Mzee wa Dodo Sehemu ya Tano
CHOMBEZO

Ep 05: Mzee wa Dodo

SIMULIZI Mzee wa Dodo
Mzee wa Dodo Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA: ALLY MBETU “DR AMBE”

*********************************************************************************

Chombezo: Mzee Wa Dodo

Sehemu ya Tano (5)

Alitaka kunyanyuka kitandani lakini aliona uvivu na kumuamsha mumewe ambaye alikuwa anakoroma, kitu ambacho hakikuwa kawaida yake.

“Baba Gift,..baba Gift,” Snura alimwita huku alimtikisa mumewe.

“Mmh!”

“Amka kuna mtu anagonga mlango.”

“Nenda kamsikilize,” Tumu alijibu bila kufumbua macho.

“Nimechoka sana mume wangu, dozi ya leo japo ilikuwa nyepesi lakini imenichosha sana.”

Tumu hakusema kitu alinyanyuka kitandani na kupitia taulo na kujifunga. Ndani hakuwa na kitu baada ya mbilingembilinge na mkewe.

Alitoka hadi mlangoni na kufungua kumsikiliza nani aliyekuwa akigonga usiku ule. Alipofungua mlango alishtuka kumuona Teddy kama mwanga. Wakati akishangaa macho yakiwa yamemtoka pima Teddy alipitisha mkono kwenye taulo na kumvuta nje.

Tumu hakuwa mbishi kwa kuhofia kubishana kungeweza kumuamsha mkewe na kujionea sinema ya bure ambayo ingekuwa na tafsiri mbaya.

Baada ya kusalimu amri Teddy alimvutie hadi sebuleni, bahati mbaya taulo baada ya kuvutwa sana ililegea na kufunguka mchungwa wa uani ukaoneka.

Mtoto wa kike hamu ya machungwa iliongezeka mate ya uchu yakamjaa mdomoni.

“Teddy vipi?” Tumu alimuuliza kwa sauti ya chini.

“Mwanao amekukumbuka kanianiasha usingizini.”

“Poa, nakuja.”

“Wapi?”

“Chumbani kwako.”

“Na mdogo wangu?”

“Basi bafuni.”

“Twende basi.”

Teddy alimshika mkono kuelekea bafuni.

“Teddy suburi.”

“Nini?”

“Nikamuangalie mama Gift.”

“Acha ujinga akikuzuia?”

“Hawezi.”

“Basi kwanza twende mara moja.”

“Je, akiamka?”

“Si juu yangu kwanza bafuni sitaki twende jikoni.”

Teddy alimshika mkono Tumu ambaye naye alikuwa hana kitu mwilini, wakawa kama wanga wawili waliokuwa wakielekea jikoni.

Baada ya kufika jikoni hakuna aliyesubiri kwani muziki ulikuwa umefika kwenye korasi wao waliingia kati kujimwaga. Waswahili wanasema sigara ya kuokota haiishi hamu na sinzia tamu kuliko lala, penzi lililo tawaliwa na wasiwasi lilinoga kweli.

Mchezo ulikuwa mtamu huku Tumu akiwa kama mnywaji wa kahawa kuungua vidole lakini kashata ikinogesha kahawa yenyewe. Kila siku Teddy alikuwa akimchanganya kwa ubunifu wake wa kuukwea mnazi wake.

Mtoto wa kike wazimu ulimpanda na kujisahau kama analipia debe bangi nje ya kituo cha polisi kwa kumsifia mkimbizaji japokuwa naye alitimua mbio kwelikweli.

Mtoto wa kike alijiachia bila kujua yupo sehemu isiyo salama na kuanza kunata na biti:

“Kanyaga mwanaume kanyaga twende sijawahi kusafiri safari kama hii, jamani kwa nini muda wa kuondoka sigara ndiyo inakuwa tamu hivi.”

“Teddy usipige kelele utamshika mkono kipofu,” Tumu alimtaadhalisha.

“Siwezi Tumu, siwezi baba Kijacho, nisiposema nitakufa kwa utamu, umezidi naupunguza kwa maneno, niache mpenzi wangu nijimwage.”

“Basi taratibu, punguza sauti mama Gift atasikia.”

“Tumu umeninusisha ugoro lazima nipige chafya na siku zote raha ya chafya iachie, niache niiache chafya ya utamu imenishika.”

“Tutashikwa Teddy.”

“Basi baba Kijacho, ona sasa kama hivi nitanyamazaje?” Teddy alilalama baada ya Tumu kupiga bomu nje ya ikulu.

Bila kujielewa Teddy raha zilizidi na kujiachia, aliteleza toka kwenye meza baada ya gari kukata bleki. Tumu aliwahi kumdaka kabla hajagusa chini, kama angechelewa angefikia tumbo na mambo kuwa mengine.

Baada ya kumlaza chini alishindwa amfanyaje kutokana na Teddy kuwa amelegea sana. Muda nao ulikuwa umekwenda sana. Alipojiangalia aligundua waliingia jikoni kama wanga bila nguo.

Alikimbilia sebuleni kuchukua taulo na kujifunga kisha alichukua khanga aliyodondosha Teddy wakati akimfuata chumbani.

“Teddy kalale chumbani.”

“Jamani baba Kijacho, niache nilale nimechoka.”

“Teddy dada yako akiamka na kukuta huku utamwambia nini?”

“Nitajua niache nilale nimechoka, nimeamini unampenda mwanao yaani katulia wakati baba yake akimkomaza,” Teddy alisema sauti ya kilevi.

“Sawa, basi amka ukalale chumbani.”

“Siwezi, niache nilale hapahapa mpenzi wangu.”

“Basi dada yako akikuuliza usinitaje?”

“Imeanza lini?”

“Mi’ naenda kulala.”

“Haya.”

Tumu aliondoka na kurudi chumbani kulala, alipofika kitandani alijitupa kama mzigo.


Snura alikuwa wa kwanza kuamka kwa vile siku ile alitaka kuwahi kazini. Hakutaka kumsumbua mtu alikwenda jikoni ili achemshe maji ya kuoga.

Alipofika alishangaa kumkuta Teddy amelala kwa kujikunja chini huku amejifunika kanga.

Alimtikisa bila kumwita kwa sauti, Teddy bila kujua nani anamwamsha alisema bila kufumbua macho.

“Baba Kijacho jamani niache nilale nimechoka.”

“Wee Teddy hebu acha kuota amka ukalale ndani.”

Kauli ile ilimshtua sana Teddy na kufumbua macho, alipomuona Snura alitahayali na kukapua macho kama mwanga.

“Snura mdogo wangu mimba yako inakupeleka kubaya, yaani utoke chumbani kuja kulala jikoni?” Snura alimuonea huruma bila kujua ubaya wa msichana wa kazi kwa mumewe.

“Dada hata sijielewi yaani nimejikuta nimekuja kulala jikoni.”

“Mimba yako inakupeleka vibaya.”

“Mmh! Wacha nikalale ndani.”

“Pole mdogo wangu.”

Teddy alinyanyuka na kwenda chumbani kwake kulala huku akijiuliza labda dada ameelewa mwenye ujauzito. Snura baada ya kuchemsha maji alikwenda kuoga na kurudi chumbani kwake.

Tumu ambaye muda wote hakuwa amelala alijifunika shuka ili kusubiri mkewe atarudi na kitu gani kuhusu Teddy. Snura alipoingia aliangua kicheko kilichomfanya Tumu ajifunue shuka na kuuliza.

“Vipi mbona unacheka?”

“Teddy mimba inampeleka vibaya.”

“Kwa nini?”

“Yaani ametoka chumbani kwake na kwenda kulala jikoni.”

“Jikoni?” alijfanya kushtuka.

“Yaani mimba mbona inamtesa mdogo wangu.”

“Ulipomuuliza amesemaje?”

“Ana la kujibu, amenichekesha aliposema baba Kijacho.”

“Eti?” Tumu alishtuka.

“Si nilimuamsha akasema eti baba Kijacho nimechoka niache nilale. Maskini kumbe alikuwa akimuota bwana yake. ”

“He! Ukamwambiaje?”

“Nimwambia aamke akalale ndani.”

“Mmh! Mimba inampeleka vibaya.”

Wakati huo Snura alikuwa akimaliza kuvaa nguo ili awahi kazini.

“Vipi mbona asubuhi?”

”Kuna kazi inabidi niwahi leo nakuacha.”

“Haya mke wangu kazi njema.”

“Na kwako mume wangu.”

Baada ya Snura kuondoka Tumu alishusha pumzi na kuamini muda si mrefu siri itakuwa nje. Alipanga kumshawishi Teddy aondoke siku inayofuata hata kwa kumuongezea fedha.

Baada ya mkewe kuondoka alimfuata Teddy na kutoka naye nje ili wazungumze bila mdogo wake kusikia. Walipofika nje walizunguka nyuma ya nyumba na kukaa kwenye sturi.

Teddy alionekana kama mtu aliyelewa kutokana na macho yake kuregea na kuzidi kumuweka katika wakati mgumu Tumu.

“Teddy,” alimwita kwa sauti ya chini.

“Abee baba Kijacho,” aliitikia huku akinyanyua macho yaliyochoka.

“Mbona upo hivyo kama umelewa?”

“Kwani hujui kilichonilewesha?” Teddy alimuuliza huku akiyalazimisha macho kumtazama Tumu vizuri.

“Ningejua nisingekuuliza.”

“Umenilewesha wewe na pombe uliyoninyesha jana usiku.”

“Pombe gani Teddy?” Tumu alishtuka.

“Eeh! Mpenzi pombe ya usiku, umesahau nimeninywesha chini nimelewa juu.”

“Mmh! Haya, sasa leo ndiyo umetaka kufanya nini?” Tumu aliuliza huku akimkazia macho kidogo.

“Mwenzangu! Kidogo nguo ya ndani inidondoke sokoni.”

“Teddy maneno kama Mzaramo?”

“Bwana wee, achana na hayo tuzungumze yetu.”

“Teddy fanya haraka ondoke mpenzi tutatia nzi kwenye togwa.”

“Yaani kilichotokea leo alfajiri, kesho safariiii.”

“Usiniambie!” Tumu alishtuka kwa furaha.

“Kweli kabisa.”

“Kwa furaha nakuongezea laki sasa hivi.”

“Wacha wee, unapeeenda haya mi naondoka chonde mdogo wangu kidole na macho, ukimgusa nyumba itakuwa ndogo kama kiberiti.”

“Siwezi kumgusa mpenzi,” Tumu alisema huku akichezea tumbo la Teddy.

“Mmh! Mtoto anataka kutoka kwa furaha naona anarukaruka.”

“Si kamsikia baba yake.”

“Nikwambie kitu?” Teddy alimwambia Tumu huku akitabasamu.

“Niambie mpenzi.”

“Nataka ukanipe tena muda huu kisha ndo basi tena mpaka kijacho aje duniani.”

“Jamani ya jana haijatosha?”

“Huku nako kunataka kama tumbo.”

“Mmh! Haya, na mdogo wako?”

“Anajua kila kitu.”

“Wewee!” Tumu alishtuka kwani alijua ilikuwa siri yao wawili.

“Ndiyo, kipi cha ajabu? Ndo maana nakwambia mheshimu mdogo wangu, muone kama muuza bangi na kituo cha polisi,” Teddy alizidi kutoa onyo.

“Sawa nimekuelewa.”

“Basi kanipe haki yangu.”

“Wapi?”

“Pa siku zote.”

“Mmh! Haya.”

Waliingia ndani kumalizia ungwe ya mwisho ambayo ingekuwa ya mwisho kwa Teddy mpaka atakapojifungua. Walipofika ndani Tumu alimpe fedha mdogowe Teddy na kumuomba akamtembeze Gift madukani wakanunue kitu chochote.

Baada ya kuondoka watu wakaingia kazini, hukuwepo shetani wako alikuwepo. Kila muziki ulipozimwa Teddy ndo kwanza alikuwa kama anaanza aliuwashwa tena.

Mtoto wa kike alitaka tui likamuliwe na kubakia jeupe lisilo na tui la nazi. Tumu naye alifanya hivyo. Mpaka wanaachana Teddy alikuwa hoi alijilaza kama amekufa. Tumu alimlaza vizuri na kumfunika kanga na yeye kwenda chumbani kujipumzisha ndipo aende kwenye mihangaiko yake kwani naye alikuwa hoi.


Baada ya mshikemshike uliomlaza hoi na kumfanya aamke jioni kama mtu aliyekuwa anaangusha mbuyu kwa wembe. Usiku Teddy aliaga rasmi kuondoka japokuwa Tumu alifurahi kuondoka kwake, lakini moyo ulimuuma kwani penzi la mwisho alilopewa siku ile lilimchanganya sana.

Alipanga siku mojamoja za mwisho wa wiki kwenda kumkomaza mtoto kwani Teddy mapenzi aliyajua. Alijilaumu kutomjua mapema kabla hajamuoa mkewe mama Gift bila hivyo basi Teddy angekuwa mkewe.

Kuondoka kwa Teddy, Snura alikuwa mtu aliyeumia sana. Lakini hakuwa na jinsi kwani hali aliyokuwa nayo hakuwa na sababu ya kumkataza kuondoka.

“Mdogo wangu Teddy ingekuwa amri yangu sikutaka uondoke kabisa, nilitaka ujifungulie hapa. Kwa vile umeamua wewe sina budi kukuruhusu ila nakuomba ujisikie huru kuja hapa ni kwenu,” Snura alisema kwa uchungu mpaka machozi yakamtoka bila kujua alikuwa akiliwa kisogo na beki tatu wake.

“Dada, najua kiasi gani unavyonipenda na kunijali, lakini hali hii sikupenda kuendelea kuwa mzigo. Kumbuka Gift anataka matunzo hivyo naamini itakuwa kazi kwa mdogo wangu.

“Kwa vile nakwenda kujifungua nitarudi na dhamila yako ya kunisomesha ipo palepale.”

“Sawa nimekuelewa mdogo wangu Mungu akutangulie kwa kila kitu na ujifungue salama atakapokwana usiogope kunijulisha.”

“Amina dada, hakuna tatizo.”

“Dada uende salama, nakuahidi kumlea Gift na familia yote kama wewe.” Tina alimuahidi dada yake kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa.

“Teddy shemeji yangu uende salama nami naungana na dada yako kukutakia safari njema pia kuwa na wewe siku zote. Kwa shukurani yangu ya kukaa nawe kwa wema nitakupa laki mbili za matumizi,” Tumu naye alitoa nasaha zake.

“Asante shemu.”

“Nami naongeza mbili,” Snura naye alimuongezea Teddy.

“Waaawooo, asanteni jamani.”

Baada ya mazungumzo Teddy alikwenda chumbani kulala kujiandaa na safari ya alfajiri. Kabla ya kulala aliendelea kumtaadhalisha mdogo wake.

“Tina mdogo wangu chondechonde usikubali kutembea na shemeji yako itakuwa aibu kwa familia, kupewa mimba na mwanaume mmoja kibaya bosi wetu haifai.”

“Sawa dada nitajitahidi.”

“Najua wewe binadamu kama utashikika baada ya ushawishi wa shemeji yako tumia kondomu usibebe mimba.”

“Dada nakuahidi hata busu lake silitaki.”

“Mmh! Haya lakini nina wasiwasi sana hasa huo umapepe wako wa kupenda kuacha matiti nje, basi huo ndio ugonjwa wa shemeji. Akiona dodo wenzio hoi yupo tayari akuhonge hata gari ili afaidi dodo.”

“Dada weee utasikia, akinilazimisha naacha kazi siwezi kujirahisi we wasi ondoa.”

“Mmh! Haya.”

Teddy kabla ya kulala alikusanya fedha zake zilikuwa zimafika milioni na ushee na kuamini maisha ya kijijini yatakuwa mazuri na mwanaye hatapata shida akijifungua.

Baada ya kuhesabu fedha alizochuma, kila mmoja alijilaza upande wake kuitafuta siku inayofuata.

Alfajiri ya siku ya pili Tumu na Snura walimsindikiza Teddy mpaka kituo cha basi. Walimkatia tiketi na kumpakia ndani ya gari.

Kabla ya kupanda ndani ya gari Snura aliitwa na mtu mmoja anayemfahamu aliyekuwa naye amemsindikiza mdogo wake lakini basi tofauti.

“Ha! Snura!” sauti ya mtu ilimshtua pembeni.

“Ha! Suzy vipi mbona huku?”

“Nipo na mdogo wangu ana kwenda mkoa.”

“Nani Mou?”

“Ndiyo.”

“Ooh! Yupo wapi shoga yangu,” alisema huku akimfuata.

“Jamani nakuja,” aliwaeleza Tumu na Teddy waliokuwa akisubiri kuingia ndani ya basi.

Snura alipozunguka gari tu, Teddy kwa haraka bila kuangalia watu waliokuwepo kituoni alimvuta Tumu na kumlisha mate kwa nguvu.

Tumu alijitahidi kujitoa lakini hakufanikiwa alikuwa mpole na kumpokea Teddy huku akijitahidi kujitoa. Aliachiwa baada ya dakika mbili.

Tumu pumzi zilimtoka kwa kasi huku akiangalia alipoelekea mkewe lakini alikuwa bado hajarudi.

“Muonee, woga wa nini hesabu zangu kubwa,” Teddy alisema huku akitabasamu.

Snura alirudi na kuwakuta wapo katika hali ya kawaida.

”Jamani samahanini,” Snura alijibalaguza.

“Hakuna tatizo dada wacha mi niingie ndani ya basi.”

“Haya mdogo wangu safari njema.”

“Asante dada,” Teddy alisema huku akimkumbatia Snura kisha Tumu.

Wakati wamekumbatiana na Snura,Teddy alimkonyeza Tumu aliyemuwa amesimama nyuma bila Snura kujua kinachoendelea.

Baada ya kupanda ndani ya gari, Tumu na Snura walipitia kazini.


Tumu alishukuru Teddy kuondoka bila ishu kubumburuka. Siri ilikuwa wazi kwa watu wote kasoro Snura ndiye hakujua ujauzito wa Teddy ni wa nani.

Baada ya muda taarifa zilitoka kijijini kuwa Teddy kajifungua salama mtoto wa kiume. Wote walifurahi kasoro Tumu ambaye alijiuliza siku Snura akimuona mtoto wa Teddy awe anafanana na Gift sijui itakuwaje.

Siku moja Snura alimwambia mumewe.

“Mume wangu wikiendi twende tukamuone Teddy kijijini tumpelekee na zawadi.”

“Mmh! Kwa nini tusimtume Tina ampelekee?”

“Tina akiondoka na Gift?”

“Si tutakuwa ofu.”

“Lakini tunatakiwa twende, kama wewe hutaki basi ni nakwenda kumuona Teddy na mwanaye.”

“Poa, mi nitakwenda siku nyingine.”

“Wiki hii ni muhimu si unajua nataka kwenda semina.”

“Sawa.”

Tumu alikubali lakini moyoni alikuwa na wasiwasi na sura ya mtoto. Taarifa za kidaku kutoka kijijini zilimkata maini baada ya kusema mtoto anafanana na Gitf kama kulwa na doto.

Tumu alijiuliza mkewe akienda hali ile ataipokeaje. Lakini hakuwa na jinsi, lakini alipanga kwenda kijini kabla ya mkewe ili kutafuta njia ya mkewe kutomuona mtoto.


Siku mbili kabla ya Snura kwenda kumuona mtoto kijijini, Tumu alikwenda kijijini kwa siri kutafuta njia ya mkewe kutoonana na Teddy. Siku hiyo aliaga anawahi katika kazi na kuondoka na basi la asubuhi bila mkewe kuwa na taarifa.

Alikwenda na kufikia sehemu kisha alimtuma mtu kwenda kumwita Teddy nyumbani kwao.

Teddy alielezwa kwa siri kuwa Tumu baba ya mtoto wake amekuja na anamwita. Japokuwa alitaka kuruka kwa furaha, lakini mpeleka habari alimwambia ule ni wito wa siri mtu yeyote asijue.

Alimchukua mwanaye na kumpeleka kwa baba yake, Tumu alifikia nyumba ya wageni . Teddy alipofika aliingia chumbani moja kwa moja.

Alipomuona Tumu alimrukia kwa furaha na kuanguka naye kitandani.

“Siamini baba Maneno kuja kumuona mwanao.”

“Mbona kawaida.”

“Yaani Maneno na Gift, Kulwa na Doto.”

“Hebu nimuone.”

Teddy alimuonesha mtoto ambaye hakuwa na tofauti na Gift alikuwa mdogo.

“Mungu wangu!” Tumu alishika mkono mdomoni.

“Vipi?” Teddy alimshangaa.

“Snura akimuona huyu mtoto kutakuwa na ndoa kweli?” Tumu aliingiwa na mchecheto.

“Itakuwepo huyu ni mtoto na ile ni ndoa,” Teddy alijibu kwa nyodo.

“Teddy acha utoto, nilikueleza utoe mimba ukakataa, huoni umenitafutia matatizo katika ndoa yangu?” Tumu alipagawa na sura ya mtoto.

“Tumu umekuja kunilaumu au kumtazama mtoto?” Teddy alikuwa mkali.

“Siyo kukulaumu bali kwa mtoto huyu ndoa yangu ipo mashakani.”

“Kwa hiyo umekuja kuua mwanangu?”

“Hapana.”

“Basi ondoka nisikuone tena wewe wala mkeo na mdogo wangu namuondoa ili tuwaache na ndoa yenu sitashindwa kumlea mwanangu,” Teddy alisema kwa hasira.

“Teddy usifike huko.”

“Ulipokuwa akikataa tusitumike mpira ulitegemea nini, naomba uondoke,”Teddy alizidi kumjia juu Tumu.

“Teddy hebu tulia nikueleze kilichonileta.”

“Si umeisha nieleza, tatizo nini?”

“Kuna vitu viwili vimenileta na tukikubalina nitakupa fedha nyingi.”

“Cha kwanza nimuue mtoto wangu, cha pili?”

“Sina maana hiyo.”

“Haya nieleze ulichonitolea nyumbani ningejua ujinga huu, nisingekuja.”

“Hapana Teddy nisikilize kilichonileta.”

“Haya nieleze.”

“Moja kuja kumuona mtoto na kumletea fedha za matumizi. Pili kukueleza kuwa Snura anataka kuja kumuona mtoto.”

“Kwa hiyo nifanyeje?”

“Hakikisha uonani naye, najua akimuona mtoto lazima atajua tumemla kisogo.”

“Sawa nimekuelewa, sasa nifanye nini ili asimuone mtoto na atakuja lini?”

“Kesho kutwa.”

“Duh! Sasa itakuwaje?”

“Nitakupa fedha uondoke hapa urudi baada ya wiki.”

“Sawa, wewe tu.”

Tumu alifurahi Teddy kumwelewa alitoa pochi na kutoa laki na matumizi ya mtoto na laki nyingine ya kuondoka kwao kwa muda.

Teddy aliipokea na kushukuru kisha alisema:

“Mtoto amepata mama je?”

“Si hiyo laki.”

“Kwa hiyo nisiondoke?”

“Basi nitakuongezea hamsini.”

Tumu alimuongezea Teddy elfu hamsini, baada ya kupokea na kushukuru na kusema tena:

“Vyote umefanya bado kimoja.”

“Kipi tena?”

“Siku nyingi sijapata.”

“Nini?”

“Kilichomleta Mwanao.”

“Siku nyingine leo nina haraka.”

“Tumu leo lazima unipe la sivyo siendi popote.”

“Tutambemenda mtoto.”

“Damu yako huwezi kuibemenda nipo hata za mkwezi.”

Tumu aliujua uking’ang’anizi wa Teddy hakuwa na sababu ya kumkatalia. Mtoto aliwekwa pembeni muziki ukaanza. Mtoto wa kike alikula kwa mikono miwili kutokana na hamu ya muhogo. Hukuwepo bali shetani wako alikuwepo. Kilio cha mtoto ndicho kilicho simamiza mpambano. Mwanzo Teddy alijifanya asikii kila alipoambiwa na Tumu.

“Teddy mbembeleze mtoto.”

“Mwache atanyamaza tu.”

Lakini kilio kiliongezeka na kusababisha mchezo kusimamishwa. Teddy alinyanyuka kwa hasira na kuona amemuharibia raha zake. Kama mtoto angekuwa mkubwa basi angemzaba vibao.

Alipitia kitenge na kujifunga chini, juu alijitanda khanga na kuacha gauni na kufuli na kumbeba mtoto begani. Tumu alijiuliza anakwenda wapi bila kusema kitu.

“Teddy wapi?”

“Nakuja.”

“Si tutoke wote.”

“Tumu utaniudhi, nampeleka mtoto nyumbani anaturushia stimu.”

“Kwa leo inatosha.”

“Weee! Yaani unipake upupu unikune kwa kulashia, mwenzio mambo ndo yanaanza.”

“Sasa mtoto unampeleka kwa nani?”

“Kwa bibi yake, umeisha muona wacha nije tule raha zetu kwa kujinafasi.”

“Teddy nataka kurudi mjini leo.”

“Basi niache niwahi.”

Teddy alisema huku akitoka bila kuchukua nguo zingine ili awahi kuutafuna muhugo alioukosa muda mrefu. Moyoni alijiapiza lazima atatumia kila njia kuhakikisha Tumu analala kijijini na kuondoka kesho yake

na gari la alfajiri.

Teddy baada ya kumfikisha mtoto nyumbani Teddy alirudi kumuwahi Tumu. Mtoto wa kike alikuwa ana ugwadu wa ajabu. Baada ya kuingia chumbani maandalizi yalikuwa madogo mchezo ukaingia hatua ya pili.

Kwa vile Tumu naye alilikosa penzi tamu la Teddy, kipindi cha pili kilikuwa piganikupige. Hukuwepo shetani wako alikuwepo, Teddy alimfanyia Tumu vitu adimu vilivyomrusha akili.

Teddy naye alichanganyikiwa na kusahau kama ana mtoto mdogo amemuacha nyumbani huku Tumu naye akisahau kuwa basi la mwisho limeondoka mpaka siku ya pili alfajiri.

Baada ya piganikupige wote walipitiwa usingizi mzito wa uchovu. Wa kwanza kuamka alikuwa Tumu ambaye alichukua simu na kuangalia muda.

Alishtuka kukuta muda umekwenda sana, alimshtua Teddy aliyekuwa bado amepitiwa usingizi.

“Teddy…Teddy.”

“Abee.”

“Muda umeenda nitapata gari kweli la kurudi mjini?” alimuuliza macho pima.

“Kwani sasa ni saa ngapi?”

“Saa kumi na mbili na robo.”

“Duh! Mungu mkubwa,” Teddy alishukuru.

“Kwa nini?”

“Leo nami nitalala na wewe mpaka kesho, haijawahi kutokea.”

“Teddy hebu acha utani nitamweleza nini mama Gift?”

“Tumu acha kuniangusha, wee mwanaume bhana.”

“Hata kama mwanaume nilitakiwa kuaga.”

“Huwezi kukosa cha kusema nakuamini baba Maneno,” Teddy alimpamba Tumu.

“Teddy acha utani hakuna usafiri mwingine zaidi ya basi?” Tumu aliuliza huku uso wake umemjaa hofu.

“Tumu suala la kuondoka leo sahau jipange kwa gari la kwanza kesho saa kumi na mbili alfajiri.”

Wakati wakibishana mlango uligongwa kwa nje kwa nguvu. Wote walishtuka ila Tumu ndiye aliyeshtuka zaidi.

“Teddy nani?”

“Nitajuaje na wote tumo ndani.”

“Nani?” Teddy aliuliza kwa sauti ya juu.

“Wee mshenzi tabia hiyo umeianza lini ya kufanya umalaya kumwacha mtoto nyumbani.

Huyu mtoto akiharibika nani atakaye laumiwa, kwa nini usirizike na mwanaume mmoja.

“Hivi baba Maneno atokee huyu mtoto utamlea mwenyewe, mbona we mwana unataka kunichumia janga nitembee barabarani nikisema peke yangu.”

“Mama unajua nipo na nani?”

“Nitajuaje na wewe unaanza umalaya.”

“Mama nipo na baba Maneno.”

“Kwa nini hajafika nyumbani?”

“Alisema akitoka hapa anakuja.”

“Muongo hebu atoke nimuone.”

“Mama sio vizuri kumufuata mkweo guest.”

“Mimi naondoka kama siyo baba Maneno utafute pa kwenda mi sifugi malaya.”

Baada ya kusema vile mama Teddy aliondoka na kuwaacha Teddy na Tumu chumbani.

“Mmh! Kweli mama yako mkali,” Tumu alimwambia Teddy.

“Ndiyo maana wanaye tuna heshima.”

Tumu akiwa amekaa alishtuka kitu na kumuuliza Teddy.

“Teddy tulitumia mpira?”

“Ili?”

“Si unajua mtoto bado mdogo unaweza kupata ujauzito mwingine.”

“Ukiingia utakuwa haujapotea.”

“Teddy mbona unapenda kurahisisha mambo!”

“Siyo mambo tumeisha pata mtoto si vibaya Maneno akipata mdogo wake.”

“Mama Gift ataniua.”

“Akuue kwa kipi, sote wanawake tofauti yetu yeye ana elimu na kazi nzuri, mimi Maimuna lakini pengine mahaba namzidi.”

“Teddy safari hii kama itaingia chondechonde itoe.”

“Kama huwezi kuitunza niachie mimi mwenyewe, Tena namuomba Mungu tulivyokutana leo nipate mtoto mwingine.”

Tumu alijikuta akichanganyikiwa baada ya kufanya uzembe mwingine wa kutembea na Teddy bila kinga. Lakini alijipa moyo na kuamini haiwezi kuingia.


Hakuwa na jinsi ilibidi aende ukweni kumuona mama mkwewe na usiku Teddy aling’ang’ania kwenda kulala na Tumu na kumwacha mwanaye na bibi yake.

Wakati wa chakula cha usiku Tumu alitaka kutumia kinga.

“Tumu ya nini mpenzi?”

“Naogopa kukupa ujauzito mwingine.”

“Kama kuingia umeisha ingia nipe raha kamili utamu thabiti.”

Tumu hakuwa na jinsi alimpatia Teddy kitu kamili.


Tumu baada ya kurudi na kutengeneza uongo kwa mkewe ambao ulikubalika. Muda wa mkewe kwenda kijijini ulikaribia na kujikuta akikosa amani ya moyo wake kwa kuhofia Teddy na wazazi wake wanaweza kufanya makosa yatakayo tia ufa kwenye ndoa yake. Akiwa amejilaza akiifikiria safari ya mkewe kwenda shamba baada ya kurudi kazini.

Ilikuwa ijumaa jioni ya siku ambayo ilibakia kesho yake ndiyo mkewe alipanga kwenda kumuona Maneno mtoto wa Teddy.

Snura alirudi jioni akiwa na zawadi za kumpelekea Teddy na mwanaye. Baada ya kutua mizigo alikwenda kukaa karibu ya mumewe aliyekuwa amezama kwenye dimbwi la mawazo.

“Dear mbona hivyo?” alimuuliza huku akimpapasa kifuani.

“Kwani vipi?”

“Nakuona upo mbali.”

“Maisha tu mke wangu.”

“Unawaza nini mume wangu Mungu kakujalia kazi nzuri pamoja na mimi mkeo, nyumba nzuri mke mzuri pia hata mtoto mzuri unawaza nini tena mume wangu?”

Snura alisema huku akimlalia mkewe na kumchezea ndevu chache.

“Mke wangu huu si muda wa kuridhika, matajiri hawaridhiki itakuwa sisi.”

“Lakini ndiyo uwaze kama huna kitu!”

“Vipi naona maandalizi ya safari?” Tumu aliuliza huku akiangalia mizigo ya zawadi.

“Niende wapi! Yaani mambo yameingiliana.”

“Kivipi?” Tumu alishtuka.

“Safari umekufa!” Snura alisema huku akimtazama mumewe kwa jicho la mahaba.

“Mbona sikuelewi, imekufa kivipi?”

“Si tulitakiwa tuondoke jumanne?”

“Ndiyo.”

“Basi safari jumatatu, hivyo tunatakiwa kesho twende kazini kuna maelezo kabla ya safari na jumapili itakuwa siku ya kujiandaa jumatatu safari.”

Kauli ile kidogo imfanye Tumu apige vigelegele vya furaha kwani muda wote alikuwa hana raha.

“Na hizi zawadi?” Tumu aliuliza swali la kujibaraguza.

“Itabidi Jumapili ushinde na Gift ili Diana ampelekee Teddy kijijini.”

“Hakuna tatizo.”

“Mume wangu usiku wa leo nina kazi na wewe nataka leo unikamue uzimalize za miezi mitatu nitakapokuwa mbali nawe.”

“Mke wangu unauliza makofi polisi?”

“Basi tukaoge tule, leo kitandani mapemaaa.”

“Wewe tu na roho yako.”

Furaha aliyokuwa nayo Tumu alihakikisha penzi atakalompa mkewe litakuwa ‘mwana ukome’ kuzikamua zote aondoke machicha ya nazi yenye tui ibakie meupe.

Usiku ulikuwa mtamu kwa wana ndoa kwa kila mmoja kujituma vilivyo ili kumfanya mwenzake aamini amepewa penzi lisilo changanywa na maji.

Kutokana na kutanange wa kufa mtu, Snura alichelewa kwenda kazini. Badala ya saa tatu asubuhi yeye alikwenda saa sita mchana. Tumu alipanga mpaka mkewe arudi toka kwenye semina atakuwa amemtafutia Teddy sehemu ya mbali ili mkewe asimuone mtoto.

Kutokwenda kwa Snura kumuona mtoto kumfanya Tumu kupumua na kujipanga kuhakikisha siri ile mkewe hajui.


Wiki moja baada ya Snura kwenda semina ya kikazi, Tumu alibakia na Diana mdogowe Teddy, kila alipokwenda kazini aliporudi alikula na kujifungia chumbani ili kuepuka tamaa ya macho.

Diana naye muda mwingi alishinda nyumbani na Gift, baada ya kazi alikuwa akiangalia mikanda ya video. Siku moja jioni baada ya kufanya kazi zote muhimu ikiwa pamoja na kuandaa chakula cha usiku.

Baada ya kuoga alikwenda kwenye mikanda ili kutafuta picha mpya. Katika kuchagua mkanda alipata mkanda wa picha za kikubwa bila kujua.

Mwanzo ilipoanza kwa watu kupigana mieleka alizima haraka na moyo kwenda mbio. Alinyanyuka na kusogea hadi dirishani kuangalia kama kuna mtu anachungulia.

Alikuta hali ya hewa ipo tulivu, alirudi kwenye kochi na kuwasha tena, mchezo uliendelea tena bado alikuwa na wasiwasi alinyanyuka na kwenda kuziba mapazia ya dirishani.

Alirudi na kuendelea kutazama kila dakika alijikuta yupo kwenye hali mbaya. Bila kujua aliondoa nguo mojamoja na kujikuta amebakia kama kuku aliyenyonyolewa manyoya.

Sauti za vilio vya ndani ya mchezo ndizo zilizomchanganya na kujikuta akijipapasa mwenyewe baada ya mashetani kumpanda taratibu.

Mkono mmoja ulikuwa kisimani na mwingine kwenye dodo na midomo aliinyonya, mtoto wa kike alikuwa kwenye hali mbaya alihitaji huduma ya haraka.

Siku hiyo Tumu naye alijikuta akiwahi nyumbani tofauti na siku zote, mpaka saa mbili kasoro usiku alikuwa ameishafika nyumbani. Alishangaa kukuta mlango umefungwa.

Aliposogea dirishani alisikia sauti ya watu wakila pilau. Alijikuta akipata wasiwasi wa Diana kuingiza mwanaume ndani. Alisogea hadi dirishani na kupiga chapo kwenye uwazi mdogo.

Macho yake kwanza yalitua kwenye screen ya tivii na kukuta picha inaendelea watu wakipigana mieleka ya kufa mtu. Alipopeleka macho kwenye kochi alimuona Diana akiwa hana kitu mwilini akiteseka na dunia.

Aliliangalia umbile changa kama lile ambalo lilikuwa halijatumika kama gari ilitumiwa kwa wiki na kuwekwa uani. Aliamini ilikuwa haijapata muendeshaji mzuri.

Kifuani dodo zilikuwa zimetulia huku Diana akizikanda kwa zamu. Midomoni alijinyonya kwa raha huku macho amefumba na kuendelea kupata sitimu kwa njia ya sauti.

Naye hakuwa na haraka alitulia ili apate burudani live bila chenga mambo ya digito hayo wee acha tu. Alijikuta naye hali ikibadilika na kuamini kilio cha wengi ni harusi.

Alikwenda hadi mlangoni na kusukuma mlango na kuukuta umerudishwa tu.

Kelele za watu kunogewa na utamu wa kutafuna mua zilizotoka kwenye video zilizidi kumchanganya Diana na kujikuta akijitandaza kama mtu aliye leba na kidole kikiwa kama kikibonyeza batani za kinanda kitu kilichomfanya azidi kusisimka na kuinyonya midomo yake kwa nguvu.

Tumu baada ya kuingia naye hali ilizidi kuwa mbaya, hata alivyovua nguo zake hakuelewa. Alijikuta katika ya mnazi huku akifurahia upepo ulivyokuwa ukiuyumbisha mnazi ule na kumfanya asahau kufa.

“Shemeji na mimi nataka mtoto kama dada!” Diana alilalamika baada ya kuweza kutawala dimba kubwa. Sauti ile ilimshtua Tumu aliyekuwa kama amepigwa bumbuwazi.

“Ha! Diana?” Tumu alishtuka huku akimshika Diana kifuani.

“Abe..be..ee,” Diana aliitikia kimawimbi huku akimiliki mpira na kutoa basi ya Tumu ya ushindwe mwenyewe.

“Di..di..di…,” Tumu gari lilimshinda na kujikuta likiseleleka bondeni kila alivyojitahidi kulizuia, tayari lilikuwa limeangukia juu ya banda la kuku na kuvunja yai moja.

Tumu akili za kawaida zilirudi na kujishtukia akiwa katika ya mnazi wa msichana wa kazi.

“Mungu wangu nimefanya nini?” Tumu alijilaumu kwa kitendo alichokitenda.

“Kwani shemu tatizo nini kiatu si kimenitosha we vaa tu?”

“Hapana Diana kosa nililofanya kwa dada yako sikutakiwa kulirudia.”

“Shemu kwani nani atajua, dada akirudi nauchuna.”

“Kwanza tumetumia kinga?” Tumu alijishtukia.

“Nikuulize wewe!” Diana alisema huku akimtazama kwa jicho niongeze hata moja.

“Mmh!” Tumu aliguna na kutembeza macho kuangaliana huenda akaona boksi la mwamvuli lakini halikuwepo.

“Diana una uwezo wa kuzaa?”

“Ndiyo shemu tena nitafurahi kuzaa na wewe yaani watoto wako wazuri kama nini.”

“Diana hayo maneno gani, akili zako za kitoto hizo. Mimi najiuliza mtoto wa dada yako nitawezaje kumficha na wewe unataka kunitafutia balaa.”

“Shemu mi siwezi kuwa mjinga kama dada, nikipata ujauzito naacha kazi unanipangia chumba changu.”

“Kweli wewe ndiyo hamnazo.”

Tumu alijikuta akijilaumu kwa kushindwa kuzuia tamaa zake za mwili. Alijiapiza siku ile iwe mwanzo na mwisho wa kutembea na Diana.

Alikwenda kuoga na kula kisha alijifungua chumbani hakutoka mpaka asubuhi wakati wa kwenda kazini. Diana kwa upande wake hakuamini kama mguu wa shemeji yake umetosha kwenye kiatu chake na kuweza kutembea bila tatizo.

Raha alizopata aliamini dada yake alifaidi na kujikuta akisema kwa sauti ya chini:

“Wacha dada azae naye shemeji mtamu bwana.”

Alijikuta akiyakumbuka maneno ya dada yake kuwa chondechonde asikubali kutembea na shemeji yake na akizidiwa basi asisahau kinga kwa ajili ya kujikinga na mimba.

“Aah! Kila mtu anataka raha, yake yameisha sasa zamu yangu.”

Kwa vile alikuwa amechoka hakuwa na haja hata ya kuoga, alijilaza usingizi haukuchelewa kumchukua.


Tumu toka siku ile akajitahidi kumkwepa Diana ikiwa pamoja na kugoma kula chakula chake kwa kisinzio cha kuchelewa kazini. Diana naye alijikuta akiteseka na kutamani tena kutembelewa kiatu chake kilichokuwa kipya.

Muda wa kurudi mkewe alirudisha ahueni kwa kujua Diana hatamsumbua tena. Snura alifurahi kukuta hali ya nyumba ipo vizuri huku afya ya mwanaye ikizidi kushamiri.

Alimletea zawadi nyingi Diana kwa kumtunzia mwanaye na nyumba yake. Tumu naye alionesha jinsi gani alipommis mkewe. Hali ya nyumba ilirudi kama kawaida huku Tumu akimaliza ugwadu kwa mkewe ili asipate tamaa za kijinga.


Kijiji hali ya kichefuchefu ilimshtua mama Teddy na kumuuliza mwanaye.

“We mwana vipi tena?”

“Hata mimi sijielewi.”

“Teddy mwanangu isiwe mimba?”

“Sijui mama.”

“Kama mimba mbona mwanao bado mdogo, halafu kwa nini uzae na wanaume tofauti.”

“Mama, baba wa Maneno ndiye baba ya kijacho kama yupo.”

“Muongo!”

“Kweli mama, kumbe siku ile nilipokutana naye labda mimba iliingia.”

“Yeye anajua?”

“Ajue wapi, mi mwenyewe nimeshtuka.”

“Sasa ikiwa mimba itakuwaje?”

“Safi tu wanangu watakuwa na baba mmoja.”

“Mwanangu, Maneno tu palikuwa kitimtim na huyu naye itakuwaje?”

“Mama kazi hiyo niachie mwenyewe wala isikupe presha.”

Wakati kijiji hali ya Teddy ikiwa tete mjini wakati wa chakula cha usiku Diana alisikia kichefuchefu cha ghafla kilicho mfanya atoke kwenye meza ya chakula na kukimbilia nje. Kitendo kile kiliwafanya Snura na Tumu watazamane.

“Nini?” Tumu aliuliza mkewe.

“Mmh! Isiwe mimba!”

“We! Temea chini!” Tumu alishtuka na kuomba kwa miungu yote ili isiwe kama mkewe alivyosema.

Snura baada ya kumuona Diana anachelewa kurudi alimfuata nje kumtazama. Alipofika nje alimkuta Diana amechuchumaa akitapika. Alisimama mpaka alipomaliza kutapika alinyanyuka na kujifuta mdomo na upande wa khanga.

“Diana, vipi mdogo wangu?”

“Hata sijui dada,” alijibu huku akijishika mdomoni.

“Kwani unajikiaje?”

“Yaani nimesikia kichefuchefu cha ghafla.”

“Kwani hali hii imeanza lini?”

“Sasa hivi.”

“Pole mdogo wangu kama itazidi nitakupeleka hospitali.”


Jioni Snura na mumewe waliporudi walimuuliza hali yake inavyoendelea, Aliwaeleza kuwa hali ya kuchukia chakula na kutapika iliendelea. Baada ya kuoga na kubadili nguo alimpeleka hospitali na kumwacha Tumu nyumbani na mtoto.

Majibu ya vipimo yalimshtua Snura baada ya Diana kuonekana mjamzito. Ilikuwa tofauti na dada yake Teddy ambaye alishtuka na kuangua kilio. Lakini kwa Diana kwake lilikuwa jambo la kawaida. Snura kwake aliona ni mikosi kwa wasichana wake wa kazi wakitulia tu watu wanawajaza mimba.

Baada ya Snura na Diana kupata majibu walirudi nyumbani, walipofika Tumu alikuwa na shauku ya kutaka kujua nini kimejili hospitali.

Alimuacha kwanza Diana aende chumbani kwake ndipo alipomuuliza mkewe.

“Vipi mke wangu za huko?”

“Mmh! Majanga,” alisema huku akijitupa kwenye kochi na kushusha pumzi ndefu.

“Nini tena?” Tumu aliuliza huku akimtazama usoni mkewe.

“Yaleyale,” Snura alisema huku akijiweka vizuri kwenye kochi.

“Una maanisha nini?”

“Nakwambia! Mbona majanga hii si bure kuna mkono wa mtu.”

“Eti?” Kauli ile ilimshtua sana Tumu na kumtolea macho mkewe.

“Kwani Diana amekwambia ujauzito wa nani?”

“Hata nilikuwa na nguvu za kumuuliza baada ya majibu kusema Diana mjamzito.”

“Mmh!”

“Mume wangu haiwezekani wasichana wangu wote wa kazi ndiyo kila siku wapewa ujauzito. Kwa mama Mariamu msichana wa kazi ana muda gani, wa kwangu ndiyo wamewaona watamu.”

“Inawezekana hata wa mama Mariamu msichana wake anapata ujauzito huenda ni fundi wa kutoa.”

“Mume wangu simshauri msichana yeyote kutoa mimba, tulimpoteza mfanyakazi mwenzetu mwaka jana kwa kutoa mimba.”

“Mmh! Kwa hiyo umemuacha tu bila kumuuliza?” Tumu alijibalaguza.

“Hata nina nguvu za kumuuliza, ajabu majibu wala hayakumshtua kama dada yake.”

“Inawezekana ameisha wahi kujifungua hivyo haoni kitu kigeni kwake.”

“Mmh, Bado! Kimuonekano haoneshi.”

“Sasa tutafanyaje?”

“Huyu akiondoka safari hii Gift namrudisha kwa bibi yake tumuone huyo mtia mimba atamtia nani?”

“Mmh! Kweli kazi ipo.”

Tumu alijikuta mtu mwenye wasiwasi mwingi kutokana na taarifa za ujauzito ule. Alijiuliza kama ni wake atambebea mbereko gani mkewe kama akijua na mtoto wa Teddy ni wake. Aliendelea kuomba miungu yote ujauzito ule usiwe wake.

MWISHO

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment