Haa! Kumbe Tamu Sehemu ya Tano
CHOMBEZO

Ep 05: Haa! Kumbe Tamu

SIMULIZI Haa Kumbe Tamu
Haa! Kumbe Tamu Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA: FRANK MASAI

*********************************************************************************

Chombezo: Haa! Kumbe Tamu

Sehemu ya Tano (5)

“Oya tuna kazi nyingi bwana. Tuchape mzigo, tulele mbele. Hayo mawaidha yako, kawape wachezaji wa Aseno.” Aliongea jamaa mmoja huku akianza kufungua mkanda wa suruali yake.

“Jamani naomba msinibakee.” Subira aliongea kwa sauti ya unyonge huku machozi yakianza kama kumlenga-lenga.

“Jamani msinibakee, nyooo.” Makasi ambaye alikuwa kakamata kamera aliongea huku kabana pua yake kwa kidole cha shahada. “Nani kakakwambia unabakwa? Sisi hata hatuna tabia hiyo. Cha msingi ukitakata tusitumie nguvu, sikiliza tutakachokwambia.”Makasi akampa rai kimwana yule.

“Nawaombeni jamani mnisamehe, Mimi siwezi.” Subira aliongea huku akitoa machozi na kuwafanya wanaume wale watulie kwa muda huku roho zikiwasuta kwa kitu wanachotaka kukifanya.

Yaani kuletewa nyodo tu! Ndio walipe kisasi? Je, Watalipa visasi kwa wanawake wangapi? Na je dunia nzima ingekuwa ina-nyodo kama za mwanadada yule, unadhani UKIMWI na ubakaji vingeisha?. Sasa kwa nini wao wanataka kulipa ujinga kwa ujinga? Ni kwa nini?

Walijiuliza mara mbili-mbili lakini hawakupata jibu na hata yule ambaye alikuwa kaanza ufungua suruali yake, alianza kuifunga taratibu. Aliona wazi kabisa kuwa lile chozi la binti yule litamtafuna kama akiamua kufanya ujinga ule.

Ni dhambi ambayo ingempeleka motoni bila hata kuuliza. Na hakika ilikuwa ni dhambi.

Baada ya kimya kifupi huku kimya hicho kikimezwa na mafua ya Subira, ndipo uamuzi ulipita ni lazima Subira alipe gharama walizogharamikia lakini si kwa kufanya naye mapenzi bali kumpiga picha akiwa uchi.

Adhabu hiyo ilienda sanjari na kupiga picha na mwanaume. Picha zikawa picha katika chumba kile. Alipoambiwa rembua, alirembua na picha kupigwa. Mara aliambiwa shika kipaza sauti, naye alitii kwa kuwa kisu na fimbo vilikuwepo kama atakaidi hayo yote.

Hatimaye zoezi likaisha na cha mwisho alichoonywa ni kuacha pozi na kejeri. Endapo atafanya hivyo, zile picha zitazagaa chunya yote ile. Mwanamke akaishiwa pozi kabisa, uso ukamshuka kama mtoto aliyekamatwa anadokoa nyama jikoni.

Hakuna aliyejua mkasa uliompata Subira, iwe shuleni kwao , nyumbani au mtaani. Waliojua ni wachache ambao walikuwa eneo la tukio. Licha ya wao kujua, lakini walikuwa hawana vithibitisho. Ni Makasi pekee ndiye alikuwa anavithibitisho vya Subira kupiga picha za uchi pamoja na wanaume.

Kwa upande wa Subira, hakika pozi zilimuisha. Akawa si yule wa tena nyodo. Taarifa zilizagaa haraka kwa yale mabadiliko. Vijana wengi walihoji kwa nini kawa vile, jibu walilopata lilikuwa ni kwa sababu sasa anataka mume. Na pia vijana wengi walipata na njia za kumuingia, hapo ndipo walipata wasaa wa kuchezea mwili wa kimwana yule.

Wengi walipomtongoza, walikuwa wanasumbuka mara ya kwanza, lakini pale waliposema watasambaza picha zake, Subira alikuwa mpole kama barafu. Japo hata huyo aliyesema atasambaza picha zake alikuwa hana wala hajui ni picha gani, lakini Subira alimpa nafasi ili tu! Asisambaziwe hizo picha.

Subira akawa branketi la wanaume kipindi kile cha baridi. Pale alipotongozwa akawa hana jinsi. Na kuna wengine wakawa hawamtongozi bali kumvuta mkono na kumshikisha mahala, hata kwenye mti. Hapo-hapo mambo yanamalizwa.

Hali hiyo ikaendelea na ikakua zaidi ya mwanzo. Hadi nyumbani kwao wakafahamu tabia chafu azifanyazo mwana-wao. Baba akasema sana, na Subira alilia sana kwa anachofanyiwa na wanaume, lakini haikuwa mwisho wa hayo.

Baba hakutaka kumuhamisha Mkoa wala Wilaya, alitaka aone mwisho wa mwanaye ni nini. Na mwisho ulikuwa ni mbaya sana kwa kimwana yule.

Taratibu nahudhurio darasani yakaanza kupungua, kutokana na wanafunzi wenzake hasa wa kiume kushtukia kuwa ni mama huruma. Nao wakawa wanajilia tu, muda wowote na mahala popote.

Miezi sita ikakata. Mitihani ya ‘Mock’ ikaja. Mwenzake Mercy akafanya vizuri sana, lakini yeye alianguka vibaya. Mercy akawa mtu wa kumfariji kwa yaliyomkuta, hapo ndipo Subira alianza kujutia tabia zake za mapozi. Akamuelezea Mercy mambo yote ambayo yalimtokea. Mercy akawa mtu wa kusikitika.

Subira hakupenda tabia ya kuvutwa na kila mwanaume. Lakini atafanya nini na kama akiwakatalia, picha zake za utupu alizopigwa na wanaume wanne tofauti, na nyingine akionekana yupo na wanaume hao wote amewashikilia maumbile yao kwa mikono pamoja na mdomo wake, zitasambazwa na kuwafikia wazazi na ndugu zake ambao ndio msaada mkubwa katika maisha yake.

Akijidai mjanja, picha zinafika huko. Na hapo elimu na kukaa nyumbani kwa wazazi wake kutakuwa ndio mwisho. Sasa atafanyake, ikambidi awe anawapa kile roho zao zinataka. Na MUNGU alikuwa upande wake, hadi anamaliza kidato cha sita hakuwa kapata mimba wala magonjwa ya maambukizi kwa kupitia ngono.

Maisha kwa upande wa Mercy na Longino, yalikuwa ni furaha sana tena sana. Longino alikuwa kafanikiwa sana katika uchezaji wake mpira. Akasajiliwa na timu ya Mbeya City. Akalipwa fedha nzuri sana na akawa-tegemeo la timu ile. Hakika aliukata, Mercy akawa kama Malaika, atake nini asipate?

Jesca na mama yake, wakawa si watu wa kuhangaika sana katika maisha yao. Wakawa si wale wa kuamka asubuhi na mapema kwenda kutafuta chakula. Mama Longino akapiga magoti na kumshukuru MUNGU kwa kumpa kipaji mwanaye.

Hata matokeo ya kidato cha sita yalipotoka, Mercy alikuwa amefaulu vizuri sana kuliko Subira. Mercy alipata daraja la pili na mwenzake Subira alipata daraja la tatu ya mwisho. Hivyo Subira matumaini ya kuendelea kusoma yakamuisha kabisa.

Lakini sababu kubwa ya yeye kufeli ilikuwa ni nini? Ilikuwa ni msongo wa mawazo uliosababishwa na zile picha alizopigwa na wakina Makasi. Msongo huo ulimtafuna mwili hadi ubongo. Subira sasa akawa amefeli kidato cha sita.Hakuwa na nafasi ya kuendelea kusoma chuo na hata nyumbani kwao alionekana si kitu licha ya kupewa kila kitu pamoja na kuthaminiwa kama mtoto pekee aliyesoma zaidi ya wengine.

Hali ya Subira ikawa mbaya zaidi pale wazazi wake walipogundua kuwa alipigwa picha za utupu na ndio sababu ya yeye kufeli. Wakakata huduma muhimu za mwadada yule. Akawa haeleweki eleweki. Vile vito vya gharama alivyokuwa akivaa, vikaanza kutitia taratibu kwa kuwa alihitaji fedha za kujikimu. Aliuza vito vyake karibu vingi sana.

Hali ikazidi kuwa ngumu pale Mercy alipoenda Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Augustino. Hakuwa na mshauri tena. Ikabidi abadili maisha yake. Kilekile kilichomuharibia masomo, ndicho aliona kinafaa kumuendeshea maisha yake.

Subira akaamua kujiuza mwili wake ili apate kipate cha kununua ‘vijiurembo’ vya kuendelea kuupamba mwili wake. Alianza kwa siri-siri lakini baada ya kupata fedha kwa kutumia kazi hiyo, akaona bora aweke hadharani mambo yake.

Tabia hiyo ikawakera wazazi wake mara kumi zaidi ya mwanzo. Wakaamua kumtimua pale nyumbani alipokuwa anaishi nao. Wakamwambia aende aonapo panafaa kufanyia kazi ile.

Hakuna aliyechukua jukumu la kumuonesha njia na kumjenga mwanadada huyu. Wazazi wake hawakupaswa kufanya kile walichokifanya. Wao kama wazazi, walitakiwa kutuliza hasia zao na kumuuliza kwa nini kaamua kufanya vile. Kama sababu ni fedha, basi wao walipaswa kutambua wamesababisha huyu binti azitafute fedha hizo kwa njia aionayo yeye.

Kwa sababu gani nasema hivyo? Ni kwa sababu wao hapo mwanzo ndio walikuwa wanampa na kumzoesha maisha ya kujipamba kwa vito vya gharama. Hivyo kama atavikosa vito hivyo katika wakati, basi ni lazima mwana wao atatafuta njia ya kupata vito hivyo pamoja na fedha.

Marafiki ambao aliwapata Subira, wakawa si marafiki wa kutembea nao hata kidogo. Walikuwa ni marafiki wa ajabu kupata kutokea katika maisha ya kawaida ya mwanadamu.

Wakazidi kujichimbia hapo Chunya huku biashara yao ikiwa inaenda vizuri kabisa. Na ni kweli walikuwa wanasoko zuri sana.

Pale walipoona pale Chunya wamechokwa, wakaingia mjini. Huko sasa kama pesa zilikuwa matunda, basi walivuna kama njugu au karanga Dodoma. Hakika walizivuna, na walivuna hasa. Hawakujua kuwa hayo yote yanamwisho na pamoja na kuwa na mwisho, yalikuwa yana ubaya wake pia. Hawakujua hilo hadi pale yalipowakuta yaliyopaswa kuwakuta.

Baada ya mwaka mmoja kupita. Wakati Mercy akizidi kukata mbuga kwa mafanikio makubwa katika masomo yake, Longino akawa anazidi kucheka kwa mafanikio ambayo alikuwa anayapata.

Timu kibao zilikuwa zinamuhitaji kufanya naye kazi. Lakini alichagua timu moja tu ya kufanya nayo kazi. Alisajiliwa na Azam FC, timu inayosemekana ina fedha nyingi kwa hapa Tanzania.

Wakamtoa kabisa na Mbeya kwa kumuhamishia Dar Es Salaam. Mama alikataa kuhama pale Mbeya kwa kuwa kiwanja na nyumba yao, vilikuwa mali ya mume wake. Hakupaswa kuviuza wala kuviacha. Alichomuomba Longino ni kumuachia pia mtoto wake Jesca akae-naye kwa kuwa akiondoka na huyo, yeye atabaki mpweke.

Longino alimuelewa mama yake vya kutosha na alipafanya pale nyumbani kwao paoekane ni nyumbani kwa mchezaji mwenye sifa za kuitwa mchezaji. Akaparemba na kupawekea kila kitu kinachoenda kwa wakati.

Akaenda kuanza maisha mapya Dar es Salaam. Huko akapangiwa nyumba ya maana na kulipiwa kila kitu kilichomuhimu kwa kila nyumba ya nyota kama yeye.

Mercy naye hakuwa nyuma kwenda kumtembelea mpenzi wake. Na kila walipokutana walikuwa ni kuifurahisha miili yao kadiri walivyoona ni sawa.

Mwaka wa pili ukaingia. Mafanikio kwa Longino yakazidi kuwa makubwa na kumfanya aanze kuandaa maisha yake kwa kununua viwanja Mbeya na Dar es Salaam. Cha Mbeya alianza kufanya ujenzi mara moja. Huku cha Dar akikiweka kama dharura tu.

Kwa upande wa Subira, naye biashara ilinoga zaidi pale alipoamua kuhamia Dar es Salaam. Na kweli alizidi kuwa mwanamke mrembo. Zile kemikali alizokuwa anazitumia, ukichanganya na joto la Sinza alipoweka makazi yake, nani angemjua kuwa katoka Mbeya? Mtoto akawa mzungu wa Kinyakyusa.

Huko Dar akawa ni mtu wa kulala na watu wenye fedha zao. Fedha za kuweza kuhamisha hata baridi ya Mbeya na kuileta Dar es Salaam, hao ndio Subira alikuwa anawahitaji. Na aliwapata vya kutosha, lakini mwisho wake ulikuwa ni kuambulia magonjwa. Magonjwa ya hatari kabisa, ambayo baadhi yalipona na mengine yalikuwa sugu kwake, hayakuweza kupona. Subira aliunasa ugonjwa wa UKIMWI. Ugonjwa ambao hadi sasa hivi unasemekana ni laana ya Mwenyezi MUNGU kwa wanzinzi.

Subira akanyakua gonjwa hilo. Na yeye alipogundua kalikwaa gonjwa hilo, akaamua kuwapa wale waroho wa wanawake. Akawaambukiza vijana na wazee, huku akizidi kuchukua fedha zao kama zake.

Mwaka wa tatu ulipoingia. Mercy akiwa hajui maisha ya rafiki yake, akakamata mimba. Mimba ambayo walipanga wawili iingie katika maisha yao. Longino akawa mtu wa furaha kuliko maisha yake yote. Mara moja akaona huo ndio muda muafaka wa kufunga ndoa na mwanamke aliyempenda, mwanamke wa maisha yake.

Baada ya miezi mitatu tangu mimba ile iingie kwa Mercy, Longino akatuma Washenga ambao walipeleka taarifa za kuomba ndoa nyumbani kwa akina Mercy. Wazazi walikuwa hawana kipingamizi hasa ukizingatia Mercy alishakuwa mtu mzima na kama shule alibakiza miezi michache kuimaliza.Hivyo walimpangia Longino mahari ya kulipa, naye Longino akafanya hivyo haraka iwezekanavyo.

Mimba ya Mercy ikiwa tayari imeonekana. Akarudi nyumbani kwa ajili ya kujiandaa na ndoa. Ndoa ambayo hawakupenda iwe kubwa kama ni ndoa ya wasanii wakubwa wa Marekani.

Mercy akafika Chunya na familia yake ilifurahi sana kumuona. Na hakika alizidi kupendeza. Na hata Longino naye aliporudi Chunya, alipokelewa kwa furaha sana na familia yake.

Jioni moja, Mercy na Longino, walipata ujumbe kuwa wanaitwa na Subira. Kwa kuwa walikuwa wamemsahau kabisa, iliwabidi wamnunulie vitu vidogo-vidogo kama zawadi kwake.

Walifika nyumbani kwa akina Subira na moja kwa moja walikaribishwa katika chumba kimoja kipana sana. Lakini walipoingia, hawakuamini macho yao kwa kile walichokuwa wanakiona katika kitanda kilichokuwamo mle ndani.

Alikuwa ni Subira, uso wake uliokuwa umekuburiwa na kemikali, ulijaa madoa-doa meusi ambayo yalikuwa hayana idadi. Alionekana kama mgonjwa wa ‘black spot’, ugonjwa uliowavamia Waafrika kipindi fulani cha Ukoloni. Walikuwa wanakumbwa na madoa mwili mzima, na ndivyo Subira alionekana hivyo.

Licha ya kuonekana na madoa hayo, pia binti yule alikuwa kaisha. Amekonda, kabakiwa fuvu pekee. Hakika aliyekuwa anamuona kwa mara ya kwanza, hakusita kudondosha machozi kwa ule mwili ulivyokuwa umekwisha.

“Vipi Subira? Mbona hivi rafiki yangu?” Mercy aliongea kwa uchungu huku akifuta machozi yaliyokuwa yanamtiririka. Na wakati huo alipiga magoti karibu na kitanda alichokuwa kalala rafiki yake kipenzi.

“UKIMWI Mercy, UKIMWI unanichukua mimi.” Subira aliongea kwa shida huku kikohozi kikifuata baada ya maneno hayo. Alipotema makohozi hayo yalikuwa yamechanganyika na usaha pamoja na damu.

Muda wote Longino alikuwa kasimama huku kaduwaa. Alikuwa haamini kama yule aliyekuwa pale kitandani alikuwa ni yule mwanadada maarufu kwa nyodo, ‘BLACK BEAUTY’ wa mtaa,. Longino chozi likamtoka bila kujitambua. Na hapo ndipo aligundua bado anampenda sana yule mwanamke.

“Longino samahani sana kaka yangu. Sikujua kama una-upendo wa kweli namna hii. Kweli una-upendo sana wewe mwanaume, natamani mimi ndiye ningekuwa Mercy sasa hivi.” Subira alizidi kuyatoa maneno hayo kwa shida.

Longino alisogea pale alipo Subira, naye akapiga magoti kama alivyofanya Mercy.

“Wewe ndiye mwanamke niliyekupenda Suby. Na bado nakupenda sana tena sana, naomba utambue hilo. Na uwepo wa Mercy katika maisha yangu, ni sawa na uwepo wako. Nawapenda sana, naomba mtambue hilo pia.” Longino aliongea kwa hisia kisha akainuka kidogo na kubusu paji la uso la kimwana yule ambaye sasa kabaki fuvu.

Busu lile lilimfanya Subira achanue tabasamu la haja kisha akamgeukia Mercy na kumtania.

“HAA! KUMBE TAMU.”Alitania huku akimwangalia Mercy.

“Tamu nini sasa.” Naye Mercy alimuuliza huku akijibu pigo la tabasamu hilo.

“Busu la ‘player’.” Subira alijibu kwa mapozi na kusababisha kila mmoja mle ndani atamani mtu yule apone mara moja. “Na mtoto wako najua ni wa kike, naomba umuite jina langu tafadhali japo ni la Kiislamu.” Aliongeza Subira.

“Usijali ‘best’ limepita hilo.” Mercy alijibu huku akimfuta jasho lililokuwa linamtoka Subira kwenye paji la uso wake.

“Long nibusu tena basi.”Subira aliomba busu lingine kwa Longino na Longino bila kusita alifanya hivyo na kuzidisha tabasamu la Subira.

“HAA! KUMBE TAMU.” Subira alitamka tena maneno hayo. “HAA! KUMBE TAMU, kumbe tamu sana, ni tamu sana.” Alizidi kuongea huku sauti yake ikizidi kufifia. “Kumbe tamuuuu.” Ni kauli ya mwisho ilitoka Subira na hapohapo umauti ukamchukua.

Subira akaaga dunia baada ya ugonjwa wa UKIMWI kumtafuna sana mwili wake. Hakufata ushauri nasaha ambao daktari alimpa baada ya kugundundua kaathirika. Yeye aliona njia bora ni kuusambaza ugonjwa ule kwa wengine, na kweli alifanikiwa kwa hilo. Hakufa peke yake.

Lakini kuathirika na virusi vya UKIMWI haimaanishi kuwa ndio kifo chako kimefika. Kama ukifata ushauri wa Daktari na washauri nasaha mbalimbali, basi utaishi muda mrefu.

Ni wakati wa Watanzania pamoja na bara la Afrika kiujumla kuamka na kutambua kuwa UKIMWI si kifo, bali ni gonjwa kama magonjwa mengine, japo lenyewe halitibiki. Elimu kubwa yapaswa kutolewa kwa vijana pamoja na wazazi ambao ndio nguzo kubwa ya vijana hawa.

Enyi wazazi, tuangalie zaidi maisha ya mbele ya vijana hawa. Jukumu la kuwafukuza majumbani kwenu kisa kabadilika tabia, si jukumu lililo sahihi. Kaa na mwanao na kisha mpe ushauri uliobora. Mfanye ajihisi kuwa yeye ni mwana-wako. Kufeli shule si kufeli maisha, mpe nguzo imara ambayo itamfanya asimame mwenyewe siku moja.

Na nyie vijana muangalie matendo yenu, yanawaumiza wazazi wenu sana. Visasi visivyo na msingi ndivyo hivyo vinazidi kuua mamia ya vijana duniani. Hamna haja ya kulipa kisasi kwa mwanamke au mwanaume aliyekukataa. Wala hakuna haja ya kulipa kisasi kwa wale waliokupa magonjwa.

Ukipata UKIMWI,ishi kwa matumaini. Ishi kwa kutegemea ushauri nasaha. PINGA VISASI, ILI UTOKOMEZE JANGA HILI.

“PINGA VISASI, ILI KUTOKOMEZA UKIMWI.” Ndivyo fulana zilivyoandikwa kwenye maziko ya Subira. Wahudhuriaji walikuwa ni vijana na somo kubwa lilitolewa kwenda kwao. Somo kuhusu UKIMWI na visasi vinavyotokea baada ya mtu kujingundua kaathirika.

Hakuna ajuaye kesho. Leo ni Subira yamemkuta, na kesho yaweza kuwa wewe, mimi au yule. Kizazi chetu kinaangamia kwa gonjwa hili. Yatupasa tusimame imara kupinga na kuelimisha juu ya UKIMWI.

Harusi ya Mercy na Longino ilifuata baada ya mwezi mmoja. Na kila mmoja alifurahia tendo hilo. Kule chuoni, Mercy ilibidi aahirishe mitihani ya kumaliza chuo (Post-Pone) aje kuifanya baadaye mwakani. Barua ikapita kwa Mkuu wa Chuo.

Baada ya miezi kadhaa ndani ya ndoa, kweli Mercy akajifungua mtoto wa kike ambaye bila kuchelewa alimuita jina la Subira, rafiki yake kipenzi wa Sekondari. Hata mtoto alipopewa jina hilo, aliweka vidole vyake mdomoni na kuanza kuvinyonya huku miguu yake ikicheza kwa furaha.

Hakika Subira alikuja katika mwili mwingine. Furaha mpya ikatawala katika maisha ya Longino na Mercy. Yule mwanamke waliyempenda, sasa alirudi kwa njia nyingine.

HUJUI KUHUSU MAISHA YAKO YA MBELE, HESHIMU KILA MMOJA AMBAYE UNAMUONA.

MWISHO.

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment