Ninah Sehemu ya Nne
CHOMBEZO

Ep 04: Ninah

SIMULIZI Ninah
Ninah Sehemu ya Nne

IMEANDIKWA NA: CHANDE ABDALLAH 

********************************************************************************

Chombezo: Ninah

Sehemu ya Tatu (3)

Nilijipigilia pombe za kutosha na nikalia kwa sauti hadi kila mmoja pale ndani akageuka na kunitazama mimi, bahati nzuri Mr Edgar aliniwahi akanikokota hadi kwenye gari tukaondoka.

Bado nilikuwa na kidonda rohoni, lakini yule mzee acha kabisa, maana alinibembeleza na kuniahidi kunitunza na kunifanyia mambo makubwa mno kwa ajili yangu.

Basi kwa hasira nikamruhusu Mr Edgar kununua hizo jinsia za bandia za kuvaa ilimradi awe ananitoa kiu yeye tu na si mtu mwingine. Mwenyew e alifurahi kusikia hivyo tena akawa tayari kunioa kabisa.

Na mimi kwa hasira siku hiyohiyo aliyonitamkia sikutaka kufikiria mara mbili nikamwambia anioe tu, sitajali.

Basi tukaanza rasmi ukurasa wa mapenzi kati yangu na Mr Edgar, nikamruhusu aniguse sehemu zote kwenye mwili wangu na kunifanya anachotaka. Alifurahi na taratibu nikaanza kumzoea na kujikuta nampenda hivyohivyo, tena nikajua mengi mazuri ya mzee huyu.

Muda wa takribani miezi miwili ilipita, tena wakati huo ndiyo tulikuwa tukipanga mikakati ya ndoa yetu kuanzia kujitambulisha kwa baba na taratibu nyingine za kidini, lakini furaha hiyo iliyeyuka ghafla siku moja niliyomuona mtu kama Brighton akiniomba urafiki Instagram.

Kwanza nilijua siyo yeye, lakini nilivyotazama vizuri nilishtuka nikaanza kupapatika, loh alibadilika mno, huko Sauzi Afrika ndiyo kumemfanya hivyo au? Nikaingia kutazama picha yake moja baada ya nyingine. loh alikuwa amewaka na kupendeza.

Nafsi ikanivuta na kukumbuka mazuri yote tuliyofanya pamoja, nikajitahidi kukumbuka mabaya aliyonifanyia ili mradi nimpotezee lakini hakuna hata baya moja lililokuja kichwani. Moyo ukaanza kutaka kuponza kichwa.

NINAH 35

Niliendelea kutazama picha zake moja hadi nyingine, mwili wangu ukasisimka nilipoona picha moja ambayo amepiga akiwa na msichana mmoja hivi chini akisindikiza na neno Bae.

Iliniuma mno, nilijua ni uchoyo wa hisia kutaka awe wangu wakati nilishafanya uamuzi, lakini moyo wangu ulikuwa unataka kufanya kitu na si kumuacha Brighton hivihivi.

Basi nikajikuta namuwazia huko alipo na yote anayoyafanya kwa huyo mwanamke wake nikawa mnyonge mpole na mwenye mawazo.

Jioni Mr Edgar aliporudi akiwa na zawadi za kila aina, aligundua huzuni yangu ambayo kila nilipojaribu kuificha haikufichika.

“vipi malkia wangu, nini tatizo?” aliniuliza Mr Edgar.

“hamna tatizo, nilikuwa na uchovu sana leo,” nilijibu kwa kuzuga.

Usiku basi kama kawaida,nililala na Mr Edgar aliyenichezeachezea lakini nikaona karaha mawazo yangu yakiwa mbali mno kiasi kwamba hata alivyovaa hilo dudu lake la raba na kuniingiza nalo akijiliza kimahaba kunipa mshawasha, nilichukia mno na kukinai ghafla.

Nikamisi ngozi kwa ngozi, nikammisi Brighton. hapana nilimkumbuka sana na Brighton siwezi kumuachia mwanamke mwingine na mimi nikaendelea kuganda na hili zee.

Nilisema nikijuta hata uamuzi wangu wa kumtega Brighton na hela baada ya kujua fika kuwa nilitakiwa kuomba msamaha na kujielezea kwanini nilikuwa karibu na bosi wake hadi picha kusambaa mitandaoni.

Ndiyo siwalaumu mapaparazi, simlaumu Mr Edgar, bali naulaumu uzuri wangu hadi picha za watu wote zikaachwa na kuchukuliwa yangu kama kielelezo cha habari zao mpaka Brighton akaona.

Nilijikuta nikiogopa ule usemi kuwa wanawake wazuri ndiyo hawajielewi duniani, sikutaka usemi huo utimie kwangu. Nifanye nini?niliwaza wakati Mr Edgar akijitahidi kuniridhisha, nikadanganya kama nimejojoa na yeye akajitoa na kujinyoosha kiuno chake maana nilimpa kazi kwelikweli na hata hakusema kama anaumia.

Nikawaza, hapana siwezi; ngoja nimuanze Brighton maana kama niliharibu bado muda upo, naweza kurekebisha makosa yangu isije ndoa halafu ndiyo nikawa siwezi kurudi nyuma tena.

Wakati Mr Edgar amelala, nikawasha simu yangu nikapunguza mwanga na kuingia tena Instagram nikatuma meseji direct kwa Brighton nikiandika; “Hi!”

NINAH 36

Basi usiku huo kila saa niliangalia simu yangu kuona kama kanijibu lakini ilikuwa hola.

Kesho yake Mr Edgar aliamka asubuhi kama kawaida na kuondoka zake kazini tena alihisi sipo vizuri kabisa hivyo akanitaka kwenda hospitali pengine nikapime kama nina tatizo nikaitikia tu kwa kichwa.

Alipoondoka nikaanza kujizungusha mle hotelini, mawazo juu ya mawazo. Kichwani wakanijia watu maaarufu kadhaa ambao wameolewa na wazee watu wazima. Nikamkumbuka Jackline Mtuyabaliwe, nikajiweka mimi kwenye nafasi yake. Hapana angalau mzee Mengi ana nguvu zake na amemzalisha watoto, je mimi na Mr Edgar hata ndoto yakuwa na watoto kweli itakuja kutimia hata siku moja kweli?

Hapo ndiyo nikakumbuka usemi niliojifunza Tandale ambao watoto wakike huutumia kwa wanaume watu wazima wanaowataka.

“Ujana wako uutumie wapi, uzee uje kula na mie.” Niliona kabisa hayo maneno yananihusu.

Nilijiuliza na kuona katika mapenzi yetu mimi ndiyo ninamfaidisha tu Mr Edgar kwa kuwa ananifaidi mimi na mimi simfaidi yeye kwa kuwa tu nina mtu ninayempenda kwa dhati ambaye ni Brighton.

Nikawaza na kuwazua, wakati huo nikaingia tena Insta nakuona kuna kiujumbe nikafungua na kutazama alikuwa ni Brighton kweli amejibu tu kwa kifupi; Hi.

Nikafurahi kama nini, palepale nikaaandika ujumbe haraka; “nakuonaaa!”

“hahaa!” alijibu hivyo tu.

Nikamuandikia tena; “unaonekana una furaha.”

“Yah, im good,” alijibu.

Nikashindwa niandike nini, nikaandika miss u, nikafuta kwa sababu niliona kama najipendekeza vile.

Lakini wakati naandikaandika hivyo na kufuta nikaona kialama cha typing.. maana yake anaandika nikatulia.

Meseji ikaingia; “vipi mzee anaendeleaje?”

Swali hilo lilinichefua mno nikashindwa kujibu nikatoka na Instagram kabisa.

Nikajisikia aibu, hasa nikikumbuka Brighton mara kwa mara alikuwa akimuitaga ‘mzee’ baba yangu mzazi, sasa kwa kumuita Mr Edgar mzee yaani nikajisikia kama vile natembea na baba yangu mzazi kwa kweli.

Maana ngozi ilimshuka, mvi zilimjaa, kila asubuhi aliamka na kutazama mikunjo mipya kwenye uso wake. Tena alifikia kipindi akiamka asubuhi anajinyoosha kwa dakika kumi nzima akivunja viungo vyake vilivyochoka. Ama kweli nilikuwa nakaa na mzee; nikajichukia.

Itaendelea.

NINAH 37

Ikabidi nichukue simu mwenyewe na kuwasha tena nikaingia insta na kuona siwezi kuvumilia tu bora nimwambie ukweli Brighton.

Nikaandika: “Brighton, I miss u, I love u nilifanya kosa naomba nisaidie nijisahihishe.” Nilipomaliza nilifumba macho nikiomba Mungu Brighton anijibu jibu zuri.

“hahaa, unanitania si ndio!” alijibu Brighton. akaninyong’onyesha.

“Siyo utani Brighton, hujui tu! Tafadhali naomba namba yako,” niliandika tena wakati huo nikawa naelekea kule chumbani kwangu.

Nikataka kuongea na Brighton nikiwa nimelala kitandani, ili sauti yake iniingie vilivyo kila kona ya mwili wangu nikimkumbuka alivyokuwa akinipapasa na kunifanya alivyokuwa akinifanya.

“Baada ya muda mfupi, alinitumia namba yake ya whatsapp yenye code za Sauzi. Sikulaza damu palepale nikampigia kwa video call.

Nikamuona nadhani alikuwa gym, tena alikuwa ametengenezeka mwili wake hadi raha. “Hallow, Ninah!” alisema, na kunitazama kwa furaha.

Na mimi nikamtazama kwa wivu na matamanio; “Brighton, umebadilika jamani!” nilisema.

“Aah hamna mbona kawaida tu! Niambie?” alisema akijifanya hajali nilivyomsifia.

“aah Brighton kama nilivyokwambia, nimekumiss kweli, nisaidie mwenzio najua nimekosea, tafadhali turudiane!” nilijibaraguza.

“Ninah hapana, lakini wewe si mke mtarajiwa wa mzee au?” alisema akizidi kunichefua na hilo neno mzee.

“Brai, sijapenda ujue, halafu yote ni kwa sababu yako, wewe hujui tu!”

“Sababu yangu kivipi? Nilikuwa masikini ndiyo maana ukatembea na bosi wangu upate hela au? Kama ni hivyo nisamehe na it’s over mbona mimi nipo vizuri tu, hapa cha msingi tuongee tu kama washkaji. Mimi nina mpenzi wangu huku na tunatarajia kuoana mwezi wa kumi na mbili,” alisema Brighton, moyo ukanitikisika nikiwa siamini kabisa.

“yaani Brighton umenisahau haraka hivyo?” nilisema na kilio na kubembeleza juu.

“Yah ilibidi nitafute mtu wa kunisahaulisha kuhusu wewe, ambaye angalau naendana naye, wewe sio levo zangu. Na nimeweza kukusahau kabisa yaani, kwa sababu kipindi kile nilikuchukia mno,”

NINAH 38

“Brighton, mbona mimi nilikusamehe mengi baby wangu, tena hadi nilikufumania, nikakubali kuishi na wewe kwenye hali ya kimasikini, leo mimi kuwa na Mr Edgar tu tena kwa ajili yetu, ndio ufikie hatua ya kukubali kuchukua shilingi milioni 50 na uniache! Kweli Brighton? haukunitendea haki,” nililalamika.

“Nilikuwa mjinga kukataa hela za baba ako mwanzoni aliponitaka niachane na wewe, unajua alitoa ofa ya shilingi ngapi? Kifupi hela za Mr Edgar hazifikii hata nusu yake. Nilikataa kwa ajili yako, usinilaumu tu; jua na mimi nilijitoa kwenye uhusiano wetu, wewe ndiyo uliyeharibu tena ukiwa na akili zako timamu. Eti nikusamehe hapana haitatokea,” alisema Brighton na kuzidi kunichanganya. Nikashtuka ina maana baba alimfuataga Brighton na kumtaka aniache! Jamani alikataa kwa ajili yangu.

Ila sasa alichukua kwa sababu aliona nimemsaliti waziwazi.

“Jamani Brighton, nisamehe.”

“Siyo rahisi tuwe tu marafiki, by the way nilikufollow ili nikutakie ndoa njema maana taarifa za bosi wetu kutarajia kukuchumbia wiki hii, zimefika hadi huku ofisini, kuna wenzetu watakuja lakini mimi sitakuja nisamehe kwa hilo, si unajua tena sitaki wafanyakazi wenzangu wa zamani niliowatambulisha wewe kama mke wangu leo hii waone nashuhudia nikipinduliwa ok bye, Ninah.”

“Jamani Brai usikate!” nilisema lakini Brighton alishakata, nikaanza kulia na kulia hadi basi.

Kwa hiyo Brighton ndiyo siwezi kumpata tena, au ameogopa kwa sababu amesikia nataka kuoelewa na Mr Edgar? Nikatae harusi nini? na kama nikikataa harusi je, Brighton yeye atamkataa mchumba wake huyo aliyenaye huko kweli?

Niliona sina pakutokea; nikatamani kumwambia siri ya Mr Edgar kuwa hawezi kuniingilia huenda itampoza asinichukie, lakini nadhani itakuwa ni aibu zaidi kumwambia kuwa ananiingizaga raba la dildo huku chini. Loh nimejishusha na kujidhalilisha vya kutosha kisa hela au?

Hapana, nifanyaje sasa. Wakati mzee wa watu, ameshatangaza hadi huko Sauzi kuwa anataka kunioa.

Nilianza kufikia mwisho wa kufikiri, lakini yote haya kisa kilikuwa wazi kuwa ni shetani wa mkufu. Nimemkosea Brighton nakiri, nifanyeje mwenzenu?

NINAH 39

Basi nikatafuta cha kuwaza na akili yangu ya mwisho ikanituma nimwambie ukweli Mr Edgar, kuwa kwa muda wote tulioishi nilidhania kama nimempenda kumbe bado moyo wangu ulikuwa kwa Brighton.

Lakini nilipowaza hivyo, nikawa namuonea huruma Mr Edgar, nilijua hiyo huruma itaniponza, lakini nifanyeje? sasa muda ukawa unakimbia upande wangu na ishu ya uchumba ilikuwa imekolea maana siku chache zijazo tulipaswa kwenda kwa baba yangu.

Nikaona njia sahihi ni kumfanyia vituko vidogovidogo ili mradi basi Mr Edgar aelewe kama simpendi ili apunguze kasi maana ilikuwa too much.

Aliporudi kwa mfano usiku ule nikamuweka wazi kuwa baba yangu na mimi tumegombana, hivyo itakuwa ngumu kwenda kwake.

“Ninah, usijali hakuna linaloshindikana, nitatangulia kuongea naye najua tu kama mzazi lazima atakusamehe tu, usiwe na wasiwasi,” alisema Mr Edgar akinikata pointi yangu.

“Mh halafu, nilitaka kwenda nje ya nchi kidogo nikashangaeshangae kabla ya kutambulishana,” niliweka kigingi kingine.

“ooh usijali lakini kweli kukaa hapa hotelini kunachosha inabidi niandae safari ya siku tatu, sema unataka twende wapi?”

“Hapana Mr Edgar, nataka kwenda peke yangu,” nilisema mzee wa watu akashtuka mikunjo ikamjaa usoni.

“Okey, sema unataka kwenda nchi gani?” alisema Mr Edgar.

Nilikaa kimya.

Kifupi nilitaka kwenda Sauz Afrika lengo langu nikifika tu Sauz nashuka na kumtafuta Brighton kwa udi na uvumba tena ndani ya siku hizo tatu nilikuwa na uhakika kuwa nitampata na pengine akiniona hivi uso kwa uso asingeweza kuchomoka maana huyo msichana wake, naona hafui dafu kwangu hata kidogo, halafu nilijipa moyo kuwa Brighton bado ananipenda maana kama hanipendi kwanini alikataa kuja Tanzania kwenye hiyo Engagement yangu, kama si kuumia roho huko.

Wakati huo Mr Edgar alinitazama na kusema huku anatetemeka: “Ninah hii yote ni kwa ajili ya Brighton si ndiyo?”

“aah hapana! Kwanini unasema hivyo?” nilisema nikifanya nakana.

“Usinidanganye, mmekuwa mkiwasiliana!” alikoroma Mr Edgar huku macho yakimuiva mno, alinitisha kwa kweli kwa sababu sikuwahi kumuona akiwa katika hali hiyo hata siku moja.

NINAH 40

Wakati najing’atajing’ata akafungua kudude fulani hivi ambacho siku zote kilikuwepo pale mezani na kukibonyeza, Mungu wangu huwezi amini eti nilisikia sauti yangu ikimbembeleza Brighton; ina maana Mr Edgar aliniwekea mtambo wa kurekodi humo ndani!

“Samahani ni wivu wangu tu, niliiweka hii rekoda ambayo inajiwasha na kurekodi sauti yoyote itakayotokea humu ndani, kwanini Ninah ukaniaminisha tutaoana na kuishi pamoja, lakini kumbe hinipendi! Sikulaumu kwa kutonipenda, lakini kwanini unipe moyo?” alilalamika Mr Edgar lakini sasa kwa sauti ya upole halafu akawa anatiririkwa jasho kweli pumzi zikamkata mbele yangu akadondoka chini kama mzigo.

Aisee nilichanganyikiwa nikapiga simu haraka reception kuomba msaada, tuliondoka na gari hadi hospitalini. Wakati huo nikijilaumu kama chochote kitamkuta Mr Edgar basi ni sababu yangu tu.

Moja kwa moja, Mr Edgar akiwa kwenye kitanda cha magurudumu aliingizwa kwenye chumba cha wagonjwa wa emejensi na kuanza kufanyiwa huduma ya kwanza, nilitoa maelezo yote mapokezi na kusubiri.

“Wewe ni mwanaye?” aliniuliza Dokta baada ya kutoka mle ndani.

“hapana mchumba wake,” nilijibu nikiwa na hofu ya atakachokisema.

“Aah mzee amepata stroke, amepooza upande mmoja wa mwili wake, pengine kuna ndugu yake yoyote tunaweza kuwasiliana naye zaidi yako?” aliuliza yule Dokta, masikini sikuwa hata namjua ndugu yake hata mmoja. Nilichofanya ni kumpigia simu Brighton haraka na kumwambia kilichotokea, nikamtaka awataarifu kazini kwao huko Sauz na kunisaidia kutafuta ndugu zake, huwezi amini alifanya kwa moyo mmoja na baada ya masaa machache, nikaongea na mdogo wake, Mr Edgar, Tsoza aliyesema angefika kesho usiku kwa ndege.

Nilichanganyikiwa na kuhitaji kutiwa moyo. Nikiwa sina rafiki yoyote zaidi ya Mama Sele nilimpigia na alifika haraka na kuambatana na mimi usiku mzima, Tukaenda kule hotelini na kulala kisha tukarudi hospitali asubuhi.

Mwenzangu akishangaa kila kitu kuhusu mimi na kuwa na maswali mengi mno lakini sikumwambia chochote zaidi ya kumuahidi nitaongea naye mambo yakitulia. Ooh mkufu!

Sasa nikawa katikati maana nilitaka kumuacha Mr Edgar lakini majanga yametokea, mwenzangu amefikia hatua ya kupooza kwa ajili yangu, kwa hiyo siwezi kumtelekeza kwa chochote maana nikimuacha tu dunia nzima itajua nimemuacha kisa amepooza na eti nilikuwa naye kwa ajili tu ya starehe na mali zake; nitakuwa mfano mbaya kwa wanawake wote duniani.

Nilijua lazima nilitakiwa kuwa karibu naye sasa zaidi kuliko kipindi kingine chochote, hata kwa kuigiza lakini nisimuache, akya Mungu niliona kabisa nazidi kumkosa Brighton na matumaini ya kuwa naye yalipotea kabisa. Kwa kifupi nisahau kuhusu Brighton.

Nililia mno usiku ule na Mama Sele akawa ananibembeleza akiwa haelewi chochote. Hakika nimekamatwa nisipopapenda.

Sasa nikatambua kwanini tunaitwa wanawake, tunatakiwa kujitoa zaidi na si kushindana na mwanaume, eti kwa kuwa Brighton alichepuka na mimi nichepuke halafu nione nimelipiza, kumbe mtazamo wake unakuwa tofauti mno, nakubali nilifanya dhambi na sasa nitailipia kwa kubakia na Mr Edgar.

Basi asubuhi nilienda kumuona Mr Edgar hospitali, wakati huo baadhi ya wafanyakazi wenzake walifika na kushughulika na mambo ya gharama na taratibu nyingine. Wengi wao walikuwa wakitaka kuonana na mimi ili kujua kilichotokea.

Nilisimulia kwa kurudiarudia kila saa maana kila dakika alikuja mtu fulani, kisha akaja mtu fulani na wote hao mimi ndiyo niliongea nao, wengi niligundua hawakunishangaa kuniona laivu, pengine Mr Edgar aliweka picha yangu ofisini kwake na kuining’iniza akiandika kabisa bango: “HUYU NDIYE MPENZI WANGU JAMANI ONENI”

Sikuwa na kumbukumbu nzuri ya sura za watu, lakini nilipomuona Imelda yule mfanyakazi rafiki yake na Brighton, nilificha uso wangu kwa aibu, nilichelewa alinifuata haraka na kunipa pole.

Niliitikia kwa soni, maana nilijua tayari alifahamu histori yangu nzima kuwa nilikuwa mke wa Brighton na sasa nimempindua kwa bosi wake.

Nitafanyaje, sikuwa na cha kufanya maana shetani aliniandama na ameniumbua kwa kweli.

Nakumbuka usiku huo ndiyo ndugu yake Mr Edgar alitua na moja kwa moja akafika hapo hospitali. Nilishangaa akiwa ni kijana mdogo halafu hendsamu boy wa maana.

NINAH 42

Akaniuliza nikamhadithia jinsi tulivyogombana mambo ya kawaida tu na Mr Edgar na kufikia akadondoka ghafla mbele yangu. hakuonekana kushangaa sana kuhusu hayo maongezi badala yake niliona akionekana kunishangaa mimi.

“Aah kwa hiyo wewe ndiye beautiful Ninah ambaye kaka yangu amechanganyikiwa kwajili yako?” alisema akanishangaza.

“Naitwa Ninah!” nilijibu maana nilijishtukia tulianza tu kuongea wakati hata jina sikumtajia.

“Yah kweli ni mzuri, na kaka yangu ana haki ya kudondoka kwa presha kwa ajili yako, hii ni brazilian?” alisema Tsoza akinizunguka na kunitazama nywele zangu akizishika kabisa.

“Tsoza, samahani, nilidhania tupo hapa ili kuzungumzia hali ya mgonjwa?” nilimkatiza maana alinichanganya.

“Ooh, kaka! Kweli anaumwa na pengine anaweza kufa kabisa, kwani unajali nini? unajua nini Ninah, labda tukakae sehemu tuongee nikupe shilingi ngapi uondoke, maana najua upo na kaka yangu kwa ajili ya hela tu,” alisema Tsoza.

“Sikia kaka, pengine hatujuani, kaka yako na mimi tulikuwa tumefikia hatua ya kutambulishana na kuoana kabisa, na sikuwa kwa ajili ya hela, nilikuwa kwa ajili ya mapenzi!” niliongea kwa hasira tena nikikomaa kuwa nilikuwa nampenda japo moyo wangu ulijua ukweli.

“upo kwa ajili ya mapenzi?” aliuliza Tsoza akacheka kwa nguvu mno.

“Sikia kesho, asubuhi nitasaini cheki ya dollar 1000 nitakupa uondoke zako, muache tu kaka yangu asikupe tabu, kama ulikuwa unadhani utajiwekaweka ili uolewe na wewe uingie kwenye mirathi, hautaweza!” alisema Tsoza, nikamshangaa maneno anayoyaongea.

ITAENDELEA

Ninah Sehemu ya Tano

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment