Heka Heka Sehemu ya Pili
IMEANDIKWA NA: JAPHET NYANG’ORO SUDI
*********************************************************************************
Simulizi: Heka Heka
Kwa hivyo kuna wasichana waliokuwa wakiingia na wasichana waliokuwa wakija kuchukuliwa na wanunuzi ambao mwisho wa siku wangewasafirisha nje ya ncho.
Pamoja na kupewa huduma bora za afya, malazi na chakula lakini hakuna aliyekuwa akijua hatima ya maisha yake na hivyo kufanya kuwa na hali ya huzuni sana katika himaya hivyo. Kwa msichana kama Regina ambaye alilelewa kimaadili katika utoto wake, mambo hayo alikuwa akiyafananisha na sehemu ambayo mama yake alikuwa akimwambia kuwa kuna sehemu inaitwa kuzimu.
“Mwanangu ukiwa mtenda mabaya utaenda kuzimu, sehemu hiyo imejaa mateso makubwa” Alisikika mama Regina akimwasa mwanae mara kwa mara. Maneno haya yalikuwa yakimwingia sana Regina ambaye alipokuwa anacheza na watoto wa rika lake, ilikuwa ni kawaida kumsikia akisema “Mie sipigani nisije kwenda kuzimu”. Maneno kama hayo yalikuwa ni dalili tu kuwa mama yake alikuwa ameanza kufanikiwa kumfanya mwanawe aishi maisha ya maadili.
Hali ilikuja dhihirika pale Regina alipokuwa akiongezeka kimo. Nidhamu na uchaji wake ulimvutia kila aliyemwoa na kukaa na mtoto huyo. Lakini mtazamo wa Regina ulianza kubadilika mara baada ya vifo vya ghafula vya mama na baba yake, ambao walikufa kwa wakati mmoja kwa njia ya ajali. Kwa vile wazazi wake hao hawakuwa na ndugu wengine hapo kijijini, Regina alichukuliwa kulelewa na mama mmoja ambaye alionekana kuwa na uwezo kijijini hapo. Regina aliendelea kuwa katika maadili, lakini vifo vya wazazi wake vilikuwa vikimpa mawazo sana. Uzuri wa msichana huyu ulikuja kunogesha hali ya maadili aliyokuwa nayo.
Taratibu Regina akawa kama ua linalochanua katikati ya nyuki wengi, japo kuwa si wote watengeneza asali. Harakati za ndani na nje dhidi yake zikawa zinaongezeka kila kukicha. Mama mlezi akawa anajitahidi kumwelimisha Regina. Lakini mama huyu alikuwa tofauti na mama mzazi ambaye mafundisho yake na maelekezo yalikuwa na msingi katika mungu. Mama mlezi alikuwa akipenda kutumia vitisho na mafumbo ambayo hata hivyo Regina kwa umri wake akawa havielewi.
Si vijana wa mtaani na shuleni tu ambao ndiyo walikuwa wamechanganywa na uzuri wa Regina, bali hata baba mlezi. Baba huyu mlezi alianza kuzidisha zawadi na sifa kwa Regina. Alijifanya kuwa karibu naye, kuwa rafiki, hasa baada ya kugundua kuwa Regina alikuwa akimwogopa sana mama yake mlezi. Baba huyo akatumia mwanya huo kujifanya rafiki. Kwa mbinu hizo pamoja na nyingine nyingi hatimaye baba huyo aliuharibu usichana wa Regina. Alipofika kidato cha pili mama mlezi aligundua kilichokuwa kikiendelea kati ya Regina na baba yake mlezi, hivyo akaamua kumfukuza nyumbani. Maisha ya Regina yakazidi kwenda gizani.
Alianza kuhisi wenda ndiyo yuko kuzimu ambako mama yake alikuwa akimwambia. Maisha yake yaliamia sokoni kariakoo ambako alianza kuwa anafanya kibarua cha kuwasaidia wakinamama wauza nyanya kupanga nyanya pembezoni mwa soko hilo. Mshahara wake ikawa ni chakula cha mchana na usiku. Hakuna aliyemjali kwa mavazi wala mahitaji mengine aliyokuwa nayo kama msichana. Lakini pamoja na yote haya uzuri wa Regina bado ulikuwa unaonekana.
Vijana wengi wabeba mizigo sokoni hapo walikuwa wakirusha ndoano zao, lakini msimamo wa Regina uliwafanya wabaki wanakula kwa macho tu.
Safari yake ya kuja kwenye jengo hili la mzee Harken Kalm, iliwadia miaka kadhaa baadaye. Siku yenyewe alikuwa katika shughuli zake sokoni hapo, pale baba mmoja nadhifu alipokuja sehemu aliyokuwa amepanga mafungu yake ya nyanya. Baada ya kununua nyanya baba huyo hakusita kumsifia Regina kuwa ni mzuri na kumwuliza jina lake. Sifa haikuwa jambo geni kwa Regina, na siku zote hakuwa anaona tashishwi kutaja jina lake pale alipoulizwa. Huo ukawa mwanzo wa baba huyo kuja nunu nyanya kwa Regina.
Taratibu baba huyo akaaanza kuwa anakuja na vijizawadi kama nguo, viatu na mafuta, kumpa Regina. Regina alivipokea kwa hadhali kubwa. Mwaka ulipita huyo baba akifanya hivyo, huku akimwita Regina kama mwanae. Regina alijikuta taratibu akianza kumwamini baba huyo.
Ikatokea wakati Regina aliugua, yule baba alipokuja na kuulizia akaambiwa kuwa Regina anaumwa na kuwa amelala chini ya meza moja sokoni hapo. Baba huyo aliomba aonyeshwe alipokuwa Regina, alipofika alimwomba Regina akubali ili ampeleke hospitali. Kwa kuzingatia yote aliyokuwa amefanyiwa kwa mwaka mzima na baba huyo ambaye hakuonyesha nia au kiu ya kumtamani kimapenzi kama wafanyavyo wengine, Regina akajikuta amekubali kwenda.
Kweli kituo cha kwanza baada ya kutoka sokoni hapo na Regina, baba huyo alimpeleka Hospitali. Baada ya kupimwa na kupewa dawa, alimwomba Regina waende naye kwake. Uamuzi huo ulikuwa mgumu sana kwa Regina hasa ukizingatia yale ambayo yameshawahi kumkuta huko nyuma. Baada ya mvutano wa muda mrefu hatimaye Regina alikubali kwenda na baba huyo, ambaye ni Bob Sepeto. Hivyo Regina akajikuta amefika kwenye himaya ya Harken Kalm.
Kila mfanyakazi aliyemwona Regina katika jumba hili alitaka awe wake. Jambo moja lilimwokoa Regina ni kuwa, mzee Harken Kalm alikuwa amewaondolea nguvu za kiume sehemu kubwa ya wafanyakazi wake. Hii ilijumuisha walinzi, wapishi na watu wa usafi. Hivyo Regina akawa salama, japo baadae Bob Sepeto alimchukua na kufanya mke wake wa pambo tu, kwani Bob naye alikuwa amehasiwa.
Huyu ndiye Regina ambaye amekuwa na bahati ya kutoka mara kwa mara ndani ya jumba hili kwa kivuli cha kuwa mke wa Bob Sepeto.
Katika maisha yake alikuwa hajawahi kuvutiwa na mwanaume yeyote yule mpaka pale alipokutana na sura ya mpelelezi Jacob Matata pale kwenye ukumbi wa hoteli ya Miami. Hakumbuki ni nini kilimvutia kwa haraka toka kwa Jacob, lakini anachokumbuka ni kuwa mara macho yao yalipokutana tu kulikuwa na mvutano uliomfanya kwa mara ya kwanza akubali kupeleka macho yake chini mbele ya macho ya mwanaume. Alipomwangalia Jacob mara ya pili na kukutana na tabasamu lake, hapo akahisi mwili wote ukimsisimka na kujikuta ameachia tabasamu ambalo hakumbuki kama amewahi kulitoa tangu amezaliwa.
Ni hapo ndipo alipojikuta anavuka miiko ya kutotembea, wala kucheza muziki na mtu yeyote tofauti na watu wa kundi la Bob Sepeto. Jacob alipokuja na kumwomba wawe pamoja na baadaye wacheze, Regina alijua ni kiasi gani ilikuwa hatari, lakini kuna nguvu fulani ambayo alishindwa kuizuia juu ya kijana huyo. Hapo ndipo alipojikuta amemsababishia kijana wa watu kipigo na yeye mwenye kutoruhusiwa tena kutoka ndani ya jumba hili.
Aliweza kuona huruma, upendo wa kweli na udadisi viliyokuwa ndani ya macho ya Jacob. Haya yalimfanya amwamini na kuona kana kwamba anaweza kuwa na funguo za matatizo yaliyokuwa yakimkabili.
“Dokta mbona waonekana una mawazo tofauti na kawaida yako” Regina aliuliza kwa upole alipokuwa ameingia sehemu ambayo wafanyakazi wa mzee Harken Kalm hutumia kwa kujipatia chakula. Regina aliamua kumwuliza Dokta Eve, baada ya kuona tangu ameletwa hapo siku mbili zilizopita hakuwa katika hali ya kawaida.“Hayakuhusu bibie, kwani hata nikikuambia hutaweza kunisaidia” Eve alisema kwa sauti ya chini lakini iliyooyesha dhahiri hasira aliyokuwa nayo. Jibu hilo lilimfanya Regina atabasamu na kujua kuwa kuna mambo yalikuwa yamempata Dokta Eve.
“Sawa Dokta waweza ona kuwa siwezi kukusaidia lakini wawili si sawa na mmoja” Regina alijaribu tena kwa sauti ya upole zaidi. Hapo Eve aligeuza kichwa na kumwangalia Regina ambaye alikuwa tayari ameshamshika mabegani kwa upendo.
“ Nashukuru kwa kujali kwako, lakini sitakuwa tayari kukuambia tatizo langu” Eve alisema huku akiwa anafuta machozi.
“Si mbaya kama umeona kuwa ni vema ukifanya hivyo, lakini nadhani mimi na wewe tuko katika hali moja na isingekuwa vibaya kama tukishirikishana na kushauriana katika matatizo tuliyonayo katika kambi hii na..” kauli ya Regina ilikatishwa na ishara ya Dk. Eve iliyomtaka kunyamaza haraka. Regina alipogeuka, alimwona Bob Sepeto akiwa anakuja pale walipokuwa wamekaa. Alipofika aliwasabahi na kumvuta Regina ambapo waliongea maneno machache na kisha akaondoka na kuwaacha wasichana hao wawili wakiendele na maongezi yao. Kiumri Eve alikuwa mkubwa kuliko Regina.
Tangu siku hiyo walijikuta wamekuwa marafiki wakubwa sana. Hakuna la Regina ambalo Eve hakulijua na kadhalika siri za Eve, Regina alizijua zote japo urafiki wao waliamua kuufanya kuwa wa siri.
Jambo moja hakuna aliyejua na kuwa tayari kumwambia mwenzie, nalo ni juu ya uhusiano wao kila mmoja na mpelelezi Jacob Matata. Hakuna aliyekuwa tayari kusimulia matukio yaliyomkuta akiwa na Jacob Matata. Kila mmoja alikuwa akimwaza Jacob kwa mtazamo tofauti. Regina alimchukulia Jacob kama mvulana pekee aliyotokea kumpenda lakini hakuwa na uwezo wa kumwona tena wala kuwasiliana nae. Kadhalika Eve alikuwa na mawazo kama hayo.
Eve hakuwa anajua kuwa Regina ndiye msichana ambaye Jacob alikuwa akimwongelea kuwa amechukuliwa na watu wasiojulikana. Kadhalika Regina hakujua kuwa Eve ndiyo msichana aliyemwokoa Jacob alipokuwa amepigwa kule Miami hoteli wakati wakicheza muziki pamoja.
Siku moja wakati wakiwa wanapata chakula cha mchana katika moja ya sehemu za kulia chakula za jumba hili, Eve na Regina walikuwa na maongezi ambayo yalionekana kuvuka mpaka siku hiyo.
“Mdogo wangu Regina, hivi ni kitu gani ambacho kwa sasa unakihitaji kuliko vyote? Eve aliuliza kwa sauti ya kawaida kama kawaida yao wanapokuwa wakiongea. Walifanya hivi ili kuzuia wasisikiwe na walinzi wa jumba hili ambao walikuwa wengi na wenye silaha kali. Kabla ya kujibu swali aliloulizwa, Regina aliyafumba macho yake na kuyafunika kwa viganja viwili vya mikono yake. Ukweli ni kuwa swali hili lilikuwa limegusa sana hisia za Regina.
“ Eve, msichana ni ku..” alisita kidogo na kuangalia kushoto na kulia, kisha akaendelea.
“msichana ni kupenda na kupendwa na kisha kuwa na familia ni jambo ambalo nina kiu nalo sana kwa wakati kama huu, japo kutokea kwake nakuona kama ndoto tu” Regina alisema huku akijifumbata.
“Kwani inamaana hujawahi kupenda Regina? Eve alizidi kudadisi.
“Mmmh, Eve nawe umeamu kweli leo” Alisema Regina akionyesha aibu kidogo.
“Unajua Regina haya ni mambo ambayo yanatukabiri kwa sasa na inabidi tuyaongelee japo hatujui hatima yetu” Alisema Eve huku akikisogeza kiti chake jirani zaidi na alipokuwa amekaa Regina.
“Eve, nimewahi kupenda, tena si siku nyingi sana zimepita tangu pale nilipokutana na mtu ambaye aliuteka moyo wangu kwa ghafula. Ila nashi……” Regina alishindwa kuendelea na badala yake akaanza kulia. Kwa vile Eve alikuwa ameshajisogeza karibu na pale alipokuwa Regina, ilibidi amkumbatie na kuanza kumbembeleza ili anyamaze.
“Nyamaza mdogo wangu mpenzi, mbona wataka kunitia machungu zaidi. Lengo langu halikuwa kukuumiza bali tufarijiane na kutafuta namna ya kusaidiana” Eve alisema huku akijaribu kushindana na kasi ya machozi yaliyokuwa yakitoka machoni kwa Regina. Baada ya juhudi za kitambo kidogo hatimaye Regina alinyamaza
“Eve, kama wiki moja iliyopita nilikutana na kijana ambaye kwa mara ya kwanza alinifanya nijisikie na nijue kupenda. Kweli nilimpenda ghafula na bado yuko ndani ya moyo wangu. Lakini la kusikitisha ni jinsi alivyofanyiwa kijana huyo kwa kule kuwa karibu nami” Alipofika hapo Regina alinyamaza tena na kuangaza huko na huko kana kwamba mtu aliyekuwa akiangalia kama kuna mtu aliyekuwa akifuatilia mazungumzo yao.
“Kwani alifanywa nini” Eve alihoji baada yakuonekana kuingiwa na habari hii ya Regina.
“Alipigwa vibaya sana, akaanguka chini kama hakufa basi. Jambo hilo liliniuma sana. Tangu hapo sina raha, sijui ni namna gani nitakutana na kijana yule niliyempenda ghafula naye kuonekana kunipenda” Hapo Regina alionekana kufuta machozi tena
Baada ya kusikia kisa hicho cha Regina, Eve naye alimsimulia juu ya pendo alilo nalo juu ya kijana mmoja aliyemwokota kwenye ukumbi wa Miami Hoteli akiwa amezimia baada ya kuwa amepigwa na kundi la akina Bob Sepeto. Alisimulia mengi kuhusu kijana huyo ambaye yeye alimtaja kama Nico Badala ya Jacob Matata.
“Umesema ulimwokota kwenye ukumbi wa Miami Hoteli, ilikuwa lini hiyo? Regina alitia shaka na kuuliza
“ Ndiyo, na ilikuwa siku ya jumamosi wiki ile iliyopita. Nilipomwudumia na kupona tukawa tunatembeleana, tangu hapo nikajikuta nimempenda sana kijana huyo” Eve alieleza
“Ulipomwuliza alisema ni kwa nini walimpiga? Regina aliuliza huku tayari akiwa ameshaanza kuhisi kuwa wenda mtu huyo ni Jacob Matata mvulana ambaye amekuwa akiwa akimfikiria kila dakika inayopita.
“Anasema alikuwa anacheza muziki na msichana mmoja aliyekutana naye ukumbini hapo, lakini sababu hasa ya wao kumpiga hakuwa anaijua…” Eve alipofika hapo ilibidi akatize maelezo yake pale alipomwona Regina akiwa anasimama na kunyoosha mikono juu.
“Kwani vipi Regina mbona umefurahi hivyo ghafula? Eve alihoji kufuatia furaha aliyoionyesha Regina ghafula.
“Nimegundua kuwa unayemzungumzia ndiye kijana ambaye nilikuwa namwongelea na mimi, namshukuru Mungu kusikia kuwa kijana huyo yu mzima” Tayari Regina alishabaini kuwa anayeongelewa na Eve ni Jacob Matata. “Umesema unayo namba yake ya simu? Regina alihoji kwa furaha.
“Ndiyo ila kama ujuavyo kuwa nimenyang’anywa simu yangu na humu ndani ni wachache sana wenye simu, nao ni wale walio karibu sana na mzee Harken Kalm. Hivyo namba hizi haziwezi kutusaidia lolote” Eve alisema huku akiwa anafungua pochi yake na kuanza kupekenyua ndani. Mkono ulipotoka ndani ya pochi hiyo ulikuwa umeshikilia kijikaratasi kidogo.
“Hizi hapa ndiyo namba zake za simu, japo sijui tutatumia njia gani kuhakikisha tunawasiliana na Nico” Alisema Eve huku akimkabidhi Regina zile namba. Furaha aliyokuwa nayo Regina ni kana kwamba alikuwa amempata Jacob mwenyewe. Waliachana huku kila mmoja akiwa na mawazo yake. Regina aliapa kuwa kwa vyovyote vile angetumia kila njia kuhakikisha kuwa anawasiliana na kumpata. Alijua fika kuwa yeye kuonana na Jacob ingekuwa ngumu, lakini alihitaji kuwa anasikia sauti yake tu.
Eve kwa upande wake alishangaa kutambua kuwa msichana aliyekuwa anamnyima usingizi Jacob huko nje alikuwa ndiyo huyu Regina waliyekuwa naye ndani ya jumba hili. Kutokana na upendo aliokuwa nao kwa Jacob, Eve akajikuta anaapa kumpata Jacob na kuhakikisha hawi na Regina japo hakujua ni namna gani angeweza kutekeleza hilo. Taratibu ile hali ya urafiki wa kweli aliyokuwa nayo juu ya Regina ikaanza kutoweka. Na ndipo ile hali ya kutaka kuyaharibu zaidi maisha ya Regina.
Msonyo alioutoa Bob wakati Jacob anaongea na Regina kwenye simu asubuhi hiyo ulilifikia sikio la mpelelezi Jacob Matata upande wa pili. Jacob alitambua kuwa adui yake alikuwa amefanya namna ambayo angeweza kumsikia wakati wakiongea na Regina, kwa hiyo tayari aliukuwa ameshasikia muungurumo wa injini ya boti waliyokuwa wanaitumia. Kule kusonya kulitafsiriwa na Jacob kuwa mtu aliyekuwa amemsimamia Regina wakati akiongea, alikuwa amegundua kuwa alikuwa Jacob alikuwa anamdanganya Regina kuwa alikuwa akienda kambini hapo kwa usafiri wa gari. Hii ilifanya akili ya Jacob kuchukua uamuzi wa kutoendelea na safari kama alivyokuwa amedhamilia, kwani alishajua kuwa adui zake muda si mrefu wangetanda majini na kuanza kumtafuta.
“Unasikia mzee, naomba ukatie nanga kwenye miti ile pale na uniache hapo wewe urudi” Jacob alisema huku akifungua kibegi chake na kukagua kitu fula kabla ya kukifunga tena. Mzee yule aliyejitambulisha kwa Jacob kwa jina la Maduka hakuwa na la kupinga. “Kwa nini umeamua kushukia hapo ili hali kambi tuliyokuwa tunaiendea haiko mbali sana toka hapa? Aliuliza mzee huyo huku akiwa anazungusha usukani wa boti hiyo kuelekea kule alikoomba Jacob waende.
“Kwa hiyo tumekubaliana kuwa utaenda na kuja nichukua jioni sawa? Badala ya kujibu swali la mzee Maduka, Jacob aiuliza swali huku wakiwa sasa wanakaribia ufukwe. “Hiyo itakuwa kazi sana, unaonaje kama utaniongezea hela ili nikae hapa nakusubiri mpaka jioni? Mzee maduka alitoa pendekezo. Jacob hakujibu haraka kana kwamba alikuwa hajasikia. Alikuwa akifanya upembuzi yakinifu juu ya hilo. Sawa, lakini sidhani kama tutaenda wote huko kambini, wewe itabidi ubaki hapa.
Tayari walikuwa wameshafika ufukweni, mzee Maduka alitoa nanga na kuitupa majini. Wote walitelemka. “ Kwa vile utakuwa hapa muda mrefu na bahari huwa iabdilika wakati wowote, naona tuivute boti hadi nchi kavu na kisha tuifunike majani kwa usalama wako” Jacob alitoa pendekezo hilo wakati wote wakiwa nchi kavu tayari. Mzee Maduka alijua Jacob anamwonea huruma, lakini Jacob alikuwa ameshahisi kuwa jamaa wangeanza kuzungukia pwani hiyo kwa msako. Hivyo ilitakiwa waifiche boti yao kwa maji ili isionekane kwa urahisi. Kazi hiyo ilifanyika kwa haraka sana mpaka mzee yule akawa anashangaa.
Walipomaliza tu mara walisikia mlio wa boti zikija kwa kasi. “Nenda jifiche kwenye kichaka kile pale, usitoke kwa namna yoyote tafadhali!!! Jacob aliamuru huku na yeye akienda kujificha kwenye kichaka kingine. Alichukua kibegi chake na kutoa darubini ndogo nakuanza kuangali boti hizo zilizokuwa zimeenea eneo lote sasa. Darubini hii ilikuwa ndogo lakini ilikuwa ni ya kisasa na yenye uwezo mkubwa sana, pia ilikuwa na uwezo wa kupiga picha pale mtumiaji alipohitaji kutunza kumbukumbu ya matukio anayoyaona kwa mbali sana.
Jacob alijatihidi kadiri alivyoweza kuiga picha za wengi kati ya jamaa hao waliokuwa ndani ya boti hizo ambazo zilikuwa ni aina ya zile ziendazo kwa kasi. Jinsi walivyokuwa wameificha boti yao na namna walivyokuwa wamejificha, ilitosha kabisa kuwafanya wasionekane na watu hawa ambao dhahili walikuwa tayari kuua. Walikuwa na silaha nzito nzito na za kisasa.
Hali hiyo iliendelea kwa masaa kadhaampaka pale hali ilipokuwa shwari kabisa. “Sasa wewe baki hapa ila uwe katika hali ya kujificha mpaka hapo nitakaporudi” Jacob alisema huku akiwa anweka darubini yake ndani ya kibegi chake. Alienda pembeni kidogo, hapo alitoa bastola mbili, moja aliifutika hapa na nyingine akaifutika kule. Akatoa visu kadhaa na kuvifutika huku na huko na dhana kadhaa, darubini na vifaa vingine aliviacha ndani ya kibegi chake hicho. Yote haya aliyafanya sehemu ambayo alijua kuwa Mzee Maduka alikuwa hamwoni. Bila kuaga tena, Jacob huyo akatokomea vichakani.
Sehemu aliyokuwa amekusudia kwenda ni kambi ya Koboyo, hii ilikuwa ni kambi ya uvuvi. Kwa maelekezo aliyokuwa amepewa na Regina juu ya sehemu waliyokuwa wanashikiliwa, Jacob aliamini kuwa kambi hii ingekuwa jirani sana sehemu waliyokuwa wakina Regina. Hivyo alikuwa ameamua kwenda hapo ili akapeleleze machache toka kwa wavuvi kambini hapo kuhusiana na sehemu ambayo Jacob aliamini kuwa ilikuwa ya hatari.
Baada ya kumtafuta Jacob kwa muda mrefu bila kumwona wa kuona dalili ya boti eneo lote, Bob Sepeto hakuamini kuwa kweli Jacob hakuwepo maeneo hayo. Aliwaamuru walinzi wengine kurudi kambini huku akituma wapelelezi waende kambi ya Koboyo ili kuangalia kama Jacob alikuwa hapo au angeenda hapo. Baadhi ya walinzi aliwaacha waendelee kuzunguka kando kando ya bahari kuanzia hiyo bagamoyo mpaka mjini.
Wapelelezi waliokuwa wametumwa na Bob kwenda kambi ya Koboyo walikuwa ni wale askari wake watiifu na aliowaamini katika swala zima la kutumia miili na silaha katika mapambano. Walikuwa wamebeba silaha nyepesi nyepesi tu na hawakuwa katika sare yoyote. Walikuwa wakizunguka kila kona ya kambi hiyo, huku wakijifanya wavuvi au wachuuzi wa kawaida wa samaki.
Mzee huyu na yeye alikuwa alikuwa amechangamka huku akionekana kuanza kukolewa na pombe. Lakini kwa wenyeji wa eneo hilo siku hiyo walikuwa wakimshangaa kwani hakuwa amelewa katika kiwango walichokuwa wamezoea kumwona akilewa.
Mzee huyo hakuwa ni yule waliyekuwa wakimjua siku zote bali alikuwa ni Jacob Matata ambaye tayari alikuwa ameshajibadirisha sura na kuvaa ya mzee huyu. Alipokuwa ameshafika kambini hapo na kugundua kuwa kulikuwa na walinzi kibao ambao wengi wao walikuwa na sura yake,Jacob alienda nyuma ya choo fulani na kujificha mpaka pale alipokuwa amekuja mzee mmoja. Mzee huyo aliingia chooni ili ajisaidie. Hapo ndipo Jacob Matata akatumia fursa hiyo kumuhadaa na kumuua bila kufanya makelele yoyote.
Kwa kutumia darubini yake Jacob alimpiga picha mzee huyo sehemu ya usoni, kisha huyo akatokomea vichakani tena huku mwili wa marehemu akiutumbukiza chooni. Vichakani huko alitumia dakika kadhaa kabla ya kutoka tayari akiwa ameshajibadirisha sura na kuwa sawa na yule mzee marehemu. Alifanya hivyo kwa kutumia vifaa vilivyokuwa kwenye kile kibegi chake kidogo.
Alikaa kambini hapo kwa muda mrefu huku akiwa anauliza hili na lile kwa wenyeji, bila kushukiwa na yeyote. Mara kwa mara alikuwa akigongana na walinzi wa waliokuwa wametumwa na Bob Sepeto, hawakumtambua japo yeye aliwatambua na mara nyingine kufanikiwa kuchukua picha za wengi wao kwa kutumia darubini yake ndogo iliyokuwa na uwezo huo.
Ilipofika jioni tayari alikuwa ameshakamilisha sehemu kubwa ya taarifa alizokuwa akizihitaji. Hakuona sababu ya kuondoka mapema kiasi hicho. Hivyo akaendelea kuwepo hapo ili kuruhusu kigiza kuingia zaidi. Ilipofika saa mbili, Mpelelezi Jacob Matata akaona huo ni wakati muafaka wa yeye kuondoka. Lakini aliona si busara kwake kuondoka hivi hivi.
“Mwanangu naomba ukanisaidie kuvuta mtumbwi wangu, maana nahitaji kwenda kutega nyavu zangu” Jacob alimwambia mmoja wa watu aliokuwa na hakika kuwa alikuwa ametumwa kuja hapo ili kumtafuta. “Na nyie wazee kwa usumbufu, haya twende haraka kwani unaenda kutegea upande gani? Aliuliza jamaa huyo huku akionyesha ishara ya kuwa tayari kwenda kumsaidia mtu aliyedhani kuwa ni mzee kumbe ndiye Jacob Matata ambaye wote walikuwa wakimtafuta.
Jacob aliongozana na jamaa huyo huku akiwa anajiandaa kwa shambulio la ghafula na kali. Alijua kuwa ilitakiwa atoe pigo ambalo halitampa jamaa hata nafasi ya kupiga kelele. Walikuwa tayari wameshafika ufukweni kwenye mtumbwi.
“Haya shika huko na….” Kauli ya jamaa ilikatizwa na pigo kali la kareti toka kwa Jacob. Jamaa hakuwa ametegemea pigo hilo, na kwa kuwa lilipigwa sawasawa toka kwa mtu aliyejua vizuri lilimnyamazisha jamaa huyo milele. Haraka haraka Jacob alimbeba jamaa na kumwingiza ndani ya mtumbwi huo. Humo alimvua nguo zote na kutoa kisu chake. Kwa kutumia kisu hicho, Jacob alimchora jamaa maneno fulani. Baada ya hapo alitoka ndani ya mtumbwi huo na kuanza safari ya kuelekea kule alikomwacha yule mtu aliyekuwa amemkodisha. Saa tatu na nusu ilimkuta Jacob na jamaa yake tayari wakiwa wameshafika kwenye ufukwe ulioko jirani na eneo la kivukoni Dar es salaam.
“Bob nilikwambia kuwa Jacob Matata si mtu wa kumchukulia mzaha hata kidogo. On sasa inaonyesha ameshafanya upelelezi wa kutosha hapa kwenye kambi aliyokuwepo bila nyie kujua. Siju watu wako walikuwa wanafanya nini. Sasa ni lazima muongeze ulinzi kwenye ukanda huu, nami nitaongea na marafiki zangu walioko kwenye vyombo vya usalama ili wanisaidie kulinda upande huu” Mzee Harken Kalm aliongea kwa hasira huku ngozi yake ikiwa imebadilika na kuwa nyekundu utadhani nini. Muda huu mzee huyu anaongea na Bob Sepeto mkuu wa walinzi wake, ilikuwa ni saa saba usiku. Hali ndani ya kambi hiyo ilikuwa shwari kabisa. Lakini si kwa upande wa walinzi na wana usalama wote wa kambi hiyo. Kwani dakika chache zilikuwa zimepita tangu pale yule mtu aliyekuwa ameuawa na Jacob na maiti yake kuwekwa kwenye mtumbwi ufukweni mwa bahari ilikuwa imeonekana. Hali hii iliwafanya watu hao wahae katika kutafuta wakidhani Jacob bado alikuwa maeneo hayo. Kilichowatia kiwewe zaidi ni ile salamu waliyoikuta imeandikwa kwenye mwili wa marehemu. Maandishi hayo yalisomeka hivi; Jacob anasema siku zenu zinahesabika’Kwa kumbukumbu alizokuwa nazo mzee Harken Kalm, hakuwahi kutishiwa na yeyote na wala hakuwa anapenda hiyo itokee. Leo ilikuwa ni mara ya kwaza, tena la kutia aibu ni kutoka kwa mwafrika mwenye umri mdogo Jacob Matata.
Amri ya kutafutwa Jacob popote pale ilitolewa, huku yeyote ambaye angafanikiwa kumwua ilihaidiwa kuwa angezawadiwa kiasi kikubwa cha pesa na mzee Harken Kalm.
Dakika arobaini na tano zilipokatika ilikuwa kama wiki moja ka Kalm, yalipokatika masaa mawili ilikuwa kama mwaka. Tayari alikuwa ameshakunywa mvinyo kiasi kikubwa. Muda ulikatika lakini pamoja na mzee Harken Kalm, kusambaza vijana wake kila kona ya jiji hakuna aliyefanikiwa kumtia Jacob Matata machoni. Jitihada zilifanyika na maharamia hawa ili kujua yalipo makazi ya Jacob na nyendo zake. Wakuu mbalimbali wa usalama walitumika ili kujaribu kumuhujumu, lakini haikujulikana Jacob alikuwa akiishi wapi.
Kwake yeye maisha yalikuwa yakiendeshwa kama kawaida tena bila ugumu wowote. Alikuwa akiishi kwenye nyumba iliyokuwa ikilindwa masaa ishirini na nne na vijana wauaji wa mzee Harken Kalm. Walikuwa wameshajua nyumbani kwake na kwa hivyo muda wote walikuwa wakipalinda wakitegemea kumwona Jacob akija hapo.
Ni kweli Jacob alikuwa akilala ndani ya nyumba hiyo siku zote kwani ndiye aliyewapokea siku ya kwanza walipokuja. Walipokuja nyumbani hapo siku ya kwanza, vijana hao katili walimkuta mzee mmoja aliyekuwa amevaa miwani mweusi. Pasipo kujua kuwa ndiye Jacob Matata, walimwuliza yeye ni nani katika jumba hilo. Kwa vile Jacob alitegemea kuwa jamaa hao wangefika hapo alikuwa ameshawaandalia jibu la kuwalidhisha na kuwafanya wasione umuhimu wake na kumwacha kama mzee aliyekuwa amepewa hifadhi katika nyumba hiyo.
Jamaa hao hawakuwa wakiacha nyumba hiyo ibaki bila kuwa na mtu wa kuhakikisha kuwa Jacob asingeingia bila wao kuwa na taarifa. Mara zote alipouliza kama Jacob alikuwa ametokea, Bob Sepeto alipata jibu la kuwa “ ….hapana, isipokuwa yule mzee mwenye miwani mweusi ndiye ameingia kulala…” Hivyo alikuwa akiwadhihaki mara zote ambazo walikuwa wakikutana naye bila wao kumtambua.
Baada ya muda fulani Jaob akawa amefanikiwa kujenga urafiki nammoja wa vijana wa mzee Harken Kalm. Kijana huyu alijulikana kama Ikwagama Zulu, mwenye asili ya Afrika ya kusini. Jacob alifuatilia na kugundua kuwa Zulu na wenzie walikuwa wakipenda kula kwenye mgahawa wa Jeff Inc fast food. Hivyo Jacob akioonekana katika sura yake ya kizee akawa anapenda kwenda pale. Mara kwa mara gari la akina Zulu na wenzake ilipokuwa ikiegesha aliifuata na kujifanya kuomba msaada. Zulu akawa ni mwenye huruma kuliko wenzake kwa kuwa anapenda kuongea na mzee huyu ombaomba. Kwa tabia hii wakajikuta siku, wiki wakawa wameshajenga urafiki wa mwombaji na mtoa msaada, huku wakiwa wamepeana majina ya babu na mjukuu.
Jacob alipoona ameshazoea sauti na matendo kadhaa muhimu ya Zulu, siku moja alijifanya kumtaka chemba ili ampe habari muhimu. Walitoka ndani ya mgahawa na kuelekea upande wa nyuma kwenye kichohoro. Ghafula Zulu alishangaa kumwona mzee huyu akiwa kabadilika na kuanza kumpa mapigo makali ambayo hayakuchelewa kuuchukua uhai wake. Baada ya kumwua zulu, Jacob alimvuta mpaka sehemu fulani ambapo alitoa kizibo cha tanki moja la kuhifadhi taka za chooni toka nyumba fulani ya jirani. Hapo aliuvuta mwili wa Zulu na kuutumbukiza humo. Alifunika tanki hilo na kuingia kwenye kona moja ambapo alitoa kikoba chake na kuvaa sura fulani aliyokuwa ameshaiandaa usiku uliopita. Alibadilisha ngu na kuvaa zile alizokuwa amemvua Zulu kabla hajamtumbukiza kwenye tanki. Hapo akawa ameshabadilika toka sura yam zee ombaomba na kuwa Zulu mlinzi wa mzee Harken Kalm. Alifungua kkoba alichokuwa nacho, humo hakuhitaji chochote kikubwa zaidi ya vikasha kadhaa vilivyokuwa na ngozi za sura za bandia. Alivifutika vitu hivyo sehemu aliyijua yeye katika mwili wake. Kisha akachukua silaha aliyzokuwa amempora Zulu na vitambulisho vyake. Huyo akarudi pale alipokuwa amewaacha wenzie na Zulu. Mambo yote hayo yallifanywa na Jacob Matata kwa kasi na umakini mkubwa na hivyo kumchukua dakika chache tu.
Kwa Jacob aliona ametumia dakika chache, lakini haikuwa hivyo kwa wafanyakazi wenzie na Zulu. Kwa masharti ya kazi yao, mnapokuwa sehemu kwa kazi maalumu hairuhusiwi kuwa mbali na wenzio bila sababu maalumu. Hii ilifanyika hivyo ili kuondoa uwezekano wa kuhujumiana au mtu kutekwa pasipo wenzake kujua. Hivyo kiongozi wao hapo tayari alikuwa amewasiliana na Bob Sepeto mkuu wao na kumtaarifu juu ya lile lililokuwa limefanywa na Zulu siku hiyo.
Hivyo wakati Jacob alipokuwa anafika ili kujiunga tena na walinzi hao akiwa katika sura ya Zulu, ni wakati huo huo ambao watu wanne toka kwa Bob Sepeto walikuwa wameshawasili eneo hilo kumchukua Zulu. Kitendo cha Zulu kutokuwa na nidhamu na kutoweka bila taarifa katika wakati mgumu kama huu kilimchukiza sana Bob Sepeto. Kwa kuzingatia sifa za Jacob na utaalamu aliokuwa ameusikia hakumwamini tena Zulu. Hivyo alikuwa ameshatuma watu wake ambao ni maalum kwa kuua wafanyakazi wasio waaminifu. Hivyo wakati Jacob anafika kwa lengo la kwenda kuwahadaa wale watu na kujifanya kuwa ndiye Zulu, tayari wauaji toka kwa Bob Sepeto walikuwa wakimngojea tayari kwa kumwua.
Jacob alipoingia kwenye mgahawa alielekea pale walipokuwa wamekaa wenzie na Zulu, alipoanaglia hakuona mtu. Kwa haraka sana alizungusha macho hapa na pale bila kuona yeyote kati ya wale jamaa. Ndiyo hakuona yeyote kati ya wale, lakini aliona kitu. Aliona macho ambayo kwa utaalamu aliokuwa nao aligundua kuwa yalikuwa na kila dalili ya hatari. Mbaya zaidi ni pale Jacob alipogundua kuwa macho hayo yalikuwa yakimfuatilia yeye kwa usiri mkubwa.
Ili kuhakikisha kuwa watu hao walikuwa mahali hapo kwa sababu yake, Jacob aligeuka na kujifanya kama vile anaelekea nje. Alitembea kwa hadhali kubwa huku mkono wake akiwa anaupeleka tayari kwa kutumia bastola yake.
Hawa ni nani tena, na wamejuaje kuwa ni mimi? Jacob alijiuliza huku akiwa tayari ameshafika malngoni. Hakuwa na hakika kama watu hao walikuwa wanamtafuta kama Jacob au kama Zulu ambaye sura yake ilionyesha hivyo. Alikuwa ameshatoka nje na kutaka kuvuka barabara, mara akasikia vishindo vya mtu aliyeonekana alikuwa akija kwa haraka. Alipotaka kugeuka akaona gari moja ikija kwa kasi upande ule aliokuwa amesimama. Hapo akajua kuna jambo na mambo yameiva.
Alikuwa na uwezo wa kuruka mapema lakini hakufanya hivyo kwa sababu moja kubwa, alitaka kuwafundisha hao jamaa. Gari ilikuja kwa kasi pale alipokuwa amesimama. Nusu sekunde baadaye eneo hilo lilindima kwa mlio wa breki ya gari hilo huku watu wakipiga kelele za hofu.
Wakati gari inafika miguuni Jacob alishahisi kuwa kulikuwa na mtu nyuma yake. Kwa wepesi wa ajabu alijipindua na kuruka hewani kwa kurudi nyuma. Wakati anatua tayari alikuwa uapnde wa nyuma wa yule mtu aliyekuwa ameimama nyuma yake, alimsukumia kwenye taili za gari ambalo taili zake zililalamika kwa kitendo cha dereva kujaribu kumkwepa mwenzie. Wao walitegemea Jacob ndiye angekuwa akisubiri taili imsage, lakini dereva alichanganyikiwa kuona kuwa mtu waliyetegemea kummaliza alikuwa ameruka kwa staili ambayo alikuwa hajawahi kuona na wakati huohuo akamsukumia jamaa yao kwenye mataili.
“Mmalizeni!!! Dereva wa gari lililokusudia kumgonga Jacob alipiga kelele. Wakati ukulele huo ukiishia hewani, risasi zilimiminika kuelekea pale alipokuwa amesimama Jacob. Kwa mshangao zilikuta hewa, kwani Jacob alikuwa amewahi na kujiviringisha chini. Bado akiwa anaviringika chini Jacob aliachilia risasi mfululizo ambazo ziliwamaliza jamaa wote.
Hii ilikuwa ni simu ya tatu kwa siku hii ya leo. Ilionekana kuwa mpigaji wa simu hii alikuwa ni mmoja. Muda ambao simu hiyo ilikuwa ikipigwa na ujumbe uliokuwa ndani ya simu hii vilimfanya Bi Anita aamini kuwa mpigaji wa simu hii kama hakuwa ni shetani mwenyewe basi bila shaka alikuwa ni mtu mwenye mawazo ya shetani. Alifikiri ni jinsi gani mtu huyu alijiamini kiasi cha kumpigia simu mara kwa mara kiasi hicho bila kuogopa. Alijaribu kufikiri sauti hii ambayo si ngeni sana kwake ilikuwa ni ya nani au aliwahi kuisikia wapi. Hakuweza kupata jibu lolote la kweli. Simu iliyokuwa ikitumika ilikuwa ni ile ya mezani, Bi. Anita hakuwa na uwezo wa kuona namba za mpigaji.
Baada ya kufikiri sana ndipo akaamua kumtuma moja kati ya vijana wake ili aende shirika la simu kuulizia mmiliki wa namba iliyokuwa imepigwa mara tatu kwenda ofisini hapo.
Muda mfupi mara baada ya Bi. Anita kumtuma mtu wake kwenda kuulizia juu ya mpigaji huyu, mara simu yake ya mezani iliita. Kabla ya kuinyanyua, Bi. Anita alichukua kifaa fulani ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kunakili maongezi ya kwenye simu. Baada ya kuipachika sehemu fulani jirani na mkonga wa kuongelea na kusikilizia Bi. Anita aliipokea simu hiyo.
“Nani unaonge? Aliuliza Bi. Anita kwa sauti ya kukereka kidogo.
“ Ni yule rafiki yako anayeomba nafasi ya kukushauri” Ulijibu upande wa pili.
“Urafiki gani unaombwa pasipo na pande mbili kujuana? Huo si urafiki bali ni mtu mmoja anayemjua mwenzie kutaka kumteka asiyemjua mwenzie” Alisema Bi. Anita.
“Nashangaa sana pale unaposoma kuwa hunijui ili hali kila leo unafikiri namna ya kupata nafasi ya kuonana na mimi. Unanifahamu ila sema hujui niko wapi japo ningependa ujue niko wapi. Nashindwa kukujulisha kuwa niko wapi kwa vile bado hatujawa na mtazamo sawa. Tukiwa marafiki unaruhusiwa kujua niko wapi.” Ilipofika hapo sauti hiyo ilisikika ikicheka kicheko cha kebehi. Kwa kushindwa kuficha chuki yake Bi. Anita alijikuta akifumba macho.
“Okay, pamoja na kuwa umekataa kusema jina lako na mahali ulipo lakini bado sikuelewi pale unaposoma kuwa nakufahamu ili hali sikufahamu, labda ungenikumbusha tuliwahi kuoana wapi. Na ni mitazamo gani tunayotofautiana? Bi. Anita aliuliza huku mtu wa upande wa pili akionekana mwenye furaha isiyo kifani. Sauti yake ilionyesha hivyo.
“Ngoja kwanza nikukumbushe uliniona wapi. Wiki mbili zilizopita saa kumi usiku ulikuja kuniona pale Benki ilipovunjwa na kuibiwa mabilioni ya Shilingi. Ni kweli kuwa hukuiona sura yangu lakini matendo yangu uliyaona. Wiki moja baadae ulikuja kuniona pale mabilioni ya Shilingi ya kampuni ya kutengeneza bia yalipoporwa, ilikuwa ni saa tisa alasiri Juzi usiku ulijkuja kuniona pale Shinyanga katika tukio ambalo nilikuwa nimeenda kuchukua madini, japo nyie masema ni kuiba. Nasema tuna tofauti za kimtazamo kwa vile mara zote ambazo umekuwa ukija kuniona na kufanikiwa kuiona sura yangu kwa njia ya matukio yangu umekuwa ukionyesha masikitiko na hasira kuu. Tofauti na mimi ambaye hata hivyo mara kwa mara nimekuwa nikiwa hatua chache sana toka pale unapokuwa umesimama. Kwani licha ya kuwepo kwenye matukio hayo kwa njia ya matendo lakini mara nyingi kiwiliwili changu huwepo kwa vile huwa na hamu ya kumwona rafiki yangu ambaye ni wewe.
Kinachonishangaza ni kuwa mara zote umekuwa ukichukia pale ninapofurahi, unalia pale ninapocheka, unajiandaa kupigana sehemu ambayo naona inafaa nijiandae kusheherekea. Unalinda sehemu ambayo ningependa iwe wazi masaa ishirini na nne. Hizo ndizo tofauti za kimtazamo zilizopo kati yangu na wewe. Lakini Nadhani wakati umefika ambapo tunatakiwa kuzika tofauti hizo, kwani tusipofanya hivyo waweza kufa kwa shinikizo la moyo. Nimetangulia kusema kuwa najua kwa sasa unatafuta namna ya kukifikia kiwiliwili changu. Ningefurahi sana kuwa mwenyeji wako kwani kwa hivi sasa nimetoka kuchukua benki statement inayoonyesha kuwa mamilioni ya pesa niliyochukua pale kampuni ya bia na benki tayari yameshaigia kwenye akaunti yangu. Pia nimepokea taarifa kuwa yale madini niliyochukua kule Shinyanga yameshapata mnunuzi.
Nasikitika kwa vile unataka niendelee kuwa maskini huku tukiwaachia wazungu watajirike. Nadhani ungeniona hapa nilipokaa ungechoka kabisa kwani watu wanaosubiri taarifa za mapato na matumizi ya pesa hizo wengine wana cheo kuliko cha kwako. Naamini unaweza kuwa mmoja wao. Unaweza kuwa unapata mamilioni ya Shilingi kwa mwezi kwa kazi ngumu ya kuwa unaweka miguu juu ya meza na kustarehe, tofauti na sasa ambapo unapokea vishilingi vichache ili hali unakesha katika kutafuta namna ya kufika mahali nilipo na kuharibu starehe yangu na wakubwa wako.
Vipi rafiki umefikia wapi katika kutafuta mpenyo wa kunifikia. Inashangaza kwa sababu badala ya kutumia muda wako kutafuta pesa, wewe unautumia katika kupanga mipango ya kuwaharibia wenzio wenye shida na pesa na wanaojua matumizi yake. Juhudi hizo ungezielekeza pengine bila shaka ungekuwa tajiri kama mimi na wale walio na mtazamo kama wangu. Oooh Samahani nimekuwa msemaji sana. Ila kumbuka kuwa unawajibu wa kufanya jambo kwa ajili ya mtukio haya usinyamaze kana kwamba huyaoni” Ilimaliza sauti hiyo kwa kicheko ambacho kilisaidiwa na vicheko vya watu wengine waliosikika kuwa walikuwa karibu sana na mwongeaji.
“ Kama ulivyosema kuwa tunatofautiana mtazamo, hivyo kwa vile wewe una maneno mengi wakati huu basi mimi sina maneno mengi ili kwamba wakati nitakapokuwa na maneno mengi wakati kichwa chako kikiwa kinaelekea kwenye kitanzi tayari kwa kunyongwa nawe hutakuwa na maneno mengi. Kwa sasa niache niendelee na kazi uayoiona kama kazi kichaa, wasalimie hao wanaovuna wasipopanda na kukusanya wasipotawanya. Waambie watalipa udhalimu wanaowafanyia watu waliowaamini na kuwapa heshima ya kuwaongoza kumbe wao wanawadhihaki” Maneno hayo Bi. Anita aliyaonge huku akiwa bado amefunika macho kutokana na uchungu. Hata hivyo maneno hayo yalipokewa kwa vicheko toka upande wa pili. Kisha Bi. Anita hakuona haja ya kuendelea kuhojiana na hao watu, hivyo akaadhimia kukata simu. Wakati anataka kuweka chini mkonga wa simu kuna neno akalisikia neno lenyewe lilikuwa ni “….Kesho Leadera Club saa tatu usiku….” Aliuweka chini mkono wa simu.
Maneno yaliyoongewa na huyu mtu anejiita kama rafiki yaliutibuwa kabisa ubongo wa Bi. Anita, akajikuta anatamani sana kupokea taarifa toka kwa kijana wake juu ya mmliki wa namba ya simu iloyokuwa ikitumiwa na mtu anayejiita ‘rafiki’.
Alitulia tuli juu ya kochi lake kubwa huku akijaribu kuyatafakari maneno yote yaloyokuwa yakisemwa na ‘rafiki’ . Alishangaa, kwani kwa uzoefu na utaalamu alionao ulionyesha kuwa mara nyingi wahalifu hutafutwa na siyo kujileta kama huyu. Ikitokea kuwa amejileta basi ujue kuwa kuna hila imefichika ndani ya moyo wake na kuwa adui huyo ni moto wa kuotea mbali.
Alifikiri ni jinsi gani wizi huu mfululizo ulivyopelekea jeshi la polisi kupakwa matope na watu mbalimbali kwa kile kilichoosemwa kuwa lilikuwa limeshindwa kuhakikisha usalama wa watu na mali zao.Hali hii ilipelekea mkuu wa jeshi la polisi na waziri wa mambo ya ndani wajiuzulu mara baada ya shutuma dhidi yao kuzidi.
Kuona hivyo Rais kwa kutumia njia ya siri kabisa aliweza kumtaarifu Bi. Anita juu ya haja yake ya kutaka ofisi fukuzi ijiingize katika kutafuta ukweli juu ya matukio haya ya wizi wa kimataifa.
Masaa machache tu mara baada ya kupokea jukumu hilo toka kwa Rais, Bi. Anita alipokea simu toka kwa mtu huyu anayejiita ‘rafiki’ . Katika simu hiyo ya kwanza ‘rafiki’ alisema alikuwa anampongeza Bi. Anita kwa kupewa jukumu hilo gumu, la siri na la kitaifa.
Baada ya Bi. Anita kutafakari kwa kina juu ya ujumbe huo toka kwa ‘rafiki’ ndipo kwa siri akamtumia taarifa Rais kumtaka kutowasiliana naye kwa njia yoyote zaidi ya wao kuonana ana kwa ana. Bi. Anita alimweleza Rais kuwa sababu kuu yeye kufanya hivyo kuwa amegundua kuwa kuna mtu anavujisha siri. Alishangaa zaidi pale alipopokea simu ya pili toka kwa ‘rafiki’. Katika simu hii ‘rafiki’ alikuwa anmpongeza Bi. Anita kwa kuwa makini na kubuni njia nzuri ya kuwasiliana na raisi. Kwanza Bi. Anita aliogopa lakini baadaye aliamua kufuatilia ili kujua juu ya mtu huyu anayejiita ‘rafiki’. Ndipo hapo akaamua kumtuma mtu kwenda shirika la posta na simu ili kujua mmiliki wa namba ya simu iliyokuwa ikitumiwa na ‘rafiki’. Wakati akisubiri taarifa toka Posta na simu ndipo alipopokea simu hii ya tatu toka kwa ‘rafiki’, safari hii rafiki akiongea kwa kirefu.
“Bosi, watu wa posta na simu wanasema namba hiyo ni ya biashara na inamilikiwa na msichana mmoja aitwaye Joyce” Alisema huyu kijana ambaye alionyesha hofu hasa mara baada ya kuiona sura ya Bi. Anita. Sura ya Bi. Anita ilionyesha wazi wazi hasira, ilikuwa ya baridi sana.
“Huyo Joyce wamesema anaishi wapi?
“wamesoma wakati anakuja kumchukua namba ya sanduku la posta na hiyo namba ya simu ya biashara alijiandikisha kama anaishi kinondoni makaburini. Kwa hiyo hawajui kama bado anaishi hapo au alishahama. Nimejaribu kuwaulizia kama wanajua sehemu yake ya biashara wakasema hilo hawajui”.
“Sawa hebu Fanya utaratibu ili uweze kupata anapoishi kama ukimpata mlete hapa pasipo yeye kujua, nafikiri nikisema hivyo unanielewa”
“ Ndiyo bosi” Alisema kijana huyo aliyeonyesha kila dalili kuwa alikuwa mtii na tayari kufanya lolote aliloambiwa na bosi wake.
Kijana huyo alipoondoka, Bi. Anita alizama tena katika mawazo juu ya mtu huyu ajiitaye ‘rafiki’. Aliwaza mengi, Hatimaye akafikia pale ‘rafiki’ aliposema kuwa yuko na watu ambao wengine ni wana vyeo kulioko yeye Bi. Anita. Alifikiri juu ya mtazamo wa viongozi wengi wa afrika pale wanapokabidhiwa madaraka na wananchi, wengi hudhani kuwa wamepewa nafasi ya kujinufaisha binafsi. Hivyo wanapoingia madarakani tu, husahau wajibu wao kwa wananchi na badala yake hutimiza wajibu kwa matumbo yao na uchu walionao.
Mawazo yake hayo yaligutuliwa baadaye na sauti ya mtu aliyekuwa akibisha mlango.
“Ingia ndani” Alisema huku akiruhusu viganja kupita juu ya uso wake kwa staili ya kufuta, bila shaka hii ni dalili ya kuhama kimawazo na kurudi ofisini. Yule kijana aliyemtuma kwa joyce binti mwenye namba za simu zilizokuwa zimetumiwa na ‘rafiki’ alikuwa amesharudi.
“Bosi, nimeenda lakini tofauti namatarajio yetu, sijamkuta Joyce tuliyekuwa tukimtaka. Badala yake nimekutana na maiti ya Joyce. Pembeni yake nilikuta karatasi hii ambayo ina namba za sanduku la posta”. Alisema huku akimkabidhi Bi. Anita hicho kijikaratasi ambacho hakikuwa na lolote zaidi ya namba za sanduku la posta. Alipofika hapo Bi. Anita alivuta pumzi ndefu kisha akasimama.
“ Sasa inabidi uwe makini zaidi, inaonyesha hawa watu wanafuatilia kila tunalolifanya na inawezekana kuna mtu wa karibu sana anayewapa taarifa juu yetu. Mchukue Mike mwende mkaangalie kwenye hilo sanduku la posta kuna nini. Ila narudia inabidi muwe makini kwani bila shaka kutakuwa na watu wanaowatazama. Pia mkiweza kumtambua yeyote anayewafuatilia itakuwa vizuri zaidi. Haya kazi njema”. Alisema Bi. Anita huku uso wake ukiwa umeelekezwa dirishani.
Jambo moja lilianza kuusumbua ubongo wa Bi. Anita, nalo si jingine ila ni lile la kujiona yuko uchi. Kwani inaonyesha adui alikuwa akijua kila kitu kuhusiana na yeye.
Dakika kumi baadaye yule kijana wake aliyekuwa ameenda posta alikuwa tayari amerudi.
“Eeh yalikwendaje? Aliuliza pale alipokuwa tayari ameshakaa.
“ Hakuna cha ziada zaidi ya karatasi hii” Alisema huku akimkabidhi Bi. Anita ile karatasi aliyoichukua posta.
Kama kawaida ya mwandishi wa karatasi hizi, hakuwa na maneno mengi, safari hii alikuwa ameandika; NAMTAKA JACOB MATATA LA SIVYO JIANDAE BADO “PIGO LA MAUTI”. RAFIKI.
“Jacob!!! Jacob anahusiana vipi na mambo haya, na kwa nini wanamtaka? Bi. Anita alijikuta akifoka huku akipiga ngumi juu ya meza.
Kwa mara ya kwanza ndipo mkuu huyu wa kitengo hiki maalumu cha usalama alikumbuka kuwa zilikuwa zimepita situ kadhaa bila kumwona wala kusikia Sauti ya Jacob Matata.
Baada ya kusoma ujumbe huo ambao bila shaka ulikuwa umetoka kwa ‘rafiki’ ambaye bila shaka alijua kuwa utamfikia, mawazo ya Bi. Anita yaliweza kuona kila dalili ya hatari iliyokuwa mbele yake. Kwa jinsi alivyolichukulia swala hili alijiona kuwa anacheza na moto. Ofisi yake ilikuwa imesheeni kila aina ya wataalamu katika fani hii ya ukachero. Lakini makachero hawa walikuwa wanatofautiana kiuwezo na ngazi, hivyo akajiona mpumbavu kwa kuwa anamtuma huyu kijana kuanza kufuatilia jambo hili. Isitoshe yeye Bi. Anita kazi yake ni kuapanga nani afanye nini wapi. Kazi yake haikuwa kufanya kazi bali kupinga nani afanye nini na kumpa mazingira na mamlaka ya kufanya hivyo. Hivyo akaona umuhimu wa kushughulikia suala hili.
“ Asante nimepata ujumbe aliotaka niupate, waweza kwenda” Alisema Bi. Anita huku akinyanyua mkonga wa simu.
Kitendo cha kusikia kuwa Jacob Matata yuko katika harakati za kuweza kuifikia himaya yake hii kilimkera sana mzee huyu. Hivyo pamoja na kuwatuma vijana wake chini ya bob Sepeto kumfuatilia Jacob Matata lakini pia aliamua kuwatumia vibaraka wake serikalini ili aweze kupata nyenendo za mpelelezi hatari Jacob Matata.
Hivyo kwa nyakati tofauti tofauti alianza kuulizia juu ya mpelelezi Jacob Matata. Hapo Edipo alipoweza kupata taarifa juu ya makazi ya Jacob Matata na kitego alichokuwa akifanyia kazi. Hapo akaamua kutumia mbinu mbalimbali ili kuweza kumpata mtu huyu hatari.
Ni katika harakati zake hizo, ndipo mzee Harken Kalm simu yake ilifika kwa Mkuu wa Jacob Matata, Bi. A nita, na kujitambulisha kwa jina la ‘rafiki’. Katika hali ya kumtisha na kumshawishi Bi. Anita atoe taarifa za Jacob Matata, ndipo akamtumia ule ujumbe kwa njia ya posta.
Saa tatu kaso robo usiku siku iliyofuata iliwakuta makachero kadhaa hatari toka ofisi fukuzi wakiwa tayari wanarandaranda maeneo ya ukumbi wa leaders club. Bi. Anita aliamua kufanya hivyo mara baada ya kuabahatisha kumsikia mtu anayejiita ‘rafiki’ akiwaambia wenzie kuwa wakutane hapo saa tatu usiku huo. Hivyo alikuwa amewatuma ili kuweza kuangali uwezekano wa kumpata huyo mtu aliyejiita ‘rafiki’.
Kwa upande wake mzee Harken Kalm au ‘rafiki’ kama alivyojitambulisha kwa Bi. Anita, alikuwa ameongea hivyo makusudi kabisa. Alijua fika kuwa kama Bi. Anita angesikia asingeacha kutuma makachero Leaders Club ili wajaribu kumkamata. Lengo lake ilikuwa ni kumwinda mpelelezi Jacob Matata.
“Mkienda hapo hakikisheni mnaangali kama Jacob atakuwa miongoni mwa makachero watakaotumwa pale leaders Club. Hivyo mkimwona mleteni akiwa hai au maiti yake” Hii ilikuwa ni sehemu ya mwisho ya maelezo ya mzee Harken Kalm kwa vijana wake chini ya uongozi wa Bob Sepeto mwenyewe.
Hivyo wakati makachero toka ofisi fukuzi wakiwa wanafanya doria maeneo hayo kwa siri, vijana toka kwa mzee Harken Kalm nao walikuwa katika msako wa kuona kama Jacob alikuwa maeneo hayo na kama alikuwepo wamkamate au kumuua. Vijana wa mzee Harken Kalm hawakuwa wakimjua kachero yeyote mwingine zaidi ya Jacob Matata ambaye walikuwa wamepewa picha zake. Lakini hii haikuwazuia kuweza kuwatambua makachero wengine waliokuwa eneo hilo. Hii ni kutokana na ujuzi waliokuwa nao juu ya makachero.
Jacob kwa upande wake alikuwa amepata taarifa za kuwa na watu wanomtaka hapo Leaders Club. Taarifa hizo alizipata kupitia kwa Bi. Anita. Bi. Anita alimtaka Jacob awepo mahali hapo ili kuona kama wangeweza kuwanasa jamaa hao. Yeye Jacob ndiye aliyekuwa wa kwanza kabisa kufika eneo hilo. Alikuwa ametafuta mahali pazuri na kuegesha gari alilokuwa amekuja nalo. Hivyo aliweza kuwaona makachero wenzake wakati wakiingia eneo hilo. Kama alivyotarajia makachero hao hawakuja na gari. Walikuja mmoja mmoja kwa miguu, aliangalia jinsi walivyokuwa wamejipanga.
Hata pindi kundi lingine la vijana wa mzee Harken Kalm linaingia Jacob aliweza kuona na kuhisi. Lakini hakuwa na papara, alijua fika kuwa alihitaji muda. Pamoja na zana nyingine za kazi mikononi mwake alikuwa ameshikilia picha kadhaa. Picha hizo ndizo zile alizokuwa amezichukua wakati ule alipokuwa ameenda kwenye kambi ya Koboyo. Hivyo kwa kutumia picha hizo aliweza kuwatambua baadhi yaowaliokuwa wakifika eneo hilo usiku huo.
Jambo moja lilimfurahisha Jacob ni kuwa watu wa pande zote mbili hakuweza kutambuana. Vijana wa mzee Harken Kalm hawakuashiria kuwajali sana makachero waliokuwa wakipishana nao, kadhalika makachero hawakuweza kujua kuwa watu waliokuwa wakipishana nao na wakati mwingine kuongea nao ndiyo walikuwa watu wabaya hasa.
Jacob Matata hakushuka toka ndani ya gari, mpaka pale ilipotimu saa sita na dakika ishirini usiku. Muda huo watu wote walikuwa wametokomea ndani ya ukumbi. Kila kundi likijaribu kuangalia uwezekano wa kumwai mwenzake. Ni wakati huo ambao Jacob aliangaza macho huko na huko bila kuona mtu. Alikusanya dhana zake na kuzipakia sehemu mbalimbali za mwili wake. Taratibu na kwa hadhali Kubwa kama mtu anayekwenda kupokea mkate wa bwana, Jacob alishuka ndani ya gari na kulifunga kabla ya kuanza kuondoka.
Safari yake iliishia kwenye gari moja waliyokuwa wamekuja nayo vijana wa mzee Harken Kalm. Hapo kwa hadhali ya ziada alizunguka mpaka upande wa nyuma wa gari. Akafungua buti ya gari hiyo ili aweke vitu vyake na kisha mwenyewe aingie. Aliweka begi lake, kisha wakati anajiweka sawa ili aingie alishitukia Sauti ikimwamuru tokea nyuma, “tulia hivyo hivyo, la sivyo utanilazimisha kutumia silaha yangu” alitii na kutulia maana aliweza kuuhisi ubaridi wa mdomo wa bastola kwenye kichwa chake.
Hiyo ilikuwa ni Sauti ya Bob Sepeto ambaye hakuwa ameingia ndani kama wengine badala yake alijibanza sehemu ili kuweza kuona hali ya hapo nje. Alikuwa macho kama paka mwenye njaa. Aliweza kumwona na kumtambua Jacob , tangu pale aliposhuka kwenye gari na kuanza kuelekea kwenye gari hii ambayo Bob Sepeto na kundi lake walikuwa wamekuja nalo.
“Najua una hamu ya kuitumia na wala haina haja ya mimi kukulazimisha” Jacob alisema hayo huku akiwa anavuta muda wa kuangalia ni namna gani angeweza kujinasua hapo.
“Nadhani unijui vizuri bwana Jacob, nimekwambia tulia hivyo ulivyo na nisingependa mahojiano na wewe” Bob alisema hayo kisha akaachilia konde zito lilotua shingoni kwa Jacob na kumfanya apepesuke. Kwa upande wake Jacob aliona kuwa hiyo ilikuwa nafasi yake ya pekee. Alijifanya kama anayetaka kuanguka kufuatia lile konde. Bob akafanya kosa jingine kwa kurudi nyuma nukta chache, kufumba na kufumbua teke la Jacob lilikuwa limetua kwenye mbavu zake, akateteleka.
Jacob akaja kwa judo kwa nia ya kummaliza Bob, akakuta Bob kisha jipanga na kuikwepa. Sasa wakawa wanatazamana damu ya Jacob tayari ikawa inachemka tayari kwa mapambano. Aliruka kama anayetaka kupaa na kuachia teke kali ambalo hata hivyo Bob aliliona na kuachia ngumi iliyompata Jacob. Kufuati umahili huu ambao Bob aliuonyesha, Jacob akajua kuwa alikuwa anapambana na mtu hatari hivyo ilimbidi kutumia ujuzi zaidi.
Alichuka hatua chache za staili ya aina yake, alipokuja geuka, tayari alikuwa ameshamkata Bob kareti nne mfululizo, bobo akaenda chini. Jacob akamfuata hapo chini na kumpa mateke matatu ya mbavu, Bob akalegea. Kwa vile Jacob alikuwa amesimama jirani mno na Bob, kufumba na kufumbua Jacob alijikuta yuko chini. Bob alifanikiwa kumchota mtama wa staili ambayo wachina wameibatiza jina la ‘shishogh’.
Jacob alipoamka hakumkuta Bob, alikuja taamaki gari aliytokuwa ameshaweka vitu vyake ikiwa anawashwa. Alisimama haraka na kutaka kukimbilia upande wa dereva. Alikuwa ameshachelewa, Bob alikuwa ameshatia gari moto na kuanza kuondoka kwa kasi.
Kuona hivyo Jacob Matata alifanya alifanya mambo matatu kwa wakati mmoja, alianza kukimbia kuelekea alipokuwa ameacha gari lake huku akiwa anakwepa risasi toka kwa Bob aliyekuwa anaondoka na gari kwa kasi huku akiachia risasi kuelekea alipokuwa Jacob.
Bob hakumwogopa Jacob, ila aliona ingemchukua muda mrefu na nguvu nyingi mpaka kumshinda Jacob. Hakuona kuwa pale ilikuwa ni mahali sahihi kwa ajili ya vita yao. Hivyo aliamua kutumia hila ili amvute Jacob Matata waende nae kwenye uwanja ambao aliamini kuwa wangeweza kuwa na nafasi nzuri ya kupambana.
Wakati gari ya Bob inatokomea gizani, tayari Jacob alikuwa ameshawasha gari na kuliondoa kwa kasi.
Milio ya mataili ya magari viliwashitua makachero wote waliokuwa ndani ya ukumbi wa leaders club. Kwa nyakati tofauti wote walito nje, lakini si wao tu walioshituliwa na milio hiyo bali hata watu wa kundi la Bob walishituka sana.
Walipotoka nje hawakuona lolote kwani wale mafahali wawili wakati huo tayari walikuwa mtaani wanafukuzana. Ni vijana wa Bob Sepeto ndiyo waliogundua tofauti, hawakuliona gari la bosi wao-Bob Sepeto.
“Bosi salama na uko wapi? Mmoja alikumbuka kumwuliza Bob kwa njia ya simu.
“Ninaelekea mchangani lodge, njooni hapo baada ya kama dakika kumi toka sasa” sauti hii ya Bob ilikuwa ya utulivu kiasi kuwa isingekuwa rahisi kwa kijana wake huyu kuamini kuwa Bob alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kutisha.
Jacob alifanikiwa kuliona gari la Bob Sepeto kwa mbali sana. Hii ilitokana na muundo wa gari hilo na kwa vile magari yalishapungua sana barabarani. Vinginevyo isingekuwa rahisi hasa kwa vile ilivyokuwa usiku.
Dakika chache baadaye, Bob sepeto ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia Mchangani Lodge. “Kuna mgeni wangu anakuja kuniulizia mwambie niko namba 15A” alisema hayo alipokuwa anapita mapokezi. Hakugeuka kumwangalia yule binti wa mapokezi wala hakusimama, alipitiliza moja kwa moja kwenda kilipokuwa chumba namba 15A.
Sekunde kadhaa baadaye mpelelezi Jacob Matata aliingia, hakwenda mapokezi kuuliza badala yake alipitiliza moja kwa moja. Alitembea taratibu kana kwamba mtu aliyekuwa na hakika na alipokuwa akienda. Jacob alifanya hivyo makusudi, maana alitegemea kuwa Bob Sepeto angekuwa katika mkao wa kumsubiri.
Huyo alitembea na kibaraza mpaka alipofika mwisho, akaingia kushoto na kukuta upenyo fulani kwa ajili ya mafundi wa hoteli hiyo. Hapo alibana na kusikiliza kwa makini, alitaka kujua kama kuna mtu alikuwa anamfuatilia. Alitulia hivyo kwa takribani dakika moja na ushee.
Bob Sepeto alikuwa chumbani ameshajiandaa kwa mpambano na mtu aliyekuwa amezisikia sifa zake nyingi. Damu yake ilikuwa inachemka tayari kwa pambano ambalo yeye aliamini kuwa lingekuwa zito. Dakika kumi na tano zilipita bila kuwepo na ishara yoyote ya Jacob kutokea. Bob alikuwa amejilaza kitandani huku akiwa ameshikiria gazeti. Ingekuwa ni mimi au wewe bila shaka yoyote tungeweza dhani kuwa alikuwa amezama katika habari zilizokuwa katika gazeti hilo, lakini haikuwa hivyo kwa Bob Sepeto. Alikuwa macho kama nini. Jacob aliyekuwa dirishani akimsanifu hasimu wake huyo naye aligundua kuwa Bob alikuwa makini sana, gazeti ilikuwa geresha tu. Baadaye Bob Sepeto alija gundua kuwa alikuwa amezidiwa kete kwa Jacob kufanikiwa kufika pale dirishani bila yeye kuwa na habari.
“Hongera, ingia ndani” Alisema Bob bila kugeuka wala kuangalia pale dirishani.
“Asante! Alisema Jacob huku sasa akiwa anafungua dirisha ili aingie ndani. Haikuwa rahisi kuamini alifikaje pale.
Jacob alipoingia na kufika ndani, Bob aliweka gazeti pembeni tayari kwa kumpokea mgeni wake huyu ambaye hata hivyo aliingia katika stahili ambayo hakuitegemea. Jacob alishatambua kuwa, Bob hakuwa mtu wa kuendewa kwa papara. Hivyo alipokanyaga sakafu ya chumba hicho alijisogeza kwenye kona moja ya chumba hicho kulipokuwa na kiti akakaa mkao egesha. Kwa jinsi chumba kilivyokuwa Bob alikuwa juu ya kitanda huku akiwa ameupa mgongo mlango. Kwa vile Bob alikuwa anatazamana na Jacob, hivyo Jacob alikuwa akitazamana na mlango pia.
Jacob alijitengeneza vizuri kwenye kiti na kuweka miguu katika mtindo wa nne. Sasa walikuwa wamekaa kama marariki waliokuwa wanaenda kwenye maongezi ya muda mrefu. Huku kila mmoja akiwa katika hadhari la hali ya juu kwa hasimu wake, Jacob alishangaa pale alipoona kitu kama chuma chembamba kinacheza kwenye kitasa cha mlango. Akawa chonjo zaidi. Bob aligundua tofauti katika macho ya Jacob, hivyo hisia mbili zikamjia kichwani. Kwanza alidhani ni danganya toto ya Jacob kumfanya ageuke na kutoa nafasi. Pili alidhani ni wale vijana wake aliowaamuru kuja hapo hotelini watakapoona amechelewa.
Sekunde chache baadaye Jacob alikuwa amerukia upande mwingine wa chumba huku mwili wa Bob ukiwa amelala pale kitandani na damu zikiwa zinatoka kisogoni kwake. Jacob aliwahi na kulenga usawa wa pale kilipokuwa kimetokeza kile chuma kilichotoa risasi iliyommaliza Bob. Jacob hakufanikiwa kummaliza. Haraka aliparamia mlango kwa lengo la kumwahi muuaji wa Bob lakini alipofika nje ya mlango hakukuta mtu zaidi ya kijikaratasi kilichokuwa chini. Kabla ya kukiokota aliangalia huku na huko, ili kuangalia kama kulikuwa na mtu alikuwa amemtega. Alikiokota kiaina na kuangalia kulikuwa na nini. NAMTAKA REGINA KWA BEI YOYOTE ILE, BANZI. Hayo ni maneno yaliyokuwa kwenye kikaratasi hicho. Kifo cha Bob na huo ujumbe viliitibua akili ya Jacob. “Hivi kuna upande mwingine tofauti na hawa unaomwitaji Regina? Alijiuliza huku akitokomea. “Banzi ni nani na anahusika vipi katika kisa hiki? Jacob akatabasamu nakuachilia pumzi “Kazi ipo” akanong’ona.
Sekunde chache baadaye Jacob alikuwa amerukia upande mwingine wa chumba huku mwili wa Bob ukiwa amelala pale kitandani na damu zikiwa zinatoka kisogoni kwake. Jacob aliwahi na kulenga usawa wa pale kilipokuwa kimetokeza kile chuma kilichotoa risasi iliyommaliza Bob. Jacob hakufanikiwa kummaliza. Haraka aliparamia mlango kwa lengo la kumwahi muuaji wa Bob lakini alipofika nje ya mlango hakukuta mtu zaidi ya kijikaratasi kilichokuwa chini. Kabla ya kukiokota aliangalia huku na huko, ili kuangalia kama kulikuwa na mtu alikuwa amemtega. Alikiokota kiaina na kuangalia kulikuwa na nini. NAMTAKA REGINA KWA BEI YOYOTE ILE, BANZI. Hayo ni maneno yaliyokuwa kwenye kikaratasi hicho. Kifo cha Bob na huo ujumbe viliitibua akili ya Jacob. “Hivi kuna upande mwingine tofauti na hawa unaomwitaji Regina? Alijiuliza huku akitokomea. “Banzi ni nani na anahusika vipi katika kisa hiki? Jacob akatabasamu nakuachilia pumzi “Kazi ipo” akanong’ona.
“Leta habari kijana, yamekwendaje? Sauti nzito iliuliza
“Kama kawaida mzee huwa sifanyi makosa, Bob Sepeto hatunae duniani! Alijibu kijana huyu kwa sauti ya kujivuna kidogo.
“Vizuri sana Banzi, sasa hebu anza kufuatilia nyendo za Jacob Matata. Hakikisha hampati Regina wala hawafikii vijana wa mzee Harken Kalm. Nakutahadhalisha, Jacob si mtu wa kumwendea ovyo” Ilimaliza sauti hiyo nzito na kukata simu. Sauti hiyo nzito ilikuwa ikitoka mdomoni mwa mwanamume mmoja wa makamo. Aliminya namba kadhaa kisha akaongea “enhe leta habari kijana, yamekwendaje? Aliuliza huku macho yakiwa yametua darini.
“Hapa nilipo niko hatua sita toka alipokaa mrembo Regina! Ulijibu upande wa pili
“Vizuri, uliwahi kabla mambo hayajaharibika? Sauti hii nzito iliuliza tena
“Kabisa, nilikuta ndiyo wana mgombania, lakini hakuna aliyefanikiwa kummpata”
“Vizuri Ponte, bila shaka utafanikiwa kumleta Regina akiwa salama. Nina hamu naye sana na ndiye atakayekuwa malkia wenu” Ilisema sauti hii nzito na kukata simu.
ITAENDELEA
Heka Heka Sehemu ya Tatu
Also, read other stories from SIMULIZI;