Penzi Zito Sehemu ya Kwanza
IMEANDIKWA NA: PROSPER MGOWE
*********************************************************************************
Chombezo: Penzi Zito
Sehemu ya Kwanza (1)
Alikuwa akitoka shuleni kuelekea nyumbani kwao. Alikuwa na mawazo mengi juu ya masomo pamoja na maisha yake hakuelewa ni kwanini toka asubuhi ya siku hiyo alikuwa akitafakari juu ya jambo hilo.
Akiwa tayari amekwisha yaacha mazingira ya Shule, Ghafla mawazo yake yalikatishwa na sauti iliyotokea nyuma yake “BryanBryan”. Ilikuwa ni sauti ya kike lakini ilikuwa vigumu kwake kuitambua, inawezekana ni kwa sababu ya mawazo aliyokuwa nayo. Lakini hiyo sauti kwake haikuwa ngeni, Aligeuza shingo taratibu ili kuona ni nani aliyemuita, alikuwa ni Mercy aliyemuita. Bryan alimsubiri kando kidogo ya njia. ” Mambo vipi Bryan? Mercy alianza kwa kumsabahi Bryan” Ah safi tu” alijibu Bryan.
“Mbona leo uko hivyo? Aliuliza Mercy. Badala ya kujibu alinyamaza kwa sekunde kadhaa kasha naye akamuuliza kwani nikoje? Nakuona kama una mawazo mengi au naogopa? Hapana ni kweli siku ya leo siko kawaida, Sasa unawaza nini Bryan ili hali wewe bado mwanafunzi? Nawaza maisha Mercy ” Kwa nini unasema hivyo wakati wewe bado mwanafunzi tena ndio kwanza uko kidato cha pili” Nina haki ya kuwaza hivyo kwa sababu sina hakika kama nitaendelea na shule mpaka mwisho. “He! Hebu acha utani wako Bryan” Mercy alisema huku akionyesha kutoamini Bryan kwa kile alichokiongea.
Ni kweli Mercy kwa sababu maisha ya nyumbani kwetu ni magumu mno, Mama yangu hana kipato cha kutosha kuweza kuniendeleza na masomo yangu ya Sekondari na isitoshe hana karo ya term hii kuipata kwake kwenyewe ilikuwa shida, yaani mpaka mama auze mandazi,vijisenti atakavyodunduliza ndio aniwekee kwa ajili ya karo, hapo bado nyumbani hatujala wala hatujavaa. Na isitoshe safari hii ngano imepanda bei na mama yangu hata hela ya mtaji hajafikisha, Yaani hata sielewi tutaishije maisha haya.
Bryan alijaribu kumuelezea Mercy maisha ya kwao kwa uchungu mwingi mno. Muda wote huo Mercy alikuwa akimsikiliza Bryan kwa makini huruma ilimjaa ila hakuelewa ni vipi angemsaidia Bryan.
“Bryan” Mercy aliita “Ndio nakusikiliza unasemaje aliita na kuuliza.
“kuna kitu kimoja naomba nikuulize kama hutojali” “hakuna shida we uliza tu”
“Hivi bana yako alishafariki au bado yupo hai? Bryan alinyamaza kama sekunde kadhaa kisha akaguna “Duh” ni story ndefu sana lakini nitakueleza kwa ufupi tu. “Hakuna shida kwani shida yangu ni kutaka kujua kuhusu hilo tu.
Lakini kabla hata Bryan hajaanza kumsimulia Mercy juu ya Baba yake walikuwa tayari wamefika kwenye kituo cha daladala.
“Oya nyie madent hamuendi?Sauti ya konda iliwashitua .
“Mercy twende tupande hii” Bryan alimwambia Mercy. Hapana ngoja kwanza mpakatumalize maongezi yetu Bryan alikubali na kumruhusu konda waende.
Mercy ni binti wa pekee katika familia ya Mzee Josephat. Familia hiyo ilikuwa na watoto wa nne, wa kwanza Irene na wa pili Jacobo akifuatiwa na Isack na kitindamimba ambaye ni Mercy. Hawa wote walikuwa na maisha mazuri kwa sababu wote walikuwa na Elimu nzuri na kila mmoja alikuwa anakazi yake kasoro Mercy ambae alikuwa bado anasoma ndo kwanza yupo kidato cha pili.
Mzee Josephati pamoja na Mkewe Mama Irene walijitahidi kumpatia Mercy kila hitaji ilimradi tu Binti yao asome kama ndugu zake.
Mercy na Bryan hawakuwa wakisoma darasa moja, Mercy alisoma kidato cha pili B, wakati Bryan alisoma kidato cha pili mkondo A .Lakini wote walikuwa kidato kimoja. Hawakuwa marafiki kiasi kwamba wakutane na kuanza kuongea zaidi ya dakika tano,hiyo haikuwahi kutokea. Ilikuwa kila walipokutana ni salamu na kila mtu anaendelea na shughuli zake.
Toka siku nyingi Mercy alikuwa akimpenda Bryan lakini tatizo lilikuwa likimtatiza ni vipi ataweza kumueleza Bryan anavyojisikia juu yake.Alihofia kuwa baada ya kumueleza Bryan jinsi anavyojisikia juu yake angeonekana kuwa yeye Malaya, Lakini alijiapiza ipo siku lazima angemtobolea.
Wakati Mama yuko kidato cha nne alipewa namba na mvulana mmoja aliyekuwa anasoma Chuo Kikuu Dar es-salaam aliitwa Enock Mwansasu.Mama yangu alifukuzwa Shule baada ya kugundulika kuwa ni Mjamzito.Baada ya kufukuzwa Shule Mama alimuendea yule Mwanaume aliye mpa Mimba na kumueleza kuwa ana mamba yake.
Yule Mwanaume ambaye ndio Baba yangu alikubali ile Mimba na kuhaidi kuwa atamtunza yeye na kiumbe kilichokuwa Tumboni. Baba aliendelea kumtunza Mama na kumtimizia kila hitaji ambalo mama alihitaji mpaka nilipozaliwa mimi. Baadaye baba alihitajika aende Urusi kwa Masomo yake kwa kipindi cha miaka mitano, Lakini Baba alimuomba Mama asijali kwani safari sio kifo, kwa hiyo ipo siku atarudi kama Mungu akijalia basi watafunga ndoa. Kwahiyo waliagana na kila mmoja akiwa na majonzi ya kumkosa mwenziwe kila mmoja alionyesha kuwa ana penzi la dhati kwa mwenziwe. Baada ya hapo Baba alisafiri na kwenda nje kusoma.
Huku nyuma Mama aliendelea kutumiwa misaada mbalimbali na baba.Hali hiyo iliendelea takribani miezi sita (6) halafu hali hiyo ikakatika ghafla, kukawa hakuna msaada wala msaidizi. Mama kuona hivyo akaamua kufungua genge kwa akiba ndogo aliyokuwa nayo. Hilo banda ndio lilimsukuma mpaka akajenga nyumba ndogo ya udongo yenye vyumba viwili na sebule na hilohilo banda limenisomesha shule.
Tuliendelea kuishi hivyo na Mama yangu huku tukiwa tumepoteza matumaini ya kumuona Baba katika maisha yetu.
Ilipofika mwaka 1994 tulivamiwa na wezi wakavunja nyumba yetu pamoja na genge letu wakachukua kila kitu walichokiona kuwa kwao ni cha thamani na kasha wakatokomea.
Hali hiyo ilimlazimu Mama yangu awe omba omba tuliendelea kuishi kwa kazi hiyo mpaka Mama alipopata mtaji wa kuanzisha biashara yake ya maandazi ambayo mpaka sasa ndiyo inatusaidia. Na sasa hivi ninavyoongea na wewe Mama yangu ni Mgonjwa sana na mimi peke ndio tegemeo lake sijui nitafanya nini.
Bryan alipomaliza kusema hayo macho yake yalilengwalengwa na machozi. Na kwa upande wa Mercy yeye uso wake uliingiliwa na simanzi kuu. “Pole sana Bryan kwa matatizo hayo”.Alisema Mercy kwa upole huku akimtazama Bryan machoni. “Asante japo sijapoa”. “Usijali sana Bryan kwani Mungu hamtupi mja wake”Mercy alijitaidi kumfariji Bryan.
Maneno yale kidogo yalimtia nguvu Bryan, Muda ulikuwa umekwenda sana kwa hiyo wote wakakubaliana wapande Hice lakini kabla ya kupanda kwenye daladala Mercy alitoa noti ya shilingi Elfu mbili na kumpatia Bryan. Nashukuru sana Mercy kwa wema wako naomba Mungu akuongezee. “Usijali Bryan” Alisema Mercy huku akitabasamu.
Mercy na Wazazi wake walikuwa wakiishi mtaa wa Area D Mkoani Dodoma na Bryan alikuwa akiishi katika mtaa wa Chadulu katika Mkoa huohuo.
Daladala ilipofika njia panda area D Bryan alimuaga Mercy na kuteremka kuelekea kwao. Moyo wake ulikuwa ukimuenda kasi ambavyo si kawaida yake.
“Hivi kwa nini moyo wangu uko hivi? Mh Sio bure huko nyumbani lazima kutakuwa na jambo”Aliwaza Bryan na kuanza kuongeza ukubwa wa hatua. Alipofika hatua chache kabla ya kufika kwao alisikia kelele. “Jamani majirani naombeni msaada.”Alikuwa ni mama wa Makamo alikuwa ni jirani yao Mama Musa. Alionekana akitokea upande wa Maliwatoni kwa akina Bryan huku akiwa anamkokota mtu. Mtu huyo alionekana amelegea mno na mdomo wake ukiwa wazi huku povu jingi likimtoka.
Alionekana anahema kwa taabu sana. Mtu aliyekokotwa hakuwa mwingine bali ni Bi Sara ambaye alikuwa ndiye Mama yake Bryan. Bryan alishituka sana alipomuona Mama yake yupo katika hali ile. Akaanza kukimbilia kule aliko Mama Musa na Mama ili kufahamu kumetokea nini.
“Hah Mama amekuwaje? Bryan alishitukiaamemuuliza Mama yake swali hilo bila kujali hali aliyokuwa nayo.
“Fanya haraka kaite Taksi” Alisema Mama Musa huku akiwa anaendelea kumkokota Bi Sara kuelekea kiliko kituo cha taksi.
Bryan hakuuliza swali zaidi alitoka pale mbio kuelekea kwenye kituo ch Taksi.Ulikuwa ni mwendo wa dakika. Ulikuwa mwendo wa dakika tano kutoka kwao mpaka kituo cha taksi.
Huku nyuma wakina mama wajirani walishakwishafika kumsaidia Mama Musa.Baada ya muda mfupi taksi ilifunga breki miguuni kwao kwa kundi la wakina mama “Tufikishe General” Alisema Mama Musa huku akifungua mlango wa wa siti ya nyuma ya taksi alisaidiana na wakina mama wenzake kumpakia ndani ya taksi.Bryan alikaa siti ya mbele.Mma Musa na jirani yake Mama Rashidi pamoja na Mgonjwa Bi sara wlikaa nyuma. Na safari yakwenda hospitali ikaanza. “Jikaze bwana wewe ni mtoto wa kiume”Alisema Dereva walipokuwa njiani, baada ya kumuona Bryan analia. Bryan hakujibu zaidi ya kuendelea kulia kilio cha kwikwi.
Mama Bryan alikuwa mgonjwa takribani wiki sasa. Japo hakuwa serious sana alikuwa ansumbuliwa na BP pamoja na Athima.
Siku moja akiwa ndani amejipumzisha akaja jirani yake mama Musa kumtakia hali, “Haya wajionaje leo mama Bryan” Mama Musa alianza kwa kumsabahi jirani yake.
“Namshukuru jalia leo ahueni” alimjibu mama Bryan. Waliendelea na maongezi kwa muda kama robo saa. Baadae Mama Bryan alimtaka radhi mama Musa kuwa anaomba amsubiri kwa nukta chache anaenda chooni mara moja. Naomba nikusindikize kwa sababu siamini kama utajiweza” Alisema mama Musa. “Usijali nitajikongoja”Alijibu mama Bryan. Mama Musa alimuacha mama Bryan aende peke yake japokuwa alikuwa hamuamini sana hali yake.
Baada ya Mama Bryan kutoka nje kwa kulegalega hukunyuma Mama Musa hisia zake zikawa hazimpi kabisa kuendelea kubaki mule sebuleni, akatoka nje na kusimama mlangoni. Zilipita dakika 5 bila Mama Bryan kutoka msalani. Baada ya dakika hizo kupita Mama Musa alisikia kishindo kutoka msalani kama mtu amedondoka vile.
Mama Musa aliuendea ule mlango wa choo kwa haraka na kusukuma kwa bahati nzuri ulikuwa umerudishiwa, ulipofunguliwa hakuamini kile alichokiona kwani Mama Bryan alikuwa ameanguka pembeni ya shimo la choo huku povu likimtoka mdomoni. Mama Musa alimuinua na kumbeba mpaka nje.
Ndani ya taksi wakielekea hospitali Mgonjwa alikuwa bado hajazinduka, kufika maeneo ya bunge Mama Musa na Mama Rashidi wakamuona mgonjwa kwa taabu anafumbua macho. Mioyoni mwao wakaanza kupata matumaini kuwa mgonjwa wao anapata ahueni katika siti ya mbele hakuna aliyeelewa kinachoendelea nyuma si Bryan wala Dereva.
Katika siti ya nyuma mambo yakawa sivyo na matarajio kwani Mama Bryan alianza kutupa miguu pamoja na mikono na baadaye akaanza kugeuzageuza macho halafu akajinyoosha na kisha kukakamaa.
Mama Musa alikuwa kaduwaa na Mama Rashidi kubung’aa wasijue cha kufanya.
Mzee Josephati na Mkewe Bi Maua walikuwa wamepumzika sebuleni wakiangalia TV na mara wakasikia hodi, “karibu mlango umeludishiwa tu” alijibu Bi maua na mara akaingia Mercy. Usoni mwake alivaa sura ya simanzi kana kwamba kulikuwa na msiba mkubwa mno.
“Shikamooni” aliwasalimu wazazi wake “Marahaba” waliitikia kwa pamoja. “Vipi huko utokapo ni kheri au shari”? Bi maua alimuuliza binti yake baada ya kugundua hayuko katika hali yake ya kawaida. “Heri tu mama” alijibu Mercy huku akijilazimisha kutabasamu.
Mama yake alielewa kuwa kuna tatizo linalomtatiza binti yake lakini hakutaka kumsonga sana kwa maswali alimuacha aende kwanza akapumzike.
Mercy alipoingia chumbani kwake alijitupa kitandani bila hata kubadili uniform hata kula chakula hakikukumbuka tena kwa kipindi hicho. Hiyo yote ilisababishwa na fikra juu ya Bryan ni jinsi gani ataweza kumsaidia?. Ni vipi ataweza kumtatulia matatizo yake aliyonayo na kumfanya aweze kuishi kwa furaha na ni vipi ajieleze mpaka aeleweke juu ya hisia zake kwa Bryan. Na si hivyo tu alikuwa anatamani siku iishe upesi akaonane na Bryan.
Dereva hakujua kilichotokea bali aliendelea kutereza akielekea hospitali.
Walipita getini na kuingia ndani kabisa hospitalini. Dereva alifunga breki na kufungua mlango wa upande wake alishuka na kasha akazunguka upande wa pili na kumfungulia Bryan.
Huku nyuma Mama Rashidi na Mama Musa walishuka na kumuomba dereva awasaidie kumbeba mgonjwa. Na Bryan naye bila kuambiwa alitaka kushiriki katika hatua hiyo. “Ah hapana Bryan we acha pumzika tu” Mama Rashidi alimkataza Bryan. “Kwanza shika hii mia tano ukale mgahawani kwa sababu toka utoke shule haujagusa chakula aliongea Mama Musa.
Bryan ikamlazimu aichukue ile hela japo kwa shingo upande. Lakini akili na mawazo yote ni juu ya mama yake ambaye kwa yeye anavyomfahamu ni Mgonjwa Mahututi alianza kutembea kwa hatua ndogondogo huku akiwa amenyong’onyea kuelekea kwenye mgahawa uliopo pembeni kidogo na hospitali ya General. Alipofika Mgahawani akaagiza chakula na badala ya kukila akawepo anakitazama utafikiri ndo kwanza anakiona.
Aliendelea kukitazama kile chakula takribani dakika tano kana kwamba kile chakula hakikuagiza yeye.
Mercy alikuwa ndani ya daladala akielekea Dodoma Sekondari shule ambayo alikuwa akisoma. Moyoni mwake alikuwa na furaha tele akiamini hiyo akiamini ni siku nyingine tena ya kwenda kuonana na Bryan. “Oya kuna anaeshuka hapa bohari”? ilikuwa ni sauti ya konda.
“Shusha” Mercy alijibu. Mercy alishuka na kumlipa konda nauli kisha akavuka barabara akielekea shuleni kwao.
Alipofika shule alikuta wenzake wametawanyika kutoka assembly kuelekea madarasani. Aliangaza macho yake huku na kule asijue wapi kwa kumpata Bryan. Baadaye akaamua kwenda darasani kwa akina Bryan ili kuuliza kama amekuja.
Alipofika darasani kwa akina Bryan alimuendea moja kwa moja rafiki yake Martha ambaye ni Monntress wa darasa hilo. “Sema shoga mambo vipi”? Mercy alimsabahi shoga yake huo. “Safi tu, issue vipi?” Martha alijibu na kuuliza, “Poa alijibu Mercy”. “Bryan ameshafika?” “hapana naona leo kachelewa kidogo lakini atafika muda si mrefu” kwa maneno yale alinyong’onyea lakini alijipa moyo kuwa bado nukta chache Bryan angetokea kipindi kipindi cha kwanza kiliisha, hakuna Bryan kuonekana cha pili na hatimaye cha tatu Bryan hakutokea.
Mercy ilikuwa ni huzuni kubwa mno kwani alijihisi ni ni mpweke kuliko.Katika vipindi vyote hivyo vitatu hakuelewa somo hata moja na zaidi aliona walimu wote wanaofundisha ni kero kwake. Alijishangaa kwa nini Bryan amemuingia kiasi kile, ukizingatia Bryan mwenyewe hawana siku nyingi toka wazoeane. Alizikusanya daftari zilizokuwa juu ya meza yake na taratibu alinyanyuka kwenye kiti alichokuwa amekalia na taratibu akaulenga mlango wa kutokea kwenye ofisi ya walimu.
Alipoingia Ofisini alimkuta mwalimu wake wa darasa Mr Innocent “Morning Sir”
“Have a good day what’s ya problem”, “I’m not feel well I think this is Malaria” “So you want go to the hospital”, “Yes Sir” Okay you may”.
Alikula robo ya chakula kile kasha akalipa hela na kunyanyuka. Mapigo yake ya Moyo yalikuwa yakienda mbio mno. Mwendo wake ulikuwa wa haraka mno pindi alipotoka mgahawani hapo akielekea hospitalini.
Pengine ungemuona usingeweza kuelewa anatembea au ankimbia. Ilikuwa nusu kutembea nusu kukimbia akaingia hospitalini na moja kwa moja akaenda mapokezi. “Samahani dada sijui mgonjwa aliyeletwa muda mfupi kabla ya sasa sijui yupo sehemu gani? “Salamu kwanza kaka angu. Lakini usijali sana wameingia katika chumba cha docta” “Samahani kwa hilo dada angu, shukrani” Bryan alijibu na kuondoka kwa mwendo wake uleule kabla hajasukuma mlango wa docta, mlango huo ulifunguliwa na Mama Musa pamoja na Mama Rashidi walitoka ndani ya chumba hicho.”Vipi?”Akina mama hao walimuuliza Bryan kwa pamoja.
Bryan kabla hajajibu aliwatazama wakina mama hao machoni kwa nucta kadhaa, Na kugundua macho yao yameiva na kuwa mekundu kuliko kawaida. Hivi ilimaanisha wametoka kulia muda si mrefu na hilo alilitambua na mara ghafla fikra zake zikaunda picha nyingine katika ubongo wake “Nataka kumuona mama yangu” alijibu Bryan huku mapigo yake ya moyo yakizidi kumuenda kasi.
ITAENDELEA
Penzi Zito Sehemu ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;