Balaa Sehemu ya Pili
KIJASUSI

Ep 02: Balaa

SIMULIZI Balaa
Balaa Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA: HALFANI SUDY

*********************************************************************************

Simulizi: Balaa

Sehemu Ya Pili (2)

Usiku uleule Tano alirudi Kilwa Kivinje. Kuendelea na kazi yake ya ulinzi pamoja kumuwinda Dr Yusha. Maana usiku wa siku hiyo pia, ilikuwa lazima waipata mioyo kumi na tano katika chumba cha kuhifadhia maiti. Alifika Kivinje mishale ya saa tano usiku. Na kuikuta kazi ya kutoa mioyo imeshaanza.

Asubuhi mji wa Kilwa Masoko uliamka na taarifa mbaya tena. Taarifa ya kifo cha Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya Kilwa, Ndugu Alex Mwasola. Mwasola alikutwa ameuwawa nyumbani kwake. Muuza maziwa ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kushuhudia maiti ya Mwasola. Alikuwa na ratiba ya kumpelekea maziwa kila siku. Siku hiyo aligonga sana mlango nje, aliposukuma mlango ulifunguka na alipoingia ndani, alilakiwa na maiti ya bosi wake. Mwili wa Mwanasheria Mwasola, umelala juu ya sofa huku ukiwa umetapakaa damu kifuani. Alirudi nyuma na kuondoka bila kuaga. Hakumsimulia mtu kuhusu tukio lile, muuza maziwa aligeuka bubu.
Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, katika ofisi ya Mwanasheria watu walikuwa wamejaa. Ilikuwa siku ya kazi kwahiyo watu walijaa kufata huduma katika ofisi hiyo, watu wengi walikuwa wamekaa nje ya ofisi hiyo kwa kadri ya saa tano, bila Mwanasheria kutokea. Walijaribu kumpigia simu lakini simu yake iliita bila kupokelewa. Bahati mbaya Mwasola alikuwa hajaoa na wala hakai na mtu yeyote nyumbani kwake. Ilibidi atumwe mlinzi kwenda kwa Mwanasheria kumwangalia. Ilipo ofisi ya mwanasheria na mtaa wa National hakukuwa mbali sana. Yule mlinzi aliyetumwa kwa Mwanasheria alikutana na balaa.
Picha mbaya kama aliyokutana nayo Muuza maziwa. Mwili wa Mwanasheria ukiwa umelala sofani huku kisu kikiwa kinaning’inia kifuani mwake, na damu zilizoanza kukauka kifuani. Yule mlinzi alishindwa kuvumilia, alipiga makelele, makelele yaliyowajaza kwa kasi majirani.

Walimkuta Mwanasheria ameuwawa!
Illikuwa majonzi na kilio kikubwa sana kwa majirani.
Baada ya muda mfupi, askari Polisi waliwasiri. Haikujulikana hata ni nani aliyewapigia simu Polisi hao.
Walianza kufanya uchunguzi mle ndani, baadae wakauchukua mwili wa Mwanasheria na kuupeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Muda mfupi tu habari za kifo cha Mwanasheria zikasambaa Kilwa nzima. Zilisambaa mpaka kilabuni na kumfikia Mwanasheria mlevi.

Taarifa za kuuwawa kwa Mwanasheria zilimstua sana Mwanasheria mlevi. Alilala kilabuni siku ile Mwanasheria. Na aliyemletea taarifa za mauaji hayo ni rafiki yake kipenzi katika ulevi, mama Kindumba.

“Mwanaaa” Mama kindumba aliita kilevi huku akifupisha jina la Mwanasheria.
“Nambie mama kindumba” Mwanasheria nae aliitikia kwa sauti ya kilevi pia.
“Umesikia wajina wako kauwawa!”
“Nani tena?”
“Mwanasheria”
“Mama kindumba unaumwa nini, Mwanasheria si mimi hapa” “Mwanasheria wa ukweli bana”
“Unaamaanisha Bwana Mwasola?”
“Ndiyo huyo huyo”
“Haaaa!”
“Ndo hivyo wamemkuta kapigwa bonge la kisu nyumbani kwake”
“Aisee, lakini poa bora nibaki Mwanasheria peke yangu”

Mwanasheria mlevi alitia mzaha uliomchekesha kila mtu pale kilabuni. Bila kujua balaa iliyoko ndani yake..
“Ngoja nimpigie Dokta Yusha alikuwa rafiki yake sana”

Simu hiyo ya Mwanasheria kwenda kwa Dokta Yusha ilizua kizaazaa kipya..

Walimkuta Mwanasheria ameuwawa!
Illikuwa majonzi na kilio kikubwa sana kwa majirani.
Baada ya muda mfupi, askari Polisi waliwasiri. Haikujulikana hata ni nani aliyewapigia simu Polisi hao.
Walianza kufanya uchunguzi mle ndani, baadae wakauchukua mwili wa Mwanasheria na kuupeleka hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Muda mfupi tu habari za kifo cha Mwanasheria zikasambaa Kilwa nzima. Zilisambaa mpaka kilabuni na kumfikia Mwanasheria mlevi.

Taarifa za kuuwawa kwa Mwanasheria zilimstua sana Mwanasheria mlevi. Alilala kilabuni siku ile Mwanasheria. Na aliyemletea taarifa za mauaji hayo ni rafiki yake kipenzi katika ulevi, mama Kindumba.

“Mwanaaa” Mama kindumba aliita kilevi huku akifupisha jina la Mwanasheria.
“Nambie mama kindumba” Mwanasheria nae aliitikia kwa sauti ya kilevi pia.
“Umesikia wajina wako kauwawa!”
“Nani tena?”
“Mwanasheria”
“Mama kindumba unaumwa nini, Mwanasheria si mimi hapa” “Mwanasheria wa ukweli bana”
“Unaamaanisha Bwana Mwasola?”
“Ndiyo huyo huyo”
“Haaaa!”
“Ndo hivyo wamemkuta kapigwa bonge la kisu nyumbani kwake”
“Aisee, lakini poa bora nibaki Mwanasheria peke yangu”

Mwanasheria mlevi alitia mzaha uliomchekesha kila mtu pale kilabuni. Bila kujua balaa iliyoko ndani yake..
“Ngoja nimpigie Dokta Yusha alikuwa rafiki yake sana”

Simu hiyo ya Mwanasheria kwenda kwa Dokta Yusha ilizua kizaazaa kipya.

“Hallo Dokta Yusha “
“Nambie Mwanasheria”
“Una taarifa za msiba Dokta”
“Nani tena amefariki Mwanasheria?”
“Mwanasheria Mwasola ameuwawa!
” Acha utani Mwanasheria, Mwasola ameuwawa! “
“Kachomwa kisu Dokta”
“Etiiiii”
“Ndiyo hivyo Dokta”
“Nakuja Masoko sasa hivi, ahsante sana kwa taarifa Mwanasheria”
Simu ikakatwa.
Dokta Yusha aliipokea simu ile akiwa katika benchi la wagonjwa. Lakini mtu wa pembeni yake hakuwa mgonjwa, alikuwa ni Tano wa Six killers, katika harakati zake za kumuwinda Dokta Yusha. Alisikia kila kitu alichoongea Dokta Yusha, huku akishangazwa na taarifa kwamba Mwanasheria kauwawa ilhali Dokta alikuwa anaongea na Mwanasheria.

Dokta Yusha alinyanyuka pale kwenye benchi, akiwa na Lengo la kwenda Kilwa Masoko kwenye msiba. Alipanda gari yake na kuondoka bila ya kujua kama kuna mtu alikuwa anamfata nyuma kwa kutumia pikipiki. Sasa Tano aliamua kuumaliza mchezo, kumuua Dokta Yusha kisha kwenda Kilwa Masoko kumuua huyo Mwanasheria mpya!
Hii inaitwa LIWALO NA LIWE! Tano aliona mchezo unaelekea kubaya, aliamua kuumaliza leo!

Walipofika karibu na kijiji cha Mpara gari la Dokta Yusha lilipata tatizo la kiufundi, lilizima ghafla na kusimama. Ilikuwa bahati mbaya kwa Dokta Yusha..na bahati nzuri sana kwa Tano wa Six killers

Dokta Yusha alisimamisha gari. Na kuanza kulikagua, Tano nae alisimama pale na pikipiki yake.
Hatari ilikuwa inamkaribia Dokta Yusha!

“Vipi tena kaka” Tano aliuliza huku alimsogelea Dokta Yusha.
“Gari linanisumbua kidogo” Dokta alijibu huku akilichungulia gari lake kwa chini, uvunguni.
“Ngoja nikusaidie kidogo”
“Sawa”

Dokta Yusha alifanya kosa, kukaribiana na Tano, tena wakiwa wawili porini lilikuwa ni kosa kubwa sana. Tano hakuelekea kwenye gari, Tano alimfata Dokta Yusha pale chini. Dokta Yusha alimtazama yule jamaa na kuingiwa na woga kidogo, alishangaa jinsi ya yule dereva pikipiki alivyokuwa anamfata kwa kasi, tena kishari!
Dokta Yusha nae alisimama, alijipanga kwa shari yoyote.

Tano alitoa kitu kwenye mfuko wa ndani wa koti, ilikuwa bastola!
Sasa Dokta Yusha hakuwa na mshangao tena, alikuwa makini. Kitu ambacha Tano alikuwa hajui, Dokta Yusha alikuwa amepitia mafunzo ya uaskari kabla ya kuwa dokta, mafunzo ya uaskari magereza huko Kiwira, Mbeya. Na kufanya kazi kama askari magereza mkoani Mtwara. Dokta Yusha hakuwa mgeni kuitumia bunduki, hakuwa mgeni wa kutazamana na bastola. Ndio maana bastola aliyooneshwa na Tano haikumtisha kabisa, zaidi ilimuongezea umakini.

Tano yeye alimchukulia Dokta Yusha kama raia wa kawaida, raia ambaye atatetemeka baada ya kuoneshwa bastola, au labda atajikojolea baada ya kuona bastola ikimuelekea usoni mwake.
Lakini haikuwa hivyo kwa Dokta Yusha!

Tano na Dokta Yusha walikaribiana sana, Tano alifanya kosa la kiufundi, alimkaribia sana Dokta Yusha na ukaribu ule ulizua jambo!

Dokta Yusha alirudisha nyuma mguu wake wa kulia, na kuuleta mbele kwa kasi na nguvu kubwa sana!
Mtindo wa kuupeleka mguu namna ile huitwa teke!
Teke lile la Dokta Yusha lilifika ulipokuwa mkono wa Tano ambao ulikuwa umeshika bastola, bastola ilisukumwa kwa kasi na kujisweka pembeni ya barabara. Sasa Dokta Yusha na Tano walibaki mikono mitupu, wakitazamana kama majogoo.

Tano alitabasamu, alifurahi sana na ujanja aliouonesha Dokta Yusha, alimuona kama amejipalia mkaa wa moto, Tano alijiweka vizuri kimapambano!

Dokta Yusha naye hakutetereka, hakutetemeka, alimwangalia jinsi Tano alivyosimama na kupanga ngumi, yeye alikuwa amesimama tu kawaida.
Tano alimfata Dokta Yusha kwa kasi kwa teke lilikuwa linaelekea tumboni kwa Dokta Yusha, kwa kasi ya ajabu Dokta Yusha alijisogeza pembeni kidogo, kukwepa lile teke. Tano akapita kwa kasi na lile teke lake hadi pembeni mwa barabara kwenye nyasi fupi. Tano alisimama tena huku akiwa amefura kwa hasira, kukwepa vile na Dokta Yusha ilikuwa ni dharau kubwa sana kwake, akajipanga tena upya, kwa bahati mbaya alikuwa anaongozwa na hasira. Ni kosa kubwa sana katika mapambano kuongozwa na hasira.

Dokta Yusha alicheka kwa sauti kubwa kwa dharau, alicheka kwa lengo la kuzidi kumtoa Tano wa Six killers mchezoni, na kweli kicheko kile kilipokelewa tofauti kabisa na Tano muuaji, kicheko kiliibadirisha ile hasira ya Tano na kuigeuza kuwa jazba!
Dokta Yusha alifanya vile makusudi, kwa jinsi alivyomuona amesimama Tano na jinsi alivyopanga ngumi, alijua Tano siyo wa kiwango chake. Tano alikuwa mahiri zaidi yake. Sasa alikuwa anatumia mbinu ya kumpandisha hasira Tano ili apoteze umakini, huku yeye akifikiria namna ya kujiokoa na alifanikiwa tena kwa hilo!

Tano alifura kwa hasira na jazba ya hali ya juu. Moyoni mwake kulikuwa kunafukuta!

Alirusha ngumi kwa mkono wake wa kulia, ngumi ya nguvu iliyorushwa na mtu mwenye nguvu, Dokta Yusha alijaribu kuikwepa, lakini hakufanikiwa kuikwepa yote, mkwaruzo wa ngumi ile ulimpata kidogo katika sehemu ndogo ya mbavu ya kushoto, alisikia maumivu kidogo, lakini hakutaka kuonesha kama alisikia maumivu, Tano hakusubiri, ngumi ya kushoto sasa ilikuwa inaelekea katika mwamba wa pua wa Dokta Yusha, kwa kasi na umakini Dokta Yusha alifanya mambo mawili ya kustaajabisha sana…
Dokta Yusha, aliikwepa ile ngumi, huku nae akipiga ngumi yake kwa nguvu iliyotua barabara katika mbavu za Tano!
Tano hakuamini kasi aliyoitumia Dokta Yusha kukwepa ngumi ile, pia hakuamini uzito wa ngumi wa Dokta Yusha, sasa tano akajua anapambana na mtu anayejua anachokifanya. Hakujiuliza tena, sasa aliamua kupiga mapigo ya kifo, mapigo ambayo yakimgusa mpigwaji yanaondoka na roho yake….Balaa!
Tano alianza na teke lilikwenda kwa kasi kama umeme, teke liliombatana na uzito wa kilo kadhaa. Dokta Yusha aliliona teke lile, teke liliolekezwa shingoni kwa lengo ya kuondoka na shingo yake, aliinama kidogo, teke likapita, ila upepo wa teke lile ulimyumbisha Dokta Yusha na kumdondosha chini, akiwa amelala pale chali, tano aliruka juu na kushuka chini huku akiwa amekitanguliza kifuti cha mguu wake wa kushoto, kifuto kilichoelekezwa katika upande wa kushoto wa kifua dokta Yusha, pale unapokaa moyo!
Dokta Yusha alijisogeza kidogo pale chini akiwa amelala vile vile, na kifuti cha dokta Yusha kutua katika lami, nguvu iliyoambatana na kifuti kile, na kutua kwenye lami ngumu, goti la Tano liligeuka palepale!
Tano alitoa ukelele mkubwa sana. Dokta Yusha alisimama na kwenda pale alipolala Tano huku akiwa amelishikia goti lake.
Dokta Yusha alijisachi mfukoni, na kutoa simu yake ya mkononi. Aliitafuta namba ya OCD ya kilwa, na kumpigia. Alimuelekeza kila kitu kilichotokea pale barabarani, na OCD alimwambia kwamba watafika askari pale baada ya muda mfupi.

Tano hakuwa na ujanja wowote, alikaa pake huku akilia, akisubiri hatma yake, mambo yalikuwa yameshaharibika.

Baada ya muda mfupi gari la polisi lilifika, likiwa na askari polisi sita waliovaa sare zao safi za jeshi la Polisi, wakiwa imara na bunduki mkononi kila mmoja. Walimbeba Tano na kumpakia nyuma ya gari ile ya Polisi. Dokta Yusha alipanda mbele ya gari ile, na safari ya kuelekea kituo cha polisi Masoko ilianza.

Dakika kumi zilitosha kuwafikisha askari wale wakiwa na Tano wa Six Killers katika kituo cha Polisi cha Masoko. Askari wawili walimshusha Tano msobemsobe, hawakujari kabisa makelele yake aliyokuwa anayapiga kutokana na maumivu akiyoyapata kutoka na maumivu ya kwenye goti. Kwa bahati mbaya askari wale hawakuwa na huruma kwa Tano, kwa kuwa hawakuwahi kufundishwa kumuonea huruma Mhalifu katika mafunzo huko chuoni Moshi.
Tano aliingizwa ndani ya kituo cha Polisi tayari kwa kuanza kuhojiwa.

Na alivyowekwa tu katika sakafu ya Polisi alikumbana na maswali mfululizo toka kwa askari wale. Kila askari alikuwa anauliza swali lake kwa sauti kubwa na ukali.
Tano alihisi kama wanampigia kelele, hakujibu kitu, alinyamaza kimya!

Dokta Yusha yeye aliitwa ofisini kwa mkuu wa upepelezi Wilaya. Alieleza kila kitu kilichotokea tangu alipopokea ile simu ya Mwanasheria mlevi. Simu iliyomtaarifu juu ya msiba wa Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, nae kuamua kwenda kilwa Masoko kwenye msiba.

Dokta Yusha alivyomaliza maelezo yake tu hapohapo wakatumwa askari kwenda kumkamata Mwanasheria. Mkuu wa upelelezi wa wilaya alihisi Mwanasheria mlevi anahusika na mbinu zile chafu!
Askari walewale waliomleta Tano waliingia tena kazini kumtafuta Mwanasheria mlevi popote alipo

Mwanasheria bado alikuwa kilabuni, hana hili wala lile. Alikuwa anakunywa pombe huku akiongea neno kila linalomjia kichwani mwake. Bila kujua kama askari sita wenye silaha walikuwa njiani wanaelekea pale kilabuni kumkamata yeye, akituhumiwa kupanga mauaji ya Dokta Yusha! Ghafla! Vumbi lilitimka pale kilabuni, gari ya Polisi lilifunga breki kali sana! Askari walikuwa wameshuka kabla hata ya breki ile. Walishuka kwa mbwembwe na bunduki zao mikononi. Walevi walitimka mbio, pombe zote ziliwatoka vichwani. Mwanasheria mlevi hakusogea hata hatua moja, alikuwa ameshazungukwa na askari polisi watatu. Midomo ya bunduki ikielekezwa kichwani kwake! Mwanasheria hakuwa jasiri kama Dokta Yusha, yeye alikuwa anatetemeka, hakuweza kuuzuia kabisa mkojo usimtoke. Kuelekezwa bunduki kichwani kwake ? Alikosa la kusema, askari walimuamuru asimame, na kumuelekeza pa kuelekea, ndani ya gari ya Polisi. Alifika ndani ya gari, na kukaa chini bila kuambiwa..machozi yalimtoka na kudondoka katika sakafu ya bodi ya gari ile. Askari hawakulijari lile chozi, hawakuwa na muda wa kulijari chozi la Mhalifu, walidandia gari na kuondoka kwa kasi kubwa sana, safari kituo cha Polisi Masoko. Laiti wangemjua Mwanasheria mlevi… Walipofika kituo cha Polisi, Polisi hawakuuliza, ilikuwa ni mateke, ngumi na vifuti kwa Mwanasheria mlevi. Polisi walikuwa wanampiga Mwanasheria bila kujua kwanini wanampiga, na Mwanasheria nae hakujua kwanini anapigwa! Mwanasheria alipoteza fahamu kituo cha Polisi. Wote wawili Tano na Mwanasheria walipelekwa kituo cha afya Masoko, chini ya ulinzi mkali sana wa askari Polisi. Kama ilivyo kawaida katika hospitali nyingi Tanzania, wahalifu huwa hawapati huduma nzuri pindi wanapoumwa. Labda kwa kuwa wanakuwa hawana wauguzi wa kuwapa pesa wagonjwa( hongo). Hali hiyo iliwakuta Tano na Mwanasheria pale kituo cha afya Masoko. Waliachwa wamelala katika vitanda vyao wakiwa na pingu zao mikononi. Saa kumi na mbili jioni, Mwanasheria alizinduka, ni kudra za Mungu tu ndizo zilimuasha. Mwanasheria hakupata huduma yoyote ile pale kituo cha afya. Mwanasheria aliamka na maneno yake, Mwanasheria aliamka na lawama za kutosha, lawama kwa Polisi, lawama kwa Serikali, lawama kwa mfumo mzima wa nchi, lakini lawama hazikusaidia, ukweli ulibaki palepale, Mwanasheria alikuwa amelala kitandani akiwa hoi bin taaban na pingu zake kitandani ! Tano wa Six killers naye alikuwa katika wakati mgumu sana, mguu wake ulikuwa umeumia vibaya sana, alikuwa anagugumia kwa maumivu. Lakini hakuwa na jinsi, alikuwa amelala katika kitanda kidogo cha kituo cha afya akiwa dhooful hali, huku akiwa hana namna ya kuwapigia wenzie ili awataarifu kwamba alikuwa mahali pale, kwa kuwa simu yake ilikuwa katika kituo cha Polisi.
Kundi la Six Killers walikutana kwa kikao cha dharura. Kikao kilichokuwa kinaongozwa na Don Genge mwenyewe, kikiwa na ajenda kuu mbili. Ajenda ya kwanza ilikuwa ni makabidhiano ya mioyo kumi na tano iliyopatikana kwa siku ile ya pili. Mambo yalienda sawa, na Dokta Sharifa alikabidhi deli kubwa jekundu lenye mioyo kumi na tano. Ajenda ya pili, ilikuwa inahusu kutoonekana kwa Tano. Masaa zaidi ya sita, Tano alikuwa hajaonekana, na simu yake ilikuwa haipatikani! “Hii ni siku ya tatu ya Mpango huu, kwa asilimia 90 mpango wetu umeenda sawa, lakini Kwa bahati mbaya sisi hatufanyi kazi kwa asilimia 90. Huwa tunafanya kazi kwa asilimia 100, au zaidi ya hizo ikiwezekana. Tano hajulikani alipo, na hizo ndio asilimia 10 tulizozipoteza. Natoa masaa mawili, Tano akiwa hai au amekufa mwili wake uwe hapa!. Baada ya masaa hayo mawili, tutaenda kutoa mioyo tukiwa na Tano kama atabahatika kuwa hai, mmebaki wa tano, hakikisheni mnarudi na Tano! Mnaweza kwenda…” Six killers walitoka mle ndani kwa lengo kuu moja, kwenda kumtafuta muuaji aliyepewa namba Tano.

Mbili alitoka nje, na kukutana na Sita. Walijipanga vizuri kwenda kumtoa Tano katikati ya maaskari wawili wenye bunduki!

Askari hawakuwa kizuizi kabisa kwa Mbili, bunduki hazikuwa tishio kabisa kwa Mbili. Alipewa namba mbili katika kundi la Six killer’s kwa kuwa alikuwa mahiri kuliko wanakikundi wanne waliobakia. Wakiwa na Sita, walijiandaa kwa uvamizi.

Kule ndani Mwanasheria alikuwa anaendelea kuongea kama ilivyo ada yake. Askari Polisi walijaribu kumnyamazisha bila mafanikio yoyote. Kilabu sasa kilihamia katika kituo cha afya. Makelele yale yale ya Mwanasheria yalichangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umakini kwa askari wale wawili. Wote walikuwa wanajitahidi kumnyamazisha Mwanasheria na kusahau kabisa suala la ulinzi.

Mbili na Sita walikuwa nje ya wodi ile. Walisikia kila kitu kilichokuwa kinaendelea kule ndani. Walijipanga vizuri.

Moja, mbili taaaaa…..wote kwa pamoja waliukumba ule mlango wa wodi kwa kutumia miili yao ya kimazoezi na wote kujikuta wako ndani. Kila mmoja kwa namna yake na bastola zao mkononi.

E bwana weee!

Mbili alijiviringisha kwa mtindo wa sarakasi na kujificha nyuma ya kitanda alicholala Tano huku akibonyea kidogo ili kile kitanda kimfiche, Sita nae alijiviringisha kwa kasi na kumfikia moja kwa moja askari mmoja na kumkaba shingoni, huku akimtumia kama ngao!
Huku bastola yake ikimtazama yule askari mwengine. Askari wote wawili waliwahiwa vizuri sana. Yule askari aliyepigwa kabali ilinasa kisawasawa, alijaribu kujitoa bila kutegemea, huku yule askari mwengine aliyeoneshwa bastola hakuwa na lolote la kufanya, alibaki ameganda kama sanamu. Six Killers walihamishia balaa wodini.

Ghafla! Yule askari aliyesimama alijishika kifuani, kulikuwa na majimaji mekundu, damu! Bastola ya Mbili yenye kiwambo cha kuzuia sauti ilikuwa imefanya kazi iliyotumwa. Yule askari aliyesimama alikuwa amepigwa risasi takatifu ya kifua. Aliyumba kidogo huku akipiga kelele, na kudondoka chini mzimamzima kisogo kikitangulia kufika chini !
Askari alikuwa mfu zamani sana kabla hata hajaigusa sakafu ya hospitali.

Sita naye aliongeza nguvu katika ile kabari, yule askari alikosa pumzi, nguvu zikamuishia, alilegea. Sita alimuachia yule askari, akadondoka chini. Vitendo vyote vilivyokuwa vinatokea Mwanasheria mlevi na Tano walikuwa wanashuhudia kila kitu, kimyakimya.

Wakati Tano akiufurahia ujio wa watu wale wawili aliokuwa anawafahamu vizuri sana, Mwanasheria mlevi alikuwa katika mshangao mkuu, hakutegemea wala kuelewa kinachotokea mle ndani wodini.

Mbili na Sita walikisogelea kitanda alicholala Tano. Waliliangalia lile jeraha kubwa la Tano pale mguuni, wote walimuonea huruma. Walimbeba na kutokomea nae kusikojulikana!

Baada ya robo saa kutokea kwa tukio lile, mganga wa kituo cha afya Masoko aliingia katika wodi ile.
Mganga alikutana na Balaa !
Miili ya askari wawili ilikuwa imelala chini, ikiwa haina uhai. Na mwili wa mgonjwa mmoja ukiwa haupo huku mwili wa Mwanasheria mlevi ukiwa juu ya kitanda, ukiwa umeloa jasho, hakika Mwanasheria aliyaona matukio ambayo hakutegemea kuyaona katika maisha yake. Alikuwa anatetemeka huku anatoa jasho!

Daktari hakuamini kabisa madhara yaliyotokea mle wodini. Alijishika kichwa huku akipiga kelele za kuomba msaada. Ndani ya dakika chache manesi na baadhi ya watu waliokuja pale hospitali walijaa katika wodi ile. Kila mmoja alistaajabu kilichotokea mle ndani, ilikuwa ni balaa !
Nesi mmoja alipiga simu kituo cha Polisi kuwataarifu juu ya mauaji yale. Askari waliwasili baada ya muda mfupi sana, na kushuhudia unyama mkubwa waliofanyiwa askari wenzao. Huku Mwanasheria mlevi akiwa ni shuhuda pekee aliyeshuhudia kila kitu. Nusu saa baadae, kundi hatari la Six Killers walikutana tena na bosi wao. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwao, kuitekeleza kazi ile ya masaa mawili kwa nusu saa tu. “Hongereni sana vijana wangu, mmefanya kazi kwa haraka sana, ila sina uhakika kama mmeifanya kwa umakini ninaouhitaji” Don Genge alikuwa anaongea huku akiwaangalia Mbili na Sita usoni. “Hakika tumefanya kazi kwa umakini mkubwa mno Bosi” Mbili alijibu kwa kujiamini. “Mmeua watu wote waliowashuhudia? Kuanzia huyo askari aliyekupeni siri mahali alipo Tano, Mganga mkuu pamoja na huyo mgonjwa aliyelazwa pamoja na Tano?” Mbili na Sita waliangaliana usoni, waligundua kuwa walikuwa wamefanya kosa! “Tumefanya kosa, dakika kumi” Mbili alijibu kibabe. “Naongeza kumi na tano” “Sawa mkuu” Waliondoka. Walikuwa wamepewa dakika kumi na tano kuhakikisha yule askari aliyewapa siri, Mganga mkuu na Mwanasheria mlevi wanauwawa! Kundi zima sasa kasoro Tano tu walinyanyuka na kuingia tena kazini. Dakika kumi baadae kundi zima la Six Killers lilikuwa limerejea tena. Wakiwa wamefanikisha kuwauwa watu wawili kati ya wale watatu. Askari na mganga mkuu walikuwa wameelekea kuzimu kwa mtindo tofauti, wakati yule askari aliuwawa kwa bastola nyumbani kwake, Mganga mkuu wa hospitali aliuwawa kwa kisu ofisini kwake. Wote wakiwa hawajawahi kutumia hata senti tano katika zile laki moja walizokuwa wamepewa. Tatizo lilikuwa kwa Mwanasheria mlevi, walienda mle wodini hawakumkuta yule mgonjwa, na kwa bahati mbaya hawakuwa wameishika kabisa sura yake. Lilikuwa kosa la kubwa sana walilolifanya wauaji wale wazoefu. Askari Polisi sasa walikuwa wanamlinda Mwanasheria mlevi kupita kiasi. Jeshi la Polisi hawakuwa wanajua kabisa kama kuna watumishi walihusika katika kutoa siri, na kupokea hongo kutoka kundi la Six Killers. Nusu saa baadae taarifa mbaya zikalifikia jeshi la Polisi. Taarifa mbaya za vifo ! Kifo cha Sajenti Alex Omolo wa kituo cha Polisi Masoko, na kifo cha daktari Mosha Gabriel, Mganga mkuu wa kituo cha afya Masoko. Askari walitapakaa mtaani kuwasaka watu waliowauwa Afande Alex Omolo na Dokta Mosha Gabriel. Askari walifanya msako kimyakimya. Lakini ilikuwa kama wanawatafuta watu ambao hawakuwahi kuwepo duniani. Msako wao haukuwasogeza kabisa karibu ya Muuaji! Wakati askari wakimwagika kama njugu huko Kilwa Masoko kuwatafuta watu waliowauwa Afande Alex na Dokta Mosha, Kundi hatari la Six Killers walikuwa wapo njiani kwenye gari wakielekea hospitali ya wilaya Kilwa Kivinje huku wakilaumiwa vibaya mno na Don Genge kushindwa kumuua mgonjwa aliyewashuhudia wakati wanafanya mauaji. Ilikuwa ni lawama nyingi sana, kundi zima walikuwa kimya wakati Don Genge akifoka! “Six killers huwa hatufanyi makosa. Kosa lolote inamaanisha kujiweka katika hali ya hatari, na mipango yetu kukwama. Ona sasa, yule Dokta mpumbavu bado anaishi, yule mgonjwa mpumbavu bado anaishi. Ni makosa haya, Dokta mpumbavu anamfahamu Tano, Mgonjwa mpumbavu anawajua Mbili na Sita. Ni makosa makubwa sana, lazima wafe!” Kundi la Six Killers walimwacha Tano katika nyumba yao iliyokuwa kama kambi ya muda mfupi huko Ngome, akipatiwa matibabu na daktari waliyemkodi. Wao walikuwa wanaenda Kilwa Kivinje kufanya kazi yao hatari! Ya kutoa mioyo ya wagonjwa kumi na tano kama ilivyo ada.

Ingawa askari Polisi walimtaka Dokta Yusha akae pale kituo cha Polisi kwa usalama wake. Lakini Dokta Yusha hakukubali kabisa, Dokta Yusha alipinga katakata. Alikuwa anataka kutoka ili akamzike rafiki yake Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa, pia alikuwa anataka arudi hospitali Kilwa Kivinje kuwaona wagonjwa wake. Polisi hawakuwa na jinsi, walimruhusu Dokta Yusha atoke pale kituo cha Polisi. Katika mtaa wa National, katika nyumba aliyokuwa anaishi Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kulikuwa na umati wa watu mkubwa sana. Watu wengi wakilia kwa uchungu mkubwa mno, msiba huu ulikuwa msiba mkubwa sana ndani ya Kilwa Masoko. Alivyotoka kituo cha Polisi, Dokta Yusha alienda moja kwa moja msibani. Alishiriki vizuri kwenye shughuli za mazishi. Hadi Mwanasheria alivyopumzishwa katika makazi yake ya milele katika makaburi ya Sanga. Baada ya mazishi, Dokta Yusha alielekea hospitali Kilwa Kivinje ambako kundi la Six killers Don Genge nao walielekea huko. Huko wakiwa na mikakati ya kumuua yeye na Mwanasheria mlevi. Kundi la Six killers walikuwa wamejipanga vizuri sana huko Kilwa Kivinje. Kutokana na kutokuwepo kwa Tano, ratiba zao zilibadirika kidogo. Kazi ya kumuwinda Dokta Yusha sasa alipewa Sita. Huku waliobaki walikuwa wanalinda eneo la chumba cha kuhifadhia maiti ili operesheni yao ya kutoa mioyo iliyotarajia kufanyika usiku wa siku hiyo iende vizuri. Kwa bahati nzuri siku hiyo ilitokea ajari ya basi katika kijiji cha Somanga. Ajari ilioua watu thelathini na kujeruhi saba, Six killers walikuwa na uhakika wa kupata mioyo thelathini ambayo, mara mbili ya oda yao, bahati ilioje? Saa moja usiku Dokta Yusha alikuwa anaelekea Kilwa Kivinje. Kwenda kuwaangalia watu aliowapenda sana. Ambao sasa walikuwa wagonjwa, Mkewe kipenzi Nasra, rafiki wa mkewe, Hasina na mkwe wake. Njiani roho ilikuwa inamdunda sana, bila kujua kwanini hali ile ilimtokea. Laiti Dokta Yusha angejua anayoenda kukutana nayo huko basi angeusikiliza moyo wake, Dokta Yusha alikuwa anaenda kwenye balaa kubwa sana! Na moyo wake uliligundua hilo mapema sana. Lakini hakuusiliza moyo wake, au labda hakuuelewa moyo wake unamaanisha nini? Nusu saa ilitosha kumfikisha Dokta Yusha Kilwa Kivinje. Na moja kwa moja alienda katika wodi waliolazwa wakina Nasra. Hali ya wagonjwa wale wawili ilikuwa vilevile. Mkewe kipenzi Nasra na rafiki wa mkewe Hasina walikuwa wamelala katika usingizi ule mbaya, usingizi nzito usiojulikana mwisho wake. Huku Mzee Mpaukha naye akiwa kalala kwa kujifunika nusu shuka safi ya hospitali, shuka iliiyoiashia kifuani, uso ukiwa wazi. Dereva alikuwa amejifunika shuka la hospitali gubigubi sawa na mgonjwa mwengine aliyelala kitanda cha pili toka pale alikolala dereva. Kumbe jirani yule alikuwa ni Sita wa Six killers, akiwa amejificha kwa kujifunika gubigubi katika kitanda kimoja katika wodi ile. akiwa amepania kummaliza Dokta Yusha kabla hajaenda katika jukumu lake lengine la usiku ule. Dokta Yusha kama kawaida yake alienda kwenye kitanda alicholala mkewe kipenzi, Nasra, alimwangalia kwa muda mkewe, bado alikuwa katika hali ya kutia shaka. Alipiga hatua chache na kukisogelea kitanda cha Hasina, nae alikuwa taabani kwa ajari ile. Alisogea tena hadi kitanda alicholazwa Mzee Mpaukha, Mzee Mpaukha alikuwa amelala, hakutaka kumsumbua, alimshuhudia akipumua vizuri. Alikiangalia kitanda alicholazwa dereva wa Mzee Mpaukha, alimwona amejifunika gubigubi. Alikisogelea taratibu kile kitanda, alikuwa anasogea Huku akiiona kuwa kitanda cha pili kutoka kitanda cha dereva Musa nacho kulikuwa na mgonjwa aliyejifunika gubigubi kama Musa, alipanga kwenda kumwangalia nae, bila kujua dhamira mbaya ya mgonjwa aliyelala kitanda kile. Kitanda kililaliwa na Sita wa Six killers. Na lengo lake kuu ni kumuuangamiza Dokta Yusha. Dokta Yusha alifika kitanda alicholazwa dereva Musa. Aliifunua lile shuka na kumwangalia Musa usoni. Alistuka sana! Alikuwa daktari, na hakuhitaji kifaa chochote kile kutumia ili kumpima dereva Musa, macho ya kidaktari yalitosha kumwambia kwamba alikuwa anatazamana na mtu ambaye ameshafariki ! Nguvu zilimuisha Dokta Yusha. Kwa hali aliyomuacha nayo dereva Musa, haikumuingia akilini hata kidogo kama Musa angefariki, moja kwa moja alijua kwamba ameuliwa! Kwa jinsi hali aliyoiacha, angeamini kama mkewe Nasra ama Hasina wangekuwa wamefariki, maana ndio ambao walikuwa katika hali ngumu, lakini siyo dereva Musa. Dokta Yusha Alijua kwa vyovyote vile kuna mchezo mbaya ulikuwa unaendelea mle wodini. Kwa mwendo wake uleule wa taratibu alikuwa anakisogelea kile kitanda alicholazwa mgonjwa mwengine, ambaye nae alijifunika gubigubi, au pengine alifunikwa gubigubi baada ya kuuwawa kama dereva Musa. Bila kujua kitanda alichokuwa anakisogelea ndio kitanda alicholala Sita. Muuaji hatari toka kundi la Six killers, ambaye ndiye alimuua dereva Musa kwa kumnyonga shingo muda mfupi uliopita. Dokta Yusha alikifia kile kitanda ambacho alilala mtu hatari sana. Aliishika ile ncha ya shuka taratibu na kuanza kumfunua yule mgonjwa. Hamadi! Dokta Yusha alikuwa anatazamana na mdomo wa bastola. Moyo wa Dokta Yusha ulipiga kwa kasi sana. Kilikuwa ni kitendo cha ghafla ambacho hakukitegemea kabisa. Sita wa Six killers alinyanyuka pale kitandani na kukaa kitako. “Hongera sana Dokta Yusha, uko vizuri sana, tumeona ulichomfanyia Tano,

hongera Dokta Yusha” Sita alikuwa anaongea huku akiipangusa vumbi bastola yake kwa kutumia shuka la hospitali. “Mwisho wako umefika Dokta Yusha, nakuuwa! Ndio nitakuuwa baada ya mateso kidogo lakini” Sita aliongea kwa kujiamini sana. Dokta Yusha aliamua kutulia, alijua kuwa na wasiwasi hakutomsaidia, aliamua kuwa makini ili ajue anatoka vipi katika kisanga kile kipya. “Unaona wagonjwa wako wote wamelala, sipendi tuwasumbue, tutoke humu ndani kimyakimya nikakusulubu huko nje, sitaki niwamalize hawa kwa ujinga wako” Sita alimtahadharisha Dokta Yusha. Dokta Yusha hakuwa na jinsi, aliongoza mwenyewe mlangoni, huku akifuatwa na Sita wa Six killers na bastola yake. Wakiwa wameongozana walifika nje, Dokta Yusha alisimama akisubiri maelekezo toka kwa Sita. “Elekea chumba cha kuhifadhia maiti” Sita alitoa maelekezo kwa sauti ya chini. Bila kujishauri Dokta Yusha alielekea katika chumba cha kuhifadhia maiti, huku akifuatwa nyuma na Sita. Dokta Yusha hakuwa anajua balaa alilokuwa anaenda kulishuhudia katika chumba cha kuhifadhia maiti. Waulikuta mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti upo wazi. Waliingia ndani. Hali aliyoikuta Dokta Yusha mle ndani ilimstua sana! Aliona maiti zimelazwa bila mpangilio mle ndani, tena sakafuni. Maiti zenye majeraha ya kutisha sana, ambayo ni ngumu kutazamwa na macho ya kawaida. Aliangalia watu aliowakuta mle ndani, wote wakiwa makini na shughuli zao za kinyama, walikuwa hawamwangalii kabisa yeye. Macho ya Dokta Yusha yalitua kwa Dokta Sharifa, daktari wa kike alikuwa makini bila wasiwasi wowote, akiishughulikia maiti iliyolazwa juu ya meza mbele yake.

Macho ya Dokta Yusha yalitua kwa Dokta Sharifa, daktari wa kike alikuwa makini bila wasiwasi wowote, akiishughulikia maiti iliyolazwa juu ya meza mbele yake. Dokta Yusha aliitazama kwa makini ile maiti akitaka kujua Dokta Sharifa alikuwa anaifanyia kitu gani. Bila wasiwasi wowote Dokta Sharifa alichomeka kisu kwa nguvu kidogo kifuani kwa yule maiti aliyekuwa amelazwa katika kitanda kilichokuwa mbele yake. Mwili wa Dokta Yusha ulimsisimka kwa hofu na woga, alifumba macho ili asiushuhudie unyama ule. Alipofumbua macho aliona moyo wa yule maiti ukiwa mkononi mwa Dokta Sharifa ! E bwana eee! Nesi mmoja alienda pale kwenye meza iliyolazwa maiti akiwa na deli jekundu, ule moyo ukawekwa humo. Na Dokta Sharifa alianza kuushona ule mwili. Dokta Yusha sasa alikumbuka, alikumbuka kuhusu kile kidonda alichokutwa nacho mama Mpaukha kifuani. Kumbe mama Mpaukha alifanyiwa mchezo huu mbaya, mama Mpaukha naye alitolewa Moyo! Hasira zilimpanda Dokta Yusha, mishipa ya kichwa ilimsimama huku machozi yalikuwa yanamtiririka bila kupenda. Alitamani awauwe watu wote waliokuwemo mle ndani, lakini hakuweza, atawauwa vipi ilhali yeye ndiye aliyekuwa katika hatari zaidi ya kuuwawa! Chozi la Dokta Yusha lilimsha shangwe mle ndani. Watu wote walikuwa wanamcheka Dokta Yusha alivyokuwa analia. Dokta Yusha alijiona kama yupo katikati ya mashetani wenye roho mbaya. Alipangusa machozi kwa kutumia kiganja chake cha mkono wa kushoto. Aliwaona manesi wawili wakichagua maiti nyingine pale chini, ilikuwa mithili ya wanunuzi wakichagua nguo katika soko la Tandika. Wakaipata maiti wakiyoitaka. Wakaibeba na kuipeleka kwenye ile meza iliyokuwa mbele ya Dokta Sharifa. Dokta Sharifa aliendelea na kazi yake huku akitabasamu. Kwa mara nyingine tena, daktari katili wa kike Sharifa Juma alichomeka kile kisu chake kifuani mwa ile maiti mwengine. Aliifanyia kama alivyoifanyia ile maiti ya awali. Safari hii Dokta Yusha alithubutu kuangalia, aliangalia kila hatua ya kikatili iliyofanywa na mabaradhuli wale. Alibaki anatikisa kichwa tu kwa masikitiko. Hakutegemea kabisa kama kitendo kile cha kikatili kinafanywa na daktari wa kike anayeheshimika zaidi wilayani Kilwa, Dokta Sharifa. Ama hakika hali ilikuwa ya kusikitisha sana. Dokta Yusha aliangalia upande wake wa kulia, alimwona Dokta Zaidi Kilumba akiwa ametulia tuli kitini. Akitabasamu huku akimwangalia Dokta Yusha kwa dharau. “Una dhamana kubwa sana Dokta Kilumba, umeaminiwa na Taifa kuiongoza hospitali hii, kuwahudumia wananchi maskini, tena wagonjwa. Kinachofanyika hapa siyo haki Dokta Kilumba. Ndio! Hii siyo haki kabisa Dokta, kwanini unafanya hivi vitu ? Kumbuka maadili ya kazi ya udaktari, Kumbuka kiapo ulichoapa Dokta, kinafanana na kinachofanyika hapa Dokta?” Dokta Yusha alisema kwa hisia na uchungu mkubwa sana. “Hahaha eti maadili ya kazi, hahaha eti kiapo cha udaktari, kiapo cha udaktari nd’o nini, kwa taarifa yako hii kazi tumelipwa hela nyingi sana! Tofauti na hizo zinazowafanya madaktari wagome kila siku. Unazungumzia maadili ya kazi, hivi kuna maadili mbele ya pesa?” Dokta Kilumba alikuwa anaongea akiwa amekaa palepale katika kiti, anaongea bila wasiwasi wowote. “Mtalipa Dokta kwa huu unyama mnaofanya hapa, naapa mtalipa!. Hata mkiniua mimi kizazi kijacho kitakuja kulipa damu za watu hawa wasio na hatia!” Dokta Yusha munkari ulianza kumpanda. “Tulipe damu gani Dokta Yusha wakati hawa wameshakufa, hizi ni maiti Dokta?” “Usibishane nae, yeye tunamtoa moyo leo akiwa anajiona. Ili tulipe vizuri hizo damu anaozisema huko mbinguni kama kupo!” “Mletee hapa!” Sita akamshika mkono na kumvuta. Kumpeleka pale alipo Dokta Kilumba. Alipofikishwa pale ndipo Dokta Yusha alimuona mtu mwengine kabisa, ambaye hakuwa amemuona pindi alipoingizwa mle ndani. Na hakuwa amemuona kabisa katika maisha yake. Mzee mwenye sura ya kikorofi, alikuwa na sharubu mithili ya Karl Peter’s ‘mkono wa damu’. Mzee mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, mrefu sana, kwa majina alikuwa anaitwa Don Genge. Dokta Yusha alidhani ile sauti ya kuitwa imetoka kwa Dokta Kilumba, la hasha. Haikuwa hivyo, kumbe alikuwa ni jasusi Don Genge mwenyewe. “Hahaha hiki ndio kifaranga kinachowasumbua?” Don Genge aliuliza kwa kejeli huku akiubinua kwa juu mdomo wake mpana. “Ama kweli maajabu hayana mwisho duniani. Wewe ndio umemvunja goti komando Tano? Kwa nguvu gani ulizonazo mpumbavu wewe, kwa akili gani ulizonazo mjinga wewe? Don Genge alikuwa anauliza maswali bila ya kusubiri majibu toka kwa Dokta Yusha. Kamtie kwenye gari tuondoke nae kambini tukaone uwezo wake mpaka Komando Tano ashindwe kumkamata na kuambulia kuvunjwa goti.” Kwa haraka Sita alimsukasuka Dokta Yusha na kumpeleka kwenye gari. Gari aliloingizwa dokta Yusha ni yale magari yenye bodi zenye visanduku nyuma. Mara nyingi hutumika katika mahospitali kusafirishia dawa. Kundi la Six killers nao walikuwa wanautumia gari aina hiyo kusafirishia mioyo. Na leo hii gari hiyohiyo ilitumika kama mahabusu inayotembea kwa Dokta Yusha. Ndani ya kile kisanduku kulikuwa na giza totoro, pia kulikuwa na joto sana, maana hakukuwa na uwazi wa kupitisha mwanga wowote katika kisanduku hiko. Kilikuwa kisanduku kidogo sana kilichompa shida sana Dokta Yusha. Ilimbidi ajikunje sana ili akae vizuri mle ndani ya gari. Hakukaa vizuri lakini alikaa. Baada ya nusu saa alisikia kelele za miguu ya watu ikielekea pale kwenye gari aliyokuwa ndani yake. Mara alisikia mlango wa ile bodi ukifunguliwa. Ulifunguka. Yule jamaa aliyetambulika kwa jina la komando Sita aliingia na kuweka deli, deli la kuhifadhia mioyo ya maiti. Baada ya kuweka lile deli jekundu yule jamaa alitoka nje. Kile kisanduku kikafungwa tena. Giza likarejea kwa kasi! Akiwa kule nyuma ya gari alisikia gari likiwashwa. Na safari ya kuelekea kusikojulikana ilianza. Gari lilitembea sana, takribani saa sita lilikuwa halijafika lilikokuwa linaenda. Dokta Yusha aliamini safari ile ilikuwa ni nje ya wilaya ya kilwa, au nje ya mkoa kabisa. Maana hakukuwa na sehemu ndani ya kilwa ya kutembea saa nyingi namna

ile. Sasa alianza kulizoea giza, na kuyaona vizuri mandhari ya kule nyuma kwenye kisanduku. Kwenye sakafu ya gari ile, aliyaona madeli matatu yakiwa yamewekwa pamoja. Hakujua ni madeli ya nini, ingawa alihisi yatakuwa ya mioyo. Dokta Yusha hakutamani hata kuhangaika kuyafungua. Aliangazaangaza mle ndani ya gari, hakuona kitu kingine zaidi ya yale madeli mekundu. Mara gari lilisimama, ishara kuwa lilikuwa limefika ilikokuwa inaelekea. Saa zaidi ya nane walizitumia barabarani. Ilichukua kama robo saa ndipo akaja kufunguliwa kule nyuma. Dokta Yusha akaona tena mwanga halisi wa dunia. Alishuka mwenyewe bila kuambiwa. Alikuwa amechoka sana kukaa mle ndani ya kisanduku. Joto kali ndani ya kisanduku na kukosa hewa kulimuadhibu barabara Dokta Yusha. Alishuka chini, alikutana na nyumba ndogo ya kisasa. Nyumba iliyonakshiwa kwa rangi ya bluu. Huku chini kukiwa na michirizi ya rangi nyeusi. Juu iliezekwa na bati za vigae toka Afrika ya Kusini. Nyumba hiyo ilikuwa imezungukwa na ukuta mkubwa sana wenye rangi ya bluu pia. Ulikuwa ukuta mrefu ulioipita hadi nyumba yenyewe. Yaani kama mtu akiwa kwa nje ataishia kuuona ukuta tu. Hatuiona nyumba ile. Dokta Yusha aliingalia kwa makini nyumba ile huku akiangalia mandhari ya sehemu ile. Alikiri kuwa hakuwahi kufika hata siku moja mahali pale. Hakujua kabisa nyumba ile ilikuwa mahali gani ndani ya nchi ya Tanzania?

Sita wa Six killers alimshika mkono Dokta Yusha na kuizunguka nyumba ile kuelekea nyuma kwa kupitia mkono wa kushoto. Walipofika uwani Dokta Yusha macho yake yalitazamana na kibanda kidogo mithili ya stoo. Sita alifungua kile kibanda kwa funguo na kumsukumia Dokta Yusha mle ndani.

Kilikuwa ni kibanda kidogo kwa nje, na ndani pia. Dokta Yusha alisimama hatua kama mbili toka katika mlango wa kile chumba na kuanza kukiangalia. Kilikuwa ni chumba ambacho hakukuwa na kitu chochote zaidi ya kiti kimoja tu cha chuma. Kuta yake ilipakwa rangi nyekundu ambayo ilikuwa inaumiza macho ukiitazama muda mrefu.
Dokta Yusha alipiga hatua za taratibu kuelekea katika kile kiti. Alikuwa na lengo la kwenda kukikalia kiti kile. Maana hakukuwa na sehemu nyingine ya kukaa zaidi ya kwenye kile kiti. Alikikaribia kabisa kile kiti, alitaka kukaa lakini aligairi. Alikitilia mashaka kile kiti. Kwanini kile kiti cha bati kiwekwe katika chumba kile, ni kweli kimewekwa kwa lengo la kukalia tu? Au kuna lengo lengine, siku zote wasiwasi akili. Dokta Yusha hakukaa, alirudi kinyumenyume hadi ukutani. Akakaa chini taratibu huku akikiangalia kwa makini kile kiti cha chuma.

Dokta Yusha alikaa pale chini sakafuni huku akitafakari mustakabari wa maisha yake. Aliona mambo yamebadirika kwa kasi sana, tena yakianzia siku ya sherehe ya ndoa yake.
Aliwakumbuka wagonjwa aliowaacha hospitali. Mkewe kipenzi Nasra, rafiki wa mkewe, Hasina na mzee Mpaukha, alijua watakuwa katika hali ngumu sana kwa kutokuwepo yeye, pia alijua jinsi walivyoikaribia hatari ya kutolewa mioyo na wale mabaradhuli. Alimfikiria dereva wa Mzee Mpaukha, Musa akijua kwa vyovyote kwa sasa atakuwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, akisubiri kutolewa moyo .
“Kwanini moyo? Itakuwa wanafanyia nini hiyo mioyo? Tena bila shaka mioyo ya maiti ndiyo inayohitajika ndio maana wameweka kambi hospitali tena katika chumba cha kuhifadhia maiti. Lazima nijue undani wa sakata lile, na Lazima nihakikishe watu hawa wenye nia mbaya wanafikishwa katika vyombo vya sheria” Dokta Yusha aliwaza hayo bila ya kujua yupo sehemu hatari kiasi gani, bila kujua atatoka vipi ili akawafikishe katika vyombo vya sheria ilihal alikuwa tunduni akisubiri adhabu yake, bila shaka adhabu ya kifo!

Wakati akiwaza hayo alisikia mlango ukifunguliwa kwa nje. Ukafunguka kidogo na mtu mpya alisukumwa kwa nguvu kuingizwa mle ndani. Dokta Yusha alimwangalia vizuri mtu yule walitambuana.

“Wamekuleta huku Dokta”
“Nawe wamekuleta huku”

Ilikuwa ni kushangaana tu. Mtu yule alikuwa ni mmoja wa askari wa kituo cha Polisi Masoko. Tena ndiye askari aliyemhoji dokta Yusha alipoenda Polisi …..

“Eeh imekuwaje ukafika huku” Dokta Yusha aliuliza kwa wahka mkubwa.
Huku akiwa amesimama yule askari alianza kuelezea.
“Ulivyoomba kutoka pale Polisi ili kwenda kwenye mazishi ya Mwanasheria tulikukubalia, lakini ulivyotoka tu tulikubaliana tukufuate kwa nyuma, na ni mimi ndiye niliyepewa jukumu hilo. Nilikufuata kwa nyuma kila ulikoenda. Mpaka wanakuingiza kwenye gari mimi nilikuwa nashuhudia. Lakini nikiwa nimejibanza nyuma ya wodi moja nikisubiri muda muafaka wa kuja kukuokoa, nikiwa pale nyuma ya wodi nilipojificha nilistukia nimepigwa na kitu kizito kisogoni. Toka hapo sikujua nini kiliendelea. Nimeamka toka ndani ya gari dakika kama sita zilizopita na wakanileta moja kwa moja humu”
“Hivi tuko wapi hapa Afande?”
“Hata sifahamu, maana nilizimia kabisa, nimezinduka nimejikuta nipo humu”
“Itakuwa tuko mbali sana Afande, saa nane tumetumia mpaka kufika hapa”
“Saa nane?”
“Ndio, Afande”
“Mh itakuwa wametuleta wapi washenzi hawa” Yule askari alikuwa anaongea huku anapiga hatua kuelekea kukaa katika kile kiti pekee cha chuma mle ndani. Alikikaribia kile kiti na kusema.

“Sijui watakuwa wana mpango gani hawa wanaharamu”
“Nooooo afande usikae hapooooo!” Dokta Yusha alipiga kelele kali kumuonya yule askari asikalie kile kiti chuma, lakini alikuwa amechelewa sana.

Jamaa alikaa kwenye kiti kilichotokea………..Dokta Yusha alifumba macho!
Kiti kilibadirika rangi na kuwa chekundu sana, askari hakutoa hata ukelele mdogo, rangi nyekundu ya kiti ilienda sambamba na rangi ya askari yule. Kumbe kiti kile kilikuwa na shoti ajabu ya umeme!
Dokta Yusha alithubutu kufumbua macho, macho yalimtoka pima! hakutegemea kabisa kitendo kile. Ingawa alikuwa anahisi kiti kile sio kizuri tangu alivyoingia katika chumba kile, lakini hakudhani wala kufikiria kwamba kina madhara namna ile. Yule askari alianza kubadirika rangi tena, akawa mweusi tii huku akikakamaa ilhali kiti kilibaki na rangi yake ileile nyekundu. Dokta Yusha aliyaangalia yote huku huku akitetemeka, mikono yake ikiwa kauziba mdomo wake. Alikuwa anaangalia picha mbaya sana!
Huku akitetemeka dokta Yusha alisimama, kwa kiasi kikubwa akisaidiwa na ukuta katika kumsaidia kunyanyuka pale chini. Alivyosimama tu alikaribishwa na kitu kingine, harufu, ule mwili uliokakamaa pale chini ulianza kutoa harufu kali sana!
Dokta Yusha alijitahidi kubana pumzi ili harufu ile isiyoeleweka isiingie puani mwake, ilikuwa ngumu sana, maana kuendelea kubana pumzi kulimaanisha anakiita kifo chake mwenyewe. Hata hivyo hakutaka kabisa kuvuta harufu ile, aliendea kuziba pumzi huku anaachia mara chache chache, akiwa katika hali hiyo ngumu sana katika maisha yake, mara alisikia kelele za mlango, ishara kuwa mlango ulikuwa unafunguliwa. Mlango ukafunguliwa, aliingia Sita wa Six killers kwa majigambo makubwa sana. Alienda hadi pale ukutani ambako Dokta Yusha alikuwa amesimama.

“Hahaha Dokta nawe unahisi harufu, siamini. Wewe ni daktari bwana unakutana na harufu mbaya zaidi ya hii. Hebu simama” Sita alisema kwa urafiki zaidi.

Dokta Yusha alimwangalia Sita huku akionesha sura ya upole sana. Lakini sura yake ya upole haikusaidia kitu. ‘Maji aliyavulia nguo…………..’
“Haya toka nje” Sita wa Six killers alimwambia huku akionesha kwa kidole cha shahada mahali mlango ulipo.

Dokta Yusha alitoka nje ya chumba kile huku akifuatiwa na Sita. Alipotoka tu nje, alikutana na jamaa mmoja akiwa amekaa katika kiti cha plastiki huku anavuta kiko. Jamaa yuleyule aliyekuwa anaongea kwa majivuno na kujiamini kule katika chumba cha kuhifadhia maiti. Alikuwa anaitwa Don Genge.
Dokta Yusha alisimamishwa mbele ya Don Genge huku nyuma yake akiwa amesimama imara Sita. Pembeni ya Don Genge upande wa kushoto walikuwa wamesimama watu wawili, na upande wa kushoto walikuwa wamesimama watu wawili. Don Genge alikuwa kati mithili ya Mfalme.

“Naitwa Don Genge, umeshawahi kulisikia hilo jina” Don Genge aliuliza punde tu Dokta Yusha alivyowasiri pale.
Dokta Yusha alikataa kwa kutingisha kichwa.
“Wewe ni bubu?”
“Hapana”
“Kwanini unapenda sana kufatilia mambo ya watu?” Don Genge aliachana na mwendelezo wa swali la awali na kuuliza swali jipya.
Dokta Yusha alikaa kimya, kimya ambacho kilimkasirisha sana Don Genge.
Don Genge alinyanyuka, akamsogelea Dokta Yusha huku akitabasamu. Ghafla, Don Genge alirusha kibao kilichotua sawia katika shavu la kushoto la Dokta Yusha. Dokta Yusha aliyumba kidogo, kisha akasimama tena wima. Alijishika shavu lake la kushoto kwa mkono wake wa kulia.

“Kwanini unapenda kufatilia mambo ya watu?” Sasa Don Genge aliuuliza uso wake ukiwa karibu sana na uso wa Dokta Yusha.
“Nisamehee sirudii tena” Dokta Yusha aliamua kuomba msamaha bila ya kujielewa.
“Hakuna mtu aliyewahi kuingia katika nyumba hii, akatoka hai, wote wameuwawa, tena kikatili sana! Ila wewe utakufa kifo cha tofauti…..” Don Genge aliacha kuongea, aliacha maneno yale yamuuingie vizuri Dokta Yusha. Akavuta kiko kidogo, halafu akampulizia moshi Dokta Yusha. Dokta Yusha alikohoa kutokana na ule moshi.
“………Utakufa kifo cha tofauti sana, utakufa kwa njaa!
Siku nyingi nilikuwa najiuliza hivi binadamu anaweza kukaa siku ngapi bila kula? Lakini nitapata jibu la hilo swali kupitia wewe” Don Genge alikuwa anaongea wakati Dokta Yusha alikuwa anaendelea kukohoa kutokana na ule moshi. Lakini Don Genge hakujari kama kasikia ama hajasikia.
“Hebu mrudishe ndani kule”
“Hapana, musinipeleke katika kile chumba” Dokta Yusha alikuwa anakataa kurudi tena katika chumba kile chenye harufu ya mbaya na ya kuchukiza.
“Kile ndio chumba chako, lile ndio kaburi lako, usilikatae, ulipende Dokta, peleka huyo!”

Sita alimshika suruali kwa nyuma Dokta Yusha mithili ya kibaka ashikwavo na askari na kumrudisha katika kile chumba chenye harufu kali sana…

Hali ilikuwa ngumu sana katika chumba kile, ambacho nd’o ilikuwa selo ya Dokta Yusha, au kubali la Dokta Yusha kama alivyosema Don Genge. Lakini Dokta Yusha ilimbidi akae katika selo ile, hakuwa na jinsi. Aliishi mule kwa hofu kubwa sana, kila kitu alichoongea Don Genge bado kilikuwa kinarindima katika kichwa chake, kwamba kile kitakuwa chumba chake, pia litakuwa nd’o kaburi lake.

“Nakubari kitakuwa chumba changu, tena kwa muda bila shaka, lakini haliwezi kuwa kaburi langu kamwe” Dokta Yusha alijisemea mwenyewe kwa ujasiri.
Sasa alikuwa anaivuta harufu yote ya chumbani, hakuwa anaziba tena pua, aliamua liwalo na liwe, harufu yoyote iingie puani mwake, lakini lazima atoke mle ndani.

Usiku uliingia, usiku ambao Dokta Yusha alipanga nd’o uwe kilele cha yeye kuishi katika selo ile, lazima atoke mle ndani. Ndani ya chumba kile kulikuwa na giza kubwa sana. Dokta Yusha alinyanyuka kwenye sakafu alipokaa na kuusogelea mlango. Alishika komea la mlango na kujaribu kulizungusha taratibu.
Mlango ulikuwa umefungwa!

Dokta Yusha ilimpasa kutafuta njia nyingine mbadala ya kumuwezesha kutoka katika chumba kile cha kifo. Ilimpasa kutumia akili za ziada kutoka katika chumba kile cha mauti.

‘Lazima nitoke humu, siwezi kufa kikondoo humu’
Dokta Yusha aliangalia juu ya kile chumba, alikutana na vigae vilivyowezekwa vizuri sana kule juu. Hakuna mjanja atakayeweza kufanya chochote ili kupita katika vigae vile. Ilikuwa ngumu sana!
Dokta Yusha alirudi nyuma, akarejea tena ukutani, akauangalia ukuta, akautomasa ule ukuta kwa kidole, ulikuwa ukuta mgumu sana!

Mlango, ukuta, bati vyote havikumruhusu kabisa Dokta Yusha kutoka katika chumba kile cha hatari.

Dokta Yusha alichoka, alikaa chini ili kusubiri kukiona kifo cha njaa jinsi kinavyokuwa.

Saa kumi kamili alfajiri ilimkuta Dokta Yusha akiwa macho. Alikuwa hajasinzia hata kidogo, muda wote alikuwa anafikiria namna ya kutoka katika chumba kile lakini hakupata namna ya kutoka.
Mara, alisikia tena kelele za mlango kwa nje, ishara kama ya mwanzo kuwa mlango ulikuwa unafunguliwa.

‘Ama zake, ama zangu!’

Aliingia tena Sita, akiwa kashika bunduki aina ya SMG mkononi. Alisimama pale mlangoni na kumwangalia Dokta Yusha. Sita wa Six killers alikuwa ameenda kuhakikisha tu kama Dokta Yusha hajafanya ujanja wowote wa kujaribu kutaka kutoroka. Sita alimshuhudia Dokta Yusha akiwa amekaa palepale alipomwacha awali. Akadanganyika kwamba Dokta Yusha hajafanya kitu chochote kile cha kujaribu kutoroka.
Alijidanganya. Dokta Yusha alitafuta sana njia ya kutoka mle ndani lakini hakuipata.
Sita aligeuka nyuma ili arudi nje kuendelea na lindo lake.
Kwa kasi ya haraka Dokta Yusha alinyanyuka pale chini na kupiga hatua mbili kubwa sana, hatua zilizomfikisha mpaka pale mlangoni. Alipokuwa Sita wa Six killers.
Wakati Sita anataka kugeuka nyuma kujua sababu ya vishindo viwili alivyovisikia, alichelewa sana!
Alikuwa kakabwa vizuri sana na Dokta Yusha. Kabali maridadi iliyomtetemesha Sita na kuidondosha bunduki chini.
Dokta Yusha hakujari, alimvuta Sita kwa nyuma kwa nguvu. Mwanzoni Sita alijikomaza lakini baadae Ilibidi ajilegeze, maana kukomaa ilimaanisha kuumizwa zaidi na ile kabali.
Kujilegeza nako lilikuwa kosa kubwa sana alilolifanya Sita. Kosa ambalo atalijutia mpaka kesho, kama kuna maisha baada ya kilichomtokea pale. Dokta Yusha alimvuta Sita kwa nguvu na kujikuta akimsukumia pale katika kiti cha kifo!
Balaa!
Sita alibadirika naye, mwili ulibadirika sambamba na kiti, Ilikuwa ni rangi nyekundu mithili ya tanuru la moto!
ITAENDELEA

Balaa Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment