Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi, Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu Sehemu ya Pili
KIJASUSI

Ep 02: Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi, Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu

SIMULIZI Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi, Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu
Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi, Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA THE BOLD

************************************************************************

Simulizi: Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi,  Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu 

Sehemu ya Pili (2)

Kesho akajutana na yule myahudi na kumpa jibu lake kuwa ni immposible kuvunja na kuiba main vault ya Antwerp inayohifadhi almasi zote zilizopo katika mji huo.. Akampa ile peni ambayo imerekodi mandhali ya Vault pia akampa na maelezo ya mdomo kwanini haiwezekani kuiba katika ile vault na akamsisitiza zaidi juu ya matabaka ya ulinzi (security levels) ambayo yana protect vault hiyo. Matabaka hayo yapo kama ifuatavyo..

1) Combination dial ambayo unatakiwa uingize tarakimu nne za siri

2) Sehemu ya kuingiza funguo maalum

3) Sensor ya mitetemo (seismic sensor)

4) geti la Chuma lililo sambamba na mlangi

5) sensor ya sumaku (magnetic sensor)

6) Kamera ya nje ya mlango

7) Keypad ya kuzima alarm

8) sensor ya mwanga (light sensor)

9) Kamera ya ndani ya vault

10) sensor ya joto na mjongeo (heat & motion sensor)

Jumlisha; walinzi na ulinzi unaozunguka jengo hilo.. Natarbartlo akmsisitizia yule myahudi “..it is immposible to rob the Antwerp diamond center vault”..

TUKIO LILIVYOTEKELEZWA

Miezi kama mitano ikapita ndipo Notarbartolo akapokea simu kutoka kwa yule myahudi na safari hii alimuomba wakutane nje kidogo ya mji wa Antwerp… Baada ya kuonana yule myahudi alimchukua Notarbatolo mpaka kwenye nyumba moja inayofanana na ghala kubwa.. Ndani yake Notarbatolo alikuta kitu ambacho hakutegemea kabisa… Yule myahudi alikuwa ametengeneza replica inayofanana kabisa na main vault halisi ya kuhifadhia almasi ya hapo mjini Antwerp.. Pia akamtambulisha kwa watu watatu ambao pia aliwakuta hapo! Natarbartolo amekataa kabisa mpaka leo hii kutoa majina halisi ya watu hawa lakini anawasimulia kwa nicknames walizokuwa wanatumia, kulikuwa na The genius (huyu ni mtaalamu wa mambo ya kidigitali na eletroniki), kulikuwa na The monster ( huyu alikuwa ni mekanika na mtaalamu wa umeme) na kulikuwa na mzee wa makamo ambaye walimuita The King of Keys (huyu ni mtaalamu wa kufungua vitasa na makufuli ya aina zote pamoja na kufoji funguo)..

Yule myahudi aliwaambia kazi ya ile replica ni wao wafanye mazoezi na kuitafiti na hatimae wajue namna gani wataweza kuingia ndani ya vault ya Antwerp pasipo kugundulika..

Iliwachukua miezi mitano Natarbartolo na wenzake kufanya mazoezi na kutengeneza perfect plan itakayowawezesha kuingia katika vault na kuiba pasipo kugundulika..

Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi, Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment