Hii ni Dunia au Kuzimu Sehemu ya Tano
KIJASUSI

Ep 05: Hii ni Dunia au Kuzimu?

SIMULIZI Hii ni Dunia au Kuzimu
Hii ni Dunia au Kuzimu Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA: AHMED JIRIWA

*********************************************************************************

Simulizi: Hii Ni Dunia Au Kuzimu?

Sehemu ya Tano (5)

Ni sauti za wadudu wa porini pekee ndiyo waliokuwa wakitamba kwa sauti zao za kupendeza na kuushangilia usiku. Giza lilikuwa halisemeki ndani ya msitu wa kutisha ndani ya kisiwa hicho cha Madagascar. Miti minene, miti ambayo ilikuwa si ya kupandwa na binadamu bali ukiwa ni uoto wa asili. Tereza alikuwa si wa kwenye nafsi tena bali Tereza huyu alikuwa ni Tereza halisi anayejitambua huku akiwa anakumbukumbu zake. Alikuwa Tayari ameondolewa kutoka kule kwenye himaya ya Dokta Lee na washirika wake. Hakuwa akiongea wala kusikia kama ilivyo ada ya maisha yake mapya. Jumba kubwa la kutisha lilikuwa likimtazama yeye tu, lilikuwa ni pweke sana. Kimya kilikuwa kimetanda kama ilivyo ada ya jumba hilo. Chumba alichopo kilikuwa kiking’ara kwa mishumaa mbalimbali iliyokuwa ikiangaza ndani ya chumba kile. Tereza alikuwa akiimba wimbo mmoja tu ndani ya kichwa chake nao ni Baba!, Baba!, Baba!, hakuna kitu alichokuwa akikiwaza zaidi ya baba yake binti huyo ambaye kwa kipindi hicho alikuwa amepoteza kabisa haiba yake ya urembo. Hakuwa yule tena, hakuwa Tereza wa chuoni ambaye alikuwa akiwadatisha wanaume wengi kutokea mataifa mbalimbali, huyu alikuwa mchafu aliyepoteza hadi rangi yake halisi. Akiwa amekaa pale, upepo ukaanza kuvuma kidogo kidogo kisha ukavuma kwa ukali mkubwa sana. Madirisha yalifunguliwa kwa upepo ule. Tereza alilifuata dirisha lile ambalo lilifunguka akalifunga mara baada ya kuchungulia nje kidogo na kuona jinsi nje kulivyokuwa kukitisha. Alikuwa mwoga sana Mwili mzima ulianza kumtetemeka hofu ya kweli. Alijiuliza akilini juu ya mahala alipo lakini hakupata jibu hata kidogo. Nguvu ya kusema atoke na kukimbia mule msituni ili atafute mahala pa kujihifadhi hakuwa nalo. Ni kama akili yake iligandishwa hivi, mara mlango ulifunguliwa kwa kishindo kikuu kisha kitu cha ajabu kikapita na kumzunguuka kama vile upepo wa kisulisuli uzunguukavyo kisha kikatoka kwa kasi ilele na mlango kujifunga tena. Tereza aliogopa sana akajikuta akirudi nyuma lakini hapohapo akakumbwa na kizunguzungu kikali sana lakini hakikumpeleka chini wala hakujisikia kuanguka, aliona kama anageuzwa juu chini, chini juu. Ile hali haikukoma hata kidogo. na muda huo huo akaona hali ya kile chumba ikibadilika na kuwaka mwanga mkali ambao haukujulikana unapotokea. Akajikuta ameganda na kuushangaa mlango na mara kiumbe chenye umbo la binadamu kikaingia lakini kiumbe hicho kilikuwa kama kiko kwenye maji au taswira ionekanavyo kwenye maji maana kilikuwa kikichezacheza kwenye mawimbi. Jinsi kilivyo kwenye mawimbi yale na jinsi ambavyo hakuwa na umbo zuri la kupendeza ukichanganya na kuwepo katikati ya mwanga mkali, ilihitaji moyo wa hali ya juu kuweza kuyatazama maujiza yale, vilikuwa ni vioja visivyoeleweka kwa kweli. Kiumbe kile hakikujulikana ni Malaika au Shetani maana alikuwa akitisha kwa sura na rangi yake ya ajabu. Alikuwa na rangi nyekundu ya ngozi kiumbe yule lakini alivaa vazi jeupe lenye kuburutika hadi chini. Alikuwa ameganda pale mlangoni akimshangaa binti yule na yule binti akikishangaa kiumbe kile, walitashangaana.

Mwanga ule mkali ukaanza kupotea taratibu na hatimae ukabaki mwanga wa kawaida ambao haukua ukiumiza macho hapo sasa Tereza alijikuta akiongeza hofu kubwa kwenye maisha yake ndani ya jumba lile kwani kile kiumbe kiliweza kuonekana sura yake halisi. Alikuwa mbaya sana, mwenye ngozi isiyoeleweka kama ni ya kukatika katika au ni yenye ramani. Wakati Tereza akiwa kwenye hali ya kushangaa, kiumbe kile kikatoka pale kwa kasi kubwa kisha kuanza kuzunguuka mule ndani, kasi yake ikasababisha, upepo kuanza kuvuma taratibu na hatimaye kuwa mkali kabisa. Kiumbe kile kikakaa kwenye pembe moja ya chumba kikiwa hewani mithili ya kama kina mbawa kisha kuukusanya upepo ule na kumpulizia nao Tereza. Binti yule akaanza kupiga kelele kali mno, haikuwa kelele ya maumivu bali ilikuwa ni kelele ya hofu. Nguo zikaanza kumtoka mwilini na hatimae akawa hana nguo hata moja kwenye maungo yake. Kile kiumbe kinatoka pale kwa kasi kubwa na kumvamia Tereza na kuanza kumuingilia kimwili. Giza likarudi na kuwaficha. Tereza alihisi hali mbaya sana kipindi wakati kiumbe huyo akiwa anamuingilia. Maumivu yalikuwa makali mno kiasi kwamba kilio alichokuwa akikitoa hapo ni sawa na mwanaume anayetiwa jando pasipo ganzi yoyote ile. Alilia kilio cha maumivu ya kuzidi kiasi kwamba Jumba lote lilimezwa na kilio chake. Huo ukawa mwanzo wa mateso ya kutisha ya Tereza.

“Nani kati yetu anajua huyu binti alipokwenda?” lilikuwa ni swali lililoulizwa si chini ya mara tatu kwenye kikao kilichokaliwa usiku wa manane baada ya kile cha mchana ambacho kilikaliwa na jopo zima la watu wa himaya hiyo ya Dr. Lee na Washirika wake. Jibu lilikuwa haligeuki wala kubadilika kila lilipoulizwa swali hilo, jibu lilikuwa ni lilelile kuwa hakuna ambaye alijua. Wakabaki kutazamana usoni kama ni mara yao ya kwanza wanakutana nyakati hizo watu hao watatu.

“Hakuna?” akauliza tena yule ambaye aliuliza hilo swali kwa mara ya kwanza na jibu kukosekana.

“Hakuna mkuu!” majibu ya pamoja yaliwatoka watu wawili hao ambao hawakuwa wengine bali ni Lady Devil na Lonto kijana hatari aliyeshiriki mauwaji ya binti wa waziri mkuu huko nchini Malawi kisha kukimbilia Ungamo mara baada ta kutoroka chini ya ulinzi mkali wa polisi huku wakiacha majonzi makubwa kwa jeshi hilo la polisi baada ya kuuwa polisi wote wakati wakiwa katika harakati za kutoroka. Alikuwa ni yeye na Bande Sir. Walipofika ungamo, Lonto alikimbilia Kisiwani Madagasca baada ya kuonekana anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Dr. Lee kwa kupeana msaada na Merina hivyo akachukuliwa huko.

Huku nyuma Bande Sir akakutana na kikosi hatari kilichokuwa kikiongozwa na Rais wa zamani Julio Mobande Julio. Akaomba kuwa chini ya kikosi hicho. Julio akamwambia kuwa hawakuwahi kumpa kazi mtu ambaye kwao hana faida yoyote ile bali wanatoa kazi ikiwa anaweza kufanya jambo la kinyama lenye kuwafurahisha wao. Akaingia kwenye makubaliano ya kufanya jaribio lolote lile ambalo atapewa. Bande Sir akatafutiwa binti mrembo sana kisha akatakiwa kumuingilia kimwili mbele yao na kumuuwa kwa kifo ambacho hata wao hawajawahi kukiona. Bande Sir akafanya kama ilivyotakikana. Alimuingilia huyo binti pasipo kuwa na haya yoyote ile wala soni kisha akakabidhiwa silaha ambayo aliihitaji kwa ajili ya kumuuwa binti huyo. Akapewa bastola yenye kuingia risasi sita kisha akajaziwa risasi kwa kiwango cha bastola hiyo. Walikuwa wamekaa wakitazama jinsi mtu huyo atakavyoweza kuuwa kwa kifo kipya ambacho wao wenyewe hajawahi kukiona. Risasi ya kwanza ya Bande ilifumua goti la mguu wa kushoto wa binti yule, kilio cha yule binti kikawa ni chereko kwa watazamaji na muuwaji aliyepewa kazi ya kuuwa mtu asiye na hatia. Risasi ya pili ikavunja bega la kulia, binti akazidi kulia kwa maumivu makali huku akiwa ananing’inia kwenye minyororo ambayo ilikuwa imefungwa kiunoni mwake. Risasi ya tatu ikapita kwenye bavu za matiti ya binti yule, yaani ilipita kwenye ubavu wa titi moja lililokuwa limesimama vema na kutokea kwenye titi jingine. Julio na wenzake wakawa hawana mbavu, Pombe zilikuwa zikinywewa kwa sifa kali sana huku wakimsifia huyo jamaa jisi alivyo na shabaha ya kutumia silaha. Zilisalia Risasi tatu pekee na moja kati ya hizo ilipangwa kukata nyororo na mbili pengine ndizo zimtoe uhai binti huyo. Akapanga kwa sekunde tatu atakuwa ameuwa na kumdondosha kutokea pale juu alipofungwa, watu hwakuamini, akapangiwa dau na kuanza. Kila sekunde alitoa risasi na kupiga mahali palipokusudiwa. Risasi ya nne ilipiga chini ya kitovu binti akabaki kuachama mdomo pasipo kupiga kelele, ya tano ikakata nyororo ile na ikiwa wakati anakuja chini, risasi ya mwisho, ikachimba kwenye shingo. Binti yule akafika chini sakafuni angali maiti tayari. Hapo hapo Bande Sir akapewa nafasi ndani ya kundi hilo lifanyalo mambo yake kwa siri sana. Akapewa mipango kabambe ya kundi hilo ikiwa ni njama za kuweza kuzama ikulu kwa kutumia akili nyingi lakini pia ikiwa ni kutaifisha mali za Backa ili ziweze kuingia kwenye mifuko yao ya Benki. Zikafanywa njama za kumuingiza mtu huyo serikalini na kwa kuwa Julio alikuwa ni Rais wa zamani hilo halikuwa gumu, hawakuangalia uraia wala nini vyote hivyo vilifunikwa, Bande Sir akawa Mbunge wa kuchaguliwa kifedhuli na hatimaye akapewa uwaziri wa ulinzi na usalama. Hilo ndilo lilikuwa lengo haswa la Julio kumpata mtu makini ambaye angeweza kumficha kwenye kitengo kile ili iwe rahisi kwa yeye kufanya yake pasipo na kipingamizi cha aina yoyote ile. Hiki ndicho kitu kilichomshangaza Petii kwa mara ya kwanza wakati anagundua kuwa Bande Sir alikuwa ni waziri tena wa ulinzi wakati nchini malawi alitambulika kama muhalifu, hicho kikampa ugumu hata wa kuchelewa kuianza kazi kwa kuhofia kuleta mgogoro wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.

“Lonto, nini tunafikiri hadi sasa na mkijua kuwa huyu binti hakutakiwa kutoroka hadi pale ambapo tungeamua kumuangamiza? Mchana hakuna kitu cha msingi sana kilichotoka kwenye mkutano ule tuliyojadili haya, kinachonipa hofu ni uondokaji wa huyu binti, usiku mkubwa tena haikujulikana ametumia njia gani kutorokea maana hata kamera zetu za ulinzi hazija ng’amua kitu!” alisema Dr. Lee ambaye ndiye aliyekuwa akikiongoza kikao hicho cha siri. Mara nyingi huwa wanakutana kwa siri watu hao hasa pale wanapohisi kuwa jambo lililofanyika si la nguvu za kibinadamu.

“Tuanahaja ya kufanya maombi usiku huu?” akauliza Lady Devil/Merina.

“Haja hiyo haipo kwani bado hatuja kamilisha kile akitakacho King Bondo, kumbuka kuwa watu kuanzia mia moja na kuendelea watakao kufa kupitia mpango wetu wa maangamizi yeye ndiye atakaye kunywa damu zao, akishakunywa hapo sasa nadhani amani yetu ya kumtumia yeye ndipo itakapoanza, kwa sasa hatatusaidia chochote” alijibu Dr. Lee. Kimya kikachukua nafasi yake lakini wakapanga jambo moja la kuhakikisha wanamtafuta Tereza kwenye kila pori japo waliamini haitasaidia lakini wasikae bure na hapo mpango wao wa maangamizi utakapoanza ndipo wangeweza kujua nini wafanye. Backa alikuwa ametulia kimya kitandani kwake ambapo alikuwa amelala, hakuwa akijua chochote wala kukumbuka chochote, kichwa chake kilipoteza kabisa kumbukumbu kutokana na maumivu makali ya mara kwa mara ambayo yalikuwa yakijirudia kila wakati. Maumivu yanapojenga mazoea kwenye mwili hata akili nayo hupoteza uwezo wake wa awali na kubakiwa na hali ya yale maumivu ya kila wakati. Mwili wake ulikuwa umenyongea sana, sura yake ilipoteza uhalisia wa awali kwani nywele na ndevu zake zilikuwa nyingi sana kiasi cha kufunika kichwa chake. Nguo ambazo alikuwa amevaa pindi anaingia hapo, hakuwa amebadilishwa hadi kipindi hicho. Hakuna wa kumjali, chakula alichokuwa akipewa cha kupitia kwenye mipira na mipira iliyowekwa kwa ajili ya kupitisha haja zake, ndivyo vilivyokuwa vikimpa uhai. Mwili wake haukuwahi kujua maji tangu kuingia humo, haukuwahi kujua mafuta wala dawa ya kutuliza maumivu bali kuongezeka kwa maumivu kila wakati ndiyo iliyokuwa hali ya maisha yake. Alikuwa amekonda sana na alikuwa ni mtu mwenye kujikuna pale alipopata wasaa wa kufanya hivyo kwani muda mwingi mwili wake unakuwa ni wenye kukakamaa sana na kumpelekea yeye kushindwa kujikuna au kusimama kwa miguu yake. Pamoja na mateso yote hayo na hali aliyo nayo, hakuacha kutabasamu na ukimuona amekunja sura basi ujue kipindi cha maumivu kimekaribia.

“Nitaiangamiza Ungamo kwa mikono yangu mwenyewe ama kwa akili yangu mwenyewe” yalikuwa ni maneno ya Bencov kila mara alipokuwa akiwa mbele ya kitanda cha Backa. Aliyafurahia mateso aliyokuwa akiishi nayo bwana huyo na hakusita kusema kuwa Backa ndiye atakuwa mtu wa mwisho kufa kwani hawezi kumuacha hai ingali aliuwa familia yake yote na kumuacha yatima asiye na baba wala mama. Ni uonevu mkubwa sana kuishi kwa mateso yasiyokuhusu, Nani anajua kuwa Rais wa zamani Julio ndiye aliyehusika na vifo vya hao warusi kama si yeye na watu wake, Backa anaishi kitandani maisha yake yote huku akikumbana na mateso ya kila baada ya masaa nane kwa sababu ya mpuuzi mmoja mwenye tamaa ya madaraka ya kuishi Ikulu kifalme na utajiri usio mali yake.


“Mauwaji ya watu wasiofahamika yanazidi kuendelea huku muuwaji akizidi kuiacha hoi serikali kwa kuacha kadi yenye bendera ya Tanzania. Jana majira ya saa tatu asubuhi juu ya alama, huko mjini haika kumekutwa mtu mmoja akiwa ameuwawa kwa kifo cha utata sana, kifo hicho kilionesha kuwa mtu huyo, alipambana kwanza kabla ya kukutwa na mauti hayo”

“Fu*k!” alitukana Bacon kisha akaweka pembeni gazeti alilokuwa amelishika mkononi mwake akiisoma makala hiyo ambayo haikuwa ikionekana ni nani alikuwa mwandishi wa makala hiyo. Hizi habari za mauwaji mbona ni za watu wetu tu na hakuna mauwaji mengine yanayotangazwa humu. Ninani wa kupeleka habari hizi kwenye chombo hiki cha habari ambacho ni bubu. Huyu mwandishi ni nani sasa? mbona hajajidhihirisha hapa na hata namba yake ya simu hajaweka. Eti, na mwandishi wetu? Aliwaza Bacon kisha akasimama baada ya kuwa alikaa sana kitini akilisoma gazeti hilo ambalo mwisho alichafuliwa kabisa na makala hiyo ya ajabu. Nani huyo wa kurusha taarifa hizo?

Tujue tu kwamba Frank hata kama alikuwa akishirikiana na Roi lakini hakuacha kutuma habari kwa mtu wake ambaye walikuwa wakipanga mengi gizani. Nia kubwa ya Frank kichaa ilikuwa ni kuhakikisha habari za wahalifu zinasomwa na kila mmoja na mtu huyo aliyekuwa akimfikishia habari na picha alikuwa hafanyi makosa kabisa. Kumbuka kuwa wakati Frank akifanya biashara ya kuuza magazeti kipindi hicho cha nyuma, alikuwa na rafiki yake mkubwa sana ambaye walikuwa wakifahamiana tangia shuleni, sasa huyo ndiye aliyekuwa amepanga kumsaidia rafiki yake Frank kuzianika habari kila kijana huyo makini atakapokuwa akizikamata. Alifanya yote lakini hakufanya ujinga wa kutaja mtu ambaye alikuwa akishirikiana naye ambaye alikuwa akimjua kwa jina kabisa. Roi alilijua hilo japo hakuwa akimwambia kitu chochote kuhusiana na hilo kwakuwa alimkuta akiwa katika harakati hizo basi aliamua kumuacha aendelee nazo alichokuwa akikikipenda Roi toka kwa Frank ni umakini. Kitu ambacho hawakukijua wao ni kuwa hakuna jambo lisilowezekana na wewe ukifanya ‘A’, wenzako wanafanya ‘Be’

Saa 06:25 za magharibi, mlango ulifunguliwa kwa fujo sana kwenye ofisi za kampuni moja ya gazeti la Siri kali. Binti ambaye alikuwa ndani ya mawani ya jua alikuwa amevaa viatu virefu vya mchuchumio huku akiwa na suruali ya kuvutika ya rangi ya kijani. Alifika ndani humo ambapo alimkuta binti mmoja aliyekuwa ametulia nyuma ya kompyuta ya kizamani. Dede alivua ile mawani na kuiweka pembeni kisha akanyoosha shingo yake, mchoro wa ajabu ukajionesha kwenye sura yake uliokata sura yake. Macho yake ya urembo yakajionesha lakini yalitisha kutokana na kukosa tabasamu.

“Nataka kuonana na mkurugenzi eidha meneja wa kampuni hii” akasema Dede.

“Kwa miadi ya kikazi, binafsi?” akauliza yule binti huku akimalizia kuchapa kitu fulani kwenye kompyuta ile.

“Vyote vinaweza kuwa sababu ya mimi kuwa hapa” akasema tena Dede, yule dada akanyanyua sura yake kwa mara ya kwanza kumtazama vizuri huyo mgeni mwenye sauti ya kike lakini akionesha kuwa kiburi kama si jeuri. Mh! akaguna kidogo kisha akajikaza.

“Hakuna utaratibu wa kumuulizia mtu kwa namna hiyo dada yangu” Dede alisimama kisha akasogea hadi karibu kabisa na meza aliyopo huyo dada ambaye bila shaka alikuwa ni katibu muktasi.

“Kwanza huu si muda wa kazi, huu ni muda wa ziada tu, labda uje kesho” akaeleza zaidi huyo dada huku akiwa na hofu kidogo maana mgeni huyo alianza kumtisha.

“Kazi nyingi makini na za kinafiki, hufanywa muda wa ziada hasa kwa wana habari maana huwa hakuna umbea na hata pesa yake, huwa ni tamu kwa sababu imekuja kwa muda wa ziada….vipi kama nikibadilisha utaratibu wa kumuulizia meneja?” akauliza Dede baada ya kuongea kwa kina kidogo kisha akakikamata kicharazio cha ile kompyuta kisha akakipiga kwenye ile meza kwa nguvu sana, kicharazio kile kikalia kwa kuona kimeonewa maana kwa kishindo kile kisicho na huruma ni wazi kiliharibu ubora wake. Kilichanguka sana.

“We’ dada! Unaakili timamu kweli? Unakujaje kwenye ofisi za watu halafu unafanya ubabe wa kijinga!”

“Ni kwa sababu unenifundisha jinsi ya kumuulizia meneja ama mkurugenzi wa kampuni hii, huoni kuwa nimeharibu sasa?” alijibu Dede akiwa hana hata wasiwasi. Yule msichana akasimama kwa maneno makali ambayo masikini ya Mungu, hata hakufika nayo mbali, kofi moja zito ambalo hakuwahi kupigwa kwenye maisha yake likamfanya abadili mtindo wa kupiga kelele sasa akaachia yowe kali la uchungu. Watu hao makini walifanya umakini katika kujua hayo na ubabe sasa unatumika.

John kwa jina moja, huyu alikuwa ni muandishi wa habari wa zamani sana ndani ya kampuni hiyo inayohusika na kuchapisha magazeti kadhaa kama gazeti la Siri kali ambalo ndilo linalompa ujira, na magazeti mengine. Ukitambo wake na ufanyaji wake wa kazi, ulifanya kujipa umaarufu huku akijijengea imani kubwa sana kwa mkurugenzi au bosi wa kampuni hiyo ambaye kumuona kwake ilikuwa ni shughuli japo huwa ndani ya kampuni hiyo mara nyingi. John alijikuta akijizolea cheo kizuri kilichokwenda kuupandisha mshahara wake kwa kiasi fulani na kumfanya hata aweze kumiliki kigari ambacho kwa namna moja ama nyingine kilikwenda kumpunguzia adha ya usafiri. Hakuna kitu kilichoweza kumfanya kijana huyo ambaye kihistoria alisoma shule moja ya msingi na sekondari pamoja na Frank kichaa kabla ya kijana Frank kufanyiwa upindishipindishi wa elimu yake na watu wenye nyadhifa zao na kusababisha elimu yake kumwagika mchangani kama Alimasi. Habari za siri ambazo hazikuwa zikitolewa na gazeti ama chombo cha habari chochote kile ispokuwa hicho, ndizo zilizompa umaarufu naye kulipa umaarufu gazeti hilo la siri kali na kulifanya kuwa ni miongoni mwa magazeti pendwa sana ndani ya mji huo wa Pande na nchi ya Ungamo kwa ujumla wake. Hakuna aliyekuwa akijua kuwa kijana huyo alikuwa akiletewa hizo habari na kijana mwenzake ambaye alikuwa na lengo fulani na maisha ya wanyonge huku akitaka wanaofanya hayo yote waaibike kwa tabia zao au waangamie kwa mikono yake ikiwa ni kulipiza kisasi cha wazazi wake. Wengi walikuwa wakijiuliza hilo kuhusiana na John alivyokuwa akizipata habari maana muda wote alikuwa akiwa wa mwisho kutoka ofisini na wa kwanza kuingia ofisini. Ni wapi sasa alikokuwa akizipata habari tata na zenye kutikisa Taifa kama hizo. Jibu walilikosa na hawakuwa na ujasiri wa kumuuliza moja kwa moja. Kitendo cha John ambaye alikuwa amevishwa cheo cha umeneja huku akiwa bado yu ajifanya hajapenda kuiacha kazi yake, akatoka kule aliko mwanzo na kuanza kuandika makala tata na mwisho kuficha jina lake. Hiki kikamfanya awe wa mwisho kuondoka kila siku ofisini kwani mara nyingi alikuwa akifanya hakiki/hariri ya makala zake kabla hazijachapishwa kwenye gazeti.

Kishindo cha kuvunjwa kwa kicharazio cha kompyuta ya katibu muktasi wake, alikisikia lakini akaambiwa na mawazo yake kuwa hilo halikuwa jambo la kwanza ofisini hapo, kwani hata gilasi za maji mara nyingi huwa zikianguka na kupasuka, mbona ni kawaida. Ukelele wa katibu muktasi wake, huu ukamgutusha na kumpa wasiwasi. Amedondoka? akajiuliza mawazoni lakini nafsi ikamwambia hapana hawezi kudondoka kwenye ofisi yenye kapeti lenye kushika kiatu.

Atakuwa amefanyaje sasa? akaiuliza nafsi yake tena kama angeweza kujibiwa kama awali lakini hili hakujibiwa, akajishangaa kwanini haamki na kwenda kuhakikisha kunani huko.

“Wanawake bwana!” akasema huku akijinyanyua kitini. Kitambi chake kidogo kilichoanza kudhihirisha mafanikio yake madogo yaliyoanza kujikusanya kwa kasi kikajionesha. Akapiga hatua za haraka na kuukabiri mlango, alikuwa akitaka kurudi ili amalizie kazi yake na arejee nyumbani mapema. Alimkuta Katibu muktasi wake akiwa anajizoazoa kutokea chini huku akiwa amelishikilia shavu lake lililokuwa likimchonyota kwa maumivu makali ya kofi alilopigwa.

“Huyu ndiye bosi na mhariri wa makala za FUKUFUKU NA MATUKIO YA NCHI wa gazeni lenu la Siri kali?” Dede alitumia nafasi ya woga wa yule dada kumuuliza kwa sauti kali ya kufoka akijua ni lazima angejikanyaga.

“Ndiyo,…….ndiyo…huyo huyooooo dada!” alijibu huku akiwa na hofu ya kupokea kofi jingine la mwana ukome. Aisee! Lilikuwa ni kosa kubwa sana la mwaka ambalo alilifanya huyo dada. Dede aligeuka kwa haraka sana na kumtupia macho yule kijana. akapiga makofi kwa kumpongeza huyo kijana kisha akamsogelea.

“Hongera kwa kufukua habari za siri na kuzitupia kwenye gazeti lenu la siri kali, mimefarijika kukutana nawe kwani nataka uitangaze na hii ya kifo chako na uipambe kwa rangi na maandishi ya kupendeza” alisema Dede huku akichomoa bastola kutoka kwenye mkanda maalumu mapajani mwake. Macho yalimtoka yule dada lakini John hakubaki hapo alikimbilia ndani ya ofisi yake na kukakamata simu. Dede aliukabili ule mlango lakini akakumbuka kitu akasita na kuuachia kisha akamuelekezea bomba la bunduki yule dada. Risasi za kichwa mbili zikatosha kukifumua kichwa chake. Nafasi ile ikawa imetumiwa vema na John kuweza kuitafuta namba ya Frank kichaa ambayo aliisevu ‘My best’

Ilikuwa ni habari ya kufurahisha sana ambayo walikuwa wakibishania watu waliopo ndani ya sebule ya nyumba ya siri, muda huo wa saa kumi na mbili kwenda na dakika arobaini na kitu. Frank, Roi na Petii, walikuwa wamekaa mbele ya Luninga wakitazama habari za michezo ambazo zilikuwa zikirushwa na kituo fulani cha habari. Mabishano yaliyokuwa yanaendelea luningani hayakutofautiana na yaliyokuwa yakiendelea hapo sebuleni, kila mmoja alikuwa akivutia kwake mithili ya muwamba ngoma, kuwa timu fulani ni bora zaidi kuliko nyingine kwanza nidyo inayoongoza ligi na huku mwingine akijinadi na kujitapa kuwa wako mbele kwa baiskeli ya miti. Ilikuwa ni ilimradi tu kila mtu alikuwa na kile akipendacho toka ndani ya mtima wake. Walikuwa mahali hapo wakisubiri muda wa wao kuingia kazini ufike na si kitu kingine. Kelele za mabishano zilikuja kukoma baada ya simu ya Frank kuita. Frank alipoitoa simu hiyo mfukoni mwa suruali yake, akakuta anayepiga ni My best kama ambavyo mwenzake alimhifadhi hivyo kwenye simu yake. Akapokea huku akinyanyuka akijua labda ni habari zao za siri. Akashtuliwa na neno.

“Ninakufa ndugu yangu” Frank akashtuka na kuiweka vizuri simu yake sikioni lakini kabla hajaongea kitu, mlio wa bunduki na sauti ndogo ya maumivu ikamfanya adondoshe simu chini sakafuni. Watu wote pale wakapatwa na mshangao.

“Nini Frank!” Roi akauliza kwa sauti ya juu sana.

“muandishi wa makala ya FUKUFUKU NA MATUKIO YA NCHI amepigwa risasi muda huu na kishindo chake ndo kimefanya nimedondosha hii simu” alijibu Frank huku mwili ukiwa unamtetemeka sana kwa hasira.

“Wamenitukana, wameniacha yatima kabisa ndugu yangu ama rafiki aliyebakia ni huyu Brother Roi, ni lazima waniuwe na mimi sitakubali. Wamenikanyaga nyoka mkia makusudi sasa sina budi kuzitoa sumu zangu” aliongea Frank huku akiinama na kuiokota simu na kutoka mule ndani akaelekea upande wa nyuma wa ile nyumba, aliporudi alikuwa si yule Frank ambaye alikuwa akicheka muda huo bali alikuwa ni yule M.Y.S ambaye mimi na wewe tulikuwa tukimfahamu hivyo japo jina hili tukiwa hatulijui maana yake. Kifupi ni kwamba M.Y.S ilikuwa imebeba maana ya Maisha Ya Shida. Na alijipa jina hili kutoka na J.M.J au Julio Mobande Julio, kuibadilisha dira nzima ya maisha ya kijana huyo. Huyu ndiye alikutwa hivi na Petii sasa leo anarudi huko kwa awali.

“Nitaishi nawe Brother Roi kwakuwa ninandoto za kuleta jambo la faraja kwa Taifa hili nikiwa nawe hata kama kuna nguvu za kishetani bado sitakutupa lakini sitakuwa kama yule uliyenizoea tena mimi ni M.Y.S au waweza niita (Maisha Ya Shida). Jina hili nilibatizwa na J.M.J Rais wa zamani wa Taifa hili ambaye anafahamika kama Julio Mobande Julio. Brother Roi, Julio amenifanya nimeishi kwa mateso makubwa sana sababu ikiwa ni akili yangu mwenyewe, yeye aliamini kwa akili yangu ningekuja kuwa msomi nisiyekubali kuburuzwa, alitaka nife masikini lakini Mungu akanisaidia na kuanzisha biashara, huyu mtu akaniharibia tena na kuniulia kabisa wazazi wangu kwa kifo kibaya kisha kuniahidi na mimi kifo kabla hajaingia Ikulu bila kura za wananchi. Nimeuwa binti yake sasa naingia kazini kwa kumuuwa yeye nami niishi kwa amani” alisema Frank au M.Y.S kama alivyoamua kujiita kisha akaondoka kwa kasi hadi nje akadandia pikipiki kubwa.

“Frank tulia kwanza…..!” alikuwa akisihi Roi lakini haikusaidi.

“Nimekufungua sasa brother na umejua kuwa hii nyororo si ndogo, tutakutana mitaani” akasema Frank kisha akawasha pikipiki na kutoweka.

“Hii nini maana yake Roi?” akauliza Petii.

“Yule aliyekuwa akiandika makala za kila vifo vya hawa wajinga, wamemshtukia na huyu ndiye aliyekuwa akimpa habari hizo” alijibu Roi.

“Sasa itakuwaje si wanaweza kumuuwa maana amechanganyikiwa?” akauliza tena Petii.

“Frank ni mafia mimi ndiyo nakuambia kama ulikuwa hujui na aliyemfundisha ngumi si wa daraja la kawaida. Frank, Roi, watausoma moto huu” akajibu Roi kisha akatulia Petii akashangaa kwanini kwenye hayo majina yeye hakuwepo, inamaana si chochote kwenye hilo kundi? akauliza lakini akajibiwa kuwa kifo kitakachofuata ni cha Bande Sir kisha yeye ni lazima aondoke ndani ya Taifa hilo na arudi nchini kwao kwani vita hiyo hakuwahi kuiota hata ndotoni. Petii hakujibu kitu akakaa kimya lakini hakutaka kuafiki maneno ya huyo kijana kuwa hawezi kupambana na vita hiyo.

Mitego iliyotegwa na pande mbili ilikuwa bado ikifukuta lakini mtego mmoja ndiwo uliokuwa ukileta hali ya kutisha kidogo maana ulionekana ukija kwa kasi sana kwenye kunasa. Mtego huu ulikuwa ni wa Salama mke wa Rais Mabandu, Ufuatiliaji wa kijana aliyepewa kazi ya kufuatilia ilikuwa imempeleka hadi kwenye kikao cha usiku cha Salama kwenda kukutana na watu wake wa siri. Kitu ambacho mfuatiliaji hakuwa makini ni jinsi ya ufuatiliaji wake. Alikuwa ameshaonekana na watu makini na sasa akawa anasubiriwa aingie kwenye mikono ya watu hao. Wakati Salama akiwa anaingia kwenye ukumbi mdogo wa mikutano uliopo katikati ya mji, mfuatiliaji aliyewekwa na Rais kumfuatilia mkewe alikuwa nje ya ukumbi ule akiwa na simu yake sikioni akitoa taarifa mahali huku akiwa ndani ya gari yake. Wakati akiwa anashangaa, vioo vikapasuliwa kisha akatolewa nje akiwa amewekewa silaha kichwani waziwazi bila kificho. Akaswekwa ndani ya chumba kidogo huku akipigwa kwa mateke kadhaa ya mbavu akafungwa kamba na kuachwa mahala hapo hadi walengwa watakapomaliza mikutano yao. Baada ya dakika thelathini, mlango wa chumba alichowekwa, ulifunguliwa kisha wakaingia watu wawili, mmoja alikuwa ni Jarome na mwingine alikuwa ni mke wa muheshimiwa Rais aliopo madarakani.

“Nani alikutuma unifuatilie mimi nisiyependa kufuatiliwa?” akahoji Salama kwa sauti kali. Yule kijana akaweka ubishi na kugoma kujibu. Jarome akatoa bastola na kuchangua goti la kijana huyo.

“Funtastic!….hakuna ahuweni wala afuweni, swali ni lile lile, ni nani alikutuma unifuatilie?” pia kijana yule akawa analia tu pasipo kujibu kitu, Jarome akasema kuwa kijana huyo anaonekana hajihurumii kisha akalikanyaga lile jeraha la moto ambalo punde lilitoka kusababishwa naye. Kijana huyo akaona kama roho inamtoka akaamua kuweka wazi ili aepukane na balaa la maumivu, kweli kabisa aliepukana nayo kwani aliposema tu ni muheshimiwa Raisi ndiye aliyempa kazi hiyo, Risasi ikakifumua kichwa chake naye akaporomoka chini bila kelele.

“Tumemuuwa” Alisema Jarome kwa sauti nzito kisha akaishusha simu chini akiwa anatabasamu baya la kifedhuli kisha akafungua kinywa chake.

“Kuna haja ya kufanya maamuzi haraka sana, huyu mumeo ni kiburi au ana matatizo gani?” alihoji Jerome kisha akamkazia macho Salama.

“Kama ambavyo tumejadili pale kwenye kikao, huyu mtu hadi sasa sijajua anategemea nini, amekuwa nunda hataki tena kujadili na mimi kitu chochote” alijibu Salama.

“Ok, liache hilo yapo masaa machache tutajua cha kufanya” aliongea Jarome kisha akatoka mule ndani kwa hasira. Baada ya Salama kuondoka kabisa eneo lile, Jarome alikwenda kuonana na Rais Julio na kupanga jambo la mwisho ambalo litamliza huyo Rais, moja lilikuwa ni kumuondoa duniani binti yake. Rais akaamrisha kuwa simu zipigwe kwa vijana na watoe majibu kuwa kazi waliyotumwa ya kumuweka chini binti wa Rais Mabandu imefikia wapi. Simu ikapigwa lakini majibu yaliyorudi hayakuwa rafiki. Kila mmoja mule ndani akabaki na mashaka makubwa kwenye moyo wake. Inamaana Rais ameshtuka juu ya mpango wao mbaya na kama ameshtuka na kuamua kumuhamisha binti yake kuna nini ambacho amewandalia watu hao. Hofu kubwa ambayo ilimshika Jarome ni kuhusu Salama, kama Salama atabanwa vizuri ni wazi atatoa siri za machimbo yao yote. Hali zao kwa ujumla zinaweza kuwa hatarini sana.

****

“Tunafanyaje kuhusu first Lady mkuu?” aliuliza Jarome. Rais akainama kwa muda mrefu kidogo na alipoinuka akawa amepata jibu na maamuzi sahihi juu ya first Lady.

“Mpigie simu mwambie arudi kuna jambo la msingi……au mwambie kuwa mumewe amemtowesha binti yake na haijulikani alipo hivyo kunaweza kuwa na hatari juu ya jambo hilo kwake na kwao pia. Jarome akafanya hivyo kwa muda huo huo akafikisha ujumbe. Simu hiyo ikajenga mawazo hasi kwenye ubongo wa Salama. Binti yake ametoweshwa? Na nani? Kama ametoweshwa inamaana mumewe anajua aliyemtowesha binti yake. Yule ni binti yangu mimi na kama amemtowesha kwa mipango yake ya kutaka kunigeuka, hapa amenoa ni lazima nifanye kitu. Akawaza Salama akiwa kwenye gari. Akawaza mawili arudi nyuma au aende kwanza Ikulu akajue nini pumba na upi mchele. Baada ya kuwaza sana, akakata shauri na kuamua kwenda kwanza nyumbani kisha arudi nyuma kwa ajili ya majadiliano na maamuzi makali kwa Rais Mabandu. Salama alikuwa ni mtu hatari sana na mwenye tamaa kubwa, maisha ya kuwa first Lady hakuridhika nayo hata kidogo. Acha huo u-first Lady akapewa na nafasi adhimu yenye mshahara mzuri na makapikapi manono ambayo yangeweza kumfanya atulie lakini, haki ya manani waswahili wa zama hizo hawakukosea pale waliposema ya kuwa, Penye miti mingi hakuna…

Hilo naamini hadi sasa kwani sidhani kwa mtu fakiri mwenye kusota kwa kuisakanya miambili, angeweza kuichezea nafasi ya mtende kama ile, nafasi ile kwa bahati mbaya huwakuipata wale ambao hawaridhiki na kilichowatokea na badala yake wanataka hicho na kujaribu kupata zaidi ya hicho. Wakajikuta wakitumia njia ambazo si sahihi kibinadamu.


SAA MOJA NYUMA.

Simu aliyopigiwa muheshimiwa Rais Mabandu, ilikuwa ni simu ya kishenzi na yenye kuchanganya kidogo kwani kitendo cha kupokea simu ile na kusikia neno moja tu la ‘tumemuuwa’ kisha simu hiyo kukatwa, ilikuwa ni lazima imchanganye. Wamemuuwa tayari? Hii ni picha niliyokuwa nikiifikiria na kumbe kweli fikira zangu hazikuwa mbali na hali halisi. Mtego umenasa. Aliwaza kisha muda huohuo hakuchelewa, akanyanyua mkonga wa simu na kupiga kwa muhudumu wa mapokezi akaomba mtu kutoka kitengo cha uchunguzi ndani ya hiyo Ikulu afike ofisini kwake. Muhudumu huyo akapiga simu kwenye kitengo husika kisha akafikisha hizo taarifa, dakika kadhaa kijana mmoja akawa mbele ya Rais.

“Kuna mtu amenipigia simu kwenye simu hiyo hapo (akasonta kidole mahali simu hiyo ilipo). Nataka nipewe taarifa zake ndani ya masaaa haya” akatoa maagizo. Kijana huyo aliibeba simu kama ilivyo akaondoka nayo. Baada ya yule kijana kutoka, akapiga tena simu kisha akasema.

“Liyambo najua uko kimya kwa sababu nilitaka uwe kimya, sasa nahitaji turudi kwenye nafasi inayotakiwa tuwasaidie waliokuwapo kwa njia yoyote ile nzuri ifaayo”

“nakusikiliza Muheshimiwa” akajibu Liyambo.

“Hakikisha sauti yako inakuwa salama kiusalama zaidi” akamtahadharisha halafu akaendelea.

“Mtaarifu Inspekta Bogo mwambie aje ofisini kwangu mara moja…..ooh! No, nataka kukutana nanyi nyote wawili kwwenye ofisi yangu leo hiii ikiwezekana muda usiwe mrefu sana kuanzia sasa”

“Inspekta….!”

“Najua ni lazima ushangae lakini kuna jambo nimelitazama kwa macho ya ziada na nimegundua haliko sawa, kujeni huku na tutaongea mengi” akashusha simu chini akairudisha kwenye kikalio chake, akapumua kwa nguvu kisha akajilaza kitini. Joto lililokuwa likifukuta mwilini mwake akaona hata kiyoyozi kilichopo mule ndani hakikuwa na msaada kwake. Akabaki kutulia kama mgojwa wa Kiharusi.

Nguvu ya kufanya kitu haikuwepo tena alikuwa na jambo moja muhimu tu akilini mwake nalo ni kuwachanganya wajinga hao. Kengele ililia na alipoitazama kompyuta yake ikamuonesha mtu aliyopo mlangoni, akabonyeza kitufe cha kuruhusu, mlango ukafunguka. Akaingia IGP Liyamho na Inspekta Bogo wakiwa kwenye mavazi yao ya kawaida, hawakuwa wamevaa mavazi ya kazi. Wakakaribishwa kitini wakakaa. Moja kwa moja wakaingia kwenye jambo lililofanya makutano hayo. Rais alieleza kila kitu na nia yake juu ya Taifa lake la Ungamo pamoja na watu wake, mwisho akampa kazi Insp. Bogo rasmi ya kuanza kufuatilia kile ambacho atataka akifuatilie. Akamwambia kuwa kikubwa anachokitaka ni kujua nyendo na mipango haribifu ya watu wanaotishia amani ya nchi kisha atajua nini cha kuwafanya mwishoni. Muda huo huo, yule kijana aliyeambiwa aichunguze namba iliyompigia Raisi, aliingia na ripoti iliyokamilika akamkabidhi muheshimiwa. Raisi Mabandu akamwambia Bogo aichukue hiyo ripoti iliyokuwa imeonesha mahali simu ilipotoka na utambulisho wa mtu huyo. Bogo akaipokea kazi ile kwa mikono miwili maana kitendo cha kutolewa kwake kwenye upelelezi ule, hakuwa amekubaliana nao kwa asilimia zote. Hiyo ikawa ni furaha kwake lakini Punde kengele ikalia tena kuashiria kuwa kunaugeni mwingine mlangoni. akatazama akamuona ni mkewe. akawapa maelekezo watu wale walioko pale akawaambia wapite kwenye mlango mwingine kisha awakute nje kwenye gari ambayo aliwaonesha gari hiyo ilipo akampa Bogo ufunguo wa gari ile, akawajulisha walinzi wake waaminifu kuwa wasifanye kitu chochote juu ya watu hao. Mlango mwingine ukafunguliwa kisha first Lady akaingia pasipo kuwa na wasiwasi wowote hadi kwenye kiti akaketi na kumtazama mumewe kisharishari. Ni kama si yeye aliyefanya mauwaji ya kijana wa Rais ndani ya masaa mawili nyuma.

“Nataka kujua binti yangu umetoroshea wapi, unataka kujichukulia maaumuzi wewe mwenyewe tu kila wakati hujui kama hata mimi yule mtoto ananiuma. Haya, umemkatishia masomo yake pasipo kunieleza pia hutaki kuniambia ni wapi alipo?” akahoji Salama. Rais Mabandu akashusha pumzi nzito kisha akaweka pozi na kumtazama mkewe kwa tuo kubwa huku moyoni kukiwa na mjadala mzito kuhusu yeye. Inamaana hajui kuwa watu wake wanataka kumuuwa binti yake? Au anashirikiana nao katika kutekeleza hilo. Halafu mbona amemuuwa kijana wako uliyemtuma! Huyo si binadamu na kama ni binadamu basi anamapungufu makubwa, viungo vyake muhimu vitakuwa si vyote mwilini mwake. Mjadala huo ndivyo ulivyokuwa ukimjadili Salama moyoni mwa Rais Mabandu. Utulivu mkubwa alionao huku akiwa anamtazama mkewe, ulikuwa ni wa kupisha mjadala huo.

“Inamaana hujanisikia?” akahoji tena akiwa ameinama kidogo kisha kukirudisha kichwa chake mahala pale.

“Kuhusu nini?” swali la kukera likamtoka Rais, swali ambalo lilikwenda likapandisha ghadhabu za mkewe na kuja juu, lawama zikashushwa, akafikia hatua ya kusema kuwa huwenda anampango hata wa kumuuwa kwani hali ya maisha yao tangu bwana huyo kupata madaraka hakuilewa kabisa. Lawama hizo zikaleta masikitiko makubwa usoni mwa Mabandu lakini moyoni alitabasamu kisha tabasamu hilo likabadilika na kuleta hasira. Moyo wake ulivimba kwa chuki dhidi ya mkewe. Wewe kidudu mtu, mg’ata na kupuliza usiye na nia nzuri na Taifa hili bila shaka, nini kinachokufanya kushusha lawama kwangu? Akauliza moyoni akiwa amebadilika lakini uso wake ulikuwa bado upo katika hali ya kupoa juu ya lawama zile.

“Hivi Salama mke wangu, unajua ni jinsi gani nilivyo na mapenzi mazito dhidi ya binti yetu….!”

“Najua mume wangu lakini ulipaswa kuniambia mahali alipo si kwa kufanya maamuzi ya pekee hii si sawa” akakatishwa kauli Mabandu.

“Nimekuelewa lakini tambua kuwa hali ya nchi kwa sasa si shwari, kifupi imechafuka, hakuna wa kumuamini humu hata Panya kama wamo. Naomba jambo hili tukalizungumzie mahali” akaweka ombi muheshimiwa Mabandu. Salama akalipukwa na furaha kubwa moyoni mwake na kujua kuwa kila kitu kinakwenda kuwa wazi na alipanga kumuuliza hata habari za kuhusu mpelelezi huyo ambaye anasumbua Ungamo. Alichelewa Rais Mabandu yule aliyekuwa akimjua yeye alikuwa si huyo hata kidogo. Huyo alikuwa ameamua kuuweka upole na hofu pembeni na kukaa kwenye nafasi yake ya kweli kama Rais. Mipango yake ilikuwa ni kumuweka pabaya mkewe na kumkamua siri zote kisha kutafuta mbinu mbadala za kuweza kumhukumu nazo. Kitu ambacho kilikuwa ni fumbo kubwa kwa mkewe huyo. Kabla ya kutoka humo ndani, Rais alipiga simu na kuomba msafara wa magari mawili tu kisha akasema.

“Tafuta hoteli yenye hadhi ya juu nataka kufanya kile nilichokupa habari yake” akairudisha simu. Wakatoka taratibu huku Salama akijiona hii Ikulu inzima atakwenda kuitawala yeye kama mfalme fulani baada ya muda pindi Mobande Julio atakapo ingia ndani humo. Mwendo wake, maringo yake hata na majigambo yake vilikuwa ni vyenye kupitiliza mno na kwenda kuzaa kiburi kizito kilichopinduka mipaka ya kufikia hatua ya kumuona mumewe si kitu.

Msafara wa magari ulikuwa tayari umekwisha kuandaliwa, yalikuwa ni magari mawili tu ambayo yalikuwa na vioo vya giza. Ndani ya gari hizo kulibebwa watu wasiozidi wane kwa idadi yao, hao walikuwa ni watu muhimu sana na ulinzi aliouamini kiongozi huyo wa nchi. Hakutaka kuwa na jopo kubwa la walinzi wa kufuatana nao kwani wengi wao hakuwa akiwaamini. Gari zile mbili hazikufunguliwa milango yake, zilikuwa zimefungwa hivyo hivyo na badala yake gari ambayo ndiyo aliyowatanguliza kina Liyambo, ikafunguliwa mlango na mlinzi wake mkuu akaingia huku mkewe akifunguliwa mlango wa upande wa pili wa nyuma ya gari ile kama Mabandu alivyoingia naye akaingia, mlango ukalokiwa. Mbele kulikuwa na watu wawili hawa hakuwaelewa kwani walikuwa wamempa mgongo kiasi cha kushindwa kujua ni akina nani. Hawakuwa watu wale watumiwao na Rais kwa ajili ya safari zake zile azijuazo. Hao walikuwa ni akina nani? Akajiuliza.

Si hivyo tu bali hata gari iliyotumiwa na Raisi haikuwa ile iliyozoeleka. Hili lilimchanganya sana, kwa kiongozi kama Rais anayehitajika ulinzi wa kutisha leo anasafiri kwenye gari ambayo yenyewe haina ulinzi binafsi yaani vioo vyake havikuwa Bullet pruff. Kichwa chake hakikuwa sawa. Gari zikaondoka Ikulu kwa kasi huku nyuma kukiwa na gari ya asikari ya kuzugisha ambayo ilikuwa ikifuata nyuma lakini baada ya kona kadhaa ile gari haikuonekana tena. Hapo ndipo hofu ilipoongezeka kwa Salama, akatamani apige simu lakini akakosa nafasi.

“Wapi mkuu?” swali kutoka kwa Insp. Bogo ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari hiyo kwa kasi kubwa akauliza huku akigeuka nyuma kiasi. Sura yake ikaonwa na Salama. Mungu wangu! Moyo wake ukampasuka, Bogo, huyu si mpelelezi kwenye jeshi la polisi, alimjua vema. Sasa hapo yupo kwa kazi gani, hilo akalifanya liwe ni jambo la kulijengea mashaka zaidi.

“Huku kuna hoteli kweli Mabandu?” akauliza kwa hofu na kujikuta akisahau kumuita mtu huyo kwa heshima yake kama mume au muheshiwa. Hofu ile changa sasa ikawa ni yenye kutengemaa. Hakujibiwa, Rais Mabandu akawa ni mtu wa kutabasamu kila wakati huku macho yake yakifumbafumba kwa utamu ama uhondo wa kasi nzuri ya gari ile ambayo kwa mbali ilikuwa ikiyalazimisha macho yake yapokee mzinzio wa kausingizi uchwara.

“Fuata hiyo gari iliyokupita sasa hivi?” Mabandu badala ya kujibu swali la mkewe badala yake akajibu swali la dereva wake ambaye kwa wakati huo alikuwa ni Insp. Bogo. Hii ilitafsiriwa kama dharau kwa Salama huku akisahau kuwa dharau mbichi aliianza yeye. Shuwaini. Akaanza kuhangaika pale kitini mara atazame mbele, mara ageuke nyuma, kule walikokuwa wakielekea kulikuwa hakuna hoteli wala ndugu wa hoteli. Walikuwa wamekwisha kuiacha lami siku nyingi sasa gari zile zilikuwa zikifuata barabara ya vumbi. Ile maana ya ‘nitafutie hoteli yenye hadhi aliyokuwa akihitaji muheshimiwa kumbe ilikuwa ni hiyo. Makubwa.

Gari zile tatu zilisimama mbele ya nyumba ndogo iliyo ndani ya uzio mkubwa, nyumba hii ilikuwa ikiishi mifugo tu kama Kuku na Nguruwe. Mlango wa muheshimiwa Rais ukafunguliwa na Liyambo na Inspk. Bogo pia walishuka akaachwa Salama pekee mule ndani.

“Mteremsheni na huyo mtu humo ndani” akaagiza Rais kisha akatulia kuyatazama yale maeneo kwa uzuri. Salama akashushwa, akaaza kutamba kwa vile awezavyo lakini mitambo yake ilikuja kukoma kwa maneno machache tu aliyoyatoa Rais Mabandu.

“Unaweza ukahujumu vinginevyo lakini kamwe huwezi kuihujumu Ikulu” kauli hii ilimtoa macho kweli kweli Salama akasema.

“Unataka kuniambia mimi huniamini mume wangu?”

“nakuamini sana mke wangu na ndiyo maana nimekuleta uje kuishi huku hadi useme kila kitu kuhusu hao unaokula nao njama”

“Kina nani sasa?”

“Mimi sijui na kama ningelikuwa najua nisingelikuleta huku, na yote haya yameletwa na mitego yangu niliyoitega mara baada ya kuona unaanza kupewa onyo na watu unaoshirikiana nao juu ya Taifa hili. Umeuwa mtu niliyemtuma akuchunguze kwa siri bila kujua kuwa ule ulikuwa ni mtego mbaya sana nimekuwekea. Mtu niliyempa kazi alikuwa hana taaluma yoyote ya upelelezi na mapigano bali nilimpa kutokana na ujanja ujanja wake, kama ungemuacha bila kumgusa, mngenisumbua sana kuwajueni lakini kitendo cha kumuuwa halafu msivyo na akili mkajitapa kuwa tumemuuwa. Zama zenu zimefika sasa. Mabandu yule mliyekuwa mnakaribia kumtia upofu, amegeuka na kuwa mwingine, ngoja tuone mwisho wa mchezo utakuwaje” aliongea muheshimiwa huyo kisha akatoa amri ya kukung’utwa kwa kila kitu alichokuwa nacho huyo mwanamke. Kifaa maalumu cha kuchunguzia kikapitishwa. Alikamatwa na bastola ndogo ya kuweza kuificha hata kwenye makalio na vitakataka vingine. Amri moja ikatolewa ya kumuweka ndani ya kijumba kile kidogo maalumu kwa ajili ya mapumziko ya muda fulani kisha waanze kumuhoji bila huruma hadi aseme. Kazi hiyo na nyingine zinazofanana na hizo akapewa Insp. Bogo kijana makini. Gari mbili zikageuzwa na kurudi zilikotoka lakini moja ikabaki. Watu wawili wenye silaha kali ukimuondoa Bogo, wakabakishwa kwa ajili ya ulinzi wa binti huyo. Wakati gari zinaingia Ikulu, ile gari ya polisi iliyokuwa nyuma hapo mwanzo nayo ikaingia kama vile ilikuwa pamoja kwenye msafara ule kumbe ile ilikuwa ni geresha tu.

Frank kichaa alifika mahali kwenye tukio akakaa mbali kidogo ya lile eneo huku akiwa anajivuta taratibu. Haikujulikana ni wapi pikipiki alilitelekeza. Mwendo wake na jinsi alivyojiweka ilikuwa ni ngumu sana kumjua lengo lake kwa haraka. Mkononi alikuwa amekamata jifuko chafu lililojaa chupa na takataka nyingine. Hakuwa amevaa viatu wala kandambili, ailikuwa yeye na pekuwa pekuwa na miguu yake. Akafika hadi kwenye umati wa watu, akalitupa fuko chini na kusimama huku akijichekesha akiwa anatazama mbali kabisa na tukio kana kwamba kuna habari ya baba wa Taifa ile iliyokuwa ikirindima kipindi cha nyuma mbele ya wanajeshi wa jeshi la Tanzania ambayo ilikuwa ikiwahamasisha wanajeshi hao jinsi ambavyo wameshindwa kumvumilia Nduli Amini na walikuwa wakipokea hamaso la kuwa sasa achapwe. Kicheko chake hakikuwa na sauti, hiyo ilimfanya aweze kusikia kile kilichokuwa kikizungumzwa na mashuhuda wa tukukio lile.

“Wameuwawa kwa kupigwa risasi!” akasikia sauti moja ikitoa taarifa kwa mtu aliyechelewa kufika mahali hapo kama yeye. Akapata picha kuwa waliouwawa walikuwa wawili.

“Hata sijui ilikuwaje, sisi tulisikia tu mlio wa kwanza wa bunduki baada ya muda tena ukasikika wa pili ndipo tukapiga simu polisi huku tukija huku baada ya kuona umati mkubwa wa watu ukija huku” yule shuhuda ambaye alikuwa ni jirani na kampuni hiyo kama maelezo yake yalivyosikika, akazidi kuongea alichokisikia awali. Frank kichaa akajua kuwa hakuna ambalo angeng’amua juu ya waliofanya mauwaji hayo.

“Masikiniiii!” sauti za watu zikasikika kwa umoja wao, Frank kichaa akageuza shingo yake kutazama kule ambako kulikuwa na mlango wa kuingilia ndani ya kampuni. Miili miwili ilikuwa ikitolewa ndani ya kampuni ile. Sauti za vilio vidogo vya akina mama na akina dada wenye uchungu dhidi ya watu ambao hawakuwa na hatia kuuwawa, vilisikika. Chozi zito la uchungu likamtoka Frank kichaa. Alikuwa akilia kwa ndani ya moyo kijana huyo.

“nimeshuhudia, kweli wamekuuwa, nami sina budi kuwauwa. Mungu ananishuhudia jinsi ninavyolia mbele yako basi na ashuhudie jinsi nitakavyo fupisha maisha yao. Sitakuwa na makosa kwenye hilo kwani wahenga walisema kuwa auwaye kwa upanga naye hufa kwa upanga. Na pia kupitia maneno ya vitabu takatifu pia kuna maneno haya kuwa Fisadi anayefisidi uhai wa mtu asiye na hatia naye auwawe vivo hivyo. Sina hakika kama haya nayatoa kichwani mwangu kutokana na hasira au ni kweli yapo na yalishazungumzwa, sijali, nitauwa kwa hili na ninaanza na yeyote nitakaye mkuta mbele yangu mwenye kushiriki haya” alisema Frank kichaa kwa uchungu mkubwa sana akaondoka kwa kasi ya hatari huku akiwa amekamata fuko lake la taka. alipita chochoro ile na hii akaja kutokea kwenye kichaka fulani hivi akashusha mizigo yake na kukaa chini. Alilia sana kwa uchungu mzito, kilio chake kilikuwa kilio cha mengi, aliwalilia wazazi wake na alilia hivyo kwa sababu yule mtu aliyetaka awe shuhuda wa kuyaona malipizi yake juu ya watu waliosababisha maisha ya wazazi wake kuwa mafupi, ndiyo ameuwawa naye. Ni nani atakuwa shuhuda sasa. Alikuja kusimama kisha akasema.

“Nisamehe Mungu wangu kwa kila baya nitakalo kwenda kulifanya lakini naamini wewe pekee ndiwe shuhuda wa kila jambo. Wakati Frank kichaa akiwa anashahadia kwa Mungu, huku kwa Dou mambo yanapamba moto.

Mtego wa Dou ulikuwa bado upo katika kutegwa kwa mtindo wa kipekee sana na mtego huu ulikuwa wa tofauti kuliko mitego mingine. Roi alikuwa yupo katika kutegwa pasipo mwenyewe kujua na mtego huo ulikuwa mitaani. Picha za Roi aliyekuwa akiitwa shujaa aliyefanya TN RACE kuchukua nafasi ya kwanza kwenye mashindano ya Afrika mara baada ya kuiangusha kampuni ya Black Skeleton ya Don Dou ambayo ilikuwa ikitaka kushinda kitemi, zilikuwa zikisambazwa kwa kila kijana, mama dada, kaka na watoto wenye kujitambua. Picha hizo zilikuwa ziko na dau kubwa la pesa, likawa kama shindano bubu ambalo liliibukia maskani na kuja kwenye majumba ya watu. Dou alifanya hivyo kwani alijua fika kuwa mtu huyo anafahamika na wengi na ni mtu anayepita kwenye mitaa mingi hivyo kwao ni rahisi kujua chimbo zake na kumuangamiza. Juu picha, chini ya picha namba za simu na dau la shilingi laki tano (500,000). Kwa yeyote atakayekuwa wa kwanza kumtia machoni kijana huyo maarufu kisha kutoa taarifa kwa namba hiyo, basi utakuwa umejishidia kitita hicho cha shilingi Laki tano. Nani wa kuiacha pesa hiyo kwa kipindi ambacho kila mtu alikuwa na mipango yake kichwani inayohitaji keshi ya pesa na si mipango ya pesa. Kila mtu akasema mbona mimi namjua huyu jamaa, nilimuona kule siku ambayo alinisambaratishia yule bwege kibaraka wa Dou. Wengine wakathubutu kusema kuwa, anapendelea kukaa mitaa fulani, mimi namjua huyu. Hawakujua kama hiyo ilikuwa ni mipango ya Dou, hawakujua hata kidogo.

Masaa yakasonga kiajabu tangu kutolewa kwa shindano hilo la mhadao kwa vijana wenye uchu wa pesa kwa kutimiza malengo yao. Siku ya pili isiyotegemewa kwa kijana mmoja kama angeweza kuwa ni yeye ndiye mshindi, Roi asiyejua chochote kilichokuwa kikiendelea mtaani kwenye vijiwe vya vijana. Akafika mjini kwa ajili ya kufanya mambo fulani ya siri, aliposhuka tu garini, akaonewa na kijana huyo. Simu ambazo baada ya shindano hilo bubu kutangazwa, vijana wengi wakaingia ubia na mitandao kwa kuzijaza simu zao salio kila wakati ili tu kama wakikutana na kijana huyo, tatizo vocha isiwe kikwazo. Simu ya kijana huyo haraka sana ikawekwa sikioni na muda mfupi ikapokelewa na upande wa pili. Akasema kuwa kijana huyo yupo mjini mtaa, akataja na hadi sehemu alipo. Akahitaji pesa yake lakini hakujibiwa kuhusu hitaji la pesa yake baada ya kuwa wa kwanza kutoa hizo habari za kumuona kijana huyo makini na maarufu kwa kumsaidia Tamimu na kampuni yake. Alichokisikia kijana huyo kwenye simu kabla ya kukatwa ni ‘Bingo’. Akajiuliza ‘Bingo?’ Kivipi? akajaribu kupiga tena, simu haikuwa hewani tena na alijibiwa kabisa kuwa namba hiyo haipo. Moyo wa huyo kijana ukauma sana kwa kukosa pesa aliyoikusudia lakini kuna kitu cha ajabu sana alikipata kichwani mwake kwa muda huo nacho ni maadui. ndiyo, huwenda hao walikuwa ni wafuasi wa Dou ambao walishindwa vibaya sana na kuuliwa mwenza wao sasa wanataka kulipa juu ya kijana huyo. Akapata wazo la kumkabili kijana yule ambaye picha yake alikuwa nayo lakini akahisi huwenda si sahihi. Mabishano kati ya nafsi yake na macho yamuonayo kijana yule ambaye huwenda akawa matatizoni muda wowote kuanzia muda huo. Muda huohuo akasikia sauti za gari zikija kwa kasi sana eneo hilo. Kijana huyo akakimbia alipo Roi akampatia ile picha kisha akaelekeza zinaposikika sauti za muungurumo wa gari zinazokuja kwa kasi. Alikuwa amepata kigugumizi cha ghafla sana kutokana na kitu kile alichokisababisha. Roi alikitupia macho kile alichopewa kisha akatazama sauti za magari yanayokuja. Alichelewa kufanya kitu kwa muda huo. Risasi zikaanza kurindima kama mvua eneo hilo bila kuangalia watu wanaohusika wala wasiohusika. Roi alijitupa chini akabingilia hadi alipokuja kugeuka na kusimama alikuwa tayari mikononi mwake akiwa na bastola mbili. Akaanza kupeleka majibizano kwa kasi kubwa. Kundi la wale watu waliovamia lilikuwa kubwa sana tena sana hadi akapatwa na mshangao. Hakuchoka kupeleka majibizano. Aliwadondosha kwa wingi sana pamoja na wingi wao lakini walijuta kuja eneo hilo.

“Nipo duka la vipuli vya magari hapa mjini, nimefanyiwa ambush” alisema Roi alipokuwa amepata upenyo wa kuweza kupiga simu mara baada ya kuona kuwa zana zake zinakwenda kuisha risasi.

Simu aliyopigiwa Petii, ikamfanya anyanyuke alipokuwa amekaa kule kwenye nyumba ya siri na kuchukua silaha za kutosha kisha akapanda gari na kuingia barabarani kwa kasi kubwa. Roi alikuwa amefanikiwa kuwaangusha sana lakini kutokana na wingi wao, akawa amefeli kuwamaliza. Risasi zilikuwa zimekwisha kabisa. akajificha nyuma ya gari akiwa anasubiri muujiza wa Muumba tu hapo uweze kutokea. Alitoka kiaina sana nyumbani hakuwa amebeba silaha nyingi zaidi ya mbili tu za kujihami. Risasi zikaanza kuvuma tena kama mvua na kuichakaza ile gari na kuifanye ibaki matundu. Risasi moja ikauchapa mkono wa Roi na kumsababishia maumivu makali, alilia kwa sauti moja ya uchungu kisha akanguka chini. Alijua kama atajitokeza na kujisalimisha ni wazi asinge pona. Akalala chini akiugulia maumivu na kutulia kimya. Wale jamaa walikuwa wakipiga hovyo huku wakisonga mbele hadi walipomkaribia.

“Aisee yuko hapa chini amedondoka!” alisema mtu mmoja kwa sauti ya juu akiwajulisha wenzake.

“yupo hai au amekufa?” akauliza mwingine.

“Anapumua bado”

“Ni vema, anatakiwa afike kwa Dou akiwa hai” alisema huyo mtu. Roi akanyanyuliwa kutokea pale chini akapigwa ngumi nyingi nzito zilizomfanya kuteuka damu kisha akapakizwa kwenye gari akiwa kalegea. Hakuweza kuthubutu kurusha ngumi kwani watu wale wenye silaha hawakuwa na huruma hata kidogo. Akaamua kutulia na kuangalia nini kingeweza kujiri. Msafara wa kumtoa pale Roi ulimfikisha kwenye nyumba ya Don Dou ambayo ilikuwa mafichoni. Huko akahifadhiwa kwenye chumba kibaya akisubiri hatima ya kufikishwa kwake pale. Maumivu ya kuchanwa nyama za mkono na risasi bado yalikuwa yakimsumbua sana.

Petii alifika kwenye tukio akakuta umati tu wa watu lakini wahusika hawakuwepo. akapiga simu ilikuwa haipatini. Akajua Roi ametekwa. Akasogea kwenye kundi dogo la vijana mashuhuda wakasema kuwa, wameweza kuona wale jamaa kuondoka na kijana huyo. Petii alirudi garini akiwa kachanganyikiwa hakujua ni kwa namna gani angejua mahali alipopelekwa huyo kijana. Petii alirudi nyumbani na kutulia kitini akiwa hajui moja wala mbili lakini kuna kitu alikumbuka nacho ni kuhusu mtu ambaye yuko nyuma ya Roi ambaye mara nyingi walikuwa wakiwasiliana kwa simu ya siri. Akazama ndani ya chumba ambacho marachache sana alikitumia kufurahia penzi tamu na Roi hasa wawapo mazingira hayo. Akasachi sehemu muhimu akaona kifaa kidogo mfano wa simu ndogo, akakichukua. Kila alivyojaribu kuwasha kifaa kile hakuweza, alilifanya zoezi lile kwa muda mrefu sana hadi akachoka kabisa na kuamua kuacha lile zoezi akijipa muda wa kutafakari njia nzuri ya kufanya liwezekanalo.

Mitaa yote ilijaa habari za kutekwa kwa Kijana ambaye wao walidhani wanacheza mchezo wa kuzidi kumpa sifa huyo kijana pindi wanahamasishwa kuingia kwenye lile shindano, kumbe ulikuwa ni mtego wa kuweza kumkamatisha pasipo kujua. Vijana walikaa kundi kwa makundi wakijadili kile ambacho kilitokea, wakajiuliza mengi sana hivi ni kweli wamewezaje kuingia kwenye shindano lililokuwa fumbo kubwa kwao. Wameshiriki shindano pasipokumjua mtengenezaji wa shindano hilo kwani kila kijana alisema kuwa amefuatwa na mtu wa hivi, mwingine vile. Hakukuwa na mtu mmoja ambaye kwao wangeweza kumpata kirahisi na kumbana. Walikiri kuwa wamemuuza mtu.

Habari za kukamatwa kwa Roi zikammkuta Frank, akapata picha zilizokuwa zikisambazwa mitaani. Akachoka. Akarudi mitaani kwake kwa ajili ya kufanya uchunguzi Ilikuwa ni lazima afanye chunguzi na amrudishe Roi kazini kabla mambo hayajawa mabaya. Pitapita yake mitaani, ikamfikisha kwenye vikundi kadhaa vya vijana waliokuwa kwenye majuto makubwa mno japo vijana hao hawakujua ni nani kati yao aliyetoa taarifa. Huu mpango ulikuwa kabambe sana. Aliwaza Frank kisha akapita kwa mtindo aujuao mwenyewe akatokea nyuma ya mtaa ule, huko akashika ujia uliompeleka hadi kwenye baa kubwa kabisa, hapa akakaa nje kusubiri jambo. Si mara ya kwanza kufika hapa hii ilikuwa yapata mara ya tatu ama nne, ila safari hii alikuja maalumu kwa kazi moja nayo ni kujua chanzo cha tukio lile. Alishajua kuwa kuna watu wamemwagwa kila kona kwa ajili ya kumtafuta Roi, sasa hapo alitaka kuwa na uhakika je, kuna habari yoyote ambayo itampeleka mahali husika. Huyo alikuwa ni Frank. Umaarufu wa baa hiyo kubwa, ulifanya ipokee watu mbalimbali maarufu na wasio maarufu, watemi na wale ambao walikuwa hawatabiriki. Alikuwa amesimama kwenye ukuta mfupi wa baa ile huku akiweka umakini mkubwa kabisa. Umakini wa yeye mwenyewe pia umakini wa kusikiliza jambo.

“Hivi tunaweza kumpata huyu jamaa kweli, ni wiki sasa tangu tuwe hapa lakini hata dalili hakuna” aliongea mtu mmoja ndani ya baa ile, Frank akazunguusha jicho lake lenye nguvu na kupata kumuona mtu aliyesema lile.

“Hatuwezi kutoka hapa hadi tujue mwisho wa hili, hii ni amri si unajua” aliongea mwingine.

“Daaah!” mmoja kati ya wale vijana watatu akaonesha kuchoshwa lakini yule ambaye alisema kuwa hapo hawatakiwi kutoka hadi kieleweke, akapokea simu iliyokuwa ikimsumbua kwenye mfuko wa suruali yake, akaiweka sikioni na kusikiliza. Mwishoe anatamka neno moja tu la hakuna shida kiongozi kisha anaishusha ile simu.

“Hapa hatutakiwi kuwepo tena, windo letu limekamatwa lipo kwa jamaa mmoja sijui anaitwa Dou sijui nani na mpango ni kwenda huko ikiwezekana kumchukua. Ila sisi tumeambiwa turudi kambini hadi Boss atakapotoa agizo” aliongea hivyo huyo mtu, vijana wale wakanyanyuka na kuondoka lile eneo kwa hatua za taratibu. Frank akafuata nyuma na hakuna aliyemtilia mashaka kichaa yule hata kidogo. Msafara ule haukutumia usafiri wa gari wala pikipiki kutokana na mahali walipo na kambini kwao kuwa karibu. Frank alikuwa akifuata kanuni zote za mtu aliyekichaa lakini akili yake ilijua nini inafanya. Ufuataji wake kama asingelifanana na kichaa, angelikwisha dunguliwa zamani sana na wadunguaji makini wa kambi ya BBD ambao wanafahamika kama Mbega. Sema tu ni nani ambaye angethubutu kupoteza risasi yake ya gharama kumdungua kichaa kama yule. Laiti wangalijua kuwa huyo si kichaa bali kuna kitu amegundua kwao na kitakwenda kuwagharimu, wasingeli cheza naye hata kidogo.


Kilio cha maumivu makali kiliendelea kusikika ndani ya jumba la maajabu, jumba ambalo Tereza alihifafhiwa, kile kitendo cha kuingiliwa kimwili ndicho kilichobadili mfumo mzima wa mwili wake, tumbo kubwa lililokuwa likikuwa kila siku lilikuwa limeumuka vya kutosha kiasi kwamba kama unapitisha kitu chenye ncha kali, lingeweza kupasuka na kupiga mzinga, lilikuwa limewamba haswa. Tumbo hilo hilo ndilo lililokuwa likimletea maumivu makali kiasi cha kushindwa kukaa wala kusimama, Tereza maisha yake mapya yakawa ni kulala kitandani kama mgonjwa wa mahututi.

“Mungu wangu nakufa mimi, nakufa eeee, mamaaaaaaaaaaaa!!!” alipiga kelele kubwa akilitaja jina la mama yake aliyoko kuzimu, alitamani afe sasa na siyo kuishi tena. Utanisamehe sana kwa kukuchagua wewe kuwa mtu wa kubeba kiumbe ambacho ni mkombozi kwetu, najua utapitia kwenye maumivu makali ambayo hukuwahi kupitia lakini nasi tutakurudishia furaha siku moja. Alikuwa akiyakumbuka maneno aliyokuwa akiambiwa na kiumbe ambacho hakuwahi kujua kama ni binadamu au jini maana hakikuwahi kumtokea kikiwa kamili, siku zote kilikuwa kikiishi ndani ya mwanga mkali uchezao mithili ya mawimbi ya maji. Hapo hapo kukasikika kelele za vilio vikali sana, vilio hivyo vikamfanya kukunja sura yake na kupambana na maumivu yake kwani hakutaka sauti yake ichangamane na sauti za vilio vile. Vilio vilikuwa vikali vya kupokezana, vikilia hivi kabla havijaisha, vinaibuka hivi. Ilikuwa ni hali ya kutisha si kidogo.

“Mkombozii, mkombozii,!!” hizo zilikuwa ni miongoni mwa sauti za ajabu zilizokuwa zikisikika. zilipokuja kukata zile sauti, Tereza akaanza kuvuja damu kutokea sehemu za siri, damu nyingi sana iliyomfanya abaki akiachama kinywa chake. Damu ambayo hakuwahi kuiona kabla, damu nyeusi tiii! Tena nyeusi kweli. Hali ile ya kuvuja damu ikapunguza yale maumivu. Akajua sasa ule muda wa kuingiliwa umewadia kwani tayari ilikuwa imeshatimu siku ya saba kama ada ya sheria zake za jumba hilo. Ilikuwa ni lazima aingiliwe ili mtoto akuwe kwa ukuaji ule wautakao wao.

Bado watu walikuwa hawaelewani hata kidogo ndani ya himaya ya Dr. Lee. Bencov alitaka kujua binti wa Backa amekimbilia wapi, hakutaka kitu kingine aliamini huenda bwana huyo akawa amemtorosha binti huyo. Kelele zake zilikuwa zikimpa hasira sana Dr. Lee kwani hata yeye mwenye anaumiza kichwa muda wote kwa ajili ya swala hilo.

vijana walitumwa kila eneo kwa ajili ya kumtafuta lakini majibu yalikuja kuwa hawakufanikiwa kumuona, hili lilikuwa likimchanganya kila mmoja.

“Tambua kuwa hawa wamekuja hapa kwa ajili yangu, Backa na baba yake walitakiwa kufa kwenye mikono yangu na si vinginevyo” aliwaka Bencov akiwa mwekundu kwa hasira kali.

“Najua Bencov lakini tambua kuwa sote tunaona jinsi vijana wanavyoleta majibu hasi ya kuto kumuona huyo binti kila mahali sasa mimi nifanye nini” alijitetea Dr. Lee. Bencov alichomoa bomba la bunduki kisha akaishika vizuri na kusema kuwa anakwenda kumuangamiza Backa muda huo huo. Aliikamata bastola ile ya maangamizi ambayo inapoteza kabisa ushahidi kwa muda mfupi mtu akipigwa nayo. Wote pale wakabaki kumshangaa kwa macho ya kuuliza lakini hawakupata muda huo. Bencov akazama ndani na kukifuata chumba cha Backa, wakati anagusa tu mlango wa chumba hicho, simu yake ya siri ikaita. Akasitisha zoezi la kufungua mlango akapokea simu.

“Boss, Yule kijana muuwaji amekamatwa na kikosi cha Rais wa zamani bwana Julio mobande na wamegoma kutupatia yule mtu wanadai wanataka kumtesa akiwa mikononi mwao na kumuuwa” ilisikika sauti ya upande huo wa pili. Hilo jambo likamharibu kabisa, inakuwaje watu walioko chini yake waweze kuwa na kiburi kiasi hicho. Wao ni kama nani.

“Hao wafu watarajiwa hawawezi kuwa na kiburi kiasi hicho, nakuja mwenyewe kesho na wataniambia” aliongea Bencov kisha akarudi mbio hadi alipowaacha wenzake.

“Beda, tunaondoka muda huu kuelekea Ungamo, Dr. Lee hakikisha vijana wako wanajua huyu binti alipokimbilia na ikiwezekana, no siyo ikiwezekana. Nataka wamlete akiwa hai na nimuuwe pamoja na baba yake. Naelekea Ungamo kwenda kumuuwa Roi, yupo kwenye mikono ya watu wangu tayari” alisema Bencov. Yale maneno ya kusema kuwa Roi yupo kwenye mikono ya watu wake, yakamuacha Dr. Lee na Lady Devil wabaki vinywa wazi, vichwani mwao walikuwa na maswali yanayowiana, hivi kweli akiyekamatwa ni Roi au wamemfananisha lakini hawakuwa na jibu. Bencov na mlinzi wake aliyejichora matatuu baadhi ya sehemu ya mwili wake, wakaondoka.

“Sina hakika kama ni yule mjinga nimjuae mimi ndiyo eti, amekamatwa, hawa watakuwa wamemfananisha tu” alisema Merina. Dr. Lee akamgeukia Merina na kumwambia.

“Ngoja tuone”

UNGAMO, JIJINI PANDE.

Gari za kifahari zilikuwa zikitimua vumbi zito maeneo ya Muavengero Kaskazini, kwenye majumba ya watu walioshiba utajiri wa pesa na baadhi ya wanasiasa. Kasi zile za magari yale, zilikuja kukomea kwenye kasri moja kubwa sana. Hiyo ilikuwa ni jioni ya siku ambayo Bencov aliingia na ndege ya shirika la Ethiopia kutokea nchini Madagascar. Watu watatu walishuka kutokea kwenye gari mbili tofauti, Bencov alishuka kutokea kwenye gari ya mbele akiwa na kijana wake wa kumlinda, Bacon yeye alishuka kwenye gari ya nyuma akiwa pekee mdomoni akiwa na pisi kubwa la sigara yenye kilevi. Wakazama moja kwa moja ndani ya lile kasri wakipishwa na walinzi ambao walikuwapo hapo kutengeneza ulinzi. Walifika ndani na kumkuta Julio Mobande akiwa na Kitema kama mlinzi wake, pia kulikuwa na Bande Sir pamoja na Jarome. Wakakaribishwa kiti wale mabwana wakakaa kisharishari.

“Sina muda wa kupoteza kwenu, nadhani sasa mnataka kuharibu utaratibu kwa kwenda kinyume. Nini mnafanya? Nadhani mnajua kuwa huyu mbweha mweusi aliniulia vijana wangu na nikaapa kumtafuta popote pale sasa iweje ninyi mnae na hamtaki kunipatia?” aliongea kwa jeuri kubwa Bencov. Julio akagusa pua lake kidogo kabla ya kusema kuwa.

“Huyo kijana amekamatwa na Don Dou na wamemshauri sana amtoe kwa vijana wako lakini amegoma katakata na amesema huyo kijana amemkamta yeye na yeye ndiyo mwenye maamuzi ya nini amfanyie. Amesema kuwa Roi amemfanya kuukosa ushindi wa kuwa mmiliki wa nafasi ya kampuni yake kushiriki mashindano makubwa ya dunia kwa sababu yake, pia hiyo haitoshi amemuulia kijana wake na kusabisha yeye kuswekwa rumande, hawezi kumuachia na atamuuwa mwenyewe kwa mikono yake” alitoa maelezo Julio Mobande.

“Huyo Dou yupo chini ya nani?” akauliza Bencov.

“Yupo chini yangu na mimi ndiye niliyefanya mpango wa kumtorosha mahabusu” alijibu Julio.

“hainingii alilini mtu aliye chini yako awe na maamuzi na amri ya kukupinga, nijuavyo mimi wa chini anafanya kazi kwa ajili ya wa juu….Iko hivi, tunakwenda kwa Dou kumchukua kuyo mtu mguu wenu, mguu wangu” aliweka amri Bencov hadi Bande Sir akashangaa.

Tukirudi upande wa pili wa karata tunamuona firs Lady akiwa kwenye mateso makali ya kutakiwa aseme kila kitu anachokijua kuhusu washirika wake. Ubishi wake unapelekea hadi Insp. Bogo kupewa amri na Rais ya kuto kumuonea huruma hata kidogo. Kichapo kikawa kinashuka kwa kila swali alilokuwa akiulizwa huku akitakiwa kujibu kwa vile ajuavyo.

“Unatakiwa uelekeze kila kitu kuhusiana na watu wako”

“sijui kitu mimi mnanionea bure” alijibu Salama lakini hapo kipigo cha kuogopesha kutoka kwa Insp. Mwenye hasira kikashuka. Alipigwa ngumi mbili moja ya kifua moja ya mdomo, damu zikawa zinamtoka kama bomba la maji. Haikutosha, alipigwa kofi moja la uso lililomlete maluweluwe ya nguvu sana hapa sasa akaona kifo hakiko mbali, heshima yake kama mke wa Rais haikuwa ikiheshimika tena. Akadiriki kusema kuwa yuko radhi kutapika kila akijuacho. Akatapika na kusema kila kitu hadi ile ya siri aliyofichwa Dou. Kijana huyo haraka sana akapiga simu kwa Raisi kusema kile alichoambiwa na mkewe. Raisi akashtuka sana tena sana kwani hakutegemea kusikia hizo habari kuwa mkewe angeweza kushirikiana na watu hatari kiasi kile lakini wakati akiwa anayapishanisha hayo mawazo akilini mwake, akapokea simu iliyokuja na taarifa kuwa mpelelezi kutokea Tanzania ametekwa. Kazi hiyo moja kwa moja ikatua kwenye mikono ya Bogo akiambiwa yule mwanamke amuache kule kule kwanza ajifunze kitu. Bogo akafunga safari kuanza kuchunguza mahali alipohifadhiwa Roi ili ijulikane kama ni mzima au amekufa.

Frank baada ya kugundua kuwa ngome moja ya watu wanaoharibu amani ameiona, alinoti kwenye kitabu chake cha kumbukumbu. Kisha akaapa kuwa kupitia pale ataanza uchunguzi wake wa kimyakimya. Alilifuata pikipiki lake kubwa na kubadili muonekano kidogo kisha akalipaki mahali ambapo ni njia panda kutokea kwenye ile ngome ya BBD na kulikuwa hakuna njia nyingine ya kupita pasi na hiyo. Pale akawa anashuhudia kila tukio na kila msafara unaotoka ndani ya ngome na kuingia. Hata msafara wa Bencov kutokea uwanja wa ndege aliuona lakini wakati huo huo kabla hata hajameza mate, msafara ule ulipita tena kwa kasi kubwa. Akaujengea mashaka, mashaka hayo yakapelekea kuanza safari ya kuufuatilia nyumanyuma. Aliufuata ule msafara hadi mahali ulipoishia pasipo mtu yoyote kugundua. Hakutaka kutoka mahali hapo akatulia mahali na kusuburi nini kingeweza kujiri. Baada ya subra za kusubiri kwake, aliwaona watu wakitoka mule ndani ya jingo ambalo hakuwa akijua nani mmliki wake. Jingo ambalo lilitangaza thamani ya kupotea kwa pesa nyingi katika ujenzi wake. Macho yake alihisi labda yalikuwa yakimdanganya labda juu ya kile alichokuwa akikishuhudia. Watu weupe watatu walioingia ndani ya jingo lile, walitoka wakiwa si wao pekee bali kuliongezeka tena watu watano ama sita. Kati ya wale watu walioongezeka, wawili aliwafahamu, Rais wa zamani Julio Mobande Julio akiwa na mlinzi wake Kitema, hawa aliwafahamu sana na alikuwa akiwatafuta kwa udi na uvumba huku nao wakimtafuta. Inamaana hapo ndipo waishipo watu hao. Akawaza. Kisha akashuhudia msafara ule ukitoka pale kwa kasi kubwa, gari ziliongezeka mbili nyingine na kufanya msafara ule kuwa wa gari nne. Frank kichaa akaunga tela kimya kimya kama ada yake. Na msafara haukuwa mrefu sana wakaingia kwenye nyumba nyingine ya wastani. Frank akaweka tuo mahali kusikilizia. Akiwa ametulia pale kuna mtu alikuja akiwa kwenye nguo ndefu ya kofia akamtupia Mwanasesere mdogo kisha akamwambi afanye chini juu Mwanasesere ule uingie ndani ya lile jingo, hiyo ndiyo njia pekee iliyobakia ya kumuacha huru Roi.

TURUDI NYUMA KIDOGO.

Akili ya Petii ilikuwa kama inataka kuganda kwa namna alivyochanganywa na ile hali, afanye nini likawa swali kichwani mwake. Aligeukia tena kile kifaa ambacho ndicho kilikuwa ni msaada pekee. Akafikiri kwa muda wa kama dakika mbili tatu akapata jibu na kujiona kuwa ni mtu wa namna gani sasa kama atashindwa na kile kitu kidogo. Akakishika na kubonyeza kitufe kidogo cha rangi nyekundu, kile kifaa kikatoa mwanga ambao si mara moja ulikuwa ukiwaka na kukata bila majibu stahiki. Kilipozima akakibonyeza tena, safari hii kilipowaka akabonyeza na cha kijanani haraka mara alamu ikasikika kuonesha kuwa inaunganisha mahali.

“kiongozi nipe ripoti nini tatizo?” ilisikika sauti kutoka kwenye upande wa pili wa kile kifaa.

“No, siyo kiongozi, Roi yupo hatarini kwani ameingia kwenye mikono ya watu hatari sana” alisema Petii kwa hamaniko.

“Shusha ghadhabu mrembo, nipe habari hizo kwa utulivu imekuwaje?” uliongea tena upande wa pili wa kifaa hicho. Petii akaeleza kila kitu kilichotokea hadi kilipoishia.

“Shiit! Asante sana kwa taarifa nitawasiliana nawe kwa muda mfupi hakikisha hutoki hapo ndani kwani inaweza kuwa hatari kwako” ulisema upande wa pili wa kifaa kile. Petii akajibu sawa.

Amiri baada ya kupokea zile taarifa akaanza kazi ya kutafura mahali alipo huyo mtu kupitia GPS ya simu na baadhi ya vifaa vya siri, hakukuwa na majibu, hiyo ilileta majibu kuwa huwenda alifanyiwa sachi kali na kisha vifaa hivyo kuharibiwa. Alichoka, kwani kila njia aliyoitumia kumtafutia ilishindikana. Hadi inaingia siku nyingine hali ilikuwa ni ileile. Hatari ya Roi kupoteza maisha ikamjaa, akaona huo utakuwa ni uzembe. Ni ipi sababu ya kuja huku sasa kama huyu mtu akifa? aliwaza Amiri akiwa kwenye gari yake ya kazi yenye kila aina ya mitambo midogo yenye kazi kubwa, gari ambayo kama utapata kuiona na kuhadithiwa yaliyomo ndani unaweza kuhisi uzushi lakini huo ndiyo ukweli wenyewe kuwa gari hiyo ilikuwa daraja la juu sana. Hiyo ndiyo ilikuwa kazi ya Zomba, mzee wa kubuni kile apendacho. Aliunganisha mitambo Amiri kisha akamtafuta Hussein Babu moja kwa moja ndani ya kitengo. Akampa zile taarifa za kupotea au kutekwa kwa Roi na juhudi za kumtafuta alizozifanya ambazo ziligonga mwamba.

“Amiri hili jambo ni la hatari sana ujue, hiyo siyo njia ya kuitumia tena, unaruhusu mtu analala kwa siku nzima, ni makosa hayo imaaana kama wamepanga kumuuwa baada ya masaa kadhaa?” alihoji Babu akiwa kwenye hasira kali sana. Amiri alibaki kimya akijua ni kweli alikosea.

“Mtafute kwenye GPS iliyopo mwilini mwake, au hiyo nayo uliifanya?”

“Hapana mkuu”

“Fanya hivyo haraka nasi ngoja tuangalie huku lakini hakikisha unanijulisha kila hatua uipigayo”

“Ok,” alijibu kwa heshima Amiri kisha akajilaumu sana kutokulifiria hilo mapema. Alivuta kompyuta yake mpakato ya kazi kisha akaanza kazi ya kuunganisha mawasiliano yaliyopo kati ya Mfumo wa ndani ya mwili wa Roi uliounganishwa na kompyuta hiyo. Alitafuta kwa muda hadi pale hali ilipokaa sawa. Akaona kijitaa chekundu kikiwakawaka. Akakivuta na kutafuta ‘location ya alipo mtu huyo. Jibu likaja mahali alipo hadi nyumba aliyohifanyiwa na namba kabisa ya nyumba hiyo. Akawasha mtambo wa kwenye gari yake, akaingiza zile namba za nyumba kisha akahusisha na jina la mtaa kama ilivyoonekana kwenye kompyuta yake. Mtambo ule ukamletea ramani nzima ya eneo hilo. Akawasha dira, safari ya kuelekea huko ikauma. Wakati yeye anafika mahali ilipo nyumba ya Dou. Tayari ule msafara ulikuwa umeshaingia ndani ya eneo lile. Akauona hivyo akasita kwenda moja kwa moja hivyo ikambidi abaki mahali, hapo ndipo alipokutana na huyo kijana Frank ambaye alikuwa makini sana kutazama kule uliko ule msafara. Akamkumbuka, alikuwa akimuona kijana huyo mara kwa mara akiwa na Roi wakifanya kazi pamoja. Aliona uwezo wa kijana huyo katika kazi hasa kipindi alipokuwa akiwaangamiza wale jamaa waliokuwa wamewekwa kumtega Roi kwenye Hoteli ya Bi Rozi. Hapo ndipo alipomuibukia na kumpa ile kazi ya kuhakikisha Mwanasesere ule mdogo unafika ndani ya lile jingo kisha baada ya kumkabidhi yeye akarudi garini mwake.

Sauti ya kipigo ilikuwa ikisikika kutokea ndani ya chumba kimoja kilichopo ndani ya jingo lile la Dou. Miguno ya mtu aliyekuwa akipokea kipigo kile, nayo ilikuwa ikisikika vilevile kuashiria kuwa kila pigo lililokuwa likitua mwilini mwake lilikuwa likimpa maumivu makali ya kuzidi huku ukizingatia alikuwa na jeraha la kuchanwa kwa risasi mkononi nwake.

“Mimi sitaki uongee chochote mjinga wewe, ninekuleta hapa ili nikuuwe na utakufa taratibu tu” alikuwa akiongea Dou huku akishusha ngumi za hatari kumuelekea Roi. Roi alikuwa amepigika sana, sura ilikuwa imeumuka kwa kipigo kilichokuwa kikiendelea mahali hapo. Dou alijivuta na kupiga ngumi moja nzito iliyotua juu ya mwamba wa pua wa Roi hadi kijana huyo akagumia kwa maumivu makali kisha akalegea na kujifanya amepoteza fahamu kwani alijua kuwa kama atajifaya kichwa ngumu mahali hapo ni kifo na si kitu kingine.

“Ushindi wangu ulifia mikoni mwako wee bwege kwa kujifanya ni hodari wa mapambano kumbe ni mjinga tu, umepoteza ndoto zangu za kuwa mfalme wa mji wa Sami Ado, umefanya mji ule ambao unautajiri mkubwa urudi mikononi mwa Serikali. Unadhani nitakuacha wewe bwege” alibwata sana Don baada ya kumuona Roi amepoteza fahamu. Akataka kumshushia pigo moja baya la kwenye shingo lakini kuna mlizi mmoja aliingia mule ndani kisha kumfanya kusitisha kile kitu baada ya kumwambia kuwa kunaugeni umefika na unamuhitaji yeye haraka sana. Dou alizishika nywele zake nyeupe na kuzirudisha nyuma kwa hasira kali kisha akatoka mule ndani na kukuta ugeni ambao haukuwa mdogo sebuleni hapo. Alivua gloves zilizokuwa zimejaa damu na kuzitupa kando.

“Karibuni sana, karibuni mkae” alikaribisha Dou huku akikaa kitini. Wale watu nao wakakaa wote kisha wakaanzisha maongezi ya kile kilichowafanya wafike mahali hapo.

“Dou kama unavyoona hapa kuwa sikuja mwenyewe, kumbuka kuwa nilivyokutoa mahabusu, tulikubaliana kwamba utafanya kile ambacho sisi tunataka lakini leo umekwenda kinyume”

“Hapana mbona mimi sijaenda kinyume nanyi” alijibu Dou kwa dharau kubwa sana.

“Kama hujakwenda kinyume mhona umegoma kutukabidhi huyo mtu wakati unajua kuwa sisi tunamuhitaji kwa udi na uvumba na ni mtu aliyeumiza vichwa vya watu wengi sana, huyo ni mtu hatari Dou usidhani ni mtu mdogo. Huyo ni jasusi mkubwa na mwenye weledi wa aina yake si mtu wa kumuweza wewe” alisema Julio Mobade.

“Ha ha haaaaa! Julio Mobande Julio! kama ni mtu hatari mbona nimemtia mikononi, uhatari ni kwenu ninyi mlioomba msaada kwangu, mimi kwangu ni mtoto mdogo sana na nimepanga kumuuwa mwenyewe sitaruhusu auwawe na mtu mwingine zaidi ya mikono yangu” alijitapa Dou.

Mabishano yalikuwa ni makubwa sana Pale sebuleni na walishindwa kufanya kitu kwa sababu Dou kwa muda mfupi tu aliweza kuwa na walinzi wenye silaha kali ambao kila alipo walikuwa wememzunguuka. Hicho ndicho kilichokuwa kikimpa jeuri sana. Kitu ambacho wao hawakukijua ni kile ambacho kilikuwa kikiendelea nyuma ya pazia. Frank kichaa alikuwa ametoka pale alipokuwa mwanzo baada ya kupewa yule Mwanasesere. Alikuwa tayari ananyata kuelekea kwenye ukuta wa nyuma wa nyumba ile ya Dou. Kila mlinzi aliyekutana naye alikuwa hana bahati, alimpiga kwa mapigo ya kuto kumchelewesha na ya kimyakimya, aliwavunja shingo kwa hasira kali kisha akampachika yule Mwanasesere kwenye kijidirisha kidogo cha juu ambacho alielekezwa na Mtu asiyemjua. Baada ya kuupachika ule, alirudi lile eneo alilokuwapo mwanzo na kusubiri kile alichoambiwa kinaweza kutokea huku akiambiwa awe juu ya pikipiki tayari kuwa mwokozi. Yule mwanasesere alipowekwa pale dirishani, Amiri alishamuona kupitia kwenye mitambo yake iliyopo garini hivyo moja kwa moja akaanza kazi yake. Yule mwanasesere alijizunguusha pale dirishani na kupita kwenye dundu dogo ukadondokea ndani kwenye bega la kushoto la Roi kisha ukasimama. Amiri alikuwa makini sana asije akaharibu mpango wake wa kuweza kumuokoa Roi kitaalamu kabisa. Mtaalamu wa kucheza na kompyuta vile atakavyo. Alikuwa akicheza na kompyuta mithili ya mtu achezae gemu. Alikinyanyua kisafirisha sauti na kukiweka mdomoni.

“Amka Roi, amka brother” sauti kali ilikita kwenye masikio ya Roi aliyejifanya amepoteza fahamu, na aliweza kuonekana kwenye mitambo ya Amiri kutokana na Ule mwanasesere kuwekwa kamera ndogo ambayo ilikuwa na uwezo wa kurusha picha. Roi alikurupuka na kumgeukia yule Mwanasesere.

“Tazama kwa makini, kamba ngumu ni ya mkono wa kulia pekee, vuta kwa meno mkono mmoja wa mwanasesere kisha vuta huo mkono wa kushoto ambao hauna kamba ngumu, huo mkono unamakali ya kuweza kukata hizo kamba” ilisikika sauti. Roi hakupoteza muda akafanya kama alivyoelekezwa kisha akajikunja huku akiuvuta mkono wake wa kushoto, akatumia mdomo wake kukata kamba za mkono wa kushoto japo kwa shida hakuwa na jinsi zaidi ya kujiokoa. Kamba zilipoachia, alikata na kamba zilizofunga mkono wa kuume kisha akakata za miguuni, akawa huru akiwa ameushika ule mwanasesere.

“Uachie huo mwanasesere chini kisha sauti hii hutaisikia tena, tazama kwa makini ukiona baadhi ya vipande kweye ukuta wowote hapo ndani jua kuwa ndipo utakapotokea. Ni haraka mno kwani hakutakuwa na muda mwingine wa kupoteza, nyumba hiyo inalipuka” Roi akauachia ule mwanasesere kisha akaanza kushuhudia unavyojigawa na kumenyeka pale chini, baadhi ya vipande vikajikusanya katikati na vipande viwili vikasogea kwenye ukuta aliokuwa akitazamana nao.

Malumbano yalipokuwa yakiendelea na kutokufikia muafaka, Bencov akapokea simu.

“Nijuze kitu Dr. Lee” alisema Bencov kisha akatulia kidogo kusikiliza.

“Unachoongea unakimaanisha kweli!” alishangaa Bencov, akatulia tena.

“Ok,” akasema kisha akaamrisha vijana wake kuondoka bila kuaga. Julio Mobande alimtazama Dou kwa tuo kubwa Dou naye alimtazama Julio kwa dharau za hali ya juu mno.

“Kumbuka makubaliano yetu Dou” alisema Julio.

“Nakumbuka muheshimiwa hakuna hata moja nililovunja” alijibu Dou kwa dharau huku akiachia tabasamu la kifedhuli. Julio akaondoka na watu wake kwa ghadhabu kubwa. Don Dou akatoka nje na kuangalia msafara ule uliokuja kumchefua, akazishika nywele zake na kuzirudisha nyuma kisha akacheka sana kicheko ambacho kilikuwa ni cha ushindi bila kujua kuwa wenzake walipanga kumvamia usiku na kumuangamiza lakini wakiondoka na mateka yule au kuwauwa wote kwa pamoja. Walichelewa. Nasema walichele kwa sababu hata kile kicheko cha Dou hakijafika mwisho, kishindo kizito kikasikika. Kishindo kile kilimfanya Dou kupatwa na mshtuko wa hali ya juu sana lakini hakukaa kizembe, alikimbia kwa kasi kubwa na kujirusha mbali na ile nyumba. Ukuta uliokusudiwa na Amiri kuvunjika baada ya kuuchezesha ule mwanasesere vile atakavyo. Kile kishindo cha kuvunjika kwa ukuta kilitosha kumtoa Roi pale ndani na kujirushia nje kabisa, kabla ya kishindo kingine cha pili cha mlipuko, Frank alifika na pikipiki kubwa, Roi akadandia kisha akaliondoa kwa kasi kubwa sana eneo lile. Mlipuko mkubwa ukaibuka na kuisambaratisha ile nyumba yote. Dou alipoinuka kutokea pale chini, hakuamini alichokiona, nyumba yake ilifumuliwa na mlipuko ule. Alipiga kelele sana, zilikuwa ni kelele za maumivu makubwa mno. Chuki dhidi ya Julio na watu wake ikajijenga moyoni mwake. Alianza kuwachukia kwa kiasi kikubwa sana kuanzia hapo. Hakuna mlinzi wake hata mmoja aliyeweza kuokoka kwenye mlipuko ule. Aliumia sana. Mawazo yake aliamini kuwa Roi amekufa kwenye ule mlipuko, mawazo ya kuwa huwenda kijana huyo ametoroka hakuwa nayo yeye bado aliamini Roi ni mtu mdogo sana kwenye nyanja kama zile. Dou alitoa simu mfukoni na kumpigia simu Julio kisha akampa maneno ya vitisho sana.

“Kwa kitendo cha kisaliti mlichonifanyia naapa mbele ya Mungu sitokuwa nanyi pamoja, Fanyeni yenu nami nifanye yangu, mlikuwa na lengo la kuniuwa mimi lakini mimi nimepona na aliyekufa ni yule mjinga mliyekuwa mkimuhitaji, mimi siyo wa kufa kwenye bomu kizembe” alibwata Dou kisha akakata simu na kutoweka eneo lile na kwenda anapopajua yeye.

Julio Mobande Julio alishtuka kupita kiasi, kitendo cha kuambiwa kuwa nyumba ya Dou imelipuka na kusababisha kifo cha Roi kilikuwa si cha kawaida. Hakuumizwa na vitisho vile bali kilichomuumiza ni jinsi ambavyo anahusishwa na mlipuko ule. Je, ni kweli yeye ama vijana wake wanahusika kwenye lile tukio? Kama siyo yeye ni nani sasa, au ni nani sasa? Alijiuliza sana Julio lakini hakupata majibu kichwani mwake kwa haraka. Akawaza kwa muda mrefu, wazo alilowaza likawazuka kwa muwazaji kuwazuwa, akakata shauri na kuamua kumpigia simu Bencov mwenye hasira kali dhidi ya Dou.

“Nyumbani kwa Dou kumetokea mlipuko mkubwa uliosababisha kifo cha Roi na kuismbaratisha nyumba nzima ya Dou” alitoa taarifa hiyo Julio.

“Ati nini?” alihoji Bencov. Hakuweza kuamini kwa haraka jambo kama lile. Akafikiri kwa muda na kukumbuka maneno ya Dr. Lee.

“Kama ni Roi ndiye ameingia Ungamo kazi ipo, yule ni mzimu si binaadamu yule” alikumbuka Bencov. Kisha akaifikiria gari ndogo ambayo ilikuwa umbali mdogo kutokea kwenye nyumba ya Dou. Hakuamini moja kwa moja kuwa amekufa na pia hakuamini moja kwa moja kuwa ametoroka.

“Muheshimiwa, nimepata kugundua chimbo za wasaliti na wenye mipango mibaya na Taifa hili kwa kufuata maagizo yako na kupitia maelekezo ya first Lady. Kingine nilichokigundua ni kwamba hata yule waziri wa ulinzi na usalama pia ni miongoni mwa maharamia” Insp. Bogo alikuwa akimfikishia taarifa Rais moja kwa moja kutokana hata kazi hiyo alipewa yeye moja kwa moja. Rais akashusha pumzi nzito na kutulia kitini kwa muda kidogo kisha akamwambia kijana huyo ampe muda wa kufikiri ni kipi cha kufanya. Bogo akatoka mule ndani ya ofisi na kumuacha Rais Mabandu akiwa ni mwingi wa mawazo sana.

Roi alikuwa yupo kwenye matibabu ya haraka na ni ndani ya jengo lao la siri ambalo kulikuwa hakuna mtu aliyekuwa akilifahamu. Risasi iliyokuwa imekaa kwenye nyama ya mkono ilitolea kisha akachomwa na moto mkali ili kuondoa sumu iliyokuwepo, akapakwa dawa na kufungwa bandeji. Majeraha mengine madogodogo, yalipakwa dawa kisha baada ya hapo wakaingia mezani na kuona jinsi ambavyo wangeweza fanya. Frank akatoa kila kitu alichokigundua kupitia chunguzi zake hadi kufikia kutokea kwenye lile jingo ambalo alikuwa amehifadhiwa yeye. Mipango ikapangwa ya kuvamia usiku ili kuweza kusambaratisha kila kitu kilichopo ili nao waweze kungia kwenye mpango mwingine. Wakati wao wakiwa wanapanga hayo, Muheshimiwa Rais Mabandu, alikuwa kwenye kikao kizito yeye na wanausalama anaowaamini, walikuwa kwenye mpango wa kuhakikisha wanamaliza hilo tatizo haraka zaidi.

“Nini mnafikiria kwenye hili?” aliuliza Rais,

“Sisi hatuna tunachofikiri tena, kama kila kitu kikowazi ni bora hili likamalizwa mapema kwani kama tutawapa mwanya ni wazi hawa wajinga watatuzidi” alitoa wazo.

“nataka jeshi la wananchi lihusike mnasemaje?” akaeweka hoja mezani. Watu wakatazamana, kisha wakasema kuwa hiyo haitakuwa sahihi kwa watu wadogo kama wale kuwaingizia jeshi, cha kufanya ni kutumia jeshi la polisi pekee.

“nadhani jeshi la polisi linatosha, tutachukua vijana wenye uweledi mkubwa kwenye utumizi wa silaha na mapigano kutoka huko na si kulisumbua jeshi” alisema mjumbe mmoja ambaye alikuwa anacheo kikubwa huku akiwa ni mshauri wa karibu sana wa Rais. Mkuu wa majeshi ndani ya nchi hiyo akaafiki hilo na kuahidi kuwa endapo mambo yakiwa magumu basi hakuna budi kutumia nguvu ya jeshi. Kikao hicho kikawa kinaelekea mwisho huku kikileta uhakika wa ushindi kwao. Mara simu ya muheshimiwa ikaita, akaitazama kwa muda kabla haja nyoosha mkono kuiruhusu.

“kunataarifa imetufikia hivi punde mkuu!” ilisema sauti ya upande wa pili, aliisikia mwenyewe lakini akaamua kutoa mkono kwenye spika ya kutoa sauti nje ili kuruhusu kila mmoja asikie.

“Taarifa!? Taarifa gani?” alishtuka sana mkuu huyo wa nchi.

“Watu wanakufa mtaani kama kuku, kwa uchunguzi wa haraka uliofanywa ni kwamba hospitali zote za hapa mjini na pembeni ya miji yote, zimejaa sana na wagonjwa wanazidi kumiminika. Haijajulikana ni ugonjwa gani” ikasema hiyo sauti, kila mmoja pale akakumbwa na taharuki kubwa sana.

“Hebu nyoosha maneno tafadhali, nashindwa kuelewa”

” mkuu, hali ni mbaya sana tuma watu waende kujionea wenyewe huko mitaani” ilisisitiza hiyo sauti. Muheshimiwa Rais kwa hasira na kuchanganyikiwa aliirudisha ile simu kwenye kikalio chake.

Hiyo taarifa iliyomchanganya Rais ndiyo ile iliyompa raha Bencov wakati akiwa barabarani kurudi kambini, aliamini kwa asilimia miamoja baada ya masaa sabini na nne, Ungamo itakuwa inahemea mipira. Habari zikasambaa kuwa wanachi wa Ungamo wamekutwa na hali ya kushangaza sana kwani wanakufa hovyo na kutokewa na vitu vya ajabu. Miili yao inavuja damu kwenye sehemu zilizowazi na baada ya muda hali ya kupoteza maisha ndipo inapowakuta. Hofu ikatanda.

“Roi hali ni mbaya ndani ya nchi hii kuwa makini sana, hawa wajinga wanampango mbaya sana na siyo ndani ya Taifa hili tu bali hata nchini Tanzania mkoani Arusha hali hiyo imeibuka” simu ilipigwa kwa Roi na kupewa hizo taarifa.

“Nini sasa hii Amiri?” alihoji Roi.

“Hakuna kitu kinajulikana kwenye hili ila cha kufanya kuanzi sasa acha kula vyakula vya mitaani nenda kwenye maduka makubwa (super market) kwa ajili ya kununua vyakula ninamashaka na hilo, haiwezekani ugonjwa huu usambaye hivi ghafla tu” alisema Amiri kisha akakata simu.

Hofu ilikuwa imetanda kweli si kidogo kweli kwenye nchi hizi mbili za Afrika. Ni ugonjwa gani ulioibuka? Kila mtu alikuwa akijiuliza namna hiyo. Madaktari walikuwa wanapiga kelele kuhusu kuongezeka kwa wagonjwa ndani ya hospitali zao lakini nao wakijikuta wakikumbwa na ugonjwa huo baada ya siku moja. Unaambukiza? jibu la swali hilo hakuna aliyekuwa nalo.


ARUSHA NCHINI TANZANIA.

Hali ya ubaridi ilikuwa kali sana chini ya mlima wa Oldonyo Lengai, wakazi wa kijiji hicho walikuwa wamegubikwa na mashuka yaliyovaliwa kwa asili ya kimasai (Lubega). Yalikuwa ni majira ya saa tatu na madakika yake asubuhi, kijana mmoja wa kimasai mwenye umri mkubwa upatao miaka ishirini, kwa mila na desturi zao vijana kama hao walikuwa wakiwaita Morani alikuwa bomani akisweka Ng’ombe kwa lengo la kuwatoa ili kuwapeleka machungani. Walifanikiwa kutoka Ng’ombe wawili tu nje ya Boma lile lakini wengine wote wakaanza kuangua na kutapatapa kisha kimya kikatanda. Hofu kwa Morani yule ikaibuka, wazo la nini tatizo hakuwa nalo. Alipandisha mori na kupiga kelele kali sana, ilikuwa ni jambo la kushangaza na la kushtukiza sana. Muda mfupi watu wakajaa eneo lile kwa ajili ya kushuhudia kitu ambacho kimesababisha kijana yule kupiga kelele. Hawakuami kile walichokishuhudia pale. Wakati wakiwa wanashangaa hilo jambo, ukelele mkali ukasika kutokea kwenye nyumba moja ya Tembe, walipoangaza macho yao wakaona mama mmoja akitoka mbio huku akipiga kelele za kilio.

“nini?” aliuliza Olaiboni mmoja wa kimasai.

“mumewangu, wanangu! Wanatokwa na damu mwilini tu na wamedondoka chini!” aliongea yule mama huku akiwa analia si kidogo.

“Laana hiii?” Aliongea Olaiboni mwingine kwa lugha safi ya kabila hilo. Mara wakaanza kumtenga yule mwanamke aliyekuja na kilio pale na kusema kuwa mumewe na watoto wake wanatokwa na damu, walikuwa wakimtenga huku wakimsontea vidole vya shahada. Damu zilikuwa zikimtoka mtu yule. Hofu ikamtanda yule mama baada ya kuona damu zikianza kumtoka kwenye kila sehemu iliyo wazi, kwenye vinyweleo vya ngozi yake, puani, kinywani na sehemu nyingine. Wale wengine wakajikuta wanapata woga na shauku ya kutaka kujua nao kulikoni. Hali ya hofu ikaibuka zaidi baada ya kujikuta nao wakitokwa na damu. Vilio vikasikika, hali ya kuchanganyikiwa ikaibuka. Nani abaki kwenye ardhi ile yenye maajabu, watu wakakimbia hovyo kujaribu bahati zao za kuokoa maisha. Pale waliamini pengine ni laana tu ndiyo ilitokea. Watu walilia hai zao. Si hapo tu bali kila pande hali ikawa tete hakuna wa kumuomba mwenziye msaada. Rais wa nchi ya Tanzani akalihutubia Taifa kuhusiana na hali ya hatari hiyo iliyojitokeza, madaktari wakuu wa nchi wakaagiza wananchi waache kutumia maji na vyakula. Wale nini sasa, wanywe nini sasa. Ilikuwa ni pata shika nguo kuchanika.

“Huyu ameshapoteza maisha dakatari” alisema muuguzi mmoja aliyekuwa akimfanyia vipimo mgonjwa aliyekuwa yupo katika hali mbaya.

“Mbona hii hali inazidi kututisha namna hii, hii hali inatokana na nini?”

aliuliza Dokta mmoja kutoka kwenye Hospitali ya KCMC Moshi.

“Hakuna anayejua dokta” alijibu daktari mmoja, mara akapokea simu kutoka kwenye ofisi ya dokta mkuu.

“Ndiyo, Dokta” alisema kisha akasikiliza.

“Ndiyo, sawa hakuna shida” akajibu tena kisha simu ikakatwa. alipokwisha kuirudisha simu mfukoni akasema.

“chukua damu na sampuli nyingine kutoka kwenye mwili wa huyo marehemu aliyekufa sasa hivi, tunatakiwa maabara na ikiwezekana tujue chanzo cha haya ni nini?” alisema Mganga huyo mfawidhi wa hospitali hiyo ya KCMC. Madaktari waliyopewa hiyo kazi wakafanya hivyo. damu ilipatikana japo haikuwa nyingi, zilichukuliwa na sampuli nyingine kisha jopo zima la madaktari likaelekea maabara. Uchunguzi ulifanyika kwa kina sana, uchunguzi huo haukuchukua muda mrefu sana na hatimaye majibu yakatoka kuwa magonjwa na vifo hivyo chanzo chake ni sumu ambayo inatokea kwenye vyakula. tatizo ni kwamba haijajulikana ni sumu ya aina gani. Hapo ndipo watu wakatahadhrishwa kuwa makini.

Habari za kwenye televisheni zilizidi kuwafanya watu wafurahi sana baada ya kuona mamia ya wananchi wa Tanzania na wale wa Ungamo, wakipoteza maisha na kudondoshwa na ugonjwa wa kutisha mithili ya kuku wa mdondo. Bencov alikuwa akifurahi sana juu ya suala lile.

“Unatazama Luninga” alingea huku simu ikiwa sikioni kwake.

“Kwanini nisitazame, naona jinsi mpango wetu wa maangamizi unavyofanya kazi kwa kasi kubwa….enhe! Vipi kuhusu Roi?” alijibu mtu wa upande wa pili wa simu kisha akabakisha swali mwishoni.

“Yule alilipuka yeye na nyumba moja ya mjinga mmoja anayejiita Don Dou lakini hata kama alipona kule basi atakuwa ameuwawa na huu mapango wa maangamizi” alijibu Bencov.

“Kwa ninavyomjua yule jini, hawezi kufa kwa bomu ila kwa huu mpango hachomoki hakuna dawa ya kumponya mtu anapokumbwa na ugonjwa” mtu wa upande wa pili wa simu alizidi kujitapa.

“Ha ha ha haaaa!” acha wapukutike kwanza wakome kuchezea watu wenye akili nyingi kuliko wao” alicheka kwa furaha kubwa kisha akahitimisha na maneno yake ya majigambo.

UPANDE MWINGINE WA MJI HUO WA PANDE.

“Roi uongozi wangu umenitaka nirudi nchini kwangu hata kama sijamaliza huu mpango, hali imekuwa mbaya sana kwenye hii nchi hivyo wameniambia kuwa hali ya hapa si shwari hivyo wanahofia kuonekana hata mkono wao umechangia” alisema Petii. Roi akatulia kimya akiwa anamuangalia binti huyo mwenye urembo wa aina yake kisha akamuuliza.

“nini umeujibu uongozi wako sasa?”

“Nitaondokaje ikiwa mtu muhimu bado anatamba na huyo ndiye muhusika mkuu. Lazima Bande Sir afe kwanza ndipo nitakuwa radhi kuondoka” alisema Petii.

“Ok, Frank inabidi huu mchezo uanzie kwa Julio kwanza kabla ya huko kwenye ngome ya Mining” alisema Roi, Frank akasema vyote vinawezekana. Walipokubaliana hivyo, wakaamka na kukusanya zana za kazi. walichukua kila walichokiona kinafaa kwa ajili ya kazi.

Yalipotimia majira ya Saa nne usiku, wakajitia garini na kuondoka. Mambo yalikuwa katika muingiliano mkubwa sana Kwa upande mwingine Rais Mabandu alikuwa ametuma vijana wake kwa ajili ya kuja kumtia mikononi Julio na watu wake. Walikuwa si askari kidogo, walikuwa ni askari wengi sana na waliokamatia silaha za kivita. Gari zao zilikuwa zikikimbizwa kwa kasi kubwa mno. Wakati wao wakiwa wanaingia kwenye jumba hilo ambalo muda huo kikao kilikuwa kikifanyija juu ya mustakabali wa mipango yao ya kukamata dola yanavyokwenda mrama kuhusiana na hali ya nchi ilivyokuea ikisonga. Watu walivyokuwa wakifa kama kuku huku wakimuona Bencov akiwa anafurahi hali hiyo. Hapo ndipo walipojua kumbe mpango wa maangamizi ulikuwa ni kwa Taifa zima na si kwa wale waliokuwa wakitegemea wangeuwawa na wao waishi kama wafalme ndani ya udongo huo. Roi na watu wake wakati wakiwa wanakunja kona ili kuishika barabara iliyokuwa inawapeleka huko, waliona gari si chini ya sita zilizokuwa na askari wa kutosha ambazo zilikuwa zikielea kule walikokuwa wakielekea wao.

“Brother Roi, nini kule mbona kama gari za askari zile?” aliuliza Frank.

“ndiyo zenyewe hebu tusubiri mbele hapo tuone kinachoendelea” alijibu Roi kisha wakaweka gari mahali ambapo wanaona kwa uzuri kwenye lile jumba, walikuwa makini kabisa na silaha zao kwa lolote lile litalojitokeza. Mirindimo ya risasi ikarindima mara tu baada ya gari kufika lile eneo. Walinzi wote waliokuwapo nje walipoteza maisha. Hali ya taharuki ikawakumba waliyopo ndani ya lile jumba. Bogo na kundi lile la askari wakawa wanazidi kusonga mbele. Lilikuwa ni shambulio la ghafula sana hivyo hawakuwa wamejipanga kwa lolote lile. Mlinzi mmoja aliyejitahidi kujipenyeza na kufika ndani kule kwenye kikao alisema kuwa, hali ya nje si hali na hakuna hata mlinzi hata mmoja aliye hai. Bande Sir akasimama na kuto bastola yake kisha Kitema naye akasimama.

“Mkuu huku, nifuateni mimi” alisema kitema huku akiwa muongozaji wa msafara ule wa kumtoa Julio ndani ya lile jumba. Bande Sir, aliaminika kwa shabaha hivyo yeye akawa anapita njia nyingine ili kuweza kuwapunguza askari hao waliovamia. Hata Risasi moja ya Bande Sir ilikuwa haipotei bure, kila aliyokuwa akiitoa kwenye mdomo wa bunduki yake ilikuwa ikiondoka na maisha ya Askari mmoja.

“Mwambie kiongozi aongeze nguvu huku hali ni mbaya sana” alipiga kelele askari mmoja aliyejeruhiwa kwenye miguu yote miwili.

“Goo, goo, movu muvu!” sauti ya mkuu wa kikosi kile cha askari ilisikika ikitoa amri. Askari wakajaa mule ndani na kuanza kumimina risasi hali ikawa mbaya sana kwa watu wote waliokuwamo kule ndani walikuwa wameuwa isipokuwa Rais Julio, Bande Sir na Kitema hawa ndiyo walikuwa bado lakini Jarome yeye alishindwa kujitetea akajikuta akinywa risasi nyingi sana za kifua bila kujizuia.

Njia ambayo walipitia watu wale wawili Julio na Kitema nayo ilikuwa imeshazingirwa na askari makini kabisa.

“Mkuu hapa hatuwezi kutoka salama hata kidogo, askari wametanda kote” alisema Kitema.

“Kitema hakikisha kabla hujakufa wewe umewauwa wote mimi nitoke hapa nikiwa hai, hivi unadhani nitakuwa mjinga kiasi gani nifeli kwenye kuikamata dola. Lazima niikamate Dola. Nenda uwa wote mimi nitoke hapa!” alifoka Julio. Kitema akakamata bastola na kutoka mule ndani kupitia kwenye chochoro ile walikusudia kuipita wao kwa ajili ya kusafisha njia mkubwa wake apite. Alinyata kwa akili nyingi sana kisha akajirusha kwa mtindo wa kuvutia halafu akabingilia huku bastola yake double pipe ikimwaga njugu vizuri. Dakika moja mbele njia ile ilikuwa njeupe kwa Julio kupita. Walipita hapo wakaingia kwenye bomba kubwa kisha wakatokea umbali mkubwa kidogo kutokea pale. Wakakuta gari ikiwa inaungurumishwa injini yake, walipoangalia vizuri, alikuwa ni Bande Sir ambaye alifanikiwa kutoroka na kufika mahala pale. Jingo lile lililipuliwa lote wakiamini wahusika wote walikuwa mule kumbe walifanikiwa kutoka kupitia njia ya siri. Waliingia kwenye ile gari kisha Bande Sir kuitoa kwa kasi kubwa.

“Petii ingiza gari njia hiyo hapo kulia, kunawajinga wanataka kutoroka, ni dhambi kubwa kuwaacha waende” alisema Roi huku akiitazama ile gari iliyokuwa ikipelekwa mkuku mkuku. Petii alifanya kama alivyotakiwa, kazi ya mfukuzano ikaanza. Walifukuzana hadi katikati ya mji huko, wafukuzwaji wakajua kuwa nyuma kuna gari ilikuwa ikiwafuatili. Wakashindwa kufanya maamuzi ya kueleweka kwani tayari walishachelewa. Risasi moja ambayo Frank aliituma ilikwenda kupiga gurudumu la gari ile na kwa kuwa ilikuwa ikigeuza ili kubadilisha njia, ikabingilia vibaya sana. Petii alisimama pembeni kidogo ya gari ile kisha wakashuka kutokea garini. Waliwaona wahanga wao wakiwa wanajitutumua ili waweze kutoka. Wakawavuta kila mmoja na wake kisha kuanza kuwashushia kipigo cha kufa mtu. Bande Sir alikutana uso kwa uso na Petii. Akajikuta akikumbuka mbali sana. Alikumbuka kipindi akiwa anamtesa binti huyo kwenye chumba cha barafu kwa lengo la kutaka kumuuwa kwa kutumia baridi kali.

“Wewe ushukuru Mungu ninge….!” Hajamaliza alichotaka kusema, akala ngumi nzito ya mdomoni na kumfanya amwage mate kama mjinga fulani. Wakati wakiwa wanazidi kutoa Dozi, walivamiwa na askari waliokuwa wanatokea huko walikotoka wale wajinga. Wakawekwa chini ya ulinzi na kisha kuambiwa kuwa wawaache. Kila mmoja alikuwa na machunhu kwa mtindo wake dhidi ya wale watu. Petii alikuwa na machungu yake, Frank ndiyo usiseme machungu aliyonayo kwa Julio Mobande Julio. Alikumbuka siku ambayo anashuhudia wazazi wake wakifa kwa mateso makali sana, mama yake akibakwa kwa sababu ya mjinga huyo halafu leo eti akubali aende kuishi gerezani kwa amani akila ugali wa serikali. Alimtazama Kitema akakumbuka kipigo cha Mbwa koko alichopigwa naye kisa kutokuwa makini barabarani, akakumbuka kesi ya alivyotaka kumuuwa wakati akiwa anapeleka magazeti kwenye nyumba ya mteja wake mkubwa wa siku nyingi. Alifumba macho kwa hasira sana. Watu wale watatu walikuwa wakielekea garini wakidemezwa na askari ili waje kupandishwa mahakamani siku moja na wajibu mashtaka ambayo pengine wangeyakana na kuisumbua mahakama.

“J.M.J!” alipiga kelele Frank Kichaa kisha akasema huku kila neno analosema likitoka na risasi ambazo alizioga Julio Mobande Julio.

“Unamkubuka baba yangu, unakumbuka kifo cha mama yangu baada ya amri yako ya kumdhalilisha, unakumbuka kifo cha muandishi wa habari, kaka yangu ndungu yangu John, unakumbukaaaa!” alimminia risasi za kutosha sana alipotaka kugeukia kwa Kitema akashangaa risasi nyingine kadhaa zikitoko kwenye bomba la Petii na kumshukia Bande Sir. Askari wale waliokuwa wamewashika wale wahalifu wakashangaa walivyobakiwa na miili iliyokuwa si hai tena. Frank akataka kumaliza kazi lakini Bogo akamuwahi na kumlaza Kitema kifuani mwake na kumuogesha na risasi za kifua.

“hatuwezi kuondoka na kuku mdogo kama wewe ikiwa kuku wakubwa wamekufa” alisema Hivyo Bogo huku wakiwataka watu hao waondoke kwani alijua fika wanakazi kubwa sana ya kulikomboa Taifa kisha wao wakawa radhi kuondoka na maiti.

Asubuhi kulipokucha hali ilikuwa ya furaha na mshangao mkubwa baada ya taarifa ya habari kutangaza vifo vya watu waliokuwa kwenye mpango mbaya wa nchi hiyo. Taarifa hizo zilikuwa mbaya sana kwa Bencov hakuamini kama jumba lile lingevamiwa na kulipuliwa. Wakati Bencov akiwa na mshangao wa nafsi yake, Dok. Lee alikuwa akifikiri yake juu ya mauwaji yale ya kushtukiza.

“Lady Devil huyu ni Roi kweli, huu mtindo wa kuuwa kwa kushtukiza naujua ni wake, itakuwaje kama akijua kuwa sisi tupo hapa” alisema kwa hofu kubwa sana Dr. Lee.

“Ondoa shaka mkuu hawezi kujua kitu na hata akijua tayari tutakuwa tumeshaikamata Dunia” alisema Lady Devil.

“Kweli eeeh!”

“Yaa,” alijibu Merina kisha wakazidi kuitazama ile taarifa iliyokuwa ikiendelea.

NDANI YA BBD MINING COMPNY.

“Ni lazima tufanye maamuzi ya kweli kabisa na dhamira iliyo wazi. nadhani mnajua kuwa tupo hapa kwa kazi gani si ndiyo. Huu ndiyo muda wa kutumia silaha zetu za kuuwa na kupoteza hakuna kumuacha mtu hai tena hata kidogo. Sasa hivi huko mtaani bado wanashindwa watangaze kifo cha nani na wakiache cha nani. Tunaipa serikali hii siku tatu kisha tunaingia mitaani na kutega mabomu yetu ya sumu na kuanza kuwaangamiza wote tukiwa na imani kwa hilo, hakuna hata kiumbe mmoja atakaye pona” aliongea Bencov akiwa amezunguukwa na kundi kubwa la vijana wake wote. Aliwapanga katika makundi yao na idara zao, wadunguaji walitakiwa kuweka ulinzi mkali na walitahadharishwa juu ya kuacha kiumbe chochote kitakachopita. kwani kama wataacha basi wajiandae maana ingeweza kuwagharimu kwa gharama kubwa lakini kwa upande mwingine hali ilizidi kuwa mbaya, bado tatizo lilikuwa halija julikana huko nchini Tanzania japo habari za uchunguzi wa mwanzo zilisema kuwa ni sumu itokayo kwenye chakula, sasa ilikuwa ni chakula gani?

Hussein Babu alipata mashaka hata kwa vijana wake walipo nchini Ungamo, alikuwa hana amani kabisa kutokana na hali hiyo tete kuwashambulia wana wa nchi hizo mbili tu. Akaingia ndani ya ofisi yake kisha akatulia na kupiga simu.

“Vipi kijana ni mzima wewe?”

“Mimi ni mzima kabisa Father na jana tu nilipotoka kwenye mipango yao ya kutaka kuniuwa, nimewaanza kwa kishindo. Nimeuwa mizizi ya kati ya mti huo mbaya bado mizizi mikuu. Vipi hali ya huko lakini lakini pia aliyeko nyuma yangu hana shida yuko salama”

“Hali ya huku bado ni mbaya kijana wangu, kila siku tunaokota watu barabarani wakiwa wanavuja damu na kupoteza maisha hatuelewi tatizo nini. Wataalamu wa Afya kutokea shirika la afya duniani wamekuja nchini kufanya chunguzi zao kuhusiana na ugonjwa huu. Tunasuburi tuone lakini hali ya nchi si shwari”

“Fadther naamini kazi hii niifanyayo mimi inashabihiana na hiyo…..!”

“Kivipi?”

“Sina jibu zuri la kukupa lakini cha kufanya sasa hivi ni kuongozana na Dokta Lyimo hadi kwenye mashamba ya mazao.

na chunguzi hizi zianzie huko mkoani Arusha ambako ndiko kwenye chanzo cha ugonjwa huo” alisema Roi. Hussein babu mkuu wa kitengo cha Siri ambacho ni kipya kabisa kuanzishwa baada ya kuona hakuna vitengo ambavyo vinaweza kupambana na kashikashi za namna hiyo, alipata kitu kutoka kwa Kijana wake anayemuamini. Akafikiria ni kwanini kijana huyo amemfikiria Dr. Lyimo. Hakupata jibu la haraka lakini akaona kuna kitu cha ziada. Wakati wataalamu wa afya wakichukua sampuli na kuondoka nazo kwenda nazo kwao, Hussein babu na Dr. Lyimo walikuwa wanaingia kazini. Walikuwa ndani ya ndege ya kukodi ambayo ilikuwa ikiwapeleka mkoani Arusha. Muheshimiwa Rais wa Tanzania bwana Martin John alikuwa ametulia kimya. Akisikilizia majibu yatakayotoka kutokea pande mbili hizo. Si kama alikuwa haoni kama wananchi wake walikuwa wakipoteza maisha la! angefanya nini sasa wakati hakuwa na njia stahiki ya kutatua tatizo lile.

Ndege ndogo ya kukodi ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Kilimanjaro. Wakashuka watu wane, alikuwepo Mkuu wa kitengo cha siri father Hussein Babu pamoja na Dr. Lyimo akiwa na madaktari wawili wasaidizi. Babu alikuwa na imani sana na Daktari huyu kutokana alikuwa akimtumia mara nyingi kwenye chunguzi tata kama hizo. Waliingia kwenye gari iliyokuwa imeandaliwa maalumu kwa kazi hiyo ya kuwachukuwa watu hao hadi huko waendako. Waliondoka hapo mjini na kuelekea moja kwa moja kwenye chunguzi. Mida ya mchana wa saa sita na robo, walikuwa ndiyo wanaingia kwenye shamba moja kubwa sana la mahindi lililokuwa likitumia kilimo cha kisasa, kilimo cha umwagiliaji. Walichukua sampuli tofauti kama mahindi ambayo yamesha chavushwa na yale ambayo hayaja chavusha pia walichukua baadhi ya magugu shamba na kuyahifadhi mahali salama kisha wakaondoka na kurudi Moshi mjini. Walipofika hapo wakaomba kuzitumia maabara za hospitali ya KCMC. Halikuwa jambo gumu kupewa maabara hizo kwa ajili ya kazi ya kuliokoa Taifa. Dr. Lyimo akaingia kazini akiwa na wasaidizi wake lakini pia na baadhi ya madaktari wengine.

“Hapana usichukue vitu viwili ukachanganya sehemu moja, chukua kimoja kimoja ili tupate majibu sahihi” aliongea Dr. Lyimo.

“Naomba nisogezee hiyo Tube yenye kemikali ya rangi ya kijani” aliagiza Dr. Lyimo. Kemikali ikasogezwa na kuanza kazi ya kuchunguza Sampuli za magugu shamba alizokuwa amebeba ambazo si za kutambulika. Akijaribu kwa kila moja, majibu aliyokuwa akipata alikuwa akiyanoti pembeni kisha mwisho kabisa, wakakusanya chunguzi zote na kuchukua zile zilizokuwa zikifanana. akachukua na sampuli ya vipimo kutoka kwenye miili ya wagonjwa na baadhi ya maiti. Wakaunganisha na zile zilizokuwa zikifanana.

“Shit! Hii nini maana yake?” aling’aka Dr. Lyimo.

“Ni nini Daktari?” aliuliza Hussein Babu ambaye alikuwa kwenye mavazi ya kidaktari.

“Kuna kitu kipo hapa na utakuwa ni mpango wa maangamizi huu. Huu ugojwa unaosababisha hivi vifo umesababishwa na sumu inayoitwa Diebrainaphine. Na sumu hii ndiyo iliyoweza kutungisha huu mmea unakwenda kwa jina la Partathunum” alisema Dr. Lyimo kuhusu majibu ya vipimo vyake.

“Mungu wangu! Kwa maana hiyo unataka kuniambia hawa wagonjwa wote wanaangamizwa na huu ugonjwa?” aliuliza Hussein Babu.

“Na ni ugonjwa wa kutengeneza huu cha kufanya sasa ni kuchunguza zile mbolea ambazo zililetwa na wale wataalamu waliosema wametoka shilika la chakula Duniani” alisema Dr. Lyimo na kwakuwa walibeba kila kitu, wakafanya hivyo. Ile mbolea ilipochanganywa tu kidogo na kemikali, ikaleta majibu. Hapo wakapata majibu ya haraka. Wakaondoka hapo wakiwa na majibu stahiki kabisa. Baada ya siku mbili majibu mengine kutokea huko duniani yakaingia. Yalikuwa sawa kabisa na hayo yaliyochunguzwa na madaktari wa Tanzania. Ikaandikwa ripoto ambayo ilimfikia mh. Rais. Baada ya ripoti hiyo kazi ya kuwatafuta wale waliojiita ni watu kutokea shilika la chakula duniani ili kujua kama je kweli ndiwo au kuna mpango uko nyuma ya hilo.

Habari kamili zikasambazwa za kutokutumia mbolea ile ambayo ilipewa jina la Diet Plls kumbe ilikuwa imebeba sumu mbaya ya Diebrainaphibe ambayo ni angamizo. Ikatumwa ndege maalumu ya kumwaga dawa na kuangamiza mazao yote shambani yaliyokuwemo na yadiyo kuwemo huku watu wakitakiwa kuacha kuitumia mbolea hiyo hatarishi. Kitengo cha Babu kikaanza kazi ya ufukunyuzi wa kimtandao kwa watu wale.

PANDE.

Ramani iliwekwa mezani, Ramani ambayo ilitakiwa kutumiwa na vijana watatu tu. Roi, Frank na Petii ambaye aligoma kuondoka hadi mtanange huo utakapokuwa umefika mwisho.

“Kama nilivyowaambia kuwa kwa maelezo yako ya uchunguzi kama Frank kichaa ulivyoona ni kwamba, hii ngome zamani ilikuwa ni mgodi mkubwa wa machimbo ya madini ya dhahabu. Hivyo humu kunatakiwa kuwa na umakini mkubwa kwani hata kama mashimo yatakuwa yamefunikwa lakini hakuwezi kukosa semu zao za kujihami wawapo na shida. Huwa sipendi kuona mtu akiwa anatoweka kwenye hili, nataja kuona tunauwa kila kiumbe cha pale.” aliweka tuo Roi kisha akanywa maji na kuwatazama vijana wale kisha akaanza kuelekeza.

“Tunashambulia hapa kwa siri sana hadi tukifika hapa ambapo ni mahali pa wazi, tutakuwa tumeshawamaliza hawa wote ambao wewe ulisema unewaona wakilanda. Lakini pia ulisema pia umeona vibanda vya wadunguaji, hilo litakuwepo hatuwezi kudharau. Tutapita kushoto wote kisha tutakuja kukaa hapa. Sasa hapa ndipo vita itakapoanza lakini tutakuwa tumewapunguza makali maana kutakuwa hakuna hata mdunguaji mmoja tutakayemuacha” alisema Roi. Wakatikisa vichwa kisha wakakamata zana za kazi na kuingia kwenye gari ya kazi. wakaingia garini watu wawili, Petii na Frank. Roi alielelekea ndani kwanza aliporudi alikuwa na mavazi ya moja kwa moja mafano wa suti.

“Ya nini haya” aliuliza Petii. Roi akawatazama kisha akajibu.

“Kumbukeni vifo vya askari wa Backa kipindi Backa anavamiwa kwa ajili ya kutekwa, zile silaha mavazi yake ndiyo haya” Wote wakakosa usemi tena Petii alivua nguo ya juu bila hata kuona aibu yoyote akalivaa hapo hapo. Safari ikauma.

Kimya kilizidi kuwa kingi lakini hali hiyo ya ukimya haikuwa ikiwapa wasiwasi walinzi wa Bencov kabisa. Walikuwa wakilanda hapa na pale huku kwenye mikono yao wakiwa wamekamata silaha za ajabu ambazo mbele kwenye ncha, zilikuwa zimetengeneza rangi nyekundu. Hizo zilikuwa ni silaha hatari sana ambazo uhatari wake ni kukufuta kwenye usawa wa dunia. Panya watatu walikuwa wameshavamia hapo kimya kimya na walikuwa wakipita hapa na pale bila kufanya kelele kwenye vichaka wanavyokanyaga. Walipofika mahali wakasisitiziana umakini na kuacha papara kisha wakakubaliana wakutane kwenye sehemu ya wazi kabla ya kuachana tena. Kila mmoja akapita njia yake. Mavazi yalikuwa ‘special’ kwa eneo lile hivyo pamoja na kwamba shughuli imefanyika mchana lakini haikuwa rahisi kugundulika. Mlinzi wa kwanza alikutana na Roi. Alipokuwa anazunguuka kutokea sehemu moja kwenda nyingine, Roi alikuwa akimsubiri ageuke tu. Na kweli alivyofanya hivyo, alinyata kwa nyuma na kumuweka alama nyekundu kwenye koo kwa kutumia kisu chake chenye makali ya kuzidi. Kwa haraka akamvuta na kumuingiza hahali ambapo si rahisi kuonekana. Alipo mhifadhi yule, ile anatokea tu kwenye ile kona ili kuweza kusonga mbele zaidi. Kuna mlinzi alikutana naye uso kwa uso. Wakati yule mlizi anataka kushuti tayari kisu kilishatumwa zamani na kuzama kooni mwake kisha Roi hakutaka hata yule bwege aanguke chini ili kutoa kelele ya kishindo. Alikimbia kwa kasi kubwa akamdaka na kuzunguuka naye huko akammaliza askari mwingine kwa kumpa kisu cha mgongo bila kelele, ilikuwa ni kwa kasi kubwa sana. Tambua kuwa visu vyote vilikuwa na sumu mbaya sana ambayo haiongopi ikutanapo na damu moto.

“Frank alikuwa si mpezi sana wa visu yeye alikuwa anapiga mapigo ya kuvunja bila kelele. Ni mwepesi na mshapu wa kutumia mikono yake. Alimkabili mlinzi mmoja akiwa kwenye lindo huku akiwa na eir phone masikioni akisiliza muziki. Alipiga pigo la kutisha lilitua kwenye mgongo akang’oka na pingili mbili za uti wa mgongo kisha akamsukumia kwenye ukuta na kumuacha hapo muziki ukizidi kumburudisha. Kwa upande wa Petii, mambo yalikuwa mazuri pia kwani naye alikuwa akifanya yake kwa kuwadungua kwa kutumia bunduki zisizopiga kelele. Hadi wanakutana eneo la wazi tayari walikuwa wamekwisha kuwamaliza Sungusungu wote. Walikuwa wamebakisha vikosi viwili tu navyo ni Mbega/wadunguaji na Mbwa. ili kuweza kuzama ndani.

“Kazi nzuri hadi sasa tulipofika, tumebakisha wadunguaji na kwa maelezo ya Frank kutokea hapo hatujui nini tutapambana nacho. Tunapita kuoshoto kulia na mbele. Mimi napita mbele ambapo ni kugumu zaidi kwani ni rahisi kuonekana na wadunguaji, Petii utapita kushoto huko si sana na Frank maliza kulia haijalishi kunaugumu namna gani” alipokwisha kutoa maelekezo, hakungoja majadiliano mengine, akasonga mbele nao wakafuata nyuma kwa kupitia kule walikokubaliana. Wakazidi kusonga huku kile walichokitarajia kukutana nacho wakawa hawakioni. Mwendo ulikuwa mrefu na ngome ilikuwa kubwa mno. Wakapoteza umakini na kuona huwenda bado mbali lakini kwa Frank alikuwa makini zaidi kwani alikuwa akikaribia. Kumbuka kuwa hawakuwa wakitumia mawasiliano ya aina yoyote kwa kuogopa kunaswa kwa mawasiliano yao. Kumbe wakati wanazidi kusonga, watu wawili walikuwa wameshaonekana na wadunguaji wawili. Petii na Roi walikuwa hatarini zaidi. Hatua tatu za mbele Roi akasita mara risasi ikachimba chini na kutifua mchanga. Roi akacheza na hisia huku akijirusha na kujibu mashambulizi bila kumkosa yule bwege akadondoka chini. Shida ilikuwa kwa Petii ambaye alichapwa risasi moja ya kifua ambayo ilimtupa mbali sana kisha akatulia kimya. Kazi kubwa akawa ameibeba Frank akawa anapambana na wadunguaji wawili. Lakini kwa utaalamu wa hali ya juu ulitumika na kuweza kuwamaliza wadunguaji wote sita. Kila kikundi kilikuwa kimebeba watu sita tu.

“Petii yuko wapi?” aliuliza Roi.

“Mh! Hata sijui!” alijibu Frank lakini hapo hapo wakaanza kusikia michakacho kutokea porini na hatimaye wakarukiwa na kundi la watu sita ambao hawakuwa na bunduki bali visu. Hapo ndipo Roi alipotumia mafunzo yake ya mwisho ya ujasusi huko ughaibuni lakini pia ndipo aliposhindwa kumtafsiri Frank ni kiumbe wa aina gani. Mapigo ya Frank yalikuwa ni ya hatari sana maana alikuwa akiruka na kudansi hewani kisha anatua chini na kubingilia akija akinyanyuka, ujue anakwenda moja kwa moja hewani. Kwa mtindo ule, wale maadui wakabaki watu wa kushangaa tu na mwisho wakajikuta wakifanyiwa mchezo ambao tangu utotoni mwao hawakuwahi kuucheza. ‘mwenzetu, kagongwa na gari’ Pigo moja la Frank kunyanyuka majaaliwa. Waliwapiga wale wajinga hadi wakaja kutokea kwenye mlango wa nyuma wa kuingilia kwenye lile jingo lenye lango lilioandikwa BBD MINING. kwa upande wa mbele. Hapo walimtumia mtu wa mwisho kuchezea kichapo kuvunja huo mlango. Waliruka hewani kwa pamoja na walipokuja kwa mbele, walimsukuma na kumfanya aanguke kwa kishindo hadi mlango ukaingia ndani naye. Dede na Bacon wakiwa pamoja na Bencov sambamba na beda, walishtuka sana kuona uvamizi ule kwani hakukuwa na kamera zozote zilizokuwa zikimulika nje ya jingo hilo la kizamani. Mshtuko ule ukamfanya Bencov sambamba na mlinzi wake kujivuta nyuma kisha kuwapa uwanja Dede na Bacon mbele ya vidume hivyo vilivyoingia ndani bila hata michubuko. Wakagawana vijana hao. Dede alijaa kwa Roi na Bacon alikutana na Frank. Dede kwa mbwembwe nyingi alikuja hewani kama kipanga na kushusha kucha ambazo zilipishwa pasipo kuacha madhara. Huku Bacon alikwenda mzima mzima kama Roboti kisha akavamia na kupiga mapigo ya nguvu yenye mvumo mkubwa sana lakini kijana Frank akamwambia kuwa bado mapema sana kuruhusu kupigwa hivyo akayapisha. Dede ndiye aliyejifanya anamoto wa hatari, moto usiozimika. Wakati wakiwa wanapambana Huku kwa Petii ndiyo alikuwa akianza kutikisa miguu.

Lakini kwa upande mwingine wa msitu mkubwa wa Kutisha huko Kisiwani Madagascar hali ya kutisha ilianza kuleta shida. Sauti moja kali sana ilisikika kutoka msituni. Sauti ambayo ilisababisha bahari kuleta mawimbi mwakubwa. Kiumbe cha ajabu chenye sura nzuri ya kile kilikuwa kimelala chini kikipiga mikono tu lakini miguu ilikuwa haionekani, tumbo kubwa la rangi nyeusi lilikuwa limetapakaa sakafuni. Maumivu yaliyokuwa yakipitia hicho kiumbe ndio sababu ya kelele hizo. Siku za kujifungua za Tereza zilikuwa zikikaribia lakini pia Hali ilikuwa tete zaidi katikati ya msitu wa kutisha wa Dabaa Lonzo. Babu mwenye nywele nyeupe na ndevu nyeupe ambazo zilikuwa chafu, alikuwa ndani ya usingizi mzito lakini ghafula anashtuka akionekana akiwa na hofu kubwa zaidi, mwili wake wote unaloa jasho. Nini amegundua kingine? Kuna ndoto ya ajabu ameota au nini? Sisi tunashindwa kung’amua lakini yeye anaamka na jina moja tu kutoka ndani ya usingizi ule Frank. Nini hii mambo? Miti nayo inatikisika kwa hofu kubwa, mbaya zaidi ni ndoto ya mchana.

Pigo moja alilopewa Frank na Bacon linampeleka chini na kumfanya ashinde kunyanyuka vizuri kwa maluweluwe ya pigo lile. Bacon anajivuta na kutaka kumaliza kazi lakini kwenye kichwa cha Frank, kunakuja kumbukumbu za hatari sana, kumbu hizi ni za kutisha sana na haamini kama zinaendelea duniani. Anakumbuka na ndoto ile aliyowahi kuota huko nyuma, hali ikabadilika.

Mara hapo wakati Bacon anakaribia kuleta pigo la mwisho kwa Frank, kule msituni babu Seki ndiyo alikuwa akilitaja jina la Frank akiwa anatoka usingizini. Frank alinyanyuka na kukamata mikono ya Bacon ambaye alikuwa juu ya kichwa chake kwa lengo la kuvunja shingo ya Frank kisha Frank alinyanyuka naye juu akamrudisha kwa mbele na kuinyonga mikono akiwa hewani. Sauti kali ya mivunjiko ya mifupa ilimfanya Bencov na Mlinzi wake wa karibu waingie kwenye mlango mdogo wa mule ndani na kupotea. Frank alikuwa akipigana mapigo ya babu ambayo alijifunza akiwa msituni kule mara baada ya kusababisha kifo cha mtoto wa Rais wa zamani Julio Mobande kwa kumbabatiza na gari moshi. Bacon alikosa nafasi ya kupiga yowe kwani kabla hajatua chini, pigo jingine la hisia lilitua kwenye koromeo na kuling’oa kabisa. Pigo lile likamfanya Dede aliyekuwa anakuja kushambulia kwa Roi aduae. Roi akamuangalia Dede kwa huruma sana kisha akampiga pigo moja la kifua, Dede akaenda chini. Roi akamuagiza Frank acheki kwenye kile chumba walichoingia wale warusi. Frank alipoingia mule ndani. Roi akamuinamia Dede na kumnong’oneza sikioni.

“Sijawahi kuuwa mwanamke katika maisha yangu ni kwa bahati mbaya sana huwa nafanya hivyo. Nakuacha hai najua kwa pigo nilililokupiga huwezi kufanya chocho lakini unanisikia. naitwa Roi. Nenda kawasimulie Brazil” alipokwisha kusema hivyo, akamuachia na busu moja kubwa sana. Dede akafumbua macho akapepesa na kumtazama Roi kisha akayafumba tena. Roi akamkumbuka mtoto huyo wakati anamsulubisha kitandani akataka kumbusu tena lakini Frank alikuwa ndiyo anatoka kwenye kile chumba. Ikabidi amuachie na anyanyuke.

“Kuna handaki bila shaka watakuwa wametoroka kabisa ndani ya mji huu” alisema Frank.

“unauhakika gani kusema kuwa watakuwa wametoweka ndani ya mji huu?”

“Handaki hilo ni kubwa sana ambalo linauwezo wa kupita hata Treni”

“Bila shaka hizo njia walikuwa wakizitumia kusafirishia madini kinyere/kwa siri. wakiwa wanaongea hayo, Dede alikuwa amefungua macho muda wote alikuwa akimtazama Roi pasipo kummaliza lakini pale mada ilipobadilishwa na Frank ya kumjadili huyo binti kama kafa ama laa, Dede alifunga macho yake na kubaki akiwa amejifanya kupoteza fahamu au amekufa. Alikuwa mwenyewe na mbele ya watu hao ambao wanapiga kama mizimu angefanya nini lakini pia aliamini duniani kuna binadamu na watu.

” huyo achana naye, huwa sina muda wa kumuuwa mwanamke” alijibu Roi.

“kaka hawa ni hatari zaidi ujue kuliko wanaume” alikazia Frank.

“Kunakitu cha thamani sana alinipatia na haya ya kumuacha aende ni malipo yangu kwakwe. Brazil ninafamilia hivyo ninaimani siku moja anaweza kuwa mwenyeji wangu hivyo sitapenda umguse” Maneno hayo yakamfanya Frank acheke sana lakini pia yalimfanya Dede apumue kwa nguvu hadi matiti yake kupanda juu na kushuka hali iliyopelekea Frank kuona, akazidisha kicheko na kutoka mule ndani.

“Muwahi Petii haraka sana tuondoke” alisindikiza kwa maneno hayo Roi kisha akatoa ufunguo wa gari mfukoni na kumpatia Dede.

“mbele ya lango la hii Ngome kuna huo usafiri, tutaonana tena” akasema kisha akatoka na kumucha Dede akiugulia maumivu ya tumbo huku akijitazama kama ametoka kweli akiwa hai. Hakukuwa na Bencov wala nani. Wao walikuwa ni vibaraka tu ambao hata vifo vyao havina doa la maumivu kwenye mioyo ya waliowaweka hapo. Walipewa majina ya waasi wa Kampuni hiyo Yeye akilibeba jina la shangazi wa Bencov huku kiongozi wao ambaye kwa macho yake ameshuhidia akifa kifo kibaya kilichopelekea hadi bosi wao kukimbia, akibeba jina la baba mkubwa wa Bencov lakini Benson ambaye alikuwa ni mpenzi wake, akibeba jina la baba mzazi wa Bencov. Lakini ni majina tu bila kuwa na thamani ya kweli. Kama si huruma ya mtu huyo wa kiafrika ni wazi historia yake ingefukia hapo. Ama kwa hakika akapata kujua kuna watu na viatu. Na katika hao wao ni viatu na mvaaji ameichoka thamani yao. Akashusha pumzi nzito huku akijizoazoa na kujilazimisha kuondoka mahali hapo asije kuingia kwenye watu wengine wenye hasira naye. Moyoni alimshukuru Mungu kwa kumuumba mwanamke. Kwani bila hivyo adingemjua Roi na asingemkosa kizembe kwa risasi pia asingeiona huruma yake mahali hapo.

Petii alinyanyuka lakini alishindwa kutembea kutokana na uzito wa silaha iliyompiga. Frank akafanya jukumu la kumbeba. kumpeleka mahali gari ilipo, wakati Frank akiwa anatokea upande wa mbele, alimuona Roi akiwa anashuka kwenye gari lililopo mbele kabisa ya lango la BBD Mining. kitu ambacho kilimfanya azidi kucheka hadi anafika kwenye gari akampakiza Petii. Hata petii alipomuuliza anachochekea, hakuwa na jibu lolote na hadala yake alibaki kimya, Petii akataka kujua kinachomfanya Frank kucheka kiasi hicho lakini Frank alishindwa kusema kutokana na kuoneshwa ishara ya kugunga kinywa na Roi. Frank akanyuti huku akimuachia maswali Petii. Muda mfupi tu wa kuwa hapo, waliona gari moja ndogo ikiondoka kwa kasi kubwa ikielekea mjini.


HALI YA NCHI ILIKUWA IMEPOA sana kiasi cha kuwafanya watu waendeleee na mambo yao ya kila siku lakini walitakiwa kuchoma mazao yao yote ya vyakula ambavyo walipanda kwa kutumia mbolea ya Diet Pills kama walivyo tangaziwa. Watu kufa na kuumwa ikapungua sana. Roi alitoka mwenyewe taratibu hadi kwenye kampuni ya TN. Race. Akamkuta Tamimu wakapiga soga za hapa na pale kisha Tamimu akamwambia kijana huyo kuwa kunazawadi yake ya gari ambayo alitakiwa kupewa siku ya kwanza kabisa wakati amesaidia yeye kuwa bingwa mbele ya Dou. Roi akamwambia kuwa mbona hilo analijua sana na hiyo zawadi ataichukua siku ambayo anaenda Tanzania. Wakati wakiwa wanapiga vinywaji na kupiga soga, kuna kishindo kikasikika mahali na kutulia kimya sana. Machale yakamcheza Roi baada ya kishindo kile kusikika.

“kuna kitu kitakuwa kimedondoka” alisema Tamimu aliyekuwa amelaza mikono kwenye meza na kuinamisha kichwa kidogo mbele.

“Hapana hicho ni kishindo cha mtu…..!” alisema Roi huku akitazama mahali kiliposikika hicho kishindo. Hajamaliza kusema, akaona kivuli cha mtu. Hapo hapo akakisukuma kiti cha Tamimu ambacho kilibinuka na Tamimu akajibingilisha kwa chini. Kisu kilichorushwa kistadi kikapasua chupa za mezani. Inamaana mtu huyo alilenga shingo ya Tamimu. Roi hakupoteza muda. Alijibinjua na kukamata chupa moja ambayo ilikuwa na kinywaji ndani. Kwa ufupi ni kwamba ilikuwa bado haijatumika, akairusha mahali ambapo adui yupo kwa nguvu nyingi kisha akachomoa bastola yake ndogo na kuilenga ile chupa. Chupa ile ilikwenda kupasukia karibu kabisa na Sura ya adui. Yule mvamizi akapata maluweluwe hadi anakuja kukaa sawa, Mateke kama mane hivi ya chapchapu yakakichakaza kifua chake, teke la tano likambabatiza na ukuta.

“Dou, kumbe bado upo hai!” alistaajabu Roi.

“Aah! Mshenzi wewe, unashida gani na mimi kila siku unaniharibia mipango yangu” aliongea Dou.

“Ni kitu kidogo tu kama unataka nikae mbali nawe ni kuachana na hili”

“Lipi?”

“Hili unalolifanya la kutaka kumuuwa mtu ambaye hana vita nawe”

“Ha ha ha haaaa! Wewe kweli mjinga, yaani mtu ameharibu ndoto zangu halafu nimuache atanue, wewe ndiyo unatakiwa uondoke uachane na vita hii isiyokuhusu”

“Kumbuka kuwa hakuna tena mtu ambaye atakutoa gererzani pindi utakapoingia tena”

“Usinitishe bwege wewe!” Alisema Dou huku akiruka kwa mapigo ya hatari sana. Roi akarudi nyuma lakini hakupata muda wa kuweza kuyakwepa yote, ilikuwa ni mitindo ya kuogopesha sana aliyokuwa akiitumia Dou mahali hapo. Roi alikula ngumi kavu za uso hadi akaziona nyota. alipokuja kuwa sawa alimuona Dou akiwa amejiweka sawa akimtazama.

“Nataka nikufundishe jinsi watu wanavyopigana. Alisema Dou huku akija tena, sasa wakawa wamekutana katikati, walipeana distance ndogo sana. mikono ikawa ndiyo iliyokuwa ikicheza hapo kati. walitumia mwendo huo kwa muda wa kama dakika moja nzima ndipo Dou alipobadili ghafula na kujigeuza akaja na pigo moja la ajabu ambalo lilimpata Roi mbavuni. Roi akarudi nyuma, pasipo kutulia, Dou alikuwa juu akija kama Popo gizani. mateke mawili ya kuisabia yaliyotua kwa vishindo tofauti, vikamaliza safari ya Roi kwenda mpaka chini. Dou alijufuta mikono huku akizunguuka pale kwa tambo kubwa.

“nilitaka kuwa mfalme wa Sami Ado, usifikiri ufalme ule nilijipa tu kizembe, nilikuwa na lengo la kutengeneza falme kubwa ambayo baadae ungekuwa tishio na inayoogopwa sana ndani ya Afrika hii” alibwata Dou kwa kila pigo alilokuwa akitoa. Roi aliamka na kujiweka sawa lakini akakuta Dou ameshafika na maguo yake marefu ya moja kwa moja akampiga Roi pigo baya lililomfanya kijana huyo kutoa mguno wa kulisikia pigo hilo kwani lilikwenda kuibua maumivu makali sana kwenye kifua chake.

“Mh!” aliguna Dou kisha akazikamata nywele zake na kuzirudisha nyuma akasema.

“Mwalimu aliyekufundisha anaoneka alikuwa akihitaji kufundishwa kama wewe mwenye, mbona uko mlaini hivyo” wakati anasema hivyo, Roi alikuwa amesimama kama goigoi, lile pigo lilikuwa si zuri kwake, Dou akasema kuwa sasa anakwenda kumtoa nje ya mchezo. Kwa jinsi ambavyo huyo kijana alivyosimama, akajua ni kumaliza tu na kuondoka. Akaja mkavu na kuleta pigo moja la komfuu la kunyoosha mkono mmoja mbele kisha kuuzungusha akiwa na lengo la kuleta madhara kwenye shingo la huyo kijana. Roi alikwenda msamba mdogo na kupiga ngumi moja nzito sana chini ya kitovu. Pigo hilo huwa mara nyingi halina mtaalamu wa kulizuia au kukaza tumbo, labda kwa mtindo mwingine. Pigo hilo likiingia sawasawa, madhara yake ni makubwa sana kwani linaweza kupasua kibofu cha mkojo. Dou aliganda kama sanamu kisha akatulia kwa muda. Roi akajua anamaliza kazi lakini Dou alijigeuza na kutaka kuleta madhara kwa mapigo ya nyumanyuma. Roi akajirusha kando na kujisukuma kwenda juu, akajizungusha na kumpiga teke moja zito kwenye shingo. Dou akaenda chini lakini kabla hajafika chini alirusha kisu ambacho kilichana fulana ya Roi kwenye upande wa mbavu za kushoto. Ilikuwa ni hatari sana sema tu bahati ililala upande wake. Dou akajinyanyua kwa kasi kubwa huku usoni akiwa anavuja damu. Mkononi alikuwa na kisu kumoja kirefu sana kama Jambia. Hakuweza kuthubutu hata kukitumia hicho kisu, mbele yake kulikuwa na mitutu kama sita hivi ya bunduki. Alikuwa ni Inspekta Bogo akiwa na vijana watano wa jeshi la polisi.

“Huna ujanja tena, angusha silaha yako chini kabla hujadhurika” alipaza sauti Insp. Bogo. Dou akadondosha silaha ile chini kisha akakubali kuvishwa pingu mbele ya mitutu ile ya bunduki. Bogo alimtazama Roi kisha akampigia saluti na kumpa hongera kwa kuweza kumleta huyo muasi wa nchi kwenye mikono ya Serikali kwa mara nyingine. Pia Tamimu alipewa kongole kwa kuweza kutoa taarifa mapema juu ya uwepo wa huyo kiumbe. Dou akachukuliwa na polisi akiwa amefungwa pingu na nyororo za miguu ikiwa ni kumlinda asitoroke hata kwa bahati mbaya.

Miguno ya mapenzi ilikuwa ikirindima ndani ya chumba kimoja kwenye nyumba ya siri ambayo Roi alitakiwa aendelee kuwepo hapo hadi amri kutoka kwa mkuu wake itakapotolewa baada ya uchunguzi uliokuwa ukifanywa na kitengo chao kukamilika. Ilikuwa ni saa 2:06 za mchana. Ikiwa ni baada ya siku tatu tangu kutulia kwa hali ya hewe ndani ya taifa la Ungamo baada ya kutuliza ghasia ile ambayo imemalizika robo tu, nusu na robo ikiwa bado. Anaonekana Petii akiwa juu ya mwili wa kijana mkakamavu wa Kitanzania akijishughulisha kupokea raha na kutoa raha. Walikuwa wakinyonyana ndimi zao vijana hao wawili kwa raha zao. Ilikuwa ni burudani ya aina yake sana huku kila mmoja akionekana kufarijika na kile alichokuwa akikifanya, nguo zikatupwa kando na kuanza kucheza mchezo wa kikubwa, mchezo wenye heshima kwa mwanaume kuufanya kwa sababu kuna wengine cha kushangaza hawafanyi na sijui sababu, ila sina hakika labda wanafanya kinyume chake, Mungu anawaona na atawahukumu. Mchezo ambao huruhusiwi wewe wala mimi kuuona na ndiyo maana walilitafuta shuka lilipo na kujifunika kukunyima chabo.

“Sitakusahau hata iweje” baada ya dakika arobaini na tano ndipo wanapata wasaa wa kuongea na Roi ndiye aliyekuwa anatamba hadithi za uwongo hapo.

“mimi ndiyo sitakusahau ila wewe unawanawake zako huko unafikiri utanikumbuka!”

“Wewe huna,…..haya nidanganye kuwa huna….tuache utani na maneno mengi, umenifurahisha sana. Nini kinafuata kwako baada ya hapa?” aliuliza mwishoni Roi wakiwa bado wamejifunika shuka.

“Tambuwa kuwa nimemaliza kazi yangu na niko huru kurudi nyumbani lakini sitarudi nyumbani hadi nijue nini kinafuata, najua yule mrusi amekimbia Roi, hivyo hata kama ni Urusi tutakwenda wote hadi mwisho wa mchezo” alisema Petii. Roi akamwambia sawa lakini alikuwa hajui nini kikombele yake. Kwa hiyo hata hiyo sawa aliyoitikia aliona ni kawaida tu kutokana na kuwa hakuwa akijua mchezo ulivyo. Mara hapo hapo kompyuta ndogo ya Roi ya kazi ambayo ilikuwa iko on, ikaleta ujumbe. Roi akashtuka na kukurupuka, Kompyuta hiyo huwa haiingii ujumbe kizembe, huwa inaingia ujumbe wa kazi tu. Akaelekea mbele ya ile Kompyuta akiwa mtupu kabisa kisha akafungua ujumbe upande wa barua pepe na kufungua barua pepe iliyoingia. Akaitazama akiwa kasimama vile vile mwishoe akajikuta anakaa taratibu. Akaisoma hadi mwisho, akashusha pumzi nzito kisha akaizima hiyo kompyuta na kuvaa nguo zake haraka na kuwataka wakutane sebuleni.

“Jamani safari iliyopo mbele yetu ni ya Madagascar, mchezo unakwenda kumalizikia huko. Nimepokea ujumbe kuwa watu waliosababisha huu ugonjwa ambao umeuwa ndugu zaetu wengi na kutuachia majonzi, walikuwa ni watu kutokea huko madagascar. Hawakuwa watu kutokea shirika la chakula duniani bali waligushi vyeti pampoja na hati za kusafiria huku wakiwa wamevaa sura zisizo zao. Huo ulikuwa ni mpango maalumu kabisa uliopangwa na watu wenye nia mbaya na bila shaka huu mpango utakuwa na sababu kubwa ndani yake. Kwanini ni nchi hizi mbili pekee?” aliongea Roi akiwapa taarifa wenzake ambao walikuwa kimya wakimsikiliza hatua kwa hatua.

“Nina mashaka hata sumu iliyotumika kuwaulia wale askari kisha Backa kutekwa yeye na binti yake, ilitengenezwa na hao watu, niwaambie tu kitu kimoja ni kwamba, kazi iliyopo mbele yetu ni kubwa mno na tunaweza hata kupoteza uhai wetu kama tusipokuwa makini. Nimepewa siku moja ambayo ni leo, kuanzia kesho tunatakiwa tuwe Madagascar” alizidi kusema Roi. Frank akashusha pumzi kubwa sana kisha akakumbuka mengi kichwani mwake, kikubwa alichokumbuka ni ndoto ambayo aliwahi kuiota kipindi cha nyuma, akakumbuka jinsi ambavyo alimuuliza mwalimu wake lakini hakupewa jibu zuri akaambiwa aje kwanza awamalize mahasimu wake ndipo arudi kwani atakuwa amepata mwanga wa kuifasiri ndoto yake hiyo. Kichwa kilimuuma sana kwa muda huo mfupi lakini hakujua sababu hasa za kichwa hicho kuuma.

“Kila mtu ajiandae mapema kwa mavazi ya kazi na zana nadhani yale mavazi tuliyoyatumia kuangamiza kile kikosi cha yule mrusi, ndizo tutakazozitumia huko” alisema Roi kisha akanyanyuka na kuingia chumbani kwake ambako alipita kwenye njia aijuayo mwenyewe na kutokea chini ya ardhi. Huko alichukua kila kitu ambacho kinafaa kwa safari, alichukua kila kitu na vingine kuwapa Frank na Petii kisha wakafungasha mizigo ya kwenye mabegi na kuisubiri siku inayokuja kwa hamu.

“Yalikuwa ni majira ya saa 04:01 za jioni. Frank bado alikuwa akiitafakari safari ya Madagascar lakini hakuwa akipata fumbuzi ya wazio lake kila ubongo wake ulivyojitahidi kufukunyua ili ilete majawabu aliishia kushusha migumio tu ya kukata tamaa.

“Frank!” aliita Roi akiwa kasimama pembeni ya kijana huyo. Frank hakuitikia bali alibaki kasimama vivo hivyo tu.

“Umekuwa ni mtu wa ajabu sana usiyetabirika na nimependa uwezo wako lakini natakiwa nijue ni nani aliyekufundisha au ulijifunzia wapi mapigano, samahani sana kama nitakuwa naingilia mambo yako” aliongea Roi. Frank alitulia kimya kisha akamgeukia Roi na kusema.

“Aliyenifundisha ni mtu makini sana na alikuwa na Lengo na mimi la kutaka nitimize kile nilichomuomba anisaidie” aliongea Frank kisha akageuka kabisa na kuendelea.

“Nakumbuka ni siku ambayo nilikuwa nakimbia kifo, siku ambayo nilimtia uchungu wa kufiwa yule mjinga aliyekuwa Rais wa zamani”

AKAKUMBUKA.

“Msitu ulikuwa mkubwa sana, wakati naianza safari nilikuwa na jambo moja kichwani mwangu kuwa nakwenda kujificha na kuishi msituni lakini siku nitakayo rudi nitarudi kwa ajili ya kumalizia n’ngwe kubwa niliyoibakisha lakini safari ilivyokuwa ikizidi kusonga nami, nikaanza kuifuta imani yangu ya kuwa siku moja nitarudi. Niliamini kuwa maisha yangu yote yanakwenda kuishia msituni na sitaweza kurudi tena. Nyuma sikuweza kurudi tena Roi kwani askari wengi waliotumwa na yule balaadhuli asiye na huruma wala hofu ya Mungu, walikuwa wakinifukuza kwa risasi kali na mbwa waliokuwa wanajua kuinusa harufu ya kile wanachokitafuta. Nikaingia ndani ya msitu wa hofu, msitu mkubwa, msitu wenye giza ambalo sikuwahi kuliona popote duniani. Sikukata tamaa japo nilikuwa nimechoka sana lakini sikukubali nikamatwe kisha niuwawe huku maneno makali ya kukashifiwa na matusi yasiyohimiliwa na moyo wenye nyama kama wangu, matusi ya kushindwa kulipa kisasi cha wazazi wangu ambacho niliapa ningelipa kwao. Wakati nazidi kusakanya Mbuga ile yenye miti mikubwa iliyofungama na kuijengea jina tishi la Msitu mnene. Nilikuja kujikuta nimepiga mweleka na kudondoka chali miguu na mikono ikiyangayaga huku roho ikimangamanga mithili ya itakayo kuacha mwili. Nilikuwa niko kwenye mteremko mkali wenye majani makavu. Nilisererershwa na kuburutwa kwa umbali mrefu sana hadi bondeni kwenye kondo za maji. Bahati ilikuwa upande wangu kwani sikuweza kupigishwa kwenye mti wala kisiki na sikupata kutua kwenye mawe na majabali makubwa yalichongana yenye mianya hafifu kwavyo ilivyofungamana. Sikuwa na haja ya kupoteza wakati, nilipiga mbizi kwenye kile kijito kidogo kisha nikatumia nguvu ndogo nilizo nazo kupanda mlima ambao sikuwa nikijua mwisho wake. Iliniwia ugumu sana lakini sikuwa na njia mbadala zaidi ya kuendelea kukimbia. Nilikimbia japo kwa shida hadi kufika juu ya ule mlina nilikuwa hoi bin taabani. Sikuwa na uwezo wa kukimbia tena, nilidondoka na kutulia kimya. Sikujua nilikaa kwa muda gani pale chini lakini nilikuja kushtuka baada ya kusikia milio ya bunduki, nilipoangalia kule kolongoni niliona kundi kubwa la askari wakiwa wamesimama kwenye ule muinuko wa upande wa pili. Risasi zilinikosa kwa sentimita chache lakini muda huo huo niliona kitu cha ajabu sana kilichokuwa kikiwatokea wale askari Kulitokea wanyama mithili ya Dubu, walijeruhiwa sana wale askari, kundi la wanyama lilikuwa kubwa sana kuzidi wale askari.

“Mungu wangu! HII NI DUNIA AU KUZIMU?” nilijikuta kiongea hiyo kauli mwenyewe bila hata kupenda. Hofu ilikuwa kubwa. Wale askari walitafunwa wote wakapotezwa, sauti za wale wanyama ikanifanya kuwa na hofu ya kuzidi. nikaamka na kuanza tena kutimua mbio nikadondo, nikaamka, nikadondoka tena. Nilipokuja kuamka, nilijikuta nikitazamana na mzee mwenye ndevu nyingi nyeupe na nywele nyeupe zilizofunika uso wake. Nilipiga magoti pasipo taraji. Mzee yule alikuwa haneni jambo bali ni wa kunitazama muda wote tu.

“Nisameheme babu” niliomba radhi huku nikiamini ule ulikuwa ndiyo mwisho wa maisha yangu. Hakuwa na silaha ya aina yoyote ile zaidi ya mkongojo mfupi uliomsaidia kusimama ukimtazama kwa woga. Nilipoona hasemi jambo, nikajua huwenda si kiumbe kifaacho kwangu, nilijua labda ni mzimu, shetani, kibwengo au kilembwekezi. Nikakurupuka na kutimua mbio ndefu sana za uchovu wa kuchoka kwa kwenda mwendo mrefu. Babu yule hakusumbuka kunifukuza lakini nilipokuwa nakimbia, nikasikia mvumo mkubwa ukinifuata kisha ukanipita juu vuuuu! Nikamuona yule babu akiwa anadanda mti wa mbele na kutua tena mbele tangu. Nikadondoka kwa kishindo na kuanza kulia kwa kukata tamaa lakini ghafula mawazo dhidi ya hitaji la msaada wa kulipiza kisasi changu, ikanijia, nikajikuta nacheka huku machozi yakinitoka. Babu yule akanitazama kwa makini sana huku akiwa anazungusha kichwa chake kilichofunikwa na nywele akanisogelea na kuniuliza.

“wewe ni kiumbe kutokea wapi?” Nilishangaa lakini nilipata faraja baada ya kujua kuwa ni kiumbe mtu yule babu na anaongea lugha ninayoifahamu.

“Nimeto…..kea..Pande!” Nilimjibu nikiwa na hofu sana.

“Umepotea, au nini kimekuleta hapa?” akaniuliza tena.

“Mh!,mh!…Nilikuwa….kuna watu….nafukuzwa!” nilimjibu nikiwa bado na hofu kubwa sana. Yule babu akaangalia juu kisha akataka nimpe sababu za kufukuzwa kwangu, nikamsimulia mwanzo mwisho. Akaniuliza lengo langu nini. Nikamjibu kuwa nilipe kile nilichofanyiwa. Babu hakusema kitu, aliondoka bila kusema kama amekubali kunisaidia au hakukubali. Sikuwa na chaguo zaidi ya kumfuata.

Huwezi amini Roi kuanzia hapo mimi na yule babu hatukuongea tena kwa maneno zaidi ya vutendo tu, mazoezi mazito yakaanza hadi nikawa fiti. Siku za mwisho za kutaka kurudi nyumbani ndipo nikaanza kuota ndoto za ajabu zilikuwa ni za ajabu sana na nilipomwambia kuhusiana na ndoto zile hakuwa akinipa majibu lakini siku niliyokuwa namuaga, ndiyo aliyoniambia kuwa. Vita yangu imeingiliwa na angamizo. lakini mimi si wa kulimaliza angamizo hilo bali nije kupambana na nilichokitaka kisha nirudi kwake kwa ajili ya kumaliza hatua ya mwisho ya kufasiri ndoto ambayo ni njia ya kumaliza angamizo hilo”

Kumbukumbu ya Frank iliishia hapo kisha akageukia kule alikokuwa amegeukia mwanzo.

“Kitu kimoja brother Roi ambacho nataka unisaidie, ni kuacha niende nikamalize hatua ya mwisho ya ndoto mbaya niliyoiota kisha nifuatane nawe hadi Madagascar” alisema Frank.

“Lakini mbona angamizo limeshakwisha Frank. Angamizo ni hili gonjwa ambalo limeuwa sana….”

“No,”

“Nini sasa?” alizidi kuhoji Roi.

“Lipo angamizo kubwa, angamizo linalohitaji kufasiriwa kwa ndoto yangu ya kutisha” alisema Frank akiwa anamgeukia tena kijana huyo.

“Mh!” akaguna Roi kisha akazama kwenye tafakuri nzito sana. Kijana huyo alikuwa akimhitaji sana kwa ajili ya msaada, kwake alikuwa ni mtu muhimu mno.

“unajua kuwa kesho tunatakiwa kusafiri kwenda Madagascar?” ilibidi kuuliza Roi.

“Najua lakini ninaimani kufasiriwa kwa ndoto hakutafuni masaa mengi labda madakika” alijibu Frank.

“Now” alisema Roi.

“unamaanisha?” Frank akauliza.

“Namaanisha mguu wako mguu wangu hadi kwa huyo babu kisha tunarudi leo hata kama ni usiku ili kesho tuwe Madagascar” alivyosema hivyo Roi hakukuwa tena na muda wa kupoteza kwani waliingia ndani wakamtaarifu Petii kuwa wanatoka kidogo lakini watarudi. wakatoka nje na kuchukua usafiri wa pikipiki kubwa na kuingia nalo barabarani. Kasi ilikuwa kubwa sana mwendo aliokuwa akitembea Frank haukuwa wa kitoto. Walizidi kuikata lami mwisho wakaicha lami na kuingia kwenye changarawe na kuishika barabara ya mguu mmoja. hatimaye wakaingia kwenye msitu mkubwa lakini haikuwa njia ambayo alitumia Frank wakati anaingia humo msituni kwa mara ya kwanza bali walitumia njia ambayo, Frank alielekezwa na babu aitumie wakati anatoka msituni. Walizidi kuzama katikati ya msitu hadi wakaenda kutokea sehemu yenye mteremko wa saizi, hapo palikuwa wazi kwa juu hakukufungamana sana. Mbele kulikuwa na msitu mkubwa wa kutisha sana.

“Tunazama ndani ya ule msutu kaka” alisema Frank.

“Frank tusidanganyane, mbele kule ulipoanzia msitu hakuna njia kabisa kuna moshi mzito halafu unaniambia tunapita kwenye ule msitu?” Roi alistaajabu.

“njia si ile pale inaingia ndani ya msitu, huo moshi uko wapi kaka”

“Frank come on, kama siyo moshi basi ni ukungu ule, hakuna njia ndugu yangu. Mabishano yalikuwa makubwa sana lakini Frank alipinga kabisa kuwa eti, hakuna njia wakati yeye njia anaiona. Akaliondoa pikipiki kwa kasi kubwa sana. Roi aliona wakienda kugonga kwenye ukuta mkubwa sana wenye mawe. Ukungu ulikuwa mzito si kifani. Akataka kupiga kelele lakini alichelewa kwani tayari Frank alishapita katikati ya ule moshi mzito kisha pikipiki likazuiwa hapo na wao kila mmoja alichomolewa kwa namna yake wakarushwa juu huku wakipigwapigwa kwenye matawi ya miti kisha kurudishwa chini, wakaanza kubingilia kwenye korongo kubwa. Hawakuweza kuonana hapo tena kila moja alijikuta akitulia sehemu yake. Roi akitua kwenye tambarale lililo katikati ta giza la msitu huo huku mbele yake kukiwa na mwamba mkuwa sana. Akiwa anashangaa asijue nini la kufanya, upepo mkali ukavuma na hatimaye akasikia mvumo vuuuu! Kisha kishindo kidogo mbele yake.

“Mungu wangu!” alishtuka Roi nusura akimbie alikuwa ni babu mwenye mwele nyingi nyeupe na ndevu zenye ushabaha na nywele hizo. Babu yule hakuongea kitu bali alikuja kwa kasi sana na kuanza kuleta shambulio kwa Roi. Roi kama mzimu alisimama na kuleta pingamizi kwa babu huyo. Mapigo ya yule babu yote yakaishia kwenye mikono ya Roi.

“mh!” Babu akagumia kisha akakaa tenge, akaja kwa mtindo mwingine wa kulala kishazari akiwa angani, mateke aliyokuwa anapiga yalikuwa yanakuja kwa kasi kubwa, na vile alivyolala kishazari, Roi akawa kapinda mgongo nyuma maeneo ya kiunoni huku akiwa anazunguuka pale chini kufuatana na mwendo wa babu yule. Mikono yake ilichoka sana kuweza kuhimili kasi ya kuzunguka na jinsi ya kukinga. Akajikuta akiruhusu mateke matatu yote kumuingia mwilini. Babu akashuka huku akikenua tabasamu kwa chati. Roi alikuwa ametupwa nyuma na kuserereka kwenye majani makavu. Akasimama. Babu akawa anakuja kwa kasi ya kimbunga, Roi akakumbuka Pigo moja alilokwisha kufundishwa na mwalimu wake kwenye mkasa uliopita akafumba macho lakini ghafla kumbukumbu ya Frank ni wapi alipo ikamjia, historia mbaya ya viumbe wa ajabu pia ikamjia kichwani, akajikuta akipoteza hisia za lile pigo.

“Fraaaaaaank!” akaita kwa sauti ya juuu sana. Babu ambaye alikuwa ameshafika na kutaka kuachia pigo moja lenye madhara makubwa lilikuwa limeishia katikati. Ngumi kakamavu ilikuwa inakaribia kupiga chini kidogo ya chuchu ya kushoto ya Roi. Mkono wa Babu ukawa unatetemeka huku akiwa amefumba macho. Roi akashangaa kwanini babu huyo hakufanya alichokikusudia akamuangalia vizuri kisha akatengeneza picha ya simulizi aliyosimuliwa na Frank. Mara hapo hapo Frank alikuja na kushangaa mkao wa babu ulivyo. akampiga kofi huku akimuita kwa jina alilokuwa akipenda kumuita.

“Lonzo”

“Frank wewe ni mshenzi sana” alisema huyo babu huku akirudi katika hali ya kawaida. Akamtazama Roi kwa hisia kali kisha akasikitika sana.

“Kama si hisia zako juu ya Frank. Ningekuwa si hai tena” Alitoka hapo huyo babu kisha akawaambia.

“Humu hakuja wahi kuingia gari wala baiskeli, ni rahisi kuingia humu kama ulishawahi kuingia na kutoka salama lakini kama hujawahi kuingia, huwezi kuingia kamwe na ndiyo maana uliona Moshi Roi” Roi akashtuka. Jina, ndiyo, jina lake amelijuaje. lakini haikusaidia kuwaza kwake. Babu akatupa mkongojo wake chini kisha akasema.

“Zuuuumbeee na Mulungu! Ni leo, nimeona ni leo, ni leo, ni leooooooo!” sauti yake ya kurudia kila hatua hilo neno ni leo, likawa linampa shida kichwani Frank. Kumbukumbu za ajabu zikawa zinamjia. Ni mwanamke, anaujauzito. mateso King, king, king, kiiiiiing. Mawazo yalimfanya ashike kichwa kwa jinsi yalivyokuwa mazito.

“Hahahaa, hahahaaa, hahahaaaaaaaa! Ni wewe ndiye uliyekuwa ukisubiriwa kwa ajili ya fasiri ya ndoto zangu mbili na yako, yako haieleweki hata ukiota mara kumi huwezi kuielewa zaidi ya kukuogopesha tu, ulitatakiwa uje nizichanganye ndipo tupate ndoto kamilifu” alisema yule Babu ambaye Roi alimfahamu kwa jina moja tu Lonzo kutokana na Frank kumuita lakini jina lake kamili aliitwa Seki Lonzo. Akasema huyo babu.

“Nakwenda kwenye fasiri ya ndoto yako sasa Frank ili mjue huko mnakokwenda kesho mnakwenda kufanya nini.

” Mwaka elfu tisa mia na ishirini na mbili, ninyi, wala si wazazi wenu, hamkuwapo katika dunia labda koo zenu. Kulikuwapo na viumbe waliokuwa hawafanani hawa walikuwa wakiishi katika dunia moja huko chini ya ardhi. Dunia hiyo ilikuwa ikifahamika kama NUSU YA DUNIA. Kutokana haikuwa na ukubwa kama ilivyo dunia hii bali hiyo ilikuwa na ukubwa wa robo tu ya dunia hii. Kwasababu wao waliishi kwa pamoja pasipo mabara wala miji, zaidi kwao zilitumika falme. Viumbe hawa walikuwa hawana utofauti na viumbe waishio juu ya mgongo wa Dunia lakini walikuwa ni wakubwa na wenye uwezo wa ajabu. Waliweza kubadilika vile watakavyo na kuishi mahali watakapo pasipo kudhurika na kitu chochote. Ugomvi wao mkubwa hawa ilikuwa ni katika tawala, hawakuwa wakiishi bila uongozi na hawajawahi kuzikana pindi mwenza wao anapoaga dunia/anapofariki. Walichokuwa wakikifanya ni kumla kila kiumbe anaepoteza maisha. Kuishi kwao kwa miaka mingi kukapelekea hata wao wahisi njaa kwa kipindi kirefu kwani hawakuwa na kitu kingine walichoweza kula zaidi ya kutafunana wenyewe kwa wenyewe pindi mmoja wao akifa. Siku isiyo na jina Utawala uliokuwa uko madarakani ukabadilishwa kwani kwa muda mrefu Dunia hiyo ilikuwa ikiongozwa na falme moja inayokwenda kwa jina la Biondo na mfalme wao walimuita King Bondo. Bondo wa kwanza akafariki dunia, akashika Bondo II naye akafariki dunia. Akaja akashika Bondo wa tatu. Huyu alipofariki Dunia wakakubaliana wabadili uongozi na waweke falme nyingine ambayo ni ya Kaisai ambao wao mfalme wao walimuita Kasai. Hawa walikuwa ni viumbe wanaotumia rangi nyeupe japo wao walikuwa na ngozi nyekundu na walikuwa wapole hakuna wa kupata kutokea mwenye upole kuliko vimbe hao. Sharti moja lilikuwa ni kila falme hula nduguye afapo lakini mfalme akifa huliwa na koo inayokamata madaraka. Hapa ndipo palipozuka mtiti Kasai walitaka kumla Bondo kwa kuwa wao ndio waliokamata madaraka, Bondo wakasema hawawezi kumdhalilisha ndugu yao kwa kumuacha aliwe na kasai.

Vita ya malumbano ya mdomo ikaanza. mwisho wa vita hiyo ya malumbano ya mdomo ilikuja kwisha na kuibuka vita ya malumbano ya kumwaga damu baada ya kiumbe kutoka Biondo kuja na bendera nyeupe iliyojaa damu. Hilo lilikuwa ni tusi kwa kaisai ambao hutumia nyeupe safi. Vita kali sana ikapiganwa vita ambayo ilirithishwa vizazi na vizazi na hatimae mfalme Kasai akauwawa na Biondo. Wao wakakamata madaraka na kumla Kasai ikiwa wao waligoma kuliwa mfalme wao.

Ogopa sana mtu mpole hasa unapomuuzi. Kaisai walichukia, walikasirika wakaamua kufanya kweli hadi Bondo au king Bondo akakimbilia juu ya mgongo wa Dunia hii tuishio sisi. Amekuja kujipa nguvu kwa kufanya maangamizi ya wanaadamu kisha yeye anywe damu za wanaadamu wote watakaokufa lakini Jamii ya kaisai nao wakamtuma kiongozi wao kuja huku ili naye atafute mbadala. Bondo alifanikiwa kwa kumhadaa mzee mmoja ambaye alikuwa si wa kuishi bali kufa baada ya kujeruhiwa na moto vibaya sana huko nchini Tanzania. Akamhuwisha na kumfanya kuwa hai kwa nguvu zake zilizo bakia kisha wakaingia makubaliano ya mzee huyo kutengeneza sumu ya kufanya maangamizi ili yeye aweze kunywa damu hiyo kwa wingi na kupata nguvu za kurudi Kwenye Nusu Dunia yao akaimalize jamii ya Kaisai. Hakujua kuwa, Kaisai viumbe wapole na wenye nguvu wametumia akili nyingi nao wakaja huku. Wamepandikiza kiumbe cha ajabu sana chenye nguvu nyingi kwenye mwili wa mwanamke ambaye ndiye aliyetengeneza Sumu ya maangamizi ya kumpa nguvu Bondo. Mwanamke huyo anakaribia kujifungua lakini kwa makubaliano au ahadi waliyokubaliana ni kwamba Ni lazima yeye na baba yake huyo binti baadaye waje warudi kwenye maisha yao ya kawaida. Kumbuka Bondo amemuhadaa yule mzee kuwa atamrudisha katika uhai wa kweli wa kuweza kutembea na kufanya mambo yake kama awali, lakini uwezo huo hana. Dr. Lee alishakufa zamani pale anatumia nguvu za Bondo tu. Kitu alicho kipanga Bondo ni kuingia kwenye mwili wa Dr. Lee na kumfanya asimame. Akisha simama ataangamiza wenzake wote kisha kumchukua Backa ambaye yupo katika mateso ambayo hakuna kiumbe aliyewahi yapitia. Akishamchukua atapaza sauti yake kuu ambayo itaupasua moyo wa Backa na kufanya Tereza aliyebeba mimba ya kiumbe mpya wa Kaisai asizaliwe.” akaweka kituo hapo huyo mzee kisha akatulia na kuokota mkongojo wake. akasema.

“Najua hii vita ni ngumu na kubwa lakini itakayochukua muda mfupi. Ni wewe tu utakayeweza kumfukuza Bondo kwenye mwili wa Dr. Lee kisha urejee porini ukisubiri siku za mlango wa kwao ufunguke aingie. Roi tambua kuwa kiongozi wa Kaisai hana nguvu tena nguvu zote amezimaliza kwa makuzi ya kiumbe hicho kipya” Kimya kilitanda. Roi akajua kumbe ujio wake hapo ulikuwa unafaida kubwa sana. Alitamani kusitisha kazi hiyo na arudi zake Tanzania lakini kila akimuangalia Frank, alihisi hatendi haki. Frank alijitoa kuwa naye na lazima yeye ajitoe pia kumrudisha Backa nyumbani ambaye alikuwa ni mtu pekee kwao waliyemhitaji sana.

“Tazama pango lililopo mbele yako, ingia kwenye hilo pango, ingia hadi mwisho na ukishatokea. Ujue mizimu na ndugu wa Kaisai watakuwa wanakutazama wewe na nguvu zao watazikusanya ziwe kitu kimoja kwa ajili ya ushindi wako nao wapate ushindi kwa siku za usoni. Ingia sasa na mkishapo mnaweza kwendaaaaaa!” sauti ilipaa, Roi akaingia kwa hofu lakini alijivika ujasiri na kuweza kulikabiri pango lile ambalo ndani lilikuwa jeusi tii! Alisonga mbele hakukata tamaa kwa jinsi alivyokuwa akijigonga kwenye mawe. Mbele yake aliona rangi nyeupe ya kung’aa, akajua pale ndiyo palikuwa nje. Lakini kumbe hapakuwa nje bali walikuwa ni wanajamii wa Kaisai ambao walikuwa wakimsubiri na kumapa nguvu kwa kutumia njia za maajabu na kihisia kwani wao hawakuweza kuja duniani kutokana na njia kufungwa. Roi alitoka mbio akijua ni nje lakini alishangaa akiwa hewani akianguka kwa kasi kubwa kuelekea chini. Kabla hata hajapiga kelele, akajikuta akitua kwa kishindo chini tii!” Akashangaa ni wapi alipo, alipogeuka nyuma akamuona Frank yuko juu ya pikipiki inamaana wote walijikuta wapo nje ya ule msitu wa Dabaa Lonzo, msitu wa maajabu.

Ilikuwa ni saa tatu za usiku, taa zilikuwa zikimulika kila upande. Bencov alikuwa amejiinamia kwa kushindwa kuimaliza Ungamo kutokana na mtoto mdogo kwake, Roi. Roho ilimuuma sana. Alikuwa hapo ndani ya Madagascar kwa lengo moja tu la kumuuwa Backa ili nafsi yake ilizike kwani hakuona haja ya kuwa hapo tena. Akimuuwa huyo nafsi kwake itakuwa nyeupe kabisa kuliko kuendelea kuishi na muuwaji wa wazazi wake. Aliona kama vile hata yeye ameshiriki kuwauwa wazazi wake. Lakini kitu kilichokuwa kikimnyima raha ni kimoja tu, ni mara si chini ya sita alishajaribu kutaka kumtoa Backa duniani lakini anazuiwa na Dr. Lee kufanya hivyo kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu. Mwili wake ulikuwa ukimtetemeka kwa hasira kali kwani hata ule ushirikiano yeye na Dr. Lee ulipungua akawa yuko pale kama mjinga fulani tu.

“Boss, hatuwezi kuwa hapa tena, lazima tufanye kitu tuondoke” Beda mtu wa karibu sana na Bencov alishauri.

“Unataka tufanyaje Beda” alihoji Bencov.

“Kesho asubuhi tunauwa kimya kimya kuanzia huyo anayemuita Lady Devil kisha Lonto halafu tunalipua hili jingo wote hawa wakiwa ndani nasi tunatoweka” lilikuwa ni wazo zuri sana kwa Bencov, alimuangalia Beda kisha akamuuliza kwanini wazo kama hilo hakulitoa mapema. Beda akasema kuwa alikuwa anahofia ukaribu wao ulivyo lakini sasa anaona ni sawa tu kufanya hivyo kutokana na ushetani wa wenyeji wao. Beda hasikusita kueleza mambo ya ajabu aliyokuwa anakutana nayo humo ndani akiwa anataka kumuona Dr. Tereza na mengine mengi yanayofanana na hayo kama ibada zao na vitu vingine. Bencov akapata picha hata zile harufu mbaya alizokuwa akizisikia za kama mzoga uliokuwa umeharibika vibaya. Hawakuwa wakijua kuwa wakati Bondo akija ndani ya jingo hilo huwa anachukua nguvu zake na kumuacha Dr. Lee katika hali ya uzoga na ndiyo maana hata ibada zilifanyika kwenye chumba chenye giza zito. Ile harufu mbaya ilikuwa ni ya Dr. Lee na ni tofauti na kama wao walivyokuwa wanadhani.

Moshi mzito ulikuwa ukivukizwa kwenye chumba ambacho mara nyingi Dr. Lee, Merina au Lady Devil pamoja na Lonto walikuwa wakikitumia kwa maombi yao ya kishetani. Lugha za ajabu zilikuwa zikitumika humo ndani. Sauti za muungurumo ambazo zilikuwa hazisikiki hapo kabla zilianza kusikika. Muungurumo ulizidi kisha Dr. Lee akasema kwa sauti ya chini yenye matumaini.

“King Bondo ameshakunywa Damu za wahanga wote kuanzia Tanzania hadi Ungamo yuko njiani anakuja kwa kasi kubwa sana nafikiri atafika hapa kesho au usiku mkubwa” baada ya kusema hivyo, wote pale wakanyanyua sura zao na kutazamana.

“Ushindi ni wetu na dunia ni yetu” alisema Merina bila kujua kuwa hapo walipo wako na mfu aishie kwenye nguvu za Bondo na Bondo akija anaingia kwenye mwili wa Dr. Lee kisha anafuta ushahidi wa kisasi cha baadae kisha anatoka na nguvu zake zote akiuwacha mwili wa Dr. Lee katika uzoga.

USIKU MKUBWA.

TEREZA alikuwa akilia kwa sauti kubwa sana, maumivu yalikuwa yakizidi kwa kasi kubwa lakini hakuona wa kumpa msaada, ule muda wa kujifungua ulikuwa ukikaribia. Ama kwa hakika kila kiumbe atazaa kwa uchungu. Tereza alikuwa na tumbo lililovimba vibaya sana huku likiwa na michirizi ya kama litakalo kupasuka. Hali ilizidi kuwa mbaya na alizidi kulia, sauti za kilio zilimfikia Bondo ambaye alikuwa njiani kutokea Ungamo. Anga alikuwa akiitawanya vibaya sana. Lakini kwa upande mwingine, Roi na watu wake walikuwa wemeondoka usiku uleule kutokea ungamo kuelekea Madagascar kutokana na hali ambayo ilikuwa ikimtokea kichwani Roi baada ya kupewa nguvu za ajabu na mizimu mapangoni ndani ya msitu wa Dabaa Lonzo. Saa nane za usiku wanaingia ndani ya uwanja wa kimataifa wa kisiwa hicho. Kichwa na hisia ndizo zilizo kuwa zikimuongoza Roi. Walichukua hoteli karibu kabisa na linapopatikana jumba la Dr. Lee.

HATARI YAIBUKA.

Saa kumi na mbili za asubuhi, mzizimo mkali unaibuka ndani ya jumba hilo alilokuwa akiishi Dr. Lee, siku hii ndiyo siku ambayo Bencov na kijana wake walipanga kufanya mauwaji ya kushtukiza, walikuwa wameshandaa kila kitu kwa ajili ya mauwaji. Waliamka asubuhi hiyo pasipo kuamini kuwa siku hiyo ingekuwa na mzizimo wa namna hiyo. Hawakujua kuwa Kiumbe chenye nguvu za ajabu kilikuwa ndani ya himaya hiyo na kilikuwa tayari kimeshazama kwenye mwili wa Dr. Lee. Mwili wa Dr. Lee ulianza mabadiliko madogo madogo kama kufunguka kwa sehemu zote ambazo alikuwa amefungwa. kama magozi ya mikononi, mask usoni ilikatoka na kuanguka kisha kumuacha na sura yake ile aliyo ihitaji. Lee aliamka kwenye Baiskeli yake na kusimama dede kukisogelea kioo. Akacheka sana baada ya kuona yuko vile alivyokuwa akihitaji awe. Alikuwa ni Dokta Lee kweli lakini roho ilikuwa ni ya kiumbe mwingine kabisa. Alicheka sana pasipokujua kicheko chake ni kitu kibaya kilichoweza kumtisha kila mtu mule ndani. Lee alianza kuuwa walinzi wote kwa kuwakamata shingo kisha kunyonya damu zao kwa kutumia hisia ya macho na mguso wa mishipa yake, kila aliyekuwa akimuachia alikuwa hana damu mwilini mwake. Aliunguruma kwa sauti kubwaa. Ndani ya dakika tatu alikuwa kasafisha walinzi wote. Kipindi hicho Lonto na Lady Devil walikuwa wanashangaa uwezo wa Dr. Lee kusimama na vitu vya ajabu ambavyo alikuwa akivifanya. Lonto alijua ni kwa wengine tu na si kwao kwani wao walikuwa ni watu wa karibu sana na mtu huyo. Alikuja kujikuta anakamatwa shingo na kunyanyuliwa juu kisha kutazamwa kwa hisia kali na jicho jeusi la kutisha kisha mishipa ya Dr. Lee ikaanza kuvimba na kupokea damu kutoka kwa Lonto. Merina alipoona hali hiyo ikabidi atafute namna ya kuokoa uhai wake kwani hapo hapakuwa salama tena. Alikimbia na kutaka kupita kwenye dirisha ambalo alianza kuminyana nalo kufungua. Dr. Lee aliutupa mwili wa Lonto na kuanza kumfuata Merina kwa kasi ya ajabu kwani hakutakiwa kumuacha mtu hata mmoja King Bondo, ambaye alikuwa akiuongoza mwili ufu wa Dr. Lee. Merina alikuwa akikazana kufungua dirisha huku akipiga kelele kwani kifo cha maumivu kama kile hakupenda kitokee kwake.

“Heeey! Mnakufa leo wewe na mashetani wenzako!” sauti ya Bencov iliyoshika silaha ya maangamizi ilikuwa ikipayuka huku Beda akiwa kaubeba mwili wa Backa ambao alitaka akaumalizie nje ya jingo lile huku akilipua moto. Dr. Lee akageuka kama Roboti jicho moja jeupe lenye mchanganyiko wa damu huku moja likiwa jeusi tii! Linalong’ara. Bencov alijikuta akirudi nyuma huku silaha ikimpa uzito, alijaribu kupiga risasi, hapo ndipo alipochoka na kuamua kuitupa kabisa silaha yake. Lee aliiwekea kiganja cha mkono ile rasasi akaikamata kisha akaiangalia kwa macho ya mshangao kisha akaiachia chini na kuwafuata kwa kasi ya umeme. Beda aliuwachia chini mwili wa Backa kisha akajaribu bahati yake ya kupiga mkono. Alidakwa hewani akazungushwa kisha akashikwa shingo pamoja na bosi wake. Damu zao zikawa mali halali ya King Bondo. Alipoiachia chini ile miili, akageuka nyuma ambako alimuacha Merina, akaona dirisha liko wazi ikimaanisha kuwa Merina alisha kimbia. Akatega sikio vizuri Lee, akasikia sauti kali ya kilio kutokea porini, akajua kuwa sasa Kiumbe chenye nguvu kina zaliwa na yeye hawezi kuona mahali alipo na kutafuta ni sawa na kuchelewa. Kikishazaliwa inamaana juu ya huu mgongo wa dunia siyo kwake tena kwani mtawala wa pande zote atakuwa amepatikana. Akautazama mwili wa Backa akajua hiyo ndiyo kinga iliyobakia ili Tereza asiweze kujifungua kwa hisia kutokana baba yake atakufa kwa kelele mbaya huku moyo ukipasuka. Akaunguruma Lee kama Simba dume. Kisha akaubeba na kutoka nao nje taratibu.

Roi alizidi kuwapitisha wenzake kwenye njia za ajabu hadi wanakaribia nyuma ya jingo kubwa alilokuwa akiishi Dr. Lee huku akifanya mpango wake wa maangamizi. Hapa walimuona binti akija kwa kasi sana upande wao. Roi akamtazama kwa hisia kali akamkubuka alikuwa ni Merina. Merina alikuwa akikimbia bila kuwa makini kutokana na kitu cha ajabu alichokiona kule ndani. Akajikuta amemkumba Roi na kabla hajafanya chochote, akakamatwa shingo lake.

“Ulinikimbia Tanzania Merina na kuniachia machungu sana moyoni, niliahidi kukuwa pindi nikikutia machoni. Leo ndio unakufa sasa” alisema Roi akiwa katika hasira kali. Akageuka nyuma.

Akiwa amemning’iniza Merina akiwa anampa maumivu makali mno.

“Frank, na Petii, hakikisheni Huyu malaya anakufa ndipo mnifuate” akaagiza Roi kisha akamrusha Merina Nyuma kwa nguvu nyingi huko akapokewa kwa kichapo kikali cha mwanafunzi wa babu. Roi akaondoka kwa kasi ya umeme ambayo unaweza kusema kapotea kwa jinsi alivyokuwa kwenye kasi hiyo. Akaja kukaa kwenye lango la kutokea ndani ya jumba lile.

Tereza aliitanua miguu yake akiwa katika hisia za maumivu makali sana, muda wa kujifungua kiumbe cha ajabu chenye nguvu kubwa, ndio ulikuwa umefika. Alikuwa akishika chochote kilicho karibu. Damu zilikuwa zikimwagika hapo si utani. Hakukuwa na kiumbe chochote cha kumsaidia kwa Kaisai alikuwa hana nguvu tena za kumkabili huyo mama wa mfalme wao. Alianza kujifungua sasa, sauti kali zilikuwa zikizidi kupasua ngoma ya Bondo au Lee. Alikuwa akizidi kutoka na mwili wa Backa kwa ajili ya kupaza sauti katikati ya uwanja ili asitishe kujifungua kwa Tereza. Hakuamini macho yake Bondo baada ya jicho lake jeusi lenye nguvu kumuona kiumbe mpya aliyesimama nje ya mlango. Alikuja kwa kasi kubwa kisha akamrusha Backa ambaye alianza kukakamaa kutokana na kuingia kwenye kipindi cha maumivu makali. Roi aliruka hewani akaudaka mwili wa Backa usifike chini. Hilo lilikuwa kosa kwa Lee alimzawadia Roi mateke mazito yaliyompeleka juu huku akiwa na mwili ule. Bondo au Lee alimfuata huko huko juu kisha akamuadhibu Roi kwa kichapo cha kutisha sana. Hawakushuka chini. Bondo alijua kuwa Roi hawezi kuuachia ule mwili ulikuwa na nguvu za kibinadamu na kwa umbali ule ni wazi ungepoteza maisha. Alitumia nafasi hiyo kutoa kipigo cha aina yake. Roi alipigika sana hadi akawa analegeza mikono na kutaka kuuwachia mwili wa Backa.

Huku nako kwa akina Frank mambo yalikuwa mazito, Merina alikuwa ni mtu hatari sana pamoja na uwawili wao lakini palikuwa na kazi kubwa sana. Merina aliweza kupangua mapigo na kuleta mashambuli kwa wote wawi. Frank akatumia akili ya kuzaliwa na ile ya kufundishwa na Babu Lonzo hapo ndipo alipomuweza huyo mtoto. Kitendo kile cha kuruka hapa na kukaa pale kisha kuja kupiga mapigo yaliyokuwa yakiondoka na baadhi ya nyama mwilini mwake, kilimbadilisha nguvu Merina na kujikuta akifa kama kuku bandani. Walipomaliza ile kazi, walikimbia na kuja huko kwenye maajabu ya mwaka.

“Mama weweeee! Haya mambo ni ya Duniani Kweli au Kuzimu Frank?” alishangaa Petii baada ya kuona Roi amepigwa pigo moja zito lililomtoa kule juu hadi chini akiwa na ule mwili. Aliuweka pembeni ule mwili wa Backa kisha akamtazama Bondo aliyekuwa anatua chini kwa tambo. Wakafuatana kwa kasi ya aina yake huku vumbi likitimka eneo hilo kisha wakakutania hapo katikati, Kitimutimu kikainuka watu walipigana kwa nguvu zao za ajabu lakini hawakudumu sana Roi akachezea tena na tena hadi chini. Ama kwa hakika moto huo ulikuwa si mdogo kwa kijana huyo. Pigo alilopigwa likamchosha kabisa.

Kule porini Tereza alikuwa akizidi kujifungua sasa mtoto alikuwa ameshaanza kuja duniani. Bondo akahisi hilo, akaangalia mahali alipo Backa akageuka na kutaka kuufuta ule mwili ambao ulisha maliza kipindi cha maumivu. Hakufika, mbele alikutana na Frank pamoja na Petii walikuwa wanajua lengo lake. Bondo akakasirika akarukia na kuwakamata shingoni. Kabla haja vuta hisia za kunyonya damu, Frank mzee wa kujikunja na kujikunjua, alijipindua na kumtandika Bondo teke la kwenye mdomo, Bondo akatema jino. Alikasirika sana alimrusha Frank juu kisha akampiga ngumi nzito ya kifua, Frank akatupwa mbali akiwa hana fahamu. Petii ndiyo alikuwa hana bahati kwani alinyonywa damu yote. Kile kitendo cha kuutupa mwili wa Petii chini, Roi aliona wakati ananyanyuka.

“Bondoooo!” alipiga kelele. Kelele zile zikapaa. Tereza akazidi kusukuma, alibakisha kidogo tu kumleta kiumbe kipya duniani. Bondo aligeuza shingo akiwa tayari anamwili wa Backa mikononi. Tambua kuwa Tereza alibakisha kidogo kuutoa mwili mzima wa mtoto mwenye nguvu duniani.

Bondo alipokea ngumi yenye ujazo iliyopiga kwenye uti wa mgongo. Ngumi ile ikazama kwenye mwili ule. Roi alipoitoa ngumi yake, Bondo akauwachia mwili wa Backa chini. Roi akageuka na pigo jingine la shingo, shingo ikalala upande mmoja. Akazunguuka kwa mbele kwa kasi kubwa sana. Alipotaka kubiga ngumi ya moyo, akakumbwa na harufu kali sana ya mzoga akajua Bondo ameshahama na kukimbia mji. Mwili uliooza wa Dr. Lee ukaanguka chini kama gogo bovu.

Kiumbe kipya kikawa Kimezaliwa na kimekuja Duniani na kumfanya King Bondo kuyakimbia makazi yake yaliyomfanya kurejesha nguvu zake kwa kumhadaa Dr. Lee ambaye maisha yake yalishafika mwisho baada ya kuwa alijeruhiwa vibaya na moto wa mionzi

Frank na Roi walihuzunika sana mbele ya mwili wa Petii ambao ulikuwa hauna Damu. Hawakuwa na Jinsi zaidi ya kuubeba na kuondoka na mwili wa Baacka hadi ndani ya jumba la Dr. Lee. Walifika naye ndani kisha wakaingia kwenye chumba kimoja . Walipofungua mlango walikutana na mwili wa mrembo uliokuwa kitandani. Hakuwa mwingine alikuwa ni Tereza.

Baada ya kufanikisha kumleta yule kiumbe mpya duniani, alipoteza fahamu. Hivyo akarudishwa hadi humo ndani akiwa amepoteza fahamu vivo hivyo. Hakuwa akijulisha kama alikuwa akiitunza mimba kubwa kuliko uwezo wa mwili wake pia haukuweza kumjua kama alijifungua. Mwili wake ulikuwa ni ulelue isipokuwa alikonda sana kutokana na kashikashi za mateso na karaha. Roi na Frank hawakujua wafanye nini, walibaki tu pembeni ya miili hiyo mitatu Hadi pale Tereza alipoanza kujitikisa hatimaye kufungua macho. Baada ya muda alisimama kabisa kisha kuinama chini ya uvungu na kutoka na kichupa kidogo cha dawa ambacho alichoma kwa bomba la sindano na kuivuta dawa yote na kumchoma baba yake kwenye mshipa mkubwa wa shingo. Kama unaku Backa alitulia kwa muda wa dakika tatu ama nne kisha akaanza kutetemeka kwa nguvu kisha kutulia tena. Baada ya masaa mawili, Backa alintanyuka kutokea kwenye maisha ya nusu kifo na kurudi tena duniani. Tereza alimkumbatia baba yake kwa furaha kubwa sana. Kama unakumbuka dawa hiyo iliyomuamsha Backa, ndiyo ile ambayo Tereza wa ajabu alikuwa akiitengeneza usiku wa manane.

Sauti ya Helkopta ilisikika nje ya jumba hilo. Wakatoka wote wane kwa furaha kubwa kisha wakafika mbele ya Helkopta hilo. Tereza alikuwa wa kwanza kuingia kwenye Helkopta kafuatia Backa ambaye alikuwa hana nguvu sana ya mwili wake kutokana na ukosefu wa chakula kizuri kwa muda mrefu. Roi aliinua simu kisha akasema maneno macheche.

“Tupokee uwanja wa ndege Tereza wako anarudi” kisha akakata simu yeye na Frank wakaingia kwenye Helkopta hilo la Jeshi kutoka Ungamo. Helkopta ilipaa angani na kulicha jeshi la polisi la madagascar likifanya uchunguzi wa lile jumba kisha kulilipu lote.

IKULU YA PANDE.

Shangwe ilikuwa kubwa sana hakuna ambaye alikuwa kwenye majonzi tena. Roi ni nani, Roi ni yule yule sasa ambaye nguvu za watu za asili ameziacha lakino ameacha jina kwa kiumbe wa ajabu ambaye bado yupo duniani anayetakiwa kwenda kuleta ukombozi kwa jamii yake. ROI JR.

Mikono ya pongezi na zawadi kutoka kwa Rais lakini pia hawakusita kutumia muda mdogo kuwaombea dua waliopoteza maisha kwenye mziki ule. Mh. Backa alipewa pole kwa yote yaliyomkuta lakini haikuwa na njia ya kuyazuia kwani Usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Roi akasindikizwa uwanja wa ndege pamoja na maiti ya Petii. walipofika kwenye uwanja huo wa kimataifa wa Tao De Air Port. Waliiga maiti ya Petii huku machozi yakiwatoka vijana wawiwili. Roi na Frank. Alikuwa mwenzao, alikuwa mshirika wao.

Baada ya hapo Gari ndogo matata sana ikaingia kwenye ndege kubwa kutokea Ranzania ambayo ilimfuata Kijana wao. Gari hiyo ilikuwa ni zawadi ya pekee kutpka kwa Tamimu. Ubavunu iliwa na maandishi makubwa ya TN. Race.

Backa alifurahi sana wakakumbatiana kwa mara nyingine lakini pia alikabidhiwa hati zake za mali zaje zotr na Tamimu. Ambaye baada tu ya Back kutekwa alituma mti na kwenda kubeba kila kitu.

Roi akapunga mkono. Dege likachukua kasi na kuamsha matairi yake kuikamata anga.

ROI JR, AZALIWA NI KIUMBE CHA AJABU KINACHOTAKIWA KIKALETE UKOMBOZI HUKO KWENYE DUNIA NYINGINE. KUMBUKA KUWA BONDO AMETANGULIA TAYARI JE ITAKUWAJE?”

NI NDANI YA MOTO NWINGINE WA KUTISHA ZAIDI. HAPA ROI MTOTO NDO MAHALA PAKE,

NUSU DUNUA (HALF WORLD)

ASANTE MUNGU KWA KUFIKA HAPA.

MWISHO.

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment