Wito wa Kuzimu Sehemu ya Kwanza
IMEANDIKWA NA: HASSAN O MAMBOSASA
*********************************************************************************
Simulizi: Wito Wa Kuzimu
Sehemu ya Kwanza (1)
MWANZO**
Akiwa ameketi ofisini kwake aliendelea kufanya kazi iliyokuwa ikimuhusu sana na ilitakiwa kufanywa ndani ya siku hiyo, kazi hiyo ilikuwa ni muhimu sana kuwasilishwa bungeni kwa siku iliyokuwa ikifuatia kutokana na unyeti wake. Ilikuwa ni kazi ambayo ripoti yake muhimu ndiyo ilikuwa imefika mezani kwake kwa siku hiyo , aliingojea sana kwa hamu hiyo ili aweze kukamilisha maelezo mengine kwa ajili ya kuwasilisha wajibu huo. Ilikuwa katika muda ambao hakua akitaka kabisa kuonanana mtu yeyote ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi, ndiyo maana alimpa agizo Katibu Mukhtasi wake la kutoruhusu mtu aje kuonana naye kwa muda huo aliokuwa hapo ofisini.
Haikuwa kawaida kabisa kwa yeye kufanya hivyo lakini kutokana na unyeti wa suala hilo ilimbidi afanye hivyo, ripoti hiyo ambayo alikuwa akiiandikia kazi yake ilikuwa ikihitajika sana kwa udi na uvumba. Ilikuwa ni kaba koo kwa baaahi ya watu lakini pia ilikuwa ni ilikuwa yenye manufaa kwa hadhira ya watu waliyokuwa wakiiongojea kwa hamu sana iweze kukamilika. Hakuna mwenye nia nzuri aliyekuwa hakiitaka ripoti hiyo isifike kwa watu ijulikane, hofu yakupoteza kibarua pamoja na kuonekana ni mzembe ndiyo ilimfanya ajifungie humo ofisini kwake akiwa anaiandaa ripoti hiyo iweze kuwafikia walengwa wake. Tarakilishi ya mapakato aliyokuwa akiitumia kwa siku zote ilikuwa ipo mezani na faili lililokuwa limesheheni makaratasi yaliyochapishwa lilikuwa lipo wazi huku kalamu ya wino ikiwa ipo katikati ya faili hiyo.
Aliendelea kufanya kazi yake kwa ufasaha sana lakini ufasaha huo uliyokuwa upo kwenye kazi yake uliondolewa mara moja baada ya karaha kuingia, karaha ambayo ilimpunguza ufanisi ambao ingembidi aweze kutulia vizuri aweze kuurudie ndiyo ilivamia ndani ya eneo hilo. Karaha hiyo ilivamia kwa kuita kwa mlio wa simu yake ya mkononi ambayo ilikuwa ipo jirani kabisa na Tarakilishi yake ya mpakato humo ofisini kwake., aliitazama simu yake hiyo akakuta namba ni ngeni kabisa ikiwa ina jina tu kuashiria kuwa aliyekuwa akipiga namba hiyo alikuwa akitumia mtindo wa kuweka namba binafsi(private number). Alipoiona namba hiyo aliacha kufanya kazi na kisha akaichukua simu hiyo akaitazama kwenye kioo chake aliitazama namba hiyo binafsi kwa muda wa sekunde kadhaa kama aliyekuwa akijifikiria kitu na hatimaye aliamua kuipokea na kisha akaweka spika ya nje huku akiendelea kufanya kazi zake.
“Ndiyo nani mwenzangu” Aliongea
“Heshima yako mheshimiwa” Sauti ya mtu aliyempigia tena ikionekana ni ya mwanamke ilisikika
“Ndiyo nakusikiliza” Mheshimiwa aliongea huku akiendelea kufsnya kazi zake.
“Kama jina langu ulivyoliona Mheshimiwa mimi ni Malikia wa kuzimu, nimetumwa kukuambia uache hicho uanchokifanya la si hivyo utatumiwa wito wa kuzimu”
“Hivi wewe umekosa kazi ya kufanya mpaka uchukue muda wako mwingi kuweza kuiweka namba yako hivyo na kisha unipigie simu halafu uongee huo utumbo wako”
“Nimekuambia tu Mheshimiwa achana na hicho unachokifanya, kuwa mtoto wa kike haimaanishi onyo langu haliwezi kukufikia. Sauti hii nyororo ninayokuonya nayo jua ikifika siku utatamani hata irudie tena kukuambia nilichokuambia lakini haitawezekana”
“Malaya mkubwa wewe”
Mheshimiwa aliongea kwa hasira sana na kisha akaikata simu hapohapo, aliisogeza mbali na eneo alilokuwepo na kisha akajariu tena kutulia aweze kukamilisha kazi hiyo aliyokuwa akiifanya. Alijaribu kuuweka ule umakini aliokuwa ameuweka hapo awali lakini ilishindikana kabisa kuwepo, hapo alijikuta akifunika Tarakilishi ya mapakato liyokuwa akiitumia. Umakini wote ulivurugika na hata hamu ya kuendelea na maandalizi ya kazi haikuwepo kabisa, moyoni alilaani kupigiwa simu na mwanamke ambaye ndiyo alikuwa amemchanganya kabisa kwa maneno hayo aliyomwambia.
MASAKI
DAR ES SALAAAM
Muda huohuo nyumbani kwa mtu muhimu sana kwa kampuni moja ya kiserikali na pia mtu muhimu katika idara nyeti, mtu wa kuleta barua alifika mara moja ndani ya nyumba hiyo akiwa na barua muhimu sana kwa mwenye nyumba hiyo ambaye alikuwa yupo mapumzikoni baada ya kumaliza kazi nzito ambayo ilihitajika muda mrefu sana kuiandaa. Mtu huyo wa barua alimpatia mmoja wa wanfamilia ya mwenye nyumba hiyo na kisha akaondoka bila ya kuaga, mwanafamilia huyo naye hakutaka kabisa kushughulika na kuichunguza hiyo barua yeye aliichukua na moja kwa moja aliiwasilisha kwa mwenyewe ambaye alikuwa yupo sebuleni akiwa amekaa. Baada ya kumpatia mzigo wake aliingia ndani moja kwa moja akiwa ameshafikisha ujumbe stahiki kwa mhusika, mwenye nyumba hiyo ambaye alikuwa ndiyo kwanza anaianza likizo yake aliichukua barua hiyo na kisha akaitazama kwenye sehemu ya nje ya bahasha.
Alikutana na jina lake ndiyo lipo juu ya bahsha ikimaamnisha yeye ndiye alikuwa mlengwa wake, baada ya kuliona jina hilo aliiachana bahasha kuweza kuona kilichomo ndani yake. Alikutana na bahasha nyingine nyeupe kabisa ikiwa na stempu yenye picha ya mwanamke akiwa anaonekana mgongo ambao haukuwa umefunikwa na kitu chochote kile, alipoiona picha ya stempu alijikuta akishangaa sana kwani haikuwahi kuonekana stempu ya namna hiyo kwenye barua ya aina yeyote ile na wala haipo kwenye maduka yanayouza stempu. Alijikuta akiitazama picha hiyo ya stempu kwa sekunde kadhaa akiwa ameingiwa na shaka na kisha akapeleka macho yake katika upande mwingine wa bahasha hiyo, napo alikutana na na mhuri wenye rangi nyekundu ambao ulikuwa una nembo ya moto katikati. Juu ya nembo katika sehemu ya juu ya mhuri huo alikutana na maneno yaliyokuwa yakisomeka kwa ufasaha kabisa, maneno hayo ndiyo yalimfanya hata azidi kuwa na shaka sana na barua hiyo ilipotoka.
‘KUZIMU’ ndiyo neno ambalo lilikuwa lipo juu ya nembo hiyo sehemu ya mhuri, kuona neno hilo alijikuta kwa haraka akijaribu kuminya bahasha aone ndani ya kulikuwa kuna nini kwani haikuwa kawaida kabisa kuwahi kupokea barua ya namna hiyo. Alipoiminya bahasha hiyo alijikuta akiguna. Baada ya kubaini kitu alichokihisi kwa viganja vyake vya mikono alivyokuwa ameiminya bahasha hiyo kidogo tu, alikata shauri na kuamua kuifungua bahasha akiwa anataka kujua kile alichokuwa ametumiwa na kipo ndani ya bahasha hiyo.
Kazi ilivurugwa ikavurugika kwake Mheshimiwa na akajikuta hata akiwa hana hamu ya kufanya kazi tena zaidi ya kuwa na hamu ya kwenda kupumzika hotelini alipokuwa amefikia, alifunga vitu vyake vya muhimu kabisa na kisha akatoka nje ya ofisi yake akiwa amechanganyikiwa. Aliufunga mlango wa ofisi yake pia na kisha akaelekea moja kwa moja hadi kwa Katibu Mukhtasi wake ambaye alikuwa akiendelea na kazi kama kawaida.
“Ninatoka sasa hivi nitaurdi kesho mchana nikitoka kwenye bungeni” Alimuambia
“Sawa mheshimiwa ila kuna barua yako imeletwa sasa hivi na mtu wa posta” Katibu Muhktasi alimuambia
“Ok nipe nitaenda kuisoma hotelini akili ikiwa sawa” Alimuambia Katibu Mukhtasi wake ambaye alifungua mtoto wa meza yake akatoa bahasha nyeupe ambayo ilikuwa na mstari mwekundu kwa juu akampatia Mheshimiwa, alipoipokea barua hiyo aliitazama sehemu ya juu akakuta kukiwa hata hamna stempu ya barua. Hilo suala hakujiuliza kabisa yeye aliichukua barua hiyo akafungua koti lake la suti akaiweka kwenye mfuko wa ndani wa koti hilo na kisha akauweka vizrui mkoba wake wa begani akawahi kutoka nje
Kituo chake cha kwanza baada ya kutoka nje ya jengo la ofisi yake ilikuwa ni ndani ya gari lake la kifahari ambalo lilikua limeegeshwa kwenye eneo maalum ndani ya ofisi hiyo, aliingia ndani ya gri hiyo na kisha akauweka mkoba wake wa begani ambao ulikuwa una tarakilishi yake katika kiti cha nyuma. Baada ya hapo alitoa funguo za gari yake na kisha akaliwasha na kuliondoa ndani ya eneo hilo akiwa ana haraka ya kuweza kufika hotelini alipokuwa akiishi aweze kupumzisha kichwa chake kutokana na kuvurugwa kabisa na mwanamke aliyekuwa amempigia simu. Aliwasha taa ya pembeni ya upande wa kushoto alipofika barabarani kutokea kwenye maegesho, na taratibu akaliingiza barabarani na kuelekea huko hotelini alipokuwa akiishi.
Muda ambao Mheshimiwa alikuwa akitoka ndani ya ofisi yake ni muda ambao ndani ya nyumba ya mtu yule muhimu sana katika shirika la serikali na pia idara nyeti kulitokea jambo la kustajaabisha sana, Mlinzi aliyekuwa yupo getini katika nyumba hiyo ndiyo aliweza kulishuhudia jambo kwa macho yake mawili kipindi linatokea. Yeye mwenyewe alipatwa na mshtuko mkubwa sana hadi akarushwa mita kadhaa kutoka kwenye eneo hilo alilokuwa amekaa. Ulikuwa ni mlipuko mzito sana ambao ulitokea katika sehemu ya chini ya nyumba hiyo ya ghorofa na ukaenda kuathiri hadi sehemu ya juu, mlipuko huo uliambatana na kurushwa kwa vioo vya nyumba hiyo kwa umbali mrefu baada ya madirisha kupasuka kwa nguvu sana. Mlipouko huo ulimrusha mlinzi hadi akaenda kujibamiza kwenye uzio wa ukuta wa nyumba hiyo, mlipuko huo uliathiti kabisa hata matairi ya magari ambayo yalikuwa ymeegeshwa jirani kabisa na nyumba hiyo. Mlipuko huo ulipotokea hata hakusikika kelele ya aina yeyote ndani ya nyumba hiyo ambao mabosi wa mlinzi huo walikuwepo, mlipuko huo ndiyo chanzo cha mkinzi huyo kuweza kushuhudia hali nyingine kabisa ambayo hakuwahi kuishudia katika kipindi chote cha maisha yake akiwa ni kama mlinzi katika sehemu tofauti hadi akafikia kuwa mlinzi wa ndani ya nyumba hiyo.
Baada ya kujibamiza ukutani kutokana na mshtuko uliotokana na mlipuko huo, alitulia papo hapo akiwa na maumivu sana hasa katika eneo la mgongoni ambalo alikuwa amegonga ukutani. Hakuwa hata na nguvu ya kunyayuka kutokana jinsi alivyokuwa ameumia . Alibaki akiwa ni mwenye kufumba macho kwa maumivu hapo chini alipokuwa ameanguka baada ya kujigonga ukutani. Alishindwa hata kuhema kawaida kwa jinsi alivyoumia hata sauti zilizopo jirani na eneo hilo alikuwa akisikia kwa tabu sana kama vile alikuwa ana masikio mabovu. Macho yake yalikuwa yenye kuona kwa tabu sana haswa kutokana jinsi alivyojigonga hapo ukutani katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku mgongo ukiwa ndiyo ulioathirika zaidi, hadi ving’ora vya gari la zimamoto vinasikika vikiingia ndani ya nyumba hiyo alikuwa akivisikia kwa mbali sana kama vile vilikuwa vipo mita nyingi zaidi kutoka pale alipokuwepo. Yote hayo ilitokana na kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko huo ambao umesababisha ajigonge sehemu mbalimbali za mwili wake, kuchanganywa na maumivu hayo ya eneo hilo alilojigonga ndiyo kulifanya hadi awe katika hali hiyo. Alikuwa ni mwenye kuhisi na kuona kile kilichokuwa kikiendelea karibu yake lakini hakuwa mtu mwenye uwezo wa kufanya chochote kile,hadi wanakuja watu wa huduma ya kwanza wanambeba katika eneo hilo na kumuweka kwenye kitanda cha wagonjwa yeye hakuwa na uwezo wowote wa kuwapinga au kuwaruhusu wamnyanyue.
Muda huo kwa upande mwingine kabisa gari ya kifahari aina Toyota landcruiser V8 ilionekana ikiingia kwenye hoteli moja maarufu sana, gari hilo liliingia hadi sehemu ya maegesho na kisha likasimama kwenye eneo hilo. Haikupita muda gari hilo lilizimwa, kuzimwa kwa gari hilo hakukuonesha kuwa kulikuwa na dalili yeyote ile ya mtu kushuka ndani yake. Ilipita dakika takribani tano haikuonekana dalili ya mtu yeyote kushuka ndani yake, bado hakukuwa na binadamua yeyote aliyekuwa akijali juu ya kutoshuka kwa mtu aliyekuwa yupo ndani ya gari hilo. Mazingira tu yaliyokuwa yakilishangaa hilo gari kama ilivyo msomoji unavyoshangaa jinsi ya kukaa kwa muda mrefu mtu aliyekuwemo ndani ya gari hilo bila kushuka, vilivyokuwa na hamu ya kuona mtumiaji wa gari hilo kushuka kama ilivyo kawaida yake akizima gari hilo bado viliendelea kuangalia pale kwenye gari hilo kumuona akishuka. Wanadamu waliokuwa wapo na mambo yao wala hawakushughulika kabisa katika kumtazama huyo mwenye gari kungojea ashuke, kimya ndani ya gari hilo kiliendelea kutawala kama ilivyokuwa limezimwa gari hilo baada tu ya kufika kwenye eneo la maegesho la magari hapo hotelini.
Muda mfupi baadaye wale waliokuwa wapo karibu na eneo hilo waliweza kushuhudia gari hiyo likivunjika vioo kukiambata na mlipuko mkubwa sana, gari hiyo lilirushwa juu kabisa lilipolipuka na kisha alikatua chini likabiringita na kwenda kuyazonga magari mengine yaliyokuwa yapo jirani nalo. Mayowe ya watu yalisikika baada ya kutokea mlipuko huo na kisha kila asiyekuwa na ustahimilivu aliamua kukimbia kabisa kwani waliingiwa na uoga mkubwa sana. Watu waliokuwa wapo ndani ya hoteli hiyo ya hadhi ya nyota tano hawakubaki hata mmoja kila mmoja alikimbia kutokana na hofu ya nafsi yake, hakuna aliyekuwa hapendi kuendelea kuishi duniani hivyo kusikia pamoja na kushuhudia huo mlipuko waliona ni ishara tosha ya kutaka kuporwa uhai wao ikiwa tu watabakia ndani ya eneo hilo. Ili kuyanusuru maisha yao iliwabidi wakimbie kabisa tena wakina mama ndiyo walikimbia huku wakipiga kelele kabisa.
Muda mfupi baadaye eneo hilo lilikuwa ni kimya kabisa kutokana na kutokuwa na watu huku gari lililolipuka likiwa linateketea, ilichukua karibu robo saa badaye ndiyo maaskari wa kawaida pamoja wale wa kikosi cha zimamoto wakawa wamewasili katika eneo hilo. Utepe maalum wa kuzuia watu wasiingie katika eneo hilo wakati uchunguzi ukiwa unendelea ndiyo ulizungushiwa ,askari wa jeshi la polisi kwa pamoja walianza kazi mara moja katika kulifanyia uchunguzi suala hilo na pamoja kutoa kile kilichokuwa kikistshiki kutolwa ndani ya eneo hlo la tukio.
MAKAO MKUU YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI
MAKAO MAKUU JESHI LA POLISI
DAR ES SALAAM
TANZANIA
Ndani ya ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania IGP Jumanne Mbwambo ambaye ndiyo alikuwa ana muda mfupi tu tangu apandishwe cheo na Mheshimiwa Rais, aliingia ofisini baada ya mkuu wa jeshi la polisi IGP Rashid Chulanga kumaliza muda wake.Muda huo IGP Mbwambo akiwa yupo ofisini kwake simu ya mezani iliita kwa mfululizo jambo ambalo lilimpelekea aipokee kwa haraka sana kwani mara nyingi sana simu huwa ni za muhimu sana, simu hiyo alikuwa akipigiwa kwa ajili ya kazi za kiofisi tu na inabidi aipokee kwani inakuwa na umuhimu wa kila jambo. IGP Mbwambo aliichukua simu hiyo na kuipokea kwa haraka sana na kuiweka sikioni mwake, alitulia kusikiliza mpigaji wa simu hiyo alikuwa akisemaje. Utulivu humuingia akipokea simu kutokana na kupokea simu ambazo huwa na taarifa tofauti kwa kipindi tofauti cha muda hivyo umakini ulikuwa unahitajika sana zaidi hata ya atembeavyo eneno lenye vumbi kulinda macho yake yasiathiriwe, alitulia kabisa na sikio lake moja ndiyo likawa linafanya kazi zaidi kuliko jingine katika kusikiliza taarifa hiyo.
“Jambooo” Aliitikia baada ya kusikia salamu ya kiaskari kutoka upande wa pili wa simu .
“Unasemaa!” Aliongea kwa mshangao mkubwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mwanausalama aliyempigia simu.
Uwezo mkubwa na upana wa njia za mawasiliano ilisababisha habari mbili tofauti zilizotokea kwenye sehemu tofauti kusambaa kwa kasi sana mithili ya moto wa kifuu hadi zikafika sehemu mbalimbali za nchi hii, polisi nao ambao waliokuwa hawana uaminifu katika kazi yao walivujisha tarifa hii mapema sana kwa watu wao wa karibu na kupelekea taarifa hii isambae kwa muda mfupi kwa kila mtu. Taarifa hiyo ndiyo ilikuwa imefika kwa IGP Mbwambo ndani ya muda ambao watu wa kawaida tayari ilikuwa imshawafikia, ilikuwa ni taarifa yenye kushtusha sana hasa kwa kuzingatia watu hao waliouawa ni watu walikuwa ni wazito sana ndani ya serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Watu waliokuwa na jina kubwa na wenye vyeo vikubwa katika sehemu tofauti ndani ya serikali, watu ambao mmoja alikuwa na vyeo viwili lakini hakuweza kujifahamu kabisa kimoja zaidi ya kukifahamu kile kinachojulikana na hadhira ya watanzania. Watu ambao walikuwa wakijulikana kutokana na kazi zao pamoja na mchango wao kwa watanzania ndiyo hao taarifa ilikuwa ipo mezani kwake. Hakika ilimchanganya kwa kutokea kwa vifo hivyo ndani ya muda ambao hakutarajia kabisa, kufa kwa mlipuko katika sehemu mbili tofauti ni jambo ambalo halikuwa la kawaida kabisa. Vifo vyao vyote watu hao vilikuwa vinalingana kabisa na ilimpelekea kabisa kuvihusisha kuviona ni vifo vilivyosababishwa na watu wa aina moja kutokana na jinsi vilivyotokea.
Mmoja alimtambua kabisa kuwa alikuwa anasubiria masaa mahcache tu aweze kuanza hatua ya awali ya kuanika cha ndani ambacho haakikupaswa kuanikwa nje kwa wahusika, mmoja alimtambua alikuwa ni mkuu wa shirika kubwa la kiserikali nchini . Alipofikiria nyadhifa zao hao watu hakuwa kabisa na hisia kuwa walikuwa wameuawa kwa sababu moja. Vuguvugu la kifo cha mmoja ambaye ni Mheshimiwa alihisi ni kutokana na kile ambacho alikuwa akienda kukizungumza leo, vuguvugu la pili hakuweza kabisa kuhusisha na kifo hicho kutokana na mtu huyo wa pili aliyeuawa ndani ya jiji la Dar es salaam kuwa hahusiki kabisa na sababu hiyo ya kifo hicho cha kwanza. Suala hilo lilimfanya akune kichwa hasa kutokana na hali hiyo iliyotokea na mwishowe aliamua, akiwa katika fikra hizo simu yake ya mezani iliita kwa mara nyingine jambo ambalo lilimfanbya asitishe fikra zote alizokuwa akiziwaza na macho yote akayaelekeza kwenye mkonga huo wa simu. Hakutaka hata kusubiri kwa sekunde kadhaa baada ya kuyaekeza macho hayo kulipo mkonga wa simu, haraka sana aliunyanyua mkonga huo na kuuweka sikioni mwake alipobaini kuwa simu hiyo ilikuwa ikitoka ndani ya jengo hilo tena kwa mtu ambaye alikuwa ni mkubwa wake kikazi.
“Ndiyo mheshimiwa…..nimezipata muda si mrefu nilikuwa nikizifikiria sana taarifa hizo muda huu….ndiyo mheshimiwa nitaagiza vijana sasa hivi waweze kufanya kazi….sawa nitakutaarifu” IGP Mbwambo aliongea na simu hiyo na alirudisha mkonga mahala pake baada ya simu hiyo kukatwa.
Baada ya kuuweka mkonga huo mahala pake alichukua simu yake ya mkononi kisha akagusa juu ya kioo akiwa ni mwenye kutafuta kitu ndani yake, hatimaye aliacha kugusa simu hiyo na aliipeleka moja kwa moja sikioni akionekana alikuwa akipiga simu kwa mtu mwingine. Baada ya simu hiyo kugusa tu shavu lake alitulia kimya sana mithili ya maji yanavyotulia mtungini, sikio lake moja hilo ambalo simu ilikuwa imeligusa lilikuwa limeweka umakini mkubwa sana kuliko sikio la pili jambo ambalo huwa ni kawaida sana anapokuwa anaongea na mtu muhimu sana akiwepo kikazi.
“Jeph njoo ofisini kwangu haraka sana uje na Mutonga” Baada ya hapo alikata simu na kisha akaiweka mezani akiwa ni mwenye kusubiria jambo liweze kutimia.
DODOMA
Muda huo tayari kamihsna wa polisi wa Dodoma John Faustin alikuwa tayari ameshatoa taarifa ya kila kilichotokea mkoani humo, Kamishna John alithibitisha kabisa kutokea kwa tukio hilo mkoani kwake na akatoa ahadi ya kushughulikiwa jambo hilo kwa haraka sana na jeshi la polisi ambalo lipo chini yake mkoani Dodoma. Baada ya kutoa ahadi hiyo mbele ya wanahabari aliondoka kwa haraka sana kwenda eneo la tukio kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea, alitumia muda mfupi tu akawa amefika eneo la tukio ambapo alikuta vijana wake wakiwa wanaendelea na kazi na umakini wao uliongezeka baada ya yeye kuwasili.
Alipokea heshima kutoka kwa maaskari tofauti ambao walikuwa wapo chini yake, baada ya hapo aliuliza juu ya kile kilichokuwa kikiendelea hapo. Kamishna John aliridhishwa sana na ufanyaji kazi wa vijana wake ambao walikuwa wameshafanya utafiki wa kila kitu, muda huo alikuwa yupo Mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi(ASP) ambaye ndiye aliongoza uchunguzi huo wote wa tukio hilo lilitokea.
“Afande haya mabaki ya bomu hili lililolipuka hapa hatujafikiwa kuyaona kabisa, ingawa kwa mlipuko mzito uliotokea inaonesha kabisa hilo lilikuwa ni bomu” ASP alieleza.
“Sawa, je gari hii ilivyoingia hapa hakushuka kabisa Mheshimiwa Bai?” Kamishna John aliuliza
“Hakushuka kabisa Afande kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili, gari lake lilipofika parking lilitulia tu hakukuwa na dalili ya kushuka mtu kabisa hadi muda ambao mulipuko unatokea”
“Ok uchunguzi ufanyike mara moja mimi ninarudi ofisini naomba matokeo hata ya vipimo vya daktari juu mwili wake uliokutwa ndani ya gari yanifikie mwenyewe pindi yatakapokamilika”
Baada ya hapo Kamishna John alipanda gari lake alilokuja na kisha akaondoka ndani ya eneo hilo, askari waliopo chini yake waaliokuwa wamebakia katika eneo hilo waliendelea kuchakarika na wajibu wao uliowafanya wawepo ndani ya hapo.
Muda huo upande wa ofisini kwa IGP Mbwambo baada ya kusubiri kwa kipindi cha muda wa dakika kadhaa vijana wawili waliokuwa wamevaa nguo za kiraia waliingia humo ofisini, vijana hao walipofika mbele ya IGP Mbwambo kila mmoja alitoa heshima kwa kubana mikono kisha akakamaa. IGP Mmbwambo aliwaruhusu wote kwa pamoja waketi kwenye viti viwili vilivyokuwa vipo mkabala na meza iliyokuwa ipo mbele yake. Vijana hao ambao walikuwa na miili ya wastani na mmoja alikuwa amevaa maavazi ya kileo sana na mwingine alikuwa amevaa suti, walikaa kwenye viti hivyo na kila mmoja akawa ameyaelekeza macho kwa IGP Mbwambo ambaye alikuwa amekaa akiwa anawasubiria kwa hamu kubwa waweze kuketi kwenye viti vyao.
“Jeph” IGP Mbwambo aliita huku akimtazama yule kijana aliyevaa mavazi ya kileo.
“Mkuu” Jeph aliitika
“Mutonga” IGP Mbwambo alimuita na yule kijana wake aliyekuwa amevaa suti nadhifu sana.
“Taarifa za matukio mawili tofauti yaliyotokea nafikiri mnazo, matukio ambayo yamepelekea kifo cha Mheshumiwa Bai na mkurugenzi mkuu wa NSSF. Jambo nililowaitia hapa ni kuhusu suala hilo” IGP Mbwambo aliongea na kisha akaweka kituo na kuwatazama vijana wake mmoja baada ya mwingine kama walikuwa wakimsikiliza. Baadaya hapo aliendelea, “Mheshimiwa huko tayari ameshacharuka na anahitaji kwa kina uchunguzi juu ya suala hili uanze, hii imenifanya niwaite nyinyi hapa”.
“Jeph wewe kuanzia muda huu unatakiwa uondoke kwenda Dodoma kuhakikisha suala hilo wahusika wanapatikana, wewe Mutonga utabaki hapahapa jijini Dar es salaam uhakikishe wahusika hawa wanapatikana haraka iwezekanavyo. Hii ni amri kutoka kwa Mheshimiwa na uharaka wa kazi hii umesababisha nisiwape kazi hii polisi wa kawaida, ndiyo maana nikaiweka chini yenu CID nina uhakika mtaikamilisha ndani ya siku chache tu” IGP Mbwambo aliendelea kuwaeleza.
“Ndiyo afande” Wote kwa pamoja waliitikia
“Sasa basi taratibu zote zipo tayari nafikiri muende ofisini kwa Mheshimiwa ana jambo jingine la kuwaeleza” IGP Mbwambo alihitimisha maelezo hayo ambapo vijana hao wa kitengo cha siri cha jeshi la polisi walinyanyuka, wote kwa pamoja walikakamaa kiheshima na kisha wakapeana mikono na IGP Mbwambo halafu wakaondoka ndani ya ofisi yake.
CID ambalo neno linalotokana na neno la kingereza ambalo kirefu chake ni ‘Criminal investigation department, hii ni idara ya siri ya jeshi la polisi ambayo hujihusisha na utafiti wa mkosa makubwa ya kiuhalifu. Idara hii maofisa huwa hawavai sare kabisa na wana muonekano wa tofauti kabisa na Askari wa kawaida, Maaskari wa ndani ya idara hii wengi wao huwa ni mapolisi wa kawaida wanaovaa sare kwa muda miaka miwili ndiyo huhamishwa kwenda idra hii baada ya kupata mafunzo zaidi tofauti na Askari wa kawaida ndani ya jeshi la polisi. Hawa ndiyo wanaouhusika upelelezi mzito ndani ya jeshi la polisi, pia ni mojawapo kati ya sehemu tatu muhimu sana ndani ya nchi hii wakiwemo na Usalama wa taifa, Millitary Intelligence na wao. Uharaka wa kazi hiyo ndiyo ulimfanya IGP Mbwambo aweze kuwatumia kwani hao watu walikuwa hawajulikani kabisa kwa raia wa kawaida, pia walikuwa ni wepesi sana katika kufanya kazi zisizoeleweka kabisa.
OFISI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI
Baada ya Japhet na Mutonga kutoka ndani ya ofisi ya IGP Mbwambo, moja kwa moja walielekea kwenye ofisi ya waziri wa mambo ya ndani ya jengo hilohilo, huko walikutana na waziri akiwa amekaa mkao wa kuwangoja wao tu waweze kufika kwenye eneo hilo aweze kuwapatia maelezo ambayo yaliwafanya awaite hapo. Jeph na Mutongta walipoingia tu ndani ya ofisi hiyo kila mmoja alitoa heshima kwa waziri kwa kukakamaa kiheshima. Wote kwa pamoja waliruhusiwa kuketi kwenye viti vilivyopo mkabala na kisha wakatulia kimya.
“Vizuri kwa kuwahi kufika vijana wangu, kila kitu nafikiri mshaelezwa na Mbwambo kilichobakia sasa ni mimi kuwapa maelezo muhimmu tu. Jeph wewe kwanza shika tiketi ya ndege nimeamua kukupatia ili uwahi kufika Dodoma na kazi hii uianze mara moja” Waziri aliongea huku akimpatia tikiti hiyo ambayo tayari ilikuwa imeshafika ofisini kwake.
“Asante Mheshimiwa” Jeph alishukuru
“Mutonga wewe hutoki ndani ya jiji hili ila unaweza kuwa msaada kwa mwenzako hivyo uwe tayari kwa lolote, wewe pokea hii hapa” Waziri aliongea huku akimpatia Mutomnga mkoba wenye vifaa muhimu vya kufanyia kazi.
“asante Mheshimiwa” Mutonga alishukuru.
“Nimeamua kuwapatia kila kitu cha muhimu na cha ziada katika kazi hii nikiwa kama askari mstaafu hivyo natambua sana ugumu wa kzai hiyo mnayoenda kuifanya, sasa basi nahitaji kazi hii imalizike haraka iwezekanvyo kutokana na uwepo wenu ndani ya miji ambayo matukio yalitokea. Vijana wangu nawaamini sana ndiyo maana mkateuliwa kwani hamkuwahi kuharibu kazi tangu muhamishiwe CID, natumaini kazi hii mbele yenu vijana wa kazi itakuwa imekwisha kabisa. Niwatakie kazi njema” Waziri alihitimisha na wote walinyanyuka kwenye viti vyao wakatoa heshima, walipeana mikono na Waziri na kisha kila mmoja akageuka nyuma na kutoka ndani ya ofisi hiyo.
Taarifa ya kifo hicho cha waziri ilifanya kikao cha bunge ambacho kilikuwa kikingojewa kwa hamu sana ndani ya siku hiyo kuweza kughairishwa, watu waliokuwa wakisubiiri kwa hamu sana kikao hicho walijikuta wakiingiwa na simanzi baada ya kupokea taarifa ya kifo cha Mheshimiwa aliyekuwa anakuja kuianza kazi yako nzito ambayo alipewa muda iweze kukamilika. Hiyo ndiyo ilikuwa habari kubwa kwa baadhi ya vituo vya redio na telvisheni ndani ya siku hiyo watanzania walimuona Mheshimiwa kama mtu shujaa kabisa aliyekuwa akijaribu kulitetea taifa lake, walilaani sana waliokuwa wamesababisha kifo chake ambacho hadi inafikia majira hayo ilikuwa ikiaminika alikuwa ameuawa kwa kutumia bomu la kutegwa. Mamia ya makundi ya watanzania walikuwa wamejikusanya wakiwa wanaongea suala hilo huku kila mmoj akiwa na hisia zake juu ya kulieleza suala hilo, ilikuwa ni huzuni sana na hata watanzania waliohojiwa na vyombo mbalimbali vya habari ambavyo viliwatembelea katika mitaa wanayoishi kusikiliza maoni yao walionesha hisia zao jinsi walivyohuzunishwa na suala hilo lililomkumba Mheshimiwa. Nyumbani kwa Mheshmiwa ambako alikuwa ametoka siku iliyopita tu kuja jijini Dodoma kulitawaliwa na vilio vya wanafilimia hao ndani ya jiji la Dar es salaam, hadi jioni ya siku hiyo unafika tayari watu walikuwa wameshaanza kuja hapo nyumbani kwake kuwafariji wanafamilia wake kutokana na kipindi hicho kigumu.
Giza la siku hiyo lilipoingia tu na jioni ikafukuzwa mbali na usiku uliokuwa ukitaka kuchukua zamu yake kwa haraka sana, Mutonga tayari alikuwa yupo ndani ya uzio wa nyumba ya Mkurugenzi mkuu wa shirika la mfuko wa hifadhi ya jamii Bwana Mabina. Muda huo utepe ulikuwa umezungushiwa ndani ya nyumba hiyo lakini kutokana na cheo chake na pia idara yake anayofanyia kazi alipita bila kizuizi chochote langoni mwa uzio huo ambapo kulikuwa na Askari aliyekuwa akilinda humo asiingie mtu wa kawaida ndani. Akili yote ya kikazi iliamka pindi tu alipoingia ndani ya lango hilo, macho yake ya umakini yalikuwa yakiangaza kila pande ya nyumba hiyo kama afanyavyo mgeni akiwa anaingia ugenini. Alipitiliza moja kwa moja hadi kwenye baraza la nyumba hiyo ambayo hadi muda huo ilikuwa ikionekana kama gofu kutokana na kuungua sana, barazani hapo Mutonga alitaka kuingia ndani ya nyumba hiyo lakini akasita na kisha akaanza kutembea kuzunguka nyuma ya nyumba hiyo huku akiwa makini kutazama mandhari ya hapo nyumbani ilivyo. Alitembea kuizunguka nyumba akiwa ni mwenye kutazama kila upande na hatimaye alirejea pale barazani, alipiga hatua kusogelea eneo la nyumba hiyo ambayo lilikuwa halina mlango kutokanana mlango wa nyumba hiyo kuvunjwa na mlipuko uliotokea. Macho yake yote yalikuwa yapo kwenye eneo hilo la mlango alipolifikia kwa muda wa sekunde kadhaa, aliporidhika kulitazama eneo hilo alitoa mipira ya mikononi mfukoni mwake ambayo aliivaa mikononi kisha akashika sehemu zenye mabaki ya mbao ambayo yalikuwa yamegeuka mkaa kabia baada ya kuungua.
Mutonga alipiga hatua kuingia ndani ya nyumba baada ya kumaliza kuyaangalia mabaki yaliyokuwa yapo mlangoni, alitokea kwenye sebule pana ya nyumba ambayo kimuonekano ilikuwa ni sebule moja ya kifahari lakini kwa muda huo ilikuwa ni kama gofu huku vitu vya ndani ya nyumba hiyo viliyokuwa vimejengwa kwa malighafi ngumu vikiwa vimebakia na vingine visivyoungua vikiwa vina rangi nyeusi kutokana na kupitiwa na mlipuko. Mutonga alitembea ndani ya eneo la sbule hadi kwenye kila kingo yake akiwa anaitazama kwa umakini sana, aliridhika kulitazama eneo lote pindi macho yake yaliyokuwa yapo makini sana ndani ya eneo kufuata kufuata yake aliyoishika mkononi alielekea ulipo mlango wa jikoni. Mlango wa sehemu maakuli ulimvutia sana kuutazama na akajikuta kabisa akivutika kuusogelea pia ingawa kimuonekano ulikuwa hauvutii kabisa kwa jinsi ulivyoungua, alijikuta akipiga hatua kuelekea eneo hilo la jikoni ambapo kulikuwa kumemvutia sana.
Mwanga wa kurunzi ukiwa upo mbele yeye nyuma hadi ndani ya chumba hicho cha jiko ambacho hakikuwa kisichotamanika hata kukitazama kwa mtu aliyekuwa akiyajua mandhari ya hapo jikoni kabla ya kutokea kwa tukio , Mutonga alibaki akiyatazama mandhari ya jiko hilo ambalo lilionekana lilikuwa ni la kisasa sana kabla hata halijakumbwa na tukio la kulipuka. Muale wa Kurunzi ulimsaidia kuona mambo mbalimbali yaliyokuwa humo jikoni ambayo mengine kwa asilimia kubwa yalikuwa na masizi ya kuungua, sehemu ya jiko ambazo hazikuwa zimejengwa kwa malighafi yenye kuungua na moto bado zilikuwa zimebaki majivu matupu huku zile zilizokuwa zimejengwa na miti migumu zikiwa hazina tofauti na mkaa. Mutonga akiwa humo jikoni aliweza kushuhudia mitungi mitatu ya gesi ikiwa imetoboa ukuta sehemu za mbele na nyuma sehemu za nyuma za mitungi hiyo zikiwa zimebaki humo ndani ya jiko.
Alipoona mitungi hiyo ndipo alipoweza kutambua kuwa mlipuko uliotokea ndani ya nyumba hiyo haukuwa mkubwa sana, mitungi hiyo ilimbainishia kuwa hiyo ndiyo iliyoongeza mlipuko humo ndani na kuufanya uwe mkubwa sana. Alinyanyua kichwa na kukishusha kuafiki mawazo yake hayo na kisha akatembeza Kurunzi kuangalia katika pande nyingine za ndani ya chumba hiko cha jiko. Hakuweza kushuhudia kabisa kitu kingine ndani ya jiko hilo, ilimbidi atoke humo jikoni baada ya kuona hakukuwa na cha maana. Alipomulika kurunzi yake sehemu ya mlangoni wakati wa kutoka alijikuta akisita baada ya miale ya kurunzi yake kutua mahali tofauti na alivyoingia. Miale ya Kurunzi kipindi anaingia akiwa yupo sebuleni aliweza kuliona jiko kwa ndani bila ya kuwepo kwa kizuizi chochote lakini muda huu hapo kwenye kizingiti cha jiko aliona kizuizi kilichokuwa kikizuia miale ya Kurunzi hiyo isiweze kufika sebuleni. Kizuizi hicho hakikuwepo kabisa na wala hakikuwa kimeinyima miale ya Kurunzi yake uhuru wa kufika mbele zaidi.
Kizuizi alichokiona mbele yake kilikuwa ni kizuiaji kilicho na uhai na chenye sifa sawa na yeye, Kizuizi hiko kilikuwa ni sifa za mafichoni tofauti na yeye tu ndiyo kilimfanya awe tofauti na yeye kwa hilo tu. Kizuizi hiko chenye mvuto kikiwa kimeacha asilimia kubwa ya vitu vyake vyenye mvuto wazi ndiyo kilionekana hapo mbele yake kikiwa kimezuia miale hiyo ya Kurunzi yake isiweze kufika mbele zaidi alipojaribu kumulika. Hakika alikuwa ni binadamu kama yeye tena mwenye jinsia ya kike tofauti na yeye, alikuwa amesimama mbele tu akimtazama yeye kama aliyekuwa akitarajia ujio wake mahala hapo. Mwanamke huyo alikuwa amevaa kaptula fupi sana ambayo iliacha sehemu ya mapaja yake yaliyojaa nje ndiyo alionekana hapo akiwa amesimama tena akimtazama yeye jinsi alivyokuwa akimuangalia. Alionekana wazi huyo mwanamke alikuwa akimtazama kwa muda mrefu sana tangu alipokuwa akimulika humo ndani kupekua lakini hakumuona hadi hapo alipokuwa akitaka kutoka humo ndani, Mutonga alishtuka san kutokana na ughafla wa ujio wa mwanamke huyo. Ilimchukua sekunde kadhaa kumzoea baada ya kumuona ni mwanadamua wa kawaida, pamoja na kumzoea huko bado alikuwa na maswali kichwani mwake juuu ya ujio wake mahala hapo ambao haukuwa wa kawaida kabisa. Hakukuwa na kiumbe yeyote aliyekuwa ameruhusiwa kuingia humo ndani na Askari aliyekuwa langoni lakini huyu mwanamke alifika hadi ndani haikueleweka aliingia vipi, kiupande mwingine aliona ni kama uzembe wa askari aliyekuwa akilinda hapo mlangoni. Ilimbidi apate uhakika tu wa huyo mwanamke kuwemo humo ndani, ndipo aweze kujua kuwa alikuwa humo ndani kwa muda gani na nani kamruhusu aingie.
“Unafuata nini huku?” Mutonga aliuliza
“Wewe hapo ndiyo nimekufuata na si kingine” Mwanamke huyo alijibu
“Hey usilete mchezo we binti hebu toka nje haraka iwezekanavyo”
“Sitoki mpaka nipate nilichokifuata”
“Ok unachokitaka ni nini we binti katulie na mumeo au bwana wako si huku kwenye kazi za watu”
“Roho yako tu si kingine maana inaonekana unafuatilia kile usichokijua mwanzo wala kati yake”
“Nini wewe?”
Swali lake hilo halikujibiwa hata kidogo kwani yule Mwanamke alifyatuka pale alipokuwa amekaa, alikuja na mapigo ya karate ya namna tofauti ambayo yalimuwia vigumu sana Mutonga kuyazuia yote. Mengi ya mapigo hayo yalimuishia mwilini mwake na kumfanya aende chini moja kwa moja. Kurunzi ambayo ilimuwezesha kumuona Mwanamke haikuwepo tena kwenye mkono wake tayari ilisharuka mbali sana na ikawa inamulika ukutani na si katika eneo hilo alilokuwepo ambapo ingemuwezesha kumuona huyo Mwanamke aliyempiga mapigo ya ajabu mengi. Giza nene lilikuwa katika eneo hilo alilokuwepo huyo mwanamke ambalo lilimzuia kabisa kuweza kumuona, akiwa yupo ndani ya Giza hilo Mutonga alishindwa kabisa kumuona Adui yake alikuwa yupo upande gani. Alijikuta tu akipokea kipigo cha haja ambacho kilimletea maumivu katika mwili wake ambayo yalimfanya hata atamani kupiga kelele. Alipofungua mdomo wake pale alipozidiwa na maumivu alijikuta akizuiwa, mikono ya Mwanamke huyo ilitua kwenye kinywa chake kumzuia huku akiendelea kumshushia kipigo. Kipigo kilidumu kwa muda mrefu ambacho kilimnyima kabisa Mutonga muda wa kujiteteta kwani uwepo wa giza ulikuwa umemnyima wasaa huo. Mwanamke huyo aliyekuwa akimpiga alionekana kabisa alikuwa akilimudu vyema giza hilo, hiyo ndiyo ilikuwa hatua kubwa aliyomzidi Mutonga katika mpambano huo. Ndani ya muda mchache tu baadaye Mutonga hakuwa na nguvu hata ya kuweza kusimama kutokana na kuelemewa na kichapo alichokuwa amepewa na huyo mwanamke, alikuwa hata hawezi kujihami kutokana na kipigo hicho. Hapo alibaki akiwa anahema tu kama mkimbiaji wa mbio ndefu asie na pumzi, alibaki akikodoa macho ndani ya giza hilo asimuone Adui yake aliyempa kipigo cha namna hiyo hadi akawa hajiwezi.
“Malkia wa kuzimu haingiliwi kwenye kazi yake hata siku moja, haya na wewe ungana na Bai pamoja na Mabina katika kuelekea kuzimu bila ya kupata wito kama wao” Mwanamke huyo aliongea na kisha mlio wa kuvunjwa kwa kitu chenye mvupa mlaini kilisikika.
Baada ya kushuka ndani ya ndege la shirika la ndege la Fastjet, Jeph hakutaka kupoteza aliamua kutoka ndani ya uwanja wa ndege wa hapo jijini Dodoma akiwa yupo na mkoba wake mdogo tu wa mabegani. Alikuwa ni mwenye kuvaa mavazi ya kileo kama ilivyo kawaida yake na alitembea kimaringo, macho yake yalikuwa yamefunikwa na miwani ya giza na alikuwa akitembea huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini na kuufanya mkato wa nywele zake uliowekwa kiujana zaidi kuonekana kwa mtu yeyote aliyekuwa akipita mbele yake. Miondoko yake ya kiujana zaidi ambayo huweka manjonjo mengi zaidi na kumfanya azidi kuvutia kila akitembea wala hakuiacha kabisa, ilikuwa ishajenga mazoea na sasa imekuwa ni tabia yake.
Alitoka hadi nje kabisa ya uwanja huo baada ya kupitia kila eneo ambalo lilikuwa na utaratibu maalum uliotakiwa kupitiwa, alipotoka hadi nje hakutaka kupoteza muda kabisa aliagiza Teksi na akaondoka ndani ya eneo la uwanja wa ndege. Teksi hiyo ilimpeleka moja kwa moja hadi katikati ya jiji la Dodoma ambako alifikia kwenye hoteli maarufu sana jijini hapo, alichukua chumba kwenye hoteli hiyo na moja kwa moja akaenda chumbani kwake akiongozwa na Mhudumu wa hoteli hiyo.
Alipoingia ndani ya hoteli hiyo haukupita hata muda mfupi mlango uligongwa, Jeph akiwa amevaa taulo tu alienda kuufungua mlango huo ambako alikutana na yule Mhudumu aliyemleta humo ndani kwa mara ya kwanza. Mhudumu huyo alikuwa na Bahasha nyeupe mkononi mwake ambayo alimpatia, Jeph aliipokea ile bahasha kisha akamtazama Mhudumu huyo wa hotelini usoni mwake kwa macho makali.
“Umeopata wapi hii?” Alimuuliza
“Kuna mkaka mmoja ameileta na ameteja hadi jina lako na chumba ulichokuwepo” Mhudumu alijibu na kupelekea Jeph agune kwani hakuwa amempa mtu yeyote taarifa za ujio wake ndani ya hoteli hiyo zaidi tu ya watu wa ngazi za juu waliokuwa wamempa kazi hiyo.
“Ok nashukuru” Ilimbidi amshukuru tu Mhudumu huyo kuweza kumuondoa ndani ya eneo hilo ndiyo aweze kuiangalia Bahasha hiyo ilikuwa na kitu gani ndani yake, Mhudumu huyo alipoondoka ndani ya eneo hilo aliitazama Bahasha kwa sekunde kadhaa kisha akaingia chumbani kwake na kufunga mlango.
Alienda kujitupa kitandani na kisha mikono yake ikashika sehemu ya kufungulia Bahasha aliyoletewa, aliivuta sehemu ya kufungulia bahasha hiyo ndani akakutana na bahasha nyingine iliyokuwa haitofautiani kabisa na bahasha ambazo walizipokea Mheshimiwa Bai na Mabina muda mfupi kabla ya vifo vyao. ‘WITO WA KUZIMU’ ndiyo neno lililokuwa lipo juu ya Bahasha ambalo lilimfanya afinye uso wake kama alikuwa akitazama kitu chenye umbo dogo kupitiliza. Taratibu alianza kushika sehemu ya Bahasha hiyo iliyokuwa imegandishwa kwa gundi imara na akaanza kuivuta, alijikuta akisita kuifungua baada ya kusikia mlio wa Simu yake ya mkononi iliyokuwa ipo sentimita kadhaa kutoka hapo alipo. Jeph aliiweka bahasha hiyo kando na akaichukua simu yake ya mkononi, aliitazama na akaona namba iliyokuwa ikimpigia iikuwa ni muhimu na aliipokea kwa haraka sana.
“Ndiyo Mheshimiwa….nimefika salama sasa hivi nipo hotelini napanga mipango….nashukuru Mheshimiwa sitakuangusha” Simu iliyokuwa imempigia ilikatika yeye akairudisha simu mahala pake ilipokuwa imejipumzisha baada ya yeye kuiweka na kisha akaishika Bahasha kwa mara nyinyine kabisa, kwa haraka kabisa aliifungua bahasha hiyo kwani alikuwa na shauku ya kujua kile ambacho kilikuwa kipo ndani yake.
Kishindo kizito kilisikika kwa ghafla nje ya hoteli maarufu sana jijini Dodoma, kishindo hiko kilitokea ghorofa ya pili ya hoteli hiyo kwenye chumba kimojawapo ambacho kilikuwa kimepata Mpangaji ndani ya muda mfupi tena ikiwa haijafika hata nusu saa tangu alipokilipia na kingia ndani ya chumba hicho. Mayowe ya watu waliokuwa wapo nje ya hoteli hiyo pamoja na ndani ya hoteli hiyo yalisikika kutokana na kushuhudia jinsi tukio hilo lilivyotokea. Walishuhudia mwanga mzito sana wa moto ukitokea kwenye dirisha la chumba cha hoteli ambao ulifanya hadi vioo vya dirisha kupasuliwa kwa nguvu sana na kuruka nje, watu waliokaa chini ya ghorofa la hoteli hiyo walikimbia wote baada ya fito la dirisha la hoteli hiyo kuwaangukia hapo chini walipokuwa wamekaa. Haikuchukua hata muda mrefu milango ya dharura ambayo hutumiwa kukiwa na moto ilisheheni watu waliokuwa ndani ya hoteli ambao wote kwa pamoja walikuwa wakihangaika kuweza kuokoa maisha yao kutokana na dhahama iliyotokea ndani ya hoteli hiyo ya kifahari. Wafanyakazi wa hoteli hiyo nao hawakuwa na ujasiri wa kuweza kuweza kubaki ndani ya hoteli yao, wote walijichanganya na wateja wa kawaida katika kukimbia balaa hilo katika jioni hiyo ambayo giza lilikuwa limeshaufukuza mwanga na kuchukua riziki yake.
Ilichukua dakika takribani tano ndiyo vikosi vya uokoaji vya jeshi la polisi viliweza kuwasili ndani ya jengo hili na kuanza kazi yake, muda huo kwa msaada wa wahudumu waliokuwa wapo mapokezi waliweza kumtaja aliyekuwa yupo ndani ya cumba hicho ambaye ndiyo alikuwa na muda mchache tu tangu achukue chumba hicho hadi anakumbwa na mlipuko wa bomu . Polisi kwa muda huo wengine walikuwa wakishirikiana na wenzao wa zimamoto katika kuhakikisha kuwa moto huo unazimika upesi iwezekanavyo, magari ya kuzima moto yalianza kazi kwa mara moja katika kuhakikisha kuwa moto huo unazimwa haraka iwezekanavyo waweze kuokoa yule aliokuwa yupo ndani ya chumba hicho.
Muda huo kwa upande mwingine kabisa ndani ya eneo la Mwandege kata ya Vikindu nje ya jiji la Dar es salaam katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, kijana asiyetambulika alileta barua katika nyumba moja ambayo ilikuwa ni ya kisasa ikiwa imejengwa mitaa kadhaa nyuma ya eneo la Mwandege Magengeni. Kijana huyo alijieleza kwa ufasaha kuwa alikuwa ametumwa kuleta barua ndani ya nyumba aliyoifikia, alimkuta mwanamke wa makamo akiwa ndiyo huyo aliyemfungulia mlnago wa nyumba aliyoifikia. Mwanamke huyo alipopokea maelezo ya kijana huyo aliikubali barua hiyo na kisha akamshukuru kwa kufikisha hapo. Kijana baada ya kuufikisha mzigo ambao alidai alikuwa ameagizwa hakutaka kupoteza muda aliondoka ndani eneo la hapo akarudi alipokuwa ametokea, alimuacha Mwanamke huyo ambaye aliambiwa mzigo huo ulikuwa ni wa mumewe akiutazma kwa shauku kubwa sana. Akiwa bado yupo kwenye lango kuu la magari la ndani ya nyumba yake aliishika Bahasha nyeupe aliyoipokea ambayo haikuwa na alama yeyote ya uchafu akaifungua, wahka wa kutaka kujua kle kilichokuwa kipo ndani ya Bahasha ndiyo ulimjaa huku akisahau kabisa kuwa Bahasha aliyoipokea haikuwa ikimuhusu kabisa zaidi ya yeye kuwa mfikishaji ujumbe kama yule Kijana aliyemletea. Mwanamke huyo kwakuwa muda huo mume wake aliyepaswa kuipokea Bahasha hakuwepo alijikuta akiifungua Bahasha isiyomuhusu akakutana na Bahasha nyingine ndani, kiherehere kilimzidi akajikuta akiisoma Mbebeo wa barua aliokutana no kwa ndani ambao ulimfanya azidi kuwa kiherehere akajikuta akituliza macho yake kwenye Bahasha nyingine kabisa. Aliyasoma maandishi aliyokuwa yapo juu yake akiwa na macho yenye umakini mkubwa sana akajikuta akitokwa na mguno,pamoja na mguno huo alioutoa baada ya kusoma maandishi ya juu ya Bahasha hiyo ya pili iliyokuwa ipo ndani ambayo ilikuwa na mstari ya rangi nyekundu kama Bahasha zilizowahi kuwafikia Mheshimiwa Bai na Mabina. Bado hakusita kabisa kuifungua kabisa bahasha hiyo yeye ndiyo alipatwa na hamasa ya kutaka kuifungua wala hakujali kabisa uzito wa maneno hayo yaliyokuwa yapo juu ya bahasha yenyewe pamoja na mhuri wake wa kutisha. Hakuwahi kuiona pia stempu kama hiyo iliyokuwa imebandikwa juu ya bahasha hiyo lakini hilo hakujali kabisa yeye akili yake yote ilikuwa ipo kwenye kuifungua bahasha hiyo tu na si vinginevyo.
Alishika bahasha hiyo kwa wahaka mkubwa sana wa kuifungua kabla ya mume wake hajarudi kwani hakuwa ameenda mbali kabisa, uwepo wa mume wake ulimfanya aharakishe katika kuifungua kwa kuhofia huenda anaweza kumkuta na kwkuwaa hajajua kilichomo humo ndani yake wala kukisia. Papara ya kujua kile kilichokuwa kimo ndani ya mzigo uliomfikia ilikuwa ikimsumbua sana na wala hakuhofia kabisa kuwa papara hiyo ingeweza kumfanya hata apatwe na kile ambacho hakuwahi kupatwa nacho katika maisha yake yote. Yeye alichojali ni kuifungua tu hiyo na kuangali ndani, wahka huo wa kuangalia kile ambacho kilikuwa hakimuhusu ulimfanya hata asahau tahadhari aliyowahi kupewa na Mume wake juu ya vitu kama hivyo vikija ndani ya nyumba hiyo ikiwa yeye hayupo ndani ya nyumba hiyo. Mwanamke huyo alishawahi kuonywa kabisa kuwa asifungue kitu kitakacholetewa yeye ikiwa hamjui mletaji, onyo hilo alilipuuzia kabisa na wahka wa kutaka kujua kilichomo humo ndani ndiyo ukawa umelitangulia hatua kadhaa mbele onyo alilowahi kupewa na Mume wake. Alijikuta akiifungua kwa haraka na hata kabla hajaona kilichomo ndani yake mwanga mkali ulitoka ulitoka ndani yake,hata kabla sekunde haijafika alijikuta akirushwa kwa nguvu huku akiteketea kwa moto na kwenda kujibamiza sehemu ya juu ya lango hilo na kisha baadhi ya viungo vyake vikatawanyika na kuruka upande tofauti. Huo ndiyo ulikuwa ni mwisho wa Mwanamama huyo aliyekuwa na wahka wa kufungua kile kilichokuwa hakimuhusu, mdharau mwiba mguu huota tende na ndiyo hayo yaliyomkuta hapo mlangoni mwa nyumba yake umbali wa mita kadhaa kutoka mahali nyumba yake ilipo.
Asubuhi iliyofuata ndiyo taarifa za vifo vyote vilivyokuwa vimetokea usiku uliopita viliweza kuzagaa na kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi tu, muda huo tayari IGP Mbwambo alikuwa ameshapokea taarifa ya kufariki kwa vijana wake ambao hawakuwa na hata saa ishirini na nne tangu awapatie kazi ya kwenda kuifanya. Tangu aipate taarifa hiyo hakuwa na amani kabisa na kichwa chake kilivurugika. Hakuelewa kabisa kwanini watu wa aina moja walikuwa wakisababisha mauaji hayo ndani ya sehemu tofauti za miji ya nchi ya Tanzania, vifo vya watu wawili waliokuwa sehemu tofauti kwa bomu na pia kifo cha kijana wake aliyekutwa amevunjwa shingo ndani ya nyumba ya Mabina vilimfanya achanganyikiwe kwa muda alipokuwa ameipokea taarifa akiwa yupo ofisini.
Tayari kabisa alikuwa ameshapokea simu ya Waziri wa mambo ya ndani pamoja na Rais Zuber Ameir juu yajambo hilo,tishio la kigaidi ndani ya nchi hii ndiyo lilikuwa lipo ndani ya kichwa chake hakuwaza kabisa jingine juu ya kutokea kwa vifo hivyo. Watu kufa vifo vya aina hiyo tena katika muda ambao Tanzania ilikuwa na mahusiano mazuri sana na mataifa mengine na wala haikuwa na ugomvi na nchi yeyote, wanausalama wa jeshi la polisi waliokuwa wakitumiwa kwa ajili ya kazi nzito kama hizo na hata kufanya utafiti wa matukio ya kigaidi ndiyo hao walikuwa tayari wameshauawa ndani ya siku hiyohiyo waliyokuwa wamepewa kazi iliyokuwa ikihitajika kukamilishwa haraka iwezekanavyo. IGP Mbwambo alisita kabisa moyoni katika kutoa wanausalama wengine waende kufanya kazi hiyo kwani alikuwa alihofia kuweza kupoteza zaidi vijana wake aliamini kabisa kuwa suala hilo halikuwa ndani ya uwezo wao kabisa. Alijishauri sana na hatimaye alitaka kupiga simu lakini alisita baada ya kuwahiwa na mlio wa simu yake ya mezani hiyo aliyotaka kuipiga, ilimbidi aipokee simu hiyo kwa haraka sana.
“Ndiyo Mhehimiwa……sawa nakuja sasa hivi” Aliongea baada ya kusikiliza agizo alilopokea kwenye simu hiyo, ilimbidi atoke kwa haraka ndani ya ofisi yake kuwahi huko alipokuwa ameitwa kwani ilikuwa ni amri ya Mkubwa kuliko wote.
BAADA YA ROBO SAA
IKULU
MAGOGONI
DAR ES SALAAM
Ndani ya chumba cha mkutano ndani ya Ikulu Rais Zuber alikuwa ameshaitisha kikao cha haraka sana kutokana na hali iliyokuwa ikitokea ndani ya Tanzania katika sehemu tofauti. Wazri mmoja,wanausalama watatu pamoja na raia mmoja kufa katika ndani ya siku moja katika vifo vilivyokuwa vikihusiana na ndiyo suala ambalo lilimfanya kwa haraka sana Rais Zuber aitishe kikao hicho cha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini. Mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa Professa Moses Gawaza, Mkuu wa jeshi la polisi IGP Mbwambo, Mkuu wa majeshi nchini Jenerali Marwa, Mnadhimu mkuu wa jeshi nchini Luteni Jenerali Belinda na pamoja na Rais Zuber mwenyewe ndiyo walikuwa wahudhuriaji wa kikao hicho cha dharura ndani ya Ikulu.
“Jamani hii sasa ni too much haiwezekani ndani ya siku moja watu muhimu ndani ya serikali yetu wateketee bila ya sababu. Ni siku nyingi zimepita tangu ubainike wizi wa mabilioni la shilingi katika mamlaka ya mapato, Tanesco, bandarini na katika mapato ya mgodi wa almasi uliogunduliwa Dodoma. Mapato haya yangeweza kuisaidia wanafunzi wa ngazi zote nchi nzima kusoma bure na hata wananchi kupata matibabu bure, lakini kutokana na walafi wa watu wachache waliopo ndani ya serikali yangu mapato hayo yameishia ndani ya matumbo yao. Iliundwa kamati nafikiri baadhi yenu mlikuwa hamjui kuwa kamati hiyo ilikuwa ikiwahusu kina nani zaidi ya kuwajua kuwa ilikuwa ikiwahusu mawaziri wawili pamoja na mbunge mmoja, ilipewa jukumu la kufanya utafiti wa kila kitu kwa muda wa mwezi mmoja tu na kisha ripoti hiyo iwasilishwe bungeni na wahusika wachukuliwe hatua. Sasa basi napenda mtambue kuwa kamati hii haikuwa peke yake katika kufanya kazi hii, bali vijana wangu waliopo chini ya Moses hapa walijumuika nao katika kufanya uchunguzi huo. Vijana hao ndiyo waliaandaa ripoti nzima ya uchunguzi huo na kisha ikawasilishwa kwa kamati iliyoteuliwa kuikamilisha kazi hii,kundi hili liliongozwa na Mabina mkurugenzi wa NSSF na msadizi wake Jama Wa Majama” Rais Zuber aliongea na alipofika hapo aliweka kituo akawatzama wote kama walikuwa wakimsikiliza na kisha akaendelea.
“Kundi hili lilifanikisha kufanya uchunguzi wao na kila Mhusika tayari alikuwa ameshawekwa kwenye faili na wakawasilisha kwa Bai ambaye ndiyo kiongozi wa kamati maalum iliyoundwa, faili hilo lilipomfikia Bai hakuchukua muda aliuawa kwa bomu. Watafiti wakuu wa hilo suala mmojawapo ambaye ni Mabina nafikiri mnatambua kabisa kuwa hatunaye duniani naye kauawa kwa bomu, siku hiyohiyo mke wa Jama naye kauawa kwa bomu akiwa yupo getini tu mwa nyumba yake. Hilo suala liliingia pengine baada ya vijana wa CID wa kuaminika kuaawa ndani ya siku moja katika miji tofauti, hapa inaonekana wazi kuwa kuna mtu anatuzunguka na si vnginevyo. Nimewaita hapa ili niwasikilize na nyinyi juu ya suala hili” Rais Zubber aliongea na kisha akaketi chini, muda huo simu ya Moses iliyokuwa ipo mezani ilitetemeka mara tatu kuashiria kuwa ulioingia ulikuwa ni ujumbe mfupi. Moses aliufungua ujumne huo na kisha akausoma ambapo aliishiwa nguvu kabisa alipoumaliza ujumbe huo, alijikuta akinyoosha mkono juu baada ya kuumizwa alipousoma huo ujumne na kupelekea Rias Zuber amruhusu azungumze.
Moses alisimama kisha akakamaa kiheshima kumpa heshima yake Rais Zuber na kisha akaongea, “Kwanza napenda niwape taarifa mpya ambayo imenifikia sasa hivi kupitia simu ayngu ya mkononi,waziri aliyesalia wa kamati maalum pamoja na wabunge wote wameuawa kwa bomu ninavyoongea hivi sasa”
Taarifa hiyo iliwamfanya kila mmoja aliyekuwa humo ndani kushtuka na kuona kuwa nchi ilikuwa ipo kwenye hatari kubwa sana, wote walisikitika kwa kipindi cha muda mfupi na kisha wakanyanyua macho yao kumtazama Moses aliyewapa taarifa hiyo.
“Vijana wote waliokuwa wakifanya utafiti chini ya Mabina nao hawapo duniani wameuawa kwa namna hiyohiyo, aliyesalia ni Jama tu ambaye hajulikani yupo wapi hadi sasa kwani nyumbani kwake ametoweka baada ya kupokea simu iliyokuwa imemuambia angeletewa Wito wa kuzimu hapo nyumbani kwake. Majirani zake wamesema ametekwa na watu wasiojulikana lakini yeye amepiga simu kwa Secretary wangu na kumpa taarifa kuwa yupo salama ila hajataja mahala alipo” Moses aliendelea kueleza na watu wote ndani ya chumba hicho cha mkutano walitulia kumsikiliza.
“Mheshimiwa Rais, na wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini napenda kusema neno lifuatalo. Suala hili limefikia katika ngazi ambayo si ya jeshi la polisi tena bali ni ngazi ya Usalama wa taifa pamoja na Millitary intelligence maana hivi ndiyo vyombo vynye dhamana ya kuilinda nchi yetu hii dhidi ya mambo kama hayo. Hivyo kazi hii haipaswi kushughulikiwa na chombo cha kuhakikisha sheria zinafuatwa ndani ya nchi bali ni vya usalama wa nchi, hivyo basi suala hili lipo ndani ya uwezo wetu na naamini kabisa hadi kufikia hivi sasa suala hili litakuwa limeshafika mikononi mwa EASA hivyo napenda jeshi la polisi likae kando na liwe linatoa ushirikiano na si kujiingiza moja kwa moja kwani kufanya hivi nikuendelea kupoteza vijana wa jehi hilo. Ni hayo tu” Moses alipomaliza kuongea maneno hayo aliketi kwenye kiti chake.
“Daddy ona ona nimeweza na mimi kutengeneza kite, ngoja niirushe kama wewe” Mtoto mdogo alimuambia baba yake wakiwa wapo jirani kabisa na bwawa la kuogelea ndani ya nyumba ya kisasa sana.
“Woow! Thats my boy upo very sharp, umenishinda hadi mimi baba yako” Baba mtu ambaye alikuwa ni kijana mtanshati sana aliongea huku akimkumbatia mwanae na kumbeba kiupendo zaidi.
“Daddy nikufundishe na wewe kabla mammy hajaja hapo na kukucheka umeshindwa kutengeneza wakati mimi nimeweza”
“Enhee! My boy umeongea nifundishe fasta kabla hajarudi yule ameenda kufuata icecream tu, akirudi atanicheka”
“Ok Daddy” Mtoto huyo aliitikia na kisha baba yake akamshusha chini, kwa haraka mtoto huyo alianza kutengeneza Kishada cha baba yake lakini hakumaliza kwani sauti ya Mama yake akicheka ilisikika na kumfanya aache na kumuangalia.
“Loh! Yaani wewe Nor huna haya kabisa yaani unampa Jerry ndiyo akutengenezee Kite. Hiloooo! Mtoto anakushinda” Alitokea Mwanake akiwa amevaa mawazi ya kuogelea ambapo alikuwa amejifunga mtandio kiunoni na sehemu ya juu ipo wazi.
“Mummy usimcheke Daddy hawezi kutengeneza namsaidia, I love him” Jerry aliongea
Mwanaume huyo aliyekuwa akisaidiwa kutengeneza Kishada na mtoto wake hakuwa mwingine ila ni Norbert Kaila akiwa na Norene mpenzi wake wa siku nyingi pamoja na Mtoto wao nyumbani kwao katika bwawa la kuogelea, alikuwa ndiyo ana siku kadhaa tangu arudi kwenye kwenye kazi nyingine ya kijasusi nchini Burundi alipoenda kushirikiana na Jasusi mwenzake Allison Frank ambaye alishirikiana naye katika kisa cha JINAMIZI pia ndani ya nchi ya Tanzania, muda huo alikuwa yupo mapumzikoni yeye na mpenzi wake ambaye ni jasusi mwenzake aliyekuwa maepewa likizo na yeye. Ulikuwa ni muda wa kufurahia yeye na familia yake na alikuwa yupo ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu mfululizo hakuwa ametoka nje kabisa, alichojali yeye ilikuwa ni kufurahia na familia yake katika muda huo ambao alikuwa amepewa na mkuu wake wa kazi. Ulikuwa ni muda ambao alikuwa akiusibiri kwa hamu sana aweze kupata na sasa ndiyo huo, hakutaka autumie kimakosa kwani alitambua familia yake nayo ilikuwa ikitamani sana muda huo upatikane aweze kukaa nao.
“Haya mtu na baba yake” Norene aliongea
“Na utuache kabisa, Jery mwanangu nitengenezee fasta kubwa kabisa kushinda hiyo Kite ya Mummy wako” Norbert alidakia.
“Ok Daddy” Jerry alijibu huku akiendelea kutengeneza Kishada kwa ajili ya baba yake, kamba ya Kishada hicho alichokuwa akikitengeneza ilipeperuka kwa bahati mbaya na ikapelekea anyanyuke aikimbilie huku wazazi wake wakiwa wanamtazama wakiwa wana furaha sana.
Muda huo Jerry alivyonyanyuka tu kwenda kufuata kamba ya Kishada alichokuwa akikitengeneza, ndiyo muda ambao simu ya mkononi ya Norbert iliita na kumfanya aitupie jicho lakini kabla hajafikiria hatua ya kuipokea tayari Norene alishaipokea na kuiweka sikioni.
“Mkuu….. ndiyo huyu hapa” Norene aliongea na kisha akampatia simu Norbert na kumpa ishara ya kijasusi zaidi.
“Heshima yako mkuu…..sawa muu nipe dakika kumi na tano tu nitakuwa hapo ofisini” Norbert aliongea na kisha simu ikakatwa, aliiweka simu pembeni na kisha akashusha pumzi kwa maneno aliyoyasikia.
“Vipi Nor mbona hivyo?” Norene aliuliza
“Haki ya Mungu hii kazi ni balaa yaani nimetoka Brundi majuzi tu sasa hivi naitwa kwa ajili ya kazi nyingine, muda wa kukaa na familia hamna kabisa yaani”
“Nor muhimu kufuata majukumu ila naomba uwe makini sana najua unamuona Jerry alivyo mdogo pale bado anahitaji malezi yako”
“Hilo usihofu ngoja niwahi ofisini nikamsikilize”
Norbert kwa haraka alinyanyuka mahali alipokuwa amekaa kisha akaingia ndani, alitumia muda wa dakika takribani tano akwa amemaliza kujiandaa amako alitoka akamkuta Jeery akiwa ameshamaliza kutengeneza Kishada alimchomuagiza
“Daddy look” Jeery aliongea huku akimuonesha Baba yake, Norbert alipoona kishada alichomuagiza kilikuwa kimekamilika alimnyanyua juu kwa furaha na kisha akawa anakiangalia Kishada alichomtuma amtengenezee.
“Its so nice my boy, mpe Mummy aniwekee ninaenda kukuchukulia zawadi nikirudi tu ninaanza kukichezea” Norbert aliamua kumdanganya mtoto wake na kisha akamshusha na kumuacha akienda kwa Norene.
“Byee daddy” Jerry alimuaga huku akimpungia mkono, muda huo Norbert alikuwa akichangamka sana kuelekea kwenye maegesho ya magari hapo nyumbani.
“Byee” Alijibu huku akikazana kuelekea kwenye moja ya magari yaliyokuwa yapo hapo eneo la maegesho ambalo halikuwa mbali sana kutoka kwenye eneo ambalo lilikuwa na bwala la kuogelea.
“Mheshimiwa Rais hata mimi sishauri kabisa vijana wa jeshi la polisi waingie kwenye hii ishu, wao wawe wanatoa msaada tu mdogo ukihitajika” Jenerali Marwa aliongea kisha akaketi kwenye kiti chake, muda huohuo IGP Mbwambo naye alinyoosha mkono.
“Ndiyo Mbwambo” Rais Zuber alimruhusu, IGP Mbwambo alipopokea ruhusa hiyo alisimama na akatoa saluti kwa Rais Zuber.
“Mheshimiwa Rais sipo tofauti na wenzangu kutokana na hali hii ilivyo, vijana waliopotea kwenye kadhia hii ni wa kitengo cha CID na ndiyo kitengo chenye uwezo mkubwa ndani ya jeshi la polisi. Sasa basi haina haja ya kumaliza vijana wengine ikiwa vijana wenye uwezo mkubwa kuliko wao wapo ndani ya nchi hii wapo, mimi nipo tayari kutoq msaada tu ambao ni lazima utoke kwangu na vijana wangu tu. Hili suala nimeliacha kwa wenzangu” IGP Mbwambo aliongea na alipomaliza alikaa chini.
“Vizuri sana je kuna mwenye la ziada?…….. Ok sasa basi kuanzia hivi sasa vijana wa Usalama wa taifa na wa Millitary intelligence waingie kazini maana inaonekana hili kundi kubwa sana hivyo kikosi kiongezwe , sina la ziada ni hayo tu” Rais Zuber aliongea akatoka ndani ya chumba hicho cha mkutano akiwaacha wakuu hao wa vyombo vya ulinzi na usalama wakitazamana usoni mwao kila mmoja kutokana na agizo hilo la muda ambalo lilikuwa la ghafla sana.
Hakuenda tofauti na alivyotoa ahadi yake kwa mkuu wake wa kazi, Norbert ndani ya dakika kumi tu tayari alikuwepo nje ya hoteli ile ambayo ilikuwa ndiyo ina ofisi za EASA tawi dogo la Dar es salaam maeneo ya Ilala mtaa wa Lindi. Alishuka akapitiliza mapokezi ambako aliwakuta wasichana ambao aliwazoea kuwakuta. Siku hiyo kutokana na haraka aliyokuwa nayo aliwapungia mkono tu na kisha akaingia kwenye lifti kwa haraka sana, lifti hiyo ilishuka chini hadi kwenye sehemu ambayo ofisi zao zipo ikasimama. Alishuka kwenye lifti hiyo na kisha akaanza kutembea kuufuata ukumbi mwembamba ambao ulimpeleka hadi eneo lenye mlango ambao ulikuwa na sehemu ya kuweka alama ya mkono, hapo aliweka kiganja chake cha mionzi ya kijani ilitokea kwenye eneo hilo na kisha mlango huo ukafunguka huku ukitaja maneno ya kumkaribisha kupitia spika za tarakilishi iliyokuwa imeunganishwa hapo. Norbert aliingia ndani na mlango huo ulijifunga na kisha alianza kutembea akipita vyumba mbalimbali vya ofisi ambako kulikuwa kuna wafanyakazi aliwasalimia kwa uchsngsmfu.
Norbert alienda hadi kwenye mlango mlango uliokuwa na maandishi yaliyosomeka ‘CE’, aliufungua mlango huo akaingia ndani kwenye ofisi ambayo alizoea kumuona Norene. Ndani ya ofisi hiyo alimkuta Msichana mwingine ambaye hakuwa mgeni kabisa kwake ambaye alikuwa hapo kutokana na Norene kuwa likizo, Msichana huyo alikuwa akifahamiana naye sana.
“Naona wewe kijogoo umekuja leo, mke wako umemkosa” Msichana huyo alimuambia
“Kwa akaliaye kiti hicho siku zote ni mke wangu sasa sijamkosa huyo hapo nimemkuta” Norbert aliongea na yeye
“Loh! Lione hivi ukijogoo utaacha lini wewe?”
“Simba akiacha kung’ata na mimi ndiyo nitaacha”
“Na huyo mkeo ana kazi nakuambia”
“Si useme tu wewe ndiyo una kazi sana kuwa na mume kama mimi maana nimekuambia kuwa anayekalia hicho kiti hapo ni me wangu”
“Ha! Ha! Babu wee hapo umenikosa, kwanza ingia huko mkuu anakusubiria kwa hamu sana”
“Doh! Na Mzee wenu huyu nakuambia bora astaafu akapumzike maana ananishtukiza kila kukicha”
“Ndiyo raha ya kuwa Secret service hiyo, acha uionje. Ingia anakusubiri kwa hamu sana”
Norbert alipoambiwa maneno hayo alisogea kwenye mlango uliokuwa upo pembeni ya mlango wa chumba cha Katibu Mukhtasi, aliufungua mlango huo akaingia ndani ambapo alikutana na CE kama kawaida yake akiwa yupo anamsubiria kwa hamu kubwa. CE alipomuona Norbert yeye aliangalia saa yake ya mkononi na kisha akamtazama usoni, Norbert alitoa heshima hapohapo kwa mkuu wake huyo wa kazi na kisha akasogelea kiti kilichokuwa kipo hapo mbele yake akakikalia.
CE alimtazam Norbert kwa mara ya pili na kisha akaitazama saa yake ya mkononi halafu akasema, ” dakika tatu zaidi umechelewa kisa kuongea na mke wako mwingine hapo mlangoni, N001 wanawake ni sumu mbaya sana kwenye kazi zako”.
Maneno hayo yalipita tu bila ya kujibiwa na Norbert kwani alikuwa akiuona ni wimbo aliokuwa akiiimbiwa kila siku na mkuu wake huyo tangu aanze kazi hiyo, alifikia hata kuhamishwa makzi na kupelekwa uswahilini akitegemewa angeweza kuacha hiyo lakini hakuiacha. Maneno hayo yalikuwa ni maneno ambayo alikwisha yazoea kutoka kwa Mkuu wake, hakuyajibu hata siku moja alimuacha alalamike na kisha atakaponyamza aweze kumuambia kile kilichokuwa kimemfanya amuite hapo kwani kuitwa kwake namna hiyo kwa ghafla sana huwa kulikuwa na jambo ambalo lilikuwa limeambatana na wito huo.
“NOO1 je unajua kilichomkuta Bai,mke wa Jama,maCID wawili wa kuaminika na pia vijana wa usalama wa taifa waliokuwa na kazi maalum ya kuandaa ripoti ya kamati ya Bai?” CE aliullza
“Ndiyo nafahamu kutokanaa na wigo mpana wa vyombo vya habari” Norbert alijibu
“Sasa basi suala hilo linawigo mpana tofauti unavyofikiria na pia na sisi limetukumba, Open service wa shirika letu wa nchini Kenya walishirikiana sana na vijana hawa wa TISS katika kuandaa ripoti kwani kuna kitu ambacho kilikuwa kinahusiana sana na nchi hiyo katika ripoti yaoo. Nao katika muda tofauti wameuawa kwa bomu na haijulikani mtu anayeawaua ana mkono mpana kiasi gani” CE aliongea na kisha akamtazama Norbeet kama kweli alikuwa yupo pamoja naye, alipoona yupo pamoja naye alifungua faili lililokuwa lipo hapo mezni mwake na kisha akapitisha macho juu ya faili hilo.
“Huu ni utafiti wa mwanzo kabisa ndani uliofanywa na Open service, sasa kila kitu ndani ya tukio hilo unahitajika wewe ndiyo ukimalize ukiwa ni Secret service pekee uliyebaki bila kazi. Nimeamua kuvunja mapumziko yako kwa ajili ya hili kwani N002,N003,N004,N005,N006 wa daraja moja na wewe wote wana kazi nje ya nchi hii hivyo uliyebaki ni wewe tu. Hatuwezi kuona taifa linaanza kukumbwa na tishio la kigaidi wakati wewe upo ukiwa umejipumzisha tu, N001 nahitaji uingie kazini mara moja vifaa vingine utavichukua hapo kwa mke wako wa pili sina la ziada. Nakupa siku kumi tu kuanzia leo hilo suala liwe tayari ” CE alihitmisha na kisha akamkabidhi faili hilo Norbert ambaye alilipokea kisha akasimama wima na akaatoa heshima, aligeuka nyuma na kisha akaanza kupiga hatua taratibu kutoka ndani ya ofisi hiyo.
“Norbert” CE alimuita kwa jina lake halisi pale alipotaka kushika kitasa cha mlango baada ya kuufikia, Norbert aligeuka nyuma alipoitwa jina lake hilo kwani haikuwa jambo la kawaida kabisa kuitwa hivyo.
“Umekua sasa hivi,fanya uwezavyo umuoe Norene uachane na ukapera maisha yanaenda haya. Unaweza ukaenda” CE alimuambia na Norbert alitoka humo ndani baada ya kumpa tabasamu hafifu akionesha alikuwa ameuridhia ushauri wake alioutoa kwake.
Norbert alitoka hadi nje ya ofisi iyo akaelekea hadi kwenye ofisi ya Katibu Mukhtasi wa CE, alimkuta akiwa anaendelea na kazi akiwa hajutambua ujio wake mahala hapo. Baada ya kuona hivyo alinyata hadi karibu yake na kisha akamgusa maeneo ya fumbatio na kupelekea Msichana huyo aruke sana na kisha akageuza macho na kumtazama.
“Nor bwana ushaanza mambo yako nina kazi mwenzio” Alilalamika kwa kitendo hicho alichofanyiwa.
“Oooh! Hata mimi nilikuwa na kazi na ndiyo hii naianza hapa” Norbert alijibu kimafumbo na kupelekea Msichana huyo asimuelewe hata kidogo.
“Sasa kazi yako ndiyo utake kuniharibia yangu”
“Kazi yangu naifanya kwako tu yaani na ndiyo hivi nimeanza”
“Looh! Lione ndiyo unachowaza hiko tu, hebu twende nikakupe vitu vyako”
“Poa usisahau na kile nilichokuwa nakitaka hapa nikaanza kukigusa”
“Muone jogoo pori wewe” Msichan huyo aliongea baada ya kuomuona Norbert alizidi kuongelea mambo ya gwaride lisilo rasmi tu badala ya kuzugumzia vitendea kazi atakavyovitumia kwa ajili ya kazi hiyo.
“Tena tangulia mbele kabisa maana nakujua wewe” Msichana huyo alimuambia huku akisimama ampishe Norbert apite mbele lakini hakupita badala yake na yeye alisimama tu bila kwenda mbele.
“Mimi chuma sharti niwe nyuma ya sumaku jua nikiwa mbele nitavutwa kuelekea nyuma tu, sasa chagua hapo nikae mbele au nyuma maana utachelewa kuja kumalizia kazi yako tu” Norbert aliongea na kupelekea Msichana huyo akose ubishi na kuamua kufuata njia ambayo angekuwa yupo mbele ya Norbert. Safari yao iliishia kwenda sehemu nyingine kabisa ambayo ilikuwa na vifaa vingi vya kijasusi, yule Misichna alimuongoza hadi sehemu ambapo kulikuwa na kitu kilichokuwa kimefunikwa kwa kitambaa kigumu sana. Alienda hadi mbele ya kitambaa hicho na kisha akageuka nyuma kumtazama Norbeet akiwa na tabasamu, taratibu alikifungua kitambaa hiko na Pikipiki ya kisasa ambayo ilikua vikolombwezo vingi sana zaidi ya pikipiki ya kawaida ndiyo ilionekana ambapo Norbert aliachia tabasamu alipoiona tu.
“Duh! Ndiyo maana hii kazi inahitaji haraka nyingi kukamilika” Norbert aliongea
“Ndiyo hivyo kazi kwako” Msichana huyo aliongea
“Kumbe kanipa hii ndege ya ardhini ndiyo maana nataka kazi hii ikalimike upesi”
“Hilo unalo babu wee, pocket za ndani ya hii pikipiki zina kila kitendea kazi chako. Nafikiri sina la ziada tena kufikia hapa”
“La ziada lipo bibie umemaliza ya kwako bado ya kwangu tu”
Norbert aliongea huku akianza kumsogelea huyo Msichana, na yeye pia tayari alikwishatambua kuwa Norbert alikuwa akitaka kitu gani alitulia na kubaki akimtazama tu. Norbert alipomfikia karibu zaidi aliupeleka mkono wake ukashika kiuno cha huyo Katibu. Msichana huyo alitoa muhemo wa hisia baada ya mkono wa Kidume cha mbegu kutua kiunoni hapo, alishindwa kabisa kumtazama Kidume ambaye alikuwa akimtazama sana kwa macho yasiyo na aibu hata kidogo kama ilivyo kawaida yake akiwa na anatazamana na uso wa msichana yeyote . Norbert alianza kuufanya mkono wake ufanye matembezi yasiyo rasmi kwenye mwili wake na kupelekea atoe miguno, alijiachia zaidi kwa kujisogeza mbele na akajikuta akiegemea kifua cha Norbert ambaye hakufanya makosa kabisa. Yeye aliamua kusogeza papi za midomo yake zikakutana na papi za midomo ya Msichana huyo, taratibu walianza kubadilishana shurubati ya midomoni kwa huku yule Msichana akionekana ni mwenye kuishiwa nguvu kabisa kutokana na kitendo hicho alichokuwa akifanyiwa na hata alipoachiwa papi za midomo yake bado alijikuta kisogeza zaidi kichwa cha chake kwa Mhamasishaji wake akiashiria kuwa alikuwa akitaka kitu hicho kiendelee. Norbert hakutaka kufanya ajizi kabisa yeye alitaka kuleta midomo yake kwa mara ya pili lakini alisita ghafla na kisha akarudi nyuma hatua moja kwa kasi sana, muda huo mlio wa kufunguka kwa mlango ulisikika na kisha akaonekana Mfanyakazi mwenzao wa shirika hilo akiingia humo ndani akiwa amebeba vifaa vipya vya kijasusi kwa ajili ya kuvihifadhi humo kwani hiyo ndiyo ilikuwa ghala kuu.
“Fuguo yako hii hapa, code number ya hiyo pikipiki ni jina la mkuu wako wa kazi tu” Msichana huyo aliongea kuzuga huku akimpatia funguo hiyo Norbert kwani ilibaki kidogo tu waweze kufumwa humo ndani wakiwa wapo ndani ya ulimwengu mwingine, Norbert alizipokea funguo hizo huku akimtazama Mfanykzi huyo Mwenzao anayehusika na humo ndani ya chumba cha kuhifadhia vitu. Alikuwa akitamani sana Mfanyakzi huyo atoke lakini hakutoka kabisa yeye ndiyo kwanza alienda kwenye kiti chake cha kazi baada ya kuweza vitu hivyo, hapo Norbert hakuwa na ujanja tena wa kuendelea na kile ambacho alikuwa amekianza na ilimbidi aoke humo ndani kwa kutumia Pikipiki hiyo aliyokuwa amekabidhiwa. Msichana huyo aliamua kutoka humo ndani akimuacha Norbert akieiendea hiyo pikipiki na kuikwea na kisha akaichomeka ufunguo, aliiweka namba za siri kwenye Pikipiki hiyo na kisha akaiwasha.
Lango jingine kabisa lililokuwa lipo humo ndani ya ghala ya zana muhimu ulifunguiwana Mtu yule aliyekuwa akihusika na humo ndani, Norbert kwa taratubu kabisa aliiondoa Pikipiki hiyo humo ndani akimuacha Mhusika wa hapo akimpungia mkono baada ya yeye kumpungia mkono na kisha aliufunga mlango wa hapo ndani baada ya N001 kuweza kuondoka kabisa.
BAGAMOYO
Ni ndani ya eneo ambalo lipo mita kadhaa tu kutoka ilipo stendi kuu ya magari ya jijini Bagamoyo, mtaa wa pili kutoka anapoishi mtunzi mahiri wa riwaya Ibrahim Marijani Gama. Ndani ya mtaa huo kwenye nyumba ambayo ilikuwa na uzio wa ukuta pamoja na lango lililonakshiwa vizuri, ilionekana gari aina ya Mazda yenye muundo wa Altezza ikiwasili neneo la jirani ya lango hilo. Gari hilo liliegeshwa mbele ya lango kuu la kuingila ndani ya nyumba hiyo, mlango wa gari hilo ulifunguliwa na akashuka Msichana mwenye umbo la kirembo sana akiwa amevalia suruali nyeusi iliyokuwa imemkaa mwilini, juu alikuwa amevaa blauzi nyeupe ambayo ilikuwa nyepesi sana kiasi cha kufanyia brazia aliyokuwa ameivaa ndani yke kuweza kuonekana. Mguuni alikuwa amevaa kiatu kirefu sana ambacho kilimfanya azidi kupendeza sana. Msichana huyo aliposhuka tu aliweka miwani ya giza yenye urembo wa kike kwenye macho yake na kisha akaanza kupiga hatua kuelekea kwenye lango la nyumba hiyo mkoba wake ukiwa upo kwapani mkanda wake ukiwa unaning’inia begani.
Alifika hadi mbele ya lango la Nyuma iliyopo mbele yake ambapo alibonyeza kengele ya mlangoni, haukupita muda mrefu mlango huo ulifunguliwa na Mwanamke wa makamo alionekana akiwa mlangoni ambaye alimkaribihsa hapo nyumbani kutokana na huyo Misichana kuwa mgeni mbele ya macho yake.
“Za saa hizi dada yangu?” Msichana huyo alimsabahi Mwanamke huyo aliyemkuta hapo mlangoni.
“Safi tu mdogo wangu, nikusaidie nini?” Mwanamke huyo alijibu na kisha akamuuliza juu ya shida iliyokuwa imempeleka hapo nyumbani kwake.
“Kuna dada mmoja anaitwa Sakina anaishi ndani ya nyumb hii sijui nimemkuta?”
“Haswaa umemkuta mdogo wangu ndiyo mimi hapa Sakinabinti wa Majaliwa”
“Dada yangu nimetoka Mlandizi nimeelekezwa nije hapa kwako nina shida sana na wewe”
“Mlandizi kwa mdogo wangu karibu sana ndani” Mwanamke huyo alimkaribihsa na kisha akasogea hapo mlangoni kumpisha Msichana huyo mrembo aingie ndani ya nyumba hiyo, Msichana huyo bila ya hofu ya ndani ya nyumba hiyo ngeni ambayo hakuwahi hata mara moja kuingia alipita. Ukimya wa ndani ya nyuma hiyo wala haukumtia hofu hata kidogo yeye aliona ni kawaida na aliingia ndani na kisha akasimama akimsubiri mwenyeji aje kumuongoza njia.
Mwanamke uyp mwenyeji hapo ndani ya nyumba hiyo alitembea akakaa mbele yake ambako alimuongoza hadi wanaingia ndani ya nyumba hiyo, alipelekwa hadi kwenye sebule ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa ni kubwa sana na ilikuwa imetawaliwa na ukimya sana. Alikaribishwa kwenye kochi mojawapo la kisasa la ndani ya sebule hiyo na kisha mwenyeji wake akatoka hadi kwenye sebule maalum ya kulia chakula, baada ya muda alirejea akiwa na kinywaji mkononi mwake ambacho alimuwekea mgeni wake mezani na kisha akaketi pembeni yake.
“Nisamehe sana mdogo wangu kinywaji kilichobaki ndiyo hicho tu, hivyo karibu hivyohivyo” Mwanamke huyo aliongea huku akifungua kinywaji hicho.
“Dada yangu usijali tu yaani mgeni hachagui ukaribisho wa kupewa” Msichan ahuyo aliongea kumtoa hofu sana
“Ndiyo mdogo wangu niambie”
“Dada yangu nimekuja hapa kwako nikiw nimefuata maelekezo yote niliyopewa, na kikubwa nilikuwa na shida kubwa san”
“Nakusikiliza mdogo wangu niambie”
“Shida yangu kuu ni ile laptop ya marehemu iliyokuwa ipo kwenye kabati chumbani kwako tu na si kingine” Kauli hiyo ilifanya yule mwanamke ashtuke sana kwani muongeaji alikuwa amebadilika ghafla na alikuwa amevaa sura isiyo na mzaha hata kidogo
“Kwani wewe ni nani?”
“Haina haja ya kunijua mimi ni nani timiza nilichokuambia” Msichana huyo aliongea huku akitoa miwani ya giza aliyokuwa ameivaa na kupelekea macho yake ya kirembo yaliyokuwa yamejaa ukali kuonekana kwa Mwanamke. Pamoja na hayo mwanamke huyo hakuwa na hofu hata kidogo hasa akiutazama muonekano wa Mgeni wake ambao ulikuwa ni wa kidhaifu sana.
“Sikiliza kama umetumwa nenda kawaambie hao waliokutuma wamegonga mwamba, mimi ndiyo Sakina Bint wa Majaliwa ukisikia mwingine jua ni wa kuchongsha. Kama kakutuma huyo mke mkubwa wa marehemu hapa imeshindikana tena na utoke huna hata hadhi ya kukinywa hicho kinywaji nilichokukribisha”
“Nafikiri hutambui unaongea na nani Sakina, sasa naongea kwa mra ya mwisho leta laptop ya marehemu sasa hivi”
“Sileti tuone uta nifanya nini” Kauli hiyo alipoiotoa Sakina alijikuta kipigwa teke la pembeni la ghfla sana ambalo lilimtoa kutoka hapo kwenye kochi hadi akangukia upande wa pembeni chini kwenye sakafu ya nyumba hiyo. Mwenyewe alibaki akiwa ameshangazwa kwa jinsi Msichan huyo alivyokuwa na nguvu za miguu hadi kufikia kiasi cha kuweza kumrusha hivyo mtu mwenye mwili kama yeye, alipoanguka chini alikuwa ameumia haswa hata kunyanyuka ilikuwa tabu tu ingawa alikuwa anaweza. Aliishia kujigeuza tu akawa amelala chali huku akifumba macho kwa maumivu, hali hiyo haikusaidia kabisa katika kumfanya Msichana huyo aweze kumuachia kutokana na majibu ya jeuri aliyokuwa amemjibu. Yeye alimuongezea teke la tumboni na kumfanya azidi kuwa na maumivu zaidi, uso wa msichana huyo ulikuwa tayari umeshabadilika na ukiwa umevaa sura isiyo ya kibinadamu kabisa kwa jinsi alivyomuadhibu.
“Haya nyanyuka mwenyewe tena ukiguna maumivu tu kwa sekunde chache wakati nakupa amri hii nakuongeza tena, uongoze njia unipelke ilipo lapatop hiyo”
Hakuwa na ujanja tena wa kuweza kuipinga amri hiyo kutokana na mapigo hayo mawili ya nguvu aliyokuwa amepewa ndani ya dakika zisizozidi mbili tu, mwenyewe aliongoza njia na kumpeleka huko kulipokuwa na kitu hicho alichokuwa akikitafuta Mgeni wake.
Uchungu wa kipigo hakika aujuaye mpigwaji, maumivu yote ya kipigo haulizwi mpigaji. Majibu yake aliyokuwa akiyajibu aliona wazi ilikuwa ni dharau kubwa sana kwa Msichana huyo aliyeingia hapo ndani ya nyumba yake, ilikuwa ni sawa kunenepa ilihali aliyekuwa anakudai anakonda huku ukidai hali ni ngumu ndiyo mana hujalipa deni. Kipigo hicho kilimtosha wazi kuongoza hadi ndani ya chumba chake ambapo alienda hadi kwenye mtoto wa kitanda wa pembeni, hapo alifungua na kutoa Tarakilishi ya mapakato ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye mkoba maalum na alimpatia Msichana huyo huku akiwa bado anaugulia maumivu hayo.
Msichan huyo aliichukua Tarakilishi hiyo ya mapakato na kisha akaifungua na kuitazama muundo wake ilivyo, baada ya hapo alimkazia sana uso Bi Sakina ambaye alikuwa akiugulia maumivu akiwa amesimama wima. Alisonya kwa nguvu sana na kisha aliachia teke la pembeni ambalo lilimpata kwenye goti, mfupa wa goti wa Bibi Sakina ulitoa sauti ya kugoka na yeye mwenyewe akabaki akitoa ukelele wa maumivu. Alianguka chini moja kwa moja akabaki akishikilia goti lake ambalo lilikuwa limepatwa na kadhia hiyo ya kupigwa na miguu ya mrembo ambayo ilikuwa ni imara na yenye nguvu sana.
“Weee! Kelele kabla sijakuongeza pigo jingine” Msichana huyo aliongea na alipoimaliza kauli yake tu alimuongeza teka jingine ambalo lilimfanya aende kujipigiza kitandani akajeruhika zaidi hata alivyojeruhika hapo awali.
Baada ya kumpa pigo hilo mwenye nyumba na Mwenyeji wake aliamua kufungua mkoba wake aliokuwa amekuja nao, alitoa Bahasha na kisha akaiweka chini kwenye miguu yake. Hakutaka kupoteza muda baada ya kuiweka bahasha hiyo, aliamua kugeuka nyuma na kisha akaanza kutoka humo ndani ya cnumba hicho. Alitembea kwa mwendo wa madaha ambao haukuwa ukiendana kabisa na kazi ya ukatili hiyo aliyokuwa akiifanya, alipofika mlangoni alishika kitasa cha mlango huo na kisha akanyonga na kupelekea mlango ufunguke. Alipiga hatua kutoka nje lakini alijikuta akisita na kisha akageuka nyuma na kumtazama Mmiliki wa jengo hilo ambaye alikuwa amemfanyia uonevu mkubwa sana, alionesha sura ya huruma sana alipomtazama Mwenyji wake kama alikuwa akijutia sana kwa kile alichokuwa akikifanya kwake.
“Ubishi wako ndiyo chanzo cha yote haya, chukua malipo yako hayo ambayo laiti ungenipa kwa amani tu hii Laptop ungeyapata na ufaidike. Bakshishi yako hiyo pamoja na wito” Aliamuambia Bi Sakina na kisha akatoka ndani ya chumba hicho na akafunga mlango
Hakutaka kusubiri kitu kingine kabisa yeye alitoka moja hadi lilipo gari lake hapo nje, aliingia ndani ya gari hiyo na kisha akaketi kwenye kiti kwa haraka sana. Akiwa bado ni mwenye haraka aliwasha gari na kuliweka gia na kisha akaondoka katika eneo na kwenda kusimama mita kadha mbele, alipolisimisha gari hilo tu mlipuko mzito ulisikika kutoka nyuma yake na ilimpelekea aangaze macho huko unapotokea mlipuko huo. Aliweza kuishuhudia nyumba ya ambayo alikuwa ametoka kuingia muda mfupi uliopita tu ikiwa inateketea kwa moto, usoni aliachia tabasamu alipoiona nyumba hiyo ilikuwa ikiteketea kwa moto.
Baada ya hapo alichukua simu yake ya mkononi ya kisasa na kisha akatafuta sehemu ya majina na alipopata jina alilokuwa akilitafuta aliweka simu hiyo sikioni, akiwa ameweka simu hiyo sikioni mguu wake wa kulia ambao alikuwa ameutoa sehemu ya mafuta na kuupeleka sehemu ya breki akiurudisha ulipokuwa awali. Aliliondoa gari kwa mwendo mkubwa sana huku mkono mmoja ukiwa upo sikioni, mkono mwingine ulikuwa upo kwenye usukani kuweza kuliweka gari kwenye muelekeo mzuri kabisa.
“Kazi imeshaisha imebaki kwako uende Kiwalani sasa hivi ukachukue Laptop nyingine hadi zote tano zitimie” Aliongea na kisha akakata simu bnada ya mtu aliyekuwa amempa maelekezo kumuambia kuwa alikuwa ameyaelewa maelekezo yake.
Akiwa ndani ya pikipiki yake mpya kituo chake cha kwanza kilikuwa ni ndani ya nyumba yake ambayo alikuwa akiishi na mpenzi wake,Norbert alipofikisha pikipiki hiyo eneo la maegesho tu aliizima na kukimbilia kwenye eneo la bwawa la kuogelea ambapo alikuwa ameiacha familia yake ikiwa ipo inacheza kwenye eneo hilo kwa pamoja. Jerry alipomuona tu alimkimbilia kwa haraka na alipofika miguu kwake alimnyanyua na kumuweka mikononi mwake, Norbert alimbeba Jerry na akaelekea hadi kwenye kochi la kupumzika jirani kabisa na bwawa la kuogelea. Aliketi jirani na mpenzi wake huyo na kisha akambusu mdomoni, wote wawili walikumbatiana kwa upendo mkubwa sana wakiwa wamemuweka mtoto wao katikati yao.
“Nipe ripoti ya huko” Norene aliongea baada ya kuachiana
“Aisee hii kazi ni kiboko, nina gunia jipya yaani nikitoka hapa naingia mzigoni” Norbert aliongea
“Yote heri tu ila kwangu la muhimu uende salama na urudi salama sitaki nije kulia mimi na mwanao hapa”
“Hilo usihofu kabisa, nitunzie mwanangua mimi naingia mzigoni” Norbert aliongea na alipomaliza alinyanyuka pale alipokuwa ameketi.
“Jerry acha nikakuchukulie zawadi my boy nitarudi sasa hivi” Alimwambia na kisha akaondoka eneo hilo baada ya kumbusu mpenzi wake na pia kumkumbatia mtoto wake. Alitumia pikipiki aliyokuwa amekuja nayo hapo, aliondoka hapo nyumbani kwake na safari ya kuelekea huko kazini ndiyo ilianza.
Robo saa baadaye alikuwa yupo ndani ya eneo la Yombo Kiwalani ambalo ndiyo alipanga kuanzia kazi, aliingia ndani ya kitongoji hicho ambako alielekea hadi kwenye mtaa ambao ulikuwa na nyumba chache sasa. Mtaa huo ndiyo ulikuwa ni lengo lake la kwanza kabisa kuweza kuianza kazi hiyo aliyokuwa amepewa. Ilikuwa ni miti kadhaa kila baada ya nyumba kuashiria kuwa eneo hilo ndiyo watu walikuwa wakihamia mida hiyo kwa kasi, baada mwendo mfupi ambao ulikuwa umemjaza hamasa ndani yake hatimaye alikuwa akikaribia kufika kwenye nyumba ambayo alikuwa akitarajia kwenda kuanzia kazi.
Kila alipozidi kuikaribia nyumba hiyo ndiyo mapigo yake ya moyo yalivyokuwa yakimuenda mbio sana, akiwa amebakisha mita chache kabisa aifikie alisikia sauti ya honi ya nguvu sana kutoka nyuma yake, alipoangalia kupitia vioo vya pembeni aliiona gari aina ya Subaru impreza ikiwa inakuja kwa kasi sana. Mlio huo wa honi ya gari hiyo ambayo inasifika sana kwa mwendo, alitaka kuongeza mwendo aendane na kasi ya gari hiyo lakini kutokana na ukaribu wa eneo ambalo yupo aliamua kusogeza Pikipiki yake pembeni na gari hiyo ikapita kwa kasi sana. Gari hiyo pamoja na mwendo huo wa kasi ambao ilikuwa imempita nao ilikwenda kusimama palepale kwenye nyumba hiyo aliyokuwa anaelekea, Norbert bado akiwa anaisogelea hiyo nyumba aliweza kushuhudia ndani ya gari hiyo akishuka Kijana mwenye asili ya shombe ambaye mikononi mwake alikuwa ana michoro mingi sana. Kijana huyo aliposhuka tu ndani ya gari hiyo aliangalia katika upande ule ambao alikuwa anakuja Norbert.
Kitendo cha Kijana huyo kumuona mtu kwenye pikipiki kilifanya asite kabisa kuingia ndani ya nyumba hiyo, aliganda akimtazama huyo mwenye pikipiki hiyo ya kisasa. Alijikuta akitoa tabasamu tu alioiona pikipiki hiyo na hadi inafika karibu yake alijikuta akiisimamisha, mwenye lengo kama lake na nyumba hiyo ambaye alikuwa yupo kwenye pikipiki alijifanya alikuwa akitaka kuipita nyumba hiyo. Aliposimamishwa alisimama na kisha akafungua kofia ya aliyokuwa ameivaa kichwani, yule kijana mwenye asili ya Shombe alitoa tabasamu baada ya mwenye pikipiki kusimama.
“Unaendesha chombo cha ndoto yangu, Ha! Ha! Nikupongezae kwa kumiliki chombo kama hicho” Aliongea akionekana kuvutiwa sana na pikipiki hiyo
“Thats my dream” Mwenye pikipki aliongea huku akishika sehemu ya tenki la mafuta la pikipiki hiyo
“Sina kingine mkuu ni kukupa hongera tu, nice Bike” Kijana huyo aliongea na kisha akamuonesha ishra ya ngumi, Norbert aligonga ngumi hiyo kuangana naye na kisha aliiondoa pikipiki kwa mwendo wa kasi sana kuelekea mbele zaidi.
Kijana huyo aliingia ndani ya nyumba hiyo akionekana alikuwa akiifahamu zaidi, alitoa funguo ambazo ndiyo alitumia kuingia nazo ndani ya nyumba hiyo. Aliingia ndani akiwa amehakikisha kuwa nje ya nyumba hiyo kulikuwa kupo salama sana, baada ya kuingia ndni ya nyumba hiyo alifunga lango kuu la nyumba hiyo kama vile kulikuwa hamna mtu ndani ya nyumba na yeye ndiye alikuwa akiingia pekee.
Kufunguliwa kwa mlango wa mbele ambao ulikuwa ni mlango mkuu ndani ya nyumba hiyo, kulimshtua sana Mwanamke aliyekuwa amekaa kwenye kochi la kisasa akiangalia filamu. Alishtuka sana alipoona mlango huo ukifunguliwa na kisha kiatu cha kisasa aina ya raba kikitanguliwa, mwanamke huyo aliweza kumshuhudia Kijana ambaye hakuwahi kumtia machoni mwake kabla na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kuweza kuonana naye.
Aliingia yule kijana ambaye alikuwa ametoka kuongea muda mfupi uliopita na Norbert akiwa ni mewnye mavazi ya kisasa sana, mwanamke huyo alibaki akimkazia macho sana kijana huyo mgeni ndani ya macho yake. Alibaki akijiuliza alikuwa ameingia vipi ndani ya nyumba hiyo hadi afike hapo, milango ilikuwa imefungwa lakini aliweza kuingia ndani ya nyumba hiyo.
“We ni nani na umeingia vipi hapa?” Alijipa ujasiri sana ingawa moyoni alikuwa na hofu sana, ujasiri wake ulimuwezesha kuuliza swali hilo.
“Ni mimi hapa nisiye na jina, nisiyezuiwa hata kwa mlango wa chuma ndiyo nimeingia” Kijana huyo aliongea na kisha akasogea hadi jirani na huyo Mwanamke, alijibwaga kwenye kochi na kisha akaachia tabasamu akimtazama huyo mwanamke.
“Unashangaa kuingia ndani ya nyumba hii ukiwa umefunga milango, Haaaa! Mzimu toka lini ukazuiwa na mlango wewe. Haya hebu kanipe Laptop ya marehemu haraka sana”
“Wee nani?”
“Mzimu kutoka kuzimu nimetumwa kuja kuchukua laptop na Marehemu, sitaki kupoteza muda ongoza njia ilipo unipe”
“Sitoi nakuambia”
“Oooh! Hujui kuwa unaongea na Mzimu wewe, haya ongoza njia mwenyewe” Kijana huyo alipoongea maneno hayo yaliambatana na mkono wake kuingia kinenani, alipoutoa ulikuwa na Bastola jambo ambalo lilimfanya Mwenyeji azidi kuingiwa na hofu zaidi. Alitetemeka akawa anajaribu kujisogeza pembeni ya kochi alilokuwa amekaa pembeni ya kijana huyo, hiyo haikusaidia kitu kabisa kutokana na uwepo wa chombo hicho cha moto kisicho na mzaha kabisa. Chombo ambacho kikikohoa basi ni hatari tupu kwa mkoholewaji wake, mwenyeji wake aliingiwa na ubaridi wa ghafla kwenye moyo wake alipoelekezewa hiyo silaha.
“Ongoza njia ukanipe” Aliamriwa
Mwenyewe bila ya kupenda aliongoza njia na kwenda kutoka hicho kilichokuwa kikihitajiwa, alitembea kwa uoga akiwa anaufuata ukumbi mwembamba ambao ulikuwa upo kwenye njia ya kwenda huko chumbani kwake ambapo kulikuwa na kitu hicho ambacho Mgeni mvamizi wake alikuwa akikihitaji kwa haraka sana. Kutembea huko kulimbidi avuke kizingiti cha hapo sebuleni ndiyo aweze kuingia kwenye ukumbi mwembamba unaotenganisha vyumba, ukumbi huo ambao mwanzoni mwake kulikuwa kuna mlango wa jiko kwa upande wa kushoto.
Mwanamke huyo alitangulia kuongoza njia ambapo ilimbidi avuke vizingiti mbalimbali akianzia hicho cha jiko ndiyo aweze kufika chumbani kwake, alikipita vizuri kizingiti cha hapo jikoni lakini kwa aliyekuwa yupo nyuma yake kuna jingine jipya kabisa liliibuka. Yule Kijana alipotanguliza tu bastola yake kipindi akimuongoza yule mwanamke katika usawa wa mlango wa jiko, alijikuta akitoa yowe la maumivu la kabla hajakaa sawa miguu ya mtu ambaye alikuwa akibembea kwnye dari ya huko jikoni ilijitokeza kwa kasi na kisha yeye mwenyewe akaonekana.
Alionana ana kwa ana na Dereva wa pikipki ambaye alikuwa akimsifia kuwa alikuwa ana pikipiki nzuri, muda huo aliokuwa akionana naye huyo Dereva hakuwa na ujanja tena kwani silaha yake ilikuwa ipo mbali kabisa . Akiwa hata hajafikiria jambo jingine la kufanya alipokea mapigo manne ya karate yaliyokuwa yamejaa siha ya kutosha, alienda chini moja kutokana na mapigo hayo. Akiwa bado yupo hapo chini aliongezewa mapigo mengine ambayo yalimfanya hata siwe na nguvu kabisa ya kuendelea kupambana, alipokea kipigo kikubwa sana na pigo la mwisho kabisa alilokuwa amepokea kutoka kwa Dereva huyo wa pikipiki kwenye kofia lake kichwani ilikuwa ni kichwa cha pua ambacho kilimpata sawia kutokana na Dereva huyo kuvaa kofia ngumu. Alianguka chini kama mzigo akawa hana ujanja tena wa kupigana na adui yake.
Baada ya kutoa kipigo hicho kizito ndipo aliweza kugeuka na kumtazama mwanake yule ambaye alikuwa amekaa chini muda huo akiwa amejikunyata kwa uoga sana, alimsogelea hadi karibu kabisan na kisha akavua kofia yake aliyokuwa amevaa. Norbert ndiyo alionekana mbele ya huyo mwanamke ambapo alimuinua akiwa ni mwenye huruma, baada ya kumuinua huyo mwanamke alimtazama usoni na kisha akamgeukia adui yake ambaye hakuwa na nguvu hata ya kusimama hadi muda huo.
“Sipo hapa kwa ajili ya kukudhuru bali ni kutoa msaada, nafikiri mimi si mgeni kwenye macho yake. Hivyo punguza hofu kabisa na unisikilize kwa umakini sana, nenda katoe kile alichokuwa akikitafuta huyu nakusubiri hapa hii ni kwa usalama wake tu eneo hili halikufai” Alimuambia huyo mwanamke.
Mwanamke huyo kusikia kauli hiyo alitikisa kichwa kwa haraka sana kuitikia na kisha akaelekea chumbani kwake upesi, alimuacha Norbert ambaye alimrudia yule Mpinzani wake na kuanza kumpekua kwenye mifuko yake. Alimkuta akiwa na bahasha kubwa nyeuope pamoja na pochi ndogo,aliichukua hiyo pochi yake na kisha akaifungua na kukuta kukiwa na kadi na vitambulisho mbalimbali. Norbert aliiweka hiyo pochi mfukoni mwake na kisha akachukua bahasha hiyo nyeupe na kuanza kuifungua, alifungua kwa taratibu sana na akakutana na bahasha nyingine ndani ikiwa na stempu yenye picha ya mgongo wa mwanamke aliyejifunika shuka hadi kiunoni. Bahasha hiyo haikuwa tofauti kabisa na bahasha zile ambazo zilikuwa zikiwafikia wale wote ambao hadi muda huo hawakuwa na uhai. Norbert alitaka kuifungua bahasha hiyo lakini alisita bada ya kusikia sauti ya mtu mwenye viatu akija nyuma yake.
Aligeuka kwa kasi ya ajabu na kusimama pembeni akiwa ypo kujihami zaidi, alimuona yule mwanamke akiwa ameshika mkoba wa mabegani akiwa tayari amevaa kwa ajili ya kuondoka. Hapo alishusha pumzi na kisha akaamua kuachana na bahasha hiyo, aliiweka bahasha hiyo chini na kisha akamshika mkono Mwanamke huyo na kutoka naye humo ndani ya nyumba hiyo kwa kutumia mlango wa nyuma wa nyumba ambao ndiyo aliutumia kuingia humo ndani.
Kitendo cha ujio wa Mwanamke huyo akiwa tayari ameshajiandaa na akiwa amebeba mkoba wa mabegani, ulikuwa ni wokovu tosha kwa Norbert na laiti kama angelitambua hilo asingesita kumshukuru huyo mwanamke kwa kuweza kumsogelea akajua ilikuwa ni adui akikaribia kumvamia. Jambo hilo lilifanya aache kabisa kuitazama bahasha hiyo, hakujua kabisa kisanga ambacho kilikuwa kikiwapata wale ambao walikuwa wakifungua bahasha ya namna hiyo. Ujio wa mwanamke huyo ulimfanya apuuzie bahasha hiyo kwa kuona kuwa angemtia wasiwasi zaidi huyo mwanamke kwa kumpekua huyo Kijana ambaye yupo hai muda huo hakuwa na nguvu. Aliamua kuiacha bahasha hiyo huku akimtazam huyo kijana ambaye alikuwa akiona jinsi Norbert alivyokuwa akitaka kuipekua hiyo bahasha, kijana huyo alipoona Norbert akitaka kufungua hiyo bahasha alijikuta kicheka mwenyewe na alipoiacha alinuna kwani aliona alikuwa amegunduliwa fikra zake.
Norbert alipoiacha ile bahasha na kutoka ndani ya nyumba hiyo hadi wanafika kenye Pikipiki yake ambayo alikuwa ameigesha kichakani, mlipuko mkubwa sana ulisikika kutoka eneo ambalo nyumba hiyo ilikuwepo. Mlipuko huo uliambatana na milipuko mingine mitatu mfululio kuashiria kuwa ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na vitu viwili ambavyo vilikuwa ni mlipuko mkubwa sana ikiwa vitapata moto au vikisogelewa na moto. Mwanamke yule aliweka mkono kinywani mwake alipoiona nyumba yake ikiwa imetoa mlipuko huo, machozi yalianza kumtoka kila akifikiria jinsi ambavyo alikuwa ametumia ushawishi wa nguvu kutoka kwa mwanaume wake ambaye hadi muda huo ni marehemu. Ushawishi huo ndiyo ulifanya kajengewa nyumba hiyo ambayo kwa muda huo ilikuwa ikiteketea, alipofikiria suala hilo aliona kabisa hakuwa na wa kumuegemea mwingine ambaye angeweza kufanya hadi ajengewe nyumba kama hiyo pamoja na kuwekewa Samani ndani ya kisasa.
Kilio chake hicho Norbert hakukijali kabisa yeye aliwasha pikipki yake baada ya kuwa amepanda na kisha akaingiza barabarani akiitoa kule kichakani ambapo alikuwa ameificha, aliondoka eneo hilo kwa kutumia njia nyingine kabisa siyo ambayo alikuwa amekuja nayo hapo awali ambayo ndiyo ilikuwa ni njia kuu ya vyombo vyote vya msaada kuweza kuingia ndani ya mtaa huo. Aliamua kupita upande mwingine ambao ungeweza kumfikisha hadi ilipo barabra kubwa aweze kutoweka ndani ya eneo hilo baada ya kusababisha habari nyingine kabisa.
ITAENDELEA
Wito wa Kuzimu Sehemu ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;