Hasara za kumwamini Mtu
Never trust a person that has left you down more than two times.Once was a wearing,twice was a lesson and anything more than that is simply taking advantage!
Tunazaliwa tukitegemea wengine kututunza na kutulinda, kwani vinginevyo tusingeweza kuishi. Tunahitaji chakula, mawasiliano ya mwili, fadhili, utulivu na usalama, kati ya wengine. Ana de la Mata, mtaalamu wa saikolojia katika Kituo cha Kisaikolojia cha Cepsim, anaelezea kuwa tuna msukumo wa kibaolojia wa kiasili ambao unatupelekea tuweze kuwasiliana na wale wanaotutunza na haswa kuwaamini,swala ambalo mala nyingi hutupatia maumivu makali pale tunapobaini tunaowapenda nakuwaamini wao hawaaminiki[msemo huu unaendana na ule usemao siyo wote wakuchekeao wanakupenda,wengine wapo tu kuona mwisho wako na wanatamani uwe mbaya].
Hivyo basi kabla hujaamua kumwamini mtu katika maisha yako iwe kiurafiki,kiundugu,kimahusiano,ujirani n.k ni vyema ukajitahidi kumfahamu mtu huyo kiundani zaidi kwani ni wengi wameumizwa kwasababu wamekurupuka kuwaamini wasiotakiwa kuaaminiwa.zifuatazo ni hasara za kumwamini mtu kwa asilimia kubwa;
Kujivunjia heshima
Hii inatokea pale ambapo unaamua kutoa siri zako nakumwambia ndugu au rafiki yako ukiamini itakuwa ni kati yenu wawili kumbe unasahau hakuna siri ya watu wawili, mwisho wa siku uliyemwambia nae anamwambia mtu mwingine na mtu mwingine mwisho wa siku inakuwa sio siri tena jambo linaloleta karaha kwako kwakumuamin na kumuambia hiyo siri yako.
kupata maumivu ya kifikra nakujiona umepoteza;
Inapotokea umemwamini mtu kupita kiasi itakupelekea kupata maumivu ya ndani na kifikra pale ambapo unatambua yule unayemwamini ni kama chui au mbwa mwitu kwako ambapo mda wowote anaweza kukulalua, hii inakuvunja moyo na mda mwingine inakufanya ujione umepoteza thamani yako machoni mwa watu lakini pia utaona kama umepoteza mda wako kwa kumwamini mtu ambaye siyo sahihi kwako.
Unapomwamini mtu kupita kiasi ni raisi kwake yeye kukudhuru wewe,
Inaweza kuwa kiafya, kiuchumi au kijamii mana imani unayokuwa nayo juu yake itakufanya uwe muwazi sana kwake nakumwambia kila kitu chako,suala hili litampa uwanja mkubwa kwayeye kukuumiza wewe nakufanya chochote anachotaka iwe ni kukuumiza kiafya au kiuchumi