Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA THE BOLD
************************************************************************
Simulizi : Plata O Plomo Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja [ Pablo Escobar]
Sehemu ya Tatu (3)
Ushindani mkubwa wa kibiashara kati ya magenge haya mawili unaweza kuwa sababu kubwa ya wao kuingia vitani lakini hii iliepushwa kutokana na vikao vya makubaliano walivyokaa awalinkuhusu kugawana soko.
Sababu kubwa zaidi na ya msingi iliyochochea vita hii ilikuwa ni Pablo kuamua kuacha kuheshimu makubaliano akiyoingia na Cali Cartel kutokana na genge hili kujihusisha na vitendo ambavyo Pablo alivipinga kwa nguvu zote.
Haijulikani ni kichaa gani kiliwapata viongozi wa ngazi za juu wa Cali Cartel lakini ilipofika miaka ya kati kati ya 1980 Cali Carteli wakaanza kujihusisha na imani zenye utata za “Kusafisha Kizazi/jamii” (Social Cleansing). Cali Cartel walisimamia mauaji ya mamia ya watu kwenye mji wa Cali pasipo sababu ya msingi wakidai kuwa watu hao wanaichafua Cali.
Mauaji yao yaliwalenga walemavu, machangudoa, watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja, watoto wa mitaani, na watu wasio kuwa na makazi.
Baada ya kuwaua waliwaandika maandishi kifuania “Cali limpia, Cali linda” (Clean Cali, beautiful Cali (Cali nadhifu, Cali inayopendeza)
Vitendo hivi vilimkera Pablo na ikampa sababu ya kutokuheshimu makubaliano yake na Cali Cartel kuhusu kugawana soko na akaamuru watu wake wafanye biashara nchini marekani katika mji wowote ule wanaojisikia.
Kitu hiki kikiwakera viongozi wa Cali Cartel na ili kumuonyesha kuwa wamechukizwa wakaanza kutoa ufadhili kwa kikundi cha wapiganaji kilichokuwa kinajiita Los Pepes amacho ni kifupi cha Los Perseguidos por Pablo Escobar (People Persecuted by Pablo Escobar (watu walioumizwa na Pablo Escobar)).
Kikundi hiki kilikuwa kinaundwa na ndugu za watu waliouawa na Pablo au Wapambe wake na walikuwa wamejiapiza kumsaka na kumuua Pablo popote alipo. Kitendo cha mabosi wa Cali Cartel kuanza kukipa ufadhili kikundi hiki kilichochea moto wa vita ya magenge amabao haukuwahi kuonekana hapo kabla.
Katika kipindi hiki Colombia ilishuhudia mauaji ya kutisha ambapo wafuasi wa magenge yote mawili walikuwa wakitafutana usiku na mchana. Mauaji haya yaliwahusu mpaka marafiki, ndugu na wanafamilia wa makundi yote mawili. Katika mwaka 1988 pekee idadi ya vifo ilifikia zaidi ya watu 21,000 na mwaka 1989 idadi iliongezeka mpaka vifo zaidi ya 28,000.
Hiki kilikuwa ni moja ya vipindi vigumu zaidi kiusalama kwa Pablo kwani alikuwa na lundo la maadui waliokuwa wakimtafuta. Kulikuwa na serikali ya marekani inamtafuta, serikali ya Colombia inamtafuta, Kikundi cha Los Pepes kinamtafuta, na genge la Cali Cartel linamtafuta. Kutokana na suala la usalama kuwa tete mno ilimlazimu aame kutoka katika ‘pepo’ yake ya Hacienda Napolés na kwenda kujificha katika nyumba za maficho juu ya milima ya mji wa Madellín.
Ilikuwa inambidi abadili makazi mpaka mara nne kwa siku moja. Nyumba zake nyingi hizi za juu ya milima alikuwa anazitumia kuhifadhi pesa na silaha na ilitokea siku walienda kwenye nyumba yake iliyopo karibia kabisa na kilele cha mlima na ilikuwa iko ndani ya msitu mnene.
Siku hii kulikuwa na baridi lisilomithirika na kutokana na nyumba hii kujengwa maalumu kwa ajili ya kuhifadhi fedha na silaha haikuwa na mfumo wa joto wala umeme. Ilifikia kipindi cha usiku baridi lilizidi na kupitiliza kiwangi cha kawaida mpaka ikaanza kutishia afya ya mtoto wake wa kike aliyekuwa naye pamoja na familia yake.
Kutokana na kutokuwepo na namna nyingine yeyote ya kupasha moto nyumba hiyo ili kupunguza baridi, ili mbidi Pablo achome moto maburungutu ya fedha usiku kucha ili kuipatia joto familia yake na hasa mtoto wake wa kike ambaye alionekana kuathiriwa zaidi na baridi. Mpaka asubuhi kunakucha na baridi kupungua kufikia kiwango cha kawaida Pablo alikuwa ameteketeza maburungutu ya hela ya kiasi cha dola milioni mbili za kimarekani.
Baada ya Juhudi za Cali Cartel kumpata Pablo kutozaa matunda, walitoa kandarasi kwa Jorge Selcado ambaye alikuwa ni muhandisi na Mwanajeshi. Jorge alikuwa maarufu kwa kuandaa timu maalumu za mauaji ya kuratibiwa kiumakini (assassination teams) na mara zote mipango yake inakuwa ya mafanikio.
Baada ya Jorge kupewa ‘ofa’ hii na mabosi wa Cali Cartel aliwasiliana na watu wake ambao walikuwa ni wanajeshi wa kukodi (mercenaries) kutoka nchini uingereza ambao walikuwa wamewahi kutumikia katika jeshi la Uingereza kitengo maalumu cha Anga (SAS – Special Air Services).
Timu hii ilikuwa na watu kumi mbili na iliwasili Colombia na kufanya mazoezi kwa miezi kadhaa ili kujiandaa na zoezi lililopo mbele yao. Walifahamu kuwa kwa kipindi hicho Pablo alikuwa amejificha mahali kusiko julikana kwenye milima, hivyo walisubiri wapate taarifa kuwa amerejea kwenye ‘pepo’ yake ya Hacienda ili wafanye shambulio la kushitukiza.
Siku hiyo haikuchelewa sana kwani timu ya Mpira ambayo Pablo alikuwa anaishabikia na kuifadhili ilifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Colombia. Hivyo Pablo alirejea jijini Medellín ili ajumuike kusherehekea ushindi huo.
Kikosi hiki kilichotumwa kumuua Pablo walijiandaa na Chopa mbili za kivita zilizobeba silaha nzito na mpango wao ulikuwa wamshitukize Pablo nyakati za asubuhi na kufanya shambulizi nyumbani kwake Hacienda Napolés.
Ili mpango huu uwe na ufanisi walikubaliana kuwa washambulie kutokea nyuma ya milima na chopa ziruke katika mfumo maalumu wa kijeshi wa usawa wa chini chini kabisa (nap-to-earth) ili wasiweze kuonekana kutokea mbali.
Keshi yake chopa ziliruka kuelekea Hacienda Napolés kama walivyopanga wapitie nyuma ya milima huku zikiruka chini chini, lakini wakiwa kwenye milima hiyo kwa bahati mbaya chopa moja ilimshinda rubani kutokana na kuruka chini chini na ikagonga kwenye mlima na kudondoka.
Zoezi ambalo kilipangwa kuwa la kwenda kushambulia na kumuua Pablo likageka kuwa ni zoezi la uokoaji na mpango huu ukaishia hapo hapo.
Baada ya kufeli kwa zoezi hili serikali ya Colombia iliwasiliana na Pablo kujaribu kumuomba ajisalimishe.
Waliharibu kumbembeleza kwa kila namna ambayo waliweza na kumuahidi watakubaliana na masharti yoyote atakayoyasema. Serikali ilifikia kipindi walikuwa ‘desperate’ kutokana na aibu waliyokuwa wanaipata kimataifa kwa kushindwa kumdhibiti muhalifu mmoja aliyeifanya nchi yao ya Colombia mpaka kubatizwa jina la ‘Capital of death’ (mji wa kifo). Hivyo matamanio yao ilikuwa tu kuutangazia ulimwengu kuwa wamemkamata Pablo.
Baada ya Pablo kutafakari kwa kina na kuona jinsi usalama wake na familia yake kuwa ni mdogo kutokana na maadui wanaomzunguka kila kona akakubali ombi la serikali kujisalimisha lakini akawapa masharti matatu.
Moja, kipindi hicho serikali ilikuwa imefanya mchakato na kubadili kifungu cha katiba kuruhusu kukabithi raia wake kwa nchi za kigeni (extradition). Pablo akawaeleza waitishe kikao maalumu cha Bunge na kurudisha kifungu cha zamani kinachokataza raia wa nchi hiyo kukabidhiwa kwa nchi za kigeni. Serikali ikakubaliana na sharti hili. Kikaitishwa kikao maalumu cha bunge na kifungu hicho cha katiba kikarejebishwa.
Pili, Pablo aliwapa sharti kuwa anataka atengenezewe gereza maalumu katika sehemu atakayoichagua yeye na yeye na wahandisi wake ndio watakaochora michoro ya namna gereza hilo anavyotaka liwe. Serikali wakakubaliana na sharti hili na gereza kikajengwa kama ambavyo Pablo aliamuru.
(Tafadhali rejea aya ya kwanza ya makala hii kuhusu namna ambavyo gereza hili likikuwa tofauti na gereza lingine lolote duniani).
Gereza hili lilipo malizika Pablo mwenyewe alilipa jina La Catedral (The Cathedral) lakini watu wengi walilipa jina la utani ‘Club Escobar’ na wengine waliliita ‘Hotel Cathedral’.
Sharti la tatu aliwaambia serikali yeye ndiye atakaye chagua askari wa kumlinda. Serikali ikakubali pia sharti hili.
Baada ya masharti yote kukamilika yakafanyika makubakiano maalumu ya kisheria ambapo Pablo Escobar licha ya uhalifu wa kutisha alioufanya kwa miaka karibia ishirini alipewa adhabu ya kifungo cha miaka miatano pekee.
Baada ya makubaliano. Pablo alijisalimisha na kupelekwa kwenye makazi yake mapya, gereza la La Catedral.
Baada ya Pablo kujisalimisha mwaka 1991 serikali ilitangazia ulimwengu kwa mbwembwe zote kuwa wamemkamata Pablo Escobar na amehifadhiwa katiba gereza la siri.
Ikikuwa ni kweli kuwa Pablo alikuwa gerezani lakini ulimwengu mzima walifichwa ukweli halisi kwani katika gereza hilo Pablo aliishi kama mfalme na aliendelea kutoa maagizo kwa wafuasi wake na kuendesha biashara yake ya miahadarati akiwa ndani ya La Catedral. Tena kwa sasa Pablo inawezekana alifurahi zaidi kwani alikuwa uhakika wa usalama wake kutokana na kulindwa na jeshi la serikali ambao wao walimuona kama mfungwa huku yeye akiwaona kama walinzi wake binafsi.
Kitendo hiki kiliwaumiza sana Cali Cartel ambao walihangaika usiku na mchana wafahamu hili gereza lilipo. Baada ya mwaka mkoja wakapata taarifa kuhusu mahala ambapo gereza anahifadhiwa Pablo. Kutokana na ulinzi mkali wa kijeshi waling’amua fika kuwa hawataweza kuvamia gereza hilo na kumuua Pablo hivyo mshauri wao wa masuala ya kijeshi akawashauri Jorge Selcado akawashauri kuwa namna pekee ya kumuua Pablo ndani ya La Cathedral ni kulipua gereza hilo kwa mabomu mazito kwa kutumia ndege maalumu ya kivita.
Cali Cartel wakanunua ndege ya kivita aina ya A-37 Dragonfly na wakaweza kupata dili la magendo kuuziwa mabomu mazito ya kivita ya uzito wa paundi 500 kutoka kwa generali wa jeshi ka El Salvador.
Hivyo Jorge akarusha ndege na kuelekea El Salvador katika uwanja wa ndege wa kiraia asubuhi alfajiri ili kuchukua mabomu.
Kwa bahati mbaya mabomu hayo yalikuwa kwenye maboksi makubwa manne na ndege aliyoenda nayo Jorge ilikuwa ndogo isingeweza kubeba maboksi yote hayo. Wakahangaika kunga’aniza maboksi yaenee ndani ya ndege lakini maboksi matatu pekee ndiyo yalienea. Zoezi hilo la magendo lililopaswa kuchukua dakika chache tu likatumia zaidi ya dakika ishirini ambapo palianza kupambazuka na watu kufika uwanjani hivyo ikambidi Jorge aruke na maboksi matatu na kulitelekeza boksi moja uwanjani hapo.
Baada ya raia kushikwa na butwaa kuhusu walichokiona hatimae polisi walifika na baada ya masaa machache walipewa taarifa za siri kuhusu mpango huo wa Cali Cartel kununua mabomu hayo ili kulipua La Catedral. Skandali hii iliteka vyombo vya habari siku hiyo na ikapekekea Cali Cartel kuachana na mpango huo wa kulipua La Catedral waliamini kuwa taarifa hiyo itakuwa imemfikia Escobar na ameshachukua tahadhali.
KIFO CHA PABLO El Mágico
Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;