Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi, Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA THE BOLD
************************************************************************
Simulizi: Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi, Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu
Sehemu ya Tatu (3)
SIKU YA TUKIO..
Siku moja kabla ya tukio, yaani February 14 2003 Notarbartolo alienda mchana kwenye vault kana kwamba kuna almasi ameenda kuhifadhi lakini akajitahidi akae karibu na kifaa cha kuhisi joto na mjongeo (heat/motion sensor) na kwa kutumia hair spray aliyoificha ndani ya jaketi lake akapulizia juu ya kifaa hicho hivyo kukifanya kisiwe na uwezo wa kuhisi mabadiliko yoyote ya joto au movement ndani ya vault…
Ilipowadia siku ya tukio lenyewe.. February 15
Notarbartolo na wenzake waliendesha gari mpaka karibu kabisa na jengo lenye vault! Jengo lilikuwa na ulinzi mkali kwa mbele lakini nyuma ya jengo hakukuwa na ulinzi mkubwa kwani watu wa ulinzi walikuwa na imani kubwa sana na teknolojia yao inayosaidia kulinda jengo lao..
Wote wakashuka kwenye gari isipokuwa Notarbatolo alibaki kwenye gari! Baada ya kushuka wote wakazunguka nyuma ya jengo ambako walitumia ngazi ambayo The genius alikuwa ameificha hapo mchana wake wakapanda mpaka ghorofa ya pili.. Baada ya wote kupanda katika balcony ya ghorofa ya pili ilibidi wakae mbali na madirisha kwani yote yalifungwa vifaa vya kuhisi joto na movement na vikigundua tu kuwa kuna mabadiliko ya joto au movement basi alarm inalia..
Alichokifanya The genius alichukua kitambaa kirefu kilichotengenezwa kwa polyester kujifunika na kusogolea kifaa kile cha heat and motion sensor.. Kutokana na yeye kujifunika kwa nguo yenye material ya polyester hii ilipelekea kifaa kile kushindwa kudetect kilichokuwa kinatokea na alipokifikia karibu kifaa kile akakifunika kabisa na nguo ile kwahiyo korido ikawa iko salama kwa wao wote kupita.. Wakafungua madirisha wakaingia ndani na kuanza kushuka ngazi kuelekea chini kwenye vault..
Baada ya kufika chini nje ya mlango wa vault ambako kulikuwa na giza kutokana na kuzimwa taa.. Wakatumia fursa hiyo kuzifunga kamera kwa mifuko meusi na kisha wakawasha taa.. Baada ya kuwasha taa ilikuwa sasa ni jaribio la kufungua mlango na hapa ndio wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani wakikosea kitu kimoja tu maana yake alarm italia na mchezo utaishia hapo..
Kumbuka kuna matabaka kumi ya ulinzi wanayotakiwa wanayotakiwa kuyavuka mpaka waingie ndani.. Tabaka la kwanza ni lile la combination dial ambapo wanatakiwa waingize tarakimu nne za siri! Kabla ya siku hii ya tukio Natarbartolo alifanikiwa kumshawishi muhudumu wa vault wabadilishe mtungi wa tahadhali ya moto (fire extinguisher) jambo ambalo hawakulifahamu ni kwamba mtungi ule ulikuwa na gas ndio lakini ndani yake Natarbatolo aliweka kifaa maalumu kilichokuwa kinachukua data za kamera ya nje ya mlango wa vault! Kwa kutumia kifaa hicho Natarbartolo alinga’amua tarakimu nne za siri ambazo zilikuwa zinahizatijika kuingizwa… Kwahiyo waliingiza tarakimu nne na wakawa wamefanikiwa kwa hatua hii ya kwanza… Bado hatua tisa ili wafanikishe.!
Hatua ya pili chabgamoto ya pili ilikuwa ni namna gani wangeweza kudiable kifaa cha kuhisi usumaku (magnetic sensor) hii yenyewe ilitengenezwa katika katika hali ya kwamba plate moja ya sumaku iliwekwa kwenye mlango na nyingine ilifungwa kwenye ukuta pembezoni mwa mlango kwa maana ya kwamba mlango ukifungwa kunakuwa na magnetic field inatengenezwa pale katikati kwa maana ya kwamba kama mtu ukifungua mlango unadisturb ili magnetic field na alarm inalia…
Kwahiyo alichokifanya The genius alichukua plate ndogo ya aluminium aliyoitengeneza nyumbani alafu akaifunga na tape ya gundi kali na kunasisha katika zile plate za sumaku huku na huku yaani iliyopo ukutani na mlangoni (ametumia aluminium ili asiweze kudisturb magnetic field).. Baada ya hapo akafungua screw na zile plate na kuziweke pembeni ya mlango! Kwahiyo zile plate mbili bado zilikuwa na magnetic field katikati yake lakini zilikuwa zimewekwa pembeni ya mlango..
Kwahiyo tayari matabaka matatu yalikuwa yameshakuwa disabled bado matabaka saba.. Kumbuka kamera ya nje tayari ilishafungwa na mfuko mweusi.
Hatua ilifuata ilikuwa ni kudisable alarm inayo monitor seismic sensor na geti dogo la ndani. Kifaa hiki kilifungwa kama keypad pembeni kwenye ukuta, kilichokuwa kinatakiwa ni kuingiza tarakimu nne za siri kama pale juu kwenye mlango.. Tarakimu hizi za siri nazo walikuwa wameshazifahamu kwa kutumia kile kifaa kilichopo ndani ya fire extinguisher kwahiyo waliingiza tu tarakimu na tayari wakawa wamefanikiwa kudisable tabaka hili..
Tukio La Ujambazi Lililofanikiwa Zaidi, Kusisimua Na Kuushangaza Ulimwengu Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;
- Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Kwanza
- Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Pili
- Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Tatu
- Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Nne
- Plata O Plomo – Ulimwengu Wa Siri Kiganjani Kwa Binadamu Mmoja (Pablo Escobar) Sehemu ya Tano