Penzi Zito Sehemu ya Tano
IMEANDIKWA NA: PROSPER MGOWE
*********************************************************************************
Chombezo: Penzi Zito
Sehemu ya Tano (5)
Bryan akaikumbuka barua yake aliyoificha kwenye mvua ambayo mpaka muda huo hakuwa akifahamu ilipotoka na wala aliyemuandikia. Bryan alitaka kukusanya mtihani kabla hajamaliza kufanya maswali yote ili akaiokoe barua yake. Lakini zilikuwa zimebakia dakika 4 na maswali alo’ kuwa hajayafanya yaliyokuwa takribani kama 7 hivi. Kwa hiyo aliamua kungoja mpaka dakika ziishe.
Muda wa kufanya mtihani ulipokwisha wanafunzi wote walikusanya paper zao na mmoja baada ya mwingine kuanza kutoka nje kwa sababu mvua ilishapungua kwa muda huo. Bryan akili yake yote ilikuwa ni juu ya barua alo’tumiwa ambayo hakufahamu ilipotoka aliiendeea mpaka pale alipokuwa ameiweka. Alipofika na kuangalia barua yake ilipokuwepo nguvu zilimwishia kwani barua hiyo haikutamanika tena ilikuwa imelowa chapachapa. Akaichukua kinyonge na kuifungua lakini hakuambulia kiu kwani wino ulijichanganya changanya mno kiasi kwamba hata jina la muandishi akashindwa kulitambua.
Akiwa bado kasimama na barua yake hiyo mara Mercy akatokea na kumbusu shavuni Bryan akakwepesha
“Why Bryan?” Mercy aliuliza akionesha kusononeka.
“Hapana Mercy si unaona macho ya watu?” Mercy hakujibu zaidi ya kumtazama tu Bryan machoni.
“Enhe Vipi mtihani Mercy?”
“Ah kawaida tu sijui kwa wewe” ” Ulikuwa mgumu kiasi chake” Alijibu Bryan ” Sasa hiyo barua vipi mbona imelowana? Bryan akaanza tena kumpa kisa kizima mpaka ikawa vile.
“Mi nahisi aliyetuma hiyo barua ni Christer” Aliongea Mercy huku akicheka cheka.
“Hakuna kitu kama hicho” Bryan aliongea huku akijaribu kuamini huenda ni kweli lakini hakuwa na uhakika.
“Hivi Bryan naweza kukuuliza swali?. Uliza tu Mercy” Alijibu Bryan.
” Hivi ni kweli unanipenda” Aliuliza Mercy huku akimtazamaBryan kwa jicho la chati.
” Yaani mno, pengine ni zaidi ya unavyofikiria” Alijibu Bryan huku akimtazama Mercy kwa jicho lilelile la chati
“Mi nahisi kama vile nadanganywa” Aliongea Mercy huku akiwa kamkazia macho Bryan.
“Niamini Mercy” Bryan aliongea hivyo huku nafsi yake ikimnanga kuwa alikuwa akimghiribu Mercy.
Zilikuwa zimepita siku nyingi baada ya Bryan na Mercy kuhitimu O level, kwa sasa kila mmoja alikuwa akiyasubiri matokeo ya kidato cha nne kwa hamu zaidi. Katika kipindi hicho chote Bryan na Mercy waliendelea kuishi kama wapenzi lakini hata siku moja hawakuwahi kupata nafasi ya kufanya mapenzi. Sio kwamba hawakupenda iwe hivyo, wote walipenda lakini kwa Mercy ilikuwa zaidi isipokuwa tu Bryan alikuwa akikwepa kwepa kutokana na sababu zake mwenyewe ambazo yeye anaamini ni za msingi.
Sababu ya kwanza hakupenda hata siku moja awe mlangai, asije akamkubalia Mercy ilihali penzi lake lipo deep kwa Chrster; japokuwa hafahamu pa kuonana naye ila imani yake ilimwambia ipo siku watakuja onana.
Sababu nyingine ilikuwa kwamba hakupenda kuwavunjia heshima wazazi wa Mercy ambao kwake yeye aliwachukulia kama wazazi wake wa kumzaa na hakujua awashukuru vipi kwa kumfikisha hapo alipo. Hizo ndizo sababu za kumkwepa Mercy. Isipokuwa alichokuwa akijaribu kukifanya Bryan ni kutomkwaza Mercy na kumfanya muda wote aonekane ni mwenye matumaini Fulani katika maisha yake.
Bryan alifanya hivyo kwa kuhofia kwamba angemuonyesha kwamba hamtaki angeweza kumuanzishia visa vya ajabu ajabu na kumfanya yeye kujihatarishia ajira yake. Bryan aliamini kuwa kwa sababu Mercy ndiye aliyemtafutia ajira pia huyo huyo anayeweza kumkosesha ajira. Hivyo ndio maana Bryan alimpa Mercy respect kwa kuhofia hilo.
Tembea yake, muonekano wake na ongea yake ni dhairi alionekana yeyeni champion. Akiwa ni mwenye makampuni kadhaa ndani ya jiji la Dar es salaam alikuwa na kila alichostahili kuwa nacho kigogo wan chi.
Huyo si mwingine bali ni yule yule Mr Enock Mwansasu, baba mzazi wa Bryan aliyemtelekeza mama yake. Mr Enock Mwansasu alikuwa ni tofauti na mwonekano wake kiundani, ingekuwa ndio kwanza unamuona ungeweza kusema ni mtu wa maana sana ni zaidi ya mstaarabu, mtu anayejali watu sana, kumbe vivyo aonekanavyo sivyo alivyo.
Alikuwa ni mwanaume mwenye kila sifa mbaya, mshenzi, Malaya tena tena asiye na haya. Hakuwa hivyo kabla isipokuwa hayo yote yalitokea baada ya kurejea kutoka masomoni Urusi.
Alishawachezea wanawake kibao tu na kuwatendea visivyo, wengine aliwaghiribu na kufanya nao mapenzi kisha kuwaacha kwa nyodo na matusi kibao, wengine aliwajaza mamba na kuwakana. Hakuwa na mapenzi ya dhati hata nukta na hakuwahi kuzijutia dhambi zake hizo hata siku moja na aliendelea kuvunja sheria kama kawaida, hiyo yote ni jeuri ya pesa.
Alikuwa kaegemea meza iliyo mbele yake. Daftari alikuwa kazifunga alikuwa hatamani tena kuendelea kujisomea. Sio kana kwamba alikuwa amechoka kusoma isipokuwa mawazo yalikuwa yamemtinga mno. Ni christer huyo ndiye alomwandikia Bryan barua ili kumweleza anavyojisikia juu yake lakini mpaka sasa hapakuwa na jibu lolote hicho ndicho haswa kilichomfanya Christer azame katika dimbwi la mawazo kwa muda huo ajiulize maswali mengi. Alijiuliza huenda Bryan hajampenda? Au kanichukulia mimi ni Malaya sana? Kama sivyo hivyo kwa nini sasa aunyanyase moyo wangu? “Lakini najua ipo siku tutaja onana tu” Christer alijifariji lakini aliumia sana moyo na hakujua afanye nini kwa muda huo.
“Dah Ama kweli penzi kizungumkuti” Alijisemea Christer.
Zilipita siku kibao, sasa hakutaraji tena kupokea barua kutoka kwa Bryan kwani alishasubiri vya kutosha na sasa ameshachoka.
Ilikuwa ni jumamosi Christer alikuwa akitoka katika majengo ya Library ya mkoa na kuelekea maeneo ya Zuny Ice cream kupoza koo, Alipofika zuny alitafuta sehemu moja ambayo haikuwa na mtu ndipo akakaa, akaagiza juice na keki mbili. Baada ya vitu vilivyoagizwa kuletwa akaanza kunywa juice kwa taratibu lakini mara kabla hajaanza kumega keki alijihisi kijasho chembamba kikimtoka na midomo ilibaki wazi huku akiwa ameshika kipande cha keki mkononi.
Akajihisi amefreeze kwani kila kitu mwilini mwake alikihisi akifanyi kazi kama kawaida. Hiyo yote ilisababishwa na kile ambacho alikuwa akikitazama mbele yake.
Alikuwa amemuona mvulana ambaye alikuwa amemtafuta kwa muda mrefu bila mafanikio na hatimaye sasa amemuona pasipo kutarajia.
Ama kwa hakika akili ya Christer aliamini kabisa yule kijana aliyekuwa ametazamana naye, aliyekuwa amekaa mbele ya meza yake akinywa juice alikuwa ni Bryan, lakini cha ajabu na cha kushangaza huyo kijana ambaye christer aliamini kuwa ndiye Bryan alionekana kutomfahamu hata chembe binti aliyeko mbele yake.
Wakati Christer anatafuta pozi la kumuingia yule kijana, lakini hakuonekana kuwa na wazo lolote juu ya yule binti ambaye yeye hakumfahamu kabisa.
Christer akajiinua kutoka sehemu ambapo alikuwa amekaa na kwa hatua za hesabu akaanza kmuelekea yule kaka.
“Habari yako kaka” Christer alimsabahi kwa sauti ya utulivu.
“Safi tu dada’ngu karibu” alijibu yule kaka kwa sauti ya chini. Christer alimuangalia yule kaka usoni kwa sekunde kadhaa na kisha akakunja uso kidogo na kuachia hali ya kawaida kwa wakati huo kulikuwa na mawazo mawili katika kichwa chake yanayopingana. Wazo moja likikubali kuwa yule kaka alikuwa ndiyo Bryan halisi lingine likakataa kwamba yeye siye. ” Sijui tunaweza kujumuika pamoja?” Christer aliuliza. ” Hiyo tu haisumbui, unaweza mrembo ukakaribia” Alijibu yule kaka kwa sauti isiyo na kutetereka.
Christer alishukuru na kuhamishia vitu vyake kwenye meza ya yule kaka ambaye mpaka wakati huo hakujua anaitwa nani.
“Okey” may be nafikiri tungeanza kwa utambulisho, ” Sifahamu mwenzangu unaitwa nani?” Alianza yule kaka kwa kumswali Christer. Naye Christer alimjibu kama ifuatavyo;
“Najua sura sio ngeni kwako hata ya kwako siyo ngeni kwangu lamda nikukumbushe tu, ni kwamba mimi naitwa Christerbey”.
Yule kijana alimuangalia christer usoni kwa utafiti huku akijtahidi kuvuta kumbukumbu kama amewahi kumuona sehemu na kisha naye akasema
“Nashukuru kukufahamu christer kwa upande wangu mimi naitwa Lone”
Christer alishituka kidogo ni dhairi alikwishagundua ameingilia mlango wa kutokea, kwani alifananisha kwenye hamna. Kuanzia hapo Christer alianza kumtazama Lone kwa sura tofauti na kwa udadisi zaidi. Lakini kilichompa maswali na kumfanya achizike zaidi ni vipi Bryan na Lone wafanane kiasi kile?
“Na kuhusu kuonana kabla huenda ametufananisha” Lone aliendelea. ” Oh, samahani ni kweli hatukuwahi kuonana kabla nilikufananisha tu.” Alijihami Christer.
“Haina shida sana” Lone alimpoza kutoka muda huo kila mmoja aliendelea kunywa na kula pasopo kusema neno.
Zilipita takribani dakika 7 ukumya ukiendelea huku kila mmoja akimuangakia mwenzake kwa jicho la wizi na kisha Christer akavunja ukimya.
“Vipi Lone mbona kimya?”
“Ah, mi nakusikiliza wewe”. Lone alijibu kwa kubabaika kidogo. “Hivi Lone unaishi maeneo gani?” Christer alimswali Lone.
Mimi nimefikia Bahi road kwa aunt yangu mmoja hivi lakini mimi ni mzaliwa wa Dar-es-salaam”
“Okey nashukuru kufahamu hivyo”. Christer aliongea. Lone kwa ghafla bila hata yeye kutarajia alijihisi anahisia nzito sana za mapenzi juu ya Christer, tatizo ni jinsi ya kuanza kumueleza, je, aanze na step ipi, lakini alijiamini hawezi akamuacha kiumbe huyo wa uzao wa Eva hivihivi.
“Hivi ni kweli nimuache mtoto mzuri kama huyu hivihivi? No” haiwezekani.
Aliwaza Lone huku akimuangalia Christer usoni kwa macho yenye mng’ao.
Christer alipomuangalia Lone machoni alihisi moyo wake umelipuka kwa furaha, kwani alihisi ni kama nuru flani katika maisha yake na mara Christer akachana bonge la tabasamu. Lone alipomuangalia christer alijiuliza maswali mengi. “Huenda ameshayasoma mawazo yangu?” Au lamda ndo pozi lake? Lone alishindwa kupata jibu kamili. “Enhe Christer hivi unasoma wapi vile? “Lone alianza tena kumdodosa maswali” Nasoma Msalato Girls” alijibu Christer.
Kidoato cha .”” Tatu” Alimalizia Christer
Lone alichukua glasi yake ya juice na kunywa funda moja wakati Lone akifanya hivyo Christer glas yake alikuwa akiigongesha gongesha kwa taratibu kwenye meno yake.
Wakati vitendo hivyo vikiendelea kila mmoja alikuwa akiwaza la kumwambia mwenzake
“Nikwambie kitu” kila mmoja alimwambia mwenzake kwa pamoja.
Pia wote wakacheka nakisha Christer akasema “ungeanza wewe kuniambia hicho kitu”
“Hapana nafikiri ungeanza wewe kwanza” Lone alimbishia Christer” Hapana ungeanza wewe kwanza kwa sababu baba ni kichwa katika “
“A, ah Unafahamu kwamba Ladies first? Ukishalijua hilo nafikiri kutakuwa hakuna tena ubishi. Aliongea Lone.
Sawa umeshinda Lone, na nimekubali kushindwa” Aliongea Christer akikubali kushindwa, “Haya anielezee hicho kitu chenyewe” Aliongea Lone kwa usongo.
“Sa’skiza Lone nina vitu vingi sana vya kuongea na wewe” aliongea Christer na Lone akadakia ” Ehne cha kwanza”” Ungeanza wewe” Na cha pili”” Si ukishamaliza wewe?” Alijibu Christer na wote wakacheka.
“Acha usanii wako Christer mimi niko serious aliongea Lone.
S’kiza Lone naona muda unatutupa mkono, sasa cha kufanya naomba kama bado upo Dodoma hii naomba Jumamosi unijie shule, nitakuwa free! Aliongea Christer.
Okey nitafanya hivyo kikubwa tuombe uzima” alisema Lone. Wote wakaamka wakainuka vitini na kabla ya kuondoka Lone aliongea.
“Naomba nikukiss kama hutojali” Christer aliguna kidogo kisha akasema” Okey you may” huku akicheka cheka.
Lone alimchumu Christer shavuni naye Christer alifanya hivyo.
“Thank you” alisema Christer
“You too” alijibu Lone”
Baada ya hapo wote waliagana kwa miada ya kuonana tena Jumamosi.
Ni siku nyingine tena baada ya siku nginyi kupita Bryan na Mercy walikuwa wakitokea maeneo ya Internet café kutazama matokeo yao na kila mmoja akilini mwake alikuwa anawaza lake na mara Mercy akaanzisha maongezi.
“Bryan” Mercy aliita.
“Sema Mercy” Alijibu Bryan akionekana kushtuka kidogo, hiyo inaashiria kwamba alikuwa katika lindi la mawazo.
“Matokeo ndio kama hivyo tulivyoyaona, sasa mwenzangu unashauri kitu gani?” Aliongea Mercy. “Ngoja kwanza Mercy tuyafikishe kwa wazazi ndipo tuyajadili iweje”. Aliongea Bryan.
Kiukweli ni kwamba matokeo ya Bryan yalikuwa mazuri kuliko ya Mercy. Kwa sababu Mercy alipata 0 na Bryan alipata one ya point saba.
Walipofika nyumbani waliwaeleza wazazi wao yaliowajiri kwa siku hiyo.
Wazazi wao hawakufurahishwa na matokeo ya Mercy japokuwa walikuwa wakiamini binti yao ataendelea kusoma kwa njia moja au nyingine. Lakini pia walimpa pongezi nyingi sana Bryan kwa kufanya vizuri.
“Hongera sana Bryan, hongera baba” Walimpongeza baba na mama Mercy kwa kumpa mikono. Mercy akiwa na majonzi chungu mbovu na machozi kibao yakimtiririka kwa vile alivyouvurunda kwenye mtihani na asijue nini cha kufanya.
“Oooh, mwanangu Mercy usilie hivyo ni bahati mbaya tu, kwani hakuna mtu anayesoma kwa malengo ya kufeli. Isipokuwa ni bahati mbaya tu” Mama Mercy alijitahidi kumfariji mwanaye na kumuhaidi asivunjike moyo kwani ataendelea kusoma kwa namna yeyote ile.
Ilikuwa ni jumamosi ya kutimiza agano. Christer aikuwa nje kidogo ya maeneo ya shule akimngojea Lone. Mara baada ya nukta kadhaa akaona taksi moja ya kijivu ikimjia upande wake na kusimama pembeni yake kidogo na vioo vikashushwa. “Hi” ilisikika sauti ya Lone kutoka ndani ya gari.
“Hallow” alijibu Christer huku akichanua tabasamu.
“Ingia twende dada” Aliongea taksi driver. Christer alifungua mlango wa nyuma na kujitoma ndani na moja kwa moja safari ikaanza mpaka WIMPY wakashuka Lone na Christer na yule taksi driver akapewa chake na kupotea. Waliingia wimpy na kuchagua sehemu tulivu na kuketi. Waliagiza makulaji na mazungumzo yakaanza.
“Enhe za tangu kuachana” alianza Lone.
“Ah nzuri tu, sijui wewe” Alijibu Christer. Mimi heri tu”alijibu Lone. “Nimefurahi kukuona” hukuakimtazama usoni aliongea hayo Christer.
“Hunishindi mimi Christer” alijibu Lone. Christer alimuangalia Lone.
Christer alimuangalia Lone toka chini hadi juu nab ado isitoshe kummaliza, alirudia tena na tena mpaka na tena lakini bado aliona macho yake yakimdanganya nab ado alitamani aendelee kumuangalia hivyo tena na tena. ” Vipi Christer mbona unaniangalia hivyo” Ilimbidi Lone aulize baada ya kushtukia kwamba vile aangaliwavyo sivyo.
“Unajua Lone kunamtu nakufananisha naye yaani hivyo ulivyo naye pia yuko hivyo hivyo ndio maana nakuangalia sana”.
“Anaitwa nani huyo mtu?” Alizidi kuhoji Lone. “Kuna kaka flani anaitwa Bryan yaani mnafanana sana ama kweli nimeamini duniani wawili wawili”
“Lo aisee” Lone aliishia kuguna na kuyapuuza kwani hayo yalikuwa hayamuhusu sana na zaidi hayakuwa na faida kwake hivyo akayaacha kama yalivyo.
“Enhe” Christer nafikiri huu ni muda muafaka wa kuangalia kilichotuleta sasa nakusikiliza” Aliongea Lone.
“Unajua Lone katika maisha ya binadamu huwa anafanya au anatafuta kitu ambacho kitamfanya afarijike na ajisikie kujazika kama sio kukamilika alimradi ajisikie furaha”. Aliongea Christer. “Yaani unamaanisha kwamba;..” Alidakiza Lone.
Kabla ya kuendelea Christer alinyamaza kwa muda na kumtafiti lone machoni ataupokea vipi ujumbe anaotaka kumwambia Lone.
“Nakusikiliza”, aliongea lone. “Lone samahani kama nitakuwa nimeenda wrong na kile nitakachokwenda kukieleza kwako, lakini kiukweli mimi nafanya kama moyo unavyonituma”
“Enhe endelea” aliongeza Lone. “Ilove you Lone in a million reason” aliongea Christer huku sura yake ikiwa imevaa huzuni Fulani hivi.
“Wooooow so thanks u’r ma’ sweet sex lady” Aliongea Lone na kumkumbatia Christer huku usoni mwake kukiwa na tabasamu la butwaa.
“I’ll be your light shining bright “Aliongeza Lone. Baada ya hicho kikao cha dharula kwisha wote walinyanyuka na kwenda kituo cha taksi.
“Eh bwana suka tufikishe bahiroad” Lone alimwambia dereva.
“Okey buku mbili” “Haina shida” alikubali Lone.
Ilikuwa ni majonzi na simanzi mtimani mwa Mercy kwani alijua siku si nyingi Bryan ataondoka kwenda Tabora alipopangiwa kwenda kusoma masomo yake ya Adivance na kwa upande wa Bryan ni hivyo hivyo kwani alishindwa kuimagine maisha yake bila Mercy.
“Mercy usihuzunike sana kwani safari sio kifo naenda masomoni tu halafu nitarudi” Bryan alimfariji Mercy.
“Itanichukua muda mrefu sana Bryan mpaka nije kuizoea khali ya ukiwa” Aliongea Mercy huku machozi yakimlengalenga.
Alitamka Bryan alikuwa ndani ya taksi akielekea stendi kuu ya mkoa akisindikizwa na Mercy pamoja na mama Mercy.
Walipofika katika kituo cha basi Mizigo ya Bryan ikashushwa katika basi linalokwenda Tabora. Mama Mercy alimuaga Bryan kwa huzuni na kumtakia kheri katika masomo yake.
Muda wote ambapo mama Mercy alikuwa akiagana na Bryan Mercy alikuwa kasimama nyuma ya taksi huku machozi yakimtiririka pasipo kukoma. Huzuni alokuwa nayo haikumithilika alitamani sana aondoke pamoja na Bryan lakini haikuwezekana alishindwa kupata picha ya maisha yake bila Bryan, alihisi hayatokuwa maisha. Mercy akiwa katika hali hiyo mara honi ya basi analotakiwa apande Bryan ilipigwa.
“We Mercy njoo umuage kaka yako haraka, basi linaondoka” mama Mercy aliongea bila kufahamu mwanaye yupo katika mood gani kwani wakati ule na alipomuangalia usoni alimuona akibubujikwa na machozi.
“He we mwenzetu vipi?” Aliuliza mama Mercy.
“Unaumwa?” Alizidi kudadisi
“Mh mh?”
“Umeibiwa?”
“Mh mh?”
“Sasa tukuelewe vipi? Alizidi kuhoji mama yake.
“Mama Bryan, Bryan ananiacha mama peke yangu mama” Aliongea Mercy huku akilia kilio cha kwikwi
“He, kwa hiyo hutaki aende shule abaki na wewe tu”mama Mercy aliuliza na Mercy hakujibu.
“Mercy” aliita Bryan
“Abe” aliitika kama anadeka hivi
“Kwa heri Mercy , Aliongea Bryan kwa huzuni.
Mercy hakujibu lolote isipokuwa alizidi kumuangalia Bryan kwa macho yenye mjao wa machozi.
Umbali waliokuwa wamesimama kati ya Bryan na Mercy ni kama hatua nane hivi Bryan alitamani sana amkumbatie Mercy lakini alimuheshimu Mama yake Mercy.
Bryan akampungia mkono wa kheri Mercy na kugeuka kuanza kuielekea basi.
Kwa kasi ya ajabu Mercy alianza kukimbia kumuelekea Bryan alipo na alipomfikia alimkumbatia kwa nguvu zote pasipo kumuogopa mama yake.
Kichwa cha Mercy kilikuwa kifuani kwa Bryan, huku akikilowesha kifua cha Bryan kwa machozi ya huzuni.
“Bryan naomba usinitupe, popote uwapo naomba usinisahau” Aliongea Mercy kwa masikitiko.
“Siwezi kukusahau Mercy kwani wewe ndio mhimili wangu” Aliongea Bryan kwa sauti ya chini
“Nakupenda zaidi ya sana na nakutakia maisha mema” Naye Bryan alimaliza.
Waliachana na Bryan akamtazama kwa aibu mama aliyekuwa kaegemea taksi akiwatazama na kumpungia mkono wa mwisho mwisho.
Bryan alitoka mbio kuelekea basi ambalo lilishaanza kuondoka na kuingia ndani.
“Mr, naona ulishachizika na mtoto, ukasahau kabisa kama unasafari”. Konda alimtania Bryan, Bryan hakujibu zaidi ya kucheka tu.
Alienda mpaka kwenye seat yake ya dirishani na kisha akaketi.
Basi lilizidi kujongea huku nje mama Mercy alizidi kumpungia Bryan mkono pamoja na Mercy aliyekuwa kakiuma kidole chake cha shahada cha mkono wa kushoto huku mkono wa kulia ukimpungia Bryan kwa taratibu mpaka basi lilipoondoka kituoni hapo. Baada tu ya basi kutoweka Mercy aliangua kilio kilichowashtua hata watu wengine waliokuwako kituoni hapo.
Basi lilizidi kujongea huku nje mama Mercy alizidi kumpungia Bryan mkono pamoja na Mercy aliyekuwa kakiuma kidole chake cha shahada cha mkono wa kushoto huku mkono wa kulia ukimpungia Bryan kwa taratibu mpaka basi lilipoondoka kituoni hapo. Baada tu ya basi kutoweka Mercy aliangua kilio kilichowashtua hata watu wengine waliokuwako kituoni hapo.
Mama Mercy alimkumbatia mwanaye kwa nguvu na kumtuliza na kisha wakaingia ndani ya taksi na kurudi nyumbani.
Lone alikuwa ni mtoto wa Mr Enock Mwansasu (Baba yake Bryan) Isipokuwa yeye Lone alizaliwa na mama tofauti na mama yake Bryan.
Mimba ya Lone ilitungwa kipindi Mr. Enock alipokuwa Chuo Kikuu mwaka wa kwanza, kipindi hicho alipokuwa ameenda Sanawari Arusha pamoja na wanafunzi wenzake kufanya project. Ndipo siku moja alipokutana na Esnaty msichana mrembo ndipo Mr Enock alipomuelezea hisia zake naye Esnaty bila ajizi alimridhia na baada ya maridhiano ikawa kweli wakamake Love.
Kiukweli Mr. Enock hakumpenda Esnaty ile deepest zaidi isipokuwa alichokihitaji kutoka kwa Esnaty ni short time Love na baada ya Mr Enock ku make love na Esnaty alimbwaga na kuendelea na shughuli zake zilizomleta Arusha mpaka kurudi tena College. Hakuwahi kuonana tena na Esnaty hata alipoondoka na hakuna hata mmoja kati ya wao aliyekuwa na contact na mwenzake.
Mr. Enock hakumpenda kumpa nafasi Esnaty nafasi katika moyo wake kwa sababu alikuwa na mchumba huko Dodoma ambaye malengo yake ni kuja kuwa mke wake na mchumba huyo ndiye mama yake na Bryan. Hata hivyo Mr Enock alijutia sana tendo alilofanya na Esnaty kwa kujua alikuwa amemsaliti mchumba wake hata hivyo ilikuwa siri yake na alitubu moyoni mwake.
Kwa upande wa Esnaty baada ya masiku tele kupita akaanza kujihisi ni mjamzito na alipokwenda hospitali kupima kweli alikutwa ni mjamzito.
Siku, miezi ikazidi kukata na mara siku za kujifungua zikakaribia. Ni siku hiyo Esnatry alipougua uchungu nakukimbizwa Hospital na kufikishiwa wodi ya wazazi.
Katika vipimo vya daktari vilionyesha ya kwamba mtoto aliye tumboni ni mkubwa na hawezi kupita kwa njia ya kawaida kwani mlango wa uzazi wa Esnaty ni mdogo na hata wangejaribu kumzalisha kwa njia yabomba isingewezekana kwani wangemharibu mtoto na angeweza kuwa taahira au mgonjwa wa kifafa.
Hivyo njia mbadala walioiona madaktari ni kwenda kumfanyia Operation.
Operation ilifanyika na hatma ya yote mtoto alitoka salama ambaye ndiye Lone na kwa bahati mbaya Esnaty alipoteza maisha.
Hivyo Lone hakuwahi kumuona mama yake alilelewa na bibi yake pamoja na watu baki tokea udogo wake. Maisha waliyokuwa wanaishi katika Mji wa Arusha hayakuwa ya hali ya juu wala ya chini kabisa isipokuwa yalikuwa standard level.
Maisha yalizidi kwenda na umri wa Lone ulizidi kuongezeka alianza shule ya msingi na hata Sekondari.
Alipomaliza kidato cha nne matokeo hayakuwa mazuri na ndugu zake uwezo wa kumsomesha shule za private hawakuwa nao.
Siku moja usiku Lone alikuwa amepumzika chumbani kwake akaanza kukumbuka background ya maisha yake. Hakuelewa imekuwaje mpaka aanze kufikiria mambo yalopita katika maisha yake. Alijaribu kumImagine mama yake alifananaje lakini katu hakupata picha. Alijaribu kumkumbuka baba yake lakini wapi tena hakuwa hata na idea yake. Sio siri Lone aliumia sana na hata machozi yakamtoka na mwisho akapata wazo kuwa labda ajaribu kumtafuta kupitia vyombo vya habari kwani ilisadikika kwamba bado yuko hai.
Siku zote Lone alichokuwa akikiwaza ndicho alichokuwa akikifanya. Hivyo alisambaza matangazo magazetini na hata redioni na kisha yeye akatulia kusubiri matokeo ya matangazo yake.
Kwa bahati nzuri Lone alifanikiwa kumpata baba yake kwa kujulishwa kwa kupitia vyombo vya habari kwamba baba yake yupoDar Salaam. Lone alifurahi sana kwa adhma hiyo kufanikiwa na alifurahi zaidi pale alipogundua kwamba baba yake aliishi Dar ;es Salaam kwani toka zamani alikuwa akipenda kuishi Dar japokuwa hakupafahamu.
Ndugu zake walimchangia fedha kwa ajili ya nauli na zilipotimia Lone akasafiri kutoka Arusha kuja Dar;es Salaam. Mr. Enock alifurahi sana kukutana na mwanae na mwanae kadhalika. Lakini shughuli ilikuwa kwa mama”ke mdogo Lone. Damu zao zilikuwa tofauti hazikupatana hata nukta.
Kwa muda wa wiki mbili tu Lone alishachoshwa na visa vya pale kwao. Alishatukanwa sana, alishanyanyaswa sana, alishasingiziwa mambo kibao. Lakini hayo yote alipomwambia baba yake, wala hakuyatilia uzito wowote yeye jibu alilotoa ni kwamba huyo ndiyo mama yako na hivyo ndivyo jinsi alivyo kwa hiyo yakupasa umzoee.
Majibu hayo yalimnyong’onyeza Lone mpaka ikafika hatua akawa haipendi nyumba ile pamoja na waliomo humo japokuwa alikuwa na kila kitu ndani na hapo ndipo akawaza kutoroka kwenda Dodoma, kwa sababu aliwahi kusikia tetesi kwamba kuna shangazi yake yupo Dodoma; Lakini kabla hajaondoka alimuachia ujumbe Baba yake kwamba yeye ameondoka nyumbani na amekwenda Dodoma na hataki mtu yeyote amfuate kwani amechoshwa na maisha ya pale nyumbani kwake.
Na ilimuuma roho sana kwa sababu hakuwahi kufikiria kama kuna baba wa aina ile, tabia yake haieleweki wala hajali utu wa mtu licha ya mtu baki hata mwanae wa kumzaa alishindwa kuelewa yule ni baba wa aina gani.
Lone alipiga safari hadi Dodoma na kuanza kazi ya kumuulizia shangazi yake kwa bahati nzuri alimpata alikuwa akiishi bahiroad.
Kiuwezo shangazi yake huyo alijaliwa nyumba kubwa yenye kila kitu ndani na gari dogo moja kwa ajili ya kutembelea (yote hayo aliyafanya kwa juhudi zake binafsi) hakuwa na mume wala bwana.
Lone alipofika alipokelewa vizuri na shangazi yake huyo. Baada ya salamu na utambulisho. Lone alieleza mkasa mzima toka alipokuwa Arusha, Dar Salaam mpaka wakati huo yupo Dodoma.
“Hilo ndio tatizo la kaka’ngu sijui ameshachanganjikiwa na maisha? Maana hashauriki wala haonyiki, dharau tu zimemjaa sijui anafikiri hiyo mimali atakufa nayo” Aliongea kwa uchungu shangazi yake Lone.
“Mwanangu Lone”
“Naam shangazi”
“Usiwaze sana hayo yote ni mapito tu ya maisha wewe kaa hapa kuwa huru nitaishi na wewe kama mwanangu”
“Asante sana shangazi”
Huo ndio ukawa mwanzo wa Lone kukaa kwa shangazi yake.
Walipokuwa njiani kuelekea Bahiroad Lone na Christer, mmoja wao akatoa kauli iliyomshangaza mwenzie.
“Dereva simamisha gari” Aliongea Christer, Lone alishangazwa na kauli ile.
“Kwani vipi Christer” Lone alihoji.
Samahani Lone huko Bahiroad sitoweza kwenda kwenda”
“Kwani vipi Christer?” Lone aliuliza kwa mshangao.
“Kwani huko bahiroad tunaenda kufanya nini Lone” He swali gani tena hilo Christer?”
“Hapana haiwezekani” Christer alijibu.
“Hapana nini” nitachelewa kurudi shule lamda tupange siku nyingine”
Lone hakuwa na lakufanya ilibidi amuamrishe dereva kwa shingo upande ageuze gari na amrudishe Christer shule.
Nyumbani kwa akina Mercy, Mercy alikuwa mwenyemajonzi tele mtimani pamoja na uchungu mwingi wa kuachwa pekee, Mercy aliona kama dunia imemgeukia kwani kilichokuwa chini ya jua kwake alikiona ni bure.
Hata rafiki zake walipokuja walomboa tu. Faraja pekee alokuwa akihitaji katika maisha yake ni Bryan tu. Takribani kama wiki tatu sasa tangu Bryan aondoke kwenda shule, Mercy alikuwa yupo katika hali mbaya mno. Kwani siku zote yeye alikuwa ni mtu wa kulia kucha kutwa na kulala tu. Kuna muda Mercy alighafirika hata kula yote hiyo ni sababu ya mawazo juu ya Bryan kiukweli Mercy alitia huruma sana.
Wazazi wake walipogundua binti yao yupo katika hali hiyo, Walifanya maamuzi ya kumtafutia sehemu yenye mchanganyiko wa watu tofauti ili kuchelea binti yao asije kuharibikiwa kisaikolojia. Hivyo walifanya hima katika hilo na kuamua Mercy akasomee mafunzo nursing huko Mvumi.
Taratibu zilifanywa na hatimaye Mercy akaenda Mvumi. Japokuwa Mercy alikuwa huko na akakutana na watu wa aina tofauti tofauti lakini Mercy alijihisi kumpenda sana Bryan na alihisi kutomsahau kamwe. Ilikuwa haipiti saa kwa Mercy pasipokumkumbuka Bryan.
Hali kadhalika kwa Bryan hali ilkuwa ni hiyo hiyo, hakuna saa linaloisha bila kumbukumbu za Mercy kupita ubongoni mwake, lamda akilala na hata hivyo alalapo, ndoto si chini ya ishirini katika usiku mmoja ziingiazo zinazomhusu Mercy. Ama kwa hakika watu hawa walipendana sana japokuwa mapenzi yao yalikuwa na utofauti.
Mr Enock baada ya kukuta ujumbe ulioachwa na Lone, aliusoma na kuupuza, “Ah, shauri lake” ndivyo alivyojisemea Mr Enock.
Lakini kila siku zilipozidi kukata alihisi kitu Fulani kikimhimiza kwamba amfuatilie Lone.
Ilikuwa imeshapita miezi takribani tisa hivi tangu Lone aondoke Dar-es- salaam.
Ni asubuhi moja tulivu. Mr Enock akiamka akiwa tofauti na siku zote. Aliingia bafuni akajimwagia maji chapchap na kisha kuingia chumbani kwake, alichagua suruale moja nyeusi na shati la bluu na viatu vyeusi vilivyobinuka mbele pamoja na miwani yake nyeupe.
Alivivaa na kisha akachukua koti lake jeusi na kuliweka begani funguo za gari mkononi. Alitoka chumbani kwake na kuelekea jikoni alipo mkewe.
“Hello mama watoto” Aliita Mr Enock,
“Sema Mr”
“Naenda Dodoma asubuhi hivi nimemkumbuka sana mwanangu Lone” “Halooooo unalo hilo utajiju mwenyewe na misafara yako ya ajabu ajabu eti nimemkumbuka mwanangu, katika watoto yule naye mtoto” Aliongea Mrs Enock.
“Usitake kunitibua asubuhi asubuhi we mwanamke unasikia? Yule mtoto ni damu yangu lazima nimfate huko aliko.” Aliongea kwa jazba Mr. Enock.
“Mh mh” mkewe aliguna kishambenga” Umesikia we mwanamke nikirudi sitaki kukukuta humu ndani kuanzia muda huu kusanya kila kilicho chako halafu upotee, kwanza una bahati ya kuishi na mimi miezi yote hii “Aliongea Mr. Enock kwa jazba zaidi.
“Nisamehe ..”
“Hakuna ndo nimeshasema” Mr. Enock alisema na kufunga mlango kwa nguvu. Baada ya hapo aliingia ndani ya Lexas na kutia moto gari na kutoweka.
Lone alimsindikiza Christer hadi shuleni huku akilalama alivyomfanyia haikuwa fair. Walimshusha Christer kwa miadi ya kuonana tena wiki mbili mbeleni na wao wakageuza kurudi mjini. Ukweli ni kwamba kilichomfanya Christer aghaili safari ya kwenda Bahiroad ni kwamba alihisi dhamira yake ikimsuta kwamba alikuwa bado akimpenda Bryan kuliko Lone hiyo ndiyo sababu iliyomfanya aghaili.
Lone alipofika nyumbani kwao alihisi macho yake yakimuwasha na kutoa machozi pengine ni kwa ajili ya hali ya hewa ya vumbi la Dodoma lakini hakuwa na uhakika zaidi.
“We Lone” shangazi yake aliita. “Naam shangazi” Lone aliitika.
“Huko ndani unafanya nini sasa hivi?
“Nimelala” “Kisa?”
“Macho yananiuma shangazi”
“He mara hii, itakuwa vumbi la Dodoma kesho uende Mvumi ukapime yasije yakawa matatizo makubwa”
Sawa shangazi”
Asubuhi yake alimsindikiza Lone mpaka stendi ya mabasi ya Mvumi. Walipofika shangazi alimkabidhi kiasi cha fedha kwa ajili ya matibabu na chakula na baada ya hapo waliagana na kila mtu akatawanyika.
Lone alipofika hospital ya Mvumi alipata matibabu na kuandikiwa baadhi ya dawa. Macho yake aliambiwa hayahitaji miwani kwani matatizo hayakuwa makubwa sana. Lone aliwashukuru wahudumu wa pale na kuanza kuondoka. Alipofika kwenye lango la kutokea nje akakutana na binti mmoja aliyekuwa kavaa sare za kiuguzi. Lone hakuelewa kama yule binti ni Nesi kamili au mwanafunzi tu. Lone alipomuangalia usoni alikili ustadi wa Mungu. Kipindi chote hicho Lone alipokuwa akimtathmini mwanadada huyo yeye alikuwa akija upande wa Lone huku kichwa chake kimelazwa shingoni upande na macho yakiangalia chini.
Walipokaribiana huku dada huyo hajajua aliyeko mbele yake, Lone akajikuta akimshika mkono kwa vile walipishana kwa karibu mno.
“Hello mrembo mambo” Lone maneno yalimtoka. Mercy aliinua macho yake kumtazama aliyekuwa akimsalimu.
“Waoooow Brya;. “Aliyesema hivyo si mwingine bali ni Mercy na kisha kwa ghafla akasita na kumuangalia Lone kimkazo zaidi. Hakuna aliyeongea neno zaidi ya kumtazama tu, na mara baada ya nukta kadhaa Lone akavunja ukimya.
“Hallo baby naomba dakika chache tu nizungumze nawe kama hutojali” Lone alimwambia Mercy huku mikono yake akiwa ameikusanya pamoja hiyo ilimaanisha kumplease Mercy.
Mercy alishusha pumzi ndefu badala ya kujibu na hakujibu kitu zaidi ya kutingisha kichwa kuashiria kukubali ombi la Lone na kwa pamoja walibadili mwelekeo sehemu moja.
Walielekea sehemu moja iliyotulia yenye majani ya kijani kibichi pamoja na baadhi ya maua pamoja na miti mingi ya kivuli palivutia sana.
Walitulia chini ya mti mmoja wa kivuli wakiwa wamekaa ilihali kila mmoja kumface mwenzie Lone alianza kwa kusema.
“Naomba nikufahamu jina lako”
“Naitwa Mercy” Alijibu kwa kifupi”
“Nashukuru kukufahamu U-binti na jina lako ni zuri pia.
“Asante” Alijibu kifupi pasipo mazungumzo ya nyongeza.
“Naitwa Lone japokuwa hupendi kufahamu jina langu”
“Asante” Mercy alijibu.
Kiukweli Mercy alikuwa katika dimbwi la mawazo akimtafakari Lone. Alikuwa akijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu iweje Lone afanane na Bryan kiasi kile?
Pia Lone alishtuka pale Mercy alipotaka kulitaja jina lake kama Bryan japokuwa hakutaka kuonyesha mshtuko wake dhahiri.
Aliwaza huenda huyo Bryan ni mtu maarufu sana japokuwas hakufahamu huo umaarufu wake unatokana na nini. Huenda ni kicheche sana au anafedha zaidi au ni handsome kuliko, lakini potelea mbali mi hayanihusu sana.
Hayo yote Lone aliyawaza
Kwa pamoja wote wakarudi katika mood sawa. “Lone” Aliita Mercy kwa sauti ya upole.
“Naam Mercy”
“Bryan huwa mnawasiliana naye” Mercy aliuliza akiwa na uhakika Lone anafahamiana na Bryan.
“Bryan ndio nani?”Lone aliuliza. “Kwani wewe unaitwa Lone nani?”
“Mi naitwa Lone Enock Mwansasu” “Na ;mi namuulizia Bryan Enock Mwansasu”
“He mi mbona sifahamu kama nina ndugu wa namna hiyo hebu naomba unipe historia yake angalau kwa ufupi”. Mercy akamueleza kila kitu isipokuwa juu ya uhusiano wao. Na Lone akafanya vivyo hivyo kamueleza Mercy juu ya historia yake.
Kila mmoja alisikitishwa na stori ya mwenzake na kila mmoja alimpa pole mwenzake. Kwa sasa Lone alikuwa akifahamu Bryan ni nani japokuwa hakuwa akimjua lakini alitamani siku moja akutane nae na hilo aliamini itakuja tokea.
“Kwa hiyo wewe na Bryan nani senior na nani junior?”Mercy aliuliza.
“Mimi itakuwa ndiye senior” Alijibu Lone.
Kwa kila jicho la Mercy lililomtazama Lone hakika halikuona tofauti na Bryan.
“Samahani Mercy pamoja na hayo yote tulio yaongea bado kunakitu kinaitatiza akili yangu” Lone alizidi kuongea.
“Mercy” Lone aliita.
“Nakusikiza endelea” alijibu Mercy.
“Kiukweli ni kwa” Lone alishindwa kuendelea.
Kilichomfanya ashindwe kuendelea ni yale macho alokuwa akitazamwa na Mercy kwa muda wote Lone alokuwa akiongea Mercy alikuwa akimtazama yeye (Lone) Usoni pasipo kukopeza kope za macho yake.
Kwa hali hiyo alimfanya Lone aone aibu na kujidharau kwa kiasi Fulani huenda hayuko timilifu hajamfikia hadhi yake. Lakini kama mwanaume alijipa moyo naye ajaribu bahati yake. “Lone” Mercy aliita. Lone alijibu.
“Mbona kimya” Aliuliza Mercy.
“Nilikuwa bado natafuta maana ya hilo jicho nitazamwalo nalo” Lone alijibu.
“Usijali endelea mi nakuskiza”
“Mercy naomba unielewe kwa nitakayoyasema naomba usijibu kitu mpaka nitakapokwambia naomba unijibu” Lone alisema na Mercy alijibu kwa kutingisha kichwa.
“Kiukweli ni kwamba nikiweka hadharani kile kilichofichama ndani ya moyo wangu kwanza naomba uangalie mawingu”.
Mercy aliinua kichwa chake na kutazama angani na kisha Lone akanyoosha mikono yake mbele kuashiria na Mercy ampe na mikono yake. Na Mercy alifanya hivyo pasipo ubishi. Hata yeye Mercy mwenyewe alijishangaa huo udhaifu wa kutenda kila aombwacho atende aliutoa wapi? Kwani tangu Bryan aondoke hakuwahi kuwaza kwamba atatokea mtu atakeye mfanya moyo wake uwe na impession naye zaidi ya Bryan.
Lone aliongea.
“The sky is blue, my love is true between me and you. Just belive me baby siyo kwamba naanzisha mimi kukupenda wewe, yalianza zamani sana toka Adamu na Hawa, toka enzi za mababu zetu na hata Ngoswe na Mazoea. Mercy ninavyokupenda huenda ikawa ni zaidi ya Romeo kwa Julieth naomba usadiki haya nikwambiayo” Aliongea Lone kwa hisia za mapenzi zaidi na huku kila neno alitamkalo likiishia na pumnzi zito.
Mercy pasip kutarajia akajikuta akimkumbatia Lone kwa nguvu na kumkiss kama mara tatu hivi non-stop.
“Naomba unijibu kwa maneno, Mercy” Lone aliongea.
Mercy alikaa kimya takriban dakika mbili hivi akionekana kama anakummbuka mambo Fulani yaliyopita .”Lone naomba unipe muda nifikirie nitakujibu kesho kutwa nikija Dodoma mjini”Mercy alimuomba Lone .
Lone alikubali japo kwa shingo upande .
Waliachana kwa miadi ya kukutana kesho kutwa ,Lone alipata lift ya taxi na kurudi na Mercy akaendelea na shughuli zake.
Christer siku hiyo alikuwa ametoka kwenda shopping mjini.
Alipokuwa katika mizunguko yake ya hapa na pale mara ghafla gari ikafunga breki miguuni mwake na alipogeuka kuangalia kilichokuwa kikiendelea .Sura yake ilikutana na sura mzee mmoja wa makamo .”Binti hujambo? “Ni Mr Enock kwa sauti nzito na yenye kukwaruza .”Naomba jumapili tuonane NAM hotel nina mazungumzo kidogo umesikia binti?”
“Hapana siwezi , sitokuwa na na “
Wakati Christer akijing’atang’ata kuongea hayo, Mr Enock alichomoa kitita cha shilingi elfu hamsini na kumkabidhi..Christer alijiuliza apokee au asipokee,lakini aliona ni bora apokee kwani bahati kama hizo ni adimu sana .
“Hivi unaitwa nani mrembo?”
“Christer “
Mr Enock alichukua vidole vyake viwili na kuvielekeza mdomoni mwake na kumuonyesha tena Christer na kisha akamwambia afike saa 11 jioni bila kukosa .Mr Enock aliondoka kuelekea Bahi road kwa dada yake .Alipofika alibisha hodi, mlango ulifunguliwa na dada yake .Walisalimiana na dada yake kwa furaha kisha Mr Enock akaeleza kilichomleta.
Mda huo wote Lone alikuwa kesharudi ,aliposikia sauit ya baba yake alipita mlango wa nyuma na kuondoka na kwenda kwa rafiki zake aliapa hatarudi mpaka baba yake aondoke. Baba Lone aliagiza aitiwe Lone,Lone hakuwepo chumbani hivyo alisema atamsubiri mpaka arudi.
Ilikuwa ni jumapili Mercy aliporudi kwao kwa ajili ya likizo.
Alipofika tu sebuleni alimkuta Bryan katulia juu ya sofa yuko ndani ya suti ya cream ndani alivalia shati jeupe.
Baada ya Mercy tu kutokeza wote walipigwa butwaa na kufikisha macho ili yawape ukweli zaidi Baada ya kila mmoja kuamini kile alichokuwa akikiona alisema.” Waaaoow!” Na kila mtu akimkumbatia mwenzie kwa nguvu akiyashirikisha machozi ya furaha .
“Kwanza umependeza “Bryan alimwambia Mercy aliyekuwa kavaa sketi ndefu nyeusi iliyomtight vema pamoja na blauzi nyeupe.
“Sikushindi Bryan” alijibu Mercy.
“Enhe mbona ghafla hivi”Mercy aliuliza huku akitabasamu.
“Si surprise nilitaka nije nikufumanie”
Wote wakacheka na kisha Mercy akaenda kuwasalimu wazazi wake waliokuwa bustanini na kisha akamrudia Bryan .Ama kwa hakika ilikuwa furaha isiyokifani ni hadithi na vicheko vilivyotawala .Jioni ya siku hiyo Bryan na Mercy walipanga kwenda kula chakula NAM hotel na kwa kweli wakaanza kujiandaa mtoko wa jioni hiyo.
“Ni siku ya pili sasa tangu Lone aondoke tangu juzi hajaonekana “””Ah shauri zake bwana mimi jumatatu naondoka zangu Dar ila akija mwambie namhitaji arudi Dar tuje tuyamalize”Aliongea Mr Enock .
“sawa kaka”Alijibu shangazi yake Lone .
Muda huo ilikuwa ni saa kumi ,Lone alikuwa kwa marafiki zake akiongea na simu na Christer .Kwa hiyo njoo hapa stendi ya taxi halafu nitakwambia ninapotaka nikupeleke leo “Lone aliongea.
“Sawa”Upande wa pili ulijibu.
Muda si muda Christer alifika na kumkumbatia Lone na kumkiss “Vipi dear mzima wewe? Lone aliuliza.
“Wa afya hofu zaidi juu yako”
“Namshukuru mungu sijambo” Alijibu Lone wote wakaingia ndani ya taxi na kisha Lone akamwambia dereva awafikishe Nam hotel. Christer alishtuka kiaina ila akajikaza lakini wasiwasi ulimjaa mwili mzima ukijua leo ameunguza picha mpaka nega.
Safari ilianza taratibu kuelekea huko huko Nam hotel.
Kwa upande wa Mr Enock nako, “Dada mi sasa hivi, ntarudi usiku” Mr Enock alimuaga dada yake.
“Kaka na wewe bado hujatuliaga tu sasa wapi tena, usije ukagonganisha na wakwe zako huko,” Aliongea shangazi yake Lone.
“Ah nshakuzoea na maneno yako” alitoka na kuingia garini moja kwa moja mpaka Nam hotel.
Bryan na Mercy walikuwa wamefika Nam hotel walikuwa sehemu moja hivi tulivu mno na tayari walikuwa wameshaanza kujichana huku stori zikiendelea.
Punde si punde Lone na Christer waliingia huku wameshikana mikono waliingia na kuelekea sehemu ile ile waliokuwako Bryan na Mercy. Hakuna aliyekuwa amemuona mwenzake hii ilitokana na kila mtu kufall kwa mwenzake.
Christer na Lone walichizika zaidi kiasi kwamba Lone akapamia meza ya akina Bryan na Mercy hapo ndipo kila mtu alizinduka kana kwamba walikuwa wamelala fofofo.
Lone kutazama anamuona Mercy yuko na mtu.
Bryan kutazama anamuona Christer yuko na mtu.
Kwa upande wa wale wasichana walitazamana kwa macho makali sana. Kisha Mercy “Hallo Lone mpenzi wangu hapa anaitwa Bryan” Huku akimkiss Bryan.
Kisha naye Lone akamtambulisha yule dada na kwamba ndiye mahabuba wake. Alionge huku akimkiss shavu.
Bryan na Christer walitazamana kwa shauku pasipo kusema neno kisha wakakonyezana.
Wakati wakiwa katika hali hiyo Mr Enock aliingia na kisha kupigwa na butwaa.
“Ha Christer?” Alishangaa Mr Enock.
“He, baba yangu” Aliduwaa Bryan.
Mr Enock alishangaa kusikia mtu akimuita baba ilihali pale hana mtoto zaidi ya Lone.
Kumuangalia usoni ni Lone vilevile. Mr Enock alikaa chini ili apewe full story.
Kwa upande wa Lone na Bryan walipotazamana kwa makini ilikuwa ni kama vile kila mmoja akijiangalia kwenye kioo kwani walifanana kupita kiasi.
Baada ya kila mmoja kupata full stori kutoka kwa mwenzake. Mr Enock alimaliza kwa kumtambulisha Bryan kama mdogo wake Lone.
Baada ya hapo Mr Enock aliomba afahamiane na upande wa wazazi wa Mercy na ikawa hivyo.
Sekunde ziliyoyoma, dakika zikakatika, saa zikasogea, siku zikaenda, umri ukaongezeka na mwisho kabisa Bryan alifunga ndoa na Mercy na Lone na Christer.
Miezi kadhaa baada ya ndoa yao Lone na Christer wakiwa katika nyumba yao yenye kila hitaji Lone alimkumbushia Christer siku ile hotelini.
“Oyaaaa mamaa” Lone aliita.
“Sema babaa”
“Unakumbuka ulivyotaka kutupanga na mdingi siku ile hotelini?”
“Ah, mkwe naye mapepe hajatulia hata kidogo” Christer aliongea na kisha wote wakacheka, na maisha yakaendelea.
Huku nako kwa akina Bryan na Mercy wakiwa wameyapatia maisha vilivyo nao walikuwa wanataniana.
“Unasikia dear?” Aliongea Mercy.
“Nakusikiliza laazizi” Alijibu Bryan.
“Nisingekomaa sasa hivi shemeji yako ndiye angekuwa analalia kitanda chako saa hizi.”Aliongea Mercy huku akicheka.
“Duh, hata sielewi kipi kilichonichizisha kwa shem, ilhali mtoto mrembo kama wewe unang’aa kama hii silver yangu ulikuwepo”
Wote wakacheka na kugonga na maisha yakaendelea kuwa matamu.
MWISHO.
Also, read other stories from SIMULIZI;