Wito wa Kuzimu Sehemu ya Pili
IMEANDIKWA NA: HASSAN O MAMBOSASA
*********************************************************************************
Simulizi: Wito Wa Kuzimu
Sehemu ya Pili (2)
Kutokea kwa mlipuko ndani ya nyumbe ya mke mdoago kabisa wa mmoja wanausalama wa siri waliohusika na utafiti wa ripoti ya Mheshimiwa Bai, kulishtua sana Idara ya usalama wa tafia kwa mra nyingine kabisa ambao ndiyo walikuwa wapo kazini kuhakikisha wahusika wote wliokuwa wakihusika na milipuko hiyo watiwe nguvuni. Muda huo wanafika hapo eneo hilo la tukio ambapo hata baada ya kuzimika kwa moto ndani ya eneo hilo walitambua kabisa kuwa tarakilishi ambayo ilikuwa na kitu chao muhimu ilikuwa imeshaondolewa na aliyewawahi kabla yao. Hii iliwachanganya sana kwani Tarakilishi hiyo ilikuwa ni Tarakilishi ambayo ilikuwa na kitu muhimu sana ambacho kingeweza kufanikisha watuhumiwa waliokuwa wakihusika na upotevu wa vitu vya umma wanafikishwa ndani ya vyombo vya sheria. Tarakilishi hiyo ndiyo ilikuwa na nenosiri la kila kitu juu ya wahusika wa kuhujumu nchi hii, ilikuwa ni moja ya kati ya tarakilishi tano ambazo walikuwa nazo wanausalama waliokuwa wamebeba siri hiyo kama kumbukumbu ikiwa faili kuu litapotea.
Uunguaji wa faili kuu katika mlipuko mmoja na Mheshimiwa Bai uliwafanya wahangaike kuyafuata mafaili hayo ambayo watunzaji wake wengi wao walikuwa wamekufa mmoja baada ya mwingine kwa mlipuko. Taraklishi ambayo ilikuwa imetunza mafaili hayo nayo ilikuwa imeishia ndani ya mikono mibaya. Walichanganyikiwa kutokana na kupotea kwa tarakilishi hiyo, waliona kabisa kuwa kazi yao ilikuwa ikielekea kuwa ngumu zaidi. Walihesabu kuwa tarakilishi hizo zilikuwa zimebaki nne tu huku moja tu ikiwa inajulikana mahali ambako ilikuwepo na nyingine zikiwa hazijulikani mahali zilipokuwepo. Wakiwa ndani ya eneo hilo walipokea taarifa nyingine kabisa ya kuteketea kwa nyumba ya Mwanausalam mwingine ambaye alikuwa ameficha huko Tarakilishi moja inayojulikana ilikuwa na siri kubwa sana. Wanausalama walichanganykiwa kwa taarifa hiyo na wakaona walikuwa na kazi ya ziada, wakiwa ndani ya eneo hilo la tukio huko Bagamoyo waliona kuwa hawakuwa na kingine ambacho kingewafanya wawepo ndani ya eneo hilo ikiwa kile ambacho kilikuwa kimewaleta ndani ya eneo hilo kilikuwa kimechukuliwa na wabaya wao. Wote kwa pamoja waliondoka kwa njia walizokuwa wakizijua wao tu wakiwaacha Maaskari wa jeshi la polisi wakifanya kazi, hakika waliwahiwa kwa kila walichokuwa wakikiangalia.
Baada ya kumuokoa ndani ya balaa zito Mwanamke yule kituo cha kwanza ailikuwa ni ndani ya nyumba ya Shirika alilokuwa akilianyia kazi, alimuweka mwanamke huyo ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa na kila kitu alichokuwa akihitajika kupewa mwanadamu. Mkoba wa yule mwanamke ambao ndani yake ndiyo ulikuwa na Tarakilishi ya mapakato ambayo ilikuwa na siri iliyokuwa ikitafutwa. Ulihifadhiwa ndani ya nyumba hiyo ambayo si rahisi kabisa kufikiwa na raia wa kawaida. Baada ya kuuuhifadhi mkoba ule ndipo Norbert alipokumbuka kuwa alikuwa na anahitajika kuichunguza pochi ya mfukoni ya yule Kijana ambaye hadi muda huo alikuwa ni marehemu. Norbert aliitoa ile pochi na kuanza kuifungua na kisha akaanza kutazama kitambulisho baada ya kingine kilichokuwa kipo ndani ya pochi hiyo.
Alikuja kubaini kuwa mtu yule alikuwa akiitwa Kelvin na alikuwa akifanya kazi katika kampuni kubwa ya utengenezaji magari, kitambulisho hicho kilichoonesha kila kitu juu ya kazi yake hiyo aliyokuwa akiifanya huko. Alibaini mtu huyo alikuwa ni mtaalamu aliyebobea katika uundaji maumbo ya juu ya magari, Norbert alipomaliza kukitazama kitambulisho hicho cha kwanza ambacho kilimwambia hivyo juu ya Kijana yule. Alitazama vitu vingine vingi ambapo aliona kabisa kuwa kulikuwa na kuna kadi nyingi za mawasiliano za kampuni ile ya uundaji magari na uungaji vifaa vya magari. Hii ilimpa ishara tosha kuwa mtu huyo hakuwa na kitambulisho hicho kwa kufoji bali alikuwa ni mfanyakzi halali wa pale, uwepo wa kadi hizo ulimpa uhakika kabisa kuwa alikuwa akizitumia kwa ajili kuwapatia wateja wake pindi watakapohitaji mawasiliano zaidi kwenye kampuni hiyo. Alikutana na kadi mbalimbali za benki ambazo hakuona maana yeyote ile kwake, aliachana na kadi hizo na kisha akatazama kadi nyingine ya kampuni hiyo aliyokuwa akifanyia kazi Kelvin ambayo ilionesha hadi mahali alipokuwa akiishi.
Baada ya kumaliza kupitia kadi hizo zote aliamua sasa kuingia kazini kwa mara ya pili baada ya kufanikisha kumuokoa mwanamke huyo, aliamua kuiacha pikipiki yake aliyokuwa akiitumia kwa ajili ya kazi na kisha akachukua gari mojawapo ambayo ilikuwa ipo ndani ya uzio wa nyumba hiyo. Alitoka na gari hilo hadi nje kabisa ya uzio baada ya kufunguliwa lango kuu la kuingiza mgari ndani hapo, alianza safari ya kuelekea huko alipokuwa akitaka kwenda kuanza kazi hiyo iliyokuwa imekatisha vizuri alivyokuwa akivitaka kuwa navyo katika muda huo wa kufurahi na familia yake.
DAKIKA KUMI NA TANO BAADAYE
BUGURUNI ROZANA
Gari yenye rangi ilikwanguka katika sehemu kubwa ya bati lake ilionekana ikiwa imeweka kituo kidogo kabisa kwenye lango la kuingilia ambalo lilikuwa limefungwa muda huo, honi ndani ya gari hilo zilisikika zikilia kwa mara moja ambapo muda mfupi aadaye lango hilo la kiksasa la kufunguliwa kwa mashine lilifunguka na kisha gari hiyo ikaingia ndani. Iliingia kwenye eneo ambalo lilikuwa na mitambo mingi sana ambayo ilikuwa imekaliwa na vijana wa kike na wa kiume waliokuwa wamevaa sare za aina moja wakiifanyia kazi. Kutokana na muonekano wa gari hilo ulivyo ilikuwa ishatambulika kabisa ilikuwa na tatizo gani, hivyo kwa maelekezo ya mmoja wa wafanyakazi wa kike wa ndani ya jengo hilo alielekezwa moja kwa moja hadi mahali ambapo kulikuwa kukifanyika huduma maalum ya kuhusu tatizo la gari hilo. Huko ilikuwa ni ndani kabisa kwenye chumba kilichokuwa kimetengenezwa kwa muundo maalum mithili ya banda la kulazia magari, taa tupu zenye mwanga mkali ndiyo zilikuwa zikimulika ndani ya banda hilo kutokana kutokuwepo kwa nafasi ya kupitisha mwangaza wowote ndani humo.
Yule mfanyakazi ambaye alikuwa amemuelekeza dereva wa gari hilo kuegesha humo, aligonga sehemu ya mbele ya gari hilo na kisha akamuashiria Dereva wa gari hilo ashuke, hapo mlango wa gari hilo ulifunguliwa kwa taratibu sana na kisha Norbert akiwaa amevaa kinadhifu kama ilivyo kawaida alionekana mbele ya msichana huyo ambaye alitoa tabsamu murua la kumfanya mteja aone kuwa hakuwa akiliwa hela yake bali ilikuwa ni haki yeye kutoa. Tabasamu hilo lilirudishwa na tabasamu sumu la Mzee wa watoto wazuri na akaangaza ndani ya eneo hilo. Eneo hilo aliweza kuona kuwa kulikuwa na mabinti zaidi ya wanne ambao wote walikuwa ni warembo sana kama alivyo binti yule aliyekuwa amemuelekeza kuleta gari humo ndani.
“Karibu sana Feather garage, naitwa Cellina mhusika mkuu wa kitengo hichi cha kupiga rangi” Msichana yile ambaye ndiye alimuelekeza kuingia humo ndani alimkaribisha akiwa tayari amesogea mbele yake, alimpatia na mkono huku akiachia tabasamu kwa mzee wa mwenye sumu ya matabasamu.
“Asante sana nimekaribia” Norbert aliitikia.
“Hiki ni kitengo cha upakaji rangi magari je ni style ipi uipendayo katika upigwaji rangi yako?”
“Rangi kama ya uremmbo wako” Norbert aliweka utani kidogo
“Ha! Ha! Ha! Handsome utani tuache, unataka muundo upi ngoja uletewe uchagua” Baada ya kungea hivyo alitoa ishara na binti mmojawapo alikuja na Tarakilishi ya kugusa kioo mithili ya simu akampatia, Norbert aliipokea tarakilishi hiyo na akaanza kupitia mitindo mbalimbali ya rangi. Alipoupata mtindo aliokuwa akiuhitaji alimpa Cellina ambaye alimtazama kwa jicho la kuhakiki kama ni rangi hiyo pia alikuwa akiihitaji, Jicho hilo lilifanya Norbert amkonyeze na kisha aachie tabasamu.
“Vipi hadi rangi ya jicho lako nalo napaswa kuchagua” Norbert alieka utani baada ya kuona binti huyo alikuwa akimtazama alipompatia tarakilishi hiyo, hiyo ilimfanya huyo binti acheke kwa mara nyingine na kufanya urembo wake aliotunukiwa uzidi kuonekan dhahiri.
“Boy you are so funny,ok I think uje the day after tomorrow gari itakuwa tayari”
“Ok nilikuwa na kingine kinachohitaji kupendezwa kwa rangi zaidi ya hizi za kutengeneza”
“Sijakuelewa boy”
“Hutanielewa mpaka nikuelewesha na muda huu wa kazi hutakuwa na muda wa kutosha niweze kukuelewsha kuhusu hili”
“Ok be specific”
“Mpiga rangi hupendezesha vingi sana, hivyo nina kingine ambacho ninahitaji ukipendezeshe zaidi ya hiki”
“So ni business outside ya office”
“Ni more than Business Cellina, nafikiri nikiwa na contact yako” Msichana huyo alipoambiwa hivyo alianza kujifikira huku akizungusha mboni yake ya jicho kwenda pembeni kwa madaha, alikaa kimya kwa sekunde kadhaa na kisha akarudisha mboni yake kumtazama Norbert. Hatimaye alinyoosha kiganja chake cha mkono akihitaji kupata simu ya Norbert aweze kuandika namba zake za mawasiliano, hiyo ilikuwa ni kitendo ambacho alikuwa akikisubiri kwa hamu sana mzee wa kazi na kwa haraka kabisa aliingiza mkono wake kwenye mfuko wa suruali akatoa simu ya gharama sana ambayo ilimuacha mdomo wazi binti huyo.
Binti huyo aliipokea simu hiyo na kuandika namba zake kwa haraka sana na kisha akairudisha simu hiyo kwa Mhusika, ilipofika mikononi mwa mmiliki aliiminya namba hiyo aliyokuwa amepewa kuhakiki kama ilikuwa ikifanya kazi. Muda huohuo simu ya yule binti ilianza kuita ndani ya mfuko wa suruali yake aliyovaa. Norbert kuusikia mlio huo alitoa tabasamu tu na kisha akambania jicho binti huyo, baada ya hapo aliwapungia mkono wengine ambao walikuwa wakiendelea na kazi zao na kisha akaondoka mahali hapo. Alikuwa amefanikisha hatua ya awali katika kuingia ndani ya himaya hiyo, hakuwahi kuingia ndani ya jengo hilo hadi sehemu aliyokuwa amefikia na ndani ya siku hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kuingia humo.
Muda huo kwa upande wa ndani kabisa ya kampuni hiyo ya utengenezaji magari, hali ilikuwa si nzuri kabisa kwa bosi wa eneo hilo katika muda ambao alikuwa akitarajia kabisa kuwa mwenzake angekuwa amerudi muda mfupi tu kutokana na kazi aliyokuwa amemkabidhi. Simu zake zilikuwa hazipatikani kabisa tangu waweze kupata taarifa ya kulipuka kwa nyumba waliyomtuma na gari lake kuwepo nje ya nyumba hiyo, taarifa za kuonekana kwa mwili uliokuwa umeharibika ndani ya nyumba hiyo kiasi cha kushindwa kutambulika zilikuwa zimefika hapo. Uchunguzi wa pili a kuhusu mwili huo bado ulikuwa uanaendelea hvyo haikujulikana alikuwa ni jini gani, muda huo ndani ya ofisi hiyo Mkuu wake ambaye alikuwa amemuagiza Kelvin hakuwa mwingine isipokuwa ni yule Msichana ambaye alikuwa amesababisha tukio kule Bagamoyo. Mbele ya meza yake muda huo kulikuwa na kijana wa kizngu maarUfu kama Scorpio, huyu ni kijana mmojawapo kati ya vijanA walioingia na Askofu Valdermar ambao walijaribu kumuua Norbert ndani ya msitu wa Serengeti kwa bomu.
Haya yalikuwa yametendeka kwenye kisa cha WAKALA WA GIZA ambacho kiliwapa hasara kubwa kwa upande wao, muda huo alikuwa yupo nchini kwa kazi maalum ambayo alikuwa ameagizwa itimie. Alikuwa akimtazama yule Mwanamke ambaye ana mwili wa wastani pamoja na umbo la wastani ambalo lilikuwa limejengeka kimazoezi haswa, Scorpio alionekana kuchangnyikiwa kabisa kwa taarifa hiyo iliyokuwa hapo.
“Inamaana mpaka sasa hivi hakuna taarifa yake?” Scorpio aliuliza
“Ndiyo hivyo yaani haijulikani na mlipuko ule ni vyombo vyetu vile haiwezekani awe amefungua yeye bahasha” Msichana huyo alijibu.
“Josephine twende wenyewe tukapate taarifa hizo tusisubiri zitangazwe zimfikie Mheshimiwa, tukizipata tutajua ni jinsi gani ya kumtuliza akijua” Scorpio alimuambia msichana huyo ambaye hakuwa mwingine ila ni Josehine ambaye muda huo mwili wake ulikuwa umepungua kidogo, baada ya kusalimika kutoka kuuawa na pia kuwekwa mikononi mwa wanausalama katika kisa cha WAKALA WAGIZA sasa amerejea akiwa na muonekano mwingine kabisa.
.
Hadi kurejea kwake kazini alikuwa ameshaacha maafa mengi sana ikiwemo kupoteza maisha kwa Mutonga kule kwenye nyumba ya Mzee Mabina, sasa anaaamua kuungana na Scorpio katika kutafuta ukweli juu ya mwenzao ambaye hakuwa amerejea kabisa tofauti na kazi waliyompa muda iliyokuwa ikitaka ifanyike
Josephine Hilarius au maarufu kama Leopard Queen kama alivyokuwa akijiita ndani ya kisa cha WAKALA WAGIZA, ni mmoja kati ya wasichana hatari sana kuendelea kupumua kwa nchi hii ya Tanzania. Uendeleaji wake kupumua ndani ya nchi tayari ulikua umesababisha mambo mengi sana, msichana huyu aliponea chupuchupu katika kisa tajwa hapo kutokana na Norbert kumuacha akiwa hajiwezi akajua kuwa ndiyo alikuwa hajiwezi baada ya kupigwa chuma la pazia la mgongoni kimakosa na Marehemu Mzee Ole. Sasa amerejea baada ya kutoroka huko kukwepa mkono wa dola usimtie mkononi, umbile lake lile kubwa lililojaa haswa kiasi cha kufikia kumtamanisha mwanakikundi mwenzake lilikuwa limepungua kabisa na muda ingawa halikuwa limepoteza mvuto kabisa tena ndiyo kwanza ulizidi.
Kifungashio nacho hakikukimbia kabisa pamoja na kupungua kwa mwili bado kilikuwepo kimejaa huku kikijengeka kwa namna tofauti sana, ilikuwa ni mazoezi ya viungo ndiyo yaliyokuwa yameufanya mwili wake uweze kuwa namna hiyo kwa kipindi hiko ambacho alikuwa amepotea kwenye ramani ya macho ya mtu aliyebakia kidogo amuangamize. Nywele ambazo zilikuwa zikificha sehemu kubwa ya jicho lake ndiyo ulikuwa mtindo wake, miwani ya giza kamwe haikumtoka alipokuwa akizunguka katika sehemu mbalimbali majira ya kati. Hadi muda huo hakuwa ametambulika kabisa kuwa mwanamke hatari aikuwa amerudi ndani ya jiji hilo akiwa na jina jingine kabisa.
Kuja na jina hilo tayari alikuwa ameshafanya maafa makubwa kuliko hata yale ambayo aliyafanya hapo awali, Malkia wa kuzimu ambaye alikuwa akiwapigia watu simu na kuwaonya mambo kabla hawajaletewa wito wa kuzimu ndiye alikuwa huyo hapo akiwa tayari ameshavipa vyombo vya adola kizunguzungu kwa maafa ambayo alikuwa ameyafanya kwa kipindi tofauti cha muda akiwa yupo nchinI. Alikuwa yupo pamoja na kundi la Jack Shaw au Askofu Achim Valdremar pamoja na yeye mwenyewe ndani ya nchi hii.
Malikia huyu wa kuzimu akiwa pamoja na Scorpio walitoka hadi sehemu ya ndani kabisa ya ofisi hiyo na wakachukua gari aina ya toyota Altezaa ya rangi nyeusi, wote kwa pamoja waliingia na Scorpio ndiyo alikuwa dereva wa gari hilo. Walitokea katika lango jingine kabisa tofauti na lile lango ambalo alikuwa ameinglia Norbert, walipotokea huko walizunguka upande wa barabarani wakaja kutokea Rozana. Walipokuwa wakiipita stendi ya Rozana Josephine kwa macho yake mawili alimshuhudia Norbert akiwa amechukua usafiri wa pikipiki za kukodisha almaarufu kama ‘Bodaboda’ na kuingia kwnye barabara hiyo akawa anaelekea yalipo makutano ya barabara ya Chama. Alipomuona tu uso wake ulibadilika na ukawa ni uso wenye hasira sana hadi Scorpio aliyekuwa akiendesha gari aligundua hilo.
“Vipi Josephine kuna harufu ya kifo au ugonjwa?” Scorpio aliuliza kwa kimafumbo zaidi, aliposema ugonjwa alikuwa akimaanisha mleta balaa na aliposema harufu ya kifo alikuwa akimaanisha walikuwa wakiwindwa.
“Kuna ugonjwa ambao ulisababisha kazi ya mwanzo mimi na kina Benson ikikwama” Josephine alijibu na kisha akamuashiria mbele ambako waliona pikipiki ikiitafuna barabarba hiyo kuelekea Buguruni Chama.
“N001 ndiye yule kwenye pikipiki nafikiri umemuona” Alimpa utambulisho wa mtu huyo ambaye alikuwa amekaa kwenye pikipiki
Scorpio alipoupokea utambulisho huo uso wake uliweka sura isiyo na mzaha hata kidogo na kwa hasira kabisa, alianza kuongeza gia kwa nguvu sana. Hakujali kabisa kituo cha polisi kilichokuwa kipo jirani na eneo hilo yeye aliongeza wendo wa gari tu. Kutokana na Toyota Altezaa kuwa ni yenye kuundwa kwa ajili ya mashindano ilishika mwendo mkubwa sana na hadi makelele yake yaliyokuwa yamezoeleka ikinguruma yakazidi. Muda huo pikipiki aliyokuwa amepanda Norbert ilikuwa ikiwasha taa ya pembeni kuashiria kuwa ilikuwa ikiingia upande wa Kushoto kuelekea yalipo makutano ya barabara ya Tazara, hivyo ilipunguza mwendo pasipo dereva wake kutambua kuwa ilikuwa ikijiwa na gari kwa nyuma ikiwa ipo mwendo mkali sana. Dereva wa pikipiki alipokuwa akijaribu kukata kona Scorpio alikuwa yupo gia namba sita kwenye gari yake na mwendo akiwa yupo kilomita 180 kwa saa, kabla hata pikipiki haijakata kona aliibamiza nyuma kwa nguvu sana majira hayo ya mchana ambako hakukuwa na Askari wa usalama wa barabarani wa aina yeyote yule na kisha Mzungu kichaa aliyekuwa yupo kwenye usukani wa gari hilo alikata kona kuingia upande wa kulia akiwa na mwendo huo akisababisha matairi ya gari hilo kuteleza kama vile gari la mashindano.
Watu waliokuwa wameshuhudia tukio hilo kama vile walikuwa wakishuhudia tukio la filamu moja ya mbio za magari ya kimarekani lakini ilikuwa ni halisi kabisa, Mzungu Scorpio alipoibamiza pikipiki hiyo kwa nyuma wala hakujihangaisha kabisa kuweza kuijua yeye aliweza kumuangamiza Norbert aliamini kwa mzinga ule aliokuwa amepiga sehemu ya nyuma ya pikipiki hiyo lazima awe ni marehemu hadi muda huo. Alitokomea katika eneo hilo akiwaacha wale watu wasio na umakini katika macho wakiwa wameshindwa kukariri namba za gari hilo, wote waliokuwa wapo ndani ya eneo hilo walishika vichwa kwa jinsi pikipiki hiyo ilivyopatwa na msukosuko.
Muda ambao walikuwa wakikaribia kuigonga pikipiki ile, tayari Norbert alikuwa ameshawaona kwa kutumia kioo cha pembeni cha pikipiki hiyo baada ya kutupa jicho. Walipokaribia kuigusa pikipiki hiyo yeye alijichomoa kwenye kiti cha nyuma na kujitupa pembeni ambako alipiga sarakasi moja matata na kisha akabiringita kuelekea upande ulipo kituo cha daladala cha chama ambacho kilikuwa kipo karibu na shule ya msingi. Alipokoma kubiringira ndiyo gari ile ilikuwa ikiteleza kueleka barabara ya Mandela njia ya kwenda Tabata kwa ushupavu wa macho yake upeo wake wake mkali aliweza kusiona namba za gari hilo, muda huo tayari ile pikipiki ilikuwa imerushwa hadi barabara ya upande wa pili kati ya barabara hiyo ya njia mbili iliyokuwa ikielekea Ubungo na kuangukia mtaroni pamoja na dereva wake.
Hakutaka kupoteza muda yeye ajiinua kwa haraka sana na kisha akajifanya ni mtu ambaye alikuwa amechangaywa na ajali hiyo, alikimbia kwa kasi huku akiweka mikono kichwani kama kichaa hadi ilipo sehemu ambako kulikuwa na mashine nyingi za upasuaji mbao jirani kabisa na reli inayoelekea Kurasini pamoja na shimo la Udongo. Alikata kona akaingia ndani kwenye moja ya mitaa huku akikimbia kwa kasi na kundi la watu lilikuwa likimfukuza likiona kuwa alikuwa amechngayikiwa hivyo alihitaji kuwekwa chini atulizwe, aliongeza mbio zaidi hata wale waliokuwa wakimfukuza aliweza kuwapoteza kwa kona nyingi ambako aliiingia kwenye maeneo ambayo hawakujua kabisa kama kaingia kutokana na mitaa hiyo kuwa imebanana sana. Baada ya kuwapoteza watu hao ndipo alipokumbuka kuangalia vitu vyake akakuta vikiwa vipo salama kabisa kama alivyokuwa ameviacha kwenye mifuko yake ya suruali. Hapo alitoka na kutafuta pikipiki kwa mara nyingine tena na kisha akaingia barabarani akielekea katikati ya eneo la Bugurunina si kule ambako alikuwa ametokea, aliipita buguruni akaingia hadi Mitaa ya Ilala na hatimaye alienda kutokea Ilala Boma ambako aliunganisha na kuelekea kule ambako alikuwa akihitaji kuelekea kwa muda huo akitoka kule alipokuwa awali.
“Kwisha habari yake yule sidhani kama pale atapona ndiyo maana sikujihangaisha kumuangalia” Scorpio aliongea
“Shenzi kabisa mwanaharamu yule akafie mbele huko” Josephine aliongea kwa hasira sana
“Sasa yule alikuwa anawashinda nini nyinyi kazi rahisi kama hivyo”
“Ni mtu ambaye anatumia akili sana kuliko unavyomfikiria, anajua informationa zote kuhusu Don na mkewe”
“Sasa hivi ataenda kutoa information hizo kaburini tu si kwingine shenzi kabisa”
“Yaani kndi letu mwanzo alilimaliza ndani ya siku zisizopungua tano likaisha ni bora tu akafie huko mbele”
“Kweli alikuwa hatari sana huyu kiumbe sasa tuwape hasara hao wananchi wake aliokuwa akihakikisha kuwa wanakuwa salama”
“Hio ndiyo la muhimu kuwapoteza lengo wasijue tunafanya nini ndani ya muda huu shenzi kabisa” Josephine alionge na kisha akatoa simu yake ya mkononi na kubonyeza baadhi ya namba na kisha akaigusa kwenye kioo kwa mara kadhaa na akaiweka sikioni mwake.
“Hakikisha mnaanza kusambaza silaha zetu” Alipoongea maneno hayo alikata simu na kisha akairudisha mahali ilipokuwa awali.
Muda huo tayari walikuwa wameshapoteza kabisa ushahidi kama walikuwa wanafuatiliwa kutokana na nchi hii kutokuwa na teknolojia ya hali ya juu ya kamera barabarani kwa ajili ya ufuatiliaji magari, waliiingia Tabata ambako walienda hadi ilipo njia ya Kinyerezi na kisha wakaeelekea hadi Ukonga. Kwa kutumia nji za mkato waliweza kufika hadi Kiwalani ambako walielekea kwenye eneo ambalo mwenzao alikuwa ameenda, hapo walikuta gari ambayo ilikuwa ikitumiwa na mwenzako ikiwa bado ipo palepale kutokana na ulinzi wa gari hiyo. Ilikuwa na ulinzi mkubwa sana na ilihitaji neno la siri kuweza kusogea kwa matairi yake jambo ambalo iliwawia vigumu maafisa wa jeshi la polisi kuivuta gari hiyo, eneo hilo bado maafisa wa jeshi la polisi walikuwa wapo wakiendelea na taratibu ndogondogo baada ya mwili kuwa imeshaondolewa. Hiyo iliwabidi watulie mahali kuweza kusubiri hadi maofisa hao waondoke kwani waliamini kabisa wasingeweza kukaa kwenye eneo hilo baada ya kukamilisha uchunguzi wao, waliamua kushuka na kuanza kujichanganya na watu ambao walikuwa wapo karibu na eneo hilo ili kuweza kupata umbea kwa kila kitu ambacho walikuwa wameshuhudia kwenye eneo hilo. Muda huo ndipo walipoweza kubaini kuwa aliyeuawa ndani ya nyumba hiyo alikuwa ni mwanaume na si mwanamke kama walivyokuwa wakidhania, hapo walijua kabisa aliyekuwa amepoteza maisha ndani ya nyumba hiyo alikuwa ni mwenzao aliyekuwa yupo kazini katika kuchukua ushahidi ambao ungewaweka mabosi wao matatani.
Majira ya jioni askari wa jeshi la polisi waliondoka kwenye eneo hilo wakiliacha gari hilo ambalo walikuwa wakienda kutafuta mtaalam wa kuja kusaidia kulitoa eneo hilo kwa kucheza na Tarakilishi, hawakujua kabisa kuondoka katika eneo hilo walikuwa wakiharibu kabisa kwani gari hilo wenyewe hawakuwa mbali nalo na walikuwa wakisubiri tu waweze kutokomea katika eneo hilo wawze kuchukua mali yao na kuondoka nayo katika eneo hilo. Walipoondoka kabisa wote na kuwaacha baadhi ya raia wakiingia kwenye eneo hilo kwa kutoacha ulinzi wakiona kuwa hakukuwa na kingine cha ziada tofauti na nyumba zingine za wanausalama, Josphine ndiyo alikuja kusogea hadi jirani na gari hilo ambalo lilikuwa limefungwa vizuri milango yake.
Alipolifikia gari hilo alitoa rimoti mfukoni mwake ambayo alibonyza milango ikatii amri ikafunguka, aliingia ndani ya gari hiyo katika muda ambao watu waliokuwa akiingia kuangalia mabaki ya nyumba hiyo hasa wauza chuma walikuwa hawamtilii maanani kabisa. Watu waliokuwa wapo jirani gari hilo majira hayo ya usiku waliweza kushtushwa na mlio wa kuwaka kwa gari hilo pamoja na taa za mbele kuwashwa. Wakiwa hawajajua ni nani aliyeingia ndani ya gari hiyo walishtukia ikianza kujongea kwenda mbele kuifuata barabara ya mkato iliyokuwa ikielekea barabara kuu, ile Toyote Altezza ilikuwa imetangulia mbele na gari hiyo ikafuata nyuma katika kuliacha eneo hilo.
Kituo cha kwanza kukifikia ilikuwa ni ndani nyumba ya shirika lao, huko Norbert aliingia moja kwa moja hadi wakati namba za gari ambalo lilikuwa likifanya jaribio la kutaka kumuua lilikuwa zilikuwa zipo kwenye kichwa chake. Alienda moja kwa moja hadi kwenye Tarakilishi zenye uwezo mkubwa sana ambazo zilikuwa zipo ndani ya nyumba hiyo na akawasha mojawapo na kisha kuingiza neno la siri kuweza kuzitumia. Norbert alichoamua kukifanya basda ya kufanya hivyo aliamua kuingia kwa njia isiyo rasmi kabisa katika tovuti ya mamlaka ya mapato nchini TRA, ujuzi alionao ambao aliupata kwenye mafunzo ya kiujasusi katika uchambuzi wa Tarakilishi haukumuwia vigumu kabisa kuweza kufika kwenye eneo ambalo angeweza kuandika namba za gari hilo na kuweza kumpata mmiliki wa gari iliyokuwa ikidhamiria kupoteza uhai wake muda mfupi uliopita. Aliingiza namba za gari hilo na kisha akasubiri kwa muda na haikufika hata muda mrefu aliweza kuona gari hilo husika, haikika haikuwa namba ya gari dogo bali ilikuwa ni namba ya lori ambalo ilikuwa halipo barabarani na mmliki wa lori hilo ndiyo ilichnganya zaidi.
Ilikuwa ni namba ya lori ambalo lipo chini ya Nouther brothers ambayo alikuwa akitambua kabisa wamiliki wake walikuwa tayari wameshaiaga dunia kwa kukatishwa pumzi na yeye mwenyewe. Nouther hiyo brother ilikuwa ikisimama mbadala wa kaka wawili waliokuwa wenyeji wa jiji la Arusha ambako ni kaskazini. Watu hao aliwambua walikuwa ni Filbert Ole maarufu kama Mzee Ole pamoja na mdogo wake Wilson Ole ambao wote ni marehemu hadi muda huo, alijiuliza kuwa kampuni hiyo ilikuwa ni chini ya nani ikiwa watu hao walikuwa ni marehemu lakini hakupata jibu kabisa Alipotaka kujiaminisha kuwa namba hizo zilikuwa zimebuniwa tu jambo hilo alikataa katakata aliona kulikuwa na uhusiano wa jambo hilo. Aliamua kuangalia kabisa namba ya chesesi ya gari hiyo iliyokuwa imesajiliwa, hapo alibaini kabisa gari hilo ambalo ni Lori kubwa la mizigo lililokuwa na limesajiliwa kwa namba zile zilizokuwepo kwenye ile gari iliyojaribu kuyatoa maisha yake. Zilikuwa zimesajiliwa kwa namba jingine na hata alipoangalia picha za gari hilo aliona kuwa ilikuwa ni lori ikiwa namba za usajili tofauti na awali.
Hakika ulikuwa ni uozo na uzembe mkubwa sana uliokuwa umefanywa na watu waliokuwa wapo mamlaka ya mapato kwa kuisajili gari moja mara mbili, Norbert aliangalia mmiliki a gari hilo na akaona kuwa lori hilo lilikuwa limehama umiliki na sasa lilikuwa lipo chini ya umiliki wa kampuni ya usafirishaji mafuta kutoka bandarini jijini Dar es salaam na kuelekea nchi za jirani ambazo ziolikuwa zikitumia bandari hiyo.
“Huu ni uzembe mkubwa sana au ni wizi uliofanyika hapa kwa kutumia mgongo wa mtu haiwezekani kabisa suala hilo” Norbert aliongea huku akichukua kijitabu kidogo na kunakili anuani zote za mmiliki mpya wa gari hilo la mizigo ambalo hadi muda huo lilikuwa lipo barabarani likifanya kazi kama kawaida. Baada ya hapo aliamua kuingia kwenye mtandao kwa mara nyingine akaaanza kutazama tovuti ya kampuni ile iliyokuwa ikimiliki gari hilo, aliweza kuichunguza tovuti hiyo kwa umakini mkubwa sana ambako alibaini kabisa kuwa kulikuwa kuna mmiliki mmoja ambaye alikuwa ni mwenye asili ya bara Hindi na hakukuwa na mwingine. Norbert alinakili anuani za makazi ya mmiliki huyo akiwa amemuweka kwenye orodha ambaye alitakiwa kuipitia kwa ajili ya kazi yake hiyo iliyokuwa ikimkabili.
“Tandu ana miguu mingi sana na kila mguu hutoa mchango wake katika safari yake,nina imani yote nitaifikia” Aliongea mwenyewe huku akimkazia macho mmiliki wa kampuni hiyo ya usafirishaji.
Majira ya usiku magari yote mawili yaliyoondoka eneo la Yombo kule kulipotokea mlipuko, yaliingia ndani ya nyumba moja ya kifahari sana iliyopo maeneo ya Kibada. Josephine pamoja na Scorpio walishuka na wote waliingia ndani ya nyumba hiyo ambako walipokewa na Mzungu mwingine anayeItwa Spider ambao ni watu wa karibu sana wa Askofu Valdermar. Alikuwa ni yuleyule ambaye alikuwa naye pamoja na Scorpio katika siku ambayo walimuwekeea Norbert bomu katika msitu wa Serengeti wakijua alikuwa ni mtumishi wa kiimani aliyekuwa amekataa kwenda kinyume na matakwa yao, sasa wamerejea nchini kwa pamoja wakiwa muonekano tofauti sana na ule wa kiutumishi wa Mungu. Safari hii walikuwa na muonekano wa watu waliokuwa wakijiweza kiuchumi ambao walikuwa wameamua kuja kuishi nchini Tanzania, wote kwa pamoja waliingia kwa kazi moja maalum na waliingia kwa nyakati mbili tofauti sana kama vile watu wasiojuana hata kidogo.
Walikuwa wakitambulika kama wazungu waliokuwa na uraia wa nchi tofauti kabisa na idara ya uamiaji lakini yote ilikuwa ni kuipumbaza serikali isiwe na shaka juu yako, wazungu hawa walipoonanaa hapo ndani waligoengesha mkono yao kihuni zaidi na kisha Josephine na Spider wakakumbatiana kama ilivyo salamu wakikutana pamoja. Wote waliongoza njia hadi ndani kabisa na nyumba huyo ya kifahari kwenye sebule pana kabisa, hapo walikutana na Askofu Valdermar mwenyewe akiwa ameketi akiwa na mavazi ya kulalia tu.
Mikononi mwake alikuwa ameshika bilauri ya mvinyo huku akiangalia luninga, Askofu huyu wa kuzimu ali[owaona tu hao vijana wake aliweka kinywaji mezani kisha akasimama. Alienda hadi walipo vijana hao na alianza kupeana salamu na kila mmoja, alianza na Josephine ambaye walipeana mabusu ya kwenye mashavu kisha akasogea hadi Scorpio ambaye alinyooshewa mkono na Askofu huyo. Yeye kunyooshewa mkono huko kulimfanya aushike mkono wa Askofu huyo kuzimu na kisha akaubusu halafu akakumbatiana naye, baada ya hapo kila mmoja alitafuta mahali pa kukaa kwenye sebule hiyo kwani tayari walikuw wamaeshajulikana kuwa walikuwa na zaidi ya jambo la kuongea muda huo.
“Ujio wenu unaashiria kabisa kuwa kuna jipya lipi hilo” Askofu Valdermar aliuliza
“Madam knbwa zaidi ni kwamba Kelvin amekwenda na maji, hii inaonekana kuna mtu yupo nyuma ya nyayo zetu akitufuatilia” Scorpio alieleza
“Je hakuacha ushahidi wowote huko eneo la tukio wa kuwaweka ninyi hatiani? Waliulizwa
“Aliacha Subaru ile ambayo ina pean code ila tumeiwahi tayari na tumeileta hapa ndani” Josephine alijibu
“Vizuri sana sasa ibadilini namba za usajili pamoja na stika zote” Aliwapa amri na kisha akawatazama mmoja baada ya mwingine na akauliza, “ni nyinyi mliyeigonga pikipiki Buguruni mchana wa leo?”
“Ndiyo Madam ni sisi” Josephine alijibu
“Kulikuwa na haja gani ya kumgonga ile pikipiki kinyama namna ile ikiwa dereva mwenyewe ni normal person? Waliulizwa
“Chanzo ilikua si dereva bali abiria aliyekuwa amembeba” Scorpio alijibu.
“Ok nipe habari yote si nusunusu” Alihitaji kupewa habari yote
“Norbert Kaila ndiyo kiumbe aliyekuwa abiria wa ile pikipiki its better to be wanted for his murder rather to let him (ni bora kuwa tunatfautwa kwa mauaji yake kuliko kumuacha) apumue ndani ya mgongo wa ardhi” Josephine alifafanua kwa maelezo ambayo yalihitaji ufafanuzi zaidi kwa mkuu wao huyo.
“How(kivipi)?” Alihitaji ufafanuzi
“Ni jasusi wa EASA mwenye code N ya kwanza kabisa maarufu kama N001 nafikiri ushasikia habari za huyo mtu” Josephine alifafanua
“Oooh! No! Sasa mmejiweka pabaya zaidi nyinyi, maiti yake haijonekana eneo la ajali zaidi ya kuonekana ya dereva wa pikipiki tu yule” Askofu Valdermar safari hii alisimama wima alipoongea maneno hayo kisha akawatazama vijana wake.
“Hii inaonesha amekwepa mdomo wa kifo na kama alikuwa hajajua uwepo wenu basi ndiyo mmempa ishara ya kuweza kuwafuatilia” Aliwaambia na wote walichoka na taarifa hiyo kwani hawakutegemea kabisa kama angeweza kutoka kwenye ajali ile ndiyo maana hawakuhangaika kabisa kuangalia kama alikumbwa na kadhia ile.
“How come? Amepona vipi pale huyu?” Scorpio aliuliza kwa mshngao sana
“Inaonekana ni mwenye hisia za ajabu na pia uwezo wa juu wa kutumia sense organs zake, sasa wekeni macho ya umakini na kuanzia sasa ni mwendo wa kupoteza ushahidi tu hakuna jingine tumeni wito kwa watu tofauti kabisa maana washajua hawa tupo after ile ripoti” Askofu Valermar aliwaambia
“Ingependeza zaidi na huyu kiumbe tukampoteza ndani ya siku chache tu kwani yeye ndiye aliyeipoteza timu nzima iliyobaki kidogo tuichukue nchi hii” Josephine aliongea na kumfanya Askofu Valdermar amuangalie huku akikumbuka vifo vya vijana wake ambao wengine alikuwa akiwatumia kimapenzi kabisa tofuati na mume wake wa haramu.
“Huyo hakikisheni mnamleta kwangu akiwa yupo hai ni mimi ndiyo nitajua nini cha kufanya, kwa sasa andaeni silaha nataka ziende kwenye masanduku tofauti ya posta usiku huu huu asubuhi yaanze kazi” Aliwapa amri na kisha alinyanyuka hapo sebuleni akiwaacha vijana wake wenyewe.
“Hivi kaponeje yule kiumbe na mzinga ule niliobamiza?” Aliuliza akionekana ni mwenye kuchnganyikiwa kabisa
“Scorpio yule ni mwanaharamu msikie tu, ana akili kama ana dawa vile” Josephine aliongea
“Inaonekana ni kiumbe mwenye uwezo wa hali ya juu sana na kama hawa Africa wapo wachache sana na inabidi wapotezwe kabisa tuzidi kupata madili” Spider naye alichangia
“Kabisa Spider huyu mara ya pili akionekana mbele ya mcho yetu basi ni kumpiga risasi tu hata kwa sniper au kumuua kwa mkono” Scorpio alichangia
“Akili nyingi zinahitajika kuweza kupigana na kiumbe huyu kuliko hasira. Benjamin na Thomas walipotea walipoleta hasira kwa huyu kiumbe, ni mtu mwnye kutumia akili hata akiwa amewekewa silaha na si mwenye kuingiwa na hofu kabisa” Josephine aliongea na kisha akainuka akaenda hadi lilipo jokofu la vinywaji ndani ya nyumba hiyuo, alitoa chupa moja ya mvinyo na akaelekea mezani ambako alichukua bilauri akaumimina mvinyo huo. Baada ya hapo alirejea sebuleni walipo wenzake ambao walikuwa wakiongea mambo yao ya kawaida tu
“Madam atajua jinsi ya kuwatuliza waheshimiwa Laptop tunsyo moja na bado neno la siri sidhani kama lina maana ndani yake” Aloongea alipofika mbele yao ukiwa akiwakaribisha bilauri hiyo ya mvinyo kiishara.
“Nenola humo linasemaje?” Spider aliuliza
“BARA JANGWA ndiyo nimelikuta kwenye faili lenye neno la siri bado hatujajua jinsi la kulidadavua hili,Laptop aliyoenda kuifuata Kelvin ilikuwa na neno siri jingine na baadhi ya ushahidi hivyo tatu zilizobakia ambazo ni namba mbili tatu na nne ndiyo zina ukamilifu wa hili fumbo kwa mujibu wa kibaraka wetu aliyekuwa yupo TISS. Ya mwisho ina vielelezo vingine vyote ila kiumbe mmoja anayeitwa Jama aliyeshiriki utafiti huu bado anapumua na sumu ilimpata mke wake, tujue maneno ya siri yote yakikusanywa mbele yake wakubwa tumewaweka pabaya na sisi ulaji hatuna kabisa jamani” Aliwafafanulia na kuwafanya wote wazame kwenye tafakuri ya kile walichoambiwa.
[9]
ASUBUHI ILIYOFUATA
Norbert akiwa yupo katika muonekano wake wa kinadhifu akiwa ni mwenye suti nyeusi pamoja kofia aina ya hat nyeusi ambayo alikuwa akipenda kuitumia kwenye kazi yake, alienda hadi kwenye ofisi za kampuni ya usafirishaji mafuta maarufu sana nchini. Ilikuwa ni kampuni ile ambayo umiliki wa lori lililokuwa mali ya Nourthers brother ulihamia hapo, akiwa ni mwenye mkoba wa namba mweusi alifika hadi eneo la mapokezi kwenye kampuni hiyo ambako alikuta watu wakiwa wanasubiria kuweza kupata huduma. Yeye pia ilimbidi asubirie kwenye viti maalum vya kusubiria kwa wageni huku akiwa akipigwa na kiyoyozi pamoja kupoteza muda kwa kusoma jarida, ni ndani ya siku ya pili kati ya siku kumi ambazo alikuwa amepewa kuhakikisha hiyo kazi ilikuwa ikikamilika vilivyo.
Baada ya kusubiri kwa kipindi kifupi cha muda hatimaye aliruhusiwa aingie ndani kwenda kuonana na bosi wa kampuni hiyo, alikuwa hana miadi kabisa na bosi wa hapo lakini kutokana na muonekano wake ulivyo kama mtu aliyekuwa akitoa harufu ya pesa kila akitembea. Aliruhusiwa kwenda kuonana naye baada ya kuonekana na kamera iliyokuwa ikionesha watu moja kwa moja chumbani kwa bosi huyo, uso wake ulikuwa umefichwa kwa asilimia kubwa na kofia aliyovaa jambo ambalo lilifanya aweze kupoteza utambulisho kama ni Norbert Kaila yule mwandishi wa habari ambaye alikuwa ni nuksi sana akiwa kazini kwa watu wenye mipango michafu.
“Naam Mr Mashishanga karibu sana” Alikaribishiwa na Bosi yuleyule ambaye aliyekuwa ameona picha zake kwenye tovuti za kampuni hiyo
“Thanks a lot Khemiri, nipo kwa ajili ya kuongea biashara maalum so sorry sikutoa apointment mapema. Nina mzigo upo njiani na meli ukiwa upo kwenye matenki ya mafuta ya semi trela nahiraji opite bandarini bila kukaguliwa na pia kampuni yako yenye kuaminiwa iweze kunisafirishia hadi kwenye headquarters zangu” Aliongea kuzidi kumvuta mwenyeji wake kwani alikwisha tambua kabisa kuwa mtu huyo alikuwa akishiriki michezo michafu kabisa kwenye serikali.
“Ok Mr Mashishanga ni mzigo wa aina gani na kama ni zaidi ya petroleum nafikiri nahtaji kuongea na wewe out of this office the daya after tomorrow, ujiandae kulipa hela zaidi ya hapo maaa ni dangerous game tunacheza. Kukwepa kodi na kusafirisha mzigo wa aina hiyo uanozungumza maana nishaujua tayari”
“OK hamna tabu kabisa” Norbert alipokubali hivyo simu ya mezani ya kampuni hiyo iliita na kumfanya Khemiri ampe ishara ya kumuomba radhi na kisha akaipokea simu hiyo na kuongea na huyo aliyempigia simu
“Ndiyo Fina…. ngoja nimuone” Khemiri aliongea na kisha akatazama kwenye kioo kimojawapo kati ya vioo vya Tarakilishi vilivyokuwa vikitazama upande wake halafu akasema,”Ok akitoka huyu mwambie aingie”
Alikata simu na kisha macho yake yote aliyarudishwa kwa Norbert aliyekuwa akisubiri amalize kuongea na simu hiyo halafu akasema,”Mr Mashishanga nafikiri mzigo wako bado una siku kadhaa kabla haujafika bandarini sasa basi the day after tomorrow tutaongea then niende nikachukue kibali kwa Mheshimiwa mzigho huo upitishwe bila ya kukaguliwa”.
“Ok Mr Khemiri kadi yangu ya mawasilino ni hii hapa nafikiri tutawasilina zaidi”
“Ok pokea na kwangu kabisa nafikiri kila mmoja sasa anaayo mawasiliano na mwenzake kilichobaki na kuingia deal”
“Ok asante have a nice day” Norbert aliongea na kisha akapeana nkono wa kuagana na alitoka humo ofisni, alipofungua mlango aliweza kumshuhudia Spider akinyanyuka upesi kwenye sehemu ya kupumzika wanaosubiri kuonana na Khemiri. Alimpita kama hamjui vile ingawa moyoni mwake alishaanza kuweka shaka kabisa ya juu ya ujio wake mahala hapo haukuwa wa kawaida kabisa, alijua wazi mtu huyo hakuwa mfanyabiashra yeyote zaidi ya kuwa mhlifu na alikuwa yupo hapo kwa ajili ya kazi maalum. Uwepo wa mahusiano baina yake na bosi wa hapo alihisi kabisa, alijipa tahadhari kabisa na bosi huyo hata katika siku ambayo angeonana naye wazungumze kuhusu suala hilo.
ILIPOTIMU SAA NNE ASUBUHI
Jeshi la polisi lilichangayikiwa kabisa kutokana na kutokea kwa milipuko katika ofisi za serikali na hata ofisi binafsi, watu mbalimbali walikuwa wameuawa ndani ya milipuko hiyo kwa saa kadhaa tu tangu kuingia kwa siku mpya. Jambo hilo lilipofika kwa raia wa kawaida wa ndani ya nchi hii yenye amani waliingiwa na hofu kabisa wakiona kuwa ugaidi ndiyo ulikuwa umeanza kuikumba nchi nzuri ambayo haikuwahi kukumbwa na mlipuko wa ina hii tangu ulipotokea ule mwaka 1998 kwenye ubalozi wa Marekani. Wale ambao ambao walikuwa na hofu kubwa sana ya kupoteza maisha yao wakiwa wapo ofisini walirudi wote majumbani mwao wakiwa salama huku baadhi yao wakiishia njiani baada ya pumzi zao kukatika kabla hata hawajafika kwenye nyumba zao. Milipuko mingine kabisa ilitokea kwenye baadhi ya daladala na pia magari binfasi jambo ambalo lilzidisha hofu kubwa sana kwa wananchi waliokuwa wakitumia vyombo vya moto barabarani, nusu saa baadaye kwa hofu kulipuliwa kwa ofisi mbalimbali ilibidi kampuni zile za kiserikali na hata binafsi zifunge ofisi zao. Mamia waliokuwa wakirudi makwao kwenye jiji la Dar es salaama walishiriki matembezi yasiyo na hisani kutokana na hofu ya lipuliwa wakiwa ndani ya vyombo vya moto, wengi walihisi kuwa hao waliokuwa wakifanya matukio hayo walikuwa ni mgaidi waliokuwa wakijitoa mhanga na pia walikuwa wakitega mabomu kwenye ofisi mbalimbali.
Siku hiyo madereva wa daladala pamoja Teksi waliilaani kuliko siku zao zote zilizowahi kutokea ndani ya maisha yao, waliona kabisa kuwa kulikuwa na kasumba ilikuwa imeingia ndani ya jiji la Dar es salaama ambayo ilikuwa imepanga kuhakikisha wanakosa ulaji kwa siku hiyo. Barabara zilizokuwa zikitumika katikati ya jijizote zilikuwa tupu jambo ambalo halikuwahi kutokea hata pale ulipotokea mgomo wa madereva wa mabasi ya usafiri, wale wenye magari binafsi nao waliogopa kabisa kutumia magari yao kwa siku hiyo kutokana na kuhofia huenda magari yao hayo yalikuwa yametegwa bomu hivyo wangekatishiwa maisha yao wakiwa wapo njiani.
Ilikuwa ni siku ambayo shirika la posta nchini lilikuwa limetumia sana vyombo vya vyao usafiri kuelekea sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam kusambaza barua, haikuwahi kabisa kutokea suala kama hili na siku hiyo ndiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa. Wafanyazi wa shirika hlo walitumia muda mwingi sana kuzunguka ndani ya siku hiyo masaa kadhaa kabla ya kutokea milipuko hiyo kusambaza barua mbalimbali ambazo zilikuwa zimeingia, ilipotokea kasumba ya mlipuko walikuwa tayari wameshasambaza barua nyingi sana hata wenyewe waliruhusiwa kwenda majumbani mwao na barua za siku hiyo ambazo hazikumalizika kabisa zingekuja kusambazwa siku inayofuata. Siku hiyo hawakuhisi kabisa kuwa wao ndiyo walikuwa wametumika kama nnjia ya kusambaza kasumba hiyo iliyokuwa ikisumbua ndani ya jiji, waliona ni ugaidi na wala hawakutambua kuwa silaha hizo zilizokuwa zikiwangamiza watu wao ndiyo walikuwa wakizisambaza ndani ya siku hiyo.
Siku ambayo haitokuja kusahaulika ndani ya nchi ya Tanzania kwa jinsi magari ya zimamoto yalivyofanya kazi ya zaida ya kuzima moto katika sehemu mbalimbali zilizokuwa zimetokea milipuko, walikuwa wakihangaika barabarani ambako magari mengi yalilipuka na hata kwenye baadhi ya ofisi ambazo zilikuwa zimepatwa na balaa hilo. Hakika walifanya kazi ya ziada nao lakini katu hawakuthubutu kuyatelekeza magari yao hata kulipotokea milipuko hiyo, waliendelea na kazi ya kuzima moto na pia kuokoa baadhi waliokuwa wamejeruhiwa wakishirikiana na vikosi vya uokoaji ambao nao walikuwa wamejitoa mhanga wasikimbie kazi yao ili tu waokoe maisha ya majeruhi ambao walihitajika kupata msaada waweze kuendelea kuvuta pumzi ndani ya dunia hii.
Muda ambao wafanyakazi wote wanaruhusiwa kwenda makwao kwa hofu ya kukumbwa na tukio la kigaidi wakiwa hapo maofisini, Norbert alikuwa yupo kwenye ofisi ambazo alikuwa akifanyia kazi Moses hapa nchini.Ilikuwa ni ndani ya maabara ya umoja wa mataifa kwenye chumba cha ofisi ya Moses ambako walikuwa wapo wawil tu, ndani ya muda huo kila mmoja alikuwa tayari ameshampa taarifa aliyokuwa akikifahamu yeye kwa upande wake. Walibadilishana mawazo na wote hawakuona kabisa kiini kilichokuwa kikiwapa mwangaza juu ya suala hilo, wala hawakuona dalili zozote za utegwaji wa mambomu mazito kwenye suala hilo. Wote waliona kuwa hilo suala lilikuwa na zaidi ya jambo nyuma yake.
Muda mfupi baadaye wakiwa wamekaa hapo ofisni simu ya Norbert ambaye alikuwa kifahamika kama mwandishi wa habari kwa waandishi wa habari nchii, iliingia ujumbe mfupi wa maneno ambao alipoufungua tu alibaki akiguna na kisha aliinua uso wake kumtazama Moses. Ilikuwa ni habari juu ya kushuhudiwa kwa mtu akiwa amekumbwa na mlipuko kwenye hadhara kwa mara ya kwanza, jambo hilo lilimfanya Norbert aguna kwani alikuwa ameshapta uhakika wa jambo walilokuwa wakilitafuta kwa jinsi walivyoshuhudia ujumbe huuo mfupi wa maneno ambao uliingia kwenuye simu yake.
“Vipi kuna mpya?” Moses alimuuliza alipoona mguno umemtoka.
“Hii ni zaidi ya mpya na sasa ndiyo napata jibu ya chanzo hata cha kulipuka ile ya nyumba ya mwanausalama kule Kiwalani, hapa nimetumiwa na mwandishi wa habari mwenzangu yeye anasema ameshuhudia mtu akifungua bahasha nyeupe kwenye kituo cha daladala na alikumbwa na mlipuko akafia hapohapo” Norbert aliongea
“Ooooh! Damna hawa watu wanasambaza Mail bomb, inabidi tahadhari itolewe mapema kabisa la si hivyo jiji litaisha hili”
“Yap ni mail bomb hizi na katika msambazaji mmoja tayari nilikuwa nimemuweka chini ya ulinzi nilimpompekua nilimkuta akiwa na bahasaha ndani yake. Nilipoifungua bahasha hiyo nilikutana na ujumbe na bahasha nyingine yenye stempu ya mwanamke kisu akiwa ameonesha mgongo na kisha ina mhuri pamoja na neno lililosomeaka ‘wito wa kuzimu’, aise nilipotaka kuifungua hiyo bahasha ya ndani nilimuona yule jamaa akicheka kumbe alikuwa akijua nilikuwa nafungua kaburi. Sasa inabidi kuwasaka tu hao wanaopelekea bahasha hizo mikoani kabla hata hawajaleta maafa zaidi naamini tutapata na kingine tulichokuwa tukikihitaji ndani ya muda muafaka”
“Muda huohuo tujishughulishe na kumtafuta Jama Wa Majama nafikiri Tanzania itabaki huru kabisa ikiwa atakuwepo”
“Kwani huyu jama katekwa au kayeyuka kujihami”
“Kayeyuka kujihami ana maadui wengi sana wanaomuwinda kwani yeye ndiye pekee aliyebaki katika watu wale waliofanya utafiti baada ya kubaini kulikuwa madudu makubwa kwenye wizara zaidi ya mbili”
“Aise basi poa ila muonye shem asije akapokea mzigo kama huo tu si unajua ana kichanga itakuwa msala sana kwako”
“Hilo usihofu sana, nitafannya sasa hivi”
Mail bomb au Letter bomb au kwa kugha ya kiswahili bomu kwa njia ya barua, ni bomu ambalo hutumiwa mtu kwa njia ya barua. Hili bomu ambalo hutengenezwa kwa njia ya barua likiwa nalengo la kuua au kujeruhi mpokeaji wake. Bomu hili hutengenezwa kwa asilimia 75 za unga aluminium na silimia 25 za unga wa madini ya chuma, vitu hivi huwekwa kwenye kitu ambacho ni kigumu sana kupitisha joto na hewa na kisha hufungwa kwa nje na kuwekwa bahasha ya kawaida tu. Barua hii kamamtumiaji akiipata na kuifungua bila ya kujua basi maisha yake huwa yanakatikia hapo kwani ndiyo namna ambavyo inalipuka , hii ilikuwa ni tishio sana katika miaka ya nyuma katika bara la Amerika na Ulaya ambako vikundi mbalimbali vya uhalifu vilikuwa vikiua raia kwa namna hiyo pasipo wenyewe kutambua. Mtindo huo hakuwa kusikika sana ndani ya ukanda huu wa Afrika ya mshariki na muda huo ilikuwa ni mara ya kwanza kusikika katika ukanda huu, ulikuwa tayari umemaliza mawaziri wawili pamoja na wanausalama wa vitengo tofauti pasipo wao kujua kuwa ilikuwa ni bomu la njia ya barua. Maaskari wa jeshi la polisi walihisi kuwa hiyo ilikuwa ni ni tukio la ugaidi wa kujilipua kwa mhanga lilivyoanza kukumba jiji la Dar es salaam
Kuingia ujumbe maneno ambao ulikuwa na taarifa juu ya kushuhudiwa mtu akifa kwa mlipuko kwenye kituo cha daldala baadaya kufungua bahasha hiyo, Norbert ndipo alipotambua kuwa maadui wa nchi hii walikuwa wakitumia mabomu hayo kuweza kuwapoteza lengo na kulikuwa na zaidi ya kitu walichokuwa wakikifanya. Aliona hiyo ilikuwa ni njia mojawapo pia ya kuvichnganya vyombo vya usalama visiweze kufanya kazi yake kwa ufasaha kabisa. Yeye mwenyewe alikuwa amesalimika kabisa kutoka kwenye kifo kama hicho haswa baada ya kutaka kufungua sehemu ya ndani ambayo ilikuwa ipo kwenye mfumo wa bahasha ambao ilikuwa imetuna kidogo, hapo ndipo alijua kuwa sehemu hiyo ya ndani ilikuwa ni maarufu kwa jina la isolation ambayo laiti kama ingeonekana nje tu basi angekuwa ni maiti yeye na wote waliokuwa ndani ya nyumba ile kule Kiwalani.
Bahasha ya ndani ilikuwa imewekwa mihuri ikiwa stempu ambazo hazikuwahi kuonekana kwenye ofisi za posta, stempu hizo Norbert alibaini kabisa kuwa zilikuwa na lengo la kuzidi kumshawishi mpokeaji afungue bahasha hiyo hasa kwa kuweka mhuri ambao ulikuwa ni kama utani vile kwani hakukuwa na mhuri kama huo. Pia aliweza kubaini kuwa bahasha ile yenye muhuri ilikuwa imesambazwa kwa kufichwa ndani ya bahasha nyingine kwani ingeleta kabisa wasiwasi kwa wasambazaji wa kawaida na hata isingemfikia mlengwa ikiwa tu itaonekana jinsi ilivvyo kwa ndani. Hakika kulikuwa na watu wenye akili zaidi waliokuwa wakicheza na akili zao ndani ya kipindi cha muda mfupi kabla hajaweza kubaini.
“Kazi hii ishafika mikononi mwangu jana tu ikitoka kwa CE wacha niingie kazini, waambie waliokuwa wapo kazini kwenye kazi hii wawe off sipendi kuingiliwa kazi labda nikihitaji mtu. Nina siku tisa hadi sasa za kuikamilisha kazi hii sasa ndani ya siku siku hizi sipendi kazi yangu iharibiwe na yeyote yule nafikiri uanielewa” Norbert alisema
“Hilo halina shaka nafikiri ni kuwaambia vijana wangu pamoja na millitary intelligence waliokuwa wapo kazini wawe off ikiwa wewe umeingia kwenye kazi hiyo” Moses alisema
“Kabisa”
“Oki kila heri najua unaenda kucheza makida na rafiki kifo”
“hakika ni makida kweli jana yenyewe nimecheza naye Bugurni Chama, ningechelewa kucheza basi ningekuwa ni marehemu kwa jinsi Altezza ile ilivyobamiza kwa nguvu pikipiki niliyokuwa nimeipanda”
“Kuwa mwangalifu tu usije ukanilizia shem wangu Norene, pia ukijogoo huo uwe makini”
“Hata kuli huhitaji liwazo katika muda wa kazi hivyo na mimi nitajitaji pia sitaki uzito uzidi si unajua kazi yenyewe sifa wepesi”
“Haya ndugu kila la heri tu kwenye kazi yako hiyo”
Muda huohuo Norbert aliondoka ofisini hapo kwa Moses akimuacha akiendelea na kazi nyingine, yeye alikuwa hajaondoka kabisa ingawa wafanyakazi wa maabara hiyo pia walikuwa wameondoka majumbani kwao. Hakuwa na uoga kuhusu milipuko iyo iliyokuwa ikitokea, aliendelea na kazi zake kwani alikuwa ni tegemezi sana ndani ya maabara hiyo hivyo hakutaka alemae kwa kitu kidgo kama hicho. Ujasiri wake wa kimafunzo ndiyo ulimuongoza kubaki hapo na si kitu kingine kile, hakufunzwa uoga kabisa hivyo kuondoka kisa suala hilo kuhofia kupoteza maisha haikuwa ndani ya ubongo wake kabisa.
ROBO SAA BAADAYE
Simu ya kuondolewa kwa vijana wa kijeshi wa kitengo maalum waliokuwa wakifuatilia matukio hayo, ilikuwa tayari imeshafika kwenye meza ya Jenerali Marwa. Alikuwa ameipata simu hiyo muda mfupi kutoka kwa Moses akiwa anamuambia juu ya uwepo wa jasusi hatari kazini, alitakiwa aondoe vijana hao kwenye kazi hiyo wasije wakaharibu kazi ya jasusi wa kuaminika aliyekuwa ameingia kazini
Jenerali Marwa alipoipata simu hiyo moja kwa moj aliamua kumuita Mnadhimu mkuu wa ndani ya ofisi yake, haikuchukua muda L.J Belinda aliwasili ndani ya ofisi hiyo akiwa ametimia kimavazi kama ilivyokuwa kawaida. Alikuwa na kofia yenye rangi ya damu mzee pamoja na gwanda la kiofisi ambalo lilikuwa lipo kwenye muundo wa sketi na shari, ilikuwa ni nadra sana kuvalia gwanda hilo lakini kutokana na ni sehemu ya vazi la ofisini L.J Belinda alilivaa lakini hakuwa mpenzi wa kuvaa sketi kabisa akiwa yupo eneo la kazi. Alipoingia ofisini kwa mkuu wake kwakuwa alikuwa kamili kimavazi alitoa saluti ya heshima kabisa na si ile kiukakamavu ikiwa hayupo kamili kimavazi
“Keti kwenye kiti Belinda” Jenerali Marwa alimpa amri akitikisa kichwa kwa ishara kukubalia pale alipopewa saluti hiyo.
“Ndiyo Afande” L.J Belinda aliitikia
“kuna suala jipya limeingi hapa mezani kwangu kutoka TISS ambao walikuwa wapo kwenye kazi moja na vijana niliokuwa nimewaweka chini ya amri yako” Jenrali Marwa aliongea na kisha akaweka kituo halafu akaendelea, “sasa basi inahitajika uwaambie hao vijana waachane kabisa na kazi hiyo kwani N001 ameshaingia kazini na ana siku tisa tu za kuimaliza hiyo kazi hivyo hataki kabisa kingiliwa kazi yake”
“Ndiyo mkuu nimekuelewa”
“OK fanya hivyo sasa hivi ongea na section kamanda wa section iliyoingia kazini”
“Afande”
“sina la ziada ni hilo tu” Jenrali Marwa alihitimisha na muda huo huo L.J Belinda alisimama kwenye kiti, alitoa saluti na kisha akageuka nyumana kutoka humo ofisni kwa mkuu wake.
Hadi kuingiz ndani ya siku hii ya pili Norbert alikuwa ameshafinikisha kwa kiasi kikubwa cha kumteka Cellina kwa siku ambayo alikuwa amewasiliana naye tangu achukue namba yake kule kwenye ofisi yao alipoleta gari lililokuwa likihitajika kupigwa rangi. Muda huo majira ya jioni walikuwa wapo ndani ya hoteli moja wakiwa wapo pamoja, Cellina alionesha ni jinsi gani alikuwa amevutika na Norbert katika siku hiyo tu hasa akiwa na muonekano wake wa kipesa. Binti huyu hakuwa tofauti kabisa na mabinti wengine wale waliokuwa wakimpenda mtu mwenye uwezo wa juu kiuchumi ingawa alikuwa akijiweza kabisa kiuchumi, yeye mwenyewe ndani ya siku hizo alijikuta akivutika kabisa hasa akiuangalia utanashati na uzuri wa sura aliokuwa nao mwanume huyo mkware aliyemuita mahala hapo. Hakika alivutika kwa kila kitu alichokuwa nacho huyo kidume cha jogoo ambaye alikuwa akipenda kufuata kila mtetea utakaopita mbele yake, hakujua kabisa kijogoo huyo alikuwa akimfuata yeye na pia ameonesha dalili za kuvutika naye akiwa na lengo la kupata kile ambacho alikuwa hakijui kabisa kutoka kwake.
Muda huo alikuwa ameshapewa maneno ya sumu ya kuchoombeza na akawa amelainika kimsimamo zaidi hata ya alivyolainisha usiku uliopita alipopigiwa simu naye. Usiku ulipita alikuwa akijivuta sana kuweza kukubali ombi hilo lakini ndani ya siku hiyo mpya hakuwa na namna zaidi ya kukubali tu kwani moyo wake ulikuwa ushalainika kwa kila kitu.
“Ila Norbert kuna kitu nataka nikuulize” Cellina aliongea
“Ok kuwa huru bibie uliza tu” Norbert alimtoa hofu
“Hivi niko peke yangu kweli na huo uhandsome wako”
“Hilo swali mazingira ya eneo hli nafikiri yanakujibu kabisa”
“Kivipi?”
“Hapo ulipokaa kwenye meza hii nikiondoka mimi utabaki na nani?”
“Nitabaki peke yangu”
“Ok ndiyo ulivyo wewe kwenye vyumba vya tufaa jekundu lilipo kifuani mwangu”
“Mhh! Nawe una maneno”
“Huwa moyo wangu kama automatic doors za Ghorofa ambazo zikisogelwa kwa karibu hufunguka zenyewe, ndiyo na mimi nikipata kinipacho upendezo wa moyo basi maneno hujitoka automatically”
“Mh!” Aliguna huku akitabasamu kisha akatupa jicho kando baada ya kuona jicho la Norbert halikuwa na dalili ya kushuka lilipokuwa likimtazama usoni.
“ni sauti yenye kuburudisha kila unapoitoa, hata huko kuguna ni burudani tosha ndani ya moyo wangu”
“Mh1 Hay sina usemi mie”
Jioni iiibadilikana hatimaye ikawa usiku wakiwa bado wapo hapo mezani, waliendelea kula na kunywa ambapo Cellin aliagiza vinywaji vyenye kilevi kwa kiasi kikubwa sana katika muda wote ambao walikuwa wapo hapo mezani, Norbert alikuwa akitumia kilevi lakini hakuacha kuwa pembeni na kinywaji kilichokuwa kikondoa kilevi kwakuwa alikuwa yupo kazini. Aliona hatari ya kujiachia na kutmia kilevi kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni kuharibu kazi na hata kuweza kuropoka yale yaliyokuwa yakihusiana na kazi. Taratibu kinywaji kilianza kumchangamsha Cellina na akajikuta, alisogeza kiti jirani kabisa na Norbert na hata ile haya ya kike aliyokuwa nayo hapo awali ilimtoka kabisa. Ilikuwa ni mwendo wa kujiachia kwa kumkumbatia Norbert kimahaba zaidi katika eneo hilo la hoteli ambalo kila mtu alikuwa akiendelea na mambo yake, hakujali kabisa eneo alilokuwepo ni la wazi yeye alianza kumpa mabusu motomoto Norbert huku akiongea akionekana ni mwenye furaha kupitiliza. Norbert naye alijua kuongea naye kwa kumuambia maneno ambayo yalikua yakifurahisha zaidi na kumfanya azidi kuwa na furahs kupitiliza.
Haikuchukua hata muda mrefu Cellina alihitaji kwenda kupumzika baada ya kilevi kuwa kimezidi, alikuwa akionesha dalili za kusinzia na akimuegemea Norbert huku akimbusu kila mara, Ilikuwa ni hatua ambaye ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na kijogo huyu huyu ambaye alikuwa akiwinda mtetea huyo kwasababu maalum sasa mtetea huyo aliyekuwa yu mbioni alikuwa ameshafikia hatua ya kumdonoa kichwani ili aweze kupata burudiko. Hakutaka kabisa kupoteza muda tena ikiwa tayari ameshaingia ndani ya anga zake, alichokifanya ni kunyanyuka naye na kisha akaelekea hadi sehemu ya ndani hoteli hiyo kwenye eneo la mapokezi. Alipofika hapo Cellina alikuwa bado amemugemea huku mkono wa Norbet ukiwa umezunguka kiunoni mwake, alichukua chumba na kufanya malipo papo hapo na kisha akaongozana na Mhudmu wa hapo hotelini kwenda kuwaonesha chumba chao. Ilikuwa ni ghorofa ya juu kabisa ya hoteli hiyo ambapo walipelekwa hadi kwenye chumba chao ambapo Mhudumu alifungua mlango wa chumba hicho kisha akawakabidhi funguo ya mlango huo na akaondoka akiwaacha wawili, Kijogoo alimaarufu kama kidume mpando alijisokomeza ndani ya mlango wa chumba hicho baada ya mlango tu kufunguliwa akiwa ameshikilia kiuno cha mrembo wake alimyemuwekea windo akanasa. Mlango wa chumba chao kufungwa ndiyo hatua iliyofuata baada ya wao kuingia tu ndani yake, kilichofuata hapo ilikuwa ni kukumbatiana kiuhuru zaidi na mwenye jinsia mbondeko alikuwa ni mwenye papara kabisa na alikuwa akilazimisha kulana ndimi akionekana ni mwenye kuhitaji sana suala hilo.
Hakujua kabisa kuwa huyo aliyekuwa naye alikuwa yupo hapo kwasababu maalum, yeye alichokuwa akiwaza ni penzi tu kutokana na kuchangamshwa sana na kilevi alichokuwa akikitumia. Hitaji ya kutengeneza nishati katika mwili nalo lilimfanya kijogoo aweze, yalikuwa ni majibizano ya kimapasho ya miili.
“Mamba na windo meno ndiyo huongea” Norbert alijisemea moyoni.
Aipomaliza kutoa kauli hiyo kwa haraka sana alishambulia shingo ya binti huyo aliyekuwa yupo kwenye hali ya kilevi, aliishambulia kwa kutumia ulimi na kuzidi kumchanganya kabisa hadi akawa ni mwenye kukishilia kichwa chake na na kuanza kufanya kama anakichana kwa kucha zake ndefu za kike. Binti huyo alizidi kunogewa kabisa na mtindo huo aliokuwa akiufanya hadi akajikuta akihema akijigeleza zaidi muda huo waliokuwa wamesimama na kupelekea, mambo yalipozidi jambo aliishia kutamka neno Norbert kwa kila muda kwa jinsi alivyokutana na mtu ambaye alikuwa akijua kuutumia ulimi ipasavyo nje ya matumizi yake ambayo yalikuwa yameumbiwa. Ilikuwa ni kitendo hiko tu ambacho kilimfanya hadi ajihisi hakuna na nguvu kabisa mwilini, kilipokuja kusitishwa alijikuta akishikiliwa kichwa chake asiache kufanya zoezi hilo.
Ilikuwa ni kama makusudi kwani kidume hiki hakikushusha kichwa chake shingoni, badala yake alibadili mtindo na kuzidi kumfanya ajione kuwa alikuwa akikaribia kukosa burudani kama angeendelea kukazania kilekile. Muda mfupi baadaye Cellina hata hakujielwa alikuwa ametolewa muda gani vizuizi kwani, huo wote ulikuwa utundu wa Mzee wa toto katika kumfanya awe kichaa kabisa kwa mambo aliyokuwa akiyafanya. Alikuja kujihisi akiongezekewa na nyuzijoto mwilini mwake baada ya kukutana na ngozi kama yake, hapo alijikuta akiwa anakuwa kichaa kabisa kwa kupagawa na ubunifu adimu aliokuwa akipewa. Ilichukua saa kadhaa akiwa yupo juu ya ubunifu huo huku bado kilevi kikiwa kipo kichwani, alipokuja kuchoshwa zaidi mwili wake alijikuta akipitiwa na usingizi akiwa amelala juu ya kifua cha huyu Mamba asiyeacha windo hata kama angekumbwa na shibe.
[8]
Asubuhi na mapema ndipo Cellina alipokuja kuamka akajikuta akiwa yupo kifuani, alipofumbua macho tu alikutana na macho yaliyokuwa yakimtazama usoni ambapo alijikuta akitabasamu tu mwenyewe. Alijikuta akimbusu kwenye papi zake za mdomo na kisha akampa salamu ya asubuhi hiyo, ilikuwa ni ndani ya siku ya alhamisi ambapo ilikuwa ni siku ya kazi katika subuhi hiyo mapema sana.
“Vipi umeamkaje?” Cellina aliuliza
“Nimemka fiti sana hadi naona uvivu kwenda job” Norbert alijibu na kusababisha Cellina acheke sana
“Huyooo muone vile uamke fit ushindwe kwenda job, si mzima wewe”
“Kweli vile mimi ufit wangu ukizidi nashindwa hata kwenda job yaani sijui kwako wewe hapo”
“Mimi nikiwa fit ndiyo naenda job kabisa”
“Vipi ukitega?”
“Wee kuna mkurugenzi mkuu pale ukitega umekwisha yaani kazi huna”
“Mmmh! Mkurugenzi mkuu huyo wa jinsia gani asiyejua ufiti ukizidi kupitiliza mtu hubidi kupumzika”
“Ni mdada mmoja huyo tunamjua kwa jina la Madam ana msaidizi wake mzungu wakali hao balaa”
“Wakali wana meno ya simba nini wachovu tu”
“Ngoja nikuonesha uwaone tulipiga nao picha ya pamoja ya ofisi wapo kikazi muda wote sura zao” Cellina alipoongea hivyo alijitoa kifuani mwa kidume cha mbegu na kisha akajisogeza kivivu hadi upande ambao aliiona pochi ya makwapani, alitoa simu yake ya kisasa kwenye ile pochi na kisha akafungua baadhi ya mafaili akamuonesha picha ya huyo aliyemtaja bosi wake.
Norbert alivutika zaidi na picha hiyo na akajikuta akiitazama kwa umakini sana, baada ya hapo aliachia tabasamu lake lililokuwa likificha kila kitu chake ambacho alikuwa hataki kabisa kijulikana na kumbe wa kawaida. Aliitazama picha hiyo kwa mara ya pili ambapo alijionea mwenyewe kuwa watu hao aliokuwa ametajiwa kama wakuu wa Cellina walikuwa ni watu ambao alikuwa akiwafahamu undani wao kabisa, walikuwa ni watu ambao walikuwa na zaidi ya jambo kwa uwepo wao ndani ya jiji hili. Walikuwa ni watu ambao alijipa akili nyingine ya ghafla ya kuweza kufuatilia miendenendo yao, walikuwa ni viumbe ambao alikutana katika mazingira tofauti kabisa. Walikuwa binadamu wa jozi moja ambao alikuwa akiwindana kila akionana nao. Hapo alibaini kuwa kulikuwa na uhusiano mkubwa sana kati ya watu hao na yule Kelvin ambaye alikumbana naye kule Yombo.
“Josepine na Scorpio wapo jijini, nahisi hata kutaka kuuawa Buguruni ni kazi ya mokono wao au wametuma kijana wao” Norbert alijisemea ndani ya moyo wake kisha akamtupia jicho kwa tabasamu Cellina
“Umewaona mabosi zangu hao wakali balaa yaani, inabidi tu leo niende job ingawa nimechoka sana kazi yako si ndogo”
“Mmmh! Watu wenyewe wachovu hao wana mikwara mbuzi tu yaani mimi ningekuwa na mabosi kama hao wala sitishiki ndiyo kwanza ningewaendesha tu”
“Wee unasema tu unafikiri kazi siitaki hasa yule Madam ni katili balaa, kuna mwenzangu huyo alitaka kufukuzwa kazi na yule MZungu ila alirudishwa kihongo tu”
“Hee kihongo kivipi?”
“Kalala na mzungu yule alipoambiwa hivyo kwa sharti la kurudi kazini, hakuna na kazi nyingine kwa taaluma yake itakayomlipa zaidi ya hiyo. Alipofikiria kuwa alikuwa akikaribia kwenda kuingia kwenye gereji bubu mtaani zisizolipa ilimbidi tu atii matakwa kwani hakuwa na wa kumshtakia”
“Kumbe ndiyo tabia zake huyo jamaa anaonekana mpole”
“Yaani acha tu ni mhuni huyo balaa na hafai”
“Haya hapo ujanja kabisa tena muda unaenda tujiandae nikakushushe kazini kwako”
Wote kwa pamoja waliingia ndani ya bafu la kisasa lilipo humo ndani ya chumba hicho na kusafisha miiili yao, walipotoka tu nje ya chumba hicho walikimnbilia kujiweka sawa kimavazi kama walivyokuwa wameingia ndani ya hoteli hiyo jana yake. Cellina alijipamba kama kawaida kutokana na kuwa vipodozi kwenye mkoba wake kama ilivo hulka ya baadhi ya wasichana kutembea na vipodozi mkobani. Baada ya hapo wote kwa pamoja walitoka hadi nje ambako aliiingia kwenye gari jingine kabisa alilokuwa amekuja nalo usiku uliopita Norbert, waliondoka kwenye hoteli hiyo huku Cellin akiwa hatambui kama alikuwa amegawa madini adimu sana kwa kidume huyo bila malipo yeyote yale. Hakujua kabisa kile ambacho alikuwa akikiongea mule ndani kilikuwa kina thamani gani kwa huyo aliyetoka kutumia naye kitanda kimoja, kuweza kupagawawishwa ndani ya usiku mmoja tu alijikuta akitoa ambayo yalikuwa hayatakiwi kutolewa kabisa pasipo kutambua kuwa alikuwa akifanya kosa kubwa sana. Aliona alikuwa amepatwa mwanaume ambaye alikuwa mwenye mvuto hata akitoka naye watu watamsifia kuwa ana mwanaume pasipo kutambua kuwa alikuwa akigawa ramani ya vita kwa adui bila kujitambua, muda huo waliokuwa wapo ndani ya gari kuelekea huko ofisini kwake alikuwa akimtazama sana Noebert kama alikuwa anamuona kwa mara ya kwanza. Kila alipokuwa akifikira sana kile ambacho alikuwa amefanyiwa usiku ulipita alikuwa hamalizi kumtazama, ingawa alikuwa na ulevi bado aliweza kuipata burudani iliyokuwa ikitolewa ndani ya kumbi wa mraba ambao walikuwa yeye na mburudihaji wake. Hakuwa akiwaza kabisa kuwa alikuwa ameuza udhaifu wa bosi wake kwa adui wa bosi yake ambaye alikuwa akitaka sana kuuufahamu na pia alikuwa amewaanika mabosi zake kwa mtu ambaye alikuwa ana uhasama nao na kumfanya atambue kuwa watu hao walikuwa wapo ndani ya jiji hilo. Iliwachukua robo sa tu wakawa wamefika eneo la Buguruni Rozana ambapo ndiyo kilikuwa kituo cha mwisho cha safari ya Cellina, hapo aliagana na Norbert kwa mabusu motomoto na kisha akaelekea kazini kwake.
Hapo ndipo Norbert alipoondoa gari na kuelekea yalipo makutano ya barabara ya Chama, aliingia kwenye barabara ya Mandela alipofikia kwenye eneo hilo kuelekea upande ilipo Ubungo. Baada ya robo saa nyingine alikuwa yupo eneo la Ubungo kwenye makutano wa barabara tatu tofauti ambazo ni barabara ya Morogoro,Sam Nujoma na Mandela. Hapo aliingia kwenye barabra ya Morogoro kwenye upande ambao ilikuwa ikitoka nje ya jiji la Dar es salaam, aliendesha kwa muda wa robo saa nyingine kutokana na msongamano wa daladala akawa amefika Mbezi ambapo aliingia kwenye barabara ya vumbi iliyokuwa ikielekea Mbezi Luxury, Muda huo wote alikuwa na akifuata ramani maalum iliyokuwa ipo ndani yz gari yake ambayo ilikuwa ikimuelekeza mahali pa kwenda. Alifanikiwa kufika hadi maeneo hayo ya Mbezi Luxury kisha akaelekea hadi mwisho wa maelekezo yake, safari yake iliishia kwenye lango la nyumba moja ya kisasa zaidi ambako alipiga honi alipofika hapo. Lango dogo la eneo hilo lilifunguliwa na kisha Mlinzi aliyekuwa amevalia sare maalum alitokea na alienda kwenye gari lake akagonga kioo, Norbert alishusha kioo cha gari lake na kisha akampa tabsamu huyo Mlinzi.
“Ndiyo mzee” Mlinzi aliongea
“Kaboneka nimemkuta?” Aliuliza
“Kabisa umemkuta nimuambie nani?”
“Muambie Kaila, Norbert Kaila yupo nje hapa anihitaji kuonana naye kikazi zaidi”
“Ok mzee subiri dakika moja” Mlinzi huyo alipoongea hivyo alikimbia akaelekea ndani ya lango hilo, huko alitulia kwa kipindi kifupi cha muda tofauti ilivyokuwa dakika moja aliyokuwa ameizungumza. Hiyo ilikuwa ni kawaida ya waswahili na wenyewe kwa wenyewe walikuwa wamezoeana kwa ahadi zisizo na muda, Norbert aliendelea kusubiri kwa muda mfupi ambako lango kubwa la Magari lilifunguliwa na kisha akaingiza gari ndani moja kwa moja. Alielekezwa eneo maalum la kuegesha gari na kisha akaenda kuegesha kwenye eneo hilo, baada ya hapo alilizima gari na kisha akashuka na kuingia ndani ya nyumba kwa msaada wa maelekezo ya Mlinzi.
Muda ambao Norbert alikuwa yupo ndani ya gari akiwa anelekea kwenye makutano ya barabara ya Chama maeneo ya Buguruni, kijana mwingine aliyekuwa yupo chini ya kina SCorpio alikuwa yupo ndani ya gari dogo aina ya Lexus yenye muundo wa altezza mbayo ilikuwa ni tofauti kabisa na ile ambayo walikuwa akiendesha kina Scorpio walipojaribu kumuua adui yao. Mtu huyu naye alikuwa akielekea eneo ambalo alikuwa ameelekea Norbert akiwa na lengo moja tu la kwenda kuchukua kile ambacho alikuwa amekifuata Norbert. Kaboneka alikuwa ni mdogo wa mmoja wa wanausalama ambaye alikuwa na Tarakilishi ambayo ilikuwa na siri kubwa ndani yake, hivyo yeye alikuwa amegizwa kwenda kuichukua isije ikafikia mahala pabaya. Hakutambua kabisa kuwa huko alipokuwa akienda kulikuwa na mwingne kabisa ambaye alikuwa amemtangulia katika kuhakikisha kuwa alikuwa akiichukua tarakilishi, gari hiyo ilikuwa ipo kwenye barabara ya Nyerere ikiwa inatoka upande ambako Kariakoo ipo kuelekea huko alipokuwa akienda adui yake mkubwa waliyekuwa wakigombania naye kitu kimoja.
Muda mabo Norbert anawasili ndani ya eneo la nyumba ya Kaboneka, mtu huyo alikuwa yupo kwenye njia ya vumbi iliyokuwa ikielekea huko, alipofika eneo la jirani ya uzio wa nyumba hiyo alisimamisha garii lake na hakutaka kabisa aonekane kama alikuwa ni mtumiaji wa gari hilo kipindi anaingia ndani ya nyumba hiyo. Baada ya hapo aliruka uzio wa nyumba hiyo akatokea ndani, akiwa na umakini wa hali ya juu alienda hadi eneo ambalo kulikuwa na kibanda cha Mlinzi na kisha akagonga mlango wa kibanda hiko. Mlinzi wa nyumba hiyo ambaye alikuwa hajui chochote alikutana na pigo la kijasusi ambalo hupigwa kama kofi shingoni, pigo hilo lilimpa usngizi wa lazima ambAye yeye hakutarajia kabisa kama angeulala na kisha mtu huyo aliingia ndani ya kibanda hiko akamkalisha kwenye kiti. Baada ya alimuweka kwenye kiti na kumlaza kiwiliwili chake juu ya meza yake, alimalizia kwa kuitoa bahasha moja nyeupe ambayo aliiweka jirani na meza hiyo kisha akatoka humo ndani na kurudishia mlango. Baada ya hapo alitoka moja kwa moja na akaenda kwenye hadi kwenye baraza la nyumba kubwa ya kisasa ambayo ilikuwa ipo humo ndani, aliingia ndani ya baraza la nyumba hiyo na kisha akausogelea mlango ambao ndiyo ulikuwa ni sehemu itakayomuwezesha kuingia ndani ya nyumba hiyo.
Norbert baada ya kuingia ndani ya nyumba hiyo alipokea ukaribisho kutoka kwa mtu ambaye alikuwa akija kumuona ndani ya muda huo, alikuwa ni Kaboneka mwenyewe ambaye alikuwa ni mtu mzima wa makamo. Alimkaribisha hadi ilipo sebule ya nyumba yake ya kisasa ambako waliketi naye kwenye kochi hilo, Kaboneka alikuwa ni mtu ambaye alikuwa akifahamu vyema harakati za Norbert akiwa yupo kwenye kazi zake kama mwandishi. Alikuwa ni mwandishi ambaye alikuwa akimuhusudu sana kwani ni yeye ambaye alikuwa amefanikisha kufichuliwa kwa maovu mengi ndani ya serikali kwa kutumia makala zake kwenye jarida ambalo lilikuwa likitoka katika kila baada ya miezi sita au kukiwa na jambo muhimu sana ambalo jamii ilikuwa ikipaswa kulifahamu. Uhodari wake katika kuelezea makala tofauti ulimfanya aingiwe na furaha kabisa kwa kuweza kuonana na mwandishi mwenyewe ambaye inasemekana ni mwenye akili ya hali ya juu kiasi cha kushindwa kuwekwa mikononi na wabaya wake, mtu huyo aliyekuwa akimuhusudu alikuwayupo hapo mbele yakea akiwa amekuja kiofisi kuonana naye hivyo alijikuta kifarijika sana.
Kabla hata hajaanza kuzungmza naye kitu ambacho kilichokuwa kimeleta ndani ya eneo hilo alichukua simu ya kisasa kabisa na kisha akaomba kupiga naye picha ya pamoja, hilo lilikuwa ni jambo ambalo halikupigwa na Norbert kwani aliona alikuwa ni kiasi gani alikuwa amekubalika na mwenyeji wake. Alikubali kupiga naye pichana kisha akakaa kwenye kochi ili aweze kuongea naye.
“Karibu sana Bwana Kaila ni faraja sana kuweza kunitembelea ndani ya nyumba yangu nahisi ujio wake una zaidi ya jambo” Kaboneka aliongea
“Hakika Mar Kaboneka ujio wangu wa kiofisi ndani ya nyumba hii una zaidi ya jambo nafikiri wewe ndiyo mdogo wake Marehemu Lutonja kaboneka” Norbert aliongea
“Hakika ndiyo mimi kabisa”
“Katika utafiti wangu wa uandishi wa jarida ambalo lipo mbioni kutoka ndani ya majuma mawili yajayo,umeonesha kuwa wewe ni mmoja kati ya watu wanaoweza kunisadia niweze kupata kile ambacho kingeweza kuioko nchi hii”
“Ndiyo Kaila”
“Uchunguzi wangu wa awali ambao umetaka kunigharimu maisha yangu umebaini kuwa kuna laptop tano ambazo zilikuwa zimehifadhiwa siri kubwa sana na ya maneno ambayo yalikuwa ni neno siri ya kutambua mahali lilipo faili lenye utafiti mzima uliofanywa ambao ulitakiwa kuwasilishwa bungeni na Mheshimiwa Bai” Norbert alipoeka kituo hapo aliona mwenyeji wake alikuwa akimsikiliza kwa umakini kabisa.
“Moja kati ya hizo laptop ishaingia kwenye mikono yangu na ipo mikononi mwa mwanausalama wa EASA ajulikanae kama N001 ambaye alikuwa akihitaji kwa kazi yake. Moja imechukuliwa na wasiojulikana bado naisaka nipo radhi nife ila ukweli ujulikane na moja unayo wewe, hivyo ujio wangu ndani ya eneo hili ni kuhusu hiyo Laptop nilikuwa nikihitaji yenyewe au neno muhimu lililopo” Norbert aliendelea kuongea na alipoweka kituo tu mlango wa mbele wa nyumba hiyo uligongwa mara mbili, kugongwa huk nkwa malngo huo kulitoa sauti ya kuwa ulikuwa umegongwa na kitu kigumu. Kiutambuzi kabisa wa kugongwa kwa namna hiyo Norbert aliweza kutambua kuwa aliyegonga mlango huo alikuwa ni mwenye mkono uliokomaa sana, alijua kabisa mgongaji wa mlango huo hakuwa yule Mlinzi bali kulikuwa na mtu wa ziada.
“Aaargh! Yaani huyu mlinzi badala apige simu kunipa taarifa anakuja kugonga mlango” Kaboneka alinyanyuka na akiwa anaenda kufungua mlango
“Mr Kaboneka wait” Norbert alimsimisha kisha akaongea kwa sauti ya chini, “Kama mlinzi alikuwa na utaraibu uliomuwekea nakuomba usifunue mlango na unisikilize mimi kwani huyo anayegonga mlango hakika siyo mlinzi”
Ilikuwa ni kauli ambayo haikuwa ya kawaida kabisa kwa Kaboneka, alimtazama sana Norbert asijue alikuwa amefikiria nini hadi akaweza kuitoa kauli hiyo kwenye kinywa chake. Kauli hiyo ilifanya hata site kufungua mlango kwa sekunde kadhaa na akabaki akimtazama huyo aliyeitoa. Ilikuwa ni kauli ambayo ilijaa ukweli mtupu hasa alipijifikira, haikuwahi kutokea Mlinzi wake akaja kugonga mlango kama hivyo. Hilo suala lilikuwa lisilopingika kabisa. Alikuwa ameajiri Mlinzi kutoka kampuni ambayo ilikuwa na walinzi wenye utiifu mkubwa na hakuwahi kuvunja masharti ya waajiri wake kabisa, hakika alizidi kumuhusudu sana Norbert alimuona ni kiumbe wa ajabu sana kwa ajinsi akiliyake ailivyokuwa ikifanya kazi.
Wakati akimtazama hivyo mwenyewe ambaye aliona alikuwa ametoa kauli ya kawaida kabisa alinyanyuka kwenye kochi hilo alilokuwa amekaa na kisha akaenda kukaa kwenye kochi jingine ambalo lilikuwa lipo pembezoni mwa mlango. Kaboneka alibaki akimtazama sana na muda huo mlango uligongwa tena kwa namna ileile ambayo ilionesha mgongaji alikuwa akigonga mlango wa kitu kigumu sana ikiwa ugongaji huo utasikika kwa mtu mwenye uwezo wa kawaida. Lakini kwa jasusi mkubwa na mwenye uwezo wa hali ya juu kama huyo aliyekuwa ametawala ugeni wa humo ndani ya nyumba hiyo. Huyo alijua kabisa mlango huo ulikuwa ukigongwa na sehemu ya kupigia konzi ambazo zilikuwa zimekomaa sana ndiyo maana sauti ilikuwa ikisikika namna hiyo, ndiyo maana aliamua kuketi eneo hilo kwani alishatambua kabisa kuwa mgongaji hakuwa mtu wa kawaida hata kidogo bali alikuwa ni binadamu wa namna tofauti.
Alimpa ishara Kaboneka ya kuweza kufungua mlango huo akiwa ameambatanisha na ishara ya kumtaka awe na amani, hapo ndipo mwenyeji wa nyumba hiyo alizungusha sehemu ya kitasa ambacho hufunguliwa kwa ndani tu ikiwa mlango utajifunga. Kitendo cha kuungua mlango tu alikutana na na mdomo wa bastola ambao ulimuelekea kwenye paji la uso, alishtuka sana kwani alikutana na yule kijana ambaye alikuwa ametoka muda si mrefu kumpa usingizi wa dharura mlinzi wake kwenye ofifs ya getini. Alijikuta akitaka hata kupiga kelele lakini alipomtazam huyo aliyemuwekea bastola, alikutana na kidole cha shahada ambacho kilikuwa kipo mdomoni. Hapo alibaki kimya na akawa anamkodolea macho huyo Mvamizi aliyetia mguu kwenye kizngiti kikubwa cha nyumba yake, aliashiriwa arudi nyuma ili Mvamizi wake aweze kuingia. Kaboneka naye alitii kabisa na alianza kurudi nyuma taratibu, Mvamizi naye alipiga hatua moja kuingia ndani akijua wako wawili akiwa ni yeye kiumbe asiye wa kawaida pamoja na kiumbe wa kawaida. Hakujua kulikuwa kuna kiume asiye wa kawaida pia alikuwa akimngojea yeye, alipopiga hatua ya pili kuingia ndani alitegeshewa mguu na Norbert na kupelekea ayumbe. Ilikuwa ni kitu ambacho hakukitarajia kabisa, akiwa anayumba baada ya kutegeshewa ulimfanya ajikwae. Alituliziwa kitu kizito sana sehemu ya kiunoni ambacho kilimfanya aende chini na bastola imtoke mkononi kwani hakuwa ametarajia kabisa kukutana na jambo kama hilo, bastola nayo ilikuwa imeruka mbali kabisa na eneo hilo aliloangukia. Alipotaka kutambaa kwa haraka aifuate ili aweze kuihami, mshushaji wa dhoruba kali iliyomkuta hadi akasalimia na sakafu alifanya mchezo mdogo sana wa kitoto akawa ameifkia bastola hiyo. Alipiga sarakasi ambayo hutumiwa sana na wacheza sarakasi na hata watoto wanaopenda kujifunza sarakasi, mtindo wa hatua za mwanzo kabisa katika kujifunza saraksi ndiyo aliutumia kiumbe mwenzake asiye wa kawaaida ambaye alikuwa akitetea nuru kwenye nchi yake
Wengi sarakasi hii huifahamu kwa jina la ‘Roll’ ambalo ni neno la kingereza lenye maana ya ‘Biringita’ kwa lugha ya kiswahili. Saraksi hii hutumiwa sana na wale ambao wanahitaji kukwepa kitu kinachowajia miguuni au kuruka kizuizi ambacho walikuwa wameshindwa kukiruka kwa namna ya kawaida. Hufanywa kwa kuanza kuruka kama mtu muogeleaji anayejirusha kwenye maji, kisha mrukaji akiifikia sakafu huweka mikono na kujibiringisha. Norbert ndiyo alifanya mtindo huu alipomuona mpinzani wake alikuwa akitaka kuifuata silaha, alitangulia juu yake kwa hiyo sarakasi na kisha akaiwahi yeye silaha na kuishika mkononi halafu akamtazama huku akitabasamu.
Muda huo Kaboneka alikuwa amekaa kando akiangalia vitu vya ajabu vilikuwa vinafanywa na mgeni wake, alumuona ni kiumbe wa tofauti sana kwa jinsi mambo hayo alivyokuwa akiyafanya. Ilikuwa ni vitendo ambavyo alikuwa akivishuhudia kwenye sinema za mapigano tu na hakuwahi kuvishuhudia moja kwa moja, ila ndani ya siku hii aliweza kuvishuhudia kwa mtu ambaye anahusudu sana kazi zake akikifanya tena kwa wepesi wa hali ya juu. Muda huo Norbert alikuwa akimtazama jinsi Mpinzani wake alivyokuwa amegwaya baada ya kuzidiwa kete katika mchezowa wa kifo, alibaki akimkodolea mcho tu asijue la kufanya kwani alikuwa amezidiwa ujanja na hadi akili ya kufikiria mambo.
“Karibuni ndugu sema utahitaji kinywaji gani?” Norbert alimkaribisha Mvamizi huyo ambaye alikaa kimya tu hakujibu chochote.
“Inaonekana ni muoga wewe basi niambie umekuja kuchukua laptop siyo ili uwafiche mafusadi waliokupa ugali nini?” Alimuuuliza tena lakini hakujibiwa na badala yake alitukanwa.
“Wooow! Ngojera nzuri sana hizo ila hapa umeingia nyumba ya wachonga masanamu si waimba ngonjera” Alimuambia na kisha alianza kumsogelea kwa taratibu huku akiichezea bastola kwenye mkono wake, alipofika karibu yake yule kijana ndipo akili yake ilifanya kazi na akajifanya amekaa kitako huku akinyoosha miguu mbele. Alipoona Norbert akikaribia jirani alifyatua miguu yake akiwa na lengo la kumpiga chini kidogo ya ugoko ili aanguke.
Hila hiyo taayri ilikuwa imeshaonwa muda mrefu sana na alipotaka kuifanya tu, miguu ya Norbert ilitanuka kwa upesi mithili haikuwa imepewa amri na mwenye umiliki nayo. Miguu ya Mvamizi ilipenya katikati ya miguu ya Norbert na kumfanya hata sehemu za mifupa ya kiunoni mwake ishtuke. Alikuwa ametumia nguvu nyingi kuliko kawaida wakati akifyatua miguu hiyo ndiyo maana hata alishtuka mfupa wa kiuno, alibaki akiwa anasikia maunmivu ya kushtuka mfupa huo. Akiwa hata maumivu ya kushtuka mfupa huo hajayazoea alijikuta akipewa teke zito lilimpata kwenye taya hadi akapata hitilafu kwenye meno yake na kutema damu, kichwa chake kilienda chini moja kwa moja na ambapo alibaki akiwa amefumba macho kwa maumivutu.
“Nani aliyekutuma wewe?” Aliulizwa lakini hakujibu chochote aliishia kutema mate yaliyokuwa yamejaa damu ambayo hayakumpta Norbert.
“Anhaa mpole unajifanya jeuri ngoja nikupe zawadi yako” Norbert alipoongea hivyo alimsogelea hadi karibu na kisha alianza kumpa kipigo cha paka mwizi, alipoaacha kumpiga alimtazama jinsi alivyokuwa ameumia sehemu mbalimbali za mwili wake.
“Nasema” Hatimaye Mvamizi alikiri
“Nimetumwa na..” Hakumalizia kauli yake alitokwa na fahamu kwani kipondo alichokuwa amepewa hakikuwa cha kawaida hata kidogo, Norbert hapo alitokwa na mguno wa fadhaa na kisha akamtazama mwenyeji wake ambaye alikuwa ametulia kwenye kochi huku akishangaa sana kwa jinsi alivyoona mtu akipewa kipigo.
“Kazi ninayoifanya kufichua maovu lazima niifunze michezo ya kujihami kwani uandishi wa habari wa namna hii ni hatari sana, niishukuru JKT pia kwa kuweza kunifundisha namna za kuzitumia silaha” Aliongea huku akimtazama Mwenyeji wake ambaye alikuwa amekaa kimya tu hakujali alimuambia kwa mara anyingine, “kwa sasa maisha yapo hatarini sana na unawindwa , ninachokuomba ni uchukue ile laptop ya kaka yako na ufuatane na mimi hakuna kukaa humu tena”
Kilichofuata hapo ilikuwa ni Norbet kuitoa risasi ile bstola hata kama fahamu zikimrudia muda ambao polisi watakuwa wamewasilia hapo, asiweze kabisa kujitetea kwa kuoambana nao. Baada ya hapo alitoa kitambaa mfukoni mwake na kisha akafuta alama zake za mkono na akamshikisha yule mvamizi, alipomaliza hapo aliketi kwenye kochi akiwa anamsubiri mwenyeji wake.
Kaboneka aliposikia maneno hayo wakati Norbert anaanza kumshikisha bastola mvamizi hakutaka kupinga kabisa yeye aliiingia ndani na akatoka na mkoba wa Tsarakilishi ya mapakato ambao ulifanana kila kitu na ule wa Mwanammke aliyekuwa amemuokoa kule Kiwalani. Walitoka hadi nje na kisha waliingia kwenye gari la Norbert, walipotaka kuondoka Norbert hawakuona dalili za kufunguliwa na kibanda cha mlinzi wa nyumba hiyo. Norbert alipiga honi na hakukuwa na dalili za kuja kwa Mlinzi huyo, aliamua kushuka mwenyewe na kwenda kufungua lango kubwa kwani akili yake tayari ilikuwa imempa hisia kwamba Mlinzi huyo alikuwa tayari amekatishwa pumzi na Mvamizi yule. Alipofungua geti alirudi garini na kisha akalitoa hadi nje, baada ya kulifikisha nje alifunga lango hilo. Hapo alitoa simu akabonyeza baadhi ya namba na kisha akaongea baada ya simu kuokelea, “Jina lililojitokeza kwenye simu yako si ngeni nafikiri unalitambua wazi, sasa njoo hadi nyumbani kwa mdogo wa Kaboneka mkubwa umchukue mhalifu wako na mwenyeji yupo salma kwenye mikono yangu” Alikata simu na kurejea tena garini ambapo aliliondoa kwa kasi sana.
Muda mfupi baadaye yule Mlinzi aliweza kuzinduka kutoka kwenye usingizi ambao alikuwa amelazwa kwa lazima, kitendo cha kuweza kufungua macho alikutana na bahasha ikiwa ipo mezani kwake ambayo hakuijua ilikuwa imeletwa na nani. Muda huo bado mawazo yake ya kutambua kile ambacho kilikuwa kimepita muda mfupi kabla hajaingizwa usingizi haikuwa imekaa sawa, ilipokuja kukaa sawa ndipo alipokumbuka kuwa kulikuwa na mtu ambae alikuwa amevamia ndani ya nyumba hiyo na kumpiga kofi la ajabu ambalo lilimlaza. Hakuwahi kuona mtu analazwa usingizi wa jabu na kofi na hiyo ndiyo ilikuwa mara ya kwanza na ilimtokea yeye mwenyewe.
Akili ya kuzunguka na kutazama usalma wa nyumba hiyo baada ya kuhisi kuwa aliyempiga kofi lile la maajabu hakuwa mtu wa kawaida ilimjia, alipotaka ainuke na kumfuata alijikuta akishindwa kutokana kuwa na shauku ya kuifungua bahasha hiyo. Kwani aliamini kabisa ilikuwa ikimlenga yeye na si mtu mwingine ndiyo maana ilikuwa ipo hapo mezani. Laiti mletaji angetaka kufikisha kwa bosi wake muda ule aliokuwa hana fahamu. Ingekuwa tayari imeshafika kwa bosi wake, aliifungua bahasha hiyo kwa papara akakutana na bahasha nyingine ambayo haikutofautiana na bahasha zile ambazo zilitoa maisha ya watu. Kuona bahasha hiyo iliyokuwa na maneno yaliyokuwa yakiashiria nguvu za giza, akili zake zilimpa wazo jingine kabisa. Aliona kuwa hiyo ilikuwa ni maalum kwa bosi wake kutokana na fedha alizokuwa nazo, alianza kufikiria kuwa bosi wake huyo alikuwa akijihuisha na mambo ya kishirikina. Hapo aliona ni namna gani anaweza kuwa mtu muhimu sana kwa bosi wake ikiwa ataijua siri yake, aliona kupandishiwa mshahara na bosi wake huyo kulikuwa kunafuata na hata kuonwa kama alikuwa ni mmoja wa ndugu zake. Wahka wa kutaka kujua kilichomo ndani ya bahasha hiyo ulimzidi kila idara, hapo akajikuta akiishika bahasha hiyo taratibu na kuanza kuivuta gundi iliyokuwa imewekwa.
Hakika umbea hauna jinsia kabisa kwani yeyote yule huutekeleza ukimjia ndani ya moyo wake, kitendo cha kuifungua bahasha hiyo aliona Moto wa ghafla ukimvaa naa kisha alirushwa hadi mlangoni ambapo alitokeza hadi nje baada ya mlango wa nyumba hiyo kuvunjika kutoka na mlipuko huo uliotokea. Huo ndiyo ukawa mwisho wake huyo mlinzi kwa wahka wa kufungua asichokijua.
Askari wa jeshi la polisi walipowasili ndani ya eneo la nyumba hiyo, walikuta mwili wa Mlinzi ukiwa umeungua na hata ukiwa hautazamiki kutokana na mlipuko ule mkubwa ambao ulimkumba akiwa yupo ndani ya chumba kidogo. Habari za kutokea mlipuko ndani ya nyumba hiyo zilikuwa ni muda mfupi tu tangu zianze kuzagaa ndipo walipowasili, walipoingia ndani ya nyumba hiyo kwakuwa walikuwa wana maelekezo kabisa. Walimkuta yule Mvamizi akiwa hana fahamu na bastola yake ikiwa ipo mkononi mwake, hawakutaka kusubiri kwani walikuwa wameshaelezwa kila kitu juu ya nyumba hiyo kutembelewa na Jasusi hatari ambaye alikuwa amemuokoa mmiliki wake. Walichoamua kukifanya ni kuchukua ile silaha wakiwa wamevaa mipira na kuitia kwenye mfuko wa laioni, kilichofuata hapo ilikuwa ni kumfunga pinfgu yule Mvamizi na kwenda kumtupa kwenye gari lao kwani hawakuona hata haja ya kumkimbiza hospitali ikiwa alikuwa amepoteza fahamu tu na ingemrudia muda wowote ule. Taarifa ya kutokea mlipuko mwingine ndani ya nyumba ya Kaboneka tayari zilikuwa zimeshafika kwa baadhi ya wananchi kupitia wanahabari ambao walikuwa wameshafika ndani ya eneohilo, vyombo vya habari mbaliimbali viliiripoti taatifa hiyo moja kwa moja.
KIBEWANI
TANGA
Majira haya ndani ya kijiji hichi cha udigoni ambacho kipo karibu na Kijiji ch Duga Maforoni, taarifa hii ilikuwa ikisikilizwa na Mzee mmoja ambaye alikuwa amevaa nguo zilizokuwa zimechakaa sana. Mzee huyu alikuwa amekaa kwenye kibaraza cha nyumba yake ya udongo iliyokuwa imeezekwa kwa makuti akisikiliza taarifa hiyo, aliisikiliza hadi taarifa hiyo ilipoisha alibadili na kuweka kituo kingine cha redio na taarifa ikawa ni ileile tu kwani ndiyo ilikuwa taarifa kubwa iliyokuwa imepamba jiji la Dar es salaam. Ilikuwa ni taarifa ambayo ilikuwa ikiwatisha baadhi ya raia waliopo ndani ya jiji hilo, lakini kwake yeye aliyekuwa yupo mbali kabisa na jiji hilo aliona ahueni kabisa kwani alitambua kabisa kuwa mlipuko huo ulitokea ndani ya nyumba ya mtu aliyetajwa ulikuwa na lengo maalum. Baada ya taarifa hizo kuisha aliamua kuinuka hapo chini kivivu zaidi tena akitumia nguvu nyingi zaidi na kisha akaitwaa redio yake na kuingia nayo ndani ya nyumba yake iliyochoka kabisa. Alifika hadi ndani ya chumba chake ambacho kilikuwa kikipitishwa mwangaza mdogo sana na akaiweza redio hiyo pembezoni mwa kitandani chake, baaada ya hapo aliketi kitandani kwa uchovu uleule huku akiangalia maeneo ya dirishani kwa tahadhari zaidi, aliketi kitadani alipeleka mikono yake hadi chini kbisa kwenye sakafu ya udongo na kisha akavuta sehemu moja ya udongo huo uliokuwa umeshindiliwa. Sehemu hiyo ilifunguka kama mfuniko ambapo ndani yake kulionekana kukiwa na mkoba unaofanana na mikoba ile miwili ambayo muda huo ilikuwa ipo mikononi mwa Norbert, alipouona mkoba huo alitoa tabasamu lake la kizee na kisha akafunika tena ambako hakukuonekana kama kulikuwa na mfuniko. Baada ya kuufunika mfuniko huo alijilaza kwenye kitanda cha kamba kilichokuwa humo ndani, alilala chali akawa anaangalia paa la nyumba hiyo.
“Ipo siku tu” Aliisemea mwenyewe huku macho yakiwa yapo juu
Kukamatwa kwa kijana mwingine aliyekuwa chini ya Askofu Valdermar ilikuwa ni pigo jinginye kubwa sana kwao, muda huo watu waliokuwa wakiwafanyia kazi walikuwa wamewaita katika nyumba ambayo walikuwa wameifanya ndiyo makao yao wa kukutana. Wakubwa wao wawili waikuwa wamechukia sana hasa walipofikiria kuwa walikuwa wakienda kuhadhirika ndani ya siku zijazo ikiwa hawatoithibiti hali hiyo, hilo lilikuwa ni suala ambalo walikuwa hawataki kabisa kuona likitokea. Wote walikuwa tumbo joto kwani walikuwa wakitambua kabisa kuwa huyo alikuwa ni kijana wao, mipango yao sasa ilikuwa imeanza kwenda mrama kwani ilikuwa ni Tarakilishi ya pili hiyo wameikosa kati ya tarakilishi zote tano walizokuwa wakizitafuta. Sasa ilikuwa imebaki moja tu ambayo ilikuwa na nenosiri jingine ambalo lingeweza kupata neno kamili kabla hawajaamua kuitafuta ile ambayo ilikuwa na siri kuliko zote. Tarakilishi ya mwisho kabisa kupatikana na ambayo ingeweza kuwaweka pabaya ilikuwa ni Tarakilishi aliyokuwa nayo Jama, Tarakilishi hiyo ilikuwa ina kila kitu,tayari siri nyingine kutoka kwa wanausalama wasio waminifu ilikuwa imeshafika mbele yao kuhusu tarakilishi zile. Wote walikuwa wameshajua kuwa nenosiri hayo yaliyopo kwenye tarakilishi nne tofauti yalikuwa yakiunganishwa ndiyo nenosiri kamili ya kuweza kufungua tarakilishi ya Jama ambayo ndiyo ilikuwa na kila kitu kuhusu wao kilikuwepo humo ndani. Watu hawa walikuwa wamezipata taarifa ambazo walivujishiwa kabla hata ripoti yenyewe ikiwa haijakamilika kutoka kwa wanausalama ambao hawakuwa waminifu kabisa, kupitia taarifa hizo ndiyo walibuni mpango mzima wa kuweza kuwafanya wasiwe ndani ya kuti kavu. Hapo waliweza kuleta mpango wenyewe wa kuwamaliza wale wote waliokuwa wamefanya utafiti huo ili kuweza kuchukua siri hizo, hakika mpango huo ulisukwa na ukasukika na ulipangwa ukapangika.
Mpango huo ulianza ndani ya siku ambayo Mheshimiwwa Bia alifariki kwa bomu la barua, na kisha wakafuata maofisa wa kitendo cha CID katika jeshi la polisi katika kumalizwa na mpango huo. Walikuwa wameupa jina la wito wa kuzimu. jina la mpango huo lilikuwa na linawakilishwa na barua bomu walizokuwa wakizituma kwa watu ambao walikuwa wameshikilia siri hizo. Muonekano wa barua hizo ambazo zilikuwa zimekaa kama barua za watu waliokuwa wakiabudu shetani ndiyo waliutumia kuwafanya wahusika wawe na wahka wa ufungua barua. Muonekano huo ulikuwa umeundwa na mhuri ambao waliutumia kupiga juu ya barua pamoja maneno yaliyokuwa yakiashiria nguvu za giza, stempu ya barua hizo waliunda wenyewe na hawakutaka zijulikane kama walikuwa na stempu ambazo zilikuwa hazihusiki kabisa ndani ya shirika la posta ndiyo maana walivika bahasha nyingine kwa juu. Zilikuwa ni stempu walizompiga picha mwanamke akiwa hana nguo ya juu akiwa ameonesha mgongo pekee uku chini akiwa na nguo ambayo iliuwa imeegeshwa tu.
Sasa mpango huo unaanza kuingia doa kwa mara ya pili tena ikiwa bado kazi yenyewe ni mbichi kabisa haijaweza kukamilika hadi waseme kuwa amani ipo, wakuu walikuwa wapo kwenye meza moja ya kulia chakula muda huo na timu nzima waliyokuwa wameiteua kuweza kukamilisha kazi hiyo. Timu nzima ilikuwa ikitambua kuwa wakuu hao walikuwa wamechanganyikiwa sana kutokana na taarifa hiyo iliyokuwa ipo mezani kwa muda huo. Wakuu hao waliokuwa wamepewa jina Roho mmojawapo kutokana na kazi yake ya kufanya hila za kukinga mambo yao yasiharibike na mwingine alikuwa amepewa jina la Moyo kutokana na kuwa ndiyo mtu pekee aliyekuwa akirahisha kabisa mipango yao kama itaingia ugumu wowote. Wote wawili walikuwa ni watumihi wa umma wa ngazi za juu kabisa ndani ya serikali ambao walikuwa wakipewa jina la Waheshimiwa lakini waliyokuwa wakiyafanya hayakufaa kabisa wao kupewa jina hilo.
“Jamani bwawa letu linaingia ruba mapema yote hii, nguvu zote tulizotumia na hata maelfu ya watu tuliowapoteza kwa wito wa kuzimu kweli iwe kazi bure” Mheshimiwa Roho aliongea
“Hata mimi nashangaa yaani imekuwaje hamjui kama tunafanya mipango kutufanya tule ugali wote hapa na pia kujitajirisha, sasa iweje kiumbe mmoja aharibu mipango yetu” Mheshimiwa Moyo naye aliingilia kwa ghadhabu
“Jamni tatizo ni kwamba kazi hii imeingiliwa katika muda mbao tulikuwa hatujapewa taarifa kuwa kuna mwanausalama yeyote yuo kazini, hivi ingekuwa tuna taarifa kama ambavyo Bwana Roho ulifanya pale CID walipoingia kazini huyu mtu angepeumua kweli ” Askofu Valdermar aliongea
“Jamani si niliwambia mimi kuwa hii kazi waliopo ndani yake ni Milliatary intelligence pamoja na TISS” Mheshimiwa Roho aliwaka
“Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mezani kwangu kutoka kwa kibaraka wetu aliyepo jeshini amesema kuwa watu hao wameacha hiyo kazi baada ya mtu mahsusi kuingia kazini sasa siyo hao, hata TISS hivyohivvyo wamepewa agizo la kujitoa na kazi ipo kwa nani sasa?” Askoafu Valdermar aliuliza
“I think ni EASA hawa” Mheshimiwa Moyo alikisia jambo ambalo lilimfanya Josephine ashtuke kabisa.
“Waheshimiwa kama ni hawa EASA wapo kazini basi aliyekuwa yupo nyuma ya haya masuala ni Norert Kaila si mwingine tu” Josephine aliongea
“Are sure Josephine?” Mheshimiwa Moyo aliuliza
“Yes, kwasababu ni yeye ndiye tulimuona jirani na maneno ya garage yetu kule alifuata nini na tulipojaribu kumuua pale Tazara alikwepa kwa kuruka kwenye pikipiki means katujua huyu hakuna jingine tu”
“Hivi huyu mtu ndiyo kweli atusumbue kichwa jamini?” Mheshimiwa Moyo aliuliza
ITAENDELEA
Wito wa Kuzimu Sehemu ya Tatu
Also, read other stories from SIMULIZI;