Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Nne
KIJASUSI

Ep 04: Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar)

SIMULIZI Plata O Plomo - Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar)
Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Nne

IMEANDIKWA NA THE BOLD

************************************************************************

Simulizi : Plata O Plomo  Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja [ Pablo Escobar] 

Sehemu ya Nne (4)

Licha ya serikali kufahamu kuwa Pablo alikuwa anaendelea na biashara zake licha ya kuwa ndani ya gereza serikali ilifumfumbia macho kadiri ambavyo ulimwengu ulivyo amini kuwa Pablo Escobar yuko gerezani anajutia.

Lakini uvumilivu huu uliisha mara baada ya kuzuka skendali katika vyombo vya habari kwamba Pablo aliwaita marafiki zake wa kibiashara wanne walioko uraiani waende akawape maelekezo, walipofika huko aliamuru walinzi wanaomlinda wawapigwe risasi marafiki zake hao kwa madai kuwa wamemdhulumu hela na ilisemekana miili yao ilifukiwa ndani ya gereza.

Skandali hii ilikuwa kubwa kiasi kwamba ilitishia kurudisha tena upya zama za serikali kuumiza kichwa kuhusu Pablo. Ili kuepusha mambo yasiharibike kabisa serikali ikaamua kuwa Pablo inabidi afungwe kwenye gereza maalumu la kijeshi na aishi maisha ya kifungwa kama mfungwa mwingine yeyote.

Kutikana ma makubaliano kuwa polisi wengine isipokuwa wanajeshi wanaomlinda hawaruhusiwi kusogea hata maili 12 karibu na La Catedral, hivyo serikali ikatuma waziri muandamizi na maafisa wengine watatu wa ngazi za juu serikalini kumpelekea taarifa hiyo Pablo kuwa anaamishwa gereza.

Baada ya kupewa taarifa hii Pablo akiwageuzia kibao na kuamuru wanajeshi wanaomlinda waweke chini ya ulinzi vuongozi hao wa serikali. (Kumbuka wanajeshi hawa wanaomlinda aliwachagua yeye hivyo ni dhahiri walikuwa maswahiba wake wakikuwa tayari kumtii Pablo kuliko rais wa nchi)

Baada ya taarifa kufika serikalini kuwa Pablo amewaweka chini ya ulinzi viongozi wa serikali waliotumwa kufanya nae mazungumzo juu kuhamishwa gereza. Serikali ikatuma kikosi cha wanajeshi 600 kulizunguka gereza hilo na kumtaka Pablo ajisalimishe.

Pablo akawajibu kuwa wakithubutu hata kukanyaga hatua moja ndani ya uzio wa La Catedral basi ataamuru viongozi hao aliowashikilia mateka wapigwe risasi.

Mabishano haya yalidumu kwa takribani masaa kumi mpaka ambapo giza lilipoingia kikosi cha wanajeshi waliokuwa wamelizunguka gereza walivamia ndani ya La Catedral lakini jambo la ajabu waliwakuta viongozi hao wa serikali wamefugwa kwenye viti na kuzibwa midomo lakini walikuwa salama salimini ila Pablo na wapambe wake hawakuwepo. Na watu waliokutwa ndani ya La Catedral walidai Pablo na wapambe wake hajaonekana/ameondoka kwa taribani masaa manne yaliyopiata.

Ni kwa jinsi gani Pablo aliwatoroka wanajeshi amabo walikuwa wamelizunguka gereza kila kona kitendawili hiki mpaka leo hakuna aliyekitegea. Hakukuwa na njia yoyote ya chini kwa chini wala handaki, hivyo huu utata wa jinsi alivyowatoroka haujapata jibu la kuridhisha mpaka leo.

Kufumba na kufumbua jinamizi la aibu kwa serikali ya Colombia na Marekani kilikuwa limerudi. Na serikali zote mbili ziliapa kwamba sasa imetosha ni lazima walizike jinamizi hili.

Kamandi ya Oparesheni maalumu za kijeshi za marekani (Joint Special Operations Command) kikaunda kikosi kazi maalumu cha kijeshi kilichoelekea nchini Colombia kuungana na kikosi maalumu cha jeshi la Colombia kikichoundwa maakumu kwa ajili ya kumsaka Pablo kilichoitwa ‘Search Block’ na kwa pamoja wakaanza msako mkali wa kumtafuta Pablo. Pia walishirikiana na kikundi cha Los Pepes kilichoapa kumteketeza Pablo na ukoo wake wote ambao walitumia mwanya wa msako huu kuua watu 300 waliokuwa na uhusiano na Pablo, yaani ndugu zake, marafiki na wafanyabiashara wenza.

Baada ya mwaka mzima wa msako mkali hatimae siku ya desemba 2, 1993 jeshi la Colombia lilifanikiwa kunasa mawasiliano ya simu kati ya Pablo na wasaidizi wake. Wakatumia ‘triangulation technology’ kung’amua mahali alipo ambapo alikuwa katika mtaa wa Los Olivos katika mji wa Madellín. Baada ya kufanikiwa kufahamu nyumba aliyojihifadhi pasipo kupoteza mda wakafanya shambulio la kushitukiza.

Wakati wanawafanyia shambulio hili la kushitukiza Pablo alikuwa yupo na mlinzi wake binafsi mmoja tu Alvaro de Jesús.

Baada ya kuanza kushambuliwa nao wakarudisha mashambulio ya risasi kwa vikosi vya jeshi la serikali. Majibizano haya ya risadi yalidumu kwa dakika kadhaa ndipo Pablo na mlinzi wake wakakubali kuwa hakuna namna wao watu wawili wataweza kuwashinda kikosi kizima cha kijeshi chenye silaha nzito. Hivyo wakaamua warushe risasi huku wakiwa wanakinbilia juu ya paa la nyumba. Lakini kabla hawajafika juu kabisa ya paa la nyumba mlinzi wa Pablo alidunguliwa na risasi na kufariki papo hapo na Pablo mwenyewe alipigwa risasi mguuni na akajikongoja mpaka juu ya paa.

Baada ya wanajeshi wa serikali kuvamia nyumba na kufika juu ya paa walimkuta Pablo amelala chini amefariki akiwa na tundu la risasi aliyopigwa kwenye sikio kwenda ndani ya kichwa.

Haijulikani ni nani alimpiga hii risasi lakini marafiki zake wa karibu pamoja na kaka yake wa kuzaliwa wanasema kwamba siku zote Pablo akikuwa anasema kuwa hatokubali kupigwa risasi ya mwisho na adui yake. Kama ikitokea ameshambukiwa na adui na hana namna ya kujiokoa basi atajipiga risasi sikioni itokee upande wa pili. Serikali haijawahi kupinga au kuthibitisha suala hili la Pablo kujipiga risasi mwenyewe lakini huo ndio ulikuwa mwisho wa Pablo juu ya uso wa dunia.

Mpaka leo hii nchini Colombia hasa katika mji wa Madellín kila mwaka wanafanya kumbu kumbu ya kifo cha Pablo kama shujaa wao lakini kwa watu wengi duniani Pablo amebakia kama muhalifu aliyeitesa na kuisumbua dunia kadiri atakavyo.

Binafsi nadhani namna nzuri ya kumkumbuka Pablo ni sentesi moja maridhawa iliyotolewa na Virginia Vallejo aliposema; Amando a Pablo, Odiando a Escobar.! Akimaanisha kuwa lazima kuna upande fulani wa nafsi yako utampenda Pablo kama mtu mwenyenye jitihada, umahiri na uthubutu lakini upande wa pili wa nafsi lazima utamchukia Escobar kutokana na uhalifu wake.

Lakini kwa namna yeyote ile historia ya Dunia itaendelea kumkumbuka Pablo kama binadamu aliyeufinyanga ulimwengu wa siri na hatari wa biashara haramu na kuufanya uwe jinsi ulivyo leo hii. Vizazi vyote vijavyo vitaendelea kusimulia historia ya kusisimua ya Pablo El Mágico. Pablo El Zar de la Cocaína. Pablo Emilio Escobar.

Jiunge na Group langu la WhatsApp kusoma simulizi mpya kila siku. Kuna malipo ya 5,000/- kwa mwezi. Wasiliana nami 0759 181 457


MENGINEYO….

MALI NA FAMILIA BAADA YA KIFO CHA PABLO ESCOBAR

Pablo ana ndugu na familia ambao bado wako hai mpaka sasa lakini labda nielezee kidogo kuhusu wale ndugu zake wa karibu zaidi (familia yake – mke na watoto)

Baada ya kifo cha Pablo familia yake kwa msaada wa serikali ya Colombia ilibidi wahame nchi kwa kuhofia usalama wao. Nchi nyingi zilikataa kuwapa ukimbizi (asylum) na ikawabidi watumie passport ya utalii kukimbilia nchini Msumbiji.

Baadae serikali ya Colombia ilibidi wafanye makubaliano maalumu na serikali ya Argentina ili kuwapatia ukimbizi familia ya Pablo. Makubaliano haya yalifanikiwa na familia ya Pablo ikahamia Argentina wakitumia majina ya bandia.

i)Mkewe – Maria Henao Vellejo

Mke wa Pablo bado yungali hai mpaka sasa. Maria alianza uhusiano na Pablo kipindi ana miaka 13 na Pablo akiwa na miaka 24 na miaka michache baadae wakafunga ndoa.

Baada ya kifo cha Pablo na kufanikiwa kupata ukimbizi nchini Argentina Maria alibadilisha jina na kujiita Isabel Santos Caballero

ii)Mtoto wake wa Kiume – Juan Pablo Escobar Hena

Pengine huyu ndiye mwanafamilia maarufu zaidi katika ndugu wa Pablo walio hai. Alizaliwa mwaka 1977, na Juan anafahamika kuwa alikuwa karibu mno na baba yake kiasi cha kuwa kama marafiki na wanafanana mno kwa sura. Pia alikuwa ndio moja ya watu walioaminiwa kwa asilimia 100 na Pablo. Ingawa toka kipindi Pablo mwenyewe yuko hai Juan alikuwa hakubalini na biashara za baba yake.

Baada ya kupata ukimbizi nchini Argentina Juan alibadilisha jina na kwasasa anaitwa Juan Sebastian Marroquín.

Mwaka 2009 alichapisha kitabibu kilichoitwa ‘Pecados de mi Padre’ (Sins of my Father) kwa lengo la kuwaomba msamaha wahanga wote waliokutwa na madhira kwasababu ya baba yake.

Hivi karibuni amechapa kitabu kinaitwa ‘Pablo Escobar – My Father’ ambacho kinaelezea maisha ya baba yake na genge lake la Medellín Cartel. Pia Juan ni muhandisi na msanifu wa majengo na pia anamiliki kampuni ya mavazi yenye kutumia jina na picha za Pablo Escobar.

iii) Mtoto wake wa kike – Manuella Escobar Henao

Huyu binti alizaliwa mwaka 1984. Huyu ndiye alikuwa roho ya Pablo. Alikuwa anampenda kupitiliza kiasi kwamba alimdekeza katika viwango visivyo mithirika. Huyu ndiye mtoto wake ambaye ilimbidi Pablo achome moto dola milioni mbili ili kumkinga na joto.

Kuna kisa kinaeleza kuwa Manuella alipo kuwa mtoto alimwambia baba yake kuwa anataka Unicorn (kiumbe cha kufikirika kama farasi mwenye mbawa na uwezo wa kupaa). Inasemekana kwamba Pablo alinunua farasi akafanyiwa upasuaji kuwekwa pembe mbele ya kichwa chake, pia akawekewa mabawa ubavuni pande zote mbili ili afanane na Unicorn. Farasi huyu alikufa baada ya siku chache tu.

Pia ni Manuella aliyesababisha Pablo atoe sharti la kuwekewa Telescope gerezani ili awe anamwangalia kila siku jioni akiwa anaongea nae kutoka nyumbani.

Kwa kifupi Manuella alikwa roho ya Pablo.

Baada ya kupata ukimbizi nchini Argentina Manuella alibadilisha jina na kujiita Juana Manuella Marroquín Santos.

Pia Manuella ndiye ndugu pekee wa karibu wa Pablo ambaye anaishi kwa usiri mkubwa mpaka sasa. Hajawahi kufanya mahojiano na vyombo vya habari na hataki, hajawahi kuchapisha andiko lolote na hataki watu wamfahamu.

iv) Roberto Escobar – Kaka wa Pablo Escobar

Huyu alikuwa ni kaka wa damu wa Pablo Escobar na alikuwa ndiye muhasibu Mkuu wa Medellín Cartel. Baadavya kifo cha Pablo, Roberto alikamatwa na alifungwa miaka 10 gerezani kutokana na uhusika wake katika genge la Medellí Cartel. Baada ya kutoka alichapisha kitabu kilichoitwa ‘The Accountant’s Story’ kinachoeleza maisha ya Pablo na Medellín Cartel.

Kuhusu Mali zilizoachwa na Pablo..

Kwanza kabisa tufahamu kuwa wahalifu wote wakubwa hasa wa biashara ya mihadarati mali zao zinakuwa katika aina tatu. Nitaeleza aina hizo na zilienda wapi baada ya kifo cha Pablo..

Aina ya kwanza: vitu vinavyotunza thamani mfano majumba, mashamba, mahoteli na magari adimu ya kifahari (limited editions). Pablo alikuwa navyo vyote hivi na baada ya kifo chake baraza la wawakilishi lilipisha muswada maalumu ambao baadae ulikuja kusaidia kupatikana Sheria ya kuzuia watu kujitajirisha kiharamu (Unjust Enrichment laws). Hii iliwapa mamlaka serikali kuchukua mali zote zisizohamishika zilizomilikiwa na Pablo.

Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Tano

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment