Kitisho Sehemu ya Tano
KIJASUSI

Ep 05: Kitisho

Kitisho Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE


Simulizi : Kitisho

Sehemu ya Tano (5)

HALI YA GINA ILIRUDI NA KUWA NZURI, ijapokuwa bado alikuwa wodini lakini huduma aliyoipata kutoka kwa Dr. Khadrai na jopo lake ilimfanya aweze hata kuongea. Kichwa kilimzunguka alipojaribu kufikiri ni wapi wenzake wote watakuwepo.

“Khadrai, hivi hauna dawa ya kuniondolea maumivu kabisa niingie kazini?” akauliza. Khadrai akabaki kucheka tu.

“Gina, naona akili yako haiku sawa, endelea kulala, hali yako ni mbaya sana usifanye lolote la mikikimikiki,” akajibiwa.

“Moyo unaniuma sana kuona siwezi kufanya lolote,” akamwambia Khadrai.

“We Gina tulia hapa, hakuna baya litalotokea kama unavyowaza,” Khadrai akampa matumaini. Alipotaka kuondoka, Gina akamzuia, “Khadrai, naomba mkoba wangu,” akamwambia na Khadrai akampa, Gina akapekua ndani na kutoa bastola moja aina ya Beretta, akaikagua ipo sawa akaitia ndani ya shuka mkono wa ke wa kulia.

“Ya nini Gina?” Khadrai akuliza.

“We nenda! Nenda!” akamwambia huku akimpa ishara ya mkono.

Kgadrai akatoka ndani ya kile chumba na mara akakutana na watu wawili waliosimama mbela yake, wakamwonesha vitambulisho, maafisa wa polisi.

“Tunahitaji kumwona WP Gina kikazi,” wakamwambia huku wakipita kuelekea ndani ya kile chumba. Wakafungua mlango na kukuta Gina amelala kimya, drip mkono ni mwake na mipira ya oksijeni puani mwake. Khadrai akapigwa na butwaa maana hakumwacha Gina na oksijeni isipokuwa drip tu.

“Gina, Gina!” akaita mmoja wao. Gina akabaki kimya kabisa kama hasikii ilhali alikuwa akisikia kila jambo, mkono wake wa kulia tayari ulikamata bastola iliyokuwa haina usalama na risasi moja ilikuwa tayari ndani ya chumba cha shughuli.

Baada ya kuona kimya cha Gina wakatazamana na kupeana ishara kwa kubaniana macho, mmoja wao akaurudisha mlango na Yule mwingine akaenda na kuondoa ule mpira wa oksijeni. Gina kama umeme, alichomoa bastola yake kwenye shuka na kuanza na Yule aliyekuwa akifunga mlango, alimlenga shabaha na kufumua bega lake kisha akajibiringisha na kudondokea upande wa pili wa kitanda akiicha sindano ya drip ikichomoka yenyewe. Kutoka uvunguni alimchapa risasi Yule mwingine na kuvunja mifupa ya ugoko, alipodondoka akammalizi risasi ya moyoni. Kisha akasimama na kumtazama Yule aliyekuwa akifunga mlango wakati huo akimwagika damu begani hana la kufanya.

Gina alizunguka kitanda na kusimama kando ya marehemu Yule na kumtazama huyo aliyemjeruhi.

“Nimekujeruhi makusudi fala we!” akamwambia kwa hasira, akafyatua risasi nyingine na kupiga bega la pili, “Niambie, watu wangu wako wapi?” akamwuliza.

Yule jamaa alibaki analia tu, “Umentia kilema cha maisha weweee!”

“Nini kilema nakuua kama usiposema,” akamwambia.

“Utanionea tu huyu uliyemuua ndiye anajua kila kitu,” akajibu huku akibuujikwa damu.

“Jeuri siyo?” Gina akamuliza na kumkanyaga kwa nguvu bega lake.

“Aaaaaaiiigghhh! Nasema, nasema, nasema!”

“Sema!”

“Wapo Kerege, Bagamoyo,” akajibu.

“Na wewe bosi wako nani?”

“Mtu mkubwa, mkubwa serikalini,” akajibu.

“Nani mtaje kwa jina!” Gina akang’aka.

“Kigogo, Ki-go-go,” akaongea kwa taabu. Gina akaelewa anachokifanya akamwahi na kumtandika ngumi ya shavu, Yule jamaa akatema kidonge cha manjano, kidoge cha sumu kali ambacho huficha kinywani wanapozidiwa kwa maswali huwa ni bora kujiuwa kuliko kutoa siri.

“Shenzi sana wewe, ulifikiri utaniwahi? Sasa utaenda kueleza yote kwa wanaojua cha kukufanya,” Gina alilalama, kisha akachukua simu ya Khadrai nakubofya namba Fulani Fulani.

“Ndiyo Inspekta Simbeye (…), Agha Khan hapa hospitali haraka,” akatoa ujumbe upate wa pili na kumwacha Yule jamaa akipewa huduma ya kwanza ili kuzuia damu zisiendelee kumtoka. Gina aliiweka vizuri bastola yake na kuirudisha kwenye pochi yake. Khadrai alikuwa hana amani kabisa, akamtazama Gina bila kumuuliza chochote, Gina akaweka vizuri kilichochake.

“Vipi Gina?” Khadrai akatupa swali.

“Hapa hakuna usalama, najua wapi nitakwenda, asante kwa msaada wako.”

“Lakini Gina hali yako bado mama,” Khadrai akamwambia.

“Najua, lakini kwa hali ilivyo ni hatari,” Gina akajibu huku akitembea kwa kuchechemea kidogo kutokana na lile jeraha lake.

Dakika kumi na tano baadae, Inspekta Simbeye akaingia katika ile hospitali akifuatana na vijana wake mahiri kabisa waliobeba silaha za kutosha, wakateremka na kupanda mpaka ghorofa ya tatu.

Baada ya kukamilisha mambo yao ya kiusalama waliondoka na ule mwili pamoja na Yule majeruhi kwa mahojiano zaidi.

“Gina, pole sana, unajisikiaje lakini?” Simbeye alimuuliza Gina.

“Maumivu makali sana, lakini hapa siwezi kulala, pia sina amani kwa kuwa sijui watu wangu wako wapi,” Gina akajibu huku amejilaza katika kitanda cha kitabibu.

“Pole, sasa itabidi upelekwe Lugalo mahali ambapo pana usalama zaidi,”

Wakakubaliana hilo na utaratibu wa kila kitu ukafanyika. Ijapokuwa Gina alikubali kwa shingo upande kwa kuwa yeye alipenda kuingia msambweni kuwasaka wenzi wake.

Inspekta Simbeye, aliyekuwa akilitumikia jeshi la Polisi kwa kofia mbili, moja kama Inspekta wa Polisi lakini ya pili ni ile ya Ukachero wa serikali, Usalama wa Taifa, aliwekwa pale kwa mpango maalumu wa kuchunguza maafisa wa Jeshi hilo kama kuna lolote baya wanalolifanya juu ya nchi hii.

Kerege – bagamoyo

WAJUMBE WA KIKAO KILE CHA DHARULA walipiga makofi baada ya kupewa taarifa kuwa watu wao wote wamepatikana isipokuwa mmoja ambaye wao kama wao hawakuona kama anaweza kuwa na dhara lolote.

“Kazi imekwisha!” Pancho aliwaambia wenzi wake.

“Vijana wamefanya kazi ngumu na nzuri wanastahili pongezi,” mwingine aliongezea.

Baada ya furaha yao hiyo kukamilika na kugongeana bilauri kama ishara ya kupongezana,; Pancho Panchilio aliwataka watu wake kuteremka kuzimu ili kushuhudia kile kilichoitwa ‘Hukumu ya Mwisho’.

“Na tutawafuatilia mbali katika uso wa dunia,” Pancho aliwaambia wenzi wake. Kisha kila mmoja akavaa uso wake wa bandia akiwa sehemu yake ambayo mpaka hapo hawakuweza kuonana sawasawa. Wakavaa kisha Pancho akiwa katika guo jeusi akifuatiwa na wajumbe wake watatu wakatoka na kuteremka ngazi kuelekea bondeni walikopenda kukuita Kuzimu.

§§§§§

Scoba aliendlea kusukuti huku bado akiwa kasimama hakujua lipi lakufanya mbele ya kamera ile. Baada ya kuumiza sana kichwa akakumbuka kipande kimoja cha kisa ambacho aliwahi kusimuliwa na Kamanda Amata jinsi anavyozipita kamera kama hizo, akatabasamu kisha akajirusha kwa kutanua miguu na kunata ukutani, akiwa katanua miguu yake na kukanyaga huku na kule na mikono hivyo hivyo, akanata juu kabisa na kuanza kujivuta kwa namna ambayo wewe huwezi hata kidogo, ukimtazama unaweza kusema na mjusi au kenge.

Aliifikia ile kamera na kuushika waya wake kutoka nyuma akauchomoa, kisha akajiachia na kutua chini taratibu. Kisha akaenda kwa mwendo wa kasi mpaka katika zile ngazi, alipofika tu alikutana uso kwa uso na mtu mmoja aliyekuwa akipanda juu, Scoba akaruka na kutua juu ya ukingo wa ngazi uliotengenezwa kwa mabomba ya aluminiam akaseleleka na mguu mmoja akamtandika teke Yule mtu kisha akajiachia na kumshukia pale chini; kabla hajasema lolote akambana koo kwa goti lake.

“Wako wapi?” akamwuliza.

“Akina nani?” Yule bwana aliongea kwa taabu.

“Wako wapi watu wangu? Mmewaweka wapi?” akauliza kwa ukali lakini kwa sauti ambayo haiwezi kwenda popote.

“Hakuna watu wako huku aliyekwambia wapo ni nani?” Yule bwana akajibu kiujeuri. Scoba akamnyonga mkono na kuuvunja, Yule bwana akapiga yowe la uchungu, Scoba akaona itakuwa noma, akamkamata na kumvunja shingo kisha akaichukua bunduki yake aina ya S.M.G na kuteremka ngazi mpaka kwenye maboksi Fulani akajificha. Watu wawili wakapita eneo lile wakitangulizana, akatulia na kusubiri Yule wa pili ili amputeze lakini alighairi baada ya kusikia mazungumzo yao matamu.

“Wanauawa wote, tena sasa hivi,” mmoja akamweleza mwenzie.

“Yaani ni historia,” mwingine akamuunga mkono. Alipopita wa kwanza akamwacha wa pili akamkata na kabala moja matata sana kisha akamvuia kwenye maboksi taratibu na kumtuliza. Yule wa kwanza akajkuta kila akiongea hakuna kuungwa mkono akageuka kutazama kulikoni akakutana macho na Scoba. Bila kuchelewa Scoba alirusha kisu maridadi kabisa na kumchoma koromeo, akajibwaga chini.

§§§§§

Madam S alifunguliwa minyororo na kukokotwa kuelekea katika chumba cha mauaji, Chiba naye akachukuliwa kikondoo namna hiyo, Dr. Jasmin kwa kuwa yeye hakuteswa kama wengine alitembea mwenyewe mpaka ndani ya chumba kile cha kutisha.

“Wafunge pale huyo bibi na huyo kijana mtukutu, kisha mlete huyo rembo mbichi hapa,” JoKi alitoa amri nayo ikatekelezwa. Walipomaliza wakaambiwa wakamlete Kamanda Amata li kazi ya mauaji ianze kama ilivyopangwa. Amata akaletwa, na ye kama kawaida akatuliaa na kukokotwa mpaka ndani ya chumba kile kinachonuka damu mbichi na iliyoganda, macho yake yalikuwa yakiwatazama wote waliojipanga mle ndani wakiwa na silaha nzito nzito. Mara hiyo hiyo Pancho na watu wake waliingia ndani ya chumba kile na kusimama mahala Fulani.

“Sasa tunataka tuanze shughuli yetu, karamu ya damu, JoKi! Nataka ufanye kazi hii kama nilivyokuagiza, lakini kwanz ahuyo mrembo lazima aingiliwe nah ii ni motisha kwenu vijana wangu haya na muanze kazi sasa ya kumuingilia,” Pancho akatoa amri, vijana wawili walioshiba kimazoezi wakamvamia Jasmin, mmoja akaanza kumvua nguo kwa nguvu huku mwingine akishusha zipu yake kuuchomoa mshedede.

Yule jamaa aliyekuwa akimvua nguo Jasmine alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuchapwa makonde mawili matamu kabisa, akapepesuka pambeni na kujipanga upya, alipomwendea Jasmin ili ampe kibano alikutana na mapigo matano ya karate ya haraka haraka yaliyompeleka chini. Yule mwingine alitoa macho baada ya kujikuta dudu lake likikatika vipande viwili.

“Aaaaaaiiiggghhhh!!!” alipiga kelele huku akijiangalia, kila tu akashtuka waliposikia sauti ya kisu kikitua ardhini huku kikiwa kimekata dhakari ya Yule bwana.

“Shit! Muue huyo mwanamke haraka!” JoKi alitoa amri huku akiwakinga Pancho na wenzake.

“Nini JoKi?” Pancho akauliza.

“Tumevamiwa!” akatamka neno hilo na hapo hapo alishuhudia minyororo aliyofungwa Kamanda Amata ikikatika kwa shabaha maridhawa kutoka kwa Scoba. Amata aliruka sarakasi maridadi na risasi nne zilichimba chini, alipotua chini tayari alikuwa na shingo ya mtu, alimkamata na kumzungusha kichwa, Yule bwana akatoa macho na kuachama kinywa chake,kisha akambwaga chini. Alipogeuka huku na kule, JoKi hayupo, Pancho na watu wake hawapo.

“Scoba fungua hao, fanya juu chini wafike kwenye gari, hii kazi niachie mimi niimaize, pumbavu zao,” Kamanda Amata akampa maagizo Scoba kisha yeye akajibana mahali na S.M.G mkononi, akanyata kwa tahadari akiwa hajui wapi wale watu wamepotea ghafla namna hiyo. Mara taa zote zikazimika, giza likachukua nafasi ndani ya jingo hilo.

Scoba akaivaa miwani yake na kuendelea kuona vizuri kabisa, akawafungua Chiba na Madam S.

“Asante T.S.A 4, hakikisheni humu ndani hatoki mtu akiwa hai,” Madam S alitoa amri mara moja kama cheo chake kilivyo.

Mara sauti ikasikika kutoka katika vipaaza sauti vizivyoonekana.

“Ak! Ak!Ak! Ak! Hii ndiyo himaya ya Shetani, Taifa ndani ya nchi, hamjafanya lolote na hakika hamtatoka humu mkiwa hai, lazima muongee na bwana ngurumo,” ile sauti ikacheka tena kwa dhihaka.

“Usimsikilize huyo hanithi, Scoba ongoza mbele Jasmine linda nyuma ninyi ndio mna nguvu kwa sasa mi namaliza kazi,” Kamanda Amata akatoa maelekezo kisha kwa mwendo wa taratibu alipita kwenye ujia mrefu ulioonekana ukienda mahala Fulani.

“Nitakukamata tu, na leo itajulikana mbivu na mbichi,” akajisemea. Mara nyuma yake akasikia kama mtu aiyetua ghafla kwa miguu laini, akageuka ghafla na kujikuta akipata pigo moja kali la kung fu, akayumba na kusimama tena, akajikuta akipigwa ngwala tamu, akapaa hewani na kujibwaga chini, akajikunja na kujiinua kwa ustadi. Alikuwa ni Naima aliyemtembezea mchezo huo.

“Malaya mkubwa wewe! Sasa umeingia mikononi mwangu!” Kamanda akaunguruma.

Mara ile sauti ikasikika tena ikicheka na cheko lake likifanya mwangwi,

“Mtoto wa kike kutoka Kigoma lazima akuoneshe kazi”.

Mara taa zikawaka, Naima akajizungusha huku akipiga vijikelele kama nyau, akampelekea pigo la kwanza Kamanda akaliona, la pilia akaliona la tatu akaliona, la nne Kaliepa kwa chini na kujizungusha kwa kasi, aliupiga mguu wa Naima lakinia Naima aliruka sarakasi hiyo ile ngwala ikamkosa, Naima alitua sakafuni na kupiga teke kali huku akiruka tik tak; hilo lilimpata Amata na kumuinua juu juu na kumbwaga chini mzima mzima.

Naima alitua sakafuni na kusimama kwa madoido huku akimwonesha ishara ya mkono Amata akimwambia, “ Come to me boy, come to me boy”.

Dharau hizo Amata alizichoka, akajirusha kujiinua, Naima akataka kumwahi, akaruka teke ambalo lilikusudiwa kutua kidevuni mwa Amata lakini akaikinga mikono yake na kuudaka mguu wa Naima, akauzungusha kwa minajiri ya kuuvunja lakini Naima naye akaruka hewani na kujizungusha sambasamba na akili ya Amata na mguu wa pili akirusha teke lingine lakini Amata akaliepa na kumwachia, wote wakaanguka chini. Amata akawahi kuinuka na kujiweka sawa, Naima alipoinuka alikutana na mapigo kumi na mbili ya karate, kwa kasi aliyoitumia Kamanda Amata , Naima aliweza kuyakinga mapigo manne tu na nane yaliyofuata yalimwacha hoi.

“Come to me bitch!” Kamanda Amata akamwita kwa dharau, Naima damu zilimtoka kinywani na puani, alijifuta bila mafanikio.

“Hesabu ushakufa Naima!” Amata alimwambia.

Naima akasonya na kujitutumua kumvamia Amata, akakutana na kono lenye nguvu lilimtandika ngumi moja ya maana katika ziwa lake la kushoto. Naima alisimama ghafla akiwa katoa macho, akijitahidi kuongea lolote lakini alijikuta hawezi. Alipotaka kuanguka Amata akamwahi, akamtazama husoni, akambusu kwenye paji la uso. Mara taa zikazimika akasikia sauti ya bastola inayoondolewa usalama, akawahi kuruka na kumwacha Naima akifumuliwa vibaya na risasi hizo.

“Tulia, fuata maelekezo yangu, sasa hivi sina masihara na kiumbe yoyote Yule, nipeleke walipo mabosi wako,” akaamuru.

JoKi akiwa mikono juu, akatulia kama alivyoamuriwa, akataka kugeuka, Kamanda akamzuia.

“Sijakwambia ugeuke, nimekwambia unipeleke walipo vinyamkera wako,” akamwambia tena. JoKi akatafakari jambo,

“Sasa bila kugeuka nitakupelekaje walipo? Hivi ninyi mnachokifanya mnakijua? Mtajuta kuzaliwa ndani ya nchi hii,” JoKi akaongea.

“Funga domo lako kibaraka tu wewe, na sasa utatujua sisi ni nani, mlifikiri jaribio lenu litafika wapi? Haya nioneshe hao vinyamkera wako,” Amata akaamuru.

“Siwezi kukuonesha na huna la kunifanya,” alijibu JoKi huku akigeuka mzima mzima na kukutana na Amata aliyekuwa amefura kwa hasira.

“Ha ha ha ha, Kamanda Amata, nasikia tu unavyovuma katika visa vyako vya kubahatisha, safari hii maji yapo shingoni ee?” akaongea kwa ngebe zilizompandisha hasira Amata, akaiweka vizuri bunduki aliyoishika mkononi mwake.

“Amata, wanaume wakutanapo huweka silaha chini na kupambana kwa mikono,” akaongea kwa dharau huku mikono yake kaiweka kiunoni kana kwamba anaongea na mtu wa kawaida mbele yake.

“Najua hila zako, ichukue wewe utumie kunishambulia,” Amata akamwambia huku akimrushia ile bunduki. JoKi akainua mikono yake ili kuidaka na ndilo kosa alilolifanya. Konde moja la kilo nyingi lilitua sawia mbavuni, la pili na la tatu, JoKi akawa hoi, akajaribu kujipanga lakini Amata hakumpa nafasi kwani alimvurumishia makonde yasiyo na idadi mpaka akaenda chini na kuanza kubingirika kwenye ngazi, akafka chini akiwa hoi.

“Kelele zote mi nilijua unaweza mchezo kumbe hamna kitu, boya tu, haya simama sasa,” Amata akamwambia JoKi. Bado JoKi alikuwa pale chini, Kamanda Amata akamsogelea. Joki alifyatuka kasi na kumtia ngwala Amata, lakini hakukubali, aliruka beki na kusimama kwa miguu yake miwili, wakati huo tayari JoKi nae alikuwa wima. Kamanda Amata alirusha teke lililopanguliwa vyema na JoKi. JoKi alipeleka mashambulizi ya karate kwa Kamanda lakini mapigo yote yalikingwa kwa ufundi wa hali ya juu. Wakasimama pande ofauti wakitazamana kama majogoo hasimu, yenye uhasama wa kudhulumiana tetea.

JoKi alifyatuka na kucheza karate kadhaa kwa kumwelekezea mapigo ya hatari Amata, lakini alijikuta hapati kitu baada ya Kamanda Amata kuyacheza vizuri na kubaki imara akimtazama JoKi aliyeishiwa cha kufanya. JoKi akajikunja na kuanza upya mashambulizi, safari hii alikuja na ujanja mwingine ambao umakini kwa kamanda Amata ulihitajika. JoKi alipeleka mashambulizi makali ya mikono na wakati huo huo akibadilika na kutumia miguu yake. Kasi ya mashambulizi hayo ilimfanya kamanda Amata apate tabu kucheza na akili mtu huyo, lakini yote ya yote Kamanda Amata aliyakinga kwa ufundi. JoKi alimpiga ngwala ya nguvu na Amata .lirushwa juu, lakini akiwa hewani alijigeuza na kutumia mguu mwingine na kumzabua teke kali la shavu na kumvunja taya. JoKi akayumba na kujibamiza ukutani huku akijishika taya lake la chini lililohama mahala pake. Hakumjali, alimpa mapigo makali na kumwacha akiwa hoi sakafuni hajielewi, akamfuata na kumkamata kichwa chake akambamiza ukutani kwa nguvu kisha akamwinua mzima mzima.

“Nioneshe walipo,” akamwambia huku akiwa kamkunja vyema shati lake, damu zikimvuja.

“Wapo safe house,” akajibu huku mabonge ya damu yakimtoka kinywani.

“Safe house ndo wapi?” akamwuliza.

“Ipo chini kabisa ya jingo hili, lakini huwezi kufika kabla hujauawa,” akamjibu huku akitoa cheko la ajabu kisha akatokwa na uhai.

§§§§§

Kazi nzito ilikuwa upande wan je ambako Scoba na Jasmin walikuwa wakiwadhibiti walinzi wa jengo hilo. Watu wa kijiji hicho walikimbia mbali wakisema majambazi yamevamia jumba hilo.

Chiba alipita huu na kule na kutokea kwenye mlango mmoja ulioandikwa ‘Control Room’ akauchezea huo mlango kidogo tu na kujikuta ndani. Chumba kikubwa kilichojawa na mitambo ya mawasiliano, kompyuta na vitu vingine, kutoka pale ndipo alipoona kamera zote za usalama za eneo lile jinsi zilivyokuwa zikifanya kazi na kuangaza kila eneo, alitikisa kichwa baada ya kuona ugumu wa kazi yao ulikuwa wapi kwani walionekana kila walipokwenda, jambo la kwanza alizima tambo uliokuwa ukiwaunganisha watu wote wa jengo hilo kwa simu maalum za ndani ‘Voip’. Baada ya hapo akaelekea mahala palipokuwa na kitu kama kabati lenye switch mbalimbali, akaelewa ni switch za milango, akaibofya na kufungua milango yote ya jumba hilo kisha akaharibu mfumo mzima.

Akiwa katika shughuli hiyo akasikia mlio hafifu wa bastola inayoondolewa usalama.

“Nani alikwambia?” sauti ikatoka nyuma yake, “Haya mikono kichwani kisha geuka taratibu,” aliamuriwa. Chiba aliweka mikono kichwani na kugeuka kwa kasi na kuipiga teke ile bastola kisha akajirusha sarakasi na kuichukua mikononi mwake, Yule bwana alijikuta hana ujanja, macho yakamtoka. Kisha akamuongoza kwenye mitambo yake.

“Nioneshe mabosi wako walipo,” akamwamuru. Yule bwana hakuwa na aujanja aliwasha luninga mojawapo iliyowaonesha wale mabwanyenye kila mmoja akiwa katika harakati za kuiacha himaya hiyo, Chiba alibaki kinywa wazi, hakuamini kile anachokiona, aliwatambua watu wale kwa uwazi kabisa bila kificho akajikuta akiishiwa nguvu. Alipogeuka nyuma kumtazama Yule kijana hakumuona, katoweka. “Shiit!” akang’aka na kuiweka bastola yake vyema mkononi mwake kisha akaanza kuzunguka humo ndani kumtafuta.

Yule kijana alijificha kimya upande wa pili wa mashine zile, mkononi alikuwa na kisu akimvizia Chiba kufika upande huo ili amfanyie kweli, masikini, hakujua anacheza na kiumbe cha aina gani katika tasnia hiyo ya mchezo wa visu. Katika kupita akitafuta, Chiba alimwona Yule kijana akichungulia, akajifanya hamwoni kabisa na kuendelea kutafuta huku kampa mgongo. Yule kijana akaona hapo ndipo pa kumpata adui yake, akatoka mzima mzima na kisu mkononi kumpamia Chiba kwa nyuma. Chiba alimkwepa na kumdaka mkono, akauzungusha na kumnyanyua kisha kumbwaga chini na kumbana vyema.

“Nipe namba za milango!” akamwamuru.

“Sizijui,” akajibu huku akikunja sura kwa maumivu.

Chiba akaunyonga mkono kwa nguvu, “Taja, kabla sijakumaliza,” akamlazimisha huku akiunyonga ule mkono.

“Nataja, na-ta …” kabla hajamaliza, Chiba alishuhudia Yule kijana akitoa macho na kisu kimedinda shingoni mwake,

“Wamemuua!” akajisemea; kwa kasi ya ajabu alikichomoa kile kisu na kukirusha upande kilipotokea huku yeye mwenyewe akibiringika kuliacha eneo lile, akashuhudia risasi zikiufumua mwili wa Yule kijana ilhali mtu aliyemlenga akidondoka jirani na mlango bila uhai. Chiba akasimama chapchap na kuangaza macho huku na huko, chumba kilikuwa kimya, hakuna mtu zaidi yake na zile maiti mbili tu. Akahakikisha usalama kisha akazipekua zile maiti na kupata funguo moja ambayo hakujua hata ni ya kitu gani, akaitia mfukoni. Hakuzijali maiti akapanda juu ya kiti cha magurudumu kilichokuwa hapo na kuanza kucheza na zile kompyuta. Alishangaa kuona kuwa wale jamaa walikuwa wamejiunganisha na vitengo vyote muhimu vya serikali wakipata siri mbalimbali za vitengo hivyo.

Akaendelea kupekuwa na kukuta habari nyingi za Usalama wa Taifa zikiwa katika moja ya kompyuta hizo.

“Ni nani hawa?” akajiuliza bila kupata jibu. Akasogeza kiti chake na kuelekea kwenye luninga kubwa iliyoonesha jingo lote ndani na nje na kuanza kukagua sehemu moja baada ya nyingine, akatazama vyumba mbalimbali vya jingo hilo na kugundua kuwa bado walikuwa hawajafika hata nusu ya hifadhi ya jingo hilo.

“Shiit!” alijikuta aking’aka na kujisukuma kwa nguvu mpaka kwenye meza ndogo yenye simu na kuiyakua kisha akabofya namba fuklani na kuweka sikioni.

“…Inspekta Simbeye, Chiba anaongea hapa!” akaijibu sauti ya pili iliyoitikia simu hiyo.

“…Oh, Chiba, nafarijika kusikia sauti yako Kamanda wangu, nipe dondoo,” akamwambia.

“…Inspekta naomba haraka iweekanavyo uje na vijana wa kazi wasiopungua kumi na tano wenye silaha nzito zilizoshiba, eneo ni Kerege, Bagamoyo, plot namba KG/BY 1230p…” kisha akakata simu. Alipogeuka kwenye luninga hakuwaona wale Mabwanyenye kwenye vyumba vyao, wametoroka! Akazima swichi kubwa na umeme ukakatika kila kona ya jengo lile, akilenga kuwanasa kama walikuwa wakijaribu kutoroka na chombo chochote kitumiacho umeme, kisha akachukua silaha kutoka kwa mmoja wa maiti wale na kutaka kutoka kwenye kile chumba, akakumbuka kitu; akarudi.

Akaenda kwenye moja ya kisanduku na kutaka kufungua akashindwa, akagundua kuna funguo hutumika, akafikiri kidogo na kuchukua kale kafunguo alikochomoa ka Yule jamaa, akatumbukiza na kuzungusha kidogo tu, mlango ukafunguka. Ilikuwa na sisytem unity iliyounganisha kompyuta zote ikiwa na maana kuwa ilihifadhi data zote za wale jamaa. Kwa kutumia ile bunduki akavunja kufuli lililokuwako nyuma ya dubwasha hilo, akaondoa funiko lake na kutazama anachokitaka, akafyatua waya nene nene zilizojaa huko, akavuta dubwasha Fulani kubwa kubwa na kulichomoa kutoka kwenye system ile, akatikisa kichwa kwa ushindi, kisha akatokomea nalo.

§§§§§

“Hapana, lazima niende!” Gina alimsisitizia Inspekta Simbeye.

“Gina nimekuleta huku ili upumzike, sasa acha tupeleke kikosi katika eneo la tukio,” Inspekta Simbeye akambembeleza Gina lakini Gina hakukubaliani na bembelezo hilo. Mwisho alikubali kwa shingo upande kubaki Hospitali ya Lugalo chini ya uangalizi wa madaktari wa kijeshi.

Inspekta Simbeye alichukua vijana wachache wanaojua kazi, kikosi maalumu cha kukomesha ujambazi kilichoundwa na Kamanda Toss kikaingia kwenye Land Cruiser za Polisi. Kutoka kituo kikuu gari hizo zilichukua uelekeo wa Makongo mpaka Mwenge waipomchukua Inspekta huyo na kuongoza kwenda Kerege. Kwenye gari hizo hakuna aliyeongea, kila mmoja alikuwa kimya kabisa akiitafakari shughuli inayomkabili, bunduki zilikuwa tayari zimejazwa risasi na magazine za akiba zikipachikwa kwenye vikoba maalum tayari kupokea zile zilizopo chemba pale itakapobidi.

KEREGE

KAMANDA AMATA BAADA YA KUHAKIKISHA JOKI AMEKATA ROHO; akaondoka upesi eneo lile, kila alipokuwa akipita kutazama tazama alikuwa safari hii milango iko wazi kabisa, hakuna tena milango ya siri, kazi ya Chiba ilisaidia. Akaiendea lifti ili aweze kushuka chini kabisa ya jengo hilo. Kwa mbali akiwa anasikia milio ya risasi za piga nikupige alijua wazi kuwa huko kazi inaendelea.

Ghafla akasimama kwenye moja ya kona za ndani ya jingo hilo baada ya kusikia michakacho ya viatu vya mtu anayekuja upande wake, akajiandaa kwa shambulizi la dharula, alipohisi mtu huyo amekaribia, alijitoa mzima mzima lakini pigo lake likakingwa kwa ustadi wa hali ya juu.

“Oh, sorry asee! Chiba vipi?” kumbe alikuwa Chiba.

“Yeah, hapa ni kujilinda muda wote, tuelekee chini, hawa jamaa wako huko,” Chiba akatoa maelekezo na kisha wote wakateremka kwa kutumia ngazi kwa maana Chiba alikuwa amezima umeme na kufanya lift zote zisifanye kazi. Haikuwachukua muda kuwasili chini kabisa ya jingo hilo kubwa na la kisasa, “Lilijengwa kwa miaka mingapi hili?” Kamanda akajiuliza, huku wakiufuata mlango mmoja baada ya mwingine, lakini vyumba vyote vilionekana tupu.

“Hawapo Chiba, laiti ningewapata!” Kamanda alimwambia Chiba huku akiiteremsha silaha yake kutoka mikononi na kuiweka mahala pake.

“Nimempa taarifa Inspekta, yuko njiani,” Chiba akatoa taarifa kwa Kamanda.

“Safi sana Chiba, kumbuka hapa sote hatuna mawasiliano na dunia ya nje,” kamanda akaitikia kisha wakaendelea kupekua chumba kimoja na kingine. Katika moja ya vyumba hivyo kulionekana kuna mlango wa siri lakini ulikuwa wazi ndani yake, akausogelea na kuchungulia ndani yake, ulikuwa ujia mrefu sana uliopotelea gizani.

“Hii ni njia ambayo kwa vyovyote wametorokea,” Kamanda akamwambia Chiba.

“Kila mmoja alikuwa na njia yake Kamanda, hapa alitumia mmoja wao,” Chiba akajibu. Kamanda Amata akageuka kumtazama kama akihoji kitu, lakini mwisho aliuliza.

“Umejuaje?” akamwuliza.

“Nimewaona katika dakika zao za mwisho kutoroka lakini mshenzi mmoja akanivamia; katika kupambana naye ndipo nilipowapoteza sikuona wametorokaje lakini walikuwa vyumba tofauti,” akaeleza.

“Umenikiwa kuona sura zao?” akauliza tena.

Chiba akatulia kwa nukta chache kwa maana aliwaona mara hii wakiwa hawana vinyago na aliwatambua kuwa ni vigogo wakubwa serikalini, “Je kama walitumia sura za bandia kutughilibu?” akawaza, kisha akamtazama Amata.

“Hapana, walificha sura zao kama kawaida,” akajibu.

“Ok, tutawajua tu, usiguse kitu watu wa Foresinc Bureau waje kufanya kazi yao ya kunasa alama za vidole na nyinginezo,” kamanda akamwambia Chiba huku wakitoka na kuelekea chumba kingine, nako wakakuta mambo hayo hayo, wakatoka na kupita vyumba vingine kama vitatu vilivyoonekana viko katika mtindo huohuo. Wakaviacha na kuendelea na uchunguzi wao zaidi na zaidi. Katika ghorofa ya chini wakagundua jambo ambalo liliwatia hofu, mioyo yao ikashtuka, kama wangekuwa na mioyo myepesi wangeziamia au hata kufa kabisa.

“Hawa ni mashetani!” Chiba akasema.

“Nin hiki?” Kamanda akauliza huku akivuta hatua ndani ya chumba hicho kikubwa, “Hawa jamaa hawastahili kuishi kabisa, ningewatia mkononi wangejuta kuzaliwa,” akaongeza.

“Kamanda, hapa msaada wa haraka unahitajika, nafikiri vijana watakuwa tayari nje,” akasema Chiba.

§§§§§

LAND CRUISER ZA POLISI ziliingia kwa fujo eneo lile na vijana wa kazi wakaruka tayari kuanza kudhibiti eneo hilo. Ilikuwa kama sinema ya kizungu vile. Inspekta Simbeye akawapanga vijana kuzunguka jingo hilo na wengine kuingia ndani kupitia lango kuu, haikuchukua dakika kumi tayari walizingira na risasi kadhaa zilirindima ndani ya wigo huo, kisha kundi la watu waliokuwa katikanulinzi wa jingo ilo waliwekwa chini ya ulinzi.

“Hivi hili jumba lina milikiwa na nani?” Simbeye akajiuliza bila kupata jibu. Vijana wake bado wakiwa katika sakasaka hiyo upande wa pili wa jingo walipomweka chini ya ulinzi Madam S na Jasmine. Kutii sheria bila shuruti, Madam S akiwa kachafuka damu zilizoganda, alisalimisha silaha yake na Jasmine akafanya hivyo kisha wakatiwa pingu. Inspekta Simbeye aliwaona wakiletwa kwake wakiwa na pingu mikononi, wakaamuriwa kukaa chini pembeni kidogo kwa wenzao.

Scoba alitokea pale ambapo gari ya Gina iliegeshwa baada ya kutekwa na kuletwa huku, moja kwa moja akaliendea lango na kulifungua na kuchungulia nje kwa minajiri ya kuwashambulia waliopo huko na apate jinsi ya kutoa gari hi;lo na kuwaokoa wengine kama walivyopanga, alishangaa alipoona vijana wenye silaha wakiwa wamewalaza chini vijana wengine kama kumi hivi tena kifudifudi, kwa jinsi alivyowaona tu akajua ni Polisi, akajitokeza mzima mzima na bunduki yake mkononi.

“Jisalimishe kama ulivyo, weka silaha chini,” amri ikatoka upande wa nyuma yake, Scoba akafanya hivyo na kuamuriwa asogee mbele, akafungwa pingu na kulazwa chini kama wenzake.

§§§§§

“Inspekta!” Kamanda Amata aliita wakati alipokutana na Simbeye katika uwanja wa himaya hiyo, huku akishangaa huku na kule kuwaona wenzake wote wamepigwa pingu isipokuwa yeye na Chiba ambaye bado alimwacha ndani.

“Kamanda Amata! Pole kwa kazi na janga hili,” akampa pole huku akimpa mkono.

“Asante Inspekta, tunafuga mashetani nchi hii Inspekta, naomba vijana kama watano hivi na wewe mwenyewe, pamoja na mama yangu muache huru hakuna baya hapa tupo kazini, tuingie ndani ya jengo hili, tupite na muone wenyewe mchezo wa kuwapa watu viwanja bila kujua nia na malengo yao,” Kamanda alilalama. Madam S na Jasmine wakafunguliwa pingu zao, Scoba naye alkadhalika.

“Usishangae hawa ni watu kama wewe!” Inspekta alimwambia mmoja wa polisi ambaye alishangaa amri anayopewa ya kuwaweka huru watu hao.

Muda si mrefu, vijana watatu wakaingia ndani ya himaya hiyo wakiwa na suti nadhifu, mach yao yakiwa yamezibwa na miwani nyeusi, hakika walikuwa watanashati na nyuma yao aliwafuata mzee wa makamo mwenye mvi kadhaa kichwani mwake.

“Karibu sana Bwana Hosea, nafurahi umefika,” Inspekta alimkaribisha wakapeana mikono kisha wote wakaongozana kuingia katika jingo hilo.

Hakuna aliyekuwa akiongea, kila mmoja alikuwa makini kutazama kila kilichopo ndani humo, hakuruhusiwa mtu yeyote kugusa chochote kwa mikono uchi.

Chiba aliliongoza jopo hilo baada ya kukutana nao humo ndani, akawaingiza chumba cha mawasiliano, jopo hilo likabaki hoi.

“Tazama huu mtambo, unanasa habari kutoka ofisi zote za serikali, simu zote za kiofisi kuanzia za Rais na watu wake zote zinanaswa hapa, ona hii kompyuta ni kubwa sana inafanya mambo mengi sana, inanasa picha kule Uwanja wa Ndege, nah ii kama unavyoona inaonehsa mazingira yote ya Ikulu,” Chiba alikuwa akieleza.

Hosea akabaki kajishika kiuno, taratibu jasho lilikuwa likimtiririka.

“Nani mmiliki wa jumba hili, na alikuwa na lengo gani na Taifa hili?” akauliza, lakini wote walikuwa hawana jibu.

“Hatujamaliza, twendeni huku chini, naomba muwe na roho kavu kwa unyama uliopo huku,” Chiba akawaambia kisha akawafikisha ‘Kuzimu’, “Hapa ndipo wanapotumia kuua wabaya wao, mnauona ule mwili, mnaweza kuutambua, Mkuu?” akauliza. Hosea na vijana wake wakauendea na kuuangalia vyema, wakaugeuza huku na huko.

“Hapana simfahamu huyu,” Hosea akajibu.

“Ni mwandishi anayetafutwa na jeshi la Polisi kwa miezi mingi sasa, ameuawa mbele ya macho yangu,” Chiba akawaeleza.

“Chilese Zuberi,” Inspekta Simbeye akataja jina la Mwamndishi huyo, akachuchumaa kumwangalia vizuri na jeraha baya la risasi likiwa limeharibu kabisa sehemu ya nyuma ya kichwa chake.

Walipotoka hapo wakaelekea kwenye chumba kingine, na kukuta miili ya watu watano iliyofungwa kwa kuning’inizwa.

“Unyama gani huu?” akajiuliza Hosea. Wakatazama mwili mmoja baada ya mwingine na kuitambua miili ile kuwa ni ya watu ambao walipotea katika mazingira ya kutatanisha na hawakuonekana tena, mmoja wao akiwa Mwanasiasa machachari kabisa.

“Nimegundua kitu,” Simbeye akasema huku akiwageukia wenzake.

“Nini Inspekta,” Hosea akauliza.

“Kutokana na watu tuliowakuta humu wakiwa marehemu, na mikasa yao ambayo jeshi la polisi lilichukua kama vyanzo vya upotevu wao, kuna mtandao unaofanya kazi hii,” Simbeye akasema.

“Yeah, upo sahihi, siku zote wanalaumiwa Usalama wa Taifa pindi miili hii ikiokotwa haina kuchwa au meno, lakini hii nyumba ya nani? Lazima ukweli ujulikane,” Hosea akaongeza. Walipomaliza kukagua kila kona mle ndani wakatoka nje na kukuta tayari jeshi la Polisi limefika zaidi na waandishi wa habari kama kawaida yao walikuwa wametanda nje wakijaribu kupata habari hii na ile.

Madam S, Chiba, na Jasmine wakaingia kwenye gari maalum iliyokuja hapo, iliyofunikwa kwa vioo vyeusi, bila kupoteza muda ikaondoka eneo lile. Kamanda Amata na Scoba walibaki pamoja na vijana wa Polisi kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Akiwa kafuatana na vijana wawili wenye silaha waliingia vyumba vya chini na kupita ile milango iliyoonekana kama njia waliyotorokea wale mabwana, walitembea katika njia tofauti, moja ya njia hizo alipia Kamanda Amata na kijana mmoja wa Polisi mwenye silaha, njia nyingine aliingia Scoba na kijana mwingine nay a tatu aliingia Inspekta Simbeye na kijana wake. Cha kushangaza njia hizo tatu hazikukutana, kila moja ilikwenda kutokea mahala pake, na zilitokea kwenye nyumba tatu tofauti, utata. Mara tu baada ya hilo, uchunguzi mkali juu ya nyumba hizo, umiliki wake na uhalali wa kuwa hapo uliendelea; Mjumbe wa shina na Mwenyekiti wake walikuwa katika hali ngumu ya kuhojiwa hili na lile. Walipopata majibu ambayo kwayo yaliridhisha wakawaacha na kuondoka zao.

SHAMBA – baada ya siku 3

MADAM S, CHIBA, JASMINE, SCOBA, GINA NA KAMANDA AMATA wote walikuwa wameketi katika meza kubwa ya duara, kila mmoja mbele yake alikuwa na kabrasha lililojaa makaratasi. Walikuwa na majeraha ya hapa na pale, Gina bado alikuwa akiendelea kuuguza jeraha lake lakini sasa akiwa chini ya uangalizi wa Dkt. Jasmine.

Ukimya ulichukua nafasi kwa kila mmoja, walikutana tena katika meza hiyo ambayo daima wakikaa hapo basi ujue kuna maamuzi magumu ya kufanya. Gina alijigeuza na kujiweka vizuri kitini kwake huku mikono yake ikiwa juu ya meza na sura akiwa ameikunja kidogo.

“Pole sana Gina,” Madam S alimpa pole mwanadada huyo, akajikohoza, “Niliwaita siku tano zilizopita tuonane kwa kikao cha dharula lakini baadae nikagundua kosa nililolifanya, anyway, haina haja ya kuljadili bali tuangalie lile ambalo sasa ndio nimewaitia kabla ya kutazama lile nililotaka niwaeleze siku tano zilizopita ambalo litamhusu Kamanda zaidi,” akaongeza, alionekana wazi hata uongeaji wake haukuwa ule wa kawaida kwani bado alihisi maumivu ya hapa na pale na alihitaji mapumziko. Kipindi hicho cha siku tatu, T.S.A wote walikuwa pamoja Shamba, huko Gezaulole, wakipumzika na kuweka mikakati mipya, hakuna aliyejua walipo isipokuwa wao wenyewe.

“Kurasa ya kwanza kabisa kuna majibu kutoka kitengo cha utambuzi wa alama za mikono na vidole,” madam Sakawaambia na kila mtu akapekua jalada lake na macho kuyatumbulia hapo.

“Is it?” Gina alikuwa wa kwanza kupayuka.

“Yes It is,” Chiba akadakia. Wote wakamtazama kwa jicho kali.

“Una maana gani?” Madam akamuuliza.

“Nilikuwa nasubiri tu haya majibu kama yataoana na yangu, nilipozifanyia crossmatch hizi alama za vidole ambazo nilizipata kwenye vitasa vya milango ya mwisho ya vile vyumba vya chini, licha ya hivyo tu niliwahi kupata baadhi ya picha zao sekunde chache kabla hawajatoroka lakini sikuwa nauhakika nao kwani siku hizi teknolojia imekuwa; mtu anaweza kutengeneza sura ya Rais na kuivaa, hivyo sikuliweka wazi hili, lakini niliwaona na kila mmoja alikuwa mahala pake, bila kinyago cha usoni,” akawaeleza kisha akanyanyuka na kuiendea droo ndogo akatoa flash na kuipachika kwenye kompyuta mpakato, kisha akawasha chombo cha kutolea picha ukutani na dakika moja baadae picha zilianza kuonekana.

Pancho Panchilio, mfanyabiashara mkubwa nchini, mshawishi wa mambo mengi ya kisiasa, mwenye asili ya Kihindi, watu wengi walimjua kama si kwa jina basi kwa sura. Mhindi huyu alilindwa kwa jinsi zote, hagusiki. Alikuwa tajiri sana mwenye malori makubwa ya kusafirisha, aliwekeza kwenye sekta ya usafiri hasa sekta ya anga. Kwa ujumla alikuwa mwema mbele ya Watanzania, alitoa misaada mingi hapa na pale, alijenga mahospitali, mashule na kusaidia watoto yatima sehemu mbalimbali za nchi.

Picha ya pili nayo ilitia shaka kwa wote angu waliposoma katika lile jalada na sasa wakiona ushahdi ule wa Chiba kwa njia ya picha. Kigogo mkubwa serikalini, aliyepewa dhamana na Wasakatonge kisha anawazunguka na kuwafanyia mambo yasiyoelezeka kwa maandishi. Maisha yanakuwa magumu kila uchwao ilhali wengine wakitunisha matumbo yao kwa njia mbadala za unyonyaji na ukandamizaji.

Picha ya tatu nayo ilikuwa yaleyale, Kigogo mwingine kwenye wizara Fulani naye alikuwamo ndani ya jopo hilo la udhalimu.

Haikuishi hapo, Chiba kutoka katika Hard Disk aliyoichomoa katika ile kompyuta yao, alifumua majina mengine ya watu mbalimbali ambao kila mwezi huchukua mgawo wa pesa lukuki kwa mambo yao binafsi, wapo viongozi wa juu, wa kati na wa chini; si wanasiasa tu hata wafanyabiashara nao walikuwapo tena wengi.

“Inatosha!” Madam akamwambia Chiba, naye akazima ule mtambo wake.

“Sasa nataka operesheni ianze mara moja, taarifa tayari zipo panapohusika, lakini Pancho Panchilio akamatwe mara moja, pamoja na hawa vigogo wawili. Leo hii wanatakiwa kuwa pale kituo cha kati kwa mahojiano zaidi.

KATIKA JENGO NYETI LA SERIKALI

“Boss kuna mgeni anataka kukuona,” sauti nyororo ya Katibu Muhtas ilipenye kwenye sikio la Mheshimiwa Sikotu Sambwene, mmoja wa watu wazito na ‘vingunge’ katika Serikali.

“NIlikwambia sitaki kuonana na wageni au hukunielewa?” Sikotu akauliza kwa ukali, “Mwambie sina muda wa kuonana na watu sasa; aje mwezi ujao,” akaongeza kuongea kwa ukali uleule. Akiwa bado katika kumfokea huyo Katibu wake; mlango ulifunguliwa na Madam S akajitoma ndani mzima mzima na kusimama kando.

“Mgeni wako ni mimi,” akamwambia Mh. Sikotu. Mheshimiwa Yule alijkuta katika wakati mgumu, alijitupa kitini na kumtazama mwana mama huyo aliyeingia kibabe katika ofisi hiyo.

“We; nenda,” akamwambia Yule Katibu wa Mheshimiwa.

“Unafuata nini hapa?” Skotu akauliza.

“Sina jibu la kukwambia ninachokifuata, maana bila shaka unajua ninachokifuata kwako, nina swali moja tu ambalo ukinijibu shida yangu itakuwa imeisha,” Madam S aimwambia Sikotu huku akiwa kasimama mbali kwa tahadhari.

Mhesimiwa Sikotu akajifuta jasho ilhali mashine ya kupoza hewa iikuwa bize ikifanya kazi hiyo, akaweka kitambaa chake ndani ya koti lake na kumtazama mwanamama huyo aliyesimama mbele yake.

“Unasemaje?” akauliza.

“Unafahamu nini au kipi juu ya jumba kubwa la kifahari lililoko Kerege kitalu namba KG/BY 1230p?” akauliza Madam S. Sikotu akabaki kaduwaa, hakuwa na jibu. Madam S hata kabla hajapewa jibu hilo akatupa swali lingine.

“Unajua nini juu ya mwandishi wa habari mashuhuri aliyepotea miezi miwili nyuma?”

“Hivi we mwanamke una kichaa!” Sikotu akang’aka huku akiwa wima macho yamemtoka.

“Na ukichaa wangu ndio umenifikisha hapa leo, ulifikiri ukijiziba sura mbele yangu sintokujua? Kwa taarifa yako kutokana na kazi yangu, sauti zenu wote nyie nimezikariri, hukuweza kujificha mbele yangu ulipokuwa ukiongea, Sikotu, kiongozi mwenye dhamana, unajishusha hadhi kwa tamaa yako ya pesa mzee, utastahafu kwa fedheha baba, hebu jiangalie hapa,” Madam S akamtupia picha kumi na tano zinazomwonesha ndani ya jengo lile ambazo zilinaswa kwa kamera za usalama. Sikotu alizitupia jicho na machozi yakaanza kumtoka.

“Mwisho wa ubaya ni aibu, na mshahara wa dhambi mauti,” Madam S akainua akakusanya picha zake na kuzirudisha mkobani.

“Tutaonana mahakamani,” akageuka na kuondoka, akaufunga mlango nyuma yake na nukta hiyo hiyo vijana wawili waliovalia sare za jeshi la polisi waliingia ndani ya ofisi ile, pingu ikawekwa mezani.

“Siwezi kwenda popote, kwanza ni ninyi ni nani? Nani kawatuma? Ninyi mna kibali cha kunikamata mimi? Mnaitaka kazi yenu au?” Sikotu alikuwa kama akiweweseka, akavua koti na kulitupaa kando, mwili wote ulikuwa umelowa kwa jasho kana kwamba kamwagiwa maji.

Mmoja wa wale askari akatoa waraka ulioidhinishwa kukamatwa kwake, akamwonesha kwa mbali huku akimkatalia kuushika kwa mikono yake. Sikotu hakuwa na la kufanya aliahangaika, Yule askari kijana akamsogezea pigu ikiwa wazi ajipachike mikono yeye mwenyewe. Sikotu akavuta saraka katika meza yake akaitoa bastola iliyokuwamo ndani yake, wale askari wakaweka silaha zao tayari wakimwamuru kuweka chini bastola yake. Akaitumbukiza kinywani kwa minajiri ya kujilipua.

“Weweeee aaacchhhaaaaa!!!” mmoja wa askari akapiga kelele na wakati huo huo mlio wa risasi ulisikika na Mheshimiwa Sikotu akabwaga chini huku damu zikicafua vibaya shati lake, bastola yake ikitupwa mbali.

“Ha ha ha ha haujafa kiongozi lazima ufike mahakamani,” Sauti ya Chiba ilisikika nyuma ya wale askari, wakageuka na kumwona kijana huyo aliyekuwa ndani ya suti nadhifu akiiteremsha bastola yake. Chiba alipiga mkono wa Sikotu kwa risasi yake na kuumiza vibaya kiganja chake kabla hajajilipua.

WAKATI HUO HUO – ofisi nyingine ya serikali

“Una la kujitetea hapo?” Scoba na Gina walisimama mbele ya meza kubwa wakimtupia swali hilo mtu mkubwa mwenye tumbo la maana akilikuna kwa mbali. Alionekana wazi kuchanganyikiwa kwa hilo, hakuwa na la kujitetea.

“Gina, mtie pingu!” Scoba alitoa amri na Gina akaitekeleza. Gavana wa benki kuu ya Tanzania, Dkt. Shekibindu akavikwa pingu na kutolewa ofisini mpaka nje kwenye gari ya polisi, na moja kwa moja akapelekwa kituo cha kati kwa mahojiano zaidi.

WAKATI HAYO YOTE YAKITUKIA…

Kamanda Amata alisimama mikono yake akiwa kaikutanisha nyuma ikining’iniza bastola yake ndogo ya Kiitaliano ijulikanayo kama Beretta, huku usoni kajivika miwani safi nyeusi, suti yake ilimkaa vyema mwilini, kiatu chake kilichong’azwa kwa kiwi hakikuongopa kuonesha taswira ya kila kilichokaribu.

“Hajaonekana kabisa ofisini,” Msichana aliyeonekana kama Katibu wa Pancho Panchilio alimjibu Amata kwa swali aliloulizwa sekunde chache zilizopita.

“Tangu lini?” akauliza tena.

“Ana siku nne sasa, mara ya mwisho aliondoka hapa majuzi akiwa kama aliyechanganyikiwa, sikujua anakwenda wapi na wala hakusema, tangu hapo hakurudi tena,” Yule msichana akaendelea kueleza.

“Unapajua nyumbani kwake?”

“Hapana, mimi ni mfanyakazi tu huwa tunaonana hapa ofisini bas,” akajibu.

“Ok, naomba niingie ofisini kwake,” Kamanda akaomba.

“Pamefungwa, na funguo ni moja tu anayo mwenyewe,”

“We niruhusu au nikataze,” Kamanda akasisitiza.

“Sawa ingia, mi nakwambia hayupo,” Yule mwanadada

akaendelea kujibu.

“Usihofu, mimi ni afisa wa polisi,” akamwonesha kitambulisho bandia cha upolisi. Akauendea mlango na kuufungua kwa jinsi zake zilezile. Ilikuwa ofisi pana yenye kila kitu ndani yake, hakukuwa na mtu, akaiendea simu na kuitazma kisha akabonyeza kitufe cha kuiruhusu itoe ujumbe wowote uliopo.

“…Mheshimiwa booking yako imekamilika na tiketi yako tutakutumia soon katika email yako… enjoy your flight…”

Akili ya Kamanda ilisimama ghafla, “Katoroka!” akajikuta anajiuliza bila kupata jibu, akaiendea kompyuta ya mezani na kuipekua hapa na pale mpka alipopata email ya Panchilio ambayo ilikuwa wazi bila kufungwa akapekua e mail zilizoingia saa sabini na mbili zilizopita. Ilikuwa ni hiyo email ya tiketi ya ndege iliyoondoka saa arobaini zilizopita na ndege moja ya shirika la huko Uarabuni, safari yake ilionekana kuishia Bangalore, India.

“Hayawani huyu kaniwahi,” akawaza huku akitoka na nakala ya ile ytiketi aliyoitoa kwenye mashine kule ndani.

“Unaitwa nani?” akmwuliza Yule binti alipokuwa akitoka.

“Naitwa Ruth,”

“Mwenyeji wa wapi?” akamwuliza.

“Wa Arusha,” akajibu.

Kamanda Amata akamtupia jicho la wizi huku akiiondoa miwani yake usoni na kutuza muono wake juu ya kifua cha binti huyo kilichojaa vyema, matiti yaliyowekwa ndani ya sidiria yakitamanisha kila lijari. Kamanda akameza mate, akajikohoza, akaingiza mkono mfukoni na kutoa kadi ndogo ya kibiashara akampatia.

“Tuonane jioni ya leo, Hotel ya Land Mark, saa mbili kamili usiku,”

Ruth akamtupia jicho kijana huyo aliyekuwa akiipachika tena miwani usoni mwake, akaibetua midomo yake na kuuma chanda chake kwa meno ya mbele.

“Ok!” akaitikia. Kamanda Amata akauona mshtuko wa wazi mbele yake kutoka usoni mwa Yule dada, akageuka nyuma na ndipo alipogundua kuwa hawako peke yao, watu wawili walisimama nyuma yake, waliojazia kimazoezi. Akageuka na kupita katikati yao akaondoka na kuwaacha. Alipolifikia gari lake akasimama na kugeuka nyuma, akawaona wale vijana wamesimama mlangoni wakimwangalia. Akasimamisha tax na kuondoka huku akiliacha gari lake palepale.

HATIMA

“Pancho Panchilio ametoroka,” kamanda alimwambia Madam S walipokutana katika mgahawa wa Steers.

“Atapatikana tu, na lazima tumpate iwe kwa mvua iwe kwa jua,” Madam akajibu.

GEREZA LA UKONGA saa tatu baadae

“Mmefurahi sasa sio? Maana rafiki zenu wamekuja kuungana nanyi, msijali tunamleta na Yule Gabacholi, tunamfuata hukohuko India,” Madam S akamwambia Kanayo na Mahmoud Zebaki waliokuwa wakitumikia kifungo chao.

“Tunakata rufaa!” Kanayo akajibu.

“Kateni tu kwani nimewafunga kamba, hiyo ni haki yenu kimsingi na kikatiba,” Madam S aliwajibu huku akinyanyuka na kuondoka.

Kanayo akasonya kwa gadhabu, “Our day will come!”(Siku yetu inakuja) akamwambia Madam S. akageuka kumtazama Kanayo O Kanayo, “Yes, will come soon, we shall face each other in the battle field,” (ndiyo inakuja punde tu, tutaonana kwenye uwanja wa mapambano)

§§§§§

Aiwa chumbani kwake, alimtazama Gina aliyekuwa mbele yake na vazi jepesi la usiku, Amata alijikuta akipata shida maeneo ya kati kwajinsi mwili wa mrembo huyo ulivyokuwa ukiita. Gina akageuka na kumtazama.

“Vipi? Arts of War ni ipi kwa mi na wewe sasa?” alimuuliza huku akijilaza ktandani na kuruhusu sehemu kubwa ya mwili wake kujiachia wazi.

“…mwili huo uliookotwa kando kando ya pwani ya Coco ni wa msichana wa kati ya miaka 25 na 30. Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Ndugu Sekuru, amethibitisha kutokea tukio hilo na uchunguzi unaendelea kuwabaini waliofanya mauaji hayo…”

Sauti ya Mtangazaji wa TV ilimtoa Kamanda Amata katika kifua cha Gina na kutupia macho katika kioo hicho.

“Shittt!” akang’aka, “Wamemuua Ruth!” akaongeza huku akisimama.

“Ndio tatizo lako, ukisikia mwanamke kauawa unahuzunika lakini mwanume unapotezea, mwanaume Malaya wewe!” Gina akalalamika huku akikaa kitandani.

“Gina, huyu ni sekretari wa Pancho Panchilio,” akamweleza.

“What? Usinambie,” Gina naye akahamanika.

“Kwa nini wamemuua msichana mzuri kama Yule, masikini Ruth!”

8 8 MWISHO 8 8

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment