Msako wa Mwehu Sehemu ya Tano
KIJASUSI

Ep 05: Msako wa Mwehu

Msako wa Mwehu Sehemu ya Kwanza
Msako wa Mwehu Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA: BADI M. BAO


Simulizi: Msako Wa Mwehu

Sehemu ya Tano (5)

Kisha lile gari la mbele aina ya “Land cruiser GX-R” rangi nyeupe likawa linaongoza njia huku Kachero Yasmine analifuata kwa nyuma. Wakauzunguka uwanja wa mpira wa miguu na kushika njia ya darajani inayoelekea kota za wanajeshi wa kambi ya Lugalo kisha wakashika njia ya kuelekea Makongo juu. Wakatembea kama mwendo wa kilometa moja gari ya mbele ikawasha indiketa kuingia barabara ndogo ya upande wa kushoto wa barabara. Wakaenda kama meta 600 wakakutana na nyumba moja ya roshani iliyojengwa kifahari imezungushiwa ukuta nyumba yote.

Gari likapiga honi, punde si punde mlinzi wa nyumba akawa analisukuma geti ili magari yaingie. Moja kwa moja magari yakaegeshwa kwenye eneo la maegesho ambapo kulikuwa na magari mengine ya kifahari zaidi ya matatu yameegeshwa. Haraka haraka wakashuka watu watatu waliokuwa kwenye gari la mbele na kuwalaki akina Kachero Manu. Walikuwa wanaume wawili na mwanamke mmoja. “Salaamu aleikum karibuni sana wageni wetu jisikieni mpo nyumbani” yalikuwa ni makaribisho toka kwa mume wa yule dada aliyekuwa anaendesha gari. “Waleikum salaam tumeshakaribia shukrani sana” akajibu mwanaume aliyefuatana na Kachero Yasmine.

Wakaongoza msafara kuelekea ndani ya nyumba hiyo ya roshani tatu. Wakati wote wanatembea kuingia ndani Kachero Yasmine alikuwa anaithaminisha nyumba hiyo gharama yake. “Kuisimika nyumba kama hii si chini ya bilioni 1.5, hawa watu wanaishi kwenye ukwasi wa hatari” alikuwa anajisemea moyoni mwake. Mpaka wakafika kwenye sebule maalumu iliyotengwa kwa ajili ya mazungumzo yao. Kulikuwa na masofa ya chini kwa chini huku yakizungukwa na zulia zito lenye marembo marembo yaliyonakshiwa vizuri. Pia kulikuwa na mito midogo midogo iliyozagaa. Mmoja wa watumishi wa kike wa kwenye ile nyumba akiwa amevaa vazi la stara lililofunika mwili wote akaleta mchapalo wa visheti vikavu vya sukari, tende nyeusi na chupa ya kahawa na vikombe vyake.

Akawakaribisha na kuondoka zake. Kachero Yasmine na yule mwanamke mwingine wakanyanyua kahawa yao na kubeba mchapalo wao kwenye visosi viwili vidogo wakaomba ruhusa na kujitenga kando, huku wakiwaacha wale wanaume watatu sasa wanazungumza wenyewe soga zao. “Ukhty Yasmine mie naitwa Ukhty Ranilah ndio muongozaji wa NUSRA COMMETTE akaunti ya Facebook” wakapeana mikono kwa nyuso za bashasha.

Kisha akaendelea na maongezi yake Ukhty Ranilah, huku Kachero Yasmine anamsikiliza na kusukumizia visheti kwa kahawa. “Ile akaunti nimeifungua feesabil-llah hakuna anayenilipa, nataraji thawabu kwa Allah kesho yaumu kiyama” akaweka kituo na kuchota tende kwenye kisosi akamung’unya na kutema kokwa za tende kiganjani kisha akateremshia tarumbeta la kahawa kavu kama mafundo matatu, akaendelea na mazungumzo yake.

“Huwa napokea maombi kutoka pande zote wanaume kwa wanawake, wanaotafuta wachumba. Kisha tunafanya uhakiki wa taarifa za muombaji nikijiridhisha ndio nawaunganisha hao wachumba. Sasa wewe nilipata taarifa zako toka kwa mfanyabiashara mmoja mkubwa sana nchini Sudani, na hapa Tanzania ana vitega uchumi vyake kadhaa mkoani Tanga, anaitwa ‘Akhu Nufeil’. Alinipa taarifa zako kuwa kakupa anuani ya barua pepe yangu. Ni mtu Mchamungu sana, ndio maana hakutaka aongee na wewe moja kwa moja kwa sababu anajua angepata madhambi mbele ya Allah kuongea na mwanamke ambaye sio maharimu wake wakiwa faragha. Hivyo akanipa kazi pindi ukishanitumia meseji nikufanyie usaili nikijiridhisha kuwa unamfaa ndio tupange mipango ya ndoa. Je wewe huyo mchumba ni kweli mlionana ana kwa ana?” baada ya kuzungumza kwa dakika kadhaa Kachero Yasmine akatupiwa swali na mwenyeji wake Ukhty Ranilah. Kachero Yasmine akajifanya kuinama chini kama kisichana kidogo tena bikira kisichoelewa mambo ya kikubwa huku anajifanya kutafuna kucha. Baada ya kitambo kifupi akatoa jibu.

“Ni kweli tulionana Simba Hoteli, Jijini Dodoma, lakini hakunieleza lolote kutoka moyoni mwake ila lugha ya vitendo ilinijulisha kuna kitu kitaendelea baina yetu” alijibu kwa unyenyekevu huku anajifanya hawezi kumuangalia machoni mshenga wa “Maso Maso” .

“Sasa ile mahari yako uliyoitaja ya Dola za Kimarekani $5,000 nimeshamwambia na amekubaliana nayo ni wewe tu utuelekeze kwa wazazi wako tulete tuje kuoa haraka iwezekanavyo” alisema Ukhty Ranilah huku anamkazia macho Kachero Yasmine. “Bahati nzuri nimekuja na kaka yangu wa damu makusudi ili aweze kupokea posa na mahari, baba yangu kampa idhini na mamlaka ya kumaliza kila kitu, kama unavyojua dini yetu haipendi uchumba sugu” akajibu Kachero Yasminie kwa sauti ya upole yenye kuonyesha yupo tayari kwa ndoa.

Baada ya kupata muafaka wa pamoja kati ya Ukhty Ranilah na Kachero Yasmine, wakarejesha mrejesho wa waliyoafikiana kwenye baraza la wale wanaume watatu kwa majadiliano zaidi. Mpaka kufikia saa 4:00 usiku wakawa wamefikia muafaka wa ndoa kufanyika baada ya wiki moja siku ya Ijumaa baada ya swala. Ndoa ilipangwa kufungwa katika msikiti wa Sinza-Palestina, “Masjid Noor”. Hapo ndio ilisemekana ndio jirani na nyumba ya kaka yake Kachero Yasmine.

Kiuhalisia yule hakuwa kaka wa damu wa Kachero Yasmine, bali alikuwa ni Afisa Usalama ambaye alipangwa katika mbinu za kumtia mbaroni gaidi “Maso Maso”. Walichagua eneo la Sinza, kwa kuwa ni jirani na nyumbani kwao “Maso Maso” wakahisi huenda akashawishika kulala nyumbani kwao wamtie mbaroni kirahisi. Ikishindikana kumkamata siku moja kabla ya ndoa, watamkamata ndani ya msikiti wakati anafungishwa ndoa na Shekhe.

“Masjid Noor” ni moja ya misikiti mikubwa sana iliyopo Sinza. Upo pembezoni mwa barabara ya Shekilango, barabara ambayo inaunganisha barabara ya Mwai Kibaki na barabara ya Morogoro. Upande wa kusini msikiti huo umepakana na ukuta wa Hospitali ya serikali ya Sinza Palestina.

Siku hiyo ilikuwa ni Ijumaa, siku maalumu kwa ibada ya pamoja kwa waislamu wa sehemu mbalimbali. Waumini walikuwa wamefurika kuanzia ndani mpaka nje ya msikiti. Magari pia yalikuwa yameshonana pande zote mbili za magharibi na mashariki ya msikiti. Waumini wengi wao wakiwa wamevaa mufti, vazi la kanzu nyeupe na barakashia na tasbihi zao mikononi walikuwa wametulizana kwenye mazulia ya rangi ya kijani yaliyotandikwa msikiti mzima wanamsabihi Mola wao.

Wanausalama nao walikuwa wametanda ndani na nje ya msikiti kuhakikisha wanamtia mbaroni “Maso Maso”. Walikuwa katika hekaheka za kutaka kumlengesha wamtie nyavuni. Walimvizia nyumbani kwa mama yake maeneo ya Sinza-A walidhania huenda katika harakati za harusi atateleza kidogo kwenda nyumbani kwao kuweka mambo sawa, lakini haikuwa hivyo abadan. Karata yao ya mwisho ilikuwa ni kumkamatia ndani ya msikiti.

“Maso Maso” alikuwa tayari yupo ndani ya msikiti na rafiki zake watatu. Wakiwa wamevalia mavazi sare ya kanzu nyeupe na kilemba kichwani kilichozungushiwa hegali nyeusi. Kiunoni wakiwa wamejining’iniza majambia ya urembo ya kutoka Omani. kwa “Maso Maso” halikuwa jambia la kawaida kama zinazojulikana, bali ilikuwa ni silaha maalumu. Silaha ambayo kama ukimuendea kibwege atakuchakaza nayo. Kipindi cha hotuba ya swala ya Ijumaa wakati inaendelea, gaidi “Maso Maso” alikuwa alikuwa hana utulivu. Alishahisi ameingia choo cha kike kukubali kuja Jijini Dar es Salaam kuja kufunga ndoa yeye mwenyewe. Mwanzoni alipopewa taarifa sio salama kwake kuja mwenyewe alipinga sana wazo hilo. Alitamani usiku wa kwanza wa ndoa aufaidi na mkewe huyo aliyetokea kumpenda kuliko maelezo. Licha ya kutambua anasakwa kwa udi na uvumba kwa utundu wake alifanikiwa kutoka mafichoni na mpaka kuingia msikitini bila kushitukiwa. Alipokuwa msikitini kuna sura alikuwa kila akizutupia macho haziamini kabisa. Akili yake ikafanya kazi haraka sana zaidi ya kompyuta, akamnong’oneza kitu rafiki yake, wakaelewana.

Msomaji hotuba ya swala ya Ijumaa msikitini alipomaliza hotuba zake mbili, aliashiria muda wa kusimama kwa ajili ya swala kuu ya Ijumaa umetimia. Waumini walipokuwa katika harakati za kusimama ili imamu wa msikiti aanzishe swala, “Maso Maso” akavua kilemba chake na hegali yake akamkabidhi mwenzake na kuanza kuzipasua safu za watu waliojipanga anarudi nyuma kuelekea mlango wa chooni. Hakuna aliyemjali walijua ni muumini ambaye ametengukwa na udhu hivyo anaenda kutia udhu bombani. Hata baadhi ya wana usalama aliwapita bila kumtambua hasa kwa kuwa sasa alikuwa kichwa wazi na wao walimuona akiingia amejifunika kichwa chake. Alikuwa amejibadilisha muonekano wake alinyoa kabisa ndevu zake, kidevu kilikuwa kinang’aa kama balbu. Alipofika maeneo ya mabomba ya kutilia udhu akapitiliza chooni moja kwa moja, akakuta vimefungwa kuashiria kuna watu wanakidhi haja zao, huku wengine wamesimama kusubiria toka ingia ya chooni.

Akaunga foleni ya kutaka kusubiri, lakini Imamu alivyoanza kisomo chake cha swala machale yakamcheza. Akaanza kuondoka maeneo yale ya chooni na kuelekea chumba kingine kilichojitenga. Hamna aliyemjali kumfuatilia kila mmoja alibanwa na haja akili zao zilikuwa ni kupata nafasi ya kuingia chooni wakatoe chenye kuupa udhia mwili. Mpaka alipofika kwenye chumba hicho akasimama na kusoma maandishi makubwa yaliyobandikwa mlangoni hapo ya lugha ya kiarabu yalisomeka “GHURFAT LIGHASIL ALJUTHATH”. Alivyoyasoma akatabasamu akajaribu kunyonga kitasa kikakubali, hakikuwa kimefungwa na ufunguo. Akaingia mpaka ndani, kilikuwa ni chumba maalumu cha kuoshea maiti.

Chumba ambacho siku zote kilikuwa hakikosi maiti za kuoshwa kuanza za watoto wachanga wanaozaliwa wamefariki hadi za watu wazima kutokana na ujirani na hospitali ya Sinza Palestina. Kwa haraka haraka alikuta kuna maiti tatu zikiwa tayari zimeshavikwa sanda na kupambwa zinasubiria kuingizwa kwenye jeneza, ziswaliwe zikazikwe. Pembezoni kulikuwa na mabaki ya kitambaa kikubwa cha sanda na pamba zake zinazotumika kuziba kwenye matundu yote ya mwili wa maiti kuanzia sehemu ya haja kubwa, masikioni mpaka puani. Akaanza kujiweka pamba za puani akiwa na lengo ajiviringishie sanda nae wamuhesabie kuwa ni marehemu iwapo wataingia chumba hicho. Alipoanza kujiweka pamba za masikioni, akasita kidogo. Akaamua aghairishe zoezi hilo la kujifanya maiti.

“Mhudumu wa hiki chumba akija akakuta maiti zipo nne badala ya tatu atapagawa na kupiga kelele za uwoga ndio nitakaposhikwa” aliwaza kimoyomoyo “Maso Maso”. Akaangazaangaza mule chumbani akaona kidirisha kidogo, ambacho kinaweza kumpitisha mtu. Akafanya bidii kukikwea mpaka akafanikiwa kupapachua kidirisha kidogo cha Aluminiamu na kufanikiwa kutoka nje ya msikiti. Akaruka mfereji mwembamba unaotenganisha ukuta wa msikiti na ukuta wa hospitali. Akapanda ukuta wa hospitali na kurukia ukuta wa ndani ya hospitali ya Sinza Palestina.

Ni kitendo alichokifanya ndani ya dakika chache sana tena kwa umahiri wa hali ya juu. Alipojitupa chini akajikuta yupo ndani ya uzio wa hospitali. Akakuta mbele yake kuna tanuri, kizimba cha kuchomea taka za hospitali kinafanya kazi na hamna mtu yoyote. Akaenda mbele kwa kulipita tanuri hilo, mpaka akajitokeza kwenye korido la hospitali. Akakutana na mmoja wa wahudumu, akamsalimia na kunong’ona nae baadhi ya mambo. Akaelekezwa anachotaka, akaagana nae na kuelekea kwa huyo mtu aliyekuwa anamhitaji akiwa katika mwendo wa haraka. Yule mtumishi alikuwa anamsindikiza kwa macho hasa baada ya kumuona hata viatu hajavaa anatembea peku peku

Muadhini akatoa wito wa ikama, akazungumza maneno ya kiarabu yanayowataka Waumini wasimame kwa ajili ya kuanza kuswali. Waumini waliposikia hayo maneno wakasimama na wakajipanga safusafu. Imamu akafanya juhudi za kuhimiza waumini wanyooshe vizuri safu zao.

Alivyomaliza msisitizo wake akaelekea kibla na kuifungua swala yake kwa takbira. Swala haikuwa ndefu sana, imamu alisoma sura za Kurani fupi fupi ili asiwachoshe waumini waliowasili msikitini tokea saa 6:00 mchana. Ambao wengi wao walikuwa bado hawajapata mlo wa mchana na pia wanarejea kwenye shughuli zao za kujitafutia tonge la siku.

Baada ya swala kwisha tu, Imamu akasimama akiwa na uso wa bashasha na kutoa tangazo, “Salamu Aleikum Warahmatullah Wabarakatuhu, awali ya yote tunamshukuru Allah kwa kutuwezesha kutekeleza ibada hii ya swala ya Ijumaa. Tunaomba swala yetu hii mbele ya Mola iwe ni yenye kukubaliwa”. Msikiti mzima ukaitikia “Ameen”.

Kisha Imamu akaendelea “leo hatuna mawaidha hotuba yetu imejitosheleza kikubwa ni kuifanyia kazi, ila tuna matangazo matatu tu, tangazo la kwanza ni kuhusu michango yetu ya upanuzi wa msikiti bado inaendelea likipita kapu mbele yako usisite kutia chochote kitu, Allah atakulipa. Tangazo la pili hapa msikitini sasa hivi tutapitisha Nikaha, muumini mwenzetu anaozesha dada yake hivyo wale wenye wasaa wa wasubirie kushuhudia ndoa hiyo. Nawaomba wale waoaji toka Tanga wasogee mbele tayari kwa kuanza kwa shughuli hiyo. Na tangazo la tatu baada ya ndoa kutakuwa na swala ya maiti, tubakie kuswalia kuna mlundi wa thawabu unapatikana mithili ya mlima Uhudi uliopo nchini ‘Saudi-Arabia’ kwenye kuswalia maiti, wabillahi tawfiq” Imamu akawa amemaliza matangazo yake.

Waumini wenye haraka zao wakawa kwenye hekaheka za kutoka milangoni wanapigana vikumbo na wale wenye kuhitaji fadhila za kushuhudia ndoa wakawa wanajivuta mbele ili kusubiria shughuli ianze. Kaka feki wa Yasmine ambaye wakati wote wa swala alikuwa na furaha akijua wanakuja kumtia mbaroni “Maso Maso” uso wake ghafla ulipigwa na taghayari ukapoteza uchangamfu wake. Alikumbwa na bumbuwazi baada ya kuona hamuoni mlengwa wake “Maso Maso'”. Shekhe akaitisha ubani na chetezo cha moto na kuanza hotuba ya ndoa mpaka akamaliza. Akamuita muoaji na muozeshaji wamsogelee karibu ili ahitimishe shughuli.

Uzalendo ukamshinda kaka feki wa Yasmine ikabidi aulize, “yupo wapi Bwana harusi, kutuma mwakilishi hayakuwa makubaliano. Nimemuona kabisa yupo ndani ya msikiti na tumeswali nae nashangaa ameyeyuka. Hii ni dharau kubwa anatuonyesha shemeji yetu mtarajiwa”. Rafiki wa “Maso Maso” huku anachekea tumboni ikabidi ajitutumue kumjibu “kapatwa na udhuru tumbo la ghafla la kuharisha ameshindwa kuhudhuria, kanituma nimuwakilishe”.

Shekhe ikabidi aingilie kati kuleta suluhu baina yao kutetea mpunga wake anaolipwa kwa kufungisha ndoa. “Inajuzu ndoa kufungwa kwa kutumia muwakilishi haina shaka kabisa”. Kishingo upande ikawa hana budi bali kukubaliana na hali halisi.

Ndoa ikapitishwa, muwakilishi wa Bwana harusi na mwenzake wakapelekwa upande wanaoswalia wanawake wakambeba mke wao Yasmine na kutokomea nae kutoka viwanja vya pale msikitini. Ukiona manyoya, jua ameliwa tayari. “Maso Maso” alishawatimulia vumbi tayari wana usalama kama kawaida yake, gaidi maluhuni kabisa.

“Tukamate tu hawa washirika wake, halafu tunawabinya na kuwaswaga kisawasawa kwa vipigo takariri watatuekeza yupo wapi huyo mshenzi” aliropoka kwa hasira mmoja wa wana usalama. “Hiyo njia ni kama vile kuitaka asali kwa kupiga manati kwenye mzinga wa nyuki, unaweza kula asali lakini ujiandae kwa manundu usoni. Vita dhidi ya ugaidi inahitaji akili na maarifa na sio nguvu tupu. Usiwe na wasiwasi Kachero Manu yupo Tanga tayari na hata huyu Bibi harusi waliyembeba leo wamepeleka maafa wasiyoyatarajia” alizungumza mmoja wa Maofisa ambaye alionekana ana busara zaidi kushinda wenzake.

Wakakubaliana wafanye msako wa haraka haraka huenda akawa amejichomeka miongoni mwa makundi ya waumini wanaotoka msikitini. Zaidi ya nusu saa za msako hakukuwa na dalili yoyote ya kumnasa “Maso Maso”. Wakafunguliwa na mmoja wa viongozi wa msikiti kila chumba cha ofisi, mpaka chooni walipita kote wakaambulia patupu.

Walipoingizwa kwenye chumba cha kuoshea maiti, wakazikuta maiti kama tatu zimelazwa kwenye meza kubwa. Wakaanza kupekenyua sanda ya kila maiti wakitarajia huenda ameleta ujanja wa kujigeuza marehemu, wakaambulia patupu. Wakati baadhi ya Maofisa wameshatangulia kutoka nje ya chumba, mmoja wao akasita kutoka nje. Akawa anaangaza mule ndani akaona kuna hitilafu kwenye dirisha dogo la juu. Aliliona kama vile limetegeshwa halijajishikiza kisawa sawa. Alivyowaita wenzake wakakagua wakakuta kweli limenyofolewa.

Wakathibitisha ushahidi wa kimazingira ametorokea kupitia dirishani. Haraka haraka wakatoka nje kwenda hospitalini kumsaka huenda amejisweka humo akisubiria mambo yatulie ndio achomoke. Kikosi kikaanza kukimbizana hospitali.

Maarufu mtaani akijulikana kama “Dr.Jembe”, lakini jina lake halisi alilopewa na wazazi wake ni Juma Chembea. Aliajiriwa zaidi ya miaka 8 iliyopita na sasa alikuwa na Cheo cha Daktari Msaidizi “Advance Medical Officer”. Alihamishiwa hospitali ya Sinza miezi kama 9 iliyopita akitokea hospitali ya Tuangoma, Kigamboni. Muda mfupi tu aliohudumu Sinza umaarufu wake ulisambaa kama moshi, Sinza yote utasema ni mzoefu hapo miaka kadhaa. Mbwembwe na mikogo yake ya kutembea ni katika vitu vilimfanya avume kila kona. Kama ni ugonjwa wa pumu basi ulimpata mgonjwa, udaktari ulifika mahali pake.

Kwanza popote utakapomkuta “Dr.Jembe” lazima awe amevaa koti lake jeupe, hata akija kula kwa mama lishe kitaa. Bila kusahau kifaa cha kidaktari, stethoskopu shingoni mwake lazima ining’inie kama wale wacheza ngoma za kisukuma, wanavyojining’iniza nyoka shingoni. Pia umaarufu wake ulivuma kwa vichenchede vya mashuleni kwa kuchoropoa mimba. Hao vichenchede ndio waliompachika jina la “Dr.Jembe”. Wasichana wa shule walikuwa wakinasa mimba, sasa hawana hofu ya kufukuzwa shule wanapeana taarifa za kumsaka Dr.Jembe arekebishe mambo. Lakini toka wiki iliyopita “Dr.Jembe” hakuwa na furaha kabisa, alikuwa kwenye msongo mkubwa wa mawazo. Sio “Dr.Jembe” yule aliyezoeleka wakati wote ni mcheshi na tabasamu fokofoko lisilokauka usoni mwake.

Alikuwa amebakiza wiki mbili tu afunge ndoa yake, lakini michango ya harusi toka kwa ndugu, jamaa na marafiki ilikuwa bado inasuasua. Kwa kupenda sifa kwake alitaka iwe bonge la sherehe ya kufutu ada, na kuacha gumzo. Bajeti ya kamati ya harusi ilipangwa kuwa milioni 50, lakini mpaka Ijumaa hii ya leo makusanyo ya michango kwa mweka hazina ilikuwa inasoma milioni 5 tu. Kila aliyekuwa anaguswa achangie anaruka kimanga na jibu pendwa katika zama hizi, la “vyuma vimebana”. Alikuwa ofisini kwake kimwili tu, lakini kimawazo hakuwepo kabisa. Aliziona dalili kabisa za kwenda kufungia ndoa kijijini kwao, huko Mlembule Wilayani Mpwapwa, Dodoma. Ambapo huko bajeti ya milioni 5 ingetosheleza na chenji kubaki na kuacha gumzo la miaka kadhaa kwa uzuri wa sherehe hiyo.

Huko kijijini kwao, pombe ya kienyeji ya laki 5, watu wangelewa mpaka kutambaa kwa magoti. Disko Joka (DJ) wa kule kijijini elfu 30 tu ingetosha kuporomosha segedansi la nguvu usiku kucha na maspika yake yanayokoroma kama kishindo cha radi. Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kwa mkewe mtarajiwa, Bi Chausiku. Alikuwa nae mpenda ufahari na mbwembwe kama mumewe. Chausiku alipania awanyooshe mashosti zake wa Tandale kuwa ameolewa na mlalaheri. Mashoga zake ambao nao walimkoga kwenye ndoa zao. Hivyo kama “Dr.Jembe” angeleta wazo la ndoa yao kwenda kufungwa kijijini Mlembule, Chausiku angeweza kuzusha varangati na tifu lisilo na ukomo baina yao.

Sasa akiwa kwenye dimbwi hilo la mawazo mbagombago, akasikia mlango wake unagongwa kisha ukafunguliwa. “Samahani daktari kuna mgeni wako” ilikuwa ni sauti ya unyenyekevu ya mmoja wa manesi aliyelambishwa mwekundu wa msimbazi na gaidi “Maso Maso” ili amtafutie daktari mjanja mjanja wa haraka. Yule nesi bila kufanya ajizi akampeleka kwa “Dr.Jembe” akiwa na uhakika mia kwa mia hawezi kumuangusha. “Dr.Jembe” alionyesha kutaka kusitasita maana hakuwa na miadi ya kukutana na mtu yoyote siku hiyo.

“Njagu nini wanataka kuniotea wanitulie mchanga kitumbua changu kutokana na kuchoropoa mimba za mabinti wa watu!” alikuwa anawaza nafsini mwake. Akaamua kuvaa ujasiri wa kiume na kumwambia amruhusu apite. “Habari yako Bwana daktari naomba msaada wako nimenasa” aliongea gaidi “Maso Maso” huku anavuta kiti na kuketi. “Dr.Jembe” aliingiwa na hofu huenda ni majinuni kaingia ofisini mwake, maana “Maso Maso” aliingia anapekua bila viatu. Halafu kanzu yake ilichafuka vumbi katika harakati za kuparamia ukuta.

“Eleza shida yako” alijibu kwa ukali kuonyesha hataki utani kazini na watu wehu. “Maso Maso” akakohoa kidogo kuiweka sauti sawa, kisha akajieleza. “Nataka unisaidie kutoroka maeneo haya ya hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa mahututi ‘ambulance'”. “Dr.Jembe” akaona yale yale ya ukichaa asiyoyataka ndio analetewa na huyu mgeni ofisini mwake.

“Toka toka toka shenzi wahidi nanusu wewe huu muda wa kazi unakuja kuleta masihara” alifoka “Dr.Jembe” mpaka povu jeupe la hasira mdomoni mwake likaonekana huku akisimama kuashiria anataka kwenda kufungua mlango amfurushe nje ya ofisi.

Msongo wa mawazo wa ukosefu wa pesa za kufanya harusi alitaka kuhamishia kwa gaidi “Maso Maso”. “Maso Square The Duduman” hakuwa na muda wa kupoteza tena, alikuwa anakimbizana na muda. Alitambua wakati ni upanga, uchezee ukukate au uutumie vizuri kukata mambo yako unayotaka kuyatekeleza ndani ya wakati. Wakati “Dr.Jembe” tayari ameshasimama, “Maso Maso” akamuwahi haraka haraka akavuta kiti na kufika mlangoni kabla ya daktari na akafanikiwa kufunga mlango. Akachomoa funguo mlangoni kisha akatoa bastola yake ndogo na kumnyooshea mdomo wake “Dr.Jembe”.

“Ukitaka ukubali kutekeleza matakwa yangu kwa hiari yako nikupe chauchau, au ukatae nikudonyoe shaba za kichwani uende kuzimu sasa hivi, memsapu wako abatizwe jina jipya na kuitwa mjane wa marehemu” alitamka “Maso Maso” maneno yaliyoonyesha hatanii anachoongea na ana maanisha kwa vitendo atafanya faya kun fayaa kama atabisha kutekeleza. “Dr.Jembe” alikuwa anacheza tetemo mwili mzima huku jasho jekejeke lile la uoga likimtiririka, taharuki imemkamata. Usifanye mchezo hata kidogo na kifo. Kifo hakimjui kwamba huyu ni mfalme au shamba boi, kila mtu kitamfika, na kila mmoja anakikwepa. Kifo hakina kinga, kusema utafanya hili na lile ili ukiepuke.

“Kama unaogopa kifo namna hiyo usingekuwa unachoropoa mimba za wasichana wetu mashuleni ha ha ha” ‘Maso Maso” alizidi kumchokonoa zaidi ili kumfanya atoe maamuzi ya haraka

Huyu ni gaidi wa mapenzi pia, serikali pia imtangaze kuwa ni mtu hatari kwa akina dada na mabinti zetu mashuleni” alijisemea moyoni akiwa tayari ameshaanza taratibu kutekwa na muonekano wa “Maso Maso” na kusahau kwa muda kazi aliyotumwa. “Maso Maso” alikuwa amevalia singlendi rangi nyeupe kata mikono na bukta nyepesi ya rangi ya kahawia, iliyoacha wazi sehemu kubwa ya miundi yake isiyo na vigimbi kama wale wanaume walima matuta ya viazi wa kule Mbeya.

Alipomuona mkewe tu katika uwanda wa macho yake akanyanyuka kwenye kiti na kwenda kumkumbatia na kumsalimia. “Salaamu aleikum mke wangu, laazizi wangu wa pekee aliyekabidhiwa funguo za moyo wangu na Maulana”. Kachero Yasmine alijikunyata chini ya uvungu wa kwapa ya kushoto ya gaidi “Maso Maso” kama kinda la njiwa aliyefiwa na ***** akipata jotojoto la kwapa. Kwapa ambalo lilikuwa limenyolewa nywele zake lipo kipara na laini kama unyayo wa mtoto mchanga aliyezaliwa juzi. Harufu ya kijashojasho cha kwapa ya “Maso Maso” kilichochanganyika na harufu ya unyunyu wa bei juu sana toka nchi za Ughaibuni, ulikuwa unazalisha harufu mpya ya kuvutia ambayo hajawahi kuivuta maishani mwake tokea azaliwe.

Ilikuwa ni harufu ya marashi si marashi, miski si miski ilikuwa ni baina wa baina. “Atakuwa jini mahaba huyu sio bure, najikuta nampenda kwa kila sekunde inayokatika” alijisemea Kachero Yasmine. Huku bila kujijua akajikuta tayari kwa utundu wake ameshapenyeza viganja vyake laini kama sufu chini ya singlendi ya gaidi “Maso Maso”, na kuanza kupapasa nywele za malaika ya kifuani kwa “Maso Maso”‘ zilizokuwa zinaonyesha zimestawi barabara. “Maso Maso” alielewa anapotaka kufikishwa na Kachero Yasmine, hakutaka kuharibu mambo mesini. Himahima “Maso Maso” akamchomoa mkono kiupole kisha akakibusu kiganja cha mkewe na kumvutia mezani kwenye mlundi wa anuwai mbalimbali za maakuli na mashrabu za kila aina.

Alipokaa chini Kachero Yasmine, na “Maso Maso” nae akaenda kukaa kiti mkabala na mkewe huku anamkazia macho, kitendo ambacho Kachero Yasmine alikuwa anaona aibu na soni iliyopitiliza mipaka. Pale pale mezani “Maso Maso” akabinya kengele iliyopo chini kidogo ya meza ile. Ilipolia tu kengele baada ya dakika moja wakajitokeza watumishi wapya machoni mwa Kachero Yasmine wapo wawili. Kila mmoja akabeba sahani yake na kuwafuata waajiri wao kuwauliza maakuli wanayotaka. “Mtukufu Seyyidat mke halali wa kiongozi wetu utapenda kula nini na kunywa mashrabu gani usiku huu”? aliulizwa Kachero Yasmine kwa sauti nyororo ya kubembelezwa na yule mtumishi. “Nipatie sharubati na kipande kimoja cha keki” alijibu kwa kujitutumua Kachero Yasmine, huku moyoni akilaani na kuujutia mchezo alioamua kuucheza.

Wote wakaandaliwa chakula kisha wale watumishi wakawaacha peke yao ndani ya mesi ile yenye kila kitu cha kifahari kuanzia vikombe, sahani, visu, vijiko na masufuria ya kisasa ya kuhifadhia chakula. Kila mmoja akawa ametingwa na harakati za kushibisha tumbo lake. Alikuwa ni “Maso Maso” aliyewahi kumaliza, kisha akamsubiria mkewe amalize, akaenda kumnyanyua kutoka kitini na kumpeleka hadi kwenye sinki la kunawia maji na kumnawisha kisha akamfuta na kitambaa safi.

“Maso Maso” akarudi mezani akachukua sahani maalumu iliyotengwa na kukatwa nyama steki iliyochomwa kwa ustadi na kupakwa vumbi vumbi jeupe juu yake. Akafungua chupa ya tomato sosi akanyunyizia na kuanza kutafuna vipande kama viwili kwa kutumia uma, kisha akaweka ile chupa ndogo ya tomato ndani ya sahani akashika sahani mkono wa kulia huku mkono wake wa kushoto ameuviringa kwenye kiuno cha Yasmine. Akawa anaukandamiza shadidi kwa kukitomasa kiuno cha Yasmine huku kichwa cha Yasmine na nywele zake nyingi za shombe shombe la Kipemba zimeegemea kwenye bega la “Maso Maso”.

Tayari “Maso Maso” alikuwa ameshampa shakawa kubwa ya joto la mapenzi Yasmine ambaye dalili zilionyesha kabisa hajiwezi tena, ameshamfanyia ugaidi wa mapenzi hapindui tena. Lakini karata muhimu ya kukamatwa kwa “Maso Maso” kwa namna ramani ilivyochorwa na Bosi wake Kachero Manu alikuwa ameishikilia Kachero Yasmine. Vinginevyo watatwanga maji kwenye kinu. Wakawa wameshafika chumbani kwao, “Maso Maso” akafungua mlango kisha wakaingia wote chumbani na kufunga mlango kwa funguo.

Yasmine alivyoingizwa chumbani alikuwa nusu chizi wa mapenzi tayari. Hasa ukichukulia alikuwa hajawahi kuchapwa na fimbo ya Musa tokea azaliwe. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza maishani kujifungia na mwanaume shababi, ghulamu mwenye viwango vyake kama “Maso Maso”

Akashajiika kujaribu walau leo tu siku moja aikonge na kuisuuza roho yake, kisha baada ya hapo akili ikishamkaa sawa atatekeleza majukumu yake. “Kazi na dawa, ananiona nani bwana kama nimefaidi penzi la gaidi wa mapenzi” alijisemea moyoni mwake Yasmine wakati “Maso Maso” amemuachia kiuno na kwenda moja kwa moja pembezoni mwa kitanda na kuvua singlendi yake nyeupe. Yasmine akaingia kwenye chumba cha kubadilishia nguo kinachoelekea bafuni. Alitaka achague vazi ambalo litampendezesha zaidi, azidi kuikoroga akili ya “Maso Maso” ili wote wawe nusu vichaa wale tunda la uzima kwa shemere bila kuwaza.

“Maso Maso” alivyobaki peke yake akaenda kwenye redio yake ya kisasa na kuweka santuri ya muziki laini iliyokusanya nyimbo za mahaba anazozipenda. Kisha akaiendea sahani yake ya vipande vya nyama iliyonyunyiziwa unga unga wa miti shamba toka nchini Congo, maarufu kama “vumbi la Congo”. Unga ambao una uwezo wa kumfanya kidume adumu kwenye tendo la ndoa kwa saa nyingi bila kuchoka. Yasmine anatokeza tu chumbani anasikia mziki mororo uliochujwa kwenye vyombo vya kisasa. Wimbo uliokuwa hewani ulikuwa ni ‘My heart will go on’ ulioimbwa na mwanamuziki mkongwe ‘Celine Dion’. Kwa namna ulivyokuwa unaimbwa utasema umetoka hivi karibuni kumbe ni wa tokea mwaka 1997.

“Maso Maso” alikuwa sasa amejilaza kitandani anamuangalia mkewe anavyokuja huku kifua chake kipo wazi, vile viriba viriba vya umbo la mstatili ambavyo vijana wanavitafuta kwa kukesha kwenye majumba ya mazoezi “six packs” vilikuwa vimejichora tumboni mwake vinaonekana dhahiri shahiri hata mtu mzima mwenye uoni hafifu unaotokana na uzee. Yasmine alivyoviona vile viriba vya tumbo la “Maso Maso” ndio vilimzidisha hanjamu yake ya kufanya mapenzi.

Yasmine alikuwa amevaa kitopu cha rangi ya nyekundu ambacho kiliyaacha mabega yake meupe ya Kipemba yakiwa wazi, ndani ya kitopu kile chepesi hakukuwa na sidiria kwani “Maso Maso” aliweza kuziona chuchu za Yasmine zikiwa zimesimama dede kama zinataka kukitoboa kile kitopu na kukifanya kijivute kwa mbele katika harakati za kuzuia mtoboko. Chini Yasmine alikuwa amejifunga mtandio mwepesi wa rangi ya maziwa ambao ulikuwa umepambwa na maua ya rangi ya zambarau. Umbo lake namba nane ya ukweli lilikuwa sasa limejichora ipasavyo kwa vivazi vile alivyovaa. Yasmine alikuwa mzuri haswa, sio vivazi hivyo ndio vilivyompaisha aonekane mlimbwende bali ni uzuri halisi aliojaliwa na Subhana. Kama kuna orodha ya wanawake 10 bora Afrika waliopata kujaaliwa uzuri huo wa shani na Rabuka, basi Yasmine alikuwemo ndani ya 3 bora.

Mziki wa taratibu uliokuwa ukipigwa ulizidisha hisia za kufanya tendo la ndoa baina yao. Yasmine katika kumchanganya akili “Maso Maso” akawa anakatika mauno taratibu kwa ufundi mkubwa kufuatisha midundo ya muziki huo.

Uzalendo ukamshinda “Maso Maso” akagutuka kitandani na kuanza kumfuata mke wake pale anapocheza. Mwanzoni mkakati wake ilikuwa hakutaka kucheza mechi yake ya kwanza katika usiku wa fungate kwa papara alijua wazi kuwa anapaswa kumfanyia haki mtoto mbichi kama Yasmine ampagawishe kisawasawa katika uwanja ule wa fundi seremala wa futi 6*8.

Yasmine sasa alikuwa anakatika aste aste huku amempa mgongo mumewe huku akitingisha makalio yake ambayo hakunyimwa alipewa ya kutosha kiasi chake. Alipomfikia mkewe kwa macho yake yenye ithibati ya ‘TBS’ kwa kujua kuchagua watoto wazuri akaanza kuufanyia inspeksheni vizuri ule mtandio mwepesi aliojifunga chini pasi na kuushika. Uchunguzi wake ukazaa matunda kwa kujua ulipoanzia kufungwa ule mtandio. Haukuwa umefungwa imara ndindandinda la hasha. Ulikuwa umeegeshwa tu, na kushindiliwa pindo lake ndani ya chupi ya rangi nyeupe.

Yasmine alifanya hivyo makusudi ili asipate tabu mumewe kuuvua. “Maso Maso” akafanikiwa kuingiza kidole kwenye pindo ya mtandio na taratibu kwa ncha ya vidole vyake akafanikiwa kulifumua fundo hilo. Mtandio huo ukaanguka chini mwaaaaa sasa mambo yakawa hadharani bila mficho. Makalio au vijana wa Mjini wanaita ‘Chura’ wawili wa mviringo walikuwa wamebebwa ndani ya chupi nyepesi. Akaanza kupapasa makalio kama anavyopasa mpiga kinanda mahiri kwenye kazi yake. Yasmine akageuza uso wake kumtazama mumewe kwa jicho la mahaba huku anatabasamu kuonyesha kufurahishwa na mpapaso huo wa kitaalamu wa makalio yake. Macho yake makubwa yalikuwa yamelegea kama mtu aliyekunywa vidonge vya usingizi halafu anailazimisha kesha kwa kuyalazimisha macho kufunguka.

“Najiona ni mwanaume mwenye bahati ya kipekee katika sayari hii ya dunia kuwa na mke mrembo kama wewe Yasmine” alijikuta “Maso Maso” anaropoka maneno hayo ya mahaba baada ya kushajiishwa vilivyo na mapenzi sheshe yale bulibuli toka kwa mkewe Yasmine. “Ahsante my love nakupenda sana” alijibu Yasmine kwa sauti ya kivivuvivu huku nafsini mwake kukiwa na majuto, kwanini alikubali kazi ngumu inayompa majaribu, anayoshindwa kuvumilia.

Walikuwa wakiendelea kucheza muziki ule kwa mtindo wa kugandana “zero distance” na kwa mahaba makubwa. Laiti ungewaona wanavyocheza kiustadi mkubwa usingekubali kuwa huyu “Maso Maso” ni mfiadini. Kumbe wachamungu wakiwa hadharani tu mbele ya macho ya watu lakini wakiwa sirini wanayajua wao na Mungu wao wanayoyafanya. Yasmine sasa alikuwa amebakiwa na chupi tupu iliyositiri kipochi manyoya chake na chura wake. Huku macho yakiwa yamemtoka “Maso Maso” hayabanduki kuangalia mapaja meupe ya binti wa Kipemba kwa uchu wa fisi.

Walikuwa wakiendelea kucheza muziki ule kwa mtindo wa kugandana “zero distance” na kwa mahaba makubwa. Laiti ungewaona wanavyocheza kiustadi mkubwa usingekubali kuwa huyu “Maso Maso” ni mfiadini. Kumbe wachamungu wakiwa hadharani tu mbele ya macho ya watu lakini wakiwa sirini wanayajua wao na Mungu wao wanayoyafanya. Yasmine sasa alikuwa amebakiwa na chupi tupu iliyositiri kipochi manyoya chake na chura wake. Huku macho yakiwa yamemtoka “Maso Maso” hayabanduki kuangalia mapaja meupe ya binti wa Kipemba kwa uchu wa fisi.

Alimuweka kwenye wakati mgumu sana Yasmine, huku anabinywa binywa maembe dodo yake, kifuani yaliyochongoka na “Maso Maso”. Matiti ambayo yalikuwa yanatomaswa mithili ya mteja anayetaka kuchagua embe bora la kula sio rojo la juisi. Yasmine akaanza kuhema juu juu kama mtu aliyepandisha Jini subiani na kuanza kunena kwa lugha isiyoeleweka. Kipemba si Kipemba, Kichina si Kichina tabu mtindo mmoja. Alikuwa tayari ameshaingia kwenye kumi na nane ya lango la timu pinzani, akiguswa tu kidogo na beki refarii anafunika penati bila ajizi.

“Maso Maso” alishaona dalili zote za kuvikwa taji la ushujaa dakika 90 zikikaribia kuanza za mechi hiyo kali ya kuvunja springi ya meli. Ila hakutaka kuharakisha kuanza kwa pambano, akazidisha mbwembwe na vikorombwezo ili kuleta amsha amsha na mashamu mashamu kwa wachezaji wa pande zote mbili. Akaanzisha uchokozi wa mieleka ya ulimi kwa ulimi akaanza kudendeka nae.

Yasmine akajikuta hana nguvu tena, hawezi kujizuia akamuachia “Maso Maso” awe kama rubani wa ndege na yeye kubaki kuwa maamuma tu, asiyejua ndege rubani anaipeleka wapi na kituo cha Nyegezi kipo wapi na atashushwa kwa mitindo ipi, na wala hakutaka kujua tena, alishakuwa kichaa wa mapenzi.

Tayari alianza kuishiwa nguvu huku vidole vyake Kachero Yasmine vimeanza kutambaa juu ya kufuli alilovaa gaidi “Maso Maso” kuanza kupimisha urefu na saizi ya bakora ya gaidi. “Maso Maso” alivyoona hivyo, akajua tayari kituo cha Nyegezi wanakaribia kufika abiria anahitaji kushushwa. Akambeba mkewe kwa mikono miwili mpaka kitandani akamtupia juu ya uwanja huo wa godoro la “Super Banco Original”, uwanja wa tokea enzi za Mababu na Mabibi zetu, ulioleta mabilioni ya watu waliomo ulimwengu hivi sasa. Yasmine alivyotua tu akajilaza kifudifudi huku ameibana miguu wala hatikisiki.

Yasmine alikuwa kama yupo ndotoni, nusu mfu nusu hai, alikuwa amepewa mambo adimu aliyokuwa anayakosa kipindi chote cha miaka 28 ya uhai wake. “Maso Maso” alivyomuona Yasmine kama anataka kupoteza fahamu, akaenda kwenye friza ndogo ya chumbani akachukua vipande virefu vya barafu kama vinne. akaviweka kwenye sahani ndogo akapanda navyo vile vipande kitandani.

Yasmine alikuwa anashuhudia hayo yote lakini anashindwa kuzungumza, alikuwa anaona ni mambo mapya kabisa kupata kutokea machoni mwake, daktari anataka kufanya operesheni ya kumpasua mgonjwa kwa kutumia vipande vya barafu, hajawahi kusikia hii hata kwa mashoga zake wanavyosimuliana huko saluni.

Akajisemea nafsini mwake “ama kweli ufundi wa mapenzi kuzidiana duniani”. Alivyofika navyo vile vipande akakibana kipande kimoja kwa ncha ya meno yake ya mbele kisha akaanza kumsugua nacho kuanzia chini ya maoteo ya nywele kisogoni anashuka nacho hadi kwenye mfereji wa uti wa mgongo na kushuka nacho chini karibia na pingili ya mwisho ya uti wa mgongo kisha anapanda nacho tena juu.

Huu mchezo wa barafu wa panda shuka ulisababisha Kachero Yasmine arudiwe na fahamu zake akaanza kujinyonga nyonga na kupwiripwita kama nyoka aliyemwagiwa mafuta ya taa. “Maso Maso” macho yake yalimwiva na kuwa mekundu kama kavuta bangi, alikuwa mlaini kwa Yasmine huwezi kudhania ni yule anayewanyima usingizi zaidi ya Watanzania milioni 55 hawalali kwa raha, hawali wakanenepa kwa sababu ya ufedhuli wake wa matendo ya kigaidi.

Akalichukua dekio la mdomoni lile linaloonja ladha ya utamu wa chakula na kuanza sasa kupangusa maji ya kwenye kisima kilicholoweshwa tepetepe juu ya chupi ya Kachero Jasmine. Dekio lilipotua tu kwenye antena Kachero Yasmine alishindwa na uvumilivu, alipiga makelele huku akitaja jina “Maso Maso” halisi, “Masoud Masoud My love…Weeeeeh utaniua mtoto wa mwenzio”. Jambo ambalo “Maso Maso” lilimshtua na kumfanya asite kuendelea na zoezi la kupiga deki.

“Masikio yangu yanaleta taarifa sahihi au ninaota mbona ananitaja kwa jina langu halisi la Masoud Masoud, amenijulia wapi kwa jina hili wakati jina feki la kufungia ndoa ni Abu Nufeil!” ni swali alilokuwa anajiuliza ndani ya sekunde kadhaa “Maso Maso” bila kupata jibu. Wakati huo huo yupo kwenye fikra hizo simu yake ya upepo ya tahadhari anayoitumia “Maso Maso” kwa dharura ikaanza kupigwa.

Ikabidi anyanyuke kitandani na kwenda kuichukua simu kwa ajili ya kuipokea. “Hallow Hallow…ovaaah….!”, ikabidi atoke haraka nje ya chumba ili Yasmine asisikize maongezi yake. Alivyotoka chumbani ikawa nafuu kwa Kachero Yasmine amenusurika kuvunjwa kizinda chake cha ubikira na gaidi “Maso Maso”. Kama “Maso Maso” angeendeleza utundu wake angefanikiwa kumla Kachero Yasmine katika usiku huo wa fungate.

Na yeye fahamu zikaanza kumrudia sasa kengele ya tahadhari ikalia kichwani mwake. “Kuna mazungumzo gani ya siri yaliyomfanya hata aache kuendelea na moja ya starehe tamu za dunia!” alijiuliza Kachero Yasmine. “Au wamenigundua kuwa mie ni shushushu hivyo wanampa taarifa?” Akakurupuka haraka kitandani na kukaa, anapanga na kupangua mipango ya kujiokoa kwenye mdomo wa mamba aliojiingiza kwa hiari yake mwenyewe.

Himahima akaenda mpaka pale ilipo sasa sahani ya nyama na sosi ya nyanya. Akachukua ile sosi ya nyanya akafunua chupi yake nyeupe akaminyia sosi ya kutosha tu, kisha akaifunga chupa na kurudi kitandani mbio mbio. Ile anatua tu kitandani hamadi! na “Maso Maso” huyo anarudi chumbani.

Sasa Kachero Yasmine alikuwa na akili timamu anamthaminisha “Maso Maso” bukta yake ilikuwa imetuna kama vile ameficha mguu wa mtoto mdogo mwenye umri wa nusu mwaka. “Aisee…leo mbona chamoto ningekionja, “Maso Maso” ana uume mkubwa utasema amechanjia dodoki..!.Leo huyu angenitoboa kizazi huenda ningekimbizwa Hospitali ya Mkoa ya Bombo, hawa wengine hawatakiwi kufanyiwa majaribu, ukiwabipu wanakupigia” alijiwazia Kachero Yasmine huku akijiona ana bahati sana kuepuka kucheza mechi ya kitandani na “Maso Maso”. Alivyoingia ndani ya chumba akaenda moja kwa moja kwenye zile nyama zake za madawa ya kuongeza nguvu za kiume na kuanza kuzishambulia tena.

Alivyotafuna vipande kadhaa vya nyama ile akaanza kuja kitandani alipojilaza Yasmine kama mbogo aliyejeruhiwa risasi na jangili. Yasmine hakutaka tena amruhusu afanye utalii wa mwili wake tena alishaijua shughuli ya “Maso Maso” ni gaidi wa kila sekta.

Alivyotaka kumgusa tu, Yasmine akaaanza kupiga kelele. “Aaaah Aaah nakuf…aaaah tumboo langu”. “Maso Maso” akashtuka na kuanza kumsaili tatizo lililompata. “Umepatwa na nini mke wangu mpendwa, nimuite daktari”?.

“Hapana ni ada tu za wakubwa za mwezi, wekundu wa msimbazi wamekuja wamelowesha kiwanja, hamna mechi tena wiki nzima mpaka nijitwaharishe, sasa huwa tumbo linaniuma hiyo hali ikinikuta” alifafanua kwa lugha ya mafumbo ambayo “Maso Maso” alielewa nini anachomaanisna mke wake baada ya kuiona chupi imelowa damu.

Kumbe usilolijua ni kama usiku wa giza, kachezewa picha la kihindi bila mwenyewe kufahamu. Biashara ikawa imeishia hapo kwa siku hiyo. “Maso Maso” akakumbuka kuitwa kwa jina la “Maso Maso” wakati mizuka ya mahanjamu imempanda Kachero Yasmine. Ikabidi amuweke kitimoto kwanini anamuita jina hilo.

Kachero Yasmine akakataa katakata kulijua jina hilo la Masoud Masoud. “Mie mume wangu nakujua kwa jina la Abu-Nufeil na ndio limeandikwa kwenye cheti cha ndoa yetu hilo ulilotaja ndio kwanza nalisikia kwako” alijitetea Kachero Yasmine huku akijilaumu sana kwa uzembe ambao unaweza kumgharimu maisha yake.

Kwa jinsi alivyomaliza viapo vyote vilivyoambatana na vilio feki, “Maso Maso” alimuelewa mkewe akajipa udhuru mwenyewe kuwa huenda alisikia vibaya. Akamuamini akaleta dhana ingine kuwa huenda huyo Masoud aliyekuwa anamtaja wakati anamsugua antena, ni mpenzi wake wa zamani ambaye alikuwa anamfikisha vilivyo.

“Maso Maso” aliaga siku hiyo hiyo kutokana na simu ya upepo aliyopigiwa kuna viongozi wa “Al-shabaab” toka Somalia walihitaji kuonana nae mkutano wa dharura. Ila kwa mkewe aliaga kuna mzigo wa biashara anatakiwa aende kuuangalia Mombasa hivyo hana budi ang’oe nanga usiku huo.

Yasmine akazuga kama na yeye anatamani sana afuatane nae, lakini kiuhalisia alitamani abakie hapo nyumbani ayasome mazingira vizuri. Hivyo usiku huo huo majira ya saa saba usiku “Maso Square The Duduman” akatimka zake, na kumuacha mkewe Kachero Yasmine akiwa amebaki makazi yake mapya na kundi la watumishi na masuria wa kumhudumia.

Kachero Manu katinga Kijiji cha Majimoto kuwafukunyua Magaidi

“Loooh salaleee…hasara tupu umepata wewe Babu, umelala mchana kweupeee mwenzako natakata tu, limeshaisha hili huniwezi wewe Mzee achana na bao tukuchangie pesa ukaperesheni busha hilooo” watazamaji wote wakaangua kicheko cha kwa kwa kwa, kumcheka Mzee Shadhili anavyotaniwa na mpinzani wake Kachero Manu.

Mzee wa watu alibaki kimya kama kumwagiwa maji baridi, anatafakari namna ya kuzichanga vyema kete zake za mchezo wa bao aweze kumgaragaza mshindani.

Ghafla Mzee Shadhili akaanza kupiga makelele “Sefu eeeeh…Sefu….ongezaa kikombe cha kahawa limeisha hili, aingie mwingine” alijitapa baada ya kufanikiwa kumsoma mpinzani wake na kugundua namna ya kumfunga mchezo huo uliokuwa una ushindani wa hali ya juu na kuteka hisia za mashabiki wao. Mzee Shadhili alisema maneno hayo huku anagida kahawa kwa mkupuo mmoja akaweka kikombe chini na mbwembwe na kuanza kuzisambaza kwa madaha kete zake kwenye mashimo ya upande wake wa kaskazini. Mzee Shadhili ndio alikuwa mbabe wao wa mchezo wa bao kijiji kizima cha Majimoto kilichopo jirani na mapango ya Amboni. Ndani ya wiki tatu tu alizokaa kijijini hapo Kachero Manu alijipambanua kama mshindani wa kweli wa Mzee Shadhili.

Kachero aliingia kijijini kwa gia za msimamizi wa mashamba ya zao la hiliki ya mwarabu mmoja anayekaa Tanga mjini. “Al-shabaab” walivyomtoa kule kambini Dibungo walivyomleta huku Amboni lengo lilikuwa ni kuchunga usalama wao pale kijijini. Alitakiwa anuse na kupeleleza kama kuna wanakijiji wanawafahamu na kuwachukulia vipi.

Walijua sasa serikali itakuwa wanafanya bidii ya kuwasaka kwa bidii na maarifa hivyo nao walitakiwa waweke watu makini kama Komandoo aboubakr (Kachero Manu). Haya yalikuwa ni kinyume kabisa na matarajio ya Kachero Manu. Alijua kuletwa kwake Amboni anakuja kuwekwa karibu na gaidi “Maso Maso” ili iwe rahisi kuandaa hujuma za kumkamata.

Mpaka sasa pia alikuwa hana mawasiliano kabisa na Kachero mwenzake Yasmine kinyume kabisa na matarajio yao kuwa watawasiliana kwa njia waliozoelekezana kwa haraka zaidi. Kuna wakati alikuwa anahisia mbaya kuwa huenda Yasmine ameuliwa na magaidi. Hisia ambazo kuna wakati usiku zilimletea njozi za mang’amung’amu na majinamizi. Anaota Yasmine amekamatwa, amefungwa minyororo kwenye viguzo anakatwa shingo yake kwa kuchinjwa na jambia lenye makali. Wakati mwingine anaota amebebwa na maharamia wa “Al-shabaab” kwenye meli kubwa na kutoswa katika kina kirefu cha bahari baada ya kufungwa shingoni jiwe zito. Pia mawazo juu ya mkewe nayo yalikuwa yanamsumbua.

Ambaye baada ya kuokolewa kwa watekaji aliomba ruhusa kazini likizo ya dharura na kurudi kwao Mwanza kwa wazazi wake kutuliza mawazo. Sasa alikuwa ndio anakaribia kurudi jijini Dodoma na hana mawasiliano nae kabisa. Alishaanza kutaka kuanza kukata tamaa ya kumkamata “Maso Maso”. Alikiri kweli magaidi wapo makini na usalama wao.

Angewashangaa sana mtu mgeni kama yeye wamuweke karibu na kiongozi wao mkuu tegemeo, Afrika Mashariki na Kati, “Maso Maso”. Katika harakati za kutaka kupoteza mawazo na kutengeneza fikra mpya za namna ya kumkamata “Maso Maso” bila msaada wa Yasmine akaamua wakati mwingine ajichanganye na raia wa mtaani, achezee nao pamoja mchezo wa bao ambao alikuwa anaumudu vilivyo.

Pia ajichanganye nao kwenye vijiwe vya kahawa kupata mpya mpya za pale kijijini. Haikumchukua muda wa siku nyingi kupata jina na kujitokeza kuwa mshindani mkuu wa Mzee Shadhili katika mchezo huo wa bao uliosambaa sana katika nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania Bara (Tanganyika), Zanzibar na Kenya.

Kweli bana baada ya muda mfupi Kachero Manu akawa amekubali kipigo cha pili mfululizo toka kwa Mzee Shadhili. Ikabidi anyanyuke kiunyonge ampishe mpinzani mwengine. “Aingie mwingine mbona mnaogopa ogopa, nimekuja kugawa dozi hapa huyu Manamba mwacheni aende kijiweni kwa Sefu akamsaidie kuuza kahawa” alizungumza kwa kebehi na majigambo ya ushindi mzee Shadhili.

“Aah…leo umeniotea tu, ngoja nitulize bongo yangu narudi sasa hivi usinikimbie tu” Kachero Manu akajitetea kwa kipigo alichochapwa. Akawa anajivuta kwa unyonge kuelekea kijiweni kwa Sefu kwenye kahawa mkabala na pale wanapochezea mchezo wa bao. Alianza kwa kuwasalimia, “Asalaamu Aleikum, Je Waungwana hamjambo?.

Baadhi yao wakamjibu “Waleikum salaam Mtwana wajisikiaje na hali weye”, huku wengine wakiendelea na maongezi yao ya siasa yalikuwa yamepamba moto. “Naam mie ni Mtwana wala sibishi ila nyie Bwana ni wavivu hamtaki kazi ngumu kabisa, pale shambani kwangu vibarua wa kulimia hiliki wanatoka Kigoma nyie mpo tu mnasogoa siasa sijui shusha Tanga, pandisha Tanga safari iendelee nakusikieni tu toka nipo kulee kwenye bao” aliwapiga madongo baada ya kumtania kwa kumuita Mtwana.

Soga zikaendelea zilizoamsha vicheko, huku wanasogezana Kachero Manu apate nafasi ya kukaa kwenye benchi. Alipokaa tu akapewa kikombe cha kahawa ns kashata za ufuta ili soga zizidi kuchangamsha kijiwe.

Ghafla wakiwa wamezama kwenye mazungumzo ya hapa na pale ya kusogeza muda jua lizame, likapita gari rangi nyeusi ambalo hakuna aliyeweza kudhibiti aina ya gari kutokana na mwendo wake wa kasi. Lilikuwa linayoyoma kutokomea mashambani. “Hili gari kama linawahisha mgonjwa hospitali” alichokoza mada mpya Kachero Manu makusudi kwa matarajio huenda akaambulia chochote kitu. Kwa majasusi kwao chochote mbele yao ni fursa. Na kweli uchokonozi wake ulizaa natija aliyokuwa anaihitaji.

“Gari lile habari zake Bwana mtafute dereva bodaboda anaitwa Juma Mavideo, huyu aliyetoka sasa hivi kumletea mkaa Bwana Sefu! ” alijibu mmoja wa wana soga pale kijiweni. “Yaani kijiji chetu sasa wageni wametapakaa, huyo wa kwenye gari lililopita ni Mwarabu mmoja, lakini Juma Mavideo anasema nyumba anayohisi anakaa haiendani na hadhi yake, ni mashambani ndani ndani hukoo” alizungumza mwingine.

Kachero Manu alivyoangalia muda kwenye saa yake ya mkononi ulikuwa unasoma saa 12:00 jioni, ikabidi aage kimtindo, akiwaacha wameendelea kukaa mbumbumbu wanaukaribisha umaskini bila kujijua kwa soga zao zisizo na faida. Alichomoka ili akamtafute huyo Juma Mavideo huenda akaambulia chochote kitu. Hasa hapo aliposikia yule aliyewapita na gari la kifahari ni mtu mgeni, mwarabu, anatembelea gari la thamani lakini nyumba anayoishi haiendani na hadhi yake.

Ilimchukua robo saa tu, Kachero Manu kumtia mkononi Bwana Juma Mavideo. Alikuwa anaitwa hivyo kutokana na shughuli yake ya ziada mbali ya bodaboda ilikuwa ni kurekodi video za matukio ya sherehe pale kijijini. Alikuwa maarufu kwa shughuli hiyo hata ukimuuliza kwa watoto wadogo wanakuonyesha. Alichofanya ni kwenda kijiwe cha madereva bodaboda kumuuliza.

“Habari za sasa hivi vijana, samahani Bwana Juma Mavideo nimemkuta…!” aliuliza Kachero Manu pale kijiweni. “Daah una bahati mbaya umepishana nae muda sio mrefu kaelekea kwenye mishe mishe zake nasikia kuna ngoma ya sherehe ya kukesha kumtoa mwali kesho hapo juu mashambani” alijibu mmoja wa wale madereva bodaboda huku wengine wakiendelea na maongezi yao.

“Nikimbize mara moja basi nina shida nae kubwa sana” akaomba Kachero Manu. Bila kufanya ajizi yule dereva bodaboda akaingurumisha ikakubali, wakakwea na kuanza kukata vichochoro na vijia vidogo vidogo kuelekea huko ngomani. Baada ya muda wa robo saa na ushee hivi wakawa wameshawasili kwenye eneo la tukio.

Kulikuwa ni eneo lililojengwa nyumba zile za mbavu za mbwa. Ngoma ya baikoko ilikuwa hewani inarindima kwenye uwanja huku kigiza sasa kikianza kunyemelea eneo lile. Inaonyesha sherehe hizo zilianza kurindima tokea jua la mtikati kutokana na wachezaji wake kuwa wamejashuka vilivyo huku wamechafuka vumbi haswa. Ngoma hii ilikuwa imeanza kujipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania kutokana na manjonjo yake wakati wa uchezaji wake. Kachero Manu akamalizana malipo na yule dereva bodaboda kisha akaanza kumsaka Juma Mavideo. Wakati anapasua makundi ya watazamaji alikuwa anashuhudia ustadi na uhodari wa ukataji viuno kwa wachezaji wa ngoma hiyo. Ikawa ni kivutio kikubwa sana kwa mtazamaji yeyote na mpenzi wa ngoma za asili.

Viuno vya akina dada hao vilifungwa kanga moja tu, vilikuwa vinazungushwa mithili ya kukosa mifupa kiunoni. Kuna wakati wapiga ngoma walibadili midundo ngoma ikawa inageuka kuwa mduara wa segere kama ilivyozoeleka. Mirindimo ya ngoma hiyo sambamba na kiuno cha jimama mmoja kilichokuwa kikizunguka kama feni mbovu iliyokata mota vikayafanya macho ya Kachero Manu yamkodolee kwa muda kama ujuavyo macho hayana pazia.

Lile jimama tinginya tinginya lilivyomuona Kachero Manu amelikodolea macho ndio likawa linazidisha kuzungusha kiuno kiuchokozi na kwa madaha kujionyesha kwa watazamaji kuwa amejaa tele kama pishi la mchele huku anamuangalia kwa tabasamu pana, na macho yake anarembua na kumkonyeza. Ni kana kwamba anamwambia lugha ya ishara Kachero Manu, ni wewe tu kama unataka usijivunge tuongee biashara, tukamalizane. Kachero Manu akampuuzilia mbali na kuendelea kuangazaangaza kumsaka mlengwa wake. “Huyu jimama anadhani mie ni mwanaume wa jicho la nje..!” alijisemeza moyoni mwake Kachero Manu.

Mungu si Athumani ghafla bin vuu, Juma Mavideo huyu hapa mbele ya Kachero Manu, anainama katika mapozi tofauti tofauti anamalizia malizia kupiga picha za mwisho mwisho kabla giza halijashitadi. Kachero Manu, akamgusa begani na kumnong’oneza sikio lake la kushoto “Juma nakutafuta sana nakuomba chemba kidogo”.

Juma akageuka kumuangalia anayemuita kisha akajibu, “nisubiri kidogo nikadake mshiko wangu wa advansi ya kazi nakuja sasa hivi usijali”. Kachero Manu akakubaliana nae akajivuta pembeni kidogo na ule umati wa watu uliokuwa bado unaserebuka kwa nguvu tena sasa kwa nguvu ya pombe ya kienyeji, kama ilivyo pombe ya ngomani ni “litekela mwene”, unajichotea utakavyo haina kipimo cha unywaji.

Pombe hizo za kienyeji zilikuwa zimejazwa furifuri kwenye ndoo za plastiki. Jambo hilo la watu kuwa wamebobea kwenye ulevi lilimfurahisha Kachero Manu kwa sababu ingepunguza umakini wao wa kujua nani kamchukua Juma Mavideo. Kila wakati macho ya Kachero Manu yalikuwa juu juu huku na huko pia anaangalia muda kwenye saa yake ya mshale. Haikuzidi hata dakika kumi Juma Mavideo huyu hapa. “Salaamu aleikum kaka yangu, niambie shida yako” zilikuwa ni salamu zake kijana Juma huku akimpa kiganja cha mkono wa kulia kachero Manu. Wakashikana mikono kwa upendo huku wanajongea pembeni kuanza mazungumzo yao.

“Kuna mtu ana madini ya dhahabu ya dili katoka nayo Nyarugusu huko sasa kuna mwarabu katupita na gari moja jeusi pale kijiweni kwa muuza kahawa ulipoleta gunia la mkaa jioni, sasa nikiomba unipeleke nimeambiwa wewe unaweza kuwa unapajua” alijieleza Kachero Manu huku macho makavu kumbe anaongea uwongo mtupu akimjaza pampu ya tamaa ya pesa kijana wa watu.

Juma Mavideo kutajiwa mzigo wa dhahabu akili zikampaa, akashindwa hata kuuliza maswali ya udadisi yeye akaanza kuwaza mgao tu. “Ahaaa vizuri, si unamaanisha lile gari rangi nyeusi eeh la polisi?” aliuliza Juma Mavideo. Swali ambalo lilikuwa mtihani kwa Kachero Manu.

“Nadhani ni hilo hilo labda mie nachofahamu kuna mwarabu nimeelekezwa anatumia hiyo gari ndio taita wa madini nimeambiwa” alijibu Kachero Manu huku akisubiria mrejesho toka kwa Juma. “Itakuwa huyo huyo Bwana maana nishakutana nao kama mara mbili kule ng’ambo ya mashambani, ingawa siijui nyumba rasmi anayoishi ila tutafika tu, na huku hamna magari yanakujaga sana” alijieleza Juma kwa kujiamini huku anatikisa funguo zake za bodaboda yake kwa vidole vyake vya mkono wa shoto. “Sasa wewe unahitaji pesa kiasi gani kwa kunipeleka huko? “aliulizwa swali na Kachero Manu ili kuzidi kumsukasuka ajue ni kazi ya pesa ndefu atalipwa sio porojo za paukwa pakawa.

“Sasa kaka yangu wewe jichinje mwenyewe kisu nakuachia nakusikiliza tu najua hatuwezi kushindwana sie sote watoto wa kiumeni. Maana hapa umenichomoa kazini na bado ilikuwa nirudi tena kijiweni kwenye mishe zangu za bodaboda kutimiza hesabu yangu ya siku”, alizungumza kimashaufu na kutingisha kiberiti kujionyesha ni mtu muhimu sana kufanikisha mchongo huo wa pesa ndefu, na bila yeye mambo hayatajipa.

Baada ya mvutano wa hapa na pale wakafikia makubaliano. Safari ikaanza ya kuelekea huko.”Ila inabidi tupite kwenye kidebe tukajaze mafuta si unajua huku hatuna vituo vya mafuta” alisema Juma wakati tayari kachero Manu ameshakwea nyuma ya pikipiki. “Utaniacha pale wewe kajaze halafu unipitie si unajua nina mali adimu sitakiwi kuonekana ovyo” alizidi Kachero Manu kumtia shemere Juma.

Lengo la Kachero Manu hakutaka kuacha hata chembe ya ushahidi kwa sababu alijua huko wanakokwenda kuna kufa au kupona. Hisia zake mpaka akaamua amfuatilie huyo Mzee wa kiarabu zilimtuma kuwa baadhi ya washirika wa “Al-shabaab” wameanza kutafuta maficho hasa baada ya nyaraka za siri zilizonaswa na Kachero Manu kule Simba Hoteli, Dodoma, zenye majina yao kutua mikononi mwa serikali. “Wewe Juma nakukubali aisee umejuana nae vipi mtu muhimu kama huyu, ambaye ana utajiri chekwachekwa” alidodoswa Juma na Kachero Manu wakati tayari ameshajaza mafuta pomoni kwenye tenki la pikipiki sasa walikuwa wanakata msitu kuelekea huko mashambani.

Lengo la Kachero Manu hakutaka kuacha hata chembe ya ushahidi kwa sababu alijua huko wanakokwenda kuna kufa au kupona. Hisia zake mpaka akaamua amfuatilie huyo Mzee wa kiarabu zilimtuma kuwa baadhi ya washirika wa “Al-shabaab” wameanza kutafuta maficho hasa baada ya nyaraka za siri zilizonaswa na Kachero Manu kule Simba Hoteli, Dodoma, zenye majina yao kutua mikononi mwa serikali. “Wewe Juma nakukubali aisee umejuana nae vipi mtu muhimu kama huyu, ambaye ana utajiri chekwachekwa” alidodoswa Juma na Kachero Manu wakati tayari ameshajaza mafuta pomoni kwenye tenki la pikipiki sasa walikuwa wanakata msitu kuelekea huko mashambani.

Juma Mavideo alikuwa analikimbiza pikipiki kwa mwendo wa kasi hakujibu swali la Kachero Manu, akawa anakanyaga mafuta na alikuwa analimudu ingawa alikuwa ‘chordo chupa na kizibo chake’ ananuka pombe ya ngomani balaa.

“Hapo mbele kwenye kona hapo pana mti wa msufi mkubwa, gari yao siku moja iliharibika, ilikuwa usiku kama saa 4 hivi sasa kuna fundi wao alitoka Mjini nikapewa kazi ya kumleta, kwa sababu mie hamna kijana anavijua vichochoro vyote vya Amboni kama mimi” alijibu Juma swali aliloulizwa kwa mbwembwe zote huku anaikamua pilipiki vilivyo.

Ghafla kutokea mbele yao ikawa inasikika sauti ya gari linakuja uelekeo wa kutokea mbele yao. “Ingiza porini haraka, huenda watu wabaya wanataka kutupora madini” alitoa amri Kachero Manu na Juma Mavideo akatii bila shuruti, wakalisweka pembeni haraka haraka, Juma akazima pikipiki yake na taa zake. Punde si punde likajitokeza gari linatembea mwendo wa pole pole limeshusha vioo, ndani kuna msichana amejifunga mtandio kichwani na mwanaume anayeliendesha gari. Waliweza kuwatambua vizuri kwa sababu dereva aliwasha taa ya ndani ya gari kana kwamba kwamba kuna kitu yule msichana alikuwa anatafuta ndani ya gari.

“Kaka kaka hili ndio gari lenyewe linalombeba yule mwarabu” alikuwa ananong’ona Juma kumwambia Kachero Manu, huku anatetemeka mwili mzima kule kichakani walipojisweka. Kachero Manu akatikisa kichwa kuonyesha kukubaliana nae huku ametingwa na ananakiri namba za gari hiyo ya polisi.

Baada ya gari lile kupita safari yao ikawa inaendelea tena, huku wanatumia matairi ya lile gari kama ndio dira ya wanaoelekea. Ilikuwa ni safari ya mwendo mrefu takribani masaa mawili, mpaka wakawa wamekaribia kufika. Juma akazima bodaboda ghafla pale yalipoishia yale matairi ya lile gari.

Akaanza sasa kumsomesha Kachero Manu, “sasa kaka yangu mpaka hapa ndio mwisho wa safari yangu, hapo mbele kuna nyumba moja nadhani ukiuliza hapo utapata jibu wapi anapoishi. Unajua analetwa na gari ya manjagu sasa wale jamaa hawana udugu wala urafiki unaweza bambikiziwa kesi ya wizi au mauaji ili wakufyedede vizuri”.

Kachero Manu akabaki anatabasamu tu, akistaajabishwa na uoga wa Juma Mavideo wa ghafla, maana safari yao nzima akiongea yeye tu kujisifu ujanja, sasa ametepeta kama chapati za maji. “Mie nakupa nusu saa tu vinginevyo nasepa zangu, bado uhai naupenda mke wangu ndio kwanza nipo nae mwaka wa pili hata mahari yangu haijajilipa vizuri bado. Maadamu umeamua kujifunga bogi mie nakutakia kila kheri” aliongea kwa sauti kubwa Bwana Juma kusisitiza Kachero Manu asichelewe kurejea huko anakokwenda.

Kachero Manu akawa anatokomea kwenye uoni wa upeo wa Juma kuelekea alipoelekezwa, kikubwa alichoshukuru hawakukanyaga chechele wakapotea njia bali wamefika salama wanapopakusudia. Jukumu la Juma lilishaisha tayari, sasa imebaki kazi yake.

Kachero Manu akaanza kutembea kupita kwenye mafukutu ya nyasi zilizoshonana kwa msaada wa mbalamwezi huku akichukua tahadhari kubwa. Mpaka alivyotembea kama dakika 5 akaanza kuona mwangaza kwa mbali unatoka kwenye nyumba iliyoonekana kuwa ni ya kibanda cha miti, iliyokaa kiungani kwa kujitenga.

Akazidi kukisogelea kibanda kile kwa umakini mkubwa. Mbele yake akauona mti mkubwa ulio karibu na nyumba ile. Akajificha kwenye mti mmoja huku akitafuta mbinu ya kuingia kwenye kibanda kile. Alipoona kimya hamna michakato yoyote inayoendelea pale akachomoka kwa kasi kwa mwendo wa kunyata kuzungukia upande wa kushoto wa nyumba. Akafanikiwa kufika mlango wa nyuma. Akaweka sikio lake kwenye uwazi mdogo sana wa baina ya mbao na mbao pale mlangoni. Akawa anasikilizia kama kuna lolote linaloendelea. Akaona kimya kimetamalaki kwa kiasi kikubwa.

Giza la nje lilikuwa msaada mkubwa kwake, mwanga uliokuwa unaangaza ni wa mbalamwezi tu. Akaachana na mlango na kuanza kuzunguka na kiambaza kuchungulia kwenye madirisha ya chumba tofauti tofauti. Chumba zote tatu zilikuwa vina giza isipokuwa kimoja tu kulikuwa na mwangaza wa koroboi.

Kilikuwa ni chumba kina pipa moja kubwa la plastiki lilikuwa lina maji kiasi. Pia kulikuwa na vyombo vichache vya kupikia. Akaamua aingilie kupitia dirisha hilo. Haikuwa kazi ngumu kulinyofoa dirisha hilo kutokana na kuwa ilikuwa ni nyumba ya udongo na miti. Akachidikia chumbani, wakati anashangaa mle chumbani anafikiria kitu cha kufanya, akasikia michakato ya viatu ya mtu anayekuja kwenye kile chumba.

Kachero Manu akafanya maamuzi ya kupiga mbizi kwenye pipa lile la maji. Kweli Bwana yule mtu aliingia chumba kile kile akaenda mpaka vyombo akaviparanganyua na kuchukua kitu anachokitaka, akajifanya anaondoka zake na kufunga mlango. Kachero Manu alipiga mbizi kwa zaidi ya dakika 10, kisha akaibuka na kuruka nje ya pipa hilo. Ile anatua chini tu, akapigwa na gunia zito la mchanga kisogoni mwake. Lilikuwa ni pigo takatifu ambalo kama angepigwa mtu tefutefu asiye na mazoezi kama Kachero Manu lazima angefuata njia ya marahaba, malaika wangempokea kaburini. Akaanza kuyumbayumba kama mlevi aliezidiwa na pombe, kisha akaanza kuona nyota nyota na huku kuna watu warefu wasio na mwisho wamevaa nguo nyeupe wengi sana.

Ambao wanaimba nyimbo za mapambio huku wakimzunguka duara. Akajiona mwishoni anazama kwenye shimo refu sana yenye kiza kinene. Alichokuwa hakifahamu Kachero Manu ni kuwa kulikuwa na mlinzi mmoja yupo juu ya mti anafanya doria ya eneo zima, kwa bahati mbaya hakumuona na huyo ndio aliyepanga shambulizi dhidi yake. Kachero Manu akapoteza fahamu akiwa ndani ya nyumba ya mtu asiyemfahamu.

Kachero Yasmine nyumbani kwa “Maso Maso” mafichoni alipo, alikuwa anaishi maisha ya fawaishi, maisha ya gharama ambayo hakutaraji kama kuna siku ataishi hivyo. Ilikuwa ni nyumba yenye kila kitu zaidi ya hoteli ya nyota tano, laini hakuipata furaha hata chembe ya hardali.

Sekunde ziliyeyuka kama kama plastiki kwenye moto, na dakika zilikatika, yakaja masaa, zikaja siku leo ilikuwa inatimia wiki moja kamili. Alikuwa hana raha hata kidogo kwanza hajui hatima yake itakuwaje kwenye kasri lile alilofungiwa ndani. Lakini tayari pia wameshapotezana mawasiliano na mkuu wake wa kazi Kachero Manu. “Sijui Kachero Manu anapitia madhila gani huko alipo au pengine ameshapoteza uhai wake. Na kama yupo hai na yeye pia ana hofu na mimi kwa vyovyote vile ukimya wangu atadhania nimepoteza maisha au nimetekwa na maadui” alikuwa anazidi kuwaza Kachero Yasmine mawazo yasiyo na kikomo mpaka kichwa kikawa kinamgonga kwa maumivu wakati mwingine.

Mawazo mengine yalikuwa yanamjia kuhusu huyu mumewe feki “Maso Maso”, ile saba ya bila tendo la ndoa kutokana na hedhi feki aliyomdanganya ndio leo inakatika. Akaanza kuyarudia kichwani mwake majadiliano yao na mumewe alipomwambia yupo kwenye siku zake jinsi alivyohuzunika na kutaka hata kulazimisha tendo la ndoa kwa nguvu.

Sasa Kachero Yasmine aliwaza sekeseke la siku ile mpaka akamtuliza kijana wa watu kwa maneno ya Mwenyezi Mungu mpaka akapoa sasa leo akija atambeba kwa mbeleko gani, hatokuwa na jinsi nyingine bali kukubali kuliwa mzigo tu.

Kwa mara ya kwanza tokea aajiriwe na Idara ya Usalama akaanza kumwaga machozi kama mtoto mdogo, akawa hawezi kujizuia baada ya kuona hatari ya kutumika kingono bila ridhaa yake. Kilichokuwa kinamuumiza zaidi ni sawa anaweza kumpa tendo la ndoa, je iwapo katika harakati hizo akinasa ujauzito je.

“Wallahi nitatoa mimba hiyo siwezi kupata mtoto na gaidi, uso wangu nitauweka wapi mimi Yarrabi toba” alikuwa anaendeleza fikra nzito Kachero Yasmine. “Lakini nikitoa hiyo mimba na kukiua kiumbe kisicho na hatia nitamchukiza MwenyeziMungu na huenda ikawa ndio uzazi wangu wa pekee hapa dunia” alikuwa anawaza huku yupo juu ya kitanda bila kupata muafaka.

Akiwa kwenye lindi hilo la mawazo akasikia sauti ya kengele inayomjulisha muda wa wakati wa mlo wa usiku upo tayari mezani. Chakula cha usiku kilikuwa kinaliwa kila ifikapo saa 1:00 usiku juu ya alama. Akakurupuka kutoka kitandani na kujiandaa kwenda kula maana tayari njaa ilikuwa inamtafuta vilivyo.

Kuna kitu kimoja katika uchunguzi wake kilikuwa hajakipatia majibu ndani ya nyumba ile. Kulikuwa na lundo la watumishi, na chakula kinachopikwa ni kingi sana. Kwanza akawa anajiuliza kuna umuhimu gani wa kuwa na idadi kubwa ya watumishi wakati nyumba nzima kabla hajaja yeye anaishi “Maso Maso” pekee na masuria wake!.

“Hiki chakula kinachopokea ni chakula watu zaidi ya 50 na kuendelea na ni chakula cha watu wenye hadhi yao, yanapikwa mabiriani humu, mapilau na kila anuwai ya vyakula vitamu” alikuwa anatengeneza majawabu ya kukisia ya dhana alizojitengenezea.

“Hiki chakula kitakuwa kinasafirishwa kwa njia za panya maana sijawahi kuona namna vyakula vinavyosafirishwa wala wakati vyombo vinaporejeshwa” alizidi kutengeneza majibu ya dhana zake. Akaelekea mesini kwenda kujipakulia mlo wake. Akawa ni mwenye kula chapuchapu arudi zake chumbani huku hofu ikitawala moyoni mwake akiombea mumewe “Maso Maso” asirudi haraka kama alivyoahidi kurudi baada ya kupita juma moja.

Matarajio yake yalikuwa huenda akapata baadhi ya ufumbuzi wa kero zake. Alivyomaliza kula tu akapitiliza bafuni kwenda kupiga mswaki kuondosha mabaki ya chakula mdomoni mwake. Alipoingia bafuni akachukua mswaki wake akaelekea kwenye kioo cha kwenye sinki na kuanza kusafisha meno yake.

Kwa bahati mbaya maji maji yenye ya mdomoni yaliyochanganyika na dawa ya meno yakadondokea kwenye kioo na kuchafua muonekano wa kioo kile. Kwa kawaida usafi unafanywa na watumishi lakini hakupenda asubirie mpaka asubuhi ndio kisafishwe, hasa akichukulia yeye ni mtoto wa kike.

Akaamua kuchukua kitambaa safi akakiloweka kwenye sabuni akaanza kusugua kwenye kioo. Kwa mshangao mkubwa alikiona kile kioo kikubwa kinacheza cheza kuonyesha hakijashikizwa kiuimara ukutani. “Hii ni kuharibika au imefanywa hivi makusudi! ” alijiuliza Kachero Yasmine.

Akaamua akichomoe kwanza aone, akakiona kinachomoka bila shida yoyote. Kilikuwa kimeshikizwa na pini mbili zilizoingizwa kwenye chuma kidogo kilichoungwa kwenye fremu ya kioo kile. Akakuta kuna duara kubwa linalotosha kabisa kupitisha kiwiliwili cha binadamu likiwa limefungwa na mbao laini.

Akaisogeza pembeni shimo likawa lipo wazi. Akarudi katika mlango wa bafuni na kuubana na ufunguo ili kutoruhusu mtu kuingia. Akapanda juu ya sinki kiuangalifu na kudumbukia kwenye hilo shimo huku akitanguliza miguu yake. Miguu ilipofika chini tu ikawa tayari imekanyaga ngazi na kushukia chini.

Akawa anateremka kwa umakini mkubwa kutokana na kiza kilichopo. Alipoteremka kama hatua 22 hivi akaona kuna kizuizi tena cha dirisha kubwa ambalo limefunikwa na pazia. Akafika mpaka hapo na kupekenyua lile pazia kiasi kidogo. Hamadi..! akaona kwa chini yake kama meta 50 kwenda chini kuna taa zinawaka huku kuna barabara nzuri ya lami imepita. Ilikuwa ni barabara nyembamba yenye uwezo wa kuruhusu bodaboda mbili kupishana. Wakati yupo pale pale kwenye kidirisha anapiga chabo akaona bodaboda mbili zinapita.

Zikiwa zimebeba majungu ya vyakula mbalimbali. Haraka haraka akafunga lile pazia na kurudi juu kwa kasi huku anatweta kwa uoga haamini alichokiona. Akarudi mpaka bafuni akakirudishia kile kioo vizuri. Alipotoka tu nje ya bafu na kuingia chumbani kwake, kengele ikaanza kulia. Akashtuka sana sio kawaida kupigiwa kengele akiwa ameshaingia ndani kupumzika hasa baada ya kupata mlo wa usiku. Akaipuuzia labda watakuwa wamekosea, wakati anajiandaa apande kitandani sasa ikaanza kulia tena mara hii ikiwa ni mfululizo.

Akakurupuka na kwenda kuitika wito kwa kufungua mlango. “Seyyidati samahani kwa usumbufu usiku huu kuna gari limekuja kukufuata limetumwa na mumeo unatakiwa umfuate alipo ubebe vitu vyako vya muhimu tu vingine uviache, huo ndio ujumbe wangu kwako mtukufu Seyyidati” alileta ujumbe mmoja wa watumishi kwa nyumba ile na kuaga akaondoka zake.

Akaurejesha mlango na kuuegemea mlango kwa mgongo wake. Akavuta pumzi ndefu kwa muda, alikuwa yupo pwetepwete kwanza akimshukuru Mungu kwa kuigundua njia ya siri dakika za majeruhi bila kushtukiwa. Lakini pia sasa alikuwa anaogopa kuwa lazima sasa ataenda kushiriki tendo la ndoa na “Maso Maso”.

“Ukitaka kuoga lazima uyavulie nguo maji hamna jinsi, tutaona huko huko” alijipa moyo na kuanza kufungasha virago vyake. Baada ya nusu saa akawa yupo tayari kwa safari, akaingia na msafara ukaanza kuelekea sehemu asipokujua. Ila alikuwa amejiandaa kuwa makini kusoma vibao na alama za kumtambulisha eneo hilo, lakini kikubwa alikuwa anaangalia muda anaoondoka pale nyumbani kwa “Maso Maso”.

Alipoingia ndani ya gari vioo vya giza “tinted” vikateremshwa akawa haoni anapotoka wala anapopelekwa. “Hawa mbwa ni kiboko aisee wamejipanga hawataki kufanya makosa, tutaonana huko huko. Ni kama vile wananitoa kikaangoni huku na kuniweka motoni huko wanakonipeleka. Unapojitwika wajibu si vyema kulalama, maadamu ni kazi niliyoichagua mwenyewe ngoja nikapambane” alijisemea Kachero Yasmine moyoni mwake. Huku injini ya gari inaunguruma kukata mitaa.

Kachero Manu alikuwa amezimia kwa zaidi ya masaa 12. Alizinduka majira ya saa 7 adhuhuri akijikuta amefungwa pingu mikononi na miguu kwenye kingo za kitanda kidogo cha chuma chenye godoro la unene wa ulimi wa ng’ombe. Alijikuta hana nguo hata moja mwilini zaidi ya chupi yake tu huku nguo zake na buti zake zimetupwa pembeni ya kitanda.

Aliposhtuka kichwa kilikuwa kinamgonga vibaya sana. Alikuwa ametundikiwa dripu za kuongeza maji mwilini. Pia alikuwa ameunganishwa mwilini na mtambo unaosaidia kusoma mapigo yake ya moyo kitaalamu inaitwa “Heart Monitor” (EKG).

Alipofumbua macho vizuri akawa anajaribu kuvuta kumbukumbu amefikaje humo kwenye chumba kikubwa ambacho kina hadhi ya kuwa ni moja ya chumba cha hospitali kubwa. “Nini kimenimpata mpaka nimefika hapa?” alikuwa anajiuliza huku anatafakari. Maumivu ya kichwa yalizidi kumzonga kadri alivyokuwa anajilazimisha kuwaza. Akiwa katika hali hiyo ghafla mlango wa chumba hicho ukafunguliwa na ufunguo akaingia mtu amevaa koti jeupe, mara baada ya kuingia akaurejesha mlango huo.

Aliingia daktari mwanaume mwenye umri wa makamo, ambaye alikuja moja kwa moja mpaka kwenye zile mashine alizofungwa mwilini Kachero Manu. Kachero Manu akajifanya kufumba macho ili aonekane bado amezimia. Baada ya daktari yule kusoma vitu alivyokuwa anavyohitaji kutoka kwenye hiyo mashine akamgeukia Kachero Manu na kumuongelesha.

“Pole sana ulipoteza fahamu kwa zaidi ya si chini ya saa 12 nashukuru Mwenyezi Mungu nimepambana kuokoa uhai wako nimefanikiwa. Vipimo vinanionyesha umeshazinduka na unajitambua sasa” aliongea yule daktari huku anatabasamu akionyesha ameshtukia ujanja wa Kachero Manu.

Kisha yule daktari akachomoa dripu lile la maji ambalo lilikuwa ndio linaishia. Ikabidi hana jinsi ila afumbue macho yake. “Bwana daktari nimefikaje hapa na kilinipata nini? ” aliuliza Kachero Manu kwa yule daktari wakati amempa mgongo anaandika vitu vyake kwenye karatasi zilizobanwa kwenye faili.

“Watakuja sasa hivi kukueleza wahusika wako mie sifahamu chochote juu yako zaidi ya kukutibu tu” alijibu yule daktari huku anakusanya kila kilicho chake na kuondoka zake, akafunga kile chumba kwa funguo na kuondoka zake. Alipozidi kuvuta fikra zake Kachero Manu taratibu akaanza kukumbuka matukio ya nyuma huku yanakatika hayana muendelezo. Njaa nayo ikaanza kumkung’uta barabara, mpaka akaanza kutetemeka, maana mara ya mwisho alishindia kahawa na kashata za machicha ya nazi kule kijiweni.

Haukupita muda mrefu mlango ukafunguliwa tena akaingia kipande cha mtu mwenye mwili ulioshiba mazoezi, amevaa maski usoni amebeba mkono wa kulia ana kikombe kikubwa kwa kutumia mshikio na mkono mwingine kabeba silaha. Alipofika akaweka kwenye meza ndogo kile kikombe. Na kuchomoa funguo mfukoni mwake na kuanza kufungua pingu za mkono mmoja wa kushoto. Kisha bila kuzungumza chochote akamkabidhi kikombe Kachero Manu anywe.

Kwa njaa aliyokuwa nayo alikuwa anakunywa ule mtori wa moto kama vile ni wa baridi baada ya dakika 3 kikombe kikawa hakina hata tone la mtori. “Nakuja muda sio mrefu tuongee kwa kina” alisema yule mlinzi na kuondoka zake kwa haraka. Lakini sauti yake yule adui ilimchanganya sana Kachero Manu. Hisia zake zilituma kuwa ni ya mtu kama anayemfahamu.

“Huyu ni nani? hii sauti ni ya mtu ninayemfahamu kwa kina, sio ngeni kabisa masikioni mwangu” alikuwa anawaza peke yake. “Halafu mbona hii pingu ya mkono wa kushoto aliyonifungua mbona hajaifunga tena vizuri kaiegesha tu!. Huyu ana kitu na mimi sio bure, ukisikia nyota jaa kukuangazia mchana wa jua la mtikati ndio huku sasa” aliwaza Kachero Manu. Sasa baada ya tumbo kupata chochote kitu, akili yake sasa ikatulizana na kutungamana, usicheze na njaa haina cha Rais wala raia wote wanahisi njaa.

Akaanza kuwaza namna alivyofikishwa hapo. Kumbukumbu zikamrudisha kisengerenyuma mpaka kijiwe namna alivyocheza mchezo wa bao na kisha kunywa kahawa, mpaka kuletwa na Juma Mavideo kwenye nyumba ambayo alipigwa na kitu kizito kisogoni na kupoteza fahamu. Akajilaumu kwa kutochukua tahadhari ya kutosha lakini alijipongeza kutokana na kufanikiwa kufahamu kuwa kuna siri muhimu inayotaka kufichwa kwa huyu Mwarabu.

“Kuna nini kinafichwa hapa mpaka nashambuliwa nusura kifo” aliendelea kuwaza na kuwazua Kachero Manu bila kupata majibu. Akamkumbuka dereva bodaboda Juma Mavideo, “sijui yupo salama na amesharejea nyumbani kwake?” Kwa mara ya pili tena yule mlinzi akarudi tena akionekana ana haraka sana na kama ni mtu ana wasiwasi mwingi.

“Komandoo Aboubakr anakuja mlinzi mwingine kushika zamu yangu, na usiku wamepanga wakuchukue kukupeleka kwa Bosi mkuu wa mapango ya Amboni kabla hawajakuchinja na bado hawajakutambua kama ni wewe kama wakijua umeshawahi kuishi kambini adhabu yake ya usaliti ni mbaya sana, umeshanitambua mimi nani? ” alijieleza kwa haraka yule mlinzi. Kachero Manu akazidi kupigwa na butwaa. “Ina maana wamenifahamu mpaka jina langu feki..!” alikuwa anawaza kisha akajilazimisha kutabasamu, tayari alishamhisi nani anayeongea nae. “Wewe ni Akhy Abu-fadhli eeh au nakosea” aliuliza Kachero Manu kwa yule mlinzi huku akijionyesha anajiamini. Huyo Abu fadhli walikuwa wanaishi chumba kimoja kule kambini kijijini Dibungo, mara Kachero Manu alivyowasili Tanga. Kwa bahati waliochaguliwa kuja kumdhibiti Kachero Manu naye alikuwepo.

Alivyomuona tu akamgundua huyu ni Komandoo Aboubakr tena rafiki yake yupo matatizoni, huruma ikamuingia ya kumsaidia kwa mshahara wa potelea pote liwalo na liwe. “Hujakosea tumeletwa mahususi kwa ajili yako, mimi nataka nirudi atakuja mwingine kukaa na wewe mpaka saa nne usiku, kisha ataondoka watakuja sasa wengine wa kambi kuu kukupeleka Amboni, huko sasa ndio huwezi kutoka hai, jitahidi uchomoke” alijieleza yule mlinzi.

Kachero Manu alikuwa anatafakari namna ya kuchomoka. “Nimeshakufungua pingu ya mkono wa kushoto kisha nimeegesha tu makusudi, narudi kambini kwetu Dibungo nategemea utachomoka tu, pambana kwa jino na ukucha halafu tuone namna ya kuiendesha hizi kambi kwa kufuata sheria za Allah. Hawa hawapo kwa ajili ya dini wapo kwa maslahi binafsi mfano huyu Mzee uliyemfuata humu ni fuska ajabu muda mfupi niliokaa humu anafanya mambo ya ajabu tu nayashuhudia” alizungumza Abu-fadhli kwa hasira huku anapigapiga ngumi ukutani. Hakutaka kuonekana anamsaidia moja kwa moja kwa kuhofia huenda kuna watu wanaowachunguza nyendo zao mle chumbani. Kisha Abu-fadhli akaondoka zake kwa haraka sana. “Ukombozi wa kweli hauletwi kwenye sahani bali huletwa kwa mtutu wa bunduki” alijisemea Kachero Manu. Haikupita hata nusu saa mlango ukafunguliwa tena akaingia mlinzi mwingine mfupi amejazia misuli vya kutosha, kifua ngao akiwa amebeba jiko dogo la umeme na spoku za baiskeli.

Nae alikuwa amevaa barakoa usoni na singlendi nyeusi akiwa amevaa suruali ya buluu ya dangilizi iliyokatwa chini kidogo ya magoti. Chini akiwa amevalia buti kubwa za rangi ya kaki. “Wewe mbwa wa motoni, msaliti wa Jihadi, nani vibaraka waliokutuma kuhujumu Mujahidina?” alifokewa Kachero Manu kwa sauti ya kwaruza roho, huku anashindiliwa mabuti ya tumboni pale pale kitandani alipolala.

“Aaah…..Aaaah….. Nakuf …..aaaah unani….o..ne..aa bu….u… re” Alikuwa analalamika Kachero Manu huku akisubiria wakati muafaka wa kumshambulia. Akaamua amtie hasira kwa kumpa maneno mabovu. “Wewe kisonoko mtambaa na ukoko karatasi ya kuchambia chooni ya Wasomali wa Al-shabaab huwezi kuniambia kitu”.

Yule jamaa akajibu kwa vitendo matusi ya Kachero, akachomeka waya wa jiko la umeme kwenye soketi ukutani, kisha akawasha swichi ili likolee moto. Kachero Manu alikuwa anamvizia ajilete kwa ukaribu amkabe kwa kutumia pingu yake ya mkono wa kushoto. Yule mjuba alikuwa kama vile ana machale anakuwa haingii kwenye mtego wa Kachero Manu. Jiko lilivyokolea moto kisawasawa akachukua spoku akawa anaipasha moto kwa kuishikilia huku mkononi amejivesha glovusi ngumu zisizopitisha moto kwa urahisi. Ile spoku ilipopata moto vizuri akaishika kwa glovusi na kumchoma nayo kachero Manu kwenye nyuma za nyuma ya ugoko wa mguu wa kulia.

“Aaaaaaaah Aaaaaah kenge wewe unaniumizaaa, kamsosi maji baridi weweee” alikuwa analalamika kwa maumivu Kachero Manu huku yule mlinzi anacheka tu kwa twezo kwani alijiandaa kumfanyia unyama wa kutisha. “Matusi hayakusaidii kitu subiri sasa spoku za moto za kwenye tundu la kupitishia mkojo ndio utakaponiheshimu”.

Kachero Manu akapata wazo jipya la kufanikisha kumkaba kwa urahisi. Akakusanya makohozi kinywaji na kumtemea bonge la kohozi usoni yule adui, na kuanza kumcheka ili amtie hasira. Yule adui kuona hivyo akakasirika na kufura akawa anachemka kwa hasira. Akachukua spoku nyingine ya moto na kutaka kuja kumchoma nayo shavuni.

Hilo likawa ni kosa la majuto kwake. Wakati spoku ya moto imebakiza sentimeta chache kutua kwenye shavu la kushoto la Kachero Manu, akadakwa kiganja chake yule adui na mkono wa kushoto wa Kachero Manu kisha kwa kasi ya haraka akakigeuza kiganja chake na kusababisha spoku imuingie kwenye jicho lake mwenyewe. “Uwiiiiiiiih……Uwiiiiiih….!, jicho langu weeeeeh…!” alipiga makelele huku anagugumia kwa maumivu makali yule mjuba wa “Al-shabaab”. Ama kweli mwosha huoshwa na mtenda akitendewa huona kaonewa alisahau kabisa kuwa dakika chache zilizopita alikuwa anampa mateso mwenzake, sasa kibao kimemgeukia.

Kachero Manu bila kupoteza wakati akaitumia ile fursa vizuri kwa kumvuta karibu kisha akampiga mbata moja matata sana ya kwenye paji la uso, iliyomchana vibaya na kumsababisha aangukie pale kwenye godoro huku akiwa anakoroma kwa kupoteza fahamu. Almanusra aende jongomeo kaburini ilikuwa bahati yake sana, usicheze na kupigwa kichwa na komandoo ambaye mazoezi yake kila siku akiwa nyumbani akitaka kupika wali nazi au mandondo, nazi huwa anaivunja kwa kutumia kichwa chake.

Himahima akamsachi mifukoni na kufanikiwa kupata funguo za pingu alizofungwa. Akatumia chini ya dakika 2 kuhakikisha yupo huru akavaa nguo zake haraka haraka, sasa muda ulikuwa unaonyesha ni saa 10 alasiri. Alipomaliza kuvaa akarudi tena kumsachi vizuri akamkuta ana bastola za kisasa mbili na mabomu mawili madogo ambayo ukiyalipua yanaweza kuteketeza mtaa mzima. Akabeba vile vitu na kutoka nje ya chumba kile alicholazwa. Akaanza msako wa chumba hadi chumba akiwa ndani ya nyumba ile ili kupata chochote kitu kitakachomsaidia.

?

Mkuu wa Magaidi mikononi mwa Kachero Manu?

Mambo yalikuwa tumbitumbi kwa Kachero Manu lakini muda hautoshi ikabidi ajitahidi ayakamilishe kwa wakati. Akaingia chumba cha kwanza kinachotazamana na kile alichokuwa anateswa. Akakuta chumba kina kitanda kikubwa kilichotandikwa nadhifu huku kukiwa na kabati lenye droo zake mbili pamoja na kioo. Hakukuwa na kitu chochote kingine.

Akavunja droo ya upande wa kushoto kwa kutumia bastola yake yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Ikabidi aanze kucheka kwa alichokiona ndani ya droo hiyo. Alikuta paketi za kutosha za vidonge vya kuongeza nguvu za kiume maarufu kwa jina la “Viagra”, na pia kulikuwa na paketi za kutosha za mipira ya kiume maarufu kwa jina la “kondomu”. Akapiga risasi droo la upande wa kulia nalo likajibu na kujimanua likawa lipo wazi. Alichokiona humo alifurahi na roho yake sana tu.

Alikuta pesa taslimu za kigeni zikiwa zimepangwa bandali bandali. Lakini kilichomfurahisha zaidi ni kuipata ramani ya kutoka walipo pale kumfikisha mapango ya Amboni walipo viongozi wakuu wa “Al-shabaab”. Baada ya kujiridhisha kuwa ndio yenyewe akaisunda kwenye mfuko wa suruali yake na kutoka nje kwa tahadhari kubwa. Hakutaka yale makosa ya kutekwa kirahisi yasijirudie tena.

Mpaka sasa alikuwa bado hatambui sehemu alipo. Akasogea kwenye chumba kingine akakuta mlango umefungwa lakini taa imewashwa. Akajaribu kukifungua kitasa taratibu, mlango ukaitika kwa kufunguka. Aliyoyashuhudia ni ya kustaajabisha. Hakutegemea Babu kikongwe kama huyo ayafanye. Alimkuta Mzee Abdallah mmiliki wa “Chops Carwash & Garage” mtuhumiwa wa mauaji ya Wabunge watano na madereva wao alikuwa anakula bata, habari hana kabisa.

Jamaa huyu aliwekwa juu ya meza uchi wa mnyama, halafu kumeletwa asali iliyowekwa kwenye kisahani, halafu zile korodani zake zinawekwa kwenye kisahani huku zinapakazwa asali, kisha msichana mbichi kabisa ananyonya korodani zake kimahaba zilizolowekwa kwenye asali.

Zinaponyonywa zile kokwa hiki kibabu kinapiga kelele za kupagawa, anazungumza maneno ya ahlan wa sahalan yasiyo na mtiririko wowote wenye kuleta maana. “Yaaaaah habibiiiii…. Zubeida mimi nataka kukununulia wewe ndege, nitakujengea ghorofa katikati ya Bahri Hindi Mashaallaah…Shallalaaaaah” Babu alikuwa hajiwezi kwa raha anayopata ya kunyonywa korodani zake.

Ndio alikuwa amekaribishwa Tanga, kashakuwa limbukeni wa mapenzi baada ya kuvitoroka vyombo vya dola vinavyomsaka kwa kesi ya ugaidi. Anavyopiga kelele hizo za maneno ya mporoto, yule binti ndio anazidisha manjonjo ya kumpagawisha Babu. Kiruka njia huyo alikuwa shombe shombe, kwani licha ya ngozi yake kuonyesha kuchanganya damu, bali nywele zake zilikuwa ni za kiarabu kwani alikuwa ameiteremsha ile shungi aliyojitanda kichwani.

Kachero Manu hakutaka waendelee na starehe zao na wamgeuze yeye kuwa kozibati. “Mpo chini ya ulinzi mafuska wakubwa nyie hata aibu hamuoni” alitoa ilani halafu akabutua risasi moja kupiga kwenye dirisha. Yule Babu alishtuka mpaka akaanguka chini ya meza, miguu juu kichwa chini. Huku yule kahaba amejifunika uso wake kwa kuona aibu ya yale waliyokuwa wakiyafanya.

Yule Babu alivyoamka akachomoka nduki utasema “Alphonce Simbu” yule mkimbiaji mahiri wa Tanzania yupo kwenye mbio za Marathoni, anakimbilia kwenye mlango mdogo uliomo mle chumbani. Kachero Manu akaikohoza kidogo tu bastola yake, akaanguka chini Babu wa watu huku damu zinamvuja gotini. Akawa anajisuwira kwa maumivu makali anayoyapata huku analalamika.

Kachero Manu akawa anamsogelea huyu Babu ambaye ni mmoja wa kiungo muhimu wa Al-shabaab na ndio aliyemfadhili “Maso Maso” kwenda masomoni Uingereza kwenda kupikwa kwenye ugaidi.

“Nitakupeleka kwenye vyombo vya dola hata ikibidi nitembee kwa miguu kutoka Tanga mpaka Dar es Salaam ukiwa mgongoni mwangu nikufikishe ukajibu tuhuma zako za ugaidi mshenzi wewe” alikuwa anafoka Kachero Manu kumwambia maneno makavu Babu Abdullah mmiliki wa “Chops Carwash & Garage” aliyekuwa bado anagaragara pale chini.

Alipozidi kumsogelea, Mzee Abdullah akaanza kucheka kicheko cha kebehi “Ha… ha… ha.. ha.. ha… ha..!” kwa sauti ya juu kisha akamwaga matusi ya kutosha kwa Kachero Manu.

Kachero Manu akashtukia kitu kisicho cha kawaida kwa Mzee Abdullah akaanza kumwendea kwa kasi akamrukia na kuwahi kumkaba shingoni, lakini alikuwa ameshachelewa tayari amezidiwa ujanja.

Mzee Abdullah alikuwa na jino bandia ambalo ni kidonge cha sumu kitaalamu kinaitwa “Lethal Pill”. Ambapo kidonge hiko kinavishwa raba kwa nje kumlinda mtumiaji kama akikimeza kwa bahati mbaya. Ndani ya hilo jino bandia kuna kemikali ‘Potassium Cyanide’ inayohifadhiwa kwenye glasi.

Hivyo anapotaka kujiua mhusika anavunja hiyo glasi hiyo sumu kwa meno yake moja kwa moja ikiingia mwilini inaenda kusimamisha mapigo ya moyo na kuharibu ubongo. Mzee Abdullah alikuwa amechagua njia ya marhaba yeye mwenyewe hakutaka kupata mateso ya Wanausalama. Alijua watamgombania kama mpira wa kona na kumletea usumbufu wa mateso mengi atakayoshindwa kuyabeba.

“Shenzi sana kasalimie jongomeo huko utaenda kujibu katika Mahakama ya Mwenyezi Mungu, hakuna ulichokikwepa…!” alisema Kachero Manu kwa hasira za mkizi mbele ya marehemu ambazo hazisaidii kitu. “Umekuja humu kwa kupitia wapi? ” aliuliza Kachero Manu kumuuliza yule kahaba, sasa kasheshe la kumkosa Mzee Abdullah lilihamia kwake yule kahaba. Yule kahaba hakumjibu kitu kwa aibu na idhilali iliyomkuta huku akiwa amejiziba uso kwa mtandio wake, akajizoazoa pale chini alipokuwa amejibweteka na kutaka kuongoza njia kuonyesha njia aliyoingilia kule kwenye nyumba ya chini ya ardhi. Kachero Manu hakutaka kumuamini moja kwa moja yule mwanamke wa mahonyo, haraka haraka akamfanyia inspeksheni ya kutosha kuhakikisha hana chochote mwilini mwake.

Alipojiridhisha ni joka la kibisa hana madhara yoyote akamruhusu aongoze njia ya kutokea akafuata mlango ule ule aliotaka atokee marehemu Mzee Abdullah. Walipoufungua mlango wakakuta kuna ngazi zinapandisha juu wakazifuata mpaka wakaja kutokeza chumba kimojawapo katika ile nyumba ya udongo aliyotekwa kachero Manu.

“Haya ongoza njia ya kurudi ulipotokea potea hapa mara moja, kabla sijabadilisha mawazo na kukuchukulia hatua kwa kushirikiana na magaidi ” yule kiruka njia hakusubiri tena amri nyingine akawa anatimka kuelekea mashambani ambapo hata hakujui anapoelekea akawa anachochora tu njia mbele kwa mbele atajua huko huko, cha muhimu kwake ilikuwa kusalimika na mkono mrefu wa dola. Kachero Manu haraka haraka akarudi ndani ya jengo lile akafanya haraka kutega mabomu kwenye ile nyumba huku akitega mabomu yale yasizidi muda wa nusu saa yalipuke.

Yalikuwa ni mabomu ambayo unaweka mwenyewe mtumiaji muda unaotaka yalipuke. Alipomaliza kutega tu akawa anasikia muungurumo wa gari kwa mbali akajua moja kwa moja ndio wanakuja walinzi wengine kuja kuchukua doria kama alivyopewa taarifa na rafiki yake Abu-fadhli. Akakimbilia juu kutoka kule mafichoni hima hima akaenda kujificha kichakani akisubiri matokeo chanya ya mitego yake.

Baada ya kutimia nusu saa huku jicho lake likiwa kwenye saa yake ya mkononi halibanduki, mabomu yalianza kulipuka kwa kishindo cha kutikisa eneo zima. Kukatimka vumbi zito kama lote eneo lile kukawa kama kuna kimbunga cha mchanga. Muda ulikuwa unasoma saa kumi na mbili kasoro ya jioni, akafanya ukaguzi wa eneo hilo sasa kukawa hamna jengo lolote lililosalia, kila kitu kuliteketea.

Akatumia gari walilokuja nalo maadui zake ambalo liliegeshwa mbali na eneo la jengo kurejea nalo Jijini Tanga kujiandaa na usiku wa mwisho wa hekaheka unaokuja mbele yake. Mipango iikuwa mpaka kufika alfajiri shughuli iwe imeshakamilika. Alitaka magaidi walie kilio cha kusaga na meno kwa pigo takatifu atakalowashushia, ambalo hawatasahau kamwe maishani mwao.

SURA YA KUMI NA TANO

“Supu limetiwa nazi”, Magaidi hatarini

Ukumbi namba -05 uliopo ndani ya moja ya mapango Amboni yasiyotumika ulikuwa umetengenezwa na kunakishiwa kwa viwango vya kimataifa. Amboni kulikuwa na mapango si chini ya 11 kwa idadi lakini ni pango moja tu ndio kinalotumiwa na serikali kwa shughuli za kiutalii. Mapango mengine ndio ambayo magaidi waliyachagua baadhi yao na kujikita humo wakijimwayamwaya kama nchi yao vile wakifanya wanavyotaka.

Hapo ndio ilikuwa kama Ikulu yao mipango yao yote inapangwa humo mapangoni. Ukumbi huo Ulipewa jina la ‘VIP HALL’ ambao walikuwa wanaingia viongozi 25 tu wakubwa wa “Al-shabaab” na wateule wanaowataka wao. Ulikuwa unatumika kwa matukio ya mikutano yao ya siri na wakati mwingine kwa matukio ya starehe. Ulikuwa kuta zake zinalinda sauti isitoke nje kirahisi huku ukiwa umefungwa viyoyozi vya kutosha.

Usiku wa Ijumaa hiyo tulivu kwao walikuwa wamemwalika msanii maarufu wa muziki anayetamba Afrika Mashariki na Kati kutoka Zanzibar maarufu kwa jina la “Bob Chollo”. Ambaye alivyopewa mualiko wa kutumbuiza muziki mubashara alipewa ofa ya kuja na maghashi wa Mjini wasiopungua 25 wanaotikisa kwenye mitandao ya kijamii hapa nchini na wale watoto wakali wa kishua wanaotaka maisha ya ganda la ndizi. Wote malipo yao yalikuwa yanafanywa kwa Dola za Kimarekani. Kupata nafasi ya kuja huku kuhudhuria hafla za mapangoni rushwa ya ngono ilikuwa inatumika kwa wale mawakala wanaopewa kazi ya kuwatafuta hawa wasanii. Kama ni msanii wa kiume wapo waliokuwa wanaliwa kiboga na wale wa kike ndio usiseme tena, ilikuwa mtindo wa nipe nikupe. Watu mitaani walikuwa wanashangaa wasanii hao wanaishi maisha ya anasa yasiyoendana na kipato chao.

Wanaendesha magari ya kifahari na kuishi katika makasri ya kifahari lakini walisahau uzuri wote wa mti wa mkakasi ndani ni kipande cha mti tu. Onyesho moja tu kama hilo la masaa yasiyozidi matatu Bob Chollo alilipwa $40,000 taslimu bila mkopo, wakati hawa visura wenye majina yao pamoja na mpiga muziki wao “DJ” kila mmoja alilipwa $15,000 za mkono kwa mkono bila hangaisha bwege.

Lakini yalikuwa ni maonyesho ya aibu yasiyoendana na utu na utamaduni wa Mtanzania. Walikuwa wanaingia ndani ya ukumbi huo wakiwa wamevaa nusu uchi, huku wengine wakifanyiwa vitendo vya ufirauni na hao viongozi wa “Al-shabaab” ambavyo wanavumilia ili wapate chauchau yao ya kutambishia Mjini.

Wengi wao walikuwa wanatakatisha pesa zao hizo za kifirauni kwa kufungua biashara ya maduka ya kuuza nguo, viatu toka China, wengine mpaka biashara za Hoteli na Baa. Hawa viongozi wa “Al-shabaab” walikuwa sana hawapo kwenye harakati za kweli za kidini, bali dini ilitumika kama ngao ya kufichia maovu yao. Wengi walikuwa wanamiliki mali za dhulma na ufisadi wanazozipata kwenye maeneo wanayotawala huko Somalia kwa kukusanya kodi na zaka. Waliokuwa wanaoumia ni watu hohehahe wale mburumatali, mazumbukuku ulimwengu huko huku wanaotangulizwa mbele kama chambo, wakidanganywa wapo vitani kusimamisha utawala wa Kiislamu kwa mgongo wa imani zao kali.

Ndio maana matendo yao yalikuwa hayaendani kabisa na mafundisho ya uislamu. Muziki ulikuwa unaporomoshwa kwa shangwe kama zote kwenye jengo hilo lililokuwa taa zake zenye mwangaza hafifu zenye rangi tofauti zenye kumurikamurika. Ukumbi ulichangamka kwa amsha amsha ya hapa na pale, huku kila mtu akiwa na furaha usoni mwake.

Ilikuwa ni ngumu ukiwa kwenye ukumbi huo kumtambua mtu labda uwe nae kwa ukaribu zaidi. “Maso Maso” nae alikuwepo ndani ya ukumbi akiondosha msongo wa mawazo wa kushinda ndani ya mapango kwa muda mrefu, huku akiwa anavuta bonge la sigara “Siga”. Kama ungemuona “Maso Maso” jinsi anavyolisakata rumba na watoto wa kishua kwa kuwabadilisha kama vile shuka, usingedhania kuwa ni namba moja hatari sana kwa ustawi wa uhai wa binadamu.

Akawa anaonekana ni kama mtu aliyepagawishwa na miondoko na swaga za uchezaji wa maghashi hao. Kutokana na kutokuwa kwake kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mrefu kutokana na kutotumia simu janja za mkononi kwa sababu za kiusalama, hivyo alikuwa zumbukuku wa starehe nyingi zinazoendelea Tanzania na duniani kwa ujumla. Wakiwa katika kilele cha starehe hizo ghafla bin vuu majira ya saa 3 usiku ikapigwa kengele ya dharura ndani ya ule ukumbi, muziki ukabidi uzimwe haraka sana.

Wale wasanii ikabidi wapitishwe mlango wa dharura na kuondolewa eneo lile mara moja kama walivyokuja walikuwa wanaingizwa kwenye magari yenye vioo vyeusi ambayo hayaonyeshi nje yanayowapeleka mpaka Tanga Mjini kutoka Amboni. Wahusika wa “Al-shabaab” kila mmoja akaingia chaka lake kujificha. Tayari disko ameingia Mmasai, supu imetiwa nazi tena imeshakuwa sio supu tena. kila kitu kilienda hobelahobela bila mpangilio, hamna tena starehe.

Taa za ukumbi zikazimwa kwa muda kukawa giza totoro kama vile hakukuwa na shamra shamra na shangwe muda mchache uliopita. Taarifa ya kutisha iliwasili mafichoni pale Amboni, kuwa wapo hatarini, adui yao anakaribia kuwateketeza kwa shambulio.

“Akhy Abu fadhli AF-Code”

“Ova Ova…!, “Nakupata vizuri kabisa AF-Code ova ova! “, Nimechomoka salama namshukuru Allah. Sasa nakuagiza nenda kwenye mtambo mkuu wa wa kulipulia mabomu ukifika nakutajia muamala wa namba za mficho ova ova!. Haina shida kiongozi nitakujuza nikifanikisha ova ova!, kazi njema ova ova!, nawe pia ova ova!”. Hayo yalikuwa ni mawasiliano baina ya marafiki wawili wakitumia msimbu wa siri katika mazungumzo yao kwa kutumia redio za upepo.

Wote wenye nia na kazi moja tu kuisambaratisha “Al-shabaab” kwa malengo tofauti. Mmoja akitaka waunde kikundi kipya kitakachopigania Uislamu bila kuwashirikisha majambazi wa “Al-shabaab” na mwengine akiwa yupo upande wa serikali anakomesha uhalifu. Haikupita hata nusu saa kambi ya magaidi ya Dibungo ikawa inalipuka mabomu mtindo mmoja, ndani ya muda mfupi ikawa kambi hiyo imegeuka Somalia ndogo kwa milipuko ya mabomu.

Haya ndio yale mabomu yalitegwa na Kachero Manu enzi anaishi kambi ya magaidi ya Dibungo, akijulikana kama Komandoo Aboubakr alipokuwa mmoja wa viongozi wa kambi hiyo. Milipuko hiyo ndio iliyosababisha magaidi wakutane kikao cha siri usiku usiku huo na kuvunja starehe zote. Kachero Manu akapewa taarifa ya mafanikio juu ya tukio hilo akafurahi kupita maelezo. Akawa sasa anagombana na usukani wa gari yake barabarani anayafuata mapango ya Amboni yalipo. Akiwa katika mchepuo mkubwa wa gari lake akasikia mtetemo kwenye soli ya kiatu chake. Mtetemo aliokuwa anausubiria kuliko hata namna mama tasa anavyosubiria taarifa ya kuambiwa ni mjamzito na daktari baada ya kuitafuta mimba muda mrefu.

Mtetemeko huo wa soli ya kiatu kwake ni zaidi ya taarifa ya mgonjwa kansa aliyekuwa watu wanasubiria wa leo au kesho kupelekwa jongomeo, aambiwe sasa amepona kabisa mzima wa afya. Chapuchapu akapaki gari pembezoni mwa barabara na kuchomoa kibati chenye ukubwa simu ya kiganjani kilichokuwa kimehifadhiwa baina ya soli ya kiatu chake.

Ndani ya kibati akakitoa kifaa chenye uwezo wa kunasa mawimbi hivyo kumtambua mtu alipo au mzigo ulipo kutokana na ‘microchip’ iliyomo ndani yake. Hiko kifaa kinatumia teknolojia inaitwa “radio-frequency identification technology” (RFID). Alipobonyeza namba za siri anazozijua yeye akaanza kupata dira na uelekeo ambao Kachero Yasmine alikuwepo muda huo.

kifaa cha “RFID” kwa Kachero Yasmine kilifungwa kwenye chupi yake maalumu aliyotakiwa aivae anapokuwa faragha na “Maso Maso” hivyo kumpa uelekeo wapi alipo “Maso Maso” iwe rahisi kumkamata. Pia mwilini mwake Kachero Yasmine alipandikizwa ‘microchip’ inayotambua nyendo zake sehemu alipo kufahamu popote alipo usalama wake binafsi.

Hizo teknolojia ndizo zilimpa kiburi Kachero Yasmine kujitumbukiza kwenye mdomo wa mamba wa magaidi akiwa kifua mbele kwa kukubali kuolewa na “Maso Maso”. “Hello Mr.Hamduni, Kachero Manu naongea hapa”, “ahaa habari za masiku tele” alijibu Mr Hamduni.

“Tunapambana Mola anatuongoza, naomba uwape Bosi wetu mkuu wa Idara ya Usalama Bwana Omega Mtanika uelekeo wa Amboni eneo ambalo tupo kama unavyosoma mawimbi ya kiteknolojia ya Kachero Yasmine. Ningeomba pia kama ingewezekana afuatane na Waziri wa Mambo ya Ndani bila kusahau wawakilishi wa vyombo vya habari vya televisheni wawepo. Tungependa tukio hili lirushwe mubashara kwa kushuhudiwa na wananchi wote Tanzania nzima na nchi za jirani” alitoa maelekezo Kachero Manu kwa njia ya simu kumpa msiri wao Kachero mwenzao aliyopo TCRA kama “Under Cover”.

Baada ya makubaliano hayo akapiga tena simu ya upepo sasa kwa rafiki yake ‘Abu-fadhli’. “Umefika wapi akhy….Abu-fadhli mie ndio naelekea Amboni sasa kwenye usiku wa kufa au kupona Ova ova! ” aliuliza Kachero Manu.

“Nisubirie pale kwenye eneo la ofisi za serikali ya kijiji cha Majimoto kisha tuondoke wote kwa pamoja, nimeshawapa taarifa za milipuko ya huku Dibungo hivyo nimeitwa kuhudhuria kikao cha dharura ambacho nina namba za siri za utambulisho wa kuingia humo mkutanoni Ova ova” alijibu Abu-fadhli, akimuelezea swahiba wake kuwa amealikwa mkutanoni.

Kachero Manu akakanyaga kibati cha mafuta sasa anaelekea ofisi za kijiji kumsubiria rafiki yake Abu-fadhli anayetokea kijiji cha Dibungo wakalianzishe mapangoni kwa pamoja.

?

“Mkutano wa dharura mapangoni”

“Salamu Aleikum wapambanaji wenzangu. Tumepata taarifa za kushtusha sana toka kambi yetu kubwa ya kijiji cha Dibungo. Imeteketezwa yote kwa mabomu na mamia ya askari wetu wameteketezwa na wengine wakiwa wamejuruhiwa vibaya.

Mmoja wa mgambo wetu mahiri sana Abu fadhli amepona na baadhi ya wana mgambo wamepona ila tayari wameshatoroka hawajulikani walipo kwa kuhofia vyombo vya dola kuwatia mbaroni”. Akapumzika kidogo kumeza mate kisha akaendelea na maelezo yake Bwana “Maso Maso”.

“Ahadi yetu tuliyoapa ni kupambana mpaka tone la mwisho la damu, hatuwezi kumsusia ngedere shamba la mahindi, tukiwapa upenyo wa kuwaogopa watatunyanyasa sana, maana Polisi ni wao, Mawakili ni wao, Mahakimu ni wao na Mahakama ni zao na Magereza ni yao watatutesa sana aheri tupambane nao kijulikane kimoja tu.

Inabidi sasa hivi hamna namna niwasiliane kimtandao na viongozi wenzangu wa “Al-qaeda” huko nchini Afghanistan na Yemen nione wanatupa msaada gani, ikiwezekana watuongezee nguvu ya wanamgambo wao. Kwa hiyo wakati tukimsubiri mwenzetu Abu-fadhli atupe taarifa rasmi ya eneo la tukio ilivyo naomna mjadala uendee huku wana mgambo wa kutosha mkihakikisha wanachukua nafasi zao za ulinzi na wawe makini wasilete uzembe wowote kulinda kambi.

Pia hakikisheni washirika wetu toka sehemu mbalimbali nchini Tanzania wanakuja sasa hivi kwenye uwanja wa mapambano, muda wa kula kuku kwa mrija waambieni umekwisha.

Wakati wa raha tulifurahi wote sasa wakati wa shida sote tuteseke kwa pamoja nina imani tutashinda, nguvu ya shetani hata siku moja haiwezi kulishinda jeshi la Allah” akapumzika kuongea kidogo kupisha makelele ya kushangilia na kupeana morali kwa maneno ya “Takbiiiir Allahu Akbar” toka kwa viongozi wenzake.

“Mategemeo ni kuwa adui atakuja hapa lazima, maana kama amefanikiwa kuteketeza Dibungo na askari wetu walioenda kutaka kumleta mateka aliyemvamia nyumbani Babu yetu mpenzi wa Jihadi hii tukufu Babu Abdullah nao wameteketezwa, kwa vyovyote kituo kinachofuata ni hapa kambi kuu.

Watakuwa bila shaka wameshapata dira ya kuwafikisha hapa tulipo. Hapa tupageuze kuwa ndio machinjio na makaburi yao, sasa tuwaadabishe kwa kuwashushia kipigo kitakatifu ambacho kitawafanya waweke maombolezo ya mwaka mzima na tutaburuza maiti zao mitaani kwenye magari na kutangaza kuwa Tanga ni nchi ya kiislamu ikiungana na Mombasa kutengeneza dola moja, Kila la kheri maandalizi yaendelee” alimalizia mazungumzo yake mafupi Bwana “Maso Maso”, Kamanda mkuu wa “Al-shabaab”, akiwaacha wenzake 24 waliobakia wakisimama kumshangilia huku wanabutua risasi hewani ishara ya kumuonyesha kuwa wanamuunga mkono wapo nae bega kwa bega mpaka dakika ya mwisho.

Wenzake wakabakia wakipanga mikakati huku yeye akienda kufanya mawasiliano na viongozi wenzake wa Al-qaeda chumbani kwake, akatokomea katika upeo wa macho yao baada ya kuondoka ndani ya ukumbi huo wa “VIP-HALL” ambao sasa uligeuka ukumbi wa mkutano baada ya muda mfupi uliopita kuwa ukumbi wa muziki.

Kachero Yasmine kutoka mafichoni nyumbani kwa “Maso Maso” mpaka hapa mapangoni ilimchukua muda wa lisaa limoja na robo tu kuwasili. Alipofika akapelekwa moja kwa moja kwenye chumba anachoishi “Maso Maso”.

Haikuwa tena sehemu ya starehe kama kule alipotoka zaidi ya kichumba kinachoingiza kitanda kimoja na sehemu ya kando ya choo pamoja na meza kubwa yenye makabrasha mbalimbali.

Alipofikishwa hakumkuta mumewe “Maso Maso” alipewa maelezo yupo mkutanoni kumbe alikuwa ukumbini huko anakula bata na tumbuizo la msanii “Bob Chollo”, mpaka walipokurupushwa na tishio la Kachero Manu sasa akili zilikuwa zimewakaa sawa ndio wakafanya mkutano wa kweli. Yasmine alivyofika tu chumbani bila kupoteza muda akabadili nguo yake ya ndani, akavaa chupi yake maalumu ile yenye utambuzi wa teknolojia ya “RFID”. Kisha akawa amepumzika tu kitandani maana huku hamna cha sofa wala nini ni mwendo wa kushinda kitandani ndani ya pango ambalo uzuri wa pekee kiyoyozi kinafanya kazi kwa nguvu ya jenereta kilikuwa kipo kazini masaa 24 ili kulipiga vita joto, vinginevyo kungekuwa hakukaliki.

Akiwa yupo kitandani anapanga na kupangua mipango mbalimbali katika serikali yake ya kichwani ghafla mlango wa chumba chake ukafunguliwa, Mzee baba “Maso Maso” akawa anaingia chumbani. Akawa hana jinsi zaidi ya kujilazimisha kwa shingo upande kunyanyuka kumlaki mumewe “Maso Maso” asije kutimuliwa kwa mangumi na mateke kisha kupewa talaka juu kwa kuonekana hajui kumpetipeti mume bure.

“Salaamu aleikum…. Oooh wao my Dear husband pole na kazi” alisema Yasmine huku amemkumbatia kwa nguvu “Maso Maso”. Ambaye nae alijibu mapigo kwa kumzungushia mikono nyuma ya mgongo wa Yasmine. “Waleikum salaam mke wangu mahabubu wangu, pole na safari karibu nyumbani kwako tena” alijibu “Maso Maso” huku sasa alimwachia mikono yake toka kiunoni.

“Maso Maso” alikuwa bado anatafuna pipi kukata harufu ya sigara alizovuta kule ukumbini. Alikuwa anamheshimu sana Yasmine na kumpenda huku mwenyewe akijua Yasmine ni mchamungu sana hivyo hatofurahia kunusa harufu ya sigara mdomoni mwake. Na hiyo ikawa ndio pona ya Yasmine asinyonywe denda na mumewe, ikawa ile hadithi ya kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi. Akapitiliza moja kwa moja bafuni kwenda kupiga mswaki.

Yasmine akawa bado amebakia kitandani roho inamdunda anasubiria dhahama ya kuombwa unyumba na mumewe. Alipotoka “Maso Maso” bafuni akatoka akiwa amevalia bukta lake nyeupe na juu hajavaa chochote yupo kifua wazi akapitiliza moja kwa moja mpaka mezani kwake ambapo kulikuwa chupa kubwa ya chai.

Akaifungua na kuvuta bakuli ndogo pembeni yake akawa anamimina maji maji kutoka kwenye ile chupa kisha akaifunga. “Karibu kinywaji hiki mchuzi wa pweza huwa nakunywa kila siku asubuhi na usiku kabla sijalala” alikaribishwa Kachero Yasmine na mumewe. “Ahsante mume wangu nimeshiba endelea tu” alijibu Kachero Yasmine kwa kujitutumua tu lakini alikuwa na mawazo kibao sana.

“Anakunywa supu ya pweza tena dozi mara mbili kwa siku, anajiandaa na kitu gani, hii supu ya pweza si wanasema ni ‘viagra’ ya asili!” alikuwa anawaza moyoni mwake huku kijasho jekejeke kile chembamba kinamvuja licha ya kwamba kiyoyozi kilikuwa kinafanya kazi yake ipasavyo.

Alivyomaliza kunywa mchuzi wa pweza akawa anakuja kitandani, Kachero Yasmine akawa anaomba kila aina ya dua kikombe cha kuingiliwa na “Maso Maso” kimuepuke. Alikuwa anajua sasa kazi inakuja ameifuata mwenyewe gharika. Maso akakivuka kitanda na kwenda kurudisha pazia dirishani kisha haraka haraka akarudi kwenye meza yake na kufungua mtoto wa meza akachomoa kompyuta ndogo akaweka modemu ya mtandao akawasha akaanza kuitumia mule chumbani.

Kompyuta ilikuwa ina vumbi la kutosha kuonyesha inatumika kwa nadra sana. Alishusha pumzi ndefu Kachero Yasmine kama mtu aliyemaliza kushuka mlima mrefu baada ya kuona kama amenusurika mumewe hana muda na yeye katingwa na kazi zake. Akaanza kupitiwa na usingizi wa mang’amung’amu huku akiwa hajiamini kama usiku wa leo atasalimika na kutakucha salama.

Saa 4:30 usiku Kachero Manu akiwa na sanjali wake Abu fadhli waliwasili mapangoni tayari kwa kazi. “Mie nitashuka na kuingia mkutanoni wewe usishuke kwanza hauna nguo walizovaa walinzi leo. Ila nitakuletea mboga sasa hivi itakayokusaidia kuingia ndani ya mkutano, usifunge dirisha nampa mboga ufunguo wa gari umpe mfueni wa nguvu” alisema Abu fadhli huku akikumbatiana na Kachero Manu wakaagana tayari kwa usiku wa kazi.

Abu fadhli alikuwa anatembea akiwa amevaa kombati za kijani huku juu amevaa kofia ya kijeshi mpaka alipomfikia mlinzi wa kwanza. “Hello nenda kanifungue kioo cha gari yangu nimesahau nitaukuta ufunguo kwako ninawahi kikao” alitoa amri Abu fadhli kwa yule mlinzi huku moyoni akimuonea huruma kitakachomkuta huko aendako. Yule mlinzi kwa kutaka kujipendekeza alikuwa anaenda mbio mbio bila tahadhari yoyote, kufika akaingiza funguo kwenye tundu la mlango, akautikisa kidogo ule funguo, mlango ukajibetua ukafunguka.

Akaingia ndani ya gari ile anataka kuwasha ili apandishe kioo, Kachero Manu akamgusa bega akageuka na kutumbua macho kama ameona mzimu wa Mababu. Kachero Manu hakutaka kumpa nafasi akamlamba kareti moja takatifu ya shingoni jamaa pale pale akakauka kwa kifo cha ghafla. Akamvua kombati zake za rangi ya kaki, chapuchapu akazivaa yeye na kujivika pama, ungemuona utasema ndio pacha wa yule mlinzi.

Akamvutia chini ya uvungu wa gari akachukua ile silaha ya yule mjuba akaikagua akaikuta imejaa risasi. Akatega bomu ndani ya gari lile na kuliacha kama lilivyo. Akaanza kutembea kuelekea uelekeo ule ule aliokuja nao yule mlinzi. Alipokaribia akaona kuna mlinzi mwingine amekaa kama meta 200 kutoka alipo yeye macho yake kodo upande anaotokea Kachero Manu.

“Sssss…Ssssss…Ssssss… ! ” Kachero Manu alipiga mluzi kumuita yule mlinzi aliye jirani na yeye. Yule mlinzi akawa anakuja haraka haraka akijua kuna jambo limetokea alipokaribia tu Kachero Manu akajifanya kama kuna kitu kwenye kichaka kilichopo jirani na alipo. Yule mlinzi akajifanya kimbelembele kutangulia mbele ili ajinyakulie sifa za ushujaa. Kachero Manu hakumkawiza kumtanguliza njia ya marhaba, akamtandika risasi mbili za mgongoni kwa kutumia bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Sasa alipochunguza akakuta wamebaki walinzi kama wanne tu aweze kuingia ndani ya jabali kubwa lililopo umbali kidogo kutoka alipo.

Akachomoa redio yake ya upepo toka kiunoni alipoipachika akaanza kuigiza anaongea na mtu huku anawapita mutawalia. “Hello ova ova..!!eeh…nakuja ndani haraka, huku nje hali ipo shwari kabisa, dakika moja nipo hapo kiongozi ova ova…!!” wale walivyomuona mwenzao anaongea na simu hawakumtilia mashaka kabisa wakamuacha tu apite huku wengine wakionekana wana uchovu wa usingizi.

Alipowavuka tu akalivuka jabali lilitobolewa katikati. Akapenya jabali lile akatembea kwenye mwangaza hafifu kama dakika 10 akaona mbele yake maandishi ‘VIP HALL-05’, akajua ndio humu humu hawa manyang’au walipojichimbia. Alipofika akauchapa mlango teke ikafunguka akajirusha ndani kwa mtindo sarakasi na kuanza kushambulia kwa ghafla.

Shambulizi ambalo halikutegemewa na yoyote kuja tahamaki watu kama 10 tayari wameshalala chali wanalamba mchanga. Abu Fadhli nae akaanza kuwafyekelea mbali kwa mtutu wake, mpaka ukumbi unabakia na viongozi kama 6 tu huku damu zikiwa zimetapakaa. Mmoja wa wale maadui ambaye alijifanya amekufa akaanza kutambaa na ukuta mpaka akajiweka nafasi nzuri akafanikiwa kumlipua risasi za kifuani Abu fadhli na kumrusha hewani alipotua chini tayari marehemu wa juzi. Mziki ukabakia kwa Kachero Manu anatunguana nao kwa kuviziana.

Katika wale 6 waliobakia, 3 wakafariki dunia huku 2 wengine wakifanikiwa kutoroka ndani ya kile chumba kwa kutumia njia za panya. Kachero Manu akakimbilia kwa rafiki yake Abu fadhli akamkuta wabaridi kabisa tayari ameshafariki. Akambusu kwenye paji lake la uso, na kuiacha maiti yake mle mle ndani huku anafuata maelekezo kile kimashine chake cha “RFID” kumfuata alipo Kachero Yasmine na “Maso Maso”.

Alipotoka ukumbini aliwakuta wale walinzi bado wapo pale nje hawajui kinachoendelea ndani kutokana na ukumbi kuwa hautoi sauti nje. “Hello nendeni kwenye lile gari mkatoe mzigo haraka sana unahitajika kwenye ukumbi wa mkutano nimeagizwa hivyo”.

Maskini ya Mungu bila kujua wanayafuata mauti walivyokaribia kufika huku Kachero Manu alikuwa anafanya makadirio yake wakashtukia gari limelipuka na wao tena buriani maisha ya dunia imewakumba. Mlipuko ule ulikuwa mkubwa ukazusha kishindo kikubwa eneo lile, haraka haraka akawa anaelekea sasa chumbani kwa Yasmine kwenda kumtia mbaroni “Maso Maso”.

“Maso Maso anayeyuka kimaajabu”

Kachero Yasmine alikuwa amepitiwa kidogo na usingizi hadi alipokurupushwa usingizi na mumewe bandia “Maso Maso”. “Yasmine Yasmine tumevamiwa amka fasta” alizungumza “Maso Maso” kwa sauti ya juu. Yasmine nae akazinduka usingizini, akafikicha macho alijiona kama yupo ndotoni.

Ndipo akagutuka kuwa ni ukweli sio ndoto. Akavua haraka haraka nguo yake ya kulalia akavaa suruali dangirizi nyeusi iliyombana vilivyo na brauzi nyeupe juu. Kisha akauliza kwa sauti ya masikitiko “kwanini unavamiwa umewafanya kosa gani mume wangu?”. “Sasa sogea hapa nikufundishe namna ya kutumia silaha kujilinda, nitakuambia siku nyingine kwanini wananiwinda” aliongea “Maso Maso” huku anamkabidhi bastola mkewe aliyoichomoa kwenye suruali yake pana kombati ya jeshi iliyoonekana imetunatuna bila kujua huyo ni bobezi kwa matumizi ya silaha.

Alipokabidhiwa tu bastola huko nje ya mlango kukawa kunatoka mlio kama wa kengele, ambao Kachero Yasmine alifahamu huyo ni Kachero Manu yupo nje ya chumba na kifaa chake cha “RFID” hivyo wakati umefika. “Tupa bastola chini na nyoosha mikono juu gaidi mwanaharamu wewe” Kachero Yasmine alifoka kwa sauti ya kazi sio tena ile nyororo ya kubembeleza aliyoizoea “Maso Maso”. “Maso Square The Duduman” hakuamini anachokisikia katika masikio yake na wala macho yake hayakutaka kusadikisha kama kweli mke wake ndio huyo aliyembadilikia. Uso wake ulipigwa na taharuki alishatanabahi huyu mke wake kumbe alikuwa ni jasusi aliyepandikizwa kwake, lakini alishachelewa. Akatupa chini bastola yake na kutii amri ya kunyoosha mikono yake juu. “Rudi kinyumenyume usilete ujanja wowote nitakusambaratisha sasa hivi” alizidi kufoka Kachero Yasmine akihofia akiwa karibu yake anaweza kuanzisha mapigano.

Wakati anarudi kinyumenyume “Maso Maso” alikuwa uso wake umebeba tabasamu kama lote hana chembe yoyote ya hofu, mpaka Kachero Yasmine akaingiwa na hofu yeye. Ghafla Kachero Manu nae akavamia ndani baada ya kuvunja mlango kwa kutumia risasi. Hiko kishindo kilikuwa kosa kubwa sana kwao kwani Kachero Yasmine alivyopepesa macho yake kidogo tu kumuangalia Kachero Manu anavyoingia, “Maso Maso” akawa ameshafika ukutani akabonyesha swichi ya mfumo wa ulinzi wa kutumia ukungu mweupe unaosambaa kwenye chumba kama moshi mweupe.

Mfumo huo kitaalamu unaitwa “Smoke Security System”(SSS) ambao Tanzania ulikuwa bado haujaingia kabisa. Kwenye huo mfumo huo ukungu unazalishwa pindi glycerine iliyochanganyika na maji yaliyotakaswa ‘distilled water’ yakipashwa joto la umeme.

Ni mfumo ambao nchi zilizoendelea unafungwa kwenye mabenki makubwa, na stoo za kutunzia bidhaa za thamani kubwa. “Maso Maso” aliwachapa kibao cha teknolojia Makachero hao. Wakawa ndani hawaonani moshi mweupe na mzito unasambaa chumba kizima. “Kamata kamata huyoo anatoroka Kamata huyooo…” Kachero Yasmine alikuwa ameshapagawa anapiga kelele bila mpangilio. Kachero Manu chapuchapu akatoa miwani yake maalumu akavaa kidogo ikawa inamsaidia kuona kwa tabu.

Akaenda mpaka ukutani na kufanikiwa kuzima swichi ya mfumo huo wa ukungu. Baada ya kama robo saa hali chumbani ikatungamana, ukungu ukawa umetoweka, tahamaki wanajikuta wapo watu wawili tu, “Maso Maso” ameshatoweka hajulikani alipo.

MWISHO

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment