CHOMBEZO

Ep 02: Tabia ya Bosi

SIMULIZI Tabia ya Bosi
Tabia ya Bosi Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA  ENOCH LIBERATUS

*********************************************

Chombezo : Tabia Ya Bosi 

Sehemu ya Pili (2)

Grace hakuamini mtu aliyemuona mbele yake alianza kulia kwa uchungu zaidi hadi Baba yake akashindwa amsaidieje katika wakati huo,Baba Grace alimuuliza “Mwanangu kitu gani kilichokukuta mbona unalia hivi na mbona unatembea kwa kuchechemea””

Grace aliendelea kulia kwa uchungu zaidi akajikuta akishindwa hata kumuelezea Baba yake kuhusu kitu kilichokuwa kimemkuta,Baba Grace alimtuliza huku akimkumbutia na kumbembeleza akimtaka aweze kunyamanza ,ila bado Grace aliendelea kulia ,alimpeleka ndani na katika muda huo Mama Grace hakuwepo nyumbani hapo,Baba Grace alimsogelea binti yake Grace kisha akamuuliza “””Binti yangu naomba uniambie mimi ni Baba yako nieleze kila kitu nitakusaidia unapoendelea kulia unanitia wasiwasi ,naomba unieleze kila kitu kilichokukuta,Baba Grace aliendelea kumbembeleza Grace.

Grace baada ya kuambiwa maneno ya kufariji kutoka kwa Baba yake alianza kuzungumza kwa uchungu huku machozi yakimchulizika katika mashavu yake,Grace alimgeukia Baba yake kisha akamwambia “”Baba nimetolewa Bikra yangu tena kwa nguvu bila mimi kuridhia” ,Askofu Habiloni Kusikia hivyo kigugumizi kilimshika ghafla akasema “”mwanangu niambie nani aliyekutoa bikra wewe kwa nguvu bila kuridhia kwako””Baba Grace alionekana kushituka sana baada ya kusikia Binti yake wa pekee ametolewa bikra tena kwa kulazimishwa.

Grace aliendelea kumsimulia Baba yake kuanzia mwanzo hadi mwisho huku bado akiendelea kulia ,Baba Grace kwa alichoambiwa na Grace kuwa aliyemtoa bikra ni “Bosi Kefason” wakati akiwa ameenda kuomba kazi katika kampuni yake, aliweza kuumia sanaa kwa kitendo alichofanyiwa mtoto wake wa pekee ambaye aliutunza usichana wake akiamini kuwa itakuwa zawadi ya Mme atakaye pewa na Mungu akitegemea kuwa ndiye mtu pekee atakaye weza kumtoa bikra yake.

Baba Grace alikasilika ,moyo wake ulimuuma sana alitaka kuchukua maamuzi magumu dhidi ya Kefason, ila wakati Baba Grace akiwa katika dimbwi la mawazo akifikiria kitu cha kufanya hiyo ni kutokana na kubakwa kwa Binti yake, Mama Grace alitia timu nyumbani hapo,Baba Grace alipopeleka macho yake mlangoni alimuona Mama Garce mbele yake,Mama Grace alishangaa sana kumuona Mme wake na Mtoto wake wote wakiwa katika hali ya Majonzi na huzuni kama watu waliokuwa wamepatwa na msiba.

Kitendo cha Grace kumuona Mama yake kiliweza kumfanya aongeze sipidi ya kulia,Grace alilia kwa nguvu akisema”””Mama yangu nionee huruma mimi,sijui nifanyeje jamani””,Mama Grace alibaki katika hali ya kushangaa akishindwa kuelewa kinachoendelea,Mama Grace alimkimbilia Grace , na kujaribu kumunyamanzisha ila Grace bado hakunyamanza alizidi kulia tu ,baada ya Mama Grace kuona Grace hamwambii kitu chochote aliona amfate Mme wake ili aweze kumwambia ni kitu gani kilichokuwa kimetokea nyumbani hapo,Askofu Habiloni alianza kumsimulia Mke wake kila kitu kilichokuwa kimemkuta Grace huku na yeye machozi yakianza kumlenga lenga ingawa alitamani kulia ila alijikaza kiume.

Mama Grace hasira na uchungu vilimpanda Mara dufu moyoni mwake ,alisimama na Kusema “”Kumbe Bosi Kefason ndiye kakubaka na kukutoa bikra yako sasa ngoja nitamuonyesha”,Mama Grace alionekana kukasilika sana alimfata Grace na kumwambia “”Mwanangu we usijari mimi Mama yako nipo subiri uone kitu kitakachomkuta huyu mtu anayejiita “”Bosi Kefason”.

Mama Grace alikuwa mtu mwenye hasira sana katika wakati huo alichukua simu yake kisha akapiga upande wa pili, maongezo yao yalikuwa hivi.

Mama Grace aliongea hallo!! habari!.

Afisa wa polisi aliitika “”salama naongea na nani””Mama Grace alijitambulisha kisha akamwambia “”nina shida ninataka nije kufungua kesi mtoto wangu amebakwa”” Afisa wa Polisi huyo katika kituo cha polisi cha hapo Jijini Tehera kwakuwa alimjua vizuri Mama Grace kama Mke wa Askofu alikubali na kusema”””Sawa Unaweza kuja kufungua kesi yako”baada ya maongezi hayo Mama Grace alikataa simu.

Mama Grace bila kupoteza muda alitoka nje bila kumwambia kitu chochote wala kumuaga Mme wake ambaye muda wote alikuwa akimukodolea macho tu wakati akiongea na Afisa polisi kwenye simu .Mama Grace alifika hadi sehemu alipokuwa amepaki gari yake na alipotaka kupanda gari Mme wake alimzuia huku akimuuliza “Mke wangu unaenda kufanya nini huko mbona unataka kushindana na binadamu wewe, nishirikishe Mme wako juu ya hili lililomkuta mtoto wetu wa pekee ili tulitatue kwa pamoja sio uchukue Maamuzi mwenyewe njoo hapa tuongee Mke wangu”,Baba Grace alijaribu kumbembeleza Mke wake ila ilishindikana,Mama Grace aliutoa mkono wa Mme wake uliokuwa umemushika katika mkono wake akasema “”We baki na binti yako acha mimi nikafungue kesi sitaki binti yake ateseke wakati bado nipo hai,lazima nimfunge Kefason ,yalikuwa maneno ya Mama Grace,kisha aliiondoa gari yake na kuondoka.

Askofu Habiloni alibaki akimshangaa Mke wake ambaye aliamua kupambana na binadamu ili kumtia mbaloni Bosi Kefason Baba Grace aliona kama mauza uza hayo yaliyokuwa yakimtokea alishindwa aanzie wapi kulitatua jaribu hilo lililokuwa limeikumba famila yake katika wakati huo ,yeye aliliona kama jaribu tofauti na Mke wake,Baba Grace aliamua kurudi ndani kuendelea kumfariji Grace ,Grace katika muda huo alikuwa akitoa kwi! kwi! tu kwakuwa sauti yote ilikuwa imesha muishia kwasababu alikuwa amelia kwa muda mrefu.

Mama Grace muda huo alikuwa barabarani mbio mbio akikatiza mitaani akiwahi kituoni,Mama Grace katika wakati huo alionekana kuwa na hasira sanaa, kitendo alichofanyiwa Mtoto Grace kilimfanya kusikia uchungu mkubwa sana, kila alipokumbuka kitendo cha mtoto wake kubakwa na Kefason uchungu na hasira vilizidi kumpanda mara dufuu.

Mama Grace alifika nje ya kituo hicho cha Polisi kisha akapaki gari yake na akatoka nje ,alinyosha moja kwa moja hadi ndani ya Ofisi ya Mkuu wa kituo cha polisi aliyeitwa”Odance” ,Odance alimkaribisha Mama Grace kisha Mama Grace akawa amekaa na kuanza kumsimulia kila kitu kilichokuwa kimemkuta Grace,maongezi yao yalianza ” Odance alimuuliza ”umesema Mtoto wako amebakwa””

Mama Grace aliitikia kwa hasira “”ndiyo amebakwa wewe unafikiri nakutania au””,

Odance alimuuliza swali la pili ‘”unaweza kuniambia mshitakiwa wa kesi yako ni yupi? Mama Grace alimjibu akimwambia “”mshitakiwa ni Kefason Lameck ndiye aliyembaka mtoto wangu Grace””

Kwanza Afisa wa polisi Odance aliposikia jina la mshitakiwa kuwa ni Kefason Tajiri mkubwa sanaa katika Jiji hilo la Tehera aliweza kushituka sana kwakuwa alikuwa akimfahanu sanaa tabia zake na uwezo mkubwa aliokuwa nao, Odance alimuuliza tena akisema “”umesema aliyembaka mtoto wako ni Bosi Kefason Lameck mumiliki wa kampuni kubwa inayojihusisha na utengenezaji wa samani na kudizaini mapambo hapa mjini””

Mama Grace aliitikia kwa kusema “”ndiyo huyo huyo mnayemuita Bosi Kefason ndiye kambaka Binti yangu””.

Kabla Odance hajachukua maamuzi yoyote huku akiwa bado akiwaza jinsi ya kuweza kumsaidia Mama Grace,ghafla simu yake ya hapo ofisini kwake iliita ,kabla hajaongea kitu chochote aliipokea akisema hallo!! Kusikia vizuri Sauti ilikuwa ya kamishina wa polisi ambaye alikuwa ni Mkuu wake wa kazi ,kwanza alipunguza sauti yake kisha akasimama na kupiga saluti kwa kamishina,kilichomshangaza Mama Grace ni kuwa kila kitu alichokuwa akiambiwa Afisa Odance alikuwa akiitikia ”Ndiyo Mkuu “”,Ndiyo Mkuu”””.

Baada ya maongezi kuisha simu ilikatwa,Odance alimgeukia Mama Grace na kumwambia “”Mama Askofu Kesi yako imefungwa hakuna kesi yoyote itakayoweza kuendelea hapa kituoni rudi tu nyumbani””,Mama Grace kusikia hivyo hasira zilimpanda sana hadi macho yake yakabadilika nakuwa mekundu alitamani amlukie Odance na amutafune tafune katika wakati huo alipomuangalia Afisa Odance alianza kucheka kwa dharau “””Hahahahaaha””,Uvumilivu ulimshida Mama Grace alisikia uchungu wa ajabu alisikia kama moyo wake unataka kupasuka alimsogelea Odance alipokuwa amekaa kwa sipidi alipomfikia alifika ana mkaba shingoni kwa nguvu huku akimshitukiza bila yeye kujianda,Odance alishitukia Mkono wa Mama Grace ukiwa umeshamkaba shingoni kwake.

“”Kweli uchungu wa Mwana aujuae Mama””

Katika sehemu ya Nne tuliishia pale baada ya Afisa wa polisi Odance kukabwa na Mama Grace…

ENDELEA….

Mama Grace katika wakati huo alionekana kukasirishwa sana na maneno ya kejeli na dharau aliyokuwa ameambiwa na Afisa Odance, Mama Grace alisema “”kumbe hunijui “”alimsogelea Odance karibu pale alipokuwa amekaa Afisa Odance huku akiwa hana wasiwasi wowote tena akiongea kwa kujiamini”” we mama toka hapa kesi yako imefungwa na hatuwezi kuisikiliza tena”.

Mama Grace kwa hasira alizokuwa nazo kutokana na kitendo alichokuwa amefanyiwa mtoto wake Grace hakujali utumishi wala nini vyote aliweka pembeni kwanza, Odance bila kutegemea alishangaa mkono wa Mama Grace ukiwa umeshafimfikia shingoni kwake,,alikabwa kwa kushitukizwa wala hakuamini kama kweli aliyekuwa akimkaba vile ni Mama Askofu.

Mama Grace uso wake ulikuwa hauonyeshi huruma wala tabasamu la aina yoyote,alimkaba vilivyo ukizingatia Mama Grace alikuwa ni jimama,alikuwa na mwili mkubwa pia alikuwa na guvu za kutosha ,mwili wake ulikuwa mkubwa zaidi kushinda mwili wa Odance..

Odance alijaribu kufurukuta ili kujitoa ila alishindwaa,wakati Odance akitaka kujihami kuchukua silaha iliyokuwa chini ya meza baada ya kuona Mama Grace hataki kumuachia ,ghafla walisikia mlango ukigongwa Mama Grace kusikia mlango ukigongwa alimuachia Odance haraka, kisha akachukua mkoba wake haraka na kutoka nje .

Wakati akitoka nje alipishana na polisi mmoja ivi mlangoni aliyekuwa akiingia Ofisini kwa Afisa Odance,Polisi huyo alipo angalia mazingira ya hapo ndani alikuwa kama hayaelewi hivi hata jinsi alivyomkuta Afisa Odance alihisi kuna kitu kilichokuwa kinaendelea humo ndani ndipo akawa amemuuliza Afisa Odance

“Polisi “”Mkuu mbona shati yako limejikunja kunja hivyo kama vile limeliwa na ng’ombe?

Odance alimjibu” hii shati nilisahau kuipiga pasi kwaiyo hivi ndivyo ilivyo kwa leo!!

Polisi akauliza tena””halafu mbona huyu Mama niliyepishana nae mlangoni alikuwa akitoka humu kwa sipidi””

Odance alitabasamu kidogo kisha akamjibu”” tulipishana kauli kidogo ndipo kukawa kumetokea mtafaruko akawa amekimbia””.

Polisi huyo alicheka na kusema “”Sawa bhana tuachane na hayo” ingawa alikuwa ameshautambua ukweli kuwa Odance alikuwa amekabwa na huyo Mama ila aliamua kupotezea hakutaka kuhoji sana ,akaeleza shida yake “nillikuwa nimefata faili lenye majina ya wafungwa”,Odance alimpatia kisha akawa ameondoka.

Mama Grace baada ya kutoka ofisini kwa Odance alirudi kwenye gari yake huku akikimbia hadi watu waliokuwa maeneo hayo wakibaki wanamshangaa,Mama Grace alijua huenda Afisa Odance angeweza kumuitia mapolisi ili waweze kumkamata kutokana na kitendo alichokuwa amemfanyia ,Mama Grace aliiondoa gari yake kwa sipidi hadi watu wakabaki wanamshanga..

Wakati akiendesha gari Mama Grace machozi yalikuwa yakimtililika kama maji ,kila alipokumbuka majibu aliyoyapata kutoka kwa Afisa Odance aliishikwa na hasira sana,aliendesha gari kwa sipidi ili kupunguza hasira na uchungu aliokuwa nao katika wakati huo. Grace na Baba yake waliokuwa nyumbani,waliendelea kumsubiri Mama Grace ili aweze kurudi ndipo wao waondoke, ila baada ya kuona muda unazidi kwenda bila Mama Grace kutokezea ilibidi wajiandae kwa ajili ya kuondoka,ingawa Baba Grace alikuwa na wasiwasi sana juu ya Mke wake kwakuwa alitoka nyumbani hapo huku akiwa na hasira yote alimuachia Mungu tu kwakuwa yeye ndiye muweza wa yote.

Baba Grace alimuanda Grace ili waende hospitalini kupata huduma ya Afya, ili kama kuna tatizo lolote la kiafya lililomkuta Grace,Waweze kulitatua mapema, Askofu Habiloni alichukua pesa ya kutumia kwa ajili ya matibabu huko hospitalini kisha alimsaidia Grace kumshika na kumpeleka ndani ya gari tayari kwa Safari.

Safari yao ya kuelekea hospitalini ilianza hiyo ni baada ya mlinzi kufungua geti wakawa wamepita,wakati wakiwa njiani Baba Grace alimpigia Mke wake ili kujua Kilichondelea kwa upande wake baada ya yeye kwenda kituo cha polisi kufuatilia kesi ya kubakwa kwa Grace,alipiga simu zaidi ya mara tano ila simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa ,Mama Grace simu yake ilipokuwa ikiita alikuwa hata haijali ,alikuwa na uchungu sana kuliko kawaida,bado kitendo alichokuwa amefanyiwa mtoto wake wa pekee kilikuwa kinamuumiza sana.

Safari ya Askofu Habiloni na Grace kwenda Hospitalini iliwachukua nusu saa tu wakawa wamefika,walifika nje ya hospitali kubwa ya jiji hilo iliyoitwa “Kimara hospital”,walipokelewa vizuri na manesi kisha Grace alichukuliwa na kupelekwa katika chumba cha matibabu,Dr aliitwa kwa ajili ya matibabu,Dr huyo alifahamika kwa jina la Stephano,Dr Stephano kabla hajaenda kumtibu Grace alimwita Baba Grace ofisini kwake kisha akawa amemuuliza.

Dr Stephano “”Bila shaka wewe ndiye mzazi halari wa Grace””

Baba Grace”” ndiyo mimi ndiye mzazi wake”

Dr Stephano”” unaweza kuniambia ni kitu gani kilichomkuta mtoto wako hadi ukaamua umlete hapa hospitalini””

Baba Grace”” Binti yangu amebakwa na ukizingatia alikuwa bado bikra kwaiyo nimemleta ilimuweze kumchunguza kama kuna tatizo lolote la kiafya alilolipata tuweze kulitibu mapema kabla halijawa kubwa”

Dr Stephano baada ya kusikia maelezo ya Baba Grace alimpongeza sana na kusema “wewe unaelewa vizuri jinsi ya kujiepusha na matatizo hatarishi kwa kuchukua tahadhari mapema zaidi ,nichukue nafasi hii kukupongeza Baba Grace ,watu wote wangekuwa na uelewa kama wa kwako watu wasingeteseka kwa kitendo cha kukosa maarifa””

Baba Grace alimjibu akisema””Asante sana Dr””

Dr Stephano alimwambia Baba Grace””Binti yako tutamchunguza pia nitampima vipimo vitatu kwanza kipimo cha Ukimwi,pili kipimo cha Mimba tatu kipimo cha kaswende”.

Baba Grace aliitikia”” sawa Dr binafsi nitashukuru sana endapo mtoto wangu kama hatokutwa na tatizo lolote'”

Dr Stephano alimjibu akisema”” usijali tutajitahidi kadri ya uwezo wetu ili kumsaidia Mtoto wako”

Kisha Dr Stephano alienda kumchunguza Grace na vipimo vyote vilichukuliwa ili kujua kama Grace amepata tatizo lolote la Kiafya.

Katika sehemu ya tano tuliishia pale baada ya Dr Stephano kuweza kumfanyia uchunguzi na kumchukua vipimo Grace ili kujua kama amepatwa na tatizo lolote la Kiafya….

ENDELEA….

Dr Stephano alimfanyia Grace uchunguzi katika Sehemu zake za siri,akagundua kuwa hakuna tatizo lolote bali tu ni mchubuko mdogo uliotokea wakati Bosi Kefason anambikri,vipimo vilipelekwa maabara kufanyiwa uchunguzi na majibu yakawa yametoka,Dr Stephano alipoyasoma majibu yale alitabasamu kisha akamgeukia Baba Grace na kumwambia “” vipimo vyote tulivyompima Grace vinaonyesha hana tatizo lolote la kiafya,vipimo vyote vimesoma negative-ve,Baba Grace kusikia hivyo alishangilia sana huku akisema”” Asante yesu,Mtoto wangu hana shida””, Asante sana Mungu uhimidiwe milele na milele.

Dr Stephano alienda kumsafisha Grace katika sehemu zake za siri kwa kuzikausha na kuzifuta damu zote zilizogandiana ndani,kisha baada ya kumsafisha alimpaka dawa maalumu kwa ajili ya kumponyesha ule mchubuko uliokuwa katika sehemu zake za siri..,baada ya matibabu Dr Stephano alitoka nje kuonana na Baba Grace.

Dr Stephano alimwita Baba Grace ofisini kwake kisha akawa na maelekezo zaidi ya kumshauri juu ya Afya ya mtoto wake Grace.

Dr Stephano””” Baba Grace mtoto wako nimeshamfanyia matibabu ,kutokana na kitendo alichofanyiwa inaonekana hakuumia sana ila endapo huyo aliyembaka kama angeendelea huenda damu nyingi zingemtoka,ila cha kumshukuru Mungu ni mchubuko tu ulioonekana “

Baba Grace””Nashukuru Sana Dr, kwaiyo naondoka naye saa ngapi au ana lala leo hapa hospitalini”

Dr Stephano “kwa tatizo hili alilo nalo mtoto wako siwezi kukushauri umuache hapa bora uondoke naye,ila wakati unataka kuondoka inabidii uje nikuandikie dawa za Grace kwa ajili ya kwenda kutumia nyumbani”

Baba Grace””” sawa nashukuru sana Dr kwa matibabu yako””,kisha Baba Grace aliondoka kwenda kumuona mtoto wake aliyekuwa amelazwa katika chumba cha kujitegemea “V.I.P,” Grace alipomuona Baba yake akija alipokuwa amelazwa alifurahi sana ,Baba Grace alipomfikia mtoto wake wote walikumbatiana kwa furaha .

Baba Grace alisema”””Binti Yangu kipenzi unaendeleaje”

Grace”” Baba naendelea vizuri,sasa hivi maumivu nayo yasikia yamepungua sio kama zamani””

Baba Grace”” sawa mtoto wangu jipange kwa kuondoka leo nimesha ongea na Dr muda si mrefu tunaondoka kuelekea nyumbani”

Grace alimjibu”” sawa Baba yangu kipenzi ,hakika najivunia kuwa na Baba kama wewe”

Baba Grace”””‘Usijali mtoto wangu ila kilicho nifurahisha zaidi leo mwanangu ni kuwa hauna tatizo lolote la kiafya,vipimo vyote walivyokupima vimeonyesha hauna shida yoyote ya kiafya nijambo la kumshukuru Mungu mwanangu””

Grace kwa furaha alimjibu akimwambia””‘” Kweli Baba yangu hata mimi namshukuru Mungu nilijua nitakuwa Nimepeta Ukimwi au Mimba ila niko salama kabisa yani Dr alivyonipa majibu kuwa sina tatizo lolote nilifurahi sana””

Baba Grace alimfariji mtoto wake kwa kumkumbatia akimwamba””mwanangu tunaye mtumikia anaweza na ana nguvu tuzidi kuimalika katika yeye atutiae nguvu””

Mama Grace yeye baada ya kufika nyumbani alipaki gari yake haraka kisha akatoka nje ya gari huku akilia na kukimbia hadi ndani,wakati akikimbia mlinzi wa geti aliyeitwa Mudy ,alimshangaa sana Mama Askofu bila kujua kilichokuwa kikiendelea nyumbani hapo,alipotaka kumuuliza Mama Grace alikosa nafasi na kwa hali aliyomuona nayo hata angemuuliza asingeweza kumjibu,Mama Grace alionekana mtu mwenye majonzi na hasira sana.

Mama Grace aliweza kukimbia hadi ndani,ila alipofika sebuleni alipitiliza hadi chumbani kwake,alipofika chumbani alijifungia ndani kisha akajitupia kitandani na kuanza kulia kwa sauti kubwa kama mtoto mdogo , muda mwingine alimlaumu Mungu kwa nini ameweza kuruhusu mambo hayo yote yaweze kutokea kwa mtoto wake wa pekee aliyempenda sanaa,Mama Grace aliendelea kulia akijuwa kuwa Mungu ameshamuacha kwa kuweza kuruhusu majaribu hayo yaweza kuikuta familia yake.

Baba Grace katika wakati huo aliangalia saa , muda wa kuondoka ulikuwa umeshawadia ilikuwa saa kumi na mbili za jioni,alimfata Dr Stephano kisha Dr Stephano akawa amemuandikia dawa za Grace kutumia awapo nyumbani alimpa dawa zilizoitwa PEP na dawa zingine huku akimwambia Baba Grace arudi tena hapo hospitalini na Grace kwa vipimo zaidi baada ya miezi mitatu,Baba Grace alienda kulipia juu ya matibabu yote aliyokuwa amepewa Grace ,kisha akawa amemsaidia kumpeleka ndani ya gari,tayari kwa safari ya kwenda nyumbani.

Walipokuwa njiani waliendelea kutaniana na kupiga stori za hapa na pale,zaidi Baba Grace alikuwa akimfariji mtoto wake,akimwondolea wasiwasi na kumtia faraja kutokana na kitendo alichofanyiwa na Bosi Kefason, safari yao haikuwachukua muda mrefu breki zilisikika nje ya geti ,Mudy aliposikia honi ya gari alifungua geti kisha Askofu Habiloni akawa ameingia, Mudy alimuuliza Bosi wake baada ya kushuka kwenye gari

Mudy””‘ Boss ni kitu gani kinaendelea mbona sielewi,Mama Grace nilimfungulia akatoka ndani ya gari na kukimbilia ndani huku akilia na wewe pia unataka upite bila kuniambia chochote ,mimi nitaikimbia sasa hii nyumba”

Baba Grace alimtuliza na kumwambia “”wewe usihofu ni mambo ya kawaida tu ila kwa ufupi mdogo wako hapa Grace amebakwa kwaiyo usishangae kuona hayo yote yakiendelea hapa nyumbani ni mapito tu na hapa unapotuona tumetoka hospitalini” Baba Grace aliongea kwa uchungu kwani hata yeye kitendo alichofanyiwa Mtoto wake kilimuumiza sanaa.

Mudy alimfata Grace na kumwambia “”pole mdogo wangu kwa kilichokukuta Mungu atakusaidia”

Grace”” Asante kaka yangu nashukuru kwa kunifariji”

Baba Grace alimshika mkono Grace na kumsaidia kumuingiza ndani,walipofungua mlango wa sebuleni walipokelewa na sauti ya kilio,wote walisikia sauti ya mtu akilia, Grace alimuuliza Baba yake

Grace”” Baba ni kitu gani kitakuwa kimemkuta Mama Mbona yuko analia hivyo”

Baba Grace”” Binti yangu hata mimi sijui ni kitu gani kilichomkuta huko alikoenda mpaka nikamuulize””

Baba Grace alimpeleka Grace chumbani kwake ili ajipumuzishe ,kisha akarudi kufungua mlango katika chumba chake ,alipojaribu kuufungua mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani,aliita sana kwa zaidi ya mara sita”” Mama Grace fungua mlango niingie”,Mama Grace alisikia sauti ya Mme wake ila hakuweza kufungua mlango zaidi tu aliendelea kulia..

Katika sehemu ya Sita tuliishia pale Askofu Habiloni alipokuwa akigonga mlango katika chumba chake ili kuweza kuingia ndani ndipo Mama Grace akawa amegoma kufungua mlango zaidi tu akiendelea kulia..

ENDELEA….

Baba Grace baada ya kusubiri muda mrefu bila Mke wake kufungua mlango,alijiongeza akawa amesogea karibu na mlango kisha akaongea kwa sauti akimwambia Mke wake””Mama Grace mtoto wako amelazwa hospitalini yuko hoi ,ulipotoka tu nilimpeleka wamfanyie vipimo Daktari amesema ana mimba “‘”

Mama Grace kusikia hivyo aliahirisha na kulia alifungua mlango haraka huku akiwa ametoa macho na kusema “” Baba Grace unachokisema ni kweli ebu acha utani kwanza Grace binti yangu yupo wapi” ,Baba Grace alimjibu akisema”””Mama Grace samahani nilikuwa nakutania bhana najua nisingekwambia hivyo usingefungua mlango kwakuwa ulikuwa umekazana kulia tu kama vile mtoto mdogo”

Mama Grace alimjibu Mume wake akisema”” Niambie kwanza ulikuwa umeenda wapi na Grace wangu, Grace yupo wapi naomba unijibu Mume wangu?Mama Grace alionekana mtu aliyepagawa alikuwa na hamasa ya kujua kama binti yake yupo sehemu salama

Baba Grace alimjibu”‘ yupo chumbani kwake tumetoka hospitalini kumpima hana tatizo lolote la kiafya hana mimba wala nini””

Mama Grace kusikia hivyo alishangilia sana kwa furaha aliyokuwa nayo alijikuta anakumbatia Mume wake na kusema “”Dahh!! Mume wangu nimefurahi sana kusikia hivyo, Ila kwa upande wangu kule kituoni nilipoenda kila kitu kilishindikana””,aliendelea kuongea kwa uchungu akisema,””huwezi kuamini Mume wangu leo nimefukuzwa kama mbwa” huku wakiniambia kesi ya binti yangu imefutwa na haitoweza kusikilizwa tena”””.

Mama Grace alianza kulia upya, Baba Grace alichukua nafasi hiyo kumliwaza na Kumbembeleza zaidi akimtia moyo

Baada ya Baba Grace kumtuliza Mke wake alimwambia akamuone Grace ambaye aliyekuwa chumbani kwake akiwa amejipumuzisha,Mama Grace alielekea chumbani kwa Grace huku akimwita “Grace mwanangu,alipofika chumbani kwake alifika anamuamisha kitandani akimwambia””Binti yangu nakuomba uamke”,Grace baada ya kusikia akiitwa na Mama yake aliweza kuamka ,baada ya kuamka alishangaa sana kumuona Mama yake akiwa mtu mwenye furaha sana huku akitokwa na machozi ya furaha .

Mama Grace aliongea”” Binti yangu pole sana kwa kilichokukuta ila nimefurahi sana kusikia hauna shida yoyote ya kiafya””

Grace””” Asante Mama yangu ni jambo la Kumshukuru Mungu”

Mama Grace”” Mwanangu sasa hivi penyewe Unajisikiaje lakini?

Grace””” Mama naendelea vizuri tofauti na wakati ule nilipokuwa bado sijapewa matibabu.

Mama Grace”” sawa Binti yangu kipenzi jipumuzishe ngoja mimi nikaandae chakula jikoni na nikuandalie maji ya moto ili nikusafishe ata miguu””

Grace aliitikia”” Sawa Mama yangu””

Mama Grace baada ya kuongea na binti yake aliingia jikoni kuendelea na mapishi,wakati huo Mume wake akiwa chumbani katika wakati huo alikuwa kapiga magoti huku akimlilia Mungu wake.

Baba Grace aliendelea kuomba kwa muda wa zaidi ya dakika ishirini na sita,alimuomba sana Mungu wake akisema “”Baba yangu uliye juu wewe ndiye wajuwa majaribu na misukosuko inayoikumba familia yangu naomba usimame juu ya hili ,bila wewe hatuwezi””,aliomba sana alipomaliza kuomba ndipo Mke wake alipopata nafasi ya kuingia chumbani kumkaribisha ili akaoge kwakuwa alikuwa bado hajaoga.

ITAENDELEA

Tabia ya Bosi Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment