Sharobaro wa Tandale Sehemu ya Tano
CHOMBEZO

Ep 05: Sharobaro wa Tandale

SIMULIZI Sharobaro wa Tandale
Sharobaro wa Tandale Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA: ZULFA HUSSEIN

*********************************************************************************

Chombezo: Sharobaro Wa Tandale

Sehemu ya Tano (5)

Kama unavyofahamu joto linapopanda kwa watu ambao wapo sehemu ambayo ni salama kwao kufanya chochote bila kubughudhiwa na mtu zaidi ya kumchukiza tu mola wao, Dullah na Atu si wakajikuta wapo kama walivyokuja duniani.

Dullah alipomtazama binti wa watu akiwa kalegea na kamtumbulia macho huku akihema, akaona akimchelewesha bila kumpa mkomboti itakuwa dhambi kubwa, sijui alimbinuaje bwana, Atu akaanza kutoa ushirikiano huku akilia kwa raha.

Rigwaride lilichezwa kwa kila mmoja kuhakikisha anamfaruhisha mwenzake,wa kwanza kupeperusha bendera ya ushindi alikuwa Atu ndipo mzee mzima akalishusha kombora lake lenye ujazo wa kutosha lililomlegeza kabisa Atu.

Baada ya wawili hao kumaliza awamu hiyo ya kwanza walipeana asante na kwenda kuoga ndipo Dullah alimwagizia Atu kilevi alichotumia, akamwita mtu wa jikoni na kuagiza michemsho ya kuku miwili ili warudishe damu.

Dullah na Atu walikunywa bia na walipomaliza kula mchemsho wa kuku, si wakaanza tena vimichezo vyao vya chumbani zaidi,miili yao ilipopata joto jamaa akamkwangua tena, awamu hiyo aliunganisha mashuti mawili ya ndani kwa ndani.

Walitoka pale saa tanu na nusu wakiwa hoi kwa kibarua walichokuwanacho na ulevi, Dullah alimpatia Atu teni moja, wakapanga kukutana tena wikiendi kisha kila mmoja akatoka kivyake.

Kama kawaida, ili kuficha harufu ya pombe Dullah alipofika gengeni kwa Chinga akanunua tango na ndizi mbivu akala na kuelekea kwao ambapo aliwakuta wazazi wake wakiwa wanaangalia runinga.

Kwa vile hakujiamini aliwasalimia na kuunga chumbani kwake alikobadili nguo kisha akachukua mswaki na kuelekea bafuni, alipomaliza kuoga aliamua kulala.

Mama yake alipokwenda kumgongea ili akale alimwambia alikula alikotoka, akamuacha na kurudi sebuleni na kumwambia mumewe kwamba siku hiyo kijana wao alionekana kuchoka sana na kazi za ujenzi kwani hawakujua kama hakwenda Madale na fundi Yassin.

Kulipokucha Dullah aliamka na kumkuta mama yake akiwa anafanya usafi jikoni, akamweleza kila kitu kuhusu kusimama kwenda site na fundi Yassin, akamfahamisha kwamba alipata kazi nyingine.

Mama alipomwuliza ni kazi gani alimwambia ya kuosha magari Posta, mama akashindwa kujizuia kucheka, akamwuliza;

“Yaani wewe Dullah ninayekufahamu umeamua kuosha magari, tena Posta?”

“Ndiyo maana yake, mbona nilikuwa nafanya kazi ya ujenzi bila matatizo, tena mama naona kazi ya kuosha magari inalipa zaidi kuliko ya ujenzi,” Dullah alimwambia mama yake ambaye hakujua nyuma ya kazi hiyo kulikuwa na nini.

Mama huyo alicheka na kumwambia alimfurahisha kwa kuamua kufanya kazi yoyote ilimradi apate fedha, kwa furaha aliyokuwanayo akaenda kumwambia mumewe.

“Mimi nilikuambia kitafika kipindi huo usharobaro wake utaisha, umeniamini mama Dullah ?” baba Dullah alimwambia mkewe,wakacheka.

Wakati mke na mume wanazungumza chumbani, Dullah alipomaliza kujiandaa akamuona baba yake akamwamkia.

“Vipi nasikia kule kwa fundi Yassin hauendi umeanza kazi ya kuosha magari Posta?” baba yake alimwuliza.

“Ni kweli baba,si unajua maisha ya leo hayahitaji kuchagua kazi!” Dullah alimwambia mzazi wake.

Baba yake alifurahi na kumwambia kikubwa afanye kazi hiyo kwa uaminifu na kuwaheshimu watu wote atafanikiwa kwaniwengine wanaweza kumpa msaada mkubwa.

Dullah alipomaliza kuzungumza na baba yake alielekea nyumbani kwa akina Ipyana, akamkuta msichana wao wa kazi aitwaye Kisa akifanya usafi, alipomuuliza kama Ipyana alikuwepo akamwambia alikuwepo.

Kijana huyo mpenda mademu wazuri alivutiwa sana na kifua cha Kisa kilichopambwa na viembe bolibo vya kuchoma akaamua kumuweka kiporo, akaelekea geto kwa rafiki yake.

Marafiki hao walipopeana hi hawakuona sababu ya kuchelewa wakaenda kupanda gari na kuelekea Posta, njiani Ipyana kila alipomtupia macho Dullah akawa anatabasamu tu!

“Vipi naona unanitazama na kuachia tabasamu kulikoni?” Dullah alimwuliza Ipyana.

Rafiki yake huyo alimwambia alifurahishwa na mambo yake hasa jinsi alivyomuaga jana kwamba anakwenda kumuona mshkaji wake kumbe alikuwa na miadi na totoz.

“Huo ndiyo uanaume, ukiwa na fedha mfukoni lazima utafute kiburudisho tena jana nilikula bata ndefu na dogo aliondoka akiwa kachoka balaa kwa swaga nilizompa,” Dullah alijisifia ujinga.

Ipyana aliishia kucheka na kumwambia lakini pale wizarani ndiyo itakuwa mwisho wake asipokuwa makini kwani palikuwa na wanawake wazuri na wenye fedha zao wapenda viserengeti boy.

“Umakini wa nini au unazungumzia ngoma nini?” Ipyana alimwuliza.

“Ndo maana yake,” Ipyana alimwambia.

Alipoambiwa hivyo Dullah alicheka na kumwambia asiwe na wasiwasi kilichozaliwa lazima siku moja kife, iwe kwa maradhi au kwa sababu zingine hivyo hawezi kumuacha mwanamke yeyote atakayejipendekeza kwake.

Kufuatia stori kunoga wakajikuta wamefika Posta, waliteremka na kwenda eneo lao la kazi, kama ilivyokuwa siku ya kwanza wafanyakazi kibao wa wizara wakiwemo mabosi waliwachangamkia vijana hao.

Siku hiyo mishale ya saa mbili kasoro alifika dada Fatuma aliyemchangamkia sana Dullah na kumfahamisha Ipyana kwamba alikuja na gari lake linguine alilotaka lioshwe na Dullah kufuatia jana yake kumuoshea vizuri gari aliloliacha nyumbani.

“Dullah nafikiri umemsikia dada Fatu kakupa tenda hiyo, kazi kwako,” Ipyana alimwambia Dullah aliyeishia kucheka.

Kabla Dullah hajasema chochote Fatu akachomoa noti ya shilingi elfu tano akawaambia ya chai na kumuomba Dullah jioni watapotoka kazini aende naye nyumbani kwake akamsaidie kazi f’lani.

“Kazi gani dada Fatu?” Ipyana alimwuliza dada huyo.

“Na wewe Ipyana bwana, akija kuifanya atakwambia ninyi si marafiki?” Fatu alimwambia.

Baada ya Fatu aliyepania kutoka na Dullah siku hiyo ili kumburudisha kufuatia kukaa muda mrefu bila kuletewa fujo za kikubwa kuondoka, vijana hao walipomaliza kuosha gari lake aina ya Love4 wakaenda kunywa chai.

“Dullah nilikwambia jana, Fatu katokea kukupenda naona sasa umeamini na leo hana kazi wala nini anataka kukupa ofa, dah kijana una balaa wewe?” Ipyana alimwambia Dullah kwa sauti ya chini walipokuwa wakinywa chai.

“We ngoja hiyo jioni ifike, mimi akijipendekeza namlamba bakora zakutosha kwani siyo dada yangu yule,” Dullah alimwambia Ipyana wakacheka.

Waliporejea eneo la kazi, kwenye saa tano kasorobo alifika mama Maduu aliyejazia nyuma aliyetokea kumtamani Dullah , baada ya salamu alimwuliza Ipyana Dullah alikuwa akiishi wapi akamwambia Tandale.

“Kumbe mnaishi eneo moja, sasa nakuomba kama hutajali saa sita twende mara moja pale Vetenary Tazara ukanisaidie kubeba mabati nitakayoyanunua tuyapeleke nyumbani kisha tunarudi, unasemaje?” mama Maduu alimwambia Dullah .

“Hakuna shida mama yangu, si hatutachelewa sana?” Dullah alimwuliza.

Mama huyo alimwambia wasingechelewa ndipo alifungua pochi na kutoa shilingi elfu kumi na kuwaambia wagawane na kwamba anakwenda ofisini kwake kumaliziakazi f’lani itakapofika saa sita kamili atamwita Dullah .

“Kwani wewe Dullah hauna simu?” mama huyo alimwuliza.

Dullah alimwambia alikuwa nayo na bila kusubiri aulizwe namba akamwambia namba zake ambapo mama huyo akazisevu, kisha akaachia bonge la tabasamu lilimchanganya sana sharobaro Dullah .

“Kaka wewe una nyota ya kupendwa, nahisi huyo mama hana kazi yoyote zaidi ya kukutunuku kwa ninavyomfahamu huenda anataka kwenda kukufanyia shopping ya nguvu, ngoja tusubiri,” Ipyana alimwambia Dullah .

Saa sita kasoro dakika tano, simu ya Dullah iliita alipoangalia namba ya mpigaji hakujua ilikuwa ya nani, alipopokea alisikia sauti nzuri ya mwanamke aliyejitambulisha aliitwa mama Maduu!

“Kumbe ni wewe mama!” Dullah aliuliza baada ya kupokea simu.

“Usiniite mama Dullah , niite anti au…” mama huyo hakumalizia sentensi yake na kumwambia Dullah amkute kwenye geti la kutokea.

Dullah aliachia tabasamu na kumwambia Ipyana alikuwa akizungumza na mama Maduu aliyemwambia amkute geti la kutokea nje, Ipyana hakuwa na la kusema zaidi ya kucheka na kumtania Dullah kwamba akirudi naye alitaka zawadi kutoka kwa mama.

Dullah alimuaga Ipyana huku akimwambia kama atapewa zawadi wala asijali angempelekea, kijana huyo aliyebadili nguo na kuvaa alizotokanazo nyumbani alikwenda kumsubiri mama Maduu getini.

Hazikupita hata dakika nne aliliona gari la mama huyo likielekea getini kisha kusimama, Dullah aliingia kwenye gari la mama huyo huku baadhi ya madereva waliokuwepo pale getini wakiwasubiri mabosi wao kuanza kumjadili.

“Jamani mmemuona mama Maduu katoka na yule dogo mgeni aliyeosha magari?” dereva mmoja ambaye wenzake walipenda kumwita Mwarabu kutokana na weupe wake aliwauliza wenzake.

“Tumemuona bwana, kwa tabia zake za kupenda viserengeti boy huenda anakwenda kujirusha naye,” dereva aliyeanzisha mada aliwaambia wenzake ambao walikubaliana naye.

Mama Maduu akiwa na Dullah kwenye gari bila aibu alimweleza kwamba hajielewi kwa nini tangu alipomuona jana yake alitokea kumpenda kiasi cha kumfikiria sana.

“Kwa binadamu hilo ni jambo la kawaida,mimi nashukuru mama kwa kunipenda,” Dullah alimwambia.

“Nimekwambia usiniite mama…niite anti,” mama Maduu alimwambia Dullah huku akikanyaga mafuta hivyo gari kwenda kasi.

“Oke anti,” Dullah alimwambia.

Dullah ambaye hakujua walikuwa wakienda wapi alitulia tu huku akijisemea moyoni kwamba mama Maduu akirogwa tu kutaka mambo angemvuruga kisawasawa.

Dullah alipokubali, mama Maduu alimshukuru na kumwambia kama atakuwa akifanya atakavyokuwa akimweleza atafurahia maisha, walipofika Maduka Mawili alikata kulia na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwake akaegesha gari na kumkaribisha Dullah sebuleni kwake.

Wakiwa wameketi kwenye sofa la watu wawili ndipo mama huyo akaingia chumbani alikobadili nguo na kurejea akiwa kavaa kanga nyepesi aliyojifunga maungoni ndani akiwa na nguo ya mwisho.

Kudadeki,Dullah alipomtupia macho mama huyo aliyefungashia nyuma balaa na yale macho yake makubwa ya kurembua, akajikuta amevurugwa kabisa na kujisemea moyoni;

“Kumbe huyu hanijui eh?”

Mama Maduu alimwuliza Dullah kama alikuwa akitumia kilevi, Dullah alimwambia hayo ndiyo mambo yake kwa sana, tena hata mivinyo mikali alikuwa akitumia.

Alipotoa kauli hiyo, mama Maduu alicheka na kumwambia kama alikuwa akipasha mambo hayo atakuwa rafiki yake, akamwuliza muda ule alitaka kunywa nini kati ya bia na mvinyo!

“Chochote utakachoniletea hakuna shida,” Dullah alimwambia.

Kwa kuwa lengo lake lilikuwa kubilingishana na kijana huyo mbichi, mama Maduu kila alipompa mgongo Dullah alikuwa akilitikisa bambataa lake pana na kumchanganya kabisa sharobaro huyo.

“Haya mvinyo upo tayari tunywe kwa raha zetu,” mama Maduu alimwambia Dullah baada ya kumimina mvinyo mkali kwenye glasi mbili zenye shingo ndefu.

Baada ya mvinyo huo kuanza kuwapanda vinchwani, Dullah ndiye aliyemvutia mama huyo karibu yake ambapo mapaja yao yaligusana, akaanza kuzishika hipsi zake laini na kumsifia;

“Anti hivi sasa tu upo hivi, je ulipokuwa msichana wa miaka ishirini na mbili au tatu si ilikuwa balaa?”

Mama Maduu alipoambiwa hivyo alifurahi na kumwambia Dullah kwamba enzi hizo alikuwa tishio hata mtu wake wa kwanza kutoka naye kimaloo alifaidi sana.

Kauli ya mama huyo, ilimkumbusha Dullah siku aliyomla kwa mara ya kwanza ‘kuku’ wa demu wake Vivian, akasisimkwa na kujikuta akimbusu mfulululizo mama Maduu.

Mama huyo aliyeisubiri kwa hamu nafasi hiyo naye alianza kujibu mashambulizi, si wakajikuta wamegusanisha vinywa vyao na kuanza kula denda ambalo a.k.a yake ni mua.

Dullah ambaye tayari alikwishakuwa kichaa wa mapenzi, hakumpa nafasi mama Maduu ya kumzidi maujanja, aligusa kila eneo hatarishi ndipo mama Maduu akaanza kuhemka na kuyazungusha kila upande macho yake makubwa yaliyolegea.

Kutokana damu ya Dullah kumchemka sana, aliifungua ile kanga aliyovaa mtumishi huyo wa serikali ambaye alitoroka kazini katika utawala huo ambao kutumbuana majibu hakukuwepo akaitupa kule.

Mama Maduu ambaye naye alikuwa mjuvi wa malovee hakuwa nyuma, alivivua viwalo vya Dullah tena bila kuacha hata kimoja na kuvitupia juu ya kanga yake, walipoangaliana wakatabasamu.

Dullah naye akaona muda muafaka wa kuleteana fujo za kiutu uzima uliwadia, si akaiondoa nguo ya mwisho ya mama huyo,wakawa saresare mauwa.

Mama maduu naye akamkonyeza Dullah na kuachia tabasamu pana kuashiria kwamba alikuwa akimsubiri amfanyie chochote alichotaka, sharobaro Dullah akameza mafunda mawili ya mate na kujilamba midomo yake.

Kwa kuwa kijana huyo mpenda mademu wazuri alitaka kumchanganya mama wa watu ili atakachokihitaji toka kwake akipate, si akamvaa na kuanza kumpa swaga zake.

Dullah hakuwa na pupa, alianza mashambulizi yake taratibu na kuongeza kasi kidogokidogo alipoona mama ameanza kuelemewa na swaga zake akaanza kuchimbua visiki kwa fujo.

Japokuwa mama Maduu alikuwa kajazia f’lani hivi lakini alikuwa mwepesi mno, licha ya kwamba alipitisha muda mrefu bila kula tende alikuwa mwepesi alikwenda sawa na biti za Dullah .

Kabumbu lilipigwa kisawasawa na mtaalam Dullah kijana wa Tandale alipogundua mama anaelekea golini ili afunge akaamua kumpisha, mama alipofika lango ile anataka kufunga wakakutana golini.

Kufuatia kukutana katikati mama huyo alishangilia kwa kujinyoosha na kushusha pumzi kwa nguvu kwani tangu alipoanza mambo ya kandanda, hata marehemu mumewe hakuwahi kufanyia mambo matamu kama Dullah .

“Da baby asante maana hapa umeniacha hoi sijui nikuambiaje, kuanzia leo wewe utakuwa mtu wangu wa kudumu, chochote ukacho niambie,” mama Maduu alimwambia Dullah akiwa kayalegeza macho yake.

“Jamani anti mbona kawaida tu, oke kama umefurahi nashukuru nikuahidi tu kwamba utazidi kufurahi,” Dullah alimwambia.

Sehemu ya 30

Mama Maduu na Dullah wakiwa pale sebuleni simu yake ikaanza kuita, alipoangalia mpigaji alikuwa bosi wake, moyo ukapiga paa!

Hata hivyo, ilibidi aipokee na kuanza kuzungumza na bosi wake aliyemuuliza alikuwa wapi akamwambia alikwenda benki mara moja. Baada ya kukata simu, licha ya kutaka kuendelea kufanya yao na Dullah alimwambia kwamba anahitajika ofisini.

Awali mama huyo alitamani kama amuache Dullah pale ili atakaporejea jioni waendelee kuburudika lakini akagundua ilikuwa mapema mno kufanya hivyo.

“My baby, nilishaamua nisurudi tena ofisini lakini bosi kaniita itabidi tuondoke ila tukitoka tu jioni tunarudi hapa kuponda raha, sawa mpenzi wangu?” Mama Maduu alimwambia Dullah .

“Hakuna shida maana kwa mambo uliyonifanyia nilitamani leo tujifungie hapa ndani hata kama mpaka asubuhi,” Dullah alimwambia, mama huyo akacheka na kumpiga kibao f’lani hivi cha mahaba begani.

Wawili hao ambao tayari kila mmoja aliujua mwili wa mwenzake, waliingia bafuni kuoga lakini kabla hawajaanza mama alitoka na kurejea na mswaki mpya akaweka dawa na kumkabidhi Dullah kisha naye akachukuwa wake wakaanza kujiswafi kuondoa harufi ya mvinyo waliokunywa.

Walipomaliza, waliingia kwenye gari na kuanza safari ya kurudi ofisini, njiani mama alizidi kumfagilia Dullah kwa mautundu aliyomfanyia hasa alipompa mkomboti wa uhakika.

Mama Maduu alipokaribia ofisini alimshusha Dullah na kumweleza asubiri kama dakika kumi na tano ndipo aende, akafungua pochi yake na kumpatia noti mbili za shilingi elfu kumi akaachia tabasamu na kumuaga Dullah .

“Da! Haya ndiyo mambo ninayoyatakaga, huyu mama sitamwacha, kwanza nimuache kwa sababu gani? Kama mapenzi anayaweza!” Dullah aliwaza.

Baada ya kupita dakika ishirini, Dullah alirudi eneo lake la kazi na kumkuta Ipyana akiosha gari la bosi mmoja wa idara ya fedha.

“Niambie kijana mwenye nyota inayong’ara, umeshamsaidia mama kazi yake?” Ipyana alimwuliza.

Kufuatia swali hilo, Dullah alicheka sana na kumwambia hakukuwa na kazi yoyote zaidi ya kukata mitaa kisha kurudi na faida ya kupewa shilingi 20,000, akatoa teni moja na kumpatia rafiki yake.

“Eh! Au umemkwangua mama wa watu maana wewe Dullah ni noma!” Ipyana alimwambia.

Dullah alicheka na kumwambia anapopata nafasi huwa afanyi makosa akimaanisha tayari alimgaragaza mama Maduu!

“Nilijua tu, wewe upewe shilingi ishirini elfu bure tu!” Ipyana alimwambia rafiki yake.

Wakiwa wanaendelea na stori zao, Ipyana alimfahamisha Dullah kwamba akiwa hayupo dada Fatu alifika pale mara mbili kumwulizia akamwambia alitoka kidogo.

“Anasemaje?”

“Anasisitiza tu jioni uende naye kwake ukamsaidie kazi ambayo nimemwuliza ni kazi gani kakataa kuniambia,” Ipyana alimwambia.

Wakiwa wanaendelea na maongezi, si wakamuona dada Fatu anaelekea walipokuwa, alipowafikia akamwuliza Dullah alikwenda wapi, akamdanganya kwamba alikuwa ameenda Feri mara moja.

“Sasa nimepata nafasi, tunaweza kuondoka muda huu?” Fatu alimwuliza Dullah ambaye alimwambia hakuwa na kikwazo.

“Oke safi sana, kwa kuwa nimeacha mkoba wangu ndani wewe tangulia pale kwenye kona nakuja,” Fatu alimwambia Dullah .

Lakini kabla hajaondoka aliingiza mkono kwenye mfuko wa siketi aliyovaa akatoa noti ya shilingi elfu kumi na kumpatia Ipyana na kumwabia;

“Hela ya lachi hiyo ngoja rafiki yako akanisaidie kazi, tukichelewa mtakutana nyumbani.”

Ipyana aliyejiona mwenye bahati siku hiyo ya kupata shilingi ishirini ya bure alimwambia hakukuwa na shida kwa upande wa Dullah wangewasiliana kwa simu.

Dullah aliyekuwa amefurahi alijua hata dada Fatu hakuwa na kazi yoyote zaidi alimzimikia, akaapa kwamba akijilengesha tu hasira zote atazimalizia kwake baada ya mama Maduu kupigiwa simu na bosi wake na kukatisha mchezo.

Kama alivyoelezwa, alipofika kwenye kona ya mtaa wa Samora na Oio hata hakumaliza dakika nne akaliona gari la dada Fatu, liliposimama alizama ndani safari ya kwenda ambako hakukujua ikaanza.

Dada huyo aliyeonekana mwenye furaha aliendesha gari kwa kasi huku wakipiga stori za hapa na pale na Dullah hadi walipofika Kinondoni nyumbani kwake.

Fatu alipoegesha gari uani mwa nyumba aliyokuwa akiishi alimkaribisha Dullah sebuleni kwake, Dullah akiwa ameketi akawa anaangaza macho huku na kule kufuatia sebule kuwa na vitu vya thamani.

Sebule ya dada Fatu ilikuwa kubwa sana, ilikuwa na sehemu ya kulia chakula, kusomea na kaunta ya baa ya ndani iliyokuwa imesheheni vinywaji mbalimbali zikiwemo pombe kali na za kawaida.

“Dullah hapa ndipo nyumbani kwangu karibu sana na jisikie upo nyumbani,” Fatu alimwambia Dullah .

“Nashukuru sana tena sana na hongera kwa haya maendeleo ninayoyaona,” Dullah alimwambia.

“Dullah bwana, asante ila ni maendeleo ya kawaida sana,” Fatu alimwambia.

Baada ya mazungumzo hayo ya kupongezana, Fatu alimwambia Dullah kwa kuwa alikuwa kijana wa kisasa aliamini alikuwa akitumia kilevi na kama hakukosea ajongee pale kaunta ajihudumie alichokihitaji.

Kauli hiyo ilimpa raha Dullah aliyekatishwa mzuka wa kulamba gambe nyumbani kwa mama Maduu aliyepigiwa simu wakati ndiyo kwanza mambo ya chumbani zaidi yalianza kunoga.

Baada ya Dullah kumshukuru dada Fatu aliyekuwa na lake jambo, walijongea kwenye kaunta ya vilevi ambapo kijana huyo mkali wa watoto wazuri alimwelekeza Fatu kinywaji alichotumia, akafunguliwa na kuanza kupasha.

“Samahani mgeni wangu, wewe endelea nakuja baada ya dakika sifuri,” Fatu alimwambia Dullah .

Fatu akaenda chumbani kwake ambako hakukaa sana akarejea akiwa kajifunga kanga nyepesi iliyoonesha jinsi maungo yake yalivyokuwa yamenona na kifuani viembe bolibo vyake vya kiuchokozi vilichomoza.

“Hivi hawa viumbe utafikiri wanaambiana, mama Maduu naye nilipofika kwake alivaa hivihivi, huyu naye mlemle, sasa kujenga heshima naye namchinjia baharini,” Dullah alijisemea moyoni.

“Dullah , nakuomba uwe huru na chochote unachokihitaji niambie hapa kwamba kila kitu kipo,” Fatu alimwambia Dullah .

Dullah aliyejua Fatu hakuhitaji chochote zaidi ya mkomboti alimtazama kwa macho Fulani hivi yenye meseji nzito, Fatu akaachia tabasamu pana.

“Dada Fatu, siyo siri umeumbika sana ten asana, hebu angalia kama hizi hipspi zako zilivyo da wewe kweli mzuri,” Dullah alimwambia Fatu huku akiwa kaishika hipsi yake pana.

Ni kama vile Fatu alikuwa akisubiri Dullah alimchokoze, alimwambia asante ndipo naye akamsifia Dullah kwamba alikuwa handsome boy na alionekana alikuwa akiyajua mapenzi.

Kitendo cha Dullah kupewa fagio hilo, si akajivuta na kukugusana na Fatu kasha akamwomba dada huyo mfanyakazi wa serikali amsogezee shavu, alipolisogeza Dullah akambusu mmwaaa.

Busu hilo lilimshanganya Fatu, sin aye akajibu mashambulizi na kwenda mbele zaidi kwa kuutoa ulimi wake uliodakwa na Dullah kama vile kinyonga anavyodaka nzi aliyekatiza mbele yake.

Wawili hao walikula denda a.k.a mua mpaka macho yakawa mekundi si baadaye wakaanza kuleteana fujo za kugusana kila eneo linaloleta muwashawasha.

“My dear, inatosha naomba usimame,” Fatu alimwambia Dullah ambaye wakati huo pombe ilianza kumchemka kichwani.

Dullah aliposimama, Fatu alimkumbatia kama siyo ‘kumuagi’ akampiga mabusu kadhaa sijui alifanyaje bwana si ile kanga aliyovaa ikamfunguka na kubaki mweupe peee!

“Kumbe ndicho ulichokuwa ukikihitaji, ngoja nikupe mavituvitu ambayo tangu ulipoanza kujihusisha na zoezi hili la kiutu uzima hujawahi kukutana nayo,” Dullah alijisemea moyoni.

Kama kawaida yake, sharobaro huyo anapokutana na vitu hivyo adimu lazima ajilambe midomo, alifanya hivyo na kumeza mafunda mawili makubwa ya mate.

Alipofanya hivyo hakusubiri anyonyolewe manyoa na Fatu, alijivua viwalo vyake, si Fatu akaachia tabasamu pana nafikiri ni baada ya macho yake kutua kwenye makazi makuu ya Dullah .

Kama vile alikuwa akisubiri hatua hiyo, mtumishi huyo wa serikali ambaye hakuona kama aliutumia vibaya muda wa kazi na kwenda kujirusha na Dullah kwake, aliyavamia makazi ya Dullah na kucheza nayo alivyopenda.

Baada ya kuleteana fujo, Sharobaro Dullah alihisi kama angeendelea kumchelewesha Fatu huenda naye angepigiwa simu na bosi wake kama ilivyotokea kwa mama Maduu, si akamvuta na wote kuanguka puu juu ya sofa la watu watatu.

Kwa kuwa tayari joto liliwapanda sana, Dullah hakumuonea huruma Fatu hata kidogo, alimpa mambo ambayo dada huyo hakuwahi kukutana nayo akaishia kulia na kucheka kwa raha.

“Dullah , asante ndiyo maana nilipokuona tu siku ya kwanza nilikupenda na sikukosea hata kidogo, kwa jinsi ulivyonifikisha hakika utakuwa mtu wangu wa kudumu, nikuulize kitu?” Fatu alijikuta akifunguka mfululizo.

“Niulize tu mpenzi wangu!” Dullah alimwambia.

“Una mpenzi?” Fatu alimwuliza.

Kufuatia swali hilo Dullah alimdanganya kwamba alikuwa naye lakini waliachana kufuatia demu huyo kumsumbua mara kwa mara akitaka fedha wakati hakuwa nazo.

“Kama hivyo, itakuwa poa, kuhusu fedha sasa mimi ndiyo nitakuwa nakupa wewe na siyo fedha tu hata gari la kutembelea nitakupa, sawa mpenzi?” Fatu alimwambia Dullah .

Dullah alimshukuru sana Fatu na kumpagawisha kabisa, si akaanza kuzigusa tena zile sehemu zilizokuwa zikimletea mushawasha Fatu, dada wa watu akaanza kuweweseka.

Kama alivyofanya awali, alipomuona alikuwa yupo hoi, si akamvuatia kwake na kumpa tena mavitu matamu, Fatu akawa hoi.

Siku hiyo, wawili hao walishinda ndani wakipeana raha, kule ofisini mama Maduu alipotoka kazini alimpigia simu Dullah bila mafanikio na hata alipokwenda kumwuliza Ipyana alimwambia alipata dharura alirudi nyumbani.

Tangu siku hiyo Dullah akawa anatoka na mama Maduu, dada Fatu na mademu wake wengine akiwemo Doreen na Atu kwani hakuwa na tatizo la fedha.

Baada ya kupita muda mrefu, Dullah ambaye alikuwa gumzo mitaani kwa tabia yake ya ukware alianza kuugua na kukohoa kulikokwenda sambamba na kupungua mwili.

Kufuatia maradhi hayo yaliyokwenda sambamba na homa za mara kwa mara, mama yake alimpeleka kupima damu akabainika alikuwa ameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Alipoambiwa alikanyaga miwaya alipatwa na mshtuko, licha ya ushauri aliopewa wa namna ya kuishi kwa matumaini, Dullah alikata tamaa na usiku wa siku hiyo akajinyonga kwa kamba ya manila hadi kufa kwenye mti wa muarobaini.

Kulipokucha habari za kifo chake zilitapakaa kila kona ndipo baadhi ya watu ambao hawakumfahamu vizuri waliwauliza wengine ni Dullah yupi aliyefariki, wakajibiwa Dullah Sharobaro wa Tandale.

Kwa heri Dullah.

Kwa heri Abdallah.

‘Innalillah Wainailah rajjiunn’

Mugu ilaze roho ya marehemu Dullah mahali pema peponi….. Amina

Mwishoooooo!.

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment