Mikono ya Jasusi Sehemu ya Pili
IMEANDIKWA NA: AHMED JIRIWA
*********************************************************************************
Simulizi: Mikono ya Jasusi
Sehemu ya Pili (2)
“Najua mwalimu…!” Alijibu huku akiwa na wasiwasi mara baada ya kukumbuka kitu ambacho aliamini hicho ndicho kilichopelekea kupigiwa simu moja kwa moja na mkuu wake wa kazi au mwalimu kama anavyomuita.
“Hujui Alan…hujui, laiti ungelikuwa unajua ungejua kwanini nasema hujui…!”
“Ni…!”
“No, Alan! Kuwa makini kijana wangu.” Akamaliza kuongea mwalimu kisha simu ile ikakatwa. Jabir au Alan kama alivyoitwa simuni na mwalimu, aliganda huku ile simu ikiwa mkononi mwake akili yake ikifikiria mengi. Machoni mwake kulikuwa na kazi tena kazi nzito na maelekezo ya kazi hiyo yalikuwa yapo kwenye mawasliano ya kawaida ambayo alikuwa akiwasiliana na mwalimu wake. Aligeuka na kumtazama Cecy aliyekuwa kifua wazi akimsubiri huku akiwa anamtazama yeye kwa macho ya kuuliza. Jabir aliirudisha ile simu kwenye nafasi yake kisha akalirudisha tabasamu na kurudi pale kitandani ambako alikaa kidogo na kufikiri kisha akanyanyuka na kuielekea tarakilishi yake akaifungua na kuiwasha, akawasha data kisha akaenda moja kwa moja hadi upande wa barua pepe ambako alikutana na ujumbe mrefu wenye maelezo yaliyoshiba lakini mwisho wa siku akakutana na ujumbe mwingine wenye maneno machache tu.
Jabir aliirudisha ile simu kwenye nafasi yake kisha akalirudisha tabasamu na kurudi pale kitandani ambako alikaa kidogo na kufikiri kisha akanyanyuka na kuielekea tarakilishi yake akaifungua na kuiwasha, akawasha data kisha akaenda moja kwa moja hadi upande wa barua pepe ambako alikutana na ujumbe mrefu wenye maelezo yaliyoshiba lakini mwisho wa siku akakutana na ujumbe mwingine wenye maneno machache tu. Ujumbe huu wa pili ndiwo hasa uliomfanya aamini juu ya mawazo yake yaliyokuwa yakipita kichwani mwake. ‘Fika jijini Nairobi haraka sana kutana na mtu anayefahamika kwa jina la Rhoda yuko mtaa wa Accra nyumba namba 66 (Accra Street).’ Ujumbe huu ulibeba taarifa hii. Akafikiri kwa kina kisha akaizima tarakilishi yake baada ya kumuona Cecy anakuja taratibu na kumfuata alipo. Cecy alimsogelea hadi alipo kisha akamshika mgongoni hata hivyo hakusubiri aongee chochote alisimama.
“Baby kama nilivyokuwa nimekueleza awali kuwa niko hapa nchini kwa likizo fupi hivyo likizo yangu inakomea hapa na natakiwa kuondoka na kwenda kuendelea na majukumu ya kikazi…?”
“Acha utani baby, usiweke masikhara kwa muda huu ambao nakuhitaji kuliko kitu kingine…!”
“Najua hata hivyo wewe pia unajua namna kazi zilivyo, siwezi kupingana na mabosi wangu hasa ninapopewa wito wa kurudi kazini.” Aliongea Jabir akiwa hana sura inayotangaza utani juu ya kile anachokizungumza na kwa wakati huo alikuwa akipanga vitu vyake tayari kabisa kwa safari.
“Unamaanisha Jabir…? Jamani mbona moyo wangu unataka kutoka mwilini, hata hivyo ni jioni sasa ni vema kama ungesubiri kesho?” Aliongea Cecy huku akimshuhudia kijana huyo akizidi kumalizia kufungasha virago vyake.
“Natakiwa kuondoka sasa na ndege ya saa kumi ambayo itanifikisha Afrika ya kusini kisha nitaweza kuunganisha ndege ambayo itanipeleka moja kwa moja nchini Uganda kabla ya kurudi nchini kwangu.” Alijibu Jabir akidanganya kwa kuwa hakupenda kuwa muwazi wa kila kitu. Cecy alichoka mwili na akili, akanyong’onyea na kujikuta akikaa kabisa kwenye kiti akiwa haelewi. Muda wa Jabir kukamilisha kupanga vitu vyake ulipokuwa umekamilika akatwaa taulo na kuingia maliwatoni. Hii ilikuwa ni nafasi ya Cecy iliyosalia hivyo hakuona kama inafaa kuweza kuchelewa naye akazama maliwatoni ambako walipoteza muda mwingi wakiwa pamoja. Saa kumi na nusu tayari Jabir au Alan kama mwalimu alivyomuita alikuwa tayari yuko ndani ya ndege kuelekea Afrika ya kusini kisha kuvadilisha ndege hadi jijini Nairobi; Kenya.
SAA 06:30 ASUBUHI. JABIR ANAJINYANYUA KUTOKEA KITANDANI AKIWA NDANI YA CHUMBA CHA HOTELI YA EKA; Eka Hotel. Muda huo aliufahamu mara baada ya kutazama saa iliyopo ukutani. Hakuwa na muda wa kulala tena alitakiwa kuwa kwa mtu aliyetakiwa kukutana naye kabla hata haijafika saa mbili za asubuhi kwa saa za Afrika ya mashariki. Alijionyoosha kwa kiasi kidogo kisha akaelekea bafuni ambako alijiosha mwili wake kwa haraka na kurejea tena chumbani. Hakuhitaji kitu chochote asubuhi hiyo zaidi ya kufika mahali ambapo alitakiwa awepo. Alitoka hadi nje ya Hoteli hiyo akazirusha hatua zake za haraka hadi alipovuka barabara ya upande mwingine ambapo alikuta kituo cha teksi. Akageuka kuitazama Hoteli hiyo ambayo alifika usiku sana wakati akiwa ndani ya muunganiko wa safari yake kutokea London; Uingereza kiaha Afrika ya kusini ambapo alibadilisha ndege na kusafiri kwa ndege ya shirika la ndege la Afrika ya kusini hadi nchini hapo. Ilikuwa ni Hoteli nzuri sana na mandhari yake ilimvutia sana na hakuweza kumlaumu dereva teksi ambaye alimfikisha hotelini hapo mara baada ya kutoka nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Ilikuwa ni Hoteli ya nyota nne yenye huduma zote za kimataifa ambayo ilikuwa iko mkabala na barabara ya Mombasa.
“Karibu kijana upate huduma…!” Mzee mmoja alimuwahi kwa kumkaribisha kwenye gari yake huku akiwa amemfungulia mlango wa mbele upande wa abiria hata hivyo Alan hakusumbuka sana na kuingia upande ule wa mbele hivyo akafungua upande wa nyuma wa gari ile baada ya kuyatathmini mazingira ya pale kuanzia madereva teksi wenyewe sambamba na gari zao kisha kuvutiwa na huyo mzee. Mzee huyo hakuwa na hiyana aliufunga mlango kisha akakimbilia upande wa dereva wa gari ile na kuingia akaliwasha. Kabla hata hajaliondoa gari maeneo hayo aligeuka nyuma kumtazama abiria wake kwa lengo la kumuuliza mahali aendapo.
“Nipeleke mtaa wa Accra.” Aliagiza Alan kabla hata mzee huyo hajauliza.
“Anhaa! Hakuna maneno…!” Akajibu na kuliondosha gari lake huku akitaja kiasi cha pesa kutokea hapo hadi mahali ambapo mteja wake angependa kupelekwa. Wakati gari ikiwa inakata mitaa hii na ile, kichwa cha kijana Alan kilirudi mbali sana kimawazo na kubwa alilokuwa akiliwaza ni jinsi alivyopewa maelekezo ya yeye kuweza kufika jijini Nairobi. Ilikuwa ni vigumu sana kujua kiundani kuhusiana na kazi hiyo aifanyayo. Alichoambiwa kupitia ule ujumbe mrefu wa maneno uliotumwa kwa barua pepe ni kwamba alitakiwa kufika kwenye ukumbi wa Serena Hotel ambapo alitakiwa afanye uchunguzi wa kina kujua jinsi ambavyo wajumbe walitekwa na namna walivyovamiwa. Nini maana ya hii yote…? Haikuwa rahisi hivyo akapanga akifika Nairobi awasiliane na mkuu wake wa kazi na ampe maelekezo ya kina yahusianayo na kazi hiyo. Alifika Nairobi usiku mkubwa sana hata hivyo hakutaka kulala hivyo mara baada ya kuingia chumbani kwake alifungua tarakilishi yake kwa ajili ya kutuma ujumbe kwa mwalimu. Alipofungua tu na kuingia upande wa barua pepe kitu cha kwanza alichokutana nacho ni ujumbe mrefu uliokithiri maelezo yaliyoshiba hadi namna ambavyo wajumbe hao walivyouawa. Alipomaliza kuusoma hakuwa na haja tena ya kuuliza swali alichokifanya ni kuifunga tarakilishi yake kisha akavaa mavazi yafaayo kumtoa nyakati hizo za usiku. Alipokwisha kumaliza kuvaa mavazi yake akasogea kwenye kioo na kujitazama. Alijiridhisha na muonekano ambao aliona, jeans ya rangi nyeusi na fulana ya rangi hiyo pia akiwa amevaa na kofia ya rangi hiyo pamoja na buti nyeusi, hakika alikuwa kwenye muonekano wa kikazi sawia kabisa. Muonekano huo ulimfanya atabasamu na kujiona kama yuko mafunzoni bado. Alifungua kioo kimoja cha dirisha akachungulia nje, giza lilikuwa limetanda sana kwa majira hayo ni taa za jiji pakee ndizo zilizokuwa zikilipendezesha jiji la Nairobi na kuliacha katika muonekano wa kuvutia. Alivaa glovu zake nyeusi kisha akafunga kifaa chake ambacho kilibeba kamba maalumu mahala salama na kuvuta kamba akapenya pale dirishani akiwa makini sana asionekane na ulinzi wa aina yoyote kwani Hoteli hiyo ilikuwa imepandwa kamera kila mahali pia kwa kipindi hicho cha kutokea chambulio baya la uvamizi jijini hapo kuliufanya usalama wa Hoteli nyingi kuwa mkubwa sana. Alan akajiachia akishuka kwenye maungio ya kioo na ukuta ili kuzuia waliopo ndani kuto kugundua chochote. Alishuka kama aliyekuwa akikimbia kwa kurudi nyuma hadi alipofika chini kabisa ya jengo lile ambako alifanya anavyojua kisha kujichanganya mitaani.
Baada ya muda mfupi alikuwa akiingia kwenye Hoteli ya Serena ambapo ndipo ulipo ukumbi uliotumika kufanyia mkutano huo muhimu. Hakupata shida sana kuweza kuingia ndani ya umbi huo kwa kuwa ramani nzima ya Hoteli ile alikuwa nayo hivyo alicho kifanya ni kuhakikisha haonwi na ulinzi uliopo kwenye Hoteli hiyo hadi alipolipata dirisha la kioo ambalo alifanikiwa kufyatua loki na kulifungua kisha akajipenyeza kwa upande wa ndani akiwa makini zaidi. Kwa kuwa umbi huo haukuwa juu sana hivyo Alan alitumia ngazi kuweza kupanda huku akihakikisha hatua zake hazifanyi kelele kwenye sakafu ya hoteli hiyo. Sasa alikuwa akitazamana na mlango wa ukumbi huo ambao ulifungwa kwa kufuli kubwa huku kukiwa kumefungwa tepe maalumu nyekundu ambazo zilikuwepo mahususi kwa lengo la kuonesha alama kuwa ukumbi huo ulikuwa kwenye uangalizi bado. Alitazama kila mahali ikiwemo kuangalia kamera za ulinzi kama zipo, alipojiridhisha na usalama uliopo, akachomoa funguo zake malaya akapachika moja baada ya nyingine hadi kufuli lile lilipotii amri. Taratibu akaufungua ule mlango na kuurudisha nyuma yake mara baada ya kuingia ndani ya ule ukumbi. Kulikuwa kimya sana huku giza likihanikiza mule ndani. Macho yake ya kijasusi yakafanikiwa kutalii kwa kasi ya ajabu hivyo muda mfupi akawa amegundua namna ukumbi ule ulivyo. Utulivu ule ukamvutia kiasi cha kuamini hakuna jambo lolote lenye kuleta mashaka. Akapiga hatua zake hadi dirishani kisha akavuta pazia taratibu hadi alipopata upenyo wa kuchungulia nje. Nje kulikuwa kumepooza sana hakukuwa hata na sauti ya muziki iliyokuwa ikisikika kwa mbali kama miji mingine ilivyo. Akalirudisha lile pazia mara baada ya macho yake kufanya uchunguzi kwenye majengo ya jirani na kuona utulivu ukiwa mkubwa. Alisogea hadi swichi kubwa ya sistimu ya umeme ilipo, akataka kuwasha taa ili kuweza kuutazama vizuri ukumbi ule hata hivyo alipingana na wazo hilo kwani hakuwa akijua kama mtu anayefuatilia jambo lile ni yeye tu au kuna wengine nyuma yake. Alichokifanya Alan ji kutoa kurunzi yake ya kijasusi yenye mwanga mwembamba na kuutazama ule ukumbi kwa mara nyingine na kwa utaratibu mkubwa sana huku kurunzi ile ikiwa kama msaada mkubwa kwake. Alan au Jabir alitazama saa yake ya mkononi ambayo ilimtanabaishia kuwa ilikuwa imetimia tayari saa tisa usiku. Akajipa dakika sita tu za kuwa pale. Aliyazunguusha macho yake kwa udadisi mpana akaona jinsi maganda ya risasi yalivyosheheni kama kwamba vita kali ya kutupiana risasi ilikuwa ikiendelea humo ndani. Alitembea taratibu akipita hapa na pale huku kichwa chake kikijenga jazanda ambalo aliamua kuliundia kichwani mwake kwa namna alivyofanikiwa kuona. Ukumbi ulikuwa mkubwa ambao ulisheheni viti vingi ambavyo vilipangiliwa kwa weledi wa hali ya juu hata hivyo alikuwa akivitazama viti vitatu tu na meza kuu. Alisogea hadi ilipo meza kuu kisha akavitazama viti vitatu vilivyopo nyuma ya meza hiyo, alijenga picha kuhusiana na wajumbe walivyokuwa wamekutana hapo kwa lengo la kuzungumzia kile hasa kilichokuwa kimewakutanisha hapo. Akakitazama kiti cha meza kuu ambacho hakuishia kukitazama tu bali alikaa kabisa na kutazama mbele. Picha ya wavamizi ikajengeka upya kichwani mwake, aliwatazama katika kichwa chake namna walivyokuwa wanaingia kisha akawaona wajumbe wawili miongoni mwa maafisa wale wa jeshi walivyonyanyuka ghafula na kukamata silaha zao mikononi huku huyu wa meza kuu na mwezake mmoja wakihamanika kwa shambulio hili la ghafula. Risasi nyingi zikamwagwa huku tayari kukiwa kumeshamwagwa moshi mwembamba wenye sumu. Kuhamanika kwa hawa wawili kukapelekea wavute moshi mwingi ndani na hawa wengine wakijikuta wakichapwa risasi.
Kila mwili mmoja ulikutwa na matundu mawili ya risasi na yote yalikuwa sehemu zilizo sawa. Hapa akasitisha ule mkanda wa mawazo Alan kisha akatazama kila mahali katika namna ya kujiwekea usalama.
Muuaji alikuwa mmoja…? Aliwaza Alan. Kuhusiana na muuaji kuwa mmoja sawa linaweza kuwa, swali likabaki kuwa hili, iweje muuaji huyo awe na kasi kubwa tena ya kuweza kuwakabili hawa watu ambao hawakuwa wadogo kwenye medani zote; wanajeshi mahiri na aminiwa. Inawezekana muuaji akawa mmoja katika kundi la hawa washambuliaji. Hili angalau likampa imani hata hivyo akakubaliana na uwezo wa muuaji ambaye alitumika kuwaangamiza wajumbe wale wawili, alikuwa na shabaha tena si shabaha tu bali shabaha kali mno. Risasi moja ya paji la uso kisha risasi nyingine shingoni kwenye miili yote ambayo alikuwa na imani kuwa ilianguka pamoja chini. Baada ya kujiuliza hivi na kujihakikishi majibu akahamia kwenye alama tatu za kucha tatu za mnyama jamii ya paka. Hapa ndipo palipokuwa na kimbembe kingine. Kipi kilitangulia kabla, risasi au kucha za mnyama jamii ya paka…? Lilikuwa swali lililohitaji utulivu kidogo. Na hiki ndicho alichoitiwa kuja kukifanyia uchunguzi na si kitu kingine. Mwalimu alikuwa akiuamini uwezo wa kijana huyu hivyo hakuwa na shaka kabisa kwenye hilo. Hakutaka kuzifuatilia kamera za jengo hilo kwa kwenda kwenye mamlaka maalumu ya ulinzi ili kujua kama shambulio lile halikuonwa kwenye kamera za ulinzi na badala yake alitaka kuifanya kazi yake kwa siri sana tena bila kelele kama hatua za kinyonga.
Alan aliurudisha mkanda wa mawazo nyuma, mkanda alioutengeneza kichwani mwake. Akarudisha matukio nyuma hatua kwa hatua na kwa haraka kubwa, hakuona kwenye urudishaji huo bali aliona kitu alipotengeneza tena jazanda jipya kichwani mwake. Ni mtu aliye katika kasi kubwa ambaye eidha alirusha silaha hiyo yenye sumu kali ama alimuwahi au kuwawahi wale wajumbe mara baada ya kuwaadhibu kwa risasi mapema kabla miili hiyo haijapoa na kuzibandika alama hizo kama nembo maalumu ili uwe ni utambulishi wake.
KAZI KAZINI.
Alan aliurudisha mkanda wa mawazo nyuma, mkanda alioutengeneza kichwani mwake. Akarudisha matukio nyuma hatua kwa hatua na kwa haraka kubwa, hakuona kwenye urudishaji huo bali aliona kitu alipotengeneza tena jazanda jipya kichwani mwake. Ni mtu aliye katika kasi kubwa ambaye eidha alirusha silaha hiyo yenye sumu kali ama alimuwahi au kuwawahi wale wajumbe mara baada ya kuwaadhibu kwa risasi mapema kabla miili hiyo haijapoa na kuzibandika alama hizo kama nembo maalumu ili uwe ni utambulishi wake.
SONGA NAYO…..
Alikuwa na maana maalumu muuaji au hii ndiyo alama ya muuaji. Kama ilikuwa ni alama tu je, vipi miili ikutwe na sumu na ionekane kuwa huwenda sumu hiyo ndiyo iliyosababisha vifo vya wajumbe hao…? Alizidi kuwaza Alan.
Waliingia wauaji wa aina mbili huku wengine wakiwa ni geresha lakini wawili hawa kila mmoja akipewa jukumu lake. Mmoja akiwa na kazi ya kuuwa kwa risasi hata hivyo mmoja akiwa na kazi ya kuuwa kwa sumu kali. Huyu wa kuuwa kwa sumu kali aliwahiwa na huyu wa risasi ambaye alikuwa na shabaha kali kupitiliza hata hivyo ili kuachaa ujumbe kuwa iliyotenda haya haikuwa mikono salama akaamua kupita kwa kasi kubwa kablda miili ya marehemu haijapoa. Kwanini…?
Akitaka alama ya sumu isambae mwilini kwa haraka wakati damu ikiwa ya moto ili kuwachanganya wahusika kama wakiamua kufanya uchunguzi wa miili hiyo.
Hatari kubwa.
“Mikono ya jasusi…hii ni mikono ya jasusi…!” Alan alijisemea kwa sauti ya chini mara baada ya kujipa uhakika dhidi ya kile alichochunguza kwa makini na udadisi mkali. Muda alioutumia kufanya uchunguzi wake haukuzidi dakika kumi na tano kwani hali ya eneo hilo kwa namna alivyoliona ilimtanabaishia dhahiri kuwa wauaji hawakuwa daraja dogo kwani hakukuwa na vurugu nyingine zaidi ya maganda mengi ya risasi. Aliondoka kwa utaratibu ule ule aliojia na kupotelea gizani.
Haya yote Alan alikuwa akiyawaza akiwa kwenye teksi akipitishwa mitaa hii na ile hakika alikuwa na kazi kubwa sana ambayo hakupaswa kuichukulia kimzahamzaha. Kichwani mwake alikuwa na maswali mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine yangemkamilishia kile ambacho alikuwa akienda kukichunguza kama mwalimu alivyomtaka afanye. Gari ilizidi kuchanja mbuga na yeye mara kwa mara hakuacha kutazama nyuma kupitia kioo cha nyuma ili kuweza kujua kama kuna gari ambayo ilikuwa ikiwafuata na haikuwa na lengo zuri kwake. Waliweza kupita mitaa mingi huku akilitazama jiji la Nairobi na kuona jinsi lilivyokuwa likivutia. Walikuwa kwenye barabara ya mtaa wa Luanda, kasi ya gari haikuwa kubwa sana wala ndogo sana hivyo kwa mwendo mfupi wakaupita mtaa wa Mombasa kisha mtaa wa Nairobi, bado Alan hakuisha kutazama nje huku taswira mbalimbali zikiendelea kujiunda kichwani mwake.
“Hapa panavutia sana rafiki, mandhari yake ni ya kipekee mno na ni pachangamfu mno.” Alianzisha maongezi Alan akijaribu kuyafukuza mawazo yaliyokuwa yamemzonga kichwani mwake.
“Hiyo ni Zarare Restaraunt upande huo wa kushoto, ni mahali safi sana bosi.” Alichangia dereva teksi huku akijaribu kupitisha kitambaa kwenye kioo chake cha mbele ili kuweza kuondoa ukungu uliosababishwa na maji wakati akiwa analifuta gari lake katika namna ya kulifanyia usafi wa hapa na pale. Kimya kilikuwa kimekwisha kuanza kuchukua mamlaka hata hivyo hayakuwa ya muda mrefu kwani yule mzee dereva teksi akaufukuza.
“Ni mwenyeji wa jiji hili kijana…?”
“Naam, nimekuwa nikifika Nairobi mara kwa mara na mara nyingi huwa nafika hapa kwa shughuli zangu za kibiashara…!”
“Ndiyo, ndiyo…!” Alijibu mzee huyo huku akipunguza mwendo wa gari yake huku akiwasha taa za upande wa kulia kuashiria kuwa alitaka kuingia upande huo.
“Ni mtanzania?” Akauliza dereva teksi, Alan akatulia kidogo kabla ya kujibu alikuwa akitazama nje akianza kuhesabu nyumba za mtaa huo maana tayari walikuwa ndani ya barabara ya mtaa wa Accra.
“Ndiyo, ni mtanzania…!”
“Nilivyokuona tu nilijua kuwa wewe ni mtanzania kwa namna ulivyo maana watanzania hujulikana hata sura zao.” Aliongea yule mzee na kupelekea Alan kucheka kidogo kabla ya kumuuliza.
“Unawezaje kumtambua mtanzania kwa kumuangalia usoni mzee…?”
“Upole na ucheshi wao hujichora sana nyusoni mwao.”
“Haya bwana wacha niwe mpole ila mzee wangu unaongea kiswahili safi na tulivu bilashaka uliishi Tanzania kwa muda mrefu?”
“Aaam! Ni kweli nazungumza kiswahili kisicho na shaka kwa kuwa niliishi Mombasa kwa muda mrefu mno takribani miaka ishirini na tano, nimekuwa na watu wa kule kwa muda wote huo hivyo ni mswahili safi kabisa na…!”
“Subiri kidogo mzee, egesha gari hapo pembeni kwenye huo mti!” Aliagiza Alan akiikata kauli ya mzee yule mara baada ya kuona alama aitakayo. Ilikuwa ni nyumba namba 64. Gari ikaegeshwa mahali hapo kisha yule mzee akageuka nyuma kumtazama abiria wake, akapewa kiasi cha pesa alichokihitaji kisha Alan akaufungua mlango hata hivyo hakutoka.
“Unaweza kunifaa sana kwa safari zangu zote za hapa Nairobi hivyo si vibaya kama nitakufahamu?” Akauliza.
“Ni vema, jina langu ni Gabriel pia naweza kukupa mawasiliano yangu ili iwe ni nafuu zaidi kunipata hasa utakaponihitaji.” Akasema yule mzee kisha akataja namba za simu ambazo Alan alionesha kama alikuwa akizinakili kwenye simu yake lakini haikuwa hivyo alipenda tu kulifahamu jina la mzee yule mkarimu. Alishuka kutoka garini na kuutazama vizuri mtaa huo huku akizirusha hatua zake za haraka akivuka barabara kuelekea upande wa pili. Nyumba namba 66 ndiyo ilikuwa hitaji lake kubwa ambalo hasa aliamini anaweza pata kitu cha umuhimu sana akikutana na mwenyeji wa nyumba hiyo. Aliyatazama mazingira ya mtaa huo yalivyosongamana kwa nyumba nyingi zilizo katika mpangilio wa kawaida, sasa alikuwa kwenye nyumba namba 65 mbele yake aliiona nyumba aliyokuwa akiihitaji ikiwa imezunguushiwa uzio mkubwa wenye lango kubwa jeusi. Alizirusha hatua zake huku akigeuka nyuma kwa tahadhari akitazama kama yupo mwenye kumfuatilia. Bado kulikuwa shwari tena kusikotia shaka, akalifikia lango kubwa la uzio wa jengo hilo kubwa namba 66 akajipa utulivu kisha akabisha hodi kwa kubonyeza kitufe cha kengele mara moja kisha akatulia tena kusikilizia. Punde akasikia mchakacho wa hatua za taratibu kwa ndani zikiwa zinasogea mahali lilipo lango hilo. Mlango mdogo ukafunguliwa taratibu kisha sura ya mwanamke ikachungulia. Alikuwa ni mwanamke mweusi aliye katika urembo wa sura.
“Nani mwenzangu nikusaudie nini tafadhali?” Alizungumza yule mwanamke kwa sauti tulivu isiyo na tashwishi yoyote pia muulizaji akiwa mtulivu. Alan alitabasamu kidogo kisha akajibu.
“Naitwa Alan ni mgeni wako na niko hapa kwa ajili yako hivyo usitie shaka.” Jibu hilo likamfanya huyo mwanamke kutulia kidogo kisha akamkaribisha hadi ndani akarudisha ule mlango na kuufunga kabisa. Alimtazama mgeni wake kwa utulivu uliojenga mashaka kiasi kisha akamkaribisha ndani zaidi akitangulia mbele. Alan akawa tayari na ufahamu kuwa aliyeko mbele yake ni mtu husika. Alikuwa mrefu mweusi mwenye umbo zuri la kile, alivaa pensi fupi ngumu ya kijeshi huku juu akiwa amevaa fulana nyepesi nyeupe ambayo uliudhihirisha mzigo wa matiti makubwa uliostiriwa na sidiria nzito, hatua zake zilimpa shida Alan nyuma maana mzigo wa makalio ulikuwa ukitikisika kwa utaratibu maalumu hakika alikuwa ni mwanamke hasa aliyeuficha urembo wake ndani ya uanajeshi imara. Hawakufika ndani walisimama kwenye bustani ya nyasi fupi na maua kisha akamgeukia Alan na kumtazama.
“Niko na komandoo Rhoda…?” Akauliza Alan kupitia ujumbe ambao alipewa na mwalimu Dao huku macho yake yakiwa juu ya sura ya mwanamke huyo ambaye alikubali kuhusiana na alichoulizwa. Walivisogelea viti na kuketi.
“Kwanini uko hapa na umepajuaje hapa na uko hapa kwa minajili ipi?”
“Ni mtanzania, niko hapa kwa kazi maalumu ambayo ilikuwa ni lazima nikutane na wewe.” Alijibu Alan akiwa anakaa kwenye kiti ambacho kilikuwa usawa wake. Hakuona sababu ya kudanganya kwa kuwa alitakiwa awe muwazi kwa mtu huyo.
“Wewe ni mpelelezi?” Akauliza Rhoda.
“Hujakosea na niko hapa ili kujua mengi kutokea kwako.”
“Alan…hili jina sijawahi kulisikia na sidhani kama lipo kwenye orodha ya wapelelezi mahiri kutokea Tanzania wewe…?”
“Ni lazima usinifahamu kwa kuwa mimi ni mtoto wa tatu kati ya watoto wane wa baba mmoja na mchanga bado hivyo uko sahihi..mwalimu amenitaka nifike hapa kwako.” Akaeleza kwa kutoa majibu sahihi. Rhoda akanyanyuka na kuelekea ndani akimtaka mgeni wake amsubiri hakuchukua muda mrefu akawa amerejea na chupa kubwa ya mvinyo sanjari na bilauri mbili akazimiminia kinywaji mara baada ya kuketi na kumkabidhi moja Alan huku nyingine ikiwa mikononi mwake wakagonga bilauri zile na kunywa pamoja.
“Nini unataka kujua toka kwangu maana sikutaraji kupokea ugeni wa namna hii japo nilipata taarifa za ugeni kwa barua pepe kutokea kwa mtu uliyemtaja punde. Namfahamu kwa kuwa ni miongoni mwa maafisa wakuu kabisa wa jeshi nchini Tanzania na alifika jana wakati wa mazishi ya meja Merceline Ong’ong’o ambaye alifariki akiwa katika misheni ya ukombozi ya kwenda kuwaokoa wajumbe waliotekwa mkutanoni.”
“Ulimfahamu vipi?”
“Kabla ya mazishi nilifahamishwa na wakuu wangu hata baada ya mazishi nilipata wasaa wa kuongea nae mawili matatu na akaniambia mengi sana moja ya mengi hayo yalihusiana na misheni ile.
Namfahamu kwa kuwa ni miongoni mwa maafisa wakuu kabisa wa jeshi nchini Tanzania na alifika jana wakati wa mazishi ya meja Merceline Ong’ong’o ambaye alifariki akiwa katika misheni ya ukombozi ya kwenda kuwaokoa wajumbe waliotekwa mkutanoni.”
“Ulimfahamu vipi?”
“Kabla ya mazishi nilifahamishwa na wakuu wangu hata baada ya mazishi nilipata wasaa wa kuongea nae mawili matatu na akaniambia mengi sana moja ya mengi hayo yalihusiana na misheni ile.
SONGA NAYO….
Mwisho wa maongezi yale akiniambia kuwa ipo namna ya kufanya uchunguzi mkubwa ili kuweza kujua dhamira hasa ya kikundi kile ni nini mara baada ya kuwateka watu wetu akaniomba kuwa karibu na jambo hilo muda wowote ili kurahisisha kazi hivyo hata nilipopokea barua ile sikuwa na wasiwasi kwani nilijua ni wajibu wangu kama mwanajeshi hasa katika kipindi cha kuleta amani kwenye taifa langu.” Alijibu Rhoda kisha akapiga funda jingine na kupandisha miguu yake katika mtindo wa nne. Mapaja yake makubwa ambayo hayakufanikiwa kufunikwa vizuri na ile pensi yakajitokeza waziwazi na kumfanya Alan kumeza mate ya uchu wa tamaa. Akilini mwake alikuwa ameshajua sababu ya mwalimu Dao kufika mazishini na kumhadaa huyu mrembo kuwa alikuwa ni afisa wa jeshi na si mwana usalama hatari kwenye kitengo cha kijasusi nchini Tanzania. Alitaka iwe rahisi yeye kufika hapo na kupata mengi kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa mwanajeshi huyo. Kimya kifupi cha kutazamana kikapita huku Rhoda akimtazama kijana huyo vizuri na kwa namna ya pekee kabisa.
“Nataka kujua kama kuna chochote uliweza kukigundua wakati ulipokuwa katika misheni ile ukiwa kama mwanajeshi wa daraja la juu katika misheni za kivita?” Aliuliza Alan kisha akaweka utulivu tena. Rhoda alifikiri kwa muda kisha akaanza kwa kusema;
“Kwa kweli kabisa tukitoa vita kali baina yetu na kikundi kile cha kigaidi, ndani yake kuna mambo makubwa ambayo yanashangaza sana huwenda kuna mambo makubwa yanafanyika kwa usiri mkubwa sana na mambo hayo waratibu wake ni watu hatari mno. Sidhanii kama vita hizi zinamuishilizio mzuri au niseme sidhanii kama ugaidi huu unaondelea katika nchi za kiafrika kuna wakati unaweza kukoma…!”
“Kwanini unahisi hivyo?” Akauliza kwa kumkata kauli.
“Jeshi la serikali ya kisomali linamatatizo makubwa sana Alan na matatizo hayo yanalitafuna jeshi lile kwa kasi kubwa kiasi kwamba itahitajika nguvu kubwa na nguvu hii isimamiwe pia na miujiza ya Mungu, jeshi lile limejaa wasaliti wengi sana ambao wanaonekana kwa asilimia kubwa kukiunga mkono kikosi cha wanamgambo wa Al shabab. Tumekutana na baadhi ya wasaliti hao na baadhi yao tumefanikiwa kuwahoji baada ya kuwadhibiti vikali vilevile kupambana nao. Kama unavyojua maafisa wakuu wa jeshi wanazo siri nyingi na siri hizi zinakwenda kuingia mikononi mwa wahalifu wa kivita hebu niambie ni lini vita ya kupambana na ugaidi duniani itakwenda kumalizika. Nchi nyingi zenye chembe chafu za ugaidi zimekuwa zikihangaika kuukomesha ugaidi hata hivyo wamekuwa wakipigwa na kupigana na vikosi hivyo vya kuiuhalifu na bado mambo kwao ni magumu na yenye kukatisha tamaa. Bado mambo ni magumu sana. Lakini mbali na hilo ambalo tumeligundua, lipo jingine hili ni hatari zaidi kama hatari yake si ya sasa huwenda ikawa ya siku za mbeleni na zinayahusu mataifa yetu haya mawili.”
“Hilo ndilo hasa nililokuwa nikilihitaji zaidi Rhoda kwani kama ujuavyoa kuwa kwa sasa tuko kwenye sintofahamu kubwa kwani kitendo cha kutekwa wajumbe wetu ambao walikuwa kwenye mkutano muhimu tena mkutano wa mwisho wa kufikia maazimio, hili ni jambo la hatari sana na linalohitaji uangalifu mkubwa wenye uchunguzi wa mapema ili maandalizi ya udhibiti wa hili yawe ya mapema.” Akasema Alan.
“Kuna siri zimechotwa kutoka kwa wakubwa wetu Alan maana sina shaka walihojiwa vikali sana na waliotumika kuwahoji hawakuwa daraja dogo, wajumbe wetu walihojiwa na watu wenye weledi wa kazi hizo na huwenda wakawa ni majasusi. Nini kipo hapa kama ilitumika nguvu kubwa kabisa kuweza kuchota siri kutoka kwa wajumbe wale ambao wako na vyeo vikubwa jeshini. Mimi naona hiki kitendo cha wajumbe wetu wale kutekwa tena wakiwa na nyaraka muhimu zilizobeba siri nzito za kiutendaji ni kama samaki kukifuata chambo nchi kavu pembeni ya mvuvi.”
“Kwanini unayo imani kuwa waliohusika na uhojiji wa maswali ni watu wa namna hiyo?”
“Si kama nahisi, lipo hakikisho la hivyo, kupitia mahojiano na mateka mmoja ambaye tulimdhibiti vilivyo ndicho kimepelekea niwe na imani hiyo kuwa waliohusika ni watu hatari. Yule bwana alisema kuwa viongozi wao wana watu wachache tu ambao wapo kwa ajili ya kufanya mahojiano na watu wetu tena ni makini na hatari pia alisema kwa hatua ambayo watu wetu wamefikia ni mbaya kupitiliza. Hili mimi na kamanda Hamidu Jumbe tulilithibitisha baada ya kufika mahali ambapo wajumbe wetu wamehifadhiwa. Ni muda mfupi sana kabla hata mlipuko ule hatari haujatokea. Wajumbe wale waliteswa vibaya mno kiasi kwamba huwezi kuwatazama mara mbili, waliumizwa mno, macho yao yalijeruhiwa, waling’olewa meno, baadhi ya mishipa ya damu ilikatwa na kupigwa vibaya sana. Yalikuwa ni mateso ambayo hudhanii kama ni binadamu ndiye mwenye kuweza kufanya jambo kama lile.”
“Mliwakuta wakiwa hai?”
“Hapana, tuliwakuta wakiwa wafu tayari na ni kama walitaka kupoteza ushahidi kabisa wa eneo lile kuanzia walinzi waliokuwepo hadi yeyote atakayefika pale…!”
“Kivipi…?” Alizidi kuhoji Alan. Rhoda akavuta pumzi na kumeza tena funda jingine la kinywaji na kuendelea kujibu.
“…tulifanikiwa kuona bomu kubwa la masaa ambalo lilikuwa limetegwa ubavuni mwa mwili wa mjumbe mmoja, tukahamanika kwa kuwa ulibakia muda mchache sana na baada ya pale ikawa tafarani nzito…!”
“Poleni sana aisee! Yaliyomikuta yalikuwa ni masaibu mazito.” Aliongea Alan kisha wakakipisha kimya kingine kifupi wakapata wasaa wa kunywa kile kinywaji wakiwa wanayashangaa mandhari ya eneo lile huku mara chache Alan akiwa anamtupia macho ya wizi mwana dada yule aliyejaaliwa umbo na rangi ya ki-Afrika.
“Hakuna kitu kingine ambacho mmeweza kugundua?” Akauvunja ukimya Alan mara baada ya kuhisi ukimya ule ungeweza kuzalisha jambo lisilo rasmi maana nafsi ya mwanaume rijali kwa viumbe hao huwa haihimili vishindo.
“Baada ya hapo?” Akauliza Rhoda.
“Hata kama si baada ya hapo?” Kimya kifupi cha jozi ya sekunde kikapita Rhoda akitafakari kisha akajibu.
“Kipo na huu unaweza kuwa na mantiki kwenu ninyi wapelelezi. Huu unaweza kuwa ni ushahidi na ushahidi huu siwezi kukupa mimi kwasababu sinao, atakupa kamanda Hamidu Jumbe kwa kuwa alifanikiwa kubakia na picha zake. Rudi Tanzania ukishafika huna budi kwenda Bagamoyo ukakutane na huyo mwanaume wa shoka…!”
“Mwanaume wa shoka?” Akauliza Alan huku akiliruhusu tabasamu la kimbea litawale usoni pake.
“Ndiyo, kamanda Jumbe ni komandoo hasa ni mbishi na ngangari kwelikweli hasa akiwa kwenye misheni ya kivita, hakika ni faraja yangu kukutana na mtu wa aina yake.” Alijibu Rhoda huku naye akitabasamu.
“Ukiwa na maana gani hasa?”
“Acha mambo yako bwana Alan unaonekana mchokozi sana wewe. Nimejifunza vitu vingi sana nikiwa karibu ya jumbe hakika sita kaa niisahau ile operesheni. Muone vile alivyo, ulikuwa umeshaweka maana nyingine mwanaume, hatari sana wewe…!” Akaongezea utani wakacheka na kutaniana haya na yale.
“Uko mwenyewe ndani ya mjengo huu?” Akatupia swali la mtego Alan.
“Yaa, niko mwenyewe ni mara chache sana nakuwa pamoja na mume wangu…!”
“Kumbe umeolewa?”
“Ulidhani kwa kuwa ni mwanajeshi mahiri siwezi kuolewa?”
“Hapana, hiyo haikuwa dhania yangu. Nilitaka kushangaa kama ungeniambia kuwa uko tu mwenyewe na huna mtu kabisa.”
“Kwanini?”
“Uzuri wako ni uga wa sumaku Rhoda unavuta kila chenye kuvutika, umbo lako ni keki ya harusi bibie hakuna asiyependa kuionja, sura yako ni mvuto wa pekee sana kiasi kwamba inahitajika ujasiri wa kuweza kukukabiri na kukueleza ukweli wa moyo hata kama umepata majeraha na michubuko ya hatari mliyokutana nayo hata hivyo bado uko bomba. Hakika Mungu amefanya upendeleo mkubwa sana kwenye uumbaji wako.” Zilikuwa ni sifa zilizomuacha Rhoda katika mshangao mkubwa sana akabaki akimtazama kwa makini huku macho yake yakiwa yamemlegea. Alishindwa amjibu nini akabakia kutazama chini tu huku tabasamu mwanana likizidi kuupamba urembo wa sura yake.
“Mumeo ni mtu wa namna gani mwenye kuweza kuwa mvumilivu kiasi cha kukuacha mwenyewe kwa siku nyingi?” Akatupia swali Alan mara baada ya kumuona Rhoda akiwa kimya.
“Mume wangu ni mwanajeshi kama nilivyo mimi, yeye ni rubani…anarusha ndege za kijeshi na mara nyingi huwa safarini akiwa sambamba na maafisa wakuu wa kijeshi, ni rubani makini sana…!” Alijibu Rhoda kisha akatulia na ukimya mfupi ukapita. Walisimama baada ya kuwa hakukuwa na maongezi mengine wakazitupa hatua zao kutoka hapo na kulizunguka lile eneo huku wakiongea hili na lile.
“Nadhani huu utakuwa ni wasaa wangu wa kukuaga na kuondoka maana muda nilionao ni mdogo sana na bado niko na shughuli nyingi za kufanya, asante sana kwa kunipa muda wako bibie.” Alizungumza Alan huku akiwa anampa mkono mwanadada huyo. Alistaajabu sana Alan kuona mwanajeshi mkakamavu akiwa na mikono laini kiasi kile. Alitabasamu na kumfanya Rhoda kutasamu pia.
“Nadhani tunaweza kuonana tena siku za usoni. Karibu sana nyumbani?”
“Nashukuru sana kwa kunikaribisha natumai nitafika nchini Tanzania panapo majaaliwa.”
HAYA SASA SAFARI IMEUMA.
“Nadhani huu utakuwa ni wasaa wangu wa kukuaga na kuondoka maana muda nilionao ni mdogo sana na bado niko na shughuli nyingi za kufanya, asante sana kwa kunipa muda wako bibie.” Alizungumza Alan huku akiwa anampa mkono mwanadada huyo. Alistaajabu sana Alan kuona mwanajeshi mkakamavu akiwa na mikono laini kiasi kile. Alitabasamu na kumfanya Rhoda kutasamu pia.
“Nadhani tunaweza kuonana tena siku za usoni. Karibu sana nyumbani?”
“Nashukuru sana kwa kunikaribisha natumai nitafika nchini Tanzania panapo majaaliwa.”
SONGA NAYO…..
Alijibu Rhoda kisha akabaki kumtazama kijana huyo namna anavyozitupa hatua zake kutoka nje ya lango lake.
Ile ilikuwa ni hatua kubwa sana kwa Alan, mazungumzo aliyotoka kuyafanya na komandoo Rhoda yaliweza kumfunulia mengi yenye maana kubwa juu ya kile alichotakiwa kukichunguza. Bado alitaka kujua kulikuwa na ushahidi gani ambao alitakiwa kuupata kwa komandoo Hamidu Jumbe, kila alipojaribu kuushurutisha ubongo wake ujaribu kumfunulia japo kidogo kwa kuunganisha matukio ya kimoja baada ya kingine, ubongo huo uligoma katakata kuweza kumfumbulia japo chochote. Muda ulikuwa unaruhusu sana kuweza kujiandaa na kuondoka hapo jijini hivyo moja kwa moja alielekea hotelini kwake na kuchukua kila kilicho chake na kuelekea uwanja wa ndege kuona kama angeweza kupata ndege ya muda huo. Saa kumi juu ya alama tayari Alan alikuwa ndani ya uwanja wa ndege wa mwalimu J. K. Nyerere. Alikuwa akitembea akitokea ndani ya uwanja huo huku akiangaza macho yake, aliona namna jiji lilivyo kwa hali yake ya hewa na kadhalika akajua hakika yuko Tanzania; Dar es salaam. Alielekea hadi mahali ambapo kuna kituo cha teksi akapokewa na kijana mmoja mchangamfu ambaye alimfungulia mlango naye akajiingiza ndani yake. Dereva yule aliufunga mlango vizuri kisha akajiweka nyuma ya usukani kisha kabla ya kuliondoa gari lake akamgeukia mteja wake.
“Tunaelekea wapi bosi?” Akauliza huku akiweka tabasamu la kibiashara usoni mwake.
“Bagamoyo tafadhali.” Akajibu Alan kisha akaitoa simu yake na kutafuta jina la mtu amtakaye. Dereva alitaja kiasi cha pesa cha kumfikisha mteja wake huko na walipoafikiana alitekenya gari na safari ikaanza. Hakufikiria ukubwa wa kiwango cha pesa alichotajiwa, alicho jali na kukifikiria kwa wakati huo ni namna ya kumpata komandoo Hamidu Jumbe. Alitaka awe na majibu ya uchunguzi wote ili aweze kuonana na mkuu wake wa kazi, alishafanya mawasiliano na mkuu wake ili kujua ratiba nzima ya kikazi ya mwanajeshi huyo ambaye alichaguliwa kuingia kwenye operesheni ile ya ukombozi. Hapo alikuwa na majibu yote kuwa mwanajeshi huyo kwa majira hayo yuko nyumbani kwake akiwa kwenye kipindi cha mapumziko mafupi. Maelekezo aliyopewa yalijitosheleza sana hivyo alikuwa na hakika na mahali aendako kwa asilimia kubwa. Safari haikuwa ndefu ya kuchosha na alikuwa akijiburudisha na simu yake kucheza wimbo huu na ule au kuchati na watu fulani muhimu aliopenda kuchati nao alimradi kuweza kufika safari yake. Pamoja na yote aliyokuwa akiyafanya katu hakupoteza umakini wake wa kuangalia kupitia kioo cha mbele cha ubavuni mwa dereva kuona kama kuna gari yoyote ambayo ilikuwa ikiwasindikiza kutokea uwanja wa ndege, kulikuwa shwari na gari zote zilizokuwa zikionekana zilikuwa na shughuli zao. Alifika mahali husika. Akalipa kiasi cha pesa kisha akazitupa hatua zake taratibu akikakatiza mitaa ile na hii. Alan alifika kwenye nyumba moja ya kisasa akaisogelea hadi alipowakaribia watoto wawili ambao walikuwa wakicheza mpira wa makaratasi. Akawasabahi nao watoto wakatoa heshima kwake.
“Baba yenu nimemkuta?” Aliuliza Alan akijipa imani kuwa wale walikuwa ni watoto wa mwenye nyumba ile ambaye kwa maelezo aliyonayo ni kwamba hapo ndipo yalipokuwa nakazi ya mwanajeshi makini.
“Kwani amerudi…?”
“Ndiyo, si ameingia sasa hivi kutoka kuangalia mpira…!”
“Mimi sijamuona kama amerudi bwana kama wewe umemuona haya…!” Yalikuwa ni mabishano ya kawaida ya watoto hao ambayo yalizaliwa na swali la Alan. Hata hivyo hawakumjibu Alan kama ambavyo aliuliza waliendelea kupigiana mpira kama vile tayari walishajibu walichoulizwa, hizi ndizo tabia za watoto wengi wadogo.
“Kwa hiyo yupo eenh…?” Alan ilimbidi kuuliza tena ili kupata mrejesho.
“Omary anasema amemuona akirudi mimi sijui kama yupo…?” Mmoja ambaye alionekana kuwa ni mdogo zaidi ya yule mwengine alijibu.
“Amerudi hukoo…si nimemuona amerudi…!” Ilikuwa ni namna ya kujibizana tena na si kujibiwa yeye. Alan akatabasamu kisha akawaacha watoto wale waendelee na shughuli yao ya kucheza mpira akazirusha hatua zake na kuukabiri mlango wa jengo hilo ambalo bado lilikuwa kwenye ujenzi wa umaliziaji wa uzio wake. Alibisha hodi kwa mara ya kwanza akasubiri kisha akarejea tena baada ya muda mfupi kupita na kupewa mrejesho wa ukaribisho. Mlango ulifunguliwa na mwanamama mwenye mwili mkubwa kiasi aliyevaa gauni refu lenye kuburutika chini huku akijipamba kwa kiremba safi kabisa.
“Karibu ndani mgeni?” Alikaribisha zaidi yule mama ambaye kwa tathmini ya harakaharaka Alan aliafiki kuwa yule alikuwa ndiye mke wa Hamidu Jumbe.
Asante sana…asante sana.” Alijibu Alan huku akiwa anapiga hatua kuingia ndani. Aliitazama nyumba hiyo kwa ndani kwa namna ya kuipeleleza, haikuwa na samani nyingi sana kama ambavyo nyumba nyingi zilivyo, kulikuwa na meza kubwa ya msitatili ya mbao ngumu ya mti wa mwembe iliyokaa pweke katikakati ya sebule huku pembeni mwa sebule ile kukiwa na kabati kubwa la vyombo, jokofu moja kubwa pembeni ya lile kabati pia kulikuwa na seti ya sofa iliyopangiliwa vema na mtu anayejua kupamba. Alan aliketi kwenye moja ya sofa na kupokelewa na foronya safi laini ambayo ilimfanya atoe sauti za uchovu. Alikuwa akiendelea kuipeleleza ile sebule kwa usiri mkubwa.
“Unatumia kinywaji gani tafadhali…?” Aliuliza yule mwanamama huku akiachia tabasamu pana usoni mwake lililokwenda kuipamba sura yake pana ya duara.
“Naomba maji tu.” Akaagiza Alan huku akikitazama chumba kimoja cha kulia chakula ambacho kilikuwa na meza moja ndefu ya duara sambamba na viti sita virefu pia vilivyoendana na meza ile. Pembeni ya chumba kile kulikuwa na jokofu dogo la kupozea maji na kwa upande wa kuume mwa chumba kile ukiingia kulikuwa na meza nyingine fupi ya kioo na kiti kimoja.
“Karibu sana…?” Alikaribishwa Alan na kuyarudisha mawazo yake pale sebuleni kwa mara nyingine.
“Asante sana shemeji…asante sana. Vipi jamaa nimemkuta…?”
“Nani…baba Omary…?” Aliuliza yule mwanamama. Alan akasita kidogo na baada ya kumfikiria yule mtoto kule nje aliyesikia akiitwa kwa jina la Omary, haraka sana akakubali.
“Yupo ndiyo, ngoja nikakuitie…?” Aliondoka yule mwanamama na kumuacha Alan akilitazama vizuri umbo lake kwa nyuma. Hakika alikubali kuwa Hamidu Jumbe alijua kuchagua mali iliyokwenda kidato.
Punde baada ya kusubiri, alitokea bwana mmoja sebuleni hapo akiwa amevaa singleti nyeupe na pensi yenye mifuko mingi ya khaki chini akiwa miguu wazi. Kwenye mkono wa kulia kulikuwa na bandeji nyeupe iliyofungwa kuanzia kwenye nyama za misuli karibu na kwapa kuja hadi karibia na kiungio cha mkono ule. Kulikuwa na rangi nyekundu ya dawa iliyoonekana kulilowesha lile bandeji kwa juu hata hivyo pia kulikuwa na plasta moja kubwa iliyopita juu ya bandeji pembeni kidogo ya jicho la kushoto. Alifika hadi nahali alipo mgeni wake akampa mkono na kusabahiana kwa furaha kana kwamba ni watu wanaofahamiana kwa muda mrefu. Alan akampa pole kamanda huyo kwa majeraha yale yaliyobakia kama alama ya misukosuko ya vita na Jumbe akaitikia kwa furaha kubwa.
Hii ndiyo Tanzania yetu.
“Karibu sana ndugu?” Alikaribisha Hamidu Jumbe huku akitaka kutwaa nafasi ya kuketi.
“Asante sana naitwa Iddiallan Simion ni askari mpelelezi kutoka kitengo muhimu na cha siri hapa nchini ujio wangu huu upo kwa maagizo maalumu kutoka kwa Luteni kanali Daniel Matia Okale.” Alijitambulisha Alan baada ya kuupokea ukaribisho. Utambulisho huo ndiwo uliomfanya Hamidu Jumbe kusita kukaa, akasimama wima na kumtaka mgeni wake waelekee kwenye chumba cha mazungumzo maana hapo alijua ni nini kimefuatwa. Alan akapiga funda la mwisho la maji na kuitelekeza bilauri pale mezani ikiwa tupu. Hamidu Jumbe alilifuata jokofu na kulifungua kisha akatoa chupa kubwa ya Konyagi na kutwaa bilauri mbili kutoka kwenye kabati palepale sebuleni kisha akaongoza hadi chumba cha mazungumzo. Hakikuwa chumba kidogo, kilikuwa ni chumba kikubwa chenye madiridha makubwa yaliyowekwa mapazia mepesi yenye kuwezesha kuona nje. Upepo kutoka kwenye miti iliyopo pembeni ya madirisha hayo ulifanikiwa kuyapiga kikumbo mapazia yale na kutawanya hewa safi ndani mule. Kulikuwa na rafu ya vitabu na makabrasha mengine mengi huku kukiwa na meza ya duara ya mbao ya Mtiki sambamba na viti vitano safi vya mbao vilivyopambwa kwa foronya laini mahali pa kukalia na kuegemeza mgongo.
“Ndiyo, kamanda karibu sana Bagamoyo?” Alianzisha mazungumzo Hamidu Jumbe.
“Nimekaribia kamanda na nafurahi kupata hewa safi ya asili kutoka pwani.”
“Hakika.” Alijibu Hamidu kisha akavuta ukimya halafu akaendelea.
“…umesema uko hapa kwa agizo la Luteni Daniel Matia Okale…?”
“Ndiyo, niko hapa kwa maagizo maalumu?”
“Yepi hayo?”
“Kuhusiana na operesheni T.W.W ambayo mlikwenda kuifanya nchini Somalia.”
UPELELEZI UNAENDELEA.
Kulikuwa na rafu ya vitabu na makabrasha mengine mengi huku kukiwa na meza ya duara ya mbao ya Mtiki sambamba na viti vitano safi vya mbao vilivyopambwa kwa foronya laini mahali pa kukalia na kuegemeza mgongo.
“Ndiyo, kamanda karibu sana Bagamoyo?” Alianzisha mazungumzo Hamidu Jumbe.
“Nimekaribia kamanda na nafurahi kupata hewa safi ya asili kutoka pwani.”
“Hakika.” Alijibu Hamidu kisha akavuta ukimya halafu akaendelea.
“…umesema uko hapa kwa agizo la Luteni Daniel Matia Okale…?”
“Ndiyo, niko hapa kwa maagizo maalumu?”
“Yepi hayo?”
“Kuhusiana na operesheni T.W.W ambayo mlikwenda kuifanya nchini Somalia.”
SONGA NAYO….
“Kipi kinachohitajika hasa kutoka kwenye operesheni ile ya ukombozi?” Hamidu Jumbe aliuliza kwa utulivu mkubwa sana na yote hayo alikuwa akiyafanya sambamba na kumimina kinywaji kile kikali kwenye bilauri zile mbili na hapo alikuwa ameweka miguu yake kwa mtindo maarufu wa nne huku mgongo wake akiuegemeza kitini akimtazama kijana huyo mkononi mwake akiwa amekamatia bilauri ile iliyosheheni kinywaji. Alan alipiga kumbo moja la kinywaji kile kikali kinywani mwake na kumeza kwa utaratibu na baada ya hapo akaweka utulivu kabla ya kuzungumza.
“Inajulikana kuwa kuna mengi ya kutisha yalitokea huko ambako mlikwenda kwa lengo la kuwatafuta wajumbe waliotumwa nchini Kenya na kutekwa kisha kuingia mikononi mwa magaidi. Yote ya yote ni kazi ya jeshi hivyo kulikuwa hakuna budi zaidi ya kupambana kufa na kupona. Mmefanya kazi kubwa sana hadi kufikia tamati mwa zoezi lile hata hivyo nilikuwa na maswali machache yanayohitaji majibu kutoka kwako kamanda…maswali hayo yako ya namna tofauti hata hivyo ni yenye msaada mkubwa kwa taifa hili kwa kuwa hadi sasa hatuna hakika kama lile suala litaisha kwa namna gani. Kuna chochote ambacho umekigundua katika vita hiyo mliyopigana nchini Somalia?” Aliuliza Alan mara baada ya kutoka kutoa maelezo marefu. Kamanda Hamidu Jumbe akafikiri kwa muda mrefu kidogo kabla ya kuzungumza chochote. Kimya chake kilikuja kukoma baada ya kujikohoza katika namna ya kuliweka koo lake sawa kisha akasema;
“Hakuna sehemu yoyote ambayo umepitia hadi kufikia hapa kwangu?” Aliuliza Hamidu Jumbe huku akimtazama Alan usoni. Alan akavuta pumzi nyingi mapafuni mwake na kuzishusha kwa mkupuo mmoja akasema;
“Hii ni hatua yangu ya pili, kuna mtu amenipa ushirikiano mzuri na mwisho wa mazungumzo yetu akakutaja wewe kuwa unaweza kunifanya nifike ninapopahitaji.”
“Kipo kitu kimoja ambacho labda kinaweza kukupa ufumbuzi wa hili kabla hatujaendelea na maongezi yetu.” Akasema Hamidu Jumbe kisha akanyanyuka na kusogea hadi kwenye ile rafu ya vitabu na kuchukua bahasha ndogo ya khaki akarudi nayo mezani. Aliifungua ile bahasha akatoa picha tatu na kuziweka mezani na kumtazama Alan usoni. Alan alizivuta na kuzichambua akitazama moja kabla ya nyingine. Alizitazama kwa umakini mkubwa zile picha hata hivyo hakuwa ameelewa kitu, zilikuwa ni picha zinazomuhusisha mtu mmoja ambaye alikuwa kwenye mikao tofauti. Picha ya kwanza ilimuonesha mtu huyo akiwa anatembea huku macho yake akiyaelekeza mbele, ya pili pia alikuwa katika mtembeo lakini hii alikuwa karibu na gari ndogo aina ya Toyota Baloon. Alikuwa amevaa jaketi jeusi lenye michirizi myeupe na myeusi mikononi na shingoni, mikononi alivaa glovu nyeusi, suruali ya rangi nyeusi na kofia ya kapelo ya rangi nyeusi pia. Alikuwa mrefu mwenye mwili wa wastani hakuwa mnene sana wala mwembamba sana rangi yake ilikuwa ya maji ya kunde. Hakuonekana sura yake kwa namna picha hizo zilivyopigwa. Picha ya tatu alionekana kwa uchache tu kuanzia juu hadi kifuani na upande wa chini akiwa amekingwa na ile gari. Alizitupa chini ya meza zile picha kisha akamtazama kamanda Jumbe usoni kwa umakini mkubwa.
“Zina mahusiano yoyote hizi picha na kile ninachokihitaji?” Akauliza.
“Ninayo imani hiyo kwa asilimia kubwa.”
“Kwa namna ipi?”
“Picha hizo nilizipiga tukiwa tumelikaribia kabisa jengo walilohifadhiwa wajumbe wetu, hili ni jengo ambalo halikuwa kwenye makazi ya watu kabisa na kutokea hili jengo lilipo hadi kufikia kwenye makazi ya watu ni kama kilomita tatu, unapata picha gani…? Hii inamaanisha kuwa jengo hili liliandaliwa mahususi kwa kazi maalumu na pengine kazi yenyewe ilikuwa hii. Kwa udadisi wangu nilioufanya bilashaka jengo hili lilijengwa kwa kazi ya utesaji na uchukuaji wa siri kutoka kwa watu wengine na ni kwa mateso makali ambayo hupelekea kifo kwa wateswaji…!”
“Kwanini unahisi hivyo kamanda?” Aliuliza Alan huku akianza kuvutiwa na yale maongezi, kifaa chake cha kunasia sauti kilikuwa kazini kwa usiri mkubwa kikiendelea kuchukua mahojiano yale muhimu. Kamanda Jumbe alimeza funda la mate kabla ya kusukumia na kinywaji kilichopo ndani ya bilauri yake kisha akaendelea.
“…jengo lile kwa ndani lilijaa harufu mbaya ya mizoga na damu chafu, hili nililihisi mapema na sidhani kama mwenzangu alikuwa na akili ya udadisi kama yangu. Tulipoingia kwenye chumba cha mateso huko ndiko kulikonidhihirishia haya niyasemayo, wajumbe wetu waliotumwa na mataifa yetu kwa ajili ya mazungumzo ya kuimarisha ulinzi au kutokomeza vitendo vya kigaidi vilivyokuwa vikiinyemelea mipaka ya mataifa yetu, walikuwa katika hali ambayo huwezi kudhani kama mwanadamu wa kawaida ndiye ambaye angeweza kufikia hatua ya kutenda yale yaliyotendwa kwa watu wale. Waliteswa vibaya sana miili yao ilijaa majeraha mabaya yanayotisha na walishapoteza maisha.” Maelezo yale ya kamanda Jumbe yalimfanya Alan azitazame zile picha kwa ukaribu mkubwa aliinyanyua moja baada ya nyingine kishapo akazitupa tena mezani.
“Hili jengo lipo hadi sasa?” Akauliza Alan alipotoka kuzitazama zile picha. Alitaka kuunganisha majibu ya kamanda Rhoda na ya Jumbe ingawa alijua kuwa kulitokea mlipuko na ukawapelekea kuwa katika hali mbaya, pengine yapo mabaki.
“Hapana…!” Alijibu kamanda Jumbe kisha akatulia na kuhema kwa nguvu kishapo akaendelea tena.
“…hapana, lile jengo ndilo lililotaka kuondoka na uhai wetu kwani tulikaa kwa dakia mbili tu mule ndani ndipo mwenzangu alipofanikiwa kuona bomu kubwa la kutega masaa likiwa limelaliwa na mmoja wa wajumbe wetu ikatubidi kutumia nguvu kubwa ili kujinasua maana tulishachelewa tayari.”
“Unahisi ni kwanini waliamua kufanya yale je, walihisi ujio wenu pale ama walihisi nini unadhani?”
“Hakuna kingine Alan, wale jamaa walijua kuwa tungefika pale hivyo wakataka kutufuta kwenye uso wa dunia kwa namna ile kama si hivyo basi walikuwa na lengo la sisi kutokuwaona watu wetu kabisa na tusizipate siri za walipo watu wetu kabisa kwani waliamua hadi kuwaangamiza walizi waliyopo ndani ya jengo lile. Na hakuna mwingine ambaye alitega hilo bomu zaidi ya mtu huyo pichani kwani ndiye mtu wa mwisho kutoka ndani ya jengo lile. Tunayo hakika hiyo kwa asilimia zote kwa kuwa mtu ambaye tulimbana na kumdadisi kwa maswali yetu alitueleza kuwa kuna watu maalumu ambao walihusika kwa ajili ya mahojiano ya watu wale na kwa kuwa yeye ndiye aliyetoka punde na kupelekea sisi kushuhudia yale basi hakuna shaka kwenye hilo kuwa ni yeye.”
“Huyo mliye muhoji amesema kuwa wapo watu maalumu na si mtu?”
“Inamaana kuwa hakuwa mtu mmoja huwenda walikuwa ni wawili ama zaidi ya hapo.” Alan akaweka utulivu na kuegamia kitini akitafakari yale aliyoelezwa, utulivu ulikuwa mkubwa sana baina yao na hakukuwa na aliyejaribu kutia neno takribani dakika tatu nzima kila mmoja alionekana akitafakari ya kwake. Ukimya ule ulikuja kukoma baada ya Alan kujinyanyua pale kitini na kuchukua zile picha na kuzirudisha kwenye bahasha na kuzitumbukiza kwenye begi lake dogo la kubeba mgongoni.
“Asante sana kamanda kwa msaada wako nadhani hiki ulichonipatia leo kitakuwa ni msaada mkubwa sana kwangu nadhani mimi nikuage sasa.” Aliongea Alan huku akisimama na kumpa mkono kamanda Jumbe. Kamanda Jumbe alisimama na kuupokea ule mkono wa kwaheri kisha akatoka naye hadi sebuleni ambapo walimkuta yule mwanamama akamuaga na kuondoka zake.
Kazi ile aliyopewa na mkuu wake wa kazi ilikuwa imekwisha kukamilika tayari kulikuwa hakuna kilichosalia zaidi ya kuwasilisha kile alichokwisha kukikamilisha na kujua nini kingine ambacho kilikuwa kinakwenda kufanyika. Alan alikuwa katikati ya jiji la Dar es salaam akifanya matembezi yake ya kawaida, aliikumbuka sana mitaa mingi ya jiji hilo japo hakuwa ameishi sana jijini hata hivyo kuna baadhi ya mitaa alikuwa akiihusudu zaidi. Alipomaliza kufanya mihangaiko yake alifunga safari kwa ajili ya kurudi kitengoni kwani baada ya mazishi ya wanajeshi wale wawili kufanyika kila mmoja alirudi kwenye majukumu yake na kazi ile ya upelelezi ikiachwa mikononi mwa mwalimu Dao. Hivyo Alan alikuwa na safari nyingine akitokea hapo hadi mjini Morogoro ambako ndipo maficho ya jengo lao la siri lilipo. Haikuchukuwa muda mrefu kuweza kujiandalia safari hiyo na kuondoka jijini hapo na kuelekea mjini Morogoro.
KITENGONI SAA 16:30 ALASIRI.
Alan alikuwa akiingia ndani ya ofisi kuu ya siri ya kitengo maalumu cha kupambana na ujasusi nchini kwa hatua zake za taratibu. Jengo lilikuwa limepoa sana kana kwamba hakukuwa na mtu hata mmoja. Aliufungua mlango mara baada ya kuugonga kwa utambulisho maalumu kisha akaingia ndani. Alisogea taratibu hadi mahali ilipo meza ya mkuu wake wa kazi kisha akapiga saluti mbele ya mkuu wake ambaye aliipokea kisha akavuta kiti na kuketi. Walitazamana kwa muda pasipokusemezana mwalimu Dao aliyekuwa akisoma jalada hili na lile alisitisha zoezi lile na kumtazama kijana wake. Haikuwa ofisi ngeni machoni mwa Alan kila kitu kilikuwa kama alivyo kiacha. Mwalimu Dao alivuta pakiti ya sigara na kuchomoa sigara mbili toka pakitini na kumkabidhi moja Alan ambaye aliipokea na kuibana kwenye kingo za midomo yake na kuvuta kiberiti cha gesi mezani pale akaiwasha ile sigara na kumuwashia na mkuu wake. Alipiga pafu moja kubwa na kuuachia moshi mwingi nje.
“Karibu sana kazini kijana wangu?” Alifungua maongezi kwa ukaribisho mzee huyo mkakamavu mwenye kipara kinachowaka kichwani mwake na kuuegemeza mkono wake wenye sigara mezani huku macho yakimtazama Alan na tabasamu likiwa usoni barabara.
“Asante sana mwalimu naona nimerudi nyumbani tena na nimerudi kwa aina ya peke yake sana hadi nashangaa.” Alijibu Alan kabla ya kuipeleka tena sigara yake kinywani.
“Hakukuwa na njia nyingine ya kukurudisha nyumbani zaidi ya hiyo kwanza nikupongeze kwa kuhitimu mafunzo yako kwa ubora mkubwa sana nimeona rekodi zako za kimafunzo na ufaulu wa mitihani yako ambayo ulikuwa ukipatiwa na wakufunzi wako, hakika umestahili sifa.”
“Asante sana mwalimu naona nimerudi nyumbani tena na nimerudi kwa aina ya peke yake sana hadi nashangaa.” Alijibu Alan kabla ya kuipeleka tena sigara yake kinywani.
“Hakukuwa na njia nyingine ya kukurudisha nyumbani zaidi ya hiyo kwanza nikupongeze kwa kuhitimu mafunzo yako kwa ubora mkubwa sana nimeona rekodi zako za kimafunzo na ufaulu wa mitihani yako ambayo ulikuwa ukipatiwa na wakufunzi wako, hakika umestahili sifa.”
SONGA NAYO…
“Asante sana na nashukuru sana kwa zawadi hii ambayo taifa langu limeamua kunipatia na pia nikushukuru wewe kwa kuweza kuendeleza vema pale ambapo father Hussei Babu aliishia nanyi mnastahili pongezi za shukurani kwa kutenda haya yaliyo mema.”
“Yote ni kwa ajili ya uzalendo.” Alimaliza Dao na kuiweka sigara yake kwenye kingo za mdomo na kuivuta kwa madaha makubwa sana kabla ya kufungua kinywa chake tena kuzungumza.
“Nini umeweza kugundua kwenye kazi niliyokupatia…?” Aliuliza na kujiweka sawa kitini.
“Mikono ya Jasusi…!”
“Mikono ya jasusi…kivipi iwe ni mikono ya jasusi…?” Akauliza mwalimu Dao kwa hamaki na kuegemeza mikono yake mezani akiwa tayari kabisa kusikiliza kile kilichotaka kuzungumzwa. Alan akaibana sigara yake kwenye kingo zake za midomo akaivuta na kuitoa kisha akamtazama kiongozi wake usoni.
“Huu haukuwa mchezo wa kuigiza…!” Akaanza kuzungumza, akaweka koma na kuendelea kwa mara nyingine.
“…huu ulikuwa ni mpango wa muda mrefu na wapangaji walikuwa na dhamira ya kile walichokipanga. Mchezo huu ulisukwa kwa nguvu kubwa hata hivyo ulitumia akili nyingi na uvumilivu mwingi. Wakati maafisa wa ngazi za juu za kijeshi wa mataifa haya mawili wakiwa wanakutana kwa ajili ya kushawishiana kuunda umoja wa kupambana na ugaidi unaojiingiza kwenye nchi zao, kulikuwa na watu wengine waliowekwa kama wachunguzi walioweza kuona hili na kutoa taarifa kwa wahusika wakuu wa mpango huo hivyo ikawa rahisi wao kuweza kuwatega na kweli wakaingia kwenye mitego yao pasipo kuwa na taarifa yoyote kama walitegwa…!”
“Unataka kuniambia nini kwenye hili unalolizungumza?” Aliuliza kwa kudakia mwalimu Dao. Alan akavuta sigara yake kisha akakung’uta majivu kwenye kibakuli maalumu cha kuhifadhia majivu na mabaki ya sigara na kusema;
“Ninachotaka kukuambia na kile nilichokigundua katika upelelezi wangu ni hiki, kwenye mpango huu walihusishwa wenyeji…?”
“Hebu ngoja Alan, unataka kuniambia ndani ya jeshi la Kenya au Tazania wapo watu ambao si waaminifu? Ingawa inaweza kuwa hivyo na hata viongozi wakuu wa usalama nchini wanaamini hivyo, nini wewe umeona zaidi?”
“Hili ndilo nililotaka kulizungumza mkuu, ukitazama vizuri kwa jicho la Tai utagundua kuwa mpango huu ulikuwa ni siri kubwa hata hivyo siri hii iliwahusisha maafisa wa ngazi za juu za kijeshi sasa kwanini uwe rahisi kuharibika na kusababisha wajumbe wale waliotakiwa kuleta maazimio mazuri kutekwa na hatimaye kubanwa kwa maswali mazito hadi kuuawa.”
“Napata wasiwasi Alan kunauwezekano mkubwa siri za mpango ule zikawa uchi tayari na kama ziko uchi hii ina maana kuwa huwenda ikawa ni hatari kubwa kwetu ama Kenya.” Akasema mwalimu Dao.
“Kinachotakiwa ni kuwa macho zaidi.”
“Si kuwa macho tu Alan bali kufanya kitu.”
“Ndiyo.”
“Enhe! Haya niambie zaidi.”
“Kuhusu kuwa uchi kwa siri huwenda ikawa kweli hata hivyo kuna uwalakini mkubwa ndani yake maana inasemekana kuwa wajumbe wale walikuwa wakaidi sana kutoa siri walizonazo na hii ikapelekea chuki kubwa kwa waliokuwa wakitumika kuwahoji na ikasababisha kuamua kuwaua. Japo napingana na hili ambalo nilielelezwa na yule mwanamama nchini Kenya ambaye ndiye aliyenieleza hili ambalo walilipata kutoka kwa mateka wao mmoja wa kikundi hicho cha kigaidi ila kwa imani yangu inaniambia kuwa nisidhani sana juu ya hilo kwani ni watu wachache sana duniani wenye uwezo wa kuhimili mateso na kukubali kufa na siri zao. Kuna mengi nimeyagundua mkuu na yamenipa mashaka makubwa mno. Nimeweza kuchunguza namna wajumbe wale walivyotekwa na wengine kuuawa na vifo vyao kuwa katika utata hakika nimegundua kuwa ile haikuwa mikono salama na waliyohusika walikuwa katika elimu kubwa. Mikono iliyotumika kuwaondoa wajumbe wale kwa namna niliyochunguza na taarifa uliyonipa ni kwamba haikuwa mikono salama bali iliyojaa ujuzi wa hali ya juu ya kutekeleza mauaji.” Alihitimisha kutoa maelezo hayo Alan kisha akaivuta tena sigara yake na kuomba utulivu wa akili huku mwalimu Dao akiwa anatafakari ya kwake kichwani.
“Lazima tufanye kitu Alan…tufanye kitu kulikomboa taifa hili lisiingie katika vita kali na mataifa haya mawili lazima iwe…!” Hakumaliza kuonge Daniel Matia Okale. Simu ya ofisini kwake ilikuwa inaita moja kwa moja na ilikuwa ni simu ambayo haikuwa ikipigwa mara kwa mara hivyo alivyoona simu hiyo inaita moja kwa moja akajenga picha kuwa kilichokuwa kikienda kutokea au kilichotokea hakikuwa cha kawaida. Simu ile ilikuwa maalumu na ilitoka Ikulu moja kwa moja. Kwanini Daniel Matia Okale alijenga hofu na hii simu? Alijenga hofu kwa kuwa maamuzi ya kupewa kazi ile yalitoka kwa mkuu wa nchi kwani kitendo cha kuuawa wanajeshi kwa mtindo ule haukuwa wa kutazamika kipumbavu hivyo hata ripoti ya kiuchunguzi iliyofanywa na madaktari wawili Dokta Limo na Dokta Lumoso ilifika mikononi mwa mkuu huyo na kutoa amuzi hilo kuwa kazi hii ifanyike kwa ubora mkubwa na kitengo chenye uwezo wa kuifanya kazi hiyo kilikuwa ni hicho chenye sifa ya kupambana na mambo hayo pekee. Aliivuta ile simu na kupachika kiganja cha mkono wake kwenye kiwambo cha sauti na kuisikiliza ile simu akiwa mtulivu. Hakuongea kitu alitakiwa kuwa msikilizaji na kwa kadiri alivyokuwa akiisikiliza simu ile ndivyo sura yake ilivyokuwa ikibadilika na kuweka tashwishi kubwa ambayo ilianza kumpa hofu Alan. Aliishusha simu ile kwenye kikalio chake na kushusha pumzi nzito akajiegemeza kitini kwa nguvu akiwa hoi kifikira.
“Kumekucha…!” Hili likawa ni neno lake la kwanza kuzungumza mara baada ya kutoka kuongea na simu ile. Alan hakuongea kitu alibakia akimtazama usoni kana kwamba kuna alama alitaka kuiona.
“Luteni Jenerali Leous Mipango amekutwa akiwa mfu ndani ya chumba cha hoteli ya Mtendele jijini Tanga.”
“Shabashii!” Alihamaki Alan akiwa haamini kile anachokisikia kutoka kwa mkuu wake wa kazi.
“Ndiyo, kifo chake inasemekana kinafanana kila kitu na kile cha Luteni Usu Makame Daudi aliyeuawa kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena huko Nairobi; Kenya. Sasa Alan nakubaliana na wewe kuwa ile haikuwa mikono salama na pia haukuwa mpango wa hivi karibuni bali ni wa muda mrefu kama si kuniambia nisingeweza kuamini kwa haraka kuwa wanaweza kutekeleza hili kwa haraka na kwa wepesi kiasi hiki, tunalo balaa hapa nchini mwetu.?” Aliongea Mwalimu Dao akiwa katika majonzi ya ghafula sana kwani Luteni jenerali Leous Mipango alikuwa ni mtu wa kazi haswa hivyo kifo chake kinakwenda kuweka pengo kubwa sana jeshini kwa kumkosa mtu huyo. Hili lilikuwa ni pigo la makusudi kutoka kwa maadui zao. Aliwaza mengi na kushindwa kujipembenulia mambo kwa wepesi, hakika walijua namna ya kupiga.
Hiyo ilikuwa na maana gani je, utakuwa muendelezo wa kuuawa maafisa wa jeshi ama ni kwa namna gani? Na kama ni hivyo je, itakuwa kwa Tanzania pekee ama hata nchi ya Kenya itahusika? Hayo yalikuwa ni maswali mazito sana kwa upande wake.
“Kwanini iwe Tanga mkuu?” Aliuliza Alan baada ya kutoka kuwaza mengi naye kichwani mwake. Upole wa majibu ya Daniel Matia Okale ulidhihirisha ni kiasi gani alivyokuwa na huzuni nyingi kichwani mwake.
“Luteni Jenerali Leous Mipango anaishi Tanga na pia anafanyia kazi kule yupo kwenye kambi ya jeshi ya Kange ni mwalimu pia wa chuo kile cha Anga cha kijeshi ni mtu wa karibu sana kwani hata Moniela alipofikishwa pale mkuu wa chuo kile alimkabidhisha kwake baada ya kusikia ametoka kwangu. Ni mtu ambaye tulifahamiana kwa uchache sana na ni katika kipindi ambacho muheshiwa Rais wa awamu hii alipokuwa akiapishwa ili kukabidhiwa kiti cha u-Rais rasmi Ikulu jijini Dar es salaam. Ni mcheshi na mkarimu sana na awapo kwenye nguo za kiraia unakataa kama alikuwa ni mwanajeshi mahili kwa namna alivyokuwa akipenda kujichanganya na watu hata hivyo alikuwa si mpenda utani awapo kazini. Ni kiraka kimepotea wakati uhitaji wake ni mkubwa sana hasa katika kipindi hiki cha sintofahamu.” Alijibu na kutoa sifa za marehemu kwa uchache mbele ya kijana Alan.
“Kwanini iwe ni kwenye chumba cha Hoteli…? Hili nalo linanipa wasiwasi kidogo.”
“Hakuna anayejua kama mimi na wewe tusivyojua kwanini imekuwa hivyo Alan na ni kosa kubwa kujadili wakati tukio limeshafanyika na hakuna hatua inayochukuliwa. Hakuna budi zaidi ya kufika eneo la tukio na kabla hujafika huko ni vema tukahitimisha kile kilichokufikisha wewe hapa ili upokee majumu mengine. Nadhani umeona namna mwili wa Makame Daudi ulivyofanywa na muuaji, sumu iliyotumika kama geresha kama ambavyo wewe mwenyewe unasema na namna alivyouawa. Umeona ni hatari kiasi gani iliyopo mbele ya macho yako. Kwanza kabisa nikuoneshe picha za mwili huo hasa kwenye hizo alama.” Aliongea Daniel Matia Okale akaamka kutoka kitini mara baada ya kukirudisha kiti nyuma akasogea kwenye meza nyingine ndogo akavuta mtoto wa meza na kutoka na picha mbili ndogo. Picha hizo zilipotazamwa na Alan, aliweza kuona mwili wenye alama mbili za matundu madogo ya risasi. Moja likiwa kwenye paji la uso na jingine likiwa kwenye shingo upande wa kushoto. Picha nyingine ilionesha alama tatu zilizowekwa mahala pamoja na zilikuwa ni alama za kucha kama za mnyama jamii ya paka ambazo zilizama kwenye ngozi ya marehemu na kuacha alama hizo ambazo kwa mujibu wa vipimo vya madaktari ilisemekana kuwa ndizo zilizoaminika kubeba sumu iliyoonekana kusambaa kwa haraka mwilini mwa marehemu Makame Daudi. Alizishusha zile picha mezani na kuvuta tafakuri pana kichwani mwake kisha akagutuka kama ambaye alikumbuka kitu. Akafungua begi lake dogo na kuchungulia ndani akatoka na picha zile tatu ambazo alipewa na kamanda Hamidu Jumbe huko Bagamoyo komandoo pekee kutokea Tanzania aliyehusika kwenye operesheni T.W.W au wenyewe wanaiita operesheni ya ukombozi huko nchini Somalia ambayo ilisababisha kupoteza kwa maisha kwa wanajeshi wawili mmoja akiwa mkenya na mwingine kutokea hapa nchini. Aliweka picha mbili mezani akimpa wasaa na mkuu wake kuzitazama huku yeye akibakiwa na picha moja mkononi mwake. Aliitazama hii picha kwa umakini mkubwa hata hivyo hakuambua kitu kile alichotaka kuambua. Alitaka kuona kitu kwenye zile glove ambazo yule mtu pichani alivaa hata hivyo hakuona na kuamua kuitupia mezani hata ile pia na kuigamia kitini akichukua sigara kutokea pale mezani na kuiwasha kwa kiberiti cha gesi ambacho nacho kilikuwa pale mezani. Pia aliamua kumkabidhi mkuu wake ile redio iliyorekodi mazungumzo yake na komabdoo Hamidu Jumbe ili aweze kuyasikiliza kwa muda wake. Aliendelea kuvuta sigara yake huku Dao akiwa anazitazama zile picha moja na nyingine hadi zilipomridhisha ndipo alizirudisha mezani na kumtazama kijana wake.
Pia aliamua kumkabidhi mkuu wake ile redio iliyorekodi mazungumzo yake na komabdoo Hamidu Jumbe ili aweze kuyasikiliza kwa muda wake. Aliendelea kuvuta sigara yake huku Dao akiwa anazitazama zile picha moja na nyingine hadi zilipomridhisha ndipo alizirudisha mezani na kumtazama kijana wake.
SONGA NAYO….
“Huyo ndiye aliyesalimika kutoka kwenye jumba lililotaka kutoa maisha ya Makomandoo wawili waliokwenda kwenye ile operesheni ya ukombozi.” Alisema Alan huku akiuruhusu moshi wa sigara aliyovuta kwa pafu kubwa kuificha ile ofisi.
“Mtazame mara nyingi huyu mtu Alan.” Alisema Dao huku naye akipachika sigara mpya kingoni mwa midomo yake.
“Usitie shaka mkuu, natumai nitajitahidi kumfanya kuwa rafiki na mtu wa karibu sana punde nikutanapo naye.” Alijibu Alan. Dao aliupuliza moshi wa sigara yake hewani na kutuliza macho yake kwenye silingboard ya ofisi ile iliyosiribwa rangi ya maziwa na kupandwa taa moja yenye mwanga mzuri wa kusomea sambamba na feni la panga boi katikati ambalo lilikuwa limetulia tuli huku kiyoyozi pekee kikiwa ndicho kinachowaburudisha mule ndani kwa kuwapa hewa safi ya kuwafanya wajihisi kuendelea kuwepo.
“Tanga si salama kwa sasa macho ya wauaji yatakuwa yakitazama kwenye mipaka yote ya jiji hilo kuona kama kuna mgeni yeyote anayeingia ambaye ataleta madhara kwao. Sina hakika kama muuaji ameua na kuondoka ila kama majasusi waaminiwa na makini, hatuna budi kuwa makini pia. Ni kazi yako ya kwanza kitengoni hata hivyo si mgeni wa kukutana na shughuli hizi za kijasusi. Gari imekwisha kuandaliwa ambayo itakupeleka hadi Tanga nikiwa na maana kuwa ndiyo gari utakayoitumia katika misheni yako kama utapenda iwe hivyo au kama hutapenda basi unaweza kutumia njia yoyote upendayo kwani kila kitu kiko sawa. Najua watapenda kukukarimu mgeni ukifika na nina hakika watakuwa uwanja wa ndege jijini hapo na watakusubiri kwenye vituo vyote vya mabasi ili kuhakikisha hujihisi mpweke mara tu utakapoingia. Namna tunavyofanya mawasiliano unajua na kama kuna tatizo linalohitaji ufumbuzi wa kitafutishi pia unajua ni wapi ambapo unaweza kupata. Nikutakie safari njema.” Akamaliza kuzungumza mwalimu Dao huku mezani akiweka kadi mbili za ATM za kampuni mbili tofauti za kibenki na vitambulisho viwili, kimoja kikimtambulisha kama mfanya biashara ambacho kilibeba jina la Jabir Azakia huku kimoja kikimtambulisha kama mwandishi wa habari wa gazeti la serikali kilichobeba jina la Abasi Mgizu. Funguo za gari alilotakiwa kulitumia sambamba na bastola moja aina ya berreta iliyojaa risasi sambamba na mfuko wa bastola hiyo uliyojaa risasi za kutosha. Alan alikisogeza kiti nyuma akapaki vitu vile kwenye begi lake dogo la kubeba mgongoni ambalo lilikuwa na uwezo wa kuficha vitu vingi vidogodogo na zana za siri za kijasusi akalifunga na kusimama huku akizirudisha funguo za gari kwa mkuu wake. Hiyo ilikuwa na maana kuwa hakupenda kusafiri kutokea hapo hadi jijini Tanga kwa kutumia usafiri wa gari binafsi.
“Najua nia yako basi ujue tu kuwa unakwenda kufanya uchunguzi wa kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango ili ujue nini sababu ya kuuliwa kwake na je ni kweli wauaji ni wale wale na wako na nia gani hapa nchini. Hivyo umakini kwako unatakiwa kuwa mkubwa kuliko ambavyo ulishawahi kufanya kwani kwa hisia za kawaida tu inadhihirisha namna wauaji hao walivyo hatari. Usafiri wa kukufikisha kwenye sehemu utakazopenda kwenda uko sehemu mbili tu, kwanza ni Hospilali ya Mkoa (Bombo Hospital). Pili ni kwenye maegesho ya magari ya Mkonge Hoteli. Gari zote utazitambua kwa alama maalumu ambayo utaipata kwenye vifaa vyako vya kazi tulivyo kukabidhi, nikutakie kazi njema yenye mafanikio kwani taifa linawaamini sana vijana wake na ndiyo maana kazi hii ikawa mikononi mwangu. Hakikisha kwanza unakutana na Dokta Limo pamoja na Dokta Lumoso ambao wameweka kambi katika Hospitali ya Bombo kwa ajili ya kuchunguza mwili wa marehemu huyo hapa ndipo utakapojua heri na shari.”
“Asante sana mkuu nadhani sasa niende maana sasa ni saa kumi na moja na dakika tano nadhani muda huu utanitosha kuwahi kituo cha mabasi Msamvu na kupata basi lolote linalokwenda Dar es salaam kisha nitabadilisha basi Chalinze hadi Tanga. Napenda kuingia usiku ili kuweza kujificha vizuri.” Aliongea Alan na kuuelekea mlango wa kumtoa mule ofisini. Alipotoka baada ya kutakiwa safari njema na mkuu wake, kituo cha kwanza kilikuwa kwa katibu muhtasi wa mkuu wake ambaye walisalimiana kwa muda mdogo sana kisha akaelekea ofisini kwa Amiri ambako hakumkuta alitoka na kuingia kwa Chars pia vilevile hivyo akaamua kutoka kabisa kwani aliamini kwa wakati ule vijana walikuwa wameshajichanganya mitaani hivyo hakuwa na hakika kama Zomba pia angemkuta. Alifika nje kabisa ya jengo lile baada ya kupanda ngazi kadhaa akitokea kwenye jengo la chini ya ardhi kisha kuikamata korido ndefu na nyembamba ambayo ndiyo iliyomtoa nje. Alimkuta dereva anayetumika na ofisi yao akiwa anamsubiri garini hivyo walisalimiana kwa bashasha kubwa sana kwa kuwa ni muda mrefu hawakuwa wameonana.
“Hatimaye tumeonana tena Alan.” Alianzisha maongezi yule dereva ambaye alifahamika kwa jina la John.
“Nimerudi kijana hata hivyo si mkaaji sana hebu nifikishe Msamvu mara moja.” Alijibu Alan na kuzungumza hitaji lake.
“Wapi hiyo kijana Dar nini…?”
“Yaa, naelekea Dar es salaam kwa sasa kuna jambo nalifuatilia.” Alidanganya Alan na safari ikapamba moto huku kimya kikiwa kikuu garini hadi wanaingia kituo cha mabasi Msamvu ndipo walipozungumza kwa uchache na Alan akapata basi la BM ambalo lilikuwa likiondoka muda huo.
SAA 22:25 USIKU BASI LA TASHRIFF LILIKUWA LIKIMUACHA ALAN KWAMINCHI. Aliamua kuteremkia kituo hicho kwa kuwa kwa usiku ule mabasi hayakuwa yakiingia kituoni hivyo moja kwa moja hupiliza hadi kituo cha mabasi madogo mjini au kituo cha mabasi cha zamani kama wengi wanavyokiita. Wakati anaachwa hapo na basi hilo, aliangaza macho yake huku na huko na kuzitupa hatua kwa uchache kabla ya kuuruka mfereji na kuiacha barabara akabaki akitazamana na teksi kama nne hivi ambazo ndizo zilizosalia eneo hilo. Mbele yake kulikuwa na Hoteli ya Nyinda; Nyinda Respective Hotel. Akayatazama mandhari ya eneo hilo kwa haraka sana na kuona namna yalivyo na utulivu mkubwa, vijana watatu waliokuwa wakimfuata huku wakinadi biashara aliwaona hata hivyo hakuwa na haraka ya kuparamia teksi na badala yake akawa anaangalia ni teksi ipi ilikuwa ikimfaa zaidi huku akitazama na dereva ambaye hakuwa akimtilia shaka kwa majira yale hivyo akawa amesimama pembezoni mwa ule mfereji akigusagusa simu yake. Akiwa hapo alifanikiwa kumuona binti mmoja mrembo, mrefu na mwenye umbo la kuvutia ambaye alikuwa amevaa suruali iliyomkaa vizuri huku juu akiwa amevaa fulana nyeupe yenye maandishi makubwa kifuani AFRICA sambamba na ramani ya bara husika huku kidani cha umbo la kopa kikiwa kinaning’inia kifuani mwake juu ya matiti yake makubwa kiasi ya kuvutia. Macho yalimtoka Alan kuona mrembo huyo akiwa anatembea kwa mwendo wa maringo huku akiwa amekamatia mfuko mweusi wa nailoni mkononi mwake. Aliikaribia gari moja miongoni mwa gari zile nne za kibiashara; Toyota Baloon.
“Naona unauwa winga…!” Kijana mmoja alimtania yule dada aliyekuwa amefungua mlango wa gari hiyo Toyota Baloon ya rangi nyekundu na kujikalisha akitazama nje.
“Umejuaje, yaani nina njaa si ya dunia hii. Hapa napiga huu msosi halafu narudisha mpira kwa goli kipa maana nahisi uchovu tu na hali yenyewe imeshakuwa ngumu leo.” Aliongea yule msichana mrembo huku masikio ya Alan yakinasa mazungumzo yale.
“Subiri bado muda hadi saa tano hivi unaweza kubahatisha kichwa cha mwisho.”
“Aah wapi! Nimeshakubali matokeo ni kesho tena.” Alijibu yule msichana na punde wakaja watu wawili wakiwa na jinsia tofauti na walionekana kulewa kiasi maana walitokea hapo kwenye grosari ya jirani na kilipo kituo hicho cha teksi. Walimfuata yule kijana aliyekuwa akiongea na yule msichana na kuzungumza naye machache kisha wakafungua mlango wa gari moja iliyopo karibu na yule kijana wakaingia na yule kijana akaondoka taratibu. Haukupita muda wakatokea tena wawili wakaingia kwenye gari nyingine na mwisho akatokea mmoja huyu alikuwa ni mwanamama mweupe kuliko bara aliloumbiwa akaingia kwa yule kijana mara baada ya kukumbatiana na kupeana mabusu ya mdomoni.
“Bora ungeolewa tu Maisara muda huu ukawa unamburudisha mumeo apate usingizi kuliko kung’ang’ana na shughuli hizi za kiume, hali mbaya mitaani tunaziweza wenyewe.” Yule kijana aliyekuwa akipeana denda na yule mwanamama mweupe kabla ya kuingia garini, alimpa madongo yule msichana Maisara.
“Acha matusi wewe unadhani hili ni shimo la taka, kwenda huko na safari zako za bure malipo ngono. Na utakufa vifuani mwa magumegume malaya wa kiume wewe nyooo!”
“Yamekuwa hayo, basi dada basiii!” Alijibu yule kijana huku akiwa analizunguusha gari lake akilitoa barabarani wote wakaangua cheko kubwa.
Pale alibakia yule msichana ambaye alikuwa akila msosi wake taratibu huku akishushia na kinywaji laini. Alan alivutiwa sana na huyu msichana na kwa kuwa alikuwa akihitaji usafiri na usafiri wenyewe ni huo akaona awahi maana chelea chelea angeweza kukuta mwana ni wa jirani. Akazitupa hatua zake ili kuwahi kabla hajatokea mteja mwingine maana kwa nyakati kama hizo wateja wengi huwa ni walevi na wanawake wanaofanya biashara ya ngono na wanunuzi wa biashara hizo kwenye sehemu za karibu na mahoteli kama ilivyo hapo. Alimkaribia.
“Habari yako dada…?” Alisalimia huku akiwa ameliweka tabasamu usoni mwake.
“Salama karibu kaka…!” Alijibu Maisara huku akiufunga mfuko wake uliokuwa na chakula chake na kuifunga ile chupa ya kinywaji na kuvitupia kwenye dashi bodi ya gari yake na kuchukua chupa ya maji ambayo aliyatumia kunawia kisha akajifuta kwa kitambaa. Alan alikuwa tayari amekwisha jifungulia mlango wa upande wa pili wa abiria akiwa anamtazama dada huyo anavyohangaika huku akivutiwa na umbo lake lililojichora kwenye suruali ile ya jeans.
“Salama karibu kaka…!” Alijibu Maisara huku akiufunga mfuko wake uliokuwa na chakula chake na kuifunga ile chupa ya kinywaji na kuvitupia kwenye dashi bodi ya gari yake na kuchukua chupa ya maji ambayo aliyatumia kunawia kisha akajifuta kwa kitambaa. Alan alikuwa tayari amekwisha jifungulia mlango wa upande wa pili wa abiria akiwa anamtazama dada huyo anavyohangaika huku akivutiwa na umbo lake lililojichora kwenye suruali ile ya jeans.
SONGA NAYO….
“Samahani…!”
“Bila samahani najua ulikuwa unajipatia chakula.” Alimuwahi Alan kabla Maisara hajasema chochote. Maisara akabaki akigumia ndani kwa ndani na kuliwasha gari lake baada ya kutekenya ufunguo. Gari ikawaka na kuungurumishwa taratibu.
“Tunaelekea wapi bosi.” Maisara aliuliza kabla hata hajalitoa gari barabarani, bado tabasamu la kibiashara lilikuwa usoni mwake likiendelea kuzitekenya hisia za Alan.
“Nipeleke Maua Inn Hotel.” Akajibu Alan. Maisara akalitoa gari lake taritibu hadi barabarani na kuondoka maeneo hayo ya Kwaminchi kwa mwendo wa kawaida. Kimya kilikuwa kikuu kwa muda kidogo huku Maisara akizidi kuwa makini barabarani na macho ya Alan yakiwa makini kutazama nje upande wa nyuma kupitia kioo cha pembeni ya dereva. Walifika kwenye mzunguuko wa ilipokuwapo ofisi ya mkuu wa wilaya Tanga wakazunguuka na kukipita kituo cha kujazia mafuta karibu na kituo cha jeshi la zimamoto. Alan alimtazama Maisara kwa jicho la pembeni na kumuona akiwa anahangaika na kutazama mbele huku akiwa makini na usukani wa gari yake.
“Wewe ni mgeni ndani ya jiji hili?” Aliuliza Maisara wakiwa tayari wamesimama kwenye mataa ya stesheni ya reli. Lilikuwa ni swali la kushtukiza na lililomtoa Alan kwenye fikira zake na kumrudisha tena garini pasipo kutaraji.
“Hapana, mimi ni mwenyeji kabisa wa jiji hili, nimezaliwa na kukulia hapa ila ni mtu ambaye mara nyingi nakuwa kwenye shughuli zangu za kikazi nje ya hapa.” Alijibu akiwa mtulivu kabisa huku akimtazama mrembo huyo vizuri. Kwa kupitia mataa ya barabarani yaliyokuwa yakimulika ndani ya gari ile aliweza kuutazama kwa ukaribu urembo wa maisara japo ni mtazamo hafifu sana kutokana na giza la ndani ya gari ambalo halikukubali kufukuzwa lote kwa mwanga ule wa taa za barabarani. Kifua chake kilichobeba mzigo mkubwa kiasi wa matiti ambao ulistiriwa vizuri kwenye sidiria na kupandishwa juu kidogo kiasi kuyafanya yajitokeze nje kulingana na sehemu ya kifua kuwa wazi kwa namna fulani kutokana na fulana yake nzuri ya kike kuwa na shingo pana. Sambamba na kidani kile kilimfanya aongeze nyongeza ya urembo wake uliyoweza kumfanya mwanaume yeyote rijali kuchanganyikiwa, nywele zake alizifunga kwa nyuma kiasi kidogo na kuzifanya zitokeze mfano wa mkia wa Farasi.
“Nilidhani ni mgeni maana wageni ndiyo wateja wetu wakubwa maana wenyeji ni mara chache sana kutumia usafiri wa namna hii.” Aliongea Maisara huku akigeuza shingo kwa mara ya kwanza kumtazama kijana huyo mtanashati ambaye alipiga suti yake safi ya rangi nyeusi ambayo ilimtoa kivingine kabisa.
“Inabidi wakati mwingine kulingana na muda ambao nimefika hapa mjini.” Alan alijibu kwa utulivu akiwa anamtaza mrembo huyo naye akichanua tabasamu.
“Biashara zako zinakuzuia kuambatana na mkeo? Samahani lakini kwa kukuuliza swali hilo.”
“Kwanini umeuliza hivyo?”
“Si vibaya mimi kuuliza hivi kaka yangu.”
“Hapana hazinizuii ila ni kutokana na kuwa bado zijafunga ndoa na sina mtu wa kuweza kutoka na mimi.” Alijibu Alan huku akizidisha tabasamu la kuchombeza, Maisara naye akatabasamu huku akiliondoa gari baada ya mataa hayo ya usalama kuruhusu. Aliiacha barabara ya Mkwakwani na kuingia barabra za namba akiivuka reli.
“Wapo wenye bahati zao ambao wanaweza kufanikiwa kukunasa mwaname mzuri kama wewe sio sisi wakina kajamba nani…!” Alizungumza Maisara akiwa anaipita barabara ya nne kwa mwendo wa kawaida sana na alifanya hivyo ili kuhakikisha haharakishi, kwanza mahali alipokuwa akielekea hapakuwa mbali na pia alishavutiwa tayari na maongezi na mteja wake huyo ambaye hata yeye moyoni mwake alikiri kuwa alikuwa ni kijana mzuri mwenye kujua namna ya kuvaa pia anayejitambua kama mwanaume wa kisasa.
“Ni dhambi na unamkosea Mungu Maisara.” Maisara alishtuka na kumtazama mteja wake. Mshtuko huo ulitokana na kuitwa jina lake moja kwa moja na huyo mteja ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana naye.
“Mbona umeshtuka sana au kwa kuwa nimeliita jina lako kwa ufasaha? Au nimekosea namna ya kulitamka?” Akauliza Alan akigoma kabisa kulitoa tabasamu usoni mwake.
ITAENDELEA
Simulizi : Mikono Ya Jasusi
Sehemu Ya Tatu (3)
“Sikuwahi kukupakia kwenye gari yangu na ni mara ya kwanza mimi na wewe kuonana, lazima nishangae kwa namna ambavyo jina langu unalijua lote hadi irabu zake.” Alizungumza Maisara akiwa kwenye sura ya mshangao bado. Alan alicheka kiasi kidogo kisha akatazama mbele baada ya kuiona gari ikikunja kuingia barabara ya nane akatazama kwenye kioo cha pembeni kuona kama bado kuko shwari alipojihakikishia usalama akamtazama tena dereva wake.
“Nililisikia jina lako wakati ukiwa unabishana na yule kijana aliyekuacha punde wakati naingia hivyo likanivutia sana jina lako na kupenda hata kutumia usafiri wako.” Alijibu kwa utulivu mkubwa sana. Maisara alikosa neno la kuongeza akajikuta yuko kimya. Bado utulivu wa mitaa mingi ya jiji la Tanga ulikuwa mkubwa sana hata barabara zake zilikuwa tulivu zenye magari machache yanayokatiza kwa awamu tofauti. Muda mfupi baadaye Maisara alikuwa akiliweka gari lake kwenye maegesho ya magari ya Hoteli ya Maua Inn kisha akamgeukia mteja wake na kumwambia kuwa walishafika kwenye Hoteli husika. Alan alitazama mandhari ya hapo yalikuwa tulivu sana huku magari ya kuhesabika yakiwa yameegeshwa maegeshoni hapo. Alitoa waleti yake na kuichana kisha akatoa kiasi cha pesa kinachotakiwa na kumkabidhi dereva teksi huyo waliyotokea kuzoeana kwa muda mfupi sana. Pesa ile aliiambatanisha na kadi yake ya biashara ambayo ilimtambulisha kama mfanya biashara kwenye kampuni moja bianfsi inayojihusisha na ununuzi na uuzaji wa madini ya Almasi huko mjini Shinyanga. Aliufungua mlango na kushusha mguu wake chini hata hivyo hakufanikiwa kuteremka mara baada ya kushikwa begani na Maisara. Akageuka kwa ghafula akamtazama.
“Kila kitu kinajionesha kwenye kadi yako ya biashara hata hivyo ningependa unitamkie jina lako kwa kinywa chako mwenyewe ningefurahi zaidi.” Alizungumza Maisara kwa sauti ya mahaba akiwa ameweka tabasamu tamu usoni mwake. Alan alitabasamu kisha akatamka:
“Jina langu ni Jabir Azakia.”
“Asante nimefurahi sana Jabir kukutana na wewe maana ni abiria wa pekee sana mchangamfu na mtanashati hakika nimevutiwa nawe.”
“Nashukuru pia kwa huduma yako mrembo nadhani ninaweza kupokea simu siku ya kesho kwa ajili ya mazungumzo zaidi na kupata chakula cha pamoja kama itawezekana.” Akachombeza Alan au Jabir.
ITAENDELEA
Mikono ya Jasusi Sehemu ya Tatu
Also, read other stories from SIMULIZI;