka nayo.

“Kuna watu ninaohitajia pumzi zao leo kabla sijaondoka,” Bill alimwambia Wambugu wakiwa ndani ya gari yao.

“Mi nilijua ushamaliza kazi kaka,” Wambugu aliijibu kauli ya Bill

“Hapana, lazima tusafishe makandokando yanayoweza kutuletea shida wakati wa kula bata,” Bill aliendelea.

“Kwa hiyo unasemaje?”

“Nina muda mchache sana wa kupotea hapa mjini, najua natafutwa, nimeshawaona, FBI ninaowafahamu, watu wa MOSSAD wapo mjini, ukiachana na wana usalama wa hapa Kenya, nafurahi tu kuwa Kamnda Amata popote alipo lazima apoteze uhai, sumu niliyompa ni mbaya sana,” akakohoa, “Wambugu!” akaita na kumtazama kijana huyu wa Kikuyu, “nataka roho ya Mellina na Kahaba Rose ndani ya masaa machache yajayo.”

Ilikuwa ni kauli iliyotaka kumfanya Wambugu ashindwe kuendesha gari lakini alijikaza kisabuni nyuma ya usukani na kumeza mate maana alihisi koo limekauka kau.

“Mi nilifikiri hao hawana maana,” Wambugu aliongea kwa upole.

“Wakishakufa niulize kwa nini nimewaua nitakwambia sababu ambayo hata wewe ungewaua, cheetah tayri nimeshamuua,” Bill alisema huku akiwasha sigara yake kuvuta akizitupia nywele zake ndefu mgongoni.

“Simamisha gari pale karibu na ile Subaru,” Bill aliamuru na Wambugu akasimamsiha kama alivyoagizwa, Bill akashuka na kulichukua lile begi, akasimama na kumwangali Wambugu, “Sikia, kama unataka maisha yako basi ufunge mdomo, hakuna ajuaye undani wa sakata hili zaidi zaidi yaw ewe, Mellina na kahaba Rose. Naomba uchunge mdomo wako, ila kazi moja ukanifanyie, hakikisha unamuua Rose na Mellina kabla hujajiua mwenyewe,” Bill aliongea huku akimrushia kile kibunda cha pesa Wambugu kupitia dirisha la ile gari, akakidaka na kukiweka kitini. “Nitakupigia simu baada ya masaa matatu ili nijue kazi yangu imefikia wapi, elewa kuwa hauko peke yako,” akageuka na kuliendea lile gari aina ya Subaru na kulitupia lile begi kiti cha nyuma kisha yeye akakaa nyuma ya usukani wa gari ile na kutokomea akiifuata barabara ya Uganda.

˜˜˜

Haikuwa rahisi kwa Madam S kuelewa kile anachoambiwa na dakatari kuwa Kamnda Amata ametoroka hospitalini, alibaki kimya huku akiwa anashindwa kuchanganyikiwa, akizunguka kutoka upande mmoja kwenda mwingine wa ofisi ile, akasimama katikati na kumtazama daktari kwa makini, “Hebu nambie, katoroka au katekwa?”

“Kweli Madam katika hilo siwezi kujibu, mi nimerudi sikumkuta kila niliyemuuliza anadai hakumuona,” alimjibu.

Madam S alitoka kwa daktari bila kuaga na kuielekea gari yake, akaketi ndani na kuitia ufunguo, switch on, kisha akabonya bonya mahali Fulani. Skrini ndogo ikachomoza na kujifungua katia ile dashboard ya gari, akaminya mahali Fulani katika skrini hio mara ramani kubwa ikatokea, akaingiza namba Fulani ambazo hutumia kumpata Kamanda Amata, kwa kujua mahali alipo lakini haikuwa rahisi kupatikana, alijishika kichwa hajui la kufanya, akawasha gari na kurudi ofisini.

Mawazo yalimtawala hakujua la kufanya, alishika hiki mara kile, alijaribu mbinu zote za kitaalam kupata Kamanda, haikuwa rahisi. Akapata wazo, akampa kazi Chiba amsake mpka amtie mkononi.

Gina aliegesha gari yake katika maegesho ya uwanja wa ndege wa Dar es salaam,

“Mtu awaye yote akikuuliza juu yangu mwambie nipo katika majukumu ya kiserikali, najua Madam S atakutafuta jioneshe kuwa hata hujui wapi nilipo zaidi ya Nairobi, kwa heri mpenzi tutaonana tena,” Kamanda Amata alimkumbatia Gina kumuaga, Gina alikuwa akitokwa na machozi ya upendo.

ITAENDELEA

Mauaji ya Kasisi Sehemu ya Tatu

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment