Magnum 22 Sehemu ya Tano
IMEANDIKWA NA: RICHARD MWAMBE
*********************************************************************************
Simulizi: Magnum 22
Sehemu ya Tano (5)
Hoteli ya Blue Moon
Kamanda Amata alijibwaga kitini, akakitoa kile kitabu alichopewa na yule mwanamke, akakiweka mezani kisha akijimiminia pombe katika bilauri yake na kupiga mafunda mawili tu, ikaisha, akjimiminia tena na kupiga funda moja kisha akitua mezani. Baada ya ukimya wa sekunde kadhaa akiwa katika kutafakari jambo, akapeleka mkono na kutaka kuchukua kile kitabu. Mbisho wa hodi ukamshtua, akachomoa bastola yake na kuiweka tayari. Hodi ile ikarudiwa tena.
Jinsi ilivyokuwa ikigongwa, haikuwa ngeni masikioni mwake kwani kati idara ya TSA kila mmoja alikuwa na jinsi ya kugonga hodi au kengele ya mlangoni. Ijapokuwa alijua kuwa hiyo ni code ya Gina, Amata hakutaka kukubaliana na moyo wake.
Trust no one! Akajisemea moyoni huku akiinuka taratibu na bastola yake mkononi, akauendea mlango na kukinyonga kitasa taratibu. Akaufungua mlango huku yeye akibaki nyuma yake.
“TSA 5!” Gina akatamka kabla ya kuingia ndani. Kamanda Amata akajitokeza baada ya kusikia sauti tamu ya msichana ampendaye. Wakakumbatiana kwa nguvu na kupeana mabusu motomoto, hata sekunde kumi hazikupita wakaangushiana kitandani na kupeana mahaba mazito waliyoyamisi kwa siku nyingi. Saa nzima ya pilika pilika za kitandani ilipokwisha, wakasindikizana maliwatoni na kujiweka sawa, kisha wakarudi tena chumbani.
“Mmefika lini?” Amata akamuuliza. Hili ndilo lilikuwa swali la kwanza la Amata kwa Gina tangu wakutane saa moja iliyopita.
“Leo hii mida kama ya saa nne au tano hivi,” akajibu.
“Umejuaje kama niko hapa?”
“Nipo na Chiba…”
“Aaaa basi hapo lazima mnipate. Sasa inabidi tutafute pa kuweka kambi maana mambo tayari yameiva, mi nimeshaliamsha dude,” Amata akamwambia Gina.
“Kinachotakiwa ni wewe kufunga kilicho chako hapa na kunifuata, tayari tumepata kambi ambayo Madam S alikwishaiandaa kwa siri…”
“Iko wapi?” Amata akauliza.
“Just do kile nimekwambia!”
“Sawa Kiongozi,” Amata akajibu na kuanza kuweka vizuri vikorokoro vyake, dakika kumi baadae alikuwa tayari kwa safari. Katika meza ya mapokezi akahakikisha ameipia kila kitu na hakujibu hata swali moja la mhudumu. Wakaingia garini na Gina akashika njia na kutokomea mjini.
“Vipi, hatuna msindikizaji?” Gina akauliza.
“Tupo peke yetu tu,” Amata akajibu huku akirudisha macho yake kutoka nyuma kuja mbele. Mwendo nusu saa uliwafikisha katika jingo lile lile upande wa maegesho. Gina akaegesha gari na kuteremka akifuatiwa na Amata, wakachukua mizigo na kupita katika njia ile aliyoelekezwa na Archimedeus.
“Karibu sana Kamanda!” Chiba akamkaribisha katika sebule ile waliyokabidhiwa.
“Asante sana, nashukuru kwa kuwa mmekuja, vipi bibi anaendeleaje?” Amata akauliza.
“Nimewasiliana naye si muda mrefu, yuko poa na ameruhusiwa kurudi nyumbani,” Chiba akaeleza huku akiweka kando mkoba wa Amata alioutwaa toka mabegani pake pindi tu alipompokea.
“Hatuna budi kuanza kazi mara moja kwani muda unakimbia,” Chiba akasema na Amata akaafiki kwa kichwa, “mpaka sasa duru zote zinaonekana zikiamini kuwa Gupter hayupo nchini hapa…”
“Ni hatari sana kwa sababu watalegeza ulinzi wakati mshenzi huyu na timu yake wamejaa tele ndani ya Addis!” Amata akamkatisha na kumjibu. Gina na Chiba wakashtuka kidogo.
“Yupo?” Chiba akauliza.
“Kabla ya yote mmekagua hiki kiapartment, kusije kuwa kuna watotot wanatusikiliza tu!” Amata akawaambia akimaanisha kama kuna vinasa sauti vya siri.
“Aaaaa Kamanda, hilo ni jukumu la kwanza, unaona kifaa hiki hapa…?”
“Yap!”
“Hiki ni kifaa kipya kabisa, hapa kilipo kikigundua tu kuwa tunasikilizwa kitapiga kelele; kwa ukimya wake ujue mambo shwari,” Chiba akamwambia.
“Ok! Gupter na washenzi wake wameingia hapa masaa ishirini na nne hivi au arobaini na nane labda…”
“Una uhakika?” Gina akauliza.
“Huwa sibahatishi mama! Mi nimefika hapa nikitokea Sierra, pale nilipata namba ya mtu wa huku ambaye nahisi Gupter alikuwa akiwasiliana naye…”
“Yupo wapi tumtaiti mapema?” Chiba akawahi kuuliza.
“Umechelewa Chiba, ndiyo maana kuna TSA 1 na TSA2, wewe ni 2, kwa maana hiyo 1 alishafanya kazi na huyu mshenzi tayari anahemea kuzimu,” Amata akaeleza.
“Umemuua?” Gina akauliza.
“Hakukuwa na jinsi kwa maana ningemwacha hai angeweza kuwapa taarifa ‘kina Guter kuwa nawasaka, hivyo mpaka sasa hata wao hawajui kuwa nipo, ukizingatia wanaamini kuwa mimi ni mfu na ninaoza tu kwenye kaburi la pamoja…” Amata akaeleza.
“Nakuamini Kamanda, lazima uoneshe heshima ya cheo chako,” Chiba akamsifia.
“Sasa ipo hivi, yule Mtaliano ni tajiri wa kukodisha majumba ya kuishi na ana nyumba zake huko mashambani, na kati ya nyumba hizi moja wapo kwapangisha kina Gupter…”
“Wapi huko?” Gina akadakiza swali.
“Aleltu!”
“Aleltu, Aleltu, Aleltu!!!”
“Huwezi kupajua bwana,” Amata akamwambia Gina huku akiweka mezani kile kitabu cha ramani, akakifungua na wote kwa pamoja wakaanza kuisoma ramani hiyo ya Jiji la Addis na viunga vyake. Wakati Gina na Amata wakisoma, Chiba alikuwa akitafuta katika mtandao, eneo lilipo, namba za nyumba na wamiliki.
“Batlomino Augusto!” akatamka baada ya kupata tafutishi za kutosha, “Hapa kuna nyumba namba na mtaa,” akaeleza Chiba.
“Twendeni tukavamie tumalize mchezo!” Gina akapendekeza.
“Mmmmmh Gina kila mara namkwambia, ‘don’t put your best foot forward’. Adui kama huyu si bwege kama waliokula pesa za EPA, wakati mwingine mwache adui hata anywe chain a wewe ukiwa unamwangalia tu kwa sababu huo si wakati mzuri wa kufanya uvamizi,” Amata akamwambia Gina.
“Unamaanisha nini, tumwache mpaka afanye mauaji mengine hapo kesho?” Gina akaongea kwa uchungu.
“Si hivyo, ili kumtia mbaroni muuaji mwenye taaluma kama huyu inabidi kwanza umsome aina yake ya kuua; anavizia? Anadhamiria? Au anafanyaje… Gupter lazima tumstadi kwa muda mrefu…”
“Hatuna muda Amata, time is now!” Gina akang’aka.
“Sikiliza Gina, wenzako tulishaanza kumstadi huyu mjinga miezi miwili ilopita, na tumegundua kwamba, mauaji aliyotaka kuyafanya Dar es salaama ndiyo atakayoyafanya hapa, nikiwa na maana kuwa, atatekeleza mauaji baada ya kikao, huo ndiyo mpango,” Amata akasema.
“Sasa tufanyaje, tuwasake tuwatait usiku huu au tufanyeje?” Chiba akauliza.
“Hawa lazima watembelewe usiku huu huu, na kukiwakuta hatakiwi kuachwa mtu, ni kuwatia tunduni tu!” Amata akasisitiza. Akaitazama saa yake, tayari ilikuwa ni saa nane inaenda tisa za alasiri.
Hoteli ya Golden Tulip – Addis Ababa
Kama ni ulinzi basi hapa ulikuwa umeimarishwa, kila aliyekuwa akiingia ndani ya hoteli hii alikuwa akipekuliwa vilivyo. Mitambo ya kisasa ilifungwa pande tafauti za hoteli hiyo kuanzia juu mpaka chini na kuhakikisha hata akipita mende anaonekana. Alasiri hiyo Martin Gupter aliegesha gari katika eneo la kuegeshea la hoteli hiyo. Ndani ya gari lake alikuwa yeye na Fredy huku wakimwacha Amanda akiwasili na gari lingine.
“Lazima tuujaribu ulinzi!” Guter akasema.
“Huo ni mchezo wa hatari sana kaka,” Fredy akamwambia.
“Sikiliza, mimi kwangu ni mchezo wa kawaida sana kwa sababu nimeshafanya kazi hiyo kwa miaka mingi, najua nini na nini cha kufanya na nijikute ndani ya hoteli…” akasema.
“Ok! Jaribu…. Unataka kuingia?”
“Yeah! Nataka kuingia na kunya bia moja, we nisubiri hapa,” Gupter akamwambia Fredy na kushuka, moja kwa moja akauendea mlango wa hoteli hiyo ambao mbele yake kulikuwa na askari kama wane hivi wakiwajibika huku na huko, kumkagua huyu na yule.
Sasa hii ni hoteli tu kwa ajili ya chakula cha jioni, huko wanakolala kuna ulinzi gani! Guter akawaza wakati akipandisha ngazi za kuingia ndani.
“Hey man! Stop for inspection please!” askari mmoja alimuomba asimame kwa ukaguzi, Gupter akafanya hivyo. Akapekuliwa kila kona ya mwili wake, na upande mmoja wa koti akakutwa na bastola, ikachomolewa.
“We ni mgeni wa hoteli hii?” akaulizwa.
“No, ila mara kadhaa hupenda kuja kupata kinywaji kidogo au kucheza poker,” Gupter akajibu.
“Sawa, sasa hutoruhusiwa kuingia na hii silaha, ni hatari kwa sasa, utaiacha hapa, na kuichukua ukitoka,” yule askari akamwambia. Wakati Gupter akimsikiliza, kulikuwa na askari mwingine akimtolea macho kijana huyu wa kizungu mwenye mustachi wa wastani na ndevu za kuote kwa mbali na sura yake ni kama iliwahi kuungua miaka mingi nyuma. Gupter alimwona askari huyu akahisi labda amemgundua, akapiga moyo konde.
“Ok, waweza kuendelea na safari yako,” akaruhusiwa. Hatua kama kumi mbele akasikia sauti ikimwita.
“Hey man!!!” askari yule yule wa kwanza akamwita tena.
Ohoooo huku kuitana mara mbili kuna jambo! Gupter akawaza na kugeuka kiuvivu kidogo.
“Wallet yako hii,” akaambiwa. Kumbe wakati anasachiwa alikuwa ameweka waleti mezani na kuisahau hapo.
“Asante sana!” akashukuru na kuichukua kisha akaingia zake ndani.
Kutoka katika maegesho, Amanda akashusha darubini yake na kushusha pumzi ndefu, akaiweka kando na kutulia kwa sekunde kadhaa. Akafungua mlango na kushuka, akaufunga kwa mguu nyuma yake na kuvuta hatua kuelekea kwenye vibanda vya kuuza mambo ya utamaduni, huko akapoteza kama saa nzima hivi akinunua hiki na kuangalia kile, lakini yote hayo yalikuwa geresha tu, lengo kuu lilikuwa ni kupata habari mbili tatu kutoka kwa wananchi hao.
Baada ya saa moja kupita, Martin Gupter akatoka kwenye mlango ule ule na kuchukua bastola yake, kisha akavuta hatua na kulielekea gari la Amanda akaingia na kuketi.
“Vipi?” Amanda akauliza.
“Ulinzi mwepesi sana kwa mtu kama mimi, nitaingia na kufanya yangu pindi ikibidi na nikitakiwa kufanya hivyo. Twende sasa tukaonane na Fadick,” akamwambia Amanda.
“Unapajua alipo?”
“Ndiyo maana nikakwambia twende,” Gupter akajibu na mwanamke huyo akaliondoa gari na mita chache nyuma akafuatwa na Fredy.
Drunken Hamidou
Mara alipotoka uwanja wa ndege, kijana huyu mpelelezi machachri wa jumuia ya ECOWAS akafika katika chumba cha siri ambacho yeye na wenzake wawili walioteuliwa kuunda timu ya kipelelezi ya kumsaka muuaji wa viongozi wa Afrika hukutana na kuweka mezani tafutishi zao. Kama ilivyo ada kwao, muda huo kila mmoja alfika kwa njia yake na kukutana ndani ya chumba hiki cha siri katika moja ya ofisi za jingo kubwa la mikutano na ofisi la Umoja wa Afrika.
“Kazi ni ngumu, viongozi wote wamefika salama, sasa sihida ni kuhakikisha huyu jamaa kweli hajaingia nchini?” mmoj wao kutoka jumuia ya SADC akawaambia wenzake.
“Tunapiga ngumi kichakani, kumbukeni mshenzi huyu naye ni kachero kama sisi hivyo anajua mbinu zote tunazotumia, nimehakikisha ulinzi mkali upo katika hoteli ambayo Mwenyekiti wa atafikia…” mwingine akasema.
“Nimemwona Amata Ric!” Drunken Hamidou akawaambia swahiba zake. Kila mmoja akashtuka na kumtazama kijana huyo, “Amata!? Wa TISS” akauliza yulle wa SADC.
“Ndiyo, alikuja uwanja wa ndege, akaenda mapokezi na baada ya dakika chache akatoka kwa mwendo wa kasi kidogo akaingia kwenye gari aina ya Range Rover na kuondoka,” akawaambia.
“Umemfananisha! Inasemekana Amata ametoweka na habari ambazo ninazo ni kuwa Idara ya usalama wa Taifa ya Tanzania, inaficha habari hii kwa aibu kwa kuwa walijinasibu kuwa wataimaliza kazi hii kwa siku chache,” mwingine akaongea kwa kujiamini kabisa.
“Narudia, nimemwona Amata Ric, na kama yeye yuko hapa basi Gupter yupo hapa, tuwe makini… Amata si mtu wa kutoweka ovyo, kama kweli alitoweka basi alitoweka kikazi, na sasa ameibukia Addis… pendekezo langu mimi tutumie dakika chache kumsaka kwa njia zote, na tukimpata tufanye kazi pamoja, kwa vyovyote yuko mbele kuliko sisi, si ajabu anamjua hata demu wa Gupter anaishi wapi…” Drunken akawaambia wenzake, ukimya ukajidai kati yao, hakuwa aliyeongea lolote.
“Hapana, hata kamati yenyewe itatushangaa, tunaacha kutegua kitendawili na kumtafuta Amata…”
Baada ya kikao hicho kifupi kukamilika, wakatawanyika, lakini kama kazi yao ili, siri hufanyika kwa siri na siri huwa siri ya siri. Kila mmoja alifika kwa mkuu wake kwa siri na kumpa taarifa aliyokuwa nayo kutokana na kazi yake ya siku hiyo.
Ni huyu Drunken Hamidou ndiye aliyetoa taarifa kwa mkuu wake na ikasambaa katika kamati ya usalama ya umoja huo kuwa Amata yupo Addis. Haikuwa rahisi kueleweka kwa wadau wa kamati hiyo, habari hii iliwachanganya kiasi na swali likawa, je TSA wapo Addis? Mwenyekiti wa baraza hilo, hakufurahishwa hata kidogo na habari hiyo, akauliza mara kadhaa kama ni kweli wana uhakika aliyeonekana ni huyo au kivuli chake, akahakikishiwa kuwa ni yeye.
Katika kikao cha jioni hiyo, wadau wa baraza la usalama walikuwa na mjadala mzito sana kuhusu jambo hilo.
“Mimi, nikiongea kama mwenyekiti, mwenye mamlaka, nasema hivi, haitakiwi kwa idara yoyote ya usalama, kutoka popote pale, kuingilia mchakato huu wa kumnasa Gupter bila kibali chetu. Na kwa kanuni hii natoa amri na itekelezwe mara moja, huyu kijana wa TSA, nani sijui…”
“…Amata!”
“Yes! Amata, akamatwe na kuwekwa ndani ili kupisha kazi yetu ifanyike kwa umakini,” akamaliza kusema na ukimya ukatawala. Hakuna mjumbe yeyote aliyejibu au kuweka neno lolote. Hoja chache zikaendelea na baadae kikao hicho kikavunjwa ikiwa bado mwenyekiti wa baraza hilo la usalama la muda akitaka Amata akamatwe. Mara baada ya kumaliza kikao, mwenyekiti yule akatoka na kuwaacha wajumbe wake, akaingia gari ni kuelekea katikati ya mji, ndani ya jengo fulani ambalo kwalo alikutana na watu wengine watatu.
“Nahitaji mnifanyie kazi moja tu,” akawaambia.
“Ipi mkuu?”
“Kuna huyu mpelelezi wa Tanzania, inasemekana yupo hapa Addis, huyu anaweza kutuharibia kazi yetu, hivyo akamatwe awekwe ndani haraka kabla ya giza hili alijaisha,” akawaambia. Wale vijana wakatazamana kwa sekunde kadhaa kisha mmoja wao akahoji.
“Mkuu, kwa nini tusimjumuishe huyo mtu katika timu yetu? Maana mpaka sasa huyu Gupter anatuumiza vichwa, sisi hapa tuna tetesi tu kuwa anaweza kuwa nchini…”
“Mmejuaje?” akahoji.
“Mpaka sasa tunafuatilia ndege ya jana ambayo ilipata hitilafu, tunahisi hawa jamaa wameingia nchini kwa kutumia njia hiyo, yaani kushuka kwa miamvuli,” mmoja wa wale vijana akaeleza. Maelezo haya yakamfanya huyu mzee kuduwaa, hakuwahi kufikiri kitu kama hicho kichwani mwake.
“Any way, vyovyote vile, nataka huyu bwana akamatwe, mkishamkamata, tutamhoji kama ana habari yoyote juu ya mtu au watu hawa,”mwenyekiti akawaambia na kuwaaga pasi na kuruhusu swali lolote.
Ujumbe kutoka Oman, uliotumwa na Jaffer Bakhari uliwasili Addis Ababa ukiongozwa na Fadicky Al Habib. Ingawa baraza la usalama la muda lilikwishamtuhumu mtu huyu kama kiongozi wa mauaji haya, bado hawakuweza kumkamata kama wengi walivyotaka. Walijua amefika na watu wengine kama kumi hivi lakini kwa sheria za kimataifa hawakuweza kuwagusa watu hao.
“Kesho ni mwisho, wakikubali, itakuwa sherehe kwetu kuikomboa nchi yetu, wakikataa basi wataendeea kushuhudia mauaji na vita visivyokwisha,” wengine wakaitika na kuunga mkono.
Watu hawa walijipanga kwa hoja nzito dhidi ya Umoja wa Afrika, wakidhamiria kuipata ardhi ya mama zao.
“Na huyu mwenyekiti ndiye anayatunyima ardhi ile, hastahili kuishi, na kesho aongozwe na dhamira yake akubali ombi letu,” akawaambia.
Akiwa katika kuongea huko, simu yake ikaita, akaitazama na kuona namba ambayo alikwishapewa kuwa itampigia. Akainuka na kuingia katika chumba maalumu ambacho hakiruhusu sauti kutoka nje.
“Yes Shooter!” akaitikia simu hiyo.
“Tupo!” sauti ya pili ikasema.
“Mpango ni kama ulivyoambiwa, haujabadilika, ikiwa positive, utafanya ulivyoambiwa na ikiwa negative utajua wewe unamalizaje mchezo,” Fadicky akamwambia mtu wa upande wa pili.
“Unafikiri kuna kikwazo? Mbegu zetu tumezipanda kila mahali na zinamea vyema, over and out!” Fadick akasema.
“Hakuna kikwazo, kila tundu linapenyeka, over and out!” sauti ya upande wa pili ikajibu.
“Uno trabajo!”
Simu ikakatika.
Martin Gupter, akashusha simu sikioni na kubaki kimya huku akitafuna bubble gum kinywani mwake. Kwa taratibu sana, akafungua mlango na kukanyaga ardhi yenye vumbi, ya kijiji hiko cha Alertu. Akavuta hatua na kuingia ndani ya nyumba hiyo, giza lilikuwa limetawala ndani mwote. Fredy na Amanda walikuwa wamebaki mjini wakiendelea kupanga hiki na kile kwa kificho kikubwa ili wasijulikane. Ni Martin Gupter pekee alikuwa amerudi muda huo akiwategemea wenzi wake usiku wa baadae wa siku hiyo. Hatua zake chache zikamfikisha chumbani, na hapa ndipo moyo wake ulipolipuka kama kombora. Juu ya kitanda chake alikuta vitu viwili ambavyo hakutegemea; bunduki kubwa ‘Magnum 22’ na ua waridi.
Nani kaweka vitu hivi? Akajiuliza, hakupata jibu. Moyowe ukadunda kwa nguvu na hofu, akavuta hatua na kukikaribia kabisa kitanda kile, macho yake yakatua vyema katika bunduki ile, kilichomshangaza zaidi ni kuwa ilikuwa ile ile ya kwake. Bunduki aina ya Magnum 22 Riffle, na juu yake imefungwa hadubini ile ile. Martin Gupter, mikono ikamtetemeka, kijasho chembamba kikamtiririka, hakuelewa kama anaota au yu macho. Akatzama huku na huko, huku akichomoa bastola yake kutoka kiunoni na kuikamata barabara kabisa. Kutoka hapo akaanza kupita chumba kimoja kimoja kuangalia kama adui yake yupo ndani ya nyumba yake hiyo, la. Martin Gupter, kila alipojaribu kufikiria juu ya hilo, alijikuta yupo njia panda, akajitupa kitini na kuinua simu yake, na kuwataka Amanda na Fredy kurudi.
Robo saa baadae, wawili hawa wakaingia katika nyumba hiyo, tayari ilikuwa usiku wa saa tatu na nusu hivi kadiri ya saa iliyoning’inizwa ukutani.
“Martin!!” Amanda akaita na kumfanya kijana huyo kugutuka kama aliyepigwa shoti ya umeme, “Vipi, mbona umetutaka kurudi mapema ilhali bado tulikuwa kazini?” Amanda akasema.
“Kila kitu kimerudi, ndugu zangu hapa kazi ni ngumu!” akamjibu.
“Kivipi? Sikuelewi!” Fredy akadakiza.
Martin akainuka kitiki na kuwapa ishara ya kuwa wamfuate, nao wakafanya hivyo, wakafika chumbani kwa Martin na kujikuta wakipigwa butwaa. Fredy akamgeukia Martin na kumwambia, “They are here!” (wapo hapa).
“Yes! Na hii sasa ni hatari, jamani uamuzi wangu ni huu, hatuna budi kuhama hili eneo haraka, maana adui yetu keshajua wapi tulipo,” Martin akasema.
Amanda akatulia kimya bila kujibu neno lolote, akili yake ilikuwa bado ikijaribu kuyapanga mambo.
“Ina maana TSA wapo hapa?” akarudia swali ambalo alishaliuliza kwanza.
“Kwani ni nani alikuwa nabunduki hii? Si ilitoka mikononi mwangu tukiwa Tanzania, kwa mara ya kwanza katika maisha yangu!” Martin akasema.
“Sawa, tuhame na tuhamie tusipopajua lakini kama tumefanikiwa kumuua namba moja wao, hawa wengine hawatatusumbua kabisa,” Amanda akasema na Fredy akatikisa kichwa huku akitoa mkoba wake kabatini.
“Jamani, sikilizeni, kule Free Town tulipomkamata yule bwege, kumbuka tulimwekea nini kitandani… si ua waridi?” Fredy akawakumbusha kwa maneno hayo. Ukimya wa sekunde kadhaa ukapita katikati yao, Amanda akamtazama kijana huyo kwa macho ya kidadisi, “Unataka kusemaje?” akauliza.
“Yule mjinga hajafa! Kwa sababu nani awape ujumbe kama huu wenzake? Hamuoni kwamba kataka kujitambulisha kuwa yupo hapa, yaani mzima wa afya…” Fredy akasema.
“Katokaje mle ndani, mle hatoki mtu labda kama hana mwili,” Martin akamjibu.
“Hajafa, na yupo hapa, kwanza Battlomino ameuawa leo, vipi kama ni yeye kampa ramani ya tulipo,” Fredy akazidi kudadavu mambo.
“Tuondokeni!” Martin akazidi kusisitiza, akaichukua ile bunduki na kulitia lile ua katika kopo la takataka, “Tukapige kambi Etonto,” akasema akiwa tayari mkoba begani.
“Etonto?” Amanda akauliza.
“Ndiyo, Etonto… kesho tutakuja mjini kwa tukio moja tu, kuua au kunywa soda!” Gupter akamjibu na kutoka nje, dakika tano baadae wawili hao nao wakatoka na kuingia garini, wakaondoka zao na kuiacha nyumba hiyo kama walivyoikuta.
“Simwelewi huyu jamaa, kama ni yeye kweli, basi si mtu wa kawaida,” Fredy akasema huku akiendesha gari kwa kasi.
“Huyu ni shetani! Tena shetani asiye na mkia,” Amanda akajibu.
“Sasa awe shetani asiwe shetani, kesho nikimtia machoni tu, nitamuua kwa bunduki hii hii, mtoto wa kahaba yule!” Martin akaongea kwa hasira.
“Nimekumbuka!” Amanda akasema na kumpa ishara Fredy asimame, “Ni vipi kama hiyo bunduki imewekwa GPS na inmfanya adui atufuatilie kirahisi?” akasema. Martin akaitazama ile bunduki na kuigeuzageuza, akafungua mlango wa gari na kutoka nje, akaitupa kwenye vichaka na kurudi garini.
“Umeitupa?”
“Nimeificha!”
Fredy akarudisha gari barabarani na kuendelea na safari.
Chiba akaegesha gari jirani kabisa na kichaka kile kile ambacho Martin aliitupa ile bunduki muda mchache uliopita. Gina akashuka na kufuatiwa na Kamanda Amata, wakaingia kichakani na kuichukua ile bunduki kisha wakarudi garini.
“Wana bahati sana, wameshtukia njama,” Amata akasema.
“Kwa hiyo!!” Chiba akauliza.
“Turudi mjini, tukajipange upya, kesho lazima tuwatie nguvuni kabla hawajaleta madhara,” Amata akajibu huku gari likigeuzwa na kurudi mjini.
Baada ya kama nusu saa hivi, wakawasili mjini na Chiba aliendesha gari kwa mwendo wa wastani huku mazungumzo ya hapa na pale yakiendelea.
“Chiba!” Amata akaita.
“Sema!” Chiba akaitikia.
“Nahisi tuna kampani nyuma yetu, nimeangalia kwa muda mrefu sana, kuna magari mawili yanatufuatilia, kila mmoja ajiweke tayari maana hatujui kama ni marafiki au maadui,” Amata akawaambia huku akiiweka bastola yake vyema, tayari kwa lolote litakalotokea, Amanda naye akafanya hivyo hivyo na kumkabidhi Chiba bastola huku yeye akiweka yake wake tayari.
“Tayari?” Chiba akauliza.
“Ndiyo, weka gari pembeni na asishuke mtu tuone!” amata akatoa maelekezo na Chiba akafuata. Akaegesha gari kando ya barabara. Amata alikuwa sahihi kabisa kwani mara baada ya kusimama, yale magari nayo yakasimama moja nyuma na jingine mbele huku wao wakiwa katikati. Vijana kama sita hivi wakateremka, kati yao, wawili wakasogelea gari walilokuwamo TSA na kugonga kioo cha mbele. Chiba akashusha kioo robo tu ili kusikiliza nini kitazungumzwa.
Wale mabwana wakatoa vitambulisho na kujitambulisha kuwa wametoka ofisi maalumu ya usalama ya AU. Chiba naye akato kitambulisho chake halisi kabisa cha TSA na kuwaonesha na Gina akafanya vivyo hivyo na Amata pia baada ya kushusha kioo mpaka chini.
“Tuna shida na Amata Ric, shida ya kikazi, tumepata taarifa kuwa yuko hapa na tumefurahi kwa kuwa tumemuona!” mmoja wao akasema. Gina na Chiba wakatazamana kisha wakamtazama Amata.
“Ngoja niwasikilize,” Amata akasema na wenzake wakamruhusu, akateremka garini na kuitia bastola yake katika kikoba chake, wakasimama pembeni kama mita nne hivi kutoka walipoegesha magari yao.
“TSA! Tumepata taarifa kuwa u hapa, na kwa sababu wewe ni mwanausalama kama sisi, mkurugenzi wetu wa idara ya AU anahitaji kukuona kwa mazungumzo ya kikazi,” mmoja wa wale vijana akamwambia Amata kwa kiingereza chenye lafudhi ya kihabeshi. Kamanda Amata akatulia kimya kama sekunde kumi hivi kisha akavuta hatua kurudi katika gari, akawaambia wenzake jambo hilo.
“No! tunaenda wote, sisi tutaamini vipi juu ya hilo? Vipi kama ni njama, je?” Gina akauliza.
“Mchezo wetu ni ule ule…” Amata akasema.
“Aaaakh! Ok, code gani?” Gina akauliza.
“300.1R” akamjibu na kuondoka. Wale vijana wakaongozana nae na kuingia kwenye gari lao kisha yote mawili yakaingia barabarani na kuondoka kwa kasi, si kwa mwendo waliokuja nao. Chiba naye akaingiza gari barabarani na kutokomea mjini, Gina akajiegemeza kitini huku mkono mmoja ukiwa umeegemezwa kwenye dirisha na kiganja kichwani.
“Code 300.1R” Gina akarudia kodi hiyo aliyopewa na Amata ambayo ni moja kati ya kodi nyingi wanazotumia kwa ajili ya kazi zao, ikiwa na manaa kwamba 300 ni masaa matatu kamili, .1 ni sekunde ya kwanza baada ya masaa hayo matatu na R ni Rescue, yaani ikifika masaa matatu bila taarifa yoyote kutoka kwa Amata basi sekunde ya kwanza ikigonga waanze mikakati ya kumuokoa, tayari atakuwa matatizoni.
Ndani ya gari lile, Amata aliketi kiti cha nyuma katikati kushoto na kulia kukiwa na wale vijana. Dereva amaye alificha macho yake kwa miwani ya giza japokuwa ni usiku alikuwa ametingwa na kazi yake wala hakujali jambo jingine lolote.
“Lini umefika Addis?” kijana wa upande wa kushoto akauliza.
“Miezi mitatu ilopita!” Amata akajibu.
“Miezi mitatu!?” yule jamaa akajiuliza na kushangaa.
“Ee, miezi mitatu…” akajibu na kubaki kimya. Lile gari likapenya mitaa kadhaa na kuibukia upande mwingine mji. Baada ya mwendo wa takribani dakika hamsini hivi wakaingia kwenye jingo moja kubwa na lile gari likateremka chini jingo hilo. Ndani tu ya jingo hilo, lile gari lilitembea kama dakika kumi na tano hivi na mwisho likaegeshwa sehemu fulani ambapo palikuwa kama stoo ka jinsi makorokoro yalivyozagaa huku na huko.
“Tumefika!” yule kijana akamwambia Amata.
“Mkurugenzi yuko wapi?” Amata akauliza.
“We teremka atakuja tu,” akajibiwa.
Kengele za hatari kichwani mwa Amata zikagonga, “Sishuki mpaka mkurugenzi afike maana ndiye anayenihitaji si ninyi,” akawajibu kijeuri.
“Asee, usitake tutumie njia za kisovieti…” kijana mwingine mwenye mwili mkubwa uliojaa nyama akasema huku akisogelea gari lile.
“Kwa hiyo si mkurugenzi anayenihitaji, mmeniteka sivyo, yaani wanausalama mnamteka mwanausalama! Haya tumieni njia mnayotaka kunishusha…” akajibu kijeuri huku akiwa bado kaketi kitini na mkanda ukiwa umezunguka kiunoni mwake. Yule bwana akasogea mpaka pale na kuwahi kuufyatua mkanda wa kiti, Amata akasogea pembeni na kumpa wakati mgumu jamaa yule, mara akaona mlango wa upande huo nao ukifunguliwa na mtu mwingine. Akafanya kama anatoka na yule bwana akampokea kwa konde moja zito tumboni, Amata akajikunja kwa maumivu na kurudi ndani ya gari. Jamaa aliyempiga ngumi akaingia mkono kumshika, Amata akakamkata mlango na kuubamiza kwa nguvu, akambana vidole na yule jamaa akapiga yowe la uchungu. Upande wa pili yule bonge alimdaka Amata na kumvuata nje, akambaga chini lakini Amata akawahi kusimama, kabla hajajiandaa akajikuta akipokea mapigo mazito kutoka kwa bonge huyo kisha na virungu kadhaa vikatua mwilini mwake na kumbakisha akiwa hoi sakafuni.
“Unajifanya mjanja kwenye ardhi ya watu!” yule bonge akamwambia Amata.
Haikupita hata dakika ishirini, Marcedec Benzi moja jeusi likaingia na kufuatiwa na Nissan Patrol short Chassis nalo jeusi pia, yakasimama na taa zake zikiwa full zikimmulika Amata usoni.
“Hah! Hah! Hah! Hah! Aaaaaah, umefufuka siyo?” sauti nzito ya mtu ambaye hakuweza kumwona vizuri ilisikika, “sikiliza kijana, hizi kazi si za kufanya kama ufanyavyo wewe, kukuepushia haya, ulishauawa wewe kule Waterloo, kwa nini hukutulia ufe?” akamuuliza. Kamanda Amata akainua uso wake kwa taabu kidogo na kumtazama huyo asemaye, hakumwona sura ila kitambulisho alichokuwa amekivaa kilimtambulisha kwa kusomeka MARILEKC FikrMARYAM. Jina tu tayari lilimpa habari kamili Amata, alilijua kwa sababu ni huyu ndiye aliyeteuliwa kuongoza kamati ya dharula ya usalama ya AU iliyokuwa na jukumu la kumsaka muuaji wa viongozi wa Afrika ambayo iliweka makao yake katika Jiji la Dar es salaam. Ni huyu, mtu wa ngazi ya juu sana katika idara ya usalama ya Umoja wan chi za Afrika, raia wa Elitrea mwenye unasaba wa karibu na Uethiopia.
“Marilekc FikrMaryam! Kumbe ni wewe… unyeihujumu Afrika na watu wake…” Amata akasema. Mzee huyo akahisi ganzi mwili mzima kwa maana jina lake daima huwa halitambuliki, akajipapasa kifuani na kukuta kitambulisho kikiwa kinaning’inia. Kwa sekunde chache, sura ikaonesha uzee mara mbili ya ule aliyokuwa nao. Marilekc akamtazama Amata pale chini na kujikuta mate yakimkauka, akameza funda kubwa na kusimama wima, kwa mkono wake wa kulia akakivua kile kitambulisho na kukitia mfukoni.
“Make him uncomfortable…” akawaamuru wale vijana nao wakaanza kumsulubu Kamanda kwa zamu. Walipiga kila mmoja kwa jinsi yake, aliyetumia mateke sawa, aliyechukua fimbo sawa, mwenye gongo twende. Dakika tano za kipigo zilimwacha Amata akiwa hoi pasi na kujitetea.
“Mwacheni!” akaamuru, na wale vijana wakamwacha na kusimama kando. Marilekc akachutama na kumtazama Amata, “unajua nini kuhusu muuaji wa viongozi wa Afrika?” akamuuliza.
“Ni-ni-ni-ttta-ju-a ni-ni, wa-ka-ti mi-mi si-hu-si-ki?” Amata akajibu kwa taabu kidogo.
“Wewe unajua, na hapa Addis umekuja kufanya nini?”
“Ni-me-ku-ja kumlinda –ra-i-s wa-ngu!” akajibu na kujinyoosha kidogo. Marilekc akawatazama vijana wake, akawaona wapo ngangari wakisubiri amri ya mkubwa wao, akarudisha macho kwa Amata.
“Nataka unipe tafutishi zote za sakata hili…” akamwambia.
“Sina!” Amata akajibu kwa neno moja tu.
“Huna!? Na zile ulizochukua Angola…”
“Anhaaa wewe ni mmoja wa-o,” Amata akasema, mara akajikuta akipokea teke moja zito usoni lililomtupia upande wa pili, damu zikamtiririka puani, akakohoa na kujaribu kujiinua, mara yule bonge akampiga teke jingine la tumboni na kumbwaga kando.
“Ni-ninyi ni wa-na-u-sssa-la-ma au ma-ja-mbazi?” akauliza.
Marilekc akasogea na kuchutama kwa mara nyingine, “Nakuuliza kwa mara ya tatu, zi wapi tafutishi za mpango huu wa mauaji ya viongozi?”
“Zipo Tanzania, wasiliana na Madam Sellina, atakupatia mpaka nilipoishia…” Amata akajibu, mara hii kwa ukakamavu kidogo.
“Sikiliza we bwege, mimi nina akili, mimi ni mwenyekiti wa kamati ya usalama, kukukamata na kukuweka hapa ni moja ya mbinu za kutaka kusaidia uchunguzi dhidi ya mauaji haya, najua wewe unajua, lakini tulipoiondoa idara yenu katika hili, tulimaanisha kuwa mnatakiwa kuwasilisha tafutishi zote mikononi mwetu…”
“…ndiyo maana mkamtengenezea ajali Madam Sellina, mlidhani mtamuua? Hajafa, hajafa, yupo hai na hivi tunavyoongea, usiku huu anatua Addis…”
“SHUT UP!!!! SON OF BITCH!” Malirekc akang’aka na kumrukia Amata, hapo ndipo alipofanya kosa ambalo alilijutia. Kamanda Amata akaviringika upande wa pili na kumshuhudia mtu mzima huyo akitua sakafuni kwenye makolokolo na uchafu, akachomoa bastola na kuifyatua, Amata akapiga sarakasi na risasi ile ikaingia moja kwa moja kwenye tenki la mafuta katika gari iliyoegeshwa jirani. Mlipuko mzito ukatokea, lile gari likabiringishwa hewani na kujipigiza juu kisha likarudi chini, mara gari lingine nalo likadaka moto.
“Ita fayaaaa!!!” kelele zikasikika, huku vijana wa Marilekc wakitawanyika kumsaka Amata asiwapotete.
“Hakikisheni hatoroki,” Malirekc akawaambia huku akijiondoa eneo lile na ving’ora vya polisi vikisikika nje.
Kamanda Amata baada ya kuruka sarakasi ile akaangukia upande wa pili lakini kutokana na maumivu aliyokuwa nayo akajikuta anashindwa hata kujisogeza. Akiwa katika kuhangaika akasikia bunduki zinazoondolewa usalama, akatulia tuli na kuweka mikono yake kisogoni huku akiwa kalala kifudifudi. Vijana wa Marilekc kutoka idara nyeti ya usalama ya AU wakamzunguka wakiwa na shot gun na wengine bastola.
“Arrest him!” (mkamateni) Malireck akatoa amri na Amata akatiwa pingu na kusombwa mpaka kwenye gari moja jeusi, akasukumiwa ndani na kufungiwa. Ving’ora vya magari ya polisi vikatulia na kubaki vimulimuli vikipendezesha eneo lile kwa taa zake za rangirangi na magari ya faya yalikwishawasili na kuanza kazi yao mara moja. Malireck akaonesha kitambulisho chake na kupigiwa saluti za heshima, kisha kwa ishara ya mkono akawaamuru vijana wake wamtoe Amata na kumkabidhi kwa wale polisi.
“Make naye huyu, asihojiwe na wala asichanganywe na mtuhumiwa yeyote, tutakuja wenyewe kumhoji, ni mmoja wa watu tunawatafuta kwa kuhatarisha usalama wa Afrika!,” akawaambia wale askari, nao wakamchukua na kumtia garini kisha wakaondoka naye kwenda kumhifadhi.
Kutoka Barabara ya Alem Gena, Chiba aliendelea kupekua kompyuta yake ndogo huku akiwa kamwachia Gina usukani. Kimya kati yao kilikuwa kama wimbo usio na mwisho kwa muda huo. Giza nalo lilikuwa limechachamaa na kuzifanya taa za barabarani kupendeza kwa rangi yake ya dhahabu.
“Moyo wangu unanambia Amata hayupo salama!” Gina akasema huku akiwa amekilaza kiti chake.
“Hapa namwona alikuwa Barabara ya Daleti na sasa anamove sijajua anaelekea wapi,” Chiba akamwambia Gina.
“Kwa nini asitupe taarifa kuwa anatoka? Hapana Chiba!” Gina akawasha gari na kulirudisha barabarani, “Nipe uelekeo,” akamwambia Chiba.
“Subiri wanakuja upande huu huu!” akamjibu na Gina akatulia lakini gari lilikuwa likiunguruma. Dakika kama saba hivi baadae, magari manne ya polisi yakawapita kwa kasi, Chiba akatazama kompyuta yake na ndipo akagundua kuwa katika magari hayo yumo Amata.
“Fuata hayo magari ya polisi!” akamwambia na Gina hakupoteza muda akaingia barabarani na kufuata nyuma. Wakiwa njiani, saa ya Chiba ikamfinya katika mkono wake wa kushoto, akainua mkono na kuitazama, ikamwonesha mwanga hafifu wa kuashiria kuna ujumbe. Saa hiyo haikutoa ujumbe wowote wa maandishi ila iliendelea kuwaka mwanga ule hafifu. Chiba akaelewa ni nini maana yake.
“Amata yupo kwenye matatizo,” akamwambia Gina.
“Ametumia kodi gani?” Gina akauliza.
“Red Code!”
“Unafikiri atakuwa kachukuliwa na polisi?”
“Bila shaka!”
Dakika kama ishirini na sita hivi, yale magari ya polisi yakaingia katika kituo kikubwa cha Akaki Kality, katikati tu ya jiji hilo. Gina ikambidi akunje kona na kuingia mtaa mwingine kadiri ya sheria ya barabara hiyo ilivyomtaka na alipozunguka akajikuta katokea upande mwingine.
“Tutajiridhisha vipi kuwa yumo?” Gina akauliza.
“Namwona hapa yupo kituoni,” Chiba akajibu.
“Ah useng* huu sasa, kazi yote itaharibika sasa na tuna saa chache sana kutoka sasa,” Gina akaongea kwa hasira yenye gadhabu.
“Tulia Gina, maadam yupo kwenye mikono ya polisi, basi yuko salama, cha muhimu sasa tufanye utaratibu wa kumpata…”
“Ni sawa Chiba, ila sasa lipi tutafanya, kumshughulikia Amata au kuendelea kuwanasa akina Gupter?”
“Huo ndiyo mtihani maana hapa sasa ni sawa na mwalimu akuulize A na B ipi kubwa, any way, tutumie busara, hatuwezi kwenda kituoni, ila hatuna budi kuripoti kwa Balozi ili hatua za kidiplomasia zifanyike…”
XIII
SIKU ILIYOFUATA
SIKU HII BARABARA ZA ADDIS Ababa hazikuwa zikipitika kwani viongozi wan chi za Afrika walikuwa wakipita kuelekea mkutanoni wakisindikizwa na pikipiki nyingi za polisi. Wanausalama wa kila aina walikuwapo, askari wa farasi, mbwa na wale watembeao kwa miguu nao walikuwapo ili mradi ‘usalama umeimarishwa’. Siku hii, shughuli nyingi za usafiri ziliathiriwa na kimuhemuhe hiki.
Asubuhi hii ya saa nne ilimkuta Amanda Keller katika Barabara ndogo ya Roosevelt, akiegesha gari lake kadiri ya maelekezo ya askari kisha akateremka na kamera yake akifuatiwa na kijana mwingine mwenye kifaa kama cha kunasa sauti. Mavazi waliyovaa usingekuwa na swali kutaka kujua kuwa hawa ni waandishi wa habari, tena wa shirika fulani kubwa huko Ughaibuni. Mwendo wao ulikuwa waharakaharaka huku wakisindikizwa na askari wawili waliokuwa wakiwasaidia kupita kirahisi katika makundi makubwa ya wanaharakati waliokuja na mabango yao kufikisha jumbe anuai kwa viongozi wao.
‘Free Somaliland’ (Somaliland iwe huru) mabango mengi yalisomeka namna hii kwa sababu katika kikao hiki licha ya kuwa na agenda nyingine ndogo ndogo, hii ilikuwa kubwa zaidi na ndiyo iliyosubiriwa na wengi katika kona za dunia.
‘How long shall kill our leaders while we stand aside and look?’ (mpaka lini wataua viongozi wetu na sisi tumesimama pembeni tukiangalia?) bango jingine kubwa liliandikwa.
Mara baada ya kuwasili katika lango kuu la jengo hilo la kisasa, Amanda na mwenzake wakakaguliwa na walipoonekana wapo ‘Clean’ wakaruhusiwa kuungana na wanahabari wengine. Hawakuchelewa, waliwahi dakika kama ishirini kabla ya kikao kuanza.
Ndani ya ukumbi huu kulikuwa na watu wachache kwenye viti, hawa walikuwa ni kama wasikilizaji au wawakilishi wa mashirika fulani fulani. Upande mwingine ambako ndiko haswa kamera nyingi zilielekezwa bado viti vilikuwa wazi, wahusika hawakuwa wameingia tayari nah ii ndiyo ilikuwa itifaki ya siku zote. Kila mtu alikuwa na kabrasha mkononi mwake akipekua kurasa hii na ile, akisoma hiki na kile.
Amanda na Martin, ndani ya jingo hili hawakugundulika kabisa kama wao ni kenge kati ya msafara wa mamba. Kwa jinsi walivyojibadili sura na mionekano yao, ingekuwa ngumu sana kwa askari wa kawaida kama hawa kuwagundua, hata wao walilijua hilo na ndiyo maana hawakuogopa hata kidogo. Hawakuwa na nia ya kupiga picha wala kuandika habari japo waliijua vyema kazi hiyo. Hapa walikuja kutazama ni jinsi gani uzito wa ulinzi uliopo kwa viongozi hawa na pia kupata uhakika nini hasa umoja huu utaamua kuhusu kuigawa Somalia vipande viwili, na hili ndilo hasa lilikuwa ni mkataba kwao wenye pesa nyingi sana toka kwa tajiri Jaffer Bakhari.
Muda ulipofika viongozi wakaingia na kuketi kwenye viti vyao na kisha muongoza shughuli akaanza kuongea maneno machache ikiwamo kutambulisha waliokuwamo ukumbini humo na kutoa mwongozo wa shughuli nzima kwa ujumla.
Wakati huo huo Gina na Chiba walifikia uamuzi wa kuacha kila kitu na kulivalia njuga swala la Amata wakishirikiana na maofisa wa ubalozi wa Tanzania. Wao hawakutaka kuwaambia polisi wa jiji hilo kuwa huyo waliyemfunga ni nani bali walitaka kumtoa kama mwanadiplomasia, lakini ilikuwa ngumu kwani mkuu wa kituo hicho alidai kuwa amri aliyopewa ni kumshikiria mpaka atakapohojiwa na watu wa usalama wa AU. Shughuli ikawa si ndogo kituoni hapo, mwisho wa yote ikaonekana, Amata ashikiliwe kwa sababu amewekwa hapo na kamati ya usalama ya AU na hakuna nchi yenye sauti juu ya umoja huo isipokuwa umoja wenyewe juu ya nchi zake.
Kwa hasira ambayo Gina na Chiba iliwakaba kooni laity wangekuwa na grenade wangelipua kituo hicho.
“Ok, nafikiri, muendelee na shughuli nyinge na baada ya mkutano tutafanya mazungumzo na watu wa usalama, ataachiwa huru tu maadam Ubalozi tuna taarifa!” afisa mmoka akawaambia akina Gina na wao wakakubaliana naye kwa kuwa hawakuwa na la kufanya, wakaingia garini na kundoka huku wakiwa kimya.
“Sasa tunaanzia wapi? Maana mi kichwa change kimeshavurugwa!” Gina akasema.
“Kwenye mkutano!” Chiba akajibu na wote wakaelekea huko. Mnamo saa saba mchana ndipo walipowasili nnje ya jingo hilo na kukuta umati wa watu umezagaa huku polisi wakiwa katika kazi nzito ya kuwaweka sawa. Kundi kubwa lilionekana likipiga kelele na kunyanyua mabango juu yaliyosomeka ‘Free Somaliland’.
“Kumekucha kaka! Sasa kwa vurugu hii huyu Gupter akiamua si anadungua kiurahisi tu!” Gina akasema huku akichukua darubini yake na kuangalia majengo yaliyozunguka eneo hilo akiwa ndani ya gari.
“Tuteremke, twende tukapande katika jingo hili kisha tuangalie huku…”
“Tugawane, na tutakayemhisi tu tule naye sahani moja,” Gina akapendekeza. Wakateremka garini na kuvaa vifaa vyao vya mawasiliano, wakatawanyika kila mtu eneo analoona lingemfaa.
“Vipi huko, kuna chochote?” Chiba akauliza baada ya dakika kama kumi hivi.
“Huku ni clean kabisa!” Gina akajibu. Chiba licha ya kuwa alikuwa akiwasiliana na Gina bado alikuwa na mashine ndogo iliyoweza kukamata mawimbi yoyote ya mawasiliano yanayopita hewani. Akaendelea kuahangaika kuzungusha nobu kidogo kidogo huku akiwasiliana na Gina. Wakati bado askari wakituliza ghasia nje ya ukumbi huo, akanasa sauti ambazo zilikuja na kupotea.
“…we have to accomplish the task ova!” (tunatakiwa kumaliza kazi)
“…target! Target!…ova” (lengo! Lengo)
“…target the table in black color…ova” (lengo meza kwenye rangi nyeusi)
“To the nest to the nest, retreat” (kiotani, kiotani) sauti ya kike ikaingilia kati, kisha Chiba akasikia mawimbi yakikatika.
Wamestuka! Akina nani hawa? Akajiuliza. Wakati akiwaza hayo ving’ora vya magari ya polisi vikasikika, tayari misafara ikaanza kuondoka eneo hilo. Chiba akatoka alipoketi na kumpa ishara Gina kisha wote wakakutana garini.
“NImenasa mawasiliano ambayo sijayaelewa,” Chiba akasema huku akimsikilizisha Gina kauli zile chache. Wakajaribu kuweka mawazo pamoja kuona kama wanaweza kugundua maana yoyote katika mzungumzo hayo, wakashindwa, walichoambulia tu ni kugundua kuwa wazungumzaji wamegundua kuwa wamenaswa hivyo wakazima mtambo.
Mara baada ya kikao kile kumalizika bila ya muafaka wowote juu ya ajenda ya kuigawa nchi ya Somalia, jopo la wajumbe waliokuwa wakidai uhuru wa nchi yao waliamua kuondoka bila kuaga na kufanya kikao hicho kisiwe na maana kwa waliobaki. Kiongozi wa mkutano huo, rais wa Gambia aliamua kukivunja kwa kuwa upande mmoja wa mazungumzo uliondoka ukumbini.
Baada ya kutoka, moja kwa moja walikwenda uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kurudi walikotoka. Kiongozi wa msafara huo Bwana Fadicky hakusema chochote hata alipobembelezwa na wanaitifaki wa AU, hakutaka kuwasikiliza aliwajibu kwa kauli mja tu, “Damu haitakauka Somalia mpaka mtupatie ardhi yetu,” hata alipokutana na mwenyekiti wa umoja huo mara baada ya mambo kuvurugika alimjibu maneno tata, “Hamtaki kukubali, nasi hatuachi,” kisha akaondoka zake.
Nje ya jingo hilo la makao makuu ambako kikao hicho kilikuwa kikifanyika, watu walikuwa wakisubiri kujua hasa ni nini kitafikiwa muafaka, vurugu zikazuka pale waliposikia kuwa hoja hiyo imetupiliwa mbali na Somalia itabaki kuwa moja.
Maili zaidi ya 10000 kutoka katika jengo hilo, katika jiji la Abu Dhabi, Jaffer Bakhari alijikuta mapigo ya moyo yakishuka, kijasho chembamba kikimtiririka, ugumu wa kutoa sauti ukamfika. Vijana wake kwa haraka wakaita madaktari wake na kuanza kumshughulikia mara moja. Hali hii ilitokana na taarifa ambayo hakuitegemea kutoka kwa mtu aliyemtuma huko Addis Ababa. Jaffer katika harakati zake, tayari alikuwa amekwishapanga kila kitu kuhusu serikali ya Somalia mpya yeye mwenyewe akiwa rais, na kutokana na utajiri wake tayari alikuwa ametenga kiasi kikubwa cha dolari kwa kuiendesha nchi hiyo huku akiahidiwa zaidi na wadau wake kuboresha elimu, afya, miundombinu na kadhalika. Lakini jibu la kikao hicho kuwa Somalia itabaki kuwa moja lilimuongezea shida na kuamsha magonjwa yaliyojificha.
“Unalopaswa kutenda, litende haraka!” ilikuwa kauli ya Jaffer akiwa kitandani akiongea na simu na mtu aliye upande wa pili. Ndani ya chumba hicho alikuwa peke yake kwa kuwa hakutaka kuwe na mtu yeyote yule wakati akiongea na simu hiyo.
Sasa wataujutia uamuzi wao, jeshi langu litaingia na kuisumbua Afrika mpaka ukamilifu wa dahari! Jaffer akawaza akiwa kitandani huku mashine zikiendelea kusoma mienendo ya viungo anuai vya mwili wake.
Martin Gupter akaitua simu yake na kuiweka juu ya dashboard, akamtazama Fredy aliyekuwa akiendesha kwa umakini wa hali ya juu na Amanda ambaye alionekana amechoka sana.
“Jamani tunatakiwa kufunga kazi hii mapema iwezekanavyo, Fredy umeshajiweka tayari?” Martin akauliza
“Tayari!” Fredy akajibu.
“Amanda! Vipi upo sawa?”
“Yes! Naye akajibu.
“Ok! Sasa mimi najua nini nitafanya cha muhimu jinsi tutakavyotoka humu nchini naomba kila mmoja ajipange, safari hii tukitumia gari moja itatugharimu, ni bora kutawanyika…” martin akapendekeza.
“Usiingilie kazi za watu, we fanya kazi ukimaliza nikute pale pale nilipokwambia, mi ndo najua nini natakiwa kufanya kukuokoeni ninyi, na kama wakitugundua mi najiuzulu kazi hii…” Fredy akasema wakati akiegesha gari kando ya bustani kubwa iliyo pembezoni mwa mji huo.
“Nahitaji kutengeza sumu mbaya kabisa kwa ajili ya kuwamaliza wabaya wetu!” Martin akaeleza.
“Safari hii sumu?” Amanda akaeelza.
“Ndiyo! Nataka nimmalize kwa sumu….”
“Hapana Martin mi naona huyu ni wa kumdungua tu, kwa sumu inaweza kutuletea shida na kukamatwa…” Fredy akasema.
“Anyway, nipeni muda nifikiri, dakika kumi tu!”
“Mimi nilishakuandalia kila kitu!” Amanda akasema. Martin akageuka na kumtazama, “Kila kitu?” akauliza.
“Yes! Njoo…” Amanda akamwita Martin, wakazunguka nyuma ya gari na Fredy akafungua buti. Ndani ya buti hilo kulikuwa na kasha kubwa tu lililotengenezwa kwa mbao. Amanda akakamata mfuniko na kuufungua, akauweka kando. Gupter hakuamini anachokiona bunduki mpya, kubwa, ilikuwa imelala kimya huku kikasha kidogo cha risasi kikiwa kando, ndani ya kasha kubwa. Martin akamatazama Amanda.
“Unanipa risasi ngapi?” akamuuliza Amanda.
“Moja tu, najua shabaha yako haikosei,” Amanda akamjibu na kijana huyo akafunga buti.
“Turudi mjini!” akawaambia wenzake.
Ofisi Nyeti ya Usalama Addis
“Nashangaa ni vipi muuaji ameshindwa kufika, na nilimpania nimtie nguvuni, yaani angejuta kuzaliwa dume,” mmoja wa wajumbe wa kamati ya usalama akawaambia wenzake.
“Ameogopa, anajua kwa vyovyote angefika hapa hasingechomoka,” mwingine akadakia.
“Kwa kweli, hata kama hajaja atasakwa tu, huyu waliyemkamata jana sijaelewa habari yake imekaaje!” mwingine akaongeza kusema.
“Mmmh huyu wamemuhisi tu, lakini inaonekana Mr. M ana uhakika kuwa huyu jamaa ana data za muuaji, kwa sababu katuambia kuwa hata tafutishi za wale vijana zimemtaja sana huyu kuanzia Angola, Ivory Coast cha kushangaza inasemekana ni Mtanzania…” mjumbe wa kwanza akasema na wakati huo huo Mr. M akaingia kikaoni.
“Wajumbe hatuna haja ya kuchelewa, bado tnahitaji kuimarisha ulizi kila mmoja katika upande wake maana kuanzi saa tisa alasiri, viongozi watawasili katika Hoteli ya Golden Tulip kwa ajili ya chakula cha pamoja. Mwanzoni ilipangwa kuwa mlo huu maalum ufanyike usiku lakini watu wa itifaki na mipango wamebadili kwa kuwa wanasema viongozi wengi wataanza kuondoka saa mbili usiku. La pili ni kuwa, jana tumemkamata mtu mwenye data nyingi kuhusu muuaji na inaonekana ndiye master plan wa mipango hii, yeye yupo kituoni na tutashughulika naye pindi tu viongozi wote watakapoondoka, hata hivyo kutokana na usalama wa kituo kile nimeamua ahamishwe na kupelekwa kwenye kituo kingine chenye ulinzi mkali zaidi,” Mr. M akawaambia huku kijasho kikimvuja na kuvunja kikao ili kila mmoja aingie majukumuni.
KITUO CHA POLISI – AKAKI KALITY
Kamanda Amata alikuwa kimya katika selo aliyofungiwa, akiwa kajilaza sakafuni na macho kayafumba akijaribu kukusanya wazo hili na lile, labda atapata lingine. Mara akastuliwa na sauti ya viatru vitambeavyo kuelekea uande huo. Kwa haraka haraka alisikiliza sauti zile akajua ni watu watano wanaokuja. Mara ikatulia na ukimya ukarejea, akainua uso kutazama, naam, mlangoni kulikuwa na watu watano, askari wa kawaida wenye virungu wawili, na wawili walikuwa na pingu na mnyororo na mmoja alionekana kuwa ni afisa kwa jinsi alivyovaa.
“We gaidi, amka!” yule askari akamwamuru Amata, naye akatii maana alikumbuka kauli mbiu ya jeshi la polisi la kwao Tanzania ‘Tii sheri bila shuruti’, “Mtieni disprin!” akawaambia vijana wake.
Wale vijana wawili wenye virungu wakafungua lile lango la chuma na kuingia ndani kisha wakaanza kumsulubu Amata sehemu mbalimbali za mwili kwa virungu vile na kumwacha hoi bin taaban. Baada ya kipigo hicho kilichodumu dakika kama tatu hivi wakaingia wengine na kumfunga pingu mikononi na ule mnyororo miguuni wakamwinua na kuanza kumkokota akiwa peku na suruali tu juu kifua wazi. Japokuwa aipigwa sana tangu usiku uliotangulia, Amata hakutetereka sana kwa sababu tayari mwili wake ulishajengwa katika mazingira ya uvumilivu na hiyo ni moja ya mafunzo yao, kuufanya mwili kuwa mkakamavu na wenye kuvumilia shida na maumivu. Nje ya kituo kulikuwa tayari na gari lililoandaliwa maalum kumbeba, akaingizwa ndani na mikono yake yote ikafungwa kwenye chuma maalumu ndani ya gari hilo huku wale askari waliokuwa wakimsulubu wakiketi nyuma kabisa ya gari hilo umbali kama wa mita moja hivi kutoka alipo yeye. Milango ikafungwa na lile gari likaondoka huku likisindikizwa na ving’ora vya polisi nyuma na mbele.
Gina aliendesha gari taratibu kwenye barabara za jiji la Addis huku kichwani akiwa na mawazo lukuki. Chiba yeye alikuwa ametingwa na kwenye kompyuta yake ndogo huku akiwa na kifaa cha kusikiliza masikioni mwake.
“Uelekeo!” Gina akasema.
“Tunarudi ubalozini, lazima tuhakikishe tunampata Amata leo, kwanza mpaka sasa wamevuruga utaratibu wetu,” akamwambia Gina.
“Kwa hiyo tuachane na ‘kina Gupter?”
“Sasa tufanyeje, mi nafikiri tuache kila kitu tumpate Amata, kwa maana yeye tukimpata huyo mwendazimu Gupter tutamsaka tu,” akamjibu.
“Sawa!”
Wakiwa katika mazungumzo hayo, simu ya Chiba ikaita, akainyakuwa na kuitazama, “Madam S!” akatamka.
“Mh!” Gina akaguna.
“TSA 2!” Chiba akaitika.
“HOT! Sikio?”
“Sikio zima,” Chiba akaitikia kwa fumbo.
“Nini kimempata Amata?”
“Amechukuliwa na wanausalama wa AU,”
“Imani…”
“Hatuna!”
“Uelekeo…”
“Cameroon Street, Addis,”
“TSA 1 kwetu ni muhimu kuliko upumbavu mwingine, sitisha kila misheni mhakikishe mmempata kwa gharama yoyote, kisha nipe jibu… ova and out!” Madam S akamaliza.
“Copy!”
Mazungumzo ya Chiba na bosi wake yakakamilika, akamtazama Gina akiingiza gari katika Mtaa wa Cameroon ambako ubalozi wa Tanzania ulipo. Hawakupata shida kuingia ubalozini hapo kwa kuwa walitumia vitambulisho vyao vya uraia na vingine vya kazi ambavyo bado vilificha uhalisia wa kazi yao. Katika ofisi hizo walikutana na afisa mmoja anayefanya kazi ya kuhakikisha usalama wa Watanzania waishio nchini hapo.
“Swala la huyu bwana tunalifuatilia, na nimepata ujumbe kuwa ataachiwa lakini si leo, labda kesho…”
“Shiiiiiitttt!”
“…hata hivyo hivi sasa tunavyoongea anatakiwa kuhamishwa kutoka pale na kupelekwa mahala pengine kuhifadhiwa kwa ajili ya mahojiano zaidi…”
“Noooo! Haiwezekani!” Chiba akaongea huku amesimama, sura yake ilinesha wazi makwinyanzi ya hasira.
“Kwani, ninyi ni nani hasa hata mumtake huyu mtu leo? Kwa sababu sisi tuna utaratibu wetu wa kidiplomasia na kuna taratibu za kufuata ili kumtoa, lakini kwa kesi yake ambayo imefanya akamatwe, tutakuwa na kazi ngumu kumpata kwa sababu yupo chini ya kamati ya usalama ya AU wenyewe…” yule bwana akaeleza vizuri kabisa.
“Sawa, tutakuja kesho ili tujue kinachoendelea…”Chiba akamwambia yule afisa na kupeana mikono huku wakikaribishwa tena.
Nje ya ofisi zile, Chiba akamtazama Gina kabla hawajaingia garini.
“Sasa?” Gina akauliza.
“Sasa ni kumsaka Amata kufa na kupona, na ni lazima tumpate,” Chiba akasema huku akiingia garini, akawasha kifaa chake ambacho humsaidia kujua wapi mtu yeyote wa TSA yupo kwa wakati huo endapo tu bado atakuwasha kifaa chake cha kumuunganisha na wenzake ambavyo huwekwa ama kwenye saa, au simu, ikibidi sana mwilini.
“Gina, fuata barabara ya Airport haraka, naona signal inanionesha huko…” Chiba akasema na mwanamke huyo akakanyaga mafuta kufuata uelekeo aliyoambiwa.
Barabara ya Airport
Mwendo ambao magari haya ya polisi yalikuwa yakitembea haukuwa wa kawaida, njia nzima walitawanyika wao huku gari lile ambalo Amata alikuwemo likiwa katikati. Ndani ya gari hilo Kamanda alikuwa katulia kimya huku akiwasikiliza askari wale wakiwa wanaongea yao kwa ugha ya Ki-Amharic.
Sasa nitawaonesha kama mi ni kauzu na hawatanisahau! Akawaza Amata kisha akautafuta mkojo popote ulipo akajikojolea. Mmoja wa wae polisi akamwona na kumshtua mwenzake.
“Pumbavu sana! Hivi unajua kuwa unachafua gari la waheshimiwa? We Mtanzania wa wapi wewe? Nakutia adabu!” yule polisi akamwambia kwa gadhabu huki akimwendea. Kutokana na urefu wa bodi la gari lile, huyu bwana alisimama bila ya taabu.
“Hakikisha unamwadabisha!” yule mwingine akasema.
Jambo moja pekee ni kuwa hawakujua ni nani wanayemwambia maneno yote hayo. Yule polisi akamfikia lakini kabla hajafanya lolote akajikuta akipigwa ngwala, na ule mnyororo ukamchota sawia akajibamiza kwenye bodi la gari na kuanguka jirani tu na Amata. Katika kuanguka kule, mguu mmoja ukampiga mwingine naye akasukumwa kutoka alipoketi, akasimama kuja kumsaidia mwenzake, akainua kirungu kutaka kumtandika Kamanda. Kwa ustadi wa hali ya juu, alifanya kama anataka kubinukia upande wa pili na miguu ikaelekea juu na kuunasa mkono wa yule polisi naye akavutwa na kujibwaga juu ya mwengine. Kwa kutumia miguu, akambamizia kwa nguvu kwenye chuma la pembeni, jamaa akapoteza fahamu.
Askari yule wa kwanza akajaribu kujiinua lakini akajikuta anapewa pigo la miguu akarudi chini, kimya! Kwa kutumia miguu akachukua funguo zilizokuwa zinaning’inia kwenye huku ya suruari ya mmoja wao akafanikiwa japo kwa tabu sana. Akaikunja miguu yake na kuikamata funguo hiyo kwa kinywa chake akaibana na meno na kujaribu kuzifyatua pingu za miguu, Mungu si Athumani ikafunguka. Kwa kutumia mkono ulio huru akafungua na mwingine, kisha akajifungua na ule mnyororo. Kwa haraka akachukua bastola ya askari mmoja na kufyatua risasi mbili tu moja kwenye sakafu ya gari upande wa kulia na nyingine upande wa kushoto. Ghafla lile gari likayumba na kujibamiza kwenye ukingo wa barabara na kupinduka kama mara tano hivi. Kutokana na kishindo kile mlango wa nyuma gari hilo ukafunguka nah ii ikampa Amata wepesi wa kutoka, ijapokuwa alikuwa na maumivu ya hapa na pale. Alipokanyaga nje akakuta magari ya polisi yamesimama mbele na nyuma yakitazama pande tofauti kutokana na kusimama ghafla. Hakusubiri amri, alichokifanya ni kufyatua risasi na kupiga tanki la gari lile alilokuwamo, mlipuko mkubwa ukatokea na lile gari likanyanyuliwa juu kama unyoya.
Si kwamba alikuwa anajua, bali baada ya kutoka ndipo akagundua kuwa walikuwa darajani wanauvuka Mto Bulbula. Wakati askari wale wakilitazama lile gari, Amata hakujali, alikamata ukingo wa daraja na kuruka hewani kuelekea mtoni umbali wa kama mita ishirini hivi.
“Anatoroooookkaaa!!!!!” askari mmoja akapiga kelele na wengine wote ndipo wakashtuka na kukumbuka walikuwa na mfungwa garini na ndiye aliyesababisha hayo. Haraka, wakaziweka sawa silaha zao na wengine tayari walikwishafyatua upande ule ambako Amata amekimbilia. Wakafika katika ukingo ule na kusimama huku wakielekeza mitutu ya bunduki zao majini, hakuna mtu. Maji ya mto huo yalikuwa yakienda kasi sana, Amata mara tu baada ya kutumbukia aliogelea ka kupiga mbizi na kufanya maadui wake wasimwone.
Dakika kumi zilikuwa nyingi sana, habari zikasambaa kila kona kuwa gaidi lililokamatwa usiku wa jana limetoroka. Habari hii iliwachanganya wanausalama lakini ilimfanya Gina na Chiba kufurahi sana. Wakati huo huo wakawasili eneo hilo na kukuta magari mengi ya polisi yamesimama na kufanya foleni kwa magari mengine. Gina akapunguza mwendo baada ya kuamriwa na askari kisha akaongozwa kuwa apite upande mwingine, naye akafanya hivyo. Baada ya kuliacha eneo hilo na kuvuka daraja kubwa la mto huo, Gina akaegesha gari pembeni.
“Mcheki, tujue wapi yupo tukamchukue,” akamwambia Chiba.
“Ndicho ninachofanya hapa, bado sipati signal vizuri mpaka atakapokuwa eneo zuri,” Chiba akajibu.
“Lazima katorokea mtoni…”
“Na ndiyo njia salama kwa sababu hata waje na mbwa kamwe hawawezi kukupata,” Chiba akamwambia Gina huku akiendelea na kazi yake.
Kule mtoni, Amata aliibuka kama mita 500 mbele hivi, eneo aliloibukia halikuwa na majumba mengi isipokuwa machache ya kifahari yaliyojengwa mbali kidogo na mto. Akajivuta kando ya mto na kuegamia mti ulikuwa jirani huku akitweta kwa kuchoka. Dakika si nyingi akasikia muungurumo wa helikopta, akajua kumekucha.
Wanatumia chopa kunitafuta, wamedhamiria! Akawaza na kuanza kuondoka eneo hilo huku akielekea kwenye yale majumba, hakuonesha kujali kama kuna chopa inayozunguka eneo la mto kumtafuta, aliendelea kutembea taratibu mpaka katika barabara ndogo ambayo ukiiona tu utajua kuwa upita gari moja. Aliposimama hapo akiwa tumbo wazi na suruari iliyotota maji, akaona gari moja jeusi likija upande wake kabla hajaamua afanye nini, gari lile likawasha taa mara tatu na kupiga honi kwa mtindo ambao ulimshtua, akasimama na kulitazama, nalo likasimama miguuni pake kabisa. Hakuuliza, akafungua mlango na kujitupia katika kiti cha nyuma, lile gari likaondoka kasi na kuendelea kuifuata hiyo barabara.
“Pole sana Kamanda!” Chiba akamwambia huku akimpa mkono.
“Usijali Chiba, ndiyo kazi yetu….” Akajibu huku akimtazama Gina anavyopenya kwenye vichochoro ambavyo hata mwenyewe havijui.
“Tuna kazi ngumu Chiba, ngumu sana!” Amata akasema.
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Adui wetu ana macho na masikio mengi, tunaye, tunazunguka naye nay u miongoni mwetu…”
“Sure?”
“Sure, twende chimbo nitakuelezeni mengi, mengi ambayo hata hamkuyategemea, kwa ujumla kazi imeisha…” akasema Amata. Ukimya ukatawala wakati Gina akaiendelea kuongoza kile chombo. Dakika kama arobaini baadae aliegesha lile gari kwenye maegesho ya eneo lile alilooneshwa tangu mwanzoni, wakateremka na kuingia kwa milango ya siri na kuibukia ndani ya jingo lile la misheni ambalo Archimedius aliwahifadhi.
Kama kuna mtu ambaye habari ile ilimchukiza basi ni huyu Bwana Malirekc FikrMaryam, simu yake iliita akiwa ofisini na wajumbe wengine wane wa kamati ya usaalma ya muda na hapa walipoketi walikuwa wakijadiliana kuhusu mtu huyo huyo. Alipoishusha simu, akajikuta kijasho kikimtiririka, akatikisa kichwa kama mtu ambaye kaingiliwa na mdudu sikioni. Baada ya kutulia ndipo akawapa habari ile wengine wote. Kikao haikikuendelea tena, akakivunja na kuwataka wajumbe kuweka ulinzi imara katika hoteli ya Golden Tulip kwani viongozi hao wa juu wa AU wangekuwapo kwa chakula na mazungumzo maalum. Yeye akatoka na kuingia katika gari lake, mja kwa moja akaelekea katika ofisi yake ya siri ambako huko alikutana na vijana wake waliomkamata Amata usiku wa jana yake.
“Hata sisi tumepata taarifa, lakini tunashindwa kujua huyu jamaa katoroka vipi katika gari lile!” mmoja akasema.
“Hilo lisituumize kichwa, cha kufanya sasa ni kuhakikisha anasakwa, popote atakapopatikana akamatwe,” Marilekc alitoa maagizo, “yaani naweza kusema kuwa tuna saa mbili tu tuwe tumemtia mkononi, ninyi mnajua ni wapi mtaanzia upelelezi wenu kumsaka,” akamaliza na kuagana nao, wale vijana wakajipanga kikazi na kuelekea maeneo nyeti katika jiji hilo ambayo kwayo walihisi wanaweza kupata fununu yoyote. Hiki kilikuwa ni kikosikazi maalumu kabisa cha AU katika medani ya kikachero na kilikuwa kinaongozwa na mtu mzima, Marilekc FikrMaryam raia wa Ethiopia ambaye amefanya kazi za kijasusi kwa miaka mingi sana na kubobea kwenye medani hiyo. Katika sakata la mauaji ya viongozi wa Afrika, umoja wa nchi za bara hili ukaona umpe kazi yeye na kumwekea watu wengine kama watano hivi wenye IQ za halia ya juu sana katika chunguzi za mtindo huu ili kumbaini adui, ndipo wakapiga kambi Dar es salaama hasa baada ya kukoswakoswa rais wa Gambiua ambaye ndiye mwenyekiti wa umoja huo.
Ndani ya nyumba ile ya siri ambayo hata ujenzi wake ni wa kumchanganya mtu Amata alifikishwa salama kabisa na Chiba na Gina. Jambo la kwanza alilolifanya ni kuingia maliwato kujisafisha na kisha kujiganga kidogo mwili wake huku Gina naye akiwa jirani kumkanda kwa maji ya moto hapa na pale.
“Fanya haraka Gina, muda umekwisha!” Amata akamwambia.
“Muda umekwisha? Kwani unataka kwenda wapi?” Gina akauliza.
“Kwenda wapi, unafikiri kazi hii imekwisha? Mpaka sasa ninahisi last target ilipo,” akaeleza.
Wanausalama wanajinasibu kuwa Gupter hayupo nchini lakini ukweli ninaokwambia ni kuwa hatan mabosi wake wapo, na mshenzi huyu anaweza kufanya madhara muda wowote tunaoongea hapa…” alipoeleza hayo Gina akaacha kumkanda na kuzunguka akasimama mbele yake.
“Bado unamtaka Gupter?” akamuuliza Amata.
“Yes! Laziamapatikane,” akajibu.
Nusu saa baadae, Amata akwa katika hali ya kawaida, si kwamba alikuwa amepona kabisa ila sehemu kubwa ya mwili ilikuwa imepata afuu, Gina akampatia vidonge vya kutuliza maumivu vyenye nguvu , akameza. Kutoka kabatini akachukua suti mpya kabisa na kujitupia mwilini mwake. Dakika kumi baadae tayari alikuwa Kamanda Amata mwenyewe.
“Sina bastola,” akamwambia Gina naye akamletea mbili na kumkabidhi, akazitazama na kuziweka vizuri, akahakikisha kuna risasi za kutosha kwenye magazine yake, akazipachika katika mikanda maalumu mwilini mwake, akavhukua koti na kuvaa juu yake. Katika sebule ya nyumba hiyo, Chiba tayari alikuwa ndani ya suti, keshavaa, kiwalo cha gharama, akahakikisha ana kila kitu mwilini mwake, nikimaanisha silaha na vitu vingine muhimu.
“Tunapiga ngumi kichakani?” akamwuliza Amata.
“No, katika tafautishi niliyoipata kule kwenye makazi yao, Gupter amejipangia kuua kwa njia mbilia ama risasi au sumu, sasa hapa hisia zangu zinaniambia kabisa kuwa huyu mshenzi atatumia sumu,” akamweleza Chiba.
“Na unajua kuwa hawa jamaa watakuwa wanakusaka kwa udi na uvumba…”
“Achana nao, kwanza wameshaniharibisa hesabu zangu, naanza na Martin Gupter na wenzake kisha nitamaliaza na wao, nitawafata na kuwaumbua bila aibu, nilimsoma Marilekc kwenye kabrasha nililolipata Angola lakni sikumjua kuwa ni huyu mshenzi… yaani AU haijui kuwa imempa kazi kibaraka, kaahidiwa uwaziri siujui unini sijui kama Somalia ikigawanyika, baada ya kuona msimamo wa Madam S ndiye aliyemtengenezea ajali siku ile pale Dar es salaam,” Amata akamwambia Chiba.
“Usinambie! Ina maana yupo kwenye kamati…?”
“Ukisema yupo kwenye kamati unakosea, ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo, yaani yeye anajua hata uwepo wa Gupter na wenzake hapa Addis, na kunikamata mimi jana ilikuwa ni kunifungia ndani ili nisitegue kitendawili chao, mbele ya vijana wake naaminisha umma kuwa mimi ni gaidi, wamenitesa sana ili niwapatie kabrasha la mpango wa mauaji nililolipata Luanda…” akamweleza Chiba ambaye alibaki kimya kabisa pasi na kusema lolote.
“Nipo tayari!” Gina akawaambia na kisha kila mtu akachukua kifaa chake.
Ndani ya gari, Chiba alikuwa akiendesha, Gina alikweti pembeni na Amata siti ya nyuma, safari ya mjini ikaanza. Chiba akatoa kitu kama simu kubwa ambayo juu yake imewekwa kioo kikubwa tu.
“Chukua ditector hii, humu ndani nimeijaza sura ya Gupter, Freddy na yule mwanamke katika mionekano tofauti, ukimhisi mtu we fanya kama unampiga picha tu, ukioanisha, hata kama kajibadili vipi, kifaa hiki kitamtambua tu,” akamwambia Amata na kumkabidhi.
“Hapa umenirahisishia kazi, nakumbuka nimetumia kidubwasha hiki katika lile sakata la Persona Non Grata,” akamwambia huku akikipokea.
“Nimeamua kukupa hicho kwa sababu, Gupter na wenzake wana sifa ya kujibadili sura na ndiyo maana hawatambuliki kirahisi,” Chiba akamwambia Amata huku akizidi kutokomea mjini.
“Sawasawa, na inaonekana wazi kuna ujanja mwingi unafanyika, laiti wangejua… ila leo siri itafichuka, na nitayaanika wazi, huwezi kutumia uzalendo kwa kuficha madhambia yako, tukipeana mikono unacheka, nikigeuka unaning’ong’a…ama zao ama zangu!” Amata akamaliza kusema na kukipachika kile kifaa mfukoni.
XIV
HOTELI YA GOLDEN TULIP
Saa 11:05 Jioni
Magari ya polisi, askari wa kwenye farasi na mbwa wote walijazana kuzunguka hoteli hiyo, ukiachana na wale waliovaa sare za kazi bado kuna ambao walifika hapo kiraia na walikuwa na kazi maalum. Makachero wa ndani na nje walikuwa kwenye shughuli mbalimbal wakihakikisha usalama wa viongozi ambao muda mfupi ulopita walikuwa wameingia ndani ya jingo hilo lenye kila aina ya starehe. Miongoni mwa wageni hao kulikuwa na marais wan chi mbalimbali za Afrika, mawaziri wawakilishi na wajumbe kadhaa achilia mbali waandishi wa habari na wafanyakazi.
Karibu kabisa na jengo hilo kulikuwa na ghorofa jingine refu, juu yake kulikuwa na askari wenye darubini na bunduki kubwa ambazo walizitumia pia kuongeza usalama wa eneo hilo na walaimriwa kuwa yeyote watakayemhisi kuwa ni mbaya basi wasisite kundungua.
Freddy aliegesha gari mbele ya supermarket kubwa ambayo jioni hiyo kulikuwa na watu wengi wakiingia na kutok ukizingatia ilikuwa mwisho wa juma.
“Umeona ee! Yaani hapa kutumia bunduki ni kujimaliza…” Martin Gupter akamwambia Freddy.
“Nimeona jamaa wamejizatiti safari hii…”
“Hata kama, lazima nitekeleze, sikiliza mpango upo hivi, wewe nisubiri nilipokwambia kwa dakika thelathini tu, ikifika ya thelethini na moja sijafika, ondoka tena kimbia usionekane na yale mapesa we tumia uwezavyo…” Martin Gupter akamwambia Freddy.
“Na vipi kuhusu Amanda?” Freddy akauliza.
“Kwa mpango niliyoupanga, Amanda naye atafika hapa dakika tatu kabla na mi pia…”
“Unatumia mbinu gani sasa kukamilisha kazi?” Freddy akahoji.
“Freddy! Muda ni tishu, siri ya kuua anaijua muuaji tu, we fanya nililokwambia,” akamwambia huku akichukua kjikoba chake kidogo na kukivaa kiunoni, lile gari likafunguka katika sakafu yake na kubaki sehemu kubwa wazi, Martin akachukua amtungi mdogo wa hewa safi akauvaa mgongoni kisha akashuka na kuuondoa mfuniko wa chemba ya maji machafu, akaingia ndani yake na kuurudishia vizuri ule mfuniko. Freddy akaondoa gari eneo lile na kuelekea mahala alikoambiwa akasubiri. Tayari mpango mzima wa ramani ya jiji hilo ulifanyika chini ya mwanadada Amanda, ambaye hakuona shida kukupa mwili wake ilimradi tu apate anachotaka. Na safari hii katika jji hili alikuwa na mapenzi mazito na matu mkubwa tu na mwisho akafanikiwa kuiba ramani nyeti ya jiji la Addis’ ambayo iliwaonesha mipangilio yote ya maji taka na maji safi na makazi ya watu na kila aina ya mpango wa mji huo. Isitoshe ilionesha mpaka njia za siri kabisa mabazo mtu mwingine hapaswi kujua. Martin Gupter aliitumia ramani hii kuweza kuifikia hoteli hiyo bila kugundulika na alihakikisha kufanikisha hilo.
Baada ya kutemba katika bomba hilo kubwa la maji machafu alifika eneo ambalo alilihisi kuwa yuko uvunguni mwa hoteli hiyo. Akawasha simu yake ya kisasa na kutazama tena ile ramani ambayo tayari alikuwa ameiweka katika mfum wa simu hiyo, akagundua kuwa hajakosea, ni hapo, akatembea kama hatua nyingine mia moja hivi na kufika mwisho wa bomba moja wapo ambalo juu yake kulikuwa na mfuniko kama ule ule wa kule alikoingilia. Akauvua ule mtungi na kuweka vizuri kisha akakamata ngazi ya chuma inayopanda juu mpaka akaufikia mfuniko, akausukuma taratibu na kuchungulia kama kuna tatizo lolote. Kama alivyoona kwenye ramani ile, hapa alipltlkea ni katikati ya hoteli ile ambapo pana bustani kubwa na nzuri, viti vya kupumzikia na bwawa la kuogelea. Siku hii eneo hili halikuwa na mtu kabisa kwani palifungwa kwa ajili ya usalama, akaingiza mko mfukoni na kuto kamera ndogo iliyopachikwa kwenye kitu kama spoku ya basikeli, akaipenyesha kwenye uwazi huo mdogo na kuizungusha pande zote, akajihakikishia kweli hakuna mtu eneo hilo, akarudisha mahala pake ile kamera na kuufungua ule mfuniko haraka, akatoka na kuufunga, akasimama nje tuli akiwa na mavazi yaliyochafuka uchafu, akavuta hatua na kuingia katika korido mojawapo kisha akapotele katika vyoo vilivyokuwa jirani hapo ambavyo watu hutumia kujisafisha mwili kabla hawajajitupa katika bwawa la kuogelea.
Dakika tano zilimtosha, akatoka akiwa kava suti safi, ya kisasa na ya gharama, sura aliyoingia nayo si aliyotoka nayo, huyu alikuwa Gupter mwingine kabisa. Jambo la kwanza alilolifanya ni kutafuta chumba cha usalama ambacho aliajua kwa vyovyote kama ni kumshuku, basi hawa watakuwa namba moja kwani wanaongoza kamera zote za usalama ndani na nje ya hoteli hii. Lakini bahati mbaya siku hii walikodolea macho zaidi kamera za ndani kwenye sherehe kuliko zile za nje.
Nyuma ya hoteli ile kulikuwa na maegesho ya magari ya wageni na siku hii kulikuwa kumejaa magari mengi sana na zaidi ya walinzi wa kawaida, kulikuwa na askari wengi waliozngira pande zote.
“Mtaingiaje?” Chiba akauliza.
“Usijali hilo niachie mimi!” akateremka na Gina akafuatia, akachukua kifaa chake na kukipachika sikioni, Gina akafanya vivyo hvyo hku na Chiba naye akakipachka cha kwake.
“Signal test!” Chiba akafanya jaribio la kuhakikisha kama vinanasa sauti. Wote wakaonesha alama ya dole gumba wakiashiri kuwa iko sawa. Mlango wa nyuma uliwaruhusu Amata na Gina kuingia ndani ya hoteli hii baada ya kuonesha vitambulisho kuwa ni wafanyakazi wa kitengo cha usalama cha hoteli hiyo. Kwa kutumia ufunguo wake usioshindwa akafungua na mlango ukatoa ushirikiano mzuri tu, wakaingia dani kwa kupitia chumba cha kufulia ‘laudry’.
“Gina, ungana na hawa wadada kwenye huduma ya mezani mimi nitaendelea kurandaranda humu ndani na kuchunguza mtu mmoja mmoja,” Amata akamwambia Gina naye hakujibu bali aliingia ndani ya chumba fulani na kutoka baada ya dakika kumi akiwa na sare za wahudumu na kuanza kusaidia kuhudumia vinywaji na mambo mengine katika meza za wageni huko ukumbi mkubwa. Kamanda Amata aliendelea kutembea kwenye korido hii na ile, akazikwea ngazi na na kutokea ghorofa ya juu ambako huko alikutana na watu wengine wakiwa wametingwa na kazi mbalimbali, hawa walikuwa waandishi wa habari. Kutoka pale aliweza kuona ukumbi wote kwa uzuri kwabisa. Hakuna aliyemjali kwani kil aliyemtazama alikutana na kitambulisho kilichoandikwa, ‘Internal Security-Golden Tulip Hotel Addis Ababa’.
Ni hapo tu aliposimama akiwatazama watu ndani ya ukumbi huo, pembeni yake alikuwapo mwanamke wa kizungu aliyekuwa bize kuandika andika huku kifuani akiwa na kamera kubwa aina ya Ricoh yenye lensi kubwa ya kuona mbali. Amata akamtazama kwa chati na kilichomshtua na kumfanya avutike naye ni alama iliyoonekana kwa mbali kwenye shavu la mwanamke huyu, alama ya jeraha, lakini iliyofanyiwa make up za gharama kuipoteza, lakini kovu ni kovu tu. Mwanamke huyu naye alimwona Amata tangu anaingia lakini hakumgundua na wala hakumjali, kilichomshtua baadae ni jinsi mwanaume huyu alivyokuwa akimtazama kwa chati na kuchezea simu yake mara kwa mara. Huyu hakuwa mwingine, Amanda Keller ambaye ni master plan wa kundi hili na daima hutumia njia ya uandishi habari ili apenye vizuri katika maeneo kama haya.
Kamanda Amata hakutaka kupoteza muda, akaliacha eneo lile na kuteremka ghorofa ya chini kwa minajiri ya kuwa afike katika eneo ambalo angeweza kuwaona watu kwa usahhi zaidi. Akatoa miwani yake na kuivaa kisha akawa anatembea taratibu kufuata korido iliyokuwa ikielekea huko. Miwani ile ilikuwa na kamera ndogo inayonasa picha jongefu na kuzisafirisha mpaka kwenye kompyuta ya Chiba ambako naye anaweza kufanya anayoweza na kuwatambua wale wawatakao.
Martin Gupter, katikati ya wahudumu wa kiume alikuwa akihudumu kama wafanyavyo wengine, tena yeye alionekana kuwa hodari sana katika kutembeza chano cha vinywaji. Kwa jinsi alivyojibadili sura yake ingekuwa vigumu kumgundua kuwa yeye ni Mzungu, hakuwa mbali na sura za kihabeshi, hakika alikuwa Muethiopia haswa.
Baada ya kama nusu saa hivi, Martin alikuwa tayari keshayasoma mazingira yote, tabua na yendo za watu. Alipomaliza kugaw avinywaji na kumjua ni nani aliyeandaliwa kwa ajili ya kuhudumia meza kuu tu.
Namtumia huyu huyu! Akawaza huku akiuacha ukumbi wa tafrija na kueleakea katika chumba maalumu ambacho ndiko hupatiwa huduma hizi. Martin Gupter aliitazama saa yake na kuona wazi muda ukiyoyoma kupita kawaida, akawaza na kuwazua kwa nini alifikiri kuwa kazi hiyo angeweza kuifanya kwa muda mfupi, hakupata jibu.
Maadam nimeahidi, sina budi kutekeleza! Akajisemea moyoni mwake, hakuna aliyemsikia zaidi ya kujisikia yeye mwenyewe.
“Martin, Time is up!” sauti ya Amanda ikamfikia masikioni kupitia kifaa kidogo mno ambachjo alikitumbukiza sikioni.
“Yes I know, and now im goind to accomplish the tasks!’ Ndiyo najua, na sasa ninakwenda kukamilisha zoezi,” akamjibu.
“Kuna sura sina imani nayo humu ndani, chukua tahadhari,” Amanda akasema tena.
“Tahadhari zote zi mkononi mwangu, jiandae uliache eneo lile,” Martin akamwambia Amanda, naye akasikia vyema. Kutoka kule juu, Amanda akaanza kujiweka sawa tayari kwa kuondoka.
kifaa cha Amata kikampigia alarm akakitoa na kukikamata kiganjani mwake, akatupia jicho kwenye kioo na hapo ndipo mapigo ya moyo yakabadili uelekeo. Akiwa pale juu ambapo alifika mara ya kwanza, alimpiga picha mwanamke huyu, picha ya wizi na sasa kile kifa kilikuwa kikifanaya crosssmatch ya picha za mwanamke huyo.
Amanda Keller! Akasoma jina la mwanamke huyo na mambo mengine mengine, hakusubiri sekunde wala nukta, akabadili uelekeo na kurudi kupanda tena zile ngazi kwa minajiri ya kumtia mkononi mwanamke yule. Kamanda Amata akiwa katika harakati hiyo akatoa taarifa kwa swahiba zake; yaani Gina na Chiba kuwa wachukue tahadahari kuhusu mwanamke huyo na waweke macho yao kodo ili kujmwona kama atajaribu kutoka tika jingo lile kwa njia nyingine. Ghafla akaibukia katika eneo lile la mwanzo, ambapo kulijawa na waandishi wa habari kutoka mashirika mbalimbali. Akasimama na kuangaza macho, mwanamke yule hakuonekana.
Wameniweza, kaeda wapi? Akajiuliza na kuanza kuteremka ngazi zile kwa haraka sana, mara hii hakuwa na sehemu nyingine za kwenda zaidi ya chumba cha usalama ambacho kina luninga nyingi zinasoonesha picha kutoka pande tafauti za hoteli hiyo. Alipoufikia mlango, umefungwa, akautikisa, umefungwa. Akatazama huku na huku asione mtu wa kumhofia, akachukua funguo zake na kuzitumbukiza kwenye tundu la kitasa hicho akazungusha kama mara nne hivi na mlango ukafunguka. Amata akajitoma ndani, lakini ghafla akasimama na macho yake yakatua juu ya miili miwili ya vijana wafu. Akachomo bastola yake na kurandaranda ndani ya chumba hicho, hakuna mtu, akatazama vyema miili ya watu wale na kujiridhisha kwa macho kuwa hawana uhai.
Martin Gupter! Akawaza na kuiridisha bastola ile haraka kiunoni akafunga mlango kwa ndani na kuiendea luninga moja wapo na kutazama matukio kadhaa hasa alitaka kuona nani alikuwa wa mwisho kuingi ndani ya chumba hicho. Baada ya kurudisha matukio nyuma kama dakika kumi au kumi na tano hivi ndipo akamwona anayemtaka. Kijana wamakamo, aliyevalia sare ya wahudumu wa hoteli hiyo, picha ikamwonesha akiingia na kuanza kuwashambulia mpaka kuwaua, kisha ikamwonesha akichakurachakura kwenye baadhi ya picha za siku hiyo, Amata akajua tu kuwa bila shaka alikuwa akifuta matukio kadhaa yanayomhusu yeye. Kamanda Amata akachukua flashi yake na kuipachika kwenye kompyuta nyingine na kuanza kunakila mienendo yote ya siku hiyo, aliporidhika akainyakua na kuitia mfukoni kisha akatoka ndani ya chumba kile, akafunga mlango kwa nje na kukivunja kitasa akitaka mtu asiingie kirahisi ili yeye apate muda wa kumsaka huyo hayawani.
Martin Guter hakutaka kupoteza muda, akaingia katika chumba ambacho vinywaj na vyakula mbalimbali vimehifadhiwa haswa kwa wageni maalumu. Hakuzuiwa kwa kuwa alishahabiana kabisa na wahudumu wa hoteli, na pia kwa kuwa alikwishaingia ndani ya chumba hicho kama mara tatu kama si nne. Ndani humo alijuwa wazi ni chano ipi na chakula gani ambacho kitachukuliwa na kupelekwa mezakuu. Akajifanya akiongea na wahudumua wengine huku akimimina vinywaji vikali katika bilauri. Hapa ndipo akafanya kile anachotaka, akatoa kijichupa kidogo cha pombe kali, lakini ndani yake kulikuwa na sumu mbaya inayoua kwa dakika thelathini tu kama aliyetumia kachelewa hospitali.
Baada ya kuhakikisha bilauri zote sita keshazifanyia hujuma hiyo, akabadili na chano chake kisha akachukua kingine na kuendelea na kazi ya kupelekea vinywaji. Askari waliokuwa mlangoni waliendelea kuweka ulinzi bila kujua kuwa muuaji anawapita kuingia na kutoka. Ni dakika hiyo hiyo ambayo Kamanda Amata alikuwa akipita kwenye korido hiyo na kukutana macho kwa macho na Gupter, akahisi vinyweleo vikimsimama tangu mbali, haraka aakachukua kile kifaa chake kama simu na kuanza kujifanya akiandika jambo fulani kumbe alikuwa akimpiga picha kijana huyo.
Martin Gupter naye alipomwona Amata akahisi kama anataka kuzimia, hakuamini kama anayemwona mbele yake ni yeye au kivuli wakati kichwani ana kumbukumbu kuwa mpelelezi huyo keshakufa zamani sana kule Waterloo. Almanusura amwage vinywaji lakini akajikaza, hali hii Amata aliigundua, akana wazi kuwa kuna kitu hakiko sawa. Akamtazama kwa nyuma akitembea na kuufananisha mwendo wake na sehemu tatu tu ambazo alimwona kwa karibu.
Ni yeye! Akawaza, na wakati huo akaufikia ule mlango ambao nje yake kulikuwa na ulinzi mkali. Alipofika alikuta kuna hekaheka ndani yake, kijana mmoja akiwa chini akitokwa na povu huku wenzake wakihaha kumsaidia. Kamanda hakuuliza, akaingia haraka na kujichanganya kusaidia.
“Nini kimetokea?” akamuuliza mmoja wa wahudumu.
“Hatujui, amekuywa tu kinywaji hicho kwenye glass mara akaanguka na hali ndiyo hiyo!” Amata akajibiwa, akainuka na kutazama huku na huku asione mtu wa msaada. Akaingiza mkono mfukoni na kuto kijichupa kingine cha plastiki ndani yake kulikuwa na vidonge kama kumi hivi akatoa kimoja na kwa nguvu za ziada wakambana mpaka akaachama kinywa na kukitumbukiza kile kidonge. Amata akamwacha na kuwaambia wahakikishe hakitemi. Akafika mlangoni na kuwapa amri wale askari kumtafuta yule kijana. Nao wakajikuta wakichanganyikiwa wasijue cha kufanya, akachomoa bastola yake na kutoka kasi kueleke ukumbi mkubwa.
“Martini Gupter yupo hapa, kila mmoja akae tahadhari sasa!” akasema, na taarifa ile ikamfikia Gina na Chiba.
“Copy!” akajibiwa.
Wakati Amata anafika katika ukumbi mkubwa, kwa kuwa alikuwa katika mwendo wa kukimbia walinzi wenye nguvu wakamdaka kabla hajaingia. Akatumia nguvu kujikwamua lakini akajikuta amebanwa na mikono mine yenye nguvu za vice.
“Poisssoooonnn!!!” akatamka kwa nguvu, lakini wale jamaa ndiyo kwanza wakambana barabara huku askari wengine wakielekea eneo hilo. Wakati wote huu Gina alikuwa upande wa ndani wa ukumbi huo na aliliona tukio hilo, akashindwa nini cha kufanya, baada ya kusikia neno ‘poison’, akili yake ikafanya kazi haraka sana na kutazama meza ya wakuu yule mwanadada tayari alikuwa akigawa vinywaji kwa waheshimiwa. Kutoka aliposimama alikimbia kwa hatua ndefundefu na kumfikia mwanadada yule, hakuna muda wa kuzungumza bali kumnyang’anya ile chano na bilauri zote zikamwagika na kuvunjika, tafrani.
Amata kutoka katika mikono ya watu wale wenye nguvu, alimwona Marilekc FikrMaryam akiwa jirani na kutoa amri kuwa wamkamate barabara. Hii ni kauli ambayo ilimtia hasira, kwa nguvu zake zote akajitutumua na kuwasukuma kando wale jamaa, wakapamiana na kuanguka kisha akawaruka huku bastola yake bado ikiwa mkononi. Akiwa hewani mmoja wa walinzi akajaribu kumshika mguu na kumkosa, Amata akaangukia ukumbini na kubiringita, alipokuja kuinuka na kupiga goti, akaweka bastola sawa na kufanya shabaha ya maana, akafyatua risasi mbili, ni yeye tu aliyemwona Martin Gupter wapi kasimama. Wakati Amata akifanya hayo yote, Martin Guter alijua wazi mbinu yake haiwezi kufaulu, kwa kutumi bastola yake akafyatua kabla ya Amata, na lengo la risasi ile lilikuwa ni kummaliza rais wa Gambia ambaye pia ni mwenyekiti wa AU. Lakini kwa hekaheka zile, risasi ikampata yule mwanadada aliyekuwa akigawa vinywaji naye akaanguka chini kama mzigo huku akitoa yowe la mauti. Walinzi wa marais wote wakawa macho tayari wakawawekea ulinzi wakuu wao na kuanza kuwaondosha ukumbini.
Amata akaanza kumfuata Gupter kwa mbio, kijana huyo alipoona kuwa njia zote zimebana, akajitupa kwenye kioo na kukitawanya vipande vipande na kuangukia nje. Amata naye akapita hapo hapo na kujikuta chini, akatzama huku na huku na kumwona Gupter akiingia kwenye gari moja wapo hapo maegeshoni. Naye akatazama huku na huko, akachukua pikipiki moja kubwa la polisi lililokuwa limeegeshwa hapo. Akwapa taarifa Gina na Chiba kuwa anamfukuza kiumbe huyo, nao akawapa kazi kuhakikisha Freddy na Amanda wanapatikana. Katika barabara hiyo Amata alipiga king’ora na magari yakaacha njia akaendelea kumtimua Gupter huku nyuma yake magari mengine ya polisi nayo yakija kwa kasi. Martin Gupter akakanyaga mafuta na gari lile lilikuwa likienda mwendo kichaa, likikata kona za hatari mpaka bodi inasugua barabara, huku bado akitafuta njia ya kumlenga Amata. Alipoona shabaha zote ni ngumu akawa amekaribia kabisa na wapi ambapo Fredy ameegesha gari, akajua sasa hapa ni kufa na kupona hakuna njia nyingine. Akafunga breki za ghafla na pikipiki la Amata llikagonga nyuma ya gari hilo. Kamanda akapaishwa juu na kutupwa mbele, akaanguka vibaya lakini kwa uzofu wake akajitahidi kutua kwa usalama, haraka akachomo bastola yake na wakati huo Martin Gupter alikuwa keshaliacha gari lile na kuingia katika lile la Fredy.
Freddy akaonesha umahiri wa kucheza na gari, akalizungusha na kusugua barabara kiasi kwamba moshi unaotokana na msuguano huo ukawachanganya polisi na magari yao yakagongana ovyo. Lakini haikuwa hivyo kwa Amata. Yote yakitukia, bastola yake ilikuwa mkononi na alipoona zile kelele zimetuli na gari likijitokeza katikati ya moshi kuja kwake hakuchelewa, akafyatua risasi ya kwanza, ya pili kisha yeye akaruka sarakasi na kutu upande wapili lile gari likapita kasi na kuacha njia likaenda kugonga mgahawa na kuingia mpka ndani. Risasi ya pili ya Amata ilizama katikati ya paji la uso la Freddy, hakuwa na ujanja, roho ikaacha mwili, gari likagonga mgahawa.
Martin Gupter akajitokeza nje ya mgahawa huo akipiga risasi ovyo na kujeruhi askari kadhaa, wakati askari wale wakitaka kumshambulia, amri ikasikika wamwache, Amata akatazama na kumwona Marilekc, hakujali, alivuta hatua na kuruka hewani kisha akagtua miguu miwili kifuani mwa Gupter na kuwenda na ye chini. Martin akainuka haraka na kumuwahi Amata kabla hajainuka, akarusha teke, Amata akaliona na kuudaka mguu kisha akauzungusha lakini kijana huyo akawa amjanja, akaruka heani na kujigeuza kisha akatua chini kwa miguu miwili na kujikunja kujiweka sawa kwa mapigano. Amata akasimama na kujifuta damu iliyokuwa ikimtoka juu ya jicho baada ya kupasuka alipoanguka barabarani.
Mapigo ya Gupter yakamfikia bila kizuizi, kila alipojaribu kujikinga akashindwa na kuanguka upande wa pili, uso wake ukakutana na wa Marilekc, akaliona tabasamu baya na dhalimu la mtu mzima huyu. Kamanda akainuka kama mbogo, Gupter alipojaribu kupelekea tena mapigo akakuntana na kigingi. Kamanda Amata aliyapangua mapigo yote na kisha akaanza kumtandika kwa mapigo ya kifo. Pigo moja zito likamvunja mbavu, Gupter kabla hajakaa sawa, akatandika pigo jingine kwenye uti wa mgongo likatengua pingili, akapewa la tatu lenye ujazo wa kilo za kutosha liakavunja mifupa miwili ya bega.
Marilekc alipoona Gupter anazidiwa, akatoa amri Amata akamatwe, akachelewa kwani kamanda aliijua hila yake, akamweka sawa Gupter na kumtandika pigo moja maridadi lililomzungusha mpaka na kumbwaga chini akiwa kinyume na sura yake, ulimi nje.
“Mwisho wa udhalimu wako umefika Marilekc, jina lako lipo kwenye mpango wa mauaji ya viongozi wetu ambao mimi mwenyewe nimeupata kule Angola. Hivi ninavyoongea vibaraka wenzako wote wamekamatwa kuanzia mjinga mwenzio Fernandes Pereira wa Angol ambaye mpango huu wewe nay eye pamoja na Ambasador Bilhani wa Tanzania mliuficha kwenye kisiwa cha Ilha Da Canzaga, mlifikiri siri haitafichuka?” Amata akazungumza kwa jaza huku mwili wa Gupter ukiwa chini na mwanamke Amanda Keller akiwa tayari kapigwa pingu na kuwekwa katika gari maalumu la wahalifu sugu, Freddy yeye aikuwa wa kwanza kukata roho kwa risasi ya Amata. Kamera za waandishi na vipaza sauti vilikuwa vimemzunguka Amata na mbele yake mtu mzima Marilekc alikuwa akimiminika jasho.
“Mwisho wa ubaya aibu, Somalia kugawanywa mara mbili ingekusaidia nini wewe? Ukamfanyia ajali Madama Selina ili upoteze ushahidi? Basi utakaa jela na kushuhudia wenzako wakifaidi maisha duniani,” akamliza na kupita katikati ya waandishi huku wengine wakitaka kumhoji na picha kadhaa zikipigwa.
Kamanda Amata baada ya hatua kadhaa mbele, akageuka nyuma na kumwona Marilekc bado amesimama palepale, akawageukia polisi na kuwaambia.
“Arrest that man!”
Wale askari wakamfuata kwa minajiri ya kumweka chini ya ulinzi mzee huyo aliyekuwa akiaminiwa na kila mmoja katika medani za usalama. Lakini hawakuhai hata kumfikia, mzee yule akachomoa bastola na kujididimiza kinywani, sekunde hiyo hiyo akafyatua na kujifumua kichwa chote kwa risasi moja tu, akaanguka chini.
Kamanda Amata akashtuka na kugeuka nyuma akamkuta ndiyo anafika chini kama kiroba cha pumba.
“Magnum 22,” akasema huku akitikisa kichwa. Kamanda Amata alikuwa na kipaji cha pekee cha kutambua aina ya bunduki kwa kusikia mlio tu pindi ikifyatuliwa. Gina na Chiba waliwasili katika eneo la tukio na moja kwa moja wakamchukua Amata na kumwingiza garini lakini. Mkuu wa polisi wale aliwafuata na kuwataka kumwacha kwani hata huyo ni mhalifu tu.
“Una uhakika na unachokisema?” Gina akamuuliza na kumwonesha kitambulisho na Chiba akafanya vivyo hivyo. Yule mkuu wa polisi akagwaya na kuwaomba tu kufika kituoni ili kuweka maelezo sawa. Amata, Chiba, Gina wakaingia garini na kuondoka eneo hilo pikipiki moja likiwasindikiza.
Na huu ndiyo ukawa mwisho wa Martin Gupter, muuaji wa kukodi aliyeinyanyasa dunia, kila kona alitafutwa asipatikane mpaka wengine akadhani kuwa ni shetani na si binadamu. Ama kweli za mwizi ni arobaini, yeye na genge lake wote walijikuta wakitumia mbinu mbovu iliyowagaharimu maisha yao nah ii ni kwa sababu waswahili husema akili nyingi mbele kiza.
TAMATI
Also, read other stories from SIMULIZI;