Behind the Curtain: September 11 Sehemu ya Kwanza
IMEANDIKWA NA THE BOLD
************************************************************************
Simulizi: Behind The Curtain: September 11
Sehemu ya Kwanza (1)
Sasa, unaweza kupata nakala za Kitabu changu cha “NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI”.
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-
Pia waweza kupata kitabu changu cha “OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI”
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-
Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457
Siku ya Jumanne, tare 11 mwezi September mwaka 2001 majira ya saa 2 na dakika 46 asubuhi mpaka saa 4 na dakika 28 asubuhi lilifanyika shambulio kubwa na baya zaidi kuwahi kutokea na kufanywa na adui katika ardhi ya nchi ya Marekani.
Majira ya saa 2 na dakika 46, ndege aina ya Boeing 767-223ER (A.A. Flight 11) iliyosajiliwa kwa namba N334AA, mali ya shirika la American Airlines ambayo iliruka kutoka Boston katika uwanja wa ndege wa Logan International Airport ikitegemewa kutua katika uwanja wa ndege wa Los Angels International Airport ambamo ndani yake kulikuwa na abiria 81 na wafanyakazi 11 ilijibamiza na kulipua jijini New York kwenye jengo la Kaskazini (North Tower) la kituo cha kibiashara cha kimataifa (World Trade Center) jengo ambalo lilikuwa na ghorofa 110.
Dakika chache baadae, ndege nyingine aina ya Boeing 767-222 (U.A Flight 175) iliyosajiliwa kwa namba N6126UA inayomilikiwa na shirika la United Airlines ambayo pia iliruka kutoka Boston katika uwanja wa ndege wa Logan International Airport na ikitegemewa pia ikatue katika uwanja wa ndege wa Los Angeles International Airport ambamo ndani yake ilikuwa na abiria 56 na wafanyakazi 9 ilinibamiza na kujilipua pia jijini New York kwenye jengo la kusini (South Tower) la kituo hicho hicho cha biashara cha kimataifa. Jengo hili pia lilikuwa na ghorofa 110.
Kujibamiza kwa kwa ndege hizi na kulipua majengo haya kulisababisha maghorofa haya kudondoka kabisa (total collapse) na yalisababisasha kudondoka kwa majengo mengine kama vile ghorofa la 7 WTC Tower na maghorofa mengine kumi yaliyomo ndani ya kituo cha cha kimataifa (WTC Complex).
Wakati haya yakitokea jijini New York, ndege nyingine aina ya Boeing 757-223 (A.A. Flight 77) iliyosajiliwa kwa namba N644AA inayomilikiwa na shirika la American Airlines ambayo iliruka kutoka katika uwanja wa ndege wa Washington Dulles International Airport ikitegemewa ikatue kwenye uwanja wa Los Angels International Airport ambmo ndani yake ilikuwa na abiria 58 na wafanyakazi iligeuza njia na kurudi nyuma na kwenda kujibamiza na kulipua jengo la Pentagon, ambalo ndio Makao Makuu ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (US Department of Defense).
Muda huo huo pia, ndege nyingine aina ya Boeing 757-222 (U.A Flight 93) iliyosajiliwa kwa namba N591UA mali ya shirika la United Airlines ambayo iliruka kutoka Newark Intenational Airport ikiwa na abiria 37 na wafanyakazi 7 na ikitegemewa ikatue katika uwanja wa San Fransisco International Airport ilidondoka karibu na eneo la Shanksville, Pennsylvania na inasadikiwa ndege hii ilikuwa njiani kwenda kujibamiza katika Ikulu ya marekani.
Mfululizo wa mashambuluo haya ya siku hii yalikuwa ni tukio baya zaidi katika historia kwa Marekani kushambuliwa na adui katika ardhi yake mwenyewe.
Jumla ya watu 2997 walifariki na watu 6000 wengine walijerehiwa vibaya mno.
Hasara ya kudondoka kwa majengo yote haya na uharibifu wa miundombinu uliotokea thamani yake inafikia shilingi za Kitanzania Trilioni 20.
Lakini tukijumlisha na harasa za mifumo, rasilimali watu, majengo, miundombinu, na kitega uchumi chenyewe cha WTC, hasara hii inafikia jumla ya shilingi za kitanzania Quadrillion 6 (Trilioni elfu sita za kitanzania).
Swali la kujiuliza iliwezekana vipi kutekeleza shambulio kubwa kiasi hiki tena kwa mfululizo kwenye nchi ambayo ndio kioo cha dunia kuhusu masuala ya usalama, ujasusi na intelijensi?? Ni nini hasa kilitokea??
Ili kulielewa kwa uzuri zaidi suala hili, yatupasa tuangalie jinsi mioango ilivyoanza kupangwa kwa umakini na ustadi mkubwa kwa muda wa miaka mitano.
Yaani ndio kusema kwamba, mipango ya utekelezaji wa tukio hiliilianzawaka 1996.!
Lakini pia, kabla hatujaanza kuitazama jinsi mipango na mikakati ya tukio hili ilivyopangwa, ni vyema kuangalia chimbuko la “mbegu” iliyochochea kuwapa hamasa watu hao kutekeleza tukio hili.
MBEGU INAPANDWA: CIA, Operation Cyclone
Mwaka 1978 yalitokea maoinduzi nchini Afghanistan yaliyomuweka madarakani Rais Nur Mohammad Taraki.
Baada ya Rais Nur Taraki kuchukua madaraka alianzisha Urafiki na nchi ya Urusi ya kipindi hicho ambayo ilikuwa imepania kueneza Ukomunisti ulimwenguni.
Hii ilipelekea December 5, mwaka huo 1978 Rais Taraki kusaini makubaliano ya “Urafiki” wa miaka 25 kati ya Urusi na Afghanistan.
Hii ikipelekea Rais Taraki kuanzisha sera Kikomunisti ambazo zilikuwa hazikubaliki katika jamii ya Afghanistan.
Mfano, Taraki akaondoa sheria iliyokuwa inaruhusu wazazi kumchagulia mchumba binti yao pia akaaruhusu wanawake kushiriki siasa.
Pamoja na hili akaanzisha Mapinduzi ya Sera ya ardhi ambayo ilidhibiti kiasi cha ardhi kinachoweza kumilikiwa na familia moja.
Hii ilisababisha zaidi ya hekari milioni 1.6 kupokonywa kutoka kwa familia mbali mbali na kurudishwa serikali.
Pamoja na hilo Rais Taraki akaanzisha kampeni ya kuwafunga gerezani wapinzani wake wa kisiasa nje ya chama chake na hata ndani ya chama chake cha People’s Democratic Party of Afghanistan.
Inakadiriwa kwamba zaidi ya wapinzani 27,000 waliuwawa kipindi cha utawala wa Rais Taraki.
Hii ikapelekea Rais Taraki kuchukiwa mno ndani ya Afghanistan na mwishoni akapinduliwa kutoka madarakani na rafiki yake aliyeitwa Hazifizullah Amin.
Baada ya Amin kuingia madarakani ilikurudisha imani ya wananchi akaanza kuondoa sera za ukomunisti akaanza kukata mawasiliano na Urusi.
Kutokana na mahusiano ya Afghanistan na Urusi kuzorota mno hii ikapelekea December 24, 1979 Majeshi ya Urusi yakaivamia Afghanistan na kumuua Rais Amin na kumuweka kibaraka wao aliteitwa Babrak Karmal.
Baada ya Karmal kuwa rais akaanza kurejesha tena sera za Ukomunisti na kujenga tena ukaribu na Urusi.
Hasira za wananchi zikawaka zaidi.
Kwanza walipinga uvamizi wa Urusi, lakini pia walipinga Sera za ukomunisti nchini mwao.
sept 12.jpg
Majeshi ya Urusi yakiigia Afghanistan Desembe 24, 1979.
Ndipo hapa vikaanza kuibuka vikundi vya upiganaji vya Mujahedeen kila kona ya nchi.
Vikundi hivi viliungana mwaka 1981 na kuunda umoja uliojulikana kama Islamic Unity of Afghanistan Mujahedeen.
Vikundi hivi vilipambana kila kona ya nchi kupinga uwepo wa majeshi ya Urusi nchini Afghanistan na uwepo wa vibaraka wa Urusi serikalini.
Ikumbukwe kwamba kipindi hiki ndicho kipindi ambacho ‘Vita Baridi’ kati Urusi na Marekani ilikuwa imepamba moto.
Ndipo hapa ambapo Marekani kwa kushirikiana na nchi nyingine za Kiarabu wakaanzisha mkakati wa kuvisaidia vikundi hivi vya Mujahedeen kupambana na majeshi ya Urusi nchini Afghanistan.
Mkakati huu ulisimamiwa na Shirika la ujasusi la CIA, na mkakati huu ulijulikana rasmi kama OPERATION CYCLONE
Operation Cyclone ilikuwa na malengo makuu mawili;
Moja:- kuwapatia mafunzo waoiganaji wa Mujahedeen.
Mafunzo hawa yalikuwa yanafanyika nchini Pakistan kwa kushirikiana na jeshi la nchi hiyo na Idara yake ya Ujasusi (ISI – Inter Service Intelligence).
Jumla ya wapiganaji wa Mujahedeen 100,000 walipatiwa mafunzo ya kijeshi kuanzia mwaka 1978 mpaka 1992.
Mbili:- kutoa msaada wa kifedha kwa vikundi vya Mujahedeen.
Msaada huu ulikuwa katika mtindo wa fedha taslimu na silaha.
Pia msaada huu ulitolewa katika awamu mbili.
Miaka sita ya kwanza (1981-1987) marekani ilitoa jumla silaha na fedha taslimu zenye thamani ya Dola bilioni 3.2.
Katika awamu ya pili (1987-1993) Marekani waliwapa vikundi vya Mujahedeen jumla ya fedha silaha na fedha tasilimu vyenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 4.2
Nchi ya Saudi Arabia nayo ikaweka ahadi ya ya “kumatch a dollar for a dollar” yaani kama marekani akitoa dola moja nao wanatoa moja, wakitoa bilioni nao wanatoa bilioni.
Kwahiyo, Mujahedeen nchini Afghanistan walikuwa na rasilimaki fedha za kutosha, silaha za kutosha na mafunzo adhimu kabisa ya kijeshi. Hivyo vita ilikuwa kali kweli kweli.
sept 13.jpg
Wapiganaji wa Mujahedeen nchini Afghanistani, 1981.
Wakati huo huo,
Nchini Suadi Arabia, kulikuwa na familia maarufu ya Bilionea ambaye ndiye alikuwa raia tajiri zaidi asiyekuwa mwanafamilia ya kifalme (wealthiest non-royal citizen)! Bilionea huyu aliitwa Mohammad bin Awad bin Laden na alikuwa ndiye mmiliki wa kampuni ya SAUDI BINLADEN GROUP, kampuni kubwa zaidi ya Ujenzi nchini Saudi Arabia.
Bilionea huyu aliuwa amezaa na mke wake wa kumi Hamida al-Attas, kijana aliyeitwa Usama bin Mohammad bin Awad bin Laden ambaye alizaliwa tarehw 10, March 1957.
Kijana huyu alisomea fani ya Uchumi na utawala wa biashara katika chuo kikuu cha King Abdulaziz University. (Japokuwa zipo taarifa zinazoonyesha kuwa huenda alisomea Uhandisi (civil engeneering)).
Wanafunzi wenzake wanaeleza kuwa alikuwa ni kijana mwenye bidii ya masomo na alikuwa muumini mtiifu wa Kiislamu dhehebu la Sunni.
Inaelezwa kuwa alitumia muda mwingi sana chuoni kujisomea Qur’an na kufanya kazi za kujitolea.
Pia inaelezwa kuwa alianza kuwa shabiki wa Klabu ya mpira ya Arsenal tangu akiwa hapa chuoni.
Pia alipendelea sana kutunga ushahiri na kusoma vitabu vya fasihi.
Kijana huyu alivutiwa na vugu vugu la Wapiganaji wa Mujahedeen lililokuwa linaendelea nchini Afghanistan.
Kijana huyu alishawishika mno na mahubiri ya mwanatheolojia wa kiislamu mwenye asili ya Plaestina aliyeitwa Abdullah Azzam ambaye mpaka sasa ndiye anafahamika kama “Baba Wa Jihad Duniani” (Father of Global Jihad).
Kijana huyu akawasiliana na Azzam, na Azzam akamshawishi na kumsaidia ajiunge na Mujahedin.
Hivyo baada ya kumaliza chuo (wengine wanasema aliondoka miezi michache kabla ya kuhitimu) alielekea moja kwa moja Afghanistan kujiunga na wapiganaji wa Mujahedeen kupinga uwepo wa majeshi ya Urusi kwenye Ardhi ya Afghanistan.
sept 14.jpg
Osama bin Laden (aliyezungushiwa duara)na wanafamilia wenzake wa Bilionea Mohammad bin Awad walipotembelea London kwa mapumziko miaka ya 1970s
Akiwa nchini Afghanistan, yeye Osama pamoja na Azzam ambaye sasa alikuwa ndiye “mentor” wake wakaanzisha Muktab al-khidamat (MAK) au kwa jina lingine ilijulikana kama Afghan Services Bureau.
Kazi kuu ya MAK ilikuwa ni kueneza propaganda na kushawishi vijana kutoka nchi za Kiarabu wajiunge na Mujahedeen nchini Afghanistan kupigana na majeshi ya Urusi.
Si hivyo tu, bali pia MAK ilikuwa na jukumu la kukusanya michango kutoka kwa watu mbali mbali duniani waliokuwa wanaunga mkono harakati za Mujahedeen.
Osama akatumia kiasi kikubwa cha utajiri wake aliorithi kutoka kwa baba yake (bilionea Muhammad bin Awad bin Laden alifariki mwaka 1967 kwa ajali ya ndege), akatumia kiasi kikubwa cha fedha kuwalipia nauli, tiketi za ndege na malazi vijana wote waliokuwa wanatoka kila pembe ya dunia kujiunga na Mujahedeen.
Kujitoa kwake huku, pamoja na uwezo wake mkubwa wa kujieleza na ushawishi, kukamjengea heshima kubwa sana kwa wapiganaji wa vikundi vya Mujahedeen.
Vita ikaendelea kati ya Mujahedeen wakiungwa mkono na marekani dhidi ya majeshi ya uvamizi ya Urusi.
Baadae Urusi ikaja kuona kwamba vita hii ilikuwa na gharama kubwa kwao. Kwanza ilikuwa gharama ya kuharibu mahusiano yao ya Kidiplomasia duniani na pia vita iligharimu kiasi kikubwa cha rasilimali fedha na rasilimali watu.
Hivyo basi kiongozi wa Urusi wa kipindi hicho, Mikhail Gorbachev akaamuru majeshi kurejea nyumbani na kikosi cha mwisho cha Urusi kiliondoka Afghanistan tareahe 15, February 1989.
Baada ya majeshi ya Urusi kuondoka, vikundi vya Mujahedeen walibakiwa na wapiganaji wengi na silaha nyingi za kutosha lakini hawakuwa na adui wa kupigana naye.
Hivyo wakaanza “kutengeneza” maadui wapya.
Wakanzisha vugu vugu la kudai kukomeshwa kwa ukandamizaji wa Israel dhidi ya Palestina na kudai “Uhuru” wa eneo la Kashmir.
Pia wakaweka msimamo kuwa hawataki uwepo wa wanajeshi wa nchi za magharibi katika nchi yoyote ya Kiarabu.
Vugu vugu hili ndilo likasababisha kuanza uadui kati yao vikundi vya Mujahedeen na mshirika wao Marekani.
Ndipo hapa ambapo viongozi kadhaa wa vikundi vya Mujahedeen wakafanya kikao cha siri ili kupanga mikakati mipya, mbinu mpya na falsafa mpya ya kumkabili adui yao mpya, Marekani na nchi za magharibi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mlinzi binafsi wa Osama Kikao hiki cha siri kubwa kilifanyika Tarehe 11 August 1988 na kiliudhuriwa na viongozi wakuu wa Mujahedeen akiwemo Ayman al-Zawahiri, Abdullah Azzam na Osama bin Laden.
Kupitia kikao hiki, kikundi kipya kikaundwa na Osama bin Laden akachaguliwa kuwa Amiri Mkuu wa kikundi (General Emir).
Ni siku hii ya kikao hiki cha tarehe 11 August 1988 ndipo ambapo kilizaliwa rasmi kikundi cha kigaidi cha AL QA’IDA, na ni ndipo hapa ambapo kizaza cha matukio ya kutisha kikaanza
Usikose SEHEMU YA PILI ambayo tutaona namna ambavyo Osama Bin Laden alitoa Fa’twa ya kwanza na Fa’twa ya pili (na impact zake).
Pia tutaangalia namna ambavyo mikakati ya tukio la September 11 ilipangwa kuanzia mwaka 1996.
Feb 20, 2017
Thread starter
182
1996: MKAKATI WA SHAMBULIO LA 9/11
Mwanzao kabisa baada ya Al Qa’ida kuundwa mwaka 1988 ilitokea sintofahamu katika uongozi wake wa juu ambapo Osama na Azzam wakatofautiana kuhusu mkakati wa namna ya kupambana na adui yao mpya Marekani na nchi za magharibi.
Osama alipendekeza kuwa Al Qa’ida ijikite zaidi katika mashambulio ya kujitoa muhanga pamoja na mashambulio yenye kulenga minundombinu na maeneo ambayo yana wamarekani au wazungu wengine.
Azzam hakukubaliana na hili na akatumia ujuzi wake wa elimu ya dini na ushawishi wake kusambaza ujumbe (fa’twa) yenye kupinga mashambulio ya kujitoa muhanga au kushambulia maeneo yenye mikusanyiko ya watu akidai kuwa mashambulio hayo yanaweza kusababisha vifo vya watoto na wanawake kinyume na dini ya kiislamu inavyokataza kuua wanawake na watoto katika vita.
Hii ilifanya mahusiano ya ‘kikazi’ na ‘kiitikadi’ kuzorota kati ya Osama na swahiba wake Azzam.
Novemba 1989 Abdullah Azzam akiwa na familia yake kwenye gari akielekea kwenye swala ya ijumaa eneo la Peshwar nchini Pakistani waliuwawa kwa bomu ambalo lilikuwa limetegwa barabarani..
Mpaka leo hii kuna utata mkubwa juu ya wahusika wa kifo cha Abdullah Azzam.
Wengine wakidai Mosaad ilihusika ili iweze kumfunga mdomo kutokana na msimamo wake mkali wa kupinga Israel kudhibiti eneo la Palestina.
Wengine wanaihisisha CIA na kifo cha Azzam.
Lakini katika ulimwengu wa masuala ya Intelijensia, wengi wanaamini Osama bin Laden yuko nyuma ya kifo cha “mwanazuoni nguli” Abdllah Azzam, Father of Global Jihad.
Vyovyote vile ukweli ulivyo, lakini kifo cha Azzam kilipandisha zaidi ‘status’ ya Osama ndani ya Al Qaida na vikundi vya Mujahedeen kwa kuwa sasa hakukuwa na mwanafalsafa wa kupinga mikakati yake.
MAANDALIZI YA AWALI
Mwaka 1991, Osama bin Laden alihmishia makazi yake nchini Sudan akiongoza wapiganaji wake kufanya mashambulio ya ukubwa wa kati mfano, shambulio dhidi ya msafara wa wanajeshi wa Kimarekana mjini Mogadishu mwaka 1993.
Mwaka 1996 alihamishia tena makazi yake nchini Afghanistan.
Fa’twa ya kwanza
Fa’twa ya kwanza kutolewa na Osama ilikuwa ni mwaka 1996 na ilikuwa na ujumbe wa moja kwa moja.
Kwanza aliwataka waislamu hasa waliojitoa kwa ajili ya dini ya kiislamu kupinga umagharibi na desturi zao. Lakini pia akaitaka Marekani kuondoa vikosi vyao vya kijeshi vilivyopo Saudi Arabia akisisitiza kuwa ardhi hiyo ni takatifu si sahihi kuwepo kwa majeshi ya “kafir”.
Fatwa hii ilijipatia umaarufu sana katika ‘ulimwengu’ wa vikundi vya kigaidi na iliwavutia wengi.
Moja ya waliovutiwa kwa kiwango kikubwa na fa’twa hii alikuwa ni Khalid Sheikh Mohammed maarufu kama KSM ambaye kwa miaka mingi amwkuwa akitamani kukutana na Osama.
Khalid Sheikh Mohammed ni nani??
Msomi wa Shahada ya Sayansi ya Uhandisi (Bachelor of Science in Mechanical Engineering) aliyoipata kutoka Chuo kikuu cha Chowan, jimboni North Carolina nchini Marekani.
Amezaliwa tarehe 14 April 1965 eneo la Bacholistan, nchini Pakistan.
Akiwa na miaka 16 pekee aliwahi kusikia mahubiri ya mwanatheolojia wa kiislamu aliyeitwa Abdul Rasul Sayyef na alivutiwa sana na mahubiri hayo yaliyohusu Jihad.
Baadae ndio akaenda kusoma nchini Marekani. Taarifa za intelijensia zinaamini kuwa kitendo cha KSM kuishi Marekani kulimfanya aichukiw zaidi nchi hiyo badala ya kuipenda au kupunguza msimamo wake mkali.
Moja ya matukio yaliyomfanya kuichukua zaidi Marekani ni kitendo cha kuwekwa jela kwa muda kutokana na kushindwa bili zake.
Baada ya kumaliza chuo, mwaka uliofuata yaani 1987 yeye na kaka yake wakaelekea Afghanistani kujiunga na vikundi vya Mujahedeen.
Baada ya vita na majeshi ya Urusi kuisha mwaka 1989 KSM akaendelea kujihusisha na mitandao ya kigaidi akitumia muda wake mwingi kuishi nchini Qatar kama muhandisi akitumia majina ya bandia.
Baadae kati ya mwaka 1993 na 1995 akaelekea nchini ufilipino ili kutekeleza mpango wa Kigaidi dhidi ya Marekani.
Yeye na wenzake watano wakapanga kuwa wachague siku maalumu ambayo watakuwa wakipanda ndege zaidi ya kumi na mbili za abiria za kimarekani (wanapanda na kushuka kabla ya ndege kuruka) lakini ndani ya ndege kwenye mizigo kwa ustadi mkubw watakuwa wanaacha mabegi yenye mabomu yaliyotegwa kulipuka kwa muda maalumu.
Wakachagua ndege za ‘kuzitarget’, na wakachagua siku watakayo Fanya hivyo.
Kabla ya tukio lenyewe kwanza wakaona wajaribu kwenye ndege binfsi ya mtu ili waone ‘impact’ yake
Hapa ndipo wakaharibu mpango wao, kwani walifanikiwa kutega bomu kwenye ndege ya mtu na ndege iliporuka wakailupua na rubani wa kijapani aliyekuwemo kwenye ndege akauwawa.
Hii ikapelekea kufanyika uchunguzi mkali wa vikosi vya ufilipino kwa kusaidiwa na CIA na hatimaye wakagundua mkakati wa KSM na wenzake.
Baada ya mkakati kugunduliwa ikambidi KSM kukimbia na kurudi Qatar, lakini nako tayari taarifa zake zilikuwa zimefika kuwa anatafutwa na marekani na ndipo hapa ikambidi akimbilie Afghanistani.
Kipindi hiki ambapo KSM alikimbilia Afghanistan ilikuwa ni mwaka 1996 na ndio kipindi hiki ambapo Osama Bin Laden alitoa fa’twa yake ya kwanza ambayo ilimvutia sana KSM na akaanza tena mikakati aweze kuoanana na Osama.
Ikanbidi atumie connections zake zote alizonazo kwenye mitandao ya kigaidi na hatimaye akafanikiwa kukuatana na moja ya maluteni wakuu wa Al Qaida aliyeitwa Mohammed Atef.
Baada ya kumueleza Atef kuhusu nia yake ya kutaka kuonana na Osama, Atef akakubaliana naye na kati kati ya mwaka 1996 Mohammed Atef akaandaa kikao maakumu katika milima ya Tora Bora kati ya Osama Bin Laden na Khalid Sheikh Mohammed.
Ni katika kikao hiki ambapo KSM aliwasilisha mkakati ambao ulitumika kutekeleza tukio la September 11.
Siku hii ambayo KSM alionana na Osama akiwa pamoja na Mohammed Atef moja ya makamanda wakuu wa wapiganaji wa All Qaida.. KSM akawasilisha mpango unaofanana kabisa na ule mpango ambao alidhamiria autekeleze nchini Ufilipino.
KSM alimuelezea bin Laden namna ambavyo mkakati huu utatekelezwa hatua kwa hatua.
Mkakati huu (KSM alivyoueleza kwa Osama mwaka 1996) ulihusisha namna ambavyo wataweza kupenyeza wapiganaji wa Al Qaida nchini marekani na namna ambavyo watateka jumla ya ndege kumi na mbili kutoka pwani ya Mashariki ya Marekani na pwani ya Magharibi.
KSM akapendekeza ndege hizi zikishatekwa ziende zikababizwe na kujilipua katika majengo yafuatayo;
- World Trade Center, New York City
- The Pentagon, Arlington, Virginia
- The Prudential Tower, Boston, Massachusetts
- The Whitehouse, Washington, DC.
- The Willis Tower (The Sears Tower) Chicago, Illinois
- The U.S Bank Tower, Los Angels, California
- Transamerica Pyramid, San Fransisco, California
- Columbia Center, Seattle, Washington
Hizi ndizo zilikuwa original targets ambazo zilipendekezwa na KSM katika kikao hiki na Osama.
Osama alikubaliana na mapendekezo ya hizi targets isipokuwa tu Jengo la U.S Bank Tower akataka liondolewe kwenye orodha (nitaeleza mwishoni mwa makala nadharia za intelijensia zinazo jaribu kufafanua uamuzi huu wa ‘utata’ kwa Osama kutaka U.S Bank Tower iondolewe kwenye orodha).
Lakini kwa ujumla wake Osama akaukubali mpango wote wa KSM na akamuomba KSM ajiunge rasmi na kuwa mwanachama wa Al Qaida.
Ilichukua miezi kadhaa (na wengine wanadai mwaka mzima) kumshawishi KSM kuwa mwanachama wa All Qaida.. Yaani KSM alikuwa ni muamini katika masuala ya ugaidi lakini alikuwa anapenda abaki kuwa huru asijifunge nankikundi chochote.!! Lakini mwishowe akakubali kujiunga na kuwa mwanachama rasmi.
Hivyo basi mwaka uliofuata 1997 KSM akaihamisha familia yake iliyokwepo Iran na kuipeleka Karachi, nchini Pakistan ili awenayo karibu yeye mwenyewe akielekea Kandahar katika harakati zake nchini Afghanistan.
Mara ya kwanza alipoingia kuwa mwanachama wa Al Qaida, KSM alipewa uenyekiti wa kamati ya habari (media committee) lakini baadae akapendishwa cheo mpaka kupewa uenyekiti wa kamati ya kijeshi. (Military Committee).
Kazi kubwa ya KSM katika kipindi hiki ilikuwa ni kukusanya taarifa za intelijensia za kutosha kuhusu Marekani na kufanya ‘vetting’ ya vijana ambao wana potential ya kuwe,a kutumika katika tukio hili kubwa zaidi kuwahi kupangwa na Al Qaida.
AL QAIDA INACHANJA MBUGA, MAREKANI WANAANZA KUSHITUKA KUTOKA USINGIZINI
Ikumbukwe kwamba mpaka kipindi hiki tayari CIA walikuwa na taarifa kuhusu uwepo wa gaidi anayeitwa Osama bin Laden na kikundi chake cha Al Qaida.
Taarifa hizi ziliwahi kufikishwa mpaka kwa Rais Bill Clinton mwaka 1998.
Kwa ajabu sana, taarifa hizi hazikupewa uzito (nitaeleza zaidi mwishoni mwa makala).
Hata katika kumi bora ya watu wanaotafutwa zaidi na FBI (FBI Most Wanted List) Osama bin Laden hakuwepo.
Ni mpaka pale ambapo Osama Bin laden alipotoa fa’twa ya pili na kilichofuata baada ya hapo ndipo Wamarekani wakaamka kutoka usingizini na kujua huyu Osama ni gaidi wa tofauti na anaweza kuwagharimu sana wasipokuwa naye makini.
fa’twa ya pili
(Naamini mapaja sasa wote tunaelewa fa’twa ni nini kutokana na ufafanuzi wa juzi)
Fa’twa ya pili ya Osama bin Laden ilitolewa mwezi February mwaka 1998.
Fa’twa hii ilikuwa na ujembe mkali zaidi kushinda ile ya kwanza na ilikuwa na uzito zaidi. Fa’twa hii iliilenga mahususi kabisa Marekani tofauti na ile fa’twa ya kwanza amabyo ikiongelea kwa ujumla nchi za magharibi.
Osama alikemea tena uwepo wa vikosi vya kijeshi katika mchi ya Saudi Arabia akidai kuwa wameisogelea mno ardhi takatifu ya Makka.
Pia akadai kuwa Israel inafanya mauaji ya Wapalestina kwa kusaidia na hela na silaha za wamarekani.
Osama akapinga pia uwepo wa Majeshi ya Marekani nchini Somalia, ambayo aliieleza kama nchi ya Kiislamu.
ITAENDELEA
Behind the Curtain: September 11 Sehemu ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;