Penzi Zito Sehemu ya Pili
CHOMBEZO

Ep 02: Penzi Zito

SIMULIZI Penzi Zito
Penzi Zito Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA: PROSPER MGOWE

*********************************************************************************

Chombezo: Penzi Zito

Sehemu ya Pili (2)

Alikula robo ya chakula kile kisha akalipa hela na kunyanyuka. Mapigo yake ya Moyo yalikuwa yakienda mbio mno. Mwendo wake ulikuwa wa haraka mno pindi alipotoka mgahawani hapo akielekea hospitalini.

Pengine ungemuona usingeweza kuelewa anatembea au ankimbia. Ilikuwa nusu kutembea nusu kukimbia akaingia hospitalini na moja kwa moja akaenda mapokezi. “Samahani dada sijui mgonjwa aliyeletwa muda mfupi kabla ya sasa sijui yupo sehemu gani? “Salamu kwanza kaka angu. Lakini usijali sana wameingia katika chumba cha docta” “Samahani kwa hilo dada angu, shukrani” Bryan alijibu na kuondoka kwa mwendo wake uleule kabla hajasukuma mlango wa docta, mlango huo ulifunguliwa na Mama Musa pamoja na Mama Rashidi walitoka ndani ya chumba hicho.”Vipi?”Akina mama hao walimuuliza Bryan kwa pamoja.

Bryan kabla hajajibu aliwatazama wakina mama hao machoni kwa nucta kadhaa, Na kugundua macho yao yameiva na kuwa mekundu kuliko kawaida. Hivi ilimaanisha wametoka kulia muda si mrefu na hilo alilitambua na mara ghafla fikra zake zikaunda picha nyingine katika ubongo wake “Nataka kumuona mama yangu” alijibu Bryan huku mapigo yake ya moyo yakizidi kumuenda kasi.

“Hebu ngoja kwanza Bryan” Mama Musa alimtuliza, “Ni ngoje vipi wakati nataka nimuone mama yangu? Bryan alijibu kwa sauti kali kiasi. “Tulia kwanza utamuona tu mama” Mama Rashidi naye alijitahidi kumbembeleza.

“Hivi kwa nini mnizuie na mama yangu amekwishafariki?” Bryan aliongea huku na yeye macho yake yakiwa yamemuiva na machozi yakimlengalenga hii ilimaanisha ana hakika na kitu anachokiongea. Kabla mama Musa na Mama Rashidi hawajajibu maswali ya Bryan yalikuwa yakija mfululizo, mlango wa chumba cha daktari ulifunguliwa na daktari akijitokea mlangoni.

Uso wake ulikuwa kama wa mtu aliyepoteza matumaini fulani. “Jamani akina mama “nasikitika kuwajulisha ya kuwa mgonjwa Bi Sara hatunae tena” Alipokuwa akizungumza hayo Doctor alikuwa amewaelekea akina mama Musa kumbe kwa nyuma yake kulikuwa na Bryan.

Kauli hiyo ya daktari ilipelekea kilio kikubwa kilichoanguliwa na mama Rashidi na mama Musa kwa upande wa Bryan alikuwa kama kapigwa na butwaa. Alijitahidi asiyaamini masikio yake lakini ukweli ukabaki palepale, mama yake alikuwa hawezi kuongea tena, hawezi akafumbua macho tena, roho iliisha achia mwili tayari alishafariki.

Alikuwa bado katika hali ya mshangao mkuu, mara kwa ghafla akaanguka na kupoteza fahamu. Mara wakaja manesi na kumbeba Bryan kwenda kumuhudumia. Maiti ya Bi. Sara ilipelekwa Mochwari. Baada ya hapo Mama Musa na Mama Rashidi waliondoka na kwenda kutoa taarifa kwa majirani wengine, ili taratibu za mazishi zianze kufanyika.

Katika wodi aliyokuwemo Bryan kwa mbali alianza kufumbua macho na baada ya kufumbua macho akaanza kuyafikicha mara tatu ili aweze kuona vizuri. Hakupaelewa vizuri mahali alipokuwepo, baada ya kuangalia vifaa vilivyokuwamo mule ndani akatambua kuwa yupo wodini.

“Iweje mpaka niwe sehemu hii”?

Hili ndio swali la kwanza lilimjia katika ubongo wake, ndipo hapo akaanza kuhangaika kuvuta kumbukumbu kwa kuunda baadhi ya matukio yaliokuwa yakimjia kichwani. Na kujikuta akipata mfululizo kamili wa tukio.

Huku akiwa katika lindi la mawazo mara mlango wa chumba alichokuwemo ukafunguliwa, akaingia nesi huku kachana tabasamu.

“Una jisikiaje kakangu? Nesi alimuuliza Bryan huku bado kaachia tabasamu.

“Sijambo” Bryan alijibu kwa kifupi bila kuongeza neno.

Hujisikii maumivu sehemu yeyote? Nesi aliendelea kumuuliza, “Hamna” Bryan alijibu.

“Basi pumzika kesho utarudi nyumbani” nesi alimwambia.

Bryan baada ya kujibu akaanza kulia huku akimtaja mama yake ama kwa hakika alileta simanzi mno. Nesi ikabidi afanye kazi ya ziada amfariji na kumtuliza., ilimchukuwa muda mrefu hadi Bryan kutulia na hata hivyo bado alikuwa analia kilio cha kwikwi.

“Usilie Bryan kichwa kitakuuma.” Nesi alizidi kumtuliza zaidi.Bryan ilikuwa haimuingii kabisa kuwa mama yake hayuko tena duniani lakini ndo imeshatokea huna budi kukubaliana nayo. Imeandikwa na imeshatimia, kazi yake haina makosa, ameumba sasa katwaa.

Mercy alikuwa anashuka katika daladala katika kituo ambacho huwa anashukia Bryan. Lengo lake lilikuwa ni kufika kwa akina Bryan japokuwa hakuwahi kufika kabla.

“Eti anti samahani” Mercy alimwambia dada mmoja aliyekuwa akipishana naye njiani.

“Bila samahani” alijibu yule dada huku akimwangalia Mercy usoni kwa macho ya utafiti

“Sijui utakuwa unapafahamu kwa akina Bryan”? aliuliza Mercy.

“Yukoje huyo Bryan”?Aliuliza yule dada badala ya kujibu.

“Okey ni mwanafunzi wa Dom sekondari eeeh? “That’s right ndiye huyo kwao ni wapi?

Nyoosha huo hapo uchochoro utatokezea Galax salon, halafu kunja kushoto, nyoosha hiyo njia utakayokutana nayo utahesabu nyumba nne zilizo upande wa kushoto nay a tano inamkungu nje basi ndio hapo utakuwa umefika.

“Asante sana dada yangu nashukuru kwa msaada wako” Mercy alishukuru.

“Hamna tabu, usijali mdogo wangu” Yule dada alijibu na kuanza kuendelea na safari zake. Naye Mercy akaendelea na safari yake.

Bryan alikuwa yumo ndani ya taksi ya jirani yao Baba Musa akielekea kwao, ambako ni yeye pekee aliyekuwa anasubiriwa ili amuage mama yake. Bryan alikuwa amelia mno kiasi kwamba macho yamevimba nab ado machozi yanatiririka, Bryan aliyafuta machozi lakini baada ya sekunde kadhaa machozi yalikuwa yakiteremka chini ya mashavu. Naye bila kukoma aliendelea kuyafuta akisaidiwa na dereva Baba Musa.

Akiwa anaendelea kufuta machozi kwa mbali Bryan alimuona mwanafunzi mwenye sare zinazofanana na shuleni kwao lakini katika mood nyingine kabisa lakini kadri alivyozidi kumsogelea ndivyo alivyozidi kumfananisha.

Bryan alimwomba Baba Musa akimfikia yule mwanafunzi anaomba asimame na ikibidi amchukue. Baba Musa akamjibu hakuna shida, lakini wakati huo anaposema maneno hayo hajamtambua aliye mbele ya upeo wa macho yao ni nani na ni kwanini asubuhi yote ile awepo mtaani anarandaranda.

Walimfikia Mercy na gari ikasimama pembeni kidogo ya Mercy.

“Binti ninaweza nikakufikisha? Aliuliza dereva,”Lakini sio mbali sana alijibu Mercy.

Bryan alisikia sauti ya Mercy akanyanyua uso wake ili kuhakikisha kama amdhaniaye ndiye. Bryan alikuwa halii tena isipokuwa macho yake yalikua mekundu mno na yalikuwa yamevimba.

“Aise kumbe ni wewe ingia twende” Bryan alimwambia Mercy kwa sauti yenye masikitiko.

“Wooow kumbe uko humu Bryan basi ngoja tuwe sote”Mercy alijibu kwa furaha kwa ajili amemuona Bryan akaingia ndani ya gari akakaa siti ya nyuma. Lakini ghafla furaha yake ikakata pindi alipomwangalia Bryan usoni kwa makini, Bryan alionekana mnyonge na mwenye majonzi huku wakiwa wanaendelea na safari Mercy uvumilivu ulimshinda na kuanza kumuuliza Bryan kulikoni. Bryan badala ya kujibu swali la Mercy aliangua kilio upya. Ndipo Baba Musa akaona ni vyema ajibu kwa niaba japo kwa kifupi.

Wakafika nyumbani kwa akina Bryan wote wakiwa wanalia yaani Mercy na Bryan kasoro Baba Musa baadhi ya waliokuwepo kilioni walimchukua Bryan na Mercy kuwapeleka ndani, ilikuwa ni muda kwa kuaga maiti. Bryan walikuwa wameongozana na Mercy katika mstari wa waagaji ilikuwa ni zamu la Bryan kuaga mwili wa marehemu mama yake.

Alipofikia jeneza alisimama kando ya mwili wa mama yake na kumuangalia kama dakika tatu hivi kama kwamba haamini kuwa yeye ndiye aliyelala ndani ya jeneza lakini hata hivyo ukweli ukabaki palepale majivu hayawezi kuwa mkaa. Aliondoka na kuwaacha watu wengine wauage mwili wa marehemu. Mercy naye ilifika zamu yake alimuangalia marehemu kwa umakini kisha akajikuta machozi yakimdondoka naye akasogea mbele kwa kupisha waagaji wengine.

Baada ya zoezi hilo kwisha msafara wa kwenda makaburini ulianza. Taratibu za mazishi zilienda kama zilivyopangwa.

Mpaka arobaini ilipokwisha matanga yaliinuliwa na watu kurudi makwao. Katika kipindi chote hicho Mercy alikuwa karibu mno na Bryan katika kumfariji na kumpa moyo, pamoja na hayo Mercy alimuhaidi Bryan kuwa atakuwa tayari kutoa msaada kwa kila atachohitaji.

“Mama kuna maongezi naomba tuongee endapo utapata nafasi” Mercy alimwambia mama yake wakati wanakula chakula cha mchana.

“Hakuna tabu mwanangu” mama yake akajibu walipomaliza mama yake alimuita bintiye Mercy sebuleni kwa ajili ya mazungumzo.

“Ehee kina tatizo gani tena? Mama yake alimuuliza huku akimtazama usoni”. Hapana tatizo ila kuna kitu nataka nikueleze na ikibidi nitahitaji msaada wako.”Enhee kitu gani ambacho unataka kuniambia” Mercy alitulia kimya kwa sekunde kadhaa kisha akakohoa kikohozi cha uwongo na kweli kisha akaanza kwa kusema.

Mama kuna kijana mmoja ni mwanafunzi mwenzangu ambaye tunasoma naye kidato cha pili ni rafiki yangu sana. Huwa ananisaidia katika masomo ambayo huwa na feli na ananiheshimu sana na mimi hivyohivyo yaani inshort tunaishi kama ndugu (kaka dada ).

“Huyo kijana anaitwa nani”? Mama yake alimkatiza, “Anaitwa Bryan” Mercy alijibu kwa utulivu. “enhee”maana yake aliashiria aendelee.

“Sasa huyo kijana anamatatizo makubwa mno” “Matatizo gani”Mama yake aliuliza kwa mshangao.

“Ni kwamba Bryan ni kijana mwenye maisha duni sana kiasi kwamba school fees yenyewe kulipa ni mgogoro, yaani mpaka afanye biashara zake pamoja na mama yake ndio wadundulize hiyo karo ya shule.Ameishi hivyo toka form one mpaka sasa form two, Uniform zenyewe zimesha chakaa yaani toka mwaka jana mpaka sasa ninavyoongea ndizo hizo alizonazo.

“Anaishi na nani?” Mama yake alimkatiza tena kwa kumuuliza swali.

“Alikuwa anaishi na mama yake” Na sasa?

“Mama yake amefariki wiki iliyopita” “Oooh masikini” mama yake alionekana kuingiwa na simanzi Mercy akaendelea, sasa tatizolinapofikia Bryan hana hata ndugu hapa Dodoma.

Baba yake je? “Baba yake alienda kusoma akiwa mdogo nje toka kitambo tena Bryan akiwa bado mdogo mpaka leo haifaamiki alipo.

“Okey nimeshakumbuka aliwahi kiniambia ana mjomba wake ambaye anaishi chang’ombe, ila huyo mjomba wake mwenyewe matatizo matupu yaani ye na pombe, pombe na yeye, yeye pombe kwake ndo kila kitu na maisha yake ni mara kumi na maisha ya akina Bryan. Naye anaishi hivyo hivyo kwa kuungaunga, ilimradi siku zinasogea.

” Sasa ombi langu kwako ni kwamba naomba umsaidie aje kukaa hapa nyumba halafu ile nyumba yao ataipangisha. Angalau umfanye houseboy itakuwa afadhali ilimradi utakuwa umemsaidia na ndio itakuwa nafuu yake kwani hakuna wakumpa msaada zaidi, mama naomba naiwe hivyo alimaliza Mercy.

Kwa sauti aliyokuwa anatumia Mercy na umakini aliokuwa nao katika kuongea vilimgusa sana mama yake Mrcy na mara ghafla ulimjia moyo wa kumsaidia kijana huyo japokuwa hakuwa akimfahamu.

“Sasa mwanangu nimekusikia na nimekuelewa vizuri sana”. “sasa mama uwamuzi wako uko vipi katika swala hili”?

“Siwezi nikakupa jibu moja kwa moja mpaka nimueleze Baba yako kwa sababu yeye ndio kichwa cha familia tuone naye atalichukuliaje swala hili, lakini kwa upande wangu mimi sina neno yaani nimeridhia.

“Sawa mama naomba ujaribu kuongea na Baba mpaka akuelewe”

“Usijali nitamueleza na kesho nitakuambia ameamua nini”?

“Thank u mama Ilove u ” “Thank u my doughter and me too”

Mercy alinyanyuka sehemu aliyokuwa amekaa na kuelekea chumbani kwake mama yake hali kadhalika.

Bryan kwa kipindi hiki alikuwa akiishi kwa mjomba wake huko cha ng’ombe. Msoto ndio ukazidi tena baada ya kupoa kwani aliyokuwa akiishi kwa mjomba wake ni hafadhali hata ya kwa mama wa kambo,kwani shangazi yake alimfanya ndio kijakazi wake, yote hayo tisa, kumi ni kwamba ilifika kipindi mpaka Bryan ananyimwa chakula, Bryan alipouliza kwa nini hakuna la zaidi ya kuambulia matusi na kejeli.

“eti unauliza chakula we unajua hizo pesa za hicho chakula zinavyotafutwa, nenda kaone mwanaamke wa kumuuliza chakula, eti chakula” shangazi yake Bryan aliongea tena kwa kubana pua.

Mambo yote hayo alishushiwa Bryan baada ya kuuliza chakula baada ya kutoka shuleni. Bryan hakumjibu kitu shangazi yake zaidi ya kuguna tu.

“Duh” kweli ng’ombe wa masikini hazai na akizaa dume tena lina matege. Bryan alijikuta machozi yakimteremka kila anapomfikiria marehemu mama yake.

“Laiti mama yangu angekuwepo haya yote yasingekuwepo, japokuwa maisha yetu yalikuwa ya kubangaiza” Aliwaza Bryan huku akifuta machozi.

Bryan alipojaribu kumueleza mjomba wake juu ya matatizo ya pale nyumbani mjomba wake alionekana kutoyatilia uzito mambo hayo.

“Huyo ndio shangazi yako we mchukulie jinsi alivyo au wewe unafikiri kuna mwingine? Aliongea mjomba wake Bryan kwa sauti ya kilevi.

“Oh. Mungu hivi mimi nitaishi katika hali hii mpaka lini? Eee mungu nauhitaji mwangaza wako”

Bryan aliongea hayo baada ya jibu alilopewa na mjomba wake.Aliachana na mjomba wake na kuelekea chumbani kwake.

Alipoingia humo ndani alisimama takribani dakika mbili, tatu kabla hajaamua afanye nini.

Taratibu alipiga magoti katika chumba chake kisichokuwa na sakafu kisha akaikusanya mikono yake pamoja na kuifumbata pamoja mbele ya kifua chake, kisha uso wake ukaelekea juu ya paa la chumba kisha akaanza kusali kutokana na matatizo aliyonayo.

“We Mercy”

“Abee mama”

“Baba yako anakuita yupo sebuleni”

“Nakuja mama”

Ilikuwa ni saa 3 asubuhi siku ya jumapili Mercy alikuwa akijiandaa kwenda kanisani ndipo mama yake alipokuja kumuita. Mercy nyuma ya drensing table alikuwa anazibana nywele zake kwa nyuma kwa banio lake la njano.

Siku hiyo alivaa blauzi ya njano na sketi ya pinki yenye kubana juu wastani na chini ilimwagika. Viatu alivyovaa siku hiyo ni vya rangi ya manjano vyenye maua ya pinki.

Hakika Mercy alipendeza kama sio kuvutia. Alijigeuza geuza pale kwenye drensing table baada ya kuridhika kuwa vile alivyo ndivyo atakiwavyo kuwa akaanza kupiga hatua za taratibu kuelekea mlango wa chumbani kwake ili aende sebuleni akawasikilize wito alioitiwa na babake.

“Shikamoo Dady”

“Fine how u doing” alijibu kwa umombo babake Mercy” “Well” aliitikia Mercy.

“Okey mama yako amenieleza juu ya matatizo yako”

“Ndio baba”alidakiza mercy

Nimekueleweni na nimekubali huyo kijana aje kuishi pamoja nasi, lakini ataishi kama houseboy”

“Woow” Asante sana baba endapo atakuwa hivyo” Lakini akija huyo kijana sitaki mambo ya upuuzi” akijaribu kwenda wrong na sheria zangu ataondoka mara moja.

“Sawa baba” Aliitikia Mercy kwa heshima zote.

Mercy alichukuwa biblia yake na kutoka kwenda kusubilia daladala ili kuelekea kanisa kuu, hiyo ni siku nzuri kwake.

Asubuhi ya kuamkia jumapili Bryan aliamka mapema kabisa na kuanza kufagia uwanja kuzunguka nyumba yao, baada ya kufagia aliingia chumbani kwake kufanya usafi, japokuwa chumba hicho kuta zake hazikuwa na rangi wala sakafu lakini yeye alikipenda sana na muda wote kilibaki nadhifu.

ITAENDELEA

Penzi Zito Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment