Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034 Sehemu ya Nne
KIJASUSI

Ep 04: Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034

SIMULIZI Vipepeo Weusi Mkakati Namba 0034
Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034 Sehemu ya Nne

IMEANDIKWA NA: THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi: Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034

Sehemu ya Nne (4)

“Now, kama nilivyokwambia kuwa mtunza kumbu kumbu huyu ambaye The Board wanamuita Book Keeper, ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRBB Bw. Vincent Mallya.. Na kumbu kumbu hizi anahakikisha ziko naye muda wote haziondoki kwenye uwepo wake” akaongea huku anafumba macho na kuangalia juu.

“Sijaelewa una maana gani??” Nikauliza tena kwa shuaku kubwa zaidi.

“Namaanisha documents ziko na Vincent Mallya muda wote”

“Sikuelewi Kaburu”

Akavuta tena pumzi ndefu ndani na kuishusha kwa nguvu.

“I cant believe that am telling you this” Kaburu akafumba macho kwa nguvu kwa woga.

“Stop playing around! Where are those damn files??” Nikafoka kwa shauku.

“Ziko katikati ya jiji la Dar es salaa, maeneo ya Posta kwenye Strong Room ya CRBB makao makuu, Golden Jubilee Tower”

“Whaaaaaatt” nikapatwa na mshituko.

“Yeah! Siri zote kuhusu The Board, wanachama wao, mikakati yao, vibaraka wao na akaunti zao za siri nakadhalika na kadhalika… Files zake zote zipo kwenye Strong Room ya CRBB makao makuu, Golden Jubilee Tower”

Kaburu akajibu huku amefumba macho na kulalia kiti.

“Nakumbuka ulinambia kuwa ‘nitazichukua kama naokota dodo kwenye mwembe’??”

“Hiyo ni misemo tu Ray! Ila sasa unafahamu moja ya siri kubwa sana katika hii nchi”

Nikajiinamia kwenye usukani wa gari. “Fuuuucckk!!” Nikatukana kimoyo moyo kwa sauti ya chini.

Strong Room??? Nimefeli akyamungu!! Inyeshe mvua au liwake jua, na hata niwe na miakili kiasi gani… Never never ever, hakuna namna ambayo nitaweza kufanikisha kukanyaga mguu wangu ndani ya strong room ya Benki kubwa kama CRBB.

“This is impossible!! But we need to think of something” nikaongea huku bado nimejiinamia kwenye usukani.

“The only way unaweza kufika kwenye strong room ni kwa kufanya tukio la ujambazi” akaongea kaburu.

“Hey hey boys! Mnafika mbali sasa, huko sasa mnatafutwa mpigwe risasi… Ray please usianze hij mipango ya kiwendawazimu sitaki kuwa mjane kabla hata hujanioa na wala sitaki kumlea huyu mtoto peke yangu..” Cheupe akafoka kwa msisitizo.

Nikainua kichwa kutoka kwenye usukani. Nikajifanya kama sijamsikia Cheupe.

“What are suggesting?” Nikamuuliza Kaburu.

“Kuna Mzee namfahamu.. Ni Mzee wa kipemba anaitwa Abdul Zakir lakini tumezoea kumuita ‘Chifu’… Matukio Mengi makubwa yanayotokea Dar na kufanikiwa yeye ndio mchora ramani, yeye mwenyewe huwa hajihusishi kuyatekeleza, yeye ni mtu wa mikakati tu.. So tukiongea naye anaweza kutoa mawazo mawili matatu ya kujenga” anakongea kaburu.

“Anaishi wapi?”

“Anishi Dar, mbagala Kizuiani”

“Let’s go see him” nikaanza kuwasha gari.

“Honey?? What the **** are doing?? Siamini kama unafikiria kitu cha hatari kiasi hicho!” Cheupe akafoka.

“Babes! Skia, umesikia kuwa mafaili yako strong room.. Hebu twende tukaongee na huyo Mzee tusikie idea zake.. Kama idea za mbaya naachana nazo”

“Na kama ni idea nzuri?? Utafanya tukio la ujambazi??”

“I don’t know what am going to do honey.. I’m still thinking” nikaongea huku naanza kuendesha gari. Sikutaka kusubiria jibu lake, niliona jinsi alivyokuwa amenuna.


Ilikuwa inapata saa tatu na nusu usiku, na ndio tulikuwa tumewasili mbagala kizuiani.

Tulipofika barabara kuu pale kizuiani, tulikata kushoto kama tunaekekea kwenye kambi ya Jeshi la JWTZ.

Katikati hapo kukikuwa na mtaa mkubwa tu.. Kaburu akanielekeza nisimamishe gari kwenye nyumba Fulani hivi nzuri tu na kwa haraka haraka nikagundua ndio ilikuwa nyumba pekee yenye uzio wa ukuta hapo mtaani.

Tukapaki gari na kushuka. Tukaenda mpaka kwenye geti la nyumba na kugonga.

“Naniiiiiii??” Sauti nyororo ya like iliitikia kutokea ndani.

“Wageni wa Mzee” aliitikia Kaburu.

Mara geti dogo likafunguliwa na msichana fulani akachungulia. Akikuwa amejitanda kanga na nyingine ameifunga kama hijabu.

“Salaam aleykum.!” Yule bint akatusalimia.

“Aleykum salaam” Kaburu akaitikia kwa ufasaha mpaka nikshtuka.

“Niwasaidie nini?”

“Tuna shida na Mzee”

“Baba Fahimu amepika” yule binti akatujibu kwa lafudhi ya pwani.

“Nenda kamuamshe mwambie Eric yuko hapa”

“Baba Fahimu akipumzika hataki mtu kumsumbua kumuamsha!”

“Sikia binti kama nikondoka hapa, na kesho Chifu akijua kuwa Eric alikuja na haukumuamsha, nakuapia walahi kesho hiyo hiyo anakutwanga twalaka urudi kwenu” Kaburu akamchimba mkwara.

“Karibuni ndani” yule binti akatupisha getini tuingie.

Nikahisi kuwa Kaburu aliongea kwa mafumbo na walielewana na yule binti kuwa tuko hapa “kikazi”.

Tukakaribishwa kwenye sebule kubwa iliyokuwa ina kila aina ya mikogo ya kiarabu.

Yule binti akatuacha na kwenda vyumbani.

Kama dakika Tatu baadae, kutoka vyumbani mwenyeji wetu akawasili sebuleni.

Alikuwa ni Mzee wa makamo tu wa kama miaka 62 tu hivi. Alikuwa na ndevu ndefu za wastani zenye mvi chache.

Alikuwa amevalia msuli na singlendi, na ingawa ilikuwa usiku kichwani alikuwa amevaa baraghashia.

“Ericccccccc” yule mzee akahamaki kwa mshangao na furaha.

Kaburu akainuka wakakumbatiana kwa furaha.

“Siamini macho yangu ati” yule Mzee akaongea kwa furaha zaidi. “Na hawa kina nani?” Akaukiza.

“Chifu hawa wanajambo Fulani wanahitaji hekima yako”

Chifu akaelewa Kaburu akichomaanisha.

“Karibu ofisini, karibuni”

Akaanza kutuongoza kutoka pale sebuleni kuelekea kwenye korido.

Tukaifuata korido mpaka mwishoni kulikuwa na chumba. Akakifungua tukaingia “ofisini”.

“Karibuni sana.. Karibuni”

Chifu akatukaribisha “ofisini” kwake. Hiki chumba ambacho mwenyewe alikiita ofisi ndio labda ilikuwa ofisi pekee duniani ambago haina viti wala meza.

Kulikuwa na zuria zuri la manyoya manyoya kimetandika kuenea kwenye chumba kizima.

Alafu kukikuwa na mito mito ya kuegemea kila pahala.

“Aiseee! Eric tuna Mengi sana ya kuongea ila kwanza niwasikilize vijana” akaongea Chifu baada ya wote kuwa tumekaa chini.

“Mzee kwanza pole sana kwa kukusumbua usiku wote huu” nikafungua maongezi ‘kisiasa’.

“Usijali kijana, shida hazina majira! Kuwa huru tu, nieleze kinachowasibu” Chifu akanijibu.

Nikaona hakuna haja ya kuzunguka mbuyu. Huyu ni ‘profesheno’.

“Chifu, hapa unapotuona tuna changamoto kubwa sana inatukabili, na ili tupate suluhu inatupasa tufanye jambo moja gumu sana”

“Jambo gani kijana?” Akauliza.

“Tunahitaji utusaidie tuingie strong room ya CRBB mako makuu” nikaongea bila kupepesa macho.

Chifu aliganda ananiangalia bila kusema chochote kwa takribani dakika nzima. Sijui alihisi nimekosea kuongea kwahiyo ananosubiri nosahihishe. Au labda alikuwa anatafsiri nilichoongea. Vyovyote vile lakini naamini hakudhani kama nitamueleza suala la “kiwendawazimu” kama hili.

“Mnahitaji kuingia Strong Room ya Makao makuu ya CRBB??” Akinuliza kwa kafudhi yake ya kipemba.

“Yes! Tunahitaji kuingia Strong Room ya makao makuu CRBB na tunahitaji kufanya hivyo haraka iwezekanavyo” nikamjibu kwa kujiamini nikiamkazia macho bila kuyapepesa hata kidogo.

Zilikuwa zimepita takribani siku mbili tangu tulipoenda Nyumbani kwa Chief siku ile usiku.

Licha ya kutushangaa kuhusu azma yetu ya kutaka kuingia strong room ya makao makuu ya banki ya CRBB lakini mwisho wa siku alikubali kulifanyia kazi suala letu na alituomba turudi baada ya siku mbili.

Kwa siku mbili zote hizi tulikuwa tumefikia katika lodge Fulani hivi ndogo maeneo ya sinza na hatuku toka nje kwa siku zote hizi. Kila kitu tulifanyia ndani. Chakula tuliagiza ndani na kila kitu.

Nilikuwa nimefanya mawasiliano na Issack na alinieleza kuwa wameshafanikiwa kumtoa Godi gerezani kwa dhamana. Nilochokuwa nasubiri sasa ni kujua mpango ambao Chifu ataupendekeza ili niweze kujua tunawezaje kumtumia Godi katika timu yetu.

Kaburu naye alikuwa nasi. Bado tulikuwa tunasubiri mrejesho kutoka kwa Baba Bite ili kufahamu kama amaefanikiwa kuzipata documents zake ama la. Na namna pekee ambayo ningeweza kufahamu hili ni kwa kuonana na watu wa usalama kwa kutumia njia waliyonielekeza siku ya kwanza kwa kwenda duka la vitabu la Stolastika maeneo ya Mlimani City.

Nilichokuwa nasubiri, nilitaka kwanza nijiue mpango utakaopendekezwa na Chief ili nikienda kuwaona watu wa Usalama Wa Taifa kama kuna jambo lingine ambalo tunahisi kuwa watu wa usalama wanaweza kutusaidia katika huu mpango wetu basi niunganishe humo humo.

Ilikuwa inakaribia kabisa mida ya saa sita mchana na nilikuwa namalizia kujiandaa ili niende Nyumbani kwa Chief pamoja na Kaburu. Cheupe atabaki hapa lodge.

“So itakuwaje kama chief akipendekeza njia pekee ya kufika Strong room ni kuivamia bank?” Cheupe akaniuliza nikiwa namakizia kuvaa.

“Obviously siwezi kufanya tukio la ujambazi lakini nadhani itabidi tuangalie nini mbadala wake tunaoweza kufanya badala ya tukio la ujambazi” nikamjibu huku nachukua begi la mgongoni.

“Be careful Ray, please! Usifanye kitu au maamuzi ya ajabu huko tafadhalu”

“Siwezi kufanya jambo la ajabu mama, uamuzi wowote nitakao ufanya nitazingatia maslahi yako na mtoto! Kwahiyo relax mama” nikambusu cheupe na kuanza kuondoka.

“Kilala heri baba!”

“Thank you!”

Nikatoka nje ya chumba na kwenda kumgongea Kaburu. Baada ya hapo tukakwea kwenye gari na kuondoka.

Kama nusu saa hivi baadae tulikuwa tumewasili nyumbani kwa chief na tulikuwa katika kile chumba chake ambacho mwenyewe anakiita ‘ofisi’

Baada ya salama na mazungumzo ga hapa na pale hatimaye tukaanza kujadili kilichotuleta hapa.

“Kijana! Lile suala lako nimelishughulikia kwa kiasi fulani hivi na nimefika mahala pazuri kidogo” chief akaongea huku anasogeza karibu makaratasi fulani hivi aliyokuwa ameyaweka pembeni.

“Hii ni ramani ya jengo zima la Golden Jubilee Tower” akatandaza kwenye zuria katatasi fulani ndefu ya mchoro wa jengo.

Akaanza kutuonyesha namna mpangilio wa vyumba na maofisi katika jengo hilo.

CRBB wenyewe walikuwa wamechukua ‘floor’ nne za kwanza za jengo. Jengo zima kwa ujumla wake lilikuwa na jumla ya ghorofa 12.

Akatueleza kuwa strong room yenyewe kwenye jengo hili iko chini kabisa kwenye ‘basement’ ya jengo.

Watu kadhaa kwenye makao makuu walikuwa na ‘access’ na strong room na watu ambao walikuwa na access hiyo ya moja kwa moja walikuwa ni meneja wa hapo makao makuu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji mwenyewe Bw. Vincent Mallya.

Wafanyakazi wengine wachache walikuwa na access lakini walikuwa mpaka wapate kibali cha Meneja au Mkurugenzi Mtendaji.

.

Chief akatuelekeza pia namna ambavyo kuna ‘procedure’ ambayo ni standard kama kwenye majengo mengine yote ya ghorofa kuwa lifti alikuwa haishuki mpaka chini kwenye basement.

Ili ufike chini kwenye basement, inabidi ushuke kwa kutembea kutoka ‘ground floor’.

Chief pia akatoa makaratasi mengine ambayo sikujua aliyapataje lakini naamini aliyapata kutoka kwenye kampuni iliyofanya ‘installation’ ya strong room.

Hapo akatuonyesha namna mfumo wa ile strong room ulivyo, sensors zake, milango, na kadhalika.

Baada ya hapo akaanza kutueleza kuhusu mfumo wa ulinzi wa benki, washika funguo za strong room na mambo mengine Mengi sana ya ulinzi ‘uliotukuka’ hapo makao makuu.

“Kwahiyo kijana kwa ufupi hicho nilichokueleza ndicho unachotakiwa kukijua kabla ya kutakabkuvamia strong room ha pale makao makuu” chief akaongea huku anakusanya makaratasi yake na kuyakunja kunja kurudisha pale pembeni.

“Kwa hiyo pendekezo lako ni nini Chief” nikamuuliza.

“Unahitaji timu! Tena timu ya watu wazoefu ili kufanikisha huu mpango”

“Kwa maneno mengine unapendekeza tuvamie benki” nikamuuliza.

Chief akatoa macho na kunishangaa. Alikuwa kama haamini nimetamka hayo maneno.

“Kijana! Utawezaje kuiba fedha za benki tena kwenye strong room bila kufanya uvamizi??” Akaniuliza kwa mshangao.

“Well, ishu ni kwamba hatutaki kuiba fedha za banki” nikamjibu huku natabasamu kwa kujishtukia. Nilijishtukia kiasi maana mpaka sasa tulikuwa hatujamueleza ukweli wa tunachotaka kukifanya kwenye strong room.

“Atiiiii??” Chief akashangaa na kumkodolea macho Kaburu.

“Chief… aaaah ni kweli.! aaah hatutaki kwenda kuiba fedha kwenye strong room!! Kuna makabrasha fulani muhimu sana yapo humo na ndiyo hayo tunataka kuyachukua” Kaburu akamfafanulia.

“Sasa mimi percent yangu ya mgao naipataje kama kumbe mnaenda kuiba mikaratasi!! Maana nilijua nitaongeza nyumba nyingine ati??” Chief akaukiza huku bado akiwa na mshangao mkubwa.

“Well, utatueleza tukulipe kiasi gani kwa huu msaada wako na sisi tutajitahidi upate hiyo hela” Kaburu akajaribu kumpoza Chief kuwa hafanyi kazi hii bure.

“Kwani hayo makaratasi yanahusu nini?” Akauliza chief.

“Ubaya ni kwamba hatuwezi kukueleza yanahusu nini.! Lakini yana thamani kubwa na tukiwa nayo mkononi, huyo tunataka kumpelekea hakutakuwa na shida yoyote kuhusu kutoa kiasi chochote cha fedha”

“Eric wewe unajua utaratibu wangu! Kwenye kazi yoyote nikichora ‘racket’ nachukua asilimia kumi ya mzigo unaopatikana… Sasa hapa mananipa mtihani ati.! Maana nashindwa kujua asilimia kumi ya makaratasi!! Mimi hilo niwaachie nyinyi sasa, tutasaidiana hili lifanikiwe na naamini hata niangusha kunipa kile ninachostahili kukipata inshallah”

.

“Haina shaka kabisa mkuu! Ondoa wasi wasi kuhusu hilo” Kaburu akaendelea kumtoa hofu Chief.

Uzuri kwa namna ambavyo niliwasoma, nilihisi kabisa Kaburu na Chief wamefanya kazi nyingo pamoja huko siku za nyuma, kwahiyo hii walau ili rahisisha kupata kuaminiwa na Chief.

“Naweza kuazima hii michoro niende nayo?” Nikamuomba zile ramani na jengo la Golden Jubilee Tower na ile karatasi inayoonyesha mfumo wa strong room jinsi ulivyo.

“Hainq shida kijana” Chief akakunja yale makaratasi na kunikabidhi.

Baada ya hapo tukaagana naye na kuanza Safari ya kurejea lodge Sinza.

“So what are you thinking??” Kaburu akaniukiza tukiwa kwenye gari.

“Hatuwezi kuingia strong room.!” Nikamjibu kwa mkato tu.

“Huwa nadhani hakuna jambo linalokushinda Ray! Kwanini hili ulikatie tamaa mapema hivi?”

“Well, moja ya vitu ambavyo mtu yoyote makini anapaswa kuvifahamu ni kujua mahali gani unapaswa kuchora mstari.. Haijalishi una akili au ujuzi kiasi gani, lakini hutakiwi kujifanya wewe ni ‘almighty’.! Lazima kuna vitu vitakuwa nje ya uwezo wako na mfano mzuri ni hili.. Tukijifanya tukavamie benki, kumbuka benki ina ulinzi mkali, tunaweza kujikuta tunapigwa risasi na kukosa vyote!! Na tusitake kujifanya kuwa tunaweza kutumia mbinu za kiakili akili kuingia kwenye vault.. Hayo mambo yako kwenye sinema tu!! Haya ni maisha halisi na uhalisia uliopo mbele yetu ni kwamba hatuwezi kuingia ndani ya vault”

“Kwa hiyo unapendekeza nini?? Au tuwapa tu taarifa Usalama wa Taifa Wamalize hili suala wao wenyewe??” Kaburu akaniuliza.

“Tatizo hao Usalama wenyewe siwaamini.. Wakizipata hizo documents mkononi mwao sidhani kama watatimiza ahadi yoyote ile tukiyokubaliana.. We need to get those by ourselves.. Na pia kuna vitu nataka kuviona kwenye hizo files” nikamjibu huku najaribu kufikiria vitu kadhaa kichwani.

.


Tulikuwa tumewasili tayari lodge Sinza na wote watatu tulikiwa chumbani kwetu tunajadili nini cha kufanya.

“Sijaelewa bado, kwahiyo tunagive up au tunawaachia watu wa Usalama Wa Taifa??” Cheupe akauliza.

“Well nadhani Ray atueleze anachofikiria” Kaburu akaongea huku ananiangalia kwa kuniinjoi.

Nahisi alikuwa anajua ni kiasi gani kichwa kilikuwa kinaniwaka moto kufikiria nini cha kufanya.

Tangu tumetoka kuonana na Chief kuna idea kadhaa nilikuwa nazifikiria lakini nikikuwa bado sijaamua ni ipi inafaa zaidi kuitekeleza.

“Wow! Wow, wow hahaha” nikajikuta nafurahi peke yangu baada ya wazo moja kukaa sawia kichwani mwangu.

“What is it” wote wakaniuliza.

“I got it.! Hahahah.. I got this” nikaongea huku nachukua funguo za gari na kuanza kuinuka.

“Hey ndio utuambie sasa What is it” Cheupe akauliza tena huku wananishangaa kama wamemuona mtu aliyechanganyikiwa.

“Tutaongea nikirudi.!” Nikainuka na kuanza kutoka nje.

“Unaenda wapi?” Cheupe akauliza.

“Naenda kutafuta dalali!” Nikawajibu huku natabasamu.

“Dalali?? What the ****” Kaburu akajibu kwa mshangao mpaka akainuka.

“Tutaongea nikirudi” nikatoka nje na kuingia kwenye gari.

Nikaendesha gari mpaka maeneo ya Shekilango. Kuna wajamaa nikawaona wamekaa kijiweni pembeni ya barabara. Nikapaki gari pembeni na kwenda kuongea nao.

Nikawaeleza shida yangu kuwa natafuta dalali.

Tatizo la Dar.. Kila mtu anajifanya “mtoto wa mjini”, kila mtu ‘dalali’, kila mtu “mdananda”, kila mtu mjuaji..

Hawa wajamaa nilipowaambia nahitaji dalali, badala ya kunielekeza nampataje dalali, wanaanza kuniuliza nataka nyumba au chumba cha aina gani… Kabla hata sijawaeleza nahitaji nini wanaanza mbwembwe kibao… Sijui kuna nyumba ya mzee nani sijui… Porojo kibao, sijui nyumba ‘Kali’, ina ’tiles’, ina ‘jipsamu, choo ndani kwa ndani.. Maneno meeengiii..

Nilikuaa nikigundua tu kuwa huyu ‘kanjanja’, namwambia tu anipe namba yake, namuahidi ‘nitamtafuta’, kisha ‘nasepa’..

Nikahangaika takribani lisaa lizima.. Mpaka mama mmoja dukani akanipa namba ya dalali anaitwa ‘Tunda’… Nilipo mpigia, kwanza nikashangaa kumbe ni ‘demu’.. Nikaongea nao kwa uchache tu na kumueleza shida yangu.. Akanijibu kwamba niende ofisini kwake kinondoni.!

Nikajisemea kimoyo moyo, haya ndio mambo mubashara! Hata kama unakuwa ‘mpigaji’ mjini, basi kuwa mpigaji ‘profesheno’.! Walau unaweka na mbwembwe za kuwa na kiofisi kama huyu dada… Sio blah blah za kuharakisha kumwambia mtu “nyumba ina jipsamu”.

Nikaendesha gari mpaka Kinondoni Mkwajuni ambapo ndiko ilipo ofisi ya huyu dada.

Dada alikuwa na mbwe mbwe kweli kweli, ukifika tu kwanza unaukizwa kama unakunywa maji, soda au juice, mara uulizwe kama uletewe matunda.. Mezani kuna ‘vijarida’ vya majengo mbali mbali hapa Dar!

Baada ya mbwembwe kuisha tukaanza kuongea kilichonileta.. Nikamueleza kuwa nahitaji kupanga ofisi. Ila nataka ofisi ndogo tu.. Isizidi vyumba vitatu na sitaki katikati ya mji ndio maana nimekuja kwake.

Tukaanza kujadili hapo nataka ofisi iwe maenao gani ambayo napendelea, ofisi iweje, bajeti yangu ikoje na kadhalika.

Baada ya hapo tukatoka na kuanza kunionyesha ofisi mbali mbali ambazo zinapangishwa.

Tukaenda ghorofa fulani hivi mwembe chai lakini sikupapenda. Sikutaka kuwa na ofisi hapa, huu ndio mtaa niliokulia. Kwahiyo sikutaka kutambulika kirahisi.

Tukatoka hapo tukaenda Mapipa, nako sikupataka! Karibu mno na Mwembe Chai. Akanipekeka Morocco, nako sikuipenda Ofisi kwa kulingana na nikichotaka kukifanya.

Baada ya hapo tukaelekea maeneo ya Makumbusho. Nyuma ya stendi ya daladala, kuna kighorofa Fulani hivi. Akanionyesha hiyo ofisi inayopangishwa.

Hii niliipenda, ilikuwa inakidhi kabisa kile nilichotaka kukifanya.

Akampigia simu mwenye nyumba na kisha tukaenda kuonana naye.

Alikuwa anaishi maeneo ya Sayansi karibu kabisa na mgahawa wa “Pweza Café”.

Tukazungumza hapo na mwishoni tukakubaliana nije nilipe kesho kodi ya miezi sita. Mwenyewe alikuwa anataka mwaka mzima, lakini ukizingatia mimi nitaitumia ofisi kwa wiki kadhaa pekee, kwahiyo nikakomaa naye mpaka akakubaki miezi sita.

Tukarudi mpaka Kinondoni ofisini kwa Tunda, nikamuacha hapo na kuondoka kurejea Sinza.


Nilipofika lodge ilikuwa inakaribia saa moja jioni. Ilikuwa kana kwamba walikuwa wananisubiri, maana nililoingia tu, Kaburu akaja chumbani kwetu.

“Naona umerudi.!” Kaburu akaongea akiwa anaingia chumbani.

“Yes! Am back, nimepata ofisi..!!” Nikamjibu huku natabasamu meno yote nje.

“Ofisi??? Unaweza kutueleza what you are up to??” Kaburj akauliza kwa mshangao.

“Ok! Mnajua maana ya neno ‘con’.??” Nikawauliza.

“corn?? Si ni nafaka sijui mahindi?? What the f*ck does corn has to do with this” Kaburu akanijibu akiwa amekereka.

“Dumbass!! Sio ‘corn’ nimesema ‘con’… C-O-N, hakuna ‘r’ katikati” nikamfafanulia.

“Oooohh con!! Yeah.. Si ni utapeli sijui nadhani” Cheupe akadakia.

“Yes! ‘con’ ni utapeli.. Sasa kuna ‘long con’, sijui hata kiswahili inasemwaje.. But ndio tunaenda kufanya hiyo, a long con!!” Nikatabasamu huku nawatazama.

“Fafanunua kidogo please!” Cheupe akaongea huku ameweka kisura cha huruma.

“Look! Obviously hatuwezi kuingia strong room makao makuj CRBB.. So that means hatuwezi kufika files zilipo.. Sasa kama hatuwezi kuzifuata files zilipo.. Inabidi tufanye files zitufuate sisi tulipo”

“Whaaaat?? How are you going to do that??” Kaburj akaliza kwa mshangao kama ameona jini.

“Wait and see!! You guys are going to fucking love this one” nikaongea na kutoa tabasamu kwa raha kabisa.

APRIL, 1974: DAR ES SALAAM

Siku mbili zilizopita kijana wa Kitanzania, Charles Bernard Kajuna mwenye miaka 36 akiwa na mkewe Sophia Ndege waliwasili jijini Dar es Salaam wakitokea jijini Nairobi ambako Bernard alikuwa ni Mkurugenzi wa Kitego cha Ukaguzi wa ndani kwenye Bank ya Detta & Boyd Bank.

Ujio wake kutoka Nairobi kurudi Dar es Salaam ulitokana na wito wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wiki moja iliyopita.

Kutokana na staili ya uongozi wa Rais, ilikuwa ni ngumu kujua ni kwanini amekuita.

Kulikuwa na utani kipindi hicho katika maongezi ya Watumishi wa uuma wakipenda kusema “ukiitwa Dar, utarudi kichwa chini au utarudi unaruka ruka”.! Wakimaanisha kwamba ukiitwa Dar kwa Rais, eidha unaenda kupandishwa cheo au kufukuzwa kazi.

Lakini Charles hakuwa mtumishi wa Umma, alikuwa ameajiriwa na kampuni binafsi, tena siyo kampuni ya kitanzania.. Alikuwa anafanya kazi kwenye benki binafsi, Detta & Boyd, Benki kutoka Africa ya Kusini iliyokuwa na matawi kadhaa nchini Kenya kwenye miaka hiyo ya sabini.

Hapa Dar walikuwa wamefikia kwenye Hoteli ya Kilimanjaro iliyopo katikati ya jiji.

Leo ndio siku ambayo alikuwa anatakiwa kwenda Ikulu kuonana na Rais.

“Sijui wanataka nini hawa watu” Charles akaongea huku akiwa mbele ya kioo anarekebisha tai vizuri.

“Labda Rais anataka kukupa Uwaziri!!” Mkewe Sophia akamjibu kwa utani.

“Hahahah natamani iwe hivyo” Charles naye akajibu kwa utani.

“Hivi mawaziri nao wanakaa Ikulu pale pale” Akauliza Sophia.

“Hahaha wewe mke wa Waziri mtarajiwa utanitia aibu sasa.. Ikulu anakaa Rais” Charles akajibu huku anatembea kumfuata mkewe aliyekuwa amekaa juu ya kitanda.

“Kwahiyo sisi tutakaa wapi??”

“Eeee taratibu mama, usianze kupiga hesabu kana kwamba naenda kupewa uwaziri kweli.. Kwanza mawaziri wote ni lazima uwe mbunge” Chales akajibu huku anamkumbatia mkewe na kupapasa tumbo lake la ujauzito.

“Mpaka mchana nadhani nitakuwa nimerudi”

“Jitahidi urudi haraka nimemwambia mpishi apike mboga za majani za kutosha, sitaki ule vyakula vyako vile vya kizungu huko unakoenda” Sophia akaongea huku anainuka akiwa amejishika kiuno ‘kusapoti’ tumbo lake kubwa.

“Mboga za majani za nini mkewangu! Umesahau ninavyokwambia kila siku?” Charles akaanza utani.

“Hahahaha sitaki huo msemo wako kuusikia tena”

“Ngoja niseme tu ilo usisahau tena!”

“Hahahahahah sitakiiii”

“Ukiwa na hela huitaji mboga za majani, vitamini zinakuja zenyewe automatic.!”

“Hahahahahahahah..!” Sophia akaangua kicheko.

Japokuwa miaka hii ilikuwa na mfumo dume uliokithiri, lakini kulikuwa na wanandoa wachache ambao mume na mke waliishi kirafiki kabisa, na moja ya wanandoa hao alikuwa ni Charles na mkewe Sophia.

Labda hii ilitokana na Charles kupata fursa ya kukaa nchini Uingereza kwa masoma kwa miaka kadhaa, labda ndio sababu alikuwa na “uzungu”, kwani licha ya tofauti kubwa ya umri, Charles akiwa na miaka 36 na Sophia akiwa na miaka 22 tu, lakini walipendana na kuishi kirafiki kabisa.

Charles akamuaga mkewe na kusuka chini ya hoteli.

Kuna gari ilikuwa inamsubiri na akapanda, safari ya kwenda ikulu ikaanza.

Kama dakika kumi baadae walikuwa tayari wako nje ya geti la Ikulu.

Baada ya kuandikisha jina na walinzi kuangalia kumbukumbi zao kama Rais anategemea mgeni huyo leo hii, hatimaye wakaruhusiwa kuingia.

Baada ya kushuka tu kwenye gari akaongozwa na wasaidizi wa Rais mpaka kwenye ofisi.

Katika miaka hiyo kabla ya kubadilishwa hapo baadae, ilikuwa ukiingia Ikulu ofisi ziko upande wa kulia mwa jengo kuu.

Kulikuwa na vyumba kadhaa vya maofisi ya wasaidizi wake, kisha kuna mlango wa kuingia ofisini kwa rais. Ukiingia tu unakutana na ‘sebule’. Subule hii ilikuwa ni mapokezi ambapo kulikuwa karibia na viti vinane ambavyo vimepangwa upande mmoja viti vinne na mwingine viti vinne na katikati kuna meza, kisha baada ya kutoka mapokezi unakutana na korido yenye urefu kama wa Mita nne au tano kisha unakutana na mlango mwingine ambao nao ukifungua unakutana na sebule nyingine yenye ‘masofa’ ya fahari kidogo na meza kubwa.

Hii haikuwa mapokezi. Hii ilikuwa ni sebule ya rais kupumzika au kungea na wageni endapo kama wakiwa ni kikundi cha watu au ugeni mzito.

Ukikatana kona kushoto kutoka kwenye sebule hii ndio unakutana na Ofisi yenyewe ambayo yumo Rais.

Walipofika hapa ndipo Sekretari wa Rais, akamuambia Charles asubiri hapo Rais ana mgeni ofisini kwake.

Mara kwanza Charles hakuelewa kwanini hakuambiwa asubiri kwenye ile mapokezi ya kwanza na matokeo yake ameletwa sehemu hii ya Rais kupumzika, lakini baadae alikuja kuelewa kuwa walikuwa hawataki mtu mwingine amuone Charles pale mapokezi.

Sekretari huyu wa Rais aliyeitwa Frederick Ndunguru, alimletea chai Charles na wakawa wanakunywa pamoja huku anampa kampani ya maongezi ya hapa na pale wakisubiri huyo mgeni aliye ndani ya ofisi atoke.

Kama dakika kumi baadae mgeni huyo alitoka, na alikuwa ni Waziri wa Fedha Bw. Abdul Aziz, mtanzania mwenye asili ya kiarabu.

“Hujambo kajuna” Wazidi Aziz akamsalimia Charles.

Charles akasimama kwa heshima, “Sijambo, shikamoo Mzee”

Waziri akaitikia na kuobdoka. Charles alishangaa kidogo kwa kutambuliwa mpaka jina na Waziri Aziz.

“Rais anaweza kukuona sasa!” Sekretari wa Rais Bw. Frederick Ndunguru alimkaribisha Charles baada ya kuingia na kutoka ofisini kwa Rais ambako alienda kumpa taarifa juu ya uwepo wa Charles.

Charles akafungua mlango kwa heshima zote na kuingia Ofisini.

Ofisi ya Rais ilikuwa maridhawa kabisa. Haikuwa na vitu vingi sana lakini ilipendeza. Kulikuwa na kabati la vitabu mkono wa kushoto, mkono wa kulia ukutani kulikuwa na michoro kadhaa ukutani pamoja na picha. Nyuma ya kiti cha Rais kulikuwa na dirisha kubwa ambalo lilikuwa lina mapazia murua kabisa.

Mbele ya Rais kulikuwa na meza ya ofisi ya saizi ya kati ya mti wa mpingo na upande wa pili wa meza kulikuwa na viti viwili kwa ajili ya kukaa mgeni kuongea na Rais.

Rais, alikuwa ananiangalia na kutabasamu nilivyokuwa naishangaa ofisi yake.. Hakuna mzee japokuwa tayari mvi zilianza kwa mbali kuonekana kichwani mwake. Ndio athari ya “mzigo” wa Urais. Mwili unaanza kuzeeka kabla ya muda wake.

“Karibu sana Kajuna, keti kwenye kiti” Rais, akamkaribisha Charles.

“Asante sana mzee, shikamoo” Charles akaitikia kwa heshima huku akiketi kwenye kiti, akitoa tabasamu fulani la kama aibu hivi baada ya kugundua Rais amegundua jinsi anavyoshangaa ofisi.

“Usijali, kila mtu akiingia humu mara ya kwanza lazima ahakikishe anapata kumbu kumbu kamili kichwani juu ya ofisi inayoendesha nchi hahahah” Rais akaongea kwa utani.

Rais alikuwa na staili adhimu kabisa ya uongozi. Licha ya kuwa moja ya viongozi wenye ushawishi zaidi barani Africa alikuwa na namna ya kumfanya mtu awe ‘comfortable’ anapoongea naye.

Akaanza maongezi kumuuliza Charles habari za Nairobi, humo humo akatumbukizia stori za hapa na pale anazozijua kuhusu Nairobi, na baada dakika kadhaa akaanza kuongea lengo la kumuita hapo.

“Charles, Kuna jambo nataka utusaidie” Rais akaongea akiwa serious.

“Ndio Mzee..” Charles akaitikia.

“Siki si nyingi tutaivunja East African Currency Board.!” Rais akaongea huku akiangalia ‘reaction’ ya Charles.

“Aisee! Sijawahi kusikia hilo Mzee ingawa niko kwenye nyanja ya banking” Charles akaongea kwa mshangao.

“Ni taarifa ya siri sana huwezi kuisikia”

“Aisee italeta mtikisiko sana kwenye sekta ya benki” Charles akagusia.

“Charles.. Unajua kipindi tunaanzisha East Africa Community, lengo letu ni kwamba ndani ya muda mchache tuwe na political federation.. Na ndio hii ikatufanya kuanzisha East Africa Currency Board tukiwa na lengo baadae ije kuwa East Africa Central Bank.. Sijui unanielewa sawa sawa Charles..?”

“Nakuelewa Mzee.!”

“Sasa miaka ya karibuni kitu hiki kinaanza kuonekana kama ndoto ambayo haitatimka… Kila nchi imekuwa na lwake sasa.. Vikwazo vimekuwa vingi, hasa wenzetu wa Kenya.. na tunataarifa kuwa wameanza michakato ya kuanzisha benki kuu yao..”

“Haiwezekani mzee! Watafanyaje hivyo ilhali wote tunatumia sarafu moja..” Charles akashangaa.

“Tuna taarifa kuwa wako na huo mchakato.!”

“Aiseee.!” Charles bado alikuwa na mshangao.

“Sasa kuna suala tunataka utusaidie Charles..” Rais akaongea akiwa amemkazia macho Charles.


WIKI TATU MBELE

Charles na Mkewe Sophia walikuwa wamepatiwa nyumba ya serikali maeneo ya Mikocheni A, nyumba ikiwa karibu kabisa na bahari.

Mkewe alikuwa analaani sana kupewa nyumba naeneo haya kwani harufu kutoka baharini ilikuwa inamkera sana ukizingatia ni mja mzito.

Siku hii majira ya kama saa nne usiku walikuja kugongewa mlango.

Charles akaenda kuwafungulia.

Kwa mshangao mkubwa ugeni huu ulikuwa ni wa waziri wa fedha Bw. Abdul Aziz na mzee tajiri na maarufu jijini Dar es salaam aliyeitwa Chifu Sekioni.

Baada ya kuwakaribisha sebuleni hawakupoteza muda, wakaenda moja kwa moja kwenye lengo la kufika hapa nyumbani kwa Charles.

“Ndugu waziri, vipi kuna dharura gani mbona usiku usiku hivi?” Charles akauliza baada ya wote kuketi.

“Hakuna dharura, ila kuna ‘ofa’ tumekuletea” Akaongea Chifu Sekioni.

“Ofa??” Charles akaongea kwa mshangao.

“Ndio! Tunataka kukufanya kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ambayo itaundwa miezi michache ijayo” Waziri Azizi akaongea bila kuzunguka mbuyu.

“Wat?? Haya maelezo unayonipa ni ya kiserikali au??” Akauliza Charles kwa mshangao.

“Hapana, siongei kama waziri hapa! Naongea mimi binafsi kama Abdul Aziz”

“Ok! Nawasikikiza” akaongea Charles.

“Kama utaoendezwa na ofa yetu, kesho atakuja kijana muda wa usiku kama huu kukuchukua na piki piki.. Kama utakuwa tayari njoo naye mpaka atakapokuleta ili upate maelezo kamili.” Akaongea Chifu Sekioni huku wanaanza kunyanyuka.

“Sijawaelewa ati mnachokiongea!”

“Una masaa ishirini na nne kutafakari” akaongea waziri Aziz kisha wakaondoka.

Wakamuacha Charles akiwa amechanganyikiwa. Hajui ni nini kimetokea pale. Huu ulikuwa utani au suala gani??

Akarudi kulala.

Kesho yake muda kama ule, kweli akaja kijana na piki piki. Bila Hiyana, charles akakwea piki piki na kuondoka na huyo kijana.

Alikuwa na sababu mbili za kumfanya aende.. Moja ni ofa aliyoambiwa kuwa wanaweza kumfanya kuwa Gavana wa Benki Kuu.! Hakuna ndoto kubwa ya ‘banker’ yeyote kama kupata fursa ya kuwa Gavana wa benki kuu.. Sababu ya pili ilikuwa ni rahisi tu, “usikatae wito, kataa maneno”

Kijana huyu akaendesha piki piki kutoka Mikocheni mpaka Upanga mtaa wa Isevya.

Hapo wakaelekea kwenye nyumba Fulani yenye geti jeusi na kugonga.

Baada ya kufunguliwa, wakaingia ndani na yule kijana akabaki sebuleni huku Charles akipelekwa kwenye chumba fulani hivi.

Chumba hiki kwa ndani kilikuwa kama chumba cha daktari mandhari yake.

Dakika chache baadae akaingia mwanamama mmoja akiwa na kibegi cheusi.

Hakuwasalimia wala nini, akaweka kibegi juu ya meza na kutoa sindano na kama kikontena hivi.

“Naomba mkono wako wa kushoto” yule mama akaongea.

“Hey, mnataka kunitoa damu ili iweje??” Charles akang’aka.

Yule mama mwenye sindano hakusema chochote, akamgeukia mwenyeweji wao na kumwangalia.

Mwenyeji wao ambaye alikuwa ni mama wa makamo hivi akaanza kuongea. Akamshika Charlea begani na kuongea kwa utaratibu..

“Charles, kama una amani na hiki kinaxhofanyika uamuzi ni wako, inaweza kugeuza na kurudi nyumbani kwako sasa hivi”

Charles akajifikiria. Akaona kama ameanza kumla ng’ombe ni vyema amalizie kabisa hadi mkia.

Akampa mkono yule mama.

Yule mama akamtoa damu na kisha kuhifadhi sindano kwenye kikontena.

Kisha akamchukua alama za vidole kwa kutumia wino na kugusishwa vidole kwenye karatasi.

Baada ya hapo yule mama akafungasha vitu vyake kwenye kibegi chake cheusi na kuondoka.

Baada ya hapo yule jamaa mwenye piki piki usiku huo huo akamchukua Charles kutoka hapo upanga na kumpeleka maeneo ya Oysterbay, mtaa wa Mzinga.

Wakaelekea kwenye nyumba moja yenye Ukuta mkubwa na geti kubwa jeusi na kugonga.

Walipofunguliwa na mlinzi, wakaingia ndani.

Ndani kulikuwa na nyumba kubwa na eneo la mbele yalipaki magari kadhaa.

Yule kijana akamuongoza Charles ndani ya nyumba mpaka kwenye chumba fulani hivi.

Ndani ya hiki chumba kilikuwa kama ofisi hivi na alimkuta yule mzee, Chifu sekioni Peke yake amekaa.

“Karibu sana kajuna” Chifu sekioni akamkaribisha kwa bashasha kwenye kiti.

Chifu Sekioni alikuwa amevaa kaunda suti nadhifu nyeusi na mkono wa kushoto usawa wa titi alikuwa na pini fulani ya dhambarau ambayo katikati ilikuwa na kama mchoro wa kichwa cha simba kwa rangi ya dhahabu.

“Tufanye haraka haraka wengine wanatusubiri” Chifu akaongea huku anaweka makaratasi mezani.

“Wengine akina nani?” Charles akauliza.

“Si umeona magari yamepaki hapo nje… Wengine wapo chumba kinachofuata wanatusubiri sisi tuanze kikao” Chifu Sekioni akaongea huku anaandika andika kwenye karatasi.

“Na unaweza kunambia “nyiny”, ni akina na nani na lengo la kuniita hapa ni nini?” Charles akauliza.

Chifu Sekioni akatabasamu.

“Tunaitwa The Board, na lengo la kukuita hapa utalijua kwenye kikao ndani ya muda mchache..”

Charles akabaki amemkodolea macho tu.

“Nikumbushe majina yako kamili tafadhali” Chifu Sekioni akauliza huku anajiaanda kuandika kwenye yale makaratasi.

“Charles Bernard Kajuna”


January, 2017

Leo ndio ilikuwa siku ambayo nilikuja kulipia ofisi.

Nilikuwa nimeongozana na Kaburi pamoja na Cheupe.

Mwenye nyumba alikuwepo, dalali pamoja na mtoto wake mwenye nyumba ambaye alikuja kama shahidi wa makabidhiano ya hela na kusaini mkataba wa kupanga.

“Nikumbushe majina yako kaka” akaongea dalali Tunda akiwa anaandika andika kwenye ule mkataba wa kupanga.

“Rweyemamu Charles Kajuna” nikamjibu.

Baada ya hapo tukasaini mkataba, nikawakabidhi hela wakaondoka.

Tukabaki, mimi, cheupe na Kaburu.

Tukaanza kukagua kagua mandhari ya ofisi.

“Iko poa?” Nikawaliza.

“Yeah! Iko poa sana ingawa bado sijui unataka kuifanyia nini?” Kaburu akajibu.

“Well now inabidi niende mjini kununua vifaa vya ofisi, meza, viti na kadhalika” nikaongea huku nimeweka mikono mfukoni nikiwaangalia wote na kutabasamu.

“Kabla ya yote unaweza kutudokeza mpango wako?? I really hate being in the dark.!” Kaburu akaongea serious akiwa amenikazia macho.

“Ok! Ngoja niwadokeze kiduchu tu.!” Nikatabasamu.

Zilikuwa zimepita siku mbili toka nilipie kodi katika jengo ambalo ndilo nilikua nimedhamiria kukifanya kuwa ofisi ili kufanikisha mpango wa kuzipata files kutoka katika strong room ya Makao makuu ya benki.

Ofisi ilikuwa na vyumba vitatu.

Chumba cha mbele kabisa tulipanga kitumike kama mapokezi, chumba kingine tutakitumia kama chumba cha mikutano na chumba kinachobakia kitatumiaka kama ofisi yenyewe.

Katika hiki chumba cha ofisi nilijitahidk walau kiwe na mzingira fulani ya kuonekana kwamba ni ofisi halisi.

Kwahiyo nilikweka kabati zuri la “kichina” na kuweka files, meza nzuri ya kichina pia, pamoja na kiti kizuri cha “executive”.!

Wote watatu tulikuwa hapa ‘ofisini’. Yaani mimi, kaburu na Cheupe.

“Mnaonaje tangazo limekaa poa?” Nikawauliza, mimi nilikiwa nimekaa kwenhe kiti, kaburu alikuwa mkono wangu wa kushoto na Cheupe mkono wa kulia wote wameniinamia wakiasoma nilichokuwa nimekiandika kwenye laptop.

“Imekaa poa nadhani, I hope it’s going this is going to work.. La sivyo tutaozea jela TISS wakitukama huu mchezo tunaoufanya” Kaburu akaongea huku kama kawaida hake akiweka tahadhari.

Katika laptop, hilo “tangazo” lenyewe nilikua nimeliandika kama ifuatavyo:

“Exciting opportunity… Kama unataka kufanya kitu cha tofauti na kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.. Si kwa faida ya kiuchumi pekee bali pia kubadili ulimwengu

Tunaitwa UNIMAX MARKETING, Tunatafuta vijana 12 wenye good Marketing Skills

Tupigie: 0718 096 811″

“Looks good.!” Cheupe naye akakubali kuwa tangazo limekaa poa.

“OK.! Napost sasa.!”

Nikaanza kupost tangazo kwenye miamtandao mbali mbali. Lakini hasa hasa nililenga mtandao wa Jamii Forums na mtandao wa Zoom.

Nikafungua anuani ya zoom na baada ya kujisajili.. Nikapost tangazo.

Baada ya hapo nikafungua anuani ya tovuti ya Jamii Forums, kisha nikatumia kama dakika tatu au nne kujisajili kama mwanachama kisha nako nikapost tangazo.

“Tayari..!” Nikaongea huku nainuka kwenye kiti na kujinyoosha.

“Kwahiyo kifuatacho itv??” Cheupe akauliza.

“Tunasubiri response ya watu watakaotutafuta”

Nikaongea huku naangalia simu mezani.

Nilikua nimechukua simu moja kati ya zile nilizonunua Dodoma na kuweka ‘line’ yenye namba 0718 096 811 kama Namba ya mawasiliano ya “kampuni” ya Unimax Marketing.

“Ray hii idea yako itatufitinisha na TISS, I can feel it” Kaburu akaongea huku anatembea tembea mule ndani ofisini.

“Usijali kuhusu TISS, wanachotaka ni file za The Board haijalishi tunazipataje” nikamjibu huku nakaa tena kwenye kiti.

“Yeah! Lakini sio muda wote ambapo ‘the end ina justify the means'” Kaburu akaongea tena akinipa tahadhali.

“Man, if you have a better idea let’s hear it… Sioni njia nyingine aisee” nikamjibu.

“It’s genius though.!” Kaburu akaongea kwa kuniinjoi.

“Hahaha.!” Nikacheka kwa kumuinjoi pia.

Tukaendelea na maongezi kwa takribani dakika kumi nyingine. Mara ghafla simu pale mezani ikaanza kuita.

“Here we go!” Nikainua simu na kuipokea kwa shauki kubwa.


October, 1974: Dar es Salaam

Charles Kajuna alikuwa na heka heka za kiofisi kwa muda wa takribani miezi sita yote hii.

Rais alikuwa amemchagua kuwa Katibu Mkuu wa Hazina, ingawa nafasi hii alikuwa amepewa kama ‘cover’ kwa ajili ya shughuli maalumu aliyokuwa amempa.

Charles alipewa jukumu kuu la kusimamia uanzishwaji wa benki kuu ya Tanzania.

Kwa miezi sita yote hii alikuwa anasafiri kila kona ya dunia ili kufanikisha suala hili.

Rais alikuwa anataka mpaka kufikia mwezi January 1975 nchi tayari iwe na benki kuu.

Charles ndio alikuwa amerejea kama wiki moja iliyopita akitokea Makao makuu ya IMF ambao walikuwa wanasaidia kuandaa muswada wa kuwasilisha bungeni ili kuanzishwa kwa benki kuu (Central Bank Legislation).

Baada ya kurejea, Charles alikuwa anaendelea na mchakato wa kutengeneza timu ya wataalamu watakaokuwa kama wafanyakazi wa mwanzo kabisa wa Benki kuu na watakaosaidia kuanza kwa shughuli za benki kuu.

Hii ilimlazimu kuchukua mpaka wataalamu wengine kutoka nje ya nchi, kwa mfano alimchagua Mr. Cleoford Truman kutoka Benki kuu ya Uingereza kuwa Meneja wa kitengo cha Currency an Domestic Banking Operations.

Vivyo hivyo kulikuwa na wataalamu kutoka nchi nyingine kadhaa.

Mwishoni mwa mwezi huo wa Octeber ndipo akataarifiwa kuwa kampuni ya ya Messrs Thomas de la Rue kutoka uingereza ambao walipewa tenda ya Sarafu na noti walikuwa tayari kuleta mzigo wa kwanza wa sarafu ndani mwezi mmoja ujao.

Kwa kuwa benki kuu ndio kwanza ilikuwa inaannza, hivyo haikiwa na Strong Room kwa ajili ha kuhifadhi kiwango kikubwa hicho cha Sarafu.

Ndipo hapa intupeleka kwenye kikao cha siri kubwa ambacho waziri wa fedha Ndugu, Abdul Aziz na mzew tajiri Chifu Sekioni ambao wote ni mwanachama wa kikundi cha siri cha The Board, walimuita Charles ili waweze kumpa maelezo ha kumshawishi Rais juu ha namna ha kuifadhi huo mzigo wa Sarafu utakao wasili.

Kipindi haya yote yanatokea, Charles alikuwa anamalizia ujenzi wa nyumba yake maeneo ya Upanga.

Kipindi kile April, alipoitwa na Rais akitokea Nairobi na baadae kukabidhiwa nyumba ya serikali maeneo ya Mikocheni A, mkewake akiwa bado mjamzito alikiwa anachefukwa sana na harufu kutoka baharini.

Hii ilimfanya katika wiki zile zile za kwanza kutafuta eneo kwa ajili ya kujenga nyumba.

Akafanikiwa kupata plot maeneo ya Upanga mtaa wa Kilombero na mara moja akamlipa mkandarasi shilingi laki moja na nusu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.

Hadi kufikia muda huu octoba, mkewe alikiwa ameshajifungua tayari mtoto wa kike aliyempa jina la mama yake, Dorothea!

Nyumba yao ya Upanga ilikuwa imeisha na ilikuwa inafanyiwa ‘finishing’ ndogo ndogo.

Sasa, katika kipindi hiki cha mwishoni mwa mwezi oktoba ndipo alipoitwa katika kikao cha siri na Waziri wa fedha Ndugu, Abdul Aziz na Chifu Sekioni.

Kikao hiki kilifanyika usiku Nyumbani kwa chifu Sekioni maeneo ya Oysterbay.

Walikuwa peke yao watu watatu tu katika sebule kubwa ya nyumba hiyo.

Baada ya maongezi ya hapa na pale, hatimaye ukawadia wasaa wa kujadili lililowakutanisha hapo.

“Kajuna, nadhani wote hapa tunafahamu kuwa mwezi ujao tunapokea shehena GA kwanza ya Sarafu” akaongea Waziri Abdul Aziz.

“Ni sawa kabisa ndugu Waziri” Kajuna akaitikia.

“Nadhani unafahamu kuwa ni kwa kiasi gani tunahangaika kupata sehemu yenye kutosha na usalama ya kuhifadhi kiasi kikubwa hicho cha Sarafu” akaendelea kueleza Waziri Abdul Aziz.

“Ni kweli lakini nadhank juzi tulishauriana mimi, wewe na waziri wa mipango kuwa shehena ya Sarafu ihifadhiwe kwenye majengo ya Makao makuu ya jeshi pale mgogoni” Charles akafafanua, akieleza kuhusu makubaliano hayo ya kuhifadhi Shehena ya sarafu kwenye makao makuu ya jeshi ambapo kipindi hicho yalikuwa yapo magogoni.

“Hiyo ndiyo sababu ya kukuita hapa Charles” akadakia Chifu Sekioni.

“Ndio Chifu!” Charles akaongea akimsikiliza Chifu Sekioni.

“Siku chache zijazo wewe na Waziri hapa mtaenda kumbrief Rais kuhusu uamuzi mlioufikia kuhusu sehemu ya kuhifadhi Sarafu.. Sasa waziri kuna jambo atalendekeza tunataka uliunge mkono kwani unafahamu katika hii ishu ya Uanzishwaji wa benki kuu hakuna mtu ambaye Rais ana muamini zaidi yako” Chifu Sekioni akafafanha kwa kirefu.

“Charles..” Akaanza kuongea, “tukienda kumbrief Rais kuhusu hifadhi ya shehena ya Sarafu nitapendekeza kuwa tusihifadhi shehena yote TPDF.. Kiasi kidogo walau hata robo ya shehena nzima tihifadhi sehemu nyingine”

“Na kwanini tihifadhi sehemu nyingine?” Charles akauliza.

“Nitampa sababu yoyote ile, mfano labda pale TPDF hapatoshi kuhifadhi sarafu zote.. Au si shahihi kimkakati kuweka shehena yote sehemu moja na kadhalika na kadhalika.. Nitatafuta sababu yenye kufaa kumpa” waziri Abdul Aziz akaeleza.

“Na ulikuwa unapendekeza hiyo robo ya shehena ikahifadhiwe wapi?” Charles akauliza kwa shauku.

“Nadhani kuna nyumba unaijenga pale upanga na bado haujahamia kwa hiyo…..”

Kabla Waziri hajamaliza, Charles akamkatisha.

“No no no!! Huo utakuwa uhuni uliopitiliza.. Hatuwezi kuhifadhi Sarafu za serikali ya Jamuhuri kwenye personal property!! Siwezi kukubali hilo” Charles akaongea kwa kupaniki mpaka akainuka kutoka kwenye kiti pale sebuleni

“Sikiliza Charles.. Kama waziri nitasimamia mchakato kuhakikisha tunakodi jengo lako kwahiyo wewe hautaishi pale.. Pia milango itaboreshwa kuwekwa milango mingine na maafisa wa TPDF watakiwa wanalinda masaa 24 kwahiyo hakutakuwa na upotevu wowote qa Mali ya umma” akaongea waziri kumpooza Charles ambaye alikuwa amekwishaanza kupaniki.

“Kwahiyo sababu hasa ya kutaka kuhifadhi sarafu kwenye private propeprty ni nini?” Akauliza Charles akiwa amepoa kidogo na kukaa chini kwenye kiti.

“Tunaamini kuwa ukisha teuliwa kuwa gavana walau utakuwa na ‘access’ ya urahisi kwenye strong room ktakayokuwa upanga kuliko strong room ya magoglni ambako kuna ofisi ya CDF.” Waziri Abdul Aziz akafafanua.

“Na sababu ya kunitaka niwe na access ya ufahisi kwenye strong room ni ipi?” Charles akahoji.

“Kuna nyaraka Chairman anataka kukupa na anahitaji zihifadhiwe sehemu salama salama haswa! Ni nyaraka nyeti mno” akaongea waziri.

“Chairman, chairman, Chairman!! Huu mwezi wa sita sasa nimekuwa mwanachama wenu lakini simjui hata kwa sura huyu Chairman zaidi ya kusikia tu kila siku.. Chairman, Chairman!!” Charles akaongea akiwa na hasira kidogo.

“Utaonana naye ndani ha wiki mbili zijazo! Anahitaji kuonana na wewe kwa sababj maalumu” akadakia Chifu Sekioni.

“Sababu gani?” Charles akaongea kwa mshangao na shauku kubwa.

“Amekuchagua kuwa ‘The Book Keeper'” akamalizia Chifu Sekioni.

January, 2017: Dar es Salaam

Kwa muda wa siku mbili zilizopita tulikuwa tunapokea simu za vijana mbali mbali ambao walikuwa wanataka fursa tuliyoitangaza katika mitandao ya Zoom na Jamii Forums.!

Kwa siku mbili hizo tulikuwa tumepokea jumla ya simu arobaini na mbili za vijana wakitaka hiyo fursa.

Kila ambaye tulikuwa tumeongea naye, hatukumueleza chochote zaidi ya kumuelekeza ofisi zetu zilipo na kumtaka afike siku ya leo saa tano asubuhi.

Katika kile chumba ambacho tulikitenga kama chumba cha mikutano kulikuwa na vijana ishirini na saba tayari walikuwa wamefika.

Pale reception kulikuwa na vijana nane ambao bado Cheupe alikuwa bado hajawaruhusu kuingia kwenye chumba cha mikutano.

“Wanakusubiri ujue!” Cheupe aliongea akiwa anaingia kwenye kile chumba kingine ambacho tulikiweka kiwe ofisi.

Mimi na Kaburu tulikuwa tunajadili mambo mawili matatu ya mwisho kabla ya kwenda kuongea na vijana.

“Naenda kuongea nao mama dakika chache tu” nikaongea huku narekebisha tai vizuri.

Wote watatu tulikuwa tumevalia suti nyeusi.

“Au labda utembee kufanana na Speech ha mwisho ya Rais Mkapa Ikulu” Kaburu akapendekeza.

Nilikua nahaha kutafuta maneno yenye kugusa kuongea na hawa vijana.

Ili tulichokipanga kifanikiwe tulikuwa tunapaswa kuwaamisha hawa vijana kuwa tunachokifanya ni halisi. Pia nilihitaji kuamsha hari zao ili tukafanye nilichokipanga kwa moyo wote.

“Kwani mnahangaika na nini?” Cheupe akauliza akiwa ananisaidia kuweka tai vizuri.

“I need a good speech! Changia mawazo mama..”

“No! Mambo ya speech hata simo kabisa hiyo sekta”

“Daaamm! Yani hapa nawaza kila movie yenye speech Kali niliyowahi kuiona, kila kitabu chenye speech kali but still nashindwa kupata maneno ninayoyataka” nikaongea huku nikielekea mezani na kuchukua kipande cha karatasi na kuanza kuandika andika.

“Wamefika wangapi mpaka sasa?” Nikamuuliza Cheupe.

“Kule ndani wako ishini na saba na hapo reception wapo wanane.. Ulisema nisiruhusu mtu kuingia kule ndani baada ya saa tano kamili.. So hao wa hapo reception walifika baada ya muda huo” Cheupe alikiwa anaongea huku anachungulia reception kuhakikisha kama yuko sahihi na idadi anazoniambia.

“OK! Twendeni tukazungumze nao..” Nikaongea huku nakunja kile kikaratasi nilichokuwa nakiandika na kukiweka mfukoni.

“Ushajua unaenda kuongea nini?” Kaburu akaongea huku ananifuata tukitoka nje kwenda reception.

“Yap! Nishapata speech ya kuongea..”

Kwanza tukaelekea moja kwa moja mpaka reception ambapo kulikuwa na vijana wanane wamekaa wanasubiri kama ambavyo Cheupe alisema.

“Habari zenu” nikawasalimia wale vijana kwa pamoja.

“NZURI.!” wakaniitikia kwa pamoja.

“Mnakumbuka tulivyoongea kwenye simu niliwaambie mfike saa ngapi?” Nikawauliza.

Wakaa kimya huku wanageuka na kuangaliana.

“Nikisema saa tano, na wenzenu wengine walishafika wako kule ndani” nikaongea huku nanyoosha mkono kwenye chumba cha mikutano.

“Aah Mkuu mimi naishi mbali kidogo” kijana mmoja akaanza kujieleza.

“Wakuu! Nashukuru sana kwa muitikio wenu wa kuja lakini hii fursa hamtaweza.. Kwa hiyo niwatakie siku njema na Mungu akipenda tutaonana wakati mwingine” nikaongea huku nawaangalia kwa sura ambayo nilikuwa nawaashiria waondoke.

Wakainuka kwa unyonge na huzuni na kuanza kuondoka.

Nilisimama pale pale nikiwaangalia wakiondoka mpaka mtu wa mwisho alipotoka mlangoni. Kisha nikageuka kwa Kaburu na Cheupe.

“Duh! That was cruel” Cheupe akaongea huku akiigiza kuweka uso wa kutia huruma.

“Hatuna jinsi, tunahitaji vijana 12 pekee so inabidi tutafute namna ya kuwapunguza!” Nikaongea huku narekebisha tena tai.

“Sasa twende tukamalizane na hawa wa huku ndani.

Tulipoingia Kaburu na Cheupe walikaa kwenye viti vilivyokuwa karibu kabisa na mlango. Mimi nikienda kusimama mbele kabisa ya chumba hiki cha mikutano nikiwatazama moja kwa moja kundi hili la vijana ishirini na saba waliokaa kwenye viti ambavyo tulikuwa tumevikodi asubuhi hii.

Nilikuwa nimesimama kama vile mwalimu mbele ya darasa.

Tulipoingia walikuwa wanapiga soga, ila walipoona nimesimama mbele nawatazama bila kusema chochote wote wakanyamaza. Chumba chote kikawa kimya.

“Habari yenu.!” Nikawasakimu.

“NZURI.!” Wamaitikia kwa pamoja.

Nikaa kimya kama sekunde thelathini hivi, kisha nikaendelea.

“Tovuti ya Zoom inapata zaidi ya watembeleaji milioni moja kila siku, pia mtandao wa Jamii Forums una wanacha zaidi ya laki tatu na nusu na zaidi ya watu milioni moja na nusu wanaitembelea kila siku.. Lakini katika jumla ya watembeleaji hao milioni mbili na nusu.. Ni nyinyi ishirini na saba pekee ambao mlielewa tangazo letu na kama hamkuelewa ndani ya muda mchache nitawaeleza maana ya siri ambayo tuliificha ndani ya lile tangazo na miezi michache ijayo watu wote hao milioni mbili unusu watajilaumu kwanini hawakuchangamkia hii fursa”

Nikanyamaza midogo na kuwatazama.

Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa kalamu ya wino.

“Hii kalamu dukani inauzwa shilingi mia mbili.. Lakini a good sales person ana uwezo wa kukuuzia kwa shilingi elfu tano na ukaridhika kabisa rohoni mwako… Sasa Dada hapa atapita na kuwapa karatasi kila mmoja wenu.! Katika hiyo karatasi nataka uandike namna ambavyo utanishawishi niweze kununua kalamu hii kwa shilingi elfu tano badala ya shilingi mia mbili.! Na una dakika kumi na tano kuandika huo ushawishi, na ukimaliza utakuja hapo mapokezi Dada atakuleta ofisini kwangu”

Nikanyamaza tena kidogo na kuwatazama.

“Kumbuka kuwa watu wote unaowahusudu na kutamani kuwa kama wao wote wana kitu kimoja kinachofanana.. they are good sales people!! Awe ni kiongozi kama Nyerere, au Luther King, au Mahatma au labda awe mjasiriamali kama Bakhressa, au Dangote au Steve jobs! Wote hawa wanafanana kwa kitu kimoja kikubwa.. Great sales skills!! Kiongozi bora ni yule mwenye ustadi wa kuuza mawazo yake kwa wananchi na kukubalika, na mjasiriamali bora ni yule mwenye ustadi wa kuiuza bidhaa yake ikapenha kwenye Jamii.. Sasa kama ambavyo nieleza kwenye tangazo, tunataka kuwapa fursa adhimu kabisa lakini kabla sijafanya hivyo nataka kujua if you have what it takes kuifanya hiyo kazi..”

Nikaangalia saa mkononi.

“Mna dakika kumi na tano ili kunishawishi!! Good morning everyone!”

“GOOD MORNING!” Wakaitikia kwa pamoja kwa hamasa.

Mimi na Kaburu tukatoka kwenye chumba tukimuacha Cheupe akigawa karatasi nyeupe na peni.

“Wow! Hotuba maridhawa kabisa” Kaburu akanipongeza.

“Huo ni mwanzo tu” nikatabasamu.

Tayari ilikuwa inakaribia saa kumi kamili jioni. Tulikuwa na “kikao” ofisini watu watatu, Mimi, Cheupe na Kaburu.

Kikao chetu kilihusu kuchambua majina ya vijana kumi na mbili tuliokuwa tunawahitaji. Tulikuwa tumetumia karibia masaa mawili kubishana kuhusu kijana yupi tumchukue na yupi tumuache.

Wenzangu Cheupe na Kaburu walikuwa hawaafikiani na mapendekezo yangu yote lakini nilitumia kura yangu ya “veto” kupitisha wale ambao nilikuwa nawataka.

“Tumepitisha haya majina lakini sikubaliani nayo hata moja.. Tumeacha majina ya vijana walionyesha ujuzi mzuri wa marketing kama ulivyotaka lakini unawaacha umeenda kuchagua waliofanya hovyo kabisa.. Hii ingekuwa ofisi ya kweli ningehisi labda wamekuhonga” Kaburu akaongea huku akionyesha usoni jinsi alivyokereka.

“Kichwa! Hata mimi sikubaliana na haya majina.. Labda utuambie sababu ambayo bado hunatuambia” Cheupe naye akaunga mkono hoja ya Kaburu.

“Ni ‘reverse psychology’”

“Nini?” Wote wakauliza kwa pamoja.

“Reverse psychology.. Unatoa misdirection ili kupata unachokitaka kwa kusoma akili ya upande wa pili” nikawaeleza.

“Unaweza ukafafanua kwa lugha ya kueleweka??” Kaburu akaongea akiwa bado amekereka.

“Ok! Juzi tumepost tangazo kwenye mitandao na tumepata response ya vijana.. Baada ya wao kurespond tu kwa tangazo letu walikuwa wanafaa kabisa kwa ajili ya mpango wetu niliowaeleza.. Kwasababu mpango wetu ili ufanikiwe tunahitaji kuwamanipulate hawa vijana ili wafikiri hiki tunachokifanya ni kitu halisi kabisa.. Sasa kitendo cha wao kutupigia simu bila kufanya uchunguzi kuhusu uhalisia wa kampuni yetu inaonyesha ni kiasi gani wako desperate.. Sasa mtu desperate hivyo ni very easy kummanipulate but we have to be sure.. Watu ambao wana good sales skills ni wajanja wajanja sana and it’s just a matter of time wangetushtukia huu uongo wetu.. That’s why wote ambao wameandika kwa weledi insha zao ‘nimewapiga’ chini.. We don’t need them, it’s just a matter of time wangetushtukia.. Hawa niliowachagua sidhani hata kama wamewahi kupewa hata umonita kipindi wanasoma.. Hawa ndio tunawahitaji.. Hawa tunaweza kuwaambia chochote na wakatekeleza bila shida yoyote.. Ndiyo hiyo nimewaambia kuwa ni reverse psychology..”

Nikawafafanulia kwa kina kabisa.

“Wow! Good thinking” Cheupe akasifia huku anatabasamu.

“Well Mr. Genius unaonaje next time ukatuambia unachokipanga kichwani toka mwanzo” Kaburu akaongea kwa kukereka lakini kwa kiasi fulani akiona aibu kwa jinsi ambavyo alishindwa kung’amua lengo langu toka mwanzoni.

“So now, what’s next?” Cheupe akauliza.

“Wapigie simu wote tulio wachagua waambie wawe hapa kesho saa tano asubuhi.


Nahisi ni kutokana na kuwarudisha nyumbani wale vijana nane jana ndiko kulikofanya hawa vijana 12 tuliowachagua jana kuwahi siku hii ya leo.

Mpaka kufikia saa nne na nusu vijana wote walikuwa wamefika tayari.

“Wote wamefika wanakusubiri” Cheupe akaongea akiingia kwenye chumba cha ofisi.

“OK! Nipe dakika mbili tu!” Nikamjibu nikiwa naandika andika kwenye karatasi juu ya meza.

“Unaandika nini?” Akaniuliza.

“Another speech!” Nikamjibu huku natabasamu nikikaribia kucheka.

“Uwiiii another speech?? Unataka kuwa mwanasiasa nini baba?” Cheupe akaniuliza huku anacheka.

“Maneno ndio yanaendesha Dunia mama! Martin Luther King hajapata heshima kubwa alliyonayo kwasababu ya kupigana vitana.. Just speeches.. Words” nikamjibu huku natabasamu.

Mara Kaburu nae akafungua mlango na kuingia.

“Vijana wanakusubiri ujue!” Kaburu akaongea akiwa ameshaingia ndani ofisini.

“Ok! Ngoja nikaongea nao sasa.. Leo nataka mniache niongee nao peke yangu.. Subirini hapa hapa ofisini” nikaongea nikiweka sawa koti la suti na kuanza kuondoka.

“Kilala heri kichwa!” Kaburu akaniaga.

Hii ilikuwa mara ya kwanza kumsikia anatamka kichwa. Nikageuka nimuone kama alikuwa ananiinjoi au vipi.

“Umemaanisha au ndio majungu yako tu ya kila siku” nikamuuliza kiutani.

“I mean it” Kaburu akanijibu akiwa serious kumaanisha alichokisema.

Nikamuitikia kwa kichwa kisha nikatoka ofisini.

Katika chumba cha mikutano leo tulikuwa tumekiweka tofauti na jana.

Tuliweka meza kati kati na viti karibia kumi na nne kuzunguka meza. Ilitoa mandhari fulani kama kuna wanaabodi fulani wazito wana kikao.

Vijana wote walikuwa wamefika na wameketi kwenye sehemu zao. Ni mimi tu ndiye nilikuwa nasubiriwa.

Nilipofika nikakaa kwenye kiti mwishoni kabisa mwa meza.

Nikakaa kwenye kiti na kisha nikaa kimya tu bila kusema chochote nikiwatazama.

Nikawatazama kwa takribani dakika nzima pasipo kuongea chochote.

Nilikuwa nataka waanze kupata ‘pressure’ ndani mwao.

Nilipoona akili zao zimetulia vya kutosha na kuna ‘kipresha’ Fulani ndani ya chumba, nikaanza kuongea. Sikusalimia wala nini nikaanza kuongea moja kwa moja nikiwa serious haswaa.

“Ni wangapi kati yenu wanaojua vitu vitano ambavyo katika hotuba yake ya mwisho kama Rais, Mhe. Benjamin Mkapa alivitabiri kuwa vitatokea baada ya miaka kumi ya yeye kuondoka madarakani.?” Nikawauliza kisha nikawa nawaangalia mmoja mmoja.

SIKU MBILI BAADAE

Huwa nachukia uongo, nachukia sana lakini kuna muda uongo huwa unasaidia.

Maana kiwango cha uongo nilichotumia kuwashawishi hawa vijana kilikuwa kinatisha.

Siku mbili zilizopita niliwapa hotuba mujarabu kabisa kuhusu taifa lao. Nikaamsha hari zao kuhusu uzalendo kwa nchi yao kisha nikachomekea suala la TISS.

Nikawaeleza kuhusu Idara ya Usalama wa Taifa ilivyl concerned kuhusu kikundi cha watu kinachoratibu kuua habari muhimu kwenye media ambazo wanahisi zitawaumia na badala yake wanahakikisha habari zinazotawala kwenye media ni habari wanazozitaka wao ili kuwaweka watu gizani wasijue kinachoendelea.

Nikawapa mifano kuhusu “Operation Mockingbird” ya CIA huku Marekani jinsi walivyokuwa wanaratibu habari zinazotoka kwenye vyombo vya habari, nikawapa mfano mwingine wa “C-Z13” Opareation nyingine ya siri nchini Singapore jinsi ilivyosaidia kuifanya wanachi wa nchi hiyo kuwa watiifu kwa kiongozi Lee Kwan Yu na kupelekea nchi kupata maendeleo ya haraka.

Nikawapa mifano mingi ya kutosha.

Baada ya hapo nikawapa mifano kadhaa ya kutosha juu ya Oparesheni zilizowahi kufanyika miaka mingi iliyopita na Idara ya Usalama wa Taifa ili kuwafanya wananchi wawe na imani na serikali yao hasa kipindi cha utawala wa Nyerere na jinsi ilivylsaidia nchi kutulia na kupata maendeleo ya haraka.

Baada ya hapo nikawaeleza kuwa Idara ya Usalama wa Taifa inataka kurudisha tena weledi huo katika utendaji wake, na imeweka dhamira ya kuunda kitengo maalumu cha maafisa ambao kazi yao itakuwa ni kuratibu habari zitakazo kuwa ‘zinatrend’ kwenye mitandao ya kijamij na pia kuratibu habari zipi ambazo zitakuwa zinapeqa kipaumbele kwenye vyombo vya habari.

Nakumbuka kipindi nawaeleza hili kuna kijana mmoja akaniuliza, “mbona nasikia kuwa Usalama wa Taifa hata sasa hivi huwa wanapandikiza habari kwenye social media na vyombo vya habari?”

Swali lake lilikuwa zuri sana na nilipaswa nitulize akili ili kulijibu kwa ufasaha.

Nikamueleza kwamba kwa sasa shughuli hiyo inafanyika kwa dharura. Yaani inafanywa pale tu ambapo labda kuna habari ambayo Idara ya Usalama hawataki ipewe kipaumbele kwenye vyombo vya habari, hivyo inapandikizwa habari nyingine ili kuua makali ya habari ya kwanza.. na kahdhalika.

Nikawasisitiza kuwa sasa Idara ya Usalama haitaki kufanya hivyo kwa dharura, inataka kiwe ni kitengo cha kudumu ambacho kitafanya kazi hiyo kila siku, masaa 24, siku saba za wiki, mwaka mzima.

Kisha nikawaeleza hiyo ndio sababu ya kuanzisha kwa ofisi hii ya “kimkakati” chini ya jina la mwamvuli “Unimax Marketing”.

Lengo ni kutafuta vijana ambao watapatiwa mafunzo na stadi kutoka TISS ili kuajiriwa kwenye kitengo hicho kipya.

Nikawaeleza kuwa wao 12 wamepita kwenye mchujo wa kwanza. Bado michujo miwili.

Mchujo wa pili itakuwa kweye ” Trials” ambazo tutazifanya kwa wiki mbili kuanzia kesho kutwa yake (leo hii) na mchujo wa tatu watakutana nao wakienda depo ya TISS kwa wale wataopita kwenye “Trials”.

Jana nilikuwa nimepokea fedha nyingine milioni tano kutoka kwa Issack Morogoro.

Niliwasiliana naye na kumueleza kuwa mimi na Cheupe sote bado tuna salaio kwenye akaunti zetu lakini hatutaki kufanya ‘withdrawal’ ili kuepuka kugundulika mahali tulipo.

Kwahiyo nikamueleza kuwa atoe milioni tano kutoka kwenye akaunti ya SOTE HUB na anitumie kwenye bus kama parcel ya kawaida.

Naye akafanya hivyo, akaweka milioni tano kwenye boksi na kuchanganya na vitabu, boksi juu liliandikwa “PHYSICS BOOS — FROM MWELE BOOKSHOP— TO ST. ANTHONY SEC SCHOOL.”

Akatuma kwa bus la aboud na nikapokea Percel ubungo na kurudi nayo Lodge tuliyokuwa tunakaa Sinza.

Kwahiyo tulikuwa na fedha nyingine ya kutosha kuendelea na mikakati yetu.

Ndipo hapa siku ya leo wale vijana 12 walikuwa wamekuja tena kwa ajili ya kuwapa maelezo kuhusu “trial” ya kwanza ya mchujo huu wa pili.

Baada ya kusalimiana nao na kuongea mawili matatu kwenye kile chumba cha mikutano, Cheupe akaja na bahasha yenye fedha ndani na kumkabidhi kila kila mmoja.

“Hiyo ni fedha yenu ya kujikimu! Tukumbuke kuwa bado hamjawa waajiriwa wa Idara ila hiyo tunachowapa ni fedha kidogo muweze kujikimu.. yaani uweze kula, uvae na usikose nauli.! Kwahiyo kwa kipindi hiki cha trials kila wiki tutawapatia laki mbili.!! Naamini inatosha walau kidogo..”

“Inatosha sana.!” Vijana kadhaa wakaitikia huku wanatabasamu.

Nikaendelea kuwapa maelezo.

“Katika hii wiki ya trials tunaangalia nini?? Japokuwa mmepita kwenye mchujo wa kwanza katika huu mchujo wa pili tunahitaji kujua if you have what it takes kuwa Afisa Usalama.. Na mnakumbuka niliwaambia ni vitu vingapi muhimu ambavo afisa wa TISS anatakiwa kuwa navyo??”

Nikauliza na kuwaangalia.

“VITATU.!!” wakajibu kwa pamoja.

“Cha kwanza.??” Nikawauliza uku nimenyoosha kidole kimoja.

“UZALENDO.!!” wakajibu kwa pamoja.

“Cha pili??” Nikawauliza tena huku nimenyoosha vidole viwili.

“SHAUKU YA KUJUA, KURATIBU NA KUFANYIA KAZI.!!” Wakajibu wote kwa pamoja.

“Cha Tatu??”

“AKILI YA ZIADA.!”

Nikatabasamau.

“Very good.! Hivyo ndivyo vitu vitatu ambavyo tutaviangalia kwenye hizi trials.. Achana na stori za vijiweni kuhusu ‘sixth sense’!! Tutaangalia kama mnavyo hivyo vitu vitatu kabla hamjaenda depo.”

Nikanyamaza kidogo, kisha nikaendelea.

“Katika hii assignment ya kwanza, nitawagawa kwenye makundi matatu na kabla ya kuwagawa nataka tuachane na majina yenu rasmi na kila mmoja wenu nitampa jina la siri ambalo tutakuwa tunalitumia kuanzia sasa.”

“Kwa wale ambao mtafanikiwa kwenda depo mtafundishwa kuhusu ‘covert communications’ na mtaeleqa zaidi hiki nilichokifanya leo.. Sasa basi, kwa kuwa mpo kumi na mbili kila mmoja wenu nitampa herufi ya alphabet lakini itakuwa ni herufi ya kijeshi.!!”

Nikanyamaza kidogo, nikawatazama kama tunaenda sambamba kisha nikaendelea.

“Mpo kumi na mbili kwahiyo tutatumia herufi kumi na mbili za mwanzo za alfabeti, yaani A, B, C, D, E, F, G, H, I, J, K na L.!! Sasa kwenye Idara herufi hizo tunazitamka kama Alpha, Bravo, Charlie, Delta, Echo, Fox, Golf, Hotel, India, Juliet, Kilo na Lima.!!”

Baada ya hapo nikampa kila kijana herufi yake.

Baada ya hapo nikawagawanya katika timu Tatu.

Alpha, Bravo, Charlie na Delta wakawa ni Team A.

Echo, Fox, Golf na Hotel wakawa ni Team C.

India, Juliet, Kilo na Lima wakawa ni Team S.

Kisha nikaanza kuwapa majukumu ya kila timu.

“Ndani ya dakika chache nikawaeleza kuhusu Target yenu kwenye hii trial.. Nyinyi Team C (team Covert) kazi yenu itakuwa ni kumonitor movement za target nitakayo wapa.. Nitahitaji kujua kila mahali alipo na anachokifanya.. Nyinyi team A (team assault) kazi yenu itakuwa ni kufanya uvamizi pale nikawaambia kufanya hivyo, kumbukeni hii ni trial kwahiyo uvamizi wenu hautakiwj kujeruhi mtu.. Nyinyi team S (team standby) Nyinyi hamtafanya chochote mtasubiri maelekezo yangu.”

Nikanyamaza kuwatazama! Walikuwa wananisikiliza kwa makini kweli kweli.

Kisha nikampa kila mmoja kisimu cha “Nokia ya Tochi” niliyokiwa nimevinunua Jana nikitokea Ubungo kupokea parcel kutoka kwa Issack.

“Tukiwa tunawasiliana, kabla hujasema chochote kwanza utanitambulisha tema yako na wewe mwenyewe kisha utasema unachotaka.. Kwa mfano, Team A, Bravo kisha unaongea.. Na hautaongea kitu moja kwa moja utanieleza kwa mafumbo”.

Nikatumia karibia lisaa lizima kuwafundisha kuhusu ‘basics’ za namna ya kuongea na kuandika ” coded message”.

Baada ya hapo Kaburu akaja na files kadhaa na kumpa kila kijana file moja.

“Fungueni hizo files.!”

Wote wakafungua files. Ndani ya kila file kulikuwa na Picha ya mtu na maelezo mafupi.

“Mnamfahamu huyo mtu?” Nikawauliza.

“Ndio.!!” Wakaitikia wote.

“Huyo ni Mkurugenzk Mtendaji wa Benki ya CRBB, Bw. Vincent Mallya.! Na huyo ndiyo target yetu.!” Nikawaeleza huku nikawaangalia usoni jinsi walivylshikwa na mshangao.

“Mallya? Amefanya nini?” Kijana mmoja akauliza.

“Well, siwezi kuwaeleza kila kitu ila kwa ufupi ni kwamba ndani ya siku yoyote wiki hii kuna files atazihamisha kutoka ofisini kwake kwenda sehemu nyingine.. Tunahitaji hizo files!! Sasa hivi ni saa kumi jioni.. Nahitaji muende mkapumzike.. Kesho saa kumi na mbili asubuhi nahitaji muwepo hapa ili niwape specifics za assignment yenu.. Good evening everyone!”

“GOOD EVENING.!” wakaitikia wote.

Nikatoka nje ya chumba chmikutano nikiongozana na Kaburu. Tukamuacha Cheupe akiwapa maelezo kadhaa machache kuhusu maandalizi ya siku ya kesho.

“Duh! Kama James Bond.. Hongera kichwa hahaha.!” Kaburu akaninong’oneza.

“Sasa nahitaji kwenda kuonana na watu wa Usalama Wa Taifa.!” Nikamueleza Kaburu tukiwa kule Chumba cha Ofisi.

“OK! Ndio ulisema unafanyaje ili kuwaona?” Akauliza.

“Kuna maelezo walinipa niende Mlimani City duka fulani hivi alafu nifanye vitu kadhaa kisha watanipa maelekezo nikaonane nao wapi” nikamueleza huku nikivua koti la suti na kubaki na shati nyeupe ya ndani.

“Aisee! I hope huu mpango utafanikiwa la sivyo watatunyonga hawa jamaa wakitushtukia mchezo tunaowafanyia.!” Kaburu akaongea huku akitoa tahadhari kama kawaida yake

“Hatuna jinsi.. Inabidi tufanye hivi.!” Nikaongea huku naanza kuondoka.

“Pia jitahidi uwasiliane na Chifu nataka twende tukaongee naye nikitoka huku kwa watu wa TISS.!”

“OK! Nawasiliana naye sasa” Kaburu wakajibu huku anaanza kubofya simu.

Nikashuka chini ya kile kighorofa chenye ofisi zetu na kuelekea mpaka sehemu zinapopaki bajaj.

Nikapanda na moja kwa moja tukaelekea Mlimani City.

Kwa kiasi fulani nilikuwa sikumbuki kwa usahihi sana yale maelekezo waliyonipa watu wa Usalama siku ile ‘walipo niteka’ kuhusu namba gani nifanye nikitaka kuonana nao tena.

Nilikuwa nakumbuka tu kwamba niende Mlimani City duka la vitabu la Stolastica kisha ninunue kitabu kwa bei ya chini na kukirejesha baadae.

Kwahiyo nilipofika Mlimani City nikaelekea moja kwa moja mpaka duka la Mlimani City kisha duka la Stolastica Bookshop.

Nikaenda kwenye shelves nankuchukua kitabu cha muandishi Robert Haris, Archangel.!

Kitabu kilikuwa kinauzwa elfu arobaini na tano, mimi ninakichukua mpaka kaunta na kutoa elfu kumi.

“Hela haitoshi tafadhali” muhudumu akanijibu huku anataka kukichukua kitabu kutoka mkononi mwangu.

“Hii ndio bei yake, ninayo hii hii” nikaongea huku nikiwa na wasi wasi kama nimeongea kitu sahihi nilichoelekezwa.

Muhudumu alikuwa ni mama fulani hivi wa makamo. Akanikazia macho ma kuniangalia kama dakika nzima. Kisha akaniachia kitabu.

Nikaondoka zangu.

Baada ya dakika kumi nikarudi tena kama ambavyo nilitakiwa kufanya kulingana na maelezo waliyonipa.

“Samahani mama hiki kitabu kuna kurasa hazipo” nikamueleza yule mama baada ya kurudi mle dukani.

Hakusema chochote, akainama chini kaunta na kuchukua kitabu kingine kama kile na kunipa.

“Samahani kwa usumbufu” akaongea huku anatabasamu.

“Usijali mama.. Shukrani!”

Nikachukua kitabu ma kutoka nje.

Baada ya kutoka tu kwenye duka nikafungua kitabu na kukuta kikaratasi kimeandika.

DAKIKA 20 KINGSTONE HOTEL, MOROCCO, SWIMMING POOL

Sikutaka kupoteza muda.! Nikachukua Taxi kuelekea Kingstone Hotel iliyopo Morocco pembezo tu mwa barabara.

Baada ya kuingia ndani ya Hotel moja kwa moja nikaenda mpaka sehemu ya swimming pool.

Nilishangaa mno. Nilkuta Baba Bite yuko na familia yake wanaogelea.

“Raaaayyyyyy.!!” Bite akaniita huku ananikimbilia baada ya kuniona.

“Wooooww! Hujambo wewe.!” Nikamkumbatia Bite huku namuinua.

“Sijambk shikamoo” kabite kakaniamkia.

“Za siku shemeji.!” Mama Bite akanisamia kwa mbali huku ananipungia mkono.

“Nzuri Shem, naona mkanikimbia bila kuniaga.!” Nikamtania kuhusu namna walivyohama ghafla kule Mazimbu.

“Nisamehe bure shemeji, ulikuwa dharura.. Si unajua tena pilika za maisha..”

“Usijali Shem.!” Nikaongea huku namshusha chini Bite arudi kwa mama yake Baada ya baba bite kufika pale tuliposimama.

Njkajiuliza sana kichwani kama Mama Bite anafahamu kuhusu shughuli za mumewe au la.

“Long time no see!” Baba bite akafungua maongezi huku tunatembea kuondoka karibu na swimming pool.

“Here I am.. Ulifanikiwa kupata documents za Kaburu.!” Nikaenda moja kwa moja kwenye mada pasipo kuzunguka mbuyu.

“Yes! Tumezipata.. Vipi umepata file za The Board?” Akaniuliza.

“Yes! Nimezipata, ila kabla sijawakabidhi nataka tukubaliane mambo kadhaa..!” Nikamjibu.

December, 1974

Ulikuwa umepita takribani mwezi mmoja na nusu tangu Waziri wa fedha Abdul Aziz na Chifu Sekioni wamtembelee Charles Nyumbani kwake usiku na kesho yake kumtuma kijana aliyempeleka maeneo ya Upanga na hatimaye kumpeleka Oysterbay ambako aliunganishwa rasmi na mtandao wa Siri wa The Board.

Mwishoni mwa mwezi Oktoba, shehena ya kwanza ya sarafu iliwasili kutoka nchini Uingereza kwa watengenezaji kampuni ya Messrs Thomas de la Rue.

Kama ambavyo walikubaliana na Waziri Abdul Aziz Charles na Waziri walishauri shehena hiyo ya sarafu ihifadhiwe kwenye makao makuu ya jeshi magogoni na kiasi kidogo ihifadhiwe maeneo ya upanga kwenye Jengo la kukodi ambalo litaboreshwa kwa kuwekewa milango ya “vault”.

Kwa kuwa wao ndio walikuwa washauri wakuu kuhusu suala hili la uanzishwaji wa benki kuu hivyo Rais hakuwa na kipingamizi chochote.

Shehena ya sarafu inapelekwa Headquarters za Jeshi magogoni na kiwango kidogo kikawekwa kwenye Jengo lililoboreshwa upanga, Jengo ambalo lilikuwa mali ya Charles.

Japokuwa mwanzoni Chifu Sekioni na Waziri Abdul Aziz walimuahidi Charles kuwa watampeleka kuonana na ‘Chairman’ wiki tatu baada ya kukubali kiasi kidogo cha sarafu zihifadhiwe upanga, lakini baadae ratiba ikahairishwa ma kusogezwa mbele mpaka leo hii mwezi Desemba.

Hii ilikuwa imepita kama wiki mbili tangu Rais amteue Charles kuwa Gavana wa muda akisubiria Rais kufanya uteuze rasmi wa Gavana.

Leo hii alikuwa safarini pamoja na Chifu Sekioni na Waziri Abdul ili kuonana na Chairman.

Walifika Dodoma majira ya saa kumi jioni wakiwa na msafara wa magari mawili mpaka maeneo ya Mvumi Makulu.

” Hiki kijiji si ndio ambapo Waziri Mkuu amenunua mashamba na kujenga makazi yake ya likizo?” Charles akamuuliza Chifu Sekioni.

Chifu hakujibu chochote.

Wakaelekea moja kwa moja mpaka kwenye nyumba tatu za kifahari za kufanana zilizopo kijijini hapo ambayo ndiyo yalikuwa makazi ya Waziri Mkuu, kipindi cha likizo kijijini kwao.

Wakakaribishwa kwenye nyumba mojawapo kati ya zile tatu ambayo ilikuwa na sebule kubwa kwa ajili ya kukaribisha wageni.

Baada ya kufika sebuleni, Chifu Sekioni na Waziri Abdul wakaondoka na kumuacha Charles pale sebuleni na kwenda kwenye nyumba mojawapo kati ya zile tatu.

Kama dakika kumi na tano baadae Waziri Abdul Aziz akarejea peke yake.

“Charles!” Waziri akamuita Charles

“Naam ndugu Waziri”

“Its time.. Umetamani miezi mingi sana kuonana ma Chairman.. Leo tunamaliza hilo suala.!” Waziri akaongea huku anatabasamu.

“Sielewi ndugu Waziri! Hapa si ni kijijini kwa Waziri Mkuu?” Charles akaongea huku anainuka.

“Usijali Charles.. Tukiondoka hapa leo hutabaki na swali hata moja.”

Waziri anatabasamu. “Twende huku Charles.!”

Wakatoka kutoka pale sebuleni mpaka kwenye nyumba nyingine ile kubwa ya mkono wa kushoto.

.

Kwenye ile nyumba nyingine ilikuwa na walinzi kadhaa wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kwa hesabu ya haraka haraka nje kulikuwa na walinzi si chini ya nane hivi.

“Are you ready Charles??” Waziri akamuuliza kajuna baadae ya kufika kwenye mlango wa nyumba kubwa.

“Niko tayari ndugu waziri” Charles akajibu kwa shauki kubwa.

Waziri akafungua mlango, na wakaingia ndani ya nyumba ambapo walitokea mbele ya sebule kubwa sana yenye samani maridhawa ya miti ya mpingo kuanzia meza mpaka viti.

Lakini kilichomshitua zaidi Charles haikuwa sebule ya thamani au ufahari wa mule ndani.

Kilichomshtua Charles ilikuwa ni walikuwa watu walioketi kwenye ile sebule.

Kulikuwa na watu wawili wameketi kwenye sebule.

Pale sebuleni aliketi Chifu Sekioni na kulia kwake aliketi Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Chande Ramadhani Chande.

“Karibu sana Charles.!” Chifu Sekioni akamkaribisha Charles baada ya kuingia na Waziri Abdul Aziz.

“Asante.!” Charles akajibu kwa hofu karibu na kuanza kutetemeka.

Charles na Waziri Abdul wakaketi kwenye viti vinavyotazamana na viti walivyoketi Chifu Sekioni na Waziri Mkuu Chande.

“Chairman.. Naomba kukutambulisha kwa ndugu Charles Bernard Kajuna.. Mpendekezwa wa nafasi ya Book Keeper wa The Board.!” Chifu Sekioni akatambulisha huku anaongea akimuangalia Waziri Mkuu Chande na kisha akageuka kumuangalia Charles.

“Charles naomba nikutambulishe kwa Chairman wa The Board.. Ndugu, Chande Ramadhani Chande.!”

Charles hakujua ajibu nini akabaki bado ameduwaa kwa mshituko.

“Hujambo Kajuna?” Waziri Mkuu Chande akamsalimia Charles.

“Sijambo muheshimiwa.…” Charles wakaitikia salamu huku asijue amuite vipi, waziri Mkuu au Chairman.


January, 2017

“Kwahiyo unaondoka saa ngapi Mkuu” nikamuuliza Kaburu.

“Nataka kukusaidia kuwapanga hao vijana kisha wakielekea mjini nitaondoka” Kaburu akanijibu.

“OK! Na nikihitaji kuwasiliana nawe inakuwaje?”

“Si unakumbula ile email niliyokupa gerezani?” Kaburu akaniuliza.

“Yeah naikumbuka, [email protected]! Ila ulisema nisiitumie tena?” Nikamuuliza

“Yeah! Unachofanya unabadilisha pale kwenye ’13’ inakuwa ’14’, kisha safari nyingine ukitaka tuwasiliane unabadili tena inakuwa ’15’.. Hivyo hivyo tena na tena”

“Ooh OK! Nimekusoma Mkuu.. So wewe na bibie mtakuwa mnaishi wapi?” Nikamuiliza kwa kumchokoza.

“Hahaha! Hiyo info siwezi kukupa Kichwa..”

Wote tukacheka.

Hii ilikuwa inapata saa kumi na mbili kasoro asubuhi. Tulikuwa ofisini kwetu na nilikuwa nimemaliza kumkabidhi Kaburu documents zake ambazo nilipewa Jana kwenye kikao changu na Baba bite, documents ambazo ziliibiwa na Obama, Askari magereza wa Gereza kuu Morogoro.

Kilichokuwa kinamfanya Kaburu aendelee kuwa na sisi ilikuwa ni kusubiri apate hizi documents.. Kwahiyo baada ya kuzipata hakukuwa na sababu ya yeye kuendelea kubaki pamoja na sisi.

Vijana walikuwa wameanza kuwasili kwa ajili ya appointment yetu ili tuanze “trials”!!

Tukatoka ofisini na kwenda kuungana na Cheupe pamoja na vijana wetu kwenye chumba cha mikutano.

Baada ya salamu na kupeana muhtasari wa masuala machache nikaendaoja kwa moja kwenye ‘point’.

“Nadhani Jana Dada Janeth aliwaeleza Team C muhakikishe kuwa mnapata mtu nje ya ofisi ya Bw. Mallya na ndani ya ofisi.. Sijui mmefikia wapi kwenye hilo” nikawauliza huku huyo “Dada Janeth” nikimaanisha Cheupe. Alijitambulisha kwa jina hilo “Dada Janeth”.

Mimi nilijitambulisha kama ” Kevin” na Kaburu aliitwa “Othman”.

” tumekubaliana kwamba Rashidi hapa atakuwa….” Kijana mmoja akaanzankujibu ila nikamkatisha.

“Nimesema tusitumie majina halisi.. Nataka muanze kujizoesha hilo.. Enhe emdele” nikamrekebisha.

Yule kijana akatabasamu kisha akaendelea.

“aaaah nilikuwa nasema kwamba tumekubaliana kwamba… aaaah Echo hapa atakodi baskeli ya kuuza Ice cream za Azam kwa wiki moja na atakuwa anafanya biashara hiyo mbele ya gjorofa la Golden Jubilee Tower ambalo kuna makao makuu ya CRBB na ofisi za target yetu Vincent Mallya.. Pia tumekubaliana kuwa siku ya leo Dada yetu hapa.. Aaaaahh Fox.. Yes Fox atahakikisha kuwa anatumia ushawishi wake wote anapata kazi hata ya kufagia au kudeki ndani ya Golden Jubilee Tower na hasa kwenye ghorofa zinazotumiwa na CRBB.!”

Yule kijana mwenye code name ya ‘Hotel’ akafafanua.

“That’s genius I like it.! Vizuri sana C Team.. I like it.. vipi wengine kuna mwenye nyongeza yoyote?”

“Ndio Mkuu..” Akaongea kijana mwingine wa A Team.

“OK! Let’s hear it.!”

“Pia na sisi tumekubaliana kuwa tutakodi boda boda moja yenye kibali cha kuingia katikati ya jiji ili itusaidie kufanya ‘assault’ pale tutakapo hitajika kufanya hivyo..” Akaeleza kijana mwenye code name ya ‘Bravo’.

“Good thinking.. I love this! You guys mnacatch up haraka sana.. Safi sana this is good.. Sasa hivyo vitu mnavyotaka kukodi msitumie hela yenu mtamuona dada Juliet awapatie hiyo fedha ya kukodi.”

Nikawaeleza na kisha nikawapa maelekezo ya mwisho mwisho na kuwatawanya waende kwenye ‘assignment’. Kila team na location yao. Kijana mmoja nikampanga awe ana-monitor nje ya benki ya CRBB tawi la Lumumba.

“So how is this going going to work” Cheupe akauliza baada ya Vijana wote kuondoka tulikowapangia.

“Well its simple.. Jana kwenye kikao changu na Baba Bite alipokuwa ananikabidhi documents za Kaburu nikamueleza kuwa files za The Board zipo kwenye strong room ya CRBB tawi la Lumumba.. Sasa naamini mda wowote kuanzia sasa Maafisa Usalama watavamia pale Lumumba kufanya upekuzi kwenye strong room kutafuta hizo files.. Kwahiyo hisia zangu ni kwamba The Board wakipata taarifa juu ya upekuzi huo wanaweza kuchukua tahadhari ya kuziamisha files kutoka Golden Jubilee Tower.. Na wakijiroga tu waziamishe files kutoka strong room ndio hapo hapo sisi tunafanya yetu..!!”

Nikawaeleza na kamalizia kwa tabasamu.

“Wooooww!! That’s genius.. All the best guys! Mimi inabidi niende sasa” kaburu akanipongeza na kuanza kuaga.

“So uhitaji tukusindikize?” Nikamuuliza

“No, usijali! I can take it from here.” Akajibu huku anaweka documents zake vizuri kwenye mkoba.

Baada ya hapo tukamsindikiza mpaka nje ya ofisi na kuagana! Lakini kabla ya kuondoka, Kaburu akabadilika kutoka sura ya utani na ucheshi ma kuwa serious.

“Kuna jambo fulani naomba nikushauri Ray.!” Akaongea Kaburu akiwa serious.

“What is it?”

“Kama mkifanikiwa kuzipata files za The Board, sikushauri uzisome kilichomo ndani.. Wapelekee tu Usalama na wamuachie Mzee wenu maisha yaendelee”

“Kwanini nisizisome?”

“Kuna baadhi ya siri ni vyema kutozifahamu.. Ukizijua unaweza ukajikuta unajutia maisha yako yote kwa nini umezifahamu.. Muda mwingine ignorance is a blessing.. Hakuna ulazima wa kujua kil a kitu! So nakusisitiza sana.. Usisome hizo files.!”

Kaburu akaongea akiwa anamaanisha haswa. Sikujibu chochote nikabaki nimeduwaa na kutafakari.

“Kilala kheri Ray, Hasnat.. Tuwasiliane kwa lolote kama kuna ulazima.. Nimefurahi sana kuwafahamu.”

Tukapena hug za ‘kishkaji’, kisha Kaburu akaondoka.

Lakini kichwani mwangu bado nilikuwa naumiza kichwa kuhusu ushauri wake! “Usisome hizo files.. Ignorance is a blessing..”

Nikahisi kuna jambo kubwa Kaburu alikuwa analijua kuhusu mimi au hizo files na asingependa nifahamu.

Hii ilikuwa yapata siku ya pili sasa tangu tuwaweke vijana wetu kwenye target nje ya ghorofa la Golden Jubilee Tower posta pamoja na mtaa wa Lumumba nje ya Tawi la Benki ya CRBB.

Kwa siku zote mbili hizi vijana walikuwa wanafuatilia mwenendo wa Vincent Mallya na kutupa taarifa Mimi na Cheupe ambao tulikuwa ofisini Makumbusho.

Walimfuatilia ni muda gani anaingia ofisini, movement zake mule ofisini hasa kama anaingia strong room.

Team C walikuwa wamefanikiwa member wao mmoja mwanadada mwenye code name ‘Fox’ kupata kibarua cha muda kudeki sakafu ndani ya Jengo, kwahiyo hii ilisaidia mno kuwa na ‘macho’ ndani ya ofisi za CRBB.

Siku ya jana ilikuwa ni ya ‘kuboa’ sana maana hakukuwa na activity yoyote yenye kuashiria kuwa unaweza kutusaidia kupata files.

“Au labda watu wa Usalama wamepanga wamkamate Mallya kisha wambane atoe hizo files?” Cheupe aliongea kwa sauti fulani hivi ya kukata tamaa.

“Nope! They won’t take that risk.. Nina hakika lazima watafanya ambush ili wasitoe mwanya wa The Board kuhamisha files..” Nikamjibu kwa kujiamini ili nimpe matumaini.

Mara simu ikaanza kuita, ni moja kati ya wale vijana ambaye nilimpanga akae nje ya CRBB Lumumba.

Nikapokea.

“Team S, Kilo..” Kijana akajitambulisha.

“Team S, Kilo… go on” nikamuitikia.

“Kuna magari matatu muda huu yamewasili.. Nadhani ni ndugu zetu.!” Akaongea kwa kifupi.

Siku ya Jana kabla ya kumpangia kukaa nje ya CRBB Lumumba, nilikuwa nimemueleza namba gani ya kuwatambua maafisa wa Usalama Wa Taifa pamoja na usafiri wao.

Kutokana na maswahibu haya niliyokuwa nayo ilinifanya kukutana na watu wa Usalama mara nyingi sana, kwahiyo nilikuwa nimewasoma vitu vingi kuwahusu.

Pia niliwapa ‘code word’ ya “Ndugu Zetu” ili kumaanisha Maafisa wa Usalama wa Taifa.

“That’s good.! Usiwapoteze.. Pia hakikisha hawatambui kuwa unawafuatilia.!”

“Sawa mkuu!” Akanijibu na kukata simu.

“Its on.. I told you.!” Nikamwambia Cheupe huku nainuka kuelekea kwenye kabati kuchukua file niliwa nimefurahi.

“So hii ina maana gani?” Akaniuliza kwa shauku.

“That means wameenda kufanya upekuzi kwenye strong room Lumumba kama nilivyo wamislead.. Mda wowote kuanzia sasa Vincent Mallya akipata taarifa juu ya upekuzi Lumumba am sure ataomba ruhusa The Board achukue tahafhari ya kuzihamisha files kutoka Golden Jubilee Tower na kwenda kuhifadhi sehemu nyingine.. Na ndipo hapo hapo na sisi tunafanya yetu..”

Nikamjibu kisha nikachukua simu na kuwapigia Team C, vijana wanaofuatilia nyendo za Vincent Mallya.

“Team C, mnanisikia?” Nikauliza baada ya simu kupokelewa.

“Nakusikia mkuu.” Akajibu tuliyempa herufi ‘Echo’ kijana ambaye alikuwa anauza ice cream nje ya ghorofa la Golden Jubilee Tower.

“Kuweni makini.. Mda wowote kuanzia sasa target anaweza kumove na mzigo tunaohitaji.. Nahitaji taarifa ya moja kwa moja kuhusu movement zake kuanzia sasa..” Nikamsisitiza nikiongea na simu sikioni huku natembea tembea pale ofisini.

“Sawa mkuu” Akanijibu, kisha akakata simu.

Damu ilikuwa inachemka na presha iko juu kadiri tulivyokuwa tunakaribia kufanikisha hili jambo. Nilijisikia kushindwa kabisa kushbiri.

Nikabaki natembea tembea tu mle ofisini nikitamani simu iite muda wowote nipewe “updates” kuhusu movement za Mallya.

“Calm down honey.!” Cheupe akaniambia baada ya kuniangalia muda mrefu jinsi ninavyotembea tembea mle ndani ofisini.

“I’m fine honey.. I’m totally ok..” Nikaongea huku najitahidi kujionyesha sijapaniki.

“Inabidi tufanikiwe kwenye hili.. Hakuna namba nyingine.. This has to work..” Nikaongea huku nikianza tena kutembea tembea.

Cheupe akaniangalia tu kwa huruma jinsi nilivyopaniki. Nahisi alitamani anikumbatie na kuniambia kila kitu kifakuwa sawa, ila kutokana na unyeti wa hili swala ikambidi atulie tu na kuniangalia kwa huruma.

Mara simu ikaita mezani. Nikakimbia haraka haraka na kuipokea.

“Ndio.!” Nikaitikia baada ya kuipokea.

“Team C, Echo.!” Akajitambulisha.

“Go on..!” Nikamuitikia.

“Kuna magari mawili yamefika nje ya jengo hapa yamenipa wasiwasi.. Gari ya kwanza wameshuka watu wawili na gari ya pili wameshuka watu watati wote wamevaa suti zinafanana”

“Suti za aina gani?” Nikamuuliza.

“Kaunda suti” akanijibu.

“Na hao wawili wakoje” nikamuuliza tena.

“Mmoja ni muhindi na mwingine ni mzee wa makamo hivi.!” Echo akanijibu.

Nikalipuka furaha moyoni ghafla.

“OK! Wasiliana na fox ndani ya ofisi.. Nataka live report kila wanachokifanya.. Target anataka kuhamisha mzigo.”

“Tutafanya hivyo mkuu.!” Akakata simu.

“Nini kinaendelea?” Cheupe akauliza mara baada ya kukata simu.

“Walinzi wa The Board pamoja na Dr. Shirima wamefika Golden Jubilee Tower.. Wameshapata taarifa kuhusu upekuzi unaofanyika Strong Room ya Lumumba.. Naamini wameenda Golden Jubilee ili kuhamisha files.!” Nikaongea huku nabofya simu haraka haraka.

Nikampigia yule kijana aliyeko Lumumba.

“Team C, Kilo.!” Akajitambulisha.

“Kuna mabadiliko yoyote?” Nikamuuliza.

“Hapana.! Bado hawajatoka tangu nikueleze kuwa wameingia ndani.!”

“OK! Usiwapoteze.!”

“Sawa mkuu!”

Nikakata simu kuwapigia Standby Team, Team S.

“Team S, Juliet” Akajibu mdada kiongozi wao.

“Nataka muanze kwenda mikocheni B kama nilivyowaelekeza.. Mkifika kaeni nyumba ya nne kutoka nyumbani kwa Mallya kisha msubiri go ahead kutoka kwangu”

“Sawa mkuu! Tunaelekea..”

Nikakata simu. Baada ya kukata tu simu nyingine ikaingia kutoka kwa kijana aloye nje ya Golden Jubilee Tower.

“Team C, Echo.!” Akajitambulisha tena kama ada.

“Go on.!” Nikamjibu.

“Taarifa kutoka ndani Fox anasema kuwa Mallya na wale watu waliokuja wameongozana wanatoka nje…. aah aah subiri kidogo mkuu..”

Akakaa kimya kama sekunde thelathini kisha akaendelea.

“Mkuu nawaona wanatoka nje.. Mallya ameshikilia mikoba miwili myeusi ya kiofisi kila mkono.. Wale jamaa waliovaa suti za Kaunda wamemzunguka.. Yule muhindi na yule Mzee wametangulia mbele.. Nadhani wanaelekea kupanda magari.!” Akanielezea haraka haraka.

“OK! Nakuondoa hewani mara moja nataka niongee na Fox ndani ya ofisi..”

Nikakata simu na kumpigia ‘Fox’ aliyemo ndani ya Golden Jubilee Tower.

“Team C, Fox.!” Akajitambulisha baada ya kupokea simu.

“Nataka utoke hapo uende nje uungane na wenzako ‘Golf’ na ‘hotel’ mfatilie gari ambazo wanaondoka nzao Mallya na wenzake.. Unakumbuka nilivyowaelekeza?? Wewe na golf mtachukua Taxi na ‘Hotel’ atumie boda boda aliyonayo.. Pia nahitaji ‘real time’ report kuhusu kila mlipo.. Fanyeni haraka kuwafuatilia kabla hawafafika mbali..”

Sikusubiri aniitikie. Nikakata simu kwani kwenye simu nyingine mezani niliona simu ya ‘Kilo’ kijana aliye nje ya CRBB Lumumba anapiga.

“Team S, Kilo.!” Akajitambulisha.

“Go on.!” Nikamuitikia haraka haraka.

“Kama dakika sasa imepita.. ‘Ndugu zetu’ wametoka pale Lumumba kwa mwendo wa kasi wanaondoka!”

“Unaweza ukahisi wanakoelekea.!”

“Tumepita DIT, na sasa tunapita Maktaba kuu, kwa upande gari zote tatu zilipo nahisi wanataka kukunja kulia hapa, kwa muelekeo huu nadhani wanaelekea makao makuu ya CRBB, Golden Jubilee Tower..”

“Wanamtafuta Mallya.. Stay with them.. Usiwapoteze..”

Nikakata simu. Kisha nikawapigia Team C walikuwa wameweka ‘tail’ kuwafuata gari waliponda Mallya na wenzake.

“Team C, Fox.!”

“Mko wapi?”

“Ndio tumepita surrender bridge”

“OK! Mkipita tu Morocco nitaarifu.!”

“Sawa mkuu.!”

Nikakata simu.

“Nataka umpigie simu Chifu awe standby.!” Nikamueleza Cheupe ampigie Chifu, yule Mzee wa Kipemba wa Mbagala Kizuiani ambaye tulienda kumuona siku ya kwanza tulipokuwa na Kaburu.

“Sawa baba!” Cheupe akaanza kubofya simu.

Wakati Cheupe anampigia Chifu.. Mimi nikawapigia wale vijana wa Team S, Standby Team niliowaambia wakae nyumba nne kutoka nyumbank kwa Mallya, Mikocheni B.

“Team S, Juliet” akajitambulisha yule mdada kiongozi wao.

“Sasa nataka muende nyumbani kwa Mallya mkafanye upekuzi.. Nataka mjiamini kabisa.. Nyinyi ni Maafisa wa Usalama wa Taifa.. Mkifika mnajitambulisha na kuonyesha vitamvulisho nilivyowapa.. Kisha mnaanza upekuzi.. Kumbukeni kuwa hakuna chochote tunachofafuta hapo.. Its just a trap.. Kwahiyo msichukue chochote kile.. Na upekuzi ufanyike kwa dakika kumi tu.! Tafadahali zingatieni dakika kumi tu kisha muondoke.. Goodluck guys.!!”

Nikakata simu. Cheupe alikuwa amenikodolea macho huku ameweka simu sikioni anamtafuta Chifu hewani.

“Hapo umeniacha baba!! Unalenga nini??”

“Well nataka taarifa iwafikie Mallya na wenzake kuwa nyumbani kwake kuna Maafisa Usalama wanafanya upekuzi.. My guess is wanataka kwenda nyumbani kwa Mallya ili wakajipange kutokea pale mahali kwa kuzipeleka files.. Lakini wakijua kuna Maafisa wanafanya upekuzi lazima wageuze.. Na nahisi wataelekea Upanga.. Na wakijiroga kufanya hivyo tu wanaingia direct kwenye mtego niliouandaa.. So am just leading them into a trap..”

Nikaongea huku natabasamu nikipokea simu iliyokuwa inaita mkononi. Alikuwa ni Fox wa Team C.

“Ndio.!”

“Aah mkuu tumepita Morocco kama dakika tatu zilizopita ila ghafla gari zimegeuza zinarudi tena muelekea wa Surrender bridge.!” Fox akaongea haraka haraka.

“Wanaenda tunapopataka.. Stay with them.. Usiwapoteze.!”

Nikakata simu.

“Umempata Chifu?” Nikamuuliza Cheupe.

“Yes huyu hapa yuko hewani nilikuwa nakusubiri umalize kuongea na sim” Cheupe akanikabidhi simu.

“Hellow Chifu! Shikamoo.!” Nikamsalimia.

“Marhaba kijana.. Za tangu jana?” Akaniitikia.

“Nzuri tu.. ah hatuna muda wa kutosha.. Ni muda wa kutekeleza tulichoongea jana.. Dakika chache zijazo wanaingia Upanga kama nilivyohisi..”

“Sawa kijana, ila una uhakika na hili suala? Umetafakari vyema??” Akaniuliza kwa lafudhi ya Kipemba.

“Chifu sijawahi kuwa na uhakika kuhusu jambo lolote maishani kufikia uhakika nilionak leo kuhusu hili.. So yes.. Nina uhakika.! Let’s do this..”

“Sawa kijana!” Akaniitikia na kukata simu.

Nikavuta pumzi ndefu nankuishusha. Nikatabasamu. Moyoni nilianza kusikia furaha ya ushindi kwa mbali inaanza kuja.

Dakika chache zijazo, nilikuwa naelekea kuziweka mkononi files zilizobeba kati ya siri kubwa zaidi na nzito Katika Taifa la Tanzania.

May 1984, Dar es Salaam

Ndugu Rais alikaa kimya kwa dakika kadhaa akitafakari ushauri wote ambao amepewa na Charles Kajuna kuhusu kunusuru hali mbaya ya kiuchumi.

Rais alikuwa ni mtu mwenye tafakuri ya kina akiwa na uwezo wa kunyumbua barabara taarifa yoyote ya kisekta inaloletwa kwake.

Pia alijulikana kuwa na msimamo mkali dhidi ya mapensekezo yaliyotolewa na Taasisi za kimataifa kuhusu kunusuru uchumi.

Kama miezi miwili iliyopita alikuwa amemfuta kazi wazriri wa fedha Ndugu, Abdul Aziz baada ya kutofautiana kuhusu namna ya kufufua tena uchumi wa Tanzania.

“Charles..” Rais alianza kuongea baada ya kutafakari muda mrefu.

“Naam..” Charles akaitika kwa heshima zote.

“Huj ushauri unaonipa ni kwa mujibu wa utashi wako kutokana na uzoefu wako wa masuala ya uchumi au ni utashi tu wa kudurufu uliotokana na semina zenu za IMF??” Rais aliuliza kwa sauti ya ukali kidogo.

“Ndugu Rais, nimetafakari sana kwa kina kuhusu hali ya uchumi jinsi ilivyo na nimefanya utafiti wa kutosha.. Na hayo ndiyo mapendekezo yangu kwako kama Gavana wako wa benki kuu.!” Charles aliongea kwa heshima lakini kwa sauti ya kujiamini.

“Kwa hiyo unaunga mkono wazo la kushusha thamani ya shilingi?” Rais akauliza tena kwa ufupi lakini kwa sauti ya ukali.

“Ndugu Rais, kama tutaendelea kushikilia msimamo wa kufix thamani ya shilingi sawa na dollar itafika kipindi tutashindwa kabisa kufanya manunuzi ya nje kwasabu hazina yetu ya fedha za kigeni itatuishia kabisa.. Kwahiyo ndugu rais nasikitika kusema kwamba hakuna namna ambayo tunaweza kuepuka kushusha thamani ya shilingi.!” Charles akaongea tena kwa kujiamini.

“Charles.. Unafahamu kuwa nilimfuta kazi Waziri wa Fedha kutokana na misimamo yake kadhaa ukiwo huu wa kushusha thamani ya shilingi..”

“Nafahamu ndugu Rais, na sikubaliani na misimamo mingi ya Waziri Abdul Aziz lakini nasikitika kumuunga mkono kwenye hili labkushusha thamani ya shilingi..” Charles akaendelea kuongea kwa kujiamini.

“Inuka unifuate Charles.!” Rais akainuka kutoka kwenye kiti chake pale ofisini na kuanza kuelekea mlangoni.

Charles akainuka na kumfuata. Wakatoka nje ya ofisi mpaka pale kwenye sebule yake ambayo huwa anaitumia kuongea na wageni wakubwa kutoka nje ya nchi.

Kulikuwa na mabadiliko makubwa sana ya kiulinzi hapa Ikulu tofauti na namna ambavyo Charles alikuwa amezoea kwa mara nyingi alipofika hapa siku za nyuma.

Kwa mfano nje ya mlango wa ofisi ya Rais kulikuwa na Afisa Usalama mmoja, pale sebuleni walikuwepo wanausalama wengine wawili, kwenye korido kulikuwa na Maafisa wengine wawili na pale “mapokezi” walikuwepo wengine wawili.

Hii ilikuwa ni tofauti kabisa na siku zote ambapo Charles alizoea kuwakuta Maafisa wa Usalama wawili kwenye Korido na wawili wengine kwenye sebule.

Hii ilimaanisha kwamba watu wa usalama waliamini kuwa kulikuwa na tishio juu ya usalama wa Rais.

Charles na Rais wanatoka mpaka nje ya Ofisi ya Rais wakapita sebuleni, wakapita pale sehemu ya wageni kusubiri na wakatoka nje kabisa, wakaanza kutembea kuelekea kwenye bustani za Ikulu.

Kwa mara kadhaa Charles na Rais wamekuwa wakifanya “matembezi” haya kwenye bustani hasa pale Rais alipokuwa anataka azungumze na mtu suala kubwa lakini wazungimze kirafiki.

Mara zote wakiwa kwenye “matembezi” watu wa Usalama walikuwa wanawafuata lakini wanakaa umbali wa karibia mita kumi au kumi na tano kutoka mahali walipo, lakini leo hii ilikuwa tofauti kabisa, Maafisa wa Usalama walikuwa wanawafuata nyuma huku wanawapa umbali wa kama mita tano tu.

Charles akaelewa kwa kiasi gani hilo “tishio” la Usalama wa Rais walilokuwa wanalihisi lilikuwa kubwa.

“Charles..” Rais akamuita tena Charles wakiwa wanatembea.

“Kuna maneno maneno nimeanza kuyasikia.!” Rais aliongea bila kumuangalia Charles.

“Maneno gani ndugu rais?”

“Nahisi kwamba kuna watu wanatufanyia mchezo kuhusu kupotea kwa dollar kwenye mzunguko na hali hii mbaya ya kudorora kwa uchumi..!”

“Aisee! Nasikitika sana kusikia hivyo ndugu, rais” Charles Akajibu kwa heshima kubwa.

“Nakwambia haya ili kukupa tahadhali kama watakufuata na wewe.. Nasikia wanapita pita kwa viongozi kuwashawishi kuhusu hayo masuala yao.. Kwahiyo jitahidi kuchukua tahadhali kama watakufata na wewe..” Rais aliongea kutoka moyoni.

“Nakuahidi kuwa mwangalifu Ndugu Rais” Charles akaongea kwa unyenyekevu mkubwa.

Wakatembea mpaka sehemu ya parking pale Ikulu ambapo kulikuwa na gari la Charles na kuagana.

“Ndugu gavana nitaendelea kufikiri kuhusu ushauri wako na naomba na wewe na vijana wako muendelee kufikiri zaidi namna gani tunaweza kujinasua kwenye hali hii.” Rais akamuaga Charles.

“Ndugu Rais, mimi na ofisi yangu tunakuahidi kuendelea kukuna vichwa kufikifia namna nzuri ya kufufua tena upya uchumi wetu..”

“Uwe na siku njema Gavana” Rais akamuaga Charles na kumpa mkono.

“Siku njema na kazi njema kwako pia ndugu Rais”

Baada ya hapo akapanda gari na hakwenda ofisini kwake benki kuu, akaelekea moja kwa moja nyumbani kwake mikocheni japokuwa ndio kwanza ilikuwa saa saba mchana.


Ilikuwa tayari inapata saa tatu kasoro usiku ndipo Charles alikuwa anaamka tangu alale mara baada ya kurudi saa saba mchana.

Hakuwa mchangamfu kama kawaida yake, kichwani alikuwa na mawazo mengi sana.

Alikuwa amejiinamia huku amekaa kitandani akitafakari.

Kwa upande fulani nafsi ilikuwa inamsuta kwa jinsi ambavyo Rais alikuwa anamuamini lakini wakati huo huo alikuwa ni mshirika wa mtandao unaomuhujumu rais kwa malengo yao. Na ubaya zaidi si tu kwamba alikuwa mwanachama wa The Board, lakini kwa miaka kumi aliyo kuwemo kwenye mtandao huu amegeuka kuwa moja ya “key members”.

“Uko sawa baba Doro?” Mkewe Sophia alikuwa anamuuliza.

Kwa dakika kadhaa alikuwa amesimama mlango wa kuingilia chumbani akimuangalia mumewe jinsi alivyojiinamia anawaza.

“Niko sawa mke wangu.!” Charles Akajibu huku anainuka kitandani.

“Hapana mume wangu hauko sawa sawa! Niambie nini shida?” Sophia akaongea huku anamfuata mumewe.

“Uchovu wa kazi tu mkewangu” Charles akaongea bila kumuangalia mkewe Na kuanza kuchukua taulo aelekew bafuni.

“Umebadilika sana mume wangu.!”

“Unasemaje??”

“Umebadilika sana baba Dorothy! Umekuwa mtu wa siri siri nyingi sana.. Hunishirikishi huzuni zako wala kuniomba ushauri kama mwanzo.. Nini kinaendelea mkewangu?” Sophia akauliza kwa sauti ya huzuni karibu aangue kilio.

“Mkewangu, mimi moja ya watumishi waandamizi wa serikali kwahiyo usiri ni sehemu ya kazi mama Doro” Charles Akajibu huku anaanza kuingia bafuni.

“Hapana mume wangu.. Hii sio kwasababu ya kazi.. Unakumbuka siku ile miaka kumi iliyopita ulipoondoka usiku usiku.. Toka siku ile uondoke na kurejea baadae usiku ule.. Haujawahi kuwa sawa tena.. Nimenyamaza miaka yote hii lakini kuna kitu Charles kilikutokea siku ile kimekubadilisha.. Umetengeneza ukuta kati yangu na wewe na hata mwanao pia..mwanzoni nilidhani labda ukipewa ugavana furaha yako itarudi.. Lakini tangu umepewa ugavana siku baada ya siku umezidosha zaidi kuwa kivyako vyako na kujenga ukuta kati yako na sisi familia yako!! Kuna nini baba?? Nini kilikutokea siku ile usiku??” Sophia aliongea na akashindwa kuyazuia machozi yake.

“Kuna muda unatakiwa mtu ufanye sacrifice kwa ajili ya maslahi makubwa zaidi.. Najitahidi kufanya sacrifise kwa ajili ya Taifa hili kusonga mbele.. Wengi wanaweza wasikubaliane na approach yangu ila ukweli ni kwamba ‘it works’! I’m very sorry Sophia.. Kuna vitu viko nje ya uwezo wangu na inanipasa kuwa hivi.!”

Charles Akajibu kwa mafumbo na kwa mkato kisha akaingia bafuni kuoga.

Sophia akajitupa kitandani kifudi fudi na kukumbatia mto kwa nguvu na kuanza kulia kwa kwikwi kwa sauti ya chini sana.

Charles alipomaliza kuoga akarudi na kuanza kuvaa. Akachukua suti yake nyeusi nadhifu kabisa. Akaitupia mwilini.

Akaweka na ‘neck tie’ nyeupe. Viatu vyake vyeusi. Kisha akachukua ‘pini’ yake ya dhambarau yenye mchoro kama wa kichwa cha simba wa rangi ya dhahabu. Akaibana kwenye ukosi wa suti upande wa titi la kushoto.

“Nataka mama Dorothy, naelekea kikaoni.. Nitachelewa kurudi.!” Charles akaaga pasipo kusubiri jibu na kuondoka.

Sophia akamuangalia kwa jicho la uchungu sana na kuimia moyoni. Alijua pasina shaka kabisakuwa hivi “vikao” vya siri vya usiku ndivyo vilivyo mbadili mumuwe.


Kama dakika ishirini baadae, Charles alikuwa amewasili maeneo ya Oyaterbay mtaa wa mzinga.

Hapa kulikuwa na nyumba ya kawaida tu, sio ya kimasikini sana na wala sio ya kitajiri, lakini ilikuwa na eneo kubwa lililozungushiwa ukuta.

Nyumba hii The Board waliubatiza jina ”Hema Ya Kukutania”.

Vikao vyao vyote vya siri kila baada ya miezi mitatu vilifanyika hapa.

Hiki nilikuwa ni kikao cha dharura kilichoitishwa na ‘Chairman’ kwasababu bado miezi mitatu ilikuwa haijapita tangu wakutane wanachama wote.

Geti likafunguliwa na Charles akaingia na kwenda kupaki gari.

Ilionyesha kuwa tayari wanachama wengine wengi walikuwa wamewasili kutokana na idadi ya magari aliyoikuta pale nje.

Nyumba hii ilikuwa moja ya nyumba chache mtaani hapo ambayo haikuwa na umeme na kutokana na siku hii kuwa na giza kubwa bila nyota wala mwezi angani kwahiyo kulikuwa na taa za chemli nyingi zimening’inizwa kwenye kona kadhaa za nyumba.

Charles akaingia ndani, kisha akafuaga korido inayoelekea mwishoni kabisa mwa nyumba ambako kuna chumba kikubwa kama ‘mesi’ ya chakula, lakini kulikuwa kumewekwa meza kubwa ndefu sana yenye viti kumi na sita kila upande na kiti kimoja mwisho wa meza kila upande.

Charles aliwakuta wenzake wote 29 wamefika, hivyo yeye akakamilisha idadi ya mtu wa thelathini.

Walikuwa wanasubiriwa Chifu Sekioni na Chairman.

Watu wote walikuwa kimya kabisa wameketi kwa utulivu, maongezi yalikuwa yanaruhusiwa pekee baada ya kikao kuisha, sio kabla.

Dakika kumi na tano baadae Chifu Sekioni na Chairman, Waziri Mkuu Chance Ramadhani Chande wakawasili ndani ya ukumbi.

Chifu Sekioni akaenda kukaa upande mmoja wa meza na Waziri Mkuu Chande akaenda kukaa upande mwingine.

Baada ya kuketi. Chairman alisubiri kama dakika tatu hivi za ukimya zikapita kisha akaanza kuongea.

“Kama mnavyofahamu kikao hiki ni cha dharura, kwahiyo hatutatumia muda mwingi kama kwenye vikao vyetu vingine. Kikao hiki kitahusu suala moja tu ambalo ni ‘future na usalama’ wa umoja huu”

Akanyamaza kidogo kuwaangalia wenzake, kisha akaendelea.

“Nianzie mbali kidogo ili twende sawa.. Umoja huu ndio unaolinda roho ya Taifa hili.. Na nikisema roho ya Taifa hili nadhani mnanielewa namaanisha nini,1% ya Watanzania wanaoendesha uchumi wa Taifa hili, 1% ambao wameushika uchumi wa nchi na kuupa pumzi.. The Board sisi ndio watetezi wao, sisi ndio jukumu letu kuhakikisha hii 1% inalindwa na ikiwezekana kushamiri ili Taifa hili lisonge mbele.. Kwa maneno mafupi sisi humu ndani watu 32 ndio roho ya taifa hili la Tanzania.”

Akanyamaza tena kidogo, akawatazama kisha akaendelea.

“Sasa kuna taarifa yetu imevuja, japokuwa imevuja kwa uchache sana.. Ndugu Rais ameanza kuwa na mashaka na Mimi..ameniwekea Maafisa wa Usalama wanichunguze kwa siri kubwa.. Na wote tunafahamu nini kinafuata Mzee wetu akiwa na mashaka na wewe.!! Nimetafakari sana na nimechukua kila aina ya tahadhari lakini yapasa kuwa mkwelj kwamba muda wowote anaweza kuniweka kizuizini au jambo bays zaidi linaweza kufanyika!! Hivyo basi kwa kuzingatia kuwa umoja huu, The Board ni bora zaidi kuliko yeyote hapa kati yetu, nikiwemo mimi mwenyewe.. Kwasababu sisi wote hapa kesho ma kesho kutwa hatutakuwepo.. Lakini The Board itaendelea kuwepo hata miaka mia mbili kutoka leo.. Hivyo inanipasa kuchukua hatua stahiki kama ilivyo deaturi yetu!”

Akanyamaza tena, akawatazama safari hii kwa muda mrefu zaidi. Kisha akaendelea.

“Nataka niwaweke wazi ninaye mpendekeza awe mrithi wangu endapo chochote kitatokea kwangu.. Labda nikiwekwa kizuizini au jambo bays zaidi likitokea.. Nataka awepo wa kushuka nafasi hii ma shughuli zetu ziendelee kama ilivyo ada.!”

Akanyamza tena. Baada ya kunyamaza Chifu Sekioni akainuka na kuanza kumpa bahasha kila mwanachama.

“Bahasha hiyo ina jina la minaye mpendekeza.. Kama mnavyokumbuka kanuni zetu.. Yeyeto atakayechaguliwa kuwa Mwenyekiti wetu ni lazima apate kura zote za ndio kutoka kwa wanachama wote.. Endapo akipata hata kura moja ya hapana basi nitahairisha kikao hiki na kuitisha kingine nikiwa na jina lingine.! Kwahiyo naomba mfungue bahasha hizo kuangalia jina ninalo pendekeza kisha andika kura yako ya NDIYO au HAPANA.!”

Chairman aliongea na wanachama wote wakaanza kufungua bahasha ili waone nani anayependekezwa na wapige kura zao.

Tulikuwa bado tuko ofisini Makumbusho lakini tulikuwa tunafanya haraka haraka kukusanya kila karatasi ambayo ilikuwa ni muhimu na tulikuwa hatutaki ibaki hapo ofisini.

Mezani simu ilikuwa inaita, nilipoangalia alikuwa ni kijana Echo, wa Team C.

“Go on..” Nialkamuitikia haraka haraka baada ya kupokea.

“..ndugu zetu wanatoka hapa Golden Jubilee kwa haraka mno.. Wanatembea haraka haraka karibia na kukimbia wanaelekea kwenye magari..” Echo, akanieleza haraka haraka.

“OK! Wanawahi nyumbani kwa Mallya..”

Nikakata simu kisha nikawapigia Team S ambao nilikuwa nimewapa dakika kumi tu wafanye upekuzi nyumbani kwa Mallya.

“Team S, Juliet”

“Mko wapi?”

“Tumeshatoka nyumbani kwa Mallya, tuko Mwenge muda huu tunasubiri maelezo yako.!”

“Nataka mtawanyike mmoja mmoja kwa utaratibu kurudi nyumbani.. Hapo mwenge mnaweza kumuacha mtu mmoja, Ubungo mkamuacha mwingine hivyo hivyo mpaka wote muishe.. Hongereni sana kwa kazi ya leo mmeifanya kwa mafanikio makubwa sana.. Mkirudi majumbani kwenu kumbukeni nilichowaeleza.. Lay low! Ni vyema hata msiondoke kutoka majumbani kwenu mpaka niwasiliane na nyinyi.. Goodluck guys!”

“Asante sana mkuu!”

Nikakata Simu kisha nikawapigia Team C.

“Team C, Fox”

“Naomba update!”

“Tupo tumesimama nje ya Sekondari ya Tambaza, hii barabara haina magari mengi kwahiyo inabidi tuweke distance kubwa sana ili wasije kushtuka kuwa tunawafuatilia.. Hapa kwa mbali nawaona wamekata kona kama wanaelekea Diamond Jubilee.!”

“OK! Tumeshafahamu wanakoelekea mpaka hapo.. Mmefanya kazi nzuri sana kwa siku ya leo.. Naomba mrejee majumbani kwa kutawanyika mmmoja mmoja kwa utaratibu na vyema mkiwa majumbani msitoke kwenda kokote mpaka nitakapo wasiliana nanyi.. Goodluch guys.. Na hongereni sana!”

“Asante sana mkuu!”

Nikakata simu.

“Hawa vijana mwisho wao itakuwaje?” Cheupe akaniuliza kwa sauti fulani ya kuonyesha kuguswa na hawa vijana.

“Itabidj nifikirie jambo ni namna gani hatiwatupi.!” Nikaongea huku namalizia kuweka makaratasi kwenye begi la mgongoni.

“Yes! Jitahidi ufikirie namna baba, wametusaidia sana na wamerisk maisha yao pasipo wenyewe kujua.. Si vyema tukiwaacha solemba!”

“Yeah! I will think of something.. Naona hapa kila kitu kiko sawa.!” Nikaongea huku nimesimama nabkujishika kiuno kuhakikisha kuwa hatujasahau kitu.

“Nadhani tuko vizuri!” Cheupe akanijibu.

“Just one last thing pasipo kusahau..” Nikachukua karatasi nyeupe na kuanza kuandika.

[email protected]

Kisha ile karatasi nikaiweka juu ya meza ya ofisi na kuigandamiza na glasi.

“Una hakika gani kuwa Usalama watakuja hapa ofisini??” Cheupe akaniuliza huku anaangalia ile karatasi.

“Sidhani kama itawachukua hata siku tatu kabla hawajang’amua mchezo tuliowafanyia.. Na waking’amua lazima watakuja hapa ofisini kupekuwa.. And I want them to find this piece of paper.”

“Kwanini usiwaandikie tu huo ujumbe kwa maneno ya kawaida badala ya kuiweka kwenye fumbo namna hiyo?” Cheupe akaongea huku anageuza geuza shingo kuangalia pale mezani ili ausome ule ujumbe sawia.

“Ni tahadhali Mamangu, in case mtu mwingine akiusoma badala ya Watu wa Usalama.. Sitaki aelewe.. Na watu wa Usalama wakishindwa kuutafsiri huu ujumbe basi hawafai hata kuwa Maafisa usalama..” Nikamjibu huku tunaanza kuondoka hapo Ofisini.

Tukatoka nje ya ofisi na kufunga milango. Kisha tukashuka mpaka pale chini ya kighorofa na kuita Taxi.

“Niwapeleke wapi Boss” Dereva Taxi akatniuliza baada ya kuwa tumepanda kwenye Taxi.

“Mbagala Kizuiani.!” Nikamjibu kwa Kifupi.

Dereva akawasaha gari na Safari ya kuelekea Kizuiani ikaanza.

Siku tatu kabla ya siku ya leo nilipotoka kuonana na Baba bite kwa ajili ya kuchukua documents za Kaburu, niliporudi nilikuwa na mazungumzi muhimu sana na Kaburu kuhusu namna ya kufanikisha mkakati wa kuzipata documents.

Wasiwasi wangu mkubwa ilikuwa najaribu kuumiza kichwa ni mahali gani ambapo The Board watazipeleka Files zao kwa dharura endapo watazihamisha kutoka strong room ya CRBB HQ.

Kaburu yeye alihisi kwa kiwango kikubwa zitapelekwa Upanga kwenye nyumba fulani ambayo umewahi kutumika miaka ya sabini na themanini kuhifadhi file hizo kabla ya Mallya kupewa Cheo Cha The Book Keeper ndani ya The Board na kuzihamishia file hizo kwenye Strong Room Golden Jubilee Tower.

Alimieleza kuwa nyumba hiyo ya Upanga ilikuwa inatumika miaka ya zamani kuhifadhi sarafu za benki kuu ya Tanzania.

Akanieleza kuwa nyumba hiyo ilikuwa imekodiwa kwa miaka mingi na benki kuu kutoka kwa mwanachama mmoja wapo wa The Board. Baada ya Benki kuu kuacha kutumia nyumba hiyo kuhifadhi sarafu The Board wakaendelea kuitumia Nyumba hiyo kwa shughuli zao nyingine.

Kaburu akanieleza kuwa katika kumbukumbu za jiji nyumba hiyo imeorodheshwa kama “ghala” lakini kiuhalisia nyumba hiyo iko tupu. Haina watu wanaoishi wala hakuna kinachohifadhiwa.

Kaburu akanieleza kuwa mara chache The Board huwa wanafanya vikao vyao humo.

ITAENDELEA

Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034 Sehemu ya Tano

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment