Fedheha Sehemu ya Tatu
MAISHA

Ep 03: Fedheha

SIMULIZI Fedheha
Fedheha Sehemu ya Tatu

IMEANDIKWA NA: GEORGE IRON MOSENYA

*********************************************************************************

Simulizi: Fedheha

Sehemu ya Tatu (3)

SIKU MBILI BAADAYE!!!!

Nikiwa bado sijaamua kujionyesha mbele ya mtu yeyote yule. Na nikiwa na namba ya simu ambayo aliitambua Geza peke yake baada ya kuiondoa hewani ile namba nyingine, mara niliisikia simu yangu ikiita. Kwa sababu kuna kipindi nilikuwa nmafuatilia kwenye runinga nilipuuzia kuwahi kuipotea!!

Ilipoanza kuita mara ya pili nikainyakua na kuiweka sikioni.

“Upo chumba kilekile!!” ilikuwa sauti ya Geza akiniuliza. Nikakubali.

Simu ikakatwa, baada ya dakika kama thelathini hivi nilisikia hodi.

Kufungua alikuwa ni Geza, alikuwa natabasamu pana usoni wakati anaingia.

Akarusha bahasha kitandani pale!!

Nikaichukua na kumuuliza iwapo ile bahasha ilikuwa inanihusu.

Akaniruhusu kwa ishara kuwa nifungue.

Nikaifungua vyema, na hatimaye ikafunguka kabisa.

Ndani ya ile bahasha kulikuwa na picha za harusi.

Harusi ya mke wangu!!

Sio sura ya mke wangu iliyonivuta, bali ndani ya ile bahasha kuna picha niliiona!!

Ni picha ya yule mwanaume ambaye naye picha yake niliwahi kuikuta katika makablasha ya mke wangu kabla hayajatokea haya ya kututenganisha.

Kuna kitu!!!

Nami nilikiri!!

“Huyu ndiye mume wake ama?” niliuliza swali la kizembe nikitegemea jibu jepesi tu.

“Wala sio mumewe ila namfahamu huyu bwana vizuri sana, na kama kweli na yeye yumo katika huu mchezo. Bwana mdogo unatakiwa upige moyo konde!!!

Ndani ya ile bahasha kulikuwa na picha za harusi.

Harusi ya mke wangu!!

Sio sura ya mke wangu iliyonivuta, bali ndani ya ile bahasha kuna picha niliiona!!

Ni picha ya yule mwanaume ambaye naye picha yake niliwahi kuikuta katika makablasha ya mke wangu kabla hayajatokea haya ya kututenganisha.

Kuna kitu!!!

Nami nilikiri!!

“Huyu ndiye mume wake ama?” niliuliza swali la kizembe nikitegemea jibu jepesi tu.

“Wala sio mumewe ila namfahamu huyu bwana vizuri sana, na kama kweli na yeye yumo katika huu mchezo. Bwana Khalfani unatakiwa upige moyo konde!!!

GEZA alinitazama kwa muda wa sekunde kadhaa kisha akaniomba nisimame.

Nikasimama upesi wima kabisa!!

Geza akatokwa na tabasamu kisha akanisogelea na kunitazama usoni.

“Wewe ni mwanaume dogo walau naweza kukuamini na kukueleza mambo mazito!! Watoto wa kike ukiwaambia simama anakuuliza nisimame kwanini? Hajui kuwa kuna kipindi anakuwa yupo jirani na bomu unamwepusha na kifo chake ule muda wa kuuliza anajikuta anapata jibu lake akiwa jehanamu ama ahera!!” Geza alinieleza huku akinionyesaha ishara ya kuketi.

“Samahani naomba nivute sigara.. najua wewe sio mvutaji lakini naomba nivute ili twende sawa!!” Geza aliniomba huku akitoa pakiti ya sigara.

“Kwani hauwezi kungoja kidogo Geza au uende kuvuta nje kisha urejee….” Nilimsihi kwa sababu sikuwa na urafiki na moshi wa sigara hata kidogo.

Geza akacheka sana huku akinisogelea na kisha kunikumbatia kwa nguvu.

“Wewe ni mwanaume dogo. Mwanaume kamili kabisa sema mapenzi tu ndo yanakulemaza na kukupunguzia asilimia. Nimependa sana mtazamo wako….. hakuna kukubali kupelekeshwa hovyohovyo!! Eti kisa tu mtu anahitaji kukusaidia…. Wanawake wakishasaidiwa huvua nguo zao upesiupesi wakidhani ile ndiyo asante inayostahili. Hakuna watu wasiojua mapenzi kama wanawake…. Wewe ni mwanaume halisi dogo”

Akairejesha sigara yake na kisha akaketi!! Na hapo akaitoa picha nyingine.

“Mtazame huyu mwanamke usoni…” aliniambia, nikaichukua ile picha na kutazamana ana kwa ana na sura ya mke wangu akiwa yu katika vazi la shera (shela). Moyo ulipiga kwa nguvu sana nikatamani kuzungumza lakini sikujua ni kitu gani sahihi kuzungumza kwa wakati ule.

“Khalfani unaona kitu gani katika picha hii, niambie mambo matatu muhimu ambayo umeyaona. Weka mapenzi kando kwanza wakati unatoa majibu!! Maana mapenzi huleta majibu ya uongo ilimradi tu kujiridhisha” Geza ulole aliniuliza huku akiwa anatabasamu. Kauli za Geza ziliyakosha masikio yangu na kuuburudisha ubongo wangu, hakika nilikuwa nimekutana na kichwa!!!

Nilitumia sekunde chache sana kutambua jambo.

Latipha alikuwa anajilazimisha kutabasamu, na ukumbi huo wa harusi haukuwa na watu.

Nikampa majibu yale Geza!! Kwa mara ya kwanza tabasamu likatoweka katika uso wake. Nikahisi nimemjibu vibaya!!

“Dogo ni wewe ama baba yako amewahi kuwa jambazi ama mpelelezi??” aliniuliza. Sikujua alikuwa anamaanisha kitu gani.

Tabasamu lake likarejea tena upya!!

“Bwana mdogo una kitu fulani spesho!! Una akili sana.” Akasita kidogo kisha akaendelea, “Mdogo wangu, mkeo, aah! Ama niseme aliyekuwa mkeo hana furaha katika kila kitu ambacho kinaendelea katika maisha yake, lakini kubwa zaidi kuna kitu kimepangwa. Kuna mchezo umechezewa dogo. Dawa ya kuchezewa ni wewe pia kuchezea. Lakini unapoamua kuchezea uwe unajua kweli kuchezea sio uwe unajifunza kuchezea, itakugharimu ni heri uache kabisa kuchezea kuliko kujifunza kuchezea!!” alimaliza Geza kisha akanitazama usoni kama anayenisubiri maneno yaniingie ili aweze kuendelea.

“ukiwa kama kijana mwenzangu tena umri wako mdogo naomba utambue kuwa duniani kuna akina Latipha wengi tu, hivyo uamuzi ni wako sasa kumtafuta Latipha mwingine muendelee na maisha ama kumchukua tena Latipha wako…. Hivi kwani kanuni za ndoa zipoje katika dini yenu maana mi sina dini si unasikia hata jina langu….” Alimaliza Geza huku akitabasamu.

“Sasa kaka ninamchukuaje Latipha wakati ameshaolewa?” nilijikuta nikiuliza kwa sauti ya kukata tamaa.

“Hah! We dogo vipi mi sijakwambia umchukue nimekwambia hivi kina Latipha wapo wengi, au kesho nikuletee Latipha mpya uoe fastafasta…” Geza alinihoji kimasihara huku akicheka.

“Namtaka Latipha wangu kaka…” nilimweleza kana kwamba ni yeye aliyekuwa akimshikilia.

“Kamchukue nenda ukamchukue….” Alinijibu Geza huku akitabasamu tena. Kisha akaendelea tena, “dogo, huyo bwana niliyekuonyesha picha yake ni mwekezaji kutoka nje ya nchini, mara yangu ya mwisho kwenda jela, sikumbuki kama ni Segerea ama Keko tulifanya wizi katika duka lake la simu tulikomba kila kitu, sema kuna mjinga mmoja akatuchoma, nikaloweshwa mvua sita jela. Jamaa yupo vizuri sana, na kwa jinsi ninavyomuona mkeo hapa hata kama hajatabasamu lakini mbona msichana wa kawaida sana huyu dogo. Kibosile kama huyu wanaanza vipi kuwa na urafiki” akasita kisha akaanza kucheka na kisha akaendelea kuongea, “Sasa dogo, huyu mkeo naye chizi mbona kifutu hivi halafu akakwambia eti anataka kugombea umiss…..” kicheko kikamzidia akacheka hadi akaketi chini.

Nilijikuta Napatwa na hasira, japokuwa aliyokuwa anayasema ni kweli lakini ni kama alikuwa akimdhalilisha mke wangu.

“Geza… naomba umuheshimu mke wangu tafadhali..” nikamuonya kidogo nikiongozwa na hasira.

“Mke? Mke yupi dogo, yaani kumbe dogo unaye mke halafu umenipotezea muda wangu mimi kuja huku kukusaidia sijui mavitu gani, yaani kweli umefikia dharau ya kiwango hicho?” Geza alinifokea katika namna ya kunidhihaki. Hasira ikanipanda nikajiapiza kuwa akithubutu tena kumsema mke wangu vibaya ama zangu ama zake palepale chumbani!!

Na mara ghafla akawa mtulivu!!

“Wewe ni mwanaume sana dogo!! Mwanaume thabiti, unaweza kuizuia hasira yako…. Safi sana. Mwanaume kamili anaweza kuongoza hisia zake….”

Dah! Laiti kama angejua kuwa nilikuwa nimekasirika kiasi cha juu kabisa wala asingenipa sifa zile lakini nilifarijika sana kama ni mtihani nilikuwa nimeshinda.

“Mdogo wangu mimi nipo mbali na mapenzi… naishi peke yangu nyumbani kwangu, siamini marafiki na mbaya zaidi siamini mapenzi. Ila ni kama damu yangu na yako imevutana. Nimejisikia kuivua suti hii niliyovaa, kuvivua viatu hivi na kisha kuvaa tena pensi kama ile uliyoniona nayo jijini Mwanza tukiwa mahabusu na kisha niingie kazini. Kiukweli naupenda sana huu mchezo wa vuta nikuvute japo ni mchezo wa hatari. Dogo nitaingia katika hii hatari kwa ajili yako, lakini sitaingia peke yangu…. Nitaiandaa njia kwa ajili yako. Tutaingia wote…… huwezi kujua tunaweza kuibuka mashujaa lakini usijisikie fedheha iwapo turtazidiwa mbinu na kuangukia pua.” Geza ulule alimaliza kuzungumza katika utulivu wa hali ya juu.

Ile kusikia neno kuangukia pua nilijikuta katika tafsiri nyingi sana, ikiwa tutashindwa katika hiyo vita basi kuna asilimia kubwa za kuishia gerezani.

Gerezani kisa mapennzi au??

Haya labda tuseme kuwa haitakuwa gerezani, je ikiwa mbaya zaidi tuishie kufa? Ah! Huenda mwenzangu ameshazoea kufa….. aah! Mi naye sasa mtu anazoeaje kufa wakati hajawahi kufa??

Yaani nife nikiwa na miaka 24 dah! Mbona mapema sana halafu kisa mapenzi.

Ila niwe muwazi Khalfani mimi naishuhudia kwa silimia zote nafsi yangu kuwa inampenda Latipha kwa dhati na timamu zote.

“Nasubiri jibu lako dogo” Geza alikoroma na kunitoa katika mawazo yale.

“Namtaka Latipha wangu….” Nilijibu kwa kukurupuka.

“Kesho saa tano na nusu usiku, tukutane ukumbi wa sinema wa Quality center, kuna filamu ya kiswahili inazinguliwa pale jitahidi kuingia saa tano na nusu… safari yetu itaanzia hapo. Uwe na usiku mwema dogo…”

Geza hakungoja jibu lolote. Akatoweka pale na kuniacha kinywa wazi nikijiuliza huyu ni mtu wa aina gani….

Nililala nikiwa sijapata jibu ikiwa uamuzi niliochukua ni sahihi ama si sahihi.

Sasa kwa nini iwe saa tano usiku, huyu jamaa wa ajabu kweli. Kwenye filamu ananipeleka mimi kufanya nini.

Nikalala bila majibu….

Asubuhi nikashtuka majira ya saa tano, ni kama muda uleule tulioahidiana lakini hii ilikuwa saa tano asubuhi.

Niliuweka mwili wangu safi kisha nikatoka kwenda kupata stafutahi! Nikajizungusha huku na kule.

Majira ya saa tatu usiku nilikuwa jirani kabisa na eneo la tukio, nilitazama kweli kama kuna uzinduzi wa filamu ya Kiswahili. Hapakuwa na kitu kama kile eneo lile.

Nikajiuliza ikiwa Geza alifanya makosa kutoa miadi siku ilea ma vipi maana kwenye ratiba hakikuwepo alichokuwa ameniambia!!

Sikutaka kuhoji kwenye simu, nilibaki pale kumngoja aje yeye mwenyewe niweze kumuhoji juu ya ahadi yake.

Hatimaye ikafika saa tano na nusu!!

Sikuamini hata kidogo kilichotokea!!

Ama kwa hakika Geza Ulole kilikuwa kichwa kingine!! Kichwa kisichokuwa cha kawaida hata kidogo!!

Hatimaye ikafika saa tano na nusu!!

Sikuamini hata kidogo kilichotokea!!

Ama kwa hakika Geza Ulole kilikuwa kichwa kingine!! Kichwa kisichokuwa cha kawaida hata kidogo!!

Geza alifika pale akiwa na tiketi mbili. Akanipatia tiketi moja kisha akaanza kutembea nami nikimfuata nyuma. Hakuwa katika vazi la suti tena bali alikuwa amevalia pensi pamoja na fulana iliyombana haswa!! Na kukifanya kifua chake kilichovimba kiasi kuonekana vyema.

Tuliingia mlango ulioandikwa namba nne. Kiyoyozi mwanana kikatupokea. Taa ya ndani ilikuwa bado inawaka kumaanisha kuwa bado filamu ilikuwa haijaanza, Geza aliendelea kuwa mbele na mimi nyuma kama mkia. Hapo hata hatujasalimiana!!

Akakifikia kiti na kuketi na mimi nikakaa kulia kwake.

Nikapata fursa ya kumtazama kidogo, alikuwa anatabasamu kama ilivyo kawaida yake!!

Kutabasamu kila wakati, Geza bwana!!

Baada ya dakika mbili hivi, taa zilizimwa kumaanisha kuwa filamu inaanza rasmi!!

Naam! Kweli filamu ilianza rasmi.

Geza akatoweka bila kuniaga, sikumuuliza nikaendelea kungoja.

Baada ya muda akarejea akiongozana mtu ambaye alikuwa amevaa suti sikuweza kuiona sura yake kutokana na hali ya ugiza pale ndani.

Geza na yule bwana walikaa mbali kidogo na mimi.

Sikujitia kimbelembele nilitulia nikitazama filamu ya kihindi iliyokuwa ikiendelea na wakati huo nikijiuliza Geza alikuwa anamaanisha nini kunieleza kuwa kuna filamu ya Kiswahili ilikuwa inazinduliwa.

“Dogo…. “ niliisikia sauti ya Geza ikiniita.. nikageuka na kukuta akiniita kwa ishara ya mkono niende mahali alipokuwa ameketi.

Nikasogea hadi pale akaniambia niketi, hivyo tukawa tumemuweka mtu yule kati.

Naam! Nikapokelewa na harufu ya marashi, marashi ambayo haikuwa mara ya kwanza kupita mbele ya pua zangu!! yale marashi ambayo nilimkuta mke wangu akinukia siku ile.

“Naam bwana mkubwa kama nilivyokwisha kukueleza hapo kabla kuwa nipo na mwenzangu katika dili hili. Nd’o huyu hapa anaitwa Khalfani, sijui kama unamfahamu, ni mtu maarufu kiasi aah! Sio kiasi ni mtu maarufu sana tu….” Geza alizungumza na yule bwana.

“Aaah! Hapana sijawahi kumsikia kwakweli. Halafu umesema upo naye katika dili gani, we si ulise….” Kabla hajamaliza nilimshuhudia Geza akimsogelea yule bwana kisha akamjaza ngumi kali ya mbavuni na hapo akamziba mdomo na kumuegemeza kwenye kiti kana kwamba hakuna kitu kilichokuwa kimetokea!!! Ule ugiza wa mle ukumbini hakuna ambaye angeweza kutambua kinachoendelea!!

Na ile kelele ya filamu iliyokuwa inaendelea, Sauti haikutoka hata kidogo, kwanini nisite kusema Geza alikuwa kiumbe mwingine.

“Sikia kiongozi sio kila dili lazima uambiwe kwa majina, hili dili huwezi amini halina jina hadi sasa unavyotuona hapa!!” Geza alizungumza na yule bwana kiurafiki kabisa kama vile hakuna kitu chochote kinachotokea hapo kabla. Yule bwana alikluwa ametumbua macho vibaya mno!!!

“Huyu jamaa unayemuona (akimaanisha mimi) ni maarufu sana… tena sana. Ndo maana hata mkewe unamjua na umefanya mpango fulani hadi aolewe…. Umelipwa shilingi ngapi kwa mpango huo nauliza…” Geza alimuuliza. Sauti haikwenda mbali kabisa. Kwa sababu sauti ya luninga ilikuwa juu zaidi.

Yule bwana aligeuka tukatazamana, sasa niliweza kubaini kiuhalisia kabisa sura yake!! Alikuwa ni yule bwana niliyekutana naye siku ile akitoka kwa mke wangu na akiwa ananukia marashi ambayo nilimkuta mke wangu ananukia.

Nikajisikia vibaya sana kwa yote yaliyotokea ambayo siyajui. Na sikutaka hata kuyajua maana yalikuwa yakiupondaponda moyo wangu!!

“Dogo huyu jamaa ndo atakupa majibu yote, tena akupe majibu yaliyonyooka. … na wewe nakuachia huu mdomo wako ili ujibu maswali na sio kupiga kelele, ukithubutu kuutumia mdomo huo kupiga kelele basi nitakufundisha namna ya kunyamaza milele!!…. Ah! Ni kweli huu ni mdomo wako na una haki ya kuutumia upasavyo… ila kwa sasa ukijifanya unajua haki ya mdomo wako nami nitakuonyesha haki ya mkono wangu!!”Geza alizungumza kwa kumaanisha, kisha akamuachia yule bwana.

Nilitamani kuuliza lakini kinywa kikawa kizito sikujua ni lipi nitaanzia na lipi lifuate!!

Baada ya sekunde kadhaa nikamuuliza yule bwana.

“Mke wangu yupo wapi? Na yupo na nani?”

“Mkeo gani?”akaniuliza. palepale Geza akafyatuka kwa kasi!!

Ilikuwa ni ngumi tena mbavuni!! Na mkono mmoja ukiuziba mdomo wa yule bwana. Safari hii yule bwana hakuhimili maumivu, hewa chafu ikamtoka!!!

Geza alikuwa hatari jama!!

“Nilikuachia mdomo kwa ajili ya kujibu maswali na sio kuuliza… huwa sionyi mtu mimi naua tu, sijui umenipa nini wewe mtoto wa kiume hadi inakuwa hivi!!” alizungumza Geza huku akiwa amemdhibiti yule bwana.

“Nakuachia sasa na ujibu kila swali hata kama ni gumu vipi?”…..

Geza akamuachia!!

“Sijui lolote kuhusu mkeo kaka….” Alinijibu huku akiwa na wasiwasi sana.

“Ile siku nakutana na wewe ukitoka kwa mke wangu ulimfanya nini na ulienda kufanya nini….”

“Siku gani? Aah! Samahani kaka…. Aah! Tafadhali naomba kukumbushwa!!”jamaa alikuwa amepagawa haswa akamuomba Geza badala ya kuniomba mimi.

Nikamkumbusha siku yenyewe.

Yule bwana akanieleza kuwa ile siku alikuwa ameenda kuonana na mke wangu Latipha, na alienda mbali na kusema kuwa Latipha alikuwa amemuita nyumbani kwake, akakiri kuwa walikumbatiana lakini akikataa katakata kuwa hakufanya mapenzi na mke wangu.

Nilimuuliza sana ni kipi alichokuwa ameitiwa Latipha akasema kuwa Latipha alikuwa akihitaji msaada wake, msaada ambao hakuweza kuufahamu kwani baada ya kufika pale Latipha alikuwa mtu wa kulia tu bila kusema lolote.

Yule bwana aliendelea kujitetea na kusema kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda katika nyumba ile, na akiwa chumbani pale ghafla Latipha alipigiwa simu na rafiki yake kuwa mumewe (yaani mimi) nilikuwa njiani kwenda nyumbani kwake hivyo kumkuta pale ingezua matatizo.

“Na hapo nikaondoka upesi sana lakini naapa kabisa sijawahi kufanya jambo lolote na Latipha ni rafiki yangu hata akiletwa mbele yangu sasa hivi sitapindisha maneno. Nife hapahapa kama nadanganya jamani….” Yule bwana aliongea katika namna ambayo hata kama huujui ukweli utalazimika tu kumuamini hakuwa anayumbayumba. Alimaanisha alichokuwa akikisema.

“Sasa Latipha wangu yupo wapi?” nilimuuliza.

Akatulia kidogo akifuta machozi yaliyokuwa yakimbubujika, kisha akanieleza kuwa ile ilikuwa mara yake ya mwisho kumuona Latipha. Mengineyo alisikia tu juu ya Latipha kupewa talaka na mumewe kisha kuolewa, harusi ambayo hakuna hata mwanachuo mmoja aliyealikwa na huo ukawa mwisho wa Latipha kuonekana chuoni. Kwa habari za chinichini ni kwamba alikuwa ameenda mapumziko ya honeymoon na mumewe mpya.

“kaka zangu yaani hata ukiletwa msaafu mimi nipo radhi kuapa. Simjui Latipha zaidi ya hapo… ila naamini kuwa analo tatizo na alihitaji nimshauri lakini walah! Hakuwahi kunambia….” Alizidi kujitetea.

Geza alikuwa mgumu sana kumuelewa yule bwana lakini kwangu mimi hakika nilikuwa nimemuelewa na kumuamini.

Gewza akatulia kwa muda kisha alichozungumnza kiliniacha hoi na kuzidi kushindwa kujua huyu bwana nimuweke daraja gani!

“Naitwa Geza ulole ama iga uone ni msukuma halisi kutoka Mwanza vijijini…. Hadi sasa ninafahamu njia themanini na nne za kumsababisha mwanadamu awe tayari kuwekwa kwenye jeneza. Najua kuua sana na wala sijisifii, kama unabisha naweza kukuua sasa hivi halafu wala sikutoi damu na wala hautapiga kelele. Nipo katika kujifunza njia ya themanini na tano ya kuua, usipokuwa makini nitajifunzia kwako na ninakuhakikishia kuwa nitaweza tu kukuua…… sasa nakuuliza swali moja tu la msingi ukijibu uongo nakuua, ukiacha kujibu nakuua, ukiniuliza swali badala ya kujibu swali nakuua pia…..…. ikiwa hujui lolote kuhusu mke wa Khalfani na unasema hujawahi kuwa katika mahusiano naye ya kimapenzi.. ni kwanini ile siku umeenda kwake alivua pete ya ndoa??? Sekunde tatu za kufikiri, sekunde ya nne nahitaji jibu lililonyooka … haya moja… mbili…..”

Geza alitulia kwa dakika moja bila shaka alikuwa akitafakari jibu la yule bwana ambaye hadi wakati ule sikuwa nikilitambua jina lake.

Baadaya fikra hizo akamuuliza yule bwana ikiwa anapafahamu mahali ambapo Latipha ameolewa, ama anamfahamu kwajina bwana aliyemuoa Latipha.

Yule bwana akatikisa kichwa na kukataa kuwa hajui lolote.

“Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yangu tangu niitwe Geza nimetongozeka nakukubali maneno matupu….sasa nisikilize, kama nilivyojitambulisha awali naitwa Geza Ulole ni askari ambaye serikali hainitambui. Sasa nakuachia kwa dhamana. Na dhamana hiyo ni roho yako…. eeh! Roho yako sijakosea. Na ninakuachia ili uweze kutusaidia upelelezi, upelelezi mdogo kabisa, nakuachia siku mbili tu za kunipatia majibu. Sichukui namba yako ya simu, sitaki kujua ni wapi unaishi. Ila baada ya siku mbili tutakutana humuhumu ndani muda kama huu bila kuwahi sana wala kuchelewa kabisa!!! NAITWA Geza Ulole kwa Kiswahili Iga Uone!!” Geza alimaliza kuzungumza kisha akasimama na kuondoka, kama ilivyokuwa kawaida yangu na mimi nikafuata kwa nyuma!!

Geza alikuwa akitembea mwendo wa taratibu, nikamfikia tukatelemsha na ngazi hadi chini. Akaongoza njia tukatoka nje!!

Ilikuwa yapata saa saba za usiku!!

“Geza…. Geza…” nilimuita baada ya kimya kuwa kirefu sana.

Akageuka kunitazama…

“Naitwa Geza Uloledogo!!” alinikoromea. Nikamuita kama alivyotaka. Hakuitika akanitazama!!

“Sasa umemuachia hivihivi je akienda kushtaki polisi…” nilimuuliza. Akatokwa na tabasamu hafifu kama kawaida yake kisha akacheka kidogo.

“Dogo una matatizo ya kusikia?” akaniuliza.

Nikamjibu kuwa sina matatizo yakusikia hata kidogo. Akacheka kidogo kisha akanisogelea karibu kabisa na kunisemesha.

“Nimemwambia jamaa kuwa mimi ni polisi na wewe umesikia, kwanini sasa unataka tupoteze muda kurudirudia mambo yaleyale….sasa aende polisi ipi tena, au unamshauri afanye wazimu wa kwenda polisi kumshtaki polisi” akakomea hapo kisha akatokwa na kicheko cha juu kidogo.

“Sasa Geza ..aah! Geza Ulole…. jamaa asiporudi itakuwaje…” nikamuhoji.

Akaacha kucheka akanijibu, “Sikiliza dogo, hapa ulimwenguni ukiwa hauna nguvu na madaraka basi jifunze kadri uwezavyo kuwa na mkwara wa nguvu…. kwa ule mkwara niliompa asiporudi yeye ni mwanaume. Na asiporudi kweli halafu nije kumkamata atajuta kuzaliwa mwanaume!!”

Geza alimaliza kisha akaita pikipiki mbili, wakafika pale.

“Kila mmoja anaenda anapojua? Na kila mmoja anajilipia…..” aliniambia kisha akadandia pikipiki moja na kumwamuru aondoke.

Akaniacha pale kana kwamba hatukuwa pamoja kabisa.

Nami nikamweleza yule bwana aliyebakia akanipeleka hotelini.


Nilifikishwa pale hotelini ndani ya dakika chache. Nikamlipa mmiliki chombo pesa yake na kisha nikapiga hatua ilikuelekea hotelini.

Mara ghafla nikasikia sauti nyuma yangu. Ilikuwa ghafla sana lakini ajabu huyo mzungumzaji mwenyewe hakuonekana kuijali ile ghafla!!

“Dogo, ujue nimekaa nimefikiri kwa kina na kisha nikaona isije kuwa unanichosha bure. Hivi ni kitu gani ulikuwa humpi mkeo naye akaridhika. Naomba unieleze wapi palikuwa tatizo je ulikuwa mvivu wa kujisachi na kumnunulia zawadi pamoja na mahitaji yake mengine, ama ulikuwa unakoroma chumbani kila siku badala ya kufanya kilichopelekea wewe kumuoa, hebu nambie ujue hapa lazima kuna tatizo tu. Si bure dogo!!” alikuwa ni Geza. Sijui alifika saa ngapi pale na hakutaka kuulizwa juu ya hilo.

“Kaka sijui hata cha kujieleza katika hili lakini kwa kiasi kikubwa sana nilifanya yote ambayo mke wangu alikuwa akiyataka…” nikaendelea na kumueleza juu ya ushauri wa kuoa upesi ambao nilipewa na mkuu wangu wa chuo.

“Nenda ukalale lakini tambua kuwa kuna kitu usichokijua kinaendelea hapa… wewe lala ila mimi sitalala. Ntakuja asubuhi hapa…..ila katika maisha yako dogo usije ukarudia kosa ulilolifanya eti kufanya mambo yote mkeo aliyokuwa akiyataka… unatakiwa kufanya mambo ambayo mkeo hakuwahi kuyategemea hayo ya kuyataka yeyote anaweza kumfanyia tu na akaridhika… USIKU MWEMA!!” alimaliza Geza na hakuaga akaondoka zake!!

Nikazidi kumshangaa Geza na maajabu yake!!

Sikujua ni wapi alipanga kwenda usiku ule mnene.

Kama alivyoagiza mimi nikalala nikiwa natumaini hafifu kabisa juu ya kumpata tena Latipha wangu ama walau kuipata Amani iliyopotea tayari. Amani nyumbani kwa mama na Amani katika jamii nzima. Lakini yale maneno ya mwisho kabisa ya Geza yalinigusa…. Kumfanyia mke kitu asichotegemea na si kile anachokitaka.

Duh!! Geza ni tatizo aisee!! Nilikiri!!!

Naam! Masaa yakasonga mbele nikiwa usingizini na hatimaye ikawa asubuhi.

Geza mlangoni kwangu!!

Nikamfungulia.

“Mkeo yupo utumwani….. ama nisiseme mkeo niseme kuna mwanamke yupo matatani. Sasa tunamuokoa mwanamke kutoka utumwani na si mkeo…..” Geza alizungumza huku akitabasamu.

“Jana nilikuwa na Sakina…..” Geza alizungumza kisha akawa kama anayesubiri nimfahamu Sakina ni nani.

Sikuwa namfahamu, nikauliza Sakina ni nani..

“We lofa kweli yaani hata jina la mama mkwe wako haulijui. Nilikuwa na mama Latipha jana usiku… na mkutano wetu ulikuwa wa mafanikio sana. (akasita kisha akacheka)……. yaani yule mama eti ameamini kabisa kuwa mimi ni afisa wa polisi. Sasa afisa gani na manywele yote haya na mindevu. Chizi kweli yule, ila ni afadhali aliniamini…..”

Geza akaelezea juu ya utumwa unaoendelea.

Akanieleza kuwa Latipha wangu alikuwa akimtumikia mumewe wa sasa ili kuzuia aibu isisambae, aibu ambayo yule mama alisema kuwa Latipha aliwahi kumkataa kata kata mwanaume fulani mwenye asili ya kiarabu ambaye alikuwa anamtaka kinguvu ili amuoe. Kilichotokea baada ya Latipha kuolewa na mimi ikawa ni kisasi.

“Geza… Geza huyo mwarabu nilimuona katika harusi yangu… alimpa Latipha zawadi” nikamuingilia kati. Na kauli hiyo ikamfanya Geza asimame wima.

“Dogo Dogo…… huyo Mwarabu ni yule yule aliyeniweka katika fedheha kwa miaka mitatu. Sasa nimekasirika….. nilikuwa naisubiri hii siku ya mimi kukasirika.”….

Sasa Geza hakuwa na tabasamu usoni.

Na hapo akanieleza jambo ambalo lilinistaajabisha!!

Ama kwa hakika ilikuwa ni FEDHEHA!!!

GEZA alinitazama huku lile tabasamu lake likififia taratibu kabisa. Na mara uso wake ulitawaliwa na huzuni.

Na kisha nikaisikia kwa mara ya kwanza sauti ya Geza ikibadilika na kuwa ya upole sana pia ilikuwa sauti ya mtu kama anayejiongelesha mwenyewe.

“sikuwahi kuwaza eti ipo siku nitaingia kujihusisha na mambo ya ukabaji na hata kufikia hatua ya kuwa mtoa roho mzuri tu, nilipomwambia jamaa ninajua njia themanini na nne za kuua sikumtania hata kidogo… aah sawa zinaweza zisifike themanini lakini naua sana tu. Huwezi amini sasa nilikuwa muoga sana wa kuua mimi yaani hata picha za kutisha nilikuwa naziogopa sana, dah! Dogo amakweli hakuna aijuaye kesho… sikuwahi kudhani. Siudhani hata siku moja nitakuja kuwa mtu mbaya namna hii…. Anyway namshukuru Mungu kuwa amenipa sura ya upole sana, yaani najua kabisa nilizaliwa ili niwe aidha mchungaji ama imamu kabisa. Basi tu, yakaingia mapenzi hapo katikati, Yule binti aitwaye Lolita nambebesha lawama hizi zote, nambebesha yeye kwa sababu nikisema tu nisimbebeshe yeye basi lawama hizi zote ntazitupa kwa Mwenyezi Mungu kwa kumuumba Yule binti mrembo kiasi kile.

Nikampenda kwa dhati lakini mpambano uliokuja kutoka nje ndo ulionibadilisha, na mimi sitakiwi kulaumiwa hata kidogo, kama walikuwa na matatizo na mimi sasa mama yangu walimuingiza wa nini. Mama alikuwa amejizeekea Yule wakamtesa mama yangu bure. Yaani dogo wakati mwingine natamani siku zirudi nyuma niuambie moyo wangu uache kuwa na mambo ya kijinga kiasi cha kupenda kupita maelezo. Yaani nilikuwa zoba kweli, lakini ile siku namwona kwa macho yangu huyo mwarabu ambaye anajitamba kuwa eti kila watoto wazuri basi ni halali yake akimsumbua mama yangu. Huo ndo ukawa mwisho wa ujinga wangu, nikaamua kupambana si kwa sababu ya mapenzi bali kuitafuta haki yangu.

Mpambano wangu wa kwanza nikaishia kutupwa jela miaka miwili, sikumbuki hata jina la kesi. Lakini Yule mwarabu alidai kuwa nimemtukana na kumpiga!!

Hilo likapita dogo, nilipotoka gerezani nikakuta mama yangu alishazikwa mwaka mmoja uliopita……

Nikajaribu kuitafuta tena haki yangu kwa sababu niliambiwa kuwa chanzo cha kifo cha mama yangu ni huyo mwarabu ambaye nasikia kwa chinichini ana ubia fulani na watu wazito serikalini.

Ile kuitafuta haki yangu nikaishia kuishi mtaani kwa mwezi mmoja tu, nikarejeshwa jela!!!

…….. sasa dogo nilipotoka mara ya pili nikatambua kuwa uiitafuta haki yako kwa ustaarabu na ukanyimwa hebu badili mbinu maana kuna usemi nilijifunzia gerezani walikuwa wanasema hivi, ikiwa kila siku wewe unafeli nab ado unatumia mbinu zilezile zilizokusababishe ufeli unategemea siku moja utafaulu basi kichwani kwako kuna mapumba tupu.

Naam! Nikaamua kubadili njia” ….. Geza akatulia kidogo kisha akatoa kigazeti fulani akakifungua. Nikaweza kuyasoma maandishi, “MTOTO WA BAISAR AKUTWA AMEKUFA BARABARANI” nilipomaliza kusoma neno lile Geza akadaikia, “Nilihusika kwa silimia 50… akanipa tena kikaratasi kingine, “BAISAR APATA PIGO TENA SASA NI KIWANDA CHAKE CHAUNGUA”…. Geza akadakia, “Ni mimi niliyetupa kiberiti baada ya petrol kumwagwa vizuri..” akasita kisha akaendelea.

“Matukio mengine sina picha zake…. Sasa baada ya kumsulubu nikajua kuwa hii tabia ya kujifanya anajua sana wanawake atakuwa ameiacha, kumbe amekugusa na wewe rafiki yangu wa ukubwani aah! Rafiki yangu wa majangani hivi huwa unaitwa nani vile??” kwa mara ya kwanza akaniuliza jina langu.

“Naitwa Khalfani..” nikajitambulisha.

“Aaah! Jina gumu hilo na sitaki kulijua, .aah! sasa Dogo swali ninalojiuliza ni moja tu, huyu bwana alikuwa anajifanya kuhitaji watoto wazuri wa kike lakini kusema na ukweli tuache masihara mkeo hana uzuri wowote kama kununa we nuna tu… ila tunatakiwa sasa kujua huyu jamaa anafanya nini na mkeo. Kwa upelelezi wangu wa hayo masaa machache nimesikia vitu viwili vikubwa. Kubwa huyo Baisar anajihusisha na madawa ya kulevya na pia sasa analo danguro… sasa ni kwamba mkeo anauzwa siku hizi ama anabebeshwa kete. Hapa ni lazima nijipe majibu, kuhusu kuuzwa sidhani.. kwa sababu hana mvuto kibiashara hawezi kuwavutia wateja, kwa hivyo hili la pili sasa mkeo kubebeshwa kete.

Aisee kama ni kweli anafanya hivi atajuta kukutana nami katika vita hii ya kimyakimya!! Tena kwa sasa sipo peke yangu nipo na mjeshi wangu hapa” akaongea huku akinipigapiga bega langu.

Sasa nikajiuliza mimi nina ujeshi upi haswa hadi anipachike masifa yote yale.

Geza alikuwa mkimya kwa muda sasa lile tabasamu lake jepesi likarejea tena.

“Dogo!! Nitakuonyesha ni kwanini jela kinaitwa kituo cha mafunzo…. Kuna mambo madogo nilijifunza huko lakini kwa hapa uhuruni yataonekana makubwa sana. Mi nakuamini sana najua hautaniangusha, unalipa kisasi nami pia nalipa kisasi. Kwa pamoja tumfanye Yule bwana ajitambue kuwa pesa zake si chochote si lolote mbele ya akili ya jela.

Dogo!! Usirudi nyuma, ukirudi nyuma maana yake umekubali kuonewa na kudhalilishwa!! Si unajua ukionekana uraiani watakachosema??” Geza akanieleza na hapo nikakumbuka kuwa kule mtaani palikuwa na skendo la mimi kuwekwa rumande kwa sababu nilifumaniwa nikiwa nyumba ya kulala wageni na shoga!! Jambo ambalo halikuwa kweli hata kidogo, mama Khalfani akachukizwa sana na kufikia hatua ya kuniona sina maana hata kidogo katika jamii. Kila mtu akawa ananitazama kwa jicho kali tena la dharau.

Yaani Khalfani ameoa halafu anaenda kulala na shoga?? Ndo maswali waliyojiuliza watu na mwishowe watu haohao kuunga mkono hatua aliyofikia Latipha mke wangu kuolewa tena.

Dah! Kweli nilikuwa nimechafuliwa!! Yaani nilivyokuwa nimeishika imani ya dini yangu vizuri leo hii nikalale na Shoga!!

Kumbukumbu hizi zikania hasira kali juu ya huyo mwarabu tajiri wa kuitwa Baisar!!

Nikajisemea kuwa ikiwa amenifedhehesha namna ile sina maana ya kuwa mtaani basi liwalo na liwe hata kama ni jeloa bora niende huko!!

“Kaka Geza Ulole nipo na wewe kwa asilimia zote!!” nilimtamkia.

Akatabasamu kidogo kisha akaniambia, “Kesho tunakutana na Yule jamaa yetu kulekule ukumbi wa sinema… tukutane huko!!!”

Akamaliza akaondoka bila kuaga kama kawaida yake!!!

Huyo ndo Geza bwana!!!

ILIKUWA nisivyodhania kabisa, nilijiongopea kuwa laiti kama mimi ndiye ningekuwa Yule bwana ambaye Geza alimchimba mkwara kuwa atokee kwenye ukumbi wa sinema basi nisingetokea.

Huenda wazo hili nililipata kwa sababu tayari nilikuwa nipo karibu na Geza hivyo nilikuwa siuchukulii uzito sana ule mkwara.

Naam! Kama alivyoambiwa asiwahi sana na asichelewe kabisa Yule bwana alifika kwa wakati, tukamkuta ndani ya ukumbi!!

Binafsi nilikuwa nahofia sana kuwa yule bwana anaweza kuwa ameongozana na maaskari hivyo watatuzunguka na kutukamata. Nilitamani sana kumweleza Geza juu ya wazo langu lile lakini niliamini kuwa nitakutana na jibu moja matata sana ambalo klingenifadhaisha!!

Naam! Kikao cha sasa kilikuwa kifupi sana, yule bwana akaeleza kuwa amejaribu kadri awezavyo lakini hajafanikiwa kumuona Latipha wala huyo mumewe. Safari hii Geza hakumuuliza swali hata moja. Bali mwishoni kabisa alimkumbusha kuwa yeyey ni polisi asiyetambuliwa na jeshi la polisi hivyo asije akajifanya anajua zaidi akaenda kuzifikisha habari zile popote pale.

Kikao kikaishia pale tukaondoka!!

Siku hiyo alinizuia kurudi hotelini!


ITAENDELEA

Fedheha Sehemu ya Nne

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment