CHOMBEZO

Ep 02: Kitunguu Saumu

SIMULIZI Kitunguu Saumu
Kitunguu Saumu Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA: CHANDE ABDALLAH 

********************************************************************************

Chombezo: Kitunguu Saumu

Sehemu ya Pili (2)

KITUNGUU SAUMU 12

“mmm hapana Friday, labda kwa sababu kichwa kinaniuma tangu jana lakini mimi ni mcheshi na utanizoea tu,” alisema Naima akijisahau kuwa jana alisema tumbo linamuuma, lakini siku hiyo akasema kichwa kinamuuma.

“enhee, Friday, hivi tunasafiri lini na nini kinafuatia tukishafika huko?” alijikaza Naima kuuliza swali hilo maana lilimkereketa mno ingawa alijishtukia asije kuharibu ikiwa ataambiwa kuwa mbona alishamwambiaga.

“aaar, tutasafiri kesho kutwa maana leo jioni naenda kuchukua passport na kugonga visa. Tukifika kule ndiyo tutapokelewa na Mzungu na kuelekezwa kazi yetu hasahasa,”alisema Friday.

“Hivi anaitwa nani vile huyo Mzungu?” aliuliza kiujanja Naima.

“Anaitwa Madam Alexandrina,” alijbu Friday, Naima akashusha pumzi maana alifahamu pengine ni libabu la kizungu, kumbe ni mwana mama afadhali. Lakini kwanini ni mwana mama badala ya mwanaume! Hilo ni tatizo na ilimtisha pia.

Nafsi yake ikamsigina kutaka kujua hiyo kazi itakuwa kazi gani, lakini akajishuku asithubutu kuuliza maana alijua lazima Friday alishawahi kumwambia Adellah awali ndiyo maana wakakubaliana, hivyo yeye kuulizia itakuwa ni kumfanya Friday amshtukie.

“aaar kwahiyo, hivi vipimo tutarudishiwa lini?” aliuliza Naima.

“leo tu jioni, na hivi vipimo ndiyo stepu muhimu sana, tukifeli hapa itakuwa tumekosa dili lote,”

“kufeli kivipi?” aliuliza Naima kwa wasiwasi tena.

“magonjwa yote yanatibika lakini tukikutwa na homa ya ini na Ukimwi ndiyo basi tena. uzuri mimi nilishapima kabla huko nyumbani, hapa narudia tu, vipi wewe ulishapimaga ukimwi hivi karibuni?” aliuliza Friday, Loh! Naima akatetema maana kipimo cha ukimwi alikuwa akikikimbia kama mama mkwe kwa kuwa alijua majanga yake huko alipotokaga.

“ndiyo mimi mwenyewe sina, lakini nikiwa na Ukimwi ndiyo inakuwaje?” alijipa moyo Naima.

“duh kama ikitokea mimi au wewe tuna ukimwi tunarudi tu nyumbani na kurudisha ile advansi,” aliongea Friday, Naima kijasho kikamtoka maana aliwaza kama akiwa ameukwaa Ukimwi hizo hela atazitolea wapi wakati Adellah alishamzima.

Itaendelea.

KITUNGUU SAUMU 13

Basi siku hiyo Naima akiwa chumbani akiendelea kujifua na kujikamua kwa vitendo huku kichwani akiwa na wasiwasi mno, mwenzake Friday alikuwa ametoka kwenda kufuatilia hayo masuala ya visa na passport. Hapo chumbani kwake ufunguo akawa ameuacha mlangoni na sio reception.

Naima akaona hapo ndiyo pakumjua vizuri Friday ni nani. Akafungua mlango wa chumba cha mwenzake na kuingia ndani. Moja kwa moja akazama kwenye begi la Friday.

Akachambua na kuona kuna vidaftari Fulani hivi, akavichukua na kuanza kuvisoma maana viliandikwa kwa mkono tu. Na tuvimichoro vya ngunga kabisa na vikatuni vya watu wakifanya mapenzi.

“jinsi ya kufanya katerero!” ilikuwa ni kichwa cha habari cha moja ya topic za kidaftari hizo, akasoma ikiwa imeandikwa,unamlaza mwanamke hivi chali akilalia mgongo, unampekechua kwenye kipekecho kwa dakika mbili na utaona kojo la mwagika.

Doh! Naima akafungua kurasa nyingine ikiwa imeandikwa: “jinsi ya ku* muda mrefu bila ku*,” humo akaandika teknik zake ikiwemo kuminya ndula, kung’ata ulimi, kupunguza mkazo wa kiuno, kuwaza kitu kingine, kutumia mitishamba nk.

Naima akaona yale aliyokuwa akiyasoma yeye muda wote ni ya kawaida, ila haya ya Friday ndiyo konki, lakini yote yalikuwa ni mafunzo ya kiume na si ya kike. Sasa ya kike atayapata wapi? Yenye mambo msanuko kama hayo? Aliwaza Naima masikini akichambua upande mwingine wa begi la Friday na kuona vifukofuko vidogovidogo, akafungua kimoja na kuona viungaunga, yaani kama mganga wa kienyeji vile.

Sasa viunga vingine hadi viliandikwa kwa majina, mfano Kiboko ya Paulina, Mkongo..

“Doh! huyu Friday sio wa nchi hii, ina maana hayo madawa yote kwa ajili ya kunisugua mimi au?” aliwaza Naima tumbo likimtetema kwa uoga, akavifungafunga vitu kama alivyovikuta na kurudi chumbani kwake.

Haraka akaanza sasa kumtafuta mtunzi wa ile stori ya Mr X.

“hallow kaka, kwanza asante kwa kunitumia kile kitabu cha bibi Gululi, kimenifungua akili sana, lakini nataka zaidi, sijui ni vipi lakini nahisi kama bado sijafuzu zaidi,” alisema Naima.

KITUNGUU SAUMU 14

“oooh asante, ila ukiniuliza moja kwa moja mada ipi unayotaka kuijua ndiyo itakuwa poa,” alijibu Mwandishi Chande.

“mh sasa mada zenyewe sizijui, wewe niambie tu mfano tukiwa tumemaliza zile mada za bibi Gululi, kuna kipi kinachofuata pale?”

“yapo mengi, mfano jinsi ya kufanya uke uwe taiti kwa wale waliozaa, kurudisha kiazi kilicholegea, kukufanya uwe na joto kali wakati wa kususu, kukufanya uwe na nguvu na usichoke mapema tendoni, kukufanya usikie ladha ya tendo, kumfanya mwanaume jeuri awahi kufika kabla yako, kumfanyia mwanaume masaji ya ajabu, kuondoa harufu ya jasho baya wakati wa kususu na mengine mengi sana,”

“uwiiiii mmh hivi wewe unayatoa wapi mbona hayo siyajui niunganishe basi na Bibi gululi.” Alilia Naima.

“doh! Kwa bahati mbaya bibi Gululi na mwanaye nimesikia hawapo Tanzania tena, walichukuliwa na Mary kwenda Marekani nadhani wamefungua darasa la kuwafunda Wazungu, kwa hiyo hapa mimi nimempata dada mmoja hivi wa Kiarabu ndiyo mtaalamu wa haya mambo, na tuseme ni zaidi yao maana anajua mambo ya unyago, anajua na madawa ya kiasili kabisa na matibabu mengi na zaidi amekuja na utaalamu wa kitandani kutoka Arabuni,” alisema Chande na kuzidi kumvuruga Naima.

“Aaaar…errrrr.. sasa ninampataje? Hivi anaongea Kiswahili?” aliongea harakaharaka Naima.

“Yah anaongea Kiswahili, ndiyo maana nimesema anajua mambo yote ya unyago na dawa za asili.”

“Samahani, sina muda sana naomba namba zake, tafadhali,” alilia Naima. Basi akatumiwa namba 0622336227 kwa tahadhari kwamba asibipu apige, zikamfikia. Akazipiga haraka palepale.

“hallow naitwa Naima, wewe ndiyo Kungwi wa Kiarabu?” alisema Naima.

“hahaaa ndiyo, nikusaidie nini Naima?” alijibu kwa ukarimu huyo Kungwi wa Kiarabu.

“nina matatizo dada angu, hapa nina safari kesho, kama inawezekana hata kwa njia ya simu huko niendako, nataka unifunde nijue kufanya mapenzi dada angu, nipo chini ya miguu yako, nifundishe kila kitu nisishindwe, najua kuna ada, nitalipa yote ili mradi nijue kila kitu, tafadhali nisaidie.” Alilia Naima.

Ikikubamba sema “Kungwi wa kiarabuuuuu!”

Itaendelea..

KITUNGUU SAUMU 15

“Mh Naima, kwa bahati mbaya hata sijui matatizo yako ni yapi hadi useme hujui mapenzi na unataka nikufunze kipi?” aliuliza Kungwi wa Kiarabu.

“Yote tu nifunze, Kungwi mimi hapa ninapoenda natakiwa niwe najua haya mambo haswa! sasa naogopa nikiwa sijui nitakosa kazi na nitaumbuka, tafadhali naomba unifunze hata kwa njia ya simu nikifika huko nitakuwa na kupigia,” alizidi kulia Naima wa watu.

“sawa, haina shida, uzuri mitandao imerahisisha wewe tu mimi nitakusaidia,”

“aya asante dada angu, asante sana, halafu eti wewe ni mwarabu kweli?” aliuliza Naima kuondoa shauku yake.

“ndiyo,”

“mh haya mambo umeyajuaje, mbona wanichanganya?”

“hahaaa! Naima, hata mimi kuna kipindi nilikuwa natangatanga, kila mwanaume niliyempata aliniponyoka na kwenda kwa mwanamke mwingine, nikajiuliza nakosea lipi? Ndipo nikaona nisipuuzie haya masuala ya unyago maana nilikuwa na sikia tu juujuu. Nikaanza kuchimba na kujifunza kwa bidii, kwa niliyotoka nayo huko nilikokua, niliwastaajabisha wanawake wenzangu na wanaume, hata wewe unaweza ukawa hivyo,” alisema Kungwi wa Kiarabu, Naima akapata moyo akaona anachelewa.

“Doh! Jamani dada angu, basi usiache kupokea simu yangu, naona kama vile nikikata hapa sitakupata tena, na wewe ndiyo mtu pekee ninayekutegemea,”

“usijali,nitakusaidia kwa moyo mmoja,” alijibu Kungwi wa kiarabu na kukata simu. Naima sasa mchecheto ukamjaa. Akaisevu ile namba vizuri na kishauku kikamfanya aingie whatsapp kumuona huyo mwarabu anayejua ufundi wa kitanda, dawa za asili na tiba zake, loh akaona tu picha nyingine pale kwenye profile, akazodoka.

Angalau sasa alipata kanafasi, akapitiwa na usingizi mzito maana hakulala kwa raha siku mbili mfululizo. Alishtuliwa baadaye na Friday aliyefika na kumgongea akiwa na daktari Yule wa jana yake.

Naima akafungua mlango na kuwakaribisha kwenye chumba chake.

“Ok, sasa hapa nina majibu ya kila mmoja wenu, niyatoe hapahaa wote msikie au kila mmoja kivyake?” aliuliza Daktari akiwa anahangaika kuchambua makaratasi kwenye begi lake.

“hapahapa kwa wote,” aliwahi kuongea Friday, Naima nusura alie.

KITUNGUU SAUMU 16

“Mr Friday, HIV, negative; Blood Pressure, Normal; UTI, nil; Malaria, nil; Hepatitis, nil; kwa kifupi huna tatizo isipokuwa una minyoo, nimekuletea dawa hapa za kutumia,” alisema Dokta akimkabidhi Friday pakiti.

Kimbembe sasa kikawa kwa Naima. Akakaguliwa na kwa bahati nzuri hakuwa na Ukimwi, wala Homa ya Ini ila alikutwa na UTI, na zaidi fangasi wa ukeni, “Candidiasis”.

Loh! ni aibu msichana kama yeye kukutwa na migonjwa hiyo inayokaa kwenye kipekecheo, lakini uzuri palepale akapewa na dawa za kutumia ikiwemo Cipro, na vijidonge Fulani hivi vya kutumbukiza ndani ya uke.

Basi wakaagana na daktari na hapo sasa Friday akatoka nje na kuongea kiingereza na mzungu wake. Akarudi na kumwambia Naima: “Okey Adellah kwanza afadhali hauna ukimwi, kila kitu tayari safari ni alfajiri kesho, upo tayari?”

“ndiyo nipo tayari,” alijibu Naima kikakamavu.

“ninakushauri hizo dawa za kunywa bora unywe ukiwa umefika kule, zisije zikasababishia matatizo kwenye ndege,” aliongea pointi Friday. Basi naye akarudi chumbani kwake, huku ndani Naima sasa akapiga magoti kumshukuru Mungu asiamini kama amevuka salama vipimo vyake na muda siyo mrefu atavuka mawingu akiikanyaga nchi ya Beyonce. Eti kuanzia kesho kutwa atakuwa anavuta hewa wanayovuta wao.

Ilikuwa ni jambo la kumshukuru Mungu mno, naye sasa hakutaka hata kutoka nje ya hoteli wala kupuyanga huko nje, maana alihofia asije akagongwa na gari bure akafa bila kuiona Marekani.

Alichofanya wakati huo, akajaribu kupiga simu ya Adellah kwa namba yake ya voda maana hiyo namba Adellah haijui, yote eti kisa ni ile milioni nne yake ilimuuma mno. Simu iliita na kupokelewa.

“Hallow!” ilikuwa sauti ya Adellah.

“Jamani Adellah ulivyonifanyia sio vizuri we wa kunidhurumu mimi?” alisema Naima.

“kwani wewe nani?” Adellah aliuliza.

“doh! Adellah leo wakuniuliza mie nani! Sawa bwana, unaongea na mie Naima,” alisema Naima, mara ghafla akajisikia mwili unamsisimka alipogeuka alishangaa kumuona Friday akiwa mlangoni akimtazama.

Loh! Ina maana amesikia kuwa yeye si Adellah bali ni Naima?!

Achecheeee!

KITUNGUU SAUMU 17

“Adellah nini!?” alihamaki Friday. Akimtazama Naima.

Naima akawa amepigwa na butwaa maneno yakigombana kutoka mdomoni, lakini mgongano huo wa maneno ulizidi kasi ya ulimi kuyatamka basi akaganda tu kama bozo.

“wewe si Adellah ni Naima?” alizidi kupigilia msumari Friday, Naima wa watu chozi likamtoka akiona vyote alivyovikosea usingizi ndani ya siku mbili za nyuma vikitoweka kwa sekunde chache tu mbele ya macho yake.

Friday naye kiherehere tu, kuingia chumbani kwa mwanamke bila kugonga hodi, japokuwa sababu yake ilikuwa nzuri tu maana alikuja na passport za Adellah ili ampatie, ndiyo amegundua sasa hayo maning’ining’i na alitaka uhakika.

“Mi…mimi ni Adellah, hapa nilikuwa naongea na Adellah mwinginewe,…aah anaitwa Naima huyo siyo mimi walaa!” alibabaika Naima midomo ilikuwa mizito balaa.

“Dah, nilihisi tu wewe demu siyo tangu mwanzo, dah umeniharibia kishenzi dah!” alilalamika Friday wakati huo akachukua simu yake na kuanza kupiga kwa Adellah orijino.

“Friday, nisamehe, unafanya nini na simu jamani.” Alilia Naima.

“nampigia Adellah mwenyewe, niache!” alifoka Friday huku akiitia simu yake Laudispika.

“namba unayoipigia haipatikani kwa sasa, tafadhali jaribu tena baadaye,” ilisikika sauti ya mashine.

Friday akapiga tena namba ya Adellah, ikasikika hivyohivyo tena. inawezekana kabisa Adellah alipogundua saa ile aliongea na Naima, akaamua kuzima simu yake kabisa na pengine kutupa laini yake kabisa ili asipatikane tena kwa kuogopa kudaiwa ile milioni nne. Loh! angejua kama fedha alizoziiba amejiibia mwenyewe, sijui angefanyaje!

Wakati huo sasa Friday, akawa anazungukazunguka mle chumbani kwa Naima akitukana na kulaani kila hatua aliyoifanya bila kuhakikisha. Naima akaomba tu samahani lakini wazo jipya likamjia tena likichagizwa na kutopatikana kwa Adellah simuni.

“Friday, sikiliza hakijaharibika kitu, fanya tu haujajua kama mimi ni Naima bali ni Adellah, kuna ubaya gani?” aliongea Naima. Friday aliyekasirika akataka kurudi na kofi amzabue huyo mshenzi wa kike aliyeongea upumbavu, lakini mkono wake akaurudishia hewani maana ubongo wake ulipata nafasi ya kuchanganua kauli ya Naima na kuona ina mantiki.

KITUNGUU SAUMU 18

“mh, tatizo Adellah anajua mambo ya unyago, wewe unaujua?” aliuliza Friday swali gumu na muhimu mno.

Naima akaona hana haja ya kuficha chochote maana kimeshabumbuluka, lakini alimsoma Friday na kugundua kuwa Friday naye anaogopa Mzungu wake akijua kama amechanganya watu tena katika hatua hiyo ya mwisho, hivyo alijua chochote atakachosema, Friday hataweza kurudi nyuma kumtafuta Adellah orijino maana kuanza tena kumtafutia viza ilikuwa ni kazi nyingine ambayo ingeifanya tiketi ya ndege ieksipaye na kuzua gharama nyingine tena.

Hivyo hapo ni lazima atamsaidia tu.

“kiukweli sijui mambo ya unyago,” alisema Naima. Friday safari hii akapiga ukutani kwa hasira.

“Naima utaniharibia, sasa kwanini ulijifanya Adellah we mjinga!”

“sikia, Friday, naomba unipe nafasi nitajifunza haraka mno, hapa nilipo sikulala siku mbili nzima najifunza, halafu nimepata mtu atakuwa ananifundisha kwa simu ni mtaalamu mno,” alilia Naima.

“acha ujinga Naima!” alisema Friday.

“hapana, ni kweli nipo siriaz, wewe mwenyewe utashangaa nitakavyojua, ngoja nimpigie Kungwi wangu, umsikie,” alisema Naima, Friday akageuka pembeni akiona ni upuuzi, akifikiria njia mpya ya kuachana na huyo Naima.

“Hallow kungwi wangu, samahani,” alianza kuongea Naima, akimminya Friday amsikilize.

“bila samahani,” alijibu Kungwi wa Kiarabu.

“ nilitaka kukusalimia lakini nilitaka kukukumbusha kuwa usisahau kunisaidia tatizo langu, mpenzi,”

“usijali, Naima tatizo litaisha tu,”

“wewe, mwambie unaumwa fangasi, acha kueleza vitu ambavyo havisaidiki!” aliropoka Friday, akiwa amechukia kwelikweli.

“aah kungwi samahani, baadaye..” alisema Naima akitaka kukata simu akichukia Friday kuongea ujinga.

“subiri kwanza! Una fangasi?” aliuliza huyo Kungwi.

“ndiyo lakini nimeshapatiwa dawa, usijali,” aliongea Naima.

“oohoo, pole sana, nilijua hauna dawa, ningekutumia dawa Fulani hivi ya kienyeji, ungepona mengi, aya bye!” alisema Kungwi wa kiarabu na kukata simu.

Naima akaduwaa kwa kauli ile.

“We unaibiwa, kungwi mwenyewe ana sauti ya kitoto hivyo! Mjini hapa,” aliongea Friday.

“ni wa kiarabu, si unajua wana sauti nyembamba,” alisema Naima, Friday akashangaa

“we subiri, ni wakiarabu? Siyo Ilham huyo? Hebu namba yake!?” aliuliza Friday akitetemekea kama sijui nini.

Itaendelea..

KITUNGUU SAUMU 19

“Mh mimi sijui jina lake, ila najua ni kungwi wa kiarabu,” alisema Naima akimshangaa Friday aliyekuwa akihangaika na simu yake.

“namba yake inaishia na 27? Halotel?” aliuliza Friday. Naima akaparangana na simu yake kuhakiki asemacho Friday cha kushangaza ilikuwa vilevile, akamuitikia kwa kichwa akihofia nini kinachoendelea kati ya Friday na Kungwi wake.

Friday akampigia Kungwi. Simu ikaita na kupokelewa.

“Asalaam Aleykum, Ilham!” alisema Friday salamu ikaitikiwa huko.

“Ilham,mbona haukuwa unapatikana hewani? Nini tatizo? Nimekutafuta mno, mimi Friday hapa.” alisema harakaharaka Friday.

“..aar vipi? Umerudi kwenye kazi yako au?”

“..ah sasa nilipona kale katatizo ka mwanzo, lakini nilipata tatizo jingine ndio nikakutafuta sana. Yaani nashukuru nimekupata dah!” alisema Friday akasimama na kutoka nje, nadhani alitaka faragha kuongea tatizo lake huko na kungwi, lakini kwa mazungumzo yalivyoenda; kidogo nafsi ya Naima ikamtulia akajua somo yake oyeeee.

Baada ya muda kidogo, Friday akaingia kwa Naima akionekana angalau ana furaha kidogo.

“sikia, huyu mdada sijui ulimjuaje lakini siyo mtu wa kawaida, uzuri ameniambia anaweza kukusaidia, kwa njia ya simu hivyohivyo, lakini nimemuomba aje kwanza na wewe unatakiwa ujitume mno.” alisema Friday.

“sawa mimi sitakuangusha,” alisema mtoto wa Kiarusha Naima.

“sikia sasa, mwanzoni tu sikujua kama ulikuwa unaongea na huyu Ilham, nimemwambia aje na dawa zake kabla hatujaondoka kesho alfajiri, nimetaka aje akuone uone advataizi yake,”

“sawa,” aliitikia Naima akistaajabu kungwi si ni wakufundisha wanawake tu, huyo Friday naye vipi? Alijuliza na kuficha shauku yake.

Lakini sasa aliona kwa kuwa Friday alijua kama yeye siyo Adellah hakuwa na haja ya kuficha maswali yake ya hatma ya safari yao huko Alabama akamuuliza Friday na kumtaka amjibu kinaga ubaga.

“huko tunaenda kwenye chuo Fulani binafsi cha mafunzo ya masuala ya mapenzi, kinachoendeshwa na huyo mzungu ambaye ni Profesa wa Sexiology, yaani mtaalamu wa elimu ya mapenzi kwa ujumla.”

“sisi kazi yetu ni kuwaonesha hao wazungu, mapenzi yetu ya kiafrika yanavyofanywa kwa vitendo na nadharia na kuwafunza,”alisema Friday.

KITUNGUU SAUMU 20

“we Friday!” alishtuka Naima.

“ndiyo hivyo, we unashangaa nini? pesa yote hiyo tunayolipwa unashangaa kuvua nguo na kufanya kwa vitendo mbele ya wazungu?”

“hapana sishangai hiko, mie mbona nipo tayari. Nashangaa unavyoniambia wazungu wanalipa hela yote hiyo ili sisi tuwafunde, si ndiyo unachomaanisha?”

“ndiyo.”

“sasa si mapenzi yamezaliwa kwao na kwetu wameyaleta wao kwa ndege, sasa sisi tunawafundisha nini kwa mfano?” aliuliza Naima.

“hahaa, mimi mwenyewe nilijaribu kuuliza, lakini Mzungu akanifafanulia kuwa mambo mengi ya asili bado yamebakia Afrika na yalianzia Afrika, huko nchi za ulaya, watu wengi siku hizi wamevutiwa na asili za Afrika kwa kila kitu sanasana haya mambo ya mapenzi, na wapo ladhi kabisa kujifunza kwa gharama kubwa, hivyo sisi ndiyo tutakuwa walimu wao, hapo hawategemei watuone tunakula denda, wala kujifanya tulalamika kiingereza, wanataka kiafrika zaidi, na tuwaelezee kila kitu kinavyofanyika, darasa limejaa huko nasikia wazungu kibao wapo tena wengine hawajui hata kiyoni kinakaaga sehemu gani kwa mwanamke na uzungu wao;” alisema Friday.

“doh! Sasa mie kizungu nitajulia wapi?” alilia Naima akiona kikwazo kila mara.

“hapana kutakuwa na watafsiri watakaoelezea, cha msingi ndiyo hivyo tuwe na mada za kutosha ili wazungu watushangae, tukiharibu tunajiharibia wenyewe tu, ndiyo maana nilimtaka Adellah,” alilalamika Friday.

“Friday, sikia nitaweza tu, kungwi si anakuja!” alisema Naima akijipa moyo.

“ndiyo,” alijibu Friday. Kidogo simu yake ikaita, akapokea.

“oh hapo reception?” aliuliza Friday.

“vipi kafika!” aliuliza Naima wakati Friday akiondoka kwa haraka.

Huko ndani kwake Naima akajiweka sawa.

Baada ya dakika chache mlango wa kwa Naima ukafunguliwa akitangulia Friday na nyuma yake akaingia mdada mwenye hijabu akiacha sura yake tu, Loh! Ni muarabu kweli.

Mkononi akiwa na hendbeg yake. Nadhani humo kulisheheni vidawa na kichwani kwake kulijaa matirio.loh!

Unamtaka kungwi akutembelee na kihendbeg chake kama Naima? Mcheki kama hujasevu namba zake pole loh!

“Karibu, asante sana kwa kuja dada angu,” alisema Naima akimkaribisha kungwi kiti kilichokuwa pembeni ya kitanda.

“Aisee Ilham kusema kweli bila ya Naima, nisingepata nafasi ya kuonana na wewe leo hii, maana tulikuwa tukiongea tu kwenye simu, karibu sana,” alisema Friday naye akiketi sambamba na Naima kitandani pale wote wakimtazama Ilham aliyekuwa akitabasamu tu.

“Enhee, Friday dawa yako hii hapa kabla sijasahau,” alisema Ilham akifungua kibegi chake na kumpatia Friday, lakini humo ndani akatoa kikaratasi cha aluminiamu kilichofungaswa akampa Naima.

“hiyo Naima ni dawa unaiingiza ndani na kidole, unavaa na pedi, maana itatoa uchafu wote, bacteria na fangasi na majimaji na kukufanya uwe mkavu na hata harufu hautaisikia, na pia itakufanya uwe taiti vizuri tu, nimekupa bure. Ila kwanza jaribu hizo dawa ulizopewa ukiona hazitibii weka hiyo, maana sitaki kuingiliana na watu wa hospitali, hiyo dawa unaiweka usiku na kuamka nayo asubuhi, masaa 12 tu kazi inakuwa imekamilika,” alisema Ilham, Naima akashukuru kama nini.

“Dah Ilham kiukweli kabisa tumekuita hapa kwa sababu kesho alfajiri tunaenda Marekani kufundisha wazungu kule kuhusu mapenzi ya kiafrika, lakini huyu mwenzangu hafahamu kabisa mambo yoyote na kama anayajua ni kwa kusoma tu juzi na jana, sasa naona tutatia aibu,.yaani ingekuwa ndani ya uwezo wangu ningekuchukua wewe badala yake!” alisema Friday, maneno yaliyomkera Naima, akaona doh isiwe nafasi yake ikabebwa na kungwi bure! akawa na wasiwasi.

“hapana, Friday, usiseme hivyo, uzuri haya mambo ni kujifunza tu hakuna uchawi mwingine, waafrika wengi tunachokosea tunafundisha watoto na kuishia kuwaharibu maana wanakuwa na shauku ya kujifunza kabla hawajakua, umri mzuri wa kumfundisha mtu ni kama wa Naima huyu, maana sasa anajielewa. Kwani umejifunza mambo gani?” aliuliza Ilham akitazama saa yake.

“Ni mafunzo ya bibi Gululi, nilitumiwa na Yule mwandishi Chande,” alijibu Naima.

“Ooh, yale ni msingi wa yote tena bora kanirahisishia, mimi nitaanzia hapo kwenda mbele, maana bila yake huko mbele kugumu,” alisema Ilham, Naima akashangaa huyo Ilham alijuaje ya Bibi Gululi!

KITUNGUU SAUMU 22

“Naima ninaweza kukutazama?” alisema Kungwi.

“sawa tu,” aliitikia Naima asijue maana ya kutazamwa huko ndiyo kupi.

“simama tu,” alisema Ilham basi Naima akasimama, Kungwi akaanza kumtazama Naima akimzunguka akimuangalia kuanzia kiuno, miguu, shepu, tumbo, shingo, macho, nywele nakadharika.

Kisha Ilham akatoa kidayari chake na kuandika andika.

“umeishazaa?” aliuliza Ilham. Swali lililombabaisha Naima.

“ndiyo,” alijibu kwa kujikaza kwelikweli, Friday kule alipokaa akaonesha kuchukia, Ilham akaandikaandika na kumtaka Friday awapishe mara moja. Friday akaondoka.

“Naima umeshawahi kufika kileleni wakati unafanya mapenzi?” aliuliza Ilham

“mh hapana, sikumbuki, sijui nina matatizo gani.” Alijibu Naima.

“wanaume wanasemaje kuhusu wewe, ni mnato au bwawa?” loh! Naima akaona haya, akatazama kama Friday ameondoka kweli na kuona kweli hayupo, sasa akameza mate na kujibu: “hapana sijui wao wananionaje wakiingiza na nihii zao!” alijibu Naima, lakini Ilham kwa utaalamu wake akajua tu hapo kuna tatizo, akaandikaandika.

“Nioneshe unavyokata kiuno,kama unacheza mziki,” Alisema Ilham, Naima akaanza kukata lakini mkatiko wake ulikuwa wa tumboni. Ilham akaandikaandika jambo.

“swali la mwisho, una miaka mingapi?”

“ishirini na sita,” alijibu Naima. Ilham akaandika na hayo na kumtazama Naima akitabasamu.

“sikia Naima, kuna vitu niliviandaa nikupe uondoke navyo huko uendako ili kama tutawasiliana nitakuwa nakupa maelekezo yote ukiwa navyo hukohuko,” alisema Ilham akitoa kifurushi kingine, kutoka kwenye hendbeg yake. Naima akavichukua na kuviweka pembeni.

“Naima, ufundi wangu wa kufundisha upo katika misingi minne, la kwanza ni mapishi, la pili ni urembo, la tatu ni mapenzi na la nne ni tiba; naamini ukiyapitia hayo yote unakuwa mwanamke kamili na amini usiamini yote hayo yameunganika na yanategemeana. Sasa mafunzo yangu mimi ni siri kati ya mfundwaji na mfundaji, na huko nimesikia mnaenda kufundisha wazungu na wazungu ni wezi wa tiba na asili za watu, je nitaaminije kama nikikufundisha utajiri huu utaenda kwenye mikono salama?” aliuliza Ilham akiwa siriaz kweli. Naima akaanza kubabaika maana hakutegemea swali hilo.

Itaendelea..

ITAENDELEA

Kitunguu Saumu Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment