Msako wa Mwanaharamu Sehemu ya Tano
KIJASUSI

Ep 05: Msako wa Mwanaharamu

Msako wa Mwanaharamu Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE

*********************************************************************************

Silimulizi : Msako Wa Mwanaharamu

Sehemu Ya Tano (5)

“Mimi ni mwandishi wa habari, nina kampuni yangu inaitwa AGI Investment, tunashughulika na utafutaji wa habari za kitaifa na kimataifa, kuandika makala mbalimbali na habari za uchunguzi,” Amata akaeleza huku akimpatia kadikazi mwanamke huyo mwenye sura ya kuvutia.

Mazungumzo yakaendeleakwa kina kati ya wawili hao, Amata alikuwa akijaribu kucmchokonoa kwa maswali ili kujua mengi kuhusu kisiwa hicho, na mwanamke yule alikuwa akijibu pasi na wasiwasi wowote. Yule mwanadada aliyejitambulisha sasa kwa jina kamili la Zulekha alimwambia mengi sana juu ya kisiwa cha Kalebbe na Amata akamweleza mengi juu ya kampuni na kazi yake.

Nusu saa ikapita katika mazungumzo yao Amata hakuendelea kunywa kile kinywaji ila sasa alikuwa ni mzungumzaji zaidi kila Zulekha alipomhamasisha kunywa zaidi yeye aliishia kumimina tu, akimwambia ‘usijali nitakunywa’.

“Utapenda kunitembelea?” Zulekha akauliza huku akiumauma ncha ya ulimi wake.

“Kama utanitembelea mimi kwanza!” akamjibu namna hiyo.

Zulekha, akatazama chini kwa sekunde kadhaa, kisha akamtazama Amata usoni bila haya.

“Unataka nikutembelee?” Zulekha akauliza huku akirembua macho yake.

“Ndiyo, kisha nami nitakutembelea wewe!”

“Good boy! Utaniweza?” Zulekha akauliza huku mkono wake ukiishika ile ya Amata pale mezani.

“Kwa nini unauliza hivyo?”

“Kwa sababu ninyi vijana wa mjini mnakula sana chips, mkifika kwenye sita kwa sita mnahema kama mbwa anayekimbilia mfupa,”

“Hah! Hah! Hah! Mi siyo aina hiyo ya mwanaume,” Kamanda akajibu na mara hiyo, Zulekha akainuka na vazi lake likajimwaga na kuacha eneo kubwa la mbele wazi. Akamtazama kijana huyu shababi kwa jicho kimahaba.

“So?”

“Let’s feast!” Zulekha akamalizia na kumpa mkono Amata, wakatembea kwa hatua za madaha kuelekea katika ngazi ambazo ziliwafikisha ghorofa ya juu, ndani ya chumba cha Amata. Kama kuna kitu ambacho Kamanda alikuwa akijipanga kujibu ni juu ya lile darubini, maana kwa ubembe wa mwanamke huyo angeweza kutaka kuchungulia, ndipo angeona nyumba yake inavyoangazwa kwa ukaribu lakini walipoingia ndani ile darubini haikuwepo. Gina mara tu baada ya kusikia mazungumzo ya wawili hao akajua safari yao itafikia ndani ya chumba hicho, hivyo akaibeba ile darubini na kutoka nayo huku moyo ukimuuma wivu.

Wawili hao wakajitupa kitandani na mabusu motomoto yakachukua nafasi yake. Amata aliufurahia utundu wa mwanamke huyo maana alikuwa akimrambaramba kila kona ya mwili wake na yeye akaonesha utundu wote anaoujua. Dakika kama arobaini na tano hivi wakabaki kama walivyozaliwa na kila mmoja akaanza kufurahia kile afanyacho mwenzake na kujikuta wamezama katika mahaba mazito. Amata akasahau kazi, Zulekha akasahau kazi. Miguno na sarakasi za ajabu ajabu zikaendelea juu ya kitanda hicho.

“Uko vizuri kijana! Karibu nyumbani kwangu, sasa tutaweza kuzungumza mengi,” Zulekha akamwambia Amata baada ya kila mmoja kuridhika na huduma ya mwenzake.

“Namwogopa mumeo!”

“A ha! Hah! Hah! Hah! Sina mume… isitoshe ndani ya nyumba ile kuna mambo mengi, we utakuja kama mfanyabiashara kisha mengine mi najua tutafanyeje,” akamsihi kijana huyo. Kwa Amata hii ilikuwa ni nafasi ya pekee kuweza kufika kwenye jumba lile ambalo ndilo haswa lilikuwa limewaleta hapo Bagamoyo. Lakini kichwa chake tayari kilimwambia hapo kuna hatari ya kulubuniwa na kutekwa kirahisi.

“Vipi mbona hunipi jibu? Au hutaki kuijua Kalebbe? Utakosa habari!”

Amata akamgeukia na kumtazama machoni, akaona hila ya wazi kabisa kwa mwanamke huyu.

Sina budi kufanya hili, the opportunitry never come twice! Akawaza na kujiinua kitandani.

“Sawa, twende zetu!” akamwambia mwanamke huyo aliyejilaza kitandani kifua wazi, matiti yake kama ya msichana anyevunja ungo yalimfanya aonekane mrembo kama samaki-mtu. Zulekha akatabasamu na kumuuliza, “Upo peke yako?”

“Yes, peke yangu,” Amata akajibu. Kisha wote wakajiandaa kwa safari, wakatoka nje ya hoteli hiyo na kuelekea gatini ambako ile boti bado ilikuwa ikimsubiri. Wakaagana na Nassoro na kuondoka zao.

  • * * Katika Kisiwa cha Kalebbe vijana wa Pancho walibaki wakitazamana baada ya kutazama picha nzuri ya Zulekha na Amata pale kitandani. Picha hii iliyonaswa na mtambo uliofungwa katika jumba hili, ni wachache tu walioujua. Wale vijana walimwita mkubwa wao wa kitengo na kumwonesha anachofanya mwanamke huyo. Walijua wazi kuwa kila picha wanayoiona lazima Pancho anaiona kama ilivyo. Wote wakajikuta wakiduwaa mbele ya sikirini hiyo udenda ukiwatoka na miili yao ikikosa utulivu kila waliposhuhudia mke wa bosi wao akibanjuliwa na Kamanda Amata.

Nusu saa ilipita na kisha wakaona sasa safari inaanza ya kuja kisiwani.

“Anamleta, hakikisheni analipa yote aliyoyafanya kwa mwanamke huyu,” Yule mkubwa wao akatoa amri kisha akawapa tahadhari wengine kuwa wampokee kama mgheni wa bosi, wasimletee matata yoyote mpaka waambiwe vinginevyo.

Ndani ya kisiwa hiki, gabacholi huyu alikuwa amewekeza vitu vingi sana kwa siri, kulifungwa darubini kubwa ya kutumia umeme ambayo iliwawezesha viajana wake kuona nyendo zote za mtu wamtakaye. Mara tu baada ya kupata taarifa kutoka kwa mtu wao, Nassoro, ndipo wakaazimia kumtuma Zulekha kwa ajili ya kumnasa mtu huyo, maana walijua mwanaume hawezi kuponyoka kirahisi kwa mwanamke mrembo kama huyu. Na hii ndiyo ilikuwa kazi kubwa ya Zulekha kwa bwana wake, Pancho.

Pancho alipata taarifa ya ugeni huo akafurahi sana na mara hii alihakikisha kumtia adabu kijana huyu ambaye bado anakumbuka mambo aliyomfanyia huko India na kwenye ndege wakati wa kurudi.

  • * *

Gina aliinuka kitini na kuibeba ile darubini, haraka akaufungua mlango wa chumba cha Amata na kuingia ndani, akapita mpaka kwenye kibaraza kilekile akaiweka tena na kuanza kuchungulia na kuiona ile boti ikipotelea majini.

“Shit! Janaume linapenda wanawake hili, limeshatekeka kilaiiniiii,” akajikuta akiongea peke yake alipomuona Amata akiwa na Zulekha katika ile boti, akasonya na kuiacha ile darubini huku akiondoka na moyo uliyojaa wivu maana alijua wazi uwa Kamanda lazima keshamtafuna mwanadada huyo. Alipofika mlangoni, akakumnbana na Chiba na Madam S.

“Rudi ndani,” Madam akamwamuru huku Chiba tayari akiwa kwenye ile darubini akitazama ile boti.

“Jiandaeni kwa kazi ya kumkamata yule mwanaharamu, Amata atatuletea taarifa kama mtu huyo yupo au la,” Madam aliwaambia huku akibofyabofya simu yake hapa na pale, akaiweka sikioni.

“Hey!!! Scoba na Jasmine! Stand by! Tukutane Ocean Breeze ndani ya nusu saa, chambo tumeshatupa mtoni bado kuvua samaki,” akamaliza.

“…copy…” akajibiwa na ile simu ikakatika. Mipango ya kina ikapangwa na mwanamama huyu, akawaweka vijana wake katika hari ya mapambano, akawatia moyo na kuwaasa hili na lile.

  • * *

“Karibu sana Kalebbe,” Zulekha akamkaribisha Amata huku akimsubiri ateremke katika boti ile.

“Asante sana, aaaaaaaaah nimefurahi kukanyaga kisiwa hiki,” Amata akajibu huku akiteremka taratibu wakati vijana wakiendelea kuifunga ile boti gatini. Kwa mwendo wa taratibu walitembea katika mchanga mweupe wa pwani ya kisiwa hicho na kufika kwenye kijumba kidogo tungekiita kibanda, lakini kilijengwa kwa unadhifu sana na kilionekana chenye thamani. Pembezoni palikuwa na nyumba nyingine nzuri tu lakini ilionekana haina watu. Yule mwanamke, akaweka kiganja chake cha mkono wa kulia katika kitu kama kioo kilichokuwa mlangoni hapo, kisha akasogeza zura yake, mwanga mwekundu ukapita kati ya macho yake, akatamka jina lake na kisha kubofya tarakimu fulani fulani, ule mlango ukafunguka, wakaingia wote wane, yaani yeye, Amata na vijana wawili na ule mlango ukajifunga nyuma yake.

Ngazi ndefu ilionekana kuteremka, wakaifuata na walipofika chini kama mita ishirini hivi, kulikuwa na njia pacha tatu. Zulekha akasimama na kumtazama Amata.

“Usiogope! Hii ni nyumba ya siri sana na ni watu wachache tu nje ya familia hii wanaopata fursa ya kuiona. Ila mtu wa kawaida akiiona na kuigundua basi huyo huwa hawezi kuishi,” akamwambia huku akimtazama. Amata akatikisa kichwa na kugeuka nyum,a akakutana machi na wale jamaa wawili walioshiba vyema.

“Ukienda kushoto, unaenda kwenye nyumba ya mzee, kulia unaenda kwenye idara ya usalama na sisi tunakwenda moja kwa moja,” akamwambia kisha akaongoza njia ile na Amata akamfuata.

Wakatokea kwenye jumba kubwa la kifahari, lenye kila samani inayostahili kuitwa ‘samani ya ndani’. Kamanda Amata aliitazama ile sebule ya kifahari, iliyozungukwa na kuta za aina yake huku upande mmoja kukiwa na ukuta wa kioo unaoruhusu kuona mandhari ya chini ya maji. Hakuweza kuamini kama katika nchi hii kuna watu wanaoishi kitajiri namna hii. Akatikisa kichwa huku akitazama tu na asijue wapi pa kuketisha makalio yake.

“Kinywaji tafadhali,” mwanadada mrembo mwenye asili ya Kihindi, wa kadiri ya miaka ishirini na tano hivi alimkaribisha kinywaji cha matunda kilichojaa kwenye bilauri.

“Asante sana mrembo … sharubati tu au kuna kingine?” akauliza huku akiwa kamshika mkono wake.

“Oh, sio hivyo, mgeni hawezi kuwa mwenyeji namna hiyo,” Zulekha alimwambia Amata huku akimwondoa yule binti katika himaya yake. Kamanda Amata bado alikuwa akishangaa mandhari safi ya jengo hilo hata akasahau kama ana kinywaji mkononi mwake.

“Huu ndiyo utukufu wa Premji Kanoon, nchi ndani ya nchi,” Zulekha akamwambia Amata huku akiichukua ile bilauri na kuitua mezani, akamkubatia kijana huyo kimahaba huku sura zao zikitazamana.

“Sasa jumba kama hili umewezaje kulijenga hapa?” Amata akauliza.

“Kawaida tu, mafundi kutoka Japan waliifanya kazi hii mchana na usiku baada ya kupata matatizo katika nyumba yetu ya Kerege,” Zulekha akaeleza.

“Mlpata matatizo Kerege?” Amata akauliza.

“Ndiyo!”

“We na nani?”

“Mi’ na mume wangu kipenzi Premji Kanoon, utamwona muda si mrefu kwani ametoka kwa kuwa kesho tunatarajia kuondoka,” Zulekha akajibu kwa ufasaha huku Amata akitikisa kichwa na saa yake ikifanya kazi ya kurekodi.

“Kwa nini mwataka kuondoka?”

“Watu wanataka kumuua mume wangu, na inaonekana ni watu wa serikali, hata swahiba wake aliyefanya mchakato wa kumuuzia kisiwa hiki amekamatwa majuzi tu, hii hali imekuwa mbaya kwake na kwangu pia kwa kuwa hana furaha, hata kitandani hanipi nitakacho…” mwanamke akafunguka na Amata akaendelea kusikiliza kwa utulivu maneno hayo.

Tungechelewa kidogo tu angetutoka kwa mara nyingine! Amata akawaza huku akimtazama mwanamke huyo usoni.

“Unaonekana ni kijana mtulivu, mdadisi, unayependa kujua mambo…”

“Na lingine umelisahau, napenda warembo kama wewe,” Amata akamalizia kusema.

“Warembo ni sumu, watakupeleka pabaya,” Zulekha akamwambia huku akiketi kitini, akawasha sigara yake na kuketi kwenye sofa kubwa la vono.

“Mr….. Spark! Pale Oceanic Breeze umefika lini?”

“Nimefika siku tano zilizopita,” akajibu.

“Spark una maswali kama mpelelezi,” Zulekha akazidi kusaili.

“Si nimekwambia kuwa mimi ni mwandishi wa habari,” akajibu jibu la uongo kabisa.

“Aaaaa! Hah! Hah! Hah! Hapo nitakubaliana na wewe, na nilishasahau kama umenambia …” akamtazama kwa kulegeza macho huku sigara aliyoibana katia ya kidole cha kati na shahada ikiendelea kufuka moshi, “… sasa Bagamoyo kuna habari gani iliyokuleta?” Zulekha aliketi sawia katika kaiti chake akimtazama kijana huyo.

“Inasemekana kuna ndege ndogo imepotea upande huu wa Bagamoyo hiyo sasa ndiyo iliyonileta kuandika hiyo juu ya hilo tukio,”

“Unashirikiana nani?”

“Mimi kama mwandishi wa kampuni ya kuitegemea, naiandika hiyo habari ya uchunguzi kwa ajili ya kuiuza kwa mashirika makubwa, niko peke yangu hapa kwani waandishi wangu wengine wana kazi nyingine za kufanya,” Amata akaeleza.

“Oh, good kazi nzuri sana,” Zulekha akamwambia Amata na wakati huohuo simu ya ukutani ikaita, akanyanyuka na kuiendea akaipokea.

“…Ndiyo, sasa hivi?… ok!” akaitazama saa kubwa ya ukutani ilikuwa ikimwambia kuwa muda huo ilikuwa ni saa kumi na moja jioni. Akarudi pale mezani na kumalizia kinywaji chake.

“Mume wangu karibu anaingia, unapenda kuungana nami kumlaki?” Zulekha akamwambia Amata.

“Yah, bila shaka,” akajibu.

**-

Wote wawili wakaongozana mpaka nje kwa upande wa pili wa kisiwa hicho, pale walikuta wanaume watatu weusi, wenye miili iliyoshiba, walionyoa ndevu zao kama Rick Ross, kutokana na ukimya wao naye hakuwasalimia, bali aliungana na Zulekha kutulia kusubiri.

Helkopta moja kubwa ya kifahari iliteremka taratibu katika pwani hiyo iliyojengwa kinamna, kisha ikazima injini yake, na utulivu ukarejea. Kamanda Amata akapachika miwani yake usoni si kwa sababu ya jua kali bali miwani hiyo ilikuwa ikipiga picha na kuzisafirisha kielektroniki kwenda kwa Chiba na timu yake. Mlango ukafunguliwa, mtu mnene kiasi, Muhindi, aliyevalia suti nyeusi ya bei mbaya, kwa mtazamo tu alionekana ni tajiri, akateremka pamoja na watu wengine wawili ambao moja kwa moja aliwatambua kwa kuwa ni watu wa juu serikalini. Pancho alipogongana macho na

Pancho akatamani kuanguka lakini akajikaza kisabuni. Alijua kuwa kijana huyo keishakufa hata alipopata taarifa ya ugeni wa dharula kutoka kwa mkewe hakudhania hata kama ni nani atakuwa amefika. Bahati mbaya sana kutokana na kikao cha siri na watu wake hakuweza hata kufungua kompyuta yake kuangali nini kinaendelea, labdal angeweza kuna yale aliyoyafanya na mkewe. Zulekha akamwendea na kumkumbatia kisha akambusu.

“Mgeni, nimekutana naye Ocean Breeze baada ya kupewa taarifa na mtu wetu, nimemkaribisha nyumbani kwa sababu najua utakuwa na aja ya kuzungumza naye kadiri ya lile alilokuja kufanya hapa Bagamoyo, anaitwa Mr. Spark,” Zulekha akatambulisha. Preji au Pancho akabaki kimya akaimwangalia mkewe na kisha Amata. Zulekha akageukia kwa Amata.

“Kutana na mume wangu mpenzi Mr. Premji Kanoon,” akamalizia. Pancho alikutana macho yake na yale ya Amata ambayo yalifichwa kwenye miwani ya rangi nyeusi, miwani iliyokuwa ikirekodi video matukio yote hayo ambayo yalikuwa yakitukia mbele yake.

“Karibu sana, jisikie nyumbani,” Pancho akamkaribisha Amata, pale alipotaka kupewa mkono alijifanya kutokuona akapita na kisha wengine wakafuatia nyuma yake. Kichwa cha Pancho kilianza kuchanganyikiwa kwa kumwona mtu huyo hatari kwa maisha yake akiwa hapo, hakuelewa kama Zulekha kamleta hapo kwa nia ya kuwa kamteka au ndiyo amelaghaiwa kwa mapenzi, lilikuwa swali lisilo na jibu. Baada ya milango miwili mitatu hivi akatokea kwenye sebule kubwa, akasimama kwa sekunde kadhaa kisha akawaambia watu wake.

“Naomba niacheni peke yangu kisha mniitie Zulekha nahitaji kupumzika kidogo,” Pancho akwaambia vijana wake na wale wageni, wakaondoka eneo lile.

  • * *

Chiba akatikisa kichwa huku akiendelea kutazama kompyuta yake, iikuwa ni kama vile yeye ndiye kakutana uso kwa uso na mtu huyo.

“Vipi?” Madam akauliza.

“Amewasili kisiwani, na alikuwa na watu wengine wawili ambao nawajua fika! Njoo mwenyewe ushuhudie,” Chiba akamjibu Madam S huku akiirudisha nyuma ile picha na kumwnesha bosi wake. Madam S akatazama zie sura na kusikitika.

“Watu wanauza nchi kila kukicha!” akasema.

“Ndiyo hivyo!”

“Wamekwisha…” akamalizi huku akitoka pale mezani. Akawaita vijana wake na kuanza kuwapanga jinsi ya kuvamia kisiswa hicho, maana walijua kuchelewa kwao kungeweza kumweka pabaya Kamanda Amata. Njia iliyohafikiwa na wote ni kupiga mbizi na kisha kuangusha mziki katika kisiwa hicho.

  • * *

Pancho alimtazama Zulekha kwa jicho kali, akameza mate ya hasira.

“Unamjua mgeni uliyemleta humu ndani ni nani?” akamuuliza.

“Ni mwandishi wa habari aliyevutiwa sana na hiki kisiwa hiki, ijapokuwa amekuja kwa kazi nyingine nikaona nimkaribishe kama fursa ya kujitangaza. Na ni wewe mwenye we uliniambia hayo,” Zulekha akajibu.

Kofi moja la kulia lilitua shavuni mwake akadondokea kitandani.

“Huna akili mwanamke! Huna akili kabisa, unaweza kuleta mashetani ndani ya nyumba hii, we hujiulizi kwa nini nyumba hii imejengwa chini ya ardhi?” Pancho akang’aka.

“Sasa mimi kosa langu nini?” Zulekha akaamka kitandani na kupiga kelele huku akiuliza, hasira zikamshika mishipa ikamtoka, “wewe mwenyewe ndiye uliyeniambia hayo leo hii unanigeuka? Nimepigiwa simu na Nassoro kijana wako mtiifu wa Ocean Breeze nikaenda na bahati nakutana na mtu huyu kwa nini nisimlete nyumbani ili aone kwa macho kila anachotaka, mara ngapi wewe umewaleta watu humu ndani na kunitambulisha kuwa ni watalii na wafanyabisahara? Hukuwahi kunambia kuwa hata mwili wangu niutumie kumkamata adui, sasa huyu nimekulea, awe adui au rafiki…”

“Naona unanipanda kichwani sasa, sivyo?” Pancho akachomoa bastola na kumwoneshea Zulekha.

“Nenda kwa huyo mgeni wako kamwulize yeye ni nani akwambie kisha uniletete jibu haraka!!!”

Zulekha akatoka chumbani na kumwacha mumewe akiwa kafura kwa hasira, alihisi kuchanganyikiwa kwani hakujua ni nini kinatokea, maana alilofanya ni lile ambalo mumewe ulitaka daima, lakini kwa nini amwadhibu kiasi hiki? Zulekha alihisi hasira kali sana dhidi ya mumewe, akapita kwenye korido ndefu na kuingia katika sebule kubwa ambako mwanzo aliketi na Amata, hakumkuta, isipokuwa kijana mmoja aliyekuwa akiangalia usalama wa eneo lile.

Kamanda Amata alikuwa kasimama mbele ya dirisha moja kubwa sana akitazama nje na shughuli mbalimbali zinazoendelea za wafanyakazi wa himaya hiyo.

“Mr. Spark!” akaita. Amata akageuka na kumwendea pale aliposimama, Zulekha hakusema lolote, akainua chupa ya whisky na kumimina kwenye bilauri iliyokuwa juu ya stuli na kumpa Amata kisha akainua nyingine na kujimiminia yeye, wakagonga chias na kila mmoja akapiga funda moja la nguvu. Lkitu ambacho alikigundua kwa mwanamke huyu ni kitu kama uvimbe katika shavu lake, akajua kwa vyovyote kuna jambo.

“Wewe ni nani?” Zulekha akauliza huku akionekana wazi sura yake kubadilika. Amata akapiga funda jingine na kumtazama mwanamke huyo wa Kihindi.

“Nimekwisha jitambulisha kwako ya kuwa mimi ni nani, bado unataka zaidi? Basi mwambie aliyekutuma akwambie mimi ni nani,” kisha akainyosha juu ile bilauri yake na kuinywa mfululizo, alipoitu kwenye stuli ilikuwa haina kitu. Akamtazama tena Zulekha pasi na kupapasa macho

“Naitwa, Amata, Kamanda Amata, Tanzania Secret Agency nambari moja; una lingine?” akamweleza mara tu baada ya kuiweka bilauri yake mezani. Na ni nukta hiyohiyo, alipojikuta amezungukwa na vijana wenye silaha kile upande. Aligeuka huku na huku na kukutana na sura zilizokunjamana kwa uchu wa kuua, Short Gun zilizosheheni risasi, zenye hamu ya kufyatuka.

“Mikono juu tafadhali,” akaamriwa na ye akatii.

Kijana mwingine akampekua na kutoa bastola mbili ndogo mifukoni mwake, visu vidogo vitatu na vitambulisho vingine vingine ikiwamo kadi za benki na kadhalika.

“Unaniambi wewe ni mwandishi wa habari kumbe ni mpelelezi?” Zulekha akamwuliza kisha akamnasa kofi na kusogea pembeni. Amata alivumilia maumivu huku akimtazama Zulekha kwa jicho baya sana.

Utalipa tu! Akajisemea moyoni. Pancho Panchilio akaingia sebuleni pale na kumkuta Amata akiwa chini ya ulinzi mkali.

“Hah! Hah! Hah! Hah! Amataaaa, Kamanda Amata, leo umejileta mwenyewe kwenye nyumba ya shetani. Uroho wako wa mapenzi ya wanawake umekukamatisha, huna maana kabisa, nashindwa kujua kwa nini serikali ikakuamini hata kukupa hicho cheo wakati wewe ni mpumbavu kati ya wapumbavu wa nchi hii! Karibu sana Kalebbe, maana ulitaka kuja kupaona kama nilivyoelezwa na mke wangu Zulekha basi ngoja nikutembeze kidogo ili ufahamu mahali hapa,”

Pancho alimchukua Amata na kumtembeza katika jumba hilo huku vijana wake wakilinda msafara huo kwa bunduki nzito kila kona ya jengo. Kila kitengo alimwonesha bila kumficha na kumwelezea lakini hakumruhusu kuuliza swali, kil kitengo alikuta vijana wakifanya kazi kwa mori wa ajabu, wengi hawakuwa Waafrika, bali Wahindi na Waarabu, weusi walikuwa kwenye ulinzi tu. Katika chumba cha rada aliweza kuona kwa picha jinsi ndege yao ilivyolipuliwa.

“Aaaaa hah! hah! hah! Umeona, ninaweza kulipua ndege yoyote inayopita hapa, siogopi!” akajitapa kisha akaamuru watoke waende chumba cha mwisho. Baada ya kuzunguka ndani ya jengo lote hilo wakasimama mbele ya mlango mmoja wa chuma. Pancho akamtazama kijana huyu na kufungua kinywa chake kusema.

“Kamanda Amata, na sasa nataka nikuoneshe kitengo hiki ambacho kila anayeingia lazima achnganyikiwe ka teknolojia iliyofungwa ndani yake,” aliposema hayo akabofya kitufe fulani na lile lango likafunguka. Kilikuwa chumba tupu, hakukuwa na chochote ndani yake. Pancho akaingia.

“Karibu ushuhudie kilichomo, usiogope,” akamwambia. Kengele za hatari zikalia kichwani mwa Amata, akaingia ndani ya kile chumba kipweke, nyuma yake wakaingia vijana wawili walioshiba kimazoezi na wale wenye silaha wakabaki mlangoni. Kwenye maeneo kama haya huwa Amata hana subira zaidi ya kupigania uhai wake tu japo kwa sekunde ya mwisho. Alivuta hatua mbili mbele na kugeuka ghafla, akamchapa konde moja mmoja wa wale jamaa waliongia nyuma yake. Yule jamaa akayumba kidogo kwa kuwa hakutegemea dhopruba kama ile. Yule wa pili akaudaka mkono wa Amata lakini kabla hajafanya lolote, alipigwa kichwa kizito na kwenda chini. Kamanda Amata akaruka hewani na kutawanya miguu yake, akawachapa mateke makali kila mmoja akaenda chini bila kipingamizi. Wale wenye silaha wakashindwa wafanyeje, maana walijua kufyatua risasi kungeweza kujeruhi watu wao.

Alipotua chini Amata akaruka sarakasi ya chini kwa chini na guu lake likatua katika koromeo la mmoja wao, akaguna kwa uchungu. Alipojigeuza alijikuta anatazamana na mtutu wa Short Gun, akajizungusha na kumtia ngwala aliyeshika hiyo bunduki, akaenda chini huku bunduki ile ikimtoka mikononi, akaiwahi na kuikamata, bila huruma aliwatwanga wote wanne kwa kirasi na kuwaacha marehemu. Si mlangoni wala ndani ya kile chumba, hakukuwa na mtu.

Uko wapi mwanaharamu? akajiuliza na kuchungulia kupitia ule mlango, nakasikia watu wanaoongea wakija upande huo, akarudi ndani na kujificha nyuma ya mlango akisubiri huku mkononi mwake akiwa kaikamatia ile bunduki aliyoichukua kwa yule jamaa.

“Ni hapa jamani, ingieni kwa makini,” sauti moja ikasema. Wale waliokuja kama ni kuokoa jahazi walishuhudia damu na miili isiyo na uhai. Amata akaendelea kutulia palepale, wale jamaa wakamwingiza mmoja kama chambo, akaangaza angaza huku na huko akiziangalia maiti za wale jamaa watatu pale chini.

“Huyu jamaa hayupo bwana,” akawaambia wenzake.

“Basi msako uanze atakuwa humuhumu ndani, kumbuka hawezi kutoroka hapa ni kisiwani,” mwingine akahimiza huku wakitoka mle ndani na kupotelea huku na huko. Amata akatoka taratibu na kufuata korido moja kwa moja mpaka kwenye ile njia panda waliyopita na Zulekha wakati wakiingia kwenye jumba hilo. Akakunja kushoto na kuufikia mlango imara wa chuma, akajaribu kuufungua kwa kutumia zile namba alizozikariri pindi alipomwona Zulekha akifungua zikakubali lakini akadaiwa alama za vidole, akashindwa. Akatafakari cha kufanya akakosa jibu. Alipokuwa akijiandaa kubadilisha mbinu akasikia michakacho ya miguu ya mtu anayetembea haraka haraka huku akiongea.

“Kawaua wote, wote watatu, huyu jamaa hafai, inabidi auawawe,” yule mtu alionekana anaongea na kitu kama simu ya upepo. Amata akamvizia, alipotokezea tu eneo lile, akaruka na kutua shingoni mwake, akamkaba kabali namba sita.

“Tulia,” akamwambia. Ile redio pale chini ikawa inaendelea kuita,

“Jota! Jota! Umepatwa na nini?” sauti ya upande wa pii ikauliza. Kamanda Amata akaitazama ile redio na kuivuta kwa mguu wake.

“Fungua mlango!” akamwambia yule jamaa ambaye sasa alimfahamu kwa jina la Jota.

“Mi sijui, “ akajibu kwa shida kutokana na ile kabali aliyopigwa na Amata, akamwachia na kumsukumizia mlangoni.

“Fungua,” Amata alimwambia huku bunduki ikimtazama mtu huyo, akapapasa namba hii na ile na kuweka alama zake za vidole kisha macho, mlango ukafunguka. Kamanda Amata akamrukia teke la kusukuma yule jamaa akaangukia ndani, kisha yeye akafuata na kufyatua risasi zilizowaangusha watu wawili waliojitokeza na kumwacha mmoja tena wa kike akiwa kasimama.

“Kamanda Amata,” Zulekha akaita, “umeniharibia ndoa yangu,” akaongeza kusema.

“Nioneshe mumeo, serikali inamtafuta kwa udi na uvumba,” Amata akamwambia.

“Wewe ni mbaya sana sivyo nilivyofikiria,” Zulekha akaongea huku chozi likimtoka.

“Nilitaka nifike hapa, na nakushukuru kwa kunifikisha na sasa ninavyokwambia namhitaji mumeo, Pancho Panchilio na sio Premji Kanoon kama unavyomjua, gaidi anayehatarisha maisha ya nchi na wananchi, ametoroka mikono ya serikali kibabe, sasa siku zake zimekwisha. Nioneshe alipo kabla na wewe sijakumaliza,” Amata aliongea huku akiwa kakunja sura kwa hasira.

“Sasa mbona unakunja sura namna hiyo, kijana mzuri hatakiwi kujizeesha mwili wake,” Zulekha alisema hayo huku akimfuata taratibu.

“Tulia hivyohivyo kabla sijakuua kwa bastola yako mwenyewe,” sauti ikasikika kutoka nyuma yake. Kutokea katika dirisha kubwa lililokuwa mbele yake aliweza kuona taswira ya mtu yule vizuri sana. Amata hakuwa na muda wa kupoteza katika eneo hilo ambalo lingeyagharimu maisha yake muda wowote. Aligeuka na kumtandika yule jamaa kwa kitako cha bunduki, akaaangukia juu ya meza huku bastola ikimtoka mikononi, Amata akachumpa kwa ustadi na kuinyakuwa huku mkono mwingine akiwa tayari na saa yake ya mkono ambayo bwana huyo aliichukua pamoja na bastola. Yule bwana akaamka na kusimama wima huku mbele akimtazama Amata aliyekuwa akiibonya ile saa hapa na pale.

“Mnaweza kuja sasa, kazi imeanza,” akaongea huku akiitazama ile saa kisha akaivaa mkononi mwake. Yule mjinga akatumia muda huohuo, akaruka tik tak kwa minajiri kumpiga mikono na kidevu cha Amata lakini akakuta anapiga hewa kwani mwenzake alikwishaondoka eneo hilo na kutua upande mwingine mpaka kwa Zulekha aliyekuwa amebaki kaduwaa. Yule bwana alipotua na kukuta Amata hayupo, akajivuta kasi kumwendea, akaruka hewani akiitanguliza miguu yake mbele. Amata akaepa na kumpa pigo moja la karate mbavuni na kuvunja ubavu mmoja, akajibwaga chini kama mzigo, alipojaribu kusimama alikutana na teke lingine katika ubavu wake wa pili, akaanguka chali na guu la Amata likatua kifuani mwake kwa kishindo.

“Aaaaaaiiiggghhh!!!” Yule jamaa akapiga yowe la maumivu huku akijaribu kwa nguvu zote kuuondoa mguu ule lakini alishindwa.

“Boss wako yuko wapi?” akamuuliza.

Akiwa katika kumuuliza akahisi kitu kizito kikikifikia kisogo chake, akageuka haraka na kutua upande wa pili wa yule mtu huku tayari mkononi bastola yake imetulia, alipocheza na kifyatulio, kijana mmoja aliyekuwa na chuma kizito mikononi mwake alijibwaga chini na kuwa marehemu. Amata akajishika kisogoni na kujifuta damu kutoka kwenye jeraha lililofanywa na pigo lile. Ilionekana mpigaji hakuwa mzoefu kwani angempata sawasawa basi lazima angepoteza fahamu lakini haikuwa hivyo. Amata akatazama alipkuwapo Zulekha katika ile sebule, hayupo, akatazama hapa na pale hasimwone.

Shit! Kaenda wapi huyu mwanamke? akajiuliza bila kupata jibu, akamgeukia tena yule jamaa.

“Hah !hah! hah! hah! Umecheza pata potea, leo nakumaliza kwa risasi yangu,” yule bwana akajigamba na kunyanyuka kwa taabu kutoka pale alipolala, wakati huo Amata bastola yeke ikiwa chini sakafuni, akaikanyaga kwa ncha ya mguu wake na kuibetua, ile bastola ikaruka hewani na Amata akaidaka kwa kono lake la kulia, sekunde hiyohiyo kifua cha yule jamaa kilitobolewa mara mbili na risasi za Amata, akarudi chini kwa kishindo.

“Buriani!” akamwambia.

Kamanda Amata akasikia sauti ya chopa, akatoka ndani ya chumba kile na kutafuta njia ya kutokea nje, ngumu. Alipofanikiwa kutoka ndani ya chumba kile akajikuta kwenye zile korido, huku na kule ving’ora vya hatari vilikuwa vikilia, kimenuka. Akakimbilia upande wa kushoto na kukutana na vijana waliovalia kijeshi na kujining’inizia silaha nzito, kabla hawajakaa sawa, akawafumua kwa risasi na kuwabwaga, akachukua shotgun walizokuwa nazo, akanyofoa na maguruneti mawili waliyokuwa nayo, akaendelea na safari. Moja ya milango mingi aliyoikuta hapo ni ule aliyokuwa anautaka. Akabonya kikengele na ule mlango ukafunguka, ndani yake kulikuwa na vijana wanne waliokuwa wamekaa kwenye luninga nne tofauti wakiongoza mitambo yote ya jengo hilo kuanzia rada, kamera za usalama na silaha zilizofungwa ardhini.

“Mtulie hivyo hivyo! Bosi wenu yuko wapi?” akawauliza huku akiondoa pini kwenye moja ya bomu la mkono (guruneti) alilokuwa nalo mkononi, wale jamaa wakatazamana na kukosa jibu.

“Najua ninyi mnafahamu, haya, mmoja baada ya mwingine, mniambie bosi wenu yuko wapi ama la, nateketeza chumba kizima na kwangu si hasara,” akawaambia tena huku akiwa amelishika lile bomu kwa mkono wake.

“Boss yupo na sasa anaondoka,” mmoja akajibu kwa kitetemeshi.

“Nioneshe alipo,” akamwambia na yule kijana akazungusha kitu fulani na kwenye luninga ya mbele yake kukaonekana helkopta iliyokwisha washa injini tayari kuondoka, rubani na watu wengine wawili walikuwa tayari ndani yake huku nje kukionekana watu kama watano wenye silaha wakiwa wameweka ulinzi.

“Umeshamkosa boss, anaondoka na mkewe,” kijana mwingine akaongea kwa nyodo wakati alipoona taa ya kuomba kufunguliwa mlango huo wa nje ikiwaka, akabonyeza kinobu cha kijani na kule nje ule mlango ukafunguka. Amata aliinua bunduki na kumfumua risasi ya mgongo.

“Aaaaaiiiiihhhhh umeniua mshenzi wewe,” yule bwana alilalama huku damu zikimvuja.

“Kufa tu, kwani we ulivyotaka kuniua kwenye ndege majuzi ulifikiri sikuoni,” akaiendea moja ya swichi kubwa iliyokuwa mezani hapo ambayo ambayo ilifanana na mkono wa gia ya gari, akabonyeza kitufe cha pembeni yake na runinga kubwa ikawaka mbele yake.

“Unataka kufanya nini wewe!” mmoja nakapiga kelele.

“Tulia mseng* wewe!” akamtuliza huku akimwonesha bastola. Kwenye kile kioo akaiona ile helkopta inayomsubiri Pancho na yeye na mke wake wakielekea kupanda tayari kuondoka.

“Hah! Hah! Hah! Hah! Haondoki mtu hapaaaaa!” akasema kwa sauti na kuitembeza ile ‘gia’ mpaka alipohakikisha ameiweka sawa ile helikopta.

Mlipuko mkubwa ukatokea, ile helkopta ikalipuka na kuteketea kabisa ikamwacha Pancho na akiwa hana ujanja, akarudishwa ndani na walinzi wake.

Kamanda Amata akabaki anashangaa kwani yeye bado alikuwa hajafanya ulipuzi ule.

  • * *

Chiba na Gina waliibuka katika kichaka cha mikoko, kila mmoja akiwa na silaha yenye akili. Chiba akamwonesha Gina ishara ya kuwa afungue mlango, Gina akaweka begani bunduki kubwa na kuufumua mlango wa chuma uliokuwa hapo, kisha wakaelea huko huku wakimwaga risasi kila upande anapoonekana adui. Wakaingia ndani na kuanza kupita kila korido na mlango wakiwapa kipigo adui zao huku wakishinikiza wapi Pancho atapatikana. Kelele za vilio na mirindimo ya risasi viligubika mle ndani vikisindikizwa na moshi wa baruti. Gina akashusha barakoa yake na kuuficha uso wake dhidi ya moshi huo uliokuwa ukimuumiza macho, na Chiba akafanya vivyo hivyo.

“Tumsake mwanaharamu,” Chiba akamwambia Gina, wakaanza kubomoa mlango mmoja baada ya mwingine wakipekua ndani kote wasimwone.

  • * *

Kamanda Amata alipotaka kuondoka ndani ya kile chumba aliona taa fulani ikiwaka kama ile ya kwanza, akaiendea na kutazama iliandikwa ‘Escape Chamber’ akajua kwa vyovyote Pancho yupo upande huo.

“Control room, Control room!” moja ya redio ndani ya chumba hicho iliita, Amata akainyakua.

“Control Room is under attack,” akajibu na kuhisi kigugumizi upande wa pili.

“We ni nani unayeongea?” ile sauti ikamuuliza.

“Mimi ni Kamanda Amata, TSA namba 1, na sasa niko njiani kuja hukohuko uliko,” akajibu na kuiweka mezani ile redio kisha akaliachia lile bomu na yeye kutoka kasi. Kilichotokea nyuma yake ni mlipuko ambao uliharibu mitambo yote ya lile jengo. Amata alitupwa mbali na kuanguka vibaya kutokana na nguvu ya ule mlipuko, akajiinua lakini mara hii alianza kusikia maumivu makali katika sehemu yake ya ubavu.

Akanyanyuka kwa taabu na kutembea huku akijitegemeza ukutani kwa mkono mmoja na mwingine akijishika ubavuni kwenye jeraha lake.

“Kamanda!” akasikia akiitwa nyuma yake alipogeuka akakutana na mtu aliyevaa barakoa usoni mwake lakini kwa mwendo tu alimgundua kuwa ni Gina.

“Gina!”

“Yap! Pole sana Kamanda, nikuondoe eneo hili,”

“No! no! itafute escape chamber ndipo alipo mtu wetu,” Kamanda akamwambia Gina, naye akainua walkie talkie yake akaongea na Chiba na kumpa ujumbe huo huku akimpa taarifa Scoba na Jasmine kuingia kazini. Haikupita muda waliungana na Chiba na kuufikia mlango huo, mlango wa chuma uliofungwa ukafungika.

“Watakuwepo hadi sasa? Maana hii ni ‘escape’” Chiba akaeleza.

“Nimeharibu system nahisi watakuwa humo ndani kwani kwa sasa hakuna mlango unaoweza kufunguka kirahisi,” Amata akawaeleza.

Gina akainua tena ule mbunduki na kuuweka begani, bonyezo moja tu, ule mlango ulifumuka vibaya, na Chiba akajitosa ndani muda huohuo, Gina akafuatia na Amata akawa wa mwisho, saka nikusake. Kilikuwa chumba kikubwa ambacho ndani yake kulikuwa na boti iendayo kasi, Amata alipoitazama akajua wazi kuwa ile boti kwa muundo wake ina uwezo wa kupita chini ya maji.

“Wapo humuhumu,” akawaeleza wenzake.

“Vaeni barakoa zenu!” Kamanda akawaambia na wote wakavaa.

“Gina,” akaita na kumpa ishara. Gina akainua bunduki moja fupi na kufyatua kitu kama bomu kilichotoa moshi mkali sana kisha wakaendelea kutazama hapa na pale. Haikupita muda wakasikia mtu akikohoa. Gina akawahi na kufungua mlango mdogo uliokuwa mahala hapo.

“Toka mwenyewe!” alimwambia Zulekha aliyekuwa kajificha hapo, “na mumeo yuko wapi?” akauliza.

“Ushasema mume wangu we wa nini?” akajibu huku akikohoa sana. Gina akageuza ile bunduki na kumpiga nayo shavuni, ikampeleka chini Zulekha, akamshika mguu na kumburuza mpaka karibu na mlango, Amata akamkanyaga mgongoni.

“Tulia mrembo, tulia hivyohivyo,” Amata akamwambia Zulekha.

  • * *

Helkopta kubwa lenye magurudumu lilikanyaga ardhi ya kisiwa cha kalebbe, wa kwanza kuteremka alikuwa Madam S, akafuatiwa na Jasmine kila mmoja alikuwa na bastola kiunoni mwake. Dakika hiyohiyo, helkopta nyingine ya polisi nayo ikafika eneo hilo a kuteremsha vijana kama kumi hivi waliotimia, kikosi maalumu cha kupambana na ujambazi chini ya Kamanda Tossi. Wakazunguka eneo kwa uhodari kabisa wakihakikisha kila anayepatikana anawekwa chini ya ulinzi na kufungwa pingu.

Madam S na Jasmine waliingia ndani huku vijana wachache wa polisi wakiwasindikiza nyuma na mbele. Nje ikafika boti iendayo kasi ‘KINYAMKERA’ ikAteremsha vijana wengine wenye silaha wakifuatana na Inpekta Simbeye, idara imekamilika. Wale vijana wakaingia ndani na wengine wakabaki nje kama kawaida. Kwa mawasiliano yao waliweza kujua Gina, Chiba na Amata wako upande gani, wakaenda huko.

  • * *

Kamanda Amata aliliangalia moja ya kabati kubwa katika chumba walichoingia mara hii, kabati hilo lilimtia wasiwasi kwa jisi lilivyokaa na mahala liliPowekwa, akaliendea na kulipapasa huku na kule, akashika kitasa na kujaribu kukivuta, hakuna mlango uliofunguka.

“We mwanamke eleza mumeo alipo kabla sijatumia nguvu,” akamwambia Zulekha.

Zulekha hakujibu isipokuwa mikono yake ilikuwa kinywani mwake kama mtu anayeshangaa jambo. Kwa hali hiyo Amata alijua wazi kuwa amtafutaye yupo eneo hilo. Juu ya kitasa kile kulikua na kitu kama jiwe la yaspi ili kuongeza nakshi ya kabati hilo, akaliminya lile jiwe na kabati zima likasogea kando, ndani yake kulikuwa na uwazi ambao bila kificho Pancho alionekana ndani yake. Kutoka ndani mle, akatoka kwa kasi kwa minajiri ya kumvamia Amata lakini kabla hajamfikia, alikutana na konde zito lililomfanya ateme damu, la pili lilitua shavuni na kuacha meno kadhaa sakafuni la tatu lilimpeleka chini mzima mzima.

“Mwanaharamu mkubwa wewe, leo nimekutia mkononi kwa mara ya mwisho,” Amata aliunguruma huku bado akijishika ubavu wake.

“Simama,” akamwamuru lakini Pancho hakufanya hivyo. Akasahau maumivu yake na kumnyanyua kisha akamsimamisha mbele yake na kumkwida shati, akampiga kichwa kimoja kizito mpaka Pancho akaona nyota za ajabu zikimzunguka.

“Wewe unaweza kutusumbua sisi?” akamwuliza.

“Mwacheee!” Zulekha akajirusha kumvamia Amata huku mkononi akiwa na kisu, hakuna aliyejua wapi kakipata kisu hicho lakini hata hivyo hakuna aliyekumbuka kumpekuwa pindi walipomkamata. Gina kwa wepesi wa ajabu, aliinua bastola lake na kumfumua Zulekha kabla hajaufikia mwili wa Amata na kumbwaga chini akiwa hana uhai.

“Kwaheri Malkia wa Kalebbe!” akasema kwa sauti ya chini huku akishusha mikono wenye bastola chini. Pancho akapagawa kwa kitendo hicho, akajitoa kwa Amata na kumfuata Gina.

“Umemuua mke wangu!” akapiga kelele.

“Na wewe nakuua,” Gina aliongea. Amata alipoitazama sura ya Gina aliona wazi hakuna mswalie Mtume, alijirusha na kumpiga teke la mbavu Pancho akajibwaga upande wa pili na risasi ya Gina akapita peupe na kukiteremsha kioo kikubwa kikubwa ambacho kiliyaruhusu maji ya bahari kuingia ndani, mshike mshike. Wakamnyanyua Pancho na kutoka naye ndani ya chumba kile wakikimbia.

Mvumo wa maji ulisikika dhahiri shahiri yakianza kujaa upande wa chini wa jingo hilo, Amata akiwa na Gina na Pancho aliyeshikwa huku na huku walijitahidi kupanda ngazi kwa haraka kuelekea upande wa juu. Kengele za kuashiri hatari zilisikika kila kona na kila aliye ndani ya jengo hilo alijitahidi kuwahi kutoka.

Madam S na Jasmine walikuwa wa kwanza kufika nje huku wakijaribu kuwasiliana na Amata na wengine. Haikupita muda, waliwaona wakitokea katika kile kibanda kidogo. Madam S akawahi na kumkamata Pancho huku vijana wa polisi wakimtia pingu tayari kwa safari.

“Umekamatika mwanaharamu!” Madam S alimwambia mbaya wake wakati akifungwa pingu.

“Peleka kwenye helkopta!” Madam akatoa amri.

“Hapana Madam! Hilo si wazo zuri,” Amata akajibu.

“Fanya uwezavyo Kamanda, hakikisha tunakutana karakana!” Madam akamwambia huku yeye na wengine wakielekea kwenye ile helikopta.

Pancho akaingizwa kwenye ile boti, akifuatana na Amata na Chiba wakaondoka na mtu wao kuelekea Dar es salaam. Boti ile iendayo kasi ilikuwa ikipita chini ya maji na haikuchukua muda kuwasili katika ofisi yao iliyo ndani ya meli mbovu maeneo ya Kurasini. Wakamshusha na kumuingiza ndani ya meli hiyo.

Pancho aliketishwa kwenye stuli ya chuma, huku Chiba na Amata wakisimama pembeni.

“Mtawafunga wengine lakini si mimi,” pancho aliwaambia vijana hao.

“hatutaki ngonjera zako, fala wewe!” Chiba akamuwahi

“Aliyekwambi sisi tunakufunga nani? Leo hii tunakuua,” Amata akajibu huku mkono wake bado ukiwa ubavuni mwake.

“Ha! Ha! Ha! Nani aliyekwambia mtu hufa kijinga hivyo?” Pancho akaongeza swali la kuuzi.

“Kama alivyokufa mkeo Zulekha kwa mkono wa mwanamke, na wewe utakufa hivyohivyo kwa mkono wa mwanamke,” Chiba akamwambia.

Mara mlango wa chumba hicho ukafunguliwa na Madam S akaingia pamoja na Inspekta Simbeye wakifuatana na Gina, Jasmine na Scoba. Madam S akamtazama Muhindi huyo kwa hasira.

“Chagua kifo chako haraka!” akamwambia.

“We Kibibi, kukukosa kule Kerege usikiri nimekusamehe, ninyi ni waharibifu wa mipango ya watu, nitakuua ndani ya dakika hii,” Pancho aliongea na sekunde hiyohiyo alijinyanyua kwa kasi na kuchomoa bastola ya Simbeye kwa kutumia mikono yake iliyofungwa pingu, akimpiga kikumbo cha maana inspekta huyo na kumwacha akienda kujibamiza mezani. Kabla watu hawajakaa vizuri alikwishamgeukia Madam S na kumnyooshea bastola hiyo.

Kamanda Amata na Chiba walijikuta wakipigwa butwaa kwa tukio hilo, wakiwa katika kujiandaa nini wafanye wakasikia bastola ikilalama.

“Pah! Pah! Pah!” kila mtu ndani ya chumba kile aliziba masikio na kuinama chini. Pancho alijikuta akitazamana na bastola ya Gina, alisukumwa na kujibamiza ukutani kisha alijibwaga ardhini huku kichwa na kifua chake vikiwa vimetobolewa vibaya kwa risasi.

Gina alaiteremsha mkono wenye bastola taratibu na kuurudisha mahala pake huku akitoa sonyo refu.

“Hakuna madhara, TSA 5 katekeleza wajibu wake wa leo,” Gina aliongea na ndipo watu walipotazama na kumwona msichana huyo akiwa anapumua kwa nguvu.

“Asante Gina, leo umefanya kazi yako hasa,” Madam S akamkumbatia Gina kisha wakatoka kuelekea mahala pengine.

  • * *

Baada ya siku nne…

AFISI NDOGO

“Kazi iliyotuumiza kichwa imekamilika, kila mmoja wenu kafanya vizuri kwa upande wake, natoa pole kwa Amata kwa majeraha aliyopata lakini ndiyo kazi yetu,” Madam S aliongea akiwa kasimama wima mbele ya meza yake ambayo nyuma yake kulikuwa na bendera ya Taifa na ile beji kubwa ya TSA ukutani. Upande wa pili kulikuwa na vijana watano, wa kike wawili na wa kiume watatu, waliosimama kwa ukakamavu huku kila mmoja akiwa na beji yake ya kazi katika mkanda wake.

“Pongezi nyingi kutoka Baraza la Usalama la Taifa, Mheshimiwa Rais anawapa pongezi kwa kzi nzito ya kuhakikisha mtandao huu unapotezwa,” akawaambia.

“Mtakwenda likizo wawili wawili kwa muda wa wiki mbili kila mmoja. Wataanza Gina na Amata kisha Jasmin na Chiba, Scoba na mimi tutakuwa wa mwisho kwa sababu maalum. Lakini kumbukeni hii ni likizo kazini, muda wowote nikiwahitaji mtafika hapa”.

Gina akamtazama Amata na kutoa tabasamu. Baada ya Madam S kumaliza kauli yake, wakaketi na kupata vinywaji huku wakibadilishana mawazo ya hapa na pale juu ya kazi yao na kila mmoja akijaza fomu za likizo

.

HOTELI YA RED STAR

“Mmmmmm Kamanda Amata, you are so sweet!” Gina alilalama huku akimpapasa Amata kifuani.

“Nashukuru kwa kuniokoa,”

“Ndiyo kazi yangu kukulinda mpenzi, nisipokulinda mimi nani atafanya hilo?” Gina akaongea kwa sauti ya kivivu, “unazeeka Amata hata mtoto huna,” akaongeza.

“We unaye?”

“Mi umri bado!”

“Unataka kunizalia mmoja?”

“Sio mmoja tu, hata ishirini…” Gina akajibu.

“Ooooh Gina,” Kamanda akajiinua na kuitazama saa yake, ilikuwa saa nne asubuhi.

“Unaenda wapi?”

“Twende tukaoge,”

“Oh, no! bado Kamanda mi nataka tena,”

“Mmmmh beibi,”

“Mmmm nini, nipe cha asubuhi bwana,”

Kamanda akarudi kitandani na kuanza kumbusu Gina kimahaba huku wote wakiwa hivyohivyo bila nguo, mchezo ukaanza upya kama si kuendelea.

Mara simu ya mkononi ya Amata ikaanza kuita kwa fujo, mlio huo haukumpa tabu kujua ni nani anayepiga. Akaitazama kwenye kioo na kuona kuwa hakukosea. ‘Madam S’ iliandika.

MWISHO

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment