Usiku wa kigodoro Sehemu ya Kwanza
CHOMBEZO

Ep 01: Usiku wa kigodoro

SIMULIZI Usiku wa kigodoro
Usiku wa kigodoro Sehemu ya Kwanza

IMEANDIKWA NA: GLOBAL PUBLISHERS

*********************************************************************************

Chombezo: Usiku Wa Kigodoro

Sehemu ya Kwanza (1)

“UKO wapi Lina?”

“Kwa dada, ndiyo tunataka kutoka kwenda saluni my dear.”

“Lina usinitibue, kwa dada saa hizi wakati unajua kanisani tunatakiwa saa nane kamili mchana, sasa uende saluni saa sita hii utamaliza muda gani? Kanisani utakuja saa ngapi na ndoa itafungwa saa ngapi au hutaki tufunge ndoa Lina?”

“Nitamaliza mapema tu.”

Mara Lina akakata simu…

“Khaa! Yaani Lina kanikatia simu mimi? Ana maana gani?” alijiuliza James. Alipopiga tena iliita bila kupokelewa…

“Afadhali isingepatikana ningesema chaji imeisha, sasa hapokei ina maana gani?” James aliendelea kuwaza…

“Lakini hili suala la Lina kutopokea simu au kukata litaisha lini? Maana ni kawaida yake. Tunaweza kuongea akakata au akawa hapokei. Huyo dada yake anayesema ni mkali sana, ukali wake ni kama wa simba? Afadhali tufunge hiyo ndoa ili aondoke kwa dada yake tuone.”


“Lina ulikuwa ukiongea na nani kwenye simu?” Semi, mume wa Lina alimuuliza baada ya kumsikia akisema anajiandaa kwenda saluni na yupo kwa dada yake tena akaita my dear…

“Ni yule rafiki yangu, Agnes anataka nimpeleke kwenye bethidei, mimi sitaki. Sasa nimemdanganya kwamba nakwenda saluni, itafika mahali atakata tamaa mwenyewe,” alisema Lina.

“Hapana mke wangu, Agnes ni rafiki yako mkubwa, nenda kwenye bethidei yake kama amekualika,” alishauri Semi.

“Mh! Haya baby, basi itabaidi niende saluni kweli halafu baadaye niende kwenye shughuli.”

“Sawa. Hakuna shida.”

Moyoni Lina alifurahi sana kwani ndicho alichokuwa akikitaka.

Alijiandaa akatoka kawaida, njiani alimpigia simu Agnes…

“Egi, dili limetiki. Shemeji yako ameikubali ile kamba. Kwa hiyo wewe uko wapi sasa?”

“Yaani fanya fasta, njoo saluni mimi nimeshafika Lina. Halafu James kanipigia simu, anasema umemkatia simu, nikamwambia kuna sababu shemeji asiwe na wasiwasi. Hebu mpigie ajue unakuja saluni.”

Lina alimpigia simu James…

“My dear nimeshafika saluni.”

“Sasa kwa nini ulikata simu?”

“Kawaida tu my dear, hakukuwa na kitu. Nilijua umemaliza kuzungumza.”

“Oke, fanya haraka mimi namalizia saluni, niko na bestimani wangu. Wewe umeshampata Agnes?”

“Ndiyo.”

Baada ya James kukata simu, Lina alibaki na mawazo kibao…

“Hivi lakini mimi Lina ni kwa nini nimekubali kuuingia mkenge kama huu? Yaani wanaume wawili, tena wote wa ndoa? Nitaishije nao sasa? Kwanza mume wangu Semi akijua, si atanichinja?”

Moyoni alijuta sana lakini kwa hatua aliyofikia, haikuwa rahisi agomee ndoa. Akapanga kwenda kugomea kanisani wakati wa kuulizwa na mchungaji, yeye ajibu hayuko tayari!


Kanisa zima lilitulia, maharusi siku hiyo walikuwa watatu. Moses na Lydia, John na Elizabeth na James na Lina.

Mwanamke mmoja ambaye alihudhuria ndoa ya Lina na Semi alikuwepo, akashangaa kumwona Lina anaolewa tena huku akijua bado yupo na Semi, akashtuka sana.

Kabla Lina hajamaliza kusema, alimkodolea macho Agnes huku akionekana kama anataka kutokwa machozi…

“Kanitumia shilingi laki moja yule kaka,” alisema…

“Kweli?”

“Kabisa.”

“Basi amekupata. Maana utakimbilia wapi?”

“Si umeona?”

Ilifika mahali, Lina alihesabu kwa kichwa akitumia kumbukumbu zake na kubaini kwamba, alishakula shilingi milioni moja na laki mbili za James, akajisikia huruma na aibu ya mwenyewe.

Siku moja ya Jumapili, James alimpigia simu Lina na kumwalika kwa lanchi kwenye Hoteli ya Riki, Lina alikubali mwaliko huo na kuwekeana ahadi ya kukutana saa saba mchana.


Kabla ya kwenda, Lina alijiuliza maswali mengi sana…

“Je, ikifika mahali akaniambia ananipenda itakuaje?”

“Je, akiniambia anataka kunioa? Maana anaonekana kama hana mke!”

“Mh! Hivi nilivyokubali kirahisi si anaweza kusema mi malaya, kwa nini sikutia ngumu kidogo?”

“Hivi nilivyovaa atanikubali kweli? Kama nipo rafu, si kwa kutoka kwenda hotelini.”

Saa saba juu ya alama Lina alifika kwenye mlango mkubwa wa hoteli hiyo, akasimama na kupiga simu kwa James…

“Nimefika, niko nje hapa.”

“Ingia, ulizia mapokezi sehemu ya baa.”

“Oke poa.”

Lina alisaidia na mfanyakazi mmoja wa hoteli hiyo hadi kwenye ukumbi wa baa, akamkuta James ameshakaa anakunywa wine…

“Mambo Lina?”

“Poa, habari yako James?”

“Mungu ananisaidia.”

“Oke. Pole kwa shughuli.”

“Pole wewe, mimi leo niliamua kupumzika, kwa hiyo sijafika ofisini kwangu.”

“Da! Hongera zenu nyie mliojiajiri wenyewe, mnaamua tu, leo siendi, leo nakwenda.”

James alicheka kidogo kisha akamwangalia Lina kwa macho matamu yaliyoonesha dhahiri kwamba anampenda, Lina akahisi aibu na kuangalia chini kwa mbali…

“Enhe, mambo mengine?” alianza Lina…

“Mambo mengine poa. Mimi nimeshakuagizia chakula, najua utakipenda. Lakini nisikuchukulea muda mrefu sana. Ni hivi Lina, kusema ule ukweli mimi nina ndoto za kufunga ndoa na wewe.”

Lina alishtuka, akamtumbulia macho kwa muda huku moyo wake ukipitisha mambo kibao. Aliwaza kuhusu siku ya ndoa yao, akawaza wamepata mtoto, akawaza wanavyotembea mitaani kama mke na mume…

“James, mbona itakuwa ngumu sana.”

“Nilitegemea hilo jibu, lakini pia nilijiandaa kwa kutaka kuujua huo ugumu.”

“Ugumu ni ugeni kati yetu, utawezaje kuzungumzia ndoa kabla ya kufahamiana kwa undani kwanza?”

“Hilo lipo automatiki. Nadhani kubwa ni kujua inawezekana au la, ndiyo iingie awamu ya kufahamiana.”

Lina aliwaza sana.

Alijiambia kwamba akisema ameolewa, angemkatisha tamaa kijana wa watu ambaye kwa siku kumi na mbili tu ameshamlambisha shilingi milioni moja na laki mbili…

“Oke, niko tayari James.”

James alinyoosha mkono na kumshika mkono Lina, akamwambia…

“Siku ya leo itaingia kwenye kumbukumbu ya maisha yangu.”

“Hata mimi pia James.”

“Lakini kuna jambo moja la msingi sana Lina. Najua wewe ni msichana mrembo, mzuri, unavutia na unaishi kwenye dunia yenye wanaume. Je, huna mpenzi kweli?”

“Mmmm…kusema ukweli nilikuwa naye, lakini tulitofautiana lugha tukaachana.”

“Lini?”

“Kama miezi miwili iliyopita. Kuanzia hapo nikasema sitaki tena wanaume, najipanga kwanza. Ndiyo maana hata wewe uliponiambia habari za kuoana nilikataa kwanza.”

“Pole sana baby. Unaweza kunieleza kwa ufupi historia ya maisha yako?”

“Mmmh! Kifupi mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya mzee Joseph Ambakucha yenye watoto watano. Nimezaliwa Kijiji cha Kilole, Korogwe Tanga.

“Baada ya kumaliza masomo Shule ya Msingi Kilole nilichaguliwa kwenda Sekondari ya Wasichana palepale Korogwe. Nilipomaliza masomo nilikwenda kusomea usekretari Tabora, nilipomaliza nikapata kazi kwenye ofisi za kununua madini ya mtu binafsi, baadaye ndiyo nikajiunga kwa wale wazungu wako pale.”

“Oke, nimekusoma. Mimi kama unavyojua. Naitwa James Wingawinga Nampapara, nilizaliwa Mpitimbi, Ruvuma. Ni mtoto wa tatu katika familia nikiwa ndiyo mtoto wa tatu mwenyewe. Nilisomea Ruvuma msingi na sekondari, baadaye nikaja Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Baada ya kumaliza chuo niliamua kuwa mjasiriliamali na kwa kuanzisha kampuni yangu ya kusafirisha nje vinyago, ndiyo inaniweka mjini.

“Nimebahatika, nimejenga nyumba Mbezi Beach, nimenunua magari matatu, nina kiwanja kingine Mbezi Beach. Uzuri sina haja ya kuwajengea wazazi wangu kwani baba yangu ana uwezo mkubwa na ndiye aliyenipa mtaji wa baishara.”

Lina alibaki ametumbua macho tu. Hakujua apongeze au achukue hatua gani!

Uhusiano wa wawili hao ulianzia hapo.

Kwa siku hiyo walipomaliza kula, Lina aliingia kwenye gari la James aina ya Toyota Land Cruiser V8 mpaka ofisini kwake, wakati anashuka, James aligeukia nyuma akachukua brifkesi na kuiweka kwenye mapaja yake na kutoa shilingi laki tano…

“Zitakusaidia kwa siku kadhaa.”

“Jamani sweet, mbona ninazo?”

“Usijali baby.”

“Jamani…” Lina aliishia kusema hivyo huku akimwangalia James kwa macho yaliyojaa mahaba…

“Nitakucheki baadaye baby,” alisema James akiwa anaingiza gia ya gari na kuondoka zake…

“Poa d.”

Lina alirejea ofisini kwake huku akijiona ni mwanamke mwenye bahati sana. Kupewa shilingi laki tano hivihivi tu, ni jambo la

kushangaza hilo…

Alihakikisha anamtendea mema yote kijana huyo kama kulipa fadhila kwa pesa anazompa. Moyoni aliwaza anunue nini na pesa zile

ambazo sasa zilifika milioni moja na laki saba, hakuwa ametumia kwa sababu mume wake, Semi naye alikuwa akijiweza.

“Nitamtumia mama akarabati ile nyumba, nyingine nitanunulia cheni ya dhahabu na hereni zake,” aliwaza moyoni. Alijikuta

amekuwa mvivu wa kufanya kazi maana hakuona hata sababu ya kufanya kazi wakati kuna mtu anampa pesa kuliko mshahara wake.

**

Usiku wa siku hiyo akiwa kitandani, mume wake hajarudi, Lina alitamani kuwasiliana na James kwa sababu tangu alipomshusha

mchana na kumpa pesa hakumtumia meseji wala kumpigia simu, akatuma meseji…

“Baby mambo?”

Baada ya kutuma meseji hiyo, akakaa kwa dakika kumi nzima bila kupokea majibu mpaka akaanza kuamini kwamba, huenda James ana

mwanamke mwingine amembana huku akijifanya anataka kumuoa. Mara meseji ya James ikaingia…

“Poa Lina, naweza kukupigia?”

Lina alifurahi sana baada ya kusoma meseji, hiyo, akampigia simu kwanza mume wake kabla ya kumjibu James…

“Baby uko wapi?”

“Nipo Morocco kwa Thomas.”

“Mmh! Usiku sasa dear.”

“Nina maongezi naye nikimaliza nakuja.”

“Poapoa.”

Baada ya kupata uhakika wa umbali aliko mume wake, Lina alimjibu James…

“Unaweza bila shaka my love.”

Papo hapo James akaenda hewani.

“Yes dear, nimekusumbua usiku sana?” alisema Lina baada ya kupokea…

“Nooo Lina, hujanisumbua. Nilitoka kuoga ndiyo nikakuta meseji yako. Hata mimi ilikuwa nikupigie usiku huu kabla sijalala ili

nikutakie usiku mwema. Mambo mengine?”

“Mambo mengine poa tu. Nimekumisi ghafla.”

“Mmm! Kweli?”

“Sana tu, kwa vile hujui tu.”

“Najua baby…najua. Hebu niambie sweet hapo ulipo upo huru kuongea?”

“Yeah!”

“Umeshaoga?”

“Nimeoga muda mrefu sana dear.”

“Hukuniambia, ningekuja kukuogesha.”

“Teh! Teh! Teh! Najua iko siku utaniogesha tani yako.”

“Kweli?”

“Kweli baby.”

“Lini? Mbona kama siamini.”

“Soon tu.”

“Upo wapi muda huu?”

“Nipo nyumbani.”

“Najua, ila ila nataka kujua, upo nyumbani sebuleni au chumbani?”

“Chumbani baby, tena kitandani kabisa.”

“Umevaaje hapo kitandani?”

“Nipo ndani ya kanga moja.”

“Du! Tu?”

“Tu! Sina cha kufuli wala funguo zake.”

“Mmh! Lina…”

“Sweetheart…”

“Natamani niwe jirani yako.”

“Hata mimi baby, natamani ungekuwepo.”

“Au nije?”

“Ha! Haa! Haaa! Baby ipo siku utakuja, ila sijakwambia tu, naishi na dada yangu lakini bonge la mnoko. Yaani ni mkali balaa!

Ananichunga kama mtoto mdogo.”

“Daa! Huyo mzuri, kumbe ananilindia mali zangu vizuri.”

“Tena bila shaka.”

“Safi sana. Ukiwa kitandani unapenda kulala vipi?”

“Mh! napenda kulala ubavuubavu au chali.”

“Sasa ukilala chali Lina si itakuwa rahisi ku…”

“Kufanyaje? Umeanza sweet mambo yako.”

“Hamna d. hivi Lina umewahi..?”

“Kuwahi kufanyaje baby?”

“Kunanihi kwenye simu?”

“Haaa! Haa Ha! Ha! Baby bwana, sijawahi.”

“Uko tayari kufundishwa?”

“Ukipenda wewe mimi niko tayari.”

“Lini?”

“Wewe tu.”

“Hata sasa hivi hapa kwenye simu?”

“Ngoja kwanza baby, nakupigia sasa hivi,” alisema Lina na kukata simu.

Mwili ulimsisimka Lina, sauti ya James kwenye simu ilimchanganya kwa jinsi ilivyokuwa nzito. Alifika mbali kwa mawazo.

Akampigia simu mume wake ili ajue yuko wapi kabla ya kumrudia James…

“Hujatoka tu baby? Kuna kitu nataka kukuagiza.”

“Ndiyo kwanza nipo katikati ya mazungumzo.

We niagize tu ili nione nitafanyaje.”

“Kama bado sana basi, nitafanya hicho kitu hata kesho, baadaye basi,” Lina alikata simu.

Palepale akamtwangia James huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi…

“Niambie baby…”

“Poa tu…”

“Enhe, nakusikiliza my love, niko sawa sasa,” alisema Lina kwa sauti iliyobadilika ghafla na kuwa kama anaogopa jambo fulani…

“Umelalaje hapo kitandani Lina?”

“Nimelala chali nimeegemea mto.”

“Kwa hiyo umelala miguu umenyoosha?”

“Ndiyo baby.”

“Huwezi kuikunja kidogo?”

“Jamani baby, naweza.”

“Hebu kunja basi.”

“Nimekunja baby.”

“Oke, nikubusu?”

“Nibusu dear.”

“Mmmmwaa…”

“Aaa! Sweet…”

“Mmh!”

“Nasisimka mwenzio.”

“Hata nikikubusu kwenye masikio kama hivi…mmmmmwaaa..”

“Aaah! James…”

“Basi nipe ulimi.”

‘Chukua baby…mmmm….mmm…”

“Mmm….mmm…mmm.”

“Sweetheart…”

“Yes baby wangu Lina…”

“Nipo vibaya mwenzio.”

“Usijali mimi nipo ubavuni mwako.”

“Karibu baby.”

“Nipo…mmmm…mmm.”

“James…”

“Yes…”

“Njoo sasa…”

Lina alizidiwa kabisa, akashindwa kuendelea na maigizo hayo akamwomba James amwache alale wataonana kesho yake…

“Noo baby, kwa nini wakati mimi nipo.”

“Nashindwa kuvumilia baby na si unajua nipo peke yangu.”

“Dada kalala?”

“Amelala muda tu.”

“Basi sawa, lala usiku mwema lakini naomba kesho uniamshe kwa simu asubuhi ya saa kumi na moja,” alisema James.

Lina akakubali huku akianza kujiuliza atafanyaje hadi ampigie simu asubuhi wakati atakuwa amelala na mume wake…

“Afadhali angesema saa kumi na mbili lakini kumi na moja mbona usiku bado,” alisema moyoni Lina baada ya kukata simu.

Nusu saa mbele mume wake Lina, Semi aliingia akiwa amechoka sana.

Alifikia mikononi mwa mkewe ambaye alikuwa ameshapashwa moto wa mahaba na James…

“He! Leo vipi mke wangu mbona kama umekuwa ghafla?”

“Nimekumisi tu mume wangu.”

“Kwa hiyo ndiyo univamie hata kabla sijaenda kuoga wala kujua hali ya nyumbani jamani?”

“Ndiyo hivyo ukae ukijua.”

“Lakini mimi leo nimeshinda kichwa hakiko sawasawa kama siku zote.”

“Pole dear, umekunywa dawa?”

“Bado, ila najua nikilala nitaamka sawasawa.”

“Pole, basi kaoge ulale baby.”

Semi alikwenda kuoga,alipomaliza alipanda kitandani kulala bila kusema kitu. Lina naye akaendelea kulala huku akikumbuka maneno ya mahaba ya James…

“Umelalaje hapo kitandani Lina?”

“Nimelala chali nimeegemea mto.”

“Kwa hiyo umelala miguu umenyoosha?”

“Ndiyo baby.”

“Huwezi kuikunja kidogo?”

“Jamani baby, naweza.”

“Hebu kunja basi.”

“Nimekunja baby.”

“Oke, nikubusu?”

Maneno hayo yalimrudia Lina kichwani mwake kwa usiku ule na kujikuta akitamani kumgeuza mume wake kwake ili mechi ianze lakini alishindwa kwa sababu ya kuambiwa anaumwa kichwa.

“Da! James kanipa wakati mgumu sana, afadhali angekuwa nyumba ya pili ningekwenda chapuchapu!” aliwaza moyoni mwake.


Saa kumi na moja kamili, Lina alitoka kitandani mumewe akiwa badi anakoroma. Akatoka kitandani akiwa na simu yake mpaka chooni, akaiwasha kisha akampigia simu James…

“Baby…” alisema baada ya James kupokea simu. Ilionekana kwamba hakuwa usingizini kwa hiyo alivyotaka aamshwe pengine alitaka kusikia sauti ya Lina kwa asubuhi au kujiridhisha kwamba kweli anaishi kwa dada yake na hana mwanaume…

“Umeamkaje Lina?”

“Niko salama sweet, wewe je?”

“Nimeamka poa.”

“Umeshatoka kitandani?”

“Hapana dear, ila najiandaa nitoke.”

Mume wa Lina, Semi alishtuka, akaangalia alipolala mkewe akagundua hayupo na ametoka na simu. Kwa mbali alimsikia akiongelea kutokea chooni, akaamka…

ALITEMBEA kuelekea chooni lakini alikutana naye anatoka…

“Vipi, mbona kama unaongea na simu chooni?”

“Si mama Pendo huyo, saa zile naamka kuja chooni na yeye akapiga sasa nilibanwa na haja ikabidi nije huku naongea naye.”

“Anasemaje muda huu?”

“Anasema hajalala tumbo, nikiwa na nafasi asubuhi nimpeleke hospitali.”

“Shemeji naye, mbona hospitali ni karibu na kwake? Yaani we utoke huku mpaka kule halafu umchukue kurudi naye hospitali au yu mahututi?”

“Hamna, kwanza mpaka akuambie mwenyewe ndiyo utajua anaumwa, mimi mwenyewe sikujua mpaka aliponiambia.”

Kulipambazuka kabisa, Lina alijiandaa mumewe naye alijiandaa, wakatoka wote. Lina alishushwa nje ya ofisi yake mumewe akaendelea na safari.

Ile anakaa tu, Lina akashika simu kumpigia James…

“Baby…”

“Yes baby, niambie.”

“Nimeingia job baby.”

“Safi sana, mimi ulivyoniamsha nikaoga lakini sijatoka nyumbani.”

“Oke. Sasa baby nyumbani unaishi na nani?”

“Niko na wasaidizi wa kazi watatu.”

“Watatu wa nini wote hao?”

“Mmoja ni mwanamke mtu mzima, ndiyo huwa anapika na kufua. Wa pili wa kiume kijana, huyu anatunza mazingira na wa tatu ni mlinzi getini.”

“Du! Kweli baby unatakiwa kuoa sasa baby wangu.”

“Kha! Kwani unadhani ni kwa nini nilikuomba uwe mke wangu Lina? Kwanza nimekupenda, pili una sifa za kuwa mke. Wewe Lina ni wife material.”

Lina alicheka kidogo, akafurahi, akaendelea…

“Sasa unatoka saa ngapi?”

“Eee, kuna email nazisubiria kwa hapahapa nyumbani nataka kutuma mzigo Ufaransa kwa hiyo naseti mawasiliano.”

“Naweza kuja?” alisema Lina kwa kusitasita, moyoni aliamini James hawezi kukubali hilo la yeye kwenda kwake.

“Wao, karibu sana Lina, tena nitafurahi sana kukuona hapa kwangu.”

Lina hakuamini masikio yake, akashangaa na kumuuliza James…

“Kweli baby?”

“Yeah! Njoo, chukua teksi nitalipa mimi hapa.”

“Ni wapi?”

“Mbezi.”

Lina alikata simu, akaingia kwa mabosi wake na kuomba ruhusa ya dharura akaruhusiwa, akaondoka.

Alitembea kwa mwendo wa haraka hadi kituo cha teksi, akaingia kwenye mojawapo…

“Twende Mbezi Beach tafadhali.”

Safari ilianza huku Lina akiwa na mshawasha wa moyo, alikuwa na maswali kadhaa…

“Je, James akitaka kuduu na mimi?” alijiuliza mwenyewe.

“Mh! Kwa kweli kwa jinsi alivyonilaza na njaa jana sitakuwa na sababu, nitakubali tu. Maana mh! Hata hivyo, ni nafasi ya pekee ya mimi na yeye kukutana kimwili kwa mara ya kwanza tena nyumbani kwake.

“Ni heshima kubwa sana atakuwa amenipa, maana angekuwa mwanaume mwingine asingekubali kuniita kwake, angeweka kikwazo.”

Lina alipoingia Mbezi ya Tangi Bovu alimpigia simu James akapewa ramani halisi ya kufika kwake. Ilikuwa ramani rahisi sana kwani walifika hadi nje ya geti, honi ikapigwa, geti kubwa likafunguliwa.

“Umeambiwa ingiza gari ndani,” mlinzi alimwambia dereva akimchungulia kwa kutumia kioo cha dirisha.

“Sawa,” teksi ikaingizwa ndani, Lina akashuka.

Ile anashuka tu, James anatokea ndani kwa mlango mkubwa…

“My wife to be,” alisema James akiachia tabasamu pana huku mikono ameipanua tayari kwa kumkumbatia Lina…

“Yes Lina’s husband.”

Walikutana wakakumbatiana, Lina akamuwahi mabusu James kama matatu, naye akarudishiwa, wakaingia ndani huku James amemkumbatia Lina kwenye kiuno.

Lina alishangazwa sana na mazingira ya nyumba hiyo. Licha ya kuambiwa mlikuwa na watu watatu na mwenyewe James wa nne, lakini ilionekana kama wanaishi watu kumi na mbili.

Maana alipozama sebuleni tu, akatokea yule mwanamke, akamkaribisha Lina kwa adabu zote licha ya kwamba alikuwa mama mtu mzima, kabla hajatoka akatokea kijana mtunza mazingira huku mlinzi naye akiingia na boksi na kuliweka sehemu kisha akatoka.

Lina alishangazwa pia na ukubwa wa sebule kwani alikuwa kama yupo kwenye ‘nusu uwanja’ wa table tennis. Mbali na ukubwa huo alishangazwa na samani za ndani licha ya usasa wake lakini hizo hakuwahi kuziona tangu azaliwe.

“Enhee, za kazi baby?”

“Poa, vipi wewe?” aliitika Lina.

“Mimi mzima sana, namshukuru sana Mungu. Lakini namshukuru zaidi kwa kukuleta wewe hapa leo.”

“Mimi mwenyewe nimefurahi sana kwa kunikubalia kuja kwako leo,”

alisema Lina huku akipepesa macho sehemu mbalimbali za sebule hiyo, akampongeza James kwa kuwa na nyumba nzuri kama ile.

Baada ya salamu, James aliwaita wafanyakazi wake wote, wakafika na kukaa kwenye sofa, kila mmoja yake…

“Huyu anaitwa Lina, ni mtoto wa mzee Joseph Ambakucha pale Kijiji cha Kilole, Korogwe Tanga. We mama si umetokea Korogwe pia?” alihoji James akimwangalia mwanamke anayemsaidia kazi za ndani…

“Ndiyo, hapohapo Kilole. Na mzee Joseph Ambakucha namfahamu sana.”

Lina alimtumbulia macho, akahisi kama mwanamke huyo anaweza kuharibu mambo japokuwa yeye hakuwa anamkumbuka kwa sura…

“Na wewe mama umeishi pale?”

“Ee! Mimi nilikuwa naishi Mgandini, wengi wananijua kwa jina la mama Tabu, nyumba yangu iko jirani na ya mzee Hussein, yule ana watoto akina Sakina, Said, Mariam…”

“Ooo! Sakina, Said wote nawakumbuka. Lakini wewe sikukumbuki kabisa…”

“Si rahisi lakini dada zako, kaka zako nawajua. Namjua Kiliana, Josephine, Anna na Yonasi.”

Basi, baada ya hapo, James akaendelea…

“Huyu sasa ndiye mchumba wangu niliyewaambia nimempata mtu wa Korogwe, Tanga ndiyo huyu.”

“Lakini sasa mbona ana pete ya ndoa kwenye kidole?” alidakia yule mwanamke.

Kumbe siku hiyo Lina aliamua kuvaa pete bwana, akasahau kuivua wakati anakwenda nyumbani kwa James.

James alishtuka sana, Lina pia alishtuka lakini akajikaza asijulikane, kilishanuka…

“Mungu wangu…Mungu wangu,” alisema moyoni…

“Eti Lina! Ni nini hiyo mpenzi? Kumbe unanisaliti?”

“Hamna! Kwa sababu nyie hamtembei sana mitaani. Siku hizi wanawake wengi wanavaa pete za ndoa ili kukwepa usumbufu wa wanaume. Mwanaume akikuona una pete ya ndoa heshima inaongezeka kidogo…”

James alitazamana na yule mwanamke anayemsaidia kazi za ndani, mwanamke akasema…

“Hiyo ni kweli, hata mimi nakubaliana na wewe. Japokuwa kuna wanaume hawajali hata kama una pete ya ndoa lakini inasaidia kupunguza upungufu.”

“Ni kweli.”

James alikubaliana na hilo kwa kutingisha kichwa huku akimwangalia Lina kwa macho yaliyojaa mahaba mazito…

“Vipi baby?” aliita Lina akimwangalia James…

“Poa tu.”

Wakati huo wale wote walioitwa kutambulishwa walishaondoka. Walibaki wawili tu.

“Hapa ndiyo nyumbani kwako?”

“Yeah! Hapa ni nyumbani.”

“Da! Bonge la jumba. Ukisikia jumba la kifahari ndiyo hili.”

“Kweli Lina?”

“Sana tu, hongera sana bwana. Kwanza bado kijana mdogo lakini umejitahidi sana.”

“Asante baby, ndiyo maana nataka tufunge ndoa ili uje kuipamba nyumba hii.”

“Hilo tumwombe sana Mungu atupe afya na uzima.”

James alisimama na kwenda chumbani kwake, nyuma Lina akawa anashangaashangaa mapambo ya nyumba hiyo yalivyokuwa na mvuto.

Mara James alitokea. Moyoni aliamini ni siku mwafaka sana kwake kuivunja amri ya sita na Lina lakini alikuwa haamini kama atakubaliwa kwani msichana mwenyewe alitoka kazini na angerudi tena kazini…

“Labda mjaribu, akisema siku nyingine sawa,” sauti ilisema ndani ya moyo wa James.

“Baby sasa, si umechoka sana ukaoge upumzike kidoo kitandani, au?” alisema James huku akiangalia pembeni kwani alijaliwa kitu kinaitwa aibu.

“Poa. Lakini nikioga nitabadili nini sasa?”

“Kwani mpaka ubadili, si unavua hizo, unaoga unavaa taulo ukilala, ukiamka unaoga tena unavaa hizo unaondoka.”

“Poa.”

“Basi simama twende.”

Lina alisimama akatembea huku akiivua ile pete ya ndoa na kusema moyoni…

“Ilitaka kuniletea balaa bure, bahati njema nimepata mwanaume mwelewa.”

Aliingia kwenye chumba cha James na kukutana na vitu vya samani ambavyo hakuvitarajia. Kitanda cha kisasa, sofa moja kubwa, stuli ndogo mbili na kitu kama meza fupi sana kwa ajili ya kupandia kitandani.

Lina alishangaa kuona ndani ya chumba hicho kila kitu ni cheupe au kimechanganywa na rangi ya krimu. Mashuka meupe, pazia jeupe, kapeti krimu, foronya nyeupe, dari nyeupe, mlango hadi madirisha na makabati.

Kilichomshangaza sana Lina na kuona chumba hicho hakina choo na bafu kwa maana ya ‘master bedroom’ kama ambavyo alitarajia…

“Mh! Bonge la chumba, kila kitu kimehusika lakini amekosa kitu kimoja tu, choo cha ndani,” alisema moyoni Lina. Lakini moyoni alisifia chumba hicho kilivyo na nyumba nzima kwa ujumla kwamba ni ya kisasa.

“Sasa ukaoge my love,” alisema James. Lina akasimama na kupokea taulo kutoka kwenye mikono ya kijana huyo. Alichojoa nguo zake zote, akabaki kama alivyozaliwa kisha akajijaladia na taulo sasa, akawa anatembea kwenda mlango mkubwa…

“Bafu liko uani au?” aliuliza Lina…

“Oooh! Sorry, bafu lile pale,” James alimwelekeza Lina bafu ambapo kwa Lina alipoona mara ya kwanza alijua pana kioo kikubwa kumbe ni mlango wa kuingilia bafuni, alijisikia aibu kubwa kwa ushamba.

“He! Sikujua mpenzi wangu, samahani,” alisema Lina huku akimfuata James na kumkumbatia kisha akampiga mabusu mawili ya pande mbili za mashavu.

James alionesha kusisimkwa mwili, naye akamkumbatia, wakatazamana. Ilikuwa ni kitendo cha mara yao ya kwanza tangu waanze kufahamiana siku kadhaa nyuma.

Lina alisisimka sana, James pia. Walijikuta wakigandana na baadaye walipanda kitandani huku Lina akiwa ametupa taulo chini…

“Baby,” aliita Lina kwa sauti tamu sana ambayo kwa mwanaume yeyote rijali angevutwa nayo hata kama angeisikia kwenye simu tu.

“Yes dear,” alipokea James akiwa kwenye macho yaliyojaa ulegevu wa mahaba ingawa hakumshinda Lina ambaye alikuwa mbendembende.

“Nahisi naota.”

“Kwa nini baby?”

“Hivi kweli?”

“Kweli nini?”

“Nipo kitandani na wewe leo?”

“Hata mimi siamini Lina, wewe ni mwanamke niliyetokea kukupenda sana. Napenda ujivunie kwa hilo baby.”

“Asante dear jamani,” alisema Lina akiwa anamshikashika James sehemu ya mgongoni.

Mechi ilianza kwa Lina kumsoma James kwamba ni mwanaume wa namna gani, anayependa nini kwenye ‘uwanja’ na nini hapendi. Kwa hiyo alichokuwa akikifanya Lina na kufanya tukio halafu ‘kumsikilizia’ James kwamba ‘anariakti’ vipi!

Mfano, katika kugalagaza, Lina alipeleka mdomo wake kwenye sikio la kijana huyo na kumpumulia kwa nguvu, James akawa hoi.

Kumbe James naye alikuwa kama Lina. Kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana kwenye mechi, Naye alijitahidi kusaka sehemu ambazo ni za msisimko kwa Lina. Alipeleka vidole kwenye kifua na kuzishika nido kwenye misumari yake ambapo Lina akawa kama amepoteza fahamu.

Kama vile hiyo haitoshi, James alipotoa mikono kwenye nido akavipeleka kwenye sehemu kuu na kumfanya Lina kuwa hoi bin taaban huku akisema maneno ambayo ili uyasikie ni lazima kulaza sikio kwenye kinywa chake…

“Baby tayari sasa,” James alimsikia akisema hayo baada ya kumsogelea kwa karibu ili kumsikiliza. James hakutaka kumsikiliza, akaamua kwenda mbele zaidi ambapo alipeleka vidole kwenye sehemu ya kukanyangia mguuni kwa Lina, kilio kikubwa kikasikika kutokea chumbani humo lakini kwa jinsi mlango na madirisha yalivyokuwa hata kama mtu angesimama kuemea mlango asingesikia kitu.

James alizidisha manjonjo kwa kumpapasa Lina sehemu ya nyuma ya magoti ambapo Lina alibaki ameduwaa, uwezo wa kusema lolote hakuwa nao tena.

James aliianzisha mechi kwa kupuliza filimbi uwanjani yeye mwenyewe, Lina akaipokea huku akimwimbia nyimbo mbalimbali za mahaba mpenzi wake huyo ilimradi mchezo uwe mzuri huku jasho likifichwa kwa kasi ya utulivu ndani ya uwanja.

Ni ndani ya dakika kumi tu, Lina akatangaza ushindi wake wa kwanza dhidi ya James huku akipokea mashambulizi ya piga nikupige bila kubutua.

Ndani ya dakika tano tena mbele, Lina akatangaza kupata ushindi mwingine wa pili huku James akiendelea kupeleka mashambulizi yenye kumpa ushindi mrembo huyo.

“Baby,” aliita Lina mara baada ya ushindi wa pili…

“Yes…”

“Upo vizuri darling.”

“Kweli?”

“Sana.”

Maneno ya Lina yalimsukuma James ambaye naye papo hapo akapata ushindi wake wa kwanza huku Lina baada ya kumsikia mwanaume wake akiwewesekea ushindi na yeye akaupata wa tatu wa bure kabisa.

Wote wakawa wanahema kwa kasi, hakuna aliyemsemesha mwenzake. Sanasana kuna wakati James alinyoosha mkono na kushika rimoti ya AC na kuongeza kidogo spidi ya kutoa baridi. Hapo, Lina alikuwa akimwangalia James kwa mbali kwa macho ambayo kama anayafumba lakini hajayafumba kabisa, unaweza kusema alikuwa akisinzia.

James alidondoka na kulala ubavuubavu akimwangalia Lina ambaye naye alipeleka mkono wake kwenye kiuno cha mpenzi wake huyo na kukishikashika kama moja ya mbwembwe ndani ya uwanja wa mapenzi.

Baadaye sana, wawili hao walirejea katika ungangari wao, walianza kuzungumza…

“Sweet,” aliita Lina kwa sauti ya chini sana…

“Yes,” James aliitika kwa sauti nzito.

“Nakupanda sana. Sijui itakuwaje?” alisema Lina huku James akiwa hajui nini maana ya kauli yake hiyo.

“Baby, kwa nini umesema hujui itakuwaje? Kwani si tumeshapanga kufunga ndoa au?”

“Ungejua niko kwenye ndoa mwenzako wala usingesema hivyo,” alisema moyoni Lina lakini kwa sauti akasema…

“Unajua siamini kama hiyo siku itafika dear.”

“Kwa nini isifike my love? Itafika tu, sisi kinachotakiwa ni kumwomba Mungu tu basi,” alisema kwa ujasiri mkubwa James.


Saa kumi na mbili, James alimwingiza Lina ndani ya gari kumrudisha nyumbani na si kazini kama alivyotoka. Ndani ya gari, kiyoyozi kilikuwa kwa kiwango cha juu huku Lina akifurahia maisha na kusema moyoni kwamba alipata mwanaume wa kweli na kulaani ni kwa nini aliwahi kuonana na mumewe, Semi na si James.

Lina alimwelekeza James na kuiegesha gari jirani kabisa na nyumbani kwake huku akimwambia…

“Kama nilivyokwambia dear, dada yangu ni noma sana baby, kwa hiyo nishushe hapa.”

“Oke. Lakini baby vumilia tu iko siku yatakwisha mke wangu. Tukifunga ndoa shemeji atatulia, ukali wote utaisha,” alisema James akimkazia macho Lina. Lina aliachia tabasamu laini lakini kila wakati alionesha kutaka kuendelea kuwa na James.

Ukweli ni kwamba, Lina aliamua kushuka pale ili kukwepa mtego wa kukutana na mumewe ambaye alijua akigundua hilo pangechimbika ile mbaya.

Wakati anashuka, Lina alimpa mdomo James, akaachia ulimi, ukapokelewa kwa kuvutwa kwa dakika kama moja nzima huku mrembo huyo akionesha kusisimka sana…

Mara, simu yake iliita, kuangalia namba ni mume wake…

“Haloo baby…”“Nahisi nimekupita ukiwa ndani ya gari upo na nani?”

“Ni rafiki yangu mbona, amekataa kufika nyumbani, ndiyo kageuza sasa hivi hapa,” alisema Lina huku akishuka kwenye gari hilo na kuanza kutembea bila kuagana na James ambaye alishikwa na mshangao.

James hakutaka kumuuliza kitu Lina, akaweka gia ya kurudi nyuma kisha akageuka na kuondoka. Lakini kichwani alipata tabu na kauli ndogo tu ya Lina ukiachilia mbali kule kuondoka. Nayo ni ile aliyoitoa wakati akipokea simu…

“Haloo baby…”

“Huyo baby ni nani? Ina maana Lina ana mwanaume mwingine? Haiwezekani…kama ni kweli nitatumia uwezo wangu wote nisambaratishe penzi lao,” alisema moyoni James huku akiingiza gari lake barabara kuu.


Lina aliendelea kuzungumza na mume wake kwa simu akijisafisha huku akikaribia nyumbani lakini alipomaliza ndipo akamkumbuka James na mazingira ya kuachana kwao muda mfupi uliopita…

“Haloo baby…”

“Daaa! Sasa pale si atakuwa ameshangaa, haloo baby, baby ndiyo nani wakati nilimwambia sina mpenzi tuliachana? Nimechemsha kweli. Nilichotakiwa kukifanya pale ni kutopokea simu ya mista,” alisema moyoni Lina, akajikuta akiumia sana.

Alisimama nje ya duka moja kabla hajafika nyumbani kwake, akampigia simu James…

“Lina,” James aliitika kwa sauti nzito…

“Baby nisamehe sana…”

“Kwani kulitokea nini Lina mpenzi?”

“Da! Yaani, unajua nini my love?”

“Ee…”

“Kuna yule jamaa yangu niliyekwambia tumeachana, ndiye aliyenipigia…”

“Sasa baby kama ni yeye, ndiyo uondoke bila kuniaga?”

“Unajua nini my love?”

“Sijui…”

“Alichonitendea, kila akipiga simu nahisi kukasirika.”

“Sasa kama ni hivyo, mbona ulivyopokea ulisema haloo baby?”

“Da! Ni mazoea yangu, mabaya sana. Napenda sana kusema baby hata kwa mwanaume ambaye si mpenzi wangu.”

“Basi uache tabia hiyo kuanza sasa, sawa Lina?”

“Sawa mpenzi wangu, nisamehe.”

“Poa, yameisha.”

“Nashukuru baby, sasa naingia ndani ukinitaka unitumie sms kama nilivyokwambia sista mnoko kweli, ananifanya mimi kama mtoto wake, tena wa chekechea.”

“Usijali d, ila na wewe ukiwa katika mazingira mazuri nipigie, sawa?”

“Sawa d.”

Lina alizama ndani kwake akiwa na amani baada ya kumaliza ishu nzito na James ambaye alimwita mchumba ingawa wakati mwingine alipokuwa amekaa mwenyewe alijiuliza nini hatima ya uhusiano wake huo.


Baada ya hapo, mapenzi yaliimarika zaidi na zaidi hadi ikafika hatua ya kukubaliana kuhusu ndoa ambapo vikao kwa James vilianza na Lina aliwahi kuhudhuria kama mara tano hivi.

Kwa upande wake, Lina aliweka kikao kwa ajili ya kitchen party tu ambapo alimtumia rafiki yake Agnes kumsimamia wakisingizia kwamba, hakuwa na ndugu jijini Dar.

Ndugu wa Agnes, kama mashangazi na rafiki zake wengine, akiwemo mama mkubwa walibeba jukumu la kusimamia sherehe hiyo mwanzo mwisho.

Siku ya kwenda kwenye sherehe ya kitchen party, Lina alimwomba ruhusa mume wake, Semi siku moja nyuma akimwambia kutakuwa na kitchen party ya rafiki yake.

Siku ya shughuli mumewe alimuuliza kisa cha kuondoka akiwa amebeba nguo kwenye begi badala ya kuvalia nyumbani, Lina alisema…

“Hili gauni nikilivalia nyumbani nitakuwa kituko mtaani, nitakwenda kuvalia kwa Eg…”

“Kwani lina nini hilo gauni?”

“Limeshonwa kwa madoido sana baby, linafaa kuvaliwa ukumbini tu.”

“Hebu tulione.”

Lina alisita kwanza akidai muda unakwenda, lakini akalitoa…

“Khaa! Sasa mbona gauni lenyewe limeshonwa kama wewe ndiye bi harusi mtarajiwa?”

“Hamna! Unajua wamealika ngoma ya kigodoro ndiyo maana magauni wamesema yawe hivi.”

“Oke poa.”

Lina aliondoka mpaka kwa Eg, akapokelewa kwa shangwe na ndugu wa Eg ambao walikuwa hawajui kama bi harusi huyo ni mke wa mtu tena kwa ndoa ya kanisani kabisa.

Akiwa kwa Eg, Lina alimpigia simu James…

“Baby, uko wapi?”

“Niko kwa Eg darling.”

“Kwa hiyo ndiyo kama hivyo, leo hatuonani siyo?”

“Hatuonani labda usiku sana maana si unajua kitchen party si ya wanaume baby?”

“Poa, kuna nini kimepungua?”

“Hakuna dear.”

Wakati mazungumzo yakiendelea, mume wa Lina alifunga breki nje ya nyumba ya Eg na kupiga honi ana shida na mke wake huyo…

“Pii pii piii!”

ITAENDELEA

Usiku wa kigodoro Sehemu ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment