Nyuma ya Machozi Sehemu ya Pili
MAISHA

Ep 02: Nyuma ya Machozi

SIMULIZI Nyuma ya Machozi
Nyuma ya Machozi Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA: ALLY MBETU

*********************************************************************************

Simulizi: Nyuma ya Machozi

Sehemu ya Pili (2)

ILIPOISHIA:

“Jimmy ukiifanya kazi kwa ufanisi nitakupa laki mbili.” “Utani huo sister!”

“Sina utani kwa jambo nitakalo kuahidi.”

“Sawa, wacha nikuache uendelee na mambo mengine.”

Jimmy aliondoka na kumuacha Kilole akitengeneza nyumba kwa ajili ya sherehe ya kutengeneza ya birhtday yake. Sebule aliipamba na kupambika ikawa katika muonekana wa kupendeza.

SASA ENDELEA…


Majira ya saa mbili usiku kila kitu kilikuwa kimepangwa sehemu yake, Kinape na mpenzi wake nao walikuwepo kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa Kilole.

Ilikuwa sherehe iliyozuka kama uyoga, ule ulikuwa mpango wake maalumu wa kuhakikisha nasambalatisha penzi la Kinape na Happy pia kumrudisha mikononi mwake. Kabla ya sherehe kuanza simu ya Happy mchumba wa Kinape iliita, aliipokea na kuzunguza.

“Haloo.. eeh .. Nipo kwa Kinape… Kuna sherehe ya kuzaliwa shemeji yake…Eeeh!… Nini? Acha utani.. Mungu wangu nakuja…Aah.. lazima nije?”

“Vipi?” Kinape na Kilole waliuliza kwa pamoja baada ya kumuona Happy akitokwa na machozi huku ameshikilia mikono kichwani. “Mama,” alijibu kwa mkato.

“Mama kafanya nini?”

“Kavamiwa na majambazi walitaka kumpora gari.”

“Wamemjeruhi?”

“Wanasema hawajamjeruhi, wanaomba niendelee na sherehe lakini lazima nikamuone mama kisha nitarudi.”

“Kinape mpeleke mwenzako,” Kilole alijifanya mwema.

“Hapana dada ninyi endeleeni tu, nitarudi muda si mrefu, inaonekana tatizo siyo kubwa, nitakwenda peke yangu.” Happy aliwatoa wasi.

“Hapana mpenzi lazima nikupeleke,” Kinape alisema.

“Lakini kama umesema mama hana tatizo basi wacha nianze sherehe na Kinape ukirudi tutaungana pamoja,” Kilole alitumia nafasi ile kumbakiza Kinape.

“Kweli kabisa dada, nisiharibu utaratibu wa sherehe kwa vile ilikuwa ndiyo inaanza.” “Ila shampeni utaifungua ukirudi.”

“Hakuna tatizo.”

Kinape alimsindikiza Happy mpaka nje, baada ya kuingia kwenye gari na kuondoka alirudi ndani kuendelea na sherehe ya mtego aliyoandaliwa yeye bila kujijua. Wakati Kinape akitoka nje kumsindikiza mpenzi wake, Kilole alitumia nafasi ile kumuwekea dawa ya kulevya kwenye juisi.

Kinape aliporudi alikaa kwenye kochi na kuchukua glasi ya juisi na kunywa kidogo huku akimtupia swali Kilole kuvuta muda labda Happy atawahi kurudi. Kilole alifurahia moyoni na kuona mpango wake umekuwa rahisi tofauti na alivyopanga wa kumtumia Jimmy kumtoa Happy kwa simu ya uongo ili kitendo kifanyike kwa haraka. Lakini simu kutoka kwao kidogo imfanye apige yowe la furaha.

“Shemu, Deus anajua kama leo ni tarehe yako ya kuzaliwa?”

“Anajua na muda si mrefu nitakufanyieni bonge la surprise na mchumba wako.” “La nini tena, mbona umenirusha roho.”

“Utaliona muda si mrefu.” “Nigusie kidogo.”

“Ukijua haitakushtua, nataka uamini nakupenda shemeji yangu.”

“Mmh! Haya.”

Kinape alisema huku akichukua glasi ya juisi na kupiga funda zingine tatu na kurudisha glasi chini. Mara alianza kuhisi kichwa kizito, alijitahidi kushindana na hali iliyomtokea kila macho yalizidi kufumba. Kilole alifurahi kuona kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa.

Taratibu Kinape alijilaza kwenye kochi, kwa hatua ile Kilole aliona tayari mpango wa awali umekamilika. Alikumbuka mlango upo wazi alikwenda kuufunga, kisha alimpigia simu Jimmy.

“Haloo Jimmy.”

“Vipi Sister, nipige ile simu?” “Hapana, njoo nyumbani haraka.”

“Nipe dakika sifuri.”

Alipokata simu mlango uligongwa, alijua Jimmy amefika, alitoka hadi mlangoni na kufungua. Alishtuka kumuona Happy mbele yake, alipotaka kuingia ndani alimshika kifuani na kumrudisha nyuma.

“Vipi dada!” Happy aliuliza kwa mshangao.

“Kinape kakufuata.”

“Kanifuata vipi wakati nimemwambia narudi?” “Amesema huenda mama yako kapata matatizo makubwa.” “Jamani! Sasa kapitia wapi mbona sikumuona?”

“Kwa kweli sijui kitu, nimembembeleza akusubiri kakataa.”

“Kwa nini asinipigie simu?”

“Mmh! Siwezi kujua.” Happy aliamua kumpigia simu Kinape mbele yake, baada ya muda simu iliita ndani.

“Mbona simu yake inaita ndani?”

“Aliisahau kutokana na papara zake.”

“Sasa nikimfuata si nitapotezana naye, bora nimsubiri ndani.” “Happy, kutokana na king’ang’anizi cha mpenzi wako nimeamua kuahisha sherehe mpaka jumamosi.”

“Hata hivyo siwezi kusumbuka kumfuata, wacha tu nimsubiri,” Happy alisema huku akitaka kuingia ndani. “Happy kuwa muelewa, Kinape baada ya kuondoka nimemweleza nimeamua kuahirisha sherehe na yeye alisema hatarudi mpaka kesho. Sasa ukimsubiri itakuwaje?” “Mmh! Wacha nimuwahi,” Happy alisema huku akigeuka na kuondoka. Kilole hakuingia ndani mpaka aliposikia sauti ya gari la Happy likiondoka, wakati huo Jimmy alikuwa amefika.

“Ooh! Jimmy karibu ndani.”

“Asante,” Jimmy alijibu huku akiingia ndani. Alipofika sebuleni alishangaa kukuta kuna kitu kama sherehe, mbele kulikuwa na keki kubwa iliyoandikwa Happy Birthday Kilole na pembeni yake kulikuwa na chupa kubwa ya shampeni. Sehemu nyingine kulikiwa na vinywaji ndani ya glasi. Alipoangalia kwenye kochi alimuona Kinape ameutwanga usingizi.

“Vipi Sister naona ulikuwa na sherehe ya kuzaliwa kwako?”

“Ndiyo, lakini sicho nilichokuitia.”

Jibu lilimfanya Jimmy asiulize kitu zaidi ya kusubiri alichoitiwa.

“Ndiyo sister lete maneno?”

“Kazi niliyokuitia sasa imekamilika nataka ufuate maagizo yangu, malipo yako nilikuambia kiasi gani?”

“Laki mbili.”

“Nitakuongezea hamsini, itakuwa laki mbili na nusu.”

“Hakuna tatizo,” Jimmy alikubali bila kujua ni kazi gani. Baada ya kuhakikisha mlango ameufunga vizuri alimuomba Jimmy amsaidie kumuingiza ndani Kinape.

Walisaidizana kumwingiza chumbani, Kilole alimpeleka katika chumba chao cha kulala kisha walimlaza kitandani. Baada ya kumlaza walitoka mpaka sebuleni kupanga mipango yao. “Sasa sikiliza kazi niliyokuitia ni hii.”

“Kazi gani?”

“Nataka unipige picha kwenye tukio lote nitakalokuwa nalifanya kisha utaenda kunisafishia na kuniletea picha zote, sawa?” “Picha za tukio gani?”

“Nitakalo lifanya muda mfupi usilishangae nina sababu zangu ila nakuomba unifichie siri hii.”

“Hakuna tatizo.”

“Basi subiri.” Kilole alisema huku alielekea chumbani kwake, Jimmy alibaki akijiuliza anataka kupewa kazi gani. Baada ya muda Kilole alirudi akiwa katika vazi la kanga moja iliyoonesha hakuwa na nguo nyingine ndani. “Jimmy,” alimwita kwa sauti ya chini. “Na..na..aam,” Jimmy alionekana kuchanganyikiwa na umbile la Kilole lililokuwa la utata kwa mwanaume shababi.

“Jimiiii, utaiweza kazi kweli?”

“Kwa nini?”

“Umeona negative umechanganyikiwa ukiona picha si utashindwa hata kuifanya hiyo kazi.”

“Niwaweza tu wala usihofu.” “Umeisha andaa kamera yako?”

“Ndiyo.”

“Basi njoo chumbani.”

Jimmy kabla ya kwenda chumbani alifikiria ameitwa na Kilole kufanya naye mapenzi kwa kisingizio cha kupiga picha. Japo alijua mke wa mtu sumu lakini kwa mwanamke aliyeumbwa akaumbika kama Kilole ilikuwa sawa na nzi kufia juu ya kidonda. Uchu wa ngono ulimjaa na kujiona kama mbwa anayejipeleka mwenyewe kwa chatu, alitembea huku mwili wake ukiongezeka joto la matanio. Alipoingia chumbani alishangaa kumuona Kinape amelala kitandani hajitambui akiwa mtupu. Hali ile ilimshtua na kujiuliza kulikoni kuwa vile. Kilole alikwisha msoma Jimmy, ilikumtoa hofu alimwambia:

“Jimmy utakachokiona humu ndani kiache kama ulivyokiona, nikisikia chochote tutaonana wabaya, Kabla ya mimi kulikimbia jiji nitaanza na wewe.

” Kilole alitoa onyo kali kwa Jimmy. “Siwezi kufanya hivyo.”

“Sawa, sasa naomba upige picha kila tendo nitalofanya na Kinape.”

“Tendo gani?”

“Usiulize andaa kamera yako,” Kilole alikuwa mkali kidogo. Jimmy hakuongeza swali zaidi ya kufuata maelekezo, muda wote bado alikuwa gizani kutokana na hali iliyokuwemo mule chumbani kwa Kinape kulazwa chali kitandani akiwa mtupu na sehemu zake za siri zilikuwa zimenyanyuka. Kabla hajapata jibu Kilole aliitoa kanga iliyostiri mwili wake na yeye kubakia mtupu.

“Jimmy,” alimwita huku akipanda kitandani.

“Aah…Eeeh…Na..naa..m.”

“Naona umepagawa, sasa kila hatua piga picha, sawa?”

“Sawa,” Jimmy alijibu macho yamemtoka pima.

Jimmy alimshangaa Kilole mambo ya aibu aliyokuwa akiyafanya mbele yake bila haya, alifanya mapenzi na Kinape aliyekuwa hajitambui kwa kumkalia juu yake. Ajabu Jimmy alijisahau kazi aliyopewa ya kupiga picha na kujikuta akipandwa na mzuka wa ngono. Alimshangaa Kilole mke wa mtu kufanya mpenzi na shemeji yake ambaye alionekana amelewa kupita kiasi.

Aliona heri kama amezidiwa angemweleza yeye kuliko kufanya mapenzi na mtu asiyejitambua. Kilole alipofumbua macho alimshangaa Jimmy aliyekuwa amesahau kazi aliyomtuma. “Jimmiiiii,” sauti kali ya Kilole ilimshtua Jimmy aliyekuwa akiangalia Blue print live bila chenga.

“Jimmy, umeisha piga picha?”

“Samahani Sister,” Jimmy alibabaika.

“Samahani nini Jimmy, kazi imekushinda?”

“Ha..ha..pana,” Jimmy alibabaika hata kamera alikuwa ameweka chini ili afaidi vizuri mambo ya wakubwa. Aliiokota na kujiandaa kupiga picha huku akitetemeka.

”Naomba upige picha kila hatua sawa?”

“Sawa.” Kilole alianza zoezi upya la kijidhalilisha mbele ya Jimmy, naye alipiga picha kila hatua.

Baada ya zoezi lake kukamilika, alimuomba Jimmy amuoneshe picha zote. Alichagua zinazofaa na zingine kuzifuta kisha alimuomba Jimmy atoke akamsubiri sebuleni. Jimmy alitoka akiwa katika hali mbaya baada ya kuzidiwa na ashki, kuna kipindi aliwaza hata ambake Kilole.

Lakini alikumbuka alikuwa kazini na kazi ile ya hatari aliahidiwa pesa nyingi, alikaa sebuleni kumsubiri Kilole ambaye alikuja baada ya robo saa akionesha ametoka kuoga na kuvalia nguo ya kulalia.

“Jimmy, mzigo wako huu hapa, hizi ni laki na nusu, hamsini za kusafishia na laki moja adivansi ukileta picha zangu nakumalizia laki na nusu. Ila kuna zawadi yako kubwa kama utakuwa msiri, kuna kazi nyingine ya milioni moja.”

“Wacha!” “Wewe tu kuonesha uaminifu.”

“Basi dada kesho saa nne nakuletea mzigo wako, andaa fedha yangu tu.”

“Hakuna tatizo, tutaonana kesho, lakini chonde chonde siri hii asijue mtu yeyote.”

“Nakuhakikishia siri hii itabakia kwa watu wawili mimi na wewe tu.”

“Haya, usiku mwema.”

Kilole aliagana na Jimmy na kurudi ndani, alipofika kitandani alivua nguo zote na kujilaza pembeni ya Kinape. Alfajiri kilevi kilipomwisha Kinape alishtuka usingizini, akili yake alijua aliyelala pembeni yake ni mpenzi wake Happy, lakini alipoangalia vizuri aligundua ni Kilole, alishtuka na kunyanyuka kitandani. Alishangaa kujikuta amelala kitanda kimoja na shemeji yake na kwa hali waliyokuwa kuwa nayo, aliamini lazima walifanya mapenzi. Alijiuliza ilikuwaje mpaka akawa kwenye kitanda cha rafiki yake wakiwa watupu na mkewe.

Alinyanyuka haraka kitandani na kupitia nguo zake bila kuzivaa na kukimbilia chumbani kwake. Alipokuwa akipapatika kama kuku aliyekatwa kichwa na kuachiwa, Kilole alikuwa akimuangalia kwa chati huku akichekea moyoni huku akisema:

“Kiko wapi, mimi na wewe nani mjanja.”

Hakujisumbua aliendelea kulala huku akichelelea moyoni, wakati huo Kinape baada ya kuingia chumbani kwake na kukaa kitandani mikono aliweka kichwani na kujiuliza kilichotokea ni kweli.

Ili kupata ukweli alizishika sehemu zake za siri na kukutana na majimaji kumuonesha kabisa katumika. Kila alivyorudisha mawazo yake ilikuwaje mpaka akalala katika kitanda cha rafiki yake kipenzi Deus na mkewe, jibu lilikuwa mbali.

Alikumbuka siku ya jana yake kwenye sherehe baada ya kuondoka Happy alibakia na shemeji yake Kilole wakipiga stori huku wakivuta muda kumsubiri Happy ili wafungue sherehe rasmi.

Wazo lake la haraka lilikuwa huenda ule ulikuwa mpango wa Kilole kama alivyomuahidi atahakikisha anamrudisha mikononi mwake. Kinape alijiapia kuwa kamwe pamoja na kufanya ujanja ule hawezi kuendelea kuwa mpenzi wake zaidi ya kuhama nyumba.

Wakati anatoka kuoga aliona simu yake juu ya kochi, aliichukua na kukuta imezimwa, alielekea nayo chumbani kwake. Alipoingia aliiwasha, haikupita muda ziliingia meseji zaidi ya kumi zote zikuwa za Happy akimlalamikia kwa kitendo alichomfanyia cha kumzimia simu.

Wakati akiendelea kusoma ujumbe wa Happy simu yake iliita, alikuwa Happy, alijiuliza atamwambia nini ili amuelewe. Lakini alijikaza kiume na kuipokea kwa kuamini hawezi kukosa cha kumueleza.

“Haloo Kinape umenifanya nini?”

“Happy mbona huniulizi nimepatwa na nini unaanza kunilaumu.”

“Kinape, nilikuambia narudi, lakini nilipofika nyumbani nikakuta hali ya mama ipo sawa, nimerudi nikasikia umenifuata na kusema utarudi kesho.

Nilipopiga simu yako kumbe uliiacha ndani kwa kuchanganyikiwa. Kinape, tulikuwa na mpango gani wa kulala pamoja na kusababisha sherehe ya shemeji yako kuvurugika?” Maneno yale yalimpa picha na kujua atamjibu nini ili kumfanya asiendelee kuumia.

“Mpenzi nilipokuwa nakuja kwenu, nilipata na ajali na kupelekwa polisi hata simu niliisahau nyumbani.”

“Sasa mbona baadaye nilipokutafuta ilikuwa imezimwa?”

“Nilikuta haina chaji.”

“Kwani ulirudi saa ngapi?”

”Saa nane usiku.”

“Ooh, pole upo wapi sasa?”

“Nyumbani.”

“Nakuja sasa hivi?” “Usije nisubiri kwenu.”

“Hapana mpenzi usisumbuke nakusubiri nitakufuata hapo hapo.”

“Sipo nyumbani, ndiyo maana nimekueleza nisubiri.”

“Kinape si umeniambia upo nyumbani sasa hivi! Mbona sikuelewi?”

“Nimetoka nyumbani sasa hivi kuelekea polisi, hivyo namalizana nao nipitie kwenu.”

“Mmh! Sawa.”

“Usisikitike dia, sawa.”

“Sawa dia, nimeumia sana kusikia umelala polisi kwa ajili yangu.”

“Hawakukupiga?”

“Hawakunipiga nipo sawa dia.”

“Ooh! Afadhari nakusubiri, una usafiri au nikufuate na gari?”

“Hapana, kuna teksi nilikodi,” Kinape alijitahidi kumzuia mpenzi wake.

“Hakuna tatizo mpenzi wangu, angalia usije ukapata ajali tena.”

“Unafikiri niligonga walaa, alijigonga mwenyewe mwendesha boda boda wala hakuumia polisi hawana dogo.”

“Mbona unaongea hivyo si upo polisi?”

“Nipo mbali nao.” “Basi kuwa makini nakupenda sana Kinape, mmmmmmwa.” “Mmmwa,” Kinape naye alijibu na kukata simu. Mara mlango uligongwa, alikuwa Kilole, bila kuitikia alinyanyuka na kwenda mlangoni, alipofungua alikutana naye uso kwa uso. “Za asubuhi shemeji?” Kilole alimsabahi Kinape aliyekuwa akimshangaa. “Nzuri.”

“Shemeji chai tayari.”

“Asante, nimeshiba.” “Imeanza lini na leo iwe ya pili, kama ulijua hunywi chai kwa nini hukuja kunieleza mapema. Si umenipita jikoni unakwenda bafuni kuoga.” “Sikukuona.”

“Basi lazima chai uinywe ndipo uende huko kwa mwanamke wako unayejifanya unampenda kuliko wanawake wote.”

“Shemu yote yamefikaje huko, tunazungumzia chai Happy kaingiaje?” Kinape alimuuliza Kilole huku akitengeneza shati lake. “Kama hutaki yote hayo, njoo unywe chai tena kuna kitu nataka unieleze kwa kituo kiniingie. Wewe si ulinikataa iweje univizie usiku?” Kilole alizungumza sauti ya kuonesha hakutendewa haki. “Mimi?” Kinape alishtuka kusikia vile. “Kwani hapa nazungumza na jiwe?” “Mmh! Bado sielewi nini kilitokea jana,” Kinape alisema akiwa ameangalia chini kwa aibu.

“Ndiyo maana nikasema kunywa chai tuzungumze.”

“Happy ananisubiri.”

“Happy wa muhimu kuliko tukio ulilonifanyia jana usiku, ulishindwa kuniambia nikakukubalia kwa hiyari yangu, ukanivizia nimelala huo si ubakaji? Nilijua bado unanipenda ndiyo maana nilikueleza nikupe penzi la siri kwa vile bado naheshimu penzi lako ukakataa.

“Lakini asubuhi nashtuka nakuona unakimbia, kweli Kinape wewe wa kunifanyia hivyo?” Kilole alimuuliza kwa msisitizo.

“Kilole hili suala linatakiwa tulifanyie kazi si la kukurupuka kulaumiana.”

“Sijakulaumu ila nimekuuliza ulishindwa vipi kunieleza una hamu na mimi, siwezi kukunyima, kwa vile wewe ndiye uliyenionesha raha na tamu ya dunia. Hili kwangu si tatizo lakini na mimi nina ombi langu nakuomba nani unitekelezee ili tuwe sawa.”

“Mmh! Hata sielewi, basi niache niende kwa Happy ili nikirudi tupange vizuri.” “Kinape umenionjesha naomba unimalizie kabisa.”

“Sawa nimekubali, nikirudi nitatimiza haja zako.”

“Kinape kuna tatizo gani ukinipa muda huu ili ukitoka usiwe na wasiwasi wa kufikiria nyumbani?”

“Mmh! Sawa.”

Kauli ile ilimfanya Kilole amsukumie Kinape nyuma na kumuangushia kitandani kwake. Kama kipanga aliyeona kifaranga cha kuku alimsaula nguo zote na yeye kutoa zake chache zilizovaa.

Kinape alijikuta akiwa kama mbwa kwa chatu, moyoni alijiapiza atatafuta kila njia ahame pale ili kujiweka mbali naye. Upande wa Kilole aliamini mpango wake umekwenda vizuri tofauti na alivyofikiria na kuapa kumfanyia mambo makubwa Kinape.

Baada ya kuondoka chumbani Kinape alibakia ameinama mikono kichwani alijiuliza maswali yasiyo na majibu, ilikuwaje akawa katika kitanda cha Deus, alichokumbuka kuamka asubuhi na kujikuta amelala na Kilole bila nguo bila kujua alifikaje pale.

Aliwaza labda ulikuwa mpango wa Kilole aliomuahidi hapo awali, lakini shutuma alizozitoa zilizidi kumchanganya kuonesha amemlazimisha kufanya naye mapenzi bila ridhaa yake. Kitendo kilicho onekana kuwa ni sawa na kubaka.

Japo hakupenda kufanya mapenzi tena na Kilole lakini kwa upande mwingine alimshukuru kwa uamuzi wake wa kutomshitaki polisi. Aliamini kama angempeleka basi angeweza kuozea gerezani, kwani ushahidi wote ulikuwepo wa kuonesha amebakwa.

Simu yake iliita zaidi ya mara sita na kukatika, aliisikia lakini akili yake ilikuwa mbali sana. Alikumbuka alikuwa na mpango wa kuonana na Happy nyumbani kwao, alinyanyuka na kwenda bafuni kuoga.

Baada ya kumnaliza kuoga na kubadili nguo, alipoangalia simu yake alikuta aliyepiga ni Happy zaidi ya mara sita. Hakutaka kumpigia alijua yote atamalizia huko huko akifika, alitoka kuelekea nyumbani kwao Happy. Wakati anatoka sebule haikuwa na mtu alitoka haraka kumuwahi Happy, alipofika mlango wa kutokea nje aliitwa nyuma na Kilole. “Kinape.”

“Naam,” aliitika huku akisimama.

“Safari ya wapi?”

“Si nimekueleza nakwenda kwa Happy.”

“Nataka nikuambie kitu kimoja, sipendi kusikia jina la mwanamke wako, kila nikisikia linanitia kichefuchefu.”

“Lakini si mchumba wangu?” “Mmh! Sasa hii chai anywe nani?”

“Nilimuahidi nitakwenda kwao muda uliopita nikizidi kuchelewa atajisikia vibaya.”

“Kinape unachekesha, nisijisikie vibaya mimi niliyekutaka ukanikataa ukaishia kunibaka.”

“Yaani sijui hata ilikuwaje hiyo jana!”

“Iweje na wewe umeamua kunibaka.”

Kauli ile ilimmaliza nguvu Kinape na kubakia amesimama kimya kama amenaswa na sumaku.

“Kinape siwezi kukulazimisha mapenzi kwa vile upo na mchumba wako, lakini sipendi dharau.”

“Lakini si nimekueleza hali iliyopo?”

“Kinape huyo Happy angekujulia wapi kama mimi ningemgomea mume wangu wee kuja mjini?”

Kilole alimuuliza huku ameshika kiuno. “Lakini mbona yamekuwa hayo….,” Kinape alinyamaza kimya baada ya mlango kugongwa. Kilole aliamini muda ule Jimmy alikuwa akileta picha, alipofika mlangoni alikutana na Happy. Japo moyoni alichukia lakini alitengeneza tabasamu la uongo.”

“Ooh! Happy karibu.”

“Asante dada,” Happy alisema huku akimtaza Kinape aliyekuwa amesimama karibu na mlango.

“Kinape unanifanya nini, nimekukosea nini mpaka uamue kunitesa hivi?” Happy alisema kwa sauti ya kilio.

“Happy mbona umekuwa mtu wa kulaumu bila kuuliza?”

“Niulize nini hapa ndiyo polisi?” “Hilo swali gani?”

“Kinape ni wazi hunipendi najipendekeza kwako,” Happy alilalamika huku machozi yakimtoka. “Happy unaniamini, huniamini?”

“Nikuamini vipi mtu muongo.” Wakati huo Jimmy mpiga picha alikuwa akiingia, ili kupoteza ushahidi Kilole alimueleza Kinape:

“Shemu naomba ukazungumzie nje mambo yenu nina mgeni.”

“Sawa,” Kinape aliitikia huku akimshika mkono Happy aliyekuwa ameiva na kuwa mwekundu kwa hasira.

“Hebu ngoja,” Happy alijitoa mkononi mwa Kinape.

“Happy hebu msikilize mwenzako,” Kilole aliingilia kati baada ya kuona Happy akitafuta msaada kwake.

“Sikiliza dada, Kinape ananinyanyasa sana.”

“Mdogo wangu ngoja nizungumze na mgeni, tutalimaliza nina imani kabisa Kinape anakupenda sana.” Kinape na Happy walitoka nje na kuwaacha Kilole na Jimmy.

Usiku baada ya kutoka kumpiga picha za aibu Kilole, Jimmy alikuwa mtu mwenye mawazo mengi sana. Toka aanze kazi ile hakuwahi kukutana na tukio zito kama lile. Tokio kubwa lilikuwa kuwapiga picha za utupu wake za watu au mastaa wa kike. Lakini la kushuhudia mtu akifanya mapenzi lilikuwa ndilo tukio lake la kwanza lililompa wakati mgumu sana. Alitamani bora Kilole angempa penzi yeye kuliko kufanya mapenzi na mtu aliyekuwa sawa na maiti asiyejielewa. Alijikuta akipata maswali yasiyo na majibu juu ya kitendo cha Kilole kufanya mapenzi na mtu anayemfahamu ni shemeji yake. Alijiuliza kufanya tukio lile huku akipiga picha alikuwa na maana gani, alijikuta akiingiwa na tamaa ya mapenzi kwa kuamini kupitia picha zile lazima na yeye ataweza kumtia mikononi. Wazo lingine lilikuwa kutengeneza pesa zaidi kupitia picha zilezile. Baada ya kuwaza sana akiwa amejilaza kitandani alijikuta akitabasamu baada ya kugundua picha zile zitakuwa sawa jiwe moja kuua ndege wawili. Hakuamini kabisa mwanamke yule pamoja na kumtisha anaweza kumfanyia lolote baya. Kabla ya kulala alirudia kuangalia picha moja moja ili aone zipi zimetoka vizuri na zipi zimeharibika, alijikuta akiwa amepiga picha chache zenye ubora. Kutokana kupatwa na kigagaziko kilichomfanya aifanye kazi katika wakati mgumu. Picha zingine alipiga ukuta badala ya watu, zingine aliwapiga mgongo au kupiga sehemu isiyohusika. Zote ambazo zilikuwa hazifai alizifuta na kubakiza chache ambazo zilikuwa zinafaa. Baada ya kuwaza sana alipitiwa na usingizi mpaka siku ya pili, asubuhi alipoamka baada ya kuoga alikwenda studio kusafisha picha zake. Kama kawaida picha zake za magumashi zilikuwa zinawahishwa kusafishwa kabla hawajaanza kazi yoyote. “Beka kama kawaida piga mara mbili.” “Za nani mwana?” “Kaka aina haja ya kujua, nifanyie kazi haraka.” Beka alimsafishia Jimmy picha mara mbili na kumpatia, alizichukua na kurudi zake nyumbani kwanza kabla ya kuzipeleka kwa mwenyewe. Alipofika alipitia picha moja baada ya nyingine, alichukua za kwake na kuziweka kwenye kabati na zilizobaki alimpelekea Kilole. * Jimmy alipofika kwa Kilole alishtuka kumkuta Kinape nusra atimue mbio kwa mshtuko, lakini alificha hofu yake na kuingia ndani. Baada ya Kinape na mpenzi wake kutoka nje walibakia wawili ndani. “Karibu ukae,” Kilole alimkaribisha Jimmy baada ya kuonesha wasiwasi, alijua baada ya kumuona Kinape. “Asante,” alijibu huku akikaa, kutokana na wasiwasi walijikuta akikaa chini. “Jimmy mbona unanitia aibu kazi utaiweza kweli?” “Samahani, unajua nimeshtuka sana.” “Hajui lolote, wasiwasi wako tu.” “Mmh! Nilishtuka sikutegemea kumkuta.” “Tuachane na hayo mzigo wangu upo wapi?” Kilole aliuliza. Jimmy alimpa bahasha ya picha, baada ya kuipokea aliichukua na kwenda nayo chumbani. Hakutaka kuzipitia alichukua kiasi cha fedha alizobakia kwenye deni lao, alipofika sebuleni alipa fedha yake na kumwambia: “Nina imani kila kitu kimekwenda vizuri?” “Nashukuru.” “Jimmy kama kuna kitu chochote nitakueleza.” “Hakuna tatizo.” “Naomba siri hii usimwambie yeyote ikivuja nitajua ni wewe, kwa hiyo usinilaumu kwa lolote litakalokukuta.” “Kwangu shaka ondoa, hakuna kitu kama hicho.” “Nakuhakikishia baada ya muda tegemea zawadi kubwa.“ “Nitashukuru sister.” “Basi baadaye.” Jimmy aliagana na Kilole na kuondoka zake, baada ya kuondoka Kilole alitoka nje na kuwakuta Kinape na Happy wakiwa katika mazungumzo ya kawaida. “Vipi jamani?” “Yamekwisha,” alisema Kinape. “Basi niwaache mimi nipo ndani.” “Hakuna tatizo.” Kilole alirudi ndani na kuingia chumbani kuangalia picha alizoletewa na Jimmy. Baada ya kufungua bahasha alichukua alitoa picha zote na kuzimwaga kitandani na kuanza kupitia picha moja baada ya nyingine. Zilikuwa picha za aibu ambazo hazikuonesha uhalisia wa watu wawili waliokuwa wanafanya mapenzi kwa ushirikiano. Picha zile zingekuwa kwa upande wa pili kwa ajili ya kumdhalilisha zingekuwa nzuri sana. Lakini kama mtego wa kuonesha wanafanya mapenzi alikuwa amefeli. Alijiuliza kama Kinape angegoma kufanya naye mapenzi, picha zile zisingeweza kumshtua kwani ilionesha wazi hakukuwa na ushirikiano wowote wa Kinape kwake. Moyoni alishukuru mkwala wake uliweza kumlainisha lakini kama angetegemea picha zile zisingemsaidia. Alijikuta akipandwa na hasira na kuamua kuzichana zote kisha aliziweka kwenye chombo na kuzichoma moto. Baada ya kuzichoma moto aliamini pamoja na kumtega na kuweza kufanya naye mapenzi bado hawezi kumdhibiti Kinape kwa vile ana uwezo wa kukataa na asimfanye lolote. Wazo lingine lililomjia ni kufanya naye tena mapenzi huku Jimmy akipiga picha wote wakiwa na akili timamu. Aliamini kwa mpango ule ataweza kumdhibiti Kinape pia hata kuweza kuvunja penzi lake na Happy ambalo kila kukicha lilimnyima raha. Alijikuta akijilaumu kwa kupanga mpango mbovu, lakini kwa upande mwingine ulisaidia kuweza kumvuta karibu Kinape mpenzi wake wa zamani. Alitoka nje na kuwakuta Kinape na Happy sebuleni wakizungumza, walipomuona waliacha kuzungumza na kumwangalia.

Uso wa Kilole ulionesha kuna kitu kimemsibu. Kinape alijua ni kutokana na Happy kuwa pale. “Dada vipi, bado unamkumbuka shemeji?” “Aah, wapi mbona nimeishazoea.” “Shemu vipi?” Kinape aliuliza. “Nikuone mara moja.” “Hakuna tatizo,” Kinape alijibu huku akinyanyuka. Kilole na Kinape walisogea pembeni, Kinape alijua lazima atagombezwa kuhusu Happy. “Kinape, kwanza samahani kwa kukukatisha kazungumzo na mpenzio.” “Bila samahani.” “Nina ombi moja, leo naomba tulale pamoja, kesho endelea na mpenzi wako.” “Hakuna tatizo.” “Basi endeleeni ma mazungumzo yenu.” Kinape alishangazwa na ustaarabu alioonesha Kilole, lakini moyoni alipanga Deus akirudi lazima aondoke. Kilole alifurahia kukubaliwa ombi lake bila masharti yoyote, alimpigia simu Jimmy kumjulisha kazi nyingine ya usiku ule. “Jimmy.” “Ooh! Sister lete mpya.”

”Ile kazi haikuwa nzuri nataka leo tuirudie.” “Kwa malipo yaleyale?” “Hapana, nitakupa laki na nusu.” “Poa, nije saa ngapi?” “Saa mbili usiku, ila ukifika usiingine ndani nipigie simu, ooh! Nimekumbuka hebu njoo mara moja,” Kilole alikumbuka kazi ile ilitakiwa ifanyiwe maandalizi ili isije kwenda kinyume kutokana na muda wa kurudi mumewe kuwa umekaribia. Wakati huo Kinape na Happy walikuwa wameondoka na kuahidi kurudi jioni. Baada ya muda Jimmy alifika, alimzungusha kwa nyuma sehemu ya dirishani ili kuandaa maandalizi ya kupiga picha za ndani. Baada ya kuandaa eneo vizuri waliagana na kukubaliana kukutana muda huo. Majira ya saa mbili usiku Kinape alikuwa nyumbani, baada ya chakula cha usiku walikwenda chumbani kulala. Kama kawaida Jimmy alikuwa amekwishafika eneo la tukio. Baada ya kupewa taarifa ya kuacha kwa mchezo mchafu, alisogea dirishani na kuchungulia ndani. Ili kupata uhakika kama Jimmy amefika alinyanyuka na kwenda dirishani kama anataka kusogeza pazia, alipoangalia nje alimuona. Alilidhika na kurudi kitandani kuendelea na zoezi lake. Naye Jimmy kama alivyoelekezwa alipiga picha kutokana na jinsi Kilole alivyokuwa akifanya bila Kinape kujua. Japo alikuwa kwenye wakati mgumu huku akijawa na mawazo mtu na shemeji yake kufanya mapenzi. Hakutaka kujua sana, lakini katika siku iliyokuwa ngumu kwake ilikuwa ile. Mpaka wanamaliza Jimmy alikuwa hoi na kujichafua kutokana na kwenda na muvu ya mchezo. Baada ya kumaliza mpango wake Kilole alimtanguliza Kinape bafuni na yeye kutoka nje kuonana na Jimmy. “Vipi umefanikiwa?” Kilole alimuuliza Jimmy baada ya kumuona. “Ndiyo.” “Hebu nione.” Jimmy alimuonesha picha alizopiga katika hatua zote, zilikuwa picha nzuri sana ambazo aliamini kama Jimmy akiziona hawezi kuruka. “Jimmy kazi nzuri.” “Lakini umenipa mateso makubwa.” “Pole nitakuongezea elfu hamsini kwa hiyo itakuwa lakini mbili. Shika laki mbili zingine kesho.” “Hakuna tatizo, kuna lingine?” “Hakuna.” “Basi kesho.” Waliagana kwa Kilole kurudi ndani huku moyo wake ukiwa na furaha, alijikuta akiingia chumbani huku akitabasamu. “Vipi mbona una furaha?” Kinape alimuuliza. “Leo umekumbusha mbali sana.” “Umekumbuka nini?” “Penzi letu lilivyokuwa tamu adhimu, hakika leo nitalala usingizi mtamu.” “Lakini kumbuka kitendo hiki ni sawa na kukata tawi tulilo kalia.” “Hii ni siri yetu.” “Hakuna siri katika mapenzi.” “Basi kwetu itakuwa siri.” “Nimefanya tu lakini si kwa moyo wangu.” “Kinape mbona unataka kutia mchanga kwenye chakula kitamu, kwa vile tumeamua kula nguruwe basi tumchague aliyenona.” “Kumbuka mwenyewe muda si mrefu atakuwa hapa.” “Tutakuwa kama hatujuani, ila siku tukipata nafasi kama kawaida.” Waliendelea kula raha zao mpaka siku ya pili, huku moyoni Kilole akiapa akifanikiwa kuzipata picha zile lazima Kinape arudi mikononi mwake na kuvunja uchumba wake Happy. * Jimmy baada ya kufika kwake alijikuta akizidi kuwa na maswali mazito juu ya kitendo cha Kilole na Kinape kumhujumu Deus. Lakini bado alikuwa wazo lake la kuhakikisha kupitia picha zake anampata kimapenzi. Aliamini kama angekuwa na kamera ya kuchukua video basi angepata mkanda ambao angeweza kuuza kwa fedha nyingi siku za mbele. Pia aliona kupitia picha zile angepata faida mara mbili, hakuwa na haja ya kuzichambua kwa vile alizipiga katika ustadi mkubwa. Aliweka kamera yake kwenye kabati na kutoka nje kwenda kutafuta mwanamke wa kulala naye kwani alikuwa kwenye hali ngumu. Jimmy aliposhtuka siku ya pili alijikuta peke yake kitandani, mwanamke aliyelala naye hakuwepo. Hakujishughulisha naye baada ya kuoga aliwahi kusafisha picha, alimkuta Beka na kumweleza amsafishie mara mbili kama kawaida. Baada ya kusafishiwa alizichukua na kuzipeleka nyumbani, alipofika alishangaa kukuta sehemu alipoweka picha alizompiga Kilole mara ya kwanza hazipo. Kilichomshangaza ufunguo wa chumba chake alikuwanao mwenyewe. Alijikuta akishtuka na kujiuliza nani aliyechukua. Alikumbuka changudoa aliyelala naye na kuondoka akiwa amelala ndiye aliyechukua zile picha, alijiuliza amezichukua ili iweje. Wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kama zikivunja lazima Kilole atamuona hana manaa hata kumfanyia kitu kibaya.

Alipanga usiku akamtafute ili amrudishie picha zake, alichukua picha alizosafisha na kumpelekea Kilole.

Kama alivyoelekezwa akitaka kupeleka picha alitakiwa amjulishe kwa simu ili azifuate mwenyewe kuliko kuingia ndani, kuondoa wasiwasi kwa Kinape. Jimmy alipofika alimpiga simu Kilole aliyekuwa amekaa sebuleni na Kinape wakitazama runinga.

Kilole baada ya kuona namba ya Jimmy aliikata simu na kuelekea chumbani bila Kinape kujua kinachoendelea. Alipofika chumbani alimpigia na kumuuliza:

“Vipi Jimmy?”

“Nimekwishafika.”

“Poa nakuja.”

Kilole alichukua upande wa kanga na kujitanda ili akirudi asionekane amebeba kitu, alipofika sebuleni Kinape alimuuliza:

“Vipi shemu?”

“Natoka kidogo.”

“Wapi tena?” “Nafika dukani.”

“Vipi utachelewa? Maana Happy kanipigia simu nimfuate ili nimpeleke hospitali hajisikii vizuri.”

“Sichelewi nisubiri, nafika dukani mara moja.”

“Hakuna tatizo.” Kilole alitoka nje na kwenda alipokuwa Jimmy, alipofika Jimmy alijitoa sehemu alipokuwa amesimama.

“Vipi tayari?”

“Tayari.”

“Poa.”

Kilole alichukua bahasha na kumpa fedha iliyobakia huku akiendelea kumsisitiza: “Jimmy nimekuamini kukupa kazi ya hatari, kama ukivujisha ishu hii ujue sitaona hatari kunyongwa kwa ajili yako. Nimekupa malipo mazuri ili kuhakikisha ufanyi uzembe wowote, au kuna kitu kimekwenda kinyume na mpango wetu?”

“Hapana.”

Jimmy alijibu akiwa na wasiwasi wa picha zilizopotea katika mazingira ya kutatanisha. Akiwa katikati ya mawazo Kilole alimshtua:

“Vipi mbona kama kauli yangu imekushtua?”

“Ha..ha..pana,” Jimmy alibabaika.

“Jimmy usiwe umefanya makosa tusije tukalaumiana, japo unaniona mwanamke kwenye hili nitakuwa zaidi ya mwanaume,” Kilole alizidi kusisitiza.

“Kilole mbona unanitisha kama uliona siwezi au huniamini kwa nini ulinipa kazi hii?”

“Si kwamba nakutisha maelezo yangu naona kama yamekubadili muonekano wako.”

“Wasiwasi wako tu, lakini nipo makini kuliko unavyofikiria.”

“Mmh! Sawa lakini zingatia hilo picha zote kwenye kamera umefuta?”

“Ndiyo.”

“Hebu nipe kamera nione.”

Jimmy alimpa kamera na kuangalia picha zilizokuwa zimebaki kwenye kamera hakuona picha ya tukio hata moja.

“Jimmy nakuamini najua huwezi kuniangusha.”

“Usihofu.”

Waliagana ili kumpumbaza Kinape alikwenda hadi dukani na kununua vitu vya kutafuna na kurudi navyo ndani. Alipofika sebuleni alimtupia bazoka Kinape na kumweleza:

“Unaweza kwenda lakini usichelewe.”

“Hakuna tatizo.”

Kinape alijibu huku akinyanyuka kujiandaa kwenda kwa mpenzi wake Happy bila kujua Kilole alimtoa kijanja ili apate nafasi ya kuangalia picha zake na kujipanga kumrudisha Kinape mikononi kwake na kuvunja penzi lao. Baada ya kuingia chumbani hakujiamini alijifungia kwa ndani na kuanza kupitia picha moja baada ya nyingine.

Zilikuwa picha alizozitalajia zenye kuonesha penzi la ushirikiano, picha zile zilimfanya atabasamu na kujikuta akiruka juu na kujitupa kitandani kuonesha alichokitaka ndicho kilichofanyika. Alijisemea kwa sauti ya chini:

“Kinape kwisha habari yake.”

Aliziweka picha vizuri na kiendelea na shughuli zake moyoni akiwa na furaha tele.


Baada ya kumaliza semina ya kikazi Deus alirudi nyumbani Tanzania, uwanja wa ndege alipokewa na mkewe Kilole na mwanaye mpenzi Gift.

Pia alikuwepo rafiki yake kipenzi Kinape na mpenzi wake Happy. Baada ya kufika Kilole alijitupa kifuani kwa mume wake kuonesha kweli alikuwa amekosa mahaba yake.

“Jamani mume wangu baba Gift, karibu sana nyumbani, yaani siamini macho yangu,” alijiliza machozi ya uongo.

“Mke wangu mbona hata wiki haikufika?”

“Basi hunipendi mume wangu, yaani nilivyoteseka unasema hivyo.”

“Basi mke wangu, mengine tutakwenda kuzungumzia nyumbani.”

Jinsi alivyokuwa akideka kwa mumewe Kinape alichekea moyoni na kuona jinsi mwanamke alivyo nyoka kwa kumdanganya mumewe anampenda kumbe anamla kisogo. “Mmh! Kinape za siku mbili tatu?”

“Nzuri tu best, za huko?”

“Eeh bwana nzuri tu, nimefurahi kuwakuta wote wazima, hii imenipa faraja kuwa wewe si rafiki bali ni ndugu wa damu kwa kuweza kuitunza familia yangu kipindi chote nilipokuwa mbali nayo.”

“Ni wajibu wangu kuilinda familia yako,” Kinape alisema huku moyoni ukiumia kwa kitendo cha kutembea na Kilole.

“Shemu vipi?” Alimgeukia Happy mpenzi wa Kinape.

“Safi, pole na safari shemu.”

“Asante, nina imani baada ya kurudi nitafanya kila niwezavyo kuhakikisha mnafunga ndoa.”

“Nitashukuru shemeji maana ndugu yako amekuwa mzito.”

“Best, umekwisha kwenda kumtambulisha shemu nyumbani?” Deus alimuuliza Kinape. “Nilisubiri urudi baada ya kufika nina imani ni muda muafaka sasa kwenda kumtambulisha mpenzi wangu nyumbani.”

Kauli ile ilikuwa kichefuchefu moyoni mwa Kilole na kujisemea kimoyomoyo: “Tutaona mimi na huyu mjinga mwenzenu nani zaidi.”

Moyoni aliapa kulivunja penzi la Kinape na Happy kwa msaada wa zile picha.


Baada ya Deus kurudi, kutokana na makubaliano kati ya Kinape na Kilole heshima ilirudi na kuitana mtu na shemeji yake. Pamoja na makubaliano hayo Kilole alitamani siku moja moja amtoroke mumewe na kwenda chumba cha Kinape kupata penzi la hamu. Lakini mara zote Kinape alikuwa makini hasa usiku alijifungia kwa ndani na kuwasha muziki kama Kilole atamfuata atasingizia hakusikia. Ilikuwa kama alivyowaza usiku mmoja Kilole alimuacha mumewe amelala na kwenda kwa Kinape.

Lakini kikwazo kilikuwa mlango uliofungwa kwa ndani, alipojaribu kugonga kwa taratibu sauti ya mlango ilimezwa na sauti ya muziki uliokuwa ukilia chumbani. Kilole alikasirika na kujikuta akipandwa na hasira akiwa tayari kutumia turufu ya picha chafu ili kumtisha Kinape na kukubaliana na masharti yake.

“Kinape mbona jana ulifunga mlango kwa ndani?” Kilole alimuuliza kwa sauti ya chini baada ya kukutana kwenye korido la msalani.

“Lini ulikuta mlango upo wazi na ulikuwa na shida gani?”

“Hujui au ndiyo ushanichezea kisha uniache?”

“Lakini hii si sehemu ya mazungumzo haya, tulizungumza nini mumeo akirudi?”

”Kuzungumza nini, mbona ulifunga mlango?”

“Jamani, si chumbani kwangu?”

“Ilianza lini ina maana unaogopa kuibiwa.”

“Ni utaratibu wangu wa siku zote.”

”Kwa nini uliwasha muziki?”

“Sasa hayo ni maswali gani?”

“Najua ulifanya vile ili nikigonga usinisikie.”

“Lakini lawama za nini, ulinieleza utakuja nikakufanyia hivyo?”

“Basi baadaye..” Kilole alisema baada ya kusikia akiitwa na mumewe. Baada ya kuondoka Kilole kuitikia wito wa mumewe, Kinape alibakia amesimama na kuona aliyoyakataa ndiyo yameanza na siku zote penzi kikohozi huwa halina siri.

Aliamini njia ya kujiepusha na tatizo lile ni kuhama kisha kufanya mpango wa haraka kukaa na Happy. Alipanga siku ile ile azungumze na Deus kwenda kujitambulisha nyumbani kwao Happy ili siku inayofuata naye ampeleke kijijini kumtambulisha kwa wazazi wake kabla ya kupanga mipango ya ndoa.

Aliamua jambo lile kulifanya kwa siri kuepuka vikwazo vya Kilole. Baada ya kufungua kinywa Kinape na Deus walitoka pamoja, njiani alimweleza dhamira yake ya kwenda kujitambulisha kwa kina Happy siku ile. “Mbona haraka sana?” Deus alimuuliza. “Nilipanga leo niende ila nilisahau kukujulisha, nataka kesho niende na Happy kijijini, isingekuwa vizuri kuanzia kwetu kabla ya mimi kujulikana kwao.”

“Hakuna tatizo, ni saa ngapi?”

“Saa mbili usiku.”

“Hakuna tatizo tutakwenda.”

Waliagana kila mmoja aliendelea na shughuli zake, Kinape ilibidi asubuhi ile ile ampigie simu Happy kumjulisha kuwa usiku wana ugeni wa kujitambulisha. Japo ilimshtua kuona imekuwa ghafla, lakini ilikuwa habari njema aliyoisubiri kwa hamu kama tone la maji katika kiu kali.

Nafasi ile hakutaka kuipoteza kwa kufanya maandalizi ya kupokea ugeni wa mchumba wake. Maandalizi yalikwenda vizuri na kumsubiri ugeni wa usiku huku Happy akiona ndoto yake ya kuolewa na Kinape imeanza kuwa kweli.


Deus kama kawaida yake alikuwa hawezi kufanya jambo lililo kuwa nje na ratiba zake za kila siku bila ya kumtaarifu mkewe. Kwa vile walikubaliana na Kinape wakutanie mjini na kwenda moja kwa moja nyumbani kwa mchumba wake. Aliamua kumjulisha mkewe baada ya kumaliza kazi zake majira ya saa moja na nusu usiku. Ujumbe ule ulimshtua Kilole kitu kilichomshangaza mumewe.

“Mbona umeshtuka hivyo?” Deus alimuuliza mkewe.

“Nimeshtuka kwa vile jambo hilo mmelifanya kwa siri.”

“Kuna siri gani kama nimekupigia simu kukujulisha?” “Mbona hamkuniambia toka asubuhi.”

“Hili suala nimeambiwa asubuhi njiani na Kinape wakati nakwenda kazini.”

“Mmh! Sawa, nawatakia utambulisho mwema.”

“Hayo ndiyo maneno, na kesho wanakwenda kijijini kwa utambulisho wa upande wa pili.”

“Atiii?” “Mbona umeshtuka tena?”

“Sasa mbona mambo mnafanya mambo kienyeji,” Kilole alikuja juu kwa hasira za kweli huku wivu ikimpanda.

“Mke wangu kwani tatizo nini, haya si maandalizi ya awali, mipango ya harusi ikianza wewe utakuwa na majukumu makubwa kuliko unavyodhani.”

“Mmh! Haya, basi endeleeni na maandalizi mema.”

Baada ya kukata simu Kilole alijikuta moyo ukimuuma kwa kusikia habari zile, Alijiapiza kupitia picha zile lazima atahakikisha Kinape hamuoi Happy, alijikuta akipoteza furaha ya siku nzima na kujuta kupokea simu ya mumewe.

Baada ya kukata simu alikwenda chumbani na kurudia kuziangalia picha upya huku akiamini picha zile ndiyo suruhu ya kuangaika kwa Kinape. Alizirudisha kwenye bahasha na kuzificha sehemu yake. Utambulisho wa Kinape ulikwenda vizuri huku familia ya Happy akionesha furaha ya mtoto wao kupata mume.

Happy akiwa ndiye mtoto wa kwanza kuchumbiwa, baba yake mzazi aliwaahidi nyumba na gari kama zawadi kwa mtoto wake wa kwanza. Kinape naye aliwaahidi kumpeleka mchumba wake nyumbani kwao siku ya kesho yake. Walipewa baraka zote za familia za wazazi wa Happy kwenda kutambulishwa kijijini kwao.


Kilole alijikuta akikosa raha na kumfanya atangetange sebuleni kama kuku anayetaka kutaga, akitoka upande mmoja kwenda mwingine, nyumba aliiona chungu. Moyoni aliendelea kujiapiza juu ya kuhakikisha Kinape hamuoi Happy.

Alijikuta amesahau hata kupika chakula cha usiku kwa ajili ya kumfikiria Kinape. Honi ya gari ya mume wake ilimfanya akimbilie ndani na kujilaza kitandani kusingizia anaumwa ili asiulizwe chakula cha usiku. Mume wake aliingia ndani alimkuta amejifunika shuka gubigubi.

“Vipi mke wangu?”

“Sijisikii vizuri.”

“Hali hii imeanza saa ngapi?”

“Wakati najiandaa kupika.”

“Basi amka twende hospitali.”

“Nimemeza dawa kidogo kichwa kimeanza kutulia.”

“Kwa maana hiyo hujapika?” “Nipike saa ngapi mume wangu, ungeniona nilivyokuwa ungenikimbiza hospitali.”

“Lakini si umekunywa dawa ya kutuliza kwa nini tusiende hospitali?”

“Mume wangu huwezi kuamini kuja kwako kama umenipa dawa, sasa hivi sijambo kabisa.”

“Mmh! Basi kama ni hivyo, jiandae baadaye twende tukachukue take a way.”

Baada ya kutengeneza uongo wake na kufanikiwa bado moyo wake bado uliendelea ulimuuma kila alipomuwaza Kinape na kibaya zaidi habari za kujitambulisha kwao na Happy alimueleza mbele ya mumewe.

“Samahani shemeji.”

“Samahani ya nini?”

“Sikukueleza mapema kuwa naitakwenda kujitambulisha nyumbani kwao na Happy, pia kesho nakwenda kijijini kumtambulisha mwenzangu.”

“Mmh! Safari njema,” (moyoni alijisemea tutaona si muda mrefu jeuri yako itakwisha)


Siku ya pili Kilole alikuwa na wakati mgumu kufikisha ujumbe kwa Kinape ili kuzuia asiweze kwenda kijijini kumtambulisha mchumba wake. Lakini juhudi zake zilikuwa bure, baada ya kuondoka na katika gari moja na mumewe. Roho ilimuuma sana kwa hila za Kinape za kumkwepa kwa kuondoka na mumewe kwenye gari moja. Alijifikiria kupiga simu kumzuia Kinape na kumweleza ukweli juu ya picha zile, lakini alisita kwa kuhofia mabadiliko yoyote yatakayo tokea kwa Kinape lazima mumewe angemtilia wasiwasi na pengine siri kutoka nje kabla ya kutimiza lengo lake.

Aliamua kumsubiri akirudi na kuingia anga zake ndipo amlipue. Kinape bila kujua kuna mpango kabambe wa kuvunja mipango yake ya kumuoa Happy. Utambulisho ulikwenda vizuri, familia ya Kinape kumpokea kwa bashasha mchumba wa mtoto wake huku wakimuahidi kumpa ushirikiano mkubwa kufanikisha ndoa ya mtoto wao.

Baada ya utambulisho walirudi mjini kujipanga kwa ajili ya maandalizi ya harusi ambayo Deus alimuahidi Kinape kuyasimamia kwa asilimia mia. Kinape aliutumia muda mwingi kumkwepa Kilole kwa kurudi muda ambao atakuwa amewasiliana na Deus kama yupo nyumbani. Hata walipokutana kwa bahati mbaya hakutaka kuzungumza kwa muda mrefu kwa kisingizio cha Deus yupo.

Moyoni Kilole alijiapiza hata kumfuata Kinape ofisini na kumweleza uchafu ule kwa kuugeuza upande wa pili kana kwamba Kinape ndiye aliyefanya mchezo ule.

Alipanga kufanya vile kabla mipango ya harusi haijaanza, lakini aliamua kuonesha kama halikumuuma baada ya kutumia nguvu bila mafanikio. Siku moja akiwa anaendelea na kazi zake alishangaa kumuona Kinape akirudi mchana ghafla huku akionekana ana wasiwasi mwingi.

“Vipi Kinape mbona leo mchana?”

“Kuna vitu nilisahau kuondoka navyo asubuhi, hivyo nimerudi kuvichukua,” alisema huku akielekea chumbani kwake.

Kilole alimsindikiza kwa macho huku akijiuliza aitumieje nafasi adimu kama ile, wazo la haraka lilimjia aanza kujiliza ili kuonesha kuna kitu kimempata na Kinape akiuliza basi afumue mzinga wa nyuki. Kinape wakati anatoka alishangaa kumkuta Kilole akilia kilio cha kwikwi.

“Shemu vipi?” Alimuuliza huku akimsogelea.

“Siamini kama unaweza kunifanya uliyonifanyia, sawa hunitaki kwa nini unataka kunivunjia ndoa yangu?”

“Kilole mbona sikuelewi!” Kinape alishangaa kusikia habari zile.

“Kinape nimekufanya nini?”

“Subiri usiondoke uone unyama ulionifanyia, nikiachika utapata faida gani?” Kilole alisema kwa sauti ya kilio.

“Mbona sikuelewi nimekufanyia nini?” Kinape alizidi kushangaa.

“Nimekuambia subiri halafu uniambie kama ulichokifanya ni haki.”

“Fanya haraka nimeomba ruhusu mara moja nifuate kalatasi hizi.”

Kilole alikwenda chumbani na kuchukua picha chafu walizopiga wakifanya mapenzi na kumpelekea Kinape aliyekuwa amesimama wima akimsubiri huku akionesha wasiwasi.

Alipofika alimpa baadhi ya picha na zingine kuziacha ndani, Kinape alipokea bahasha ya picha na kuanza kutoa picha moja, alishtuka kuziona picha zilizoonesha wakifanya mapenzi na Kilole.

“Ha! Hizi nini?” Kinape alishtuka huku akiendelea kuchambua picha.

“Nikuulize wewe, kwa nini umeamua kunidhalilisha kiasi hiki, kumbe ulikuwa na lako jambo, hebu fikiria picha hizi zimfikie mume wangu mimi nitakuwa mgeni wa nani?” Kilole aliangua kilio cha uongo na kuzidi kumchanganya Kinape.

“Wewe hizi picha umezitoa wapi?” Kinape aliuliza huku jasho la hofu likimtoka.

“Kuna mtu kazileta anasema kaziiba kwa jamaa mmoja ambaye amekula naye njama ili kunidhalilisha,” Kilole alisisitiza kama kweli.

“Nioneshe huyo aliyeleta picha hizi aeleze kazitoa kwa nani na huyo mwenye picha aseme kama mimi ndiye nilifanya mpango huu. Haki ya nani, leo ndiyo naziona hizi picha, sijui lolote maskini wa Mungu,” Kinape alizidi kujitetea.

“Kinape umebadilika baada ya kunivua nguo, shukurani yako kunidhalilisha, kwa taarifa yako najua kabisa nipo uchi pengine si mmoja aliyeziona kuna wengi. Pia wasiwasi wangu huenda zingine zimebaki na hizi ni baadhi ya hizo picha.

“Kwa maana hiyo bora nimweleze ukweli mume wangu na kumuonesha hizi picha nijue moja, anisamehe kwa kumuomba msamaha au aamue atakacho amua kwa vile siwezi kumlilia mtu. Inawezekana kabisa ulifanya makusudi ili niachike baada ya kuona nilikusaliti.”

“Kilole sijui nikueleza kitu gani ili unielewe, haki ya nani sijui lolote kuhusiana na hizi picha, pia nakuomba usimuoneshe mumeo wala kumueleza tulivyo hujumu ndoa yake, ni hatari si unajua jamaa ana bastora anaweza kuniua.”

“Naweza nisimwambie na kukaa kimya, kumbuka nimetoa laki tano ili nipewe hizi picha, kama zipo zingine wanashindwa nini kumuuzia mume wangu. Akijua uchafu wetu sura zetu tutaziweka wapi?” “Yaani nichechanganyikiwa hata sijui nikwambie nini.”

“Kinape hii ni hatari.”

“Kweli ni hatari tena kubwa, hivi Deus anavyoniamini nitamwambia nini akiona hizi picha?”

“Ndiyo maana nikaona bora nijisalimishe kwa mume wangu sina jinsi, kama picha hizi zikimfikia tumekwisha.”

“Mmh! Yaani hata sijui nani kafanya mchazo mchafu kama huu?”

“Unajua kila kitu lakini unanizunguka, kwani Kinape hapa jiji wapo wangapi?”

“Siwezi kujua labda wapo wengi.”

“Ina maana hiyo Kinape pia ni ndugu yake Deus.”

“Mmh! Yaani aliyeleta kasema hivyo?”

“Tena inasemekana umempa laki tatu, ndio maana kataka laki tano ili anipe picha.”

“Yaani, nimechanganyikiwa hata nguvu zimeniisha,” Kinape alisema huku akiketi kwenye kochi baada ya nguvu kumwisha ghafla.

“Kinape nilikuwa na maamuzi mawili?”

”Yapi hayo?”

“Moja la kujisalimisha kwa mume wangu, la pili kumuwahi Deus kabla picha hazijamfikia.”

“Utamuwahi vipi?”

”Ikiwezekana hata kumuua huoni hili likifika kwa wazazi litakuwa baya zaidi.”

“Mmh! Tumefika mbali sana huo si mpango mzuri.” Kinape alipinga mpango ule.

“Basi kama hatuwezi tumwambie.” “Bado huo si uamuzi sahihi.”

“Sasa tufanye nini?” “Tutafute njia nyingine zaidi ya hii.”

“Mimi nina siri za mume wangu kama tutazifikisha Takuru lazima atafungwa.”

“Sasa wewe utabaki na nani?”

“Na wewe.”

”Na Happy?”

“Kwa ulichokifanya heri niwe na wewe kwa vile siwezi tena kurudi kijijini.”

“Hapana, basi tutafute njia nyingine.”

”Hiyo nyingine nipe wewe.”

“Sina.”

“Basi wacha ninywe sumu ili ufurahi siwezi kuona nahukumiwa kwa kosa la kwako.

” Kilole alimtishia Kinape.

“Usinywe sumu bado tunaweza kujipanga kuhakikisha tunamdhibiti.”

“Nakupa siku moja kuhakikisha unapata ufumbuzi bila hivyo nitakacho amua tusilaumiane.” “Lakini naomba usimwambie kwanza Deus,” Kinape alijikuta akichanganyikiwa baada ya kukosa jibu la tatizo lililokuwa mbele yake.

“Ni wewe wa kunifanya nisimwambie, nataka kabla habari hizi hazimfikia tuwe tumekwishajua tumefanya nini.” “Nimekuelewa, yaani hata kazini sirudi nguvu zimeniisha,” Kinape alichanganyikiwa. “Kinape wewe mwanaume unatakiwa kuonesha unaweza kukabiliana na chochote kinachotokea mbele yako. Mbona mimi niliyetendewa sijachanganyikiwa zaidi ya kupanga mikakati ya kujiokoa na janga hili.”

“Najua huwezi kunielewa sijui lolote kuhusiana na hizi picha, kwa kweli zimenichanganya sana.” “Kwa kusema hivyo ina maana nimezipiga mimi?”

“Hapana sina maana hivyo, ila nimechanganyikiwa sijui hata nani aliyefanya mchezo mchafu kama huu.”

“Ndiyo tunatakiwa tutafute njia ya kujiepusha, kumbuka hili ni bomu likipasuka hakuna atakayepona.”

“Basi inawezekana alipoondoka aliweka mpelelezi ili atufuatilie.”

“Atufuatilie kwani anajua chochote kuhusiana na penzi letu la zamani?”

“Inawezekana kuna mtu anayetujua alipotuona tupo pamoja alimweleza na kuamua kufanya upalelezi.”

“Aweke asiweke lazima tutumie njia ya kumdhibiti kabla hajafanya lolote.”

“Sasa tutamdhibiti vipi?” “Kwa nini tusimuwekee sumu afe,” Kilole alisema bila wasiwasi. “Kilole mbona mpango huo ni mbaya!”

“Unafikiri tukimchelewesha akigundua lazima atatuua kwa risasi.”

“Tukimuua tutakosa fadhira hata Mungu atatulaani, tutafute njia nyingine ya kumdhibiti, ngoja nitoke nikirudi nitakupa jibu ila nakuomba chonde usimueleze Deus chochote kuhusiana na habari hii.”

“Siwezi hata mimi natamani kuishi maisha marefu.”

Baada ya kukubaliana Kinape aliondoka na kumwacha Kilole akifurahia mpango wake umekwenda kama alivyopanga. Aliamini jioni akirudi cha kwanza kitakuwa kuvunja uchumba wake na Happy kisha mengine yangefuata ya kumdhibiti Deus ili abaki na Kinape.

Deus akiwa ofisini kwake akipitia ripoti ya uchunguzi wa wauzaji sugu wa madawa ya kulevya, simu toka kwa sekretari wake iliita. Alipokea mkono mmoja, mwingine ukiwa bado umeshikilia kwenye kalatasi ya ripoti.

“Haloo, ofisi ya kuzuia madaya ya kulevya hapa, nazungumza na nani?”

“Msamalia mwema.”

“Ndiyo Msamalia mwema, nikusaidie nini?”

“Mkuu, ndege ya shirika la Swiss air, inayoingia saa kumi na moja jijini Dar kuna dada mmoja mwenye umbile la kati maji ya kunde nywele za kipilipili, amevalia gauni fupi jekundu chini viatu virefu na kwapani atabeba mkoba wa rangi sawa na nguo zake.

”Pia anaweza kuwa miwani ya rangi hiyo hiyo kama atakuwa ameivaa kama ataivua basi chukueni vigezo nilivyo waeleza. Dada huyu ana dawa za kulevya mkamateni na kumpekua.”

“Samahani unazungumza toka wapi?” “Si muhimu kujua zaidi ya kufuatilia taarifa niliyokupa, asante.” “Haloo…haloo…”

Deus alichelewa simu ilikuwa imekatwa. Alinyanyuka na kutoka hadi kwa sekretari kuulizia simu inatoka wapi.

“Haloo Happy, simu inatoka wapi?”

“Namba zinaonesha inatoka Itary.”

“Asante,” Deus alijibu na kurudi ofisini kwake. Alijikuta akijiuliza aliyetuma taarifa na kujiita msamalia mwema alichokisema kina ukweli au ndiyo kutaka kuwasumbua. Lakini hakutaka kuipuuza taarifa ile, aliwaita vijana wake na kuwapa habari zile na kuwaeleza wafuatilie ndege ile kama kweli yupo huyo mwanamke basi akamatwe na kupekuliwa.

Kwa vile ilikuwa imebakia saa moja kabla ya ndege kuingia, aliwahimiza vijana wake kufika eneo husika kabla ndege haijafika. Baada ya kuwapa majukumu vijana wake aliendelea kupitia ripoti ya wauza dawa za kulevya sugu.


Majira ya saa kumi ndege ya shirika la ndege la Swiss air iliwasiri uwanja wa ndege wa mwalimu JK Nyerere. Vijana wa Deus alikuwa katika kona yao kama kawaida. Baada ya ndege kusimama na mlango kufunguliwa waliteremka abiria mmoja mmoja waliokuwa katika mistari.

Dada mmoja maji ya kunde mwenye nywele fupi gauni jekundu fupi lililoishia juu kidogo ya magoti na viatu virefu alikuwa mmoja ya abiria katika ile ndege. Baada ya kutoka kwenye mlango wa ndege hakuteremka haraka aliangalia mandhali ya Tanzania kisha alivaa miwani yake nyekundu na kuteremka taratibu kwenye ngazi za ndege na kuelekea kwenye ukaguzi.

Vijana wa Deus hawakupata shida ya kumuona yule binti aliyeonekana mrembo tena bado mbichi. Walitegemea kusikia chochote kutoka sehemu aliyopitia, lakini alipita salama. Hawakuwa na haraka ya kumkamata walisubiri kuona yupo na nani pia mizigo yake.

Baada ya kutoka chumba cha usafiri alielekea kwenye gari aina ya Ranger Rover ‘Vogue’ ya rangi nyeusi iliyokuwa umepaki pembeni. Alipokaribia mlango ulifunguliwa, kabla hajaingia kikosi cha kuzuia dawa za kulevya kilifika na kujitambulisha kisha walimweka chini ya ulinzi msichana yule ambaye hakuonesha wasiwasi.

“Jamani vipi?” aliuliza huku akitoa miwani usoni. “Sisi ni askari wa kikosi cha kuzuia dawa za kulevya, tuna wasiwasi na wewe.”

“Mna wasiwasi gani?” “Tunaomba ufike kituoni kwa ajili ya upekuzi.” “Mbona mnanishangaza, ina maana wakaguzi wa kiwanjani hawafai?” Aliuliza kwa kuwashangaa askari wale.

“Samahani tunaomba ufuate maelekezo yetu.”

Wakati huo gari lao lilisimama pembeni yao na kumuomba aingine ndani ya gari. Kabla ya kuondoka yule msichana aliwaomba vitu vyake vitangulie nyumbani.

“Jamani vitu vyangu si hivi ngoja nivifungue hapahapa ili muone nimeweka wapi hayo madawa ya kulevya,” Alisema yule msichana huku akifungua pochi yake na kuvimwaga vyote vilivyokuwa ndani ya pochi kisha alitaka kufungua brif case ili vitu vilivyomo ndani avimwage chini waone kuna nini. Lakini walimkataza asifanye vile kwa vile kuna sehemu zake.

“Dada kwani tatizo lako nini, wewe twende ofisini, sisi tumetumwa tukukamate mengine anajua mkuu wetu, ingekuwa hatukutumwa wala tusingekusumbua,” askari mmoja alisema.

“Lakini kumbukeni nimechoka natakiwa kupumzika.”

“Tunajua, lakini sisi tumetumwa, hatuwezi kurudi mikono mitupu wakati mtu tuliyetumwa tumemuona.”

“Nani anayenifahamu na kuwatuma mje mnikamate, kumbukeni nitashitaki kwa kunidhalilisha,” binti yule alitishia. “Hatujakudhalilisha kwa vile hakuna mtu anayejua kinachoendelea hapa, zaidi ya wewe kumwaga vitu vyako bila kukuambia.”

“Basi turudini chumba cha ukaguzi uwanja wa ndege ili mnikague, ili niwahi nyumbani kuna mtu nimeahidiana kukutana naye.”

“Dada kuwa mwelewa, si wewe umevaa gauni jekundu?” Askari mmoja alimuuliza akisoma karatasi bila kumtazama. “Ndiyo.”

“Pochi yako nyekundu?”

“Ndiyo.”

“Miwani nyekundu?” “Ndiyo,”

“Na viatu vyako virefu?”

“Ndiyo.”

“Nywele zako za kipilipili?”

“Ndiyo.”

“Rangi maji ya kunde?”

“Ndiyo.”

“Sasa dada haya tumeyajulia wapi sisi?”

“Hata mimi nashangaa sijui nani anataka kunichafua?”

“Ungekuwa na tofauti na hii iliyoandikwa kwenye karatasi tusinge kugusa lakini kila kilichoandikwa kwenye karatasi unacho kwa asilimia mia,” walimweleza huku akimpa karatasi iliyokuwa na maelezo yote.

Askari walikuwa na uhakika kwa pale hakukuwa na ushahidi wowote kuwa yule dada kaingia na dawa za kulevya. Hata kama ilikuwa biashara yake siku ile walikuwa wamechemsha.

“Mmh! Sina jinsi twendeni lakini mnanipotezea muda bure,” alijitetea yule msichana aliyeonekana kujiamini katika mazungumzo yake.

Kama isingekuwa amri toka kwa mkubwa, waliona hakuna haja ya kumpoteza muda wake bure wangemuachia. Lakini vigezo vyote walivyoelezwa na mkuu wao Mr Deus ndivyo alivyokuwa navyo kwa asilimia mia. Hivyo hawakuwa na budi kumpeleka kwa mkuu wao. Walimuingiza kwenye gari na kumpeleka makao makuu kwa ajili ya upekuzi. Kabla ya kuondoka aliomba mkoba wake ambao hauna kitu utangulie nyumbani.

“Sasa kaka zangu kwa vile mkoba wangu hauna kitu naomba basi utangulie nyumbani.”

“Dada yetu haturuhusiwi kupoteza ushahidi wowote uliokuja nao, vyote vinatakiwa ili kukamilisha ushahidi.”

“Hakuna tatizo,” alijibu kwa kujiamini kitu kilichowafanya askari waamini hana kosa.

“Sasa Teddy itabidi nikufuate?” Dereva wa Ranger Rover alimuuliza mgeni wake.

“Noo Danny, tangulia nyumbani nitakuja sasa hivi kwa vile nakwenda kukamilisha walichotumwa na mkuu wao. Lakini kwa upande wangu sina tatizo lolote.”

Maneno ya kujiamini ya msichana yule yalikuwa na nguvu kubwa ya askari kumuachia lakini kwa vile walikuwa wakitimiza agizo la mkubwa wao hawakuwa na budi kumpeleka.

Walimuingiza kwenye gari na kumpeleka makao makuu kwa ajili ya kutimiza wajibu wa kazi. Walipofika walimpitisha chumba cha upekezi na kufanya upekuzi wote wa awali ambao haukuonesha dawa za kulevya. Taarifa alipelekewa mkuu wao Mr Deus.

“Mkuu hana kitu chochote.” “Mmempekuwa vizuri?”

“Ndiyo mkuu.”

“Mmetumia vifaa vya kisasa?”

“Vyote mkuu.”

“Mmempa chakula kigumu?”

“Kila kitu ujuacho tumekifanya lakini hatukumkuta na dawa.”

“Sasa aliyenipigia simu alikuwa na maana gani?”

“Kwani taarifa zimetoka wapi?” “Kwa msamalia mwema mmoja toka Itaria.”

“Ni kweli dada huyu anatoka Itaria.”

“Ina maana alikuwa anatudanganya?”

“Mkuu, huenda kweli anashughulika na biashara hii, lakini huenda njia aliyotumia si ile ambayo mtu aliyetutumia taarifa anaijua.”

“Inawezekana.”

“Lakini mmemuonaje?”

“Kwa kweli haoneshi wasiwasi zaidi ya kulalamikia muda wake.”

“Sasa fanyeni hivi mfuatilie mpaka atakapofikia fanyeni dolia usiku kucha ili tupate kujua kama kasingiziwa au ndiyo kazi yake.”

“Tutafanya hivyo mkuu.”

“Basi kamwachieni aende.” Kabla kijana wake hajaondoka alikumbuka kitu kimoja na kumwita.

“John hebu rudi kwanza.”

“Ndiyo mkuu.”

“Hebu mleteni hapa kabla ya kuwachia kuna maswali mawili matatu nataka kumuuliza.”

“Hakuna tatizo mkuu.”

John alitoka baada ya muda alirudi na yule msichana aliyekuwa mrembo kwenye macho ya mwanaume.

“Shikamoo,” yule msichana alimsalimia Mr Deus. “Marahaba, hujambo?”

”Sijambo mkuu.”

“Karibu ukae,” alimwambia huku akimuonesha sehemu ya kukaa.

“Asante,” Alijibu huku akikaa kwenye kiti. Baada ya ukimya mfupi Mr Deus alituliza macho kwa binti yule ambaye alikuwa ameinama chini. “Unaitwa nani?”

“Thereza Mayunga.”

“Ni Mtanzania?”

“Ni Mtanzania mwenye uraia wa Itaria.”

“Naomba Paspoti yako.” Teddy alifungua mkoba wake na kutoa paspoti na kumkabidhi Mr Deus, aliipokea na kuisoma kwa muda kisha alimrudishia.

“Okay, Wazazi wako wapo wapi?”

“Kwa kweli siwajui, ila niliambiwa niliibiwa nikiwa na umri wa miaka mitano na mwanamke mmoja aliyekuwa akikaa Itaria ambaye alinifanya mwanaye mpaka alipokaribia kufa ndipo aliponieleza kuwa wazazi wangu wapo Tanzania ila hakujua wapo wapi. Pamoja na kuniiba bado jina langu na la baba yangu hakulibadilisha.”

“Una shughulika na nini?”

“Ni mfanya biashara wa vitu mchanganyiko.”

“Hapa Dar unafikia wapi na kwa nani?”

“Nafikia Masaki kwa ndugu wa marehemu mume wangu.”

“Mumeo alikuwa Mtanzania?”

“Ndiyo.” “Okay, unaweza kwe…” Mr Deus kauli yake ilikatwa na mlio wa simu ulioingia kwenye simu yake. “Samahani,” alisema huku akipokea simu. “Bila samahani,” alijibu Teddy. Mr Deus alipokea simu na kuzungumza kwa sauti ya chini. “Eeh.”

“Mkuu simu ile ya Italia.”

“Okay, nipe nizungumze naye.”

“Haloo.”

“Haloo mkuu.” “Ndiyo.”

“Mmemuona?”

“Hebu subiri kidogo,” Mr Deus alisema huku akimuomba yule msichana amsubiri nje mara moja. “Hakuna tatizo,” alijibu yule binti huku akinyanyuka na kutoka nje. Baada ya kutoka Mr Deus alirudi hewani.

“Ehe! Msamalia mwema.”

“Nauliza mmemuona?”

“Ndiyo.”

”Mmepata hayo madawa?”

“Hatujayapata.”

“Nilijua hamuwezi kupata kitu.”

“Sasa kama ulijua hatupati kitu kwa nini umetusumbua?”Mr Deusi aliuliza kwa sauti hya ukali kidogo. “Siyo kuwasumbua, niligundua nilifanya kosa katika maelezo ya kuyapata hayo madawa, ndiyo maana nimepiga tena simu haraka.”

“Kwa hiyo tutakuwa basi tumechemsha.”

“Bado hamjachemsha.”

“Tusaidie jinsi ya kuyapata.”

“Mkoba wake mwekundu anao?”

“Ndiyo.”

“Basi huo ndio wenye dawa hizo.”

“Mbona tumempekua hatujaona kitu?”

“Huyo dada ni muuzaji wa kimataifa wa dawa za kulevya, hata siku moja hamuwezi kumkamata kirahisi.”

“Tusaidie basi tujue ameficha wapi?”

“Huo mkoba wake umeshonwa maalumu kwa ajili ya kuvusha dawa za kulevya, una karatasi za lailoni ambazo haziwezi kuruhusu vipimo vyenu kuona ndani kuna kitu gani. Juu kuna manyoya hufanya mkoba huo mtu yeyote asiutilie wasiwasi. Kwa mtindo huo, umemfanya mwanamke huyu aendeleze biashara yake haramu ya dawa za kulevya bila kushikwa.”

“Kwa hiyo una maanisha mkoba alishonwa na dawa zake kabisa?”

“Ndiyo maana nikasema huyo dada ni muuzaji wa kimataifa, huzunguka sehemu zote bila kukamatwa na kumfanya aweze kujikusanyia fedha nyingi kila kukicha.”

“Una uhakika na unachokisema?”

“Kwa nini nimewapa picha jinsi alivyo na mmempata bila tatizo, kuna kitu nilichowaeleza akakataa?” “Mpaka sasa upo sahihi.”

“Basi pasueni mkoba wake mtanipa jibu, asante.”

Baada ya kusema vile alikata simu. Baada ya simu kukatwa, Deus alitumia dakika tano kutafakari maneno ya mtu aliyejiita msamalia mwema ili kutoa uamuzi ambayo kama utakwenda kinyume unaweza kumuhalibia sifa. Aliamuru yule mwanamke aingie, aliitwa na kuingia ndani na kukaa kwenye kiti. “Samahani,” alianza Mr Deus kumtaka radhi Teddy. “Bila samahani mkuu.”

“Naomba uniambie ukweli kuhusu sehemu ulipoficha dawa za kulevya.”

“Nimeeleza kila kitu, sasa mnataka nini? Sijui lolote juu ya dawa za kulevya nashangaa kunihusisha na biashara hatari kama hizo.”

“Naomba nifanye upekuzi kwenye mkoba wako.” “Huu hapa angalia,” Teddy alisema huku akiuweka mkoba wake juu ya meza.

“Kabla sijaupasua naomba uniambie ukweli juu ya kuficha dawa za kulevya.”

“Mkoba si huo hapo fanyeni muwezavyo utajua ukweli kuwa sihusiki japo kuwa watu wananipaka matope,” Teddy alisema kwa kujiamini. Mr Deus aliagiza kisu ili aupasue mkoba mbele yake, Kabla hajaupasua Teddy alimtaadhalisha.

“Kumbuka mkoba huu nimeununua pesa nyingi robo ya bajeti ya wizara moja kubwa katika serikali yako.” “Hiyo siyo juu yako.”

“Sema unataka shilingi ngapi ili usiharibu mkoba?”

“Sihitaji fedha yoyote zaidi ya kuupasua mkoba huu.” “Haya fanya uwezavyo lakini mwisho wa siku utaumbuka.”

Mr Deus hakumsikiliza alichukua kisu na kuanza kuupasua mkoba ili kupata uhakika kwa yale aliyoelekezwa na msamalia mwema. Alipoanza kuupasua mkoba Teddy aliomba asitishe zoezi. “Samahani mkuu.”

“Bila samahani,” Deus alijibu akiwa amesitisha zoezi la kuupasua mkoba.

“Naomba tuzungumze.” “Tutazungumza nikimaliza, fedha ya robo bajeti ya wizara hata mimi naweza kuilipa peke yangu wala usiwe na wasiwasi,” Mr Deus alijibu huku akinyanyua kisu kukididimiza kwenye mkoba.

“Naomba unisikilize kaka yangu,” Teddy alikuwa mpole ghafla.

“Juu ya nini?”

“Kuhusu huo mkoba.”

“Una nini?”

“Samahani kaka yangu naomba unisilize mdogo wako.”

Mr Deus aliacha kuuchana mkoba na kumgeukia Teddy aliyekuwa akitokwa na jasho japo ofisi ya Mr Deus ilikuwa na kiyoyozi kikali.

“Mhu! Unasemaje?”

“Najua nimepatikana, lakini naomba msaada wako?” “Umepatikana kivipi na unaomba msaada upi?”

“ Kila ulichoelezwa ni kweli?”

“Na nani?”

“Simjui, lakini inaonekana ananijua vizuri, sasa nifae kwa mvua nitakufaa kwa jua.” “Sijakuelewa,” Mr Deus alimshangaa Teddy.

“Ni kweli mfuko huu una dawa na kwa sasa nipo chini ya ulinzi na ukinifisha mahakamani nitafia gerezani, umri wangu bado mdogo. Nakuomba uniokoe kwa hili nipo radhi kukupa kiasi chochote ukitakacho hata ukiacha kazi unaweza kula miaka hamsini bila tatizo.”

“Lakini unajua dawa za kulevya ni haramu?” “Najua, na ndiyo maana nipo chini ya ulinzi.” “Sasa nikiwasikiliza wote tutamkamata nani?”

“Yaweza usione umuhimu wangu kwako leo, lakini kwangu mimi wewe ni mtu muhimu kama malaika mtoa roho aliyeahilisha kuchukua roho mama mzazi muda mfupi baada ya kujifungua.”

“Kwa ubinaadamu ni kweli nilitakiwa kukusaidia, lakini kwa vile ni dhamana niliyopewa na taifa sina budi kuwa na uso wa mbuzi.”

“Si kwamba nakulazimisha au nakufundisha kazi, hata hao wakubwa zako waliokutuma wanapokea mrungula. Amini usiamini kuna viongozi katika serikali yako hata viongozi wa dini mwenye heshima katika taifa hili wanaifanya biashara hii. Unaweza kunikamata na nikafungwa, lakini bado utakuwa umechota kikombe cha maji kwenye bahari hutapunguza kitu. “Nina imani msaada wako leo unaweza kukusaidia siku za mbele, mbegu ya wema siku zote haiozi.

Naomba unisaidie kwa leo nina imani nitakapotoka huwezi kujilaumu kwa msaada wako. Sema kiasi chochote ukitakacho hata kikipita fedha za mzigo huu nipo tayari kukupa tena muda huu.”

Kauli ile ilimfanya Deus alitulie kwa muda huku akiona sura ya yule binti ilivyoonesha kuomba msaada wake. Kila alilolizungumza alililona lina uzito kwake. Taratibu moyo ulilainika na kuona kuna umuhimu wa kumsikiliza yule msichana.

“Unajua binti unanipa wakati mgumu,” Deus alisema kwa sauti ya chini.

“Kivipi kaka yangu?”

“Unajua vijana wangu wakiona nakuachia wakati mimi ndiye kiongozi wao watanielewaje?”

“Sikiliza mkuu hakuna hata mmoja anayejua huku ndani kipi kinaendelea, wengi wanajua ni mazungumzo ya kawaida.”

“Mmh! Sasa kwa kesi nzito kama hii unanipa kiasi gani?”

“Chochote ukitakacho utakachokiona kinalingana na kosa hili.” “Kwa vile wewe ndiye uliyetangaza biashara kusema ili nione kama kinalingana na kosa lenyewe.”

“Lakini huu mzigo si utaniachia?”

“Itategemea na kiasi cha mzigo utakaotangaza.”

“Milioni 50.”

“Hailingani na kosa lako, kumbuka hapa nauza kazi naweza hata kufungwa maisha ikigundulika.”

“75.”

“Okay, nisikuumize sana nipe hizohizo.”

“Na mzigo wangu?”

“Utaondoka nao, nitapataje mzigo wangu?”

“Kama una kijana wako nimuagize aende sasa hivi akachukue mzigo mimi nikiwa hapa akipata utaniruhusu niondoke.”

“Itakuwaje?”

“Nampigia simu mtu ukisikia kisha unanipa mtu wako nimuelekeze akachukue.”

“Okay, fanya hivyo.”

Teddy alichukua simu yake iliyokuwa mezani na kubofya namba kisha alisema:

“Haloo Tonny.”

“Eeh, Teddy.”

“Andaa milioni 75 kuna mtu atakuja muda si mrefu.”

“Hakuna tatizo, nitamtambuaje?”

“Nitakujulisha.” Teddy alikata simu na kumgeukia Mr Deus aliyekuwa akishangazwa na uwezo wa kifedha aliokuwa nao binti yule.

Alikubaliana na kauli ya mtu aliyejiita msamalia mwema kuwa binti yule ni mfanya biashara mzoefu pia mwenye utajiri mkubwa.

“Basi mjulishe huyu mtu wako ili nimwelekeze akachukue mzigo.”

“Hakuna tatizo ngoja nimpigie ili nikupe umuelekeze,” Deus alisema huku akichukua simu na kumpigia rafiki yake Kinape afuatilie dili lile.

“Haloo Kinape upo wapi?”

“Ndiyo natoka kazini.”

“Hebu zungumza na dada huyu akuelekeze sehemu akakupe mzigo wangu.”

“Hakuna tatizo,” Deus alimpa simu Teddy ambaye alimuelekeza sehemu ya kukutana ampe mzigo huo. Baada ya maelekezo Teddy alimgeukia Deus na kumuuliza.

“Nina imani utaamini kwamba mimi si mtu wa kubabaisha.”

“Mpaka tutakapo maliza kazi.”

Mr Deus alinyanyua simu na kumwita secretary wake, baada ya muda alifika na kukakamaa kikakamavu mbele ya mkuu wake.

“Abee bosi.”

“Mletee mgeni kinywaji.”

“Sawa mkuu.” Aligeuka na kuondoka, baada ya muda alirudi na sahani iliyokuwa juisi ya paketi na glasi mbili. Aliweka juu ya meza na kuwawekea wote kisha aliwakaribisha.

“Karibuni Juisi dada.”

“Asante,” alijibu Teddy huku akichukua glasi ya juisi moyo wake ukiwa umeanza kutulia. “Lete stori,” Deus alivunja ukimya.

“Ninalo kaka yangu, nakuahidi si leo si kesho msaada wako hutaujutia.”

“Kwa nini mnakaa na fedha nyingi kiasi hicho ndani?”

“Kaka yangu kazi yenyewe bila ya kuwa na fedha za haraka unaozea gerezani.”

Wakati wa mazungumzo simu iliingia toka kwa secretary, alipokea na kuzugumza.

“Simu ya Italia mkuu.”

“Niachie.”

“Haloo.”

“Ndiyo msamalia mwema?”

“Vipi mzigo umeuona?” “Kazi umeisha tupa tuachie tuifanye,” Deus alijibu kwa jeuri kidogo.

“Mkuu sina maana ya kukufundisha kazi bali kufanikisha kukamatwa kwa huyo malaya.”

“Asante kazi inakwenda vizuri.” “Mmeziona?” “Hiyo si kazi yako.”

“Sawa mkubwa mara hii nimekuwa adui?” “Siyo adui tunashukuru kwa msaada wako mambo mengine ni siri ya ndani hatakiwi mtu mwingine kujua.”

“Nakutakia kazi njema.”

“Na wewe pia.”

Baada ya kukata simu Teddy aliyekuwa akifuatilia mazungumzo yale alijua mbaya wake bado alikuwa akimuandama kwa kufuatilia mpango wake.

“Samahani mkuu.”

“Bila samahani.” “Naomba nimjue huyo mtu.” “Hapana ni siri ya jeshi.”

“Kaka yangu nipo radhi kukuipa pesa ile mara mbili ili nimjue tu.” “Ukimjua?”

“Basi tu nitakaa naye mbali.”

“Kwa kweli amekataa kutaja jina lake zaidi ya kujiita msamalia mwema.”

“Anatokea wapi?”

“Italia.”

“Asante kwa msaada wako.”

Mara simu iliita, Teddy aliipokea na kusema: “Eeh! Tayari hebu mpe simu nizungumze naye,” Baada ya kupewa alizungumza:

“Eeh! Umefika?” “Ndiyo.” “Hebu zungumza na mkuu hapa,” alimpa simu azungumze na Kinape.

“Eeh! Kinape umefika?”

“Ndiyo.”

“Ni yeye,” Deus alimgeukia na kumwambia Teddy.

“Nipe simu.”

Baada ya kumpa alimwambia mtu wa upande wa pili.

“Tonny mpe mzigo mpe ulinzi mpaka atakapozifikisha salama.”

“Hakuna tatizo.” Teddy alikata simu na kumgeukia Mr Deus na kumuuliza:

“Utazipeleka wapi?”

“Nyumbani.”

“Naomba uzipeleke benki ni nyingi sana sitaki upoteze nguvu zako bure,” Teddy alimshauri Deusi.

“Sawa nitafanya hivyo.”

“Deus alipigia Kinape simu na kumweleza azipeleke benki katika akaunti ya Kinape yeye angezichukua baadaye.

Tonny alimsindikiza Kinape mpaka benki ambapo aliweka fedha yote aliyopewa kwenye akaunti yake. Baada ya kuweka alimpigia simu Deus kumjulisha.

“Mkubwa kazi imekwenda vizuri.”

“Amekupa zote?”

“Ndiyo.”

“Shilingi ngapi?”

“Milioni 75.”

“Ooh, vizuri umeshaziweka benki?”

“Ndiyo natoka sasa hivi.”

“Basi tutaonana baadaye nyumbani.” “Hakuna tatizo mkuu?” Deus baada ya kupata uhakika kwa Kinape alimgeukia Teddy aliyekuwa akiendelea kunywa juisi taratibu bila wasi kama hakuna kitu cha hatari kilikuwa mbele yake.

“Teddy,” alimwita.

“Abee.” “Nafikiri kila kitu kimekwenda vizuri.”

“Hakuna tatizo, naheshimu sana kazi yako pia muda wako.”

“Asante lakini kumbuka umeniweka katika wakati mgumu sana.”

“Kawaida tu kaka yangu, nakuapia ulichokifanya leo hutakijutia maishani kwako, huenda leo usione umuhimu wake lakini ipo siku utayakumbuka maneno yangu.”

“Basi wacha nikutoe ili ukapumzike na safari.”

“Na kweli muda huu ningekuwa nimelala, hata chakula ningekula jioni baada ya kuamka.”

“Pole sana ni harakati za maisha.”

“Tunaweza kwenda,” Deus alisema huku akinyanyuka na kuweka vitu vyake sawa kwenye meza. Teddy alinyanyuka na kuchukua mkoba wake wenye dawa za kulevya na kuuweka begani kisha alitangulia kutoka, alipofika kwenye korido la kutokea nje alisimama kumsubiri Deus kuogopa maswali kwa baadhi ya watu ambao angekutana nao njiani.

Baada ya kuweka ofisi yake sawa Deus alitoka na kumpitia Teddy kwa kumshika mkono, kwa mtu angewaona kwa mara ya kwanza angeamini wale ni marafiki wanaojuana muda mrefu.

Lakini kumbe muda mfupi walikuwa chui na paka. Walikwenda kwenye gari na kuondoka kumrudisha sehemu aliyofikia, lakini Teddy aliomba aachwe sehemu ambako ataingia kwenye gari litakalomfuata na kwenda kwake. Wakiwa njiani Teddy alianzisha mazungumzo.

“Nashukuru kwa ukarimu wako.”

“Japo unanishukuru, lakini kumbuka nimenilazimisha nimeisaliti nchi yangu kwa damana waliyonipa ya kulinda nchi yangu.”

“Huenda leo huijui faida yake lakini narudia kukuapia msaada wako hautakwenda bure, ila nilikuwa na wazo moja.” “Wazo gani?”

“Najua kazi hii umepewa na taifa lakini kuna maisha badala ya kazi.”

“Hayo najua, ulikuwa na maana gani?”

“Hivi ukistaafu utalipwa kiasi gani?”

“Kiasi cha kawaida.”

“Nina imani hakitaweza kuyaendesha maisha yako?” “Ni kweli kabisa.”

“Sasa unaona unafanya kazi ya mamilioni lakini mwisho wa siku unakufa maskini.”

“Ni kweli, lakini kazi yetu inalenga kujitolea na si kujitajirisha.”

“Wewe unasema hivyo wakati wakubwa zako wanaokutisha usichukue rushwa, wao ndiyo wanaongoza kuwa na utajiri wa kutisha.”

“Sasa wewe ulikuwa unanishauri nini?” “Nataka kupitia kazi yako uweze kufaidika ili mwisho wa siku ulie kivulini.”

“Kwa hiyo unanishauri nile rushwa.”

“Kula rushwa siwezi kukushauri nina imani hii si rushwa ya kwanza inawezekana umeisha kula nyingi, inaonesha kabisa unakula za kawaida mimi nilitaka tufanye biashara kwa muda mwaka mmoja uwe trionea.”

“Kazi hii ukiifanyia tamaa huchelewi kushtukiwa na mwisho wa siku unapigwa chini au unategewa mtego na ukinasa unafia gerezani.”

“Biashara hiyo nataka tufanye sisi wawili.”

“Kumbuka biashara hii mwisho wake mbaya kwa mfano ungekutana na mtu aliyekunywa maji ya bendera ya taifa si ungepotelea gerezani?” “Kabla ya kupotelea gerezani yeye kabla ya jioni jina lake lingebakia historia midomoni mwa watu.”

“Una maana ungemuua?”

“Siku zote kazi na dawa.”

“Nani angemuua wakati wewe umo ndani?”

“Mtandao ni mkubwa, miongoni mwenu kuna mtu angemuua.”

“Kwa nini mnamuua?”

“Kifo chake ni kupoteza ushahidi ili wakubwa wako wapate nafasi ya kunitoa kwa urahisi.” “Kama kuna wakubwa wanaweza kukutoa kwa njia hiyo, kwa nini hukuitumia kuliko kutoa fedha nyingi kiasi hicho?”

“Hii ni biashara kati yako na mimi hivyo lazima tukubaliane tukishindani lazima nitumie ya upande wa pili ambayo huwa sipendi kuitumia kwa kuamini kila mwanadamu ni muelewa wote tunatafuta kwa njia ya halali na haramu.”

“Kwa nini usiokoe fedha nyingi kuliko kutoa bila sababu.”

“Njia ya pili ina faida na hasara zake, faida ni kutoka salama lakini hasara zake kwanza kutoa uhai wa mtu ambao kwa kupitia uwezo wangu wa kifedha huwa sipendi kuutumia.

“Pili mara nyingi unaweza kutoka salama lakini mzigo wako ukapotea mikononi mwa dola, mara nyingi ukikamatwa kwanza taarifa zako zinafika katika vyombo vya habari hata kama ukitoka unakuwa umechafuka. Na mzigo nao unakuwa katika stoo kabla ya kuteketezwa hivyo inakuwa vigumu kuupata. Kama nitatumia njia ya kutoa fedha nyingi lakini ukiuza unarudisha faida japo kidogo.”

“Inaonesha una fedha nyingi, kwa nini usiachane na kazi hatari kama hii?”

“Hakuna mwanadamu anayetosheka fedha kila kukicha matajiri wanabuni miradi kuongeza kipato.”

“Lakini si kwa kazi kama hii.”

“Basi kwa taarifa yako kuwa watu wana fedha kufuru kwa kazi hii, kutokana na uwezo wao wamekuwa wakiwatuliza wenye viherehere. Hebu tuachana na hayo naomba tufanye kazi niliyokueleza awali, kwa muda mfupi nimeamini wewe ni mtu muhimu sana kwangu.”

“Kazi gani?”

“Kwa vile upo kwenye kitengo hiki naomba utumie cheo chako kufanikisha biashara hii. Nakuahidi kila safari yangu ikivuka salama una milioni 250.”

“Una sema?” Deus aliuliza kama hakusikia. “Nitakapopita salama, nikifika nyumbani nakukabidhi milioni 250 hata kabla sijafanya biashara.”

“Kwa mwezi utakuja mara ngapi?”

“Itategemea mara moja au mara moja kwa miezi miwili.”

“Naomba unipe muda wa kufikiria jambo hili.”

“Kama ningekuwa mimi wala nisingesubiri kwani kijua ndicho hiki, ila napenda kukuonya kitu kimoja.”

“Kitu gani?”

“Kama utakubali kuufanya mpango huu ambao nakuhakikishia kwa mwezi kupitia mtandao wangu utatengeneza bilioni moja.”

“Bilioni moja?”

“Ndiyo, watu wanne wakiingia kwa mwezi mmoja utakuwa na kiasi gani?”

“Nimekuelewa na nini ulichotaka kunionya?”

“Nakuomba chonde chonde mpango hatari kama huu usimshirikishe mkeo.”

“Kwa nini?”

“Wanawake nawajua mvizuri si waficha siri kwenye wakati mgumu, kosa lolote litalotokea kwenye ndoa anaweza kutumia kukuangamiza.”

Kauli ile ilimshtua Deus kwani mipango yote ya awali aliyofanya, mkewe ndiye aliyekuwa msiri wake. Lakini alikuwa mstari wa mbele kumshauri mambo ya kimaendeleo hata baadhi ya fedha za rushwa aliziweka kwenye akaunti ya mkewe.

“Deus najua kabisa ulimshirikisha mkeo mambo yako ya nyuma, lakini kwa hili naomba iwe siri yako. Watu wengi wanaocheza michezo michafu kama hii huwaua hata wake zao pale wanapoona wamegundua kazi zao za hatari zinazoweza kuwapotezea maisha.

Lakini sikushauri umuue mkeo, ila nakuomba ili uweze kuwa tirionea kwa muda mfupi kwani mtando una watu zaidi ya kumi mwezi mmoja wote wakipitia katika mikono yako salama utajikuta ukitengeneza bilioni mbili na nusu kwa mwezi, unataka Mungu akupe nini?”

“Nimekuelewa nina imani ukiwa tayari nijulishe, tutaifanya kazi.”

“Nashukuru kuwa muelewa, huwezi kuamini wewe ni mtu wa kwanza kumueleza mpango huu wa hatari. Naomba usinigeuke unaweza kunishangaa pamoja na umbile langu dogo lakini nitakachokufanya hutasahau maisha yako yote.”

“Ondoa wasiwasi kazi itafanyika.”

“Niteremshe hapa watu wangu wamenifuata, mambo mengine tumia namba yangu hii ya simu ambayo ni watu muhimu tu wanayoijua.

” Deus alimteremsha Teddy ambaye aliingia kwenye gari lenye tinted na kutoweka kwa mwendo wa kasi na kumwacha Deus akilisindikiza kwa macho huku akiuona utajiri mbele yake.

Baada ya Teddy mwanamke hatari katika kuuza dawa za kulevya kuondoka, Deus alijikuta akipoteza ujasiri wa kulitumikia taifa na kujikuta akiota ndoto ya utajiri kwa kujiingiza kwenye biashara ya madawa ya kulevya. Aliamua kurudi ofisini kumalizia kazi zake ili jioni akakutane na Kinape akiamini kabisa rafiki yake hawezi kumweleza mtu yeyote siri ile kama livyomkataza.


Wakati akiwaza yale rafiki yake Kinape alikuwa na furaha ya ajabu moyoni mwake, alipofika nyumbani Kilole alitaka kujua furaha yake inatokana na nini.

“Vipi mwenzangu leo mbona una furaha umeongezwa mshahara nini?”

“Sasa hivi mimi ni milionea.”

“Una maana gani kusema hivyo?” Kilole alihoji. Alimpa picha yote ilivyokwenda, Kilole baada ya kusikiliza taarifa ile alimweleza kitu Kinape. “Mungu mkubwa.”

“Una maana gani kusema hivyo?” “Sasa mpango wetu utakamilika.”

“Una maana gani?”

“Sasa hivi ni wakati muzuri wa kumpotezea mbali Deus.”

“Tusifanye hivyo.” “Shauri yako akigundua atakumaliza wewe.”

“Kwa hiyo unanishauri nini?”

“Kwa vile benki kuna milioni 75 zinatutosha kwangu nina milioni 24 huoni milioni 99 zitatusaidia kufanya mambo mazuri baada ya kumuua tutauza majumba yake mawili na magari kisha tutafungua mradi wowote wa kutuendeleza kimaisha na kuuhama mji huu.”

“Hapana tusimuue.”

“Lazima Deus afe, ikiwezekana kazi ifanyike leo usiku.”

“Hapana tusifanye pupa tunaweza kuozea gerezani au hata kunyongwa kama ikigundulika sisi ndiye tuliyehusika na kifo chake.”

“Sasa tufanye nini?” “Hebu nipe muda.”

“Muda gani Kinape, mchicha umeisha kolea nazi fedha za kutosha tunazo tunasubiri nini?”

“Japo lolote zuri halihitaji haraka,” Kinape alimtuliza Kilole aliyekuwa na pupa. “Mpaka lini?”

“Nipe siku mbili.”

“Na ziwe siku hizo mbili, ukizidisha utakuta mzoga wa mtu ndani.”

“Unataka kujiua?”

“Nani afe, nitamnyongelea mbali Deus.”

“Punguza pupa kila kitu kitakwenda vizuri.”

“Lazima nikueleze ukweli Kinape hakuna mwanaume chini ya jua ninaye mpenda kama wewe.”

“Hilo nalijua lakini yote uliyataka wewe.”

“Lakini kukubali kwangu kuolewa na Deus huoni faida leo hii akaunti yako kuna milioni 75 hukuwahi kuota kuingiza fedha kama hizi.”

“Mmh! Na kweli.”


Deus baada ya kazi alirudi nyumbani na kupokewa kwa furaha na mkewe huku Kilole akionesha mapenzi mazito kwa mumewe ili kumfumba macho kabla kumtendea unyama. Baada ya chakula cha usiku Deus alimtoa nje rafiki yake ili ampe taarifa za utajiri wa ajabu unaokuja mbele yake.

“Unataka kuniambia kwa mwezi utakuwa unaingiza milioni 1000?”

“Ndio maana yake, nataka baada ya muda nipabadilishe kijijini kwetu pawe kama peponi.”

“Mmh! Mshiko mzito kauli ya yule dada kwa miaka mitano dunia utaishika mkononi.”

“Yaani naona kama ndoto.”

“Ungekuwa mnoko ungeishia na virushwa vya milioni kumi.”

“Basi naomba siri hii isimpe mtu mwingine, nimekupa wewe mtu wa karibu hata mke wangu sitamwambia ni siri ya hatari sana.”

“Hii ni siri nzito siwezi kumwambia mtu.”

“Hujui dhamira yangu kwako, katika kila fedha itakayo ingia asilimia kumi nitachukua wewe.”

“Unataka kuniambia katika milioni 1000 zangu ngapi?”

“Milioni 100.”

“Wachaaa, usinitie uchizi kwa furaha.”

“Lazima nikujali nataka nawe kijiji upabadilishe wajue kweli watoto wao tumekuja kutafuta maisha.” “Kweli nimeamini wewe ni zaidi ya ndugu.”

“Nathamini urafiki wetu tumetoka mbali kumbuka ndoto zetu tulipanga kufanya nini?” Baada ya mazungumzo walirudi ndani, Kilole hakuwa na haraka ya kujua walichokuwa wakizungumza kwa kuamini yote angeyajua kupitia kwa Kinape. Usiku nao ulikuwa wa raha kwa Kilole kuendelea kuonesha kumjali mumewe kwa kumpa penzi tamu ambalo lilimpagawisha Deus na kujikuta akimuahidi mkewe gari la milioni 20.

Kilole alijisemea moyoni kuwa asali ile aliyomlambisha ni chambo cha kumuingiza kwenye mtego wamlipue hakuwa na mapenzi tena na mumewe na kumuona shetani wa roho yake aliyetamani afe wakati wowote ili afaidi penzi tamu la Kinape.

ITAENDELEA

Nyuma ya Machozi Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment