Dizasta Vina – Tatuu ya Asili Lyrics
LYRICS

Dizasta Vina – Tatuu ya Asili Lyrics

AUDIO Dizasta Vina - The Verteller Album MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina – Tatuu ya Asili Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled Tatuu ya Asili, a number three song from his album titled The Verteller Album.

SIMILAR: Dizasta Vina – Kibabu na Binti

Tatuu ya Asili Lyrics by Dizasta Vina

Ah..alizongwa na zimwi,Aliskika jirani
Akitoa hoja kwa Kijiji, sababu ya kukosa elimu ya maambukizi walihisi kurogwa ndo tafsiri ya gonjwa la UKIMWI

Huo ni ugonjwa jamani Kama gonjwa mwngine,alisema mwalimu
Mwenyekiti alifoka akimwambia kaa kimya sio unaropoka kama mwendawazimu.

Elimu ya mwalimu ilikua ni nuru potevu,nuru ambayo haifiki gizani
Ikawekwa idhini mizani kuwa mizimu imechukia mgonjwa afukuzwe Kijiji Cha mbali (sauti za mwituni)

Akasindikizwa njia panda,mwisho wa makazi mwanzo wa msitu mkubwa wa Sanza
Akatengwa Kama walivyotengwa wengi,kwa mila na desturi zilizowekwa tangu enzi
Kibuyu Cha maji,furushi la matunda na makobasi yalioalika funza
Hakuna hodi inapofika kiama,Mama na nyika nyika na Mama

Na alikua peke yake,na ule mzigo mdogo mgongoni wasiwasi usoni,mtoto tumboni
Alitamani matawi yaanguke yamtunze dhidi ya baridi ya mji ulosahaulika na wabunge.

Umauti aliuhisi,alijitazama na hakuona tofauti na maiti
Alilia peke yake porini,huku sauti yake ilisindikizwa na sauti za fisi
Wadudu wenye sumu nyingi walimvizia,alikutana na visiki alipohisi njia
Mvua kubwa ilinyesha,kuonyesha hata Hali ya hewa ilimsaliti pia.

Alivuka salama mpaka ngambo,akajikongoja mpaka kando
Kando kwenye mti mkubwa,uchungu ulimshika akazaliwa mtoto mdogo huku Mama anakufa.

Ujinga uliotamalaki kwa Kijiji,ndio ujinga uliomnyima Haki ya kuishi
Alipambana mpaka ilifika tamati pumzi,akamwacha mwanae na zawadi ya virusi

Natoa nukuu kariri,mtotoalifunikwa na nguo kuukuu kwenye mwili
“Alikua na madoa makuu mawili,katikati ya mgongo,mfano wa Tatoo ya Asili”…

Dizasta Vina – Tatuu ya Asili Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment