Behind the Curtain – September 11 Sehemu ya Tano
KIJASUSI

Ep 05: Behind the Curtain – September 11

SIMULIZI Behind the Curtain - September 11
Behind the Curtain – September 11 Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA: THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi: Behind the Curtain – September 11

Sehemu ya Tano (5)

December 1998

Kwa mara nyingine tena CIA walikusanya Intelijensia na kubaini kuwa Osama atakuwepo kwenye jumba linaloitwa Haji Habash ambayo ni sehemu ya makazi ya gavana wa Kandahar.

CIA wakapendekeza lifanyike shambulio la Anga (air strike), lakini Rais Clinton akakataa kutoa ruhusa na baada ya kumng’ang’aniza sana akatoa ruhusu labda wamkamate akiwa hai (Capture Operation) lakini sio air strike.

Sababu yake kuu, ati alikuwa anahofia maisha ya watu wasio na hatia kwenye jumba hilo.

February – March 1999

CIA walipata taarifa za Intelijensia kuwa Osama alikuwa anatembelea mara kwa mara kwenye kambi za uwindaji maeneo ya jangwani mwa Kandahar ambako kulikuwa na wageni kutoka Emirates.

CIA wakajitahidi kupata Intelijensia kujua Osama huwa anakaa kwenye mahema gani akitembelea kambini hapo.

Baada ya kuwa na taarifa za kutosha kwa mara nyingine wakapendekeza kufanyika air strike siku Osama akiwa kambini hapo, lakini kwa masikitiko makubwa Bill Clinton akakataa akidai kuwa kuna taarifa kuwa moja ya wageni hao kutoka UAE ni Prince wa Emirate hivyo anahofia kuharibu mahusiano ya kidiplomasia.

November – December, 2000.

Al-Qiada walikuwa wamefanikiwa kufanya shambulizi kwenye kituo cha kijeshi cha Marekani nchini Yemen na kuna wanajeshi kadhaa.

Kwahiyo Osama alikuwa anahisi Marekani lazima watafanya oparesheni ya kisasi (Retaliation).

Kwahiyo ili kuchukua tahadhali kwa kufunga kwa muda kambi zake za mafunzo huko Kandahar na pia akawagawanya viongozi wakuh kwenye maeneo tofauti tofauti ili wasiwe sehemu moja ikitokea wameshambuliwa.

Kamanda wake mkuu wa jeshi, Mohammed Atef akajificha pembezoni mwa mji wa Kandahar, msaidizi wake mkuu Ayman al-Zawahiri akaenda Kabul na yeye mwenyewe akawa anabadilisha makazi kila kukicha.

Kwanza akaenda Kabul, kisha akaelekea Khowst, baadae akaenda Jalalabad na kisha akarejea tena Kandahar.

Akiwa Kandahar kulikuwa na nyumba sita ambazo alikuwa anabadilisha ratiba ya kulala kila siku.

CIA walikuwa wanafuatilia nyendo zake zote hizi, na baada ya kuwa na Intelijensia ya kutosha kuhusu ‘rotation’ ya movement zake wakapendekeza kwa Rais Clinton ifanyike Air Strike katika nyuma anazoishi mjini Kandahar.

Kwa mara nyingine tena, Rais Clinton akakataa kutoa approval ya air strike akidai kuwa labda wafanye ‘capture oparation’

Kutokana na risk kubwa ya capture Opararion, ikawabidi kwa mara nyingine tana CIA kuhahirisha Oparesheni.

Sasa,

CIA walikuwa wanang’ang’ana kum-neutralize Osama mapema kwa kuwa walikuwa wanaamini kuwa yuko kwenye mipango ya kutekeleza tukio kubwa sana.

Ni ajabu sana jinsi ambavyo Rais Clinton na viongozi wa juu walivyokuwa wanakwamisha juhudi za kum-neutralize Bin Laden.! Labda kuna jambo walikuwa wanalijua ambalo majasusi wengine hawakulijua..

Labda, Osama alikuwa anaachwa kwa makusudi ajinenge na mtandao wake ushamiri kwa makusudi.!!

“…lawama za tukio la 9/11 zinapaswa kuelekezwa kwa watu ambao waliicha Al-Qiada ikue na kushamiri na maamuzi ta kumpoteza kiongozi wao hayakufanywa pale ambapo fursa ilijitokeza.. Sio mara moja, bali mara nne nzima.. Rais Clinton hawezi kuepuka lawama hii..”

-Senata Marco Rubio, Mogombea tiketi ya Urais katika chama cha Republican. (Alisema haya kwenye mdahalo wa February 13, 2016).

Nimeeleza kwa kina namna gani kunaonyesha kwamba kulikuwa na dalili ya kumuacha Osama bin Laden na mtandao wake wa Al-Qaida wakue na kushamiri.. Sasa twende mbele kidogo uone upotoshaji na uongo uliokuja kufanyika wenye kutia mashaka makuba..

‘UONGO ‘ULIOTUKUKA’

Mara baada ya kutokea shambulio la 9/11 viongozi wa juu qa serikali karibia wote walijitokeza hadharani na kutoa kauli mbali mbali.

Moja wapo ya kauli hizi zilitolewa na wafuatao;

Rais George W. Bush,

“..nobody in our government at least, and I don’t think in the prior government, could envisaged flying airplane into buildings..”

(“..hakuna mtu katika serikali serikali yetu, na nadhani hata serikali iliyopita (Bill Clinton), ambaye angeweza kudhania kungekuwa na shambulio ambalo litatumia ndege kulipua majengo..”)

Kauli hii ya Rais George Bush ikafuatiwa na kauli ya Mwanamama Condoleezza Rice kipindi hicho akiwa mshauri wake Mkuu wa masuala ya Usalama (National Security Advisor).

“..no one could have predicted that they would try to use an airplane as a missile..”

(“.. Hakuna ambaye angeweza kubashiri kwamba watajaribu kutumia ndege kama silaha..”)

Kauli hii ikaja kuungwa mkono pia na Jenerali wa Jeshi la Anga (Air Force).

“..something we had never seen before, something we had never even thought of..”

(“..(hiki) ni kitu ambacho hatujawahi kukiona, kitu ambacho hatujawahi hata kufikiri..”)

Mkurugenzi Mkuu wa FIB naye wa kipindi hicho, Bw. Robert Mueller akajazia uzito kauli hizi,

“…there were no warnings signs that I’m aware of, that would indicate this type of operation in the country..”

(“..hakukuwa na tahadhari au onyo ambalo nimewahi kulisikia ambalo liliashiria kutakiwa na shambulio la dizaini hii ndani ya nchi..”)

Ukizichunguza kwa makini kauli zote hizi za hawa mabwana wakubwa wanalenga kuwaaminisha Wamarekanimambo mawili;

Moja: kwamba serikali na vyombo vya Usalama havikuwa na intelijensia yoyote kuhusu mipango ya shambulio hili.

Pili: hata kama intelijesia yao ingeshuku au kuhisi mipango ya tukio hili, kamwe wasingeliweza kudhania kwamba ndege ndio zingetumika kama silaha, kwasababu ni jambo ambalo hawakuwahi kudhania na halijawahi kutokea. Hivyo kamwe wasingeweza kuhisi shambulizi la kutumia ndege.

Kauli hizi zina uwongo wa nje nje ambao ndio unafanya wengi katika Jamii ya Intelijensia waamini kuwa kuna mambo yanafichwa kwa makusudi.

Kwanza si kweli kama Rais Bush na wenzake wanavyodai kuwa hili ni suala jipya hivyo wasingeweza kuhisi kutumika ndege kama silaha, na pia si kweli kwamba serikali haikupewa tahadhari..

Nitaeleza….

Mwaka 1994; kuna ndege binafsi ambayo ilikuwa imembeba mtu mmoja tu ambaye yeye mwenyewe akiwa kama rubani kwa makusudi kabisa aliidondosha ndege katika Ikulu ya Marekani, Washington kwa lengo la Kufanya shambulio. Kwa bahati nzuri ndege ikadondoka kwenye viambaza vya Jengo la Ikulu (lawn).

Kwahiyo hii kauli ya Bush kwamba “…nobody…. could envisaged flying airplane into building..” ni kauli ya uongo wa makusudi kabisa.

Si hivyo tu,

Mwaka 1995; nchini Ufilipino lilitokea mpango wa shambulio lililofeli, ambalo linajulikana kwa jina maarufu la Bojinka Plot. Shambulio hili ambalo lilipangwa na Khalid Sheikh Mohammed lililenga kuteka ndege za Marekani na kwenda kuzibamiza kwenye majengo. Bahati nzuri CIA kwa kushirikiana na Idara Ya Intelijensia wakaepusha shambulio hili kabla halijatokea.

Ndipo hapo ambapo miaka ya baadae KSM akapeleka wazo hili kwa Osama.

(Nilieleza kisa hiki kwenye sehemu za mwanzo za makala hii)

Kwahiyo kauli ya Jenerali wa Air Force kwamba “…something we have never seen before…” ni kauli ya uongo wa makusudi kabisa

Pia,

Mwaka 200, Federal Aviation Administration (FAA) katika ripoti yao ya Usalama wa Anga, kuna vipengele kadhaa wanaonyesha wasi wasi wao kuhusu kutokea kwa ugaidi na kuna paragraph wanamtaja kabisa Osama bin Laden.

Nanukuu kipande kifupi,

“..considering Bin Laden anti-Western and anti-American attitudes, makes him and his followers a significant threat to civil aviation particularly to United States Civil Aviation..”

(“..kwa kuzingatia mitazamo hasi ya Bin Laden juu ya nchi za magharibi na Marekani, kunamfanya yeye na wafuasi wake kuwa tishio kubwa kwa usafiri wa Anga na mahususi usafiri wa Anga wa Kibiashara/kirai nchini Marekani..”).

Hii ni ripoti ya kiusalama ya Idara kubwa ya nchi ya Marekani inayosimamia usafiri wa Anga. Wanaonyesha wasi wasi wao juu ya Usalama wa usafiri huo na wakimtaja kabisa Osama bin Laden kwa majina yake.

Inashangaza sana kwanini Bush, Condoleezza, Jenerali na Mkurugenzi wa FBI waseme kwamba, kutumika kwa ndege kama silaha ni kitu ambacho wasingeweza kukidhania au kukihisi.

Si hivyo tu,

Mwanzoni mwa Mwaka 2001 (February): NORAD (North American Aerospace Command) walipata ‘alert’ kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi kwa kutumia ndege.

Mwanzoni walidhania kwamba ndege hizo zinaweza kuingia Marekani kutokea Ulaya, kwahiyo wakaanza mazoezi katika bahari ya Atlantic ili kuona namna bora ya kudhibiti ndege hizo ikitokea hilo suala likatokea kweli inabidi wadhibiti ndege kabla haijaingia Marekani.

Kwahiyo mazoezi yao kwenye bahari ya Atlantic yalienda mbali mpaka kufikia hatua wakawa wanarusha ndege chakavu na kuzidungua.

Baadae wakahamia kwenye mazoezi ya “simulation”.

Moja ya sehemu waliyofanya mazoezi hayo ilikuwa ni World Trade Center kwa maana walihisi kuna uwezekano wa majengo hayo kulengwa.

Baadae wakaomba kibali wafanye mazoezi hayo ya ” simulation” kwenye majengo ya Pentago. Lakini ajabu ni kwamba kamati ya Majedari wa vikosi vya ulinzi (Joint Chiefs of Staff) wakatoa amri ya kusitishwa kwa mazoezi hayo wakiwapa sababu moja tu kwamba, suala hilo wanalolihisi (Shambulio la ndege) ni “too unrealistic “

Nitoe mfano mwingine ili khonyesha uongo wa kauli hii ya Rais Bush na wenzake kwamba, Shambulio la ndege ni kitu ambacho wasingeweza kudhania.

July, 2001, khlikuwa kunafanyika kongamano la G8 (G8 Summit).

Katika hali inayodhihirisha kwamb a walikuwa na taarifa kuhusu tahadhari ya Shambulio la ndege, kwenye majengo ambayo mkutank ulifanyika kulifungwa “Anti-Aircraft missile battery” ili kujihami na Shambulio la ndege walilokuwa wanalihisi kuwa linalenga kumuua Rais Bush na viongozi wengine.

Si hivyo tu,

THE PHOENIX MEMO

July 10, 2001, Afisa wa FBI, Special Agent Kenneth Williams ambaye alikuwa ofisi ya Arizona alikuwa na assignment ya kuwafanyia uchunguzi wanafunzi kadhaa katika vyuo vya urubani kutokana na wanafunzi hao kutiliwa shaka nyendo zao.

Baada ya kuwachunguza kwa miezi kadhaa, Special Agent Kenneth Williams akaandika barua kwenda FBI makao makuu kuwapa tahadhari na kupensekeza ufanyike uchubguzi kwenye vyuo vyote vya urubani nchi nzima kwani anahisi kuna mapandikizi ya ugaidi ambao wanaweza kuleta madhara.

Nanukuu sehemu ya barua yake;

“…would like to advise the Bureau and New York of the possibility of a coordinated effort by Osama Bin Laden to send students to the United States to attend Civil aviation Universities and Collages. Phoenix has observed an inordinate number of indivie of investigative interest who are attending civil aviation Universities and collages in the state of Arizona..”

(“..naishauri/naitahadharisha Idara na jimbo la New York juu ya uwezekano wa uratibu makini wa Osama bin Laden kutuma wanafunzi nchini Marekani kuhudhuria vyuo vya urubani. Phoenix tumegundua uratibu was watu kadhaa wenye kupaswa kuchunguzwa ambao wanasomea urubani katika vyuo mbali mbali jimboni Arizona..”)

Barua hii ikatumwa makao makuh ya FBI.

Kwa utatibu wa Jamii ya Intelijensia (Intelligence Community) taarifa hii ilikuwa inapaswa pia kushirikishwa watu wa CIA.

Ajabu ni kwamba baada ya barua hii kufika makao makuu, wakubwa “wakaifinya” na kukaa kimya mpaka pale wafukunyuka katika Jamii ya Intelijensia walipokuja kuiona hii barua Mwaka 2002 tukio likiwa limeshatokea.

Kama hiyo haitoshi,

March 2001, Idara ya Ujasusi ya Italia, ilinasa mawasiliano ya simu ya wanachama wa kijiwe (cell) cha ugaidi nchini jijini Milan.

Baada ya kuchambua mawasiliano hayo wakagundua kuwa walikuwa wanaongelea mpango wa ulipuaji majengo Marekani kwa kutumia ndege.

Bila kuchelewa, Idara ya Ujasusi ya Italy ikawajulisha suala hiyo wamarekani.

Mwaka 2001, Idara ya Ujasusi ya Jordan iliwatumia taarifa serikali ya Marekani kwamba wana Intelijensia ya kutosha kujiridhisha kuwa Al-Qaida wanapanga shambulizi katika ardhi ya Marekani na wanahisi ndege zinaweza kutumika.

Mwezi huo huo July 2001, Idara ya Ujasusi ya Misri inawaonya wenzao wa Marekani kwamba wana Intelijensia inayoknyesha kwamba kuna watu 20 wamepenyezwa nchini Marekani na Al-Qaida na wanne kati ya hao ishirini wanasoma kwenye vyuo vya Urubani.

Mwezi August 2001, Mossad wanawapatia Wamarekani orodha ya watu 19 ambao wameingia nchini Marekani ambao Mosaad waliamini kuwa wameenda nchini humo kwa ajili ya kufanya Shambulio.

Mwezi huo huo August 2001, Idara ya Ujasusi ya Uingereza inatuma taarifa Mara mbili kuwa wana taarifa ya Intelijensia kuonyesha kuwa kuna magaidi wamepanga kufanya Shambulio ndani ya Marekani muda si mwingi.

Mwisho mwawezi huo wa August, Uingereza inatuma tena taarifa ya tatu na kuwaambia kuwa Shambulio wanalolihisi litatumia ndege.

Kuna ushahidi kuwa taarifa hii ya tatu ilipelekwa moja kwa moja kwa Rais Bush na Wasaidizi wake.

Mwanzoni mwa mwezi September 2001, kwa mara nyingine tena Idara ya Ujasusi ya Misri wanawasiliana na Marekani kuwataarifu kuwa wana Intelijensia ambayo inathibitisha kuwa magaidi waliopandikizwa nchini Marekani wapo kwenye “advanced stage” ya kutekeleza Shambulio siku chache zijazo.

Licha ya maonyo yote haya, tahadhari zote hizo na taarifa za Intelijensia zilizoshiba, je Rais Bush na wenzake walifanya nini??

NOTHING..!!

Yes, hakuna chochote ambacho walikifanya na kwenye taarifa zao za awali baada ya tukio pasipo kujua watu watafukunyua haya masuala, wanawadanganya Wamarekani kwamba “..hawakujua na wala wasingeweza kuhisi au kudhania Shambulio kama lile lingeweza kutokea..”

Huu ni “uongo uliotukuka” kwani ushahidi unaonyesha dhahiri kuwa walikuwa na taarifa za Intelijensia kuhusu 9/11 kabla haijatokea..

Na kama ni kweli ilikuwa ni Bahati mbaya, basi huu ulikuwa ni uzembe uliopitiliza ambao hawezi hata kutokea kwenye Idara zetu za Ujasusi kwenye nchi zetu za Ulimwengu wa tatu.

Nikirudi katika sehemu ya 12, nitaeleza mambo kadhaa yanayoashiria dhamira ya kwanini tukio hili la 9/11 liliachwa litokee. Tutaendelea Ijumaa..

Good Afternoon.!!

SEHEMU YA 12

Katika sehemu ya 10 na 11 nilionyesha ni namna gani ambavyo kuna dalili zinaonyesha kwamba inawezekana Osama bin laden na al qaida waliachwa washamiri kwa makusudi.

Pia nilionyesha ushahidi wa taarifa za kijasusi ambazo ziliwafikia serikali ya Marekani na vyombo vya usalama lakini hawakuzifanyia kazi.

Katika sehemu hii ya mwisho ningependa kujadiri dhamira ya kwanini labda Wamarekani waliacha tukio hili litokee.

Nafahamu kuwa kuna nadharia nyingi ambazo zimeenea sana kuhusu “kwanini tukio hili liliachwa litokee??”

Sasa kabla sijaanza kujadili hoja zangu, ningependa niongelee baadhi ya nadharia chache maarufu na kueleza sababu zangu kwanini siziamini hizo nadharia.

Moja; kuna nadharia kwamba hakukuwa na shambulio lolote la ndege isipokuwa zilitumika ‘hologram’ kuonyesha kwamba kuna ndege.

Nadharia hii ilianzishwa na Mchumi Morgan Reynolds ambaye aliwahi kufanya kazi kwenye Wizara ya Kazi kipindi cha utawala wa Bush.

Hii nadharia binafsi naiona haina mashiko kiasi kwamba haitakiwi hata kujadiliwa.

Mbili; Kuna nadharia ambayo inafanana na hiyo nadharia ya juu hapo.. Nadharia hii inapigia chapuo sana na watu wa “The Truth Movement” pamoja na manguli wa nadharia za Conspiracy, Bw. Alex Jones.

Hii nadharia inadai kuwa ndege ya flight 77 haikulipua Jengo la Pentagon bali kilicholipua lilikuwa ni Kombora (missile).

Hoja hii inatiliwa mkazo na shimo lililotengenezwa kwenye ukuta wa pentagon baada ya kulipuka. Ukiangalia lile shimo (niliwahi kuweka Picha yake, tafadhali rejea) haliendani na ukubwa wa ndege yenyewe au umbo la ndege.

Hoja nyingine ni kwamba, Jengo la Pentagon liko chini chini sana, (ghorofa tano tu) hivyo ni ngumu kwa ndege kutoka angani kujibamiza ‘vertically’ kwa ufanisi namna ile.

Namna pekee ingewezekana ni kwa kutumia Kombora.

Kwa haraka haraka nadharia hii inashawishi kuaminika na inaonekana ina mashiko.

Lakini, binafsi nimefanikiwa kuona kipande cha video ya Security Camera iliyokuwapo ng’ambo ya Jengo la Pentagon siku ya 9/11.

Video hii yenye urefu wa kama sekunde 6 pekee inaonyesha kwamba, kabla ya flight 77 kujibamiza Pentagon, ilikata kon a kali kuelekea Pentagon na iliruka chini chini sana kiasi kwamba bawa moja likagusa ardhini na kuvunjika.

Pia nikataka kujiridhisha kuhusu uimara wa Jengo la Pentagon. Nikakuta kwamba, Jengo hili limekuwa likifanyiwa matengenezo (renovations) tangu miaka ya 1980s.

Sasa pale pale mahala ambapo flight 77 ilijibamiza kulikuwa na ‘load-bearing column’ (nguzo ya kusapoti uzito wa Jengo).

Kwa hiyo bawa moja lililobakiwa lilijibamiza kwenye nguzo hii.

Hii ndio sababu kwanini likajitengeneza shimo lisilokuwa na muonekano wa umbo la ndege.

Lakini pia eneo la tukio iliokotwa miili ya watu waliokuwemo kwenye ndege, na si hivyo tu kulikuwa na makumi ya mashuhuda walioshuhudia hili likitokea (eye witness) na wakapiga 911.

Kwa hiyo hii nadharia nayo siipi nafasi.

Tatu; Kuna nadharia kwamba hakuna myahudi/muisraeli aliyekufa kwenye lile tukio kwasababu tukio lilipangwa na Israel kupitia Mosaad kwa kushirikiana na CIA.

Ajabu ni kwamba, kuna mamilioni ya watu wanaoamini hii nadharia na imejipatia umaarufu mkubwa sana pasipo watu kujua hii nadharia imetokea wapi.

Ni kwamba;

Kwa mara ya kwanza kabisa nadharia hii kuongelewa ilikuwa ni siku ya September 17 katika kituo cha televisheni cha Al-Manar nchini Lebanon.

Kituo hiki kinachorusha matangazo yake kwa Satellite kinamilikiwa na Hezbollah, wapinzani wakubwa wa Israel.

Binafsi nikisikia jambo lolote Israel wanalisema kuhusu Hezbollah huwa lazima nitie shaka kama wanasema ukweli,l.

Vivyo hivyo nikisikia chochote kinasemwa na Hezbollah kuhusu Israel lazima pia nitafakari kabla ya kukiamini.

Uhasimu wa Hezbollah na Israel umefanya hata pale muda mwingine wakiongea ukweli mtu mwingine unakuwa na mashaka, na pia wamefanya hata pale wakiongea uongo mashaiki zao wanaamini pasipo kutafakari.

Ukweli ni upi,

Mpaka kufikia leo hii tarehe 14 March 2017, imethibitika kwamba jumla ya watu 81 wenye asili ya kiyahudi walifariki katika tukio la 9/11.

Kati ya Wayahidi hao, watu watano wa uraia wa Israel moja kwa moja ma wengine 76 sana Uraia wa Marekani.

Hii inathibitishwa na nyaraka za wizara ya mambo ya nje ya Marekani (U.S State Department) kuhusu ripoti ya waliofariki kwenye tukio ya 9/11.

Lakini pia unaweza kutazama orodha ya majina ya waliokufa kwenye tukio la 9/11.

Lakini kwa mujibu wa taarifa za ndugu jamaa na marafiki, inakadiriwa kwamba idadi ya Watu wenye asili ya Israel/wayahudi waliokufa siku ya 9/11 inaweza kufikia watu kati ya 270 hadi 400.

Kwa hiyo hii nadharia kwamba, hakuna muisrael/myahudi aliyefariki siku ya 9/11 siipi nafasi sana.

Sasa, kwenye makala nimeeleza kuwa kuna dalili kuwa tukio liliachwa litokee kwa makusudi!!

Sasa ni dhamira gani iliwasukuma kufanya hivi??

Sasa nisingependa kutoa hoja zenye kuhitimisha huu mjadala kwa kuwa suala hili ni pana na linapaswa kuachwa lijadiliwe.. Lakini ili mjadala uweze ‘kunoga’ inapswa kuwe na dondoo za kusukuma mjadala mbele…

Hivyo basi, ninatoa dondoo chache za mwisho ili kuhitimisha mfululizo wa makala hizi..

‘PUT OPTIONS’

Nieleze kitu Fulani kwa kifupi kabla sijaingia kwenye hoja yangu;

Katika masoko ya hisa yalioendelea kuna kitu kinaitwa ‘put optionts’ (au ‘put/the put’ kwa kifupi).

Put options ni nini?

Huu ni mkataba (ambazo ni hisa) ambapo muuzaji wa hisa (seller) anakubaliana na mnunuzi wake (buyer/holder) kwamba anamuuzia hisa lakini katika kipindi cha muda fulani mahususi (expiry/time of expiration) kama hisa hizo zitashuka thamani Fulani (strike price) basi muuzaji huyo atakuwa anawajibika kuzinunua kutoka kwa aliyemuuzia.

Tuchukue mfano rahisi;

Tuseme kwamba Max anauza baisikeli, alafu @TheBold akaenda kuinunua baisikeli hiyo.

Lakini @TheBold anainunua hiyo baisikeli ili na yeye aweze kuiuza huko mbeleni.

Sasa tuseme labda Max emuuzia @TheBold baisikeli hiyo kwa thamani ya 150K. Sasa ili kulinda biashara hii ya @TheBold ili naye asiingie hasara, wanasaini mkataba kwamba, labda ndani ya miezi mitatu kama ikitokea thamani ya baisikeli madukani ikishika chini ya 100K (kwafano) basi Max atapaswa kuinunua baisikeli ile ile kutoka kwa @TheBold kwa thamani watakayokubaliana wakati wa kusaini mkataba, labda tuseme 80K (hii ndio inaitwa ‘Strike Price’)

Ikitokea thamani ya baisikeli haijashuka kwa kiwango kile walichokubaliana, basi baisikeli itaendelea kubaki kwa @TheBold na muda ule waliokubaliana ukipita @TheBold hawezi tena kumwambia Max ainunue baisikeli ikitokea imeshuka thamani.

Hii ndio inaitwa ‘Put Options’! Hapa nimeielezea kwa lugha nyepesi ili walau kupaga Picha, lakini ni suala pana sana.

Lakini pia papo hapo kuna kitu kinaitwa ‘Call Options’.

Call option yenyewe ni kwamba, muuzaji na mnunuzi wa hisa wanakibaliana kwamba ndani ya muda fulani, ikitokea hisa zake zimefikia thamani Fulani (strike price) basi atazinunua kwa kiasi kadhaa.

Tukirejea kwenye mfano;

Tuaeme Max ana baisikeli.. Kwahiyo anaingia mkataba na @TheBold kwamba ikitokea ndani ya miezi mitatu, thamani za baisikeli zikipanda kufikia 150K basi anapaswa kuniuzia kwa shilingi kadhaa (mfano 130K) alafu namlipa hela kidogo (premium) kwa yeye kukubali kutake risk ya kuhold hiyo baisikeli (hisa) kwa muda huo.

Hii inaitwa ‘Call Option’.

Sasa kwenye masoko ya hisa yalioendelea huwa wanafanya mlinganisho wa put options na call options ili kuweza kufanya ‘speculation’ ya mwenendo na thamani ya hisa za kampuni kwa siku zijazo.

Mlinganyo huu unaitwa, ‘Put to Call Ration’.

Mfano ukifanya uwiano wa put to call ration na ukapata jawabu mfano 0.84, maana yake ni kwamba kwa kila hisa 100 zilizouzwa, hisa 84 zilikuwa ni put options na hisa 16 zilikuwa ni call options. (Hapa ‘speculation’ inakuwa ni kwamba hisa hizi zitadorora sana muda mfupi ujao).

Turudi kwenye mjadala,

Wiki moja kabla ya tukio la September 11 kulikuwa na mwenendo wa ajabu katika soko la hisa ambazo haujawahi kuonekana kabla.

Uchunguzi uliofanywa na Chicago Boars Options Exchange kwa amri ya kamati ya serikali ya 9/11 Commission, iligundua yafuatayo;

Siku ya September 6 na September 7 kulikuwa na ‘Put Options’ 4,7444 za hisa za kampuni ya ndege ya United Airline huku kukiwa na ‘call options’ 396 pekee.

Siku ya September 10 (siku moja kabla ya tukio) kulikuwa na ‘put options’ 4,516 za kampuni ya ndege ya American Airlines huku kukiwa na ‘call options’ 748 pekee.

Kumbuka kwamba kampuni hizi mbili ndizo ndege zake zilihusika katika ulipuaji majengo.

Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba ‘trend’ hii haikuonekana kwenye hisa za kampuni nyingine za ndege.

Hii ilimaanisha kwamba, ‘Traders’ katika masoko ya hisa walikuwa wamepenyezewa taarifa kwamba ndani ya siku chache kuna tukio litatokea na kufanya hisa za kampuni za American Airlines na United Airlines zishuke.

Kwahiyo traders wakatumia hiyo fursa kucheza na mahesabu ya ‘put to call ratio’ kujitengenezea faida ya mabilioni ya dola.

Si hivyo tu;

Hili pia lilitokea kwenye kampuni ya bima ya Citygroup Inc. kupitia ‘package’ yao ya Traveller Insurance.

Hawa walikuwa na mikataba ya kulipa fidia ya zaidi ya shilingi Trilioni moja (fedha za kitanzania) kwa makampuni wateja wao yaliyopo kwenye Jengo la WTC ikiwa litatokea shambulizi kwenye jengo hilo.

Pia hawa katika soko la hisa walikuwa wanalipa ‘put options’ ikitokea thamani ya hisa zimeshuka chini ya dola 40 kwa dola moja.

Siku tatu kabla ya shambulio kulitokuwa na ‘put option’ za kiwango cha juu ambazo hazijawahi kushuhidiwa kwenye hisa ya kampuni hiyo. Put options zilikuwa ni mara 45 kuzidi siku zao za kawaida.

Haikuishia hapo tu,

Kampuni ya Morgan Stanley, hii ni moja kati ya kampuni kubwa zaidi duniani katika masuala ya huduma za kifedha hasa ‘Investment Banking’. Wanafanya kazi kwenye nchi zaidi ya 24 na wana-manage mali (AUM – Asset Under Management) zenye thamani ya Dola Trilioni 1.454.

Makao makuu kwa kipindi hicho yalikuwa ni ghorofa ya 22 katika Jengo la WTC.

Hawa nao wiki moja kabla ya shambulio kulikuwa na kiwango kikubwa cha ‘put options’ kwenye hisa zao katika soko.

Pamoja na hao pia kulikuwa na kampuni ya REYTHEON.

Hii kampuni ni mkandarasi wa serikali katika miradi ya ulinzi (defense contractor).

Hawa kwenye hisa zao za ‘call options’ walikuwa wameziwekea ‘strike price’ ya dola 25 kwa hisa.

Siku ya September 10, kulikuwa na ‘call options’ 232.

Hiki kilikuwa ni kiwango kikubwa kuliko kawaida kwa mwenendo wa kampuni yao kwenye soko la hisa. Ilikuwa ni mara sita zaidi.

Ikimaanisha kwamba ‘traders’ walijua thamani za hisa za kampuni hii zitapanda baada ya muda mfupi (kumbuka ni defense contractor, kwahiyo baada ya uvamizi wa Afghanistan na Iraq thamani yake ikapanda juu sana).

Hivyo basi,

Mienendo ya kampuni zote hizi kwenye soko la hisa inadhihirisha kwamba traders wakubwa kwenye soko la hisa walikuwa wamepenyezewa taarifa kuwa kuna tukio kubwa litatokea na kuathiria kwa kiwango kikubwa soko la hisa.

Sasa tuhame kwenye soko la hisa na tuangalie upande mwingine!

KUDONDOKA KWA MAJENGO YA WTC

Moja ya mambo ambayo bado yana utata mkubwa ni namna ambavuo majengo ya WTC yalidondoka.

Ingekuwa inaingia akilini kama yangebomoka ghorofa kadhaa za juu.

Lakini haiingii akilini kwa maghorofa yale imara kudondoka moja kwa moja (total Collapse) na kuacha kifusi kana kwamba ni nyumba ha mchanga.

Kuna mashaka kwamba yawezekana baada ya ndege kujibamiza na maghorofa kuungua kwa dakika zile 102 kuna vitu vilipandikizwa muda huo au kabla ya siku ile ili kuyalipua majengo (controlled demolition).

Kuna tafiti ya kina imefanywa na Bw. Steven E. Jones, mwanafizikia kutoka chuo kikuu cha Brigham Young University kwa kushirikiana na Muhandisi Richard Gage, pamoja na software engineer Jim Hoffman na mwanatheolojia David Ray Griffin.

Katika utafiti wao wa mabaki ya sehemu lilipoanguka majengo ya WTC, waligundua kwamba kulikuwa na kiwango kikubwa cha Thermite na Nano-thermite.

Thermite nakosa kiswahili chake kizuri lakini ni mchanganyiko wa ki-pyrotechic ambao ndani yake una metal pawder, fuel na metal oxide.

Nano-thermite yenyewe kwa lugha nyepesi tunaweza kuiuta ni “super thermite”.

Hizi zote mbili zinauwezo wa kulipuka na zinatumika kutengeneza milipuko.

Pia chini ya kifusi cha mabaki ya majengo ya WTC kulikuwa na kiwango kikubwa cha Chuma kilichoyeyeka uji uji kabisa (molten steel). Inatia shaka na ni ngumu kuamini ati moto uliosababishwa na kuungua kwa mafuta ya ndege baada ya kujibamiza kwenye Jengo usababishe vyuma kuungua rojo rojo kabisa.

Kuna dalili kwamba, baada ya ndege kujibamiza majengo yale yalidondoshwa kwa makusudi kabisa (controlled demolition).

Hitimisho..

Pasipo kusahau kuwa tukio hili ndilo lilitumika kuhalalisha uvamizi wa chi za Iraq na Afghanistan, na ndio ilikuwa chachu ya kuanzshwa kwa vita dhidi ya ugaidi duniani kote (Global War on Terror).

Binafsi nisingelipenda kutoa hoja zozote za kuhitimisha huu mjadala, kwa sababu bado kuna vitendawili vingi vinapaswa kuchunguza na kutoka majibu ili tuweze kuujua ukweli kwa asilimia zote.

Kwa hiyo mjadala kuhusu 9/11 ni jambo endelevu na hakuna mtu yeyote mpaka sasa mwenye majibu kamili kuhusu kila kitendawili au shaka inayozunguka shambulio la 9/11.

Hata tume iliyoundwa na Rais Bush mwaka 2004 kuchunguza ukweli wa suala hili (The 9/11 Commission) ilikuja naaswali Mengi zaidi na sintofahamu badala ya majawabu.

Lakini muda ndio hutoa majawabu ya maswali yote..

Niliwahi kuandika makala huko nyuma kuhusu namna ambavyo Marekani kupitia CIA katika miaka ya 1950s waliondoa serikali halali ya kidemokrasia nchini Guatemala na kupandikiza madikteta wa kijeshi. Tuhuma ambazo serikali ya Marekani ilizikanusha kwa miaka mingi, lakini kwa kuzingatia Sharia ya watu kupata habari (Freedom of Information Act) imewezesha siku za hivi karibuni baada ya zaidi ya miaka 50 ukweli umewekwa hadharani na Marekani imeomba radhi..

Si hivyo tu, nimewahi pia kuandika namna ambavyo Serikali ya Marekani kupitia CIA katika miaka ya 1940s mpaka 1950s walimuondoa madarakani Waziri Mkuu wa Iran aliyechaguliwa kidemokrasia na kurudisha utawala wa Kifalme kabla haujaondolewa na WaIran wenyewe miaka ya sabini.

Kwa miongo kadhaa Marekani ilikuwa ikikanusha uhusika wake, lakini miaka ya hivi karibuni imewabidi waombe radhi baada ya ukweli kuwa hadharani.

Iko mifano mingine mingi sana….

Iko siku ukweli utakuwa dhahiri kabisa, kweupe bila kupapasa papasa.. Na wahusika kama bado watakuwa hai wataficha nyuso zao na kuomba radhi na kuwajibishwa…

Muda ndio jawabu kubwa zaidi.! Time will tell..

MWISHO

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment