Wakala wa Giza Sehemu ya Tatu
KIJASUSI

Ep 03: Wakala wa Giza

SIMULIZI Wakala wa Giza
Wakala wa Giza Sehemu ya Tatu

IMEANDIKWA NA: HASSAN O MAMBOSASA

*********************************************************************************

Simulizi: Wakala Wa Giza

Sehemu ya Tatu (3)

Alipiga hatua ndefu kuonesha kwamba hakuwa amefurahia maneno ya Fatma, alipofikia mlango wa kutokea nje alivutwa mkono kwa nyuma. Alipogeuka alimuona Fatms akiwa ana uso wa huruma sana akiwa anatikisa kichwa kukataa jambo, Fatma alikuwa akikataa Norbert asiondoke na alikuwa akimtazama Norbert ambaye hakuonesha mzaha katika uso wake.

        "Fatma nini achia mkono wangu niwahi nikafanye booking unanichelewesha" Norbert alimuambia.



            "Norbert please nisamehe nimekosea" Fatma aliongea kwa huruma.



        "hujakosea Fatma sema mimi niliyekuja kuleta uhusiano kazini nimekosea ukaniumbua wacha niondoke nikafanye booking hujui nina haraka ya kiasi gani" Norbert aliongea huku akiutoa mkono wa Fstma na binti huyo chozi likaanza kumdondoka hapohapo, chozi lake liligeuka machozi akawa anamtazama mzee wa warembo huku akizidi kuyadondosha machozi.



Hakika alikuwa hajiwezi kwake na kauli yake mbele ya haraka ya Norbert kuingia Dar es salaam aliiona chungu, hakujua Norbert alikuwa kaingia vipi Arusha alichojua yeye ni kuweka wivu mbele tu.



         "Nor please usiniumize naomba rudi nitakufanyia mpango uondoke na ya juoni hii" Fatma aliongea kwa uchungu pasipo kujali yupo katika eneo la kazi, upungufu wa watu jioni hiyo ambapo wengine walikuwa tayari wamepitiliza kwenda kuketi kwenye ndege kusubiri ndiyo ulifanya pasiwepo na mtu mwenye kupata faida juu ya maongezi hayo.



         "Rudi sehemu ya kazi" Norbert alimuambia.



         "Nor please usinikasirikie njoo nikupe tiketi nataka niondoke sasa hivi shift nishamaliza namsubiri mwenzangu aingie yupo anabadili nguo" Fatma alimuambia Norbett huku akiwa bado anatokwa na machozi.



        "Ok" Norbert alikubali kisha akarudi eneo la dawati mapokezi, Fatma alimpatia tikiti ya shirika la ndege la Precision, Norbert aliipokea ile tikiti kisha akaanza kuisoma halafu akaifunga akamwangalia Fatma usoni.



       "Bado nusu saa ndege iondoke" Fatma alimwambia Norbert, muda huo huo msichana mwingine wa mapokezi aliingia hapo kwenye dawati la mapokezi na Fatma akatoka akampisha.



Fatma alienda hadi sehemu aliyosimama Norbert akamshika sehemu za juu za kiwiko chske huku akimtolea tabasamu.



        "Naweza kukusindikiza sasa hivi" Fatma aliongea huku akitabasamu akawa anajongea sambamba na Norbert.



        "Halafu Fatma hivi mbona una wivu hivyo hata safari ya kikazi ya ghafla unanionea wivu jamani" Norbert alimuambia.



        "Haaa! Babu wee mimi abiria hivyo kuchunga changu muhimu"



         "Siibiwi mama ila kazi yangu emergence nyingi huwezi amini yaani hata kamera za kazi nilisahau nikatumia simu kupiga picha"



          "Teh! Pole yako mume wangu ulikurupushwa inaonekana?"



         "Kama ulikuwepo vile nilikuwa Kibaha kwa anko sina hata vifaa vya kazi napigiwa simu nije  Arusha haraka sana, bahati nzuri nilipata ndege mapema uwanja wa ndege Dar. Yaani hata nyumbani kwangu sikurudi.



        "Pole sana mume wangu ndiyo kazi hiyo, safari njema mume wangu urudi  salama"



        "Sawa mke wangu"



Walikuwa tayari wameshafika kwenye eneo la kuingia ndani ya uwanja, Fatma alimbusu Norbert mdomoni akiwa ametekwa kisawasawa na uongo aliopewa na Norbert kisha akamkumbatia kumuaga. Norbert naye alimuonesha uchangamfu kwa binti huyo kisha akaingia ndani ya uwanja akaelekea mahali ilipo ndege, aliingia ndani ya ndege akakuta tayari ndege ilikuwa imejaa na viti vichache ndiyo vilikuwa vimebakia. Akiwa na umakini wake wa kila siku alitembea huku na huko akiangaza kila pande  akaenda kuketi kwenye kiti chake akafunga mkanda, muda mfupi baadaye ndege aliyopanda ilianza kujongea taratibu kuelekea kwenye njia za kurukia.



Iliinuka sehemu ya mbele baada ya kifika eneo la kurukia kuashiria ndiyo ilikuwa inaiacha ardhi ya Arusha kisha ikakaa sawa baada ya kufika angani. Norbert hapo alifungua mkanda wake wa kiti kisha akamtazama abiria aliyekuwa yupo siti ya pembeni, abiria huyo aliyemuona alimpa hamasa zaidi ya kutaka kumjua zaidi kwani muda huo alikuwa kalala na kavaa kofia aina ya hat iliyofunika uso wake kwa sehemu kubwa. Mikono ya abiria huyo ilikuwa ni ya mzungu lakini sura ambayo ilikuwa imefunikwa na kofia ilimzuia Norbert hakuiona  , alibaki akimtazama jinsi alivyozama kwenye usingizi hata ndege ilivyokuwa ikipanda angani hakuwa na dalili ya kuamka.

Norbert alimpuuzia abiria huyo kisha akageuza macho kutazama nyuma kwa namna ambayo ingekuwa vigumu kwa mtu kumjua anatazama nyuma, huko napo aliwaona wazungu watatu waliovaa suti zinazofanana ya abiria aliyeketi jirani yake. Wazungu hao nao walikuwa wamevaa kofia aina ya hat nyeusi kama yule abiria aliyekuwa amelala pembeni yake, Norbert aliwatazama kwa umakini kisha akaachana nao akatazama viti vilivyo usawa nae kwa upande wa pili. Huko alimuona abiria mwingine aliyevaa nguo kama ya abiria aliyeketi pembeni yake, tofauti ya abiria huyo na huyu wa jirani ya Norbert hakuwa mzungu bali alikuwa ni mhindi mwekundu mwenye nywele ndefu alizozisokota kama mkia zikiwa zimeangukia mgongoni mwake.

Mwili wa mtu huyu ulikuwa umejengeka kimazoezi zaidi tofauti na miili ya wazungu wale, shingoni hadi kidevuni alikuwa na mchoro unaofanana na mabaka ya chui ambao ulimfanya aonekane tofauti kabisa na shingo za wanadamu wengine. Mtu huyo alionekana kuwa siyo mtu wa kawaida kwa macho ya Norbert hadi muda huo, alionekana ni mtulivu kuliko kawaida akiwa hageuzi shingo pande yoyote ile lakini kwa Norbert bado aliendelea kumtilia shaka mtu huyo kutokana na muonekano wake. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Norbert alibaki akiwa ameelekeza uso wake mbele lakini macho yake yalikuwa yakimtazama mtu yule kwa wizi mkubwa ili mwenyewe asiweze kumtilia shaka yoyote, muda huohuo abiria aliyekuwa amekaa pembeni yake alianza kuamka kisha akapiga muayo mrefu na akafungua mkanda wa kiti. Abiria huyo alijinyoosha kwa uchovu na hapo kofia yake ikaanguka na sura yake ikaonekana dhahiri kwa Norbert, alikuwa amenyoa mtindo wa kijogoo kichwani mwake na sikio lililopo upande wa Norbert alikuwa amevaa hereni ndogo.

Norbert alimtazama  yule mzungu na yeye akamtazama Norbert, tabasamu la ghafla la kusabahi ndiyo lilimtoka mzungu huyo na Norbert akarudisha tabasamu hilo.



          "Tanzanian(Mtanzania)" Mzungu huyo aliongea kwa kingereza chenye  lahaja ya kimarekani, Norbert alitabasamu kisha akatikisa kichwa kuitikia aliposikia kauli hiyo.



          "Woow! Nice, Thomas and you?( Wooow! Nzuri, Thomas na wewe?)" Mzungu yule aliongea huku akimpa mkono Norbert.



          "Kaila, also known as Norbert. Also You can call me Norbert Kaila (Kaila, pia najulikana kama Norbert.  Pia unaweza kama Norbert Kaila)" Norbert aliongea huku akipokea mkono wa Thomas.



          "Pleased to meet you(Nimefurahi kukutana nawe)" Thomas aliongea huku akimpa mkono na Norbert na yeye akampa mkono huku akisema, "pleased to meet you too (ninafuraha na kukutana na wewe pia)".



Kimya kilifuata baada ya hapo kwa Norbert na Thomas, kila mmoja aliwaza lake liliopo kichwani kwake muda huo wakisubiri ndege iwasili jijini Dar es salaam walipokuwa wakielekea. Thomas alirudi katika hali aliyokuwa nayo awali baada ya kuamka kumsabahi mgeni wake, Norbert akiamua kutoa simu yake kuangalia kilichojiri tanguvwakati alipokuwa ameiweka kwenye mfuko wa suruali. Aliitoa akaperuzi akisubiri muda wa ndege kutua ufike, nusu saa baadaye sauti ya mhudumu akiwatangazia kuwa wafunge mikanda ndege ilikuwa ikikaribia kutua katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ilisikika.



Norbert alifunga mkanda akatulia na Thomas naye akafunga mkanda akatulia, abiria wote pia walifunga mikanda  na ndege ikaanza kuinama kwa mbele kidogo kuashiria ndiyo ilikuwa ikielekea kutua. Muda mfupi baadaye matairi ya ndege hiyo ambayo tayari yalikuwa yametolewa nje yaligusa ardhi ya uwanja wa kimataifa wa mwalimu Nyerere, ndege hiyo ilikimbia kwa kasi sana kisha ikapunguza mwendo ilipofika  karibu na eneo la kuegesha ndege. Ilisimama kabisa jirani na jengo lenye ofisi za uwanja, milango ya ndege hiyo ilifunguliwa kisha abiria mmoja baada ya mwingine akaanza kushuka kwa utaratibu hadi chini walipoikanyaga ardhi ya uwanja huo.



Norbert alikuwa ni mmoja kati ya watu walioshuka ndani ya ndege hiyo  akiongozana na Thomas, Norbert alimuaga Thomas na akataka kuondoka lakini rafiki yake huyo waliyekutana ndani ya ndege alimuomba asubiri kidogo. Norbert alisubiri hadi pale waliposhuka wazungu wengine pamoja na yule mhindi mwekundu  ambao walivaa nguo sare na Thomas, Norbert alitambulishwa kwa watu hao ndipo naye akaondoka akiwa ameongozana nao hadi ndani ya jengo la uwanja huo wa ndege ambapo maalum kwa watu kusubiri wasafiri wanaowasili.



Katika eneo hilo Norbert alimuona Benson akiwa amesimama akaenda kumsabahi, Norbert alimsabahi kwa furaha kwa lugha fasaha ya kiswahili lakini Benson huyu hakuwa akiongea kiswahili zaidi ya kutumbukiza maneno ya machache ya lugha ya kiswahili kwa kuchanganya na kingereza. Muda huo huo Thomas na wenzake wakaja kwa Benson wakasalimiana kwa furaha huku wakigongesha mikono, hawakujua kuwa walikuwa wakimpa wasiwasi juu yao na pia hawakutambua kama walimoa hamu ya kutaka kuwafahamu zaidi. Norbert hakutaka kubaki eneo hilo baada ya kujua watu hao walikuwa wapo karibu sana na mtu aliyekuwa karibu na Jack Shaw, aliamua kuondoka kwani vinyweleo vya mwili wake vilishaanza kumsisimka hasa alipomtazama yule mhindi mwekundu ambaye alitambulishwa kama Santos.



Aliwaaga watu hao baada ya kubadilishana namba ya simu na Thomas kisha akachukua teksi uwanjani hapo, akili yake tayari ilikuwa imeshamuonya dhidi ya watu na aliamua kuondoka mapema kabla ya wao hawajaondoka. Alikuwa ni mwingi wa kutazama nyuma pindi tu teksi aliyopanda ilipoingia barabarani, Norbett kwa tahadhari zaidi aliketi koti cha nyuma kabisa na akawa anaangalia nyuma kila baada ya muda mfupi kwani vinyweleo vyake vyote bado vilikuwa vilikuwa vikimsisimka na moyo ukawa unapiga kwa hamasa ya kutomsahaulisha hatari. Teksi aliyopanda ilikuwa ipo katika barabara ya Mwalimu Nyerere na alipofika jirani na kampuni ya Scania tawi la Tanzania Norbert aliiona gari aina ya ford ikiwa ipo nyuma yake kwa gari tatu, gari tatu hizo zilienda zikahama njia ya kushoto katika barabara ya Mwalimu Nyerere ambao huwa na njia mbili.



Pamoja na gari hizo kuacha nafasi kubwa baada ya kuhama njia bado ford hiyo haikusogea zaidi mbele, walienda hadi wakafika jirani na sehemu ambayo huwa yanaegeshwa magari mengi ya kubeba vinywaji baridi vya kampuni ya SBC Tanzania. Hapo katika uwazi ule lilioacha ile ford ilikuja kuingia basi la abiria la kampuni ya UDA, Norbert alipoona hiyo gari imekuja kuchomeka mbele alishusha pumzi halafu akawa yupo makini katika kutazama nyuma. Msafara wao huo ambao ulimtia kila aina ya shaka Norbert haukufika mbali, ulikomea kwenye foleni kubwa iliyopo kwenye mataa ya Tazara ambayo ilusababisha magari mengi yasimame. Hapo Norbert alimshika bega dereva teksi kwa kumuita, dereva teksi aligeuka nyuma kuitikia wito huo.



           "Kaka naomba fanya kama nitakavyokuambia, chukua hii hela yako yote ya kutoka Jeti Rumo hadi Temeke" Norbert alimuambia huku akimpatia hela yake yote



           "Kaka mkubwa mbona sikuelewi" Dereva teksi aliuliza.



           "Ni hivi nashuka hapa nimesahau kitu ila nakuomba nenda njia hiyo hiyo kama nilivyokuelekeza ya Temeke mimi utanikuta Vetenari nikiwa tayari nimeshachukua kitu nilichokisahau" Norbert aliongea huku akifungua mlango wa gari kidogo akaokota gunia kubwa lililojaa barabarani vumbi akaliingiza ndani, Norbert aliwasha kamera iliyokuwa kwenye kifungo cha shati lake akawa analiweka gunia vizuri.



             "niwashukuru halmshauri kwa uchafu wao wa kutosafisha barabara leo hii wameniokoa" Norbert aliwaza huku akilitazama lile gunia chafu huku akitabasamu.



             "Kaka gunia chafu hilo la nini humu" Dereva teksi aliuliza



              "Hii siyo kazi yako mkubwa, sikia nimeghairi tena kupanda gari unaweza ukaenda kugeuza popote ukaendelee na kazi yako" Norbert alimuambia dereva teksi huku akilivaa gunia hilo chafu ambalo lilimchafua hata nguo zake lakini hata hakujali, dereva teksi alibaki akimshangaa sana lakini hakumjali hata kidogo.



 Alipomaliza alifungua mlango wa gari kidogo kishs akajipenyeza akatoka nje ya gari bila kuonekana kutokana na baadhi ya magari kuwa yamezima taa, alijipinda mgongo wake gunia hilo likawa limefunika hadi kiatu  chake. Kimuonekano hakuwa tofauti na ombamba wa barabarani, Norbert akiwa kajifunika gunia hilo ambalo kiukubwa ilikuwa ni sawa na gunia tatu za mkaa zilizounganisha alitembea hadi ilipo daladala ya UDA.

Alinyoosha mkono juu kuomba katika madirisha ya daladala hiyo ya UDA, alinyoosha mkono wake uliochafuliwa na vumbi la gunia hilo pamoja na weusi wa uchafu kuomba huku akitetemeka mithili ya mtu mgonjwa. Baadhi ya abiria walimpatia senti zao huku baadhi wakifunga vioo vyao kutokana gunia hilo kunuka sana, Norbert alipitisha mkono hadi alipolipita daladala hilo sasa akaiendea gari aina ya ford aliyoitilia shaka ambayo ilikuwa ipo nyuma ya hiyo daladala ya UDA.

Alipoifikia gari hiyo alikuta ina vioo vya kawaida visivyo na giza ambavyo vilikuwa vimepandishwa hadi mwisho, ndani ya gari hiyo Norbert alimuona Benson akiwa ndiyo dereva na wengine wote aliopanda nao ndege moja kutoka Arusha. Norbert aligonga kioo cha gari hiyo akiretemeka kama masikini mwenye ugonjwa au mwenye njaa kali sana, Benson alifungua kioo kisha akamtazama Norbert kwa chuki nyingi kutokana kukerwa na jinsi kioo kinavyogongwa.



         "Hey what are you want(Hey! Unataka nini?)" Benson aliuliza kisha akapandisha kioo haraka sana baada ya kuisikia harufu kali inayotoa gunia alilovaa Norbert, alimuonesha Norbert alama ya kidole cha kati huku wenzake wakiwa wanacheka.



  Norbert kwa kuona hali hiyo ilimbidi ajifanye mnyonge kisha akaanza kuomba  kwenye gari kadhaa zilizofuata nyuma, alipofika mbali na gari  waliyopanda kina Benson alitoka kando ya barabara akavua gumia hilo ambalo harufu yake ilimkera ingawa aliamua kuvumilia. Aliitazama kamera ndogo aliyokuwa ameichomeka kwenye shati ambayo muda wote ilikuwa ikirekodi matukio yote yaliyokuwa yakitendeka, aliporidhika ipo salama aliizima kisha akakunja lilw gunia ili ajiandae kulitupa lakini aliikuta akisukumwa kwa nguvu na mtu ambaye alikuja nyuma yake bila yeye kumuona.



 Norbert aliyumba kwa kusukumwa huko lakini alimudu kusimama kisha akajigeuza kwa haraka ili apambane na huyo aliyemsukuma, aligeuka akiwa amekunja ngumi lakini aliachia ngumi hizo baada ya kuona aliyemsukuma alikuwa ni masikini aliyevaa  nguo zilizochakaa na zenye kutoa harufu. Masikini huyo alikuwa ni mwanamke mtu mzima mwenye mwili mnene sana, Mwanamke huyo alikuwa akimtazama Norbert kwa chuki sana huku akihema kwa nguvu sana.



         "Huna adabu mwanakenda wewe, nimeweka gunia langu nililalie limepeperuka na upepo ndiyo ulichukue wakati nilikuwa nikilifuatilia lilipopeperuka nilirudishe. Nyinyi wapiga debe mnaovaa vizuri mkaibie watu kwenye daladala mna laana yaani hamunihurumii hata mimi sawa na mzazi wako nitalala vipi?" Mwanamke huyo aliongea huku akiweta kwa hasira, Norbert alilitazama lile gunia lililomfanya asukumwe na yule mwanamke anayefaa kumuita bibi yake kisha akasogea hadi mbele yake. CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Alimkabidhi lile gunia pamoja pamoja na peaa zote alizoomba kimaigizo ili tu awakwepe wabaya wake baada ya kuwa na wasiwasi, mwanamke alilivuta gunia kwa nguvu lakini alipoona pesa alikuwa mpole na akawa anamtazama Norbert kwa tabasamu badala ya hasira kama ilivyokuwa mwanzo. Norbert  hakujali tabasamu la yule mwanamke aliamua kuondoka lakini  aliitwa tena ikabidi aguke kumsikiliza, alisogea karibu kisha akamtazama yule mwanamke kwa umakini.



             "Baba yule dereva teksi aliyekupa msaada uingie kazini kama ni rafiki yako kimbia atakutaja" Yule mwanamke aliongea akijua Norbert ni teja aliyeiba mavazi kwa jinsi alivyochafuka na alijua yule dereva teksi kamsaidia haoo pale kwenye mataa ili aje kuibia watu, mwanamke huyo aliamua kulipa wema wa kusaidiwa vijisenti kidogo na Norbert.



              "Baba kuna wazungu wamemkaba, nilipokuwa nakufuatilia usiondoke na gunia langu nimewaona. Kimbia mwanangu" Yule mwanamke alimwambia na muda huohuo simu ya Norbert ikaanza kuita kwa kutoa mtetemo ndani ya suruali yake, Norbert alimtazama yule mwanamke kisha akaondoka eneo hilo kwa kasi ili tu amfanye mwanamke yule aamini kuwa yeye ni teja kweli aliyevaa tofauti.



 Harufu ya like gunia ambalo alijifunika ilimpa mwanamke uhakika wa kuwa Norbert ni teja na  aliamua ambakishe na mawazo hayohayo kutopokea simu yake ilipoita kisha akakimbia, simu yake ilikuwa ni ya kisasa na ya gharama kubwa sana na laiti kama angeipokea basi angempa mwanamke yule wasiwasi.



   Alipofika mbali kabisa na eneo alilokuwepo awali aliitoa simu yske akaipokea akaongea, "sema Thomas..... ila mmejitahidi sana kunifuatilia niwape hongera kwa hilo......karibuni ndani ya kidari poo" . Norbet alikata simu kisha akafungua mfuniko wa betri wa simu yake, alitoa betri na ndani kulikuwa na sehemu nne za kuweka kadi ya simu tofauti na simu nyingine. Alitoa kadi moja ya simu akaivunja kisha  akaitupa akafunga simu vile vile akaiwasha, baada ya hapo alienda kwenye kituo cha pikipiki akachukua  pikipiki ya kukodi akatoweka eneo hilo.

ILIVYOKUWA

 Sheikh Ahmed siku iliyopita alienda Musoma kuwachukua vijana wake, alirudi nao kwenye hoteli ya Singita kisha akawapa jukumu ambalo walitakiwa walitekeleze wakiwa nchini. Siku iliyofuata majira ya mchana vijana hao ambao ndiyo Thomas, Santos na wenzao watatu walipanda ndege katika uwanja wa kimataifa wa Serengeti uliopo maeneo ya Mugumu mkoani Mara.



  Kwa mipango iliyofanikisha kupenyeshwa kwa bahasha ya kaki(kuhonga), walifanikiwa kupata ndege binafsi katika uwanja huo iliwapeleka mpaka Arusha vijana hao. Huko Arusha tayari walikuwa wameshaandaliwa tikiti za shirika la ndege la Precision iliyokuwa inaondoka jioni ya siku hiyo, jioni ya siku hiyo walisafiri na Norbert pasipo kutambua wanasafiri na adui yao. Thomas alivutika sana kuongea na mwisho akaongea naye wakaunda urafiki papo, walipotua kwenye uwamja wa ndege  wa Mwalimu Nyerere walipokelewa na mtu ambaye Norbert alikuwa anamjua kuea ni Benson kumbe alikuwa ni pacha wake Benson anayeitwa Benjamin.



   Benson na Benjamin ni wahalifu  wa  kuaminika wa kundi hatari la Jack Shaw kutoka nchini Uingereza ambao walitangulizwa Tanzania wakiwa na kikundi kidogo walichokiita Cats Kingdom, kikundi hicho ndiyo kilichomteka Norbert akaja kutoroshwa na Norene. Benson na Benjamin ndiyo Panthers wenyewe waliokuwa wakiendesha mauaji mbalimbali, hawakuwa wakijulikana kama wapo mapacha kwa jamii bali walijulikana kwa watu wachache tu. Mapacha haea ndiyo walioshiriki mauaji ya Jenerali Kulika ambapo Benson ndiye mwenye alama ya mshono mkononi na Benjamin ndiye mwenye alama ya mchoro wa kipepeo, tofauti yao kubwa ilikuwa uongeaji wa lugha ya kiswahili tu na sio kufanana  kwani  walikuwa wamefanana kila kitu kinachoonekana.

Norbert hakuitambua tofauti hiyo na hata alipomsalimia wakati anakuja kupokea wenzake alimjibu kwa kuchanganya na lugha ya kingereza, bado Norbert hakuwa amehisi kitu tofauti.

Norbert alipoondoka eneo hilo ndipo Benjamin alipowauliza wenzake juu ya kufuatana kwao na Norbert, Thomas alieleza jinsi alivyokutana ndani ya ndege na Norbert akiwa hajamjua ni nani. Benjamin alimsikiliza kwa umakini sana kisha akawaeleza wote juu ya uhalisia wa Norbert, tena akawaeleza ni mmojawapo kati ya watu wanaohitajika wauawe kabla mpango wao haujaingia Tanzania. Taarifa hiyo ilipofika  kwa vijana waliotumwa kuja kuongeza nguvu baada ya Cats kingdom kupungua ilikuwa ni kuitejeleza mara moja kazi yake, wote kwa pamoja waliingia ndani ya gari iliyowafuata wakaanza kuifuatilia teksi aliyokuwa amepanda Norbert.



 Hawakujua kama mpango huo  Norbert alishaujua tayari,  waliendelea kuifuatilia ile teksi lakini pia walifanya kosa jingine kubwa zaidi kwa kuiacha  basi ya abiria  ya UDA kukaa mbele yao wakawa hawaioni vizuri teksi aliyopanda Norbert. Foleni ilipoanza tayari giza liliingia na walikaa kidogo wasubiri hadi pale daladala la UDA lilipozima taa za mbele kwenye foleni hiyo, wajiandaa kushuka lakini kioo cha dereva ambaye ni Benson kikagongwa na Norbert waliyejua ni ombaomba. Harufu kali iliyoingia ndani ya gari iliwakera wote na Benjamin akapandisha kioo kuepuka hiyo kero, Norbert wanayemsaka wakamuangamize aliwakimbia namna hiyo bila wao kujua.

Thomas na Santos walienda hadi kwenye ile teksi wakaingia bila taarifa, Thomas aliingia kiti cha nyuma na Santos akaingia kiti cha mbele lakini hawakumkuta Norbert. Dereva teksi alibaki akiwashangaa wageni ambao walimtisha na alihitaji kujihami kwani ni kawaida madereva teksi kutembea na silaha kwa usalama wao, aliingiza mkono chini ya kiti chake atoe silaha kwa haraka lakini aliwahiwa na kabali ya Thomas iliyokuwa ya haraka kushinda haraka yake. Muda huo ndiyo yule mwanamke anayetafuta gunia lake lililochukuliwa na Norbert alipita akaona hilo tukio lakini aliondoka haraka kuepusha usalama wake.

Kabali nzito ya mkono wa Thomas ambayo uligeuka kua migumu baada ya misuli kukazwa, ilizidi kumfanya dereva teksi huyo asiwe na ujanja wowote akiwa anahangaika kutoa mkono huo. Thomas naye alizidi kumkaba kwa nguvu hadi sauti ikawa haimtoki kabisa Dereva wa teksi , nguvu ziliamza kumuishia dereva teksi huyo akawa hana uwezo wa kujitetea akabaki akiwa ameshikilia mkono wa Thomas kama alikuwa akiishinikiza iendelee kumkaba.

Thomas naye hakutaka kumuachia aliendelea kumkaba kwa nguvu dereva teksi hadi akaanza kurusha miguu, mguu mmoja wa dereva huyo ulikanyaga sehemu ya kuongeza mwendo wa gari na kuifanya gati itoe mngurumo mkubwa lakini haikwenda popote kutokana na gia yake iliyo katika ipo mfumo moja kwa moja(automatic) kuwa katika P yaani parking. Kulia huko kwa gari kuliwashtua hata watu walioko mbele lakini hawakufanikiwa kuona chochote kutokana na taa za ndani za gari hilo kuwa limezimwa.

Santos aliingiza mkono chini ya kiti cha dereva akatoa jambia kubwa ambalo lilikuwa bado jipya kisha akamtazama dereva teksi kwa dharau, Santos kwa kutumia mikono yake yenye nguvu aliamua kumpiga dereva huyo kibao kimoja cha kifua. Kibao hicho kilimfanya dereva huyo aache kurusha miguu na akatulia huku akijaribu kukohoa kutokana na chachafya ya kofi lile zito la Santos, nafasi ya kukohoa nayo hakuipata kwani kabali imara ya mikono ya Thomas bado ilikuwa palepale ambayo ilamfanya abanwe kwenye sehemu ya kuegemea.



         "Abiria uliyemchukua Airport yupo wapi?" Santos aliuliza akisogeza jambia alilolipata chini ya kiti cha dereva jirani na koo la Dereva teksi hili, Thomas naye alimuachia kwa haraka na jambia hilo likagusa koo la Dereva wa teksi huyo. Santos alimkunja kwa nguvu huku akigusa koo lake kwa jambia hilo akimuacha akikohoa mara chache kisha akakandamiza jambia hilo kooni mwa dereva wa teksi, ncha kali ya jambia hilo ambayo haikumtoboa ngozi yake zaidi ya kuonesha dalili kutoboa ilimfanya Dereva teksi  huyo asiwe na namna zaidi ya kuongea ukweli.



           "Kashuka hapahapa na kavaa gunia  kaenda huko nyuma" Dereva teksi aliongea kwa tabu kisha akajaribu kukohoa tena lakini ncha ya jambia ilimkatisha kufanya hivyo kwani ingemtoboa ikiwa angekohoa koo lake likatikisika.



            "Damn! Ndiye huyo aliyekuwa anaomba kwenye hiyo gari hapo nyuma kabla hajasogea nyuma zaidi?" Thomas aliuliza akiwa haamini kama Norbert tayari alikuwa amewatoka, Dereva teksi aliishia kujibu swali hilo kwa kuchezesha nyusi kwani angetikisa kichwa kizima basi lile jambia lingemletea balaa jingine.



Thomas alitoa simu kisha akabonyeza namba za Norbert walizopeana uwanja wa ndege, simu ya Norbert iliita kwa muda mrefu kutokana na muda huo ndiyo muda ambao Norbert alikuwa anakimbia ili asogee mbali na yule mwanamke aliyempa gunia ili ajue kama kweli alikuwa akikimbia baada ya kusikia Dereva teksi  alikuwa akikabwa na alikuja kuipokea baada ya kufika mbali.
 Thomas simu ilipopokelewa aliongea, "ndiyo unajifanya mjanja siyo kuliko Sungura.......tutakunasa tu"



  Alikata simu kisha akamtazama Santos akampa ishara baada ya muda huo kuwa tayari magari yalikiwa yameruhusiwa, Santos naye alilegeza mkono wake katika kukandamiza jambia halafu akampa nafasi ya kuendesha gari dereva huyo.



           "Ingia kulia haraka" Santos alitoaa amri na dereva huyo akaweka gia huku akikohoa akakanyaga mafuta gari ikaanza kuondoka kwa kasi ili waepuke lawama za watu ambao walikuwa na haraka wapo nyuma yao, walipokuwa wakikata kona kuingia barabara ya Mandela taa za magari yaliyosimamishwa zikamulika ndani ya gari hiyo hadi Askari wa usalama barabarani aliyepo katikati ya makutano hayo akaona kile ambacho kinafanyika humo ndani ambacho kilimshtua sana.



 Askari wa usalama wa barabarani alionekana mbele ya macho ya Thomas na Santos alihangaika kuitoa simu yake ya upepo kwa haraka sana, Santos alimuamuru Dereva teksi aongeze mwendo naye akatii.



   Dereva Tulsa alikata kona kuingia upande wa kulia ilipo barabara ya Mandela, walikuwa wanaelekea Vetenari. Mwendo wa gari ulikuwa mkali na  Thomas alitumia muda wake kuangalia nyuma kwa tahadhari, milio ya ving'ora vya poliai ilianza kusikika kwa  mbali walipokuwa wanakaribia jirani na makutano ya barabara yaliyopo jirani na kituo cha mafuta cha Oilcom.



  Santos  alifungua mlango wa gari kisha akatoa Jambia shingoni mwa Dereva teksi ambaye alibaki akishangaa sababu iliyomfanya Mhindi yule mwekundu amuachie kirahisi namna hiyo mshangao wake haukupata majibu akasikia mlango wa nyuma upande wa kushoto nao  ukifunguliwa. Dereva teksi alipoona hivyo pamoja na kusikia ving'ora vya magari ya polisi aliamua kuwakamatisha Santos na Thomas, akili yake ilimpa asilimia mia kwamba Santos na Thomas walikuwa wakiwakimbia  polisi.



Aliazimia kukamyaga breki ya gari kwa nguvu ambayo itawafanya Santos wayumbe ili awazubaishe  polisi waweze kukaribia, Dereva teksi huyo hakujua kwamba hila yake tayari ilikuwa imegundulika baada ya Thomas kuuona mguu wake alipokuwa  akijaribu kuutoa kwenye kikanyagio cha mwendo aupeleke kwenye breki.



 Mguu wake huo haukufika kwenye breki tayari Thomas alishadaka kidovu chake kwa mkono wa kushoto na kisogo chake kwa mkono wa kulia , tendo hilo lilimshangaza Dereva teksi huyo akawa amesitisha kukanyaga breki bila ya kutarajia. Thomas naye hakutaka kupoteza muda alifanya tendo la haraka la kuzungusha shingo ya Dereva akaivunja kisha akaruka nje kwa mlango wa upande wa kushoto alioufungua, Santos naye aliruka nje na wote wakatumbukia kwenye mtaro wa maji machafu uliokuwa mkavu.



  Walitoka kwa haraka wakasimana kando ya pili ya mtaro huo kutoka barabarani bila ya kuonekana na mtu, walijikung'uta nguo zao huku wakisikia kishindo kizito kilichowawafanya watabasamu. Muda huo huo pikipiki zilizopakia askari wenye sare za kikosi cha kutuliza ghasia wenye silaha zilipita kwa kasi sana, wakielekea upande kiliposikika kishindo hicho ambacho waltambua ni cha ile Teksi baada ya kukosa muelekeo kutokana na Thomas kumuua dereva kwa kumvunja shingo.



 Baada ya kufanya tukio hilo walitembea hadi kituo cha daladala cha Tazara  wakakuta gari yao iliyowafuata ikiwa imeegeshwa kwenye kituo cha daladala, waliingia ndani wakiwa na sura za huzuni kutokana na kumkosa Norbert.



        "What(Nini)?" Benjamin aliuliza.



        "He escaped( Ametoroka) Thomas alijibu.



        "How(Kivipi)" Benjamin aliuliza kwa kuchoshwa na taarifa hiyo.



         "He knocked your window as a sluggard( Aligonga kioo chako kama mvivu)" Santos naye alidakia kisha akawatazama wale wazungu watatu akawaambia, "ni mtu  makini sana na sisi tuwe makini".



Wazungu  hao waliitikia kwa kichwa tu  pasipo kuongea lolote kisha wakaonesha ishara ya dole gumba kwa Santos, Benjamin aliwasha gari kisha akaliingiza barabarani akaliondoa kwa mwendo wa wastani.

 Pikipiki aliyopanda  Norbert ilikuja kumuacha katika mtaa ambao alimuelekezaa dereva ampeleke, Norbert alishuka akamlipa dereva wa pikipiki hiyo ambaye alishukuru Mungu kwa kufika mwisho wa safari kutokana na harufu kali aliyokuwa nayo Norbert. Alikubali kumbeba Norbert hadi mitaa hiyo kutokana na kusaks noti tu, laiti ingelikuwa siyo noti basi asingembeba kutokana na harufu kali aliyokuwa akiitoa. Alipopewa pesa yake aliamua  kugeuza pikipiki yake na kuondoka kwa kasi kuepuka harufu hiyo, alimuacha Norbert akiwa amesimama palepale hadi pale alilipopotea katika upeo wa macho ya Norbert.



Hapo Norbert ndiyo aliamua kutembea kusonga mbele huku akiwa makini kuangalia uwepo wa mtu anayemfuatilia, alitembea kwa mitaa takribani mitatu kisha akasogea jirani na geti kubwa jeusi ambalo lilikuwa na kibanda kidogo cha ulinzi. Aligonga geto hilo kisha akasubiri kidogo ambapo mlinzi alifungua dirisha dogo akachungulia nje, mlinzi alipomuona ni Norbert alifungua geti kwa haraka sana kisha akasogea pembeni huku akibana pua kutokana na harufu iliyokuwa inatoka mwilini mwa Norbert.



             "Mh! Bosi mbona unanuka hivyo?" Mlinzi huyo  aliuliza.



             "siyo kazi yako, mke wangu yupo?" Norbert alimuambia akiwa amelunja sura kutokana na kutopenda maneno ya mlinzi huyo.



             "Madam yupo we pita tu" Mlinzi huyo alijibu na Norbert alipita pasipo kungeza neno jingine hadi kwenye mlango wa nyumba kubwa ya kisasa. Aligonga mlango  wa nyumba mara moja kwa kutumia vidole vitatu, mlango wa nyumba hiyo ulifunguliwa na Norene akaonekana akiwa amevaa nguo laini la kulalia.



  Harufu inayotoka mwilini mwa Norbert ilimfanya hadi yeye abane pua kisha akasogea kando ya mlango kumpisha aingie, Norbert aliingia ndani kisha Norene akafunga mlango wakabaki wakitazamana kama ndiyo wanaonana. Kicheko cha ghafla kilimpuka Norene alipomtazama Norbert usoni akaona uchafu mweusi ambao ulimfanya aonekane kituko, alibaki akiwa ameweka mkono mdomoni kutokana na harufu kali iliyokuwa inatoka mwilini mwa Norbert.



               "Ulilala kwenye gari la taka nini?" Norene aliuliza huku akicheka.



                "sasa unacheka nini?" Norbert aliuliza.



                 "Wacha nicheke tu umekuwa kama zimwi vile na unavyonuka kama ulijifukizia marashi yaliyotengenezwa kwa taka za dampo" Norene aliongea.



                "Alaa! Kumbe sasa ngoja nikukumbatie tugawane hii harufu tuone utamcheka nani" Norbert aliongea akiwa na tabasamu huku akimsogelea Norene akiwa ametanua mikono amkumbatie, Norene alikimkwepa kisha akakimbia. Norbert alibaki akimfukuza nyuma huku akiwa ametanua mikono yake, Norene alikimbilia moja kwa moja chumbani kwake akaingia katika bafu la ndani huku akiwa anacheka kwa jinsi Norbert alivyokuwa anamkimbiza.



   Norene alikimbia hadi lilipo eneo maalum la kuogea lililotengenezwa kwa udongo mgumu, alipofika hapo alisimama mbele ya sinki kubwa la kuogea ambalo tayari lilikuwa limejaa maji akimuangalia Norbert kwa tabasamu pana.



               "Yaani hapo tunaingia wote kwenye sink " Norbert aliongea huku akimsogelea Norene ambaye alikuwa alikuwa akimtazama kwa tabasamu tu.



               "Toa madude yako ya mfukoni ndiyo uje tuingie wote" Norene alimuambia Norbert ambaye alitoa vitu vyake vyote vilivyokuwa na uwezo wa kuingia maji vikaharibika kisha akamfuata Norene kwa kasi akiwa ametanua mikono amkumbatie, Norbert alipomkaribia Norene hakufanikiwa kumgusa kwani alijikuta akitupwa ndani ya sink la kuogea akiwa na nguo zake baada ya Norene kutoa mtindo mmoja wa judo wa kujihami. Alimzoa Norbert kwa kumtegea mguu uliomfanya ajikwae akaingia ndani ya sinki hilo lililojaa maji pasipo kujigonga sehemu yoyote kutokana na utaalam alioutumia, Norbert aliangukia kwenye maji kifudikifudi na alipogeuka alimuona Norene akimtazama huku akicheka kwa nguvu.



                "umeniweza leo" Norbert aliongea huku akijipangusa maji usoni mwake.



                "leo mjanja mimi haya vua nguo zako mwenyewe uoge ndiyo mengine yatafuata" Norene aliongea



    Norbert alivua nguo zake ambazo tayari zilikuwa zimelowana, alioga akiwa anasimamiwa na Norene. Alipomaliza kuoga Norene alimpa taulo akajifuta maji kisha akampatia vazi maalum la kuvaa ambalo huvaliwa muda wa kulala.



              "Nimekuweza  kweli yaani niliweka maji ya kuoga nikienda kulala nioge ila wewe umejileta umeyaoga" Norene alimuambia Norbert huku akitoka bafuni na Norbert akafuata nyuma yake.

   Gari walilopanda kina Thomas liliingia  katika nyumba yenye uzio mrefu pamoja na geti kubwa, gari liliingia eneo la maegesho na wote wakashuka wakakuta wenyeji walikuwa wakiwasubiri kwa hamu sana. Walikuta Mzee Filbert Ole akiwa na faili mikononi mwake , Wilson Ole, Benson, Leopard Queen na Kamishna wakiwa wanawasubiri kwa hamu, kitendo cha wao kufungua milango na kuikanyaga ardhi ya nyumba hiyo makofi ya ukaribisho yalipigwa na Filbert Ole ambaye ndiye ametoroshwa gerezani masaa machache yaliyopita.



         "Karibuni simba wetu" Filbert Ole alipngea akiwa na tabasamu pana usoni mwake, vijana wote wa kazi walioingia humo ndani waliachia matabasamu mapana katika nyuso zao kisha wakaenda kusalimiana na wenyeji wao kwa kushikana mikono.



          " ushindi nauona kila ninapowatazama" Filbert Ole aliongea.



           "hakika ushindi lazima, tumekuja kwa ajili ya kazi sasa tunaianza kazi" Santoa aliongea kisha akaivua kofia aliyoiva kichwani ambayo ilifanya mywele zake zionekane kwa wote, sura yake  isiyo na mzaha  ilionekana ambayo iliwafanya Filbert Ole na mdogo wake Wilson watabasamu.  Filbert Ole alimkabidhi faili Santos huku akisema,
            "usiku huu anatakiwa auawe M.J Belinda ambaye ndiye huyo wa kwanza kwenye file".



    Santos aliafiki kwa  kutikisa kichwa kidhs akasema, "bastola zetu zile nafikiri zimewasili tayari tutazihitaji kwenye kazi  hii".



                 "Ondoeni shaka kuhusu hilo  bastola tayari zimewasili cha muhimu ni kumuua huyo malaya tena muwe makini sana ni komandoo" Wilson aliongea.



                  "Komandoo mmoja mbele ya makomandoo hatapona ameshazidiwa uwezo" Thomas alidakia na wote wakaachia matabasamu usoni mwake.



                   "Anawasili kwake saa tatu usiku General kampatia kazi makusudi ili aingie muda huo, nyumbani kwake kwa sasa analala peke yake hivyo kazi hiyo itafanyika kwa urahisi" Kamishna alionges kwa msisitizo.



                  "sasa hivi ni saa mbili kamili hakuna muda wa kupoteza ni kuingia kazini"Benson aliongea huku akiitazama saa yake ya mkononi, vijana wa kazi watatu ambao ni wale wazungu walioletwa pamoja na kina Thomas waliachiwa kazi hiyo pamoja na usafiri, walipewa gari maalum inayotumia ramani kuwaelekeza ilipo nyumba ya M.J Belinda ili waende kummaliza.

          MLIMANI CITY

Kazi nzito aliyopewa M.J Belinda na mkuu wake ilimfanya achelewe kutoka na hata pia achelewe kwenda kufanya manunuzi ya vitu muhimu vya nyumbani kwake atakavyovihitaji, ilikuwa ni masaa machache tu yamebaki ili iingie siku mpya ambayo ndiyo ndani yake kutakuwa na mazishi ya Jenerali Kulika. Akitumia gari yake ya kazini yenye nyota mbili mbele na nyuma, gari hiyo iliingia katika eneo la Mlimani city hadi kwenye maegesho.

Kawaida ya mwanajeshi akifika cheo chs brigadia jenerali basi gari yske huwekwa nyota moja, akiwa meja jenerali basi gari yake huwekwa nyota mbili, akiwa luteni jenerali basi gari yake huwekwa nyota tatu na akiwa Jenerali basi gari yake  huwekwa nyota nne. Nyota hizo zote huwekwa sehemu ya kuweka namba za usajili mbele na nyuma, gari hiyo ikionekana mahali popote kwenye kambi ya jeshi hutambulika aliyemo ndani ya gari ni nani kwa kuangalia idadi ya nyota zilizopo sehemu ya namba za usajili.



 Buti la kijeshi lilionekana likitoka ndsni ya gari aina ya Toyota landcruiser yenye rangi ya kijani iliyopauka, alionekana M.J Belinda mwanamke mrembo sana mwenye ngozi laini na umbo lililobeba mzigo mzito uliopo chini ya kiuno ambao uliweza  kumvuta mwanume yoyote mwenye tamaa abaki anamtazama. Ngozi ng'avu macho yake yaliyokaa kama  yanasinzia pamoja na nyusi zake nene zilizochongwa vizuri, zilimfanya atamaniwe na kila mwanaume mwenye kupenda kuwa na mwanamke mrembo lakini nguo zake za kazi zenye nishani tele pamoja na bawa moja la chuma lililopo juu ya sare vilitosha kuwafukuza wanaume wasimsogelee kabisa. Hakuna mwanaume ambaye angekuwa tayari kumfuata akiwa amevaa gwanda lenye cheo kikubwa kama hiko, umri wake na cheo chake vilikuwa vitu viwili tofauti.



Akiwa na gwanda hizo aliingia ndani ya jengo la Mlimani city kwa ajili ya kununua vitu katika  maduka makubwa(supermarket)  ya hapo, aliingia ndani ambapo alikaa kwa robo saa akatoka akiwa amebeba  mizigo ambayo alienda kuiweka nyuma ya gari kisha akaingia ndani ya gari akaondoka eneo hilo ili awahi nyumbani kwake kupumzika.



Aliliondoa gari hadi kwenye makutano ya barabara ya Mlimani city aliingia upande wa kulia kwenye barabara ya Ssm Nujoma, alienda na barabara hiyo hadi alipofika mwanzo wa barabara ya Shekilango. Aliiacha barabara ya Sam Nujoma akaingia barabara ya Shekilango, alienda na barabara hiyo hadi alipofika kwenye kituo cha daladala cha Kwa Manyola akahisi kuna hali tofauti ndani ya gari yake. Mlio wa makasha ya kiti cha nyuma ambayo hutoa mlio mtu akiwa anajigeuza aliisikia mlio wake alipotaka kugeuka kuangalia nyuma aliguswa na kitu cha baridi sehemu ya mwanzo wa shingo, msisimko ndani ya mwili wake ndiyo ulfuata baada ya kuguswa na kitu hicho cha baridi.



                       "Tulia hivyo hivyo Belinda" Alisikia ikitoka nyuma yake ikimpa amri.



                        "Moses nini unafanya sasa?" Belinda aliuliza baada ya kuibaini ni sauti ya Moses ndiyo ilimpa amri.



                         "Imenibidi ili nikufumbue macho" Moswa aliongea.



                         "sikuelewi" M.J Belinda aliongea, alipotaka kugeuka nyuma alisikia mlio wa kuondolewa usalama kwa bunduki ukisikika.



                         "Park gari hapo stendi haraka sana" Moses alitoa amri na muda huo tayari gsri iilikuwa imeshafika kituo cha Sinza Kijiweni, M.J Belinda alitii amri na akaegedha gari kituoni. Moses alimpatia simu yake ambayo ilikuwa  ina video iliyorekodiwa, M.J Belind aliipokea simu ya Moses akaitazama video hiyo hadi mwisho kisha akarudisha  simu kwa Moses huku akiwa amechoka kwa kile alichokiona.



                          "Benson ni muuaji wa General hadi sasa uamini hilo kwanza hadi uchunguzi mwingine utakapoendelea" Moses alimuambia.



                           "Umeipata wapi hii video?"  M.J Belinda aliuliza.



                           "Nor yupo kazini na ndiyo amebaini, unaweza kuendesha kwa sasa" Moses alimuambia na M.J Belinda akatii akaliingiza gari barsbarani akaondoka.





 Ndani ya dakika tano tayari walikuwa wamefika mtaa wa Megasiti ambapo ndiyo kwenye makazi ya M.J Belinda, gari lake lilisimama kwenye geti kubwa la mapambo ya mti M.J Belinda akapiga honi. Geti hilo  lilifunguliwa na mtu aliyevaa magwanda ya JWTZ ambaye ana jukumu la kuilinda nyumba nyakati za usiku, gari liliingia ndani na Moses akawa ana kazi ya kuwatazama wanajehi waliokuwa watatu walioanza kuifuata gari ya M.J Belinda.



 M.J Belinda aliipeleka gari kwenye maegesho akashuka na wanajeshi hao watatu wenye miili miembamba na mirefu wakasimama mbele yake, wote walitoa saluti kisha wakasimama kiukakamavu.



                        "Kuna mgeni yoyote aliyefika hapa?" M.J Belinda aliuliza lakini wale wanajeshi watatu hawakuongea chochote.



                        "Sajenti, Koplo na lensi Koplo inamaana swali langu hamulisikii?" M.J Belinda aliuliza lakini hakujibiwa zaidi ya wale wanajeshi kutazama kila mmoja, hali hiyo ilimkera sana M.J Belinda na akapiga hatua kusogea karibu kisha akawasukuma kila mmoja kwa hasira.



                        "Inamaana mna dharau siyo" Aliwaambia kwa hasira lakini ni kama alikuwa amewasha moto, Mwanajeshi aliyekuwa amesimama kati wenzake wawili alirusha ngumi ambayo aliikwepa kwa kuyumba upande wa kulia. Yule aliyekuwa  upande wa kulia alitupa ngumi ngumi ya uso ambayo aliinama ikapita kisha akajizungusha akakaa sawa, aliwatazama wale wanajeshi ambao walivua kofia zao wakazitupa chini na sura zao zikaonekana dhahiri kwa msaada wa taa kubwa  iliyopo uani. Walikuwa ni wazungu watatu waliojipaka  rangi nyeusi usoni wasionekane ni watu weupe, Belinda aliwajua kuwa ni wazungu kwa kupitia nywele zao ambazo zilikuwa kama singa lakini zilikuwa nyeupe zinazoelekea kufanana na mvi.



  Wazungu hao hawakumuacha hata M.J Belinda apate nafasi kujifikiria zaidi kuhusu wao, waliamua kumfuata M.J Belinda kwa mapigo tofauti. Yule aliyekuwa kati alimfuata kwa ngumi ambayo M.J Belinda aliikwepa kwa kuyumba pembeni, huko pembeni alipoyumba mwingine alimfuata kwa mateke mawili ya juu ambayo pia aliyakwepa kwa kupiga msamba yakapita.



 Mwingine alimfuata kwa mateke mawili ya kujirusha akiwa pslepsle chini kwenye msamba ambayo yalimpata barabara ya mgongo, M.J Belinda alitoa mguno wa maumivu kisha akaanguka chini na wazungu hao wakamzunguka huku wakidunda kama mabondia.

M.J Belinda aliamua ajikaze kisha akajiinua kwa sarakasi, hapo na yeye alianza kujibu mashambulizi kwa utaalamu wa juu akitumia mbinu zake za kikomandoo. Alitumia uwezo wake wote katika kupigana huku akijua alikuwa akipigana na watu wenye uwezo sawa na yeye ambao walikuwa wamemzidi idadi, alijitahidi awezavyo lakini wazungu hawa walionekana kumzidi ujanja kabisa.

 Mpambano ulimzidia ingawa alikuwa ameshamjeruhi mmoja jicho na wawili wakamzidia nguvu, alipigwa mapigo mfululizo ambayo yalimfanya Moses atoke ndani ya gari na kuingilia.  Moses aliingia kwa kurusha mateke mawili yaliyowapata makomandoo wawili chini ya shingo zao wakaenda kusalimiana na ardhi katika upande aliopo M.J Belinda  ameanguka ambaye  alimshika mmoja akavunja shingo yake akafa kisha wa pili akampiga goti la uso.



 Mpambano uliwageukia wazungu hao kwa kupewa kichapo kizito mfululizo hadi mwingine akapoteza maisha, alibaki yule aliyepigwa goti la uso  tu ambaye alitiwa nguvuni akaingizwa kwenye chumba cha mateka katika nyumba  ya M.J Belinda.

 Muda ambao Moses na M.J Belinda wanafanikiwa kuwadhibiti makomandoo wa kizungu ndiyo muda  ambao Norbert alikuwa yupo ndani ya gari aina ya Toyota Noah akitoka nyumbani kwa Norene Tabata, akiwa ndani ya nguo nyingine kabisa aliamua kutoka akimdanganya Norene alikuwa akiingia kazini kumbe kulikuwa na jingine zaido ya hiyo. Ilikuwa ni siku maalum ya kukutana na Josphine tangu alipoagana naye kwa mara ya mwisho siku ya jumamosi, pia zilikuwa zimebaki siku tatu na masaa mawili nchi ya Tanzania iingie katika mikono ya kijeshi chini ya Luteni Jenerali Ibrahim.
 Siku hiyo Norbert aliamua aende katika nyumba anayoishi Josephine akiwa na akili nusu hofu nusu amani, alitumia  dakika shirini akawa tayari yupo ndani ya eneo la Keko Michungwani. Hapo alimpigia simu Josephine aje amfuate katika muda huo wa usiku kisha akatulia amsubiei Jospine aje baada ya kumpa taarifa.

 Baada ya dakika takribani tatu  mlango wa pembeni ya kiri cha dereva wa gari hiyo ulifunguliwa, Joseohine aliingia ndani ya gari hiyo akiwa amevaa kaptula fupi ya kitambaa kigumu(kadeti) ambayo ilikuwa ya rangi ya kahawia. Alikuwa kavaa na vesti nyeupe  kwa juu iliyofanya matiti yake machanga yaonekane vyema, umbo lake la kibantu lilikuwa limeonekana vyema na nguo hizo alizovaa ambalo lilimfanya Norbert asiache kumtazama hadi alipoketi kwenye kiti ambapo mzigo wake wa nyuma ulitawanyika katika  kiti hicho ukafanya umbo lililojengeka chini ya kiuno chake sehemu ya mapaja lionekane pana sana kutokana na kaptula aliyovaa kumbana sana.



 Ilikuwa ni kaptula iliyoishia katika eneo la chini ya goti ambayo ilifanya mguu wake uliojaa uonekane vyema kwa Norbert ambaye alikuwa anatabasamu akimtazama tu, Norbert muda huo macho yake yalitua sehemu za kati ya mapaja kisha akayashusha mapajani akaweka mikononi katika mapaja hayo ambapo alimfanya Josephine amtazame kwa macho yenye aibu malegevu sana. Kitendo cha Josephine kumtazama Norbert kwa macho malegevu ilikuwa ni nafasi tosha ya Norbert kupeleka kinywa chake kwenye kinywa cha Norbert ambapo kilipokewa vizuri, walibadilisha shurubati ya kinywa a uchu humo ndani ya gari  hali ambayo iliwafanya wadumu kwa muda mrefu hadi pale Josephine alimpomtoa Norbert  kwa kumrudisha nyuma kifua chake kwa mikono yake laini.



  Norbert aliporudishwa hivyo nyuma aliamua kuleta kinywa chake kikafanikiwa akaendelea kubadilisha shurubati hiyo ya kichwa kwa muda mfupi kisha akautoa mdomo wake akuhamiaha jirani na sikio la Josephine, alilibusu kwa busu la muda mrefu sikio hilo sehemu ya juu  ambayo ilimfanya Josephine ajihisi hali tofauti iliyomlazimu amrudishe tena Norbert nyuma kwa kutumia mikono yake laini ya kirembo.



            "Nor bwana si tunaenda kwangu hebu acha" Josephine alilalamika kwa sauti inayotoka puani, Norbert naye akisitisha zoezi hilo ambalo lingefanya gari hiyo ibebe vurumai lao muda mfupi ujao. Aliwasha gari kisha akaliingiza barabarani akaendesha kwa kufuata maelekezo ya Josephine, safari yao iliishia kwenye nyumba ya kawaida ambayo ilikuwa na uzio wa matofali uliokuwa umechakaa kuoneaha ulikuwa umejengwa siku nyingi sana. Norbert alisimamisha gari katika lango la nyumba hiyo lililojengwa kwa namna ya kisasa ingawa uzio ulikuwa wa kizamani, Josephine alishuka ndani ya gari akaenda kwenye lango hilo ambalo alilifungua kwa ufunguo alioutoa mfukoni mwake.



Alilifungua lango lote na Norbert akaingiza gari hadi ndani katika mandhari nzuri yenye maua, ilikuwa ni ndani ya nyumba ya kawaida ambayo ilikarabatiwa  ikaonekana ni yenye kupendeza. Norbert alipeleka gari hadi kwenye maegesho ya nyumba hiyo kisha akalizima, alishuka ndani ya gari akafunga milango akamkuta tayari Josephine alikuwa amemalizia kufunga geti na yupo nyuma ya gari akimsubiri ashuke.



          "Karibu sana mpenzi hapa ndiyo kwangu" Josephine alimkaribisha Norbert ambaye alizungusha macho katika mazingira ya nyumba hiyo kisha akatabasamu.



           "asante mpenzi umejitahidi sana" Norbert aliongea kisha akajisogeza karibu ya Josephine zaidi akawa anatazamana  naye usoni, aliweka mikono kiunoni mwa Josephine lakini ilitolewa kwa kimadaha na Josephine ambaye aligeuka nyuma akaanza kupiga hatua kuelekea kilipo kibaraza cha nyumba yake.



  Norbert hakulitilia maanani suala hilo ingawa alishagundua hali tofauti tangu wapo ndani ya gari yake Josephine alimpomfuata, alimfuata Josephine kwa nyuma hadi kwenye kibaraza cha nyumba hiyo. Josephine alitoa ufunguo ndani ya mfuko wa kaptula yake akafungua mlango wa nyumba hiyo, alimuashiria Norbert akaribie ndani akiwa na tabasamu pana usoni mwake.



  Norbert alipokaribishwa alichungulia ndani  eneo la sebuleni kisha akasita kuingia hali  iliyomshangaza nwenyeji wake, mshangao wa Josephine katika kumshangaa huko yeye aliutumia kama nafasi nyingine akampiga busu refu sana linalohusisha kukutanisha kwa ndimi vinywani. Josephine hakutarajia busu hilo la ghafla na alibaki anashangaa zaidi  hata alipoachiwa mapigo yalimuenda mbio sana akabaki anatazama Norbert kwa jinsi alivyotumia nafasi ile, Norbert yeye alibaki anatabasamu tu alipofanya kitendo hicho kisha akachuchumaa kwa kuugemea mguu mmoja.



            "Ni nyumba ya mke wangu yenye mandhari safi hivyo sipaswi kuingia na viatu" Norbert aliongea huku akianza kufungua kamba za viatu, Josephine alimzuia kisha akainama akafunga ile kamba ya kiatu ambayo Norbert rayari aliifungua.



 Alimshika mkono kisha akaingia naye ndani wakatokea kwenye sebule pana yenye makochi ya kisasa, ilikuwa ni sebule pia yenye madirisha yaliyobeba mapazia yenye mtindo wa kisasa wa kuwekwa vyuma. Mandhari hiyo ilipendeza zaidi na Norbert alibaki akiishangaa tu hadi pale Josephine alipomvuta aende kuketi kwenye kochi la kuketi mtu mmoja, Norbert aligoma kwenda kuketi kwenye kochi hilo la mtu mmoja kisha akalitazama kochi jingine linalotazamana na kochi lile.



              "nafasi ya kukaa karibu na wewe nitaipata wapi ikiwa nitakaa kwenye kochi hilo, ngoja nikaketi kwenye kochi lile pale" Norbert alisema kisha akaenda kuketi kwenye kochi kubwa lilipo mkabala na kochi la mtu  mmoja pia lipo mkabala na mlango.



   Kochi hilo liililokuwa lipo mbele ya dirisha lililofungwa na pazia zito kwa umbali wa  sentimita kadhaa  ndiyo lilimshawishi Norbert akae alipoingia ndani ya sebule ya nyumba hiyo.



              "nikuletee kinywaji gani laazizi?" Josephine aliuliza.



              "Chochote ukipendacho wewe na mimi nitapenda" Norbert alijibu.



              "Basi mimi napenda pegi za gongo sijui utakunywa" Josephine alitania.



              "mh!" Norbert aliguna na Josephine alicheka kwa nguvu sana.



                "mwaya nakutania ngoja nikuletee wine nafikiri utaipenda" Josephine aliongea.



                 "Yap ninaipenda tena kwakuwa hiyo ndiyo uliyoichagua" Norbert aliongea huku akitabasamu na Josephine alitoka akaelekea katika ukumbi mefu uliopo jirani na sebule na aliporudi alikuwa kabeba sahani kubwa aliyofunikwa pamoja na chupa ya mvinyo iliyowekwa bilauri kwa juu ili iwe rahisi kubebwa pamoja.



 Aliviweka vitu hivyo kwenye meza ya kioo ya kisasa ambayo ilikuwa ipo jirani na Norbert ambaye alibaki anatabasamu tu, aliisogeza meza jirani na Norbert huku akitingishika sehemu zake za mapambo. Josephine alifunua mfuniko wa sahani ambayo alikuja nayo na hapo ndizi zilizokaangwa vizuri pamoja na nyama za kukaanga zikaonekana, pembeni kulikuwa kuna kisu na uma pamoja na kachumbari iliyotayarishwa vizuri.



 Josephine alipovitenga hivyo vitu alinyanyuka tena akaelekea jikoni ambapo alirejea akiwa na jagi la maji lililowekwa kwenye beseni dogo, jagi hilo alimmiminia Norbert maji ili anawe mikono kisha akakinga beseni chini yake maji yamwagikie.



            "Karibu mume wangu mtarajiwa" Josephine alimkaribisha Norbert ambaye aliishia kutabasamu tu kisha akafungua  chupa ya mvinyo akaumimina kwenye bilauri,  Norbert hakutaka kufanya ajizi alichukua kisu akazikata ndizi vipande halafu akachukua uma akachoma kipande kimoja cha ndizi  kisha akakitia kachumbari.



 Alikipeleka mdomoni akasita kisha akamuita Josephine ambaye alijongea akaketi jirani naye, Norbert alimtazama Josephine kwa tabasamu kisha akautazama uma ambao ulikuwa umebeba kipande cha ndizi ambacho kingemtoa mate mtu yoyote kutokana na kachumbari iliyopo juu yake.



              "Ikiwa kwa sasa tumefanikiwa kuwa pamoja basi chakula hiki yatupasa kuonja pamoja, mwanamke mpishi mzuri kuliko wote huwa anaonja chakula chake akiwa mbele ya mpenzi wake" Norbert alimuambia Josephine huku akimpelekea uma wenye ndizi mdomoni, Josephine aliushika mkono wa Norbert kumzuia huku akimlegezea macho.



              "Kwa ajili yako baby haina haja ya kuonja kwani najiamini nimeandaa kitu special for you, nikionja mbele yako means sijiamini na pishi langu" Josephine aliongea.



               "siyo hivyo baby maisha nikushare kila kitu kasoro mavazi tu hivyo chakula tunashare pamoja, kula please" Norbert alimuambia huku akimsogezea uma wenye ndizi jirani na mdomo huku akimtazama Josephine kwa macho makini, mboni za macho ya Josphine zilikuwa zisizotulia hata kidogo na zilikuwa zinachezacheza kama mbegu ya sufi ikiwa inapulizwa na upepo mwingi.



 Alizidi kumsogezea uma karibu na mdomo wa Josephine  ambaye alikuwa amefumba mdomo hakufungua, alipofikisha uma ule kiasi cha nusu sentimita kutoka zilipo papi za midomo ya Josephine alihisi kitu cha baridi kikugusa kichwa chake mbele ya sikio.



                 "Welcome Kaila(Karibu Kaila)" Norbert alisikia ikitoka upande ulipo pazia  na alipopeleka jicho pembeni aliona bastola ndefu ikiwa imegusa kichwani, pazia lilifunguliwa na Benjamin akaonekana akiwa yupo nyuma ya pazia  .



 Muda huo  Josephine aliutoa mkono wa Norbert kwa taratibu uliokuwa umeshika umma ili kumlisha akaushusha chini huku akitabasamu, aliinuka akamtazama Norbert ambaye alikuwa alikuwa anahema kwa nguvu sana. Josephine aliachia kicheko cha nguvu sana kisha akamtazama Norbert kwa dharau sana, Norbert aliinua macho ya mshangao kumtazama Josephine ambaye ndiyo kakolewa na kicheko.



                  "Josephine ni wewe kweli?" Norbert aliuliza kwa macho yanayoonesha kutoamini kwa kile kilichotokea.
                  "Ndiyo mimi Josephine ukipenda niite Leopard Queen  nafikiri unanitambua Norbert Kaila wa East Africa Security Agency kwa kifupi EASA, siku zote ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu Norbert. Jumamosi ulinikimbia lakini leo nimekutia nguvuni huna ujanja wa kunikimbia sasa lazima ufe ka.." Josephine aliongea kwa majigambo na alikatishwa na Norbert aliyedakia maneno yake.



                   "Kama ulivyowaua wanajeshi waliyokuwa wanalinda nyumba yA General kule Muhimbili" Norbert alidakia akamshangaza Josephine, aliupuuzia mshangao wa Josephine kisha akaendelea "Ulifikiri mchezo wenu wa kitoto sitaujua Josephine, wakati naingia humu ndani uliponifungulia nilichungulia kisha nikarudi nikashika kamba za viatu nikaanzaa kufungua nivue viatu.  Sikutaka kuvua viatu Josephine bali nilizuga kwa chungulia mazingira ya humu ndani yakoje ndiyo nikaingia" Norbert aliongea huku akitabasamu tofauti na alivyokuwa na uoga hapo awali.



                   "Tena nimechungulia kupitia tundu la pazia kutumbukiza chuma niliweza kumuona huyu bwana kupitia kofia aliyovaa kujitokeza sehemu hiyo, bado nilivyoingia ndani ukanipeleka nikakae pale kwenye kochi la mtu mmoja lakini niliamua kuja kukaa hapa si kama nimepapenda bali ili nipachunguze kwani najua kwenye pazia kuna mtu. Nilipoinuka kwenye kochi lile kuja  hapa niliona kochi hili lipo mbele  ya pazi kiasi cha sentimita kadhaa tena limeburuzwa muda si mrefu na alama za kuburuzwa kwake nikaziona kwenye tiles" Norbett aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza sana Josephine, alipoangalia pembeni mwa kochi alilokaa Norbert aliona kweli alama za kuburuzwa.



   Alibaki akimtazama Norbert aliyekuwa anatabasamu usoni mwake ingawa alikuwa amewekewa bastola kichwani na Benjamin, alijilazimisha kutabasamu lakini bado mshangao wake juu ya akili za Norbert ulibaki palepale hakutegemea kama anagekuwa na uwezo wa kufikiria kiasi kile.



                    "Nesi aliyekuona ukitoka pale wodini baada ya wewe kuua wale wanajeshi alituambia sifa zako zote zilivyo nikakuchora nikaipata sura yako kamili, ulidhani nitadanganyika nilipokuwa nawe" Norbert alizidi kuongea huku akimtazama Josephine kwa dharau.



                     "Hey! You talked too much but today you will die , thanks my love for your help. Now eat your food( Hey! Umeongea sana lakini leo utakufa,  asante mpenzi wangu kwa msaada wako. Sasa kula chakula chako" Benjamin aliongea huku akimtazama Josephine kwa  sekunde kadhaa alimpompa shukran, alitoa usalama wa bastola kisha akamuamrisha Norbert ale chakula alichoekewa.



  Norbert aliposikia amri hiyo alimtazama Josepbine ambaye alikuwa anamtazama kwa tabasamu la kejeli kisha akanyanyua ule uma aliouchoma ndizi, Norbert aliunyanyua ule uma akaupeleka kinywani mwake taratibu na akazidi kumuona Josephine  akitabasamu. Alipoufikisha karibu na kinywa chake alisita kisha akausogeza kando ya mdomo, alitoa tabasamu pana huku akimtazama Josephine ambaye ndiye aliyemleta  katika mdomo wa kifo.



                    "Wait, your love and my love too. Oooh! Our lover(Subiri, mpenzi wako na mpenzi wangu pia. Oooh! Mpenzi wetu)" Norbert aliongea huku akitabasamu kama kawaida yake.



                      "Stop talking nonsense Norbert eat your food (acha kuongea yasiyo na maana Norbert kula chakula chako)" Benjamin aliongea huku akimkandamiza Norbert na mdomo wa bastola ambao umetengenezwa kwa chuma.



                       "Siyo nonsense Benson mpenzi wangu kwakuwa nimelala naye  na wewe ni mpenzi wako kwakuwa umelala naye, au Josephine naongopa?" Norbert alizidi kuongea maneno mengi yaliyowazubaisha  maadui zake, moyo wa Josephine uliposikia maneno hayo ulipiga kwa nguvu kama ulikuwa unapasuka kwani Norbert alikuwa ameanika mengine mbele ya mpenzi wake ambaye hakumruhusu kulala na Norbert ili awekewe mtego.



   Maneno hayo yaliibadilisha sura ya Benjamin akawa ni mwenye  hasira alipoyasikia kwani hakutegemea kama Josephine atafanya hivyo, macho yake yalikazika kutokana na matuta kujitokeza katikati ya nyusi zake.



                         "Benjamin usimsikilize huyo muue anapoteza muda tu" Josephine aliongea kwa kubabaika kwani alijua  Norbert tayari alikuwa amevuruga mambo.



                         "Ohooo! Kumbe Benjamin na siyo Benson, mapacha nyinyi inaonekana. Sasa muulize mpenzi wako ijumaa alilala wapi?" Norbert alizidi kupigilia msumari katika hasira ambazo tayari zilikuwa zimepanda kichwani mwa Benson, maneno hayo yalimfanya Josephine azidi kushtuka akaanza kurudi nyuma akawa anaelekea eneo ambalo kuna kabati iliyowekwa luninga na video ya santuri.



                          "Bitch! You slept with him! ( Malaya! Umelala naye!)" Benjamin aliongea kwa hasira kisha akaihamisha bastola kutoka kichwani mwa Norbert akamuelekezea Josephine akiwa ameweka kidole sehemu ya kufyatulia, ilikuwa ni nafasi ambayo Norbert alikuwa akiisubiri kwa hamu sana aweze kujinasua kwenye mtego ule.



  Nafasi hiyo hakutaka kuichezea kabisa aliamua kuitumia vile ipasavyo kwa mtu mwenye silaha ambaye angekuwa hatari kwake akimuachia, Benjamin aliponyoosha mkono wenye bastola kumuelekea Josephine alifyatua risasi kwa haraka sana ambayo alilenga kumpiga nayo huyo binti huyo kwenye paji la uso  lakini ilimpata ya bega  baada ya Norbert kuudaka mkono huo akiwa na lengo la kumzuia. Norbert alipoudaka mkono wa Benjamin kwa kasi ya ajabu alimuinua juu kwa mtindo wa judo kisha akamwangusha juu ya meza ya kioo iliyokuwa ipo mbele yake, lilikuwa ni pigo ambalo lilimnyamazisha Benjamin papo hapo baads ya kukatwa na vioo na kichwa chake kupigizwa kwenye kioo kigumu.



  Norbert alimtazama Benjamin ambaye alikuwa anavuja damu kisha akachukua bastola yake ambayo bado ilikuwa na risasi, alimsogelea Josephine ambaye alikuwa ameanguka chuni baada ya kupigwa risasu huku akimnyooshea bastola.



                       "Norbert usiniue tafadhali" Josephine aliongea huku akijishika jeraha lililojeruhiwa na risasi ilitofayatuliwa na Benjamin ambayo ilikuwa impate kichwani.



                       "Laiti ningetaka ufe basi ningemuacha  huyo bwana wako aumwage ubongo wako" Norbert aliongea huku akikichuchumaa mbele ya Josephine akawa anamtazama kwa huruma, aliitazama na bastola ya Benjamin yenye kiwambo cha kuzuia sauti kisha akashika Josephine nyuma ya shingo.



                      "Ukawape salamu kuwa N001 hakamatwi kijinga namna hiyo" Norbert alimuambia Josephine ambaye alishtuka baada baada ya kusikia namba ya mpelelezi hatari wa EASA ambaye hakuwa anamjua kwa sura, mshangao wake huyo ulizimwa na busu zitO lisiloashiria upendo kutoka kwa Norbert ambalo Josephine alilipokea bila kupenda. Norbert alipomaliza kumpiga busu hilo alimuongeza na kitako cha bastola cha kisogoni, Josephine alizirai papo hapo.



      Norbert alimpekua Josephine mifukoni mwake akatoa simu ambayo alipekua kwenye ujumbe wa maneno hadi alipopata namba ambayo aliitilia shaka, aliipiga namba hiyo na aliiweka simu sikioni ilipoanza kuita.



                     "Siyo Leopard Queen ni N001 hapa nimepita nyumbani kwa Leopard Queen na Benjamin njoo uchukue masalia" Aliongea  baada ya simu kupokelewa kisha akakata pasipo kusikiliza upande wa pili ulikuwa unssemaje, alipomaliza alichukua funguo za mlango na geti  kisha akatoa kitambaa akafuta sehemu zote ambayo alikuwa amegusa kwa mikono yake.



  Aliondoka ndani ya eneo hilo akiwacha wenyeji wake katika hali tofauti na jinsi walivyompokea, alitoka nje ya nyumba hiyo na alifungua geti kisha akatoa gari nje halafu akalifunga geti kama zilivyo funguo akazitupa ndani ya uzio.



  Aliondoka eneo hilo la Keko kwa kasi sana akiwa na uhakika tayari simu yake ilikuwa imefika mahali husika, tabasamu pana lilikuwa limechanua usomi mwake baada ya kupiga hatua katika kazi yake ya hatari.

 Simu hiyo aliyopiga Norbert ilipokelewa na Wilson akiwa katika mapumziko kitandani, alikuwa amelala baada ya kufanya jimai na mwenza ambaye alimchukua siku hiyo. Taarifa alizozipokea zilimfanya ashtuke hadi mwenza aliyekuwa naye ambaye alikuwa amelala kifudifudi bila nguo akageuka, mwenza huyo alikuwa ni binti mdogo sana wa miaka chini ya ishirini na tano. Alikuwa ni binti mchanga kabisa ambapo kifua chake kilionekana dhahiri  kutokana na kutokuwa na nguo, binti huyo alimtazama Wilson jinsi alivyoshtuka kisha akamshika mabegani mwake kwa upendo baada ya Norbert kukata simu.



            "Baby kuna nini jamani mbona hivyo?" Binti huyo alimuuliza Wilson kwa upendo mkubwa huku akilegeza sauti.



            "Matatizo ya kibiashara tu Farida, inabidi nitoke nikaonane na washirika wangu ili tuyaweke sawa usiku huu huu" Wilson aliongea huku akinyanyija kitandani.



        "Jamani mpenzi kwahiyo itakuwaje?" Farida aliuliza.



          "Usiwe na hofu Farida tutakutana siku nyingine ngoja nikupe ya matumizi, asubuhi wewe nenda chuo tu ukaendelea na masomo" Wilson aliongea huku akivaa nguo zake, alipomaliza aliingiza mkono mfukoni akatoa kitita cha pesa ambacho alimpatia Farida kisha akambusu mdomoni binti huyo ambaye angeweza hata kuwa mpwa wake.



Wilson hakutaka kupoteza .muda alichukua funguo zake za gari akatoka chumbani humo usiku huohuo, alitembea kwa haraka hadi yalipo maegesho ya magari akaingia ndani ya gari yake akaiwasha akaiondoa eneo hilo

Safari ya Wilson iliishia yalipo makao ya muda ya vijana wa kazi waliopeww, akionekana ni mwenye kuchanganyikiwa Wilson alipiga honi mfululizo alipofika kwenye lango la nyumba ambayo ndiyo kambi ya vijana wa kazi walioletwa nchini. Lango la kambi hiyo ambayo imebeba nyumba ya kifahari ndani yake lilifunguliwa kwa haraka baada ya kutambuliwa ujio wake na mlinzi wa eneo hilo, Wilson aliingiza gari ndani kwa kasi ya ajabu hadi mbele ya kibaraza cha nyumba hiyo ambapo alilisimamisha kwa ghafla, alishuka ndani ya gari hiyo akawakuta Benson na wenzake tayari wakiwa wanamsubiria eneo hilo.

       "Nyinyi yuko wapi Benjamin na Leopard Queen?!" Wilson aliuliza kwa jazba huku akihema kwa nguvu.



      "Wilson usiwe na papara namna hiyo tuambue kuna nini?" Santos aliuliza.



        "Nimewauliza na nyinyi mnaniuliza swali tena, Benjamin na Leopard wako wapi?!" Wilson aliuliza tena akiwa na jazba sana, muda huo huo mlango wa kuingia ndani ulifunguliwa na Filbert Ole akatoka ndani akajongea hadi eneo walilopo  Wilson na kina Santos.



        "Wilson kuna nini tena mbona wahka mwingi mdogo wangu?" Filbert Ole aliuliza.
         "Kakaa nimepigiwa kwa namba ya Leopard Queen nimepokea nikijua ni yeye kumbe ni N001" Wilson aliongea kwa kulalamika, watu wote waliposikia namba hiyo ya N001 walishtuka kisha wakamtazama Wilson kwa umakini sana.



          "Eeeh! Ni..niambie kakuambiaje" Benson aliuliza akiwa na kigugumizi baada ya kubaini mtu hatari alitumia simu ya mpenzi wa pacha wake, Wilson alipokuwa akijiandaa kuendelea kuongea yeye alimuona kama anachelewa kuongea. Kumuharakisha kuongea ilimbidi amshike mkono kwa nguvu na akimtikisa huku akiita jina lake, Wilsom aliona ilikuwa ni kero akautoa mkono wa Benson ulipokuwa umemkamata na akaweka mambo wazi.



          "Ameniambia nikafuate masalia nyumbani kwa Leopard Queen" Wilson aliongea huku akikaa kibarazani bila kupenda kutokana kuchanganywa na habari hiyo, waliobaki wote waligwaya kutokana na taarifa ile hasa Benson ambaye alichanganyikiwa kabisa baada ya kusikia hivyo. Ama kweli damu ni nzito kuliko maji, kijana mwenye mgumu uliokomazwa na mafunzo mbalimbali pamoja na kazi za hatari alipatwa na uchungu alipisikia taarifa hiyo inayohusu eneo ambalo pacha wake na Leopard Queen wapo.



 Benson aliweka mikono kichwani baada ya kusikia taarifa hiyo huku moyo wake ukiwa hauamini kabisa kwani alitambua mtu aliyetembelea nyumba hiyo ni mtu hatari sana, macho yake yalianza kuwa mekundu taratibu uchungu wa kusikia habari hiyo ulimkolea.  Aliwatazama wenzake ambao nao walikuwa wamepigwa butwaa ya ghafla na taarifa hiyo na hawakuwa wakizungumza chochote, kimya chao kilimfanya atoe bastola yake  aina ya Desert Eagle akaifungua magazine akaitazama risasi. Aliporidhika risasi zipo aliirudisha magazine ndani kisha akaikoki akaimuelekezea Wilson alipokuwa amekaa kibarazani huku akihema kwa nguvu, wote walipigwa na butwaa kwa kitendo hicho cha Benson na walipotaka kumsogelea alinyanyua bastola akawaelekezea wote.



          "Sitaki kumwaga ubongo wa mtu jamani nyote wekeni mikono kichwani wakati nadili na Wilson" Benson aliongea kwa hasira.



         "Benson" Filbert Ole aliita.



           "Kimyaa! Hamujui kwamba kaka yangu yupo kwenye hatari? Hamujui kama N001 ni mpelelezi hatari mwenye ujuzi wa kila mwanausalama, mnafikri pacha wangu atakuwa salama mbele ya mtu huyo" Benson aliongea kwa hasira kisha akaelekeza bomba la bastola alipo Wilson.



          " Wilson nipe funguo za gari lako upesi" Benson alitoa amri papo hapo, Wilson alianza kutetemeka na mwishowe alitoa funguo akamkabidhi Benson ambaye aliichukua kwa nguvu kama kibaka anakwapua simu mkononi.



Benson alijongea kwa haraka hadi lilipo gari la Wilson kisha akabonyeza  rimoti ya kufungua milango huku akiwaangalia wenzake waliobaki akimshangaa, alipogusa kitasa cha mlango kufungua aingie ndani ya gari Santos alipiga hatua  moja mbele. Hatua hiyo iligundulika na Benson ambaye aligeuka nyuma kwa haraka akalifyatua risasi chini ikatua kwenye  sakafu maalum iliyopo mbele ya kibaraza, sauti kubwa ya mlipuko wa bastola ilisikika ambayo ilimfanya Santos agande hivyo hivyo asiendelee na hatua ya pili. Wengine wote waliobaki walipatwa na mshtuko kutokana na mlipuko huo wa bastola, Wilson kwa uoga alirudi zaidi nyuma kwa kusota na makalio akipanda ngazi mbili za kibaraza akiwa na uoga mkubwa.



          "Nimesema asinisogelee mtu" Aliongea kwa ukali kisha akaingia ndani ya gari akafunga milango yote pamoja na vioo akiwaacha wenzake wakiwa wamepata ujanja wa kuweza kusogea mbele lakini hawakuweza kuingia ndani ya gari hiyo. Benson aliwasha gari kisha akalirudisha nyum kwa kasi akaigeuza katika eneo hilo la maegesho, geti tayari lilikuwa limeshafunguliwa hadi muda huo na ikawa rahisi kwake kutoka ndani ya nyumba hiyo kwa kasi sana akiwaacha wenzake wakimshangaa hadi alipopotea katika upeo wa macho yao.



         "Wote muende nyumbani kwa Leopard Queen upesi sana" Filbert Ole alitoa amri, vijana wa kazi pamoja na Wilson waliondoka hadi kwenye banda maalum la magari wakafungua milango. Wote kwa pamoja waliingia ndani ya mandhari yenye magari mbalimbali yaliyoegeshwa na walichangua gari ambayo waliingia wakawasha kisha wakaliondoa eneo hilo kuelekea getini ambapo walitoka wakafuata uelekeo wa barabara aliyopita  Benson.

Baada ya kuacha balaa na kutoweka mara moja akimpigia simu mmoja wa mbaya wake, Norbert aliamua kuelekea moja kwa moja Kurasini katika nyumba ya kampuni. Ndani ya dakika kadhaa tayari alikuwa ameshaingia katika nyumba hiyo akaegesha gari katika maegesho, alishuka kwenye gari moja kwa moja akazama ndani ya nyumba hiyo kwa lengo la kukutana na mwenzake.



Muda anaoingia ndani ya nyumba hiyo ndiyo muda ambao Benson alipatwa na kiwewe baada ya kusikia ujio wa N001 ambayo imesimama mbadala ya utambuzi wa Norbert kikazi zaidi, alipoingia ndani ya nyumba hiyo alikutana na  Moses pamoja na M.J Belinda wakiwa wamekaa sebuleni katika makochi tofauti wakijadili mambo. Norbert alijongea mita chache kutoka pale walipo kisha akasimama akaweka mikono kiunoni akiwatazama kila mmoja halafu akawanyooshea vidole, alitoa tabasamu kisha akatikisa kichwa kusikita akiwatazama.



         "Ndiyo nini hivyo?" M.J Belinda aliuliza.



         "Aisee mna balaa" Norbert aliongea huku akisikitika.



            "Sikusomi ujue" Moses naye alimuambia Norbert akitumia lugha ya misimu akimaamisha hamuelewi.



            "Hivi toka lini Simba akakaa na Pundamilia aliyenona hata asimpige kucha maana anamtamanisha  hata akiwa ameshiba" Norbert aliongea kimafumbo akiwalenga Moses na MJ Belinda ambao walikuwa wamekaa pamoja, wote  waliposikia maneno hayo walibaki vinywa wazi na M.J Belinda ndiyo akamfuata kwa kasi.



           "Muhuni mkubwa ndiyo yaliyopo kichwani mwako hayo kila siku" M.J Belinda aliongea huku akimkaribia  ambaye alikuwa anacheka alipoongea hayo maneno, alipomfikia alirusha kibao cha kilegevu ambacho Norbert alikikwepa kisha akaanza kukimbia kuzunguka sebuleni hapa. M.J Belinda alimkimbiza. Norbert alikimbia kuzunguka  sebule hiyo hadi pale M.J Belinda alipoacha kumkimbiza ndipo naye alisimama, wote walirudi kwenye kochi wakaketi kisha macho yakawa yanaelekea kwa Norbert.



          "Ujio wako una jambo si bure" Moses alimwambia Norbert.



          "Nimekuja kuwaambia kazi imeanza" Norbert aliongea.



          "Aaah! Wewe kuna la ziada nafikiri unahitajika kutueleza" Moses aliongea



             "Yeah ndiyo lipo na ni hili hapa, Benson ana pacha wake anaitwa Benjamin ambaye tayari kwa sasa si miongoni mwa viumbe hai hivyo mchakamchaka umeanza kuna ulipaji kisasi" Norbert aliongea.



           "Umemkata fyuzi tayari siyo?" Moses aliuliza.



            "Of Course ningechelewa angenikata yeye kwani alikuwa na mguu wa kuku" Norbert aliongea.



             "Na sisi tuna jipya nafikiri linahitaji msaada wako kwani wewe ndiyo mtaalamu wake pekee" Moses aliongea.



           "ni lipi au kuna chuma hakitaki kunyooka" Norbert aliongea.



             "Kama ulikuwepo hebu twende basement ukakione nafikiri kwa mtaalamu wake kitanyooka" Moses aliongea huku akisimama, Norbert na M.J Belinda nao wakasimama.



Wote kwa pamoja waliifuata korido ndefu iliyoanza hapo sebuleni  hadi  mwisho, walikuta ngazi ambazo walizishusha hadi chini kiasi cha ghorofa moja. Walikuta mlango ambao waliufungua wakatokea kwenye korido nyingine fupi iliyotenganisha vyumba kadhaa, waliifuata korido hadi mlango wa pili upande  wa kulia uliotengenezwa kwa chuma. Moses aliufungua mlango hyo mzito kwa namba maalum kisha akaingia ndani wenzake wakifuatia, waliingia katika chumba chenye giza ambacho kilipowashwa taa alionekana yule mzungu aliyebaki mzima baada ya kuachiwa kichapo na Moses akiwa amefungwa kwenye kiti cha chuma kilichopo pembeni ya mapazia yanayotumika kwenye wodi za hospitali. Tayari alikuwa ana fahamu zake ingawa alikuwa ana majeraha mbalimbali kutokana na mateso aliyopewa, Norbert alipomuona mzungu huyo alimtazama huku anatabasamu tu.



          "Chuma chenyewe kisichonyooka ni hichi au kingine?" Norbert aliuliza kwa dharau sana huku akimnyooshea kidole mzungu yule.



        "hiko hiko" M.J Belinda alimjibu.



          "nilidhani ni chuma cha pua kumbe ni hichi cha kawaida" Norbert  aliongea kisha akavaa koti la kitabibu lililopo ukutani mwa chumba hicho, alitembea hadi kwenye kona moja ya chumba hicho yenye meza iliyofunikwa na kitambaa ambayo aliisukuma hadi mitaa kadhaa kutoka yule mzungu alipo.



  Mzungu huyo ndiye yule aliyepigwa goti la uso  na M.J Belinda kabla wenzake wawili  hawajauawa na Mose, alikuwa ameleta kiburi cha kutotaka kuongea neno lolote baada  ya kubanwa na Moses kwa kushirikian ns M.J Belinda ambao hawakuwa na utaalamu sana katika masuala ya kubana watuhumiwa hadi pale alipofika Norbert mtaalam aliyesomea masuala  hayo kiziada  nchini Cuba wakati akisomea ukomandoo ngazi ya juu kabla hajapelekwa Japan kujifunza Ninjutsu(Uninja).
 Tangu ahitimu mafunzo hayo hakuna mhalifu aliyewahi kubanwa na yeye akakataa kusema ukweli, wahalifu tofauti ikiwemo Tasi katika kisa cha JINAMIZI na mzungu Scott katika kisa cha SHUJAA walikuwa wabishi lakini waliongea wenyewe walipopewa kibamo kikali sana. Sasa akiwa na meza ya mteso pamoja na nguo maalum za kutesa watu tayari yupo mbele ya Mzungu aliyeleta ubishi, Norbert alimtazama tena yule mtu kisha akatabasamu zaidi halafu akachukua kibanio kimoja maalum kwa kutolea meno akawa anajongea kumsogelea yule mzungu.



          "Hana jino hata moja huyo" Moses alimuambia Norbert ambaye alisita akarudi kwenye meza ile yenye vifaa akakirudisha kifaa alichokichukua.



           "Kwahiyo kawa kibogoyo na bado anagoma, dawa mbili nampa ataongea mwenyewe" Norbert aliongea kisha akaenda ukutani akawasha swichi ya umeme, Yule mzungu alipigwa shoti sana lakini hakunyanyua mdomo wake kusema.



    Wakati shoti za umeme ambazo zilikuwa zimeunganishwa na kiti cha umeme zikiendelea kumsulubu vilivyo yeye alipiga kelele sana, alipoachiwa alikakaa kimya na hakusema chochote kuonesha yeye ni jeuri sana. Hali hiyo ilimfanya   Norbert amtese pasipo huruma hadi alipoishiwa nguvu ndiyo akamuachia, alibaki  akiwa anamtazama tu yule Mzungu kisha akasikitika.



          "Tumekwambia hicho ni chuma imara" Moses alimuambia Norbert.



             "Kila kitu kina namna yake huyu atasema tu" Norbert aliongea kisha akavua mipira aliyovaa mikononi, alitoka ndani ya chumba hicho  kwa dakika kadhaa na aliporejea alikuwa amebeba mtungi wa gesi pamoja na jiko lake.



 Aliwaacha Moses na M.J Belinda vinywa wazi lakini yeye hakuwatilia maanani, alifika hadi mbele ya Yule mzungu kwa mitaa kadha akaunganisha mpira wa gesi wa jiko na mtungi halafu akalijaribisha kuliwasha.



          "We Nor unataka kufanya nini?" M.J Belinda aliuliza



           "Bibie kuwa mtazamaji ingawa hii hutaona kila kitu" Norbert alimuambia M.J Belinda kisha akaliweka jiko la gesi chini ya kiti cha chuma ambacho kina madini ya bati katika sehemu ya kukalia. Wenzake walikuwa wanamshangaa lakini hakujali hata kidogo yeye aliendelea na kazi yake, alifunika mashuka ya hospitali yaliyokuwepo humo ndani ili waliopo nje wasione kinachoendelea.



          "Nor unajua sikuelewi" M.J Belinda aliongea.



            "Aaah! Bibie kuwa na subira hichi chuma nimekiletea asidi ili kiyeyuke kabisa" Norbert aliongea, kuteswa kwa namna hiyo ambapo Moses hakuwahi kupaona kulimvuta aingie ndani ya mapazia kuja kutazama.



  Hakika ilikuwa ni mbinu ambayo hajawahi kuiona ikitumika kwenye mateso, alisimama ndani ya kingo moja ya mapazia hayo akiwa na shauku kubwa ya kutazama jinsi ambavyo mbinu hiyo ilivuokuwa ikifanya kazi.



 Norbert aliliwasha lile jiko la gesi ambalo liliwaka lakini moto wake haukugusa sehemu ya kukalia ya kiti hicho cha mateso, alimvua yule mzungu suruali aliyovaa hadi  magotini kilazima akabaki hana nguo na makalio yake yakawa yamegusa sehemu ya bati ambayo hutumika kukalia katika kiti hicho chuma.



       "Eleza kila unachokijua kwenye mpango wenu" Norbert alimwambia akiwa ameshikilia chuma kimoja kifupi kilichosimama pembezoni mwa kiti hicho, Mzungu yule bado alileta jeuri kisha akatema ambayo Norbert aliyakwepa. Kitendo hicho kilimfanya Norbert atabasamu kisha  akachuchuma akaongeza moto kwenye jiko la gesi, akiwa na tabasamu lake lilelile usoni mwake alikishika kile chuma kifupi cha pembezoni mwa kiti akakipeleka kulia mara moja. Kiti cha mateso kilianza kushuka chini taratibu kikaufikia ule moto wa jiko la gesi katika eneo lenye madini ya bati ambayo hutumika sana kutengenezea masufuria, moto huo ulianza taratibu kupasha moto eneo hilo la bati ambayo ilisafirisha joto hadi kwenye makalio ya mzungu huyo.



        "Sasa ukaribishe ugumba katika mwili wako nakubanika makalio yako hadi korodani zako mpaka utapoongea ukweli" Norbert alimwambia yule mzungu huku akitabasamu kama ilivyo kawaida akiwa anatesa wahalifu.



Madini ya bati(aluminium) ambayo hushika joto kwa haraka yalishika joto kama ilivyo kawaida yake, taratibu joto hilo likaanza kupamba likafika katika kiungo laini ndani ya mwili  mwanaume kisichohitajika joto kali kwa ajili ya kulinda seli za manii. Moto huo ulikuwa umeleta joto ambalo lilifika kwenye korodani kwa haraka, lilianza kuwa kama joto la kawaida na hatimaye likawa joto lenye kuumiza ngozi ya korodani ambayo ilishindwa kustahimiliwa na mzungu huyo hadi akapiga kelele akiyadhihirisha wazi mapengo yaliyojaa baada ya  kung'olewa meno na Moses.



 Ukomandoo wa mzungu huyo uliisha papo hapo mbele ya kuchomwa kwa mwenyekiti wa mwili wake, alizidi kupiga kelele huku akijaribu kufurukuta lakini kamba ngumu pamoja na vyuma alivyofungwa mikinoni na miguuni zilimzuia kufanya hivyo. Alizidi kuoiga kelele huku akimtazama Norbert lakini Norbert hakuonesha kuguswa na maumivu, alikuwa akitabasamu tu huku akimtazama.



       "Nimetumwa na mabosi wangu Sir Shaw na Don Ahmed kuja kuwamaliza vikwazo vyote ili nchi iweze kupinduliwa" Mzungu huyo aliongea kwa nguvu akasababisha Norbert ainuke aende kuzima jiko la gesi.



      "Kwa lengo gani hayo mapinduzi yafanyike" Norbert aliuliza.



        "Lengo lake ni kupitisha ushoga ambao rais wa nchi aligoma kusaini mkataba wake kisha akasababisha ipite sheria ya kuzuia ushoga, aaagh!  Tulitakiwa tuwaue nyinyi halafu nchi ipinduliwe watu walazimishwe kwa lazima kuukubali ushoga" Mzungu huyo aliongea huku akiwa bado ana maumivu.



      "Ok wakubwa wenu hapa nchini ni nani na nani?" Norbert aliuliza



       "Filbert Ole, Liutenant General Ibrahim na Wilson Ole  aaargh!" Mzungu alizidi kuongea kwani tayari alikuwa ameishiwa ujanja wote kwa maumivu aliyoyapata.

“Huo mpango ulianzia wapi?” Norbert aliuliza.

       "Umeanzia kwa wakubwa ambao siwafahamu waliwapa pesa mabosi wetu aaaargh! Walipewa dola milioni 600 ambazo Rais wenu alizikataa kusaini mkataba kupitisha mpango huo"



       "Kiongozi gani aliyewapa maelekezo yote na ni wapi alipo?" Norbert aliuliza swali ambali halikujibiwa na Mzungu huyo aliyekuwa akipiga vitunu vya maumivu  Kimya chake kilipozidi alimuambia,"niwashe tena jiko siyo".



        "Mzee Filbert Ole ndiye alitupa maelekezo baada Mnadhimu mkuu wa jeshi L.J Ibrahim kumpa kazi Belinda  ili achelewe kutoka"



       "Kwa sasa yupo wapi Filbert Ole?"



       "Sipajui panaitwaje  alipoila ni Peninsula eneo katika jiji hili"



   Kauli ya mzungu huyo iliwafanya Norbert na Moses watazamane kwa muda kisha wakaafikiana jambo kwa ishara, Moses alirudi alipokuwa amesimama M.J Belinda na Norbert alimpandisha suruali juu yule mzungu akatoka.

 Gari waliyopanda Santos,Thomas na Wilson ilisimama kwa ghafla mbsle ya gari ya Wilson ambayo Benson aliichukua, wote kwa pamoja walishuka ndani ya gari waliyokuja nayo wakaenda hadi ilipo gari ya Wilson. gari hiyo waliikuta inawaka ikiwa haijazimwa huku taa za mbele za gari hiyo zikimulika lango la kuingilia nyumbani kwa Leopard Queen. Walifungua kwa pamoja milango ya gari hiyo wakakuta ipo wazi yote haikubanwa, Benson pekee ndiyo hakuwepo ndani ya gari hiyo lakini kila  kitu kilikuwepo.



Hapo walitambua kwa asilimia zote kwamba Benson atakuwa ameenda ndani ya nyumba hiyo na si vinginevyo, wote kwa pamoja waliuendea lango wa nyumba hiyo wakajaribu kulifungua lakini haukufunguka. Lango ulikuwa umefungwa kwa ndani hali iliyowalazimu waruke ukuta ili waingie kimyakimya, waliruka ukuta wakatua sehemu yenye bustani ya maua kisha wakajongea taratibu kuufuata mlango wa mbele wa kuingia ndani ya nyumba ambao upo kibarazani.

Bastola zao zikiwa zimeelekezwa mbele baada ya kuzichomoa kiunoni mwao walisonga mbele hadi mlangoni, sauti ya kilio cha ndiyo Benson ndiyo iliwapokea walipofika barazani ingawa haikuwashawishi washushe bastola waingie mithili ya Ng’ombe anaingia sehemu ya kuchinjia. Walifungua mlango wa nyumba kwa tahadhari na wakaingia ndani ya nyumba kwa kuelekeza midomo ya bastola zao, waliingia hadi sebuleni ambapo walimkuta Benson akiwa amepiga magoti ameukumbatia mwili wa pscha wake Benjamin ukiwa unavuja damu.

Benson hakujali uwepo wa vipande vya vioo yeye aliweka magoti eneo lenye vioo ambavyo vilikuwa vinamkata kwenye magoti, alikuwa akilia kama mtoto mdogo wala hakujali damu ambazo zilikuwa zikimchafua. Pembeni walimkuta Leopard Queen(Josephine) akiwa hajitambui kutokana na kutokwa na fahamu, hali waliyoikuta humo ndani iliwafanya wote wabaki wakiutazama mwili wa Komandoo wao mwenye ujuzi wa hali ya juu kushinda wao ukiwa umekumbatiwa na komandoo mwingine mwenye ujuzi zaidi.

Benson katika kulia huko hakuwa ametambua ujio wa wenzake na alipotambua aliwatazama kwa macho yake yaliyokuwa mekundu mithili matunda damu mbivu, machozi yalikuwa yakimtoka katika macho hayo ambayo yanatambulika kwa kuwa na hisia ngumu ambazo siyo rahisi kulia hapo hisia zote zililainika kwa kuondokewa na ndugu yake wa damu.

       "Aaaaaaaargh! N001 sitokuacha mzima nikikutana na wewe, utalipia damu ya ndugu yangu" Benson aliongea kwa hasira huku akiuma meno yake, uchungu wa kuuliwa ndugu yake ulikuwa ukimuuma huku akisahau kwamba yeye ni hodari sana wa kuua baba,mama, kaka na dada wa wenzake. Ama kweli nyani haoni kundule ila anaona ya wenzake tu, Benson aliendelea kulia kwa uchungu baada ya kutoa maneno hayo ya kulipiza kisasi kwa N001 ambaye ametembelea nyumba hiyo pasipo kuacha alama ambayo ni rahisi kutambulika.



  Wilson aliacha kumtazama Benson kwa huruma kutokana na jinsi anavyolia na alianda  kumtazama Leopard ambaye hakuwa na fahamu, alimtazama uzima kama upo kwa haraka na hapo tabasamu la hafifu matumaini likajaa katika uso wake.



            "Leopard Queen ni mzima jamani" Wilson aliwaambia wenzake huku akiharibu kumuinua, Thomas alikuja kwa haraka akasaidiana naye kumuinua na wakaenda kumlaza kwenye kochi wakiwa hawamjali Benson aliyekuwa akilia kama mtoto mdogo.



  Huduma ya kwanza kwa Josephine ilianza kutolewa kwa haraka huku mawasiliano yakifanywa kwa wakubwa zao, ndani ya dakika kadhaa tayari walikuwa wameshasambaza mawasiliano kwa wenzao wote ingawa waligwaya zaidi katika kusambaza taarifa hiyo. Kugwaya kulitokana na Wilson kuipiga namba ya mzungu aliyekuwa yupo chini ya kina Norbert ili ampatie taarifa, maneno aliyoyasikia kwenye simu hiyo yalimfanya aibamize chini kwa nguvu simu yake ya kisasa aliyoinunua kwa gharama.



         "Aaaargh! N001 Tenaa!" Wilson aliongea kwa ghdhabu pasipo kuijali simu yake ambayo ilikuwa ishagawanyika vipande, sauti yake ilimfanya Benson auachie mwili wa ndugu yake akasimama kwa ghafla aliposikia jina la muuaji wa ndugu yake linatajwa.



         "Yuko wapi?!" Benson aliuliza kwa hasira.



"Amepokea simu ya Golden pia" Wilson alimjibu Benson ambaye alikuwa tayari amechnganywa na kifo cha pacha wake, tarifa hiyo iliwachanganya pia kina Santos nao wakabaki wakiwa wamegwaya. Walitambua tayari walikuwa wamewahiwa na mjanja zaidi yao ambaye walikuwa wakimtambua kwa jina la     N001 badala ya kumtambua sura na jina lake halisi.



 Wote waliowahi kumtambua N001 kwa sura yake halisi tayari walikuwa ni marehemu na wachache waliomfahamu kama mpelelezi pasipo kumtambua kwamba ndiye huyo mpelelzi hatari kati ya wapelelezi watano wa daraja la juu wa EASA wenye majina yanayoanziwa na herufi 'N' akiwemo Norbert. Tayari kazi yao iliyowaleta ilikuwa imeshaingiliwa na adui yao mkubwa ambaye hawakumtambua ndiye waliyekuwa wakimuwinda wakamkosa,walichoka pasipo kuchokeshwa na walipagawa pasipo kupagawishwa na kitu  chochote.



Benson alitoa ukelele wa hasira aliposikia taarifa hiyo kisha akapiga magoti kwa ghafla huku macho yake akiangalia lilipo dari la sebule hiyo, aliweka mikono ambayo ilikuwa imetapakaa damu usoni mwake baada ya tarifa ya uhakika ya kumpata Norbert ikiwa haipo. Matarajio ya Benson ilikuwa ni kwamba Wilson alikuwa amepata mahali ambapo Norbert alikuwepo, aliposikia taarifa ya kwamba alitumia simu ya Golden kuongea ilimfanya azidi kupagawa zaidi.



 Santos naye alipandwa na hasira zaidi akapiga ngumi hewani huku akiachia matusi mfululizo kutokana na taarifa hiyo,Thomas alijikuta kiketi kwenye sofa bila ya kupenda na mikono akaweka kwenye mashavu yake kama alikuwa amepokea taarifa ya msiba wa ndugu yake anayempenda.



             "Hivi huyu N001 ni nani hasa mpaka atuchezee akiili namna hii' Santos aliuliza huku akiuma meno kwa hasira sana.



              "ni very dangerous spy wa EASA na tusipokuwa makini basi tutaisha wote" Wilson aliongea



              "Unasema nini Wilson  kwahiyo unamuhofia na wewe huyo mtu' Santos aliongea kwa hasira huku akimtazama Wilson.



               "Santos cool down, akisemacho Wilson ni sahihi kabisa tuwe makini maana tunacheza mchezo na mtu tusiyemjua ambaye anatujua' Thomas aliongea kwa utaratibu huku akimtazama Santos ambaye alikuwa amezidi kuwa mwekundu zaidi hata ya rangi yake ya uhindi wekundu kutokana na jinsi alivyoona wanazidi kupungua kutokana na kazi ya N001 ambayo anaifanya kimyakimya.



                "Come on Thoms hiyo ni ishara ya uoga kumpa sifa hivyo huyo mtu ambaye anazidi kutupa hasara na hata Don na Sir wakikusikia watakata kichwa chako" Santos alimuambia Thomas.



                "Ok kumpa sifa ni ishara ya woga siyo, vipi kuendekea hasira katika kazi ambayo unatakiwa utulize kichwa ili uweze kuifanya ni ishara ya nini? Kushindwa" Thomas aliongea kwa msisitio zaidi huku akimtazma Santos kwa macho makali, Santos naye alibaki akimtazama  Thomas akiwa na macho makali baada ya kusikia kauli hiyo ambayo ilikuwa ya ukweli ndani yake lakini ilikuwa ina karaha katika moyo wake.



                "Santos tunapambana na mtu mwenye kutumia akili zaidi kuliko nguvu vipi tutumie nguvu na hasira, fikiria kuhusu hilo Komandoo wa kuaminika miongoni mwa  makomando wa kuaminika wa Don Ahmed" Thomas aliendelea kumueleza Santos.



                "Santos akisemacho Thomas ni kweli kabisa tusitumie nguvu wala hasira mbele ya huyu N001" Wilson aliongea huku akimtazama Santos ambaye alibaki akimtazama Thomas kwa macho makali kutokana na maneno  aliyokuwa akiyaongea ambayo aliyaona yalikuwa yakimdhalilisha alipoyasikia lakini aliyaona yanafaa baada ya Thomas kuzidi kumuelezea kwa mara ya pili na kusababisha jazba iliyokuwa ikimpanda kuanza kupungua taratibu ingawa haikuwa imepungua yote hadi muda huo, maneno aliyoyaongeza Wilson yalimfanya ageuze macho pia amtazame kwa umakini halafu akashusha pumzi.



Macho yaliyokuwa yana dalili ya ukali ambayo yalipelekea uso wake kukunjika yalianza kurudi  katika hali ya kawaida taratibu, aliwatazama wenzake mmoja baada ya mwingine kisha macho yake akayahamisha kwenye kochi ambalo alikuwa amelazwa Leopard Queen baada ya kukutwa akiwa yupo chini tangu apoteze fahamu.



             "Tupo pamoja" Santos aliongea huku akiachia tabasamu fupi halafu kamuinua Benson pale chini alipokuwa amepiga magoti tangu alipokuwa akilia, alimshika mabega huku akimtazam usoni kwa umakini sana.



              "Benson hivi unahitaji kulipa kisasi kwa N001?" Santos alimuuliza Benson ambaye aliishia kutingisha kichwa kukubali.



              "Sasa ukikaa chini ukiendelea kulia ndiyo N001 utafanikiwa kumjua ni nani na ukaanza kumtafuta na kulipa kisasi?" Santos alimuuliza swali jingine Benson kwa sauti ya ukali zaidi, swali hilo halikujibiwa na Benson zaidi ya kukaa kimya huku akimtazama Santos kwa mcho yaliyokuwa yamezongwa na machozi sehemu za mboni zake.
Swali hilo kutojibiwa hakukumzuia Santos kuendelea kuongeea maneno ambayo alikuwa na uhakika yangemrudisha Benson katika hali yake ya kwaida na akaondokana na hasira iliyokuwa ikimkabili pamoja na uchungu wa kufiwa na kaka yake kipenzi. Santos alimuachia Bneson bega lake moja kisha akakunja vidole vyake vilivyokomazwa na mazoezi akiacha kidole kimoja ambacho ni cha shahada.



Alikielekeza kidole hicho cha shahada katika upande ambao alikuwa amelala Leopard Queen akiwa hana fahamu pasipo kuongea neno lolote kwa sekunde kadhaa, Benson kwa taratibu aligeuza macho upnde kilipoelekea kidole hicho cha shahada na macho yake yakatua katika mwili wa msichan wa kazi mwenye urembo wa asili wa kila aina ambao ungeweza kumvutia mwanaume yeyote yule mwenye utimilifu katika viungo vyake visivyohitajika kuonekana.



                 "Atakayeweza kukusaidia kumpata N001 ni yule ambaye amelala pale kwenye sofa akiwa hajitambui my friend, lakini ambaye anayeweza kukusaidia kumpata N001 hawezi kuwa msaada kwako pasipo kupewa msaada yeye utakaomuwezesha kukupa msaada wewe" Santos alimuambia kwa sauti iliyojaa msisitizo zaidi



                  "Unamaanisha nini?" Benson aliuliza huku akijifuta machozi kwa kutumia kiganja chake cha mkono.



                  "Come on Benson huoni kwamba hana fahamu yule na hatujui alipatwa na nini hadi akawa katika hali ile, anahitaji first aid yule ili aweze kufumbua macho na kutupa msaada katika hili" Santos alimuambia Benson huku akimminya bega lake ambalo alikuwa amemshika, Benson aliinamisha uso wake akiwa anajifikiria baada ya kuambiwa maneno hayo.



                  "Kumbuka wewe ni pekee uliyebaki mwenye taaluma ya utabibu ukiondoa Benjamin ambaye tayari hayupo nasi kimwili, hivi unafikiri ukiendelea kulia hapa huyu ambaye atakuwa msada kwetu ataweza kutusaidia vipi tumjue  huyo mtu ambaye anatuharibia mipango yetu. Try to think buddy" Snatos alizidi kumuambia Benson.



  Maneno ya Santos yaliweza kuleta athari nyingine katika ubongo wa Benson na yalisaidia kwa kiasi kikubwa katika kumbadilisha kutoka katika hali ya kulia na kuwa katika hali ya kawaida ingawa huzuni haikuwa imetoka katika uso wake, aliutoa mkono wa Thomas katika bega lake kisha akapiga hatua kumsogelea Leopard Queen aliyekuwa amelazwa pale kwenye kochi. Alipomfikia alianza kumkagusa sehemu za juu za mwili wake huku wenzake wakimtazama kwa tabsamu hafifu baada ya kuona amerudi katika hali yake ya kawaida, alimkagua Leopard Queen kuanzia usoni hadi miguuni na alipomaliza akageuka kuwatazama wenzake akiwa na uso wenye jambo ambalo alipaswa kuwaambia. Wenzake nao walimtazama kwa macho yenye shauku ya kutaka kujua kile alichokuwa nacho moyoni Benson, aligeuza tena shingo kamtazam Leopard Queen sehemu ya begani halafu akawatazama wenzake kwa zamu.



                          "Amepigwa risasi begani" Benson aliwaambia wenzake.



                          "N001 Mtoto wa Mbwa wewe" Wilson aliongea baada ya kupokea taarifa hiyo ambayo ilimtia hsira sana.



 Benson hakuijali kauli ya Wilson aliamua kumgeuka Lepard Queen kisha akamgeuza akalala kifudifudi akazidi kumkagua kuanzia sehemu za kisogoni ambapo alifunua nywele zake, alimtazama kwa umakini sana sehemu hizo ambapo alishuhudia nundu likiwa lipo kisogoni. Alimchunguza zaidi sehemu nyingine za mwili wake na hakumkuta na jeraha lolote jingine ambalo lingeweza kuhatarisha afya ya binti huyo, baada ya kuridhishwa na ukaguzi wake alimrudisha Leopard Queen alivyokuwa amelazwa chali.



                       "Yupo salama huyu hana tatizo jingine lolote, inaonekana  alipigwa na kitu kigumu kama kitako cha bastola au chuma sehemu za kisogoni ambacho kimefanya apoteze fahamu hadi muda huu" Benson aliwaambia kisha akambeba Leopard Queen akwaambia wenzake, "mbebeni na kaka yangu tuelekee chumba cha first aid".

Wilson na Thomas kwa haraka waliunyanyua mwili wa Benjamin baada ya kusikia kauli hiyo ya Benson, walifuatana na Benson ambaye alikuwa anatembea kwa taratibu kuelekea ilipo korido ndefu inayotenganisha vyumba katika nyumba hiyo huku Santos akiwafuata kwa nyuma.


Wakiwa wapo katika ofisi ndogo ya kipelelezi iliyotengenzwa ndani ya nyumba ya kampuni, simu ya Golden ambaye ndiye yule mzungu aliyekuwa akiteswa na Norbert iliita kwa kutoa mtetemo ikiashiria ilikuwa imetolewa sauti. Norbert aliipokea simu hiyo kwa haraka baada ya kuona jina linalonekana kwenye simu ndiyo lile aliloliona kwenye simu ya Leopard Queen akalipiga. Ilikuwa ni simu ya Wilson ndiyo ilikuwa inapiga, baada ya kuiweka sikioni simu aliwaashiria wenzake wake kimya nao wakafanya vivyo hivyo.

           "Ni N001 kwa mara nyingine ewe unayejiita Nouther karibu kwenye mchezo" Norbert aliongea na maneno na simu upande wa pili ikakatwa ghafla ambapo aliishia kutabsamu tu, ilipokatwa simu iyo ulikuwa ndiyo muda ambao Wilson aliibamiza simu yake chini kwa nguvu baada ya kuisikia sauti ya Norbert kwa mara nyingine ikiwa ndiyo ileile aliyokuwa ameitumia kumpigia simu kwa mara ya kwanza akimuambia kuhusu janga aliloliacha nyumbani kwa Leopard Queen. Norbert alipokata simu hiyo aliangua kicheko sana akawatzama Moses na M.J Belinda ambao walikuwa wamekaa kwenye viti wakiwa wameizunguka meza moja, wenzake nao waliingiwa na matabasamu baada ya kusikia kile alichokuwa akikiongea Norbert.



               "Na watakoma kuingia kwenye ukanda wa Afrika ya Mashariki uliomshinda Brown Stockman" Norbert aliongea huku akiifungua simu ya Golden sehemu ya  mfuniko seli kavu(betri) akatoa kadi ya simu akaivunja.



                "Wameanza acha sisi tumalize, ok tuendeleeni na mpango wa kesho maana ndiyo mazishi ya General" Moses aliongea



               "Kesho ni hivi mimi na Norbert tutahudhuria mazishi wewe Moses utabaki kisha tukitoka ndiyo tutaenda ikulu tukiwa pamoja" M.J Belinda aliongea.



               "Mose usitoke au ukitoka badili uso huo ili usijulikane kumbuka wewe ni wanted hata raia wa kawaida wakikuona itakuwa ni kifo chako sasa epuka hili suala kabisa la kuonekana uso wako kwa mtu yoyote" Norbert alimuambia Moses.



                "Ok nitafanya hivyo ila na wewe ukijogoo upunguze yasije yakukuta kama ya huyo Leopard Queen uliyetuambia" Moses naye alimuasa Norbert kutokana na tabia yake ya kupenda wanawake



                 "Usihofu wala nini sasa hivi nitamfuata yule sajenti anayemlinda Dorice mtoto wa General nafikiri siyo adui yule" Norbert aliongea kimasihara akasababisha Moses acheke kwa nguvu na M.J Belinda asikitike akiwa  anamtazama



                  "Khaa! Huyu mwanaume huyu anajifanya jogoo pori si uoe tu" M.J Belinda alimuambia Norbert.



                  "we mbona huolewi" Norbert naye alidakia.



                  "nyoooo! Haya uje unioe wewe basi nikuweke kibano usiku ucha mpaka uwe mstarabu uache hiyo tabia" M.J Belinda alimuambia Norbert huku akimtazama kwa jicho la madaha.



                  "Hey tuweni serious basi utani tupunguze" Moses aliwaambia kisha akaendelea, "Sasa na mimi sitokaa humu ndani bali nitatoka nikiwa na sura nyingine niende huko mazishini".



                  "Kwahiyo tutakuwa pamoja huko?" M.J Belinda aliuliza.



                  "Ndiyo maana yake ili nicheze na wabaya wangu bila ya wao kunijua" Moses alijibu.



                  "Ok kazi kwetu nafikiri Belinda urudi kwako ukajiandae kabisa kwani massa ndiyo yanakaribia inabidi utokee nyumbani" Norber alimuambia M.J Belinda.
                  "enhee jamani nimepata wazo" Moses alisema huku akiwa ameweka uso watabasamu baada ya kile alichokifiria kuwa ndiyo njia sahihi kwake, Norbert na M.J Belinda walimtazama kwa shauku sana kutaka kujua hilo wazo.



                   "Mnaonaje kesho nivae sura ya bandia pamoja magwanda ya jeshi niingie kinamna nyingine  hiyo kesho" Moses aliongea huku akiwatazama wenzake ambao walikaa kimya hawakuwa wameongea kitu, kimya chao kilimaanisha hawajamuelewa na ikabidi awape ufafanuzi zaidi.



                     "Yaani naingia kama dereva wa Belinda" Moses aliongea akawafanya wenzake watoe matabasamu katika nyuso zao baada ya kuuelwa mpango wake vizuri.



                      "wazo zuri sana hilo sasa msipoteze muda rudini Tabata haraka sana hakuna muda wakupotea sasa hivi nafikiri tunaelewana jamani" Norbert aliongea, Moses na M.J Belinda walinyanyuka kwenye viti vyao kisha wakampa ishara ya kumuaga Norbert na wakaondoka ofisini humo wakimuacha Norbert akiwa ameketi kwenye kiti akiwasindikiza kwa macho.

ASUBUHI ILIYOFUATA

(SIKU TATU KABLA MAPINDUZI YALIYOPANGWA)

 Majira saa nne asubuhi tayari magari yalishaanza kumiminika nyumbani kwa Jenerali Kulika kuja kuuaga mwili wake katika siku hiyo kabla ya kuelekea Pugu kajungeni kwa Mazishi, viongozi mbalimbali wa kisekali wakiongozwa na Rais Zuber Ameir ambaye ameamua aje kuhudhuria mazishi ikiwa anatambua wazi mwisho wa utawala wake ulikuwa umefika tayari baada ya kupigiwa simu siku tatu zilizopita Mnadhimu mkuu wa jeshi L.J Ibrahim.



Rais Zuber alikuwa amekaa kwenye kiti kilichopo chini ya turuba la kisasa lililokuwa limeandaliwa kutumiwa na viongozi mbalimbali, ulinzi wake ndani ya eneo hilo ulikuwa umeimarishwa tofauuti na ilivyo kawaida kutokana na amri aliyowapa wanausalama wa ikulu. Alikuwa amekaa na viongoo mbalimbali wastaafu pamoja na waliopo madarakani waliokuja kuhudhuria mazishi ya komandoo wa kuogopeka, ndani ya eneo hilo pia Norbert alikuwa yupo akiwa amekaa katika kundi kubwa la waandishi wa habari akiwa na kamera yake ya kisasa mkononi ambayo ilikuwa ina uwezo mkubwa sana. Alikuwa akipiga picha mbalimbali za eneo hilo huku akiwatazama maadui zake kama wapo eneo hilo, akiwa na kitambulisho kilichokuwa na kamba ambacho kilikuwa kifuani mwake kilimfanya asihisiwe yupo tofauti kimalengo kwa waandishi wenzake ambao walikuwa wakimfahamu vyema kwa uhodari wake wakusaka habari na kuvumbua ukweli.



 M.J Belinda naye alikuwa yupo katika turubai maalum walilokaa viongozi mbalimbali wa kijeshi akiwa yupo pembezoni mwa L.J Ibrahim, alikuwa yupo amkini katika kutazama pande zote za eneo hilo. Alikuwa yupo katika safu moja na viongozi wakubwa wa kijeshi wenye vyeo sawa na yeye huku kati yao akiwa yupo Luteni jenerali akiyewazidi cheo wote, wote walikuwa wamevaa magwanda yenye kofia tofauti kutokana na vikosi walivyomo. Nyuma yao walifuatia wanajeshi wenye vyeo vya Brigadia jenerali na kuendelea.



 Wote walikuwa wametulia huku wakitazama mbele ambapo kulikuwa kuna jeneza  lenye bendera ya taifa lililowekwa picha ya Jenerali Kulika kwa juu, upande mwingine wa eneo hilo kulikuwa kuna turubai ambalo walikuwa wamekaa familia ikiongozwa na mjane wa marehemu pamoja na ndugu wengine wa marehemu. Upande huo ndiyo ulikuwa upande uliokuwa umetawaliwa na vilio  ambavyo viliongozwa na mke wa marehemu pamoja na watoto wake, huzuni ndiyo ilikuwa imetawala turubai hilo lililokaa familia na ndugu wa marehemu ambayo isingeweza kuelezeka kwa maandishi ikatimia kuieleza pasipo kuwa na mapungufu yoyote.



Ndani ya eneo hilo pia Benson alikuwepo akiwa amevaa miwani nyeusi ambayo ilificha macho yake yaliyokuwa na huzuni sana, alikuwa yupo katika turubai ambalo lilikuwa limekaliwa na watu wa kawaida. Macho yake bado yalikuwa mekundu  kutokana na huzuni ya kufiwa na pacha wake, alikuwa amekaa jirani kabisa na Wilson ambaye anatambulika kama mfanyabiashara tajiri maarufu sana.





Mnamo saa tano na nusu ibada ya mazishi ilianza hapo nyumbani ambapo iliongozwa na askofu wa kanisa katoliki nchini, misa hiyo iliongozwa hadi muda wa saa moja kisha msemaji mkuu wa jeshi akasimama akiwa ameshika karatasi akaelezea wasifu wa Marehemu Jenerali Kulika. Msemaji huyo alisoma wasifu huo wa marehemu uliochukua takribani nusu saa na ilipotimu saa saba kamili tayari alikuwa amemaliza, shughuli iliyofuata iliyokuwa ni mlo wa mchana nyumbani hapo kwa marehemu ambao ulichukua nusu saa hadi saa saba na nusu kisha taratibu za kutoa heshima za mwisho kwa marehemu ndiyo zikafuata



Shughuli hiyo ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu ilianza kwa kutangulia viongozi mbalimbali wa kiserikali ambao walitoa heshima zao za kumuaga Jenerali Kulika akiwa yupo ndani ya  jeneza, baada ya hapo ndipo walifuata viongozi mbalimbali wa kijeshi wakifuatana kicheo.



Viongozi wa kijeshi wakiwa mstari mmoja mbele yao alikuwa yupo L.J Ibrahim ambaye ndiye mhusika mkuu wa hayo yote akiwa ameweka huzuni ya kinafiki katika uso wake, L.J Ibrahim alifika mbele ya jeneza lenye mwili wa Jenerali Kulika akatoa saluti ya kinafiki  kwa mkubwa wake huyo ambaye ndiye amesababisha afariki. Alifuatiwa na  M.J Belinda halafu M.J Marwa akafuatia akiwa yupo nyuma yake, mameja jenerali wengine walifuatia katika mstari huo na walipoisha waliingia mabrigadia jenerali hadi viongozi wote wa jeshi walipomalizika.



Ndugu wa marehemu ndiyo walifuata wakiongozwa na mke wa marehemu katika kutoa kuaga, akiwa yupo mbele kabisa akiwa ameshikiliwa na askari wa JWTZ mke wa Jenerali Kulika alijikongoja hadi lilipo jeneza la mume wake huku akilia sana akimuita mwanaume huyo aliyempenda ambaye muda huo hakuweza kuitikia witi huo. Alipouona uso wa mume wake ukiwa kama mtu aliyalala huku ngozi ys mwili ikienda kuwa kijivu ndiyo alizidi kulia huku akiwa anaishiwa nguvu, askari wa JWTZ aliyekuwa yupo pembeni  yake aliwahi kumzuia  asiende chini kisha akamuondoa eneo hilo.



Watoto wake wakiongozwa na binti yake mkubwa nao walifuata wakiwa wanalia kwa uchungu wakiwa wameshikiliwa na maaskari wengine wa kike wa JWTZ  ambao walikuwa nao begabega hadi wanauaga mwili wa baba yao. Ndugu na jamaa nao walifuata katika kutoa heshima zao za mwisho kwa Jenerali Kulika, ndani ya dakika arobaini shughuli hiyo ilkamilika na jeneza likafungwa na wanajeshi wenye vyeo vya brigadia jenerali wakalizunguka wakiwa wamesimama kiukakamavu.



Ilikuwa ni saa nane na robo mchana wanajeshi hao wenye vyeo vya brigadia wakiwa wamelizunguka jeneza la mkubwa  wao wa  kijeshi, sauti ya amri ilisikika na kwa pamoja maaskari hao wenye sare za kombati walifunika bendera ya taifa wakalinyanyua jeneza la Jenerali  Kulika kikakamavu zaidi. Maaskari hao walianza kutembea kwa mwendo wa pole kwa hatua zisizopishana hadi kwenye gari maalum la kijeshi lililoteuliwa  kuubeba mwili wa Jenerali Kulika kuupeleka katika eneo la maziko shambani kwake Pugu.



Jeneza lilipandisha ndani ya gari kwa taratibu mno hadi katika eneo maalum la kuweka jeneza hilo katika gari la kijeshi ambalo halikuwa tofauti na magari ya wazi yatumikayo kuwaaga wanajeshi wastaafu.



Misafara mbalimbali ya viongozi wa nchi hii iltangulia kuondoka eneo hilo ikiongozwa na msafara wa rais Zuber baada ya misafara hiyo kuondoka magari ya watu wa kawaida nayo yaliondoka na mwishoni kabisa ukaondoka msafara uliobeba mwili wa Jenerali Kulika kuelekea eneo la  maziko ambalo lilikuwa lina na mawindo ya watu hatari waliokuwa wanawindana.



Majira ya saa tisa kasoro robo misafara hiyo tayari ilikuwa imeshawasili katika eneo la Pugu ambalo kulikuwa kumefungwa maturubai na viti kwa ajili ya kuketi viongozi mbalimbali, dakika kumi baadaye gari lililobeba mwili wa Jenerali Kulika liliwasili na watu aote walisimama wakati jeneza liliwa linashushwa ndani ya gari hilo. Maaskari wa JWTZ walewale wenye vyeo vya Brigadia jenerali yaani bibi na bwana pamoja na nyota tatu katika mabega yao walilibeba jeneza hilo kwa mwendo wa pole kuelekea katika eneo lenye shimo lililojengewa pamoja na kuwekea mbao juu. Walitembea kwa mwendo huo hadi walipolifikia shimo hilo la kaburi wakaweka jeneza juu yake katika mbao, maaskari hao walisogea pembeni  ya shimo hilo kikakamavu  kisha watu wakaketi katika viti vyao kusubiri taratibu zingine zinazofuata.

Kikundi cha maaskari kilichokuwa pembeni kilikuwa kimejipanga mstari mmoja ulionyooka huku mikononi mwao wakiwa wameshika bunduki aina ya SAR56, kikundi hicho kilinyanyua bunduki zao juu kiutiifu baada ya kupokea amri kutoka kwa kiongozi wao kisha wakazielekeza angani. Walipiga risasi angani kisha wakazishusha chini kihatua wakifuatana na amri ya Kiongozi aliyekuwa amewapa amri ya kuzinyanyua na kuzipiga angani, walisimama mguu pande baada ya kuzishusha silaha hizo wakiwa wametulia kiutiifu. Walikuwa kama wamegandishwa na theluji jinsi walivyotulia na hata kama nzi atatua jirani na pua wasingetingishika wala kuhangaika kumtoa kwa jinsi walivyojawa na roho ya kijasiri na kikakamavu, gwanda zao za mabaka walizovaa amabazo ziliwafanya wapendeze ndiyo zilizidi kupendezesha utulivu waliokuwa nao baada ya kupiga risasi angani.

Askofu mkuu wa kanisa katoliki alisogea jirani na lilipo jenza na akendelea na utaratibu mwingine uliokuwa ukitakiwa kwa ajili ya maziko ya Jenerali Kulika kama ilivyokuwa imepangwa kwa mujibu wa ratiba ilivyo, akiwa katika mavazi yake maalum ambayo hutambulika nayo katika sehemu za ibaba askofu huyo aliiongoza ibada hiyo hadi alipomaliza kisha jeneza likanyanyuliwa na wanajeshi waliokuwa wamelibeba hapo awali wakaliweka katikati ya shimo palipokuwa pamewekwa mbao maalum kulizuia lisianguke shimoni.Wanajeshi hao walizungushia jeneza hilo kamba kisha mbao zilizowekwa juu ya kaburi zilitolewa. Walilishuusha jeneza chini taratibu, lilifikishwa hadi mwishoni mwa sakafu ya kaburi hilo iliyokuwa imesakafiwa kwa utaaamu mkubwa sana. Hapo waanajeshi walitoa kamba zilizokuwa zimelishikilia hilo jeneza kwa kuzvuta kwenda juu kisha wakarudi kusimama kwa ukakamavu mkubwa.

Askofu aliyekuwa akiongoza ibada nzima aliongea maneno ya kiroho kisha akatupa udongo kaburini kwa utaratibu mno,alipomaliza aliruhusu watu wengine kutupia udongo kaburini hasa viongozi wa juu wa serikali wakiongozwa na rais Zuber ambaye alikuwa ameongozana na ADC akiwa amevaliwa magwanda ya kijeshi tofauti na nguo za kisherehe alizoeleka kuonekana nazo naye alifanya zoezi hilo la kutupia udongo kaburini. Rais Zuber alipotupa udongo kaburini viongozi wengine walifuata kisha mwishoni ubao ukafunikwa juu ya kaburi, kutokana desturi iliyojengeka miongoni mwa waumini wa dini ya kikristo wa kutofukia kaburi zaidi ya kufunika juu na ubao kisha zege linafuata. Jenerali Kulika hakufukiwa pia,baada ya zoezi hilo kukamilika maaskari wenye bunduki mikononi mwao walipewa amri na walizinyanyua juu kwa mara nyingine kisha wakapiga risasi hewani. Baada ya tukio hilo viongozi mbalimbali wa kitaifa walianza kuondoka tararibu eneo hilo kisha viongozi wa kijeshi wakifuatia wakiongozwa na L.j Ibrahim. Viongozi hao wakijeshi wakiwa wamekuja na magari yaliyofanana walianza kuondoka mmoja mmoja, kisha watu wengine wa kawaida wakafuatia kwa kuondoka eneo hilo.


L.J Ibrahim akiwa amekaa kiti cha nyuma kwenye gari yake baada tu ya kuondoka eneo la maziko  alito simu yake akabonyeza baadhi ya namba kisha akaiweka sikioni, alisubiri kwa muda mfupi kisha akaanza kuoongea baada ya simu yake kupokelwa na mtu aliyekuwa akimpigia.



               "nipe ripoti Boy....kazi imeenda kama ilivyopangwa?....pongezi kwako Boy uje jioni kuchukua malipo ya kazi yako" Alipomaliza alikata simu kisha akatoa tabasamu lililoashiria wa kile alichokuwa amekipanga



               "buriani Belinda" Alijisemea moyoni huku akiwa na tabsamu pana usoni mwake.



Muda huo tayari gari lilikuwa linakaribia kufika maeneo ya uwanja wa ndege kwenye njia inayotoka uwanja wa ndege kuingia barabara ya Mwalimu Nyerere,gari aina ya landcruiser lilionekana likitaka kuingia barabrani pasipo kutambua kulikuwa na gari ya mnadhimu mkuu wa majeshi ilikuwa inapita. Hali hiyo ilisababisha achomeke mbele ya gari la L.J ibrahim kimakosa,Dereva wa gari alilokuwa amepanda L.J Ibrahim alijitajidi kulikwepa gari hilo pasipo kupunguza mwendo na akafanikiwa kulikwepa lakini alipoendelea na safari alikuwa na wasiwasi mkubwa sana.



             "mtu wa aina gani huyo asiyetambua kuwa gari ya three satrs general inapita hadi achomekee simamisha gari tukamtie adabu kutokana na nidhamu yake mbovu" L.J Ibrahim alifoka kwa hasira huku akimtazama  dereva wake amabaye alikuwa akitetemeka lakini hakugeuza gari kama alivyoambiwa hali iliyompelekea L.J Ibrahim apandwe na hasira.



              "we Koplo Himu nimekuambia geuza gari husikii!!" L.J Ibrahim alifoka kwa hasira huku akimtazama dereva wake ambaye alikuwa akitetemeka hadi jasho jembamba lilikuwa likitoka kichwani ingawa kulikuwa na kiyoyozi ndani ya gari.



               "mkuu kuna tatizo" Koplo Himu aliongea kiuoga.



                "Damn hilo ni tatizo lako mimi halinihusu nimekuambia punguza mwendo na ugeuze gari au unapinga amri ya senior officer wako" L.J Ibrahim alifoka kihasira alipoona dereva wake hatii amri aliyompatia.



                "Mkuu breki hazikamati nitageuzaje gari, hata huyo aliyechomekea mbele ya gari yetu nimemkwepa kwa mwendo mkali si kwamba niliamua hivyo bali breki zilikataa na nikafanya hivyo na hapa ninavyokuambia bado haikamati na mwendo haupunngui" Koplo Faimu alijitetea huku akimtazama mkuu wake kwa uoga kutokana na hofu aliyokuwa nayo bada ya kugundua tatizo lililopo kwenye gari waliyokuwa wanaitumia.



                 "nini?!" L.j Ibrahim aliuliza huku aiwa amegwaya kutokana nna taarifa aliyokuwa amepewa na dereva huyo, swali lake la mshangao halikujibiwa na dereva wake ambaye alikuwa akiiwazia roho yake kwa jinsi gari ilivyokuwa ikikaribia makutano ya barabara ya Tazara.



                  "Imekuwaje ikawa hivyo kwani gari hamkulifanyia uchnguzi wakati yanatoka kambini?!" L.J Ibrahim aliuliza huku akiwa hatulii kwenye kiti alichokuwa amekikalia, ujasiri wote wa kijeshi uliikuwa umemuisha na hakuwa na ujanja kabisa.



Akiwa na kiwewe baada ya kuambiwa maneno hayo na dereva wake alifungua mkanda wa kiti  kisha akawa anaangalia kushoto na kulia kama mtu aliyepatwa  na wazimu, haja ndogo ilimbana kwa ghafla pasipo kutarajia kama ingembana.



                   "mkuu nilikuambia hi gari naona kama siyo lakini ukaniita nimechanganyikiwa kisa nyota tatu zilizopo kwenye gari hii ona sasa" Koplo Himu alimlaumu  mkuu wake.



 Maneno hayo yaliposikiwa na L.J Ibrahim alishika kichwa chake kwa mikono miwili kama mtu aliyesahau jambo muhimu kisha akamtazama Dereva, kumbukumbu zake zilirudi nyuma kwa haraka hadi aple muda ambao alikuwa akitoka kwenye maziko. Maneno ya Koplo Himu wakati aKitilia mashaka gari walilokuwa wamepanda yalimrudioa kwenye kichwa chake lakini alijikuta anakataa kisha akakunja sura akamtazama Koplo huyo kwa hasira.



                   "tahira wewe mbona ufunguo wa gari ni huohuo" L.J Ibrahim alimuambia kwa hasira.



                  "mkuu kumbuka funguo zinafanana na zina vibango vya aina moja zote" Koplo Himu alijitetea huku akijaribu kwa uwezo wake wa udereva aliongoze gari hilo.



                  "kufanana siyo kuingiliana wewe pimbi" L.J Ibrahim alifoka.



                 "mkuu nina wasiwasi yule dereva wa Madam Belinda alinibadilishia funguo" Koplo Himu aliongea huku akihangaisha usukani kukwepa magari yaliyokuwa yameanza kwenda taratibu kutokana na kuwa nusu kilomita kutoka eneo lenye mataa, taarifa ya gari yake kupita eneo hilo haikuwepo kwa maaskari wausalama wa barabarani.



L.J Ibrahim wenyewe kwa uamuzi wake alimuamuru dereva wake asipitie njia ya mkato ya Tabata ambayo  ilikuwa imepangwa kutumiwa na misafara ya jeshi. Mpango alioupanga ndiyo ulimfanya asipite njia hiyo ili baadaye aje kuusikia kwenye vyombo vya habari ukiwa umetimia. Sasa aliona hatari ya kuchezewa mpango na mtu aliyekuwa amempangia njama hiyo, maneno ya Koplo Himu yalimpa taarifa kabisa ya kuharibika kwa mpango huo na akaona ajiokoe yeye na nafsi yake kwa kutumia mazoezi ya kijeshi aliyokuwa nayo.



Kwa haraka kabisa alitoa kibanio cha mlango gari lake lilipokuwa limekwepa gari lililokuwa upande wa kulia. Alifungua mlango wa kushoto na alijitupa kwa umahiri mkubwa katika mtaro wa maji machafu uliokuwa mkavu hapo barabarani huku akimuacha Koplo Himu ndani ya gari akiwa anahaha na usukani wa gari. Kujirusha kwake kulimfanya atue vibaya  akaumia lakini hilo hakulijali zaidi ya kujali kuokoa maisha yake kutokana na ajali mbaya iliyokuwa ikikaribia kumpata.  Tukio hilo lilishuhudiwa na watu waliokuwa wakitumia sehemu ya wapitas kwa miguu ambao walimshangaa kwa jinsi L.J Ibrahim alivyojirusha kimaridadi,  yeye hakuwajali alijiweka sawa kisha akatoka ndani ya mtaro huo huku akiwa ameuma meno kwa maumivu aliyoyapata baada ya kuangukia vibaya ndani ya mtaro.
 L.J Ibrahim aliingia sehemu ya watembea kwa miguu na alianza  kutembea kwa haraka kuepuka watu wasije wakamkariri sura, aliinamisha uso wake chini na alienda hadi ilipo stendi ya pikipiki akapanda moja ya pikipiki ambaye dereva wake alikuwa aeshikilia usukani kama anajiandaa kuiwasha. Alimpa amri dereva mahali pa kwenda bila kuongea chochote na dereva wa pikipiki alitii amri hiyo kwa kuiwasha pikipiki akaiondoa kufuata uelekeo wa Jeti rumo.

MAMBO YALIVYOKUWA

Muda ambao mazishi yalikuwa yakifanyika Norbert alibanwa na haja ndogo ambayo ilimshinda kuistahimili ikambidi aende kuitoa, aliamua kutembea kueleka vilipo vyoo vya dharura viliwekwa mita takribani tatu kutoka yalipoegeshwa magari ya wakubwa wa kijeshi. Kuelekea kwenye vyoo hivyo ilimbidi ayavuke magari ya wakubwa wa jeshii ili aweze kuvifikia. Akiwa anayakaribia magari ili ayavuke alimuona mtu akiwa yupo chini wa uvungu wa gari ambalo alilitambua ni la M.J Belinda kutokana na kuegeshwa karibu na gari lenye tatu ambalo ni la L.J Ibrahim. Norbert alijikuta akiwa na hamu ya kuangalia kile anachokifanya yule mtu ilihali haja ndogo ilikuwa imembana, alijibana miguu yake ili mtu mzima asije akaadhirika na akakaa jirani na eneo hilo yalipo malori ya kijeshi.

Yule  mtu alipotoka uvunguni mwa gari la M.J Belinda alitokomea nyuma ya vyoo akiwa yupo makini na wala hakutambua tayari alikuwa amewekewa umakini na mtu aliye makini, alipopotea kwenye upeo wa macho ya Norbert alikuwa tayari amempa wasaa mwingine Norbert kufanya kile alichoona kipo sahihi. Alitumia akili nyepesi aliyonayo kwa kutoa nyota moja kwenye gari la L.J Ibrahim alilokuja nalo maalum kwa mazishi akaihamishia kwenye gari la M.J Belinda ambalo lilikuwa likifanyiwa uchokozi na yule mtu aliyekuwa yupo uvunguni mwake. Alipomaliza alishika sikio lake la kulia akaweka vizuri kinasa sauti kilichopo ndani ya sikio lake,  halafu akatumia muda huo kumpa taarifa Moses ambaye ni dereva wa M.J  Belinda kwa siku hiyo.

        "mliwekewa utelezi muangukie kwenye shimo la umauti katika hii gari, sasa fanya kila unachoweza ubadilishe funguo ya gari la Thrree star general uichukue wewe kisha  utumie gari lake" Norbert alipotoa taarifa hiyo ndipo alipokumbuka haja ndogo iliyokuwa imembana na akatimua mbio kwenda chooni.

Baada ya Moses kupokea taarifa hiyo kutoka kwa Norbert alimfuata Koplo Himu ambaye alikuwa ameshika funguo za gari mkononi akizichezea hana akiwa habari yoyote, alimsogelea Koplo Himu alipokuwa amesimama huku akiangalia nyuma mithili ya mtu  aliyekuwa amezubaishwa na jambo ambalo lilimfanya ashindwe kutazama huko aelekeapo. Akiwa na funguo za gari mkononi alimkumba kikumbo Koplo Himu na kupelekea funguo za gari alilokuwa akiliendesha zianguke sambamba na funguo za gari la L.J Ibrahim ambazo zilikuwa mikononi mwa Koplo Himu.

         “Afande unawaza nini hadi huangalii mbele unapoelekea?” Koplo Himu alimuuuliza Moses huku akiokota funguo zilizokuwa zimesalia chini baada ya  Moses kuwahi kuokota funguo za gari  analoliendesha pasipo yeye mwenyewe kutambua.

         “afande acha tu cheki yule mtoto kule mbele” Moses aliongea huku akiomnyooshea kidole msichana mrembo aliyekuwa amevaa kitambulisho cha waandishi wa habari shingoni mwake, Koplo Himu alipomuangalia msichana huyo na jinsi alivyo mrembo alikiri ana haki ya kuwa na kiwewe namna ile hadi afikie hatua na kutoangalia upande anaoelekea.

           “afande aisee pale sikulaumu mtoto mkali yule hata ukigongwa na gari kwa kumuangalia bado sitakulaumu aisee, mungu kaumba bwana acha apewe sifa mtoto anavutia balaa yule kama  kizingiti cha msalani hajawahi kukivuka tangu aje duniani” Koplo Himu aliongea huku akijishika kidevu chake akimtazama yule mwandishi wa habri wa kike kwa tamaa kubwa.

           “ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Afande hata wewe umeona mtoto anakimbiza yule” Moses aliongea akicheka huku akingongeshana ngumi na Koplo Himu halafu wakatazama kama kuna mtu aliyekuwa akiwatazama, waliporidhika hakukuwa na mtu anye watilia umakini wowote walicheka tena kwa nguvu.

            “Sasa afande wacha mimi niende chooni mara moja maana kuonana na mdada huyo ilikuwa ajali tu nikiwa naenda chooni nikajikuta nimekatikiwa ghafla na haja ndogo lakini sasa hivi imerudi tena kwa fujo” Moses alimwambia Koplo Himu huku akigongesha naye ngumi.

             “Poa afande mazishi yakiisha omba namba kabisa usimkose mtoto yule mkali” Koplo Himu alimuambia  Moses ambaye alikuwa ameshaanza kuondoka taratibu, alimsindikiza na neno la utani,”aisee mjeda unatikiswa na urembo tu jamaa yangu kama ni vitani halafu adui yako itakuwaje si kuuliwa tayari”

             “Aaah! Afande pale usinilaumu aisee kama ni vitani labda niwe nimechemkwa na damu ndiyo nitammaliza lakini hivihivi tu sina moyo huo,cheki mtoto yule yaani angekuwa ni mkuu  wangu wa kazi ningepiga kwata mbele yake bila yeye unipa amri ya kufanya hivyo” Moses alizidi kutumbukiza maneno ya utani baada ya kubaini ni mada anazozipenda Koplo Himu ambaye aliishia kucheka huku akimtazama Moses amabye alikuwa akiishia mbele ya upeo wa macho yake.

 Moses baada ya kuachana Koplo Himu alielekea moja kwa moja katika upande wenye vyoo ambako ndiyo Norbert alikuwepo, huko alimkuta Norbert akiwa ameegemea moja ya vyoo vya chuma vilivyowekwa kwa muda akiwa anatafakari jambo. Alimfuata hadi pale alipo akasimama mbele yake akamuonesha funguo za gari, alitoa tabasamu na Norbert akajibu kwa kutoa tabsamu pia halafu akamuonesha alama ya dole gumba.

              "good umecheza ndani ya mstari sasa wacha cha moto kiwawakie wenyewe kwa ujinga wao wanaoufanya" Norbert alimuambia Moses huku akitabasamu.

               "wamewasha moto wacha sisi tutie mafuta ukolee zaidi waungue wenyewe siyo tuhangaike kuuzima, ukiwakolea watahangaika kuzima wenyewe ili mambo yasiwe mabaya kwao kumbe ndiyo wanajiharibia zaidi" Moses aliongea huku akiachia tabasamu kama alivyoachia Norbert baada ya kujua kila kitu kilikuwa kimeenda ndani ya mstari kama walivyokuwa wamepanga baada ya kuona mchezo mchafu walioelekea kuchezewa na ambao waliamini kabisa ulitokana na hila za maadui zao wasioitakia mema nchi ya Tanzania. Baada  ya  kuhakikisha kila kitu ipo sawa Moses alirudi alipokuwa awali huku Norbert akiwa anaangalia  usalama wa eneo hilo la maegesho ya magari. Alikaa jirani na eneo hilo kutokana na nafsi yake kumlazimisha aendeleaa kukaa eneo hilo, nafsi  ilimshauri awe na subira na yeye  aliifuata nafsi kwa kuwa na subira hivyohivyo.



Haikupita muda mrefu yule Mtu  aliyekuwa akichokonoa gari la M.J Belinda alirejea akiiwa  ni mwenye  kuhangaisha macho yake katika eneo la maegesho ya magari hayo,macho yake yalitua kwenye gari la M.j Belinda ambalo tayari Norbert alikuwa amelibadilisha na kuonekana ni gari la Luteni jenerali. Mtu huyo aliweka mikono kichwani kwa haraka akijua alikuwa amekosea kazi aliyokuwa akiifanya,   alijipekua haraka mfukoni akatoa spana  akiwa na lengo la kwenda kusahihisha pale alipokosea wakati alipotumwa na mkuu wake.

 Aliwaza kusahihisha hilo suala haraka sana lakini hakutambua kwamba tayari alishachelewa kwani Norbert alikuwa tayri ameshamuweka katika anga zake, alipopiga hatua moja mbele aliguswa bega na Norbert ambaye tayari alikuwa ameshajongea hadi nyuma yake. Yule mtu alipogeuka nyuma wala hakupata hata nafasi ya kumuona huyo aliyemshika begani, kitendo chake cha kugeuza shingo nyuma alikutana na pigo la haraka la kijasusi ambalo hupigwa kwa kubonyeza shingo ya mlengwa. Pigo hilo ambalo Norbert alilitoa kwa wepesi mkubwa sana lilimfanya yule mtu apoteze fahamu papo hapo na akawa anadondoka, Norbert aliwahi akauweka mkono wake begani mwake mithili ya mtu anayembeba  mtu aliyezidiwa ambaye hawezi kutembea.

Alimkokota kwa haraka kuelekea kuelkea nyuma ya vyoo ambako kulikuwa na miti mingi iliyopandwa kwa ukaribu, alimuweka chini ya mti mmoja akimuelekeza kwenye shina mti katika upande ambao siyo rahisi kwa mtu kumuona akitoka katika upande wa eneo la maziko labda atokee katika upande wa huko kwenye miti ndiyo angeweza kumuona kwa urahisi kabisa. Alimpekua mifukoni mwake akatoa vitu mbalimbali ikiwemo kitambulisho cha mpiga kura na kadi ya benki ambapo vyote vilikuwa na picha iliyoandikwa kwa jina lake huyo mtu’

          "Richard Mabina" Norbert alilisoma jina la huyo mtu ambaye hakuwa na fahamu kabisa na wala hakuwa na utambuzi wowote utakaomuwezesha kujua kama alikuwa ametajwa jina lake na  mtu ambaye alikuwa naye kwa ukaribu sana, Norbert hakuridhika upekuaji alioufanya akamsachi zaidi huyo mtu akamkuta na simu ya mkononi ya kisasa. Alichukua simu ya huyo akaibonyeza kitufe cha kuwasha kwa haraka ili aweze kuipekua lakini ilikuwa imefungwa kwa mchoro maalum(pattern)

           "Shit!" Norbert aliongea huku akiuma meno kwa hasira, alijifikiria kwa sekunde kadhaa kisha akajipekua mifukoni mwake akatoa kichupa kidogo kinafanana na kichupa cha unga maalum wa kujipodoa(poda), alifungua mfuniko wa chupa hiyo na ndani pakawa na mfuniko mwingine wenye matobo madogo.

Norbert aliinamisha kichupa hicho kwenye kioo cha simu na akaanza kukitingisha na kupelekea unga wenye rangi ya kijivu utoke kidogokidogo umwagike kwenye kioo cha simu hadi ukafunika kioo, alipomaliza alifunga kichupa hicho kisha akakirudisha mfukoni, halafu akainamisha kioo cha simu na uleunga ukamwagika wote chini. Alipomaliza kuumwaga unga wote chini alimtazama Richard ambaye alikuwa hana fahamu kisha akaachia tabasamu, alirudisha macho yake kwenye kioo cha simu na kukuta ule unga ulikuwa umebakia umechora mchoro maalum wa kufungulia simu ambapo ndiyo ulimfanya aachie tabsamu lake la ushindi wa kufanikiwa kufanya kile alichotaka kukifanya. Bila kupoteza muda aliufuaitisha mchoro ule kama ulivyotokea kwenye kioo, alikosea kwa mara ya kwanza na ikamlazimu aufuatishe kinyume na jinsi alivyokuwa akiufuatisha hapo awali. Hatimaye simu ikafunguka naa Norbert akaanza kupekua kile alichokuwa akikitafuta kwenye simu hiyo, alitikisa kichwa kama mtu aliyekuwa ameafiki jambo wakati akizidi kuipekua simu hiyo hasa katka sehemu za ujumbe mfupi wa maneno.

 Aliyajua mambo mengi kupitia simu hiyo kutokana na mtumiaji wake kutokuwa makini katika kutumia simu hiyo katika kazi zake, mtumiaji wa simu hiyo alikuwa ametumia sehemu ya ujumbe mfupi wa maneno katika kupanga mikakati yake ya hatari ambayo tayari ilibainika na Norbert. Simu hiyo alifungua mtandao wa whatsapp akapitia sehemu mbalimbali akapekua ambapo alisikia sauti ya mhusika akiwa ameirekodi na kuituma wakati anawasiiana na mwanamke ambaye Norbert hakumtambua, aliporidhika na upekuzi wake alimtazama Richard ambaye hakuwa na fahamu akiwa bado alikuwa kwenye usingizi mzito wa nusu kifo. Akiwa bado anamtazama usoni simu ya Richard ilitetemeka mara mbali kisha ikatulia na ikatetemeka tena, Norbert kwa haraka aliweza kubaini simu hiyo ilikuwa imewekwa mtetemo pasipo kuwa na sauti. Kwa haraka aliitoa simu hiyo akaipokea kisha akaiweka sikioni akatulia kimya akawa anasikiliza, aliweka utulivu  wakati akisikiliza simu hiyo ambapo mengi aliyajua.

               "Rich mbona kimya vipi hiyo kazi tayari ulivyohakiki?!" Norbert aliposikia swali hilo ndiyo akavibana viungo vyake vya kutolea sauti akaanza kuongea, alikuwa ameshaijua sauti ya mpigaji huyo

                 "ndiyo bosi tayari kazi imekwisha" Norbert alijibu huku akiongea kwa kuiga sauti ya Richard.

                  "welldone boy jioni njoo upokee ujira wako urudi garage ukaendelee na kazi" Sauti hiyo ilimuambia

                "sawa bosi nashukuru" Norbert alizidi kumuiga Richard.

                   "Hooow! Belinda will dead so soon, Ooops! Rich tutaonana baadaye" Sauti hiyo amabyo ilikuwa ni ya adui mkubwa  wa taifa Mzee Ole ilisikika vyema kwa Norbert na kisha simu yake ikakatwa, Norbert aliizima simu hiyo kisha akaifuta kwa kitamba kuondoa alama zake za vidole zisibaki katika eneo hilo. Aliitumbukiza simu kwenye mfuko wa suruali ya Richard kisha akafuta sehemu zote alizokuwa ameshikakatika nguo za vitu vya Richard halafu tarattibu akaondoka eneo hilo akiwa tayari ameshamaliza kazi yake.

Baada ya mazishi kuisha viongozi mbalimbali wa kitaifa waliondoka eneo hilo kwa zamu kwa mujibu wa ratiba ilivyo, alianza kuondoka Rais Zuber ambaye ndiye alikuwa kiongozi mkuu kisha wengine wakafuatia. Mwishoni kabisa ikawa ni zamu ya viongozi wajeshi kuondoka eneo hilo kwa mujibu waratiba ilivyo, muda huo ndiyo muda ambao Moses alitiliwa shaka na Koplo Himu kutokana na gari aliyobadilisha funguo. Moses aliwahi mapema kwenye eneo la maegesho ya magari akaingia ndani ya gari lile ambalo tayari hadi kibango maalum kilichokuwa na jina la M.. Belinda kilikuwa kimehamishiwa katika hilo gari, baadaye Koplo Himu alifika akasogea hadi ilipo gari hilo akataka kufungua lakini Moses aliwahi kumuona akashusha kioo cha gari  akiwa na uso wa tabasamu.

           "vipi afande umechanganya gari nini?!" Moses alimuuliza huku akimtazama kwa tabasamu.

           "hamna afande labda nikuulize wewe maana nilikuwa nimepaki hili gari hapa" Koplo Himu aliongea akiwa na ameshaanza kuona hali tofauti katika eneo hilo.

          "Aaah afande hebu litazame gari vizuri" Moses alimuuliza Koplo Himu ambaye alianza kulikagua gari hilo na akaridhika lilikuwa ni la Meja jenerali na siyo luteni generali.

          "Dah! Kweli afande nimechanganya si unajua haya magari yanayotolewa maalum kwa  kutumiwa na wakuu  kwenye mazishi yanafanana balaa yaani madereva tunayatambua kwa vibango hivyo vinavyobandikwa jina la mkuu anayepanda gari hilo...vipi  lakini umeshaomba namba ya mtoto yule" Koplo Himu alikubali  baada ya kuona hana sababu ya kupinga kisha akamuuliza Moses kuhusu namba ya yule mwandishi wa habari wa kike.

           "Daha mbona tayari kitambo sana nasubiri kazi iishe nianze kubonga naye" Moses alijibu huku akifungua mlango wa gari baada ya wakuu wa jeshi kuanza kujongea eneo hilo wakiwa wapo tayari kuondoka, Koplo Himu naye aliondoka haraka hadi lilipo gari lenye nyota tatu akiwa  amesimama jirani na gari hilo.



L.J Ibrahim akiwa yupo mbele ya wakubwa wengine wa kijeshi waliokuwa na kofia tofuati kabisa kutokana na sehemu za jeshi walizopo, kuna aliyekuwa na kofia ya rangi ya kahawia ambaye ni mkuu wa JKT. Pia alikuwepo mwenye kofia ya rangi ya bluu iliyopauka, nyingine zilikuwa zina rangi kijani kibichi ambazo ni za JWTZ kikosi ch ardhi.

M.j Belinda ambaye pekee kati ya mameja jenerali wa jeshi ndiyo alikuwa na kofia ambayo ilikuwa na rangi ya kipekee, yeye alikuwa amevaa kofia yenye rangi nyekundu kwasababu alikuwa ni komandoo huku sehemu ya juu ya mfuko wa kombati la kijeshi kukiwa na mabawa ya ndge mawili yakiyojengwa kwa madini ya fedha. Wakuu wote wa jeshi walisogea mahali yalipo magari yao ya kijeshi, madereva waliwapigia saluti kisha wakawafubgulia milango waingie ndani ya magari hayo. Askari wa usalama barabarani wenye pikipiki walishasogea eneo hilo kwa ajili ya kuwa kitangulizi kwa kila gari kasoro gari la L.J Ibrahima amabaye alikataa kufuatana na pikipiki ya askari yeye peke yake, misafara mingine iliyosalia iliondoka taratibu eneo hillo na ikapiga ving’ora kwa nguvu baada ya kufika barabara kubwa huku kasi ikiongezeka. Hivyo ndivyo L.J Ibrahim aliwapanda manyunyu ya mvua akavuna mafuriko, hakutambua kwamba mchimba kaburi huanza kuingia yeye kwanza ndiyo achimbe kaburi hilo. Hapo aliingia ndani ya kaburi alilochimba ili azikwe mwingine ambalo lilimgharimu sana, kaburi ambalo nusura limfukie yeye mwenyewe kwa kuchimba urefu mkubwa bila kujua mchimbiwaji alikuwa anafukia.


IKULU, MAGOGONI

Gari ya kijeshi yenye nyota mbili ilionekana ikisogea kwenye geti la ikulu likiwa limefuatana na pikipiki ya askari wa usalama wa barabarani, geti la ikulu lenye nembo ya taifa lilianza kujifungua kwa mtambo maalum baada ya kuruhusiwa na walinzi waliokuwa wapo  kwenye chumba cha mitambo. Gari hilo liliingia ndani ya ikulu hadi eneo maalum la kuegesha huku king'ora cha pikipiki ya askari kikiwa kimezimwa, mashine ya gari hilo ilipozimwa tu Moses alionekana akishuka kwa haraka hadi kwenye mlango wa nyuma wa gari hilo.

 Alifungua mlango wa gari hilo kisha akapiga saluti huku askari wa pikipiki ambaye alikuwa tayari ameshashuka kwenye pikipiki yake akipiga saluti naye, ndani ya gari hilo M.J Belinda alishuka akiwa mavazi yake ya kijeshi ambayo yalimkaa vyema kiasi cha kulionesha umbile lake la kirembo ambalo ni tofauti na balaa alilo nalo katika mafunzo ya kijeshi. Moses alifunga mlango baada ya kushuka kwake mwanajeshi mrembo kisha akatembea akimfuata kwa nyuma yake hadi eneo maalum ambapo waliwakuta usalama wa taifa wakiwa wanwasubiri wake ajili ya kuwapeleka kuonana na Rais, maofisa hao wa usalama wa taifa walikakamaa kiheshima pasipo kunyanyua mkono kupiga saluti kama sheria ya kijeshi ya nchi hii katika utoaji saluti ilivyo.

 Ndugu msomaji askari yeyote haruhusiwi kutoa saluti ya mkono ikiwa hakukamilika kimavazi kuanzia kichwani hadi miguuni, ikiwa hatakuwa na kofia tu kichwani mwake basi haruhusiwi kupiga saluti ya  mkono zaidi ya kukakamaa huku akiwa amebana mikono. Ndiyo maana hawa maofisa wa usalama wa taifa walikakamaa tu hawakutoa saluti ya mkono kwa Meja jenerali Belinda kwa mujibu wa sheria hiyo ya kijeshi, ni miongoni mwa wanausalama hivyo kufuata taratibu ilikuwa ni lazima kwao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Maofisa hao wa usalama wa taifa walimuongoza M.J Belinda na Moses hadi kwenye chumba maalum ambacho Rais Zuber alikuwa akiwasubiri baada ya kuutambua ujio wao, walipoingia ndani ya chumba hicho walimkuta Norbert  tayari ameshawasili  akiwa amekaa kwenye kiti mkabala na Rais Zuber. Wao kwa pamoja walitoa saluti kwa Rais Zuber kisha wakaenda kuketi kwenye viti vilivyo jirani na Norbert kwa upande wa kushoto na kulia, walielekeza nyuso zao mbele ambapo walikuwa amekaa Rais Zuber akiwa na shauku ya kutaka kujua kile walichokuwa nacho wanausalaa hao kutoka vitengo tofauti ndani ya nchi ya Tanzania.

            "naam two star general, Norbert na.....Sajenti Matumbo" Rais Zuber aliongea huku akimtazama kila mmoja katika uso wake na alipofika kwa Moses aliyekuwa na sura ya bandia usoni hakuweza kumjua na alisoma tu jina lililokuwa kwenye kibango maalum ambacho kilikuwa kikining'inia kwenye mfuko wa kombati la juu.

            "Mheshimiwa hapa unaotuona tumeomba kuonana na wewe kutokana na jambo zito ambalo litakaribia kuikumba nchi hii ikiwa tu tutachelewa kulizima, kwanza kabla sijalielezea jambo hilo napenda nikutambulishe kwa huyu unayemfahamu kama Sajenti Matumbo ni Moses  Gawaza nafikiri unamfahamu" Norbert aliongea huku akimtazama Moses ambaye alivua sura ya bandia aliyokuwa ameivaa usoni mwake, Rais Zuber alishtuka baada ya kumuona Moses eneo hilo ambalo hakutarajia kumuona kabisa lakini Norbert alimuashiria atulie.

            "Mheshimiwa nafikiri suala la wewe kuliongoza taifa kwa matakwa ya wananchi tunalitambua na hilo ndiyo linakufanya upendwe na wanachi wote, upendo huu wa wananchi wako pia umekufanya uwe unachukiwa na watu waliokuwa wakitaka ufuate matakwa yao kwa maslahi yao binafsi na si maslahi ya taifa. Nikupongeze kwa msimamo wako juu ya masuala ya kimaendelo ya hapa nchini, sasa naomba nirudi kwenye nia ya sisi kuwepo hapa" Norbert aliongea kwa utulivu mkubwa kisha akasitisha kuongea, aligeuka kushoto akamtazama Moses kisha akageuka kulia akamtazama M.J Belinda  halafu akayarudisha macho yake kwa Rais Zuber.

            "Kabla ya kuanza kutokea mauaji ya viongozi wa dini kwa sumu aliyotengeneza professa hapa, nadhani uliwahi kugoma kusaini mkataba wa kupitisha ushoga na usagaji ndani ya Tanzania, Sasa huo mkataba uliugomea Mheshimiwa ndiyo chanzo cha kutokea haya yote yaliyokuwa yakiendeshwa na mapacha wawili ambao mmojawapo tayari ni marehemu kwa sasa. Watu hawa walipanga njama ya kuwatumia viongozi wa dini katika shghuli zao na walifanikiwa kwa hilo kwa kumtumia Marehemu Askofu Edson  aende kuomba dawa ya Quamtanise kwa Profess Gawaza kwa kigezo cha msaada uliokuwa ukihitajika na waluteri wa Italy, hatimaye walifanikiwa kuipata sumu hiyo hatari ndiyo wakaanza kuitumia kwa kumuangamiza Askofu Edson yeye mwenyewe kisha wakaangamiza viongozi wa dini mbalimbali. Hila zote hizo walitaka wawafanye wananchi wakuone wewe kama kiongozi wa nchi umeshindwa kazi hata kuviamuru vyombo vya dola, hila hiyo waliipitisha kwa mara ya kwanza wakaiona inafaa lakini baadaye waliiona haifai wakaanza kuua viongozi wa jeshi hasa walio kikwazo chao wakitumia hiyo sumu ili waweze kumsingizia Professa Gawaza ni msababishi wapate sababu ya kuweza kuipindua serikali yako" Norbert alieleza kwa kirefu zaidi, maelezo hayo yalimfanya Rais Zuber atikise kichwa kuwa ameyasikia barabara, alisimama kwenye kiti alichokaa akaanza kutembea kulizunguka eneo ambalo lilikuwa na meza na walivyokuwa  wameielekea kwa pamoja. Aliyafikiria maelezo yote aliyopewa kwa upana zaidi kisha akarudi kwenye kiti.

           "Okay! Nimeyaelewa maelezo yako ambayo yapo kama kisa chenye kusimulia, pia ningehitaji ushahidi zaidi ingawa maelezo yako yanafanana na ukweli" Rais Zuber aliongea huku akimtazama kila  mmoja

            "hilo siyo tatizo mheshimiwa, ushahidi ni huu" Norbert aliongea huku akijisachi mfukoni akatoa kadi ya kumbukumbu ya simu iliyokuwa ipo ndani ya kadi kubwa inayoweza kuingia kwenye tarakilishi, alimpatia kadi hiyo Rais Zuber ambaye aliipokea akaenda kuichomeka kwenye kioo kikubwa cha luninga kilichopo mahala hapo. Luninga iliwaka na hapo akapata nafsi ya kushuhudia kile kilichomo ndani ya kadi hiyo ya kumbukumbu, ilimchukua muda mrefu kweza kukimaliza kitu hicho ambacho ndiyo kilimfumbua macho kujua mengi yaliyopo nyuma ya pazia.

  Baada ya kumaliza kuangalia ushahidi huo Rais Zuber alisema, "hongereni sana vijana wangu najivunia kuwa na watu kama nyinyi katika utawala wangu"

  Maneno hayo yaliwafanya kina Norbert waachie matabasamu kisha wakatikisa vichwa kuonesha wapo pamoja na kauli hiyo ya Rais Zuber, walimtazama Rais ambaye alikuwa akijiandaa kutoa kauli nyingine baada ya kuwapa pongezi vijana wake wazalendo waliokuwa wakihangaika uhakikisha nchi ya Tanzania na hata watanzania kwa ujumla hawadidimii.

                   "Sasa basi napenda niwaambie kwamba suala hili nitalifanyia kazi mimi kama amiri jeshi mkuu wa majeshi yote, Mnadhimu mkuu wa jeshi Luteni jenerali Ibrahim Salim ambaye ndiye mkuu pia wa majeshi ya majini nitamfukuza kazi na pia nimshtaki" Rais Zube aliongea kwa hasira

                   "no no hapana mheshimiwa hiyo siyo njia nzuri ya kulitatua hilo jambo kumbuka yule ndiye mwenye mwanajeshi wenye cheo kikubwa nchini, sasa akikaidi amri na kupindua nchi je" Moses aliingiia

                   "Hata kama nisipofanya hivyo ana siku tatu kati ya siku saba alizoniahidi atapindua nchi sasa ya nini tumuache" Rais Zuber alikinzana na kauli ya Moses.

                   "kumfukuza na kumuweka ndani huyu mtu jua wananchi hawatakuwa na imani na wewe hasa hawa vijana wafuata mkumbo wa mitandaoni, utaonekana unataka kuzima balaa la Professa Gawaza hivyo utajiweka pabaya katika uongozi wako mheshimiwa" M.J Belinda aliongea.

                   "okay maneno yenu yana ukweli ndani yake mnanishauri nifanye nini?" Rais Zuber aliwaomba ushauri.

                   "Cha kufanya wewe ni kutulia tu hili suala liacha mikononi mwa N001 yupo kazini tayari, nakuahidi hayo mapinduzi yaliyopangwa hayatatokea kamwe ikiwa N001 tayari ameshaingia kazini" Norbert aliongea

                   "Inabidi aongezewe nguvu huyo N001 akishirikiana na vijana hawa wa TISS nafikiri kazi itakwisha" Rais Zuber aliongea

                  "Worry out mheshimiwa, kila kitu kipo under control" Moses alimuambia

                  "okay nimewaelewa" Rais Zuber alikubaliana nao.

                     "Sawa mheshimiwa sisi hatuna la ziada tunahitaji kuendelea na kazi" Norber aliongea huku akisimama, alipeana mkono na Rais Zuber huku M. Belinda akisimama akatoa saluti na Moses akiwa anavaa tena ile sura ya bandia aliyoivua.

                       "Okay msisite kuwasiliana nami" Rais Zuber aliongea, Norber pamoja na wenzake ndani ya eneo hilo baada ya kufikisha taarifa ile ambayo ilikuwa ni muhimu rais kuipata kwa muda

MSASANI

Pikipiki aina ya bajaj boxer ambayo inatumika kukodishwa kwa ajili ya usafiri alimaarufu kama bodaboda ambayo ilikuwa imembeba L.J Ibrahim  ilisimama mbele ya geti kubwa lenye uzio mrefu, L.J Ibrahim alishuka kisha akampa dereva wa pikipiki hiyo noti mbili za shilingi elfu kumi  akamuashiria aondoke. Dereva wa pikipiki alitii amri akaondoka ndipo L.J Ibrahim aksogelea geti dogo la nyumba hiyo ambalo lilifunguliwa tu alipolikairibia baada ya mlinzi kumuona kupitia mtambo maalum. Aliingia ndani ya nyumba hiyo  bila kumsemesha chochote mlinzi huyo, alikaza mwendo hadi ilipo nyumba  ya kifahari ambapo alifika barazani akausogelea mlango akaufungua kwa nguvu akaingia ndani kama alikuwa anavamia na kupelekea wenzake waliopo sebuleni wake kukaa kitahadhari kisha kila mmoja akamuelekezea bastola wakijua ni adui yao.

              "kuwa makini  bwana uingiaji gani huo General je tungekupiga risasi" Wilson alimuambia, L.J Ibrahim aliposikia kauli hiyo aliwatazama wote kwa zamu kisha akatikisa kichwa kwa masikitiko

              "vipi General kwema huko?"  Mzee  Ole  alimuuliza baada ya kumuona ana hali tofauti.

              "Jamani mambo yameharibika ile gari mliyomtuma Richard akate breki nimefanyiwa mchezo mchezo mchafu nikaipanda mimi" L.J Ibrahim aliongea

              "what?! Huyu ni N001 tu hakuna mwingine anayeweza kufanya haya" Benson naye alidakia huku akiwa ameuma meno kwa hasira.

               "dereva wangu akabadilishiwa funguo bila ya kujijua na nyota moja ya gari yangu ikatolewa ikaenda kuchomekwa kwenye gari la Belinda, kwahiyo tukaipanda ile gari"  L.J Ibrahim aliongea

               "damn! Hivi huyu N001 ni nani mpaka atusumbue vichwa namna hii?!" Santos kwa mara ya kwanza aliongea huku akipiga ngumi yake ya kushoto kwenye tumbo la kiganja chake cha kulia.

               "Sasa hapa jamani tunapambana na mtu tusiyemfahamu inabidi tuwe makini sana la si hivyo tutaisha wote" Mzee Ole aliongea

               "First of all inabidi tumfahamu huyu mtu na mtu peke anayeweza kutusaidia tukamjua huyu mtu ni Leopard Queen pekee akahojiwe sasa hivi atakuwa kaamka" Thomas kwa mara ya kwanza aliingilia

               "Ok nyinyi kamuhojini mimi napumzika hapa nimeumia sana" L.J Ibrahim aliongea kisha akajitupa kwenye kochi, watu wote walikuwa waliokuwa na shauku ya kutaka kumfahamu N001 waliondoka sebuleni hapo wakimuacha pekee akihema. Alikuwa haamini kama ameweza kupona katika janga lile ambalo hadi muda huo lilikuwa limemkumba dereva wake, alibaki akiwa na hasira juu ya N001  ambaye alikuwa akiwafanyia michezo ya kiakili bila ya wao kumjua hata kwa sura jinsi alivyo.

NDANI YA WODI MAALUM YA SIRI

Josephine alionekana akiwa amekaa kitako kwenye kitanda huku akijifikiria  baada ya kujiwa na wenzake waliokuwa wana shauku ya kujua kile alichokuwa akikijua yeye, ilikuwa ni masaa kadhaa tangu ahamishwe kwenye nyumba hiyo akitolewa kule nyumbani kwake Keko alipokuwa amelazwa kwa dharura. Pia ilikuwa ni saa moja tangu arejewe na kumbukumbu zakevizuri tangu alipopoteza fahamu, uchungu juu ya kumuacha Benjamin katika hali ambayo ilikuwa si rahisi kupona ndiyo ulikuwa umemjia muda wote ambao kumbukumbu zake ziliporudi.



Alijikuta akilia kutokana na moyo mdhaifu wa kike aliokuwa nao na mapenzi pia aliyokuwa nayo kwa Benjamin, muda huo ambao wenzake walikuja kumuona tangu arudiwe na kumbukumbu zake vizuri, Josephine alipomuona Benson akiwa mzima hana jeraha lolote aliweza kumtambua kama shemeji yake. Aliwaangalia wote waliokuwepo hapo kwa zamu lakini hakuiona sura ya Benjamin mpenzi wake, machozi taratibu yalianza kumtoka akajua mpenzi wake atakuwa amefikwa na jambo  baya baada ya kuanngushwa katika meza ngumu ya kioo na Norbert

            “Benjamin wangu yupo wapi?” Aliwauliza wenzake huku akiwatazama kwa zamu kila mmoja katika nyuso zao lakini hakupata jibu la swali hilo alilowauliza, alianza kuwatazama kila mmoja lakini kila aliyetazamwa alitazama chini kasoro Benson machozi yalianza kumlenga katika macho yake baada ya kutoneshwa habari za kifo cha ndugu yake.

            “Sitamwacha mzima yule mshenzi lazima nimuue kwa mkono wangu” Josephine aliongea kwa hasira akawa anajaribu kuinuka kitandani lakini kizunguzungu kilimzidi akarudi kuketi, maneno hayo yalimfanya Benson aanze kulia kimya kimya akawa anahema kwa hasira huku akimtazma shemeji yake.

             “Niambie Leopard Queen nani kamuua kaka yangu? N001 ndiyo nani huyo” Benson aluliza huku machozi yakimtoka

             "N001 ndiye aliyemuua Benjamin wangu" Josphine alijibu huku akijifuta machozi, kisha akaanza kufikiria tukio zimalililotokea hadi Benjamin akauawa na Norbert. Alikumbuka busu refu alilopigwa na Norbert kabla hajapigwa na ktako cha bastola, maneno ya Norbert aliyomuambia yalijirudia kwenye kichwa chake na hapo ndipo hasira dhidi ya Norbert ilipozidi akbaki akihema.

             "N001 ndiyo nani Leporard Queen hebu tueleze tumjue akalipe ushenzi wote alioufanya" Benson alimsihi Josephine

           "ni Norbert Kaila" Josephine alijibu kisha akaanza tena kulia.

           "what!"  Wote kwa pamoja walijikuta wakiropoka kwa mshangao.

Walijikuta wakiwa hawaamini maneno ya Josephine na walibaki wakitazamana tu kisha wakapeana ishara ya macho kila mmoja, waliporuudisha macho yao kwa Josephine walikuwa na sura ya huruma kila mmoja jambo ambalo lilimshtua Josephine akawa haelewi walikuwa wamekumbwa na nini. Josephine aliwashangaa sana watu hao kwa jinsi walivyokuwa wakimtazaama kihuruma, macho yake yalipotua kwenye uso wa Benson ambaye alikuwa na uchungu aliuona ukiwa tayari umepotea katika uso wake na huruma ndiyo ilikuwa imemtawala.

           "jamani kuna nini mbona hivyo siwaelewi?!" Josephine aliwauliza, swali lake  lilimfanya Benson asogee karibu  aye zaidi akakaa kwenye kitanda kisha akamshika viganja vya mikono yake kwa upole.

           "Josephine" Benson alimuita kwa kutumia jina lake na si jina la kikazi, Josephine alipeleka kichwa juu kuitika huku akimtazama usoni   Benson.

            "Are you sure(una uhakika) ni Norbert?"  Benson aliuliza kwa upole, Josephine hakujibu kwa kinywa chake zaidi ya kuinua kichwa juu kisha akakirudisha chini kukubali.             

            "Mkumbuke mliniambia nimuwekee mtego ili tumnase, sasa ndiyo mtego kauruka na kunipiga risasi ya bega halafu akamuua Benjamin kwa kumuangusha juu ya meza" Josephine alifafanua baada ya kukiri kuwa ana uhakika . Tena alizidi kueleza,

            "baada ya hapo ndipo akaniambia niwafikishie salamu  nyinyi kuwa N001 hakamatwi kijinga namna hii".

 Wote walipoyasikia maelezo hayo hawakuwa na sababu nyingine ya kupinga na walimuona Josephine hakuwa amechanganyikiwa kama ilivyo awali bali alikuwa anasema ukweli mtupu, hawakujua kama kwenye maelezo yake kulikuwa na uongo tayari aliuongezea waoa waliamini moja kwa moja kwamba alikuwa akiongea ukweli mtupu  katika maneno hayo. Hasira dhidi ya Norbert ndiyo zilizidi kuchukua nafasi,  hakika walichotwa kabisa na uongo jumlisha ukweli ambao Josephine aliwaambia  katika maelezo yake.

            "Huyu mtu anaonekana ni hatari kiasi gani hadi kawazidi ujanja wote kwa pamoja" Thomas aliongea baada ya kuyasikia maelezo hayo.

           "Hapana huyu hana uhatari wowote bali ni mviziaji tu na hawezi kuvizia  tena mbele yetu ni lazioma afe mara moja" Santos aliongea kwa kujiamini kabisa

            "tena nitamuua kwa mkono wangu mwenyewe huyu" Benson aliongea huku akitetemeka kwa hasira alizonazo

           "Benson najua una hasira sana ila huyu mtu anahitaji kuchezewa mchezo kama anavyotuchezea mchezo inabidi tufanye nini mnajua" Thomas aliongea huku akiwatazama kila mmoja, wote walijawa na shauku ya kutaka kusikiliza wanachotaka kuambiwa , walimtazama kwa shauku ya  kutaka kusikia hiyo njia ambayo wangeitumia kumnasa mtu hatari kama huyo.

Thomas aliitamka mbinu hiyo ya kumnasa Norbeert kwa sauti ya chini ambayo ilisikiwa na wenyewe tu, hata mimi mwandishi sikupata hata wasaa wa kuisikia mbinu hiyo aliyoibuni mzungu huyo bingwa wa mbinu katika kikundi chao. Mwandishi nilipata kushuhudia jinsi wakinong'ononezana kwa suti ya chini tu juu ya mpango huo ambao walikuwa umumebuniwa na Thomas ndani ya muda mfupi tu,usiniulize nimeonaje wakipanga mpango ila tambua nimeuona nimeuina ndiyo maana nikuwasilidha kwa maandishi.

                                          SAA MOJA BAADAYE

Norbert akiwa yumo ndani ya nyumba ya shirika la EASA alipokea simu kutoka mmmoja wa marafiki zake wa karibu ambayo ilikuwa ni ya muhimu kwa taaluma yake ya habari, ilikuwa ni simu ilimjulisha juu ya mkutano uliotakiwa kufanyika nyumbani kwa Mnadhimu mkuu wa jeshi ambao ungehusisha waandishi wa habari na Mnadhimu huyo wa jeshi baada ya kumalizika mazishi ya Jenerali Kulika. Norbert alijiandaa haraka akiwa amebeba vifaa muhimu ikiwemo kamera yake ya kazi pamoja na mapambo amabyo huyatumia kama tahadhari, aliingia ndani ya gari yake akimuacha Moses ndani ya eneo hilo na aliondoka kuelekea Mbezi beach nyumbani kwa L.J Ibrahim aliposikia kuwa Mnadhimu mkuu wa jeshi alikuwa ameitisha mkutano wa pili wa waandishi wa habari.

Ndani ya nusu saa tayari alikuwa alikuwa ndani ya Mbezi Beach akiwa na amevaa suti nadhifu, alielekea moja kwa moja mtaa amabao alikuwa anaishi L.J Ibrahim ambapo alipiga honi katika geti la nyumba ya kisasa. Mlinzi wa getini alitoka hadi nje baada ya kusikia honi hiyo na alipobaini aliyekuwa akipiga honi hiyo alikuwa ni Norbert aliruhusu gari hilo liingie ndani kwa kufungua geti. Norbert aliingiza gari hadi kwenye maegesho ya magari ambapo alikuta magari mbalimbali yaliyobandikwa mabango ya matangazo ya televisheni na redio mbalimbali, hapo alipata uhakika kuwa kulikuwa na mkutano huo humo na ikambidi abebe vifaa vyake vya kazi kashuka garini akafunga milango.

Aliposhuka tu garini alimkuta mwanajeshi mwenye sare za kijeshi ambaye alimpokea kisha akamuashiria aelekee upande wa mlangoni wa nyumba ya L.J Ibrahim, Norbert aliongoza njia huku akivaa kitambulisho chake vizuri ili aweze kutambulika kama mwandishi wa habari. Alipiga  hatua zake taratibu huku mwanajeshi akiwa nyuma yake kuhakikisha anafika kwenye mkutano maalum, mkutano amabo ulikuwa tofauti na yeye alivyotarajia. Alivyopiga hatua takribani sita tangu ashuke garini alihisi kitu kigumu na chenye ubaridi kikigusa shingo yake kwa nguvu, Norbert alisita ghafla akataka kugeuka  lakini alizuiwa na mkono mgumu wa mwanajeshi aliyempokea kugeuka nyuma.

           "weka shingo hivyohivyo nguchiro wewe na uongoze njia" Mwanjeshi yule alimkaripia, hapo Norbert alijua taayri alikuwa ameingia katika hatari, hakuwa na  la kubisha ingawa alitambua mwanajeshi huyo hawezi kumuua kwa muda huo hata kama akileta ubishi.



 Alitembea huku akiwa ameshika vifaa vyake vya uandishi wa habari, alipokaribia mlangoni yule mlinzi alimpekua kisha akamuamuru afungue mlango. Norbert alifungua mlango bila kubisha na akaingia ndani kisha yule mwanajeshi akaufunga mlango kwa nyuma, alitokea kwenye sebule pana iliyokuwa imetolewa samani na kuifanya iwe kama nyumba ambayo wakazi wake walikuwa wakitaka kuhama. Humo ndani aliwakuta L.J Ibrahim. Benson, Thomas, Santos na Wilson wakiwa wamesimam na kila mmoja akiwa na bastola mkononi wakimngojea kwa hamu kubwa sana, hakika alikuwa ameingia mtegoni bila yeye kujijua kabisa. Pembeni katika kona moja ya sebule hiyo kulikuwa kuna kiti ambacho alikuwa amefungwa mtu ambaye alikuwa hatambuliki kiurahisi kutokana na uso wake kujaa damu kuashiria  alikuwa amepigwa sana, ilikuwa ni jambo amabalo hakulitarajia kwa muda huo na tayari uoga mdogo alikuwa nao ndani ya moyo wake baada ya kuwa ameingia katika anga za watu ambao alishawahikuwatororka zaidi ya mara moja.

           "Smart guy Norbert Kaila a.k.a N001 karibu katika mdomo wa kifo" L.J ibrahim aliongea huku akitabasamu, ukairibisho huo usio na amani ulisikika vyema kwa Norbert lakini hakuonesha hali ya uoga usoni ili asiwape nafasi maadui zake wazidi kumvuruga asipate wazo la kujitetea.

   Aliachia tabsamu zito sana kisha akaanza kuwatzama kila mmoja kwa tabsamu pana mithili ya bibi jarusi akimtazama mwanume wa ndoto zake siku ya harusi, aliingiza mkono mfukoni na hapo milio ya kuondolewa usalama kwa bastola ikasikika.

            "usifanye ujanja wowote Norbert utakufa kabla hujatimiza ndoto zako zakuwepo duniani" Santos alimkoromea huku akimtazama kwa hasira, Norbert aliutoa mkono aliouingiza ndani ya koti haraka ukiwa na kiboksi cha peremende za kutafuna bila kumeza za batoock.

            "Hey ni big G tu hizi" Norbert aliwaambia huku akiwaonesha, alifungua kiboksi hicho bila wasiwasi wowote kisha akachomoa kikaratsi kidogo akakifungua huku akitabasamu alitoa premende hiyo ya kutafuna tu kisha akaitia mdomoni mwake akaanza kuitafuna huku akitabasamu kama kawaida yake.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

            "dustbin hamna hapa, sasa nitaweka hizi karatasi za hii big G?" Norbert aliuliza akiwatazama watu wale waliokuwa wakimtazama kwa hasira.

            "usilete porojo wewe kwanza jibu maswali yetu kabla hujawafuata wafu" L.J Ibrahim aliongea kwa kufoka huku akigusa kifyatulio cha bastola kwa lengo la kumtisha Norbert lakini Norbert hakutishika hata kidogo ndiyo kwanza alizidikutoa tabsamu lililokuwa linakribia na kicheko.

             "sasa hizi karatasi za Big G kwahiyo nizitupe kwenye tiles hapa haya" Norbert aliongea pasipo kuonesha kuwa anawatilia maanani na akazitupa karatasi hizo kwenye sakafu ya marumaru huku akiwatazama maadui zake.



Maneno hayo yalimuudhi sana Benson akaona alikuwa akidharauliwa yeye na wenzake, kwa hasira zake alimuelekezea bastola Norbert kisha akafyatua risasi kwa lengo la kumuua lakini Thomas aliiwahi risasi hiyo akaielekezo chini. Risasi hiyo ilitoa mlipuko mkubwa sana baada ya kupiga marumaru na iliingia ndani ya marumaru kiasi cha nusu inchi, tukio hilo lilikuwa ni lenye kushtua kwa Norbert lakini hakuonesha mshtuko wowote yeye aliendelea kutabasamu tu kama aliona  jambo la kusuuza moyo wake.

           "Thomas ungeacha nimmalize huyu mshenzi dharau hizi" Benson aliongea kwa hasira.

          "Benson cool down buddy, huyu hahitajiki kufa mapema namna hii" Thommas alimuambia

          "Uniue kama ulivyomuua General Kulika ili muweze kupata kueneza ushenzi wenu"Norbert aliongea maneno ambayo yalizidi kuwachoma watu hao. Tan alizidi kupigilia msumari katika maelezo hayo, "Au mnafikiri sijui mkamuua mufti na Askofu Edson aliyekuwa mwenzenu, mnadhani sitambui kama mmetumwa na Askofu shoga anayeitwa Achim Valdermar alimaarufu kama Jack Shaw tena alipokuja Tanzania Benson ulionana naye kaika hoteli ya Kempiski".

 Maneno hayo yalizidi kumvuruga kila mmoja hapo wakabaki wakipandwa na hasira sana, walijua tayari Norbert alikuwa akijua siri zao nyingi na ilikuwa ni hatari sana kwao kama angetoka mzima eneo hilo. L.J Ibrahim ndiyo alipandwa na hasira zaidi akaelekeza bastola kwenye upande aliofungwa yule mtu aliyekuwa amejawa na damu usoni, alifyatua risasi tatu ambazo zilimpata yule kwenye paaji la uso na kifuani kisha akairudisha bastola katika usawa alipo Norbert.

             "Ndiyo unajua mengi tuone sasa kama utatoka hapa ukiwa mzima, hii siri itabaki miongoni mwetu tu.  Tumeanza na huyu mwandishi wa habari mwenzako aliyekupigia simu uje huku hadi ukaingia mtegoni" L.J Ibrahim aliongea kwa kujiamini.

               "Ok hata mimi naona ndiyo maana mkabandika matangazo yenye nembo za televisheni kwenye magari ili muweze kuninasa mimi siyo" Norbert alizidi kupoteza muda kwa kuongea maneno yenye kuudhi, aliponyamaza kimya saa yake ya mkononi ililia ambapo alibonyeza kitufe ikazima.

                "sorry saa ilikuwa na automatic alarm" Norbert alisema huku akiwa hajali vitisho alivyopewa, aliwatazama maadui zake ambapo kila mmoja alikuwa akiiiweka sawa risasi kuashiria yupo tayari kufyatua risasi.

               "Hatuna mjadala na wewe fyatueni risasi tumalize kazi" L.J Ibrahim aliwaambia wenzake, kila mmoja alijiweka tayari kufyatuia risasi lakini walijikuta wakisita baada ya Norbert kuwaonesha ishara ya mkono wasubiri.

                "Ok mpo tayari kuniua lakini hampo tayari kuishi nyinyi" Norbert aliongea huku akileegeza tai aliyoivaa, tai hiyo ilionekana tofauti na tai nyingine zilizoeleka baada ya Norbert kuilegeza, sehemu ya kupita shingoni ilionekana kuwa ina waya wa umeme. Norbert akipowageuzia tai hiyo waione kwa nyuma wote kwa pamoja walijikuta akishtuka wakishtuka, yeye ndiyo alizidi kutabasamu kwani aliona ilikuwa ni njia pekee ya kujikomboa katika eneo hilo

               "Ohh! No" Thomas alisema huku akishusha bastola baada ya kuona klekilichokuwa kipo nyuma ya tai hiyo, lilikuwa ni bomu la kutegwa   lilibanwa nyuma ya tai likiwa linazidi kupungua dakika zake. Wenzake nao walishusha silaha zao wenyewe na hawakuwa na ujanja tena baada ya kuona hilo bomu, Benson naye aliishiwa mbinu na akateremsha silaha kama walivyofanya wenzake na wote wakamtazama Norbert kwa umakini wasijue alikuwa amedhamirira kufanya nini baada ya kuwaonesha bomu hilo.

                "kufa kwangu siyo hasara sana bali kufa kwenu ndiyo hasara, hamtapata hata nusu ya malipo ya kazi mliyokuwa mnaifanya na lengo la kuifanya kazi hiyo ilikuwa ni kupata hela. Fikirieni kwa mara mbili ndani ya dakika kadhaa mtakuwa mmetawanyika viungo vyenu vyote mkiwa hamjapata chochote ilihali hamfanyi kazi hii kizalendo mseme mmekufa kishujaa, nikifa mimi shirika zima na ukanda huu wote utanitukuza N001 kafa kishujaa kwa kufa pamoaj na madhlimu" Norbert aliwapa somo lisilohitaji mtaala ambalo liliwaingia hadi kwenye mioyo yao maadui zake wakabaki hawana la kusema.

                "saa yangu ilipotoa mlio wa Alarm niliwaambia kwamba hiyo ni automatic alarm, si kweli bali ilinitaka niactivate hili bomu na mimi nikabonyeza ili kuactivate. Hii ndiyo remote ya hili bomu" Norbert aliwaambia huku akiwaonesha saa yake, maadui zake mbinu zote waliishiwa wakajikuta wakihema kwa kihoro cha kuogopa kufa.

                "ndani ya dakika hizo wote tutakuwa marehemu humu ndani, mkitaka tupone wote basi muambieni, Huyo askari aliyekuwa yupo nyuma yangu afungue mlango anipishe nitoke.Pia napenda mtambue kama mkinipiga risasi hakuna atakayeweza  kulitegua bomu lenye huu waya ulio na mawasiliano na mishipa ya neva zangu. Mkiniua tu nalo linalipuka na litateguka lenyewe nikifika umbali wa kilomita mbili kutoka hapa, sasa uchaguzi wenu msuke au mnyoe" Norbert alizidi kuwatangulia kujanja.

                  "Hisani hebu mfungulie mlango huyo" L.J Ibrahim alijikuta akitii masharti ya Norbert na yule mwanajeshi aliyemleta Norbert alipiga saluti akafungua mlango, Norbeet alipoona mlango umefunguliwa alivua saa yake ya mkononi akawarushia maadui zake ambapo saa hiyo ilidakwa na Santos akaitazama akakuta ikihesabu dakika kama za kwenye bomu.

               "Saa hiyo ni remote kwa ajili ya kutega na kutegua tu na siyo remote kwa ajili ya kulipua, hivyo msijidanganye kama mnaweza kuniua nayo. Pia inaweza kutegua bomu hili ikifika nusu ya dakika zilizowekwa lilipuke" Norbert aliongea huku akigeuka nyuma, alitembea hadi mlangoni akiwa na tabasamu la ushindi baada ya kuwazidi maadui zake ujanja.

Alipofika mlangoni alichomoa ufunguo akatoka kisha akawafungia mlango kwa nje maadui zake, alienda hadi kwenye gari lake na akaingia akaliwasha akaweka gia akaondoka kuelekea getini ambapo mlinzi alimruhusu bila kipingamizi chochote. Norbert alitoka ndani ya ya nyumba ya L.J Ibrahim akaingia barabarani kwa kasi kuhofia wasije maadui zake wakampuuza na kuanza kumfuatilia, kuendesha kwake kwa kasi kituo cha kwanza ilikuwa ni makumbusho ambapo  alitoa koleo kisha akakata waya mmojawapo wa bomu hilo halafu akaivua ile tai akaiweka kando. Aliendelea kuendesha gari kwa kasi huku akiwa  akipitia njia za panya nyingi kuliko barabara kuu kuhofia kufuatiliwa, alizunguka mitaa tofauti ya jiji la Dar es hadi pale alipohakikisha yupo kwenye amani ndipo akaelekea kwenye nyumba ya kampuni yake.

Baada ya Norbert kuondoka huku nyuma wote kwa pamoja ndiyo hasira ziliwarejea wakaona kama wamevuliwa nguo kwa jinsi walivyomkosa Norbert, walibaki wakiwa wamechoka pasipo kufanya kazi ngumu yoyote  ambayo ingewafanya wachoke. Kila mmoja alikuwa akiugulia kivyake hasira zilizokuwa zikimfurukuta ndani ya moyo wake baada ya kuzidiwa ujanja na bingwa wa ujanja, uchungu dhidi ya kuzidiwa ujanja ulikuwa mkubwa sana kwa Benson hadi akajikuta akilia akiona Mungu alikuwa akimyima fursa ya kulipiza kisasi cha kuuawa pacha wake na Norbert.

Alijikuta akiufuata ule mwili wa rafuiki yake Norbert ambaye ni mwandishi wa habari akaupiga mateke mfululizo, alipochoka alitoa bastola akaanza kuuumiminia risasi hadi bastola ilipofyatuka chuma kilichopo nje  ya bomba kurudi nyuma baada ya risasi kuisha. Alipiga kelele kwa nguvu kama kichaa na akarudia tena kuupiga mateke mwili wa yule mwandishi wa habari waliyemtumia kumnasa Norbert, aliona haridhiki  na  kuupiga huko mwili huo akaufungua kamba ngumu walizokuwa wamemfunga kisha akaulaza chini. Aliutazama mwili huo huku akihema kama kama nyoka aina ya kobra akiwa anajianda  kumkabili adui, aliukanyaga tena mwili ule hadi ukawa unatoa majimaji mdomoni lakini bado hasira zake za kumkosa Norbert hazikumuisha hata kidogo. Aliwatazama wenzake ambao walikuwa wakimtazama kwa masikitiko sana kwa jinsi alivyokuwa na hasira sana, walikuwa wamemuacha aupigwe huo mwili anavyotaka na alipoacha kuupiga huo mwili wakajua  tayari alikuwa kumbe bado hasira zilikuwa zipo ndani ya nfsi yake.

Benson alipoacha kuwatazama wenzake alirudisha macho yake kwenye mwili wa mwandishi wa habari rafiki yake Norbert ambao ulikuwa hautambuliki na wala haufai kutazamika kwa macho ya kawaida, alipoutazama ule mwili alikuwa kama ndiyo anamuona Norbert  ambaye ndiye adui yake mkubwa. Hasira zake zilizidi mara dufu hasa baada ya taswira ya maiti ya pacha yake kumjia kichwani , alijkuta akijisachi kiunoni akatoa kisu cha  kufungua na kujifunga kisha akawa anauinamia ule mwili akiwa ameshika kisu akikielekeza upande wa nchi yake chini. Alikuwa tayari ameingiwa na roho yenye zaidi ya unyama na ukatili zaidi hata wa Simba anaporarua mawindo yake. Alikuwa akidhamiria kufanya jambo baya zaidi katrika mwili huo ambalo kwa binadamu wa kawaida halimpasi kufanya, jambo halikuwezekana kufanyika kwani Thomas alimuwahi kwa kumpokonya kisu akakitupa kutoka sebule hiyo hadi sebule ndogo ya kulia chakula ambayo nayo samani zilikuwa zimetolewa.  Wilson naye alimuwahi kwa haraka akamshika madhubuti asiendelee kufanya ukatili ambao haukuwa na tija yoyote kwa maiti hiyo, Benson  aliishia kufurukuta akirusharusha miguu lakini Wilson hakuwa tayari kumuachia.

              "nasema niachie mimi huyu mshenzi nimtie adabu" Benson aliongea kwa hasira huku akilia.

              "Come on Benson huyu reporter ana kosa gani?!" Thomas alimuuliza kwa sauti ya juu, muda huo huo saa ya Norbert iliyokuwa ipo mikononi mwa Santos ilitoa mlio kisha ikawaka taa kwenye kioo, Santos alipotazama kwenye kioo alikutana na  taswira ya mkono wa binadamu ikiwa umeonesha alama ya dole la kati apamoja na maandishi yaliyoandikwa 'LOSER'

               "Damn Norbert!" Santos aliongea kwa hasira huku akiibamiza saa hiyo kwenye marumaru

Wote walibaki wakimtazama Santos baada ya kuipigiza saa hiyo kwenye sakafu ya nyumba hiyo waliyopo hadi ikavunjika kioo, sauti ya kvunjika kwa saa hiyo iliwafnya wote wanyamaze kwa ghafla na macho yao wakayaelekeza kwa Santos ambaye alikuwa akiitazama saa hiyo kwa hasira sana baada ya kuivunja. Santos aliiongezea saa hiyo kwa kuikanyaga na kiatu chenye soli ngumu hadi ikavunjika sehemu zingine zilizosalia, alipomaliza kuivunja hiyo saa alinyanyua uso wake akawatazama wenzake waliokuwa wakimshngaa.

Alipowatzama wenzake alitaka kuongea jambo ila akasita akabaki akiwa amefungua mdomo wazi kama alikuwa anataka kupiga muayo,  alinyanyua mkono juu kwa ishara wamsikilize lakini  hakuongea neno lolote. Hasira za kushindwa kutekeleza mpango wao ndiyo zilikuwa zikimtafuna hadi akawa katika hali hiyo, alikuwa akipigana na hali ya kuwa na hasira ilia arudi katika hali ya kawaida ndiyo maana alishindwa kuzungumza hadi pale hasira zake zitakopopoa.  Hasira bado ilikuwa ikimchemka ndani ya kichwa chake hadi akaweka mkono wa kuume kichwani kama alikuwa akiizuia isizidi kumchemka kichwani mwake, wote waliobaki waligeuza macho kumtazama yeye kwani walikuwa wakimtambua kama mtu mwenye hasira sana na hasira zake zikimpanda huweza kufanya jambo baya lolote. Benson aliacha kufanya vurugu zake kwa kuhofia angeweza kumtibua kabisa Santos akiwa amependwa na hasira namna hiyo, wengine waliosalia bado macho  yao yalikuwa yapo kwa Santos kumuangalia angefanyaje baada ya kuwa na hasira hivyo.

                 "Nyinyi .........." Santos aliwatukania mama zao wote kisha akaendelea, "tukikaa hapa na kuanza kujilaumu inasadia nyinyi, ndiyo atarudi hebu nyanyukeni tukajipange tena acheni us....". Santos aliwafokea wenzake kwa kujilaumu pasipo kufikiria hata yeye mwenyewe alikuwa akijilaumu pia, hasira zilimpelekea yeye kuwa namna hiyo.

 Alipoona wenzake wanamtzama tu kwa mshangao aliachia msonyo mkubwa sana kisha akatoka akaanza kutembea kuelekea sebule ndogo ya kulia chakula, alipofika kwenye sebule hiyo iliyokuwa haina samani alilisogelea dirisha akashika vyumba vinavyowekwa kabla ya kubandikwa kioo kwa nje. Hapo aliinamisha kichwa chake chini kwa sekunde kadhaa na alipokiinua alitazama nje kupitia hapo dirishani, alipoacha kutazama nje aligeuza shingo nyuma kuwatazama wenzake akawaona bado walikuwa wakimshangaa vile vile ilivyokuwa.

                 "Mnashangaa nini nyinyi? Katupeni mzoga huo tuingie kazini " Santos aliwaambia kwa ukali kisha akageuza shingo kuangalia nje kama alivyokuwa awali huku akiwa ameuma sehemu ya juu ya papi za midomo yake

USIKU WA SIKU HIYO

BARABARA YA OBAMA

 Ilpotimu majira saa sita usiku eneo la ufukwe wa bahari ambapo kupo mkabala na Ikulu kulipata kufikiwa na watu ambao ni nadra sana kufika eneo hilo, ardhi ya eneo hilo ilianza kutetemeka na hatimaye Nyambizi kubwa zipatazo kumi zikaibuka ndani ya maji  umbali mita takriban hamsini kutoka ndani ya maji. Nyambizi hizo zilijifungua kwa juu na kisha zikatoa  vyuma vipana mfano wa njia za kupandishia gari kwenye ndege, taa kubwa kutoka kwenye nyambizi hizo ziliwashwa  kisha magari ya  kijeshi aina ya hummer na jeep zilizojaa wanajeshi ambazo zipo wazi juu zikaanza kutembea kutoka ndani ya nyambizi hizo zikifuata njia maalum ya vyuma hivyo ambavyo vilikuwa vimewekwa  kapeti fano wa barabara.

 Magari yote yalikuja kusimama pembeni ya barabara ya Obama yakawa yanatazamana na ikulu, wanajeshi nao waliokuwa na silaha wakiwa wamevaa magwanda na kofia ngumu vichwani mwao walishuka kwa haraka kisha wakapiga goti moja wakiwa wameelekeza silaha zao ilipo  ikulu. Kikosi cha wanajeshi waliopo kwenye magari kiliposhuka chini chote vifaru vyenye rangi ya kijani kibichi navyo vilifuatia vikiwa na  maaskari wengine wanaokimbia kwa miguu wenye silaha wakiwa wanavifuata kwa nyuma, vifaru hivyo navyo vilienda kujipanga mstari mmoja nyuma ya magari ya jeshi kwa umbali wa hatua takribani tano. Baada ya hapo kisha walishuka askari maalum waliokuwa wapo ndani ya magari ya mizigo ya jeshi wakiwa wamebeba mizigo mikubwa sana, askari hao walienda kushuka upande mwingine ambapo vifaru vilikuwa havijafika kisha mizigo mikubwa iliyokuwa ipo ndani ya gari ikashushwa kwa kutumia mtambo maalum unaofungwa nyuma ya kichwa cha magari hato ya mizigo. Mizigo hiyo ilifunguliwa kisha askari hao wakaanza kuchakarika kwa kazi maalum iliyokuwa imewaleta hapo, ndani ya muda mfupi tayari mahema ya kijeshi yalikuwa yameshafungwa na maaskari hao.

 Saa sita kamili usiku ilipotimu  kukatimia kwa siku mbili kufikia  siku ya mapinduzi iliyosemwa,  maaskari  wa jeshi la maji tayari walikuwa wamejaa eneo hilo walikuwa wakitishia amani ya raia wa kawaida na halikufaa kupitika kabisa. Kutotumiwa kwa barabara ya Obama majira ya usiku kulifanya raia wa kwaida wasiweze kujua kile kilichokuwa kikiendelea eneo hilo kwa muda huo. Wanajeshi hao hawakuwa wamefunga jicho tu siyo kulala tu, macho yao yalikuwa makini kuiangalia ikulu kama amri ya kiongozi mkuu ilivyowataka kufanya hivyo. Ikulu yote ilikuwa imezungukwa na wanajeshi hao kwa kila pande na hakukuwa na nafasi nyingine ya mtu aliyekuwa yupo ndani ya ikulu kutoka , silaha zote za wanajeshi hao ikiwemo mizinga na bunduki za kila namna zilikuwa zimeelekea katika kila upande wa Ikulu.

Ndani ha ikulu hali ilikuwa tete kwa Rais Zuber baada kuona kikosi hicho kizito cha jeshi la maji kupitia mitambo maalum iliyopo hapo ndani, alitoa amri kwa vikosi vinavyohusika na usalama wake kukaa jirani na uzio wa Ikulu kwa pande zote huku wengine wakiwa wamekaa juu kwenye mapaa ya ikulu wakiwa na risasi maalum za udunguaji. Pamoja na ulinzi huo wa usalama wa taifa waliokuwa wamevalia suti nyeusi wakiwa silaha bado aliona hakuwa na usalama na aliingia wenye chumba maalum cha kuongoza mitambo yenye kuhakikisha usalama wa ikulu nzima unakuwepo na akabaki akiangalia jinsi maafisa wa usalama wanavyochakarika na kazi yao.  Usingizi wote ulikuwa umeshamuisha na alimuacha mke wake akiwa amelala chumbani yeye akabaki akiwa anatazama wingi wa wanajehi hao kupitia kioo cha tarakilishi, alijikuta akichachawa alipoangalia silaha nzito ambazo yeye hajawahi kuziona akiwa kama amiri jeshi mkuu tangu aingie madarakani.

             "Tanzania haina nyambizi kubwa kiasi hiki na wala sina taarifa ya kuongezwa kwa Nyambizi katika jeshi la maji" Rais Zuber alisema huku akizitazama Nyambizi hizo.

             "Mheshimiwa inamaana huna taarifa za umiliki wa silaha nzito kama hizi katika jeshi" Kiongozi mkuu wa chumba cha kuongozea mitambo aliuliza.

              "Ndiyo sina taarifa hizo hata  General Kulika kabla hajafariki aliwahi kusema  Tanzania jeshi lina Nyambizi za kawaida na alikuwa ananishauri ziongezwe kubwa mbili kwa usalama zaidi wa nchi hii upande wa majini, Nyambizi zilizokuwa zipo nilioneshwa siyo hizi kabisa" Rais Zuber aliongea huku akihema kwa wasiwasi.

              "Hebu niunganishe na Meja jenerali Belinda kwa simu nisikie anasemaje kuhusu huu uvamizi unaotaka kufanywa ili wanipindue" Rais Zuber alimuambia kijana wa usalama wa taifa aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha kuzunguka kilichokuwa  kipo jirani na mitambo mingi ya tarakilishi, kijana huyo alipopokea amri alibonyeza namba zilizopo kwenye kibonyezo cha tarakilishi kwa haraka sana halafu akasita baada ya kuona kialama maalum kilikuwa kimetokea kwenye kioo. Alijizungusha kwenye kiti hicho cha kuzungukaakageuka nyuma yake alipokuwa Rais Zuber kisha akavua spika maalum za masikioni alizokuwa amezivaa, aliijipangusa na viganja vyake usoni kisha akashusha pumzi akiwa anamtazama Rais Zuber.

               "Kuna nini?" Rais Zuber aliuliza

               "Mheshimiwa simu zote zakutoka zinatoka na kuingia ndani ya ikulu tayari wameziua kupitia mtambo maalum ambao wanao wao" Yule kijana alimuambia

                "Ohhh! No!" Rais Zuber alitoa sauti ya kukata tamaa kisha akaweka mikono kichwani kwa sekunde kadha na alipoitoa mikono hiyo kichwani alisema,"hata wao ukiwasiliana nao huwezi"

               "ngoja nijaribu" Yule kijana aliongea kisha akakigeuza kiti chake akaangalia upande wenye tarakilishi, alibonyeza vitufe vingi vilivyokuwa chini ya kioo cha taraklishi hiyo kisha akasema "tunao uwezo wa kuwasiliana nao tu".

               "Ok niunganishe nao" Rais Zuber alisema  akasogea nyuma ya kile kiti cha yule kijana karibu na kioo kikubwa cha tarakilishi kimojawapo, Yule kijana alifanya ujuzi wake na kioo hicho kikatoa alama mistari iliyokuwa ikizunguka duara huku kukiwa na maandishi 'connecting'. Baada ya muda sura ya mwanajeshi mtu mzima mwenye cheo cha Meje jenerali akiwa amevaa  gwanda pamoja na kofia ya rangi ya nyeupe  ilionekana, Rais alipoona sura hiyo kwenye kioo moja kwa moja alimtambua kama huyo ni msaidizi wa L.J Ibrahim.

             "Mugiso" Rais Zuber aliita huku akitazma kwenye kioo cha tarakilishi.

             "Yes Mr President" Meja jenerali  huyo aliongea.

             "mimi si mkuu wako kijeshi, kwanini unaleta vikosi kunizunguka" Rais Zuber alilalamika

              "wewe ulikuwa ni mkubwa  wangu lakini kuna mkubwa wangu mwingine ajaye atakayeingia hapo kwa sasa,  hivyo wewe siyo mkubwa wangu tena na ni amri kutoka kwa three star general baada ya kutopata majibu yako kwanini mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa amuue four star general na kwanini leo hii ukaonana na mtuhumiwa halafu usimkamate" Meja jenerali Mugiso aliongea.

              "Come on Mugiso! Moses ni innocent katika hilo usifanye usichokijua" Rais Zuber aliongea

              "sina uamuzi mwingine zaidi ya huo nilioambiwa na future general, maamuzi yatabadilika iwapo atatoa tamko yeye. Kutokuwa na hatia kwa Professa Gawaza kamuambie yeye ndiyo aamue. Kwa sasa ni hayo tu, nikutakie usiku mwema Mheshimiwa kesho kutwa ndiyo siku ya wewe kutoka hapo" M.J Mugiso aliongea na hapo mawasiliano yakakatika, Rais Zuber alichanganyikiwa zaidi na maneno hayo akajikuta hana uamuzi mwingine wa kutoa juu ya suala hilo.

(3)MFUNIKO

 Asubuhi iliyofuata habari kubwa iliyokuwa imetawala ndani na nje ya nchi ilikuwa ni hiyo ya kuzungukwa Ikulu na wanajeshi wa jeshi la Maji, hali hiyo ilizua hofu pia miongoni mwa raia na kuepelekea hata wananchi wa kawaida washindwe kulikaribia eneo la Ikulu kwa uoga waliokuwa nao baada ya wingi huo wa wanajeshi wenye silaha nzito. Watu pekee waliokuwa hawana hofu ya kupita eneo hilo walikuwa ni waandishi wa habari ambao walifika na kurusha habari juu ya tuko zima la kuzungukwa kwa ikulu, Helikopta za mashirika mbalimbali ya habari zilikuwa zikizunguka juu kuchukua matukio yaliyokuwa yakiendelea katika eneo hilo. Hadi jua linachomoza hakuna alyekuwa ndani ya ikulu ambaye aliweza kutoka nje kutokana na kuzingirwa huko pia amari waliyopewa wanajeshi hao ya kuhakikisha hatoki mtu ndani ya ikulu. Vyombo vya habari mbalimbali viliendelea kuripoti kuhusu suala hilo ambapo bado ilikuwa haijaeleweka chanzo cha kuzungukwa namna ile ikulu, jitihada za waaandishi wa habari katika kusaka chanzo cha  kuzungukwa kwa ikulu hiyo ziligonga mwamba kabisa na hakuna aliyeweza kupata ufafanuzi juu ya suala hilo.

Ilipotimu majira ya saa nne ndipo Meja jenerali Mugiso aliweza kuonekana akitoka ndani ya hema la kijeshi lilipo eneo hilo akiwa ameongozana na wanajeshi wenye nyota mbili wapatao wanne, Meja jenerali aliendea hadi kwenye gari la kijeshi ambapo aliingiza mkono ndani ya gari hiyo akavuta kipaza sauti kilichokuwa na waya mrefu. Alikiweka kipaza sauti umbali wa sentimita takribani mbili kutoka ulipo mdomo wake kisha akaongea, “hili ni ombi kwa sasa wala si amri kwa wote mliopo ndani ya ikulu takatifu, mnaombwa kutoka wenyewe ndani ya ikulu na mjisalimishe tuwakamte kabla rais mpya mtarajiwa hajaingia jumamosi asubuhi. Leo siku ya alhamisi mnaombwa kutoka wenyewe kabla hatujatumia nguvu kuwatoa humo, Rais uliyemaliza muda leo kabla ya miaka kumi haijaisha unapewa siku ya leo na kesho tu usiwepo humo ndani”

Meja jenerali Mugiso baada ya kutoa tangazo hilo alimkabidhi kipaza sauti mmoja wa maluteni kisha akaanza kutembea kurudi kwenye hema kuu lililowekwa eneo hilo, waandishi wa habari walimkimbilia lakini waliwahi kuzuiwa na wanajeshi wasifike anapoelekea.

           "General tunahitaji kuzungumza na wewe machache" Mmoja wa waandishi wa habari alipaza sauti na waandishi wa habari wengine wakiwa wameshika vipaza sauti walimuita Meja jenerali Mugiso jambo ambalo lilimfanya arudi tena hadi pale walipozuiwa akawaamuru maluteni wale wawaachie.

           "General inamaana muda wa urais ni miaka miwili tu hadi umuambie mheshimiwa amemaliza muda wake?" Maswali yalianza

           "General je kipi chanzo cha kuwaamuru vijana wako waizunguke ikulu?" Mwandhishi wa habari mmoj aliongea huku akimnyooshe mkono wake uliokuwa na kipaza sauti.

            "je ni sahihi kumuamuru  mkubwa wako kijeshi atoke ndani ya ofisi yake?" Mwandishi wa haabri mwingine alimtandika swali akiwa bado hajalijibun swali la kwanza.

            "Je kupanga kumuondoa rais anayependwa na wananchi namna hii huoni kama itawapa picha mbaya sana hasa upande wenu?" Mwandishi wa habari mwingine alimpa swali akiwa hajajibu mengine, maswali mengi yalikuwa yamemuandama Meja jenerali Mugiso ambaye alikaa kimya hadi pale waandishi wa habari waliponyamaza ndiyo akanyoosha mkono kama aliyekuwa akitaka kutoa kiapo huku mdomo akiwa ameacha wazi akitafuta neno la kuongea.

              "Sijawa msemaji mkuu wa jeshi mwenye mamlaka ya kuongea maneno hayo, hii ni amri nadhani mkaulize uongozi wa juu yangu ndiyo utawapa jibu" Meja jenerali Mugiso aliongea kisha akaanza kupiga hatua kuondoka.

             "Ikiwa utapewa amri ya namna hii juu ya mkeo na uongozi wa juu upo tayari kuifanya?" Swali jingine kutoka kwa mwandishi wa habari aliyekuwa yupo katikati ya kundi la waandishi wa habari kulimfanya M.J Mugiso asite kuendelea na safari kisha akageuka nyuma akarudi hadi pale uso wake ukiwa haupo kawaida.

              "Nani aliyeuliza swali hilo?" M.J Mugiso aliuliza na hapo waandishi wa habari wakamtazama yule mwenzao aliyekuwa ametulia wala asioneshe hofu yoyote, mkono wa mwandishi huyo wa habari aliyeuliza hilo swali ulinyooshwa na kupelekea wanajeshi wale maluteni wapite katikati ya waandhi wa habri wakamkamata mwandishi huyo wakamvuta mbele kwa nguvu, M. J Mugiso alipomuona mtu aliyeuliza swali hilo alijikuta akiwambia wale maluteni waliokuwa wakijiandaa kumpiga wamuache.

                "Norbert Kaila ndiyo adabu uliyofundishwa kwenu hiyo?" M.J Mugiso alimuuliza swali

                "General ni swali kama swali jingine ikiwa wewe unafuata amri za mkubwa je upo tayari kutii amri juu ya mkeo unayempenda?" Norbert aliuliza swali hilo ambalo lilimfanya M.J Mugiso amtazame kwa hasira halafu akaondoka akihofia kumuadhibu habari ile isambae na kulichafua jeshi kwa kutesa mwandishi wa habari.

                "hakikisheni mwandishi wa habari yoyote havuki eneo la kivukoni kuanzia muda huu, tumeelewana?!" M.J Mugiso alitoa amri, wale maluteni walitoa heshima kwa ukakamavu baada ya mari hiyo kisha wakaanza kuwaondoa waanhishi wa habari ndani ya eneo hilo kwa nguvu.

M.J Mugiso alirudi ndani ya hema ambapo alienda hadi kwenye eneo maalum ambalo lilikuwa na mitambo mingi ya kisasa ya mawasiliano ikiwa imepangwa kwa ustadi mzuri, kwenye kioo cha moja tarakilishi kwenye mitambo hiyo kulikuwa kuna sura ya L.J Ibrahim ikiwa inamtazama yeye baada ya kuingia eneo hilo. M.J Mugiso alitoa saluti baada ya kuiona taswira ya mkuu wake kisha akasimama kikakamavu akitoa amri, alitulia akimsubiri mkuu wake aongee na hapo mkuu wake alianza kuongea.

                "vizuri kwa kazi uliyoiongoza kwa msaliti anayeishi ikulu sasa basi kuna la ziada unatakiwa ulifanye, nimeona kupitia luninga mwandishi wa habri anakudhalilisha sasa hakikisha vijana wanamtia nguvuni ili aje kulipia kwa kauli zake zisizo na adabu" L.J Ibrahim alitoa amri ambapo M.J Mugiso alipiga saluti kisha kisha akachukua simu ya upepo akaongea, "hakikisheni mnamkamata Norbert Kaila aingizwe ndani ya Submarine haraka tumeelewana!"

                 "Mkuu" Sauti kwenye simu ya uepo iliitika kwa adabu, baada ya hapo kioo cha mawasiliano ya ana kwa ana baina ya M.J Mugiso na mkuuu wake kilikata mawasiliano na ramani ya eneo la ikulu ikatokea.

 Wakati hayo yakiendelea  L.. J Ibrahim na Mzee Ole walikuwa wakiyatazma kupitia kwenye luninga huku wakiwa wamepambwa na matabasamu katika nyuso zao, walijua tayari walikuwa wakikaribia kuimaliza kazi hata Norbert angekuwa na uwezo gani asingeweza kumuokoa Rais Zuber na balaa lililokuwa likielekea kumkumba. Mvinyo ndiyo ulikuwa umetawala katika meza yao huku wakiwa na faraha sana katika nyuso zao, walikunywa kwa kufurahi wakijua kuwa nchi ya Tanzania tayari ipo kwenye mikono yao na  Mzee Ole alikuwa akirudi madarakani na wao waweze kugawana fungu la pesa walilokuwa wameahidiwa. Muda huo ulikuwa ni muda mfupi tu tangu L.J Ibrahim atoe amri ya kukamatwa kwa Norbert  baada ya kumuona kupitia kioo cha Luninga akimuuliza swali M.J Mugiso, waliendelea kufuarahi huku wakinywa kwa pamoja chupa ya mvinyo kwa kutumia bilauri tofauti. Walikuwa wakiongea na kucheka kwa furaha sana kila walipokuwa wakiiangalia Luninga jinsi ilivyokuwa ikirusha matangazo juu ya kinachoendelea Magogoni. Hakika hatua ya ushindi wa mwisho ndiyo waliiona ilikuwa wakiikaribia kuifikia na vikwazo vilikuwa vikiondoka kimoja baada ya kingine, walibadilisha chaneli mbalimbali za luninga bado habari ilikuwa ni ileile hata walipoweka chaneli za nje ya nchi.

           "aisee kazi imekwisha nasubiri wale vijana wa nusu komandoo wamtie mikononi Kaila tuje tummalize nina uhakika hatatoka" L.J Ibrahim aliongea

           "Kabisa General" Mzee Ole aliitiki, muda huuohuo simu ya upepo iliyokuwa ipo jirani yao ilianza  kukoroma na hapo L.J Ibrahim aliichukua m kwa haraka.

           "Enhee nipeni habari, Norbert mnae hapo" L.J Ibrahim aliuliza

            "Hatujamuona mkuu hata waandishi wa habari wenzake wanasema hawajui ameelekea wapi?" Sauti ya M.J Mugiso ilisikika kwenye simu hiyo ambayo ilimfanya L.J Ibrahim aondokwe na furaha papo hapo.

            "Wajinga nyinyi!" L.J Ibrahim alifoka kwa hasira.

“Mkuu katupotea kwenye mazingira ya kutatanisha”

                 "Ye kawa mchawi kwahiyo atawapoteaje namna hiyo? Kama si uzembe ni nini?"

               "Hapana mkuu nahisi huyu mtu ana namna"

                 "Pumbavu sitaki kusikia hayo nasema kamata hao waandishi wenzake wote ndiyo watajibu alipokuwepo, mtamuachaje mtu anayedhaiisha ofisa wa jeshi fanya haraka nataka hao waandishi wa habari wawe chini  ya ulinzi mara moja"

                "Mkuu"

                    "ndani ya robo saa nataka nisikie ukiripoti tayari hao waanDishi wapo chini ya ulinzi tunaelewana?!"

                 "Mkuu"

Baada ya hapo L.J Ibrahim alikata mawasiliano na akamtazama Mze Ole ambaye alikuwa akifuatilia maongezi hayo kwa umakini mkubwa sana, alishusha pumzi kisha akasikitika kwa jinsi walivyokuwa wakkihangishwa na Norbert. Mivnyo aliokuwa na anaunywa aliuacha mara moja na akasimama na mikono akaweka kiunoni, alipigapiga chini kiatu cha jeshi alichokuwa amekivaa huku akiwa amekunja sura yake kwa jinsi wanavyohangaishwa na Norbert.

                    "General huna sababu ya kumlaumu Mugiso, kumbuka tunapambana na mtu zaidi ya komandoo"

                    "Natambua hilo Ole lakini nao ni wazembe vilevile yaani mtu tunamuona hapa kwenye tv muda ambao tunawatuma wamkamate na hadi anaondoka kwenye usawa wa kamera hii ya televisheni ya taifa wangekuwa tayari wameshamkata"

                  "No no Norbert ni mtu mwenye akili sana huenda alishahisi hayo"

                    "Ole kumbuka wale ni special force wa jeshi la maji unafikiri watamkosaje mtu kama yule"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

                     "General kumkamata huyu mtu na kumuua inabidi tutumie akili na siyo kupanic, sasa hivi anatuchezea akili kwa kupanic kwetu unafikiri tukiendelea kupanic si ndiyo atatuvua nguo za ndani kabisa huyu"

                 "Ok nimekuelewa unashauri tufanyeje?"

                 "Wapigie kina Santos huyu mtu hayupo mbali na hapo nahisi'

                     "ok" L.J Ibrahim alikubali kama alivyoambiwa na alitoa simu yake ya mkononi akwapigia hao watu alioambiwa.

ITAENDELEA

Wakala wa Giza Sehemu ya Nne

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment